
MAPYA! MWILI WA BODABODA WAKUTWA KWENYE KIROBA/ KAMA HAUPEWI UNYUMBA NA MKEO NENDA KAMSHTAKI.
🔴#LIVE:MAPYA! MWILI WA BODABODA WAKUTWA KWENYE KIROBA/ KAMA HAUPEWI UNYUMBA NA MKEO NENDA KAMSHTAKI. ⚫️ JE, UNA HABARI?
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

🔴#LIVE:MAPYA! MWILI WA BODABODA WAKUTWA KWENYE KIROBA/ KAMA HAUPEWI UNYUMBA NA MKEO NENDA KAMSHTAKI. ⚫️ JE, UNA HABARI?

DODOMA: Serikali imesisitiza kuwa, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inatoa kipaumbele cha pekee kwa ushiriki wa vijana katika maendeleo, kwa lengo la kuinua vipaji, uwezo, na ari yao katika kufanikisha ukuaji wa uchumi jumuishi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, … The post Serikali yasisitiza ushiriki wa vijana Dira 2050 first appeared on HabariLeo.

MISRI; NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri wa Nishati wa Ukanda wa Mashariki mwa Afrika, uliofanyika Aprili 29, 2026 jijini Cairo, Misri, ukiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya umeme. Katika mkutano huo wa nchi wanachama wa Umoja wa Nishati Mashariki … The post Naibu Waziri Nishati ashiriki mkutano Misri first appeared on HabariLeo.

This will be the first address to the Tanzanian parliament by a Kenyan president.

Opposition leader Sonko was excluded from standing in the 2024 election following a conviction.

The operation in Kati was part of a wider assault by the affiliate, Jama'at Nusrat al-Islam...

The dispute is tied to a recent election held in South West State.

MVUVI mmoja alifariki na mwingine kujeruhiwa vibaya walipopigwa na radi wakivua samaki baharini katika eneo la Ingini, Lamu Jumamosi. Kassim Badi Usama, 48, alifariki papo hapo ilhali mwenzake, Mohamed Wako, akiachwa na majeraha mabaya baada ya radi kuwachapa walipokuwa kwenye mashua yao wakivua huku mvua kubwa ikinyesha. Kamanda wa Polisi kaunti ya Lamu, Bw Shadrack Ruto alithibitisha kisa hicho akisema mashua ya wavuvi hao, iliharibiwa kwa kupasuliwa na radi. Bw Ruto aliwaomba wavuvi kuwa waangalifu na kupunguza shughuli zao baharini msimu huu wa mvua kubwa. Meneja wa Kitengo cha Majanga na Uokozi (EOC Lamu Iftakkar Majid aliwasisitizia wavuvi, mabaharia na wakazi kuwa waangalifu msimu huu wa mvua kubwa ili kuepuka majanga zaidi. Bw Majid aliwasihi kutafuta ushauri kutoka kwa kituo hicho cha majanga na pia idara ya hali ya hewa kabla ya kutekeleza shughuli zozote baharini. “Pia ninawashauri wananchi kutotafuta hifadhi chini ya miti wakati kukinyesha kwani hilo huwaweka kwenye hatari ya kupigwa na radi,” akasema Bw Majid. Wakati huo huo, familia ya mwendazake, inaiomba serikali kuwapa msaada kutokana na kuondokewa kwa mpendwa wao waliyemtaja kuwa tegemeo la kipekee. Binamuye mwendazake, Bw Badi Nassir, alisema kakake ameacha mjane na watoto wawili. “Binamu yangu ndiye tegemeo la familia yake. Mke na watoto wameachwa ukiwa. Serikali izingatie kuifidia familia ili angalau ijitegemee,” akasema Bw Nassir. Mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Wavuvi (BMU) eneo la Faza ambako marehemu anatoka, Bw Mohamed Ali aliomba fedha za majanga zinazotengwa kila kukicha na serikali pia kuhakikisha zinawafikia wavuvi wa Lamu wanaokumbwa na majanga.

TILIMA: KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amesema CCM ndiyo baba wa demokrasia nchini kwani ndiyo chanzo cha kuzaliwa kwa vyama vingine vya siasa na utawala wa vyama vingi. Kihongosi ameeleza hayo leo Machi 8, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata … The post Kihongosi: CCM baba wa demokrasia first appeared on HabariLeo.

BEIRUT/MIAMI/TEL AVIV/DUBAI RAIS Donald Trump amesema hana nia ya kujadiliana na Iran, na kuzua uwezekano kwamba vita vya Iran vitaisha tu wakati jeshi na uongozi wa Tehran utakapoangamizwa kabisa. Muda mfupi baada ya Trump kuzungumza na wanahabari ndani ya ndege rasmi ya Rais, Air Force One, Israel, mwandani wa Amerika, ilitangaza mashambulizi mapya kote nchini Iran mapema jana, huku vita hivyo ambavyo vimesababisha hisia kali Mashariki ya Kati na kuvuruga masoko ya mafuta duniani vikiingia wiki ya pili. “Wakati fulani, sidhani kutakuwa na mtu yeyote wa kusema, ‘tumesalimu amri’,” alisema Trump. Trump ametetea oparesheni kubwa zaidi ya kijeshi ya Amerika katika ukanda wa Mashariki ya Kati tangu uvamizi wa 2003 nchini Iraq, akisema Tehran ilikuwa tishio kwa Amerika pasipo kutoa ushahidi. Amesema vilevile Iran ilikuwa karibu mno kufaulu kujenga silaha ya kinuklia. Amerika na Israel zimejadiliana kuhusu kutuma vikosi maalum nchini Iran kutwaa madini yake ya uranium katika hatua za mwisho za vita, shirika la Axios liliripoti, likinukuu watu wanne wanaofahamu majadiliano hayo. Alipoulizwa Jumamosi kuhusu uwezekano wa kutuma vikosi vya jeshi la ardhi kutwaa vituo vya nuklia, Trump alisema ni jambo wanaloweza kufanya “baadaye”. Serikali za Saudi Arabia, Kuwait, Milki ya Kiarabu, na Bahrain ziliripoti mashambulizi ya droni yaliyotekelezwa na Iran katika mataifa yao Jumamosi na mapema jana, huku moto mkuwa ukiteketeza jengo la afisi za serikali jijini Kuwait. Ubalozi wa Amerika katika jiji kuu la Norway, Oslo, vilevile lilishambuliwa na mlipuko jana na kusababisha uharibifu kiasi pasipo majeraha yoyote, polisi walisema. Haikubainika papo hapo ni nini kilichosababisha mlipuko na nani alihusika. Saudi Arabia imeambia Tehran kuwa mashambulizi yanayoendelea kutekelezwa na Iran dhidi ya milki hiyo huenda yakaisukuma Riyadh kulipiza kisasi, watu wanaofahamu suala hilo walieleza Reuters. Kwenye jaribio la kutuliza hamaki kote eneo la Ghuba, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian aliomba radhi nchi jirani kwa mashambulizi yake dhidi ya vituo vya Amerika katika mataifa hayo Jumamosi. Alipuuzilia mbali matakwa ya awali ya Trump akiitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujisalimisha kama “ndoto” lakini akasema baraza la uongozi limekubali kusitisha mashambulizi kwa nchi jirani isipokuwa pale mashambulizi dhidi ya Irani yanapotoka maeneo yao. Matamshi ya Pezeshkian yalizua hisia mseto nchini Iran na kuilazimu afisi yake kusisitiza Iran itajibu vikali mashambulizi kutoka ngome za Amerika. Kundi la kidini lililotwikwa jukumu la kumchagua kiongozi mpya wa kiroho Iran, kumrithi Ayatollah Ali Khamenei, aliyeuawa kwenye shambulizi wiki iliyopita lilitazamiwa kukutana jana, vyombo vya habari Iran vilisema. Sehemu kubwa ya wanachama imeafikiana kuhusu mrithi , alisema mwanachama wa Baraza la Wataalamu, Ayatollah Mohammadmehdi Mirbaqeri, kulingana na shirika la habari la Mehr. Duru zilieleza awali kuwa huenda Mojtaba Khamenei akachaguliwa na baraza hilo la wanachama 88 kumrithi Ali Khamenei. Milipuko mikubwa ilisikika katika sehemu za Tehran, vyombo vya habari vilisema, huku Israel ikisema ilishambulia vituo vya makombora, vituo vikuu vya kuamuru mashambulizi na vya mafuta Jumamosi. Mashambulizi ya Amerika–Israel yamewaua raia wa Iran wasiopungua 1,332 na kuwajeruhi maelfu wengine, kulingana na Balozi wa Iran, Amir Saeid Iravani. Israeli pia ilitekeleza mashambulizi mapya dhidi ya Lebanon Jumamosi baada ya wanamgambo wa Kiislamu wanaoegemea Iran, Hezbollah, kufyatua risasi kote mpakani. Israel ilionya Lebanon kuhusu “gharama ghali mno” ikiwa haitadhibiti wanamgambo wa Hezbollah, huku idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel nchini Lebanon tangu Jumatatu ikipanda na kufikia 300.

SERIKALI imeagiza kila kaunti ndogo kuanzisha vituo vya taarifa kwa umma, vituo vya dharura na vituo vya kukabiliana haraka na mafuriko ili kuwasaidia wananchi wanaokumbwa na maafa. Hii ni baada ya miundombinu muhimu kuharibiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya nchi kutokana na mito kufurika na maji kuharibu barabara na daraja. Katika Makueni, Barabara ya Wote–Emali pamoja na daraja la Kyamelu zilifurika na kuathiri usafiri. Bungoma, daraja la watembea kwa miguu la Kimama lilisombwa na mafuriko. Katika Migori, daraja kwenye mto Migori pia liliharibiwa vibaya baada ya kusombwa na maji ya mafuriko. Jijini Nairobi, angalau shule 15 zimeathiriwa, huku madarasa na vifaa vya shule vikiharibiwa na maji ya mafuriko. Rais William Ruto alisema mafuriko hayo yamesababisha mateso makubwa kwa familia nyingi nchini. “Mafuriko yanayoendelea katika sehemu za Nairobi na maeneo mengine ya nchi yamesababisha vifo vya kusikitisha,” alisema Rais katika taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wa X. Mkuu wa Mawaziri, Musalia Mudavadi, alisema hali ya mafuriko katika Nairobi ni ya kutia wasiwasi na haikubaliki.

SIMIYU: SERIKALI imetoa fedha kiasi cha Sh milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mwamapalala iliyopo katika Kata ya Mwamapalala wilayani Itilima mkoani Simiyu. Lengo likiwa ni kuwezesha kata hiyo kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na nafuu kwani hapo awali kata hiyo haikuwa na kituo cha afya pia kusogeza upatikanaji … The post Sh mil 250 kujenga zahanati Mwamapalala first appeared on HabariLeo.

SIMIYU: KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi ametoa siku saba kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha umeme umefika katika bweni ya wasichana katika Shule ya Sekondari Shishiyu wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kihongosi ametoa agizo hilo alipofika katika shule hiyo na kukagua bweni hilo mkoani himo ikiwa ni … The post Tanesco yapewa siku 7 kufikisha umeme bweni la wasichana sekondari Shishiyu first appeared on HabariLeo.

