RAIS Samia Suluhu Hassan ametaka Tamasha la Kizimkazi kuwekwa kwenye orodha ya matamasha yanayotambulika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuwa miongoni mwa matamasha linalokuza utalii nchini. Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Agosti 24 alipozungumza katika kilele cha kufunga tamasha hilo lililodumu kwa wiki moja katika uwanja wa Mwehe, Kusini Unguja, Zanzibar. … The post Tamasha Kizimkazi kutambuliwa SMZ first appeared on HabariLeo.
Matukio mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Utalii wa Kasa katika Pango la Salaam (Salaam-Cave)Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 24 Agosti, 2024 The post Picha: Rais Samia ahudhuria uzinduzi wa Utalii wa Kasa Kizimkazi, Visiwani Zanzibar first appeared on Millard Ayo.
PRESIDENT Samia Suluhu Hassan directed the reinstatement of essential social services for the Ngorongoro Division residents The post State directs restoration of basic services in Ngorongoro first appeared on Daily News.
ASKOFU anayehubiri nchini Amerika alieleza Mahakama ya Nairobi mnamo Jumanne Agosti 20, 2024 kwamba hawezi kujihusisha na ulaghai wowote kwa vile ameekeza zaidi ya Sh1 bilioni humu nchini. Askofu David Nyamasyo Ndunda Kitonga aliyestawisha hoteli ya kifahari almaarufu Kitonga Resort iliyoko eneo la Mbiuni, Kangundo, Kaunti ya Machakos, alishangaa jinsi “anavyolaghaiwa kisha ashtakiwe kulaghai.” Askofu Kitonga alilalamikia mfumo wa haki humu nchini. Kupitia kwa wakili wake, Askofu Kitonga na mkewe Monica Ndunge Kitonga, walimweleza hakimu mkuu mahakama ya Milimani Susan Shitubi kwamba wameshangazwa na mfumo wa haki nchini. Bi Shitubi alifahamishwa kuwa wawili hao walioshtakiwa kumlaghai Gabriel Njenjere Chokera bao za ujenzi (TNG) za thamani Sh15, 199 ,240 wameshangaa sababu ya kushtakiwa. Mtu na mkewe hao walikana wakiwa na nia ya kulaghai walipokea bao za TNG kutoka kwa Gabriel Njenjere Chokera. “Hii ni deni. Hatuelewi sababu ya kuburutwa na kufikishwa kortini ilhali pia tunamdai mlalamishi,” wawili hao walimweleza hakimu huku wakiomba waachiliwe kwa dhamana. Wakili anayewawakilisha wawili hao alieleza Bi Shitubi, “Kitonga amewekeza humu nchini zaidi ya Sh1 bilioni. Atawezaje kushiriki ulaghai wa Sh15 milioni ilhali amewekeza mabilioni ya pesa katika mkahawa wa kifahari wa Kitonga Resort eneo la Mbiuni, Kangundo, Machakos?” Kiongozi wa mashtaka Wanjiru Waweru hakupinga wakiachiliwa kwa dhamana. Wakili wa mlalamishi (Njenjere) Henry Kurauka aliomba Kitonga na mkewe Ndunge washurutishwe kuweka pasipoti zao kortini kwa vile “wanaishi Amerika na wakirudi huenda wasirejee nchini kufanya kesi.” Mahakama iliwaachilia wawili hao kwa dhamana ya pesa taslimu Sh500, 000. Na wakati huo huo, Bi Shitubi aliwataka wawili hao waweke pasipoti zao kortini kama mojawapo ya sharti la dhamana. Sasa itabidi wawili hao wakitaka kusafiri wapewe idhini na mahakama. Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili, mhubiri huyo na mkewe wapewe mwelekeo jinsi kesi itakavyoendelea. [email protected]
A TOTAL of 79 households, comprising 367 people and 995 livestock, have voluntarily relocated from the Ngorongoro Conservation Area (NCA) to Msomera Village in Handeni District, Tanga Region. The post 79 households relocate from NCA to new settlements first appeared on Daily News.
MUITIKIO wa wananchi wanaoishi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kuhama kwa hiari umekuwa mkubwa baada ya leo jumla ya kaya 79 zenye watu 367 na mifugo 995 kuhama kutoka hifadhi hiyo kwenda kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga na maeneo mengine waliyochagua wenyewe. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii … The post Wananchi 367 hawama Ngorongoro first appeared on HabariLeo.
