Follow the East African economy: markets and currencies, trade and investment, banking and finance, agriculture, mining and the companies and policies that move them.
By Innocent Anaba LAGOS: The Economic and Financial Crimes Commission (EFCC) and the United States Federal Bureau of Investigation (FBI) have agreed to deepen collaboration in investigating alleged diversion and mismanagement of funds provided under United States Government-supported programmes in Nigeria. The resolve was reached on Thursday, September 10, 2026, when Assistant Law Enforcement Attaché […]
Forbes evaluated 500 banks across 89 countries, examining their profitability, strength, stability and efficiency in funding mega trade and infrastructure projects.
The Cross River Government has banned street trading around the Eight-Miles area of Calabar metropolis and urged traders illegally occupying pedestrian walkways to vacate.
The expansion of BRICS marks a qualitative leap in its representativeness and influence. Today, BRICS countries account for nearly half of the world’s population, around 30 percent of global economic output, and one-fifth of global trade. The greater BRICS cooperation has entered a stage of high-quality development.
By Godwin Oritse The Customs administrations of Nigeria and Benin Republic on Friday conducted a joint assessment of the One-Stop Border Post as part of efforts to deepen regional economic integration, harmonise cross-border procedures, reduce trade barriers and facilitate the seamless movement of legitimate goods and services between both countries. Speaking at the ceremony at […]
MTWARA: TRADERS have been urged to present challenges affecting their businesses to leaders and authorities at various levels within their local areas before escalating them to higher-level government officials. The call was made on September 9, 2026, by Mtwara Regional Administrative Secretary, Bahati Geuzye, during a working meeting that brought together investment stakeholders and traders…
The discussions focused on ways of promoting Tanzania as an investment destination and linking international investors and companies with opportunities in the country.
MAPUTO: WHEN the gates of the 61st Maputo International Trade Fair (FACIM) closed recently, Tanzania left behind more than an exhibition pavilion. It left with a question that may be more important than the exhibition itself: How can Tanzania turn the relationships, market intelligence and investment opportunities identified in Mozambique into sustained economic engagement between…
MKUU wa Mawaziri, Musalia Mudavadi, amewahakikishia wafanyabiashara wa kigeni kuwa wanaweza kuendelea kufanya biashara nchini Kenya iwapo wana stakabadhi zinazohitajika, huku mashirika ya kutetea haki yakieleza wasiwasi kuhusu unyanyasaji wa wageni hao. Bw Mudavadi alisema Kenya haijaweka marufuku ya jumla kwa wageni kufanya biashara ndogo ndogo na akawataka raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kurekebisha stakabadhi zao na kuendelea na shughuli halali “kwa ujasiri”. Alisema hayo Alhamisi alipohutubia mabalozi na maafisa wa balozi za kigeni mjini Nairobi. “Maagizo yaliyotolewa na Rais wetu Septemba 2, 2026 kuhusu biashara ndogo ndogo na rejareja yanalenga kulinda sekta zilizo hatarini za uchumi wetu, kukuza ushindani wa haki na kuhakikisha Wakenya wanapata riziki,” alisema. Alisema Kenya bado imejitolea kuimarisha ushirikiano wa kikanda na akawataka raia wa EAC kufuata sheria zinazohusu kuingia nchini, kukaa na kufanya kazi. “Kenya iko wazi kwa biashara ndogo na kubwa kwa wageni, mradi wanazingatia masharti ya uhamiaji, vibali vya kufanya kazi, usajili na leseni,” alisema. Kauli hiyo ilitolewa huku mashirika ya haki za binadamu, viongozi wa kidini na makundi mengine yakieleza wasiwasi kuhusu utekelezaji wa maagizo hayo ulioanza Septemba 7. Police Reforms Working Group Kenya ilisema wafanyabiashara kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameathirika zaidi, huku kukiwa na ripoti za misako kiholela, vitisho, unyang’anyi na unyanyasaji. Muungano wa mashirika 23 ya kiraia pia ulisema hatua za kulinda biashara za Wakenya hazifai kugeuka kuwa ubaguzi wa wageni kwa misingi ya utaifa. Mashirika hayo yalisema raia wa Burundi, Uganda, Tanzania na nchi nyingine za EAC wamekumbwa na hofu, huku baadhi wakifunga biashara na wengine kutafuta hati za kusafiria ili kuondoka nchini. Baraza la Mashirika ya Kidini nchini Kenya lililaani mashambulizi na unyanyasaji dhidi ya wageni na kuitaka Serikali kuhakikisha usalama wao. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu Kenya Davis Malombe, alitaka waathiriwa walipwe fidia na Serikali iwaombe msamaha. “Tunaomba waathiriwa walipwe fidia. Na fidia pekee haitoshi; lazima muombe msamaha na kutoa hakikisho kwamba hawatanyanyaswa tena,” alisema. Wakati huo huo, hali katika Ubalozi wa Burundi Nairobi iliripotiwa kuwa mbaya huku wanawake, watoto na watu wasio na ajira wakipiga kambi nje ya ubalozi wakisubiri hati za kusafiri. Niyonkuru Celestin alisema mchakato ulikuwa wa polepole na baadhi yao walikosa chakula na maji. Nchini Nakuru, mzee wa Nyumba Kumi Bondeni, Maalim Sharif, alisema wageni wameishi kwa amani na wenyeji na wanapaswa kupewa nafasi ya kurekebisha stakabadhi zao. “Ni ndugu na dada zetu; tunapaswa kuishi kwa amani kama Waafrika,” alisema.
