
HABARI ZA SAA, SAA SITA NA DAKIKA 55 - NOVEMBA 20, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania

TUNAPOKARIBIA uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027, ni wazi kuwa chama cha ODM kiko tayari kuendelea kuwa katika muungano wa Serikali Jumuishi na kuimarisha muungano huo ili uchukue uongozi wa urais katika uchaguzi huo. Ikiwa hili litaafikiwa basi kuna uwezekano kuwa Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki hatakuwa mgombea mwenza Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Hili linajitokeza katika kauli za viongozi wa ODM ambao wanazidi kusisitiza kuwa iwapo chama hicho kitaendelea kuwa katika Serikali Jumuishi kwa lengo la kuunda serikali ijayo, sharti kuwe na mazungumzo ili kuwa na mkataba mpya kati ya ODM na UDA. Kulingana na baadhi ya viongozi katika chama cha ODM, chama hicho kina wafuasi wengi wala hakiwezi kukubali kukaa katika Serikali Jumuishi hadi wakati wa uchaguzi ujao bila makubaliano yatakayokipa chama hicho nafasi zaidi za uongozi. Wapo waliokiri kuwa sharti ODM ipate cheo cha naibu wa rais katika uchaguzi wa mwaka 2027. Rais Ruto anaonekana kukubaliana na kauli za viongozi wa ODM anapowaambia kuwa yeye anaelewa siasa na chama cha ODM kinahitaji kujipanga naye atawapanga ‘wale wengine’ halafu watakutana waunde serikali pamoja. Swali ni je, katika huko kuwapanga wale wengine Rais Ruto atakubali mapendekezo ya ODM ya kuteua naibu wa rais kutoka kwa chama hicho? Ikiwa Rais atakubali mapendekezo ya ODM basi Prof Kindiki atakosa kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Ingawa Kindiki anaendelea kuimarika kama mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi katika ukanda wa Mlima Kenya, eneo lililokuwa ngome ya Rais Ruto katika uchaguzi wa 2022, nafasi yake ya unaibu wa urais inahatarishwa na kuwa sasa Mlima Kenya umegawanyika kisiasa. Ni bayana kuwa asilimia kubwa ya wapigakura kutoka Mlima Kenya ilimuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi wa 2022. Kubanduliwa kwa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua mamlakani kumesababisha baadhi ya wapigakura katika ukanda huo kuunga mkono upinzani, jambo linaloponguza kapu la kura za Serikali Jumuishi katika ngome ya Prof Kindiki. Ikiwa upinzani utaendelea kukita mizizi katika Mlima Kenya, huenda Rais Ruto akakosa kumteua Kindika kuwa naibu wake katika uchaguzi mkuu wa 2027 ili kumteua naibu rais kutoka ODM kwa lengo la kuungwa mkono na wafuasi wa chama hicho. Prof Kindiki amekuwa ngao ya utawala katika serikali ya Rais Ruto. Kuteuliwa kwake kama naibu wa rais kulilenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya na Rais Ruto hasa baada ya kumbandua Gachagua mamlakani. Masharti ya ODM yanazua wasiwasi ya kisiasa Mlima Kenya na iwapo Prof Kindiki hatakuwa mgombea mwenza wa Rais katika uchaguzi ujao, huenda uhusiano huo ukapungua kwa kiwango kikubwa na ufuasi wa Dkt Ruto katika ukanda huo kudorora zaidi.

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imepokea taarifa ya awali ya Kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, Sura ya 353. Akizungumza Dodoma, leo Dssemba 30, 2025 katika kikao cha Kisekta cha kupokea taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, amesema Sheria ya … The post Serikali yapokea taarifa ya awali mapitio sheria ya elimu first appeared on HabariLeo.

UWEKEZAJI uliofanywa na serikali katika Bandari ya Tanga umeanza kuleta tija kutokana na ongezeko la shehena za mizigo kutoka mataifa mbalimbali katika bandari hiyo. Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti HabariLEO kupitia vyanzo na njia mbalimbali, uboreshaji huo umefungua fursa mbalimbali za uwekezaji si tu kwa usafirishaji wa mizigo, bali pia katika sekta nyingine kama … The post Uwekezaji Bandari ya Tanga wazaa matunda, fursa lukuki first appeared on HabariLeo.

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Joyce Mwasumbi, mkazi wa Kijiji cha Kanazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge chumbani kwake. Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kanazi, Rudis Ulaya amesema tukio la mwanamke huyo ambaye ni mke wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT, Ibrahimu Mwaipopo katika kijiji hicho … The post Mke wa mchungaji ajinyonga siku moja kabla ya Krismasi first appeared on HabariLeo.

IDARA ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) imewataka Wakenya wakome kueneza uvumi kuhusu chanzo cha kifo cha mbunge wa zamani wa Lugari, Bw Cyrus Jirongo. Mkurugenzi wa DCI, Bw Mohamed Amin, alisema uchunguzi uliofanywa kufikia sasa umeonyesha chanzo cha kifo hicho kilikuwa ni ajali ya barabarani, ingawa uchunguzi zaidi unaendelezwa. “Hili ni tukio linaloendelea kuchunguzwa. Hadi sasa, uchunguzi unaonyesha kuwa ilikuwa ajali ya barabarani,” alisema akiwa Diani, Kaunti ya Kwale mnamo Alhamisi. Wakati uo huo, Bw Amin aliwahakikishia Wakenya usalama wao wakati wa msimu wa sikukuu, akisema hali ya usalama nchini kwa ujumla ni shwari licha ya visa vichache vya uhalifu na migogoro ya kijamii katika baadhi ya maeneo. Bw Amin alisema kuwa polisi wameongeza doria na operesheni za kijasusi kote nchini ili kulinda wananchi na wageni. “Tumeona ongezeko la baadhi ya visa vya kikatili, vikiwemo mauaji na biashara ya dawa za kulevya, lakini hali inadhibitiwa. Usalama wa wananchi ni suala ambalo tumelipa kipaumbele,” alisema Bw Amin. Alikiri kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika maeneo ya Trans Mara na Tana River, akisema vimedhibitiwa kwa sasa. Tayari Trans Mara, polisi wamewakamata washukiwa watano wanaodaiwa kuhusika na kuchochea ghasia, hali iliyosababisha kupungua kwa uhasama. Katika Kaunti ya Tana River, washukiwa watano walikamatwa kuhusiana na ghasia ambazo zimekuwa zikiibuka mara kwa mara. Bw Amin aliwataka wakazi wa Tana River wanaomiliki silaha haramu kuzisalimisha kwa hiari na haraka iwezekanavyo. “Nawasihi wote wenye silaha haramu katika eneo hilo wazisalimishe kwa hiari ili kurejesha amani ya kudumu ama hatua zitachukuliwa dhidi yao,” alisisitiza. Mkuu huyo wa DCI pia alitaja kukamatwa kwa maafisa wa polisi wa trafiki na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kama njia moja ya kupambana na ufisadi nchini. EACC ilikamata maafisa wawili wa trafiki Jumanne, katika barabara ya Likoni-Lungalunga wakidaiwa kuitisha hongo kutoka kwa wenye magari. “Hatutavumilia ufisadi wa aina yoyote. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa dhidi ya afisa yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo vya ufisadi,” aliongeza. Aliwahimiza wananchi wazidi kuwa makini na kuripoti mienendo yoyote ya kutiliwa shaka, akisema maafisa wa polisi wako kazini saa 24 kwa siku kote nchini. Vyombo vya usalama vimesema doria zilizoboreshwa na ushirikiano wa karibu na jamii utaendelea kuimarishwa kipindi chote cha sikukuu.

KIONGOZI wa ODM, Dkt Oburu Oginga, amewataka viongozi wazime mgawanyiko wakati ambapo tofauti zinazidi kuhusu chama kumuunga au kutomuunga Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa 2027. Akiongea wakati wa ibada ya Krismasi katika St Peter ACK Bondo, Kaunti ya Siaya, Dkt Oginga alisema kuongoza ODM ni jukumu gumu na atafanikiwa tu iwapo atapata uungwaji mkono wa wabunge na kuzimwa kwa maasi ya ndani. “Hili jukumu ni zito na nitafanikiwa tu mkiwa nyuma yangu. Nitawatumikia tu mkiniunga mkono hata kama sitoshei ndani ya viatu vya Raila Odinga,” akasema. Seneta huyo wa Siaya alisema hana nia ya kuongoza kwa udikteta akisema ODM itafanikiwa kusalia na umaarufu kupitia tu maoni kinzani kuvumiliwa na mashauriano. “Sitaki hali ambapo Dkt Oburu akisema tuende kushoto au kulia inakua hivyo. Lazima tushauriane, tuchukue msimamo mmoja na tuzungumze kwa sauti moja,” akasema. Seneta huyo wa Siaya alipuuza madai kuwa ODM inaendelea kupoteza umaarufu wake akisema wanamakinikia kupigania maslahi ya Wakenya. “Hiki chama hakitagawanyika wala kusambaratika. Kinaendelea mbele kupigania haki za Wakenya na hakuna kurudi nyuma,” akasema. Licha ya kutounga mkono Rais Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa 2022, Dkt Oginga alisema watasalia ndani ya Serikali Jumuishi hadi 2027. “Tuko serikalini huku tukijiimarisha. Hii serikali tuliingia kupitia dirishani kwa sababu hatukuichagua na tutashirikiana nayo hadi 2027,” akasema huku akishikilia hoja 10 zilizo msingi za muungano wao na UDA lazima zitekelezwe. Dkt Oburu ambaye alihudumu kama Mbunge wa Bondo kutoka 1994 hadi 2013, alisema kuwa ODM ipo serikalini kuhakikisha maeneo yao yananufaika na miradi ya serikali baada ya kubaguliwa na tawala za nyuma. “Kitambo tufike 2027, maeneo yetu yatakuwa yameendelea na unaona jinsi ambavyo Rais Ruto anavyojizatiti,” akasema. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa ibada kuandaliwa katika kanisa hilo baada ya mauti ya Kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo Oktoba 15. Raila, Dkt Oginga na familia ya Jaramogi wamekuwa wakihudhuria ibada ya Krismasi kanisani humo kila mwaka. Dkt Oginga aliandamana na Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi na Mbunge Mwakilishi wa Kaunti ya Kisumu Ruth Odinga, dadake Raila pamoja na wanasiasa wengi kutoka Nyanza. “Kile ambacho Rais Ruto anatupa ni kilicho chetu wala hatujakuwa cha mwingine. Miradi yote tunayopewa tunastahili kuwa nayo,” akasema. Wiki jana, Dkt Oginga alisema kuwa ifikapo Juni 2026, ODM itakuwa imefanya uamuzi wa kumuunga au kutomuunga mkono Rais mnamo 2027. Kauli yake ilipingwa na Gavana wa Siaya, James Orengo na Katibu wa ODM, Edwin Sifuna ambao walisema kazi ya kuamua mkondo ambao chama kitachukua kuhusu 2027 si suala la kuamuliwa na mtu mmoja. Hata hivyo, Bw Wandayi amesisitiza kuwa katiba ya ODM inampa kiongozi wa chama mamlaka ya kuamua mwelekeo na uamuzi huo unastahili kuidhinishwa na ngazi za chama. “Kiongozi wa chama ana jukumu la kuongoza chama na wanachama kwenye majadiliano ya miungano. Baada ya kufanya uamuzi huo, unawasilishwa kwa Baraza Kuu la Chama na kuidhinishwa,” akasema Bw Wandayi. Waziri huyo alimtaka Dkt Oginga atoe mwekelekeo huo kufikia Machi mwaka ujao badala ya Juni kuepusha wafuasi wa ODM kuchanganyikiwa.