Na Mwandishi Wetu Wakati shughuli mbalimbali zikiendelea katika eneo la hifadhi ya ngorongoro wananchi wameendelea kuitikia wito wa kuhama kwa hiyari huku zikishuhudiwa jumla ya kaya 79 zenye watu 367 na mifugo 995, kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni na maeneo mengine waliyochagua wenyewe. Kuhama kwa wakazi hao ni matokeo ya uelimishwaji […]
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA), inakusanya mbegu za asili kwa ajili ya kuzihifadhi zisipotee, ikiwa ni pamoja na kuzifanyia tafiti. Mkuu wa Kitengo cha Taifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea kutoka TPHPA, Mujuni Sospeter amesema hayo jijini Dodoma alipozungumza na mwandishi wetu wa HabariLeo Amesema kutokana na tafiti … The post Mbegu za asili kufanyiwa utafiti first appeared on HabariLeo.
Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imewatoa hofu watanzania kuwa shughuli za utalii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zinaendelea vizuri pamoja na uwepo wa baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuandamana tarehe 18.08.2024. Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja, kitengo cha uhusiano na umma, Hamis Dambaya kupitia taarifa kwa umma aliyoitoa […]
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rc Ayoub Mohammed Mahamoud amekasirishwa na kukemea kwa tabia iliokisiri kwenye fukwa za Bahari za kusini na Zanzibar kwa Baadhi ya Ma Beach Boys kupora wake wa Watalii wanaoingia nchini kwa shughuli za kitalii jambo ambalo limekua likikasirishwa watalii waingia nchini Rc Ayoub ameyasema hayo kwenye semina ya waongoza […] The post RC akemea Beach boy kunyang’anya wake za watalii ZNZ first appeared on Millard Ayo.
Rubani mmoja amefariki baada ya helikopta kuanguka kwenye paa la hoteli moja katika mji wa Cairns kaskazini mwa Queensland. Ndege hiyo ilianguka kwenye hoteli ya DoubleTree majira ya 01:50 usiku kwa saa za eneo hilo siku ya Jumatatu, na kuwaka moto ambapo mamia ya wageni walihamishwa eneo salama. Mamlaka inasema mtu pekee aliyekuwa kwenye helikopta […] The post Rubani afariki dunia baada ya helikopta kuanguka juu ya hoteli Australia first appeared on Millard Ayo.
TWAHA Ahmed Omar ndiye mhudumu wa matembezi ya watalii ufuoni mkongwe zaidi kaunti ya Lamu. Akiwa na umri wa miaka 80, Bw Ahmed pia ni miongoni mwa wahudumu wakongwe zaidi ambao bado wameshikilia kuendelea kutoa huduma za matembezi ya watalii ufuoni Ukanda wa Pwani ya Kenya. Licha ya umri wake kusonga hadi kuitwa babu, Bw Ahmed anashikilia kuwa katu hatoiacha kazi hiyo hadi kifo kwani humfanya kujiona yeye bado ni kijana anayefaa kula ujana. Alianza kujishughulisha na utoaji huduma za watalii ufuoni akiwa umri wa miaka 18 pekee. Licha ya kisomo chake kuwa cha chini, akiwa aliachia darasa la sita pekee, Bw Ahmed anasema ni kupitia jukumu lake hilo la matembezi ya watalii ufuoni ambapo ameweza kujifunza lugha nyingi za kigeni, ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kitaliano, na pia vijilugha vya mtaani, ikiwemo Sheng. Kwa sababu yeye tayari ni kutoka jamii ya Waswahili wa asili ya Wabajuni wa Lamu, anaweka wazi kwamba Kiswahili hakikuwa tatizo kwake kukifahamu na kukizungumza kwani anakichukulia kuwa sawa na lugha ya mama. [caption id="attachment_157017" align="alignnone" width="300"] Mzee Omar, 80, akiwa mwingi wa bashasha wakati wa mahojiano. Picha|Kalume Kazungu[/caption] Kwa babu Ahmed, ni kawaida kwake kama ibada kumpata ufuoni akiwa amejifunga kikoi cheusi kiunoni huku akivalia fulana. Uso wake mara nyingi huwa haukosi tabasamu, hali ambayo mwenyewe anadai huwavutia watalii wengi kusaka huduma zake. “Nilianza kazi hii karibu miaka 60 iliyopita. Najua wengi wanashangaa kwa nini bado nasukumana kutekeleza majukumu haya yangu licha ya kubugia chumvi nyingi. Hawafahamu naipenda na siiachi kamwe hadi kifo,” akasema Bw