…Prosecute sellers of substandard cables — Coleman MD By Providence Ayanfeoluwa Economic hardship, ignorance and dwindling purchasing power are fuelling the growing trade in fake and substandard goods in Nigeria, with consumers increasingly settling for cheaper products without fully understanding the risks involved, stakeholders have said. They said the situation had become particularly troubling as […]
ZANZIBAR: ZANZIBAR is seeking to extend private-sector participation in regional trade and investment, with the government positioning the islands as a gateway to East African, African and Indian Ocean markets. Representing Acting Minister for Trade and Industrial Development, Shariff Ali Shariff, at the East African Business Council (EABC) CEOs’ Roundtable and Invest. East Africa, Zanzibar…
DAR ES SALAAM: TANZANIA and Malawi have been urged to move beyond growing trade volumes and turn their expanding commercial ties into joint investments, manufacturing and value-added production that can create jobs and open access to wider African markets. The call was made on Tuesday by the Tanzania’s Ambassador to Malawi, Agnes Kayola at the…
The naira is trading at about ₦1,329.44 to the US dollar at the Nigerian Foreign Exchange Market (NFEM), while the dollar is quoted at around ₦1,390 in the parallel market on Friday, September 11, 2026.
…Apapa, Lekki, Tin Can dominate Q2’26 flowsBy Efe OnodjaeLagos ports handled an estimated N35.07 trillion, or about 84.6 per cent, of Nigeria’s N41.44 trillion total merchandise trade in the second quarter of 2026, Q2’26, underscoring the overwhelming dominance of the nation’s commercial capital as the country’s principal trade gateway.The latest Foreign Trade in Goods Statistics […]
—Accuses NASS of oversight failure By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief ABUJA — The Centre for Social Justice, CSJ, has urged the Federal Government to immediately release funds for the implementation of the 2026 capital budget, warning that continued delays undermine the Constitution, the Fiscal Responsibility Act and the Appropriation Act. The organisation made the […]
DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeendelea kusogeza huduma na elimu kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa karibu na wananchi kupitia Kliniki ya Viwango, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo na kuwezesha wafanyabiashara kuzingatia matakwa ya viwango. Akizungumza wakati wa Kliniki hiyo inayoendelea Kariakoo na Mwenge jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi…
MAMIA ya watu, vijana kwa wazee waliojihami kwa koleo, mawakala waliobeba kitita cha hela na madereva wa malori, wamiliki mashine na wafayabiashara wamefurika Homa Bay baada ya madini yanayoshukiwa kuwa dhahabu kugunduliwa. Mwezi mmoja uliopita, Kijiji cha Maguje, Homa Bay kilikuwa eneo tulivu ambapo mifugo walikula viwanjani na wakulima kupalilia mimea yao katika msimu wa mvua. Katika maeneo ambayo awali yalichimbwa ‘murram’, hali imegeuka huku wanaume wakichimba kwa mkono na mashine kufungua mitaro yenye kina kirefu kusaka dhahabu. Wengine wanatumia nguvu huku wakibeba mawe yaliyochimbwa migongoni kabla ya kuyapakia kwenye pikipiki au malori. Baadhi ya mawe hayo husafirishwa viwandani ambapo mashine hutenganisa dhahabu na miamba. Kando ya kware, wanawake ambao mwezi mmoja tu uliopita waliuza mboga na samaki wamefunga biashara zao za zamani. Wanaamka alfajiri kuandaa chapati, maharage na chai kwa wachimba madini. Yote yalianza na uvumi uliosambaa kwamba dhahabu imegunduliwa kijijini humo. John Okello, aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kituo cha kuchimba madini alisema uvumbuzi huo ulijiri baada ya wakazi kumwona mwanamke akiokota mawe kwenye kware. Mwanamke huyo aliokota mawe kwa karibu miezi mitano kabla ya baadhi ya wanakijiji kuanza kuuliza alikoyapeleka. “Aliyaweka kwenye gunia na kuwalipa wahudumu wa bodaboda kuyapeleka eneo lisilojulikana. Baadaye alifichua kuwa anayapeleka katika kituo cha kusafisha dhahabu,” alisema. Gunia la madini hayo huuzwa kati ya Sh2000 na Sh5000 kutegemea matokeo ya vipimo vinavyofanyiwa sampuli kutoka eneo hilo. Baada ya kuona jinsi watu wanavyosaka dhahabu kwa ari, kamati ya dhahabu iliyobuniwa kusimamia kituo hicho ilianzisha sheria za kudhibiti oparesheni hizo. Miongoni mwake ni masharti kwa wachimbaji madini kuwalipa wamiliki ardhi Sh50,000 kabla ya uchimbaji kuanza. Maafisa wa serikali bado hawajathibitisha kiwango cha mgodi wa dhahabu au kudhibiti shughuli hizo, huku wasiwasi ukitanda kuhusu usalama, mizozo ya ardhi na uwezekano wa wenyeji kukandamizwa na wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa.
