Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametangaza kufanyika kwa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) linalotarajiwa kukutanisha…
GAVANA wa Nyeri Mutahi Kahiga ambaye amekuwa mwandani wa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ametangaza kuwa bado yuko UDA wala hajahamia chama kingine kuelekea uchaguzi wa 2027. Bw Kahiga amekuwa kati ya wanasiasa ambao hujitokeza mara kwa mara kumtetea Bw Gachagua na kuishambulia serikali ya Rais William Ruto kwa kumhangaisha. Mnamo Alhamisi wiki jana, alikuwa na Bw Gachagua mjini Nyeri ambapo walihutubia mkutano wa kisiasa, wengi wakikisia ashajiunga na DCP. “Mimi bado niko UDA na huwezi kubadilisha hilo,” akasema akiwahutubia waumini katika Kanisa la St Paul Kariki, eneobunge la Othaya, Kaunti ya Nyeri, Jumapili, Januari 11, 2026. Ibada katika kanisa hilo pia ilihudhuriwa na Rais Ruto, naibu wake Prof Kithure Kindiki na viongozi wengine wa serikali. Bw Kahiga alitumia jukwaa hilo kuwataka Wakenya watofautishe siasa na masuala ya uongozi akisema kwa sasa anamakinikia kutimiza ajenda yake ya maendeleo kwa wakazi wa Nyeri. “Siku za kupiga siasa zitakuja lakini kwa sasa sote tumuunge mkono Rais Ruto ili afanye kazi yake,” akasema Bw Kahiga. Bw Kahiga pia alisema viongozi ambao wanamuunga mkono Rais Ruto wana haki ya kufanya hivyo hadharani. “Nilimpigia Ruto kura, yeye ni rais wangu na mimi ni gavana. Sijui kwa nini baadhi ya watu wanachanganyikiwa? Bado nina rais,” akaongeza Bw Kahiga akishangiliwa na waumini. Kiongozi huyo alisisitiza kuwa ni jukumu lake la kikatiba kufanya kazi na serikali ya kitaifa na kumlaki Rais kila mara anapozuru kaunti hiyo.
HUKU siasa za Magharibi mwa Kenya zikionyesha dalili za kubadilika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, chama cha Ford Kenya chini ya uongozi wa Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula bado kina nafasi ya kujijenga upya kama mhimili wa umoja wa kisiasa wa eneo la Mulembe. Hii ni licha ya kura za maoni za hivi karibuni kuonyesha kuwa vyama vikubwa kama ODM, UDA na hata DCP vinaonekana kupenya zaidi katika eneo hilo. Kura ya maoni ya Infotrak iliyofanywa katika kaunti za Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia na Trans Nzoia inaonyesha kuwa Ford Kenya inaungwa mkono na takriban asilimia nne pekee ya wapiga kura. Ingawa takwimu hizi zinaweza kuonekana kama pigo kwa chama hicho, wachambuzi wa siasa wanasema bado kuna nafasi kubwa ya Ford Kenya kujijenga upya, hasa ikizingatiwa ushawishi wa kiongozi wake Wetang’ula na historia ndefu ya chama hicho katika siasa za Kenya. Wetang’ula kwa sasa anashikilia wadhifa wa Spika wa Bunge la Kitaifa, nafasi ya juu na muhimu serikalini inayompa hadhi ya kitaifa na fursa ya kujijenga kama kiongozi wa kuunganisha siasa za Magharibi mwa Kenya. Akiwa kiongozi wa juu zaidi kutoka eneo hilo ndani ya serikali ya Kenya Kwanza, Wetang’ula anaonekana kama mhimili muhimu wa maslahi ya eneo hilo katika siasa za kitaifa. Tofauti na ANC ya Musalia Mudavadi ambayo hatimaye “ilimezwa” na UDA baada ya kujiunga na muungano wa Kenya Kwanza, Ford Kenya imeendelea kusimama kama chama huru ndani ya muungano huo. Wetang’ula amesisitiza mara kwa mara kuwa Ford Kenya haitamezwa na UDA, akilenga kukilinda kama sauti ya kisiasa ya watu wa Magharibi mwa Kenya ndani ya serikali. Ford Kenya pia kinabaki kuwa chama kikubwa zaidi kutoka Magharibi mwa Kenya ndani ya Kenya Kwanza, baada ya ANC kuvunjwa. Ushindi wa Ford Kenya katika uchaguzi mdogo wa Seneti Bungoma, ambapo Wafula Wakoli alimshinda mgombea wa UDA kwa kishindo, ni ishara kuwa chama bado kina mizizi thabiti katika ngome zake za jadi. Kihistoria, Ford Kenya ni miongoni mwa vyama kongwe zaidi nchini, kilichozaliwa kutoka harakati za mageuzi ya kisiasa za miaka ya 1990. Chama hicho kimetoa vigogo wengi wa siasa akiwemo Michael Kijana Wamalwa, Masinde Muliro (kupitia urithi wa kisiasa wa Ford), na baadaye Moses Wetang’ula mwenyewe, ambaye amekuwa mhimili wa siasa za Magharibi kwa miongo kadhaa. Katika chaguzi zilizopita, Ford Kenya imekuwa sehemu ya miungano mikubwa ya upinzani kama NASA mwaka 2017, ambapo Wetang’ula alikuwa mmoja wa vinara wa muungano huo. Ingawa muungano huo haukufanikiwa kushinda, ulidhihirisha uwezo wa Ford Kenya kushiriki katika siasa za kitaifa kwa kiwango cha juu. Mwaka 2022, Ford Kenya ilipojiunga na Kenya Kwanza, chama kilifanikiwa kuingia serikalini na kikapata nyadhifa muhimu. Hatua hii imeimarisha hoja kuwa Ford Kenya bado ni chama chenye uzito katika maamuzi ya kitaifa. Changamoto kuu kwa sasa ni ushindani mkali kutoka kwa ODM, UDA na vyama vipya kama DCP vinavyojaribu kujipenyeza katika eneo la Magharibi. Hata hivyo, wachambuzi wanaamini kuwa iwapo Wetang’ula atatumia vyema nafasi yake kama Spika na kuendeleza umoja wa viongozi wa Magharibi, Ford Kenya inaweza kujijenga upya kama jukwaa la kisiasa la kuunganisha eneo hilo. Uchaguzi mkuu wa 2027 unavyokaribia, mustakabali wa Ford Kenya utategemea uwezo wake wa kuvutia kizazi kipya cha wapiga kura, kujitofautisha ndani ya Kenya Kwanza, na kutumia historia na ushawishi wa Wetang’ula kama mtaji wa kisiasa. Katika mazingira ya siasa yanayobadilika haraka, Ford Kenya bado haiwezi kupuuzwa katika hesabu za siasa za Magharibi mwa Kenya.
BERLIN, UJERUMANI KANUNI za sheria ya kimataifa zinatumika kwa wote, ikiwemo Amerika, Waziri wa Fedha na Naibu Chansela, Lars Klingbeil, alisema Jumapili, Januari 11, 2026 akirejelea vitisho vya Rais Donald Trump kuhusu kuteka taifa la Greenland. “Uamuzi kuhusu hatima ya Greenland upo mikononi mwa Denmark na Denmark pekee. Hadhi na uadilifu kimaeneo ni sharti iheshimiwe,” alisema Klingbeil kabla ya kusafiri kuelekea Washington kwa mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka mataifa makuu duniani (G7) yenye mifumo iliyoendelea kiuchumi. Hatua ya jeshi la Amerika kupokonya Denmark kisiwa hicho chenye utajiri itatikisa mkataba baina ya Amerika Kaskazini na Uropa (NATO) na kuzidisha utengano kati ya Trump na viongozi wa Uropa. “Tunaongeza usalama katika ukanda huo pamoja kama wandani wa NATO, sio katika upinzani dhidi yetu,” alisema Klingbeil. Mkutano wa G7 utakaofanyika Jumatatu utaangazia upatikanaji wa madini muhimu huku nchi za Magharibi zikinuia kupunguza kutegemea China kwa kuzingatia hatua za Beijing kuanzisha vidhibiti vikali kuhusu uuzaji wa madini adimu katika mataifa ya kigeni. Klingbeil alisema Ujerumani inataka kupanua ushirikiano kimataifa eneo hili ili kuimarisha usalama wa bidhaa, kupunguza utegemezi na kuhakikisha mazingira ya mfumo wa uchumi yanayoweza kutegemewa. “Ndiposa ni muhimu tushauriane na washiriki wetu kimataifa na kila inapowezekana –tuchukue hatua pamoja,” alisema. China inatamalaki mfumo wa kusambaza madini adimu, huku ikisafisha kati ya asilimia 47 na 87 ya shaba, lithiamu, kobalti, graphite na madini adimu, kulingana na Shirika la Kimataifa kuhusu Nishati.