Ahmed. Anashikilia kuwa siri ya kufaulu katika kazi hiyo ni kuinoa tabia yako kwa kuzingatia ukweli na uaminifu na pia ujuzi wa maeneo anayohudumia kwa kuitambua historia ya eneo anakoishi ndani na nje, kujua ni maeneo gani yanafaa kwa matembezi ya wageni, ni wakati gani mwafaka wa wageni au watalii kufurahia maandhari fulani. Pia anashauri wahudumu kujua kinagaubaga hali ilivyo ya usalama kwa watalii kwenye maeneo unakowatembeza. “Ukitaka ufaulu kwenye kazi yetu lazima uwe na tabia ya ukarimu. Tabasamu lako ni muhimu kwani ndilo linalovutia na kuwakaribisha watalii. Hutanipata nikiwa na sura iliyokunjamana hata ninapopitia msongo wa mawazo maishani. Kufanya hivyo ni sawa na kuwafukuza wageni,” akasema Bw Ahmed. Mhudumu huyo mkongwe aidha anachambua na kuchanganua sekta ya utalii ya zamani na ya miaka ya sasa ya karne ya 21 akisema kuna mabadiliko makubwa. Anasema miaka ya sitini (1960s) na tisini (1990s), sekta ya utalii Kenya ilishuhudia sana ujio wa watalii wa kimataifa. Bw Ahmed anaeleza kuwa hata wahudumu waliofanya kazi wakati huo hawakuwa wengi ikilinganishwa na miaka ya sasa ambapo kila mmoja, iwe kijana, mtoto na hata mzee utampata akitekeleza majukumu hayo. “Utapata miaka ya zamani watalii wengi tuliowapokeza hizi huduma za matembezi ufuoni walikuwa ni kutoka ng’ambo. Leo hii utapata sekta ya utalii ikisheheni wageni au watalii wa ndani kwa ndani tu. Utapata watalii kutoka Nairobi, Nakuru, Kisumu, Naivasha na kwingineko wakizuru Lamu kujivinjari,” akasema Bw Twaha. Mkongwe huyo pia anataja kuimarika kwa teknolojia katika ulimwengu wa leo ambao ni wa utandawazi kuwa jambo linalozidi kuibadilisha sekta ya utalii nchini na duniani kote. “Kitambo watalii walitegemea sana kuzuru hapa, ambapo walitutumia sana sisi wahudumu wa matembezi ya ufuoni kutafuta hoteli na sehemu zingine za kujivinjari na hayo yote yalimaanisha walitulipa fedha nyingi. Leo hii hilo halipo. Mtalii anaingia tu mtandaoni na kujitafutia hoteli na hata kuikodisha mapema kabla hajafika Kenya,” akasema Bw Ahmed. [caption id="attachment_157018" align="alignnone" width="300"] Mzee Omar akiashiria anavyotembeza wageni ufuoni Pate bila kuchoka licha ya umri wake mkubwa. Picha|Kalume Kazungu[/caption] Pia anataja tabia za kisasa za vijana wengi wanaojiita watembezaji watalii ufuoni kuwa zisizofaa na ambazo zinaharibia sifa wale watembezaji kindakindaki. Miongoni mwa tabia hizo ni matumizi ya dawa za kulevya na hata kuwa na tabia za ukali au kuwalazimisha watalii kukodisha huduma zao. Baadhi ya wakazi wanaomfahamu Bw Twaha hata hivyo wanamsifu kuwa mtu roho safi na mpenda wote. Bw Lali Omar, mkazi wa Kiwayu anasema Bw Twaha ni mjuzi wa karibu maeneo yote ambayo ni vivutio vya watalii si Lamu Mashariki tu bali pia kaunti yote. “Huyu babu anapendwa na watalii kwa sababu ya ukwasi wake wa taarifa kuvihusu vivutio vya watalii vipatikanavyo Lamu. Utampata kwenye ngome ya Siyu akiwaeleza watalii kuhusu historia yake. Utampata Pate akieleza jinsi himaya ya Sultan wa Uswahilini ilivyovuma karne ya 15 na 16. Utampata Shanga akikueleza kuhusu chimbuko la Wachina pale nakadhalika. Ni mwanahistoria tosha,” akasema Bw Lali. Adalyn Henry, mtalii kutoka Uingereza ambaye huja Lamu karibu kila mwaka, anasema yeye hupendelea sana kukodisha huduma za babu Ahmed kumtembeza ufuoni na kwenye vivutio vya Lamu kutokana na ukarimu wake. “Unapokuwa na Bw Ahmed hutaboeka. Atakupa stori za kuvutia kuihusu Lamu hadi uridhike. Hana tabia za usumbufu kwa watalii bali huhakikisha hata kukaa kwetu hapa kunasalia kuwa kwa kumbukumbu,” akasema Bi Henry. Mbali na Bw Ahmed, mhudumu mwingine mkongwe wa matembezi ya watalii ufuoni Kaunti ya Lamu ni Bw Ziwa Abdalla aliyetinga umri wa miaka 75 kwa sasa. Bw Abdalla naye ni mzaliwa wa mtaa wa Langoni kwenye mji wa kale wa Lamu. Amehudumu kama mtembezaji watalii ufuoni kwa miaka 55 sasa.
