
SAMIA: KISIASA 2025 TULIKUMBWA NA MISUKOSUKO
SAMIA: KISIASA 2025 TULIKUMBWA NA MISUKOSUKO #globaltv #breaking #samiasuluhuhassan
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

SAMIA: KISIASA 2025 TULIKUMBWA NA MISUKOSUKO #globaltv #breaking #samiasuluhuhassan

Growing reliance on ride-hailing services is raising fresh concerns over passenger safety and accountability, with stakeholders calling for tighter verification of drivers and vehicles, stronger monitoring of accounts and clearer systems for reporting complaints.

Some fuel station workers in Tanzania are working without protective footwear, gloves or masks and with little or no training on how to respond to fires, raising concerns over workplace safety in an industry that handles highly flammable substances.

VIONGOZI kutoka kaunti za Meru na Samburu wamegawanyika kuhusu oparesheni ya usalama inayoendelea katika Kaunti ya Samburu kulenga majangili wanaodaiwa kuvamia maeneo ya Meru na Isiolo. Oparesheni hiyo ilianzishwa baada ya mashambulizi ya mara kwa mara ya majangili katika maeneo hayo na kuuawa kwa maafisa wawili wa polisi, polisi wa akiba na raia wawili Isiolo wiki iliyopita. Bunduki za maafisa hao pia ziliibwa wakati wa shambulizi hilo huko Gotu. Hata hivyo, oparesheni hiyo inayotekelezwa na kikosi maalumu cha polisi imekosolewa baada ya mamia ya mifugo kuuawa katika Wadi ya Waso, Samburu. Gavana wa Samburu Lati Lelelit na Mbunge wa Samburu Mashariki Jackson Lekumontare wameitaka serikali kusitisha oparesheni hiyo. “Watu wasio na hatia wamepoteza mifugo 700, wakiwemo ng’ombe, mbuzi na punda, katika muda wa siku nne na maafisa wa polisi wamekuwa wakifyatua risasi bila kujali. Ni jambo la kusikitisha kwamba wahalifu wachache waliwaua watu watano Isiolo, lakini hilo haliwezi kuhalalisha mauaji ya kiholela ya mifugo,” akasema Bw Lelelit. Bw Lekumontare alisema wakazi walioathiriwa wanapaswa kufidiwa na oparesheni hiyo isimamishwe ili wazee wa jamii washirikishwe katika kuwatambua majangili. Kamanda wa Polisi wa Samburu David Nkoroi alisema wakazi kadhaa wameripoti kupoteza mifugo, lakini bado hawajabaini idadi kamili ya mifugo hiyo Wabunge John Mutunga (Tigania Magharibi), Dan Kiili (Igembe ya Kati), Julius Taitumu (Igembe Kaskazini), Mugambi Rindikiri (Buuri) na Mpuru Aburi (Tigania Mashariki) nao wameitaka serikali kuimarisha oparesheni dhidi ya majangili. Wakizungumza mjini Meru Jumamosi, wabunge hao walisema wafugaji wa Meru wamepoteza karibu ng’ombe 20,000 huku watu 300 wakiuawa au kujeruhiwa na majangili wanaoendesha shughuli zao kutoka Isiolo na Samburu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Mnamo Machi, Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alitangaza baadhi ya maeneo ya Laikipia, Meru, Samburu na Isiolo kuwa hatari. Bw Murkome aliidhinisha oparesheni iendelezwe kutwaa silaha haramu mikononi mwa raia. Naibu Rais Kithure Kindiki aliunga mkono oparesheni hiyo, akisema serikali itaongeza nguvu dhidi ya majangili wenye silaha katika Isiolo na Samburu. Wakati huo huo, Bw Murkomen alijutia kuuawa kwa mifugo Samburu, lakini akasema serikali haitasitisha juhudi za kurejesha usalama katika Isiolo, Samburu, Turkana na Pokot Magharibi. Alisema oparesheni hizo zinalenga kurejesha silaha haramu na mifugo iliyoibwa, kuvunja mitandao ya uhalifu na kurejesha amani ya kudumu. Waziri huyo alisema vyombo vya usalama vimeagizwa kuchukua tahadhari zaidi ili kupunguza madhara kwa raia na mali wakati wa oparesheni. Aliongeza kuwa zaidi ya silaha 3,000 haramu na risasi 8,000 zimepatikana katika oparesheni za usalama Kaskazini mwa Bonde la Ufa na Kaskazini mwa Kenya.

MBUNGE wa Makadara, George Aladwa, amepata uungwaji mkono mkubwa katika azma yake ya kuwania ugavana wa Nairobi baada ya wajumbe na wenyekiti wa matawi ya ODM kumuunga mkono katika uchaguzi wa 2027. Katika hafla iliyofanyika katika eneobunge lake wikendi, Bw Aladwa aliidhinishwa kwa kauli moja na wajumbe wa matawi ya ODM, hatua iliyompa nafasi rasmi ya kutafuta tiketi ya chama katika uchaguzi huo. Bw Aladwa, ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la ODM, alisema yuko tayari kushindana na wagombea wengine ambao wametangaza nia ya kuwania kiti hicho. Katika hotuba yake, mbunge huyo alisema yeye ni miongoni mwa wanachama wa muda mrefu wa ODM ambao wamekiunga mkono wakati wa mazuri na magumu, hivyo anastahili kupewa tiketi. “ODM ina mgombea na nimejisajili. Nimewahudumia Wakenya kupitia chama hiki na niko tayari kuwa gavana wa Nairobi,” akasema Bw Aladwa. Pia alifichua kuwa baadhi ya viongozi wanapanga kuondoka katika vyama vyao na kujiunga na ODM kwa matumaini ya kupewa tiketi ya kuwania kiti hicho. “Kwa wale wanaotoa pesa wakitarajia kumng’oa Aladwa, nataka kuwaambia kwamba mimi si mtu wa kusukumwa pembeni na nyinyi nyote mnajua hilo. Kutakuwa na ushindani. ODM ni chama cha kidemokrasia chini ya kiongozi wetu wa chama, Dkt Oburu Oginga,” akasema Bw Aladwa. Kuhusu mpango wa mafuta wa ununuzi wa mafuta wa serikali kwa serikali (G-to-G, mbunge huyo alisema ulilenga kutatua tatizo la awali kwa kuruhusu bidhaa za petroli kuagizwa kwa masharti ya mkopo yaliyoongezwa hadi siku 180. Alisema hatua hiyo ilipunguza shinikizo la haraka katika soko la fedha za kigeni na kuipa nchi nafasi zaidi ya kudhibiti mahitaji yake ya dola. “Ikiwa mpango wa G-to-G unaelezwa kuwa wa gharama kubwa au usio wa kawaida, basi wanaotoa madai hayo wanapaswa kuwasilisha mikataba, bei za uagizaji, ada za ziada, gharama za usafirishaji na ushahidi mwingine,” akasema. “Ikiwa kuna ushahidi wa ufisadi au ukiukaji wa sheria, uwasilishwe Bungeni, kwa mashirika ya uchunguzi na taasisi nyingine zinazohusika. Madai mazito yanahitaji ushahidi mzito.” akaongeza. Mbali na Bw Aladwa, wagombea wengine ambao wametangaza nia ya kuwania kiti hicho ni pamoja na Askofu Margaret Wanjiru, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya na Mbunge wa Kasarani Ronald Karauri. Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja pia anatarajiwa kuwania muhula mwingine katika juhudi za kuwa gavana wa kwanza wa Nairobi kuchaguliwa tena tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi mwaka 2013.

KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka amezua mjadala kuhusu msimamo wake wa kisiasa baada ya kuonyesha dalili ya kuwa atashiriki handisheki na Rais William Ruto upinzani ukishindwa uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka amesisitiza kuwa siasa za ushindani kati ya Rais Ruto na vinara wa upinzani inastahili kuzingatia masuala yanayohusisha maslahi ya nchi badala ya uhasama wa kisiasa. “Ukitushinda, tunaweza kutathmini ukiwa na tabia nzuri. Tukikushinda, tutaangalia masuala haya yote. Tuangaliane kwa sababu tuna nchi na Mungu haheshimu binadamu licha ya hadhi yake,” akasema Bw Musyoka. Bw Musyoka alikuwa akizungumza jana katika Kaunti ya Siaya ambayo ni ngome ya kisiasa ya marehemu kigogo wa siasa za upinzani Raila Odinga. Hatua ya kinara huyo wa Wiper kumsifu Rais Ruto imeibua mjadala kuhusu mahali ambapo uaminifu wake wa kisiasa upo. Siku tatu zilizopita alimsifu Rais kwa kujenga barabara inayoelekewa kwake Tseikuru. “Bw Ruto kwa sababu ya kuogopa sisi ameweka bidii barabara ifike Tseikuru na namwambia awekee bidii imechelewa kwa sababu barabara hiyo ingekuwa imefika Maua. Bw Ruto anatumiwa na Mungu kwa njia spesheli. Kuweka hiyo bidii si Ruto ni Mungu. Kufikia Agosti mwaka tukikuja nyumbani itakuwa imekaribia sana,” akasema Bw Musyoka wakati wa Ukumbusho wa miaka 20 tangu mauti ya mamake. “Sasa tuna chuo cha kitaifa cha kiufundi baada ya kuongea na Ruto. Tunakubali kuwa hii inafaa kuwa chuo cha kitaifa cha kiufundi,” akaongeza. Kauli ya Bw Musyoka imekuja wakati ambapo kuna kutoaminiana ndani ya upinzani huku Rais Ruto akitumia kauli za kiongozi huyo wa Wiper kumkejeli na kusema kuwa ni kati ya viongozi wanayemtambua kazi yake. Aidha Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki miezi ya nyuma amekuwa akimsifu Bw Musyoka na kumrejelea kama kiongozi muungana ambaye anastahili kuungana na serikali ili kuwafanyia Wakenya kazi. Jana Bw Musyoka pia aliitaka serikali kuelekeza nguvu kwa wapinzani watakaokuwa kwenye debe badala ya kumlenga Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

HATUA ya Linda Mwananchi kumuidhinisha rasmi Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwa mgombea wake wa urais, inaonekana kufunga mlango kwa azma ya Gavana wa Siaya James Orengo kuwania uongozi wa nchi kupitia vuguvugu hilo. Katika mkutano huo wa Jumamosi, viongozi wakuu wa vuguvugu hilo waliamua kumuunga Seneta Sifuna huku wakisaka muungano mkubwa wa upinzani kuelekea kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027. “Leo (Jumamosi), tulikutana kama uongozi wa Linda Mwananchi na kuamua kusonga mbele pamoja, tukiwa tumeunganishwa na lengo moja la kujibu wito wa Wakenya wanaotafuta utawala bora na kuikomboa nchi. “Pia tuliamua kwamba Edwin Watenya Sifuna ndiye kiongozi wetu na mgombea wetu wa urais,” ikasema taarifa ya vuguvugu hilo. Mkutano huo ulihudhuriwa na Bw Sifuna, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Seneta wa Kisii Richard Onyonka, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi. Wengine waliohudhuria ni Mbunge wa Funyula Wilberforce Oundo, Anthony Kibagendi (Kitutu Chache Kusini), Clive Gisairo (Kitutu Masaba), Gavana wa zamani wa Meru Kawira Mwangaza na aliyekuwa rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) Faith Odhiambo. “Orengo alituma udhuru lakini sote tulikubaliana kwamba ni Sifuna pekee atakayeungwa kuwania urais. Hana nafasi sasa kwa sababu wote waliokuwepo walikubaliana kuhusu uwanizi wa Sifuna,” akasema Dkt Khalwale. Dkt Khalwale alisema wanachama walijaribu kumshawishi Bw Owino kuwania ugavana wa Nairobi kwa kutumia chama kimoja na Bw Sifuna katika juhudi za kuunganisha ngome zao za kisiasa. “Wengi walimpinga lakini sasa suala hilo ni uamuzi wake kwa sababu yeye alisimama kidete na msimamo wake,” akasema Dkt Khalwale. Bw Owino tayari amesajili The Mwananchi Party (TMP), ambayo anakusudia kutumia kuwania ugavana wa Nairobi. Mipango yake ya kisiasa imekuwa ikipingana na juhudi za kupata chama kimoja cha kisiasa, huku Bw Natembeya akisukuma Bw Sifuna kuwania kwa kutumia UDP. Bw Natembeya alisema wiki iliyopita kuwa Bw Sifuna alikuwa tayari kutangaza UDP kuwa chama atakachotumia kuwania urais. Jaribio la awali la kubadilisha jina la UDP kuwa Ukombozi People’s Party (UPP) lilikwama baada ya Kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka kusajili The Ukombozi Alliance (TUA), hatua iliyotatiza mipango ya vuguvugu hilo kuhusu jina hilo. Linda Mwananchi imetangaza mipango ya kuzindua chama cha Bw Sifuna cha kuwania urais Oktoba 3. Mmoja wa viongozi wakuu waliohudhuria mkutano wa Jumamosi lakini akakataa kutajwa jina alisema kutokuwepo kwa Bw Orengo hakupaswi kuchukuliwa kama ishara ya mgawanyiko ndani ya vuguvugu hilo. “Alisema hangeweza kuhudhuria mkutano lakini tutamuunga mkono Sifuna kama kila mtu alivyokubaliana. Hakuna mgawanyiko kama inavyodaiwa na tunaamini Orengo yuko pamoja nasi katika kumuunga mkono Sifuna,” akasema kiongozi huyo. Aliongeza kuwa maandalizi ya uzinduzi wa chama cha Bw Sifuna yalikuwa yamepiga hatua kubwa lakini akakataa kutoa maelezo zaidi. Bw Owino, katika taarifa baada ya mkutano huo, pia alisisitiza umoja ndani ya vuguvugu hilo, akisema lengo la upinzani kushinda serikali linaweza kufikiwa tu kupitia umoja wao. Bw Orengo hakuhudhuria mkutano wa faragha wa Jumamosi ambako uamuzi huo ulifanywa, licha ya kuwa ametangaza hadharani nia yake ya kuwania urais. Viongozi waliohudhuria kikao hicho walisema Bw Orengo alituma udhuru kwa sababu alikuwa na mwanafamilia mgonjwa, na kusisitiza kuwa kutokuwepo kwake hakupaswi kufasiriwa kama ishara ya mgawanyiko. Bw Orengo amekuwa akisisitiza kuwa umoja wa upinzani haupaswi kuzima azma za wagombea wengine na amekuwa akitaka uteuzi huru wa kumpata mgombeaji wa urais wa Linda Mwananchi. “Hakuna tatizo kushindana ndani ya Linda Mwananchi au upinzani. Muhimu ni kuwasilisha wagombea wote kwenye mchakato wa kuaminika wa uteuzi na, mwishowe, tupate mgombea mmoja wa kukabiliana na Rais William Ruto,” akasema gavana huyo hapo awali. Jana Taifa Dijitali ilijaribu kubaini sababu ya Bw Orengo kukosa mkutano huo na ikiwa anaunga mkono kuidhinishwa kwa Bw Sifuna, lakini hakujibu jumbe wala kupokea simu. Gavana huyo alitarajiwa Jumapili kuungana na kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i na Kiongozi wa People’s Party of Kenya Ndindi Nyoro kwa ibada katika Kanisa la Dominion Olerai kabla ya mkutano wa hadhara mjini Narok.

