KENYA imepewa leseni ya kutengeneza dawa mpya ya kumeza ya kuzuia maambukizi ya ukimwi, hatua inayoiweka miongoni mwa nchi tatu Afrika zitakazozalisha dawa hiyo kwa ajili ya masoko ya Afrika.
Kampuni ya dawa ya Merck imetoa leseni ya kuzalisha toleo la bei nafuu la Alimatravir, dawa inayotarajiwa kumezwa mara moja kwa mwezi. Nchini Kenya, dawa hiyo itatengenezwa na Kampuni ya Universal Corporation.
Hatua hiyo inatajwa kuwa ya kihistoria kwani watengenezaji wa dawa barani Afrika wamehusishwa katika mchakato wa uzalishaji wa dawa ya HIV tangu mwanzo.
Utafiti wa awamu ya tatu unaoendelea Kenya, Uganda na Afrika Kusini unahusisha wanawake vijana na unatarajiwa kukamilika mwaka ujao.
“Afrika inabeba robo ya mzigo wa magonjwa duniani. Tunatengeneza chini ya asilimia sita ya vifaa vya matibabu tunavyohitaji na asilimia moja ya chanjo tunazotumia.” akasema Rais William Ruto, katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Afya Aden Duale katika mkutano wa pembeni wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Alisema janga la Covid-19 lilionyesha madhara ya kutegemea minyororo ya usambazaji kutoka nje.
“Watu wetu walilipa gharama ya minyororo ya usambazaji ambayo hatukuimiliki. Hatutapitia hali hiyo tena,” akasema.
Rais Ruto pia alisema Afrika sasa ina fursa ya kutengeneza dawa zake badala ya kusubiri kuzinunua kutoka nje.
“Kiwanda kisichokuwa na wanunuzi si sekta ya viwanda. Ni jengo la gharama kubwa,” alisema.
Merck inasema dawa hiyo inaweza kugharimu dola tano (Sh650) kwa mtu kwa mwaka.
Dkt Nicholas Muraguri alisema ushirikiano huo utasaidia Afrika kuimarisha uzalishaji wa dawa, ajira na usambazaji.
“Ushirikiano huu si wa kusambaza dawa pekee, unahusu kubadilisha mfumo wa usawa katika afya duniani,” akasema.
Alisema tatizo la kuzuia maambukizi ya ukimwi si ukosefu wa sayansi, bali gharama na kupungua kwa ufadhili wa programu za afya.
Kenya yapewa leseni ya kuunda dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]