ZAMBIA: Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili amezitaka nchi za Afrika kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya utalii na kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Utalii. Pololikashvili ameyasema hayo katika mkutano wakati akifungua rasmi mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Utalii wa Shirika la … The post Mawaziri wa Utalii Afrika wakutana Zambia first appeared on HabariLeo.
Imeelezwa kuwa jamii inapaswa kuona na kukimbilia fursa zinazolenga kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa maendeleo kwani kwa kufanya hivyo ndio mwanzo wa mafanikio. Hayo yamezungumzwa leo na Mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya Afroroots iliyopo Mkoani Iringa, Agustino Festus wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Hoteli ya Sunset iliyopo Manispaa ya Iringa katika kikao kilicholenga […] The post Mafanikio huanza kwa kukutana na watu first appeared on Millard Ayo.
Nestled off the coast of Tanzania, Mafia Island is a serene paradise that remains a well-kept secret compared to its more famous neighbours of Zanzibar and Pemba. This unspoiled jewel offers an enchanting blend of natural beauty, rich history, and vibrant marine life, making it a must-visit destination for travellers seeking tranquillity and adventure. It […]
Nestled off the coast of Tanzania, Mafia Island is a serene paradise that remains a well-kept secret compared to its more famous neighbours of Zanzibar and Pemba. This unspoiled jewel offers an enchanting blend of natural beauty, rich history, and vibrant marine life, making it a must-visit destination for travellers seeking tranquillity and adventure. It […]
SEKTA ya utalii mjini Mombasa huenda ikazidi kudorora iwapo maandamano dhidi ya serikali yataendelea. Wadau katika sekta hiyo wamesema utalii hutegemea amani na huenda idadi ya watalii ikapungua iwapo hali ya utulivu haitashuhudiwa. Tayari baadhi ya hoteli zinasema asilimia 30 ya wageni wamefuta ziara zao wakihofia utovu wa usalama. Meneja wa mauzo katika hoteli ya Travellers , Carolynne Kurumei alisema kuwa hali hiyo imewalazimu kuwashawishi watalii angalau kubadili tarehe za ujio wao ili kupunguza idadi ya wale wanaoahirisha safari zao za kutembelea Kenya. “Tumeathiriwa sana na haya maandamano huku wageni wakihofia kuja Mombasa kwa mapumziko na hata mikutano,” alisema Bi Kurumei. Idadi ya wageni wapya kutoka mataifa ya nje kutaka kuzuru humu nchini pia imeenda chini kwa kiasi kikubwa. Mmoja wa washikadau katika sekta hiyo Mohammed Hersi, asema picha za kuogofya za utekaji nyara, mauaji na vurugu zinazopepereshwa hewani kutoka humu nchini zimewatia hofu wageni. Maswali “Watalii wanajiuliza kwa nini tuzuru Kenya wakati wenyeji hawana amani kwa sababu wanaona yote yanayojiri kwenye runinga zao,” alisema Bw Hersi. Kaunti ya Mombasa ni kitovu cha utalii hasa msimu huu wa likizo na sherehe. Wenye hoteli hutazamia kuvuna pakubwa kuanzia mwezi huu wa Julai na Septemba. “Tunaomba tu amani hali irejee kawaida kwani tunaelekea msimu wa sherehe na iwapo haya maandamano hayatasitishwa basi kutakuwa na kizungumkuti kupata wageni katika hoteli zetu, ” alisema Bi Kurumei. Katika hoteli ya Sarova Whitesands, meneja mkuu Francis Msengeti , anakiri kwamba kumekuwepo na wageni waliobadili tarehe za ujio wao ila takwimu zinaonyesha kuwa wengi wangetaka kuja ila hali ya maandamano imewaweka njia panda. “Tumeona wageni wakiahirisha safari zao baada ya kuagizia nafasi lakini tumeona pia wengi wao wangetaka kuja Mombasa kukamilisha likizo au mikutano yao,” alisema Bw Msengeti.