JUHUDI za kuzima vuguvugu la Linda Mwananchi zinaendelea kufichuka huku likiendelea kufanya mikutano ya kisiasa nchini. Kiongozi wa kundi hilo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anadai kuwa kuna juhudi za makusudi za kuzima shughuli zao, kuanzia kuvurugwa kwa mikutano yao, madai ya kujaribiwa kununuliwa kwa fedha nyingi hadi kuzuiwa kwa mipango ya kidijitali ya kuratibu shughuli zao. Akizungumza katika mkutano wa People’s Dialogue Festival uliofanyika Uhuru Park, Sifuna alisema kundi lake limekumbana na vikwazo mara kadhaa tangu lianze mikutano ya Linda Mwananchi kote nchini. “Tunafahamu kuna propaganda eti tuliitisha hadi Sh2 bilioni ili tusitishe kampeni yetu. Lakini vuguvugu hili ni kubwa kuliko mtu mmoja, hatutakubali kununuliwa,” alisema Sifuna. Mikutano yao ya kisiasa imekumbwa na vurugu au vizingiti vinavyodaiwa kulenga kupunguza ushawishi wao. Seneta wa Siaya James Orengo, ambaye pia amehusishwa na msimamo mkali wa kuikosoa serikali ya sasa, amewahi kuonya kuhusu kile alichokiita juhudi za kuzuia maoni tofauti katika siasa za Kenya. Orengo amesisitiza mara kadhaa kuwa demokrasia haiwezi kustawi ikiwa makundi ya kisiasa yatazuiwa kuwasilisha maoni yao hadharani. “Katika demokrasia, lazima kuwe na nafasi ya sauti tofauti kusikika bila vitisho au vikwazo,” amewahi kusema katika mikutano ya kisiasa na mahojiano ya vyombo vya habari. Mbali na kuvurugwa kwa mikutano, viongozi wa Linda Mwananchi pia wanadai kuwa kuna juhudi za kuwapa baadhi yao pesa ili waachane na vuguvugu hilo. Sifuna alisema propaganda pia zimesambazwa zikidai kuwa aliomba pesa ili aachane na kampeni dhidi ya serikali jumuishi. “Walianza kueneza propaganda kwamba nimeomba pesa ili kuacha vuguvugu hili. Ukweli ni kwamba sisi hatutayumbishwa na fedha,” alisema. Kundi hilo pia linadai kuwa juhudi zao za kuanzisha tovuti na nambari ya kuchangisha pesa kutoka kwa wafuasi zimekuwa zikitatizwa mara kadhaa. Kwa mujibu wa Sifuna, wafuasi wao walitaka kutumia mifumo ya kidijitali kuratibu mikutano na michango ya kuendesha kampeni za Linda Mwananchi, lakini mipango hiyo imekuwa ikizuiwa. “Tumekuwa tukijaribu kuanzisha tovuti na nambari ya kuchangisha fedha lakini kila mara tunakumbana na vikwazo,” alisema. Katika hatua nyingine iliyoibua utata, viongozi wa kundi hilo wanapinga jaribio la kusajili chama kipya kiitwacho "Linda Mwananchi Party.” Kupitia mawakili wao, Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino waliwasilisha malalamishi kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa wakisema hawahusiki na juhudi hizo. Walionya kuwa kusajili chama hicho kunaweza kuwapotosha wafuasi na hata kutumiwa vibaya kukusanya fedha kwa jina la vuguvugu lao. Kulingana na mchanganuzi wa siasa Dkt Isaac Gichuki, mpango wa kusajili jina la vuguguvu hilo kama chama ni mkakati wa kulizima. Anasema hatua ya ODM kumvua Sifuna wadhifa wake wa Katibu Mkuu ni sehemu ya mkakati wa kuzima ushawishi wa Linda Mwananchi unaoendelea kuongezeka. Ingawa uamuzi huo ulizuiwa na mahakama kwa muda, wafuasi wa Linda Mwananchi wanadai kuwa hatua hiyo ilikuwa sehemu ya mkakati mpana wa kudhoofisha vuguvugu lao ndani ya chama. Mvutano huo unajiri wakati ODM inakabiliwa na mgawanyiko wa ndani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 huku makundi mawili makuu –Linda Mwananchi linalokosoa ushirikiano wa kisiasa na serikali, na Linda Ground linalounga mkono ushirikiano huo yakikosoana. Chama hicho kinatarajiwa kufanya mkutano wa wajumbe baadaye mwezi huu ambao dalili zinaashiria utaendeleza mgawanyiko baada ya wafuasi wa Linda Mwananchi kupinga ajenda zilizowekwa. Wadadisi wa siasa wanasema kuvurugwa kwa mikutano ya Linda Mwananchi na maafisa wa usalama huku ile ya Linda Ground inayoongozwa na kiongozi wa ODM Oburu Odinga ikifanyika kwa amani ni ishara ya mkakati mpana wa kuzima vuguvugu hilo. Huku mvutano ukizidi, wachambuzi wa siasa wanasema mbinu zinazodaiwa kutumika kuzima Linda Mwananchi zinaendelea kujenga kundi hilo linaloungwa mkono na vijana ambao ndio wengi nchini. “Ni wazi kuwa kila uchao kuna njama zinazosukwa kuzima Linda Mwananchi ikiwemo madai ya mbunge mmoja kuhusisha jina hilo na kauli au shughuli za kijeshi. Wasichojua wanaofanya hivyo ni kuwa wanaendelea kulijenga jina hilo. Vuguvugu linaloanzishwa na watu huwa na nguvu zinazoweza kushinda muungano wa tabaka la wanasiasa wenye ushawishi,” akasema mchambuzi wa siasa Diana Avisa.

KUTANGAZA kwa mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako kuwa atawania kiti cha ugavana Kaunti ya Taita Taveta na kudinda kuunga mkono serikali kwa awamu ya pili kunaonekana kumtia taabani kisiasa. Msimamo wake wa kisiasa unaonekana kuwapa wengi tumbojoto, ikiwemo serikali kuu kwani anajitetea kwa kudhihirisha kuwa yeye ni mchapa kazi jambo ambalo limekuwa tishio kwa wawaniaji wengine. Wiki hii, serikali kuu ikiongozwa na Naibu Rais Kithure Kindiki walizuru Kaunti ya Taita-Taveta ajenda kuu ikiwa kushawishi mbunge huyo ambaye ameonekena kuongoza wakazi wa Wundanyi kwa mihula miwili. Hili limefanyika siku chache tu baada ya muungano wa wabunge kutoka kaunti sita za Pwani (CPG) kumng’atua mamlakani Bw Mwashako kama mwenyekiti wa muungano huo na kumchagua mwakilishi wa wanawake wa Kilifi Getrude Mbeyu kwa nafasi yake. Uchaguzi huo ulionekena kama njia moja ya kumwadhibu mbunge huyo wa Wundanyi kwa kutounga mkono Rais William Ruto kwa awamu yake ya pili ya urais mwaka wa 2027. Bw Mwashako, ambaye ni mbunge aliyechaguliwa kwa tiketi ya Wiper Patriotic Party ambaye alionekana kukataa kujiunga na chama cha UDA huku gavana wa sasa Andrew Mwadime ambaye alichukua uongozi kama mgombea huru akiingia katika mtego wa serikali na kujiunga na chama hicho. Bw Kindiki katika ziara yake naye ameapa kutumia njia zote kumshawishi Bw Mwashako kutoshirikiana na upinzani. “Wapi Danson Mwashako? Amehepa? Lazima aingie kwa serikali. Akiendelea kufuatana na watu wa DCP, tutamsafirisha,” Naibu wa rais Kindiki alionya Bw Mwashako. Hivi karibuni, Bw Mwashako ambaye ameshikilia msimamo wake wa kutojiunga na serikali, amekuwa mstari wa mbele kukashifu uongozi wa Rais William Ruto akiwa na kundi la Linda Wananchi linaloongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na mbunge wa Embakasi kusini Babu Owino. Katika mahojiano na wanahabari baada ya ziara ya Bw Kindiki Kaunti ya Taita-Taveta mapema wiki hii, Bw Mwashako alikashifu serikali kwa kuwahadaa wakazi kwa kuzindua miradi miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. “Kama ni haki yetu kujengewa barababra ya Voi kwenda Sagalla mbona wanaijenga sasa na hawakuianza mwaka jana kama walijua kwamba watu wa eneo hili ni wa muhimu? Haimaanishi kwamba kama mimi siko katika chama tawala, tuwapokonye wakazi wa Taita-Taveta miradi ya barabara, na kama watafanya hivyo, hawastahili kuwa katika uongozi kwani hawastahili kushikilia maendeleo eti kwa sababu hatuko nao,” alisema Bw Mwashako. Hata hivyo, wachanganuzi wanamuonya Bw Mwashako kutojiunga na chama cha UDA iwapo anataka azma yake kuwa gavana itimie kwani serikali imekuwa na njama nyingi na Bw Mwadime ambazo Bw Mwashako amekuwa akizipinga. “Bw Mwashako akikubali kuingia UDA atapambana na Bw Mwadime kwa mchujo ambaye amekuwa kipenzi cha serikali na kama njia ya kumwadhibu, watamnyima cheti dakika ya mwisho wakati hawezi kuhamia chama kingine,” alisema Bw Elijah Mwarondo, mkazi wa Wundanyi. Mbunge huyo wa Wundanyi ameonekana mmoja wa viongozi ambao wako na nafasi kubwa ya kuchukua uongozi wa Kaunti hiyo mwaka wa 2027 kutokana na sifa za miradi aliyotekeleza katika eneobunge la Wundanyi kwa mihula miwili iliyopita. Bw Mwashako hata hivyo, anatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa Seneta wa sasa Jones Mwaruma, Bw Mwadime, aliyekuwa Gavana wa kwanza Bw John Mruttu na mwenzake Bw Granton Samboja, pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Bandari nchini (KPA) John Mwangemi. Hadi sasa, hakuna mwanamke ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta, huku wagombea wote waliotangaza nia yao wakiwa ni wanaume. Hata hivyo, kunasubiriwa iwapo wagombeaji hao watatii pendekezo la wazee kutoka Kaunti hiyo kuwapiga msasa kabla ya kuingia debeni. Hivi majuzi, viongozi na wazee kutoka maeneo bunge ya Mwatate, Wundanyi, Voi na Taveta wamekuwa wakijadiliana jinsi ya kutoa viongozi mwaka ujao ambao watatimiza mahitaji yao. Tangu kuanzishwa kwa ugatuzi, Kaunti ya Taita Taveta imekuwa na laana ya ‘Wantam’ kwani imeongozwa na magavana watatu: Mhandisi Mruttu (2013–2017), Bw Samboja (2017–2022), na Gavana wa sasa Bw Mwadime. Kiongozi wa muungano wa wazee hao Bw Thomas Mwadeghu amesema ijapo kisheria na kikatiba kila mmoja ana haki ya kugombea kiti chochote cha siasa, muhula huu wa kisiasa utakuwa tofauti kwani wakazi wa eneo hilo wamehadaiwa kwa muda na viongozi waliotangulia. “Viongozi kutoka miungano mbalimbali eneo la Taita na Taveta wanaungana kutoa mwelekeo wa kisiasa na licha ya wagombeaji kutokea wengi, tunatarajia kufanya mchujo kulingana na matakwa ya wakazi,” alisema Bw Mwadeghu.