Under the PSPs licence, payment initiation service providers and account information service providers will be required to have Sh5 million in minimum capital.

By Chioma Obinna The Human Rights Writers Association of Nigeria (HURIWA) has raised concerns over reported killings, attacks and mass abductions in Plateau, Zamfara and Niger states, describing the incidents as evidence of a deepening security crisis. In a statement issued on Sunday and signed by its National Coordinator, Comrade Emmanuel Nnadozie Onwubiko, the rights […]

By Henry Umoru ABUJA — Presidential candidate of the Nigerian Democratic Congress, NDC, Peter Obi, has questioned President Bola Tinubu’s absence from the 81st United Nations General Assembly, UNGA, in New York. Obi raised the issue on Sunday in a post on his X handle after watching an address delivered by Ghanaian President John Dramani […]

ZIARA ya siku tano ya Rais William Ruto Luo Nyanza wiki iliyopita iliacha makovu ya uhasama na mgawanyiko wa kisiasa kati ya baadhi ya viongozi wa eneo hilo hasa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2027 zinavyoendelea kunoga. Rais Ruto alifanya ziara ambayo ilionekana ilifana katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay ambako alipigia debe azma yake ya kuwahi muhula wa pili. Hata hivyo, baada tu kuondoka, ziara hiyo imezua uhasama kati ya viongozi wa ODM ambao wanalumbana kuhusu siasa za eneo hilo. Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo Mabono alimchemkia Gavana Glady Wanga akidai ndiye alihusika na masaibu yake mbele ya Rais. Bi Odhiambo wiki hii alimfokea Gavana Wanga akidai alihusika na kuzomewa kwake katika mkutano ambao viongozi wa Luo Nyanza walikutana na Rais Ruto katika ikulu ndogo ya Kisumu. “Gladys Wanga nakuheshimu kama dadangu mdogo na mwenyekiti wa ODM lakini usichukulie hilo kama jambo la kawaida. Unawatuma watu waje wanidharau na kunishambulia katika eneobunge langu kisha unaketi kitako na kujifanya mzuri,” akasema Bi Odhiambo. Mbunge huyo alitishia kuwa huenda akaendesha kampeni kali dhidi ya Bi Wanga iwapo ataendelea kuvamiwa kwenye mikutano anayoandaa sehemu mbalimbali ya Nyanza. “Nitakukabili, na pia nitawaambia watu hawa wasikupigie kura. Najua unajishasha kwa sababu Rais aliwaambia watu hawa wakupigie kura lakini Rais huwa hapigi kura hapa, “Mimi sijui vita vyovyote vya kujificha na ukiendelea nitaendeleza vita vikali dhidi yako,” akaongeza Odhiambo. Mbunge huyo na Bi Wanga wamekuwa na uhusiano vuguvugu hasa kuhusu uongozi wa kaunti na siasa za kitaifa. Bi Odhiambo ni kati ya wabunge Luo Nyanza ambao wamekuwa vuguvugu akionekana kutounga mkono mrengo wa ODM unaoongozwa na Dkt Oburu Oginga au vuguvugu la Linda Mwananchi chini ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Katika mkutano wa Ikulu ndogo ya Kisumu, Bi Odhiambo alikuwa na wakati mgumu kuhutubu huku akipigiwa kelele na umati. “Alituma watu Kisumu wanizomee, akatuma watu pia katika eneobunge langu wanipigie kelele. Sitaendelea kumvumilia,” akasema. Juhudi za kumtaka Gavana Wanga azungumzie madai hayo hazikufaulu ila gavana huyo amekuwa akionekana kuhepa kujibizana na mbunge huyo anayehudumu muhula wake wa nne. Kinaya ni kwamba majibizano hayo yanapoendelea kama Mwenyekiti wa ODM, Bi Wanga ndiye atatia saini cheti cha chama iwapo Bi Odhiambo atapewa tikiti ya kutetea kiti chake kupitia chungwa. Katika Kaunti ya Homa Bay, kuna ushindani mkali wa kiti cha ugavana mnamo 2027 huku Bi Wanga akikabiliwa na kivumbi dhidi ya aliyekuwa Naibu Gavana Oyugi Magwanga. Wawili hao walikosana mwaka jana, Bw Magwanga akajiuzulu na itakumbukwa mnamo 2022, marehemu Raila Odinga alitekeleza jukumu muhimu la kuwapatanisha. Kupitia kupatanishwa na Bw Odinga, Bi Wanga aliishia kugombea ugavana naye Bw Magwanga akikubali kuwa mgombeaji mwenza wake. Katika kaunti jirani ya Migori, ziara ya Rais Ruto imeacha uhasama mkali kati ya Mbunge wa Uriri Mark Nyamita na Gavana Ochilo Ayacko. Bw Nyamita ambaye anahudumu muhula wa pili kupitia ODM analenga ugavana 2027 kupitia chama hicho. Bw Ayacko naye analenga kutetea kiti chake pia kupitia ODM na wawili hao watakabiliana katika mchujo wa chama. “Kazi ya Bw Ayacko ilikuwa kununua vuvuzela kwa vijana ili wazipulize katika mikutano yake ndipo waone kuwa yeye ni maarufu. Baada ya mkutano wa Kisumu, hakuenda Siaya bali alirudi hapa Migori kuhakikisha kuwa vijana wanapewa malori matatu ya vuvuzela,” akasema Bw Nyamita.
RAIS William Ruto amewajibu viongozi wa upinzani wanaokosoa rekodi yake ya maendeleo akisema kwa kufanya hivyo wanasaidia kuitangaza miradi yake kwa wananchi bila malipo. Akizungumza mjini Wundanyi, Kaunti ya Taita Taveta, Jumamosi, Rais Ruto alisema ataendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kote nchini licha ya madai kuwa baadhi ya miradi hiyo inafaidi maeneo yanayohusishwa naye kisiasa. […]

MJADALA kuhusu uchaguzi mkuu wa 2027 umechukua mkondo mpya baada ya kauli za viongozi wa kisiasa kuashiria uwezekano wa kuibuka kwa muungano wa kisiasa kati ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Huku baadhi ya wadau wakichukulia ushirikiano huo kama silaha ya kumenyana na Rais William Ruto, wengine wanahisi unaweza kuwa chanzo cha migawanyiko mipya ndani ya upinzani. Aliyekuwa Seneta wa kuteuliwa Gloria Orwoba ni mmoja wa waliozua mjadala huo baada ya kusema Wakenya wasipuuzilie mbali uwezekano wa Gachagua na Sifuna kujitokeza pamoja kwenye tiketi ya urais mwaka 2027. Kwa mujibu wa Orwoba, Sifuna si mwanasiasa wa kawaida bali ni kiongozi anayeweza kuwa mgombea mkuu wa kiti hicho. Kauli hiyo imeongeza uzito kwa mjadala unaoendelea kuhusu nafasi ya Sifuna katika siasa za kitaifa huku uchaguzi ukikaribia. Nyota ya Sifuna anayehusishwa na vuguvugu la Linda Mwananchi imekuwa iking’aa na kujijenga kama nguvu mpya ya kisiasa kuelekea 2027. Hata hivyo, changamoto kubwa imekuwa ni chombo cha kisiasa atakachotumia kwa azma yake. Orwoba anadai kuwa Sifuna tayari ana chama lakini anatafuta namna ya kukipa sura mpya ili kivutie wafuasi wengi zaidi. Ndani ya vuguvugu la Linda Mwananchi, mjadala kuhusu chama bado unaendelea. Lakini licha ya mjadala kuhusu vyama, Orwoba anaamini chama hakitakuwa kigezo kikuu kwa wapigakura. Kwa mtazamo wake, Wakenya wataangalia zaidi mgombea kuliko nembo ya chama. Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa tiketi ya Gachagua na Sifuna. Kwa mara ya kwanza, viongozi wa upinzani wameanza kuzungumzia waziwazi uwezekano wa wawili hao kushirikiana katika kinyang’anyiro cha urais. Kinachofanya mjadala huo kuwa wa kipekee ni kwamba Gachagua mwenyewe amewahi kusema hadharani kwamba yuko tayari kuwa mgombea mwenza wa Sifuna iwapo viongozi wa upinzani wataafikiana kuwa seneta huyo ndiye anayefaa kuongoza muungano huo. Aidha, amesema pia kwamba mpangilio wa kinyume unaweza kutokea ambapo yeye akiongoza tiketi na Sifuna kuwa mgombea mwenza. Kauli hizo zimezua hisia mseto ndani ya upinzani. Wapo wanaoamini kuwa ushirikiano kati ya mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika Mlima Kenya na kiongozi anayevutia vijana na wakazi wa mijini unaweza kubadilisha mwelekeo wa siasa za taifa. Hata hivyo, wengine wanatahadharisha kuwa hatua hiyo inaweza kuibua malumbano mapya kuhusu nani anafaa kupeperusha bendera ya upinzani. Aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ni mmoja wa watetezi wakuu wa muungano huo. Malala anaamini kwamba kuunganisha nguvu za Gachagua na Sifuna kutaunda kambi imara yenye uwezo wa kumpa Rais Ruto ushindani mkubwa. Kwa mujibu wa Malala, hesabu za kisiasa zinaonyesha kwamba kuunganisha Mlima Kenya, Magharibi na jamii za Maa kunaweza kuunda msingi mkubwa wa kura. Ndiyo sababu ametangaza mpango wa kuanzisha vuguvugu la “Triple M” linalolenga kuleta pamoja watu wa Mrima, Mulembe na Maa. Malala amekuwa akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Mlima Kenya na Magharibi mwa Kenya unaweza kuamua matokeo ya uchaguzi mkuu ujao. Hata hivyo, siasa za upinzani bado zinaonekana kuwa katika hatua ya mazungumzo. Chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP) kimeweka wazi kwamba kwa sasa hakitajiunga na Muungano wa Ukombozi (TUA). Badala yake, kina nia ya kushirikiana kwanza na vuguvugu la Linda Mwananchi kabla ya kuingia katika mazungumzo ya kuunda muungano mpana wa upinzani. Msimamo huo unaonyesha kuwa bado kuna tofauti za kimkakati kati ya vikundi mbalimbali vinavyolenga kumng’oa Rais Ruto mamlakani mwaka 2027. Wakati Kalonzo Musyoka na washirika wake wakisisitiza umuhimu wa muungano mmoja wa upinzani, makundi mengine yanaonekana kutaka kujijenga kwanza kabla ya kuamua namna ya kushirikiana. Kwa sasa, tiketi ya Gachagua na Sifuna bado ni wazo linalojadiliwa kisiasa na si makubaliano rasmi. Hata hivyo, kauli za Orwoba, Malala na Gachagua mwenyewe zimeifanya kuwa mojawapo ya mada zinazovutia zaidi katika siasa za 2027. Iwapo “ndoa” hiyo ya kisiasa itafungwa rasmi, inaweza kuimarisha upinzani au kuibua mvutano mpya ikizingatiwa kuwa Gachagua ni mmoja waliosuka muungano wa upinzani unaohusisha Kalonzo, Martha Karua, Eugene Wamalwa, Fred Matiang’i, Justin Muturi miongoni mwa wengine ambao awali walionekana kuungana dhidi ya Rais Ruto. Lakini jambo moja liko wazi: mjadala kuhusu Gachagua na Sifuna umeanza kuvuruga hesabu za upinzani na kufungua sura mpya ya siasa za uchaguzi

