
RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI
RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI #globaltv #raissamiasuluhuhassan #selfie
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI #globaltv #raissamiasuluhuhassan #selfie

IBADA ya mazishi ya marehemu Mchungaji Silvanus Mwakoma katika eneo la Kirutai, Voi, iligeuka kuwa uwanja wa malumbano ya kisiasa baada ya Mbunge wa Taveta John Bwire na Askofu Mkuu Liverson Mng’oda kutofautiana kuhusu mchango wa Rais William Ruto kwa familia ya marehemu. Katika hotuba yake, mbunge huyo alimsifu marehemu kama mfuasi wa Rais Ruto na serikali yake. Alitaja miradi kadhaa ya serikali katika kaunti hiyo, akisema Rais Ruto amekuwa akichangia maendeleo ya Taita-Taveta. Bwire pia alitangaza mchango wa Sh500,000 kutoka kwa Rais Ruto, huku yeye mwenyewe akitoa Sh100,000. Hata hivyo, wakati wa mahubiri, Askofu Mng’oda alikosoa vikali kauli hizo, hasa kuhusu maendeleo ya serikali katika eneo hilo. Askofu huyo alilalamikia hali ya barabara na ukosefu wa maji, akipinga picha ya maendeleo iliyokuwa imewasilishwa na mwanasiasa huyo. Pia alikosoa namna mchango huo ulivyotangazwa, akidai ulitolewa kwa mtindo wa majivuno na madai ya kustahili sifa. Katika kauli iliyowashangaza waombolezaji, Mng’oda aliishauri familia kutotumia fedha hizo kusomesha watoto wa marehemu na hata kupendekeza zirudishwe ikiwa ingewezekana. Lakini familia haikuunga mkono msimamo huo. Katika hotuba ya shukrani, ndugu wa marehemu aliishukuru serikali kwa mchango wa Sh500,000 na Bwire kwa Sh100,000. Alisema fedha hizo zitatumika kuwasaidia watoto wa marehemu. Malumbano hayo yalifanya mazishi hayo kugeuka kutoka hafla ya kuaga marehemu hadi mjadala kuhusu siasa, maendeleo na matumizi ya mchango wa Sh600,000.

SENETI imewasilisha rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwamba maseneta walikiuka haki ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ya kusikilizwa kwa haki wakati wa mchakato wa kumtimua mamlakani. Seneti pia inapinga fidia ya Sh50 milioni ambayo Mahakama Kuu ilimpa Gachagua kwa ukiukaji huo wa haki zake. Rufaa hiyo iliwasilishwa mwezi mmoja baada ya Gachagua mwenyewe kukata rufaa kupinga sehemu kubwa ya uamuzi wa Mahakama Kuu, ikiwemo uamuzi uliothibitisha kutimuliwa kwake na kuidhinisha Profesa Kithure Kindiki kuwa mrithi wake. Hata hivyo, Gachagua hakupinga sehemu ya uamuzi iliyosema haki zake zilikiukwa wala fidia ya Sh50 milioni. Seneti, kupitia Spika wake na Seneti yenyewe, inalenga kubatilisha sehemu za uamuzi wa Juni 8 zilizowalaumu maseneta kwa kukataa ombi la kuahirishwa kwa kikao cha mchakato wa kumtimua Gachagua na kuamuru alipwe fidia. Katika hati yake ya rufaa, Seneti inataka Mahakama ya Rufaa ibatilishe au ibadilishe maagizo hayo pamoja na kuamuru gharama ya kesi ilipwe. Seneti inasema majaji walikosea walipoamua kwamba uamuzi wake wa kukataa kuahirisha mchakato huo ulikiuka haki ya Gachagua ya kusikilizwa kwa haki. Inasema majaji hawakutathmini ipasavyo masharti ya Katiba katika Ibara ya 47 na 50 na hawakutambua kwamba Seneti ilitumia mamlaka yake ya kufanya uamuzi kuhusu ombi hilo. Seneti pia inasema majaji walikosea baada ya kukiri kwamba Gachagua alipewa nafasi ya kujitetea, lakini baadaye akawalaumu maseneta kwa kuendelea na mchakato huo baada ya yeye kutofika. Kwa mujibu wa Seneti, Gachagua alipewa muda zaidi kwa ombi la mawakili wake na Bunge lilikuwa na wajibu wa kukamilisha mchakato wa kumtimua bila kuchelewa. Seneti pia inawashutumu majaji kwa “kunyakua mamlaka ya kufanya uamuzi” ya Seneti na kutumia tathmini yao wenyewe kuamua iwapo ombi la kuahirisha kikao lilipaswa kukubaliwa. Hati hiyo inasema ombi la kuahirisha mchakato liliwasilishwa kwa kura na likakataliwa baada ya maseneta kuzingatia mazingira yaliyokuwepo wakati huo. Seneti pia inapinga uamuzi kwamba kutokuwepo kwa Gachagua kulihalalishwa na ugonjwa. Inasema hakuna ushahidi uliowasilishwa mbele yake wakati huo kuthibitisha kwamba alikuwa mgonjwa. “Majaji walikosea kisheria na kimantiki walipoamua kwamba kutokuwepo kwa Gachagua kulihalalishwa kwa sababu ya ugonjwa, licha ya kwamba hakuna ushahidi uliowasilishwa mbele ya Seneti wakati huo kuthibitisha ugonjwa huo uliodaiwa,” inasema rufaa hiyo. Seneti sasa inataka Mahakama ya Rufaa ibatilishe uamuzi kwamba haki za Gachagua za kusikilizwa kwa haki zilikiukwa na pia iondoe agizo la kulipa Sh50 milioni. Mzozo huo ulitokana na mchakato wa kumtimua Gachagua uliofanyika Oktoba 2024 baada ya Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse kuwasilisha hoja iliyokuwa na malalamishi 11 dhidi yake. Bunge la Kitaifa liliidhinisha hoja hiyo na kuiwasilisha Seneti, ambayo ilithibitisha mashtaka matano kabla ya kumwondoa Gachagua afisini. Gachagua na watu wengine baadaye walipinga mchakato huo, wakidai kwamba haukuhusisha ushiriki wa kutosha wa umma, kulikuwa na upendeleo, taratibu za Bunge zilikiuka Katiba na haki zake zilikiukwa. Mahakama Kuu ilikataa malalamishi yao mengi na kuthibitisha kutimuliwa kwake, pamoja na uteuzi na kuidhinishwa kwa Profesa Kindiki kuwa Naibu Rais. Hata hivyo, majaji walipata kasoro katika namna Seneti ilivyoshughulikia utetezi wa Gachagua. Walibaini kuwa Seneti iliendelea na mchakato huo baada ya Gachagua kuugua kabla hajatoa ushahidi mwenyewe.

For the newlyweds, the real ceremony begins after the celebration - with rent, food, electricity, healthcare, transportation, employment and, eventually, cost of raising children

ZANZIBAR; Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, Agosti 14, 2026, amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, Cheti cha shukrani kwa kutambua ushiriki na mchango wa NSSF katika Tamasha la Kizimkazi 2026. Cheti hicho ni ishara ya kutambua mchango wa NSSF katika kuunga mkono juhudi za Serikali…

DODOMA: THE government has secured 10 additional overseas scholarships for high-performing Form Six science students, raising to 60 the number of Tanzanian students set to pursue undergraduate studies abroad under the Samia Scholarship Extended Programme. The opportunities were secured through Russia’s Peoples’ Friendship University (RUDN) following President Samia Suluhu Hassan’s visit to Russia in June,…

“My parents are late. I dream of getting married and raising my own family. I am now 45 and I struggled hard to go to university"

KWA miezi mitano ijayo, maeneo ya Magharibi mwa Kenya yataingia katika msimu wa tohara za kitamaduni, huku wanaume wanaotekeleza jukumu hilo wakijitenga na maisha ya kawaida na kufuata kanuni kali. Wanaume hao wanaojulikana kama Ngariba kwa Kiswahili, na Omukhebi kwa lugha ya Bukusu, huamini kwamba tohara ni ibada muhimu ya kumfanya mvulana aingie katika utu uzima. Katika kipindi hicho, maisha yao hutawaliwa na nidhamu, kujinyima na uwajibikaji mkubwa. Hakuna kufanya ngono. Hakuna kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya. Hakuna kunywa pombe. Hakuna kuhudhuria mazishi. Na zaidi ya yote, hawapaswi kukiuka kanuni zinazohusiana na kisu kitakatifu kinachojulikana kama Lukhembe. Wanaotekeleza tohara hiyo wanaamini kwamba kuvunja kanuni hizo kunaweza kuathiri mchakato wa tohara na uponaji. Siminu Wekesa, aliye na tajriba kuhusu tohara, anasema marufuku hayo yanalenga kulinda heshima ya kiroho ya tohara, maadili ya jamii na usalama wa wavulana wanaopitia desturi hiyo. “Katika kipindi tunachowashughulikia wavulana katika tohara, haturuhusiwi kushiriki ngono hadi wavulana waanze kupona mwezi Oktoba kwa sababu ni kama kwenda vitani. Ukirejea au kuvunja kanuni hii, itachukua muda mrefu kwa watoto kupona kama inavyotarajiwa,” anasema Bw Wekesa. Marufuku ya ngono pia inawahusu wanaume wanaoshughulikia Busaa, kinywaji cha kienyeji ambacho hutumika katika sherehe za kitamaduni. Kifo pia kinaweza kumlazimisha Omukhebi kujiondoa katika shughuli hizo. Ngariba anayefiwa na mtu wa karibu wa familia, hasa mke, anatarajiwa kusitisha shughuli hizo na kufanyiwa tambiko la kujitakasa kabla ya kurejea mwaka unaofuata. Uvutaji sigara na matumizi ya dawa nyingine za kulevya pia hauruhusiwi wakati wa msimu huo. Wapashaji tohara wanasema baadhi ya masharti hayo yanalenga pia kuwalinda wavulana dhidi ya maambukizi na matatizo mengine ya kiafya. Rajab Kituyi, aliyeanza kupasha tohara mwaka wa 1982, anasema pombe hairuhusiwi kwa sababu shughuli hiyo inahitaji mikono thabiti, umakini na uwezo mzuri wa kuona. “Haturuhusiwi kunywa pombe, ili kuepuka matitizo ya kuona au kushindwa kushikilia kisu vizuri wakati wa tohara,” anasema. Omukhebi anatarajiwa kufanya kazi hiyo kwa usahihi mkubwa. Tohara isiyofanyika vizuri inaweza kumletea aibu na unyanyapaa Ngariba pamoja na mvulana, huku imani za kitamaduni pia zikihusisha makosa hayo na madhara ya kiroho. Kanuni hizo pia zinahusu uhusiano kati ya vizazi vya watoa tohara. Marufuku hiyo inalenga kuhifadhi heshima na uhusiano kati ya vizazi vya ngariba. Kisha kuna Lukhembe, kisu kitakatifu kinachotumiwa katika tohara. Kwa mujibu wa Bw Wekesa, kukiangusha kisu hicho, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi, ni ukiukaji mkubwa wa kanuni. Ngariba anapaswa kusitisha shughuli mara moja na kusubiri msimu unaofuata. “Ukiangusha kisu, sitisha shughuli zako hadi msimu unaofuata. Ukipuuza na kuendelea na tohara, utaleta aina fulani ya mkosi,” anasema. Ngariba anapaswa kuondoka kimya kimya na kuepuka kueleza yaliyotokea njiani kuelekea nyumbani. Bw Wekesa anasema akiulizwa maswali, anapaswa kujibu neno moja pekee, “Ahoro”. Ngariba pia wanatarajiwa kuwa watu wenye maadili mema, wenye nidhamu na wanaoweza kuwa mifano kwa jamii. Pia hawapaswi kuwa na historia ya uhalifu. Kwa jamii ya Bukusu, tabia ya mtu anayemshughulikia mvulana inaweza kuathiri namna anavyoingia utu uzima. Hasira, ugomvi na mabishano pia hayaruhusiwi. Wakati wa msimu wa tohara, watoa tohara wanatarajiwa kubaki watulivu hata wanapochokozwa. Pamoja na kanuni hizo za kitamaduni, kuna umuhimu wa usafi na viwango vya kisasa vya usalama. Bw Wekesa, ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wapashaji Tohara Kaunti ya Bungoma, anasema wazazi wanapaswa kuhakikisha mtu anayefanya tohara amepata mafunzo na cheti kutoka serikalini. “Usafi si jambo la kujadiliwa wakati wa tohara. Walioidhinishwa pekee ndio wanaoruhusiwa kufanya shughuli hiyo, na yeyote anayefanya bila cheti atachukuliwa hatua za kisheria,” anasema. Ngariba wanapaswa kudumisha usafi wa mwili, kukata kucha ziwe fupi, kuvaa vizuri na kuhakikisha mazingira pamoja na vifaa vinavyotumiwa ni safi.