GAVANA wa Siaya, James Orengo ameshinikiza kuachiliwa huru kwa baadhi ya wasaidizi wake na wafanyakazi wa serikali yake aliodai walikamatwa Jumamosi, Machi 7, 2026, siku moja kabla ya ziara ya Rais William Ruto katika kaunti hiyo. Kupitia ujumbe kwenye akaunti yake ya mtandao wa X siku hiyo, Bw Orengo alidai kuwa watu hao walikamatwa Siaya na Nairobi saa za jioni na kuzuiliwa na polisi, akitaja kitendo hicho kama ukiukaji wa katiba na misingi ya kidemokrasia. “Jioni hii (Machi 7, 2026) wafanyakazi kadhaa wa serikali yangu walikamatwa kiholela na polisi na kuzuiliwa Siaya na Nairobi kuhusiana na ziara ya rais Siaya kesho (Jumapili, Machi 8, 2026). Vitendo mbovu kama hivi vya polisi havina nafasi chini ya Katiba ya sasa inayoheshimu demokrasia. Nataka waachiliwe huru mara moja,” Bw Orengo akaeleza, bila kutaja majina ya watu hao aliodai walikamatwa na polisi. Rais Ruto alizuru Siaya mnamo Jumapili kuhudhuria sherehe ya kutoa shukrani kufuatia kuteuliwa kwa Katiba wa Wizara anayesimamia Huduma za Matibabu Dkt Ouma Oluga, katika Shule ya Msingi ya Okela, Uyoma, eneo bunge la Rarieda. Rais alizuru Siaya wakati ambapo migawanyiko na uhasama inashuhudiwa ndani ya chama cha ODM na kufuatia kuibuka kwa mirengo miwili ya “Linda Ground” na “Linda Mwananchi”. Bw Orengo anaegemea mrengo wa Linda Mwananchi unaoongozwa na Katibu Mkuu aliyeondolewa mamlakani Edwin Sifuna na unaopinga ushirikiano wa chama cha ODM na kile cha UDA chini ya serikali jumuishi. Mrengo huo pia unapinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto ukishikilia kuwa ODM itadhamini mgambea Uraia katika uchaguzi mkuu wa 2027. Nao mrengo wa Linda Ground unaoongozwa na kiongozi wa chama Oburu Oginga na mwenyekiti Gladys Wanga, anaunga mkono ushirikiano wa vyama hivyo viwili huku ukirindima “injili” ya kuchaguliwa tena kwa Dkt Ruto katika uchaguzi mkuu ujao.

MBUNGE mwakilishi wa jinsia ya kike Kaunti ya Kisumu Ruth Odinga amemtembelea kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Oburu Odinga huku kukiwa na madai ya migawanyiko ndani ya chama hicho. Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii Alhamisi, Machi 5, 2026, Ruth ambaye pia ni Katibu wa Uratibu wa ODM, alisema mazungumzo yao yalilenga kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama pamoja na mikakati ya kupeleka mbele ajenda za kitaifa. “Leo alasiri nilifanya ziara ya heshima katika afisi ya kiongozi wa chama cha ODM, Oburu Odinga, nikiwa na Mheshimiwa Catherine Omanyo. Tulikuwa na mazungumzo ya maana kuhusu kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama na kuendeleza malengo ya kitaifa yanayowahusu Wakenya wote,” alisema. Ruth alikuwa ameandamana na Omanyo ambaye ni naibu katibu mkuu wa chama hicho. Omanyo alipandishwa cheo hivi majuzi baada ya kuondolewa kwa Edwin Sifuna, hatua ambayo baadaye ilibatilishwa na Jopo la Kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa (PPDT). Ziara hiyo ilijiri huku kukiwa na madai kwamba kuna mvutano kati ya Ruth na kaka yake, Oburu. Hata hivyo, alikanusha madai hayo akisema wito wake wa kutaka utaratibu ndani ya ODM haufai kuchukuliwa kama ugomvi kati yake na kaka yake. Alisema hana sababu ya kupigana na kiongozi huyo wa chama, akieleza kuwa wito wake umekuwa kuhimiza makundi ya “Wantam” na “Tutam” ndani ya chama kushirikiana na kuzungumza kwa sauti moja. Ruth pia alisisitiza kuwa sauti za vijana zinapaswa kujumuishwa katika maamuzi ya chama, akisema hilo halipaswi kuchukuliwa kama dharau kwa seneta huyo wa Siaya. Alifafanua kuwa mara nyingi humshauri Oburu kuhusu masuala mbalimbali ya chama na kisiasa, akiongeza kuwa kutoa maoni yake ndani ya chama cha kidemokrasia kama ODM hakumaanishi kuwa anapinga uongozi wake. “Oburu ndiye kiongozi wa chama cha ODM na kila mtu anapaswa kuheshimu hilo. Ninazungumza naye mara kwa mara kama kiongozi wa chama na pia kama kaka yangu mkubwa. Lakini baadhi ya watu wameeneza wazo kwamba ninapigana naye,” alisema. Aliongeza kuwa wanaodai anagombana na Oburu ndio maadui wa kweli wa ODM kwani chama hicho kinaruhusu wanachama wake kutoa maoni yao kwa uhuru.

MWANZA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahomud amewahimiza askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuongeza uwajibikaji katika utoaji huduma kwa kufika kwa wakati katika maeneo ya matukio. Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili kuongeza ufanisi wa jeshi hilo. Naibu Waziri Ayoub … The post Ayoub ahimiza ufanisi huduma zimamoto first appeared on HabariLeo.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme ili kulinda afya za familia, mazingira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii. The post Dk Gwajima ataka wanawake kutumia nishati safi kupikia first appeared on HabariLeo.

MADIWANI katika Kaunti ya Turkana wameeleza wasiwasi kuhusu kile walichokitaja kuwa ukosefu wa usawa serikali inapokabiliana na ukame unaoathiri wadi zote 30 za kaunti hiyo, ambayo kwa sasa iko katika kiwango cha tahadhari. Kupitia hoja ya kuahirisha kikao, madiwani walisema zaidi ya familia 120,000 zinahitaji msaada wa dharura kutokana na uhaba mkubwa wa chakula katika eneo hilo. Wakazi wa maeneo ya mbali yaliyoathiriwa na ukame hawajapokea chakula cha msaada kutokana na changamoto za usafirishaji, licha ya serikali kusisitiza kuwa ina akiba ya kutosha kuzuia vifo vinavyotokana na njaa. Vijiji vya Lokipoto, Nakitongo na Kibish vimetajwa kuathirika zaidi, huku wazee, watoto na watu wanaoishi na ulemavu wakisubiri msaada ambao haujawafikia kwa sababu ya vikwazo vya usafirishaji na urasimu. Diwani wa Lokichar, Bw Samwel Lomodo, alisema baadhi ya vijiji katika wadi yake havijapokea msaada wowote. Alionya kuwa ukame umesababisha uhaba mkubwa wa maji, kupungua kwa malisho, vifo vya mifugo, ukosefu wa chakula na kuongezeka kwa utapiamlo miongoni mwa watoto na makundi yaliyo kwenye hatari. Alisema hali hiyo inaweza kugeuka kuwa janga la kibinadamu linaloathiri masomo, afya ya umma na uthabiti wa kijamii na kiuchumi. Katika kongamano la wadau lililofanyika Lodwar na kuhudhuriwa na viongozi wa eneo, maafisa wa serikali na mashirika ya kibinadamu, Waziri Geoffrey Ruku, alielezwa kuwa baadhi ya manaibu makamishna wa kaunti, wamelazimika kuuza sehemu ya chakula cha msaada ili kukodisha malori ya kukisambaza. Wabunge wa Turkana Magharibi na Turkana Kaskazini, Daniel Epuyo na Ekwom Nabuin, walieleza changamoto zinazochelewesha misaada wakitaja ukosefu wa fedha za kusafirisha chakula hadi vijiji vya mbali. Maeneo ya Kibish yaliyo takriban kilomita 400 kutoka Lodwar yameripotiwa kukosa misaada kabisa, huku wafugaji wanaovuka mipaka ya Uganda, Ethiopia na Sudan Kusini wakisahaulika. Afisa anayesimamia majanga katika Kaunti ya Turkana, Bw Patrick Losike, aliambia kamati ya Bunge la Kaunti kuwa kufikia Jumatano, wadi 22 zilikuwa zimepokea chakula cha msaada, huku zingine zikitarajiwa kupokea ndani ya siku nane. Alitaja changamoto za usafirishaji na wakandarasi kushindwa kuwasilisha chakula kwa wakati. Diwani maalum, Bi Mary Nakwapwan, alikosoa kucheleweshwa kwa misaada, akisema mifugo wamekonda na familia nyingi, hata mjini Lodwar, hukaa siku kadhaa bila mlo. Alisisitiza haja ya miradi endelevu kama visima vinavyofanya kazi na mipango ya unyunyizaji. Afisa wa Kaunti anayesimamia Kilimo na Mifugo Michael Eregae, alisema vifo vya mifugo vimefikia asilimia 10. Alithibitisha mlipuko wa ugonjwa unaoathiri mbuzi na kondoo, huku kukiwa na mpango wa kuchanja mifugo 600,000. Licha ya hatua hizo, madiwani wanasisitiza kuwa uratibu wa haraka na uwekezaji wa muda mrefu ni muhimu kuzuia majanga ya mara kwa mara ya ukame katika kaunti hiyo iliyo miongoni mwa zilizo hatarini zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi nchi.

DAR ES SALAAM: MINISTER for Community Development, Gender, Women and Special Groups, Dr Dorothy Gwajima, has said that access to clean cooking energy is a strategic national agenda that stimulates economic growth and promotes gender equality. She made the remarks on Wednesday during the Second Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) Women’s Conference, which aimed to…

MVUTANO mkali umeibuka ndani ya chama cha ODM kufuatia uamuzi kwamba hakutakuwa na uchaguzi wenye ushindani wa maafisa wa kitaifa katika Mkutano Maalum wa Wajumbe wa Kitaifa (NDC) uliopangwa kufanyika Machi 27. Badala ya uchaguzi, ajenda ya mkutano huo imepunguzwa kuwa ya kuthibitisha maafisa wa muda walioteuliwa awali, hatua inayodaiwa kupangwa na mrengo unaomuunga kiongozi wa chama Oburu Oginga ili kuimarisha uongozi wake na kuzuia mgawanyiko zaidi ndani ya chama. Taarifa zinaonyesha kuwa chama hicho kinapanga kuitisha NDC nyingine Desemba mwaka huu au mapema 2027 kujadili ajenda nyingine muhimu, ikiwemo uwezekano wa kuidhinisha muungano wa kabla ya uchaguzi kati ya ODM na UDA ya Rais William Ruto. Uamuzi wa kupunguza ajenda ya mkutano huo ulipitishwa Jumatano na Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC), hatua inayofasiriwa kama mkakati wa kudhibiti mvutano unaoendelea kufuatia mabadiliko ya uongozi baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi na mwasisi wa ODM, Raila Odinga, Oktoba 2025. Hata hivyo, mrengo pinzani unaoongozwa na Katibu Mkuu Edwin Sifuna, Naibu Kiongozi Godfrey Osotsi, Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino umetangaza kuwa hautashiriki mkutano huo iwapo nyadhifa zote za kitaifa hazitawaniwa kwa ushindani kidemokrasia. Seneta Osotsi alinukuu Katiba ya chama, hasa Ibara ya 47, inayoweka bayana mamlaka ya NDC ikiwemo kuchagua maafisa wa kitaifa, na kudai mzozo uliopo unaweza kutatuliwa tu kupitia uchaguzi wa wazi. Aidha, mrengo huo unataka orodha ya wajumbe wanaotarajiwa kuhudhuria ichapishwe mapema kwa ukaguzi wa umma, ikisema haiwezekani kuwa na NDC halali bila kukamilika kwa uchaguzi wa mashinani katika baadhi ya kaunti muhimu kama vile Nairobi na Kisumu. Kwa mujibu wa mpango wa sasa, maafisa wa muda waliothibitishwa na Baraza la Uongozi la Kitaifa (NGC) mjini Mombasa mwaka jana watawasilishwa mmoja mmoja mbele ya wajumbe kuthibitishwa au kukataliwa. Wanaotarajiwa kuwasilishwa ni pamoja na Dkt Oginga, manaibu wake watatu – Osotsi, Abdulswamad Nassir na Simba Arati pamoja na Mwenyekiti wa Kitaifa Gladys Wanga. Mwenyekiti wa ODM tawi la Nairobi George Aladwa amesema huu si wakati wa kufanya uchaguzi wa ushindani, akisisitiza kuwa uchaguzi wa mashinani lazima ukamilike kwanza kabla ya kufungua ushindani kuhusu nyadhifa za kitaifa. Alisema wanaotaka kuwania wanafaa wasubiri mkutano ujao kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Wakati huo huo, baada ya NEC kumvua Sifuna wadhifa wa Katibu Mkuu na kumteua naibu wake, Catherine Omanyo, kuushikilia, Jopo la Kutatua Mizozo ya Vyama lilitoa amri ya muda kuzuia utekelezaji wa uamuzi huo hadi kesi itakaposikilizwa na kuamuliwa. NDC ya ODM inaundwa na wanachama wa NEC, wabunge, magavana, wenyeviti wa matawi ya kaunti, pamoja na viongozi wa walio wachache na walio wengi katika mabunge ya kaunti. Katiba ya chama inaweka idadi ya wajumbe kuwa 3,000. Mkutano huo sasa unatazamwa kama kipimo muhimu cha mwelekeo wa ODM na mizani ya nguvu kati ya makundi hasimu, huku matokeo yake yakitarajiwa kuathiri mustakabali wa chama hicho kuelekea 2027.