New tourism products are expected to be launched in the country, including bicycle tourism The post PS emphasizes strategies for attracting tourists to Ngorongoro first appeared on Daily News.
Mgeni wetu ni Julia Maureen, 22. Anasomea kozi ya Utalii katika shule moja mjini Nakuru. Yeye hupenda kusafiri na kutazama filamu. BONIFACE MWANGI|TAIFA
Wageni sita wa Vietnam na Marekani walikutwa wamekufa katika chumba cha hoteli huko Bangkok, huku sumu ikizingatiwa kuwa inawezekana. Tukio hilo lilizua wasiwasi na maswali kuhusu hali ya vifo vyao. Matokeo ya Uchunguzi na Uchunguzi wa Maiti: Mamlaka ilianzisha uchunguzi kuhusu vifo hivyo ili kubaini chanzo. Uchunguzi wa maiti ulifanywa kwa watu waliokufa ili kukusanya […] The post Wageni 6 wa Vietnam na Amerika walipatikana wamekufa katika chumba cha hoteli. first appeared on Millard Ayo.
Na Renatha Kipaka, Bukoba Wamiliki na mameneja wa hoteli mkoani Kagera wameiomba serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuchukua jukumu la kuwa mawakala wa kuuza na kutengeneza mashine za risiti za kielektroniki (EFDs) ili kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara unaotokana na kufuata huduma hizo mbali. Ombi hilo limetolewa juzi wakati wa kikao baina ya maafisa […]
MAGAVANA sita wa Pwani wamesafiri Italia kusaka fedha za miradi ya maendeleo katika sekta ya Uchumi wa Baharini. Kupitia muungano wao wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani (JKP), magavana hao, wakiongozwa na mwenyekiti wao Bw Gideon Mung’aro (Kilifi), Abdulswamad Nassir (Mombasa), Fatuma Achani (Kwale)Dado Godhana (Tana River), Issa Timamy (Lamu), na Andrew Mwadime (Taita Taveta), wanasaka fedha za kuimarisha sekta ya uchumi wa baharini ili kufufua uchumi na nafasi za ajira kwa vijana. Bw Mung’aro alisema magavana hao wa Pwani waliamua kusafiri hadi Italia kusaka wawekezaji wa sekta hiyo ili kuimarisha uchumi wa baharini.Alisema wanalenga kununua mashua kubwa ambazo zitawasaidia wavuvi kuvua samaki katika bahari kuu. “Hii ni safari ya magavana kupitia muungano wetu wa JKP, magavana wote na idara zetu zote za uchumi wa baharini katika kila kaunti na hata wawakilishi kutoka serikali ya kitaifa. Tunaenda kujadili maswala ya kukuza uchumi wetu kupitia sekta ya uchumi wa baharini,” alisema Bw Mung’aro. Bw Mung’aro alisema magavana hao pia watafanya mkutano na Waziri anayehusika na masuala ya Kigeni na Biashara. “Ni mkutano ambao tunaenda kusaka ufadhili wa uchumi wa baharini hasa wavuvi. Unaona Kilifi tayari nimeanzisha boti 43. Ninataka kuendeleza sekta hii, awamu ya pili tunalenga kupeana boti kubwa ambazo zinaweza kwenda katika maji makuu,” aliongeza Bw Mung’aro. Baadaye, Bw Mung’aro atakutana na viongozi wakuu wa serikali ya Italia. Gavana huyo ambaye ana uhusiano wa karibu na Waitaliano kupitia marafiki zake akiwemo bwanyenye mashuhuri Bw Flavio Briatore, alisema atatumia fursa hiyo kusaka wawekezaji. Alisema kuwa alipokuwa meya wa Malindi zaidi ya miaka 15 iliyopita, aliunda uhusiano wa karibu na Waitaliano. Aliwarai kina mama kutoka eneo la Pwani kujitosa kwenye sekta ya uchumi samawati hasa uvuvi. “Nina bahati kwa sababu nitakuwa na mikutano na baadhi ya mawaziri wa Italia kuhusu swala la kufufua utalii. Unajua binafsi waziri mpya wa Utalii huko Italia ni rafiki yangu mkubwa, tumekuwa naye miaka mingi tunajuana akiwa Malindi, ni rafiki ya rafiki zangu kama Bw Briatore. Naibu Waziri wa Fedha pia