ALIYEKUWA Waziri wa Jinsia, Aisha Jumwa amejiunga rasmi na chama cha Wiper Patriotic Front, akisema yuko tayari kukabiliana na vyama vinavyounga mkono serikali jumuishi katika uchaguzi wa 2027. Bi Jumwa alipokelewa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka katika eneo la Kakuyuni, Kilifi, ambapo aliahidi kufanya kampeni za kuimarisha upinzani Pwani na nchini. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza nguvu za Wiper katika eneo la Pwani, huku Bi Jumwa akihusishwa na mipango ya kuwania kiti cha ugavana wa Kilifi mwaka wa 2027. Bw Musyoka alimkaribisha Bi Jumwa na kuahidi kumuunga mkono katika kinyang’anyiro hicho. Kalonzo alisema kujiunga kwa Bi Jumwa kutaimarisha upinzani katika eneo la Pwani. Bi Jumwa alisema wakazi wa Kilifi wamechoshwa na siasa za serikali jumuishi na wanapaswa kuunga mkono upinzani. “Hakuna tena serikali jumuishi katika Kaunti ya Kilifi kwa sababu wao ni wasaliti,” alisema. Alisema atashirikiana na Wiper kuipaka Pwani “rangi ya samawati” kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Musyoka aliwaonya viongozi wa upinzani dhidi ya kuvunja muungano wao na kujiunga na Serikali ya Kenya Kwanza, akisema hatua hiyo itakuwa usaliti kwa Wakenya wanaotaka mabadiliko katika uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka alisema viongozi wa upinzani lazima wabaki pamoja na kuweka kando maslahi yao binafsi wanapojenga muungano wenye nguvu wa kumkabili Rais William Ruto. Aliwafananisha viongozi watakaoacha muungano huo na mke wa Lutu katika Biblia, ambaye aligeuka kuwa nguzo ya chumvi baada ya kugeuka nyuma licha ya kuonywa. “Wenzangu katika upinzani... tukikubaliana na kuungana, na mmoja wetu aamue kurudi nyuma, atageuka kuwa chumvi,” alisema Kalonzo huko Kakuyuni, Kilifi. Kalonzo alisema upinzani unahitaji kuimarisha ushawishi wake Pwani na nchini kote ili kuondoa serikali ya Kenya Kwanza madarakani. Alisema vijana waliofikisha miaka 18 wanapaswa kupata vitambulisho na kujisajili kama wapiga kura katika zoezi la usajili wa watu wengi litakalofanyika Novemba.

WALIANZA maisha yao ya ndoa saa 10 jioni Agosti 9, 2026, lakini kufikia saa moja na nusu usiku siku hiyo wote walikuwa wamefariki. Patrick Mwangi, 28, na Jackline Wambui, 25, walikuwa wameanza maisha yao ya ndoa katika Kijiji cha Nyerere, Murang’a, lakini ikawa ndoa ya muda mfupi zaidi kuwahi kushuhudiwa na baadhi ya wakazi. Polisi wanachunguza vifo hivyo, ambavyo mwanzoni vilionekana kuwa mauaji yaliyotekelezwa na mmoja wao kisha akajiua. Inadaiwa Mwangi alimnyonga Wambui kwa kamba alipokuwa amelala, kabla ya kutoka nje ya nyumba iliyokuwa imekusudiwa kuwa makazi yao mapya na kujinyonga. Wapenzi hao walikuwa wamechumbiana kwa takriban miaka mitatu, kipindi kilichojaa migogoro kiasi kwamba wazazi wao walilazimika kuingilia kati mara kadhaa kuwapatanisha. Mwangi alikuwa mwendesha bodaboda, huku Wambui akifanya kazi za vibarua mara kwa mara. Mama ya Mwangi, Bilha Wangare, alisema bado hawezi kuelewa uhusiano wa wawili hao. “Ulikuwa upendo ulioonekana kama uchawi. Wote walikuwa na mapenzi makali ambayo ilikuwa vigumu kuelewa. Nilishiriki katika mikutano mingi ya kuwapatanisha ili wasameheane. Nadhani neno linalowafaa ni wapenzi wapumbavu,” alisema. Kwa mujibu wake, waligombana kwa sababu ya mambo mbalimbali, ikiwemo simu, pesa na burudani. Wambui aliwahi kulalamika kwamba Mwangi hakumpeleka kujivinjari mara kwa mara kama alivyotaka. Mwangi naye alimshutumu kwa kuiba Sh100,000 kutoka kwake. Wambui pia alilalamika kwamba Mwangi alikuwa akiwasaidia wazazi wake kifedha kupita kiasi, akitaka familia yake ipewe kipaumbele. Mwaka huu, alianza kumtaka Mwangi amkabidhi cheti cha umiliki cha pikipiki yake na hati miliki ya shamba la ekari 0.1 alilonunua Makuyu, Maragua. Wakati huo hawakuwa wakiishi pamoja, lakini mara kwa mara Wambui angelala katika nyumba ndogo ya Mwangi. Katika juhudi za kuwapatanisha, Bi Wangare aliwaita kwenye kikao Agosti 4 na kupendekeza waanze kuishi pamoja. Mwangi alitaka Wambui kwanza azae mtoto wake, huku Wambui akitaka cheti cha pikipiki na hati ya kumiliki shamba. Hatimaye walikubaliana kwamba Mwangi angemfungulia biashara katika soko la Irembu, naye akakubali kwamba angepata mimba haraka iwezekanavyo. Baada ya Wambui kuondoka, Mwangi alimkabidhi mama yake hati hizo akisema hamwamini. Mnamo Agosti 6, Wambui alimpigia simu Bi Wangare na kumwambia alikuwa ameamua kuolewa na Mwangi na angehamia kwake Agosti 9. Saa 10 jioni siku hiyo, Wambui alifika na kumkuta Mwangi akimsubiri. Baada ya muda mfupi, Mwangi alimbeba kwa kwenye pikipiki na wakaondoka. Walirejea karibu saa moja jioni. Bi Wangare alisema Wambui alionekana mchovu, mwenye usingizi na kama aliyelewa. Muda mfupi baadaye, Mwangi aliingia nyumbani kwa wazazi wake na kuzungumza nao. Alisalimia kila mmoja na kuwaaga. Kabla ya kuondoka, alimwambia mama yake kwamba Wambui alikuwa ameweka picha ya mwanaume mwingine kwenye mitandao ya kijamii na pia kumtumia picha hiyo. Alidai Wambui alikuwa amemwambia kwamba asipomtunza vizuri, angemwacha aende kwa mwanaume huyo. Baada ya Mwangi kuondoka, Bi Wangare alisema alipata hisia za ajabu. Alichukua tochi na kumtafuta mwanawe.Alimwita Wambui pia, lakini hakukuwa na jibu. Mlango wa nyumba ya Mwangi ulikuwa wazi. Alimulika nyuma ya nyumba na kumwona mwanawe akiwa amejinyonga. Alipiga mayowe, na mumewe Samuel Kimani pamoja na majirani wakafika. Walipoingia ndani ya nyumba, walimkuta Wambui pia amefariki. Miili hiyo ilipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Maragua Level Four. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Murang’a Cleti Kimaiyo alisema vifo hivyo vinachunguzwa, ingawa kwa mtazamo wa awali vilionekana kuwa mauaji yaliyofuatwa na kujiua. Alisema polisi wako tayari kufuatilia mwelekeo mwingine iwapo ushahidi mpya utaibuka. Shangazi ya Wambui, Tabitha Njoki, alisema kifo hicho kimeacha familia katika mshangao. Wambui alikuwa mama wa mtoto wa kike wa miaka mitano. “Aliniambia kwamba alikuwa akihamia( kwa Mwangi) kuolewa. Sikujua kwamba angekuwa katika ndoa kwa zaidi ya saa tatu tu. Mungu atuhurumie,” alisema.