WANASIASA wakuu na maafisa wa serikali wanaomezea mate nyadhifa katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 waligeuza sherehe za Krismasi msimu wa kampeni kwa kumwaga mamilioni kupitia misaada ya chakula na kufadhili michuano ya kabumbu. Yamkini ulikuwa wakati wa kushiriki zawadi za Krismasi lakini kutokana na idadi kubwa iliyoshuhudiwa kupitia picha zilizonaswa na kusambazwa na wanasiasa, ilikuwa ukumbusho wa viwango vya ufukara nchini ambavyo wanasiasa wameendelea kutumia ili kujinufaisha kisiasa. Katibu wa Wizara ya Afya, Dkt Ouma Oluga na mwenzake wa Kawi, Alex Wachira, ni miongoni mwa maafisa wa serikali waliovamia vijiji kutoa misaada kwa wasiobahatika. Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki alikaribisha mamia ya majirani zake kusherehekea Sikukuu ya Krismasi makazini mwake Irunduni, Kaunti ya Tharaka-Nithi, ambapo wanawake walipokea zawadi za chakula na wanaume pesa taslimu katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia Krismasi. Mnamo Disemba 18, Gavana Susan Kihika na mume wake Sam Mburu waliwakaribisha maelfu ya wakazi makazini mwao, Ngata, ambapo walisambaza bidhaa zikiwemo mafuta ya kupikia, unga wa mahindi, ngano, sukari, mchele, majani chai na sabuni. Kule Nyandarua, viongozi wanaoegemea mrengo wa Rais William Ruto, Sikukuu ya Krismasi walizunguka kaunti wakisambaza zawadi, kumpigia debe rais huku wakisambaza bidhaa za chakula, nguo na malazi. Mwakilishi Mwanamke, Faith Gitau na Diwani wa Ndaragwa, Mwangi Kagwe walitumia Krismasi wakisambazia wakazi zawadi. Mnamo Disemba 17, Gavana wa Kericho, Dkt Erick Mutai, vilevile alikaribisha mamia ya wakazi nyumbani kwake, Chesingoro, ambapo, kulingana na waliohudhuria, alifanya kampeni ya kuwania muhula wa pili. Seneta wa Vihiga Godffrey Osotsi aliandaa tamasha ya mziki iliyoshirikisha kwaya za madhehebu mbalimbali na kufadhili mashindano ya Mpira wa Kadanda. Gavana Gladys Wanga naye alisambaza misaada ya chakula usiku wa kuamkia Krismasi ambapo mamia ya wakazi walikusanyika nyumbani kwake Kochia kupokea mifuko ya mchele na maharage. Siku yenyewe ya Krismasi Mbunge wa Kisumu ya Kati, Joshua Oron aliandaa tamasha zake za kila mwaka za Krismasi zilizovutia mamia ya wakazi na familia za mitaani. Seneta wa Kisumu, Tom Ojienda, anayemezea mate ugavana, alishiriki Krismasi na wakazi nyumbani kwake Awasi. Katika Kaunti ya Nyeri, Bw Wachira aliandaa hafla mbili usiku wa kuamkia Krismasi katika eneobunge la Kieni ambapo alisambaza zawadi na kuitisha umoja Mlima Kenya. Gavana wa Murangá Irungu Kang'ata, Seneta Mteule Veronica Maina na Mbunge wa Gatanga, Edward Muriuki, walijitokeza wakiwa na unga wa mahindi, ngano, mchele na mafuta ya kupikia kwa raia maeneo yao kusherehekea Krismasi. Bw Kang'ata aliepuka mikutano ya hadhara kwa kutumia teknolojia kusambaza zawadi zake za Krismasi. Katika Kisii, Gavana Simba Arati alizuru hospitali ambapo aliwapa wagonjwa zawadi.

SERIKALI ya Kenya Kwanza inapanga kukarabati Barabara ya Ikulu ya Nairobi kwa gharama ya Sh1.6 bilioni. Taarifa zilizomo katika notisi ya zabuni iliyotolewa Desemba 19 zimeorodhesha kazi zilizokusudiwa kuwa sehemu ya miradi 92 ya ukarabati wa barabara nchini kote. Serikali imekadiria kuwa miradi hiyo itagharimu takriban Sh15.6 bilioni kwa jumla. Hati hiyo, iliyotiwa saini na Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Barabara za Mijini (KURA), inaelezea zabuni hiyo kama hatua ya kuimarisha ubora wa Barabara ya Ikulu." Barabara hiyo ni muhimu sana kwani inaunganisha CBD na maeneo muhimu kama vile Ikulu na afisi za serikali zilizo karibu. Polisi mara nyingi wamelazimika kuimarisha usalama na kuzuia watu kufika eneo hilo hasa wakati wa maandamano kama vile maandamano ya Gen Z ya 2024 dhidi ya Mswada wa Fedha. Mnamo Oktoba mwaka huu, afisa wa Kitengo cha Utumishi Mkuu (GSU) anayelinda Ikulu aliuawa wakati raia alipomvamia kwa mshale karibu na lango, na kusababisha wasiwasi kuhusu usalama katika eneo hilo. Kando na Barabara ya Ikulu, zabuni nyingine iliyoorodheshwa kugharimu zaidi ya Sh1 bilioni ni ujenzi wa Barabara ya Chelimo katika Mji wa Kericho kwa gharama inayokadiriwa ya Sh1.1 bilioni. Miradi yote itafadhiliwa na Serikali ya Kenya chini ya KURA. "Ili kuimarisha usawa, walengwa watawasilisha zabuni zisizozidi mbili (2), lakini wanaweza tu kupewa kiwango cha juu cha zabuni moja (1), chini ya notisi hii ya zabuni. Wale watakaotuma zabuni zaidi ya mbili (2) wataondolewa," notisi hiyo inasema kwa sehemu. Miradi mingine muhimu ya barabara iliyoorodheshwa ni pamoja na ukarabati wa barabara za Mji wa Gede-Kakuyuni katika Kaunti ya Kilifi kwa gharama ya Sh967.5 milioni, ujenzi wa barabara kuu za Eldoret City kwa Sh950 milioni, na uunganishaji wa barabara ya Oginga Odinga kutoka Subukia hadi mzunguko wa Westmall katika Kaunti ya Nakuru kwa gharama ya Sh850 milioni. Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya alitaja miradi hiyo katika Kaunti ya Kilifi kuwa hatua ya mabadiliko katika eneo hilo, akisema imekuwa ikitengwa kwa miongo mingi.

RAIS William Ruto na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta wamejipata ndani ya mzozo ambao unatishia kusambaratisha ODM kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Mirengo inayozozona ndani ya ODM sasa inalaumiana kuhusu madai ya kuuza chama hicho kwa Rais Ruto na Bw Kenyatta kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao. Viongozi wa ODM wanaounga mkono Serikali Jumuishi wamedai kuwa kuna njama ya kurejesha chama upinzani kwa kuinadi kwa Bw Kenyatta ambaye ni kiongozi wa Jubilee. Hata hivyo, wale wanaopinga ushirikiano wa ODM na serikali wamezungumzia mpango wa kuuza chama kwa Rais Ruto. ODM kwa sasa inaonekana imebaki yatima baada ya kifo cha Kinara wake Raila Odinga ambaye alihakikisha udhabiti wake kwa miaka 20 aliyoiongoza tangu ibuniwe. Kambi ambayo inapinga chama kushirikiana na Rais ni Katibu Mkuu Edwin Sifuna, Naibu Kiongozi wa chama Godfrey Osotsi na Gavana wa Siaya James Orengo. Upande unaorindima ngoma ya Rais Ruto una Kiongozi wa ODM wa sasa Dkt Oburu Oginga, Mwenyekiti Gladys Wanga na Magavana Abdulswamad Nassir na Simba Arati ambao wanashikilia wadhifa wa naibu kiongozi wa ODM pamoja na Mkurugenzi wa uchaguzi chamani Junet Mohamed. Akiongea katika eneobunge lake la Suna Mashariki, Bw Mohamed ambaye ni kiongozi wa wachache bungeni alidai kuwa rais mstaafu ana mkono fiche na anaunga mkono baadhi ya viongozi wanaolenga kusambaratisha ODM. Bw Mohamed alisimulia jinsi ambavyo kiongozi mmoja alimuita kwenye kikao cha saa nane usiku hoteli moja jijini Kisumu kumshawishi ODM iuzwe. Mwanasiasa huyo alimfahamisha kuhusu ahadi kutoka kwa Bw Kenyatta iwapo ODM ingeondoa uungwaji mkono kwa Rais Ruto. Alisema kiongozi huyo alimjia na mpango na mbinu za kutumika kujiondoa kwenye Serikali Jumuishi kwa kutaja kutotekelezwa kwa hoja 10 zilizoko kwenye muungano wa ODM na UDA. “Aliniambia Rais Mstaafu anataka kusaidia ODM na yuko tayari kuwekeza zaidi ya Sh1 bilioni chama ili tushinde uchaguzi kwa kuungana na upinzani,” akadai Bw Mohamed. “Kama Uhuru alikuwa na vyombo vya mamlaka na hakufanya Raila awe rais, sasa ndio ataweza sasa?” akauliza. Bw Mohamed alisema kiongozi aliyempa habari hizo ni kati ya wale ambao wamekuwa wakipiga kelele na kupinga ushirikiano na Rais Ruto. “Umekuwa ukisema tunataka kukiuza chama kwa Ruto na sasa unataka tukiuze kwa Uhuru. Sasa sisi ni mabroka wawili waliokaa hapa. Tuite mabroka na wezi lakini hatutaondoka kwenye Serikali Jumuishi na ni wewe utaondoka ODM, "Tumechoka kupashwa na watu waliojiunga na ODM kutoka ANC na kama una shida, nenda ukabuni chama chako ila hatutawapeleka watu wetu njia hiyo unayoitaka,” akasema Bw Mohamed. Juhudi za kupata kauli ya Bw Kenyatta kuhusu madai yaliyotolewa dhidi yake hazikuwa zimefua dafu wakati wa kuchapisha habari hizi. Msemaji wake Kanze Dena hakuwa amejibu simu au jumbe alizotumiwa kufikia wakati wa kuchapisha habari. Bw Nassir akizungumza katika eneobunge la Likoni siku mbili zilizopita alidai kuwa mrengo unaompinga Rais Ruto unataka kufilisi ODM ndani kwa ndani. “Nataka kuwaambia kuwa hawatafaulu kwa sababu watu wametuambia hakuna kukaa upinzani tena. Raila hakufaa ili tuendelee kuwa upinzani,” akasema. Mbunge huyo wa zamani wa Mvita alidai kuwa kuna watu ambao wapo ODM mchana na usiku wanafanya juu chini kuhakikisha chama kinasambaratika. “Wengine wanaojifanya wanapenda chama hata walimsaliti Raila na wanazungumzia ODM vibaya usiku. Hatutoki Serikali Jumuishi na tunawajua wale ambao wanapanga kusambaratisha chama,” akasema gavana huyo. Kinaya ni kwamba madai ya Bw Mohamed yanakuja siku chache baada ya Mabw Sifuna na Orengo kudai kulikuwa na mpango wa kunadi ODM kwa Rais Ruto. “Tunasema kuwa ODM haiuzwi na kama umedanganywa na wale ambao umewalipa pesa za mwanzo kuwa umeuziwa chama, fahamu wamekulaghai,” akasema Bw Sifuna kwenye mkutano wa kisiasa Magharibi mwa Kenya. “Hatujamtuma yeyote kujadiliana kwa niaba ya ODM. Hatujamtuma broka na mtu kama huyo ni mlaghai ambaye anataka kukulaghai,” akaongeza. Bw Osotsi naye amesisitiza kuwa ODM haitamuunga Rais Ruto iwapo muafaka wao na UDA hautatekelezwa. Seneta huyo alisema Rais ana hadi Machi 2026 kuonyesha kile ambacho ametekeleza la sivyo asahau uungwaji mkono wao. “Bila hiyo hakuina muafaka kwa sababu uungwaji mkono wa ODM unapewa kwa kufanya yanayotakikana na raia,” akasema Bw Osotsi.