ni rafiki yangu,” alisema Bw Mung’aro. Bw Briatore anamiliki hoteli kubwa mji wa kitalii wa Malindi ambao kwa muda umekuwa ukimilikiwa na raia wa Italia Hata hivyo, wakati wa janga la Covid-19 mwaka wa 2020, Waitaliano wengi walihepa Malindi na kurudi makwao. Bw Mung’aro alisema atawaregesha raia hao ambao walikuwa wamewekeza katika mji huo na wengine wapya ili kufufua sekta ya utalii wa kimataifa. “Tulikutana na Balozi wa Kenya nchini Italia, Bw Fredrick Matwang'a, kujadili maswala ya kukuza sekta ya uchumi samawati,” aliongeza. Gavana huyo alisema pia atajadili swala la upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malindi. “Waitaliano wameapa kushirikiana nasi kwenye upanuzi wa kiwanja hicho cha ndege ili kukuza sekta ya utalii. Ndio maana nimetilia mkazo umuhimu wa umoja wa Wapwani,” aliongeza.
DAR ES SALAAM; Samaki kaa wajulikanao kama ‘tuyuli’ wapo hatarini kutoweka kutokana na kuonekana kwa uchache katika maeneo ya ukanda wa Pwani. Ofisa Habari wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Ivan Kimaro amesema hayo alipozungumza na HabariLEO Digital na kueleza kuwa sifa kubwa ya samaki hao ni wakubwa na wana uwezo wa kupanda mti … The post Kaa wanaoangua nazi hatarini kutoweka first appeared on HabariLeo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kufanya filamu nyingine ya Royal Tour katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kujionea wanyamapori mbalimbali katika Hifadhi hiyo. Dkt. Samia ameyasema hayo leo Julai 15, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi. Kauli hiyo […] The post Rais Samia aahidi kufanya ‘Royal Tour’ kuitangaza hifadhi ya Katavi first appeared on Millard Ayo.
NA Mwandishi wetu Wananchi wa tarafa ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro wameendelea kuishi maisha magumu kutokana na Kushambuliwa na wanyama wakali kufuatia matukio yanayoendelea kutokea katika eneo hilo. Afisa tarafa wa eneo hilo bwana Bahati Mfungo amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali imekuwa ni ya kutisha. Katika matukio ya […]
DAR ES SALAAM; MTAFITI mwandamizi aliyepaisha Hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma kwa kutafiti kuhusu maisha na tabia za sokwe, Dk Jane Goodall ametimiza miaka 90, huku utafiti wake kuhusu wanyama hao ukitimiza miaka 64. Dk Goodall chini ya taasisi yake ya Jane Goodall (JGI) alifanya utafiti huo tangu mwaka 1964 na kuufanya kuwa utafiti … The post Aliyetafiti kuhusu sokwe afunguka wanavyopungua first appeared on HabariLeo.
KIGOMA:Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji imempa jina la barabara Mwanamazingira maarufu duniani Mama Jane Goodall kwa mchango wake katika uhifadhi na utunzaji mazingira mkoani Kigoma sambamba na mchango wake wa kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Gombe. Uzinduzi wa jina hilo la mtaa umefanywa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango ambaye amesema kupewa jina la … The post Jane Goodall apewa barabara Kigoma Ujiji first appeared on HabariLeo.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) hiyo kuhakikisha miradi ya ujirani mwema inayotekeleza ijikite katika kutatua changamoto ya wanyama wakali na waharibifu. Kairuki amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo yaliyopo Mkoani Morogoro ambayo ililenga kusikiliza changamoto na … The post Kairuki ataka TAWA kuongeza mapato, kudumisha ujirani mwema first appeared on HabariLeo.