ARUSHA: Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya, amewataka wananchi wa Monduli na Simanjiro kufafanua kwa kina namna na wakati mwekezaji wa Maasai Stepple Conservancy Ltd alivyopatiwa Shamba Na. 24 lenye ukubwa wa hekta 3,425, ili kupata msingi wa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa takribani miaka 15. Mmuya alitoa kauli…

DODOMA: WIZARA ya Viwanda na Biashara imeeleza kuwa inaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija, hatua inayolenga kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050. Imeelezwa kuwa Serikali inaweka mazingira yatakayomwezesha Mtanzania kuongeza faida katika shughuli zake za uzalishaji kwa kuhakikisha anapata miundombinu, nishati, taarifa…

KAUNTI za Mandera, Wajir na Garissa zilishuhudia ongezeko la mashambulizi ya kigaidi mwezi Julai, hali ambayo imewalazimu maafisa wa usalama kutafuta mikakati mipya ya kukabiliana na tishio hilo. Mandera iliongoza kwa kuripoti visa tisa, ikifuatiwa na Garissa ikiwa na visa vinne na Wajir viwili, kwa mujibu wa ripoti ya kijasusi iliyosambazwa kwa maafisa wa usalama katika eneo hilo. Shambulio la hivi majuzi lilitokea Alhamisi usiku ambapo watu 10 walinusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi katika barabara ya Takaba-Wargadud-Elwak, Mandera. Tukio hilo lilitokea karibu na kijiji cha Odole saa 12 jioni. Walionusurika walikimbizwa katika Hospitali Ndogo ya Elwak baada ya kujeruhiwa. Mmoja wa manusura alisema walikuwa wakijadili masuala ya siasa za Mandera wakati mlipuko ulipotokea. “Ndani ya sekunde chache kulikuwa kimya. Niligundua damu ikitiririka usoni. Nilikuwa nimekatwa vibaya usoni,” alisema. Naibu Kamishna wa Kaunti ya Mandera Kusini, Tobias Otunga alithibitisha tukio hilo na kusema uchunguzi umeanzishwa. Afisa mmoja mkuu wa usalama alisema kumekuwa na ongezeko la watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Al-Shabaab kuingia katika jamii za eneo hilo. “Ujasusi wetu umeonyesha kiwango kikubwa cha wapiganaji hao kupenyeza katika jamii zetu. Hili bado ni tishio kubwa kwa usalama wetu,” alisema afisa huyo. Ripoti za kijasusi za Julai 31 zilionyesha kuwa wafugaji wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya na Somalia waliona watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito. Wafugaji hao waliwaambia maafisa wa usalama kuwa wapiganaji hao walikuwa wameanzisha kambi za muda karibu na mpaka na kuwaonya wakazi wasikaribie maeneo hayo. Mnamo Julai 28, washukiwa wa Al-Shabaab waliwavizia maafisa wa usalama waliokuwa katika doria eneo la Quraqura-Wante, Mandera, na kuwaua maafisa watano. Wanne kati ya waliouawa walitoka Kikosi Maalumu cha Operesheni huku mwingine akiwa polisi wa akiba. Kilipuzi kingine kilicholenga kikosi cha maafisa waliokuwa wakija kutoa msaada kililipuka na kuharibu gari la polisi. Shirika la Armed Conflict Location and Event Data (ACLED) limesema ongezeko hilo ni sehemu ya wimbi pana la mashambulizi ya Al-Shabaab katika kaunti za Kaskazini Mashariki na Lamu. ACLED ilirekodi visa 25 vikiwemo vilipuzi viwili vilivyodhibitiwa katika Mandera, Garissa, Wajir na Lamu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Shirika hilo limesema baadhi ya wapiganaji hao wanakimbilia upande wa Kenya kutokana na operesheni kali za kijeshi nchini Somalia. Maafisa wa usalama pia wamehusisha ongezeko hilo na mpaka usio na ulinzi wa kutosha, uajiri wa vijana katika makundi ya kigaidi na mapigano yanayoendelea upande wa Somalia. MCA wa Garissa Hajir Dahiye ameitaka serikali kupitia upya sera yake kuhusu Jubaland, akisema usalama wa Garissa hauwezi kutenganishwa na hali ya usalama katika eneo hilo la Somalia. Mnamo Julai 26, washukiwa wa Al-Shabaab walivamia kijiji cha Abakaile, Dadaab, na kuharibu mnara wa mawasiliano. Hakuna aliyejeruhiwa katika shambulio hilo. Julai 17, washukiwa hao walifanya mashambulizi yaliyofuatana katika miji ya Fino na Arabia, Mandera, na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi. Barabara ya Elwak-Lafey-Mandera imekuwa imefungwa kwa umma tangu 2015 kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara na milipuko ya vilipuzi. Maafisa wa usalama pia wameonya kuhusu ushirikiano wa baadhi ya wenyeji na wanamgambo hao kwa kuwapa taarifa kuhusu mienendo ya maafisa wa usalama na vituo vya polisi. Mkazi wa Wajir Hassan Abdullahi alisema ukosefu wa ajira na ujinga miongoni mwa vijana unawafanya kuwa rahisi kuajiriwa na makundi ya kigaidi. “Tunahitaji mpango wa kuwafikia wananchi kutoka mashinani hadi kitaifa ili kuwaelimisha vijana kuhusu hatari za ugaidi,” alisema.

WANAHARAKATI wa haki za binadamu na wanaotetea wafanyabiashara wa ngono wameonya kuhusu ongezeko la mauaji ya wanawake Eldoret baada ya wanawake wawili kuuawa katika visa viwili tofauti ndani ya siku tano. Visa hivyo vimeibua wasiwasi kuhusu usalama katika nyumba za kulala ambazo wakazi wanasema zimegeuka kuwa maeneo hatari kwa uhalifu. Kisa cha hivi majuzi kilitokea Alhamisi asubuhi katika mtaa wa Kipkaren ambapo mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 26 ulipatikana umefungwa kwenye gunia na kutupwa katika nyumba ya kupanga baada ya waliokuwa wakiishi humo kutoroka. Siku chache kabla ya hapo, mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 38, aliyetambuliwa na wenzake kwa jina la Zeddy, ulipatikana katika nyumba ya gesti eneo la Juakali, kando ya barabara kuu ya Eldoret-Webuye. Mauaji hayo yameongeza hofu miongoni mwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono, huku mashirika ya haki yakisema yanaweza kuwa sehemu ya mtindo unaoibuka wa mauaji yanayowalenga wanawake walio katika mazingira hatari. Wakazi wanasema baadhi ya nyumba hizo za kulala wageni hazina rejista za wageni, kamera za usalama wala mifumo madhubuti ya kudhibiti wanaoingia na kutoka. Kiongozi wa Nyumba Kumi eneo hilo, Solomon Musumi, alisema Zeddy alikuwa akiishi katika mojawapo ya vyumba hivyo. Alisema Jumatatu usiku alipokea mwanaume aliyedhaniwa kuwa mteja, kabla ya wanawake waliokuwa katika vyumba vya jirani kugundua mwili wake asubuhi iliyofuata. “Eneo hili haliwezi kuendelea kuwa maficho ya wauaji. Nyumba hizi hazina rejista za wageni wala kamera za usalama, na hivyo kuwa mitego ya kifo,” alisema Musumi. Polisi wamethibitisha wameanzisha uchunguzi kuhusu visa hivyo. Kamanda wa Polisi kaunti ndogo ya Kapseret Zaphaniah Kamren alisema washukiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya Kipkaren. “Tunaahidi umma kuwa hatutakoma hadi waliohusika na vitendo hivi vya kinyama wakabiliwe na sheria,” alisema. Kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi wa Turbo Patrick Wekesa alisema uchunguzi kuhusu kifo cha Zeddy unaendelea.