RAIS William Ruto alisherehekea Sikukuu ya Krismasi akiwa kwenye makazi yake ya kifahari mjini, Kilgoris, Kaunti ya Narok, pamoja na Mama Taifa, Rachel Ruto. Bw Ruto alitua Kilgoris mnamo Jumatano baada ya kuhudhuria karamu ya Krismasi katika mbuga ya Maasai Mara. Alhamisi asubuhi, Desemba 25, 2025, Rais pamoja na mke wake walihudhuria ibada ya Krismasi katika kanisa la PEFA Ikarian Cathedral lililopo Lolgorian, Kilgoris. Kupitia ujumbe wa pamoja, Rais na Mama Taifa walihimiza kuwepo kwa umoja, amani na uwiano katika msimu huu wa sherehe. “Kuzaliwa kwa Yesu Kristu kulete matumaini, furaha na amani makazini mwenu. Tunaposherehekea, tukumbatiane pamoja na baraka zinazotuunganisha kama taifa moja,” alisema Kiongozi wa Taifa. Katika ibada hiyo kanisani, Rais Ruto aliandamana na naibu waziri wa zamani Magerer Lang’at na viongozi wengine wa eneo hilo. Baada ya ibada, familia ya rais ilitangamana na waumini, kabla ya kiongozi huyo wa nchi kuondoka. Duru zilieleza Taifa Leo kuwa Rais Ruto baadaye alitumia siku hiyo kukagua shamba lake kubwa. Katika siku za majuzi, Ruto amechagua makazi yake ya kifahari ya Kilgoris, kuwa sehemu anayopendelea zaidi ambapo amesherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na familia yake kwa miaka mitatu iliyopita na vilevile kuwakaribisha wageni rasmi katika hafla kadhaa. Kiongozi wa Taifa anafahamika kuwa na makazi manne ya kibinafsi yaliyopo kaunti za Nairobi, Uasin Gishu na Taita Taveta. Hata hivyo, makazi yake ya Narok yamkini ndiyo fahari yake mpya, yakiangaziwa kitaifa katika siku za karibuni. Rais Ruto, ambaye ni mwanafunzi wa siasa wa rais wa pili nchini Kenya, Daniel arap Moi, yamkini amegeukia kupenda makazi yake ya Kilgoris, sawa tu na hayati rais Moi alivyoenzi makazi yake ya Kabarak, katika kaunti ya Nakuru. Anageuza taratibu makazi yake Kilgoris kuwa ngome ya mamlaka. Kwa miaka 24 ambayo rais wa zamani Moi alitamalaki siasa za Kenya, makazi yake ya kifahari yaliyojengwa kwenye ekari 2,300, mjini Kabarak, Nakuru yalisalia ngome yake ya mamlaka na kituo kikuu cha siasa za taifa. Katika utawala wake, Kabarak iligeuka kuwa kituo salama, ambapo angejiliwaza kutoka vigogo wa mamlaka jijini Nairobi. Hamna shaka Moi alipenda Nakuru. Alipotaka kuepuka purukushani za jiji kuu Nairobi, angeelekea Kabarak. Ilikuwa karibu ni hakika kwamba Mzee Moi angezuru Nakuru siku za wikendi na sherehe za Mwaka Mpya.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita ametoa ahadi kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kuwanunulia sare za shule na kuwalipia bima ya afya ili waweze kupata matibabu. Mhita ametoa Ahadi hiyo wakati wa kushiriki chakula cha pamoja na watoto hao kusherehekea sikukuu ya krisimasi akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na … The post Serikali Shinyanga yaahidi kusaidia watoto yatima first appeared on HabariLeo.

JUMLA ya watu milioni 6.8 Guinea wanatarajiwa kujitokeza siku ya Jumapili Desemba 28, 2025 kuchagua rais mpya. Wagombea wa kiti hicho ambao ni tisa akiwemo kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Mamady Doumbouya, wamefanya mikutano yao ya mwisho ya kampeni za kisiasa Desemba 24, 2025 kabla ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa juma. Licha ya ahadi yake ya awali ya kurudisha mamlaka kwa raia alipochukua hatamu mwaka 2021, Doumbouya anagombea urais katika uchaguzi ambao upinzani wote mkuu umezuiwa. Tangu uhuru wake mwaka 1958, Guinea imekuwa na historia tata ya utawala wa kijeshi na wa kimabavu.

KATIKA mtandao wa kijamii wa Truth Social, Rais wa Amerika, Donald Trump alisema kuwa nchi yake imeanzisha mashambulizi makali dhidi ya ISIS Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria, ambao wamekuwa wakiwalenga na kuwaua Wakristo wasio na hatia. “Marekani imeanzisha mashambulizi makali dhidi ya ISIS Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria, ambao wamekuwa wakiwalenga na kuwaua kikatili Wakristo wasio na hatia,” Trump aliandika katika mtandao wa kijamii wa Truth Social. Tukio hili la hivi punde linajiri wakati hali ya ukosefu wa usalama ikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambayo imekuwa ikikabiliwa na ghasia kwa miaka kadhaa. Kundi la kigaidi la Kiislamu la Boko Haram lina mizizi yake nchini Nigeria pia. Mapema mwezi Novemba Trump alionya kwamba Washington inaweza kuhusika katika mashambulizi hayo, akitoa wito kwa serikali ya Nigeria kuzuia vifo zaidi na kutishia kwamba isipofanya hivyo itakabiliwa na kupunguzwa kwa misaada. Hata hivyo, ghasia zimeendelea, huku takriban watu watano wakiuawa na 35 kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, msemaji wa polisi katika eneo hilo alisema siku ya Alhamisi, Desemba 25, 2025. Kufuatia shambulio hilo la Marekani katika Siku ya Krismasi, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth amesema "anashukuru kwa msaada na ushirikiano wa serikali ya Nigeria." Kwa mujibu wa Kamandi ya Marekani ya Afrika, walengwa walikuwa katika jimbo la Sokoto la Nigeria.

ARUSHA: SHIRIKA Lisilo la Kiserikali la Pingo’s Forum linapanga kutumia zaidi ya Sh milioni 150 kwa ajili ya miradi ya maendeleo pembezoni mwa Wilaya ya Longido mkoani Arusha ikiwemo mradi wa maji na ujenzi wa nyumba za walimu katika wilaya hiyo. Hayo yalisemwa na Kiaro Tendeu ambaye ni Mratibu wa Pingo’s Forum katika kuimarisha huduma … The post Mil 150/- kuleta maendeleo pembezoni mwa Longido first appeared on HabariLeo.

ARUSHA: NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa amesema wananchi wote waliojenga maeneo ambayo barabara ya Siha wilayani Hai mkoani Kilimanjaro hadi Longido mkoani Arusha itakapopita watalipwa fidia kupisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami. Dk Kiruswa alisema hayo akiw kata ya Tingatinga wilayani Longido na kuongeza kuwa serikali iko katika hatua ya tathmini … The post Waliojenga maeneo ya barabara Siha kulipwa fidia first appeared on HabariLeo.

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea na mchakato wa kutekeleza mradi wa Bomba la Gesi kutoka Kinyerezi kwenda Chalinze utakaogharimu zaidi ya Sh bilioni 2.3. The post Mchakato wa bomba la gesi Kinyerezi–Chalinze waendelea first appeared on HabariLeo.

MKUU wa Majeshi wa Libya na maafisa wengine wanne wa kijeshi wamekufa usiku wa kuamkia leo Desemba 24,2025 baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kutoka mji mkuu wa Uturuki, Ankara. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya amesema mabaki ya ndege hiyo aina ya Falcon 50 yamepatikana kwenye wilaya ya Haymana nje kidogo ya Ankara. Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibah ametuma rambirambi zake akisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Luteni Jenerali Mohammed al-Haddad. Mkuu huyo wa majeshi alikuwa nchini Uturuki kwa mazungumzo na viongozi wa ulinzi wa nchi hiyo na mapema hapo jana alikutana na waziri wa ulinzi wa Uturuki Yasar Guler na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.

NCHINI Ujerumani, mabadiliko makubwa ya kijamii na kidini yamesababisha kupungua kwa idadi ya Wakristo, hali inayolazimisha baadhi ya makanisa kufungwa au kubadilisha matumizi. Kupungua huku kumeacha majengo wazi jambo linalofanya matumizi ya kanisa kubadilika. Kanisa la Mtakatifu Anna (St. Anna), lililoko Gildehaus, eneo la Bad Bentheim karibu na mpaka wa Ujerumani na Uholanzi, ni miongoni mwa makanisa yaliyoathiriwa. Hivi karibuni, kanisa hilo dogo la Kikatoliki lilifungwa rasmi baada ya kuandaliwa misa ya mwisho, iliyohudhuriwa na waumini wengi kwa hisia nzito. Wakati wa ibada hiyo ya kuaga, kwaya iliimba na misa ilipokamilika, waumini walishiriki katika zoezi la kutoa masalia ya watakatifu (reliquia) kutoka madhabahu, ishara ya mwisho ya kanisa hilo kuacha kuwa mahali patakatifu. Hatua hiyo, hufanya jengo lililowekwa wakfu kubadilishwa na kuwa jengo la matumizi ya kawaida. Padre Hubertus Goldbeck alisema tukio hilo lilikuwa la kugusa moyo, akieleza masikitiko yake kutokana na kufungwa kwa kanisa hilo lililohudumia waumini kwa miaka mingi. Alisema hali hiyo inawakilisha maumivu yanayowakumba Wakristo wengi nchini humo. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2024 pekee, Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Ujerumani (EKD) yalipoteza zaidi ya waumini milioni moja kutokana na watu kujiondoa kanisani. Kwa sasa, ni takribani asilimia 45 tu ya Wajerumani wanaosalia kuwa wanachama wa makanisa hayo mawili, ikilinganishwa na karibu asilimia 69 miaka 30 iliyopita.

WAKAZI na wadau wa utalii kisiwani Mombasa wametoa wito fukwe zilizo ndani ya kisiwa zifanyiwe ukarabati. Fukwe za ndani ya kisiwa, kama Madhubaha, ufuo wa Fort Jesus na Tudor, zimetelekezwa, hali inayolazimu wakazi kutegemea zile zilizo kaskazini mwa Mombasa kama vile Bamburi na Nyali. Eneo pekee la umma la mapumziko ufukweni linalosifika ni bustani ya Mama Ngina, ambayo ilifunguliwa upya Oktoba 20, 2019 na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, baada ya ukarabati uliogharimu karibu Sh460 milioni. Awali, eneo hilo pia lilitelekezwa na kulifanya kuwa maficho ya wahalifu. Imebainika kuwa, fukwe zilizotelekezwa za kisiwa hicho huwa chafu kwa sababu maji ya mvua yanayobeba uchafu huelekezwa huko, mbali na majitaka. Bw Ahmed Said Mbarak, kutoka Fort Jesus, anaamini eneo hilo likifanyiwa ukarabati linaweza kuleta manufaa makubwa hasa kwa sekta ya utalii. “Eneo hili lina uwezo mkubwa kwa sababu Fort Jesus huvutia watu wengi. Kama tungekuwa na eneo zuri la mapumziko, mambo yangekuwa tofauti. Kwa sasa ni miamba na maji ya mvua tu; kubadilisha hali hii kutahitaji juhudi kubwa,” akasema. Zamani, vijana walikusanyika hapo kwa ajili ya kupiga mbizi na kuogelea, hasa wikendi. “Siku hizi watu huja tu kuona mandhari kisha huondoka. Wakazi wameunganisha mabomba yao ya majitaka kwenye mifereji ya maji ya mvua, hali inayowafanya watu kuchukia kuogelea hapa,” anaongeza. Kwa sasa, ni wakazi wachache tu wanaoweza kustahimili maji machafu na kuingia baharini kuogelea. Katika eneo la Tudor, kuna ufuo mwingine ambao ungestahili kuwa na shughuli nyingi. Kama ilivyo katika maeneo mengine ya kisiwa, harufu ya majitaka yanayoingia baharini hapa huwafukuza watu isipokuwa wale wenye ujasiri wa kuingia kwenye maji hayo. Bw Abdalla Mangale, mlinzi wa kujitolea wa baharini katika Tudor Beach tangu mwaka wa 2020, anasema kuwa licha ya juhudi zake za kusafisha na kupamba eneo hilo, huvutia watu wachache. “Niliamua kubaki hapa kwa ajili ya watoto wanaokuja kuogelea; hapo awali ajali zilikuwa zikitokea kwa sababu hawakuwa wakifuatana na walezi. Tumejaribu kupamba eneo hili na hata kutafuta nafasi ya vyoo vya muda. Hata hivyo, kinachowafanya watu waondoke na wasirudi tena ni harufu ya majitaka. Wengine hufika majini lakini hawaingii kwa sababu wanaona maji ni machafu,” alisema Bw Mangale. Alieleza kuwa baadhi ya watalii hutembelea eneo hilo na kubaki kufurahia mandhari ya bahari pekee. “Tuna chama ambacho wawekezaji wanaweza kushirikiana nacho ili kuhakikisha jamii inanufaika. Nina matumaini kuwa hili likifanyika, ufukwe wetu hatimaye utaanza kuvutia,” alisema Bw Mangale. Serikali ya Kaunti ya Mombasa ilisema kuwa inatambua kuhusu hali ya fukwe zilizo ndani ya kisiwa. Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi na Mipango ya Miji katika kaunti Mohamed Hussein, kaunti ina mipango ya kukarabati fukwe hizo ili kutumia kikamilifu uwezo wao. “Kwa sasa tunashughulikia tatizo la majitaka kwa kuhakikisha kuwa majengo mapya yote Mombasa yanawekewa ‘biodigester’. Hii itahakikisha kuwa maji yanayotolewa kutoka kwenye majengo hayo hayadhuru tena mazingira,” alisema. Aliongeza kuwa, idara hiyo inajenga kituo cha kusafisha majitaka kitakachohakikisha kuwa maji yote yanayoelekezwa baharini ni safi. “Fukwe zina uwezo wa kuwaunganisha watu na hata kubadilisha maisha; ndiyo maana tunafanya kazi bila kuchoka kuondoa vikwazo vinavyozuia ufuo wetu kustawi. Tunataka wananchi wetu wafurahie fukwe, ndiyo maana maafisa wa afya ya umma tayari wako mashinani wakichukua hatua,” alisema Bw Hussein. Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli na Wahudumu wa Migahawa nchini, Dkt Sam Ikwaye, fukwe za Mombasa ni miongoni mwa vivutio vikuu katika eneo hili. Hata hivyo, usimamizi duni, kanuni zinazokinzana na mgawanyiko usio wazi wa majukumu kati ya serikali ya kitaifa na kaunti vimezuia matumizi kamili ya rasilimali hizi. “Ni vigumu kubaini ni nani ana jukumu la kuwekeza katika miundomsingi, usalama wa fukwe na maendeleo yake,” alisema Dkt Ikwaye. Mwenyekiti huyo wa Baraza la Utalii la Mombasa, alisema kuwa jitihada zimefanywa kuandaa kanuni zitakazoongeza thamani ya fukwe zinazotumika tayari pamoja na zile ambazo bado zimetelekezwa. “Kupitia chama cha wahudumu wa hoteli, tumeweza kushirikiana na serikali ya kaunti ya Kwale pamoja na serikali ya kaunti ya Mombasa. Kufikia sasa, tayari tumewasilisha rasimu za sheria za usimamizi wa fukwe katika kaunti hizi,” alisema Dkt Ikwaye.