PETER Mbiyu Koinange, aliyezaliwa mwaka wa 1907, alikuwa miongoni mwa kundi la kwanza la wanafunzi wa Shule ya Alliance ilipoanzishwa 1926. Mwaka 1938, aliweka historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kupata shahada ya uzamili (MA). Baba yake, Chifu Mkuu Koinange wa Mbiyu, alimpeleka Amerika mwaka 1927 kumalizia elimu ya sekondari na kujiunga na masomo ya juu, hivyo kuwa Mkenya wa kwanza kusomea Amerika. Mbali na kusomea Ulaya kwa miaka mingi, Koinange alikuwa mtu mwenye sifa bora za kielimu na kijamii. Baadaye alikuja kuwa mshirika wa karibu sana wa Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, katika kipindi chote cha uongozi wake, kiasi cha kupewa jina la utani “Kissinger”, akilinganishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika wa wakati huo, Henry Kissinger. Alianza masomo katika Chuo cha Hampton, West Virginia, kisha akaendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Ohio Wesleyan ambako alipata shahada ya kwanza (BA). Baadaye alisomea shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Columbia. Aliporejea Kenya, yeye na babake walianzisha Chuo cha Ualimu cha Kenya huko Githunguri, Kiambu, ambacho kilikuwa msingi wa shule huru katika Kenya wakati wa ukoloni. Taasisi hizi zilikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania uhuru. Kati ya 1938 na 1947, Koinange alikuwa mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ualimu Kenya, Githunguri, na kati ya 1951 na 1959 aliwakilisha chama cha Kenya African Union (KAU) barani Ulaya. Mwaka 1947 alimkabidhi Kenyatta usimamizi wa shule hiyo na akaenda Uingereza kusomea stashahada katika Taasisi ya Elimu ya Chuo Kikuu cha London, kisha masomo ya juu katika Shule ya Uchumi ya London (LSE). Koinange na Kenyatta walikuwa wamekutana awali Uingereza na waliendelea kuwasiliana hata baada ya Koinange kuondoka nchini humo. Hata hivyo, kutokana na vita vya Mau Mau na kutangazwa kwa Hali ya Hatari mwaka 1952, Koinange hakuweza kurejea Kenya kwa miaka mingi. Babake na jamaa zake wengi walikamatwa au kuwekwa vizuizini. Akiwa Uingereza, mbali na kuiwakilisha KAU, Koinange alishiriki mikutano na maandamano ya kupigania uhuru wa Afrika. Alikutana na Kwame Nkrumah wa Gold Coast, ambaye baadaye alimpa kazi kama Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Afrika mjini Accra kati ya 1959 na 1961 baada ya nchi hiyo kupata uhuru na kujulikana kama Ghana. Akiwa London, aliwasiliana pia na viongozi wengine mashuhuri wa kupigania uhuru wa nchi za Afrika kama Nnamdi Azikiwe wa Nigeria, George Padmore wa Trinidad na Fenner Brockway wa Uingereza. Nyaraka za siri za idara ya usalama ya Uingereza (MI5) zilizotolewa baadaye zinaonyesha alivyopokea barua nyingi sana kutoka kote duniani kiasi kwamba ni vigumu kuelewa aliwezaje kuzishughulikia katika enzi hiyo ambayo hakukuwa na teknolojia ya kielektroniki. Hii inaonyesha mtandao wake mpana wa kimataifa. Mpiganiaji uhuru Oginga Odinga, ambaye baadaye alikuwa makamu rais wa kwanza Kenya ilipopata uhuru, alimwalika Koinange kushiriki mkutano wa kwanza wa Lancaster House wa kuandaa Katiba mwaka 1960. Alirejea Kenya mwaka 1961, akachaguliwa Mbunge wa Kiambaa mwaka 1963 na Kenyatta akamteua Waziri wa Masuala ya Afrika katika Baraza la Mawaziri la kwanza. Baadaye alihudumu kwa muda mfupi katika wizara ya elimu kabla ya kuhamishiwa Ofisi ya Rais kama Waziri wa Nchi anayesimamia Utawala wa Mikoa kuanzia 1966 hadi kifo cha Kenyatta mwaka 1978. Licha ya elimu na uhusiano wake, Koinange aliamini Kenyatta alikuwa na sifa bora za uongozi. Ushirika wao ulikuwa mkubwa kiasi kwamba waliitana “Ngorobi” inayomaanisha mtu mbishi. Wengine walidai Koinange ndiye aliyekuwa na mamlaka halisi nyuma ya pazia, lakini aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Kareithi, alipinga madai hayo. Maisha ya Koinange yalizunguka kazi na urafiki wake na Kenyatta, hadi akasahau familia yake. Wakati wa kifo chake, hakuwa na mali nyingi, na aliacha madeni kuliko mali. Alifariki mwaka 1981, miaka mitatu baada ya Kenyatta, akiwa na umri wa miaka 74.
HIVI ajali ya barabarani ikatokea saa hii ikimhusisha ng’ombe na binadamu, utampa yupi pole na kumtakia afueni ya haraka? Bila shaka pole na sala zote ni kwa binadamu. Ng’ombe tunamgeuza nyama mara moja kwa kuwa kupona kwake hakuna manufaa mengi kwetu. Hata hivyo, mara nyingine mambo hayaendi yanavyotarajiwa. Hivi majuzi nchini Tanzania, ajali ambapo msanii kwa jina Shilole amemgonga ng’ombe kwa gari lake. Badala ya watu kumpa pole msanii wao, wengi walikimbia kwenye mitandao ya kijamii kumtolea pole ng’ombe huyo wasiyemjua, wakamtakia nafuu ya haraka. Shilole naye? Potelea mbali! Akutane na ya kumkuta eti, tena pole zake apewe na Chama (tawala) Cha Mapinduzi (CCM)! Hivi utakuwa umewafanyia watu kitu gani ndio wamliwaze ng’ombe kukuzidi? Kwani hawapendi nyama ya ng’ombe ilhali wewe binadamu ukifa hawatakula? Thamani ya uhai wa binadamu imeenda wapi? Labda binadamu mwenyewe ajithamini kwanza. Watanzania wamechoshwa na kuchushwa na wasanii wao ambao wanaiunga mkono serikali dhalimu ya CCM ambayo iliwaua maelfu ya watu walioandamana kupinga ukandamizaji na uchafuzi wa uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana. Wasanii hao, ambao wametajirika haraka kwa kushabikiwa na wananchi wa kawaida, walichemsha pakubwa walipopuuza dhuluma na mateso waliyofanyiwa raia na kufungamana na kachinja Suluhu Hassan. Baadhi yao, kama Diamond Platinumz niliyemshabikia si haba, walijitokeza na kulaani maandamano, hata wakawadharau waandamanaji kwa kuwaita wazembe wasiotaka kufanya kazi. Sasa kinawaramba kweli kwa sababu hakuna anayetaka miziki yao hiyo, mashabiki wameacha kuwafuata mtandaoni, hakuna anayetaka shoo zao, nasi huku nje tunatazama sinema yenyewe kwa tabasamu ya mwaka na mafunda makubwa ya vinywaji tuvipendavyo. Serikali yao inawaambia mashabiki watofautishe kazi na siasa na kazi, eti muziki ni kazi kama nyingineyo ambayo kwayo msanii anatia tonge kinywani, lakini Watanzania wameshupaa! Hakuna msanii anayeweza kuandaa shoo yoyote hata kwenye baa ya kijijini kwao kwa kuwa walikataa kutumia akili na kuonyesha huruma ilipohitajika zaidi. Hata mashabiki Wakenya wamewakataa. Juzi nimeona waliozoea kupitia mpakani Lungalunga na kuingia Kenya, hasa pwani, na kutumbuiza huko wakiambiwa wathubutu kufanya hivyo ili wajue kilichomtoa kanga manyoya! Wanasiasa wa pwani ya Kenya waliozoea kujizolea umaarufu kwa kuwaleta wasanii wa Tanzania nchini wametishiwa kutiwa adabu. Sijui kwa mijeledi, mawe, kutemewa mate, kumwagiliwa maji ya chumvi au kunyimwa kura, lakini wametishiwa. Binafsi, tangu zamani shabiki mkuu wa wasanii wa Tanzania, nimefuta nyimbo zao na kuacha kuwafuata mtandaoni kwa kuwa sijakolewa na uzuzu kiasi cha kuwa na ubia na watu wanaotumia ubongo kukinga shingo na jua. Kama tusemavyo Kenya, wasanii wa Tanzania watakula ujeuri wao kwa sababu wamevimba vichwa hivi kwamba hawawezi kufanya kitu rahisi kama kuomba msamaha. Kiburi kina gharama kumbe? -Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika ([email protected])
MVUTANO ndani ya chama cha ODM umechukua mkondo mpya baada ya Katibu Mkuu, Edwin Sifuna kufufua upya masuala tata yaliyoandama Uchaguzi Mkuu wa 2022, akimlaumu Mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohamed kwa madai ya ubadhirifu wa fedha na uzembe. Kauli za Sifuna, zilizotolewa Januari 3, 2026 katika mazishi ya Alice Wangari Gakuya huko Murang’a, zimezua mjadala mpana ndani ya upinzani na kufungua majeraha ya kisiasa kwa wale ambao hawakupona kufuatia kushindwa kwa Raila Odinga kwa tofauti ndogo ya kura katika uchaguzi uliopita. Akizungumza mbele ya viongozi wakuu wa upinzani akiwemo aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Sifuna alimlaumu Junet kwa kulaumu hadharani mchango wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akisema ni fedheha kumlenga kiongozi aliyebeba mzigo mkubwa wa kampeni ya Azimio, hususan Mlima Kenya. “Kwa mara ya kwanza Baba Raila Odinga alipata kura zaidi ya milioni moja Mlima Kenya. Hiyo haikuwa bahati, ni kwa sababu Uhuru Kenyatta alitusaidia kwa hali na mali,” Sifuna alisema, kabla ya kudai kuwa baadhi ya viongozi walitumia visivyo fedha hizo badala ya kuzitumia kulipa maajenti wa chama. Akielekeza lawama moja kwa moja kwa Junet, Sifuna alihoji ni lini fedha za Uhuru zilianza kuonekana kuwa ‘mbaya’, akimlaumu mbunge huyo kwa kutumia vibaya rasilmali za kampeni na kushindwa kulinda kura siku ya uchaguzi. Kauli hizo zimeungwa mkono kwa njia isiyo ya moja kwa moja na aliyekuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga, Bi Martha Karua, ambaye alisema kuwa karibu majukumu yote ya uratibu wa kampeni, ikiwemo maajenti wa chama, yalikuwa mikononi mwa Junet. Akizungumza katika mahojiano ya televisheni ya NTV Januari 8, 2026, Karua alisema alimhimiza Sifuna “aseme kwa sauti zaidi” ili ukweli ujulikane. “Baba alimwamini Junet kwa karibu kila kitu. Kama kuna mtu ana taarifa zaidi, aseme. Wamwage mtama,” Karua alisema, akifichua kuwa wagombea wengi walilalamika kuhusu majina ya maajenti kubadilishwa au kutokuwepo kabisa. Karua alikiri kuwa hakuwa na uwezo wa kufuatilia kila jambo kwani alijiunga na kampeni miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi na alikuwa akizunguka maeneo mengi, hususan Mlima Kenya, huku pia akihitajika kwa kampeni za kitaifa. Madai haya yanajiri wakati ambapo ODM inapambana na mgawanyiko wa ndani kuhusu msimamo wa chama kuelekea 2027, hasa baada ya Sifuna kusisitiza kuwa Raila Odinga hakuwahi kuagiza chama kumuunga mkono Rais William Ruto. “Sisi kama ODM, Baba hakuwahi kutuambia tumuunge mkono Ruto 2027. Aliniambia Kasongo 2027 nyumbani,” Sifuna alitangaza, kauli iliyopokewa kwa shangwe na baadhi ya wafuasi na wasiwasi kwa wengine. Hali hiyo imezidi kuchochewa na kauli ya Katibu Mkuu wa Jubilee, Jeremiah Kioni, ambaye alimshutumu Junet kwa kile alichokitaja kama kusaliti muungano wa Azimio baada ya uchaguzi. Kioni alidai Junet alishindwa kushiriki maandamano ya kutaka Azimio itambuliwe kama muungano wa wengi Bungeni na badala yake akashirikiana na Spika Moses Wetang’ula kuzima juhudi hizo. “Junet alifanya kazi na Wetang’ula kuzuia Azimio kupata haki yake. Leo yeye ndiye Kiongozi wa Wachache akizungumza kwa niaba ya wengi,” Kioni alisema. Kwa upande wake, Sifuna amejaribu kujinasua dhidi ya madai ya kushambulia Uhuru Kenyatta kwa kumuomba msamaha hadharani katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo, akisema baadhi ya viongozi wa ODM wamekuwa wasaliti wa kiongozi aliyewasaidia pakubwa 2022. Wachambuzi wa siasa wanasema mvutano huu unafufua masuala ambayo yalikumba Azimio 2022 na pia ni dalili za mapema za hali ya siasa kuelekea 2027. Kulingana na Junet Mohamed, sakata la kukosekana na kutolipwa kwa maajenti wa Azimio katika Uchaguzi Mkuu wa 2022 halikuwa kosa la uongozi wa ODM wala waratibu wa kampeni, bali lilitokana na maamuzi yaliyofanywa na watu waliokuwa karibu na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta nje ya mifumo rasmi ya chama. Katika taarifa aliyotoa Jumamosi, Mbunge huyo wa Suna Mashariki alisema fedha zilizotengewa maajenti wa Azimio zilikabidhiwa Muhoho Kenyatta, ndugu wa rais huyo wa zamani, hatua ambayo alidai iliondoa jukumu hilo mikononi mwa chama na mgombea urais Raila Odinga.