MFANYABIASHARA Ronny Raburu, anayesema ndiye aliyependekeza jina Azimio la Umoja kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga mwaka 2021, amesema amesikitishwa na uamuzi wa viongozi wa upinzani kuacha kutumia jina hilo na kulibadilisha kuwa Ukombozi Alliance. Raburu, Mkenya ambaye amekuwa akiishi Tanzania kwa takriban miaka 25, anasema jina la Azimio halikuwa tu kauli ya kisiasa bali lilikuwa na msingi wa kihistoria na kiitikadi uliotokana na Azimio la Arusha la mwaka 1967 lililoasisiwa na rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere. Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Raburu alisema anahisi urithi wa kisiasa wa Raila Odinga unasahaulika kwa haraka mno. “Nimevunjika moyo. Baba alikuwa akifanya siasa zenye misingi na falsafa maalum. Kila jambo alilofanya lilikuwa na maana yake. Inanishangaza kuona urithi wake ukiondolewa haraka hivi,” alisema. Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya ulitangaza wiki hii kuwa umeamua kubadili jina kuitwa Ukombozi Alliance kama sehemu ya kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Raburu alieleza kwamba wazo la Azimio lilizaliwa baada ya mahakama kubatilisha mpango wa Maridhiano ya Kitaifa (BBI) uliokuwa ukisukumwa na Raila Odinga na Rais( sasa mstaafu) Uhuru Kenyatta kufuatia maridhiano yao ya mwaka 2018. Kwa mujibu wake, Raila alimtafuta akihitaji jina la Kiswahili ambalo lingeendeleza roho ya BBI ya kuunganisha taifa lakini kwa lugha ambayo wananchi wengi wangetambua na kuielewa. “Alinipigia simu na kuniambia BBI imekwama na angependa jina la Kiswahili ambalo lingeendeleza lengo la umoja wa kitaifa. Alinitaka kushauriana na marafiki zangu Tanzania ili tupate jina mwafaka,” alisema. Raburu anasema alifanya mazungumzo na marafiki, wazee na watu waliokuwa na uelewa mkubwa wa historia ya Tanzania kabla ya kuwasilisha mapendekezo kadhaa kwa Raila. Miongoni mwa majina aliyopendekeza ni Azimio la Umoja, ambalo lilivutiwa na Azimio la Arusha lililotumika kama nguzo ya siasa za ujamaa na ujenzi wa taifa nchini Tanzania. “Nilihisi kwamba kwa kuwa BBI ilikuwa imeanguka, kulikuwa na haja ya kupata jina ambalo lingeendelea kuakisi wazo la kujenga madaraja ya umoja,” alisema. Siku chache baadaye, alishuhudia Raila akilizindua jina hilo hadharani mjini Nakuru. Baadaye lilikuwa msingi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya uliowaleta pamoja ODM, Jubilee, Wiper, Kanu na vyama vingine katika kampeni za urais za mwaka 2022. Hata hivyo, baada ya upinzani kuamua kujiita Ukombozi Alliance, Raburu anaamini siasa zimeondoka kwenye misingi ya itikadi na kuelekea katika misemo ya muda mfupi ya kisiasa. “Haya sasa ni maneno ya kampeni tu. Inaonekana watu wanatafuta jina litakalofaa wakati huo na kusaidia kushinda uchaguzi. Sioni falsafa iliyo nyuma yake,” alisema. Raburu, ambaye anatoka Kaunti ya Kisumu lakini ameishi Tanzania kwa muda mrefu, anasema urafiki wake na Raila ulijengwa kutokana na mapenzi yao ya pamoja kwa historia ya ukombozi wa Afrika Mashariki na nafasi ya Tanzania katika harakati hizo. Anamkumbuka Raila kama mwanasiasa aliyependa sana historia ya Tanzania, urithi wa Nyerere na mchango wa nchi hiyo katika kupigania uhuru wa mataifa mbalimbali ya Afrika. Kifo cha Raila, anasema, kilimuumiza sana kiasi kwamba hadi leo hajafuta nambari yake ya simu. “Mara nyingi narejelea jumbe tulizowasiliana. Wakati mwingine ninapoona siasa za sasa na watu wakidai Baba aliwaambia jambo fulani, natamani kuchapisha baadhi ya jumbe zake kuthibitisha ukweli, lakini naambiwa ni mawasiliano ya kibinafsi,” alisema. Kwa mujibu wa Raburu, si Azimio pekee linalopaswa kukumbukwa, bali pia mchango wa Raila katika siasa za Kenya. “Tunamsahau haraka sana. Hilo ndilo linaloniumiza zaidi,” alisema. Aidha, alisisitiza kuwa Kenya inapaswa kuendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania kwa kuwa nchi hizo mbili zimekuwa washirika wa karibu katika biashara, utalii na diplomasia kwa miaka mingi.

WALIPA ushuru nchini wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa kifedha kutokana na maamuzi ya serikali ambayo baadaye yanabainika kuwa yalikiuka sheria, yalitekelezwa vibaya au yalikiuka haki za raia. Uchunguzi wa kesi mbalimbali mahakamani unaonyesha kuwa serikali, kaunti, polisi na mashirika ya umma yameamriwa kulipa mabilioni ya pesa kama fidia, marupurupu, mishahara iliyocheleweshwa na mikataba iliyovunjwa. Kesi hizo zinahusu kukamatwa kwa watu kinyume cha sheria, mateso, mauaji ya kiholela, kufutwa kazi visivyo halali, migogoro ya ardhi, zabuni za umma na mikataba iliyokiukwa. Moja ya kesi zilizotikisa serikali ni ile ya kiongozi wa kampeni ya Nigeria, Nnamdi Kanu. Mahakama Kuu iliamua mwaka 2025 kuwa Kanu alitekwa nyara, kuwekwa kizuizini kwa siri na kuteswa kabla ya kupelekwa Nigeria. Serikali iliamriwa kumlipa Sh10 milioni kama fidia pamoja na gharama ya kesi. Katika kesi nyingine, Mahakama Kuu iliagiza polisi na Mwanasheria Mkuu kulipa Sh35.4 milioni kwa familia na waathiriwa 28 wa operesheni za polisi wakati wa maandamano ya Azimio mwaka 2023 katika maeneo ya Kisumu, Migori na Ahero. Mahakama ilibaini kuwa baadhi yao waliuawa, kujeruhiwa au kuteswa kinyume cha sheria. Mwanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu cha JKUAT, Allan Omondi, pia alitunukiwa Sh8 milioni baada ya mahakama kubaini kuwa polisi walimpiga na kumweka kizuizini kinyume cha sheria wakati wa machafuko ya wanafunzi mwaka 2019. Wiki hii, mtaalamu wa teknolojia ya habari Ndiang’ui Kinyagia alishinda fidia ya Sh5 milioni baada ya mahakama kuamua kuwa maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai walivamia nyumba yake huko Kinoo bila kibali cha mahakama na kutwaa mali yake kinyume cha sheria. Mbali na amri za mahakama, serikali imeanza kutekeleza mpango wa kufidia waathiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano yaliyofanyika kati ya 2013 na 2025. Serikali tayari imetenga Sh2 bilioni kwa mpango huo ambao unahusisha fidia kwa waliouawa, waliojeruhiwa na wale waliokumbwa na ukiukaji wa haki zao. Seneti pia inapambana mahakamani kupinga agizo la kulipa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua Sh50 milioni baada ya mahakama kubaini kuwa baadhi ya haki zake za kikatiba zilikiukwa wakati wa mchakato wa kumbandua madarakani. Kesi nyingine kubwa zinahusisha ukiukaji wa haki za binadamu uliotokea katika miaka ya nyuma. Michael Rubia alitunukiwa Sh17 milioni baada ya kubainika kuwa alizuiliwa kinyume cha sheria na kuteswa katika utawala wa zamani. Serikali pia ililazimika kugharamia matibabu yake nchini Uingereza. Mahakama ya Juu pia iliidhinisha malipo ya Sh2.5 milioni kwa kila mmoja wa wafungwa sita wa kisiasa waliokamatwa mwaka 1992 wakati wa maandamano Freedom Corner. Ilibainika serikali ilikiuka haki zao kwa kuwa walikamatwa na kuteswa. Katika kesi ya maafisa wa zamani wa Jeshi la Anga walioathiriwa baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 1982, Mahakama ya Rufaa iliidhinisha malipo ya jumla ya Sh6.25 bilioni kwa maafisa 284 walioteswa, kufungwa na kufutwa kazi kwa njia isiyofaa. Serikali pia imebeba gharama kutokana na mauaji yanayohusishwa na polisi. Familia ya mwandishi wa habari wa Pakistan, Arshad Sharif, ilitunukiwa Sh10 milioni baada ya mahakama kuamua kuwa alipigwa risasi visivyo halali katika eneo la Kajiado mwaka 2022. Katika sekta ya ardhi, Mahakama ya Mazingira na Ardhi ilitunuku Johannes Akello Omboto Sh5 milioni baada ya ukuta wa mali yake kubomolewa na maafisa waliokuwa wakitekeleza shughuli za Shirika la Reli Kenya bila kufuata taratibu. Mashirika ya umma pia yamejikuta yakilipa mamilioni kutokana na kuvunja mikataba. Hazina ya Taifa ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) iliamriwa kulipa zaidi ya Sh112 milioni kwa kampuni ya Micro-City Computers baada ya kujiondoa katika mkataba wa mfumo wa CCTV ikitaja ukosefu wa fedha. Aidha, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) kiliamriwa kulipa Sh39.9 milioni kwa mkandarasi baada ya kufuta zabuni ya mradi wa Sh799 milioni bila uwazi wa kutosha. Kesi hizi zinaonyesha jinsi maamuzi ya serikali yanavyoweza kuwa na gharama kubwa kwa walipa ushuru. Japo maafisa wanaohusika mara nyingi hawaathiriki binafsi, mzigo wa kulipa fidia na madeni hayo huishia kwa wananchi kupitia fedha za umma.

By Wole Adeshina In the chambers of the 10th Senate, legislative representation is measured by concrete outputs: bills sponsored, motions raised, and physical development brought directly to constituents. On these metrics, Senator Benson Agadaga has established himself as one of the most active lawmakers representing the South-South region. Key Sponsored Bills and Motions Border Communities […]

UCHAGUZI Mkuu wa mwaka 2027 unapokaribia, ushindani wa kumng’oa Rais William Ruto unaonekana kugeuka kuwa vita vya ndani ya upinzani huku vinara wakuu wakisaka vyama vya kisiasa na majukwaa yatakayowawezesha kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania urais. Ingawa viongozi wa upinzani wanakubaliana kwamba serikali ya sasa inapaswa kubadilishwa kupitia kura, bado hawajakubaliana kuhusu nani anayefaa kupeperusha bendera ya muungano wao katika kinyang’anyiro hicho. Miongoni mwa wanaotajwa kuwania uongozi wa upinzani ni aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Martha Karua wa People's Liberation Party, Fred Matiang’i wa Jubilee, Eugene Wamalwa wa DAP-Kenya, Justin Muturi wa Democratic Party, Peter Munya wa PNU na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Kinachoibuka sasa ni ushindani wa kisiasa unaoonyesha kila mmoja wa viongozi hao akitaka kuwa na chama au jukwaa lake kabla ya mazungumzo ya kuunda muungano wa mwisho kufanyika. Huku Kalonzo akijaribu kuimarisha muungano wa Ukombozi Alliance, Sifuna kupitia vuguvugu la Linda Mwananchi anatafuta chombo chake cha kisiasa. Naye Gachagua anaendelea kujenga chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP) huku akiacha mlango wazi kwa mazungumzo na makundi mengine ya upinzani. Katibu Mkuu wa DCP Cleophas Malala amesema wazi kuwa chama hicho hakiko tayari kujiunga na Ukombozi Alliance kwa sasa. Badala yake, amependekeza DCP ishirikiane kwanza na Sifuna kabla ya kuanza mazungumzo na vyama vingine vya upinzani. Kauli hiyo imeonyesha kiwango cha kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa upinzani, ambapo wengi wao wanaonekana kutaka kuhifadhi vyama vyao ili kuongeza uzito wao katika mazungumzo yatakayofuata. Wakati huo huo, Martha Karua na Fred Matiang’i wameendelea kusisitiza kwamba mgombea wa urais wa upinzani hafai kuteuliwa kupitia makubaliano ya viongozi wachache. Badala yake, wanataka kuwepo kwa mchakato ulio wazi, wa haki na unaokubalika kwa washirika wote. Kwa upande wake, Kalonzo ameonekana kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha muundo wa upinzani. Baada ya kugeuza Azimio kuwa Ukombozi Alliance, amekuwa akifanya mikutano ya kisiasa katika maeneo yaliyokuwa ngome za aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Wikiendi hii Kalonzo, Muturi na Wamalwa wamekuwa wakifanya kampeni za pamoja Busia na Siaya. Lakini huku Kalonzo akiimarisha Ukombozi Alliance, kambi ya Sifuna imekuwa ikisaka njia yake ya kisiasa. Hata mvutano uliojitokeza kuhusu matumizi ya jina "Ukombozi" umeonyesha tofauti zinazozidi kujitokeza kati ya makundi hayo mawili. Washirika wa Sifuna sasa wanatazamia kutumia chama cha United Democratic Party (UDP), kilichowahi kuhusishwa na mwanasiasa marehemu Cyrus Jirongo, kama chombo chake cha kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027. Katika mazingira hayo, nafasi ya Gachagua imeendelea kuwa muhimu. Kiongozi huyo amekuwa akisisitiza kuwa yuko tayari kumuunga mkono mwanasiasa yeyote atakayeonyesha uwezo mkubwa wa kumshinda Rais Ruto, hata kama si yeye mwenyewe. Kauli hiyo imebadili kwa kiasi kikubwa mjadala wa kisiasa ndani ya upinzani. Badala ya kusisitiza kuwa lazima aongoze muungano huo, Gachagua amesema mgombea anapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia nguvu za kisiasa na uungwaji mkono wa kitaifa. Hata hivyo, msimamo huo haujaondoa ushindani uliopo. Malala ameendelea kusukuma wazo la ushirikiano kati ya Mlima Kenya na eneo la Mulembe, akisema maeneo hayo yana kura za kutosha kuathiri matokeo ya uchaguzi wa urais. Baadhi ya viongozi kutoka Magharibi mwa Kenya, akiwemo Mbunge wa Bumula Jack Wamboka, wamependekeza Sifuna awe mgombea wa urais huku mgombea mwenza akitoka Mlima Kenya. Hata hivyo, pendekezo hilo linapingana na msimamo wa wafuasi wa Kalonzo ambao wanataka kiongozi huyo wa Wiper apewe tiketi ya urais huku Sifuna akichukua nafasi ya mgombea mwenza. Aidha, aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wanachama wa Jubilee kuanza maandalizi ya uchaguzi wa 2027 mapema na kushirikiana na viongozi vijana ili kuunda muungano mpana wa kisiasa. Wachambuzi wa siasa wanasema changamoto kubwa inayokabili upinzani si kuwakutanisha viongozi wake, bali ni kupata utaratibu wa haki wa kumteua mgombea mmoja anayekubalika kwa wote. Wanasema historia ya siasa za Kenya imeonyesha mara nyingi kuwa miungano mingi huvunjika kutokana na mizozo kuhusu mgombea wa urais, mgombea mwenza na ugavi wa mamlaka. Kwa sasa, upinzani unaonekana kuunganishwa na lengo moja la kumng’oa Rais Ruto. Hata hivyo, ushindani wa ndani kuhusu vyama, miungano na nafasi za uongozi unaendelea kutishia umoja huo huku saa ya uchaguzi wa 2027 ikiendelea kuyoyoma.