…Says weak links could destabilise financial system By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief ABUJA: The Central Bank of Nigeria, CBN, has urged banks, fintechs and other financial institutions to treat cybersecurity and third-party technology risks as critical financial stability issues, warning that vulnerabilities in one institution could trigger widespread disruption across the financial system. The […]
Finance Minister Ambassador Khamis Mussa Omar is leading Tanzania’s delegation at the eighth Korea-Africa Economic Cooperation Conference (KOAFEC), a four-day forum focusing on the role of artificial intelligence (AI) and digital infrastructure in Africa’s development. The conference, taking place from September 8 to 11, 2026, at the Grand Walkerhill Hotel in Seoul, is being jointly organised by the Government of South Korea, the African Development Bank (AfDB) and the Korea Export-Import Bank (Korea Eximbank). Ambassador Omar arrived in Seoul and was received at the international airport by Tanzania’s Ambassador to South Korea, Noel Kaganda, and the Acting Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance and Commissioner for External Finance, Rished Bade. The two officials later briefed the minister on the conference and its key areas of focus. This year’s KOAFEC is being held under the theme, “Harnessing AI and Digital Infrastructure for Africa’s Transformation.” The forum brings together African ministers responsible for economic and financial affairs, AI and digital transformation, AfDB officials, African businesses and international development partners. Discussions will focus on how African countries can harness artificial intelligence and digital infrastructure to accelerate development, with particular emphasis on investment, development financing, technological innovation and strengthening economic cooperation between South Korea and African countries. Ambassador Omar, who is accompanied by the Minister for Information, Communication and Technology, Angellah Kairuki, is also expected to hold bilateral meetings with heads of various institutions and organisations in South Korea. The meetings are aimed at attracting investment and capital to Tanzania, with the government seeking to expand economic opportunities and create more jobs, particularly for young Tanzanians. The Korea-Africa partnership has now reached its 20th anniversary. In recent years, South Korea has pledged $2.4 billion to support the economic and social development of African countries. At the Korea-Africa Summit held in Seoul in June 2024, attended by leaders and government representatives from 48 African countries, as well as representatives of the African Union and the AfDB Group, South Korea pledged to more than double its development assistance to Africa to $10 billion by 2030. It also pledged a further $14 billion in export financing to support Korean companies seeking to expand trade and investment on the continent.