HATUA ya ODM kutaka UDA isiwe na wawaniaji katika ngome zake za kisiasa 2027 imeibua mgawanyiko mpya ndani ya Serikali Jumuishi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Japo ODM imeonyesha kila ishara ya kumuunga mkono Rais William Ruto mnamo 2027, imeonya UDA dhidi ya kuingilia ngome zake za kisiasa za Nyanza, Magharibi na Pwani. Nia ya ODM ni kuhakikisha kwamba inasalia na wabunge wengi ili kuipa jukwaa bora la kuwa na ushawishi kwenye muungano na Rais Ruto baada ya 2027. Umaarufu wa ODM kwenye ngome zake za Gusii na Magharibi nao sasa unatishiwa na vyama vya UPA na DAP-Kenya mtawalia. Baadhi ya wanachama wa ODM pia wameonyesha dalili za kuhama wakihofia kuwa watachezewa shere katika mchujo wa 2027. Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga ambaye pia ni gavana wa Homa Bay alitoa pendekezo la UDA kutokanyaga ngome za ODM kupitia uwaniaji mnamo 2027. “Tuko kwa Serikali Jumuishi kama ODM na kati ya makubaliano yetu ni kuwa hakuna kuingiliwa kwa ngome zetu,” akasema Bi Wanga akizungumza Awasi, eneobunge la Nyando mnamo Ijumaa. Kauli hiyo imewakasirisha baadhi ya viongozi wa ODM wanaoona kuwa watachezewa shere kwenye uteuzi na pia viongozi wa UDA hasa kutoka kaunti za Nyanza ambapo ODM imetawala kisiasa. Gavana wa zamani wa Nairobi Evans Kidero aliye mwanachama wa UDA jana aliambia Taifa Leo kuwa watapambana na kupinga juhudi zozote za kuzuiwa kuwania Nyanza. Dkt Kidero alisema watu wanastahili kupewa nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka badala ya kulazimishiwa na chama. Alisema njia pekee ambayo eneo hilo linaweza kuthamini siasa za marehemu Raila Odinga ni kukumbatia demokrasia. “Kutengea chama eneo kisha kuvizuia vingine kuwasilisha mwaniaji ni ukiukaji wa demokrasia. Hatutakubali hilo,” akasema Dkt Kidero. Mwenyekiti wa UDA Kaunti ya Homa Bay Kennedy Obuya naye alisema chama hicho kitakuwa na wawaniaji kwenye ngazi zote za uongozi Luo Nyanza ili raia wawe na hiari ya kuwachagua viongozi ambao wanawataka. “UDA itakuwa na wawaniaji Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori. Watu wetu watakuwa na jukumu la kuwachagua viongozi na wafahamu kuwa hakuna Serikali Jumuishi bila UDA,” akasema Bw Obuya. Kwenye uchaguzi mdogo wa Kasipul mwezi uliopita, ODM ilishutumiwa kwa kuandaa mchujo uliopendelea Boyd Were mwanawe aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo marehemu Ong'ondo Were. Hata kabla ya chama kuandaa mchujo wake, baadhi ya viongozi wake wakuu walikuwa wakipambana Bw Boyd apokezwe tikiti. Jana, Naibu Kiongozi wa ODM Godfrey Osotsi aliwahakikishia wafuasi wa chama kuwa kitasalia imara kuelekea 2027. “Kuna watu wengi wanafikiria ODM itapasuka bila Raila. Watashangaa lakini lazima tuongee na wenzetu ili tufahamu tutapata nini baada ya uchaguzi wa 2027,” akasema Bw Osotsi. “Nilisikia baadhi ya viongozi wakisema Waluhya waondoke ODM. Sisi maslahi yetu lazima yalindwe chamani na viongozi wanastahili kukoma kusawiri ODM kama chama cha Waluo au Nyanza pekee,” akasema Bw Osotsi. Mbunge wa Uriri Mark Nyamita wiki jana alisisitiza kuwa ni uteuzi huru ndio utasaidia ODM kuendelee kuwika katika ngome zake. Mbunge huyo analenga kutumia ODM kuwania ugavana wa Migori mnamo 2027. Naye Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi ashatangaza kuwa hatatetea kiti chake kupitia ODM kwa sababu ana hakika uteuzi wa chama hautakuwa huru na utaingiliwa.

KWA kipindi cha miezi sita sasa, utulivu umeanza kurejea taratibu katika Bonde la Kerio lililojishindia jina la ‘Bonde la Mauti’ kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara. Mashambulizi hayo ambayo yameendelea tangu mwanzoni mwa mwaka huu yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 22 katika kaunti za Baringo na Elgeyo Marakwet. Hata hivyo, wakazi wameanza kurejelea shughuli zao za kawaida kutokana na operesheni ya usalama iliyoanzishwa na serikali ili kurejesha utulivu. Kwa miaka mingi, serikali ilikuwa ikitumia operesheni kali ya kutwaa silaha katika maeneo yanayosheheni majangili Bonde la Ufa Kaskazini. Lakini licha ya kutuma vikosi mbalimbali kuwapokonya raia silaha, ilikuwa nadra kwa juhudi hizo za kuondoa bunduki kuzaa matunda kwa sababu mashambulizi zaidi yaliripotiwa na wanajamii kuendelea kusafirisha silaha kimagendo. Wataalamu wa usalama walikuwa vilevile wameonya kwamba serikali haingefanikisha azma yake ya kutwaa bunduki pasipo kuainisha maeneo lengwa, wakipendekeza kubadilisha mikakati na mipango kabambe katika vijiji vilivyoathirika. Mwaka huu, serikali iligeukia kubadilisha mikakati ili kurejesha hali ya kawaida katika vijiji vilivyogubikwa na ukosefu wa usalama na kuchagua oparesheni inayoongozwa na ujasusi kuwalenga washukiwa wa uhalifu badala ya wanajamii wote. Akizuru miji ya Marigat na Kabarnet, Kaunti ya Baringo, mwezi mmoja uliopita, Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, aliashiria kwamba kupitia mikakati iliyowekwa na serikali, utulivu umerejeshwa katika Bonde la Kerio. Kulingana na waziri huyo, zaidi ya bunduki haramu 600 zimesalimishwa kwa hiari na wakazi eneo hilo, 300 miongoni mwake zikitoka Baringo. “Baadhi ya kaunti katika Bonde la Ufa Kaskazini zilivurugika kabisa kutokana na itkadi za kijadi za wizi wa mifugo na ujangili, lakini kwa sababu ya juhudi za serikali, hali ya kawaida imerejeshwa katika vijiji vilivyoathirika,” alisema Waziri Murkomen wakati huo. “Tutahakikisha bunduki zote zilizo mikononi mwa raia zimetwaliwa ili wakazi waishi kwa amani. Hatutaafikiana na viongozi wa kisiasa wanaotatiza mchakato huo. Hakutakuwa na kushirikisha umma kuhusu masuala ya kutwaa bunduki au majadiliano yoyote. Operesheni itaongozwa na ujasusi,” alisema Waziri. Kamanda wa Polisi Elgeyo Marakwet Peter Mulinge, alisema walianzisha oparesheni ya ujasusi inayolenga washukiwa wa uhalifu, waliohitajika kusalimisha silaha haramu wanazomiliki. “Operesheni hiyo ilifanikiwa kwa sababu tulichukua muda kuanisha maeneo yaliyoathirika na kuwatambua washukiwa wa uhalifu waliojihami badala ya kulenga jamii yote. “Tulifaulu kuwakamata kadhaa, waliosalimisha kwa hiari bunduki haramu walizokwamilia, na serikali kuu na ya kaunti iliwasaidia kupata namna mbadala ya kujikimu kimaisha,” alisema Bw Mulinge. Kikosi jumuishi kinachoendesha oparesheni ya usalama katika maeneo yanayohangaishwa na majangili, kikisaidiwa na polisi wa akiba nchini, kiliweza kuwatimua wahalifu waliojihami na kuimarisha maeneo – hatua iliyorejesha utulivu na kuhimiza wakazi waliofurushwa kurejea makwao. Machi mwaka jana, kwa mfano, kikosi jumuishi kinachoendesha operesheni Baringo kililipua kwa bomu Bonde la Tandare, moja kati ya maeneo yaliyoorodheshwa kama maficho ya majangili Baringo Kusini. Kulingana na Kamanda wa Polisi Baringo, Julius Kiragu, wakisaidiwa na kikosi hicho, walitekeleza vilevile uangalizi angani uliosaidia kufuatilia maficho ya washambulizi waliojihami. Kanali (Rtd) Moses Kwonyike, aliyehudumu kama mshauri wa kijeshi na mkuu wa Operesheni ya Afrika ya Umoja wa Mataifa Darfur, alisema serikali ilipasi safari hii kwa kubadilisha mikakati ya kujenga amani Bonde la Ufa Kaskazini lililosambaratishwa na mapigano. Safari hii, serikali hata ilifahamu ni nani aliyeiba mifugo siku iliyotangulia, na waliiendea,” alisema mwanajeshi wa zamani ambaye kwa muda mrefu amepinga upokonyaji silaha kimabavu. “Wahalifu walikuwa wanatudhihaki waliposikia kuhusu oparesheni mpya ya kutwaa silaha, wangetorokea vijiji vilivyo mashinani ambapo hawangepatikana, na kuwaacha raia wasio na hatia – ikiwemo wanawake na watoto – kuteseka mikononi mwa maafisa wa usalama. "Safari hii, majangili walifurushwa kutoka mafichoni mwao na wakashurutishwa kusalimisha bunduki haramu,” alisema Richard Chepchomei, mkazi katika kijiji kinachogubikwa na ukosefu wa usalama, Chemoe, Baringo Kaskazini. Alisema mwelekeo wa serikali unaolenga wahalifu na kutwaa silaha ndio bora, kinyume na kulenga jamii zima jinsi ilivyokuwa mbeleni.