DALILI zinaendelea kujitokeza kuwa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i, anaweza kujitenga na muungano mpana wa upinzani na kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027 kwa tiketi ya chama cha Jubilee, hatua inayoweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa siasa za upinzani nchini. Haya yanajiri huku Katibu Mkuu wa Jubilee, Jeremiah Kioni, akichukua msimamo mkali dhidi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akimshambulia kwa kudai Mlima Kenya unastahili kuwa na chama kimoja kikuu cha kisiasa. Bw Matiang’i anategemea kwa kiwango kikubwa kura za eneo la Mlima Kenya ambako mlezi wake kisiasa na kiongozi wa Jubilee Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ana umaarufu. Akizungumza katika mahojiano na Spice FM, wiki hii, Kioni alitaja kauli za Gachagua kama za kurudisha nyuma demokrasia na akisema zinakiuka Katiba ya Kenya inayolinda mfumo wa vyama vingi. “Nilimsikia mtu akisema eneo hili litakuwa na chama kimoja pekee. Hiyo ni kauli ya kurudisha nyuma nchi na ni kinyume na Katiba,” alisema Kioni. Kioni alionya kuwa kauli za aina hiyo zinaweza kuleta mpasuko mkubwa ndani ya upinzani na hata kulazimu Jubilee kuchukua mkondo wake wa kisiasa. “Tulipigania Katiba hii. Sitatoa kafara mustakabali wangu wa kisiasa kwa sababu ya kauli zinazotolewa ovyo. Nikiendelea kusikia maneno kama hayo, nitaondoka na nitafuata njia yangu,” aliongeza. Kauli za Kioni zimechukuliwa na wachambuzi wa siasa kama ishara wazi ya Jubilee kujitenga polepole na muungano wa upinzani unaohusishwa na Gachagua, huku chama hicho kikimjenga Matiang’i kama mgombea wake wa urais. Chama hicho, kinasisitiza kuwa kingali ndani ya muungano wa upinzani. Wakati huo huo, Dkt Matiang’i, ambaye ni Naibu Kiongozi wa Jubilee, amekuwa akionekana hadharani zaidi na kufanya mikutano ya kisiasa, jambo linaloashiria maandalizi ya kampeni kitaifa. Hata hivyo, hali hii haijapokelewa vyema na baadhi ya watu wanaomuonya dhidi ya kutegemea Uhuru kufanikisha azma yake ya urais. Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, alimtahadharisha Matiang’i dhidi ya kutegemea mno uungwaji mkono na Uhuru Kenyatta, akisema historia inaonyesha Uhuru alishindwa kumfikisha Raila Odinga Ikulu licha ya kumuunga mkono akiwa rais. “Kama Uhuru hakuweza kumfanya Raila awe Rais, Matiang’i akijiamini sana, atajipata pabaya,” alisema Atwoli. Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa huenda Dkt Matiang’i akachochewa kujitenga na muungano wa upinzani kutokana na kura ya maoni inayomuonyesha akishinda vinara wengine kwa umaarufu. Kura ya maoni ya Infotrak wiki jana inaonyesha Matiang’i kama mpinzani wa karibu zaidi wa Rais William Ruto kuelekea 2027. Kulingana na kura hiyo, Ruto anaongoza kwa asilimia 28 huku Matiang’i akifuata kwa asilimia 13. Vinara wengine wa upinzani waliotajwa ni Kalonzo Musyoka (12), Rigathi Gachagua, Martha Karua na David Maraga, waliopata asilimia kati ya tano na mbili. Asilimia 31 ya Wakenya bado hawajaamua watamuunga mkono nani. Mchambuzi wa siasa Dkt Isaac Gichuki anasema kinachoonekana kama umaarufu wa Matiang’i kinaweza kumponza asipofanya maamuzi ya busara na kuungana na wenzake katika upinzani. “Matiang’i anakumbukwa kwa nidhamu na uthabiti wake kama afisa wa serikali na sio mwanasiasa. Bila muungano mpana wa upinzani, safari yake itakuwa ngumu,” anasema Dkt Gichuki. Anasema iwapo ataamua kuwania kwa tiketi ya Jubilee atagawanya kura za upinzani lakini huenda matarajio yake katika Mlima Kenya yasitimie. “Upinzani ukigawanyika, utampa Ruto nafasi kubwa ya kushinda muhula wa pili. Lakini huenda Matiang’i akashangaa sana kwa kuwa Mlima Kenya unaweza kwenda kinyume na juhudi zozote za kugawanya kura kwa lengo la kumbandua Ruto” anasema. Huku hali ikiwa tete, macho yote sasa yanaelekezwa kwa hatua atakayochukua Matiang’i ikiwa ataendelea kusukuma ajenda ya Jubilee pekee au atajaribu kusuka upya muungano wa upinzani ili kuipa serikali ya Kenya Kwanza changamoto kubwa 2027 Wachambuzi wanasema dalili za Matiang’i zinaonekana katika mkakati wa Jubilee wa kujijenga upya hasa katika Mlima Kenya ambako kuna vyama vingine ikiwemo DCP ya Bw Gachagua eneo ambalo kulingana na kura ya maoni ya Infortrak, asilimia 36 ya wapiga kura ambao bado hawajafanya uamuzi wa mwisho. Kwa sasa, vinara wengine wa upinzani akiwemo Gachagua, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Eugene Wamalwa, Justin Muturi na George Natembeya wanasisitiza kuwa wamejitolea kuungana katika uchaguzi mkuu wa 2027 huku wachambuzi wakisema huo ndio mtihani wao mkubwa. Dkt Matiang’i amekuwa akikutana na baadhi ya vinara wa upinzani bila Gachagua, Muturi, Kalonzo na Wamalwa hatua inayoonekana kama ya kujenga mrengo wake kivyake. Dkt Matiang’i amekuwa akipuuza madai kuwa muungano huo unagawanyika akisema kusuka muungano wa vyama vingi sio rahisi na lazima kuwe na tofauti za maoni japo kauli za washirika wake zinaonyesha anajipanga kivyake kupitia Jubilee.
DAR ES SALAAM; Wafanyabiashara wapatao 500 jijini Dar es Salaam wameshiriki mafunzo maalumu ya ununuzi wa umma yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za serikali kuwawezesha wazawa kushiriki kikamilifu katika zabuni za miradi ya umma. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis … The post PPRA yawapa mafunzo wafanyabiashara Dar first appeared on HabariLeo.
ALIYEKUWA ajenti mkuu wa Azimio katika uchaguzi wa urais 2022, Saitabao Ole Kanchory, amesema kuwa endapo aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga angekuwa hai leo, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed asingekuwa akizungumza namna anavyofanya kwa sasa. Akizungumza katika mahojiano Jumatano, Januari 7, 2025, Kanchory, ambaye amekuwa akikosoa viongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) wanaounga mkono serikali jumuishi, alisema Junet na mawaziri waliokuwa viongozi wa ODM wanamsaliti Raila akiwa kaburini kutoka na mvutano unaoshuhudiwa ndani ya chama hicho. Kulingana na Bw Kanchory, jambo linalomuumiza zaidi ni mienendo ya viongozi waliokuwa karibu na Raila, akiwemo Junet Mohamed, Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi na Waziri wa Fedha John Mbadi tangu kifo chake. Alisema viongozi hao wanaendesha siasa zinazokiuka misingi na maono ya Raila Odinga, akiongeza kuwa kama Raila angekuwa hai leo, wangekuwa wakizungumza kwa tahadhari zaidi na kuonyesha uwajibikaji. Kanchory alisisitiza kuwa endapo Raila angefufuka kutoka kaburini, angewafuta kazi viongozi hao mara moja, hasa wale waliojiunga na serikali chini ya muafaka wake na Rais William Ruto. Alidai kuwa Mbadi, Wandayi na Junet wametumia vibaya nyadhifa walizoaminiwa na Raila kwa manufaa yao binafsi badala ya maslahi ya taifa, kinyume na alichosimamia kiongozi huyo marehemu. Kauli hizi zinajiri wakati ambapo ODM inakumbwa na migogoro ya ndani, huku Katibu Mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna akilaumiwa vikali kwa kupinga wanaounga azma ya Rais William katika uchaguzi wa 2027. Chama hicho kimegawanyika kuhusu mwelekeo wake baada ya Raila. Sifuna amesisitiza kuwa ODM inapaswa kusimamisha mgombeaji wa urais kumpinga Rais Ruto, akisema hata yeye ana sifa za kuwania wadhifa huo. Hata hivyo, kiongozi wa chama Oburu Odinga amedai kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kiongozi wa chama ndiye mgombeaji rasmi wa urais. Junet Mohamed aliunga mkono kauli hiyo, akisema Oburu ndiye msemaji na mbeba bendera wa chama kwa sasa, na mwenye mamlaka ya kuamua masuala ya uteuzi wa mgombeaji wa urais.
ARUSHA; WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kuweka mikakati madhubuti itakayowawezesha ku jitegemea katika uendeshaji wa shughuli zao, badala ya kuendelea kutegemea bajeti ya Serikali Kuu ili kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050. Aidha, Kapinga ameagiza Wakala wa Vipimo (WMA) ku hakikisha unawafikia … The post Taasisi zatakiwa kujizatiti utekelezaji wa Dira 2050 first appeared on HabariLeo.