IRINGA: KATIBU wa NEC Idara ya Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Matiko Chacha (MCC), amemkabidhi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Salim Abri Asas, tuzo maalumu ya heshima iliyotolewa na CCM Mkoa wa Iringa kwa kutambua mchango wake katika ujenzi na uimarishaji wa Chama. Tuzo hiyo imetolewa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM…

TANGA; WANANCHI wa Tanga wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo Septemba 26, 2026 kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi uliofanyika Viwanja vya Lamore Wilaya ya Tanga. – Mkutano huo ni hitimisho la ziara yake ya siku mbili aliyoianza jana mkoani Tanga kwa…

Approximately 8.5 million children are at risk of failing to reach full development due to challenges related to parenting, nurturing, and early childhood development. This information was released in Dodoma on Friday, September 25, 2026, by the Deputy Permanent Secretary in the Prime Minister’s Office Regional Administration and Local Government (PMO-RALG), Prof Tumaini Nagu. She represented the Minister of State in the PMP-RALG, Prof Riziki Shemdoe, in the closing of the mid-year review meeting on the implementation of the National Integrated Early Childhood Development Programme (NIECDP). Prof Nagu stated that 53 percent of children aged two to four are at risk of failing to reach full development, a condition that could affect their future lives, including earning potential as adults. “Tanzania is estimated to have approximately 16 million children, equal to 27 percent of all Tanzanians. The 2022 TDHS-MIS survey shows that 53 percent of children aged between two and four are at risk of failing to reach their full development,” she said. The Deputy Permanent Secretary noted that this challenge is driven by poverty, low levels of education, inadequate housing for children's needs, and poor availability of care, nurturing, and early development services. According to her, the impacts of failing to meet a child's needs in early stages can persist into adulthood, including reducing average income and increasing the likelihood of perpetuating the cycle of poverty. She stated that investment in early care, nurturing, and development should be prioritised and involve families, communities, the government, and various institutions, using an example from a 2018 World Health Organization (WHO) study showing that every $1 invested in integrated early care and development interventions can yield up to $17. She emphasised that the foundation of good parenting starts within the family, urging parents to cooperate to ensure children get safe environments and services enabling them to reach their potential. On her part, the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Community Development, Gender, Women and Special Groups, Ms Felister Mdemu, said the implementation of the National Development Vision 2050 requires robust investment in early childhood care, nurturing, and development. “Our cooperation should be measured not by the number of meetings we hold, but by the number of children reached, the quality of services they receive, the safety of their environment, and the development they achieve,” said Ms Mdemu. The representative of the Director of the Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN), Mr Lazaro Ernest, stated that no single sector can raise a child alone, as a child involves health, education, nutrition, protection, and social welfare. Mr Lazaro noted that it is vital to have a joint framework enabling various institutions to provide services from a broad perspective. The meeting discussed milestones achieved, existing challenges, and areas requiring strengthening so children receive essential services in early life stages.

KAGERA: KATIBU Tawala wa Wilaya ya Bukoba, Proscovia Mwambi, amesema Manispaa ya Bukoba imetoa mikopo ya zaidi ya Sh milioni 800 kwa vikundi 123 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali bila riba. Amesema vikundi vilivyonufaika ni 68 vya wanawake, 37 vya vijana na tisa…

Chadema national chairman Tundu Lissu has asked the High Court to conclude that the government was not threatened by statements he allegedly made in April 2025, arguing that key government and security officials who could have testified on the matter were not called to give evidence.

WAKAZI wa Samburu wameibua malalamishi baada ya mamia ya ng'ombe, mbuzi na punda kuripotiwa kuuawa wakati wa operesheni ya usalama iliyolenga majangili na kurejesha mifugo iliyoibwa. Operesheni hiyo ilianzishwa kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa na majangili katika mpaka wa Samburu na Isiolo, ambapo maafisa wawili wa Kitengo cha Kupambana na Wizi wa Mifugo (ASTU), polisi mmoja wa akiba na raia wawili waliuawa walipokuwa wakifuatilia mifugo iliyoibwa. Hata hivyo, viongozi na wakazi wa Samburu Mashariki sasa wanasema operesheni hiyo imesababisha hasara kubwa kwa familia zinazotegemea ufugaji kama chanzo kikuu cha maisha.Gavana wa Samburu, Lati Lelelit, alisema ingawa kaunti yake iliunga mkono juhudi za kuimarisha usalama, jinsi operesheni hiyo ilivyotekelezwa ilisababisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na uharibifu wa mali ya wananchi. “Matokeo yamekuwa mabaya sana, yakisababisha ukatili na mauaji ya kiholela ya mifugo ya wananchi,” alisema.Idadi kamili ya mifugo iliyouawa bado inapingwa. Takwimu zilizowasilishwa katika Seneti zinaonyesha kuwa mbuzi 415 na ng'ombe 102 waliuawa katika Wadi ya Waso ndani ya siku tatu. Hata hivyo, Mbunge wa Samburu Mashariki Jackson Lekumontare alisema tathmini yake inaonyesha zaidi ya mbuzi 700, ng'ombe 500 na punda kadhaa waliangamia wakati wa operesheni hiyo. Kwa upande wake, Chama cha Wataalamu wa Samburu kimesema kimeorodhesha angalau wanyama 717 waliouawa, wakiwemo mbuzi 415, ng'ombe 352 na punda 50, huku uchunguzi ukiendelea. Chama hicho kinasema hasara hiyo haihusiani tu na mali bali pia maisha ya familia nyingi zinazotegemea mifugo kwa chakula, elimu ya watoto, huduma za afya na mapato ya kila siku. Tukio hilo lilichochea maandamano katika maeneo ya Samburu Mashariki huku wakazi wakitaka uchunguzi huru ufanywe na familia zilizoathirika zilipwe fidia.Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na mwenzake wa Samburu Lelegwe Ltumbesi pia wameitaka serikali kueleza mazingira yaliyosababisha mauaji hayo ya mifugo. Katibu Mkuu wa Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu cha Samburu, Meshack Ramati, alitaka uchunguzi wa kina ufanywe kubaini idadi ya mifugo iliyouawa, maafisa waliohusika na walioidhinisha operesheni hiyo. “Serikali ina wajibu wa kulinda raia, mali yao na heshima yao. Tunataka uwazi, haki na fidia kwa familia zilizopoteza mifugo yao,” alisema.Wakazi wanasema juhudi za kupambana na ujangili ni muhimu, lakini hazipaswi kufanywa kwa njia inayohatarisha maisha na uchumi wa wananchi wasio na hatia.

MTWARA: WANANCHI mkoani Mtwara wameishukuru Serikali kwa kuanzisha huduma za ardhi kwa njia ya kidijitali, hatua inayowawezesha kupata hati miliki kwa urahisi na kupunguza migogoro ya ardhi. Shukrani hizo zimetolewa wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi Kidijitali uliofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani humo, ambapo wananchi wameelezwa namna ya kutumia mfumo huo kupata…

MTWARA: Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dk. Benson Ndiege, amewataka wakulima wa korosho nchini kuzingatia taratibu sahihi za uvunaji na uhifadhi wa zao hilo ili kulinda ubora wake na kuhakikisha wakulima wanapata bei inayostahili. Dk. Ndiege ametoa wito huo Septemba 25, 2026, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa duka la bidhaa za korosho la Tandahimba…

KIONGOZI wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, wikendi hii anatarajiwa kufanya ziara ya kisiasa katika maeneo ya Nyanza na Magharibi mwa Kenya katika juhudi za kuimarisha azma yake ya kuwania urais mwaka 2027, huku Rais William Ruto akiendelea kuongeza ushawishi wake katika ngome ambazo kwa muda mrefu zilijulikana kuwa za upinzani. Bw Musyoka ataanza ziara hiyo kwa kuzuru Bumala na Nambale katika Kaunti ya Busia leo kabla ya kuelekea Bondo, Kaunti ya Siaya, Jumapili. Akiwa Bondo, atahudhuria ibada katika Kanisa Kuu la St Michael’s All Angels Cathedral na baadaye kufanya mikutano ya kukutana na wananchi. Ziara hiyo inampeleka moja kwa moja katika maeneo ambayo kwa miaka mingi yalikuwa msingi mkuu wa siasa za marehemu Raila Odinga. Pia inafanyika siku chache baada ya Rais Ruto kukamilisha ziara ya siku tano katika eneo la Nyanza, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kujijengea msingi mpya wa kisiasa katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa ngome za ODM na upinzani kwa jumla. Kwa wachanganuzi wa siasa, ziara ya Kalonzo ina umuhimu mkubwa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kiongozi huyo wa Wiper analenga kujenga uhusiano wa moja kwa moja na wapigakura wa Nyanza na Magharibi ambao kwa muda mrefu walimuunga mkono Raila katika kila uchaguzi. Kalonzo alikuwa mshirika wa karibu wa Raila kwa zaidi ya muongo mmoja. Mwaka 2013 alikubali kuweka kando azma yake ya urais na kuwa mgombea mwenza wa Raila kupitia muungano wa Coalition for Reforms and Democracy (CORD). Mwaka 2017 waligombea pamoja tena chini ya muungano wa National Super Alliance (NASA). Katika uchaguzi wa mwaka 2022, Kalonzo alibaki kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa kampeni za Azimio la Umoja One Kenya licha ya Raila kumteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza wake. Uhusiano huo wa muda mrefu ulimfanya Kalonzo kuwa sura inayofahamika sana katika kampeni za Nyanza. Hata hivyo, changamoto kubwa sasa ni jinsi ya kubadilisha urafiki huo wa kisiasa kuwa uungwaji mkono binafsi kutoka kwa wapigakura wa eneo hilo. Changamoto hiyo imekuwa kubwa zaidi kufuatia kifo cha Raila Odinga na mabadiliko ya kisiasa yaliyojitokeza baada yake. Baadhi ya washirika wa zamani wa Raila wameanza kushirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya Kwanza huku wengine wakijaribu kuunda sura mpya ya upinzani. Kwa mujibu wa duru za kisiasa, Kalonzo anategemea ushirikiano wa Gavana wa Siaya James Orengo katika kuimarisha kampeni zake Nyanza. Orengo amebaki mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika eneo hilo licha ya kuhusishwa na vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Ziara za Kalonzo katika Kaunti ya Busia nazo zina umuhimu wa kisiasa. Busia imekuwa sehemu ya maeneo ambayo kwa kawaida huunga mkono vyama vya upinzani. Hata hivyo, katika miezi ya hivi majuzi Rais Ruto ameongeza shughuli zake za kisiasa na maendeleo katika eneo hilo, akiwavutia baadhi ya viongozi wa eneo hilo kuunga mkono ajenda ya serikali. Ziara ya Rais katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay ilijikita katika miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, huduma za maji, masoko, afya na elimu. Wachanganuzi wanasema mkakati huo umemsaidia kujenga taswira ya kiongozi anayelenga maendeleo badala ya siasa za mgawanyiko. Hali hiyo imeweka shinikizo jipya kwa viongozi wa upinzani ambao sasa wanapaswa kushindana si tu na ushawishi wa kisiasa wa Rais Ruto bali pia na mvuto wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali. Kwa upande mwingine, Kalonzo anaonekana kuwekeza zaidi katika siasa za mashinani na kujenga muungano mpya wa upinzani. Hatua hizi zinajiri baada ya muungano wa Azimio la Umoja kubadilishwa jina na kuitwa Ukombozi Alliance. Kalonzo amesema mabadiliko hayo ni sehemu ya mkakati wa kujiandaa mapema kwa uchaguzi wa mwaka 2027. Pia amekuwa akifanya mazungumzo na viongozi wengine wa upinzani akiwemo Justin Muturi, Eugene Wamalwa na Lenny Kivuti kuhusu mfumo bora wa kuunganisha upinzani. Hata hivyo, hesabu za kisiasa ndani ya upinzani zimeendelea kuwa tata kutokana na azma ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuwania urais kupitia chama chake cha Democracy for the Citizens Party (DCP). Kauli za viongozi wa DCP zimeonyesha kuwa bado kuna tofauti kuhusu jinsi muungano mpana wa upinzani utakavyoundwa. Kwa sasa, Kalonzo anakabiliwa na jukumu la kuthibitisha kuwa mvuto wake wa kisiasa unaweza kuvuka mipaka ya Ukambani na kupata uungwaji mkono katika maeneo yaliyokuwa ngome za Raila. Ziara yake ya Bondo inachukuliwa kuwa moja ya majaribio muhimu zaidi ya kupima uwezo wake wa kuvutia wapigakura wa Nyanza.