AFISA wa polisi aliyekuwa kwenye video ya Tiktok yenye kauli-mbiu ‘Ruto Must Go’ (Sharti Ruto Ang’atuke), amepoteza kesi aliyowasilisha mahakamani kuzuia Tume ya Huduma za Polisi (NPSC) kumwachisha kazi. Mahakama ya Leba ilitupilia mbali kesi ya Joyfred Maina ikisema alikuwa amewasilisha kesi hiyo huku rufaa yake aliyokata kwa tume ya NPSC ikiwa bado inaendelea. Bw Maina ambaye awali alihudumu katika Kituo cha Polisi cha Riruta alikuwa amepinga kutimuliwa kwake mnamo Septemba 2024 kutokana na video hiyo ambayo ilizua maoni kinzani, ikishabikiwa na na kukosolewa na Wakenya kwa wakati mmoja. Mahakama iliamua kuwa afisa huyo aliwasilisha kesi ilhali pia alikuwa ameiwasilisha rufaa kwa idara za NPSC zinazohusika na kufutwa. Kwa hivyo, ni vyema angesubiri matokeo ya uamuzi wa rufaa aliyowasilisha kabla ya kukimbia kortini. “Hakuna pingamizi kwamba amefuata mkondo wa kupata haki kupitia vyombo vya ndani katika idara ya polisi. Mahakama haiwezi kutoa uamuzi kabla ya rufaa yake kuamuliwa,” ikasema mahakama. Kesi hiyo ilitokana na yaliyotokea wakati wa maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali mnamo Julai 19, 2023. Kulikuwa na uhasama mkali wa kisiasa kati ya upinzani na serikali wakati huo baada ya uchaguzi wa 2022. Bw Maina alikuwa Polisi wa Utawala (AP) aliyejiunga na idara hiyo kama mlinzi wa kituo mnamo 2008. Alishiriki video hiyo akiwa amevaa sare katika hali ambayo inadhaniwa kuchangia kuibuka kwa kauli ‘Ruto Must Go’ miongoni mwa wakosoaji wa Rais. Bw Maina alijitetea tu akisema alisoma kwa sauti yale yaliyoandikwa kisha akawaonya watazamaji dhidi ya kutumia lugha kama hiyo. Mahakama iliambiwa kuwa video hiyo ilisambaa kwa kasi baada ya kuhaririwa na watu wasiojulikana na kuchochea ghadhabu za umma. Pia ilisababisha mienendo ya polisi ichunguzwe wakati wa maandamano. Makamanda wa polisi walisema video hiyo ilikuwa kinyume cha utendakazi wa idara hiyo na kuonyesha walikuwa wakiegemea upande mmoja kisiasa. Siku iliyofuatia, Bw Maina alitumiwa notisi ya kumtaka aeleze kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu. Alitakiwa kujitetea kwa makosa ya kutoa matamshi ya uchochezi, uongo, kutelekeza majukumu yake na kukiuka kanuni za utendakazi wa idara ya polisi. Baada ya kujibu notisi hiyo, Bw Maina alifutwa kazi ila baadaye akasimamishwa na kesi yake kufuata mkondo wa maamuzi ya ndani kwenye NPS. Kamati ya nidhamu ilibaini kuwa haina mamlaka ya kutosha ya kusikiliza rufaa ya Bw Maina hivyo basi ikaiwasilisha kwa makamanda wao wakuu. Mnamo Septemba 2024, NPSC ilimwondoa rasmi na kusema adhabu hiyo ilistahili kuanza siku aliyosimamishwa. Alishauriwa akate rufaa ndani ya siku 14. “Kufuatia uzito wa utovu wa nidhamu na rekodi yake ikiwemo kutelekeza majukumu, kamati inapendekeza afutwe kazi,” akasema Silas Andiema, Kamishina wa Polisi anayehusika na Masuala ya Wafanyakazi kwenye stakabadhi za korti. Bw Maina akiwa mbele ya mahakama alisema kuwa haki zake za kikatiba zilikuwa zimekiukwa akitaja kanuni za leba zinazostahili kuzingatiwa na kusikizwa kwake. Alidai kuwa mchakato wa nidhamu ulikuwa umevurugika na hakupewa notisi ndani ya siku saba kabla ya kupitishwa kwenye mkondo wa nidhamu. Alidai kuwa haki ya kujieleza pia ilikiukwa kinyume cha sheria, akisema kuwa hafai kuzuiwa kuzungumza au kutangamana na umma kwa sababu yeye ni afisa wa polisi. “Sikupewa nafasi ya kuwasilisha kesi yangu au kusikizwa wakati wa rufaa,” Bw Maina akaambia mahakama akiomba arejeshwe kazini, kufutiliwa mbali kwa kutimuliwa kwake na alipwe kwa muda ambao hajakuwa kazini. Hata hivyo, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mwanasheria Mkuu walipinga kesi hiyo wakisema alitumuliwa kwa haki na sheria kufuatwa. Mawakili walisema kuwa tabia ya afisa huyo akiwa amevalia sare ilikiuka hitaji la kisheria kuwa maafisa wa usalama hawafai kuwa na miegemeo ya kisiasa.

WASHINGTON DC, AMERIKA AMERIKA mnamo Ijumaa ilikatiza juhudi zake za kumrejesha kimabavu nchini Uganda raia wa China aliyesaidia kunakili dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na Beijing dhidi ya Waislamu wa Uyghur, wakili wa mwanamume huyo alieleza Reuters. Guan Heng, mwanahabari mwenye asili ya China, alikimbilia Amerika mnamo 2021 baada ya kurekodi video ya kinachodaiwa kuwa kambi za kuwapakia mateka katika eneo la Xinjiang, China Magharibi. Aliachilia video hiyo baada ya kuwasili Amerika ambapo alituma maombi ya kupatiwa hifadhi. Guan alizuiliwa Agosti na idara ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Ushuru wa Forodha (ICE) kwa kuingia kimagendo taifa hilo, sehemu ya msako mkali unaoendeshwa na Rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji. Angali kizuizini katika jiji la New York. Kuzuiliwa kwake na tishio la kurushwa Uganda kumezua utata, hasa ikizingatiwa alisaidia kurekodi dhuluma zilizofanyika China ambazo serikali ya Amerika wakati wa hatamu ya kwanza ya Trump ilitaja kuwa “mauaji ya halaiki.” Wafuasi na wakili wake wanasema Guan alikabiliwa na mateso waziwazi ikiwa atatoswa Uganda. Taifa hilo la Afrika Mashariki, ambapo Beijing ina umaarufu kwa kiasi fulani kisiasa na kiuchumi, mwaka huu liliingia kwenye mkataba na Amerika kuwachukua raia kutoka mataifa maskini. Chini ya sera za Wizara ya Usalama wa ndani (DHS), wahamiaji wanaweza kurushwa kimabavu katika nchi maskini ikiwa maafisa wa uhamiaji ama wana hakikisho “za kweli” kidiplomasia hawatakandamizwa au kuteswa ikiwa watarushwa huko au wamepatia wahamiaji notisi ya muda mfupi wa hadi saa sita kabla ya wakati ambao wanatoswa pahali kama hapo.

SERIKALI itawachukulia hatua madaktari wanaolipwa kwa pesa za umma huku wakiacha majukumu yao katika hospitali za serikali na kuendesha kliniki zao binafsi. Wizara ya Afya inasema tabia ya madaktari kuhepa kazi mara kwa mara, hasa katika hospitali za kaunti na zile za rufaa, imesababisha wagonjwa wanaohitaji upasuaji na huduma muhimu kuhangaika. Katika baadhi ya visa, wagonjwa hupewa tarehe za matibabu zilizo mbali katika hospitali za umma, kisha kufuatwa na mapendekezo ya kwenda hospitali za kibinafsi ambako madaktari hao hao wanahudumu. Akizungumza Jumatano, Waziri wa Afya Aden Duale alisema serikali imechoshwa na mwenendo huo na itaanza msako mkali kuanzia Januari. Alisema madaktari wanaofanya kazi kwingine ndani ya saa rasmi za kazi wanajihusisha na ulaghai na watachukuliwa hatua kali. Aliongeza kuwa Mamlaka ya Afya ya Kidijitali imeagizwa kuchukua hatua dhidi ya madaktari wanaowasilisha malipo ya bima katika hospitali za kibinafsi ilhali wameajiriwa kufanya kazi katika hospitalini za umma. Magavana kadhaa wameunga mkono hatua hiyo wakisema tatizo hilo ni kubwa na linaathiri juhudi za kufanikisha mpango wa afya kwa wote. Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, alisema madaktari lazima wabaki hospitalini kuwahudumia wananchi badala ya kugeuza hospitali za umma kuwa maeneo ya kupata wateja wa kliniki za kibinafsi. Naibu mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Muthomi Njuki, alisema madaktari wengine hutumia sehemu ndogo tu ya muda wao hospitalini kisha wanaenda kliniki za kibinafsi licha ya kupokea marupurupu maalum yanayolenga kuwazuia kufanya kazi za kibinafsi. Alionya kuwa kaunti hazitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika. Katika Kaunti ya Tharaka Nithi, Njuki alisimulia jinsi alivyofanya ziara ya ghafla katika hospitali na kukuta madaktari kadhaa hawakuwa kazini na baadaye akabaini walikuwa wakihudumia wagonjwa katika kliniki zao binafsi. Alisema baadhi ya wagonjwa hulazimika kulipia matibabu mara mbili.

MKUTANO wa Rais William Ruto na kundi la wabunge kutoka kaunti za Kisii na Nyamira uliofanyika Ijumaa katika Ikulu, ulitafsiriwa hadharani kama kikao cha kawaida cha maendeleo, lakini kwa undani wake uliashiria mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayoendelea katika eneo hilo huku aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i, akiibuka kama nguzo muhimu katika upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kikao hicho cha faragha kilichodumu takribani saa mbili kiliwaleta pamoja wabunge wanaounga mkono chama tawala cha UDA pamoja na baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambao hivi majuzi walianza kuunga mkono serikali jumuishi ya Rais Ruto na chama cha ODM. Ingawa waliohudhuria walisisitiza kuwa ajenda kuu ilikuwa maendeleo, muda na muundo wa ujumbe ulionyesha malengo ya kisiasa ya kurejesha ushawishi uliopotea katika chaguzi ndogo za hivi karibuni na kudhibiti mvuto unaoongezeka wa Dkt Matiang’i. Mkutano huo ulifanyika wiki chache baada ya wagombeaji wanaohusishwa na Matiang’i na chama cha Jubilee kushinda chaguzi ndogo za wadi Nyamira, jambo lililokuwa pigo kwa viongozi wanaoegemea UDA na kuzua maswali kuhusu umaarufu wa chama tawala katika eneo hilo. Mbunge wa South Mugirango ambaye ni kiranja wa wengi katika Bunge la Kitaifa, Silvanus Osoro, aliyekuwa kiongozi wa ujumbe huo, alipuuza madai kuwa jina la Matiang’i lilijadiliwa Ikulu. Alisema mazungumzo yalihusu maandalizi ya ziara ya maendeleo ya Rais katika eneo la Gusii, ambako miradi kadhaa inatarajiwa kuzinduliwa. Hata hivyo, kauli za baadhi ya wabunge zilionyeesha hofu ya kisiasa. Mbunge wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, alimkosoa Matiang’i akisema hana muundo thabiti wa kisiasa na juhudi zake si za kitaifa. Ajenda ya maendeleo ilijumuisha kituo cha matibabu ya saratani cha Sh4.7 bilioni kinachofadhiliwa kwa pamoja na Kenya na Saudi Arabia pamoja na miradi ya barabara katika Kisii na Nyamira. Viongozi wa UDA wanategemea miradi hiyo kama ushahidi wa uwepo wa serikali mashinani. Kwa upande wake, Seneta wa Kisii Richard Onyonka alisema hali halisi mashinani inaonyesha kuwa wakazi wengi tayari wamejipanga kumuunga mkono Dkt Matiang’i kutokana na kuchoshwa na ahadi zisizotekelezwa, gharama ya juu ya maisha na siasa za kimaslahi.