MBUNGE wa Githunguri, Bi Gathoni Wamuchomba, amemshambulia vikali aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kufuatia madai ya vitisho na shinikizo za kisiasa. Bi Wamuchomba alimtuhumu Bw Gachagua kwa kudaiwa kumtisha na kumlazimisha mara kwa mara aondoke katika Chama cha United Democratic Alliance (UDA) na kujiunga na Chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP). “Sasa Wamunyoro anajaribu kunitisha kwa kunilazimishwa kupitia mashambulizi ya mara kwa mara nijiunge na DCP. Ninalazimika kuweka wazi ukweli kwake,” aliandika Mbunge huyo kwenye ukurasa wake wa X mnamo Jumatatu January 5. Akieleza hasira zake kupitia mtandao wa X, Jumanne Januari 6, 2026, Bi Wamuchomba alimtaja Bw Gachagua kama mtu anayewachukia wanawake, akitaja matukio kadhaa anayodai yanaonyesha dharau yake kwa viongozi wa kike. “Wamunyoro ni mwenye chuki dhidi ya wanawake. Wakati wa hoja ya kumng’atua, wabunge wawili wanawake walidai hadharani kuwa aliwatukana kwa maneno yasiyofaa kuchapishwa,” alisema Bi Wamuchomba. Kwa mujibu wa mbunge huyo, aliyekuwa Naibu Rais anadaiwa kutumia baadhi ya washirika wake wakuu kuwatisha wanasiasa wa Mlima Kenya waliokataa kujiunga na chama hicho cha upinzani. Bi Wamuchomba aliwatuhumu Seneta wa Nyandarua, John Methu na Seneta wa Kiambu Karungo wa Thang’wa kwa madai kuwa vibaraka wanaotumiwa na Gachagua kuwatisha viongozi wanaounga mkono serikali katika eneo la Mlima Kenya. “Anamtumia Seneta Karungo kuwadharau wale wasio katika chama cha ‘Mlima’. Karungo bado ni Seneta wa UDA lakini anapiga kelele kuhusu chama kingine,” alisema. Aliongeza: “Kama chama hiki kina nguvu kweli, kwa nini Methu, Karungo na Nyutu wasijiuzulu kwanza, halafu tuwachague tena kupitia chama chao kipya cha ‘masikio’? Sijiungi na chama hicho, nitasalia UDA hadi 2027.” Katika kauli yake, Mbunge huyo alisema si mara ya kwanza kukumbana na vitisho kama hivyo kutoka kwa Bw Gachagua, akiongeza kuwa mwaka 2023 alipitia hali kama hiyo baada ya kupiga kura dhidi ya Mswada wa Fedha. Bi Wamuchomba, ambaye hapo awali alikuwa mfuasi sugu wa Bw Gachagua, sasa ameibuka kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakubwa, akimlaumu kwa kukosa nidhamu kisiasa.
ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua Ijumaa, Januari 9, 2026, alidai kuwa maisha yake yako hatarini baada ya polisi kujaribu kumzuia kuingia Kaunti ya Kirinyaga. Katika eneo la Sagana, maafisa wa polisi waliokuwa na silaha walizuia msafara wa Bw Gachagua alipokuwa akielekea Kagio kuhutubia mkutano wa kisiasa wa chama cha DCP kando ya barabara. Kulizuka taharuki huku Bw Gachagua na wandani wake wakikimbilia usalama wao. Wakati wa mkanganyiko huo, baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara wake yaliharibiwa. Kiongozi huyo wa DCP na wafuasi wake walilazimika kutumia njia ndefu kupitia Kandongu hadi mji wa Kagio, ambako walipokelewa na maelfu ya wafuasi. Hali ya wasiwasi ilitanda Kagio huku polisi waliokuwa na silaha nzito wakipiga doria mjini humo, hata hivyo Bw Gachagua aliendelea na mkutano wake bila woga. “Walitupiga kwa vitoa machozi na wakatufyatulia risasi,” aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Kagio, eneo la Ndia, akidai maisha yake yako hatarini. Aliapa kuwa hakuna vitisho vitakavyomzuia kuzuru kila pembe ya kaunti hiyo au kubadili mwelekeo wa kisiasa wa wakazi wa Kirinyaga. “Serikali ya Kenya Kwanza ina wasiwasi kwa sababu ninasema ukweli kwa Wakenya, ndiyo maana polisi wanatumwa kunishambulia mimi na wafuasi wangu,” alisema Bw Gachagua. Bw Gachagua alisema juhudi zake za kumng’oa Rais William Ruto kidemokrasia katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 haziwezi kuzuiwa. “Nitahakikisha Ruto anakuwa rais wa muhula mmoja,” alisema. Aliendelea kumshutumu Rais Ruto kwa kuharibu uchumi wa nchi kwa gharama ya wananchi. “Rais Ruto ameharibu uchumi na kwa kushirikiana na wenzangu wa upinzani tutampeleka nyumbani,” alisema. Alimlaumu Rais kwa kudai kuwa ana uwezo wa kuigeuza Kenya kuwa Singapore. “Kile Ruto ametuambia ni cha kuchekesha, tunapaswa kumcheka,” alisema. Bw Gachagua aliandamana na Naibu Kiongozi wa DCP Cleophas Malala, Seneta wa Kirinyaga Kamau Murango, Seneta wa Nyandarua John Methu pamoja na viongozi wengine. Awali, akiwa mjini Nyeri alipokuwa akizungumza na wanahabari, Bw Gachagua alitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa kuhusu zoezi tata la uteuzi wa wanafunzi wa Gredi ya 10, akisisitiza kuwa zoezi hilo limeegemea baadhi ya maeneo. Alitetea kauli zake za awali kuhusu wanafunzi “kutoka nje” kupelekwa katika shule za Mlima Kenya, akisema wanafunzi wa eneo la Kati pia wana haki ya kusoma katika shule bora. Alihoji kuwa baadhi ya maeneo yamepokea mabilioni ya fedha kupitia hazina ya usawazishaji tangu ugatuzi uanze lakini hayajajenga shule bora, ilhali viongozi wake wanamshambulia anapodai haki katika fursa za elimu. Alisisitiza kuwa wanafunzi wa Gredi 10 kutoka baadhi ya maeneo wanapaswa kupewa kipaumbele katika uteuzi. “Watoto wote nchini ni sawa, lakini watoto wa eneo hili wanapaswa kupewa kipaumbele bila kuwabagua wale wa maeneo mengine,” alisema. Alikanusha madai kuwa kauli zake ni za kikabila, akisisitiza kuwa uteuzi wa wanafunzi katika shule za kitaifa unapaswa kufanywa kwa uwazi na haki. Bw Gachagua aliwaambia wanaomkosoa kwa kuwa “mkali” kuhusu masuala ya Mlima Kenya kwamba hatanyamaza huku Rais Ruto akidaiwa kusababisha mkanganyiko katika sekta ya elimu. Alitaja Kaskazini mwa Kenya kama eneo lililopokea mabilioni ya fedha lakini viongozi wake wameshindwa kuendeleza shule bora za kitaifa. “Tunahitaji mazungumzo ya kitaifa kuhusu suala hili la uteuzi. Watu wa Kaskazini Mashariki ndio hunishutumu kwa ukabila ilhali wana fedha lakini hawajajenga shule bora kwa watu wao,” alisema. Alhamisi, Rais Ruto alimshutumu Gachagua kwa kueneza siasa za chuki na ukabila kuhusu mfumo wa elimu. “Sasa wameenda hadi shuleni kugawanya watoto wetu. Mmefikia kiwango gani cha kukata tamaa? Waacheni watoto wetu wasome. Watoto hao ni Wakenya bila kujali jamii wanayotoka,” alisema Rais. Viongozi kadhaa wanaoegemea UDA wamejitokeza kutetea uteuzi wa wanafunzi.