ARUSHA: KUIMARISHA tafiti za kitaaluma na kutumia matokeo yake kutatua changamoto zinazoikabili jamii ni miongoni mwa malengo ya Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI). Uimarishaji wa tafiti hizo umeelezwa kupitia programu mpya za shahada za uzamivu katika Usimamizi wa Biashara (DBA) na Uzamivu wa Falsafa (PhD). Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Profesa Peter…

Wakazi wa maeneo yanayokumbwa na hatari ya mafuriko jijini Nairobi wanakabiliwa na changamoto kubwa huku serikali ikiendelea kuwaonya kuondoka katika maeneo hayo kabla ya mvua ya El Niño inayotarajiwa kuanza kunyesha mwishoni mwa mwaka. Kwa wengi wao, swali kuu si kama wanapaswa kuhama, bali watahamia wapi. Esther Makhokha, mkazi wa Mukuru Kayaba, bado anakumbuka mafuriko ya Machi mwaka huu. Anasema jioni moja mvua iliponyesha kwa nguvu, maji yalianza kuingia katika nyumba yake huku yeye na dada zake wawili wakitayarisha chakula. Kwa kukosa muda wa kufanya maamuzi, walichukua watoto na kuwapeleka katika baa iliyokuwa karibu ambayo haikuwa imezingirwa na maji. Baadaye, yeye na dada yake walilala kwa jirani wakisubiri maji yapungue. “Nililazimika kukimbia na watoto na kulala sakafuni kwa jirani. Sitaki kupitia hali hiyo tena,” alisema. Makhokha, ambaye amekulia Mukuru Kayaba tangu utotoni, anasema hana mahali pengine pa kwenda iwapo mafuriko yatatokea tena. “Hata wakiniambia nihame, sina mahali pa kwenda. Sina pesa za kuhamia sehemu nyingine. Hapa ndipo nimeishi maisha yangu yote,” alisema. Anasema wakati wa mafuriko yaliyopita hakupata usaidizi kutoka kwa serikali ya kaunti. Badala yake, waandishi wa habari walioenda kuripoti tukio hilo walimsaidia kwa chakula, mavazi, godoro na nepi za watoto. Mkazi mwingine wa Mukuru Kayaba, Immaculate Wavinya, anakabiliwa na changamoto sawa. Mama huyo anayelea mtoto peke yake amesema amehudhuria mikutano kadhaa ambapo wakazi wamehimizwa kuhama kutoka maeneo yanayokumbwa na mafuriko. Hata hivyo, anasema ushauri huo haujatiwa nguvu na msaada wa kuwawezesha wananchi kuhamia maeneo salama. “Familia yangu iko hapa. Biashara yangu iko hapa. Nimemlea mtoto wangu hapa tangu mwaka 2015. Nikiambiwa nihame, niende wapi na kwa pesa gani?” alihoji. Kulingana naye, wakazi wengi hawajaona juhudi za kutosha za serikali kuwasaidia kuhama. Katika eneo la Nairobi Dam karibu na Highrise, Ruth Mwikali pia anahofia mvua inayotarajiwa. Anasema amesikia onyo kuhusu El Niño lakini hajapewa mwongozo wa wazi kuhusu mahali pa kwenda iwapo makazi yao yatazingirwa na maji. Wasiwasi wa wakazi hawa unajiri huku serikali ya Kaunti ya Nairobi ikisema imeongeza maandalizi ya kukabiliana na mafuriko. Gavana Johnson Sakaja amesema maeneo kama Mukuru, Kibra, Mathare na sehemu za Ruaraka ni miongoni mwa maeneo ambayo huathiriwa mara kwa mara wakati mvua kubwa inapozidi uwezo wa mitaro ya kuondoa maji. Kaunti imesema inaendelea kusafisha, kupanua na kuchimba zaidi mitaro ya maji katika zaidi ya maeneo 36 yanayokumbwa na mafuriko. Pia imeanzisha vituo 27 vya uokoaji na makazi ya muda kwa watu watakaolazimika kuhama. Hata hivyo, kwa wakazi wengi wa mitaa ya mabanda, maandalizi hayo hayajibu swali lao kuu. “Hauwezi kuwaambia watu wahame bila kuwaonyesha mahali pa kwenda,” alisema Mzee Francis Kaviti wa Mukuru Kayaba.

Kadri watu wengi wanavyotumia mitandao na apu za kutafuta wachumba, ndivyo matapeli wa kimapenzi wanavyozidi kuwanasa waathiriwa wao. Utafiti wa TransUnion unaonyesha kuwa karibu Wakenya watatu kati ya kumi wanaotumia apu za uchumba mtandaoni wamewahi kukumbana na jaribio la ulaghai. Zaidi ya asilimia 80 ya Wakenya pia wanasema wamewahi kulengwa na walaghai wa kidijitali kupitia simu zao. Mtaalamu wa usalama wa mitandao na mshirika wa kampuni ya Techrise, Polycap Oliver Oluoch Ochieng, anasema ishara ya kwanza ya tahadhari ni mtu kuharakisha mapenzi. “Ikiwa mtu anaanza kukutamkia mapenzi ndani ya siku chache kabla hata ya mawasiliano ya kawaida kama simu ya video, hilo ni jambo la kutiliwa shaka,” anasema. Pia anaonya kuhusu watu wanaokwepa mawasiliano ya video au mikutano ya ana kwa ana kwa kutoa visingizio mbalimbali kama kamera kuharibika au kuwa mbali kikazi. Kwa mujibu wake, matapeli mara nyingi hutumia picha za kuvutia zilizoibwa mitandaoni na hujenga wasifu unaoonekana mkamilifu kupita kiasi. “Mfano ni mtu kuchapisha picha za kitaalamu pekee bila picha za kawaida akiwa na marafiki au familia. Hiyo ni ishara ya tahadhari,” anasema. Anashauri watumiaji kufanya uchunguzi wa picha mtandaoni ili kubaini iwapo zimeibwa kutoka kwa wanamitindo au watu maarufu. Mtaalamu huyo pia anatahadharisha kuhusu watu wanaoharakisha kuhamisha mazungumzo kutoka apu za uchumba hadi WhatsApp au Telegram ambako ni vigumu kufuatilia ulaghai. Kwa kawaida, matapeli huanza kwa kuomba kiasi kidogo cha pesa kama vocha ya simu au mkopo mdogo. Baada ya kuona mwathiriwa yuko tayari kusaidia, huanza kuomba fedha nyingi zaidi kwa madai ya dharura za hospitali, usafiri au uwekezaji. “Ikiwa mtu anaomba pesa kwa sababu yoyote ile, huo ni wakati wa kusitisha mawasiliano,” anasema Oluoch. Mshauri wa masuala ya mahusiano Benjamin Zulu anasema watu wanaotafuta mapenzi mtandaoni hawapaswi kutegemea mawasiliano ya mtandaoni pekee. “Mtandao unaweza kuwa sehemu ya kukutana, lakini uhusiano wa kweli hujengwa kupitia mawasiliano ya ana kwa ana,” anasema. Zulu anaongeza kuwa mtu anayekwepa kukutana ana kwa ana huenda ana jambo la kuficha. Pia anawahimiza watu kutotoa taarifa za kibinafsi kama anwani ya nyumbani, nambari ya kitambulisho au hali zao za kifedha kabla ya kuwa na imani kamili kwa mtu huyo. Anashauri watu kuwa waangalifu hasa wanapopitia maumivu ya moyo au upweke, kwani hali hiyo huwafanya kuwa rahisi kudanganywa. Kwa maoni yake, mapenzi ya kweli hayapaswi kuhusisha maombi ya pesa. “Usichukue mkopo wala kutumia akiba yako kumsaidia mtu uliyekutana naye mtandaoni,” anasema. Wataalamu wanashauri watu kufanya simu za video kabla ya kuwekeza hisia zao, kuchagua maeneo ya wazi wanapokutana kwa mara ya kwanza na kuwafahamisha marafiki au jamaa kuhusu mahali walipo. Aidha, yeyote anayeshuku ulaghai anaweza kuripoti kwa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kupitia nambari ya bure 0800 722 203 au kwa simu za dharura za polisi 999, 911 au 112.

HUKU Kenya ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027, wasiwasi unazidi kuongezeka kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa ghasia za kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini. Wiki za hivi majuzi zimeshuhudia visa vya vurugu katika mikutano ya kisiasa huko Homa Bay, Embu na Garissa, hali ambayo imeibua hofu kuwa siasa za ushindani huenda zikachochea ukosefu wa usalama kama ilivyoshuhudiwa katika chaguzi zilizopita. Mashambulizi dhidi ya viongozi wa muungano wa Linda Mwananchi mjini Homa Bay na vurugu zilizoripotiwa katika mkutano wa kisiasa Nembure, Embu, ni baadhi ya matukio ambayo yamefanya hali ya kisiasa nchini kuwa katika hali ya taharuki. Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, na washirika wake pia walilazimika kuondoka haraka Garissa baada ya kukumbana na mazingira yaliyotishia usalama wao. Kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR), watu wasiopungua 11 wamepoteza maisha tangu Februari mwaka huu kutokana na matukio yanayohusishwa na mikutano ya kisiasa nchini. Tume hiyo imeonya kuwa mivutano inayoshuhudiwa katika maeneo kama mpaka wa Turkana na West Pokot, Isiolo, Embu na kaunti nyingine ni ishara ya hatari inayopaswa kushughulikiwa mapema kabla ya uchaguzi. “Tunahitaji kulinda haki za msingi kabla hazijakiukwa, si baada ya madhara kutokea,” ilisema KNCHR ikitaka uchunguzi wa kina kufanywa kuhusu visa vyote vya vurugu. Kwa upande wake, Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) imezidi kuwaonya wanasiasa dhidi ya matumizi ya lugha za uchochezi na kuajiri vijana kutekeleza mashambulizi dhidi ya wapinzani wao. Mwenyekiti wa NCIC, Kepha Nyamweya Omae, alisema vijana wanapaswa kushirikishwa katika demokrasia kwa njia halali badala ya kutumiwa kama silaha za kisiasa. Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema maeneo hatari ya ghasia za uchaguzi nchini yamebakia karibu yale yale kwa miaka mingi. Mtaalamu George Musamali anasema Nairobi, sehemu za Bonde la Ufa, Mombasa, Homa Bay, Migori, Kisii na Kiambu zinaendelea kuonekana kuwa maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kushuhudia vurugu. Maeneo yaliyotajwa mara kwa mara kama yenye uwezekano mkubwa wa kushuhudia ghasia za kisiasa ni Nairobi, Nakuru, Kericho, Kisumu, Uasin Gishu, Mombasa, Homa Bay, Migori, Kisii, Kiambu, sehemu za Bonde la Ufa, Turkana-West Pokot, Isiolo, Embu, Kitengela, Bungoma, Kakamega, Nandi na Marsabit. Haya ni maeneo yaliyotambuliwa kutokana na historia ya vurugu za uchaguzi, mivutano ya kisiasa, migogoro ya ardhi, tofauti za kikabila na ushindani wa kisiasa. “Kila uchaguzi tangu mfumo wa vyama vingi urejee mwaka 1992 umeshuhudia aina fulani ya ghasia. Mara nyingi maeneo hayo hubakia yale yale kwa sababu siasa zetu zimejengwa kwenye misingi ya kikabila,” alisema Bw Musamali. Aidha, ameonya kuhusu kuibuka kwa makundi ya vijana wanaotumiwa na wanasiasa kuvuruga mikutano ya wapinzani na kuzua hofu miongoni mwa wapiga kura. Ripoti mbalimbali zimeonyesha kuwa ghasia za uchaguzi nchini mara nyingi huchochewa na mchanganyiko wa siasa za kikabila, migogoro ya ardhi, malalamishi ya kihistoria na ukosefu wa usawa katika ugavi wa rasilimali za umma. Mwanaharakati wa haki za binadamu Ernest Cornel anaeleza kuwa vurugu zinaweza kutokea kati ya jamii tofauti au hata ndani ya jamii moja kulingana na maslahi ya kisiasa na kijamii yanayokinzana. “Kuna maeneo ambapo migogoro ya ardhi na mipaka imeendelea kwa muda mrefu. Siasa zinapoingilia kati, baadhi ya watu huona kama fursa ya kulipiza kisasi,” alisema. Takwimu zinaonyesha kuwa ghasia za uchaguzi wa 2007/2008 zilisababisha vifo vya takriban watu 1,300 na kuwafanya zaidi ya watu 650,000 kuhama makazi yao. Ingawa Kenya imepiga hatua kubwa tangu wakati huo, wataalamu wanaonya kuwa dalili zinazoonekana sasa zinafanana na zile zilizotangulia migogoro ya zamani. Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga pia ameonya kuhusu umuhimu wa kuwa na Idara za usalama ambazo haziegemei upande wowote, akisema upendeleo wa kisiasa ndani ya taasisi za usalama unaweza kutumbukiza nchi katika machafuko. Kampeni za uchaguzi zinapoanza kushika kasi, wadau wa kisiasa, asasi za kiraia na idara za usalama wanahimizwa kushirikiana ili kuzuia kurejea kwa historia ya vurugu. Swali kuu sasa ni iwapo Kenya itazingatia ishara hizi za tahadhari au itasubiri hadi madhara yatokee tena.