WAPELELEZI wametaja Konstebo wa Polisi Elijah Kibelion Kimoi kuwa ndiye aliyempiga risasi na kumuua Daktari Victoria Mutiso katika shambulizi la kikatili lililotokea wiki iliyopita. Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) ilisema Ijumaa kuwa Kimoi, ambaye tayari amekamatwa, alitumia bastola ya polisi kumuua Dkt Mutiso. DCI pia ilimtaja raia Daniel Mwangi Njoroge kuwa mmoja wa waliopanga mauaji hayo. Kulingana na DCI, Njoroge aliajiriwa na mwanasiasa Rose Mbithe Mulwa na mwanawe Christopher Mulwa kwa lengo la kumuua Dkt Mutiso. Inadaiwa mauaji hayo yalitokana na mzozo wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu ardhi ya ukubwa wa ekari 20 huko Mlolongo, Machakos. Bi Mulwa amekuwa akizozania ardhi hiyo na aliyekuwa mumewe, Dkt David Musyimi Ndetei, pamoja na mkewe Dkt Mutiso tangu 2001. Mkuu wa DCI Mohamed Amin alisema Njoroge alikodi magari mawili aina ya Toyota Prado kutekeleza mauaji hayo. Alisema Njoroge pia alishirikiana na mhudumu wa bodaboda Kelvin Ngugi Kinuthia, ambaye anadaiwa kumsafirisha Kimoi hadi eneo la tukio na baadaye kumtorosha. Dkt Mutiso alikuwa akisafiri katika teksi ya Uber iliyokuwa ikiendeshwa na Victor Job Chunguli mnamo Julai 29. Walipofika eneo la Mawensi, Upper Hill, Nairobi, Toyota Prado nyeusi ilizuia teksi hiyo.Pikipiki pia ilisimama karibu nao. Mtu aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma cha pikipiki alifyatua risasi kadhaa kuelekea Dkt Mutiso kabla ya pikipiki na Prado kutoroka. Bw Chunguli alimpeleka Dkt Mutiso katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, lakini akatangazwa kuwa amefariki alipowasili. Bw Amin alisema baada ya kuwahoji Njoroge na Kinuthia, wawili hao waliwapeleka wapelelezi kwa maafisa watatu wa polisi. Walitajwa kuwa Inspekta Kenneth Kipkemboi Sang, Konstebo Elijah Kibelion Kimoi na Konstebo Collins Kiplangat Bett. Kimoi amekamatwa huku Sang na Bett wakitoroka na wanaendelea kusakwa na polisi . “Kushiriki kwa maafisa hawa ni usaliti mkubwa kwa sare ya polisi na imani ambayo umma umeweka kwao. Lazima wachukuliwe hatua,” alisema Bw Amin. Bw Amin pia alisema bastola iliyotumiwa kumuua Dkt Mutiso ilikuwa ya polisi na ilikuwa imewekwa katika kituo kidogo cha polisi cha Nderi, chini ya Kituo cha Polisi cha Kikuyu. Wapelelezi walipokagua sanduku la kuhifadhia silaha katika kituo hicho, walipata bastola aina ya Mini Jericho yenye nambari KP47302127 pamoja na magazini iliyokuwa na risasi 12 za milimita tisa. Ukaguzi wa rejista ya utoaji wa silaha ulionyesha kuwa bastola hiyo ilikuwa imetolewa kwa Inspekta Sang. Silaha hiyo ilipelekwa katika maabara ya uchunguzi wa kisayansi ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa uchunguzi wa risasi. Kulingana na DCI, uchunguzi ulithibitisha kuwa bastola hiyo ndiyo iliyotumiwa katika kumuua Dkt Mutiso. Maganda ya risasi yaliyopatikana eneo la tukio na kichwa cha risasi kilichopatikana mwilini mwa marehemu wakati wa uchunguzi wa mwili vililingana na risasi kutoka kwa bastola hiyo. Bastola hiyo pamoja na pikipiki ya Kinuthia zimechukuliwa na polisi kama ushahidi. Uchunguzi wa mauaji hayo ulihusisha pia kuangalia picha za kamera za usalama, ushahidi wa kisayansi na taarifa nyingine za kijasusi. DCI ilisema ushahidi uliopatikana unaonyesha kuwa baadhi ya washukiwa wa mauaji ya Dkt Mutiso huenda pia walihusika katika mauaji ya wakili Kyalo Mbobu mnamo Septemba 9, 2025. Mbobu alipigwa risasi na mtu aliyekuwa nyuma ya pikipiki akiendesha gari kuelekea nyumbani kando ya Barabara ya Magadi. Mauaji hayo yalifanana na yaliyompata Dkt Mutiso kwa kuwa mshambuliaji alitumia pikipiki. Bw Amin pia alidai kuwa matamshi ya Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua kuhusu uchunguzi huo huenda yalifikia Sang na Bett na kuwafanya kutoroka. Alimtaka Bw Gachagua kuwasilisha kwa DCI taarifa yoyote aliyo nayo ambayo inaweza kusaidia uchunguzi wa mauaji hayo. Bw Gachagua alikuwa amedai kuwa maafisa wawili wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Kikuyu walihusika katika mauaji ya Dkt Mutiso. Alisema madai yake yalitokana na “taarifa za kuaminika”. “Maafisa hawa wawili katika Kituo cha Polisi cha Kikuyu ndio waliomuua wakili Kyalo Mbobu na pia Dkt Victoria Mutiso,” Bw Gachagua alisema.

KIONGOZI wa Wiper Patriotic Front , Kalonzo Musyoka Ijumaa alitangaza mabadiliko katika uongozi wa chama hicho kwa kuwateua washirika wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, huku akilenga kuonyesha umoja wa upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Bw Musyoka alimteua aliyekuwa waziri, Jamleck Kamau kuwa mwenyekiti wa chama, Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali kuwa naibu kiongozi wa chama, na wakili wa masuala ya Katiba Ndegwa Njiru kuwa msemaji wa chama. Uteuzi huo ulianza kutekelezwa mara moja na unaashiria upanuzi mkubwa wa uongozi wa Wiper vyama vya upinzani vinapoendelea na mashauriano kuhusu muungano w kukabiliana na Rais William Ruto mwaka 2027. Bw Kamau, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kigumo, amewahi kuhusishwa kisiasa na Bw Gachagua, huku Bw Njiru akiwa mmoja wa mawakili mashuhuri waliowahi kumtetea kiongozi huyo wa DCP. Bw Musyoka alisema uteuzi huo ulitokana na jukumu alilopewa na wajumbe wa chama wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe la Oktoba 10 mwaka jana. “Jukumu la kwanza nililopewa na wajumbe lilikuwa kutafuta urais wa Jamhuri ya Kenya mnamo Agosti 2027. Jukumu la pili lilikuwa kupanua na kujenga uongozi wa chama hiki hadi kiwe sura ya Kenya,” alisema. Alisema mabadiliko hayo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha Wiper pamoja na muungano mpana wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka alisema mashauriano yanaendelea kuunganisha vyama vinavyopinga utawala wa Rais Ruto chini ya mwavuli mmoja wa kisiasa. “Huu si uteuzi wa kujipendekeza, bali ni uteuzi wa imani. Kila mmoja wao anafaa kikamilifu katika chama ambacho ajenda yake pekee ni ‘Komboa Kenya’,” alisema. Kando na mabadiliko hayo ya uongozi, Bw Musyoka alisema hataruhusu tofauti kati ya viongozi wa upinzani kuvuruga juhudi za kuunda muungano mmoja dhidi ya Rais Ruto. Alisema viongozi wa upinzani wanaendelea na mashauriano ya kuleta pamoja Wakenya na akaonya kuwa mgawanyiko utawanufaisha viongozi wa Kenya Kwanza. “Tunapoendelea na kazi hii, mashauriano yanaendelea ili kuleta upinzani chini ya mwavuli mmoja wa kuaminika. Tumekubaliana kuwa mgawanyiko ndiyo mkakati pekee wa utawala huu,” alisema. Bw Musyoka pia aliwataka Wakenya kutotafsiri tofauti zinazojitokeza kati ya viongozi wa upinzani kama ishara kwamba mchakato wa kuunda muungano umevunjika. “Hata mkiona tofauti kati ya viongozi wa vyama ndani ya muungano, tafadhali msizichukulie kwa uzito sana. Tumeungana kwa sababu tukigawanya upinzani, William Ruto atapata muhula wa pili,” alisema. Alisema mashauriano yataendelea hadi vyama na viongozi wote wanaopinga serikali waungane. “Mashauriano hayo yanaendelea na hayatasitishwa hadi kila chama na kila kiongozi anayepinga serikali awe chini ya paa moja, tayari kuunda serikali moja inayosubiri kuchukua uongozi,” alisema.

WANASAYANSI wamegundua hali mpya ya kutisha ya virusi vya Ukimwi kuanza kustahimili dawa muhimu inayotumika katika matibabu ya ugonjwa huo katika nchi nne za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Utafiti uliowasilishwa katika mkutano wa International Aids Society (IAS) mjini Rio de Janeiro, Brazil, umeonyesha hali hiyo miongoni mwa watu wanaoishi na Ukimwi nchini Kenya, Tanzania, Msumbiji na Lesotho. Watafiti wameonya kuwa hali hiyo ikiendelea, maambukizi mapya ya Ukimwi yanaweza kuongezeka. Kinga ya mwili ya wagonjwa ambao virusi vyao vitakuwa vimekuwa sugu kwa dawa hiyo inaweza pia kudhoofika na kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mengine ambayo yanaweza kusababisha kifo. Dawa inayohusika ni dolutegravir, inayojulikana kwa kifupi kama DTG. Tangu 2018, dawa hiyo imekuwa chaguo la kwanza na la pili katika matibabu ya Ukimwi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema DTG ina ufanisi mkubwa, ni rahisi kutumia na husababisha madhara machache ikilinganishwa na baadhi ya dawa nyingine zinazotumika. Dawa hiyo pia inajulikana kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia virusi vya Ukimwi kuzoea na kustahimili matibabu. Daktari Loice Ombajo, mtafiti mkuu wa utafiti huo na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza, alisema sampuli za kwanza za utafiti zilikusanywa kutoka kwa watu 2,994 katika vituo 131 nchini Kenya. Washiriki hao walikuwa wametumia matibabu yenye DTG kwa angalau miezi sita. Baadhi ya washiriki waliopatikana kuwa na mabadiliko ya virusi yanayohusishwa na usugu wa DTG waliingizwa katika utafiti maalumu ili kupata ushahidi wa kusaidia kuboresha matibabu ya wagonjwa ambao dawa hiyo imeshindwa kuwasaidia. “Bado kuna ushahidi mdogo kuhusu namna ya kuwahudumia watu wanaoishi na Ukimwi ambao virusi vyao vimekuwa sugu kwa dolutegravir,” alisema Dkt Ombajo. Alisema utafiti huo unalenga kutoa ushahidi utakaosaidia wataalamu kufanya maamuzi bora kuhusu matibabu ya wagonjwa hao. Takriban watu tisa kati ya 10 wanaotumia DTG hufikia kiwango ambacho virusi vya HIV havionekani kwa wingi katika damu. Hata hivyo, baadhi yao hushindwa kufikia kiwango hicho. Dkt Ombajo alisema sababu kubwa ni kutotumia dawa ipasavyo. Alisema baadhi ya wagonjwa huchoka kutumia dawa kila siku, wengine husahau, huku wengine wakikosa hamu ya kuendelea na matibabu kutokana na hali yao. “Usipotumia dawa au ukaitumia mara kwa mara bila kufuata ratiba, virusi vinaweza kubadilika na kuwa sugu kwa dawa hiyo,” alisema. Katika utafiti huo, watafiti walifanya kazi na washiriki waliokuwa hawatumii dawa ipasavyo ili kuwasaidia kuendelea na matibabu. Takriban asilimia 70 walifikia kiwango cha kudhibiti virusi, huku asilimia 30 wakishindwa. Watafiti walilenga kundi hilo kubaini iwapo kiwango kikubwa cha virusi kilisababishwa na kuzoea dawa. Waligundua kuwa watatu kati ya kila washiriki 10 katika kundi hilo virusi vilikuwa sugu kwa DTG. Dkt Ombajo alisema hali hiyo ni ya kutia wasiwasi kwa sababu dawa hiyo inaweza kushindwa kufanya kazi hata mgonjwa akiendelea kuitumia. Tatizo jingine ni gharama kubwa ya vipimo vya kubaini hali ya dawa kwa virusi, huku nchi nyingi zikikosa rasilimali za kutosha kufanya vipimo hivyo mara kwa mara. Utafiti pia ulibaini baadhi ya wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanakumbwa na hali hiyo. Alisema hali hiyo inaweza kuongeza hatari ya mama mwenye kiwango kikubwa cha virusi kumwambukiza mtoto au mwenzi wake wa ngono.