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na taasisi za fedha kuiwezesha sekta ya fedha kupata mikopo yenye gharama nafuu ili kuisaidia jamii ya kipato cha chini kumiliki makazi bora. Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Ali Munde alisema hayo hayo Dar es Salaam akizindua huduma ya mikopo midogo ya makazi Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Khamis Mussa Omar. The post Wakipato cha chini kuwezeshwa kumiliki makazi first appeared on HabariLeo.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeeleza mikakati ya kuimarisha usafiri wa anga ikiwamo kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Pemba. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohamed amesema hayo wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika siku 100 madarakani juzi. The post SMZ kuboresha usafiri wa anga first appeared on HabariLeo.

UPINZANI umeomba Bunge kukataa Mswada wa Wizara ya Fedha kuhusu Miundombinu, 2026 na kusitisha mpango wa kuuza sehemu ya hisa za serikali katika Safaricom, ukisema mapendekezo hayo yanahatarisha ulinzi wa kikatiba wa fedha za umma na mali ya kimkakati ya taifa. Katika taarifa ya pamoja, viongozi wa upinzani waliitaka Bunge la Taifa la Kenya na Kamati yake ya Fedha na Mipango ya Kitaifa kutupilia mbali mswada huo mzima na Sera Nambari 3 ya 2025, inayopendekeza kupunguza umiliki wa serikali katika Safaricom. Upinzani pia umetaka uchunguzi huru wa kikatiba kuhusu pendekezo la hazina hiyo, pamoja na tathmini ya kina ya mali ya kimkakati kabla ya kupunguzwa kwa hisa za serikali katika kampuni hiyo ya mawasiliano, ambayo jukwaa lake la fedha kwa simu, M-Pesa, linaendesha sehemu kubwa ya malipo ya kidijitali na huduma za serikali. Kiongozi wa Wiper Democratic Movement, Kalonzo Musyoka, alisema hazina hiyo inayopendekezwa ni “suluhisho linaloleta tatizo,” akidai pengo la miundombinu nchini halitokani na ukosefu wa mifumo ya kifedha bali ni matokeo ya udhaifu katika utekelezaji wa miradi, ufisadi katika ununuzi na ukosefu wa uwazi wa kifedha. Alisema Kenya tayari ina zaidi ya hazina 60 ya umma nje ya Hazina Kuu nyingi zikiwa na majukumu yanayofanana na viwango vya chini vya uwajibikaji.

MKANDARASI anayejenga Kiwanda cha Uchapaji cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ameongezewa miezi mitatu akamilishe kazi hiyo. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema hayo alipotembelea mradi huo uliopo Makao Makuu ya TSN, Tazara katika Barabara ya Mandela, Dar es Salaam jana. The post Mkandarasi kiwanda cha TSN aongezewa miezi 3 first appeared on HabariLeo.

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said, amesema jumla ya wanufaika 41,000 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia (PAMOJA) unaotekelezwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. The post Wanufaika 41,000 kunufaika na mradi wa PAMOJA Zanzibar first appeared on HabariLeo.

MZOZO kuhusu umiliki na usajili wa chama kinachopendekezwa cha Linda Mwananchi Party of Kenya umeanza kuchukua mkondo wa kisheria baada ya aliyewasilisha jina hilo, kupinga rasmi malalamishi yaliyowasilishwa na kundi la viongozi wa ODM wanaotaka kuzuia usajili wake. Kupitia mawakili wake, Bw Charles Wanyonyi, aliyewasilisha ombi la kuhifadhi jina la Linda Mwananchi Party of Kenya, amepuuza pingamizi iliyowasilishwa na kundi linaloegemea upande wa Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna, akisema halina msingi wa kisheria. Katika barua kwa Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP), mawakili wa Bw Wanyonyi walisema mteja wao alitumia haki yake ya kikatiba kama Mkenya kuomba kusajili chama na hakuwa akimtumikia kiongozi yeyote wa kisiasa. Pingamizi hiyo iliwasilishwa na mawakili kwa niaba ya Bw Sifuna na viongozi wengine akiwemo Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Seneta wa Kisii Richard Onyonka. Pia wabunge Babu Owino (Embakasi Mashariki), Caleb Amisi, Anthony Kibagendi, Majimbo Kalasinga, Caroli Omondi na Barongo Obadiah wanawaunga mkono. Viongozi hao wanadai kuwa kauli mbiu ya “Linda Mwananchi” imehusishwa kwa karibu na mikutano yao ya kisiasa na harakati za kuwahamasisha wananchi, hivyo kuisajili kama chama bila ushiriki wao kunaweza kupotosha umma na kusababisha mkanganyiko kuhusu umiliki na mwelekeo wa vuguvugu hilo. Aidha, wameonya kuwa watuwanaohusika na chama hicho wanaweza kutumia majina yao na umaarufu wao wa kisiasa kukusanya fedha kwa njia isiyo halali. Hata hivyo, mawakili wa Bw Wanyonyi wamesema jina hilo halijawahi kusajiliwa rasmi na mtu au taasisi yoyote kama chama cha kisiasa, hivyo hakuna mtu mwenye haki ya kipekee kulihusu. Wameeleza kuwa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Vyama vya Kisiasa kinaeleza sababu pekee zinazoweza kumfanya Msajili kukataa jina, kama vile kufanana na chama kingine kilichosajiliwa au kuwa kinyume na maslahi ya umma - hoja ambazo, kwa mujibu wao, hazijatimizwa. Mzozo huo sasa umeiweka afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa, inayoongozwa na Bw John Cox Lorionokou, katika hali tete ya kufanya uamuzi wa kisiasa na kisheria. Kisheria, Msajili ana siku 14 kuchunguza ombi la kuhifadhi jina la chama. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kitaifa wa ODM, Bi Gladys Wanga amewataka wanachama wa Linda Mwananchi kueleza wazi iwapo wanakusudia kubaki ndani ya chama au kuanzisha mwelekeo wao huru. Mbunge wa Homa Bay Mjini, Bw Peter Kaluma, hata hivyo, amesisitiza kuwa ODM bado iko imara. Wachambuzi wanasema mvutano huo unaonyesha umuhimu wa chapa ya kisiasa katika mazingira ya ushindani kuelekea 2027. Wanakumbusha kuwa kabla ya kura ya maoni ya 2005, jina la ODM liliwahi kusajiliwa na Mugambi Imanyara kabla ya baadaye kutwaliwa na marehemu Raila Odinga. Hatima ya Linda Mwananchi sasa iko mikononi mwa Msajili, huku ombi hilo likisubiri uamuzi rasmi.

BAJETI ya Ikulu ya mwaka wa kifedha 2025/26 imepanda maradufu kufikia Sh16.998 bilioni kufuatia kutengewa pesa zaidi kati kati ya mwaka ambayo ni matumizi bila idhini ya Bunge. Makadirio ya bajeti ya ziada kwa mwaka wa kifedha wa sasa, yaliyowasilishwa mbele ya Bunge yanaonyesha kuwa, bajeti ya Ikulu iliongezeka kwa Sh8.42 bilioni. Kupatiwa pesa zaidi kati kati ya mwaka kulifanya matumizi ya kila mwaka ya Ikulu kuzidi ya ofisi zinazofanana katika nchi zilizoendelea kama Amerika (Sh10 bilioni), Ujerumani (Sh7 bilioni), Ureno (Sh2.6 bilioni) na karibu kufikia ile ya Ufaransa (Sh17.5 bilioni). Karibu na nyumbani, matumizi ya Ikulu ya Kenya yalikuwa ya juu kuliko Nigeria (Sh3.1 bilioni), Afrika Kusini (Sh7.8 bilioni), Algeria (Sh8.9 bilioni) na Tanzania (Sh1.7 bilioni). Sh16.998 bilioni ni kiasi kikubwa zaidi kilichotumika na Ikulu tangu 2013. Haya yanajiri huku Mdhibiti wa Bajeti (CoB) Dkt Margaret Nyakang’o akitoa onyo kuhusu uwezekano wa Ikulu kutumia bajeti yake yote mapema katikati ya mwaka wa kifedha. Stakabadhi zilizowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha John Mbadi zikitaka idhini ya wabunge kwa matumizi ya ziada zinaonyesha kuwa, Ikulu kwanza iliomba Sh2 bilioni “kwa matumizi mengine ya uendeshaji,” ambayo si dharura, Septemba 8 2025. “Kufuatia idhini ya bajeti ya mwaka wa kifedha 2025/26, Wizara ya Fedha imetoa fedha za ziada kwa Wizara, Idara na Mashirika kulingana na katiba,” alisema Waziri Mbadi katika stakabadhi zilizowasilishwa Bungeni. Maombi haya ya fedha za ziada yameelezwa kuwa ya kuimarisha operesheni na ukarabati katika Ikulu. Mnamo Juni 2025, Bunge lilitengea Ikulu Sh8.6 bilioni, ikiwa ni Sh7.7 bilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh894.91 milioni kwa maendeleo. Hata hivyo, bajeti ilipanda hadi Sh16.998 bilioni kufikia Februari, huku Sh16.1 bilioni zikiwa kwa matumizi ya kawaida na maendeleo yakiwa Sh894.91 milioni tu. Stakabadhi zinaonyesha iliomba Sh4.5 bilioni chini ya Kifungu cha 223 Septemba 2025, miezi mitatu tu baada ya kuanza kwa mwaka wa kifedha, baada ya bajeti ya awali kutumika. Wizara ya Fedha baadaye ilikubali na kutoa Sh4.4 bilioni tarehe mbalimbali. Kifungu cha 223 cha katiba kinaruhusu serikali ya kitaifa kupata fedha za ziada pale ambapo bajeti iliyotengwa na Bunge inakosa kutosha au kukitokea dharura isiyoweza kuepukika kama ukame, mafuriko au janga lisilotarajiwa. Makadirio ya bajeti ya Ikulu kwa mwaka wa kifedha 2025/26, yaliyopitishwa na Bunge Juni 2025, yalikuwa Sh8.58 bilioni na kisha yakapanda hadi Sh16.998 bilioni, ikiwa ni ongezeko la Sh3 bilioni zaidi mwaka wa kifedha 2024/25. Wataalamu wa fedha katika Ofisi ya Bajeti ya Bunge (PBO) wanasema ombi hili ni ukiukaji wa katiba na udhaifu wa nidhamu ya kifedha. Dkt Nyakang’o alionya kuwa ingawa Ikulu ilionyesha utendaji bora, ikiwa na kiwango cha matumizi cha asilimia 55, juu zaidi ya wastani wa robo ya kwanza wa asilimia 25, bado ipo hatarini kufyonza bajeti yake mapema kabla ya mwisho wa mwaka wa kifedha, jambo linalohujumu uhalali wa bajeti. Huduma za Ikulu ni pamoja na kuratibu kazi za Ikulu na usimamizi wa mafao ya kifedha kwa marais na makamu wa rais waliostaafu. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa kifedha, kuratibu kazi za Ikulu kuligharimu Sh4.7 bilioni, ikiwa ni Sh4.45 bilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh235.10 milioni kwa maendeleo. Kwa mafao ya kifedha ya marais na makamu wa rais waliostaafu, Sh452.6 milioni zilitengwa, huku Sh50.59 milioni zikiwa zimetumika tayari.