CHAMA cha ODM kwa sasa kiko katika kipindi cha misukosuko mikubwa, ambapo kila kikao na mjadala wake umejaa sintofahamu. Hata kumbukumbu za kihisia za kile ambacho kingekuwa maadhimisho ya miaka 81 ya kuzaliwa kwa Raila Odinga wiki iliyopita hazikufaulu kuziba mipasuko inayotikisa chama hicho. Kadiri hali hiyo inavyoendelea, Ida Odinga, mama mlezi ambaye kwa muda mrefu amekuwa nguzo tulivu lakini thabiti nyuma ya uongozi wa Raila, sasa amejitokeza hadharani. Katika pengo lililoachwa na kifo cha Raila, Ida anajitokeza si tu kama mjane mwenye huzuni, bali pia kama nguzo ya maadili na mkakati kwa ODM inayoonekana kuyumba chini ya uongozi wa kaka wa Raila, Dkt Oburu Oginga. Wasaidizi wake wanasema amelazimika kutoka kivulini ili kuokoa chama dhidi ya hatari ya mgawanyiko. “Mume wangu aliwaachia chama kilicho imara. Lazima mkilinde na kukidumisha, hata kama si kwa lolote, basi kwa heshima ya kumbukumbu yake,” alinukuliwa akisema kwa mkutano na vigogo wa chama nyumbani kwake wiki iliyopita, kulingana na watu wawili waliokuwapo. Katika mkutano wa Jumatano katika makazi yake ya Karen, ambapo waombolezaji walivaa jezi maalum za Arsenal kuenzi mapenzi ya Raila kwa soka, sauti ya Ida ilisikika wazi na yenye msimamo. “Baba alikuwa na mapenzi mengine, nayo ni mapenzi kwa ODM,” alisema. Ida alimkumbuka Raila kama mwanamume wa familia na mwanasiasa, akisisitiza kujitolea kwake kwa familia na chama alichoasisi na kujenga. Kwa maneno yaliyojaa huzuni lakini pia mamlaka, amekuwa akihimiza umoja ndani ya ODM na kutumia heshima yake kujaribu kutuliza jahazi linalotikiswa na majonzi ya kumpoteza kiongozi wake. “Ni tamanio langu kwamba tuhifadhi ODM kwa heshima ya Raila kama huduma kwa taifa letu,” alisema huku akiwataka viongozi “kutafakari kwa kina na kwa dhati,” na “kukaa chini, kuzungumza na kutatua tofauti zao.” Wafuasi kadhaa wamekuwa wakitoa wito mitandaoni wakipendekeza Ida achukue hatamu za uongozi wa ODM, wakimtambua kama nguvu iliyokuwa nyuma ya Raila na mlezi wa mikakati yake kwa miongo mingi. Hata hivyo, nyuma ya pazia, Ida anakabiliwa na mvutano wa kifamilia, akitofautiana kwa upole na binti yake Winnie Odinga kuhusu mwelekeo wa chama, huku hadharani akijaribu kusukuma ajenda ya maridhiano. Swali kubwa sasa ni iwapo mama huyu mlezi, akitumia maarifa ya kisiasa ya Raila, anaweza kufufua ndoto ya chama cha chungwa na kuongoza wafuasi wake katika enzi mpya bila kiongozi huyo wa kipekee. Winnie ni miongoni mwa kizazi cha vijana wakakamavu ndani ya chama, wengi wao wakipinga vikali serikali jumuishi inayoongozwa na Rais William Ruto. Sambamba na majonzi na matumaini mapya, damu changa imefurika ndani ya ODM, ikileta nguvu inayoweza kuimarisha chama au kukipasua zaidi. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameibuka kama ishara ya msukumo huo wa kizazi kipya. Ijumaa, aliandika mitandaoni: “Tunataka ODM iitishwe Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe (NDC). Ni wakati wa kuchukua uongozi wa chama. Baada ya Baba ni Babu. Babu kwa sababu. Bila Babu tabu.” Kwa upande mwingine, mwanaharakati Kasmuel McOure, aliyepata umaarufu wakati wa maandamano ya kupinga ushuru Juni 2024, anasaka ushawishi akijitangaza kuwa “Kaimu Katibu Mkuu wa ODM” na kudai muda wa Edwin Sifuna umeisha. Wafuasi wake wanaamini juhudi hizo zinaweza kufufua chama kwa kuvutia vijana waliokata tamaa. Hata hivyo, nguvu hii ya vijana ina makali makubwa. Wito wa Babu wa kuitisha NDC unaweza kuchochea mapambano makali ya ndani na kuwatenga wazee wa chama, huku ikikumbusha mgawanyiko uliolisambaratisha chama cha FORD cha Jaramogi Oginga Odinga miaka ya 1990. Takriban miezi mitatu baada ya kifo cha Raila mnamo Oktoba 15, 2025, chama alichokijenga kuwa ngome ya upinzani nchini Kenya bado kinapitia majonzi. ODM inaonekana kupitia hatua zilezile za huzuni—kukataa, hasira, majadiliano, huzuni na hatimaye kukubali hali mpya. Kadiri Kenya inavyoelekea uchaguzi mkuu wa 2027, ODM iko njia panda. Je, itajipanga upya kuzunguka falsafa ya Raila ya haki ya kijamii, ugatuzi na miungano ya kimkakati, au itapasuka vipandevipande kama FORD? Hatima ya kura zaidi ya milioni 6.9 alizopata Raila mwaka wa 2022 iko hatarini. Je, zitabaki kuwa nguzo ya ODM au zitasambaratika kwa vyama pinzani? Katika muktadha huu, kauli za viongozi kama Katibu Mkuu Edwin Sifuna za kutaka mazungumzo na umoja, pamoja na mvutano unaoendelea kuhusu matumizi ya fedha za kampeni za 2022, zinaonyesha vita vya ndani vinavyoamua mustakabali wa ODM. Kwa sasa, macho yote yako kwa Ida Odinga kuona ikiwa atafanikiwa kuwa sauti ya busara na umoja, huenda akaokoa ODM na kuiandaa kwa mustakabali mpya. La sivyo, chama hicho kinaweza kuingia katika historia kama vingine vilivyotawaliwa na migawanyiko baada ya kuondoka kwa kiongozi wake mkuu.
PWANI: Serikali imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa juhudi zake za kuboresha uendeshaji wa bandari nchini, hatua inayoongeza ufanisi, uwajibikaji na ubora wa huduma huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza mkoani Pwani baada ya kutembelea Bandari ya Nyamisati, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema maboresho yaliyofanyika yameifanya sekta ya … The post TPA yapongezwa ukuaji wa bandari na uchumi first appeared on HabariLeo.
DODOMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuendelea kudumisha mshikamano, upendo na ushirikiano kazini, akisisitiza kuwa umoja wao ndio msingi wa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Gugu amesema wakati akifungua rasmi Kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi … The post Gugu: Umoja ni ufanisi katika majukumu first appeared on HabariLeo.
RAIS wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ametangaza Januari 15 na 16, 2026 kuwa sikukuu za kitaifa ili kuwapa raia muda wa kushiriki uchaguzi wa urais na wabunge wa taifa hilo utakaofanyika wiki ijayo, baada ya kipindi cha kampeni za urais zilizojaa mvutano. Tangazo hilo lilitolewa na Rais Museveni kupitia Notisi ya Kisheria chini ya Sheria ya Sikukuu za Umma, Sura ya 174, na kuchapishwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali. “Kwa kutekeleza mamlaka niliyopewa na Kifungu cha 2(2) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, natangaza tarehe 15 na 16 Januari, 2026 kuwa sikukuu za kitaifa kote Uganda kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi kushiriki uchaguzi wa Rais na Wabunge,” ilisema sehemu ya notisi hiyo. Serikali ilisema mapumziko hayo ya siku mbili yanalenga kuwawezesha wapiga kura kote nchini kusafiri, kupanga foleni na kupiga kura bila vikwazo vya majukumu ya kikazi. Sikukuu hizo zitatekelezwa kitaifa na zitahusu taasisi za umma na za kibinafsi, huku Uganda ikijiandaa kwa uchaguzi unaotarajiwa kufuatiliwa kwa karibu sana. Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka wa 1986, anawania muhula mwingine, huku uchaguzi huo pia ukiamua muundo wa Bunge la Uganda. Takribani wapiga kura21.6 milioni waliojiandikisha watashiriki chaguzi tatu tofauti: uchaguzi wa rais, uchaguzi wa wabunge 353 wa maeneo bunge, pamoja na uteuzi wa wawakilishi wanawake 146, mmoja kutoka kila wilaya. Rais Museveni na kiongozi wa upinzani Bobi Wine ndio wagombea wakuu wa urais, huku huu ukiwa mtanange wao wa pili kwenye sanduku la kura. Museveni, mwenye umri wa miaka 81, alishinda uchaguzi wa 2021 kwa kupata asilimia 58 ya kura dhidi ya asilimia 35 za Bobi Wine, kura iliyogubikwa na madai ya wizi wa kura na ukandamizaji mkubwa wa upinzani. Kwa mujibu wa sheria za Uganda, mgombea wa urais lazima apate asilimia 50 pamoja na kura moja ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi katika mfumo wa kura wa awamu mbili, huku Waganda wengi wakiendelea kueleza wasiwasi wao kuhusu uaminifu wa mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi wa Uganda unafanyika takribani miezi minne baada ya nchi jirani ya Tanzania kufanya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, uliosababisha vurugu baada ya matokeo kutangazwa katika baadhi ya maeneo. Rais Samia Suluhu alitangazwa mshindi baada ya matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania mnamo Jumamosi, Novemba 1, kuonyesha kuwa alipata kura milioni 31.9, sawa na asilimia 97.66 ya kura zote zilizopigwa.
ZANZIBAR; RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kukua kwa uwekezaji nchini kumewezekana kutokana na uwepo wa amani na utulivu wa kisiasa, na kuwataka wanaochochewa kuvunja amani kuacha mara moja. Aidha, amesisitiza wananchi kulinda amani ya nchi, kwani maendeleo na kupeN deza kwa nchi kunatokana na amani na usalama uliopo. Rais Samia alieleza hayo jana Zanzibar, alipokuwa … The post Rais Samia: Amani ndio nguzo ya uwekezaji first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: CCM Secretary-General, Dr Asha-Rose Migiro, has called on grassroots leaders across the country to take the lead in educating supporters and citizens about the party’s rich history, its role in liberating Tanzania and promoting national unity. Speaking yesterday during a joint working meeting with grassroots leaders in Kinondoni and Ubungo as part … The post Migiro pushes for party awareness first appeared on Daily News.
WAZIRI wa Elimu, Bw Julius Migos Ogamba, amewataka wanasiasa kujitenga na masuala ya elimu, akiahidi kulinda uadilifu wa zoezi la kuteua wanafunzi katika shule za Sekondari Pevu dhidi ya hujuma na kuingiliwa kisiasa. Akizungumza katika Shule ya Sekondari ya Chebisaas Boys’ Ijumaa, Januari 9, 2026 baada ya kutangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2025, Bw Ogamba aliwakosoa vikali wanasiasa kadhaa akiwemo aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akiwalaumu kwa kujaribu kuhujumu mchakato wa wanafunzi kujiunga na Sekondari Pevu kwa maslahi ya kisiasa. “Hatutakaa kimya na kuruhusu wanasiasa kuingiza siasa zisizo na maana katika sekta ya elimu,” alisema Bw Ogamba. “Masuala ya elimu yaachwe kwa wataalamu. Nawahimiza wanasiasa hawa warudi kwenye kamusi wajifunze maana ya neno ‘kitaifa’.” Kauli yake ilifuatia mjadala unaoendelea kuhusu uteuzi wa wanafunzi 1.1 milioni waliomaliza Sekondari Msingi mwaka jana kujiunga na Sekondari Pevu. Kumekuwa na ushindani mkali wa nafasi katika shule za kitaifa, ambapo shule kama Alliance High School na Kenya High School zilipokea maombi zaidi ya 20,000 kila moja ilhali zina nafasi takribani 500 pekee. Bw Gachagua amedai kuwa “wageni” wamechukua nafasi nyingi katika shule bora zilizo eneo la Mlima Kenya kwa hasara ya wanafunzi wa eneo hilo, madai ambayo aliendelea kuyatetea jana.