MAHAKAMA Kuu imesema uchaguzi ujao wa urais nchini ulifaa kufanyika Agosti 2026, badala ya 2027, lakini imekataa kuamuru uchaguzi huo uandaliwe mara moja ikisema hatua hiyo inaweza kutumbukiza nchi katika vurugu. Jaji wa Mahakama Kuu ya Malindi Mugure Thande alisema Katiba inahitaji uchaguzi wa urais ufanyike Jumanne ya pili ya Agosti katika mwaka wa tano baada ya uchaguzi mkuu uliopita. Jaji huyo alisema Ibara ya 136(2)(a) ya Katiba inataka uchaguzi huo ufanyike katika mwaka wa tano na si baada ya mwaka huo kukamilika. Alisema mwaka wa tano baada ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022 ulianza Agosti 9, 2026. “Kufanya uchaguzi ujao wa urais katika tarehe nyingine yoyote isipokuwa Jumanne ya pili ya Agosti 2026 kutakiuka Katiba,” Jaji Thande alisema. Hata hivyo, mahakama ilisimamisha utekelezaji wa uamuzi huo hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao. Hatua hiyo inamaanisha kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haijaamrishwa kuandaa uchaguzi wa urais mwezi huu wa Agosti. Walalamishi katika kesi hiyo, Dkt Owiso Owiso, Khelef Khalifa na Ashioya Biko, walitaka mahakama itoe uamuzi kuhusu tarehe sahihi ya uchaguzi na pia iamuru IEBC kufanya uchaguzi huo Agosti 11, 2026. Jaji Thande alikataa ombi la kuamuru uchaguzi ufanyike mara moja. Alisema kesi hiyo iliwasilishwa Oktoba 2025 wakati maandalizi ya uchaguzi wa 2027 yalikuwa tayari yameanza. Alisema IEBC, wagombea watarajiwa na Wakenya kwa ujumla walikuwa tayari wamejiandaa kwa uchaguzi wa Agosti 2027. “Kuamuru tume ya uchaguzi kuandaa uchaguzi wa urais Agosti 2026 kutakuwa kutoa amri ambayo haiwezekani kutekelezwa kwa njia ya kiutendaji,” alisema. Jaji huyo aliongeza kuwa hatua kama hiyo inaweza kuingiza nchi katika machafuko. Mahakama ilisema ililazimika kusawazisha utekelezaji wa Katiba na tahadhari ya kimahakama ili kuepuka kusababisha “vurugu kubwa kitaifa ambazo haziwezi kudhibitiwa”. Mzozo huo ulitokana na tafsiri ya Ibara ya 136(2)(a), inayoweka wakati wa kufanyika kwa uchaguzi wa urais. Walalamishi walidai kuwa mwaka wa tano baada ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022 ulianza Agosti 9, 2026 na kumalizika Agosti 8, 2027. Kwa hesabu hiyo, walisema Jumanne ya pili ya Agosti 2026, ambayo ni Agosti 11, ndiyo tarehe iliyowekwa na Katiba kwa uchaguzi. Walitegemea pia Ibara ya 259(5)(c), inayoweka namna vipindi vinavyotajwa kwa miaka vinavyopaswa kuhesabiwa. Walalamishi walitaja uchaguzi wa 2013 na 2017 kama mifano ya kuonyesha kuwa Katiba haimpi rais haki ya lazima ya kutawala kwa miaka mitano kamili iwapo kufanya hivyo kutapingana na tarehe iliyowekwa kikatiba ya uchaguzi. Jaji Thande pia alisema ratiba ya uchaguzi iliyowekwa na Katiba ina uzito kuliko dhana kwamba rais lazima atumikie miaka mitano kamili. Alisema IEBC inaposhindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba, mahakama inaweza kuingilia kati. Hata hivyo, mahakama ilisitisha utekelezaji wa uamuzi kwamba uchaguzi utakaofanyika nje ya Agosti 2026 utakuwa batili hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao. Hii ina maana kuwa ingawa mahakama imesema tarehe inayofaa kikatiba ilikuwa Agosti 2026, haijaamuru Kenya kufanya uchaguzi wa urais mwezi huo. Mahakama pia ilisema muhula wa rais si miaka mitano chini ya Ibara ya 136(2)(a), na kwamba, Ibara ya 142 au kifungu kingine chochote cha Katiba hakimpi rais muhula wa miaka mitano. Kesi hiyo iliwasilishwa kupitia kampuni ya mawakili ya Otieno Ogola & Company Advocates na Osundwa & Company Advocates. Miongoni mwa waliotajwa kuwa wahusika wenye maslahi katika kesi hiyo ni Chama cha Wanasheria Kenya (LSK), Katiba Institute, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, UDA, aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, mwanaharakati Okiya Omtatah, mwanasiasa Jimi Wanjigi, aliyekuwa Waziri Fred Matiang’i na Kenya Human Rights Commission.

KIGOGO wa Upinzani nchini Uganda Kizza Besigye alizirai Jumatano wakati akihudhuria kusikizwa kwa kesi yake jijinsi Kampala. Besigye, 70, amekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhaini tangu kunyakwa na maafisa wa Uganda akiwa ziarani Kenya karibu miaka miwili iliyopita. Alitiwa nguvuni pamoja na msaidizi wake Obeid Lutale Novemba 2024 jijini Nairobi. Walikanusha mashtaka na mawakili wao wametaja mashtaka hayo kuwa yaliyochochewa kisiasa. Majaribio kadhaa ya kuwaachilia yamezimwa na utawala wa Rais Yoweri Museveni na mwanawe mkuu wa jeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

KIFO cha ghafla cha afisa wa polisi Marjori Bosibori kimewaacha wenzake na jamaa wakiwa na maswali mengi huku uchunguzi ukiendelea kubaini kilichotokea katika saa zake za mwisho. Bosibori, mwenye umri wa miaka 42 na aliyekuwa afisa wa mawasiliano katika Kituo cha Polisi cha Kisii Central, alifariki kutokana na jeraha la risasi kifuani ndani ya chumba cha mawasiliano cha kituo hicho. Afisa huyo alirejea kazini Jumanne baada ya mapumziko mafupi nyumbani kwao, Kisii. Aliripoti kazini kama kawaida, akafanya shughuli zake katika duka moja kubwa mjini Kisii, akazungumza na wenzake na hata kushiriki nao chakula cha mchana. Kwa waliokuwa wakifanya kazi naye, alionekana mtulivu, mwenye bashasha na tayari kuendelea na majukumu yake. Hata hivyo, chini ya saa 24 baadaye, alipatikana amefariki ndani ya chumba cha mawasiliano akiwa na jeraha moja la risasi kifuani huku bunduki aina ya AK-47 ikiwa imelala karibu naye. Kifo chake kimewashtua maafisa wenzake na familia yake. “Aliripoti kazini kama kawaida yake. Hatukushuku chochote. Bado siamini kilichotokea,” alisema mmoja wa maafisa aliyekula naye chakula cha mchana siku hiyo. Afisa mwingine alisema Bosibori alikuwa mtu mtulivu na aliyependa kuweka siri maisha yake ya kibinafsi, hali iliyofanya iwe vigumu kubaini alipokuwa akikabiliwa na changamoto. Marafiki zake pia wanamkumbuka kama shabiki mkubwa wa klabu ya Manchester United. Polisi wanachunguza uwezekano kuwa alijitoa uhai, ingawa wanasema bado hawajabaini kilichotokea katika saa zake za mwisho. Kamanda wa Polisi wa Kisii Central, Musa Imamai, alisema Bosibori alimaliza shughuli zake katika duka hilo kabla ya kurejea kituoni muda mfupi baada ya saa sita usiku akiwa na mwenzake. Walipofika kituoni, alimwambia mwenzake kuwa anaelekea chooni. Mwenzake hakushuku chochote. Badala yake, wachunguzi wanaamini aliingia katika chumba cha mawasiliano, ofisi yenye ulinzi mkali ambayo haitumiki sana wakati huo wa usiku, akajifungia kutoka ndani na hakutoka tena. Ilikuwa hadi Jumanne asubuhi afisa mwingine aliporipoti kazini ndipo iligundulika kuwa mlango wa chumba hicho ulikuwa umefungwa kwa muda mrefu. Baada ya juhudi za kuufungua kugonga mwamba, maafisa walivunja mlango. Ndani walimkuta Bosibori ameketi kwenye kiti bila uhai akiwa na jeraha la risasi kifuani huku bunduki ya AK-47 ikiwa sakafuni karibu naye. “Tulimkuta akiwa ameketi na damu ikitoka kwenye jeraha la risasi. Uchunguzi wa awali unaonyesha alipigwa risasi moja kifuani na risasi hiyo ikatokea mgongoni,” alisema Bw Imamai. Tukio hilo liliwaacha hata maafisa wenye uzoefu mkubwa wakiwa na mshtuko. Polisi walipata bunduki hiyo, ganda moja la risasi, magazini yenye risasi 29, ufunguo wa ofisi, simu tatu za mkononi na dawa mbalimbali. Bosibori alikuwa bado amevaa sare zake za polisi. Bw Imamai alisema alikuwa miongoni mwa maafisa wachache walioaminiwa kufanya kazi katika chumba cha mawasiliano kutokana na nidhamu na uadilifu wake. “Hii ni ofisi muhimu na ni maafisa wachache pekee wanaoruhusiwa kufanya kazi humo. Bosibori alikuwa mmoja wao,” alisema. Aliongeza kuwa wachunguzi wanachunguza kila upande wa maisha yake, ikiwemo iwapo kulikuwa na matatizo ya kifamilia au ya kibinafsi ambayo huenda yalichangia mkasa huo. “Kufikia sasa hatuna fununu zozote kuhusu kilichosababisha kile kinachoshukiwa kuwa kujiua kwake,” alisema. Mwili wake ulihamishwa hadi mochari ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii ambako unatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kubaini chanzo kamili cha kifo.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) has announced changes to its secretariat, appointing new leaders to key positions as it also approved a timetable and guidelines for preparations for its internal elections and those of its affiliated organisations scheduled for 2027.

