From: 2022-03-15 to: 2022-03-28
(FARMING AND AGRIBUSINESS )
AFISA KILIMO DARAJA LA II - 3 POST
Wizara ya Kilimo
Duties & Responsibilities

 i. Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;

ii. Kukusanya takwimu za bei na mazao kila Wiki na kila mwezi,

iii. Kukusanya takwimu za upatikanaji mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,

iv. Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,

v. Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,

vi. Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,

vii. Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,

viii. Kutoa habari juu ya technolojia mpya kwa wadau,

ix. Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,

x. Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,

xi. Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,

xii. Kuandaa, kutayarisha, kufunga na kusambaza mbegu bora,

xiii. Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,

xiv. Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,

xv. Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, mauwa na viungo,

xvi. Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,

xvii. Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji.

xviii. Kufanya utafiti wa udongo,

xix. Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,

xx. Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,

xxi. Kuendesha/kusimamia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili ilikuondoa utata juu yambegu,

xxii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa n a Msimamizi wake wa kazi.

Qualifications

Wahitimu wenye Shahada ya Kilimo au Shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vyengine vinavyotambuliwa na Serikali

Remuneration

TGS D