RAIS William Ruto anapanga kutumia zaidi ya nusu ya bajeti ijayo kwa miradi yake ya kipaumbele ikiwemo makazi, elimu, afya na miundombinu, inavyoonyesha rasimu ya Taarifa ya Sera ya Bajeti (BPS) kwa mwaka wa kifedha 2026/27. Wizara ya Fedha imetenga Sh1.66 trilioni kwa sekta hizi nne katika bajeti ya jumla ya Sh2.88 trilioni kwa mwaka wa kifedha unaoanza Julai 1, 2025. Kulingana na rasimu hiyo, sekta ya Afya imetengewa Sh167.4 bilioni, ikijumuisha Sh136 bilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh31.4 bilioni kwa maendeleo. Sekta ya Elimu itapokea Sh767.3 bilioni, ambapo Sh737.2 bilioni ni kwa matumizi ya kawaida na Sh30.1 bilioni kwa maendeleo.Sekta za Kawi, Miundombinu na ICT zimetengewa Sh194.5 bilioni, ikijumuisha Sh151.6 bilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh42.3 bilioni kwa maendeleo. Sekta ya Makazi, inayolenga kutimiza ahadi ya kampeni ya Ruto ya makazi ya bei nafuu, imetengewa Sh139.3 bilioni, ikiwemo Sh133.6 bilioni kwa maendeleo ya makazi na Sh5.7 bilioni kwa matumizi ya kawaida. Katika sekta ya Afya, serikali imepanga kuajiri wahudumu wa Afya wa Jamii (na kusajili Wakenya 35 milioni katika Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Hadi sasa, Wakenya zaidi ya 27 milioni tayari wamesajiliwa, ikiwakilisha ongezeko la zaidi ya asilimia 200 kutoka milioni 9 waliokuwa chini ya NHIF, na zaidi ya 21 milioni wakiwa wanachangiaji wapya kabisa. “Serikali inapanga kukamilisha usajili wa Wakenya wote wanaostahili katika SHA, kwa lengo la kufikia watu 35 milioni,” inasema rasimu ya BPS. Miradi ya miundombinu ya afya ni pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya afya, kukarabati na kuweka vifaa vya kisasa katika vituo vilivyopo, na ukarabati wa hospitali. Pia, serikali imeanzisha mitandao 228 ya Afya ya Msingi nchini kote na kuajiri wahudumu wa afya wa jamii 120,000 watakaopokea mishahara ya kila mwezi. Kwenye mpango wa Makazi ya Bei Nafuu (AHP pia, masoko 506 yatajengwa kusaidia shughuli za kiuchumi. Serikali pia inalenga kuendeleza miji na mipango ya upanuzi wa miji ili kupunguza msongamano katika miji mikubwa na kuunda jamii zenye mpangilio mzuri na miundombinu ya pamoja. Wizara pia itapanua ufadhili wa Hazina ya Makazi kwa kupanua Boma Yangu na kutoa mikopo ya kupata makazi vijijini. Katika sekta ya elimu, serikali inalenga kukuza masomo ya ufundi na elimu ya msingi kwa kuajiri walimu 30,000 zaidi, kujenga madarasa 20,000 mapya na kukarabati madarasa 15,000, pamoja na kufanikisha mafunzo ya walimu 50,000 kwa mbinu za elimu ya umilisi. Sekta ya miundombinu pia inajumuisha ujenzi wa mabwawa, barabara na kuongeza uwezo wa umeme kwa megawati 10,000 kupitia miradi ya nguvu za mvuke, jua, upepo na umeme wa maji. Serikali inaashiria kuwa miradi hii yote itasaidia kuunganisha vituo vikuu vya uchumi, kuimarisha uchukuzi vijijini, kukuza kilimo na kuendeleza uchumi wa viwanda.
TOFAUTI na mataifa mengine katika ukanda huu, amani na umoja wa kitaifa Tanzania si tu kwamba ni nguvu muhimu, bali pia ni mali ya thamani kwa nchi. Kwa miaka mingi, nchi imejenga mazingira ya umoja, kuheshimiana kati ya makundi mbalimbali ya kikabila na kidini pamoja na kujitoa kwa dhati kujenga dhamira thabiti ya kudumisha amani na maelewano. The post Jamii Nguzo ya Umoja wa Kitaifa first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: Serikali imesema itaendelea kuwaunga mkono wadau katika kufanikisha lengo la serikali kwa wananchi kutumia nishati safi ili kuachana na kutumia nishati chafu kwani ina madhara kiafya. Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia Kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay wakati wa uzinduzi wa mradi wa … The post Serikali kuwaunga mkono wadau nishati safi first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM; UJUMBE wa Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Asha Dachi, umekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead John Teri na maofisa wengine wa mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo Januari 9, 2025. Taasisi … The post TSN, TISEZA kushirikiana kutangaza maeneo ya uwekezaji first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: THE Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dar es Salaam Region has announced that it will begin implementing a special exercise to update and verify membership records at the branch level, with the aim of identifying party representatives who have passed away or relocated from their areas. The announcement was made today by the … The post CCM embarks on exercise to update, verify members records first appeared on Daily News.
SERIKALI imesema Idara ya Uhamiaji Zanzibar imeongeza wigo wa mapato yasiyo ya kikodi kutoka Sh bilioni 130 mwaka 2016-2020 hadi kufi kia Sh bilioni 323 mwaka 2021-2025. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alieleza hayo wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Chuo cha Mafunzo ya Uhamiaji Kitogani Kisiwani Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. The post Uhamiaji Z’bar yapaisha mapato first appeared on HabariLeo.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaendelea na dhamira ya kuweka miundombinu ya kisasa kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuzitumia fursa za biashara ipasavyo. The post Zanzibar yaahidi miundombinu ya kisasa kwa wawekezaji first appeared on HabariLeo.
MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, John Nzilanyingi, amefanya ziara katika Kata ta Mirongo kusikiliza kero za wananchi, akaelezwa pamoja na mambo mengine, uchakavu na ufinyu wa mto mirongo unavyosababisha mafuriko katika kila msimu wa mvua, hatimaye kuathiri shughuli za kiuchumi na kijamii. The post Nzilanyingi kushughulikia kero za mafuriko first appeared on HabariLeo.
TUME ya Rais inayochunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka jana imeanza kazi yake mkoani Mara, ikiwa na lengo la kukusanya maoni na ushahidi kutoka kwa makundi yaliyoathiriwa na matukio hayo. Uchunguzi huo unalenga kubaini ukweli wa matukio ya uchaguzi na kipindi cha baada ya uchaguzi, yaliyosababisha kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi, wengine kujeruhiwa na uharibifu wa mali. The post Tume ya Jaji Chande yatua Mara first appeared on HabariLeo.
BAADA ya kutangaza Hazina ya Serikali ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF) kuwa kinyume cha katiba na kutoa agizo kwamba ifungwe kufikia Juni 30, 2026, sasa Mahakama inaomba Bunge kuhakikisha sehemu ya pesa za hazina hiyo zinatumika kusaidia ujenzi wa mahakama kote nchini. Ombi hilo limewasilishwa kwa wabunge kwa sababu ya “ukosefu wa ufadhili wa kutosha” kwa mahakama, ambapo bajeti iliyotengwa ni chini ya asilimia moja ya bajeti ya taifa licha ya kukabiliana na mzigo mkubwa wa kesi 257,000.” Stakabadhi zilizopatikana na Taifa Leo zinaonyesha Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), Isaac Ruto, aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Bomet, alitoa ombi hilo kwa Kamati ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Katiba (CIOC) ya Bunge la Kitaifa. “JSC ilitoa pendekezo kwa bunge kuzingatia kutenga sehemu ya NG-CDF kusaidia ujenzi wa mahakama kote nchini,” Bw Ruto alisema katika stakabadhi ya JSC iliyotolewa kwa CIOC, inayosimamiwa na Mbunge wa Suba Kusini, Caroli Omondi.
BUKOBA: KAGERA Region has recorded significant economic and social development between 2020 and 2025 following a government allocation of 1.131tri/- for development projects. The region’s Gross Domestic Product (GDP) increased from 3.7tri/- in 2020 to 4.9tri/- in 2025, reflecting sustained growth across key sectors. In his New Year message, Kagera Regional CCM Chairman, Dr Nazir … The post Kagera records significant development gains over five years first appeared on Daily News.
GEITA: SERIKALI imekamilisha kufunga mifumo ya kunasa radi katika shule 12 zilizopo wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya kuwalinda wananchi pamoja na wanafunzi dhidi ya ajali za radi. Hatua hiyo inakuja kufuatia mfululizo wa matukio ya radi wilayani humo ikiwemo tukio la Januari 27, 2025 lililopelekea vifo vya wanafunzi saba na kujeruhi 82 … The post Serikali yaanika mikakati kudhibiti radi Bukombe first appeared on HabariLeo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza Wananchi kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mipango na miradi ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati uliopangwa. Dk Mwinyi ametoa wito huo leo Januari 02, 2026 alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Uzi Ng’ambwa pamoja na … The post Mwinyi asisitiza ushirikiano utekelezaji miradi ya maendeleo first appeared on HabariLeo.
SIKU kabla ya uchaguzi, wakati na baada ya uchaguzi mara chache huwa tulivu. Katika demokrasia, siku hizo huleta hofu, kauli za ushindani na kuibua hisia. Tanzania haikuachwa nyuma. Matukio yaliyoripotiwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 yaliviweka vyombo vya usalama katika shinikizo la kutuliza hofu huku likitelekeza misingi ya Katiba. Tathmini ya matukio … The post Mzigo wa amani na utulivu: Namna Polisi ilivyobeba uzito wa utulivu wa taifa first appeared on HabariLeo.
WAKATI Watanzania wakiungana na watu wengine duniani kote kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2026, Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi zawadi mbalimbali za mwaka mpya kwa watu wenye mahitaji mkoani Kilimanjaro. Zawadi hizo zilikabidhiwa juzi kwa wahitaji hao na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga. The post Samia akabidhi zawadi za mwaka mpya kwa wahitaji first appeared on HabariLeo.
WADAU mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wasomi na wachumi wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kuliunganisha taifa kupitia Tume ya Maridhiano aliyoanza hatua ya kuiunda. Wamesema Rais Samia ni mfano wa kiongozi bora na kwamba hata tume atakayoiunda Watanzania watakuwa na imani nayo kwa jinsi muundo wake ulivyokuwa shirikishi. The post Maridhiano, uchumi vyambeba Samia first appeared on HabariLeo.
POLISI nchini Uganda wanaendelea kumzuilia mwanaharakati maarufu huku utawala wa Rais Yoweri Museveni ukiendelea kuwaandama wapinzani na wakosoaji kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 15, 2026. Polisi walithibitisha kuwa Sarah Bireete ambaye ni mwanaharakati na mkosoaji mkubwa wa serikali hasa nyakati za mahojiano kwenye runinga mbalimbali za Uganda, anaendelea kuzuiliwa. “Anaendelea kuzuiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote,” ikasema taarifa ya polisi bila kufichua siku ambayo atafikishwa mahakamani. Bireete, ni wakili na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Kikuu cha Katiba na Uongozi (CCG) amekuwa akikosoa hotuba za Rais Museveni na baadhi ya sera za utawala wake. Hasa amekuwa akikashifu vikali kuendelea kuzuiliwa kwa wanasiasa wa upinzani na mateso wanayoyapitia dhidi ya maafisa wa usalama. CCG bado haikuwa imezungumzia kukamatwa kwa Bireete. Uchaguzi wa Januari utawakutanisha Museveni, 81, ambaye amekuwa mamlakani tangu 1986 dhidi ya Mwimbaji mwanasiasa Bobi Wine. Wine, 43, na chama chake cha NUP, wamekuwa wakilalamika kuwa wafuasi wao wamekuwa wakinyakwa na kuzuiliwa katika msafara wao wa kampeni. Amelalamika mara si moja kwamba wafuasi wake wamekuwa wakiandamwa na vikosi vya usalama lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kukomesha matukio hayo. Mwezi uliopita Mkuu wa UN kuhusu Haki za Kibinadamu Volker Turk pia alilalamikia ukandamizaji na kuandamwa kwa viongozi wa upinzani. UN ililalamikia kukamatwa na kuzuiliwa kwa zaidi ya wafuasi 550 wa upinzani. Kiongozi mwengine wa upinzani Kizza Besigye anaendelea kusota gerezani zaidi ya mwaka moja tangu akamatwe na kushtakiwa kwa uhaini.