Na Joyce Ndunguru, Morogoro Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za wanyamapori. Kairuki ametoa pongezi hizo leo Julai 8,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo mkoani Morogoro kwa lengo la kusikiliza changamoto […]
Katibu tawala Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Saidi Nguya amesema Uwepo wa huduma mbovu katika Baadhi ya ofisi za Serikali katika Halmashauri hiyo umetajwa kusababishwa na kukosekana kwa muda maalumu wa Kuwapa nafasi za kupumzika watumishi wa kada za Watunza kumbukumbu, waandishi waendesha ofisi(PS) pamoja na wahudumu Nguya ameyasema hayo wakati akizungunza na watumishi wa […] The post Das Mvomero Saidi Nguya aongoza wafanyakazi kutalii Hifadhi ya Mikumi first appeared on Millard Ayo.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ameshiriki mbio za Great Ruaha Marathon zilizofanyika ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha Ambapo lengo la kufanya mbio hizo ni kukuza utalii wa kusini na kutoa hamasa kwa jamii katika kuhifadhi mazingira Akitoa hotuba kwa washiriki wa Mbio za Great Ruaha Marathon katika […] The post Waziri mkuu ashiriki Marathon Iringa first appeared on Millard Ayo.
Ule wakati umewadia! ni msimu wa SABASABA! Unakaribishwa kwenye BANDA la GSM Group of Companies the super brands uweze kujipatia bidhaa zetu. Twenzetu Sabasaba na GSM! Banda lipo karibu na mali asili na utalii karibuni sana na hizi ni baadhi picha kutokea kwenye bando hilo lenye bidhaa mbalimbali zilizosheeni. The post Umeenda Sabasaba? Hizi ni picha zikionesha bidhaa zinazopatikana GSM Group of Companies first appeared on Millard Ayo.
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Watumishi wa kada mbalimbali wa Wilaya ya Mvomero, wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Saidi Nguya, wameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha na kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Akizungumza na mwandishi […]
Na Beatus Maganja, Dar es Salaam. MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam kuhamasisha Watanzania wawekezaji na wageni kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza katika maeneo inayoyasimamia. Akizungumza na wageni waliotembelea banda la TAWA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, […]
Ule wakati umewadia! ni msimu wa SABASABA! Unakaribishwa kwenye BANDA la GSM Group of Companies the super brands uweze kujipatia bidhaa zetu. Twenzetu Sabasaba na GSM! Banda lipo karibu na mali asili na utalii karibuni sana na hizi ni baadhi picha kutokea kwenye bando hilo lenye bidhaa mbalimbali zilizosheeni. The post Picha: Kutokea Sabasaba hawa ni GSM Group Of Companies, hizi ndio bidhaa utakazozikuta first appeared on Millard Ayo.
IRINGA; Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 06, 2024 ameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon 2024 zilizofanyika katika hifadhi ya Ruaha, mkoani Iringa. Isome pia:https://habarileo.co.tz/majaliwa-atoa-maelekezo-vikundi-vya-jogging/ Mbio hizo zinalenga kukuza utalii wa Kusini na kutoa hamasa kwa jamii kuhifadhi mazingira kwenye vyanzo vya maji vya Mto Ruaha mkubwa. Isome pia:https://habarileo.co.tz/mambo-yaiva-great-ruaha-marathon/ Aidha, lengo jingine ni kuhamasisha … The post Waziri Mkuu ashiriki Great Ruaha Marathon first appeared on HabariLeo.
THE Ngorongoro Conservation Area Authority has officially begun conducting all transactions in Tanzanian shillings, replacing US dollars The post NCAA moves to settle transactions in shillings first appeared on Daily News.
Haya ni maandamano ya kipekee yaliyotokea kwenye barabara ya Moi jijini Nairobi huku waandamanaji wakibeba na kuangusha majeneza matupu, wakifunga barabara karibu na Kituo cha Bazaar mkabala na Hoteli ya Clarion. Kitendo hiki cha ishara kilikusudiwa kuwaomboleza Wakenya waliopoteza maisha wakati wa maandamano yanayoendelea ya kupinga Mswada wa Fedha. Zaidi ya majeneza 10 yaliyokuwa yamepambwa […] The post Waandamanaji Kenya watupa majeneza matupu barabarani first appeared on Millard Ayo.