IRINGA: MKOA wa Iringa umeingia katika hatua nyingine ya mapambano dhidi ya utapiamlo na lishe duni baada ya Mkuu wa Mkoa, Kheri James, kutangaza sera ya uwajibikaji mkali kwa watendaji wote wanaosimamia masuala ya lishe. Aidha, ameonya halmashauri itakayoshindwa kufikia asilimia 95 ya viashiria vya utekelezaji italazimika kutoa maelezo na kuchukua hatua za haraka za…

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Mkoa wa Arusha, kutapunguza changamoto ya msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na kuweka wazi kuwa wajibu wa serikali ni kusimamia mradi huo ukamilike kwa wakati. Makalla ameyasema hayo leo Julai 29, jijini Arusha wakati wa…

MATAMSHI ya Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki kuwa hawezi kutoka kwa serikali ni jambo zito sana. Kwanza ni sauti inayotoka kwa mwanajeshi mtiifu kwa Rais William Ruto. Alikuwa kimbilio na chaguo lake la kwanza baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua. Gachagua mwenyewe amechafua anga ya Rais Ruto Mlima Kenya sehemu iliyochangia pakubwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa 2022. Ila sasa habari zimemfikia kuwa Waziri Wycliffe Oparanya huenda ndiye atakayekuwa mgombea mwenza wa Ruto. Hesabu hii ya Rais ikiwa itatekelezwa inaweza kumpa majeraha makubwa kuliko angesalia na Kindiki. Ni wazi kuwa Gachagua amekimbia na idadi kubwa ya wapiga kura. Swali ni je, Oparanya ataweza kumletea Rais Ruto kura zaidi? Jibu la wazi ni kuwa huenda matokeo yakawa mabaya zaidi kutokana na msisimko wa Seneta Edwin Sifuna. Oparanya anakabiliwa na upinzani mkubwa kwanza kutoka kwa gavana wake Fernandes Barasa ambaye anadhania kuwa hamtakii mema kwa kuungana na wapinzani wake katika kinyang’anyiro cha ugavana mwaka 2027. Sasa Rais Ruto atakuwa na kazi ya kuwapatanisha awali ndipo waanze kuzunguka naye nchini. Ilivyo ni kuwa Oparanya hana misuli ya kusukuma kampeni za kitaifa jinsi alivyo Kindiki. Ikiwa Kindiki na Ruto wataachana basi pacha waliovumiliana katika mateso watakuwa wametengana. Ikumbukwe Kindiki alikuwa Naibu Spika wa Bunge la Seneti na akaondolewa mamlakani na upande wa Rais Uhuru Kenyatta kwa sababu ya ushirika wake na Ruto. Wote wamekuwa na misiba tofauti ya kisiasa lakini kilio ni kimoja. Katika kampeni za mwaka 2022 Profesa Kindiki ndiye aliyekuwa wakala mkuu wa Ruto kule Bomas. Alikubali wadhifa huo licha ya kunyimwa nafasi kuwa mgombea mwenza wa Ruto licha ya wanachama kumdhania kuwa angekuwa chaguo bora. Hii inatoa sifa ya mtu mvumilivu ila wakati mwingine anajulikana kama ‘fireman”. Wapo wanaosema kuwa matokeo ya Ol Kalou yamemfanya Rais kumdhania Kindiki kuwa mtu asiyesukuma ajenda ya mlima kwa dhati ya moyo wake. Jambo lisilo na mjadala ni kuwa ikiwa Ruto atabadilisha mgombea mwenza kutoka kwa Kindiki basi hata asili mia 30 itakuwa vigumu kupata kutoka Mlima Kenya. DCP itamega sehemu kubwa ya UDA Rais akose uwakilishi wa kitaifa. Kwa waziri Oparanya ngoma hiyo ni kubwa kumzidi. Ana kibarua kwanza cha kuzima wimbi la Sifuna na gavana Natembeya ambalo limewameza Spika Moses Wetangula na Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi. Kwa ufupi ni heri Kindiki kuliko Oparanya. Paul Nabiswa ni mhariri, NTV

IRINGA: Mkoa wa Iringa umeingia katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030 ukiwa na taswira ya mafanikio yanayoonekana kwa macho: mapato ya Serikali yameongezeka, fedha za maendeleo zimeongezeka, na miradi ya afya, elimu, maji na miundombinu inaendelea kubadili maisha ya wananchi. Taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha…

IRINGA: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Kasesela, amesema CCM itaendelea kushinda uchaguzi kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanywa na serikali yake, huku akisisitiza kuwa changamoto kubwa iliyobaki si ukosefu wa kazi, bali ni baadhi ya watumishi wa umma kushindwa kuwahudumia wananchi kwa utu. Kasesela, ambaye…

ARUSHA: Ongezeko la idadi ya wagonjwa katika kambi ya matibabu iliyoratibiwa na Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, limeifanya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuongeza idadi ya madaktari bingwa na wabobezi wanaotoa huduma katika kambi hiyo. Akizungumza akiwa kambini, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dk. Dalilah…

ARUSHA: Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dk, Toba Nguvila, amewasisitiza watendaji wa serikali katika mkoa huo, kuanzia sekretarieti ya mkoa, halmashauri taasisi na mashirika yote ya umma, kufanya kazi kwa ushirikiano kisekta ili kutimiza adhma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati. Dk Nguvila ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao…

TANGA: JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limeendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu, baada ya kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 200 katika operesheni maalumu zilizofanyika kuanzia Juni 1 hadi Julai 16, 2026. Akizungumza leo Julai 17, 2026 Tanga, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa Katika kipindi hicho cha wiki sita, jeshi hilo limebainisha kuwa…

AFISA wa serikali ameieleza Mahakama ya Mombasa kuwa namna waathiriwa wa vifo vya Kwa Bi Nzaro walivyozikwa bila nguo, bila majeneza na katika makaburi ya kina kifupi ilikuwa kinyume na mila na desturi za jamii ya Wagiriama. Akitoa ushahidi mahakamani, Chifu wa eneo la Chakama, Bw Raymond Charo, alisema mazishi aliyoshuhudia wakati miili ya waathiriwa walikuwa wakifukuliwa yalifanana kwa kiasi kikubwa na yale yaliyobainika katika uchunguzi wa mkasa wa Shakahola. Bw Charo aliiambia mahakama kuwa miili kadhaa ilipatikana ikiwa imezikwa kwenye makaburi ya kina kifupi bila nguo wala majeneza, jambo ambalo alisema halikubaliki kabisa kwa mujibu wa mila za Wagiriama. “Napenda pia kueleza kuwa kwa mujibu wa utamaduni wa Wagiriama, mazishi hufanyika mchana yakifuatana na maombi kulingana na jinsia ya marehemu, na mwili huwekwa ndani ya jeneza. Aidha, kaburi halipaswi kuwa na kina kisichopungua futi sita,” alisema Bw Charo. Alieleza kuwa wakazi wa eneo la Kwa Bi Nzaro wengi wao ni Wagiriama, lakini namna waathiriwa hao walivyozikwa haikufuata utaratibu wowote unaotambulika katika mila na desturi za jamii hiyo. Bw Charo alifafanua kuwa yeye si mpelelezi wala mtaalamu wa uchunguzi wa maiti na kwamba ushahidi wake ulitokana na yale aliyojionea wakati wa shughuli ya ufukuzi wa miili. Pia, aliiambia mahakama kuwa anafahamu polisi walipata mabaki mengine ya miili ya binadamu pamoja na viungo vya miili katika eneo hilo kabla ya kuanza shughuli kubwa ya ufukuzi wa miili, ingawa hakuweza kuthibitisha idadi kamili ya mabaki yaliyopatikana. Bw Charo alikuwa akitoa ushahidi katika kesi ambayo mhubiri tata Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia kuhusiana na vifo vya waumini katika eneo la Kwa Bi Nzaro, waliokuwa washirika wa kanisa lake lililopigwa marufuku la Good News International. Mackenzie ameshtakiwa pamoja na Shallyne Temba Anindo, Kahindi Kazungu Garama, Tom Mkonwe, Julius Luwali na Johnson Richard. Upande wa mashtaka unadai kuwa kwa pamoja waliwaua watu 29 kwa kutekeleza makubaliano ya kujiua yaliyolenga kusababisha vifo vyao na vya watu wengine ambao hawako mahakamani. Shtaka la kwanza linahusu kifo cha Samuel Owino Owuoyo, mwanaume, huku mashtaka mengine yakihusu waathiriwa wengine 28 ambao wengi wao hawakufahamika majina yao, jinsia wala umri wao, na walitambuliwa kupitia ushahidi wa kitaalamu na vielelezo vilivyokusanywa eneo la tukio. Wanadaiwa kutekeleza makosa hayo katika eneo la Kwa Bi Nzaro, Chakama, Kaunti Ndogo ya Magarini, Kaunti ya Kilifi, mwaka 2025. Konstebo wa Polisi Isaiah Barasa kutoka Kituo cha Polisi cha Langobaya pia alitoa ushahidi akisema maafisa wa polisi walifika katika boma la Bi Anindo baada ya kupokea taarifa kwamba baadhi ya wafuasi waliokuwa wakiishi hapo walikuwa wameathiriwa na mafundisho yenye misimamo mikali yaliyowashawishi kujinyima chakula hadi kufa. Shahidi mwingine wa upande wa mashtaka, Allan Luwali, aliiambia mahakama kuwa Mei 18, 2024 alimuuzia Bw Garama pikipiki kwa Sh18,000 katika karakana yake. Alisema baadaye alitoa taarifa kwa maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai baada ya kupigiwa simu na mmoja wa maafisa hao aliyekuwa akihitaji taarifa kuhusiana na vifo vya watu wengi katika eneo la Kwa Bi Nzaro. Mahakama imeambiwa kuwa piki piki hii ndio iliotumika kusafirisha wafuasi was kanisa hilo kutoka mji wa Malindi hadi msitu wa Kwa Bi Nzaro. Mke wa Bw Garama, Salama Masha aliambia Mahakama katika ushahidi wake kuwa yeye ndio alimchukulia mumewe pesa ya kununua piki piki hiyo kutoka kwa chama chao.