KIGOMA: Vijana mkoani Kigoma wamesema mikopo inayotolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri imeleta mapinduzi makubwa katika shughuli zao za kiuchumi na maendeleo, huku ikiwasaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi. Mwenyekiti wa Kikundi cha Madereva wa Bodaboda Makere, George Kagoma, amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa…
MBINU mpya na za jadi za kupika na kuongeza nyama thamani zinaendelea kubadilisha sekta ya mifugo na nyama nchini, huku wafanyabiashara na wabunifu wakitumia teknolojia na maarifa mapya kuvutia walaji. Haya yalijitokeza katika Maonyesho ya Kenya Meat Expo 2026 yaliyoandaliwa na Nation Media Group (NMG) kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo. Maonyesho hayo ambayo yalikuwa Makala ya Tano yalifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Nairobi, Agosti 26 hadi 28. Wakulima, wasindikaji, wafanyabiashara, watafiti, mashirika muhimu kama vile ya kuuza nyama nje ya nchi, ya kifedha, ya malisho, wabunifu na mashabiki wa nyama walipata nafasi ya kujifunza mbinu tofauti za kupika na kuhifadhi nyama. Miongoni mwa mbinu zilizovutia wengi ni uandaaji wa nyama kwa moshi. Njia hii huhusisha kupika nyama kwa joto la chini kwa muda mrefu, huku moshi wa kuni ukiipa ladha ya kipekee. Samuel Ndung’u, mwanzilishi wa Pikmaster Sam, alionyesha jinsi nyama ya brisket huandaliwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kuvuta moshi. Kwenye mahojiano na Akilimali, alisema nyama hiyo huchukua zaidi ya saa 12 kuiva kikamilifu. “Tunapika polepole ili nyama isalie laini, yenye unyevu na ladha ya kipekee inayotokana na kuni tunazotumia,” anasema. Ndung’u, ambaye aliacha kazi katika huduma ya polisi kuingia kwenye biashara ya nyama mwaka 2014, anasema mbinu hiyo imebadili mtazamo wa watu kuhusu nyama ya kuchoma. [caption id="attachment_191925" align="alignnone" width="2560"] Joshua Nzioka wa Camp David akiwa katika maonyesho ya nyama KICC Agosti 28, 2026. PICHA| DENNIS ONSONGO[/caption] Hata hivyo, anakiri kuwa gharama za uzalishaji ni kubwa kutokana na matumizi makubwa ya kuni, mafuta na wafanyakazi. Kwa sasa, robo ya kuku katika biashara yake huuzwa kwa Sh400, kilo moja ya nyama ya kondoo kwa Sh1,800 huku hiyo iliyochomwa kwa moshi (brisket) ikiuzwa kwa Sh2,500 kwa kilo. Mbali na uchomaji wa nyama kwa moshi, Martin King’ori wa Camp David Butchery, alionyesha teknolojia ya dry ageing, ambapo nyama huhifadhiwa katika mazingira yenye kiwango maalumu cha joto, unyevunyevu na mzunguko wa hewa kwa wiki kadhaa kabla ya kuuzwa au kupikwa. Kulingana King’ori, mbinu hiyo huifanya nyama kuwa laini zaidi na kuongeza ladha yake. “Maji hupungua polepole huku vimeng’enya vya asili vikivunja protini za misuli, jambo linaloboresha ubora wa nyama,” anasema. Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, alisema sekta ya nyama ina uwezo mkubwa kuunda ajira, kuongeza mapato ya wafugaji na kuimarisha mauzo ya bidhaa za Kenya nje ya nchi. Alidokeza kwamba Kenya ilizalisha takriban tani 613,627 za nyama mwaka 2024 zenye thamani ya Sh397 bilioni. “Nyama ya ng’ombe iliongoza kwa uzalishaji wa tani 260,000 zenye thamani ya karibu Sh160 bilioni,” Waziri Kagwe alielezea. Hata hivyo, alisisitiza kuwa nchi haipaswi kutegemea nyama ya ng’ombe pekee, akitaja fursa zilizopo katika nyama ya mbuzi, kondoo, kuku, ngamia, nguruwe na sungura. Waziri alisema Kenya inapaswa kuhamia kutoka kuuza mifugo hai hadi kuuza nyama, nyama iliyosindikwa na bidhaa zenye chapa maalumu ili kuongeza mapato na ajira nchini. “Tunapouza mifugo hai nje ya nchi, tunakuwa pia tunauza nafasi za kazi ambazo zingepatikana hapa Kenya,” alisema. Maonyesho hayo yalithibitisha kuwa sekta ya nyama inaendelea kupanuka na kwamba ubunifu katika usindikaji, upishi na masoko unaweza kufungulia vijana na wajasiriamali fursa mpya za kiuchumi na kazi. Kauli mbiu ya hafla ya mwaka huu, 2026, ilikuwa kuimairisha ukuaji unaoweza kudumishwa pamoja na kukuza kizazi kijacho katika biashara ya nyama.