MAHAKAMA Kuu jijini Mombasa imewaachilia huru watu watatu waliokuwa wakikabiliwa na shtaka la mauaji, huku ikitoa onyo kali dhidi ya matumizi ya makundi ya ulinzi yasiyo rasmi (vigilante) katika kukabiliana na ghasia za uchaguzi wakati wa Uchaguzi Mkuu. Katika hukumu iliyotolewa Februari 12 jijini Mombasa, mahakama iliwaachilia huru Rama Lenga Beja, Felix Mwangovi na James Mwamuye Charo kuhusiana na kifo cha Nicodemus Karima Shikahili. Marehemu Nicodemus alikuwa mfuasi wa chama cha chungwa (ODM) na aliuawa usiku wa kuamkia uchaguzi wa Agosti 8, 2017 katika eneo la Kilifi Kusini. Kesi hiyo ilitokana na juhudi za vijana wa eneo hilo waliokuwa wakiegemea upande wa ODM kuunda kikundi cha kushika doria kwa lengo la kuimarisha usalama kabla na siku ya uchaguzi. Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulionyesha kuwa eneo la Kilifi Kusini lilishuhudia vurugu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013, yakiwemo matukio ya kuchoma nyumba na vifo ikiwemo polisi. Kutokana na hali hiyo, takribani vijana 25 walijiweka kwa vikundi kushika doria katika maeneo yaliyotajwa kuwa hatari kufuatilia mienendo ya kutiliwa shaka na kutoa taarifa kwa maafisa wa polisi wa Kituo cha Polisi cha Chasimba pamoja na wazee wa vijiji. Usiku wa Agosti 7, 2017, vijana 18 walitumwa kwa kutumia pikipiki sita kufuatilia hali ya usalama katika maeneo ya Banda la Salama, Mwarakaya, Kaoyeni na Kizingo. Shikahili, aliyekuwa amesafiri kutoka Nairobi kushiriki katika uchaguzi, alijiunga na kikundi hicho. Kwa mujibu wa ushahidi, mmoja wa waendesha pikipiki aliripoti kuona gari lililozua shaka na akaelekezwa kulifuatilia. Muda mfupi baadaye, taarifa zikasambaa kuwa alishambuliwa na pikipiki kuchukuliwa. Wafuasi wengine wa kikundi hicho, akiwemo Shikahili, walielekea eneo hilo kutoa msaada lakini wakakumbana na umati wenye hasira. Katika vurugu zilizofuatia, Shikahili aliachwa nyuma na baadaye kupatikana akiwa amejeruhiwa vibaya. Ripoti ya uchunguzi wa maiti ilionyesha kuwa alikuwa na jeraha kubwa kichwani, majeraha ya kukatwa yaliyopenya hadi kwenye fuvu la kichwa, ubongo kuonekana wazi pamoja na mifupa kadhaa kuvunjika. Alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi kulikosababishwa na jeraha la kichwa. Upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa, waliodaiwa kuhusishwa na shughuli za Chama cha Jubilee, walihusika katika mzozo huo uliosababisha kifo hicho. Hata hivyo, mashahidi 13 wa upande wa mashtaka hawakutoa ushahidi wa moja kwa moja unaowaonyesha washtakiwa wakimshambulia marehemu. Aidha, dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kufuatilia gari hilo na ambaye tukio lake lilichochea mtafaruku, hakufika kutoa ushahidi, jambo ambalo mahakama ililitaja kuwa pengo kubwa katika uchunguzi. Katika uamuzi wake wa kuwaachilia huru, jaji alieleza kuwa upande wa mashtaka haukufaulu kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba washtakiwa ndio waliosababisha majeraha yaliyompelekea marehemu kifo. "Kwa hivyo, washtakiwa wote wameachiliwa huru," Mahakama ilisema huku ikitambua kuwa kundi hilo lilianzishwa kutokana na hofu ya vurugu za hapo awali, ilionya kuwa kuundwa kwa makundi ya ulinzi yenye misingi ya kisiasa na yasiyo na usimamizi madhubuti kunaweza kuhatarisha usalama na utulivu wa jamii. Mahakama ilielekeza vyombo vya usalama, tume ya uchaguzi na wadau wengine kushirikiana kuweka mifumo ya kisheria, jumuishi na iliyoratibiwa vizuri ya usalama wa kijamii kabla ya chaguzi zijazo.

WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) isimamie shule zote nchini ziwe na matundu ya vyoo ya kutosha. The post Mwigulu akerwa ukosefu matundu ya vyoo shuleni first appeared on HabariLeo.

GAVANA Joseph Lenku na mtangulizi wake David Nkedianye wanatarajiwa kukwaruzana tena, wawili hao wakisaka useneta mnamo 2027. Katika chaguzi za 2017 na 2022, wawili hao walikuwa na uhasama mkali wa kisiasa, huku Bw Lenku akishinda ugavana mara mbili. Mnamo 2017, Gavana Lenku alimshinda Bw Nkedianye ambaye alikuwa amehudumu kama mkuu wa kaunti hiyo kutoka 2013-2017 kupitia ODM. Mwaka huo Bw Lenku alipata ushindi kupitia chama cha Jubilee. Kwenye kura ya 2022, wawili hao walifarakana huku Bw Lenku akiwika tena. Bw Nkedianye ambaye alikuwa ODM aligura chama hicho na kuingia Jubilee huku Gavana Lenku naye akigura Jubilee na kuingia ODM. Awali kulikuwa na jitihada zilizoendelezwa za kuhakikisha wawili hao wanaelewana ili kuwe na mwaniaji mmoja wa ugavana chini ya Muungano wa Azimio. Hata hivyo, wawili hao waliachwa wamenyane huku Bw Lenku akipata kura 117,600 naye Nkedianye akipata kura 75,337. Katoo Ole Metito ambaye aliwania kupitia UDA alipata kura 111,752. Mnamo Juni 2, 2023, Rais William Ruto alimteua Bw Nkedianye kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti na Mafunzo Kuhusu Wanyamapori kwa muda wa miaka mitatu. Hii ni baada ya Bw Nkedianye kuhamia UDA mnamo Septemba 12, 2023. Bw Nkedianye kwa sasa anashirikishiana na Bw Ole Metito ambaye analenga ugavana tena 2027. Wameelewana kuwa Bw Nkedianye atawania useneta naye Bw Ole Metito ambaye anafanya kazi ikulu agombee ugavana. Seneta wa sasa Samuel Seki ambaye alichaguliwa kupitia tiketi ya UDA amekuwa akihusishwa na DCP naye pia analenga ugavana. Seneta Maalum Peris Tobiko na Naibu Gavana Martin Moshisho ambao wote wapo mrengo wa Bw Lenku nao pia wanalenga kiti cha ugavana. Bw Lenku ametoa wito wa kubuniwa kwa Chama cha Kisiasa cha jamii ya Maa huku akisema anaunga kuchaguliwa kwa Rais Ruto muhula wa pili. “Ruto amerejesha mbuga ya Amboseli kwa serikali ya kaunti na naamini njia ya kumlipa ni kumpigia kura tena. Raia hawatashawishiwa na vyama vya kisiasa bali utendakazi wa kila kiongozi,” akasema Bw Lenku. Naye Bw Nkedianye amekuwa akisisitiza kuwa ndiye anatosha kuwania useneta naye pia akiunga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto. “Tutazunguka mijini na mashinani ili kujaza kura za Rais Ruto. Pia naamini kuwa ushirikiano kati ya ODM na UDA utatumika kuamua mwaniaji na kuhakikisha kura zinaelekezwa kapu moja,” akasema Bw Nkedianye.

RAIS Samia Suluhu Hassan ameendeleza nafasi ya Tanzania katika jukwaa la Afrika na kimataifa kama sehemu ya kuimarisha diplomasia ya kiuchumi ili kufi kia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. The post Rais Samia ajizatiti malengo Dira 2050 first appeared on HabariLeo.

WAZEE na wataalamu wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa wametabiri kuwa baadhi ya sehemu za Kaunti ya Kajiado zitapokea mvua kati ya Machi-Aprili 2026. Tangazo hilo limewapa wakazi wengi matumaini ikizingatiwa kaunti hiyo kwa sasa inaendelea kukeketwa na ukame. Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Ukame (NDMA) imeorodhesha kaunti hiyo kama inayoandamwa na ukame na kusema zaidi ya nyumba 64,300 zinakabiliwa na ukame. Takwimu ya hivi majuzi kutoka NDMA inaonyesha kuwa zaidi ya Wakenya milioni 2.1 waliathiriwa na ukame mnamo Januari na idadi hiyo imepanda hadi milioni 3.3 mnamo Februari. Kaunti 23 kame zimeathirika na ukame huo na serikali imetenga Sh10 bilioni kuokoa hali. Wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya Kajiado wamehama na mifugo yao hadi kaunti jirani. Mnamo Alhamisi, wazee wa Maa walifanya tambiko mjini Kajiado ili kuleta mvua. Tambiko hilo lilihusisha kuchinjwa kwa mbuzi kisha matumbo yake yakaangaliwa kutabiri hali ya hewa. Mzee Moses Ole Nkina, 70, aliongoza tambiko hilo lililodumu kwa dakika 30 kabla ya wazee hao kutangaza kuwa mvua inakuja siyo Umasaini tu bali pia sehemu nyingine za nchi. Walibaini kuwa damu kwa kiasi cha chini, ilitiririka katika sehemu ya mishipa polepole, hilo likiashiria mvua chache maeneo ya kusini. “Damu ilienea sana sehemu nyingine ya mishipa na hilo linaonyesha mvua zaidi ya kiwango cha wastani maeneo ya Kaunti ya Kajiado na mengine nchini,” akasema Mzee Nkinai lakini akasema hajui ni lini mvua itaanza. Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri ya Hali ya Hewa Kajiado Benson Lubanga alisema mtazamo wa kisayansi unalandana na njia za kitamaduni. Kwa mujibu wa Bw Lubanga, maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi yanatarajiwa kupokea mvua inayozidi kiwango cha wastani. “Kaunti hii itapokea mvua kwa kiwango cha wastani huku mengine yakipokea mvua zaidi ya wastani. Tunatarajia wafugaji wazingatie hili,” akasema Bw Lubanga. Kamishina wa Kaunti ya Kajiado Michael Yator alisema kuwa serikali inachukua hatua za dharura ili kuhakikisha kuwa hakuna anayekufa njaa kutokana na ukame huo.

NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki amesema hatetereshwi na mjadala unaoendelea kuhusu wadhifa wake akisema binafsi yeye si mtu wa kutishwa na siasa za ubabe akisisitiza kwamba kiti chake kitasalia Mlima Kenya 2027. Profesa Kindiki amesema kuwa kwa sasa kazi yake kuu ni kumsaidia Rais William Ruto kutimiza malengo yake kimaendeleo huku akiwaambia wafuasi wake kuwa atahudumu kama naibu rais hadi 2032 kisha ajipange ‘hapo mbele’. “Nimesikia watu wameleta wasiwasi huku na ninawauliza kwa hii serikali mnajua mimi ndiye nambari mbili? Nasikia kuna watu wanaongea lakini nawaambia msiletewe wasiwasi na mambo madogo madogo ambayo watu wanaongea,” akasema Profesa Kindiki akiwa Kaunti ya Meru. “Mimi ndiye naibu rais na hiki kiti hakuna mahali kinaenda. Unajua mimi nimekuwa kwa siasa kwa muda na mwanasiasa mzuri anajua siku ya kuongea na siku ya kunyamaza,” akaongeza. Tamko hilo lilionekana kumlenga Kinara wa ODM Dkt Oburu Oginga ambaye Jumatano wiki jana alisema chama hicho kinalenga wadhifa huo kinapoendelea kujadiliana na UDA. Profesa Kindiki hasa analenga kuletea Rais zaidi ya kura milioni moja za Mlima Kenya Mashariki na shinikizo za ODM zimesababisha wasiwasi kuwa huenda akakosa kuwa mgombeaji wa rais mnamo 2027. “Ukiwa mwanasiasa unaongea kila siku basi huna akili. Kuna siku ya kupiga siasa na siku ya kupiga kazi, kitu kitatusaidia ni kufanya maendeleo kwa watu wetu,” akasema. Kauli yake ilikuja baada ya baadhi ya viongozi kutoka Ukanda wa Mlima Kenya kutangaza Jumamosi kuwa wataondoka serikalini iwapo Profesa Kindiki hatakuwa mgombeaji mwenza wa Rais Ruto. Aidha, wakati ambapo Rais Ruto alikuwa Kisumu mapema mwezi huu kusambaza pesa kupitia Mradi wa NYOTA, Dkt Oginga alimwambia Profesa Kindiki asiwe na wasiwasi kwa sababu ODM haindei kiti chake. Hata hivyo, kinara huyo wa ODM anaonekana alighairi nia wikendi akiwa Pwani baada ya kusema kuwa wanalenga unaibu rais kwenye muafaka na Rais Ruto. “Wale unasikia wakiongea wasiwatie wasiwasi. Sisi ndio mafundi wa siasa. Mkiniangalia mnaona mtu ambaye anaweza kutishwa? Tusifanye siasa ya kuonyeshana madharau,” akasema. Wakati wa ziara hiyo Profesa Kindiki aliahidi ujenzi wa Daraja la Nithi akitaja kujengwa kwa Hospitali ya Meru na barabara kadhaa Imenti kama baadhi ya ahadi ambazo zimetimizwa na serikali. Profesa Kindiki kando na kupambana asalie mgombeaji mwenza wa Rais Ruto pia anapambana kuhakikisha rais anapata kura za Mlima Kenya Magharibi anakotoka hasimu wake aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

SENETA wa Nairobi Edwin Watenya Sifuna anaendelea kujijenga kama mmoja wa wanasiasa shupavu na wakili anayejua kuogelea mawimbi ya siasa za Kenya bila kuyumba. Sifuna alizaliwa Mei 22, 1982 katika Hospitali ya St Mary’s, Mumias, Kaunti ya Kakamega. Baba yake alikuwa mtumishi wa umma katika iliyokuwa Halmashauri ya Manisipaa, huku mamake akiwa mwalimu wa shule ya msingi. Ami yake, Lawrence Sifuna alikuwa mwanasiasa machachari aliyewakilisha eneo bunge la Bumala. Sifuna alianza masomo yake katika Shule ya Msingi ya Kakamega Township kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Musingu alikofanya mtihani wa KCSE. Baadaye alisomea Shahada ya Sheria (LLB) katika Chuo Kikuu cha Nairobi na kuhitimu mwaka 2006. Aliendelea na Stashahada ya Uzamili katika Shule ya Sheria Kenya mwaka 2007, kisha kufanya mafunzo ya uwakili katika kampuni ya Kairu & McCourt Advocates. Aliapishwa rasmi kama wakili wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Safari yake ya kisiasa ilianza kuonekana wazi mwaka 2013 alipojiunga na muungano wa CORD kama mjumbe wa kamati ya kiufundi na ushauri. Baadaye aliendelea na jukumu hilo ndani ya muungano wa NASA. Mwaka 2017 alijaribu bahati yake kuwania ubunge wa Kanduyi kupitia tiketi ya ODM lakini hakufaulu katika kura za mchujo. Hata hivyo, ODM ilimteua kuwania kiti cha Useneta wa Nairobi katika uchaguzi mkuu wa 2017. Ingawa alishindwa na Johnson Sakaja, alijizolea zaidi ya kura 674,000, akithibitisha kuwa alikuwa ameanza kujijengea jina katika siasa za jiji kuu. Mwaka 2018 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa ODM kuchukua nafasi ya Ababu Namwamba. Katika nafasi hiyo, alijitokeza kama msemaji mkali wa chama na mtetezi wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi. Mwaka 2019 alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Centre for Multiparty Democracy (CMD), akiongeza sifa zake katika siasa za kitaifa. Katika uchaguzi mkuu wa 2022, Sifuna alirejea tena kuwania Useneta wa Nairobi na kushinda kwa kura 716,876. Tangu wakati huo, amekuwa akihudumu kama Seneta wa Nairobi na pia Naibu kiongozi wa Wachache katika Seneti. “Sifuna si mwanasiasa wa kawaida. Ni wakili aliyekuzwa na maadili ya haki na usawa tangu utotoni, misingi ambayo ilimwelekeza kusomea Shahada ya Sheria na baadaye kuingia katika medani ya siasa kwa lengo la kupigania Wakenya wa kawaidam,” anasema katika tovuti yake.

UBABE na tofauti kali za kisiasa jana ziliendelea kuandama ODM huku mkutano ulioandaliwa Kitengela, Kaunti ya Kajiado na viongozi waasi wa chama ukitibuliwa na maafisa wa usalama. Kinara wa ODM Dkt Oburu Oginga aliwaongoza wanasiasa wanaoegemea mrengo wake katika mkutano mkubwa wa kisiasa uwanja wa Tononoka eneobunge la Mvita jijini Mombasa. Kwa upande mwingine, akthari ya wafuasi wa ODM walifurika mjini Kitengela kwenye mkutano uliosheheni ghasia. Mkutano huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama anayekabiliwa na utata Edwin Sifuna pamoja na kundi la viongozi waasi wa ODM na baadhi kutoka upinzani. Mkutano wa Kitengela ulikuja baada ya Bw Sifuna kuondolewa kama katibu mkuu wiki jana lakini akapata faraja ya muda kortini. Jijini Mombasa, Dkt Oginga alijitosa kwenye mjadala wa kutimuliwa kwa Bw Sifuna akisema Katibu Mkuu anayetambuliwa na chama ni Mbunge Mwakilishi wa Kaunti ya Busia Catherine Omanyo. “Sisi katibu wetu mkuu ni Bi Omanyo kwa sababu uamuzi ulifanywa kuwa aliyekuwa katibu wetu akae nje kutokana na utovu wa nidhamu. Hatujamfukuza kutoka kwa chama ila wadhifa wake ndio tumempokonya,” akasema Dkt Oginga. Alikuwa akizungumza katika ibada ya Kanisa la Shalom. Dkt Oginga alisema sheria za chama lazima zifuatwe na wote na wale ambao wanakosa kuziheshimu lazima waadhibiwe. “Suala la Sifuna tumelimaliza na ukikosea lazima uadhibiwe wala chama hakiwezi kuongozwa na uoga wa kukutimua. Hakuna mtu ambaye hawezi kuadhibiwa na chama akiwemo mimi,” akaongeza Dkt Oginga, nduguye marehemu Kinara wa chama hicho Raila Odinga. “Nikikosa heshima basi lazima nifurushwe chamani. Hakuna mtu ambaye ni mkubwa kuliko chama kwa sababu chama kinabuniwa kwa sababu ya watu. Hakuna mtu ambaye ataogopwa au kufikiria yuko juu ya sheria ODM,” akasema seneta huyo wa Siaya. Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga naye alisema chama kitaendelea kusimamia falsafa ya uongozi wa Raila na kuwatetea Wapwani. [caption id="attachment_184774" align="alignnone" width="800"] Kinara wa ODM Oburu Oginga akiwasili uwanja wa Tononoka na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir Februari 15, 2026 kwa mkutano wa Linda Ground. Picha|Hisani[/caption] “Raila hakuwa akifanya chochote bila kushauriana na Dkt Oburu ndiyo maana tunajua kiongozi wetu wa sasa hawezi kutuelekeza vibaya,” akasema akiwataka viongozi kutoka Pwani waendelee kuwa nyuma ya ODM. Dkt Oginga na viongozi wanaounga mkono Serikali Jumuishi wamekuwa wakiongoza mrengo wa Linda Ground, kampeni inayolenga kuhakikisha ODM inalinda ngome yake ya kisiasa. Kitengela nako kuligeuka uwanja wa vitoza machozi, polisi wakiwafurusha wafuasi wa Linda Wananchi ambao walikuwa wahutubiwe na Bw Sifuna na wenzake. Awali katika ibada ya kanisa, baadhi ya waliohudhuria na kuendelea kukosoa uongozi wa Dkt Oburu ODM ni Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Vihiga Osotsi Atsieno, wabunge Babu Owino (Embakasi Mashariki), Caleb Amisi (Saboti), Anthony Kibagendi (Kitutu Chache Kusini), Oundo Ojiambo (Funyula), Joshua Kimilu (Kaiti) na Seneta wa Kisii Richard Onyonka. Ghasia zilianza baada ya Bw Sifuna kupewa mapokezi ya shujaa mjini Kitengela. Umati huo ulionekana kulemea polisi huku baadhi ya vijana wakiwarushia polisi mawe. Watu kadhaa walijeruhiwa polisi walipowakabili vijana hawa huku Bw Sifuna na viongozi wenzake wakitimka mbio na kuenda zao. “Hata wakinimaliza leo, najua kuna zaidi ya watu milioni 15 ambao najua wataendeleza uanaharakati huu. Waliharibu jukwaa letu asubuhi pamoja na vipaza sauti na sasa wametibua mkutano wetu, bado tutaendelea kupambana,” akasema Bw Sifuna. Bw Orengo naye alivamia Dkt Oginga akidai chama ‘kimeuzwa’ kwa Rais Ruto lakini akasisitiza ataendelea kwenye mkondo wa mapambano. “Hili vuguvugu letu halihusiani na 2027 bali ni la kukomboa taifa sasa. Ni waoga tu ndio watawazima wanasiasa wanaochipuka na mrengo huu wa Sifuna ndio utaleta mabadiliko kwa nchi,” akasema Gavana Orengo. Bw Owino alisema hata kama mkutano wao umesambaratishwa, bado wataendelea kuwafikia vijana na wanawake kuhusu kura ya 2027. “Oburu Odinga na wenzake huenda wana nguzo za chama lakini sisi tuna wanachama na wafahamu hatutayumbishwa na uoga. Wanauza chama chetu lakini hatutakuwa sehemu ya mpango huo,” akasema Bw Owino. Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Winnie Odinga, mwanawe Raila hakuwa Kitengela katika mkutano ambao ulihudhuriwa na zaidi ya wabunge 20 na madiwani wa Bunge la kaunti mbalimbali. Jana taharuki ilitanda Kitengela huku polisi polisi wakiwafurusha baadhi ya vijana waliodaiwa walisafirishwa kutoka Ongata Rongai kutibua mkutano huo. Watu wasiojulikana pia waliondoa bango lililokuwa na picha za viongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi kwenye mzunguko wa barabara ya Mombasa.