MWANASHERIA mkuu na Waziri wa Fedha, John Mbadi wameitaka Mahakama Kuu kusimamisha kusikizwa kwa kesi muhimu inayohusu uhalali wa deni la umma la Sh7 trilioni inayosubiri rufaa. Wanahoji kuwa korti iliruhusu kwa njia isiyofaa kesi hiyo kusonga mbele licha ya uchunguzi maalum unaoendelea, wakisema kesi hiyo ipo chini ya jukumu la mkaguzi mkuu wa fedha za serikali kikatiba kabla ya korti kuingilia kati. Ombi hilo limetokana na uamuzi uliotolewa Juni 25, 2026 na majaji Justices Francis Gikonyo, Roselyne Aburili na Moses Ado, waliotupilia mbali hoja ya mwanasheria mkuu kwamba kesi hiyo, ambayo vilevile inaitisha ufichuzi wa deni la umma, ilikaidi kanuni za kukamilisha njia zote, ukomavu na kutenganisha mamlaka. Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor na Bw Mbadi wanaazimia kusimamisha kikao cha kusikiza kesi hiyo kilichopangiwa kufanyika Oktoba, wakionya kwamba michakato ya kesi itahujumu rufaa inayodhamiriwa na kuvuruga mchakato wa uangalizi kikatiba. Mwanasheria Mkuu hajaridhishwa na uamuzi wa mahakama uliopuuzilia mbali jaribio lake la kusimamisha kesi ili kuruhusu uchunguzi maalum unaofanywa na mkaguzi mkuu, hivyo kusababisha rufaa hiyo inayopangiwa kuwasilishwa. “Baada ya kukosa kuridhishwa na uamuzi mwanasheria mkuu aliwasilisha notisi ya kukata rufaa Juni 30, 2026 akieleza nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wote. Iwapo kesi kuhusu suala hili haitasimamishwa, rufaa inayokusudiwa itaishia kuwa kazi bure,” anahoji wakili wa serikali Samwel Kaumba, akimwakilisha mwanasheria mkuu katika nakala za korti. Kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia, Okiya Omtatah na walalamishi wengine wanane, inapinga ufaafu kikatiba wa takriban Sh6.95 trilioni za ukopaji wa umma zilizolundikana kati ya miaka ya fedha 2014/15 na 2023/24 ikiwemo mikopo ya Eurobond. Aidha, inaitisha kutangazwa kwa uhalali kuhusu mchakato wa ukopaji, uwajibikaji wa maafisa wa umma na uhalali kikatiba wa visehemu vya Sheria kuhusu Usimamizi wa Fedha za Umma. Walalamishi vilevile wanataka uamuzi kuhusu iwapo maafisa wa umma wa zamani na wa sasa, ikiwemo wanaoshikilia afisi za Hazina Kuu, Mdhibiti Bajeti na Mkaguzi Mkuu wanapaswa kuwajibika binafsi chini ya Kifungu 226(5) cha Katiba kuhusu madai ya kuelekeza, kuidhinisha au kuruhusu vitendo vinavyodaiwa kuwa haramu vya ukopaji, utowaji fedha, matumizi ya malipo ya fedha za umma kinyume cha sheria. Katika kesi mpya iliyowasilishwa, mwanasheria mkuu anasema korti inapaswa kusimamisha kesi zote hadi Korti ya Rufaa itakapotoa uamuzi kuhusu rufaa inayonuiwa kuwasilishwa.

VIONGOZI wa ODM Luo Nyanza wameapa kuwa ‘watakufa’ na Rais William Ruto hadi 2027 kutokana na uimarishaji wa miundomsingi eneo hilo. Wakiongozwa na Seneta wa Siaya, Dkt Oburu Oginga, walisema ODM haina nia ya kuwa na mgombeaji wa urais 2027 na ni Rais Ruto ndiye atapigiwa kura mwakani. Kulingana naye, wagombeaji wengine kama Rigathi Gachagua, Martha Karua, Justin Muturi na wengine hawana nafasi ya kushinda urais. “Wanapambana na kujipiga kifua na hata hawajaamua nani ni mgombeaji wao wa urais. Sisi tunajua nani atakuwa mgombeaji wetu na tutawashinda,” akasema. Dkt Oginga alisema Luo Nyanza ilitengwa na tawala za nyuma kutokana na msimamo wake wa kisiasa lakini ushirikiano kati ya UDA-ODM umebadilisha eneo hilo kimaendeleo. “Hatubaguliwi tena, tuko serikalini na tunajua mahali tunaelekea. Tuliingia kupitia dirishani lakini sasa tunajua mahali tunaenda,” akasema Dkt Oginga. Aliwataka wakazi wa Nyanza kuwachagua viongozi wa ODM pekee ili chama hicho kiendelee kuwa na umaarufu mkubwa wa kisiasa. “Nikiketi na Rais Ruto baada ya uchaguzi wa mwaka ujao, atauliza nina watu wangapi. Kwa hivyo, wapigie wawaniaji wa ODM viti vingine lakini urais tunampa Ruto,” akasema. Alikuwa akiongea katika ibada ya kanisa Kaunti ya Homa Bay. Aliandamana na Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Raymond Omollo, Katibu wa Afya Ouma Oluga, Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang na Mbunge wa Homa Bay mjini Opondo Kaluma. Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga alisema eneo la Ziwa limepata maendeleo makubwa kupitia miradi ya maendeleo, akibainisha kuwa miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea imebadilisha kwa kiasi kikubwa sura ya eneo hilo. "Tunaposema tunaiunga mkono serikali, si bure. Ni kwa sababu ya umoja wa Wakenya.. Hilo ndilo jambo ambalo serikali jumuishi imefanikiwa kulitekeleza," alisema Bi Wanga. Pia alitetea Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) dhidi ya mashambulizi ya kisiasa wakati tume hiyo ikijiandaa kuendesha uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Kwa upande wake, Seneta Moses Kajwang' alisema kuwa kwa muda mrefu wapigakura wa eneo la Ziwa waliamini kuwa maendeleo yangewezekana tu iwapo mmoja wao angekuwa kiongozi wa taifa. Hata hivyo, alisema Kenya haihitaji kiongozi wa kieneo bali mwenye mtazamo wa kitaifa. "Tutaendelea kuiunga mkono serikali. Ukweli kwamba tunataka kushika mamlaka haumaanishi hatutashirikiana na serikali," akasema seneta huyo.

HUKU upinzani ukiendelea kuonyesha wana umoja hadharani, mvutano mkali unaendelea kushuhudiwa kati ya mrengo wa Linda Mwananchi na Umoja wa Upinzani, kila upande ukipambana kudhibiti kampeni za kumng'oa madarakani Rais William Ruto. Migawanyiko hiyo ilijitokeza wazi Ijumaa baada ya aliyekuwa Naibu Rais ,Rigathi Gachagua, kumshambulia Gavana wa Murang'a, Irungu Kang'ata, kuhusu uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. “Nimesikia Kang'ata akisema anataka kuja Ol Kalou akiwa na Linda Mwananchi. Hatukuhitaji hapa. Kama unataka kupigia debe UDA, Jubilee au chama kingine chochote, uko huru kufanya hivyo, lakini kampeni za DCP ni suala la wenyeji,” akasema Bw Gachagua. Kauli hiyo iliwafanya viongozi wa Linda Mwananchi kuhamisha mikutano yao Nyahururu na kusitisha mipango ya kumpigia kampeni mgombea wa DCP. Bw Kang'ata alijiunga na Linda Mwananchi mwezi uliopita wakati wa mkutano wa kisiasa uliofanyika Thika. Matamshi ya Bw Gachagua dhidi ya Bw Kang'ata yamefichua mapambano makubwa zaidi ya kupigania ushawishi ndani ya upinzani. Duru kutoka upinzani zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi wana hofu kwamba ajenda yao ya kisiasa inaweza kudhoofishwa na kundi la Linda Mwananchi ilhali wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali tangu 2022. Magharibi mwa Kenya Mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya, amemkosoa Bw Sifuna akisema hana ushawishi wowote wa kisiasa. “Nataka kusema Sifuna hana kura Kakamega na Bungoma Didmus Barasa amemshinda kwa umaarufu. Eugene Wamalwa ndiye mwanasiasa maarufu zaidi ambaye ataleta kura kwa upinzani bila kujali atashikilia wadhifa gani,” akasema Bw Salasya. “Wamejaa kiburi na wanataka kuleta mkanganyiko. Wania urais tuone utakakofika na jinsi itakavyomalizika,” akaongeza Bw Salasya. Si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kupuuza ushawishi wa kisiasa wa Bw Sifuna na Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya katika eneo hilo. Mrengo wa Sifuna na Natembeya umeitikisa kambi ya DAP-Kenya. Wawili hao sasa wanapanga mikutano miwili mikubwa ya kisiasa katika kaunti za Trans Nzoia na Bungoma Julai 25 na 26. Bw Natembeya tayari ametangaza kuwa atatetea kiti chake kupitia chama kipya cha kisiasa badala ya DAP-Kenya kinachoongozwa na Bw Wamalwa. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022, Bw Natembeya na Bw Wamalwa walitofautiana kuhusu uongozi wa DAP-Kenya, hali iliyomfanya gavana huyo kuanzisha vuguvu la Tawe. Wakati wa ziara ya upinzani Magharibi mwa Kenya mwezi uliopita, Bw Gachagua alimtangaza Bw Natembeya kuwa mratibu wa kampeni zake Magharibi. Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi, naye amewashutumu baadhi ya wanasiasa kwa kujaribu kuelekeza shughuli za Linda Mwananchi huku wakimtumia Bw Sifuna kuendeleza maslahi yao binafsi. Alimtaja Bw Kang'ata kuwa mmoja wa viongozi wanaochochea migawanyiko ndani ya upinzani. “Linda Mwananchi haitatekwa nyara nikiwa macho. Hatutakuruhusu wewe (Kang'ata) kumtumia vibaya mwana wetu Edwin Sifuna," akasema Bw Amisi, ambaye amekuwa akiongoza kampeni za chama chake cha People Renaissance Movement (PRM) katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Seneta wa Kisii, Richard Onyonka ,anaamini kuwa hatimaye makundi hayo mawili yataungana chini ya muungano mmoja, akisema migawanyiko ya sasa inadhoofisha upinzani. Bw Onyoka amesisitiza kuwa pande zote mbili zinapaswa kuweka kando kiburi na kushirikiana. "Lazima tushirikiane kwa sababu ajenda ya Upinzani na Linda Mwananchi ni kuhakikisha utawala wa sasa unaondolewa madarakani mwaka ujao," akasema Bw Onyonka, ambaye yuko ndani ya Linda Mwananchi lakini anaunga mkono azma ya urais ya Dkt Matiang'i.