RAIS William Ruto amejitokeza waziwazi kumshawishi mfanyabiashara Suleiman Shahbal kuachana na azma ya kuwania ugavana wa Mombasa, akisema bwanyenye huyo anaweza kulitumikia taifa la Kenya vyema zaidi kwa kuunda ajira na kuwekeza katika biashara kuliko kujiingiza katika siasa za uchaguzi. Akiongea katika Ikulu ya Nairobi, Dkt Ruto alisema alikuwa amemshauri binafsi Bw Shahbal dhidi ya kuwania ugavana. “Nakumbuka nilimwambia Bw Shahbal kwamba najua unataka kuwania ugavana wa Mombasa, na nikamwambia kwamba ninapinga hilo. Nisamehe, ndugu yangu Shahbal, lakini wewe ni mjasiriamali mkubwa,” alisema Dkt Ruto. Rais alikuwa akizungumza wakati wa kutiwa sahihi kwa makubaliano ya Sh12 bilioni kati ya GulfCap Group ya Bw Shahbal na kampuni ya kimataifa ya biashara za bandarini ya DP World kwa ajili ya kuendeleza Eneo Maalum la Kiuchumi lenye ukubwa wa ekari 535 eneo la Jomvu, Mombasa. Mradi huo utawaleta pamoja wazalishaji, kampuni za usafirishaji mizigo, wauzaji wa bidhaa nje ya nchi na biashara nyingine karibu na Bandari ya Mombasa. Bw Shahbal alisema kampuni kutoka Dubai, India, China, Vietnam na Ulaya tayari zimeonyesha nia ya kuanzisha shughuli katika eneo hilo, huku baadhi zikiiangalia Kenya kama kituo cha uzalishaji bidhaa kwa ajili ya masoko ya Afrika, Ulaya na Amerika. Gavana wa Mombasa, Bw Abdulswamad Nassir aliipongeza hatua hiyo, akisema itatoa fursa kwa Mombasa kuzalisha bidhaa zilizokamilika zinazolenga masoko kote duniani.
RAIS William Ruto ameshinikizwa kuhakikisha agizo lake la kuwabana raia wa kigeni wanaojihusisha na biashara ndogo nchini halichochei ubaguzi, chuki au hatua zinazoweza kuwa na madhara kwa Wakenya wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi. Wasiwasi umeanza kutanda miongoni mwa Wakenya walio ughaibuni, huku baadhi wakisema wanaajiriwa na raia wa kigeni, wakiwemo raia wa Burundi, na kuhofia kuwa huenda wakalengwa iwapo mvutano huo utaendelea. Wasiwasi huo umeibuka baada ya baadhi ya raia wa Burundi nchini Kenya kuripotiwa kutishwa na kubaguliwa kufuatia agizo la Rais Ruto kuhusu wafanyabiashara wa kigeni katika sekta ya biashara ndogo. Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimeitaka Serikali kuhakikisha utekelezaji wa hatua hizo haugeuki kuwa kampeni ya kuwabagua watu kwa misingi ya uraia. Katika taarifa yake iliyotolewa Arusha Jumatatu, EALS ilisema imeingiwa na wasiwasi kutokana na hofu miongoni mwa raia wa Burundi na mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoishi Kenya. “Mtu akishtakiwa kwa kukiuka sheria za Kenya anapaswa kushughulikiwa kwa misingi ya sheria husika na mazingira ya kesi yake. Uraia pekee haupaswi kuchukuliwa kuwa ushahidi wa uhalifu,” ilisema EALS. Shirika hilo lilisema kuwa Kenya ina haki ya kudhibiti shughuli za kiuchumi nchini, ikiwa ni pamoja na kutekeleza sheria za uhamiaji, leseni, ushuru na ajira. Hata hivyo, lilisema utekelezaji huo lazima uwe wa haki na mtu binafsi ashughulikiwe kulingana na kosa alilotenda, bila kuangalia taifa analotoka. EALS ilionya kuwa hali hiyo inaweza kuathiri pia Wakenya wanaoishi na kufanya biashara katika nchi nyingine za Afrika Mashariki. Hofu hiyo imeongezeka kutokana na taarifa kwamba mamia ya raia wa Burundi walifika katika ubalozi wao jijini Nairobi kutafuta hati za kusafiria na usaidizi wa kibalozi. Baadhi yao walionekana wakibeba mizigo yao, yakiwemo magodoro na masanduku, huku wengine wakitafuta usafiri kurejea Burundi. Wengine walilazimika kulala katika mazingira magumu ndani ya ubalozi huo wakihofia kurejea walikokuwa wakiishi baada ya biashara zao kuvamiwa. Serikali ya Kenya, hata hivyo, imejaribu kutuliza hali hiyo kwa kutangaza muda wa siku 90 kwa raia wa kigeni wanaofanya biashara nchini kurekebisha hali yao ya uhamiaji, vibali vya kazi, usajili wa biashara na leseni. Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed alisema raia wa kigeni wasio na nyaraka zinazohitajika wanapaswa kujitokeza katika balozi za nchi zao ili kusajiliwa. Alisema watakaokuwa katika mchakato huo watachukuliwa kuwa wako nchini kihalali Serikali ikishirikiana na balozi zao kurekebisha hali yao. Serikali pia imeonya Wakenya dhidi ya kuchukua sheria mkononi mwao na kuwanyanyasa wageni. “Hakuna mtu au kundi lenye mamlaka ya kunyanyasa, kuwatisha au kuingilia shughuli za raia wa kigeni au biashara zao,” ilisema taarifa ya Ikulu. Serikali ilisema baada ya siku 90, sheria kuhusu uhamiaji, vibali vya kazi, usajili wa biashara na leseni zitatekelezwa kwa ukali na kwa mujibu wa sheria. Katibu wa Masuala ya Kigen Korir Sing’oei pia aliomba msamaha kwa raia wa Burundi waliokumbwa na unyanyasaji. “Nataka kuwaomba msamaha raia wote wa Burundi hapa,” alisema alipofika katika Ubalozi wa Burundi jijini Nairobi Jumatatu. Seneta Danson Mungatana, anayeongoza ujumbe wa Kenya katika Bunge la Pan-Afrika, ametaka Wizara ya Usalama wa Ndani kuchukua hatua dhidi ya ripoti za chuki na unyanyasaji wa raia Burundi, hasa Nakuru. Alisema masuala ya wageni kufanya biashara nchini yanapaswa kushughulikiwa kupitia sheria za uhamiaji, leseni, ushuru na ajira, badala ya makundi ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao. Nchini Burundi, Waziri wa Masuala ya Kigeni Edouard Bizimana alionya kuwa hali hiyo inaweza kuwa na madhara kwa Wakenya wanaoishi nchini humo. “Wakenya nchini Burundi wanaishi kwa amani, lakini ikiwa matamshi ya chuki dhidi ya Burundi yataendelea, mambo yatabadilika,” alisema. Mkuu wa Chama cha raia wa Burundi wanaoishi Kenya, Alexis Ntinanirwa, pia alionya kuwa mzozo huo unaweza kuathiri uhusiano wa kikanda. Alisema Wakenya wengi wanafanya biashara ndogo katika Burundi, Tanzania na Uganda. “Suala hili halitasababisha matatizo kwa Waburundi wanaofanya kazi Kenya pekee, bali pia litasababisha matatizo katika eneo hili kwa sababu kuna Wakenya wanaofanya kazi hizi ndogo katika nchi zetu,” alisema. Wakati huo huo, EALS imetaka Serikali kuweka wazi sheria na taratibu zitakazotumika katika kuwashughulikia wafanyabiashara wa kigeni. Shirika hilo pia limetaka raia walioathirika wapewe nafasi ya kupata maelezo, msaada wa kisheria na kukata rufaa pale sheria inaporuhusu. Rais Ruto amesema hatua hizo zinalenga kulinda nafasi za kiuchumi za Wakenya, hasa katika biashara ndogo zinazotegemewa na mamilioni ya watu. Amesema Kenya iko tayari kupokea wawekezaji wa kigeni, lakini wawekezaji hao wanapaswa kuanzisha biashara zinazozalisha ajira badala ya kushindana na Wakenya katika biashara ndogo kama uchuuzi na maduka madogo. Hata hivyo, hatua hiyo imezua mjadala mkali kuhusu namna ya kulinda maslahi ya Wakenya bila kuhatarisha uhusiano wa Kenya na majirani zake au maisha ya Wakenya wanaofanya kazi na biashara nje ya nchi.
EALS warns Nairobi against discrimination in the foreign trader crackdown, urging it to observe the rule of law and uphold public confidence in EAC Common Market.
Regional trade and food security could come under pressure as the World Meteorological Organisation (WMO) warns that a strengthening El Niño is expected to persist into February 2027, with effects extending across agriculture, fisheries, transport, energy and water resources.
Experts say Tanzania needs to widen bank participation, harmonise regulations, promote the use of local currencies and integrate regional payment systems with digital platforms if it is to unlock their full potential in cross-border trade.
DAR ES SALAAM: Tanzania na Malawi zimekubaliana kuongeza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili kwa kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi, kuongeza thamani ya malighafi na kutumia fursa za masoko ya kikanda, huku Malawi ikiendelea kuitumia Tanzania kama lango muhimu la biashara kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Makubaliano hayo yamejadiliwa katika mkutano wa…
Singida: The Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has handed over an infant radiant warmer and a phototherapy unit to Singida Regional Referral Hospital in a bid to support the government’s efforts to strengthen maternal and child health and improve the well-being of Tanzanians. Speaking during the handover ceremony in Singida Municipality recently, the…
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na India imeanza kuchukua hatua za kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuandaa majukwaa yanayowaunganisha wadau, kubadilishana maarifa na teknolojia pamoja na kuibua fursa za ubia wa kibiashara.
WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa wito wa kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi kwa kunufaika na fursa za ajira, biashara, uwekezaji na umiliki wa shughuli za kiuchumi. Dk. Mwigulu ameyasema hayo jana, Septemba 3, 2026, jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Tano la Taifa la Ushiriki wa Watanzania katika Masuala ya Uchumi.
AFRICA: Boosting trade flows amongst African countries remains a key economic priority. There is significant opportunity to accelerate the growing intra-African trade in order to unlock investment, catalyse industrialisation, especially processing and adding value to our natural resources. According to the Africa in Figures 2025 report released by African Export-Import Bank (Afreximbank), intra-African trade grew…
DAR ES SALAAM: THE Vice President Deogratius Ndejembi has directed the Ministry of Industry and Trade to work with cement manufacturers to urgently find a solution to rising cement prices and restore the commodity to affordable levels for Tanzanians. Speaking at the 19th Presidential Awards for Best Industrial Producers (PMAYA) held at SuperDome, Masaki in…
TANZANIA imeendelea kujijenga kuwa miongoni mwa vituo muhimu vya biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na fursa kubwa zilizopo katika sekta ya kilimo, huku wawekezaji kutoka India, Ulaya na Mashariki ya Kati wakionesha nia ya kuwekeza nchini.
As Ubungo Municipal Council demands over Sh249.4 million in rent arrears from business owners at the Magufuli Bus Terminal passenger building, traders have outlined the operational challenges driving declining sales and payment delays.
ZANZIBAR: MORE than 300 traders, entrepreneurs and producers from Zanzibar and Mainland Tanzania are expected to take part in the third edition of the Fahari ya Zanzibar Exhibition, aimed at promoting locally made products, expanding markets and strengthening business linkages. The exhibition will run from tomorrow (September 4) to Monday (September 14,) with the official…
MOZAMBIQUE: FOR much of Tanzania’s modern history, our position on the western shores of the Indian Ocean has been understood mainly in terms of trade, ports, tourism and regional connectivity. That perspective remains valid, but it is no longer sufficient. The changing global geopolitical and economic environment is giving the Western Indian Ocean a much…
The naira continued to strengthen against the US dollar on Thursday, September 3, 2026, with the Nigerian currency trading around N1,329 per dollar in the official market while the parallel market remained significantly higher.
Iran and the United States traded threats on Wednesday after some of the heaviest fighting in weeks engulfed the Middle East, deepening the foes' stalemate six months into the war.
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imewataka Watanzania na wawekezaji kushirikiana kupitia vyama na vyombo vya wafanyabiashara kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini na kuzitangaza katika masoko ya kimataifa.
MAHAKAMA imewaamuru wanandoa waliotengana kugawana kwa usawa gharama ya kuwalea watoto wao watatu, na kukataa ombi la mama kutaka baba abebe mzigo wote wa kifedha. Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Bungoma, T.O. Omono, alisema wazazi wote wana wajibu wa kuwatunza watoto wao, hasa pale ambapo kiwango chao cha mapato ni karibu sawa. Hakimu huyo aliwaamuru DA na mumewe AW kugawana kwa usawa gharama ya chakula, mahitaji mengine na malezi ya watoto hao. Pia watachangia kwa usawa karo na gharama nyingine za shule katika shule ambazo watoto hao wanasoma hadi mwisho wa mwaka wa masomo. Watoto hao, EW, SI na AJ, pia watabaki katika makazi yao ya sasa hadi kesi kuu itakaposikizwa na kuamuliwa. DA alikuwa ameomba mahakama imwamuru AW kutoa pesa kila mwezi za chakula, karo, matibabu na mahitaji mengine ya watoto. Alidai amekuwa akigharamia mahitaji ya watoto peke yake licha ya mumewe kuwa mfanyakazi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).AW alikanusha madai hayo na kusema tayari alikuwa akigharamia mahitaji ya watoto. Alisema pia alikuwa akigharamia matibabu yao kupitia bima yake ya afya. Mahakama ilibaini kuwa mahitaji ya matibabu ya watoto hao tayari yalikuwa yakigharamiwa kupitia bima ya baba yao. Hata hivyo, hakimu alisema hilo halimaanishi kuwa baba anapaswa kuachwa peke yake kugharamia mahitaji mengine. Mahakama ilichunguza taarifa za kifedha zilizowasilishwa na wazazi hao na kubaini kuwa mapato yao ya kila mwezi yalikuwa karibu sawa. DA alisema katika hati yake kwamba, alikuwa akipata mshahara wa Sh27,669 kwa mwezi baada ya makato. Baba pia aliwasilisha taarifa kuhusu mshahara wake wa KDF, matumizi na majukumu mengine ya kifedha. Hakimu alikataa hoja ya mama kwamba baba anapaswa kuwalea watoto hao peke yake.