"More importantly, Section 132 criminalises the use or threat of force, violence or restraint, as well as threats of injury, damage or harm intended to influence how a person votes"

TANGA; Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na uhai na utekelezaji wa shughuli za chama Mkoa wa Tanga kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya chama na serikali umesaidia kurahisisha upelekaji wa maendeleo kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi katika ziara yake mkoani Tanga…

Huzuni imetanda katika kijiji cha Noonkpoir, Kitengela, Kaunti ya Kajiado, baada ya watu watatu kufariki dunia na wengine wawili kulazwa hospitali wakiwa mahututi kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa pombe haramu. Mnamo Ijumaa asubuhi, Christine na jamaa zake waliomboleza kifo cha mumewe, James Maina Nguru, aliyefariki Jumatatu usiku baada ya kunywa pombe hiyo. Kwa mujibu wa wakazi, waathiriwa hao walikunywa pombe hiyo katika eneo la Migingo jioni ya Jumatatu kabla ya kufariki nyakati tofauti karibu na makazi yao. Migingo, eneo lililoko Kitengela, limekuwa likihusishwa kwa miaka kadhaa na biashara ya pombe haramu, dawa za kulevya na uhalifu. Bi Mukeira alisema mumewe, aliyekuwa fundi na baba wa watoto watatu, alirejea nyumbani akiwa katika hali mbaya baada ya kutoka kwenye baa maarufu eneo hilo. “Alikuwa akilalamika maumivu makali ya tumbo na hakuweza kusimama vizuri. Muda mfupi baadaye alianza kutapika damu na akafariki mbele yetu,” alisema kwa huzuni. Sasa mjane huyo anasema amelazimika kulea watoto wao peke yake. Familia hiyo imeamua kutofanya uchunguzi wa maiti kutokana na hali ngumu ya kifedha na imani kuwa pombe ndiyo iliyosababisha kifo chake. Mama yake Nguru, Mary Muthoni, ameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara wanaosambaza pombe hatari. Alisema mara nyingi alimuonya mwanawe kuhusu madhara ya pombe lakini hakumsikiliza. Katika eneo hilo hilo, Lynette Sirengo pia anaomboleza kifo cha mumewe, Godfrey Simiyu Kiliswa, aliyefariki baada ya kupatikana akiwa hajitambui karibu na baa inayojulikana kama “Kwa Omosh”. Alifariki siku iliyofuata nyumbani kwake. Mwanaume mwingine, Elisha Okello, naye alifariki baada ya kurejea nyumbani akiwa amelewa. Mwili wake ulipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Kitengela. Wakati huo huo, ndugu wa mmoja wa manusura amesema mgonjwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi akiwa katika hali mahututi, huku viungo vya ndani vikidaiwa kuathiriwa vibaya. Wakazi wamewalaumu maafisa wa usalama kwa kushindwa kudhibiti uuzaji wa pombe haramu, madai ambayo polisi wamekanusha wakisema wameimarisha msako dhidi ya wauzaji wa vileo haramu na dawa za kulevya. Serikali pia imeagiza operesheni kali kote nchini kukabiliana na biashara hiyo inayozidi kuhatarisha maisha ya wananchi

MBUNGE wa Saboti, Caleb Amisi, amesema kiti cha chini kabisa ambacho kiongozi wa Jubilee, Dkt Fred Matiang'i, anaweza kukubali katika muungano wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 ni Unaibu Rais, kama si tiketi ya kuwania urais yenyewe. Amisi alisema hayo alipozuru kaunti ya Kisii mnamo Alhamisi, Septemba 24, kuwa ni kudhalilisha kumzungumzia Matiang'i kwa vyeo vya chini kama Uwaziri, akisema aliyekuwa Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ameshavuka kiwango hicho. "Mtu kama Fred Matiang'i, kiti cha chini kabisa anachoweza kupewa ni Unaibu wa Rais. Kama si hivyo, basi apewe tiketi ya Urais. Hatuwezi kumzungumzia tena kama mtu wa kupewa Wizara. Amepita hapo," Amisi alisema. Mbunge huyo alikuwa Kisii kukipigia debe chama chake kipya cha People's Renaissance Movement (PRM) na kujenga uungwaji mkono wa Dkt Matiang'i katika eneo la Gusii. Kwenye ziara yake, Amisi alikutana na makundi ya vijana na kina mama katika mikutano ya hoteli na ya barabarani maeneo ya Keumbu na Kisii Mjini, ambako alielezea dira ya chama chake na msimamo wake kuhusu mustakabala wa upinzani. Alisema upinzani unapojipanga kumkabili Rais William Ruto, lazima uonyeshe heshima kwa viongozi wenye uzito wa kitaifa kama Dkt Matiang'i. "Kuna tabia ndani ya upinzani ya kutaka kumpunguza Matiang'i hadi nafasi ya uwaziri. Hiyo ni dharau kubwa. Mtu aliyesimamia wizara kubwa kama Mambo ya Ndani na Elimu, akaonyesha uwezo wa kipekee, si mtu wa kupewa tena nafasi ya waziri. Ameshavuka hapo," alisema Amisi. Aliongeza kuwa Matiang'i ndiye kiongozi anayefaa zaidi kuongoza muungano wa upinzani kutokana na uzoefu wake serikalini na mtindo wake wa uongozi unaoaminika. "Ukizungumzia viongozi ambao wamewahi kuendesha serikali kwa msimamo na nidhamu, Matiang'i yuko juu. Ndiyo maana tunasema kama hatutampatia urais, basi angalau tumpatie unaibu. Chini ya hapo ni kumkosea heshima jamii nzima ya Gusii na Wakenya wanaomuamini," alisisitiza. Amisi alisema chama chake cha PRM kimejipanga kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuimarisha umoja wa vijana na kina mama ambao ndio wamekuwa wakisahaulika licha ya kuwa na kura nyingi. Alisema jamii ya Gusii imekuwa na mchango mkubwa katika siasa za taifa lakini imekuwa ikipata nafasi ndogo katika uongozi wa juu, na wakati huu inastahili kupata nafasi kubwa kupitia Matiang'i. "Gusii imekuwa na kura, imekuwa na viongozi wazuri, lakini haijawahi kupata nafasi ya juu. Wakati huu msikubali makombo. Lazima muwe mezani, na njia ya kuwa mezani ni kumpa Matiang'i tiketi ya juu," alisema. Kauli ya Amisi inakuja wakati viongozi wa upinzani wakiendelea na mazungumzo ya kuunda umoja mpana wa kumkabili Rais Ruto, huku mgawanyo wa nafasi ukiwa kitovu cha mvutano.

Mpango wa Rais William Ruto wa nyumba za bei nafuu umepata nguvu kubwa baada ya Mahakama ya Rufaa kuidhinisha sheria ya makazi nafuu na ushuru wa nyumba, huku ikitupilia mbali kesi 42 zilizopinga sheria hiyo. Katika uamuzi wake, jopo la majaji watano lilisema Sheria ya Makazi Nafuu ilitungwa ili kutekeleza haki ya kila Mkenya kupata makazi bora na ya kutosha kama ilivyo katika Katiba. Mahakama ilikataa hoja za waliowasilisha kesi wakitaka sheria hiyo itangazwe kuwa batili na serikali iamriwe kurejesha mabilioni ya pesa ilizokusanywa kupitia ushuru huo kutoka kwa waajiri na wafanyakazi. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mwajiri na mfanyakazi huchangia kila mmoja asilimia 1.5 ya mshahara wa mfanyakazi kila mwezi kwa Hazina ya Makazi Nafuu. Waliopinga sheria hiyo, akiwemo daktari wa upasuaji kutoka Nakuru, Magare Gikenyi, walidai ushuru huo unawalazimisha Wakenya kugharamia nyumba ambazo huenda wasinufaike nazo kamwe. Pia walidai kuwa jukumu la makazi ni la serikali za kaunti na kwamba serikali kuu ilikiuka Katiba kwa kulitwaa. Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa ilisema makazi ni jukumu kati ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti, hivyo sheria hiyo haikiuki mfumo wa ugatuzi. Majaji waliongeza kuwa ushuru huo hauwezi kutajwa kama ubaguzi au unyakuzi haramu wa mali kwa kuwa serikali ina mamlaka ya kuweka kodi ili kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Hata hivyo, mahakama ilionya kuwa mpango huo unapaswa kuhakikisha pia unawanufaisha Wakenya maskini zaidi na usitumike kuwanufaisha washirika wa kisiasa au watu wenye ushawishi pekee. Uamuzi huo unaimarisha moja ya miradi mikuu ya Rais Ruto inayolenga kuongeza upatikanaji wa nyumba nafuu nchini.

ARUSHA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amezitaka nchi za Afrika kutumia changamoto za mabadiliko ya tabianchi kuibua ubunifu, utafiti na maendeleo badala ya kujiona waathirika pekee. Masauni ametoa wito huo jijini Arusha wakati akifunga Kongamano la Vyuo Vikuu Vitano lililofanyika katika Taasisi ya Afrika ya…

KIGOMA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma kimezitaka halmashauri za mkoa huo kushughulikia changamoto zinazokwamisha miradi ya maendeleo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi licha ya kukamilika kwa baadhi ya majengo. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Jamal Tamim, wakati akiongoza Kamati ya Siasa ya chama hicho kukagua miradi…

DIWANI wa Wadi ya Nairobi South, Waithera Chege, amesema rekodi ya maendeleo ya Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja haimruhusu kuwania muhula wa pili 2027. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa eneo la South B, Bi Chege alidai kuwa uongozi wa Gavana Sakaja umeshindwa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2022. Alisema baadhi ya maeneo ya Nairobi hayajanufaika kikamilifu na miradi ya maendeleo, akidai kuwa hali hiyo imeathiri zaidi wadi zinazowakilishwa na madiwani wanaokosoa utawala wa Gavana Sakaja. “Uongozi wa Sakaja umeshindwa kutumikia wananchi. Nairobi imekosa baadhi ya huduma muhimu za ugatuzi, hali ambayo imelazimu Serikali ya Kitaifa kuingilia kati na kutekeleza miradi ambayo inapaswa kufanywa na Serikali ya Kaunti,” alisema Bi Chege. Alitoa wito kwa chama cha UDA kutafuta mgombea mwingine wa ugavana wa Nairobi iwapo kinataka kuhifadhi kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa 2027. Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Alex Wachira, pia aliwataka wakazi kumuunga mkono Rais William Ruto kwa muhula wa pili. Bw Wachira alisema Rais anafaa kupewa nafasi ya kukamilisha miradi aliyoanzisha katika muhula wake wa kwanza. Alitaja marais wa zamani Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta, ambao walihudumu kwa mihula miwili, akisema Rais Ruto pia anapaswa kupewa nafasi kama hiyo.

DAR ES SaLAAM: SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewasihi wahandisi na watumiaji wa bidhaa na malighafi za ujenzi kutumia huduma ya upimaji wa hiari ili kujiridhisha na ubora wa bidhaa hizo kabla ya kuzitumia katika miradi ya ujenzi. Yona Afrika kutoka TBS ametoa wito huo leo Septemba 25, 2026 wakati wa Maonesho ya Wahandisi yaliyofanyika…

DAR ES SALAAM: BINTI aliyebuni na kutengeneza ndege nyuki (drone), Tarsila Mellita, amepokea Sh milioni 20 kutoka kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, fedha zilizowasilishwa na Msaidizi wa Rais Maendeleo ya Jamii, Jacqueline Kawishe. Fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Dk Samia wakati wa kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya…

Raia 49 wa Kenya ni miongoni mwa maelfu ya watu walio katika orodha mpya ya wanaosubiri taratibu za kufurushwa kutoka Amerika. Majina na picha za Wakenya hao zimechapishwa hadharani kama sehemu ya msako mpana wa maafisa wa Amerika dhidi ya wahamiaji wanaokiuka sheria za uhamiaji. Idara ya Usalama wa Taifa ya Amerika (DHS) imechapisha hifadhidata maarufu inayoorodhesha raia 125 kutoka Afrika wanaosubiri kuondolewa nchini humo katika siku zijazo, huku Wakenya 49 wakiongoza orodha hiyo ikiwa idadi kubwa zaidi kutoka taifa moja. DHS imepanua hifadhidata yake inayojulikana kama “Wabaya zaidi”, inayolenga watu wasiokuwa raia wa Amerika walio na rekodi za uhalifu na wanaotafutwa kuzuiliwa na kufurushwa kutoka nchi hiyo. Ingawa orodha ya awali au utekelezaji wa mpango huo katika maeneo tofauti ilikuwa na idadi ndogo ya Wakenya, kama vile watu 15 au 45, ripoti za hivi majuzi zinaonyesha kuwa Wakenya 49 sasa wako katika kampeni mpya ya utekelezaji wa sheria za uhamiaji. Kulingana na takwimu za Shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Sheria za Forodha la Amerika (ICE), raia 1,282 wa Kenya wako kwenye orodha ya watu ambao wana maagizo ya mwisho ya kuondolewa nchini lakini hawajazuiliwa. Wakenya hao ni sehemu ya orodha inayojumuisha zaidi ya watu milioni 1.4 wasio raia wa Amerika kutoka mataifa 187 duniani. Takwimu hizo zinaonyesha kuimarishwa kwa hatua za utekelezaji wa sheria za uhamiaji nchini Amerika, hali ambayo imezua wasiwasi mkubwa na changamoto za kisheria miongoni mwa jamii ya Wakenya wanaoishi nchini humo. Mbali na kundi hilo la watu ambao hawajazuiliwa, kuna idadi ndogo ya Wakenya waliohukumiwa kwa makosa makubwa ya jinai ambao wamewekwa katika orodha maalum za DHS za watu wanaopewa kipaumbele katika hatua za kufurushwa. Wakenya wanaongoza orodha hiyo kwa watu 49, wakifuatwa na raia 44 wa Ghana. Aidha, taarifa nyingine ya DHS inaonyesha kuwa raia 112 wa Nigeria 112 pia wanasubiri kufurushwa kutoka Amerika. Mauritania ina watu 12 kwenye orodha hiyo, Morocco 11 huku Afrika Kusini ikiwa na watu tisa.

