SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna, amepata ushindi mkubwa kisiasa baada ya Jopo la Kusuluhisha Migogoro ya Vyama vya Kisiasa kubatilisha uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Kisiasa uliozuia kuhifadhiwa kwa jina Linda Mwananchi Movement (LMM).
Jopo hilo liliamua kwamba chama cha Liberty National Democratic Alliance (LINDA) hakikuwa kimesajiliwa kikamilifu wala kwa muda, na kwamba kuhifadhi jina lake kulikofanywa Novemba 15, 2024 kuliisha muda wake kisheria baada ya siku 90.
Wanachama wa jopo hilo walisema kuwa mara muda wa kuhifadhi unapokwisha bila mwombaji kuendelea na hatua zinazohitajika za usajili, haki ya jina hilo hupotea moja kwa moja na haiwezi kufufuliwa kupitia uamuzi wa kiutawala.
Mgogoro huo ulianza baada ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kukataa ombi la kuhifadhi jina la Linda Mwananchi Movement lililowasilishwa na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, mwanaharakati Pauline Njoroge na rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) Faith Odhiambo. Watatu hao wanahusishwa na mrengo unaoungwa mkono na Bw Sifuna.
Walipinga uamuzi huo wakisema kuwa jina la Linda Mwananchi Movement ni tofauti kabisa na Liberty National Democratic Alliance na hivyo halikupaswa kuzuiwa.
Jopo lililoongozwa na wakili Gad Gathu lilikubaliana nao na kuamuru Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikiria upya ombi hilo ndani ya siku saba. Hata hivyo, uamuzi huo haujasajili chama kipya moja kwa moja bali umerejesha maombi hayo kwa msajili kwa hatua zaidi.
Katika uamuzi wake, jopo hilo lilisema sheria hairuhusu kulazimisha waombaji kutaja waasisi wa chama katika hatua ya kuhifadhi jina.
Zaidi ya hayo jopo liliondoa stakabadhi zote zilizowasilishwa na LINDA katika kesi hiyo, likisema chama hicho hakikuwa na uwezo wa kisheria kushiriki kwa sababu hakijasajiliwa rasmi.
Jopo lilibaini kuwa majina ya Liberty National Democratic Alliance na Linda Mwananchi Movement hayafanani kwa muundo, matamshi wala maana. Lilisema neno “Linda” ni neno la Kiswahili lenye maana yake ya kawaida, ilhali LINDA ni kifupi cha majina ya chama kingine.
Majaji waliongeza kuwa Msajili alikuwa ameruhusu vyama vingine kutumia maneno kama “Liberty”, “National”, “Democratic” na “Alliance”, hivyo kukataa jina la Linda Mwananchi kulikuwa kinyume na kanuni za usawa na haki katika utoaji wa huduma za umma.
Kutokana na sababu hizo, baraza lilitangaza kuwa uamuzi wa Msajili uliotolewa Agosti 7, 2026 haukuwa halali na kuagiza ombi la Linda Mwananchi Movement lichunguzwe upya kwa mujibu wa sheria.
Aidha, jopo lilichunguza suala la uhifadhi wa jina la LINDA na kubaini kuwa chama hicho hakikuwasilisha kwa wakati fomu rasmi ya kuomba usajili wa muda kama inavyotakiwa na sheria.
Kulingana na uamuzi huo, jina hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa siku 90 pekee kuanzia Novemba 15, 2024. Msajili wa Vyama vya Kisiasa alikiri kuwa hakukuwa na ombi rasmi lililowasilishwa ndani ya muda huo. Hata barua iliyotumwa Februari 4, 2025 haikutosheleza mahitaji ya kisheria.
Kwa msingi huo, jopo liliamua kuwa uhifadhi wa jina la LINDA ulikuwa umefutika kisheria na haukuweza kutumiwa kuzuia waombaji wengine kutafuta jina la kisiasa linalofanana kwa neno “Linda”.
Ushindi kwa Sifuna akipata idhini kusajili Linda Mwananchi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]