BUKOBA: KAGERA Regional CCM Chairman, Mr Nazir Karamagi, has appealed to Tanzanians to support initiatives spearheaded by President Dr Samia Suluhu Hassan, saying the projects are gaining international recognition and are key to national development. Speaking yesterday, Mr Karamagi said President Samia’s efforts are evident across the country and called on citizens to work hard … The post Karamagi urges Tanzanians to support Samia’s initiatives first appeared on Daily News.
SERIKALI inapanga kuanzisha kitengo maalum cha ujasusi wa kidijitali ili kudhibiti matumizi mabaya ya kidijitali, hatua inayozua hofu ya upelelezi wa serikali katika mawasiliano na ukiukaji wa haki ya faragha. Ripoti ya Rais iliyowasilishwa bungeni inaonyesha kuwa serikali pia inashughulikia mfumo wa kisheria wa ulinzi na usimamizi wa polisi wa kidijitali. Hatua hii inafuatia kile ambacho serikali inasema ni ongezeko la matumizi mabaya ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, ambayo inasema kwa kiasi kikubwa yanamilikiwa na wageni, katika kuchochea waandamanaji, kuratibu maandamano, pamoja na kusambaza taarifa potofu, propaganda, na lugha ya chuki. Ripoti ya Hali ya Usalama wa Taifa 2025 inayohusu kipindi cha Septemba 1, 2024 hadi Agosti 2025 inaonyesha kuwa waandamanaji walitumia majukwaa ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida kupanga maandamano yaliyopelekea kujeruhiwa kwa maafisa wa polisi 496, kuharibiwa kwa magari 179 ya serikali, kuharibiwa kwa ofisi 16 za serikali, na kukamatwa raia 1,792. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa polisi walijibu maandamano hayo kwa kuua raia 42 na kuwakamata jumla ya waandamanaji 1,732 kote nchini. Kulingana na ripoti hiyo, takwimu za uharibifu uliosababishwa wakati wa maandamano zinaonyesha kuwa kulikuwa na vifo 42 vya raia, polisi 496 na raia 66 walijeruhiwa, magari 142 ya polisi na magari mengine 22 ya Serikali ya Kenya (GK) yaliharibiwa, pamoja na magari 88 ya raia. Vituo au vituo vidogo 12 vya polisi viliharibiwa, silaha ndogo nane ziliibwa, silaha nne ziliharibiwa, ofisi 16 za serikali ziliharibiwa, maduka makubwa 18 yalivunjwa, kuharibiwa na kuporwa, huku benki tano na taasisi za fedha ndogo zikivamiwa na kuporwa. “Kuendelea mbele, serikali inakusudia kuimarisha juhudi za utekelezaji wa sheria kwa kuanzisha doria mitaani; kuanzisha kitengo maalum cha ujasusi wa kidijitali na kuweka mbinu za kuchukua hatua kwa haraka,” ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni na Rais William Ruto inasema. “Zaidi ya hayo, matumizi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida yalichangia pakubwa katika kuchochea waandamanaji, kuratibu maandamano, pamoja na kusambaza taarifa potofu, propaganda na lugha ya chuki.” Ripoti hiyo inasema kuwa mwaka 2024 Kenya ilishuhudia idadi kubwa zaidi ya maandamano na ghasia katika zaidi ya miongo mitatu, huku matukio 2,005 ya maandamano yakirekodiwa. Inaeleza kuwa Julai 2024 ilishuhudia maandamano 250, idadi ya juu zaidi kwa mwezi mmoja. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa maandamano yaliyotokea katika mwaka uliomalizika Agosti 2025—yakiongozwa zaidi na wanaharakati, kundi la vijana na wanasiasa—yalichochewa kwa kiasi kikubwa na wasiwasi kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha, madai ya maafisa wa usalama kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na uchochezi wa umma. “Ingawa haki ya kukusanyika kwa amani imehakikishwa katika Katiba chini ya Ibara ya 33, 36 na 37, waandaaji wa maandamano walipuuza taratibu za kisheria kama hitaji la kutoa taarifa rasmi kwa polisi kuhusu maandamano yaliyopangwa, hali iliyosababisha hatari kwa usalama,” alisema Dkt Ruto.
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta amewasifu vijana wa Afrika akiwataja kuwa rasilmali kubwa zaidi ya bara lao, na kuwataka wajitokeze kwa ujasiri, uadilifu na maono, akisisitiza kuwa mabadiliko ya Afrika yatachochewa na Waafrika wenyewe wala si suluhu kutoka nje. Akizungumza Jumatano jioni wakati wa hafla ya Future Africa Leaders Awards (FALA) 2025 iliyofanyika katika uwanja wa Loveworld Nation Arena jijini Lagos, Nigeria, ambako alikuwa mgeni wa heshima kwa mwaliko wa Mchungaji Chris Oyakhilome, Bw Kenyatta alisema utajiri wa kweli wa Afrika haupo chini ya ardhi bali unapatikana katika fikra na mioyo ya watu wake. “Tumeambiwa mara nyingi kuhusu utajiri mkubwa ulio chini ya ardhi ya Afrika, lakini rasilmali yetu kuu iko katika akili na mioyo ya vijana wetu. Ninyi si viongozi wa kesho; ninyi ni viongozi wa leo mnaoamua kesho,” alisema. Aliwasifu washindi wa tuzo hizo kwa huduma na ubunifu wao, akisema juhudi zao zinaakisi uwezo unaokua wa uongozi barani Afrika. “Kila mmoja wa vijana hawa alichagua huduma badala ya maslahi yake binafsi, jamii badala ya starehe, na maono badala ya hofu. Tunawaheshimu si tu kwa yale waliyofanya, bali pia kwa watu waliogeuka kuwa,” alisema. Bw Kenyatta alisisitiza kuwa uongozi si kuhusu vyeo bali mabadiliko, na kuwataka vijana kutumia vipaji vyao kwa uwazi kuleta athari chanya. Aliongeza kuwa Afrika haina upungufu wa mawazo au nguvu, bali inahitaji uongozi unaojikita katika maadili, unaoongozwa na maono na unaowajibika kwa wananchi. Rais huyo wa zamani alimpongeza Mchungaji Chris Oyakhilome kwa uongozi wake wenye maono na dhamira thabiti ya kuwakuza vijana wa Afrika kupitia Wakfu wa Future Africa Leaders, akisema kuwa ni “jukwaa ambalo halisherehekei mafanikio pekee bali pia linajenga dhamira ya maisha.” Alisifu jitihada za taasisi hiyo kuwekeza katika rasilmali muhimu zaidi Afrika ambayo ni watu wake. Bw Kenyatta pia alitoa shukrani za dhati kwa Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, aliyemtambua kwa heshima kama “Baba,” kwa uongozi wake wa kudumu na kujitolea kuwaongoza na kuwashauri viongozi chipukizi wa Afrika, jukumu ambalo linaendelea kuunda mustakabali wa bara. “Africa iinuke—ijengwe na Waafrika, iimarishwe na umoja wetu, na iongozwe na viongozi wanaodhamiria kuitumikia,” alisema. Kiongozi wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo Musyoka pia alihudhuria hafla hiyo.
KIONGOZI wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Dkt Oburu Oginga, amesema atakuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 iwapo ODM itaamua kuwania uchaguzi huo kivyake. Akizungumza akiwa Diani, Kaunti ya Kwale, alipokuwa akitoa ujumbe wake wa Mwaka Mpya kwa Wakenya na wafuasi wa ODM, Dkt Oburu Oginga alisema mwaka wa 2026 utakuwa muhimu kwa chama hicho kuamua mwelekeo wake wa kisiasa. Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa katiba ya ODM, kiongozi wa chama ndiye mgombea wa urais moja kwa moja, jambo linalomaanisha kuwa atakabiliana na Rais William Ruto mwaka ujao iwapo chama kitaamua kushiriki uchaguzi bila kushirikiana na vyama vingine. “Na bila shaka, iwapo tutaamua kwenda pekee yetu, nataka iwe wazi kabisa kwamba katiba ya chama chetu tayari ina mgombeaji wa urais. Na mgombeaji huyo wa urais ametajwa wazi katika katiba ya chama. Naye ni kiongozi wa chama. Mimi ndiye mgombeaji wa urais wa ODM endapo ODM itaamua kwenda kivyake,” alisema Dkt Oginga. Kiongozi huyo wa ODM pia alionya kuwa, mwanachama yeyote wa chama mwenye ndoto ya kuwania urais anapaswa kutafuta chama kingine cha kisiasa. Alieleza kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2026, chama kitakuwa kimeamua iwapo kitashiriki kivyake au kitaungana na vyama vingine, na kufikia wakati huo, ODM pia itakuwa imejua washirika itakaoungana nao endapo itaunda muungano. Dkt Oginga alibainisha kuwa, kwa sasa ODM bado iko katika ushirikiano na serikali ya Kenya Kwanza, lakini akasisitiza kuwa chama hicho hakijajiunga kikamilifu serikalini na kinaendelea kuimarisha miundo yake huku kikidumisha uhuru wake, ingawa kimeacha wazi uwezekano wa kuungana na Rais Ruto kulingana na maamuzi yatakayofanywa kabla ya uchaguzi wa 2027. “Kufikia mwisho wa 2026, chama chetu kitakuwa kimejua iwapo tutashiriki (uchaguzi mkuu wa 2027) kivyetu au tutaungana na vyama vingine,” alisema kiongozi huyo wa chama. Akiwatakia Wakenya Mwaka Mpya mwema na wenye mafanikio, Dkt Oginga alikumbuka kwa huzuni kifo cha ndugu yake, aliyekuwa kiongozi wa ODM, Raila Odinga, pamoja na hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu utekelezaji kamili wa ajenda ya vipengele 10 kati ya ODM na serikali ya Kenya Kwanza. “Tunaangalia kwa makini utekelezaji wa ajenda hizo za makubaliano tuliyofanya nao. Kuhusu kama tutafanikiwa katika utekelezaji wake, ni Mungu pekee anayejua,” alisema kiongozi huyo wa chama. Alisisitiza kuwa licha ya changamoto hizo, ODM bado ni chama imara chenye mizizi imara mashinani, na kinaendelea kujipanga upya na kuimarisha miundo yake kuelekea uchaguzi wa 2027. Pia, aliwahimiza wanachama kubaki makini na kujitolea kwa maslahi ya wananchi kama ilivyoelezwa katika malengo ya chama, akisema uthabiti wa ODM utakuwa muhimu katika mwaka huu muhimu kabla ya uchaguzi mkuu. Seneta huyo wa Siaya pia alisisitiza kuwa ODM haiuzwi, akikanusha madai yanayodokeza hivyo. “Chama hiki hakiuzwi, hakitawahi kuuzwa, ni kikubwa mno kuuzwa kwa yeyote,” alisema, akisisitiza umaarufu wa chama hicho mashinani na uhuru wake.