Kiongozi wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) na aliyekuwa Waziri wa Haki nchini Kenya, Martha Karua, amewasilisha kesi katika mahakama ya Uganda akitaka kubatilishwa kwa uamuzi wa kufurushwa kwake nchini humo na kuruhusiwa kurejea ili kumwakilisha kiongozi wa upinzani, Dkt Kizza Besigye, na mshtakiwa mwenzake. Besigye aliyekamatwa akiwa Nairobi Nairobi mwaka 2024 anakabiliwa na kesi ya uhaini. Bi Karua, kwa ushirikiano na Chama cha Wanasheria cha Uganda (Uganda Law Society), wanapinga uamuzi uliotolewa Juni 22 na Afisa Mkuu wa Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe wa kumzuia kuingia nchini Uganda na kutangaza kuwa mtu asiyehitajika nchini humo. Wanasema uamuzi huo ulikuwa kinyume cha sheria na ulifanywa bila kumpa nafasi ya kujitetea au kusikilizwa. Kupitia Kitengo cha Malalamishi cha Mahakama Kuu mjini Kampala, Karua anataka mahakama ibatilishe uamuzi huo na kuzuia maafisa wa uhamiaji kuingilia haki yake ya kuingia Uganda ili kutekeleza majukumu yake ya kitaaluma kama wakili. Katika hati zake za kesi, Karua anaeleza kuwa alisafiri kwenda Uganda Juni 22 ili kuwakilisha Dkt Besigye na Hajj Obeid Lutale baada ya kupata Cheti Maalum cha Uwakili kilichomruhusu kufanya kazi katika mahakama za Uganda. Anasema maafisa wa uhamiaji walimzuia kuingia nchini humo, wakachukua simu zake na baadaye wakampatia notisi ya kumtaka arejee Kenya. Dkt Besigye na Bw Lutale walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini na makosa mawili ya kuficha taarifa kuhusu uhaini. Upande wa mashtaka unadai walihusika katika njama za kupindua serikali ya Uganda. Mashtaka hayo yalitokana na kukamatwa kwa wawili hao jijini Nairobi mnamo Novemba 2024. Awali walifikishwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi ya Uganda kabla ya kuhamishiwa mahakama za kiraia kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu uliosema kuwa raia hawawezi kushtakiwa katika mahakama za kijeshi. Baadaye walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkuu ya Nakawa mnamo Februari 21, 2025. Hatua ya Karua kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Uganda kutokana na vitendo vya maafisa wa uhamiaji imefuatia ombi la awali lililowasilishwa na Dkt Besigye na Bw Lutale kuhusu suala hilo hilo. Mahakama Kuu ilikataa kuamua iwapo uamuzi wa uhamiaji ulikuwa halali, ikisema kuwa changamoto hiyo ilipaswa kuwasilishwa kupitia mchakato wa mapitio ya mahakama, na hivyo ikatupilia mbali ombi hilo. Karua na Chama cha Wanasheria cha Uganda wanataka mahakama itangaze kuwa uamuzi huo ulikuwa haramu, wa kiholela, usio na sababu za msingi na uliofanywa kinyume cha taratibu zinazotakiwa kisheria. Pia wanataka mahakama iubatilishe, kuagiza mamlaka za uhamiaji kutathmini upya suala hilo, na kutoa amri ya kudumu ya kutomzuia kuingia Uganda kwa madhumuni ya kitaaluma. “Uamuzi huo ni haramu, hauna mantiki na ulifanywa kinyume cha taratibu zinazotakiwa na sheria,” walisema. Katika kiapo chake cha kuunga mkono kesi hiyo, makamu wa rais wa Chama cha Wanasheria cha Uganda, Anthony Asiimwe, alisema Karua ni Wakili Mkuu na anamiliki Cheti Maalum cha Uwakili kilichotolewa chini ya Kifungu cha 18 cha Sheria ya Mawakili. Alisema cheti hicho kilimruhusu kuongoza timu ya utetezi katika kesi inayowahusu Besigye na Lutale. Asiimwe alieleza kuwa alisafiri hadi Entebbe kumpokea Karua baada ya kuwasili kutoka Kenya, lakini akakuta maafisa wa uhamiaji tayari wamemzuia kuingia nchini. Walalamishi hao wanasisitiza kwamba Karua hakupatiwa nafasi ya kusikilizwa wala sababu zinazokidhi kanuni za haki za asili kabla ya uamuzi huo kufanywa. Wanasema hatua hiyo ilikiuka Katiba ya Uganda, Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pamoja na misingi inayolinda uhuru wa taaluma ya sheria. Kwa mujibu wao, Karua amepata hasara kitaaluma na kifedha kwa sababu hawezi kurejea Uganda kutekeleza majukumu yake. “Mlalamishi wa pili ameendelea kupata madhara makubwa ya kitaaluma na jina lake kuharibiwa baada ya kutangazwa hadharani kuwa ‘ mtu asiyetakiwa’ bila msingi wowote wa kisheria,” alisema Asiimwe. Kabla ya kuwasilisha kesi hiyo, Chama cha Wanasheria cha Uganda kilijaribu kutafuta suluhu kupitia njia za kiutawala. Barua zilizoambatishwa katika kesi zinaonyesha kuwa chama hicho kiliwaomba maafisa wa Uganda kufuta uamuzi huo na kumruhusu Karua kuingia nchini. Hadi sasa, Mwanasheria Mkuu wa Uganda hajawasilisha majibu kuhusu madai yaliyomo katika kesi hiyo mpya.

ZAWADI ya gari jipya aina ya Toyota Prado TX lililotolewa na Rais William Ruto kwa mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Luo, Ker Odungi Randa, imeibua mjadala mkali wa kisiasa katika eneo la Nyanza. Gari hilo la thamani ya mamilioni lilifikishwa nyumbani kwa Bw Randa katika eneo la Boya na maafisa kutoka afisi ya Katibu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, siku chache baada ya kiongozi huyo wa kitamaduni kumuomba Rais msaada wa usafiri wakati wa ziara yake katika eneo hilo. Kwa mujibu wa taarifa, ombi hilo lilitolewa wakati wa mkutano uliofanyika Homa Bay, ambapo Rais aliahidi kulitekeleza. Afisa kutoka afisi ya Dkt Omollo, Bw Charles Osako, alisema Rais alitimiza ahadi yake kwa Baraza la Wazee wa Luo na kwamba gari hilo litasaidia shughuli na majukumu ya wazee hao. “Gari hili linaonyesha kutambuliwa kwa mchango muhimu wa wazee na viongozi wa kitamaduni katika kuhifadhi maadili, mila na utambulisho wetu,” alisema Bw Osako. Mbunge wa Lang’ata, Phelix Jalango Odiwuor, ambaye alishuhudia mazungumzo hayo, alisema baada ya mkutano wa mwisho wa hadhara Migori, Dkt Omollo alimwalika kuhudhuria kikao kati ya Rais na viongozi wa Baraza la Wazee wa Luo. Alisema mwishoni mwa mkutano huo, Bw Randa alimuomba Rais amsaidie kupata gari la kurahisisha shughuli zake za kila siku. “Kwa utulivu, Rais alimwambia angepata gari Ijumaa. Leo asubuhi timu ya Dkt Omollo imekabidhi gari hilo jipya aina ya Toyota Prado,” alisema Bw Odiwuor baada ya gari kuwasilishwa. Bw Randa alipokea funguo za gari hilo na kulijaribu kabla ya kurejea nyumbani kwake. “Nashukuru Rais Ruto kwa zawadi hii. Itanisaidia kusafiri na kukutana na Waluo walioko Nairobi, Mombasa, Uganda, Tanzania na maeneo mengine mengi,” alisema. Hata hivyo, zawadi hiyo imezua maswali kuhusu uhuru wa Baraza la Wazee wa Luo, ambalo kwa kawaida halifai kuzingatia siasa za vyama na linatarajiwa kuwa sauti ya maridhiano katika jamii. Wakosoaji wanasema kupokea gari kutoka kwa Rais kunaweza kuathiri msimamo wa baraza hilo, hasa wakati ushindani wa kisiasa kati ya vyama vya UDA na ODM unaendelea kushika kasi Nyanza. Mkazi wa Kisumu, Bw Martin Oria, alihoji jinsi baraza hilo litakavyodumisha kutopendelea upande wowote wakati litakapohitajika kutatua mizozo ya kisiasa. Lakini wengine wametetea zawadi hiyo, wakisema viongozi mbalimbali wa kitaifa wamekuwa wakiwasaidia wazee wa jamii kwa miaka mingi. Kwa mujibu wa David Dimba Jakobuya, Bw Randa ni mmoja wa wazee wachache waliosalia ambao walishiriki katika harakati za ukombozi wa kwanza na wa pili nchini Kenya. Alisema amekuwa akikabiliwa na changamoto za usafiri tangu gari lake la awali lilipoibwa miaka kadhaa iliyopita. Akijibu ukosoaji huo, Bw Randa alisema wale wanaopinga zawadi hiyo hawakuwahi kujitokeza alipokuwa akikosa usafiri. “Sikusikia mtu yeyote akilalamika kwa niaba yangu wakati sikuwa na gari. Sasa nimepewa gari, kila mtu ana maoni. Marais wengine pia wamekuwa wakitoa zawadi kwa watu wengi nchini,” alisema. Wakati huo huo, baadhi ya wakazi wamehoji iwapo gari hilo ni mali ya Bw Randa binafsi au ya Baraza la Wazee wa Luo. Hata hivyo, kiongozi huyo amesisitiza kuwa ni zawadi ya kibinafsi aliyopewa na Rais kufuatia ombi lake. Mjadala huo umechukua sura ya kisiasa zaidi baada ya Bw Randa kutoa wito kwa jamii ya Waluo kumuunga mkono Rais Ruto katika azma yake ya kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu ujao.

AFISA Mkuu Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Maeneo ya Mashambani (REREC) ni miongoni mwa viongozi wa kampuni na mashirika ya umma na ya kibinafsi waliotambuliwa kwa uongozi bora na mchango wao katika mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini Kenya. Dkt Rose Mkalama alituzwa Afisa Mkuu Mtendaji bora wa mwaka wakati wa makala ya pili ya East Africa Leadership Awards, kwa uongozi wake katika kupanua upatikanaji wa umeme nchini kupitia Mpango wa Last Mile Connectivity. Chini ya juhudi za kitaifa za kusambaza umeme, kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini Kenya kimeongezeka hadi zaidi ya asilimia 76, kutoka karibu asilimia 27 mwaka 2013. Kulingana na Dkt Mkalama, tuzo hiyo si mafanikio yake binafsi pekee, bali ni utambuzi wa kazi inayofanywa na REREC kuhakikisha umeme unawafikia maelfu ya Wakenya katika maeneo ya vijijini na mashambani. “Nina furaha kuwa REREC imeweza kufikia maelfu ya Wakenya katika karibu kila kijiji nchini kupitia Mpango wa Last Mile Connectivity,” alisema. REREC ilipoanzishwa, kiwango cha kuunganishwa kwa umeme nchini kilikuwa takriban asilimia 8. Afisa Mkuu Mtendaji huyo wa shirika hilo alisema ongezeko hilo limechangiwa na ufadhili wa serikali, ushirikiano na wabunge pamoja na utekelezaji endelevu wa miradi ya usambazaji umeme katika maeneobunge yote 290 nchini. [caption id="attachment_192455" align="aligncenter" width="300"] Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Maeneo ya Mashambani (REREC), Dkt Rose Mkalama akizungumza awali. Picha|Hisani[/caption] Anasema manufaa ya umeme yameendelea kuyapa maboma mwangaza, ikizingatiwa yamesaidia kufanikisha elimu, afya, kilimo na biashara, na hivyo kuwezesha jamii kushiriki zaidi katika maendeleo ya kiuchumi. “Kwa sasa, tunatekeleza miradi inayolenga kuunganisha taasisi za umma na jamii kwenye huduma za umeme, huku mipango ya usambazaji umeme kupitia gridi ikilenga kufikia mamia ya maelfu ya wateja,” Dkt Mkalama akadokeza. Viongozi wengine waliotuzwa ni pamoja na Dkt Lilian Nyawada, Kamishna wa Forodha na Udhibiti wa Mipaka katika Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru Kenya (KRA), na Dkt David Okeyo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Kenya Nutrition and Dieticians Institute. Kabla ya kutawazwa viongozi bora, huduma za mashirika na kampuni zao zilipigwa msasa na jopo la majaji mashuhuri kutoka World Human Resource Congress, wasimamizi wa huduma za wafanyakazi kutoka India na viongozi tajika wa kijamii. Akizungumza wakati wa kuwatuza, Mkuu wa Kitengo cha Bionuwai, Ujumuishaji na Haki za Watu wenye Mahitaji Maalum (Head of the Office of Diversity, Inclusion and Disability Rights in the Executive Office of the President) katika Afisi ya Rais, Isaac Mwaura, aliwataka viongozi wa taasisi za umma na kibinafsi kuhamasisha wafanyakazi wao kujitahidi kutoa huduma bora. “Uongozi haupaswi kupimwa kwa cheo pekee, bali pia kwa urithi ambao viongozi wanaacha katika taasisi na jamii,” Mwaura akasema. Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mt Kenya Prof Bindu Madhavi, pia alitambuliwa kwa tuzo ya Profesa mwenye ushawishi mkubwa kutokana na mchango wake katika elimu, utafiti, kunoa wanafunzi makali na masuala ya dawa na sayansi.

SHUGHULI za kawaida zilisitishwa kwa muda Mombasa Alhamisi asubuhi wakati msafara wenye ulinzi mkali ulipokuwa ukielekea katika kiwanda cha simiti cha Bamburi kutoka kambi ya jeshi la wanamaji iliyo Mtongwe. Msafara huo uliojumuisha walinzi wa usalama wenye silaha ulikuwa ukienda kwa shughuli ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya methamphetamine zilizokadiriwa kuwa za Sh8.2 bilioni. Operesheni hiyo ilihusisha maafisa kutoka Jeshi la Wanamaji, Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI), Idara ya Huduma ya Polisi, Polisi wa Kimataifa (Interpol) na Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP). Tanuri za Bamburi Cement zimeidhinishwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) kwa ajili ya uharibifu salama na uchakataji wa taka hatari na zisizo hatari. Kupitia Geocycle Kenya, kiwanda hicho pia hutumia taka zinazochomwa kama chanzo mbadala cha nishati ya joto katika uzalishaji wa simiti. Dawa hizo haramu kwanza zilipimwa uzani na kuthibitishwa kuwa zile halisi zilizokamatwa, kabla ya mahakama kutoa amri ya mwisho kuruhusu mchakato uliofuata. Hakimu Mkuu Anthony Mwicigi alisimamia shughuli hiyo na kuamrisha kwamba dawa hizo ziharibiwe, baada ya mahakama kuridhika kwamba zilikuwa zile zile ambazo zilipatikana kwa washukiwa. Washukiwa hao ambao ni raia wa Iran ni Jaseem Darzadeh Nia, Nadeem Jadgal, Hassan Baloch, Raheem Baksh, Imran Baloch na Imtiyaz Daryay. Wanadaiwa kusafirisha kilo 1,036.044 za methamphetamine zenye thamani ya takriban Sh8.2 bilioni, na kesi yao bado inaendelea katika Mahakama ya Shanzu. Upande wa mashtaka unadai kuwa dawa hizo zilisafirishwa ndani ya meli MV Mashaallah, ambayo inadaiwa haikusajiliwa na haikuwa na uraia wa nchi yoyote. Meli hiyo ilikamatwa katika bahari kuu, huku kosa linalodaiwa kutendeka kati ya Oktoba 17 na 20, 2025. Washukiwa hao sasa wataanza kuwasilisha utetezi wao mmoja baada ya mwingine huku kesi hiyo ikiendelea. Tanuri ya Bamburi Cement imewahi kutumiwa kwa shughuli kama hiyo awali. Katika mwaka wa 2025, mihadarati aina ya heroin na kokeni za Sh400 milioni ziliharibiwa hapo baada ya washukiwa kupatikana na hatia au kupoteza maisha kwa njia zisizoeleweka. Waziri wa Usalama wa Ndani, Bw Kipchumba Murkomen, alisema shughuli hiyo ya Alhamisi ilithibitisha nia ya serikali kukatiza mitandao ya ulanguzi wa dawa za kulevya kimataifa. “Leo tunatuma ujumbe sio tu kwa watumizi bali pia walanguzi wakubwa wa mihadarati. Tumeweka wazi kwamba serikali itatwaa mali za walanguzi wote na kuzitumia kurekebisha tabia za waraibu na shughuli nyingine za kukabiliana na biashara hiyo haramu,” akasema. Shughuli nzima ilifanywa kwa utaratibu na kushirikisha pande zote husika za kesi, ili kuepusha changamoto kama zile zilizoibuka baada ya serikali kulipua meli iliyodaiwa kuwa na mihadarati baharini mwaka wa 2014 chini ya aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta. Hatua hiyo ilizua utata na kutatiza kesi iliyokua ikiendelea, hadi baadhi ya washukiwa wakaachiliwa huru mwaka wa 2025 wakati mahakama ilipoamua kulikuwa na udhaifu wa kisheria, ikiwemo uharibifu wa meli husika kabla ushahidi muhimu kukusanywa.