INDIA; Serikali ya Tanzania na India zimesaini Hati ya Makubaliano kuhusu ushirikiano kwenye Sekta ya Afya katika kuendeleza tiba asilia (Ayurveda). Aidha, Tanzania imewakaribisha wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuwekeza na kuwahakikishia kuwapatia mazingira mazuri ya uwekezaji. Utiwaji saini huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Bharat Mandapam uliopo New Delhi, India kati ya … The post Tanzania, India zasaini makubaliano kuendeleza tiba asili first appeared on HabariLeo.

KIONGOZI wa chama cha Democratic Action Party–Kenya (DAP-K), Eugene Wamalwa, anadai kuwa Rais William Ruto alijaribu kumpa wadhifa wa Waziri wa Ulinzi ili kumvuta upande wake kuelekea uchaguzi wa 2027. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio humu nchini mnamo Alhamisi, Bw Wamalwa alisema kuwa baada ya Aden Duale kuhamishwa kutoka wizara hiyo kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, rais alimtumia wajumbe kumrai achukue nafasi hiyo. Bw Wamalwa alisema alikataa na kumwambia rais kuwa hana nia ya kujiunga na serikali, akichagua kubaki katika upinzani. Alidai kuwa rais, akitambua nguvu inayoongezeka ya Muungano wa Upinzani ni tishio kwa azma yake kupata muhula wa pili wa mwaka 2027, amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwarai viongozi wa upinzani kujiunga na serikali. “Rais William Ruto amekuwa akituma watu kwetu ili tujiunge na serikali yake. Baada ya Duale kuondoka Wizara ya Ulinzi, alitaka nichukue nafasi yake lakini nilimwambia siwezi,” alisema Bw Wamalwa. Alisisitiza kuwa lengo la Muungano wa Upinzani ni kuzuia kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto mwaka 2027, kurejesha sera zilizokuwa maarufu kama Linda Mama na NHIF zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Uhuru Kenyatta, na kubatilisha sera kandamizi za serikali ya sasa. Kauli yake inajiri siku chache baada ya fununu kusambaa kuwa yeye na kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, walikuwa wakishawishiwa kujiunga na serikali. Hii ilimfanya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kusema kuwa ikiwa Rais Ruto anataka kuzungumza na Kalonzo au Eugene, lazima apitie kwake kwa kuwa wote ni “binamu.” Alidai kuwa vyama vidogo vidogo vinasajiliwa ili kupunguza nguvu katika ngome za upinzani.

KIONGOZI wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amepuuza mashambulizi kutoka kwa Rais William Ruto, akimlaumu kwa kupotosha kimakusudi rekodi yake katika utumishi wa umma. Haya yanajiri huku ushindani wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 ukizidi kupamba moto. Kwa wiki kadhaa sasa, Rais Ruto amekuwa akitumia mikutano ya hadhara na majukwaa ya kisiasa kuhoji mchango wa Bw Musyoka katika maendeleo, mara kwa mara akimtaka “aonyeshe rekodi yake ya maendeleo” ya kile anachosema ni zaidi ya miaka 40 serikalini. Mashambulizi hayo yanalenga kumsawiri makamu rais huyo wa zamani kama mwanasiasa ambaye, kwa mujibu wa Rais Ruto, hakuwaletea Wakenya wa kawaida manufaa ya moja kwa moja licha ya kuhudumu serikalini kwa miaka mingi. Hata hivyo, katika majibu makali, Wiper Patriotic Front ilikanusha madai hayo, ikisema kauli za rais ni juhudi za kupotosha historia ya maendeleo ya Kenya na siasa za mapema dhidi ya kinara huyo wa upinzani. “Huu si mjadala wa haki kuhusu maendeleo. Haya ni mshambulizi wa kisiasa yanayotokana na kuhisi kushindwa,” alisema Katibu Mkuu wa Wiper, Seneta Shakila Abdalla, kupitia taarifa. “Rais Ruto anajifanya kuwa maendeleo ni mali binafsi ya mtu mmoja au utawala mmoja.” Seneta Abdalla alisema rekodi ya Bw Musyoka haiwezi kupuuzwa kwa vijembe jukwaani, akisisitiza kuwa mchango wake serikalini unapaswa kuangaliwa kwa mtazamo wa uongozi wa pamoja na mipango ya muda mrefu. Alirejelea wadhifa wake wakati wa utawala wa Rais Mwai Kibaki alipokuwa makamu wa rais, na awali akiwa waziri serikalini. “Kalonzo Musyoka alikuwa mhimili muhimu wakati wa kubuniwa kwa Ruwaza ya 2030, ambapo taifa hili liliweka ramani kabambe zaidi ya maendeleo kuwahi kuwa nayo,” alisema. “Barabara, taasisi na mageuzi zilipangwa na kufadhiliwa wakati huo, hazikuibuka juzi kwa sababu ya kampeni.” Chama hicho kilipinga vikali madai ya rais kwamba viongozi wa upinzani walihudumu serikalini kwa miongo mingi bila kuleta maendeleo, kikisema hoja hizo zinapuuza jinsi miradi mikubwa hupangwa, kufadhiliwa na kutekelezwa kwa miaka mingi na tawala tofauti. “Maendeleo ni haki ya kikatiba ya wananchi, si hongo ya kampeni wala hisani ya rais aliye mamlakani,” alisema Seneta Abdalla. “Tunachoshuhudia sasa ni jaribio la kuandika upya historia ili mtu mmoja aonekane kama ndiye mpangaji wa pekee wa maendeleo.” Wiper pia ilimlaumu rais kwa kujipatia sifa za miradi iliyoanzishwa kabla ya utawala wake, hasa katika eneo la Kusini Mashariki mwa nchi. Seneta Abdalla alitaja barabara ya Kibwezi–Mutomo–Kitui–Bondoni, akisema ilianzishwa na kufadhiliwa Bw Musyoka alipokuwa serikalini, lakini ujenzi ukalemazwa na maamuzi ya kisiasa yaliyofuata. “Ni makosa kwa rais kwenda maeneo fulani leo na kudai analeta maendeleo, ilhali miradi hiyo ilizinduliwa 2013 na ikalemazwa,” alisema. “Wakenya si wajinga. Wanakumbuka nani alianzisha miradi hiyo na nani alichelewesha.” Mbali na miundombinu, viongozi wa Wiper walipanua mjadala huo hadi masuala ya utawala na uadilifu. Seneta Abdalla alilinganisha kipindi cha Bw Musyoka serikalini na kile alichokitaja kama kukithiri kwa malalamishi ya wananchi chini ya utawala wa sasa. “Kalonzo Musyoka aliondoka serikalini bila kashfa za ufisadi, bila utajiri usioelezeka na bila mizigo ya kimaadili inayokumba serikali ya sasa,” alisema. “Hauwezi kumhubiria maendeleo wakati huduma za afya zinaporomoka, elimu iko mashakani na gharama ya maisha inazidi kuwalemea wananchi.” Mvutano huo unaashiria misimamo ya kisiasa mapema kuelekea 2027, huku Rais Ruto akijaribu kuwadhalilisha wapinzani wake na vyama vya upinzani vikichukulia mashambulizi hayo kama njia ya kuficha kutoridhika kwa wananchi na sera za serikali. “Taifa hili halitajengwa kwa matusi na propaganda,” alisema Seneta Abdalla. “Uongozi ni kuhusu taasisi, uadilifu na huduma kwa wananchi, na hiyo ni rekodi ambayo Kalonzo Musyoka haogopi kuitetea.”

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar ina fursa nyingi za kiuchumi, hususan katika sekta ya Uchumi wa Buluu na uwekezaji, hivyo amewahimiza viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutumia majukwaa ya kimataifa kuitangaza Zanzibar ili inufaike zaidi kiuchumi. The post Diplomasia ya uchumi kuitangaza Zanzibar first appeared on HabariLeo.

MAAFISA watatu wa chama cha ushirika cha wahudumu wa afya –Afya Sacco) wameshtakiwa kwa wizi wa Sh40milioni. Evans Mung’ahu Kola (meneja) alishtakiwa pamoja na Patrick Kuya Lubako na Mumina Mutinda Ing’ui kwa wizi wa Sh40,169,165.69. Watatu hao walikana mashtaka 11 walipofikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina Desemba 19,2025. Kola, Lubako na Mutinda walikabiliwa na mashtaka ya kula njama za kulaghai Afya Sacco kwa kubuni akaunti feki za kuweka pesa na kuzitoa. Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) alimweleza hakimu washtakiwa hao waliiba pesa hizo kutokana na nyadhifa zao kama wafanyakazi wa chama hicho cha ushirika. Pesa hizo hakimu alielezwa ziliibwa kati ya Aprili 20,2021 na Januari 3, 2025. Kola alikabiliwa na shtaka la kuiba Sh40,169,165.69 kutoka kwa Sacco hiyo. Nao Lubako na Mutinda walikana kuchomoka na Sh40,169,165.69 wakishirikiana na mtu mwingine ambaye hakufikishwa kortini. Lubako na Mutinda walikabiliwa na shtaka lingine la kujitajirisha na Sh10,714,999.72 wakijua zimepatikana kwa njia isiyo halali. Pia Lubako na Mutinda walikana walitia kibindoni Sh24,950,999.97 wakijua zimeibwa kutoka kwa akaunti ya Afya Sacco. Vile vile Kola na Mutinda walidaiwa kujinufaisha na Sh24,950,999.97 pesa za Afya Sacco. Pia Kola na Mutinda walikana walijinufaisha na Sh1,702,000 zilizopatikana kwa njia isiyo halali pesa za Afya Sacco zilikuwa zimewekwa katika akaunti ya Fosa. Washtakiwa waliomba waachiliwe kwsa dhamana wakieleza korti walishirikiana na wachunguzi wa kesi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja. Upande wa mashtaka haukupinga washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana. Mahakama iliombwa na DPP izingatie kiwango cha pesa kilichopotea ikiamua kiwango cha dhamana. Akitoa uamuzi Bw Onyina alisema washtakiwa wamethibitisha kwamba hawatatoroka na watafika kortini wakati wa kusikizwa kwa kesi. Aliwaachilia kila mmoja na dhamana ya Sh4milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho. Pia aliwapa dhamana badala ya Sh2milioni kila mmoja hadi Januari 6,2026 kesi itakatengewa siku ya kusikizwa.

NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew amezitaka Bodi za Mabonde ya Maji nchini kufanya tathmini ya kina ya vyanzo vyote vya maji ili kubaini hali yake. Amesema itahusu kujua uhalisia, ikiwemo uvamizi, uharibifu na athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema hayo akiwa katika ziara mkoani Songwe akikagua utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa na … The post Kundo ataka tathmini vyanzo vya maji first appeared on HabariLeo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Munde akikabidhi tuzo maalumu kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Soter Salema katika Mkutano wa 16 wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) leo Desemba 19, 2025 Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). Tuzo hiyo imetolewa kwa TSN kutokana na … The post TSN yapewa tuzo mkutano Wataalamu Ununuzi na Ugavi first appeared on HabariLeo.

ARUSHA; MKURUGENZI Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Soter Salema amesema kampuni hiyo inajivunia safari ya mageuzi ya teknolojia ikiwemo utunzaji wa nyaraka, kumbukumbu za picha na historia mbalimbali. Salema amesema hayo leo jijini Arusha mara baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Munde kutembelea banda la maonesho la … The post TSN yachomoza Mkutano Wataalamu Ununuzi na Ugavi first appeared on HabariLeo.

WANAMGAMBO wa kikosi cha RSF ambao wamekuwa wakipambana na jeshi la serikali kwa muda wa miaka miwili na nusu, walisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 wakati wa mashambulio ya siku tatu yaliyofanywa mwezi Aprili. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Desemba 18, 2025. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR imeeleza katika ripoti yake kwamba "ilirekodi mauaji ya raia 1,013 wakati wa mashambulio ya RSF kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam kati ya Aprili 11 na 13." Ripoti hiyo imeongeza kuwa zaidi ya wakimbizi 400,000 waliokuwepo kwenye kambi hiyo walilazimika kukimbia wakati wa mashambulio hayo ya siku tatu. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF yamesababisha takriban watu milioni 12 kuyahama makazi yao nchini Sudan huku maelfu wakikabiliwa na njaa.