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza wazi kukanusha madai kuwa anahusika katika mipango ya kuvuruga au kudhoofisha Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), akisema hana nia wala sababu ya kuingilia masuala ya ndani ya chama hicho. Uhuru alitoa kauli hiyo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Lugari, marehemu Cyrus Jirongo, yaliyofanyika Lumakanda, Kaunti ya Kakamega. Akizungumza mbele ya viongozi wa kitaifa na maelfu ya waombolezaji, Uhuru alisema kumekuwa na juhudi za kumhusisha na njama za kisiasa zinazolenga kuvuruga vyama vya siasa, hususan ODM, jambo alilolisema halina msingi wowote. “Mimi ni mstaafu. Sina haja ya kuvuruga ODM wala chama chochote. Kila chama kina wamiliki wake na njia zake za kushughulikia masuala yake,” alisema Uhuru, kauli iliyochukuliwa kama ujumbe wa moja kwa moja kwa Rais William Ruto na viongozi wa Kenya Kwanza. Uhuru alisisitiza kuwa anachotetea ni kuwepo kwa demokrasia imara ya vyama vingi, ambapo kila chama kinaheshimiwa na kuachiwa nafasi ya kufanya maamuzi bila shinikizo au hila za kisiasa. “Tunachotaka ni demokrasia hai. Vyama vijengwe, si kuvunjwa. Ukishindwa kushawishi watu wajiunge na wewe, usitafute wa kulaumu,” aliongeza. Kauli hiyo ilijiri huku kukiwa na madai ya mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya viongozi wa ODM na Kenya Kwanza kwamba kuna njama za nje za kukidhoofisha chama hicho au kukivuruga kutoka ndani. Uhuru alisema madai hayo ni kisingizio cha kushindwa kwa wengine kujenga maridhiano ya kisiasa kwa hiari. “Mtu akishindwa njia ya kujipendekeza kule anataka kujipendekeza, lazima atafute mtu aseme kuwa watu wanakataa kukusikiza kwa sababu ya yule na huyu.” Akimrejelea marehemu Cyrus Jirongo, Uhuru alisema kiongozi huyo alikuwa mfano wa mwanasiasa aliyethamini sana uhuru wa vyama na mazungumzo ya kisiasa, akifanya kazi na pande zote bila kuvunja misingi ya demokrasia. “Cyrus Jirongo aliamini katika heshima ya vyama vya siasa na alifanya kazi kuvuka mipaka ya vyama bila kuua au kumeza vingine. Huo ndio urithi tunaopaswa kuendeleza,” alisema. Uhuru aliwataka viongozi wanaoendeleza migawanyiko ndani ya ODM kuacha kile alichokitaja kuwa ni “fikira mbovu”, na badala yake waende kwa wananchi, wajenge chama chao cha kisiasa, waweke wazi sera zao na wazisimamie kwa ujasiri. “Toa hiyo fikira mbovu, enda zungumza na wananchi. Unda na usimamishe chama chako. Kuwa na sera zako kama mwanaume,” alisema Uhuru. Uhuru pia aliwakosoa vikali viongozi ambao, kwa mtazamo wake, huzunguka katika ulingo wa kisiasa wakitoa kauli za uchochezi zisizo na mchango wowote wa kuimarisha mshikamano wa kitaifa wala kukuza demokrasia. “Sio kuzunguka huku na kule ukitoa mambo ya upuzi ambayo haipeleki nchi mbali,” alisema. Akisisitiza maono yake kwa taifa hata baada ya kustaafu, Uhuru aliwakumbusha Wakenya umuhimu wa kudumisha umoja wa kitaifa, demokrasia na kuheshimu uamuzi wa wananchi. “Tunataka nchi iliyo na umoja, tunataka demokrasia, na tunataka matakwa ya wananchi yaheshimiwe,” aliongeza. Huku akikumbusha wakosoaji wake kuwa sasa ni kiongozi mstaafu, Uhuru aliweka wazi kuwa kustaafu hakumaanishi udhaifu wala kukubali kudharauliwa. “Sitaki kusema mengi kwa sababu mimi ni mstaafu, lakini kwa kusema mstaafu sisemi uniingize kidole kwa macho; mimi pia nitakuingiza. Tuheshimiane,” alionya. Kauli za Uhuru zilijiri wakati ambapo mvutano unaendelea kushuhudiwa ndani ya ODM, ambapo baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho wamemlaumu hadharani kwa madai ya kuingilia masuala ya ndani ya chama na kuchochea migawanyiko. Uongozi wa juu wa ODM, ukiongozwa na mwenyekiti wake Gavana Gladys Wanga pamoja na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed, umemshutumu Uhuru kwa madai ya kupanga kutumia wanachama wa ndani ya chama hicho kusababisha migawanyiko ya kisiasa katika ODM.
MWAKA 2025 umekuwa na huzuni kubwa kwa Tanzania baada ya kupoteza baadhi ya viongozi wake wakuu waliochangia kwa kiasi kikubwa katika siasa, uongozi na maendeleo ya taifa. Vifo vyao vimewaacha Watanzania wengi huzuni. The post Mwaka 2025 ilikuwa huzuni vifo vya viongozi first appeared on HabariLeo.
OFISA Habari wa Klabu ya Young Africans, Ali Kamwe, amezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha ujumbe unaogusia uwezekano wa kurejea mahusiano yake ya zamani. The post Ali Kamwe : Nitawarejea tena first appeared on HabariLeo.
BAGAMOYO: MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imevunja rekodi kwa kusajili jumla ya miradi 915 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 10.95 kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 29, 2025. Idadi hiyo ni ongezeko ikilinganishwa na miradi 901 iliyosajiliwa mwaka 2024. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya … The post TISEZA yavunja rekodi, yasajili miradi ya dola milioni 10 first appeared on HabariLeo.
MACHO ya mgeni yeyote anayetembelea kumbi za mikutano za mabunge kuanzia Dodoma, Tanzania, pale Nairobi, Kenya na hata London, Uingereza yatakutana na mandhari yanayofanana kwa namna ya ajabu. The post Kwa nini Mabunge Jumuiya ya Madola yanafanana? first appeared on HabariLeo.
KATIKA anga za siasa za Tanzania zinazohitaji umakini na ustahimilivu wa hali ya juu, jina la Najma Murtaza Giga linasimama kama alama ya uongozi uliotukuka na utumishi uliotukuka.Akiwa amehudumu bungeni kwa muda mrefu, Najma amejipambanua kama mwanasiasa mwenye weledi mkubwa, akichanganya unyenyekevu wa asili na ujasiri wa kutoa maamuzi magumu pale anapokuwa kwenye kiti cha uongozi. The post Najma Giga: Kielelezo cha hekima, uthubutu kiti cha mamlaka first appeared on HabariLeo.
KATIKA Ukumbi wa Bunge la Tanzania, kila kengele ya kuashiria kuanza kwa kikao inapolia, macho ya wengi huelekea mlangoni kwa shauku kubwa.Pale, anapita Spika au Naibu Spika akiwa amejifunika vazi refu jeusi lenye nakshi za dhahabu, akitanguliwa na msafara wa ngariba aliyebeba Siwa ya mamlaka. The post Nyuma ya pazia mavazi ya Spika! first appeared on HabariLeo.
WAFUGAJI wa mbuzi katika Kaunti ya Baringo wamelalamika kwamba walilaghaiwa na maafisa wa serikali ya kaunti wakati wa Mnada maarufu wa Mbuzi uliofanyika majuzi katika eneo la Kimalel eneo bunge la Baringo Kusini. Baadhi yao walielezea kuvunjwa moyo baada ya mbuzi wao kukataliwa kwa madai hawakutimiza “viwango hitajika” katika mnada huo maarufu ulioanzishwa na rais wa zamani, Hayati Daniel Moi mnamo 1986 kwa ajili ya kuwainua wafugaji kiuchumi. Mmoja wa wafugaji, alilalama kuwa maafisa wa serikali ya kaunti ya Baringo, waliosimamia shughuli ya ukaguzi wa mbuzi, waliwakataa mbuzi wake 20 hali iliyomfanya kutopata kiasi cha mapato alicholenga. “Tuliambiwa kuwa ni mbuzi 4,000 ambao wangeuzwa katika mnada wa mwaka huu. Hata hivyo, maafisa wa kaunti walileta jumla ya mbuzi 8,700 ambao hatujui walikowatoa. Mbuzi wangu 20 walikataliwa ilhali walikuwa na afya huku waliokubaliwa walikuwa wanane pekee. Sikupata pesa za kutosha kugharamia karo ya watoto wangu,” akaeleza. Ukora huo wa maafisa wa kaunti ulichangia bei ya mbuzi kushuka kutoka Sh18,000 hadi Sh13,000. Zamani, machifu na manaibu wao ndio walitumika kukagua mbuzi watakaouzwa katika Mnada wa Kimalel. Mnada wa mwaka huu uliendeshwa Desemba 22, na kuongozwa na Rais William Ruto.
MKUU wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude amezindua kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mpango wa serikali wa Bima ya Afya kwa wote unaolenga kuwapa fursa ya matibabu wananchi bila vikwazo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizundua mpango huo jijini Arusha, DC Mkude amesema kilio cha muda mrefu … The post Wilaya ya Arusha yazindua kampeni bima ya afya kwa wote first appeared on HabariLeo.