DODOMA; TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza Novemba 4, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na uchaguzi wa madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima, uchaguzi huo unafanyika kufuatia…

SHINYANGA: THE Parliamentary Standing Committee on Welfare and Social Development has commended Barrick Bulyanhulu Gold Mine for complying with workplace health and safety regulations and protecting surrounding communities. The committee made the remarks this week during a working visit to the mine in Kakola, Kahama District, where members assessed compliance with labour, health and safety,…

KAULI ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta kwamba bado anaamini marehemu Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2022 imezua mjadala mkali wa kisiasa, huku ikifungua upya majeraha ya uchaguzi huo na kuibua maswali mapya kuhusu yaliyojiri baada ya kura za Agosti 9, 2022. Akizungumza katika makao makuu ya chama cha Jubilee jijini Nairobi, Bw Kenyatta alisema hana shaka kuwa Raila Odinga alipata kura za kutosha kushinda urais, lakini mambo yalienda kwa njia ambayo hakutaka yajirudie tena. “Tulifanya kila kitu kuhakikisha Baba anakuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Alipata kura na hadi leo ninaamini ndiye aliyeshinda kura hizo. Tunajua yaliyotokea na hatutaki yatokee tena kwa njia hiyo,” alisema. Kauli hiyo imezua mvutano mpya kati ya viongozi wa chama tawala cha UDA, viongozi wa ODM na hata baadhi ya wanafamilia wa marehemu Raila Odinga. Mjadala huo umefufua kumbukumbu za uchaguzi wa 2022 wakati Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilimtangaza William Ruto mshindi kwa kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 dhidi ya kura 6,942,930 za Raila Odinga zilizokuwa asilimia 48.85. Baadaye Mahakama ya Juu ilitupilia mbali kesi zote zilizopinga ushindi wa Dkt Ruto na kuthibitisha matokeo hayo mnamo Septemba 5, 2022. Kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Oginga, alisema kauli ya Uhuru inathibitisha kile ambacho chama chake kiliamini wakati huo, lakini imezua maswali mapya. “Ikiwa alikuwa na hakika Raila alishinda, kwa nini serikali yake ilikabidhi madaraka kwa mtu ambaye aliamini hakushinda uchaguzi?” alihoji. Dkt Oginga alisema ODM ilitumia njia zote za kikatiba kupinga matokeo ya uchaguzi lakini baada ya kushindwa mahakamani iliamua kuacha suala hilo na kuendelea mbele kwa manufaa ya taifa. “Baada ya kutumia njia zote za kikatiba zilizokuwapo, tuliamua kulimaliza suala hilo na kusonga mbele kama nchi,” alisema. Aidha alionya dhidi ya kutumia uchaguzi wa 2022 na mchango wa Raila Odinga kama silaha ya kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027. Kwa upande wake, Bw Kenyatta alitetea nafasi yake katika kampeni za Raila mwaka 2022 na kupinga madai kwamba hakufanya vya kutosha kumuunga mkono. “Wanaposema walinishinda, je ni mimi niliyekuwa kwenye kura au alikuwa Raila Odinga? Niliwezaje kushindwa ilhali nilikuwa nasaidia Raila?” aliuliza. Rais William Ruto naye aliwahi kumjibu Bw Kenyatta katika mkutano huko Siaya, akisema ikiwa hakumshinda alipokuwa rais, itakuwa vigumu zaidi kumshinda sasa akiwa amestaafu. “Uhuru Kenyatta hakunishinda alipokuwa Rais, sasa mimi ndiye Rais na yeye amestaafu. Atawezaje kunishinda?” alihoji Dkt Ruto. Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar alikataa madai ya Bw Kenyatta na kusisitiza kuwa Dkt Ruto alishinda uchaguzi huo kwa njia halali. “Rais William Ruto alishinda uchaguzi wa mwaka 2022 kwa uwazi na kwa uhalali kamili,” alisema Omar. Naye kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ameongeza uzito wa mjadala huo kwa kudai kuwa upande wa Raila Odinga uliibiwa ushindi sio tu mwaka 2022 bali pia katika uchaguzi wa 2013 na 2017. Akizungumza Kitui, Kalonzo alisema anaamini muungano wao ulishinda mara zote tatu lakini haukutangazwa mshindi. Kauli za Bw Kenyatta pia zimegawanya maoni ndani ya familia ya Odinga. Ndugu yake Raila, Omondi Oginga, alimkosoa kwa kufufua suala hilo miaka kadhaa baada ya uchaguzi na baada ya kifo cha kiongozi huyo wa ODM. “Uhuru hapaswi kucheza mchezo huu nasi. Raila ameondoka na hatufurahii suala hili kufufuliwa tena. Alikuwa madarakani na alikuwa na uwezo wote, kwa nini hakuchukua hatua wakati huo?” alihoji. Seneta wa Narok Ledama Ole Kina naye alihoji kwa nini Bw Kenyatta anatoa madai hayo sasa ilhali alikuwa Rais, Amiri Jeshi Mkuu na ndiye aliyekabidhi mamlaka kwa Dkt Ruto. Mjadala huo umefufua historia ya uchaguzi tata nchini Kenya, hasa uchaguzi wa 2007 uliosababisha machafuko makubwa ya baada ya uchaguzi, pamoja na ule wa 2017 ambao Mahakama ya Juu ilibatilisha na kuagiza urudiwe. Sasa, huku maandalizi ya uchaguzi wa 2027 yakianza kushika kasi, kauli ya Uhuru imefanya uchaguzi wa 2022 kurejea tena katikati ya siasa za taifa.

Chadema national chairman, Tundu Lissu, has told the High Court that the treason case against him is based on speculation that he threatened the government, arguing that the prosecution has failed to establish the legal basis for the charge. Defending himself, Mr Lissu submitted as he continued his final arguments before Justices Dunstan Ndunguru, James Karayemaha and Ferdinand Kiwonde. He faces a treason charge under Section 39(2)(d) of the Penal Code (2022 Revision), with the prosecution alleging that on April 3, 2025, he acted with seditious intent to incite the public to prevent the 2025 General Election by making and publishing statements online. Mr Lissu identified nine issues for the court to determine, beginning with what he described as a legal defect in the charge sheet. He argued that Section 39(2)(d) does not criminalise an intention to mobilise ‘the public’, but refers to ‘a person or group of people’, making the wording too broad to give him adequate notice. "I have been prosecuted because of speculation and the law does not permit speculative charges. In these circumstances, My Lords, the correct answer cannot be anything other than no. This means the accused did not form any intent to persuade a person or group of people to prevent the 2025 General Election for the purpose of threatening the government of the United Republic of Tanzania," submitted Mr Lissu. He challenged the prosecution's interpretation that threatening to disrupt an election necessarily amounts to threatening the government because elections are conducted under laws overseen by the State. He attributed that reasoning to the first prosecution witness, Senior Assistant Commissioner of Police (ACP) George Bagyem. To challenge that premise, Mr Lissu cited laws administered by different constitutional bodies, including legislation governing the Judiciary and Parliament. He said the Presidential, Parliamentary and Local Government Elections Act, 2024, and the Electoral Code of Ethics govern electoral matters, which fall under the Electoral Commission rather than the Executive. He also cited judicial precedents, arguing that criminal guilt cannot be established through speculation. He noted that treason is the only constitutional offence punishable by death. "Therefore, those who prosecuted me want me hanged simply on speculation that I threatened the government. On these legal grounds, My Lords, I pray you do not accept their call, wanting me sentenced to death merely because they feel I threatened the government," insisted Mr Lissu. On the prosecution evidence, Mr Lissu said only four of the 17 witnesses addressed the incitement allegation: ACP Bagyem, John Kaaya, ACP Amini Mahamba and an undercover civilian journalist, identified as PW17. He argued that the three police officers were not at the meeting and relied on online material. "My Lords, PW17 (the 17th prosecution witness) is the only witness who is an eyewitness, the only witness who saw and heard because he was present at the meeting while the rest is just hearsay from online," explained Mr Lissu. "And that PW17 did not only see and heard but he is also the one who broadcast the event; he is a journalist," added Mr Lissu. He said PW17 confirmed that the meeting was held to explain Chadema's "No reforms, no election" position to election aspirants. During cross-examination, the witness acknowledged that he had seen nothing treasonous and did not consider Mr Lissu's words an offence. "PW17, My Lords, is not my witness; he is a witness of those who want to see me sentenced to hang; there is no treason," declared Mr Lissu. "The 17th witness is a great witness because he was present, saw, and heard. I have been in jail while the Prosecution had this evidence. If I do not speak about this, My Lords, the stones will speak," said Mr Lissu. "My Lords, on this, the prosecution witnesses' evidence contradicts each other; it means all the prosecution's evidence on this issue is completely untrustworthy," he added. Mr Lissu further argued that his defence testimony showed that his remarks were intended to encourage aspirants to boycott the election until democratic reforms were achieved, rather than incite violence. He said the prosecution did not cross-examine him on his intention or the meeting's purpose. Citing Court of Appeal decisions in Justice Katiti, Nyerere Nyague and Choha Samson @ Kibiriti, he argued that failure to cross-examine a witness on a material point amounts to acceptance of that evidence. "My Lords, the prosecution's failure to cross-examine me regarding the purpose of that meeting and the intention of my words means they cannot say they do not accept that intention; they have accepted it," argued Mr Lissu. He said defence witnesses John Mnyika (DW2), Amani Golugwa (DW3), Brenda Rupia (DW4) and John Heche (DW5), whose accounts of the meeting’s peaceful purpose were not challenged by the prosecution during cross-examination, supported the same position.

Uamuzi wa Rais William Ruto kusafiri New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) akiandamana na Mawaziri saba umeibua mvutano mpya katika Seneti, ambapo baadhi ya maseneta wanahoji iwapo ukubwa wa ujumbe huo una sababu za msingi wakati Bunge linaendelea kutafuta majibu kutoka kwa serikali kuhusu masuala yanayowakabili Wakenya. Mjadala huo uliibuka Jumatano wakati wa vikao vya Seneti Mashinani vilivyofanyika Kaunti ya Kilifi. Maseneta wa upinzani walilalamikia kutokuwepo kwa baadhi ya mawaziri wakisema hali hiyo imechelewesha mijadala kuhusu matatizo yanayowakumba wananchi pamoja na utekelezaji wa miradi ya serikali. Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, alihoji sababu ya mawaziri saba kuandamana na Rais katika mkutano huo wa kimataifa. "Kenya si taifa lililoshindwa kiasi kwamba mawaziri saba waandamane na Rais kwenda UNGA ilhali jukumu lao ni kuketi nyuma yake anaposoma hotuba," alisema Khalwale. Alisema hatua hiyo inaathiri utendaji wa serikali na pia inaongeza mzigo kwa walipa ushuru kutokana na gharama za tiketi za ndege, usalama na matumizi mengine ya safari. Lawama hizo ziliongezeka baada ya kubainika kuwa baadhi ya mawaziri waliokuwa wakihitajika kujibu maswali ya Seneti hawakuwapo nchini. Miongoni mwao ni Waziri wa Madini Hassan Joho, Waziri wa Elimu Julius Migos na Waziri wa Teknolojia ya Habari William Kabogo. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna alisema kutokuwepo kwa Bw Joho kulitatiza mijadala kuhusu kituo cha samaki cha Kilifi Central ambacho maseneta walikuwa wametembelea. Kwa mujibu wa Sifuna, wavuvi, vijana na wakazi wa eneo hilo walieleza hofu kuhusu mustakabali wa mradi huo na nafasi za ajira zitakazotokana nao. "Wananchi wana wasiwasi mkubwa, hasa vijana ambao hawajapewa hakikisho kwamba wao watapewa kipaumbele cha ajira katika eneo hilo," alisema. Aidha alisema wakazi wana hofu kuwa mradi huo huenda ukaendeshwa kupitia ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, hali inayozua maswali kuhusu nani atanufaika. Sifuna pia alikosoa viongozi wa serikali kwa kutumia muda mwingi nje ya nchi huku wananchi wakikumbwa na changamoto mbalimbali nyumbani. Hata hivyo, Seneta wa Tana River Danson Mungatana alitetea uamuzi wa mawaziri kuandamana na Rais akisema safari kama hizo huwapa nafasi ya kufanya mikutano ya pembeni, kujadiliana na mataifa mengine na kutia saini mikataba ya maendeleo. "Katika safari moja, mawaziri wanaweza kufanya shughuli nyingi muhimu za serikali badala ya kusafiri mara kwa mara kwa gharama kubwa zaidi," alisema. Mvutano huo unaonyesha changamoto iliyopo kati ya shughuli za kimataifa za serikali na hitaji la mawaziri kuwajibika kwa wananchi na Bunge.