HOSPITALI ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH) Kaunti ya Kisumu inatarajiwa kuanza kutoa huduma za hospitali ya rufaa ya kitaifa mwishoni mwa Januari. Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt Joshua Clinton Okise, alisema Alhamisi, Desemba 18, 2025 kwamba kamati ya mpito ilikamilisha jukumu lake mnamo Desemba 11 na kukabidhi rasmi ripoti yake kwa bodi ya usimamizi wa hospitali, Idara ya kaunti ya Huduma za Matibabu na afisi yake. Akizungumza na vyombo vya habari katika hospitali hiyo mjini Kisumu baada ya mkutano wa wafanyakazi, Dkt Okise alisema mchakato huo umezingatia nguzo tatu muhimu - rasilimali, sheria, na uhamishaji wa mali na fedha. ili kuleta utulivu katika hospitali hiyo kufuatia kupandishwa hadhi kwake hadi ya rufaa ya kitaifa.'Mfumo wa usimamizi wa mishahara tayari umehamishwa kikamilifu kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Kisumu hadi JOOTRH. Sasa tunalipa wafanyikazi wetu moja kwa moja, na tangu mabadiliko hayo, mishahara imekuwa ikilipwa tarehe 27 kila mwezi,' alisema.

OFISI ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya Mpango Mkakati wa Ofisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2026/27 hadi 2030/31, kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi katika mamlaka za serikali … The post Wajadili maboresho Mpango Mkakati TAMISEMI first appeared on HabariLeo.

WIZARA ya Fedha imewataka wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili kuimarisha utawala bora. Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar ametoa wito huo katika hotuba yake iliyosomwa na kwa niaba ya yake na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Munde, wakati wa ufunguzi wa … The post ‘Wataalamu ununuzi, ugavi zingatieni Dira 2050’ first appeared on HabariLeo.

MNAMO Jumatatu, Aprili 29, 2024, mwendo wa alfajiri, maji yaliyokusanyika katika shimo chini ya reli huko Kijabe, Kaunti ya Kiambu yalielekea kwa kasi vijiji vya Kamuchira, Jerusalem, Ruiru, Githioro na Georges vilivyoko Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru. Maji hayo yaliyotoka vilima vya Kijabe na Kinare yalikuwa yamekwama kwa muda kwa kuwa njia ya kutokea ilikuwa imeziba, kabla ya kuta za shimo kupasuka takriban saa tisa usiku. Yalitiririka kwa nguvu yakisomba mawe, kung’oa miti na uchafu mzito. Maji hayo yalifika vijiji hivyo vitano kwa kasi ya kutisha, yakaua zaidi ya watu 60 na kuharibu mali ya thamani ya mamilioni ya pesa. Wengine walinusurika wakiwa na majeraha, lakini wengi walipoteza makazi, mifugo na mashamba yao ya kilimo. Watu 38 waliorodheshwa kuwa hawajulikani waliko wakati timu za uokoaji za mashirika mbalimbali zilipositisha shughuli za kuwatafuta. Ingawa mvua kubwa katika maeneo ya vilima vya Kijabe na Kinare ilitajwa kama chanzo cha mkasa huo, baadhi ya manusura wanaamini ulitokana na makosa ya kibinadamu. Takriban miezi 20 baadaye, manusura wa mkasa wa Maai Mahiu bado wanasumbuliwa na athari za mafuriko hayo. Kamera za runinga na wageni mashuhuri waliondoka kitambo; misaada ya kibinadamu sasa inatolewa mara chache tu kupitia mashirika ya wahisani na wasamaria wema wanaojitolea kuwasaidia kujenga upya maisha yao. Miongoni mwa manusura hao ni Bernard Kamau, mwalimu wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 40, ambaye alipoteza wanawe wawili, Maxwel na Rowan, katika mkasa huo huku akinusurika. “Ilikuwa hali ya kutisha. Niliwasikia wanangu wakilia lakini sikuweza kuwaokoa. Hakuna uchungu mkubwa kama kujua huwezi hata kuwaokoa watoto wako,” alikumbuka kwa masikitiko. Bw Kamau aliyekuwa mmiliki wa nyumba kumi, sasa anaishi ya kupanga mjini Maai Mahiu na anahangaika kuanza maisha upya. “Serikali ilitusahau kabisa baada ya ahadi nyingi. Familia nyingi bado hazijapona kutokana na mkasa huu,” alisema. Kwa upande wake, Mary Muthoni, 61, alipoteza watu wanane wa familia na sasa anaishi katika kijiji cha Memo, Murungaru, Kaunti ya Nyandarua. Usiku wa mkasa, alikuwa amewaalika watoto na wajukuu wake nyumbani kwake Ngeya karibu na kituo cha biashara cha Maai Mahiu kusaidia kuchangisha pesa kupata dhamana ya mwanawe Isaac Mwangi aliyekuwa amezuiliwa na polisi kwa mwaka mmoja. Kati ya watu 12 waliokuwa nyumbani humo, ni wanne pekee walionusurika; wanane waliangamia. Miongoni mwa waliokufa ni binti yake kitinda mimba aliyekuwa mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza, mkwe wake na wajukuu sita. Bi Muthoni, ambaye pia aliwahi kuwa mkimbizi wa mapigano ya kikabila mwaka 1988 Londiani na 1992 Narok, alisema alipoteza nyumba aliyokuwa amepanga, mali yote na ardhi yake yenye rutuba ambayo sasa imefunikwa na mawe na tope. “Tuliahidiwa makazi mapya na serikali lakini hakuna chochote kimefanyika. Tunaishi kwa shida,” alisema. Wahisani walimchangia Sh1 milioni, akatumia Sh750,000 kununua nusu ekari na kuanza kujenga nyumba, lakini ujenzi huo umekwama kwa kukosa fedha. Bw Alex Kimani, manusura mwingine, alipoteza familia yake yote na bado anateseka kisaikolojia kufuatia kutopatikana kwa miili ya binti zake. Msamaria mwema kutoka Amerika alimjengea nyumba, hatua iliyopunguza mzigo wa kodi. Ingawa ameoa tena, maisha bado ni magumu. “Siwezi kufanya kazi kwa sababu ya jeraha la mkono na kifua. Nilikuwa nauza matunda sokoni Maai Mahiu. Serikali ilitoa ahadi nyingi lakini ilituacha baada ya miezi michache,” alisema. Rais William Ruto alipotembelea eneo hilo Aprili 30, 2024, aliahidi serikali ingewatafutia waathiriwa ardhi wajenge makazi mapya. Zaidi ya mwaka mmoja baadaye, wengi bado hawana ardhi wala makazi. Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki hivi majuzi alisema bei ya juu ya ardhi imechelewesha mpango huo licha ya Sh250 milioni kutengwa. Wakati huo huo, wahisani kama Rotary International na Scann Foundation wamejenga nyumba 18 za vyumba viwili kwa baadhi ya familia zilizoathirika. Hata hivyo, manusura wengi bado wako njia panda, wakiwa na majeraha ya mwili na akili, na wakihisi kusahauliwa. Bado wanatumaini serikali itatimiza ahadi zake, iwape makazi na kurejesha ardhi yenye rutuba iliyopotea katika mkasa huo.

MAKUMBUSHO ya Dk Rashidi Mfaume Kawawa ni makumbusho yanayoelezea hali halisi ya maisha yake, maisha ya kawaida na maisha ya kiuongozi. Kiuongozi yanaelezea nyadhifa mbalimbali alizokuwa amezishika katika serikali ya Tanzania ikiwemo ya Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais. The post Makumbusho kuenzi filamu za Kawawa first appeared on HabariLeo.

KAULI ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, aliyotoa wakati wa kikaokazi cha kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na maofisa habari wa serikali kilichofanyika Dar es Salaam, ni mwongozo muhimu unaopaswa kutekelezwa kwa vitendo. The post Maofisa habari wana dhima kuiheshimisha Tanzania first appeared on HabariLeo.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe amemuelekeza Mkandarasi Mohammedi Builders Limited wa Mradi wa Ujenzi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha, kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla au ifikapo Mei 30, 2026 kama ilivyoanishwa kwenye mkataba. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo jijini Arusha, … The post Shemdoe: Stendi Kuu Arusha ikamilike Mei 2026 first appeared on HabariLeo.

BRASILIA, BRAZIL WABUNGE nchini Brazil mnamo Jumatano walipiga kura kufupisha kifungo ambacho Rais Jair Bolsonaro aliangushiwa kutoka miaka 27 hadi miaka miwili. Mswada walioupitisha kufupisha adhabu hiyo, hata hivyo huenda ukapata pingamizi kutoka kwa maseneta, Mahakama ya Juu na Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva. Kulikuwa na fujo bungeni wakati wa kupiga kura kwa mswada huo mnamo Jumatano jioni. Mwezi uliopita Bolsonaro alianza kutumikia kifungo chake baada ya kupatikana na hatia ya kupanga njama ya kupindua utawala wa Lula baada ya kupoteza uchaguzi wa 2022. Wabunge 291 waliunga mkono mswada wa kumfaa Bolsonaro huku 148 wakiupinga. Mswada huo unalenga pia kupunguza kifungo kwa raia ambao walinyakwa wakati ambapo wafuasi wa Bolsonaro walivamia ikulu, Mahakama ya Juu na Bunge mnamo Januari 2023. Hatua hiyo inakuja siku chache baada Seneta Flavio Bolsonaro, mwanawe mkubwa wa kiume wa Bolsonaro kutangaza kuwa anapanga kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Mbunge aliyewasilisha mswada huo Paulinho da Forca alikataa vishawishi vya wabunge kuwa Bolsonaro na wote walioshiriki maandamano hayo waachiliwe huru. “Hakuna cha kuachiliwa huru kwa sababu tumezungumza na wadau wote na njia pekee ya kuhakikisha amani ni kupunguza vifungo vyao,” akasema Paulinho. Zaidi ya watu 2,000 walinyakwa baada ya maandamano hayo jijini Brasilia ambayo yalilinganishwa na yaliyotokea Amerika Januari 2021 baada ya Donald Trump kushinda urais.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Habibu Suluo (pichani) amesema nauli ya Sh 1,000 inayotumika katika mabasi yaendayo haraka ni ya mpito. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Suluo amesema nauli hiyo inayotumika sasa iliridhiwa kuwa Sh 1,000 kwa tangazo la Serikali la Agosti 29, mwaka huu. The post Latra: Nauli ya Sh 1,000/- mwendokasi ni ya mpito first appeared on HabariLeo.

MISRI: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi wamefanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Misri ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Viwanda na Uchukuzi, Kamel Al-Wazir Desemba 18, 2025 Cairo, nchini Misri. Katika Mazungumzo yao, … The post Tanzania, Misri kuimarisha kilimo, viwanda, uchukuzi first appeared on HabariLeo.