RAIS William Ruto amesema kwamba haikubaliki kwa raia wa kigeni kuja nchini kufanya uchuuzi na biashara ndogo ndogo. Anasema wageni wana ruhusa ya kuwa wawekezaji pekee, sio kushindana na wenyeji katika biashara ndogo kama uchuuzi na maduka madogo madogo. Akizungumza baada ya kukutana na sehemu ya wafanyabiashara waliofanya maandamano wiki jana kulalamikia ushuru mpya wa KRA kuhusu shehena ya bidhaa za kutoka nje katika Ikulu ya Nairobi Jumatano, Rais aliagiza mawaziri husika kuharakisha mswada bungeni unaoharamisha aina fulani ya biashara kufanywa na raia wa kigeni. "Tuko na wafanyabiashara kutoka nchi zingine, wacha nisiseme nchi gani, wamekuja hapa na kuwa wachuuzi, wanauza duvets. Bw Mukwana na Lee Kinyanjui, tayari tuko na mswada bungeni kuhusu mambo ya biashara. Katika hiyo bill, tumesema kuna biashara mgeni hawezi kufanya hapa Kenya by law. Nataka mketi chini na hawa wafanyabiashara muangalie na tuzibe mianya yote. Isitokee kwamba mtu ametoka China na amekuja kuwa hawker au kuuza duka kidogo hapo. Ichungwa, you don’t need any further instructions. Monday muamkie hiyo biashara. Hao wachuuzi wote wanafanya hii biashara kidogo kidogo wafunge na wasipofunga (ashangiliwa) tutafunga. Hatujajenga Investor Confidence ndio watu wakuje kuwa wachuuzi. Tumejenga Investor Confidence ndio watu wakuje kuwekeza," akasema Bw Ruto. Katika maandamano ya Agosti 28, 2026, waandamanaji walikusanyika katika eneo la Archives kabla ya kuelekea makao makuu ya KRA katika jengo la Times Tower katikati mwa jiji. Wafanyabiashara hao walisema mabadiliko ya kiwango kinachotumiwa kukadiria thamani ya bidhaa za uagizaji yameongeza gharama za biashara na kupunguza faida zao. Kwa mujibu wao, KRA imepandisha kiwango cha ukadiriaji kutoka 2.5m hadi 3.2m, hatua wanayodai imeongeza kwa kiasi kikubwa kodi inayolipwa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hususan kutoka China. Walisema mabadiliko hayo yamesababisha ongezeko la takriban asilimia 28, huku thamani ya bidhaa kwa madhumuni ya kodi ikiongezeka kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni.
· Express surprise over inclusion of garri by NBS · Lists causes of high food prices By Cynthia Alo Stakeholders in the agricultural sector and economy experts have raised concerns over the latest food inflation report released by the National Bureau of Statistics (NBS), describing it as inconsistent with prevailing conditions in farms and markets […]
For budget-conscious consumers, cheaper brands offer an entry point. Others, however, are willing to spare no expense for premium footwear and apparel.
ZANZIBAR: PRESIDENT Samia Suluhu Hassan has directed regional commissioners and local authorities to tackle the growing return of small traders to streets through proper planning rather than force, including improving access to markets and transport services. President Samia said the problem was becoming increasingly visible in major cities, particularly Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya…
DAR ES SALAAM: The Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE) has called on Tanzanians and investors to strengthen cooperation through business associations and chambers of commerce in order to add value to locally produced goods and promote them internationally, with the aim of accessing larger global markets. The call was made by TANTRADE Director General Ephraim…
SERIKALI ya India imesema iko katika hatua za kuchunguza fursa za kuongeza kiwango cha bidhaa za kilimo kutoka Tanzania zinazoingia katika soko la India, hatua inayolenga kuongeza mauzo ya nje, kuboresha ubora wa mazao na kukuza ajira nchini.
DAR ES SALAAM: QATAR has expressed interest in investing in Tanzania’s port infrastructure, with the two countries moving to establish a joint task force to explore strategic projects aimed at expanding port capacity and strengthening Tanzania’s position in regional trade. The interest was expressed by former Qatari Deputy Prime Minister Dr Khalid bin Mohammad Al…
MWANZA: EXPANDING cross-border trade is raising the importance of accuracy in the quantities declared on packaged goods, increasing the need for Tanzanian manufacturers to align with internationally recognised measurement standards. Geita Regional Manager of the Weights and Measures Agency (WMA), Ms Eva Ikula, said recently that manufacturers and packers need to ensure their products meet…