DAR ES SALAAM; SERIKALI imeshauriwa kufanya uchunguzi huru ili kubaini na kukomesha matukio ya utekaji yanayoendelea nchini. Zitto ameshauri hivyo leo Julai 2, 2024 kuhusu kuripotiwa tukio la kutoweka mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Edgar Mwakabela maarufu kama ‘Sativa’ anayedaiwa kutoweka Juni 23, 2024 na kupatikana Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya … The post Zitto ataka uchunguzi huru vitendo vya utekaji first appeared on HabariLeo.
Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki umetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye banda lao ili waweze kujifunza na kufaidika na ofa zinazotolewa kwa watakaohitaji kutembelea hifadhi za misitu zilizopo nchini. Akizungumza Julai 1, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Kuhamasisha Utalii wa TFS, Anna Lauwo, alipotembelea banda […]
Na Mwandishi wetu, Arusha. Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imesema itaendelea kuelimisha, kuthaminisha na kuhamisha wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ambao wanajiandikisha kuhama kwa hiyari yao wenyewe na haitayumbishwa na kelele za baadhi ya vikundi vya watu wanaowatumia wananchi hao kupata kipato kupitia baadhi ya mashirika duniani. Akizungumza na waandishi […]
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewakaribisha wakazi wa mkoa huo kujitokeza kushiriki Mbio za Great Ruaha Marathon ili kuendelea kuupa thamani Mkoa katika utalii. Serukamba amezungumza hayo leo akiwa ofisini kwake ambapo huku akitaja kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika msimu huu […] The post Waziri mkuu Kassim Majaliwa mgeni rasmi Great Ruaha Marathon first appeared on Millard Ayo.
BAMBURI, MOMBASA KALAMENI mmoja alipoteza kazi ya meneja wa hoteli baada ya wafanyakazi vipusa kulalamika kwa mwajiri wao kwamba alikuwa akiwasumbua akitaka wamlishe uroda. Jamaa alikuwa akirushia vipusa mistari na kuanza kuwahangaisha wakikosa kumeza chambo. Kitumbua chake kiliingia mchanga juzi, vipusa aliokuwa akinyanyasa na aliopendelea walipomweleza mwenye hoteli aliyemtimua kwa kupotoka kimaadili. Wakati huo huo, huko Mtwapa, Kilifi, mwandada alimkemea rafiki yake akimlaumu kwa kumshawishi kaka yake asimuoe. Urafiki wa wawili hao ulianza wakiwa wanafunzi wa sekondari na demu hakutarajia mwenzake angemchomea picha kwa kaka yake alipokubali kuwa mpenzi wake. “ Demu alipata habari kwamba mwenzake alimuonya kaka yake dhidi ya kumuoa. Alimpaka tope akisema anapenda pesa sana na angemuacha iwapo angefilisika. Alipopata habari hizo, mwanadada alimkabili shemejiye mtarajiwa na kumchemkia kwa hasira kwa kumharibia uhusiano wake na kaka yake,” alisema mdokezi. Wawili hao walirushiana cheche kabla ya mashoga wao kuingilia kati na kuwatuliza.
Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezitaka baadhi ya taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka ndani na nje ya nchi kuacha upotoshaji kuhusiana na zoezi la kuhamisha wananchi kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wanaojiandikisha kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera na badala yake kutafuta ukweli kuhusu suala hilo. […]
ARUSHA; ASKARI wa Jeshi USU la Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Zuberi Msemo na watoto wake watatu wamekufa kwa kuungua na moto unaosadikiwa ulitokana na kulipuka kwa simu au kompyuta mpakato. Tukio hilo lilitokea eneo la Matejo juzi usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa Msemo na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. … The post Moto waua askari Tanapa, watoto wake 3 first appeared on HabariLeo.
Na mwandishi wetu. Wananchi wa jamii ya kimasai wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wamefanya tamasha la kimila la kiutamaduni huku wakisema kwamba wataendelea kuhama kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine nchini Tanzania. Kufanyika kwa tamasha hilo la kiutamaduni ambalo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kabila hilo limefuta […]
MBEYA: JITIHADA zilizofanywa kufukua Mto Mambi ulioko Mbarali mkoani Mbeya zimerejesha furaha kwa wakazi wa vijiji vya Chamoto na Uhambule ambapo wameondokana na athari za nyumba zao kusombwa na maji na mazao kuathiriwa. Wizara ya Maliasili na Utalii imetekeleza jitiada hizo kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW). … The post Ufukuaji mto waondoa athari za mafuriko Mbarali first appeared on HabariLeo.