Chadema’s Vice Chairman (Mainland), Mr John Heche, has outlined two "non-negotiable" conditions the party requires before joining national reconciliation talks initiated by President Samia Suluhu Hassan.

KWA Waganda wanaotishiwa na serikali yao kwamba itaangamiza upinzani kabisa, labda nchi yao isalie na chama kimoja pekee kinachoitawala, nawapa moyo kwa kuwakumbusha kuwa hata marehemu Rais John Magufuli wa Tanzania alinuia kumaliza upinzani nchini mwake ila akafa kabla. Nia ya kuangamiza upinzani ni tishio la moja kwa moja dhidi ya demokrasia, yaani kuwapokonya wananchi uhuru na manufaa mengineyo yote ambayo wamepigania kwa miaka mingi. Ni sawa na kuwaambia wananchi kwamba hawana thamani, maoni yao kuhusu wanavyotaka kutawaliwa si muhimu, aliye na usemi pekee ni mtawala aliye madarakani, na ana wasaidizi vibaraka ambao wako radhi kumfia bila aibu. Utashi wa watu kujitawala daima hauishi, wanaokufa ni madikteta, na aghalabu vifo vyao husherehekewa kwa kuwa vinaashiria mwanzo mpya ambao, ingawa mfupi au mbaya, ni fursa ya waathiriwa kuutua mzigo mzito, ndiposa wao husherehekea mwanguko wa adui. Demokrasia haifi, madikteta ndio hufa. Magufuli yumo kaburini, Daniel Moi yumo futi sita chini ya ardhi. Mobutu Seseseko hakumbukwi tena na Wakongomani, kasri yake imejiotea magugu ovyo. Iddi Amin Dada alifia chumba cha kupanga kama mtu wa kawaida tu, Uganda haikumpa hata kaburi la kuzikwa. Mshindi ni demokrasia kwani haifi, na demokrasia inaposhinda watu huwa wameshinda. Hiyo ni ithibati kwamba nchi ni ya wananchi pia, mtawala akiringa nayo au kuikalia mguu wa kausha ajue hana tofauti na mkoloni aliyetamba kishenzi ila mwishowe akatuwachia nchi yetu shingo upande. Nusra macho yanitoke nje nilipoona polisi wakimshika mwanahabari na kugongesha kichwa chake kwenye gari wakati wa ghasia za uchaguzi wa Uganda, lakini ghafla nikakumbuka huko ni Uganda, nchi ambayo dola hutumia nguvu kuwanyamazisha wananchi. Unapoona hali ambapo vyombo vya kulinda usalama vinajitwika mzigo wa kumdumisha kiongozi madarakani, basi jua hiyo si nchi bali pori kubwa ambako watu hulana kama wanyama bila maadili yoyote. Ni mfumo uliooza, badala ya kuwafundisha polisi kutekeleza sheria kwa njia ya kisasa wanawafundisha kututumua misuli na kutumia nguvu dhidi ya raia ili waogopwe. Kisa hicho cha mwanahabari kudhulumiwa kilinikumbusha kingine ambapo marubani wa jeshi la Uganda waliokuja Kenya kwa shughuli rasmi walipotelea angani, mwishowe wakaangusha ndege na kufa nazo miaka michache iliyopita. Uchunguzi ulionyesha kuwa lilikuwa na tatizo dogo tu la mawasiliano, yaani marubani wa jeshi la Uganda walishindwa kuelewana na waelekezi wa ndege wa Kenya kwa kuwa Waganda hao walizungumza Kiganda pekee huku Wakenya wakiwazungumzia Kiingereza. Labda utashangaa ilikuwaje kwa sababu tangu hapo tunaamini kwamba Waganda huzungumza Kiingereza kwa ukubwa kwa kuwa ndiyo lugha yao ya taifa. Nakuelewa, lakini nakufahamisha kuwa katika nchi ambapo ujinga husifiwa kuliko werevu, ni rahisi kupata wajinga wengi wa kuingiza kwenye mfumo mbaya unaowadhalilisha watu. Katika mfumo mchafu, werevu na ujasiri wa kuhakiki mambo huchukuliwa kama kilema. Tatizo la kuongozwa na dikteta ni kwamba maovu yake huua wapinzani na wanaomuunga mkono vilevile. Waganda, na Waafrika kwa jumla, wanapaswa kuwa makini sana wanapohusiana na dikteta Yoweri Museveni au mwingine yeyote. Anaua watu katika jaribio lake la kuua demokrasia, sikwambii na unoko wake huo hula kwake pia. Kila ofisa wa usalama, au mtu wa mkono tu anayetumiwa kuwakandamiza wananchi, anapaswa kujua kwamba dikteta haishi milele. Mpambanaji naye aipambanie nchi yake, si yao pekee. -Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika ([email protected])

NIMEKWAMBIA kwa muda sasa kwamba Kenya ni jukwaa kubwa la sarakasi na vituko, likiisha hili linaingia lile, na yote yanatishia kukutegua mbavu. Mara RAO alituacha serikalini hatutoki; mara tochi ya Jirongo imezima na hivyo ikazima washukiwa; mara huyu kagunduliwa havai za ndani, hivyo kampuni ya chupi itamlipa ili aanze kuzivaa na kuzinadi. Hapo ndipo unapouliza: tutajuaje amevaa? Atalipwa kwa saa, siku au mwezi? Na usisahau kuna kichaa cha mbwa… samahani… cha kukumbatia miti, yaani tabia ya kuudhi sana ambapo watu wanaoiga wazo asili la mtu na kulitoa thamani. Basi na ajitokeze jasiri amtomase simba pale Masai Mara, akiponea tumvike taji ya kivutio bora cha watalii. Kwenye siasa, hebu angalia jinsi mwakilishi wa vijana katika ODM, mzee mzima wa karibu miaka tisini, anavyopigana miereka na mpwa wake kijana. Tafakari Oburu Oginga, aliyewahi kuteuliwa mwakilishi wa vijana katika Bunge la Seneti, akipigana na Winnie Odinga, ambaye hajawahi kuwawakilisha vijana popote. Hivi vita havina usawa kabisa, Winnie anaonewa. Haki itatendeka pale Winnie atakapoteuliwa mwakilishi wa wazee kwenye Bunge hilo-hilo, kisha yeye na mjomba wake huyo wajitose kwenye ulingo na kuendelea na miereka. Vinginevyo, Babu Oburu anapaswa kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuongoza ODM kwa sababu tayari amewawakilisha vijana akiwa mzee, na kwa namna fulani aliwawakilisha wazee pia kwa sababu yeye ni mzee. ata hivyo, kwa sababu Waafrika tunawaheshimu wazee, tutaisihi serikali imlipe Oburu mshahara wa miaka mitano ambapo aliwakilisha wazee bila malipo. Atakuwa na bahati kubwa ya kula mara mbili kwa kuwa tayari alikwisha kulipwa huo wa kuwawakilisha vijana. Ama tuseme aende nyumbani mikono mitupu tu kwa sababu alipokuwa anawawakilisha vijana, Babu Owino naye, ambaye ni mshirika wa Winnie, japo kijana, aliwakilisha wazee kwa jina lake tu – Babu. Aliyemdanganya Oburu kwamba anaweza kushinda miereka yoyote dhidi ya vijana machachari – Winnie, Babu na Edwin Sifuna – alimkosea sana. ODM, kama tulivyoimba pambio tukiwa watoto, itajengwa na vijana. Inatabirika kwamba vijana hao watatu, na wengine wengi wanaowaunga mkono, watakuwa kwenye siasa za Kenya kwa muda mrefu. Sijui utabiri wa wazee ving’ang’anizi unasemaje. Eti tochi ya Jirongo kamla nani? Nimeona maprofesa wakisema tusiidharau, eti tusiseme utamaduni ulikuwapo hata kabla ya tochi kuundwa. Lofa wa kawaida angesema hayo ningenyamaza, lakini sharti profesa anieleze tochi ilianza kutumika lini. Na akisema zamani walitumia kaa la moto, basi nitasisitiza turejee huko kwa makaa ili tupate matokeo ya haraka. Kaa la moto huzima upesi ukilifutika kwa udongo. Hebu na tuharakishe mambo. Usipoyacheka mambo haya yatakucheka na kukuhuzunisha, hivyo ni heri uyatangulie. Msongo wa mawazo nchini Kenya ni ugonjwa wa matajiri. -Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika ([email protected])

GHASIA ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika mawanda ya kisiasa zinavunja moyo na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Wikendi, ghasia zilizuka katika Kanisa la Witima, eneobunge la Othaya ambako aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua alikuwa amehudhuria ibada ya kanisa. Picha zilienea mitandaoni zikionyesha jinsi ambavyo wanawake na watoto wadogo walikuwa wamefunikwa na moshi wa vitoza machozi wakitorokea usalama wao. Aidha, picha nyingine zilionyesha jinsi Bw Gachagua na viongozi wengine walivyokuwa wakitorokea usalama wao kwa kutumia vijia vidogo kuhepa magenge. Kumezuka gumzo iwapo ni mrengo wa Bw Gachagua unajiandalia na kujipangia ghasia hizi kisha kulaumu serikali au vinginevyo. Shaka hii inaibuliwa na matamshi ya Bw Gachagua mwenyewe kuwa Mbunge wa Juja George Koimburi alijiteka nyara kuzuia kufika kortini mwaka jana. Bw Gachagua wakati wa ‘masaibu’ ya Bw Koimburi alikuwa amedai kwamba mbunge huyo aliteswa na kikosi cha maafisa wa usalama ‘wauaji’. Alidai hata mbunge huyo alilazimishwa kupumua kemikali hatari ambayo iliathiri sauti yake wala hangeweza kuzungumza, kwa hivyo alikuwa akizungumza kupitia maandishi. Bw Gachagua wakati huo alidai kuwa Rais William Ruto, Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat walikuwa na nia ya kuwaandama wanasiasa wanaoegemea mrengo wake na pia kumzidishia masaibu kwa kumlenga. Kukiri kwamba Bw Koimburi alijiteka nyara ilhali miezi michache tu iliyopita alitoa madai mazito kuwa serikali ilijihusisha na yaliyomfika mbunge huyo kunafanya iwe vigumu kumwamini Bw Gachagua kuhusu fujo zinazokumba mikutano yake. Ingawa hivyo, hoja si nani anajisakia umaarufu au huruma kutokana na visa hivi ila ni taswira inayojitokeza katika jamii. Mikutano ya Bw Gachagua ukanda wa Mlima Kenya imekuwa ikizingirwa na ghasia. Kabla ya tukio la wikendi, vijana waliokuwa wamebeba bakora wakidaiwa kusindikizwa na maafisa wa usalama, walitishia kusambaratisha mkutano wake mjini Nyeri. Pia katika mkutano huo wiki mbili zilizopita, Bw Gachagua alisema kuwa serikali inamwaandama kwa kutumia wahuni katika ngome yake ya kisiasa. Serikali inastahili kuchunguza ghasia zinazoandama mikutano ya Bw Gachagua eneo la Mlima Kenya kufahamu kweli ikizingatiwa sasa imefikia hali hatari. Ni dhahiri kwamba uhasama kati ya Bw Gachagua na viongozi wa eneo la Mlima Kenya wanaoegemea mrengo wa serikali ndio unaleta fujo hizi za kuaibisha. Aliyekuwa naibu rais amekuwa akiwataja baadhi ya wabunge kuwa wanahusika na kuratibu fujo dhidi yake. Madai haya yachunguzwe na ukweli ubainike kwa sababu wanaotumiwa kutibua mikutano ya Bw Gachagua Mlima Kenya ni vijana na maafisa wa usalama. Pia iwapo sasa wanasiasa wanatifuana na uchaguzi umesalia miezi 20 hivi, itakuwa aje kura za 2027 zikikaribia? Bw Gachagua mwenyewe amedai kuwa uvamizi dhidi yake una mipaka kauli ambayo inaweza kufasiriwa kuwa naye huenda pamoja na watu wake wakalazimika kujilinda. Hali ikifikia hivi, wanasiasa watakuwa wakiwatumia vijana kupambana na kando na uharibifu, mauaji yanaweza kutokea pia. Katika haya yote, vijana nao wajihadhari hata kama uchumi ni mgumu kwa sababu hakuna tija kwa kumpigania mwanasiasa ambaye kesho pengine ataungana na huyo adui wake mnayemkabili kwa sasa.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni utekelezaji wa Madini Vision 2030, imewezesha kuanzishwa kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Teknolojia ya Madini pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya utafiti wa kina wa madini. The post Tanzania, Korea kushirikiana teknolojia ya madini first appeared on HabariLeo.