VIONGOZI wa kidini katika Kaunti ya Mombasa, wamejiunga na wenzao nchini kupinga Mswada uliopendekezwa wa Mashirika ya Kidini wa 2024. Kulingana nao, mswada huo unakiuka uhuru wa kuabudu kwani baadhi ya mapendekezo yanalenga kudhoofisha nafasi ya kanisa katika jamii. Wameitaka kusimamisha mchakato mzima utakaopelekea utekelezaji wa mpango huo hadi ushirikishwaji wa umma ufanyike kikamilifu kote nchini na maoni yao yakusanywe. “Kama kanisa tunapinga kikamilifu Mswada wa Mashirika ya Kidini wa 2024 kwa sababu tunahisi hili ni sawa na kudharau taasisi za ibada na ni ukiukaji wa moja kwa moja wa haki zetu za kikatiba kuhusu uhuru wa kuabudu,” alisema Mchungaji Peter Onyango wa Kanisa la United Chapel lililo Changamwe, Kaunti ya Mombasa. Wahubiri hao chini ya muungano wa Mombasa Pastors Fellowship waliongeza kuwa, waliounda mswada huo hawakufuata taratibu zinazofaa za kisheria. “Tunaomba serikali ichukue tahadhari kubwa. Isikilize maoni ya makasisi na iondoe mswada huu. Sisi ni taifa linaloomba na tukiamua kuomba watatambua nguvu ya maombi,” akasema Askofu Tee Nalo wa Kanisa la Praise Chapel lililo eneo la Kizingo. Mswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa afisi ya msajili wa mashirika ya kidini, ambaye atasimamia utoaji na kufuta vyeti, kutunza sajili ya mashirika yote ya kidini, pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika taasisi zote za kidini nchini ili kuhakikisha zinafuata masharti. “Tunaiambia serikali ikae mbali na masuala ya kanisa. Mkiingilia kanisa basi tutaamua kuomba na tukifanya hivyo sote mtajua kweli nguvu ya maombi,” alisema Mchungaji Gabriel Gimel wa Kanisa la Imani Baptist lililo Maweni. Kulingana na mswada huo, hakuna mtu atakayeruhusiwa kubadilisha au kuhamasisha mwingine kutoka dini moja kwenda nyingine kwa ushawishi usiofaa au kwa kulazimisha, kutumia dini kukiuka haki za watoto, au kutoa mafundisho ya kidini kwa mtoto bila idhini ya mzazi au mlezi wake. Ukiukaji wa masharti haya ni kosa linaloadhibiwa, endapo mtuhumiwa atapatikana na hatia, kwa faini isiyozidi Sh10 milioni, kifungo kisichozidi miaka mitano, au vyote viwili. Mnamo Julai, Baraza la Mawaziri liliidhinisha mapendekezo kutoka kwa Jopokazi la Rais kuhusu Mashirika ya Kidini ili kulinda uadilifu wa utekelezaji wa dini. Mageuzi yaliyopendekezwa yaliandaliwa kufuatia janga la Shakahola ambapo zaidi ya watu 400 walikufa kwa njaa wakiamini walikuwa wakifunga ili wakutane na Yesu. Baraza la Mawaziri lilieleza kuwa, mswada uliopendekezwa unaunganisha udhibiti wa ndani wa mashirika ya kidini kupitia mashirika yao ya kidini, pamoja na usimamizi kutoka kwa taasisi za serikali kama vile vyombo vya usalama.

WADAU wa siasa na diplomasia wameeleza matarajio na imani yao kwa Tume Huru ya Uchunguzi ya vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu. The post Wadau waeleza matarajio tume ya uchunguzi first appeared on HabariLeo.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu wa kuneemesha neema ndogondogo na neema kubwa kubwa tumejaaliwa kukutana kwenye ukumbi huu ambapo leo maada yetu ni kuhusu kifo na mazishi ya muumini wa Kiislamu. Maswali yameibuka kwa nini Waislamu kuzikwa haraka kutokana na mauti ya Jaji wa Mahakama ya Juu Mohamed Ibrahim na mwanasiasa na waziri wa zamani Cyrus Jirongo. Jaji Ibrahim alizikwa jana katika makaburi ya Kariakor Nairobi kwenye hafla ambayo ilihudhuriwa na wakuu wa mahakama na viongozi wa kidini. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un na sote tunapitia njia hiyo hiyo ya nafsi yetu kuonja mauti. Swali hata hivyo ni kwa nini Muislamu anazikwa haraka au ndani ya saa 48? Kwa mujibu wa Mkuu wa Daawah kwenye Msikiti wa Jamia Sheikh Mohamed Sheikh, Mtume Mohamed (S.A.W) anasema kuwa mtu akifa lazima azikwe haraka iwezekanavyo. “Mtume anasema akifa, anaambia Ummah (Waislamu wanaoishi), ‘fanya haraka na unizike’.” Kwa mujibu wa Sheikh Mohamed, mazishi ya Muislamu huwa yanastahili kufanyika haraka na familia inapewa siku tatu za kuomboleza baada ya mazishi. “Msingi wa kuzika haraka ni kuepushia familia siku kadhaa za dhiki na pia kuhakikisha kuwa gharama ile ya mazishi inapungua. Mali ya marehemu inastahili kuwafaa wale ambao wamesalia badala ya kutumika kwenye matanga na shughuli zinazotokea,” akaongeza Sheikh Mohamed. Ndani ya huo muda wa saa 48 baada ya kufariki, maiti ya Muislamu huoshwa na jamii yake na marafiki kisha hufungwa vizuri kisha kuswaliwa msikitini kabla ya kuzikwa. “Muislamu huzikwa kama kichwa kinaangalia Mecca jinsi alivyofanyiwa mtume. Aidha ni vyema azikwe kwenye makaburi ili familia yake iweze kutembelea kaburu lake na kumwombea dua,” akasema. “Pia kumzika Muislamu nyumbani huwa si nafuu kwa sababu akizikwa kule nyumbani, familia yake huandamwa na msongo wa mawazo kwa kipindi kirefu kutokana na kuliona kaburi lile,” akasema. Msomi huyo wa dini anasema kuwa Muislamu anaweza kuzikwa mahala popote alipofia kwa sababu Allah anaamini ardhi yote iko sawa na inaweza kumsitiri muumini wake wakati wowote.

MPANGO wa Serikali wa kuchochea uchumi wa nchi kupitia Hazina za Ustawishaji Miundomsingi umekumbwa na pingamizi, wakosoaji wakishuku unanuiwa kuwa mbinu ya kuwinda kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2027. Mpango huo sasa umetajwa na Upinzani kuwa mkakati wa kampeni za Rais William Ruto kujipigia debe achaguliwe kwa Muhula wa Pili. Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro anasema huu si wakati wa kutoa ahadi bali kutekeleza manifesto ya 2022. Wachambuzi wa kisiasa nao wanasema kuwa Kenya haiwezi kuendelea zaidi iwapo matatizo ya kimsingi hayajatatuliwa yakiwemo gharama ya maisha, uboreshaji sekta ya afya na elimu. Tangu Rais William Ruto atoe hotuba kuhusu Hali ya Taifa katika Bunge Novemba 20, 2025, ngoma ya kustawisha uchumi wa Kenya kufikia Mataifa Yaliyostawi kama Singapore imezidi kurindima. Lakini viongozi wa Upinzani wamekuwa wakimkaba koo Rais Ruto kwa ajenda hii wakisema ni ahadi hewa kwa wananchi wanaotaabika kwa gharama ya juu ya maisha. “Hili jambo tunalosikia kuhusu Hazina ya Ustawishaji Miundomsingi na gumzo kuhusu Singapore ni maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za 2027. Tumekuwa hapa na tushawahi kusikia vitu kama hivi awali,” anasema Bw Nyoro. Anashikilia kwamba sababu pekee ya serikali kuchaguliwa ni kutimiza ahadi ilizotoa wakati wa kampeni, si kutoa ahadi mpya ilhali zile zilizotolewa bado hazijatimizwa. “Serikali ina jukumu la kueleza Wakenya inachofanya sasa, si kuwaambia inachopanga kufanya,” akasema mbunge huyo wa Kiharu. Hata hivyo, Serikali ya Kenya Kwanza inasukuma hazina ya Sh5 trilioni ya ujenzi wa miundomsingi kwa angalau miaka kumi ijayo. Ni mpango alioutangaza Rais Ruto bungeni wiki nne zilizopita akishangiliwa na wabunge. “Laiti kungekuwa na wabunge wengi zaidi wanaokosoa serikali. Lakini mnavyojua, bunge hili si la kidemokrasia kama ambavyo tungependa. Natumai labda kadri muda unavyosonga tutapata watu (wabunge) zaidi wa kuzungumzia jambo hili kwa sababu ni muhimu,” akasema Bw Nyoro akikashifu wabunge wanaounga baadhi ya sera za serikali bila kukosoa. Mtaalamu wa masuala ya kisiasa Martin Andati anakubaliana na Bw Nyoro kwa kiwango fulani lakini anahisi mbunge huyo anapinga serikali kwa sababu alivuliwa Uenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Ugavi katika Bunge la Kitaifa. Huku mpango wa serikali ukionekana wa kuvutia, wakosoaji wanaibua hofu kuhusu utumizi wa rasilimali za nchi na usimamizi wa mashirika ya serikali. “Ninachoshuku ni kwamba huenda kuna njama ya kutwaa fedha za malipo ya uzeeni. Walio uongozini wanatafuta mbinu za kuchota pesa za NSSF na kujaribu kuziweka kwenye muundomsingi,” anasema Bw Andati. Anashauri kuwa ili Kenya istawi, lazima kwanza sekta za elimu, afya, kilimo miongoni mwa nyingine ziimarishwe pamoja na serikali tawala kufuata nyayo za marais wa awali kama Marehemu Mwai Kibaki. “Rais angemalizia utekelezaji wa Ruwaza 2030 kwa sababu inaeleza bayana kabisa kinachohitajika kufanywa kustawisha Kenya,” asema Bw Andati. Rais pia anapewa changamoto kukabili zimwi la ufisadi uliokithiri katika sekta ya umma na kupunguza mikopo inayofyonza bajeti ya nchi.

RIPOTI mpya imetaja Nairobi, Kilifi, Kiambu, Machakos na Narok kama kaunti ambazo kufanya biashara na wakandarasi na wauzaji wa bidhaa ni sawa na “hukumu ya kifo”, kutokana na kucheleweshwa kwa malipo kwa muda mrefu. Ripoti ya hivi punde ya Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o, imebaini kuwa kaunti 47 zinadaiwa na wakandarasi na wafanyabiashara jumla ya Sh 177 bilioni. Kaunti hizo tano zilitajwa kuchangia zaidi ya asilimia 61 ya jumla ya madeni haya ikiwa ni sawa na Sh109 bilioni kufikia Septemba 30, 2025. Serikali za kaunti zinadaiwa Sh171 bilioni huku mabunge ya kaunti yakidaiwa Sh5.55 bilioni. Kaunti ya Nairobi chini ya Gavana Johnson Sakaja inaongoza kwa kuwa na madeni mengi ya Sh82.8 bilioni ambapo Sh62.3 bilioni ni madeni ya tangu jadi yaliyorithiwa kutoka kwa utawala uliotangulia. Serikali ya sasa imelimbikiza Sh20.5 bilioni katika kipindi cha miaka mitatu. Kaunti ya Kilifi chini ya Gavana Gideon Mung’aro inafuatia kwa deni la Sh9.6 bilioni, ambapo Sh8.2 bilioni ni deni la utawala wa sasa. Kaunti ya Kiambu inadaiwa Sh6.4 bilioni, huku deni la zaidi ya Sh2.3 bilioni likiwa la chini ya mwaka mmoja wa utawala wa Gavana Kimani Wamatangi. Machakos, chini ya Gavana Wavinya Ndeti, ina madeni ya Sh3.1 bilioni tangu alipoingia afisini. Kaunti ya Narok inadaiwa zaidi ya Sh5 bilioni, huku Gavana Patrick ole Ntutu akirithi deni la Sh265 milioni pekee. Kisheria, madeni yote yanapaswa kupewa kipaumbele katika mwaka wa kifedha unaofuata, lakini kaunti nyingi hazijazingatia agizo hilo. Uchambuzi wa madeni unaonyesha kuwa Sh46.83 bilioni (asilimia 26) ni ya chini ya mwaka mmoja, Sh24.12 bilioni (asilimia 14) ni ya kati ya mwaka mmoja na miwili, Sh19.62 bilioni (asilimia 11) ni ya kati ya miaka miwili na mitatu, huku Sh85.15 bilioni (asilimia 48) yakiwa ya zaidi ya miaka mitatu. Hata hivyo, baadhi ya kaunti zimepiga hatua ya kulipa madeni. Kaunti za Elgeyo Marakwet (Sh17.49 milioni), Lamu (Sh18.5milioni) na Turkana (Sh721 milioni) hulipa wakandarasi na wafanyabiashara kwa wakati. Kaunti nyingine zilizo na madeni ya chini ya Sh500 milioni ni Pokot Magharibi (Sh308 milioni), Nyeri (Sh342.3 milioni), Makueni (Sh402.5 milioni), Samburu (Sh457 milioni) na Baringo (Sh477.1 milioni). Kaunti ya Mombasa chini ya Gavana Abdulswamad Nassir haijalipa madeni iliyorithi ya zaidi ya Sh3 bilioni, lakini imelipa madeni ya kati ya miaka miwili na mitatu, na kubakisha Sh167 milioni pekee yaliyolimbikizwa chini ya utawala wa sasa.