RAIS William Ruto amesema kwamba haikubaliki kwa raia wa kigeni kuja nchini kufanya uchuuzi na biashara ndogo ndogo.
Anasema wageni wana ruhusa ya kuwa wawekezaji pekee, sio kushindana na wenyeji katika biashara ndogo kama uchuuzi na maduka madogo madogo.
Akizungumza baada ya kukutana na sehemu ya wafanyabiashara waliofanya maandamano wiki jana kulalamikia ushuru mpya wa KRA kuhusu shehena ya bidhaa za kutoka nje katika Ikulu ya Nairobi Jumatano, Rais aliagiza mawaziri husika kuharakisha mswada bungeni unaoharamisha aina fulani ya biashara kufanywa na raia wa kigeni.
"Tuko na wafanyabiashara kutoka nchi zingine, wacha nisiseme nchi gani, wamekuja hapa na kuwa wachuuzi, wanauza duvets. Bw Mukwana na Lee Kinyanjui, tayari tuko na mswada bungeni kuhusu mambo ya biashara. Katika hiyo bill, tumesema kuna biashara mgeni hawezi kufanya hapa Kenya by law. Nataka mketi chini na hawa wafanyabiashara muangalie na tuzibe mianya yote. Isitokee kwamba mtu ametoka China na amekuja kuwa hawker au kuuza duka kidogo hapo. Ichungwa, you don’t need any further instructions. Monday muamkie hiyo biashara. Hao wachuuzi wote wanafanya hii biashara kidogo kidogo wafunge na wasipofunga (ashangiliwa) tutafunga. Hatujajenga Investor Confidence ndio watu wakuje kuwa wachuuzi. Tumejenga Investor Confidence ndio watu wakuje kuwekeza," akasema Bw Ruto.
Katika maandamano ya Agosti 28, 2026, waandamanaji walikusanyika katika eneo la Archives kabla ya kuelekea makao makuu ya KRA katika jengo la Times Tower katikati mwa jiji.
Wafanyabiashara hao walisema mabadiliko ya kiwango kinachotumiwa kukadiria thamani ya bidhaa za uagizaji yameongeza gharama za biashara na kupunguza faida zao.
Kwa mujibu wao, KRA imepandisha kiwango cha ukadiriaji kutoka 2.5m hadi 3.2m, hatua wanayodai imeongeza kwa kiasi kikubwa kodi inayolipwa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hususan kutoka China.
Walisema mabadiliko hayo yamesababisha ongezeko la takriban asilimia 28, huku thamani ya bidhaa kwa madhumuni ya kodi ikiongezeka kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni.
Ruto aagiza sheria ipitishwe kuzuia wageni kufanya uchuuzi Kenya

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]