VIONGOZI wa kisiasa wanaohudumu Kaunti ya Taita-Taveta, wamesalia kwenye njiapanda baada ya vyama vilivyowafadhili kuingia mamlakani na kupoteza umaarufu eneo hilo huku vikionekana kuegemea kwa uongozi wa Rais William Ruto. Wanasiasa wengi waliochaguliwa kwa tiketi za chama cha ODM na Wiper, sasa wanaonekana kukimbilia kuidhinishwa na Rais Ruto ili kubakia kwenye viti vyao huku wakazi wakilalamika na kuwalaumu kwa kutotimiza ahadi zao walizotoa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Hili lilidhihirishwa na mashindano yaliyojitokeza wiki mbili zilizopita mtandaoni kila mmoja akitaka kuhusishwa na Rais Ruto alipokuwa anajipanga kuzuru kaunti hiyo licha ya tofauti vya vyama. Viongozi kutoka vyama tofauti na UDA haswa ODM ambao wameonekana kuendelea kupiga siasa bila mwelekeo rasmi katika uchaguzi ujao baada ya kuaga dunia kwa kinara wa chama hicho Raila Odinga, wameonekana wakijipigia debe kuonekana kumuunga mkono Rais Ruto ili kupata baraka za kujitosa uwanjani mwaka ujao. Ikizingatiwa kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2022, Rais Ruto alipata mbunge mmoja wa chama chake cha UDA, (mwakilishi wa wanawake Bi Lydia Haika) wakati huu dalili zaonyesha kuwa ana kazi rahisi kupata uungwaji mkono kwani viongozi hao wameanza mbio za kujitambulisha kwake. Viongozi wa zamani wakiwemo magavana wanaonuia kurudi katika siasa za 2027 pamoja na wanasiasa wanaohudumu wameweka mabango na kupiga kampeni mtandaoni wakimkaribisha kiongozi huyo wa nchi ambaye alitarajiwa kuweka jiwe la msingi wa soko la kisasa eneo la Voi siku ya Ijumaa ambayo hakuhudhuria. Gavana wa kwanza na wa pili wa kaunti hiyo Bw John Mruttu na mwenzake Granton Samboja mtawalia wameonekana wakijihusisha na uongozi wa Bw Ruto huku mwakilishi wa wanawake Bi Haika ambaye alikuwa kiongozi wa UDA katika uchaguzi uliopita eneo hilo naye akionekana kujidai ndiye anayetakiwa kumwalika kiongozi huyo. Viongozi wengine ambao wamejitokeza kualika kiongozi huyo licha ya miaka ya nyuma kuwa katika vyama vilivyompinga Bw Ruto ni pamoja na Mbunge wa Voi Abdi Chome, mwenzake wa Taveta John Bwire na wa Mwatate Peter Shake. "Tunasikitika kuona viongozi wakitaka kuidhinishwa na Rais Ruto kwa kipindi kingine badala ya kututimizia ahadi walizotoa mwaka wa 2022,” alisema Bi Phedes Saru, mkazi wa Voi. Mwishoni mwa mwaka jana katika ziara yake Kaunti ya Taita-Taveta, Rais Ruto alijitenga na kuhusishwa na viongozi ambao wanategemea kuidhinishwa bila kufanyia wakazi kazi na wasio na sera. Aliyekua mwakilishi wa kike wa Taita-Taveta Joyce Lay naye amesisitiza umuhimu wa viongozi kufanya hamasa kwa wapiga kura wafahamu majukumu ya viongozi kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2027. Wakazi wa Taita-Taveta wakiongozwa na viongozi wa makanisa na wanaharakati wa haki za kibinadamu wamekuwa kipaumbele kuhamasisha wakazi na kuchambua utendakazi wa wanasiasa jambo ambalo limewatia tumbo joto viongozi wa kisaisa. Wanasiasa wamekuwa wakikashifiwa kwa unyakuzi wa ardhi ambao umeshughudiwa miaka mitatu iliyopita bila wao kutetea wakazi na badala yake kuegemea upande wa wanyakuzi. Hata hivyo, licha ya kuelekea kuidhinishwa na Rais Ruto, wakazi wanaendelea kushawishi viongozi ambao wanataka kufanya kazi naye kuomba serikali kutekeleza miradi mbalimbali iliyoahidi wakazi wa Taita-Taveta wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita. Rais Ruto aliahidi miradi ya usambazaji wa maji, ujenzi wa barabara, ufufuaji wa reli ya zamani kutoka Voi hadi Taveta, ukamilishaji wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Voi, miongoni mwa ahadi zingine. Miongoni mwa miradi iliyoanzishwa na kukwama ni mradi wa bomba la pili la Mzima, ujenzi wa barabara ya Bura-Mghange-Mbale-Mtomwagodi pamoja na ile ya Taveta-Illasit. Wakati wa ziara yake mwaka jana, Rais aliahidi kuwa mradi wa maji ya Mzima ungeanzishwa kufikia Desemba mwaka wa 2024 lakini mpaka sasa haujang’oa nanga. Vilevile, Rais aliahidi kuwa serikali yake itahakikisha kuwa kaunti hiyo inapata asilimia 50 ya mapato ya hifadhi ya mbuga ya Tsavo.

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amesema hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa wawili kati ya 10 wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ha Sh bilioni 5.7 kwa njia za udanganyifu. The post Wawili waachiwa kesi uhujumu bil 5.7/- first appeared on HabariLeo.

GAVANA wa Nyamira Amos Nyaribo anaendelea kuandamwa na changamoto mpya baada ya Wizara ya Fedha kuzima utawala wake dhidi ya kutekeleza mradi wa tabianchi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Wizara ya Fedha imechukua hatua hiyo kutokana na madai ya ufujaji wa fedha. Katika barua iliyoandikwa mnamo Desemba 15, 2025 Wizara ya Fedha imezima kaunti kutekeleza mpango huo almaarufu kama FLLoCA kwa sababu ya ubadhirifu wa Sh22 milioni. Kusitishwa kwa mpango huo ni pigo kwa Gavana Nyaribo na kunatokea wiki chache baada ya kunusurika kutimuliwa na Bunge la Seneti. Pia anaandamwa na madai ya kushiriki ufisadi huku akichunguzwa na Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi Nchini (EACC). Waziri wa Fedha John Mbadi alisema kuwa wachunguzi kutoka Benki ya Dunia waligundua ubadhirifu mkubwa wa pesa katika Kaunti ya Nyamira. Barua hiyo ilinakiliwa pia kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Magavana Nchini (COG) Mary Mwiti. Uchunguzi “Benki ya Dunia iliwatuma mawakala wake na wakafanya uchunguzi ambao ulifichua ubadhirifu mkubwa wa fedha. Suala hili limeibua mtihani wa uwazi katika matumizi ya fedha kwenye miradi mbalimbali,” ikasema barua hiyo. Barua hiyo ilikuwa inasema kuwa pesa zilikuwa zikitumika kiholela na rasilimali nyingine zimekuwa zikitumika kwa njia isiyokusudiwa. “Kutokana na hili, kaunti hii imezuiwa dhidi ya kuendelea na mradi wa FLLoCA hadi masuala yaliyoibuliwa yalainishwe na Benki ya Dunia itume barua kwa Hazina Kuu ya Fedha,” ikasema barua hiyo. Bw Nyaribo hata hivyo alipuuza madai kuwa pesa za ufadhili wa mradi huo zimeliwa badala ya kutumika katika miradi ya maendeleo. “Watu wengine wanasema pesa zimepotea, acheni siasa hakuna pesa zilizopotea. Hata sumuni haijapotea,” akasema Bw Nyaribo akihutubu kwenye eneobunge la Borabu. Aliahidi kuwa utawala wake utatoa ufafanuzi, akisema ukweli utajulikana. Bw Nyaribo aliapa kuwa utawala wake utaendelea kutekeleza miradi yake akisema kuwa anamakinikia kuyabadilisha maisha ya wakazi wa Nyamira. “Katika miezi michache inayokuja tutasambaza maji kutoka kwa visima Wadi ya Esise. Kituo cha afya cha Isoge kitamalizika mnamo Desemba mwaka huu na pia tutafungua barabara nyingi maishani,” akasema.

ZANIZIBAR: THE Central Committee of the National Executive Committee (NEC) of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) has made several appointments of party leadership candidates drawn from the Parliament of the United Republic of Tanzania and the House of Representatives. According to a statement issued by the CCM Secretary for Ideology, Publicity and Training, Mr … The post CCM makes key appointments from Parliament first appeared on Daily News.

SERIKALI imesema imeimarisha huduma za msaada wa saikolojia na unasihi katika siku 100 za uongozi wa kipindi cha pili cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima watu 171,529 wamehudumiwa ikiwa ni hatua za kuimarisha ustawi wa jamii. The post Maelfu wapata msaada saikolojia siku 100 first appeared on HabariLeo.

MOROGORO: MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani amewashauri wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kwa ajili ya kujenga afya zao ili waepukane kupatwa na maradhi yanayosababishwa na lishe duni . Kombani amesema hayo kwenye mada yake wakati wa kongamano la University ladies and Gentleman 2026 lililoandaliwa na … The post Wanafunzi vyuo vikuu washauriwa lishe bora first appeared on HabariLeo.

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu imepokea Sh bilioni 10.5 kwa ajili ya kutoa mikopo ya masharti nafuu na imeshatoa Sh bilioni 1.3 kwa wafanyabiashara 588. Pia, imesema serikali imesajili wafanyabiashara ndogondogo 119,595 kupitia mfumo wa usimamizi na usajili wa wafanyabiashara ndogondogo (WBMMIS). The post Neema biashara za wananchi first appeared on HabariLeo.

NAIBU Mkuu wa Wafanyakazi Ikulu na Mkuu wa Utekelezaji Miradi ya Serikali katika Afisi ya Rais Eliud Owalo amejiuzulu. Katika chapisho kwenye kurasa zake za mitandaoni, Bw Owalo ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Rais William Ruto kutoka Nyanza anasema anataka kuwania urais, na kwa sababu hiyo, haingewezekana kwake yeye kuendelea kushikilia wadhifa huo. Bw Owalo ni naibu wa Mkuu wa Wafanyakazi katika Afisi ya Rais Felix Koskei na ni mmoja wa wanasiasa kutoka Nyanza walioanza kufanya kazi na Rais Ruto mapema mno, hata kabla ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kushirikiana na Rais kuunda Serikali Jumuishi. Kujiuzulu huku kunatarajiwa kuibua hisia mseto hasa kuhusiana na muda ambao hatua hii inajiri, na hatima ya uhusiano wake na Rais Ruto na serikali yake.