MBUNGE wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, Jumamosi alijitokeza hadharini wiki moja baada ya kuhusishwa na uvamizi dhidi ya msafara wa Linda Mwananchi eneo la Keumbu, Kaunti ya Kisii. Bw Jhanda jana alisema hakuna mtu ambaye atamtishia licha ya kuamrishwa afike mbele ya Idara ya Upelelezi Nchini (DCI). Uvamizi dhidi ya kambi ya Linda Mwananchi ulisababisha mauti ya mtu mmoja na kuwajeruhi wengine. Jumamosi, mbunge huyo alihutubia mamia ya wafuasi wake katika eneo la Keumbu. Alikuwa ameamrishwa afike mbele ya DCI kutokana na tukio hilo la Julai 3 ambapo kando na maafa ya mtu mmoja, wengine 20 walijeruhiwa. “Hapa inaitwa nini?” akauliza ambapo umati ulijibu “Keumbu” Umati aliouhutubia ulijumuisha vijana na akina mama huku akiongea kwa lugha ya Ekegusii. “Nchi lazima ijue kuwa kuna mbunge wa Nyaribari Chache ambaye yupo Keumbu, nyumbani na haogopi” Kujitokeza kwake kunajiri wakati ambapo kuna uchunguzi unaoendelea kutokana na uvamizi wa msafara wa Linda Mwananchi ambao uliongozwa na Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna. Aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga, ambaye alikuwa kwenye msafara wa Linda Mwananchi alinusurika bila kujeruhiwa ingawa gari lake liliharibiwa vibaya. Vincent Osiemo maarufu kama Mapinduzi aliaga dunia baada ya kupigwa na mawe na kuanguka kwenye mojawapo ya magari kisha akapigwa na umati. Upasuaji wa maiti ambao ulifanywa na Mwanapatholojia wa serikali, Dkt Peter Morebu, ulibaini kuwa marehemu aliaga dunia kutokana na majeraha ya kichwa ambayo yalisababishwa na kupigwa kwa kifaa butu. Maandalizi ya mazishi yamekuwa yakiendelea nyumbani kwao Gionseri, eneobunge la Bobasi huku akitarajia kuzikwa mnamo Julai 17. Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imetangaza kuwa imewanyaka washukiwa saba kuhusiana na ghasia hizo za Keumbu. Hata hivyo, washukiwa hao waliachiliwa huru baada ya kufikishwa kortini bila afisa wa uchunguzi au kiongozi wa mashtaka. Ingawa hivyo, polisi nao wanasisitiza kuwa uchunguzi unaendelea na wote waliohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) imewaonya wawaniaji dhidi ya kufadhili au kupanga ghasia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. IEBC imesema kuwa wawaniaji wanaoshiriki tabia hizo watapigwa faini na pia uchaguzi utafutiliwa mbali kwenye maeneo yenye ghasia. Kwenye mahojiano na Taifa Leo Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon alisema tume hiyo itahakikisha mwongozo wa uchaguzi unafuatwa kuhakikisha kuna uwazi na uwajibikaji. “Hatuwezi kumruhusu mtu mmoja kuvuruga uchaguzi ambao unafadhiliwa na walipaushuru ili awe mbunge. Kama tume, tuna mamlaka ya kumpiga marufuku, kumtoza faini au hata kumzima mwaniaji ambaye amevunja sheria kushiriki uchaguzi,” akasema Bw Ethekon. Alisema IEBC haitakuvumilia uhuni wa kisiasa na haitajali mrengo ambao mwanasiasa anaegemea. Alisisitiza IEBC itachukua hatua kali kwa kutegemea ushahidi ambao utawasilishwa. “Kama tuna ushahidi kuwa kuna mtu anawatumia wahuni, kuwalipa au kuwafadhili, basi mtu huyo anahujumu uchaguzi wa amani na atatozwa faini au kuzuiwa kuwania,” akasema. Bw Ethekon alisema pia IEBC haitakuwa na budi ila kufutilia mbali uchaguzi katika maeneo ambako kuna utovu wa usalama. Mwenyekiti huyo aliwataka wapigakura pia wanakili visa vya ghasia na aina yoyote ya uvunjaji wa sheria kisha wawasilishe ushahidi huo kwa IEBC. “Umma haufai kushutumu tume kuwa haina meno ya kungáta bali pia wanakili uhalifu na matukio mengine kisha wawasilishe malalamishi kwetu. Ni kwa kutegemea ushahidi huu ndipo tutachukua hatua,” akasema. Alisisitiza kuwa kuandaliwa kwa uchaguzi huru kunahitaji ushirikiano kutoka kwa washikadau wote. Kauli, Bw Ethekon imekuja wakati ambapo kumekuwa na ghasia za kisiasa ikiwemo ya jana jijini Kisumu na hivi majuzi dhidi ya msafara wa Linda Mwananchi katika Kaunti ya Kisii. Jana ghasia ziliibuka jijini Kisumu wakati ambapo wahuni walijaribu kuwauzuia Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuhudhuria ibada katika Kanisa la St Stephen Cathdral. Wahuni hao walizuia wanasiasa hao wawili kuondoka na kuwalazimu polisi kutumia vitoza machozi kuwatimua. Ghasia hizo zilichipuka baada ya Bw Orengo kuwahutubia waumini. Ilibidi Mabw Orengo na Sifuna waondolewe kupitia mlango wa nyuma. Jana ilikuwa mara ya kwanza ambapo Bw Sifuna alijitokeza hadharani baada ya kubanduliwa kama katibu mkuu wa ODM. "Nawashukuru sana wale ambao wamesimama nami tangu wakati nikihudumu kama katibu mkuu wa ODM," akasema Bw Sifuna. Suala hilo pia linatarajiwa litachipuka sana wakati ambapo Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen atafika mbele ya Kamati ya Bunge baadaye mwezi huu. Akizungumza katika kikao cha faragha na wabunge mnamo Februari, Bw Murkomen alidai kuwa baadhi ya wanasiasa wanayafadhili makundi ya wahalifu wakijiandaa kwa uchaguzi. "Suala la magenge ya wahalifu limekuwa gumu kwa polisi kwa sababu wanaoyafadhili wameketi katika Bunge hili, wanashikilia nyadhifa za juu serikalini na wana ushawishi mkubwa ndani ya vyama vya kisiasa. Kila wanapokamatwa, viongozi wa kisiasa huwatisha maafisa wa polisi wanaoshughulikia kesi hizo," akasema Mbali na hayo, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja naye ameonya kuwa wahuni wa kisiasa na magenge ya uhalifu watakabiliwa vikali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Alisisitiza Huduma ya Kitaifa ya Polisi haitaruhusu ghasia kuvuruga kampeni wala kuhatarisha usalama wa wananchi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa afisi za Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) za Kaunti-ndogo ya Sotik katika Kaunti ya Bomet, Bw Kanja alisema watu wanaojihusisha na uhuni wa kisiasa, uhalifu uliopangwa na makosa mengine watafuatiliwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria. "Ninatoa onyo kwa wahuni na magenge ya uhalifu kote nchini kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na hawatapata nafasi ya kuendelea na shughuli zao," akasema Bw Kanja. Aliongeza kuwa kila mtu atawajibika binafsi kwa uhalifu wake na kuwaonya wanaojihusisha na ghasia za kisiasa kwamba watakabiliwa kibinafsi na matokeo ya vitendo vyao. Inspekta Jenerali huyo alisema maafisa polisi 10,000 walioajiriwa mwezi Machi mwaka jana kwa sasa wanapitia mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi cha Kiganjo na watapelekwa katika maeneo mbalimbali nchini mara tu watakapohitimu ili kuimarisha juhudi za kuzuia uhalifu.

Just 18 minutes after it was posted online by a national paper last Friday, I saw a breaking news story saying that President Bola Ahmed Tinubu had officially renominated Vice President Kashim Shettima as his running mate for the 2027 election. The story was a pleasant surprise for me because I had earlier decided I was going […]

By Ademola Lawrence When the news first broke that students and teachers had been abducted, the nation reacted as expected. Social media erupted with outrage. Television stations ran breaking news coverage. Newspapers led with banner headlines. Political commentators dissected the incident, while citizens demanded answers from the government and security agencies. It was a moment […]

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametangaza kufunguliwa kwa Kitengo kipya kilichopanuliwa cha huduma za figo (Renal Unit) katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki. Ufunguzi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha za usafishaji damu (dialysis) na kuimarisha huduma maalumu za afya katika kaunti hiyo. Kitengo hicho cha kisasa, kilichoko katika Hospitali ya Level 5 ya Mama Lucy Kibaki, Umoja II, Embakasi Magharibi, kimewekewa mashine za kisasa na kina wahudumu wenye uzoefu katika matibabu ya magonjwa ya figo ili kutoa huduma kamili kwa wagonjwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gavana Sakaja alisema kitengo hicho kitatoa matibabu ya kina ya magonjwa ya figo, mipango ya matibabu inayolingana na mahitaji ya kila mgonjwa, ushauri wa lishe na mtindo wa maisha, pamoja na huduma za ushauri nasaha na msaada kwa wagonjwa. "Upanuzi wa huduma zetu za figo unaonyesha dhamira yetu ya kuhakikisha wakazi wa Nairobi wanapata huduma bora na nafuu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu. Kituo hiki kitaboresha matokeo ya matibabu kwa wagonjwa wanaoishi na magonjwa ya figo," akasema Gavana Sakaja. Gavana huyo alibainisha kuwa kitengo kipya ni sehemu ya uwekezaji unaoendelea wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi katika huduma maalumu za afya, unaolenga kupunguza hali ambapo wagonjwa wanaenda hospitali nyingine na pia kuleta huduma bora za matibabu karibu na wananchi. Hospitali hiyo imewahimiza wagonjwa wanaohitaji huduma za matibabu maalumu ya figo kupanga miadi kupitia Kitengo cha Figo kilichotengwa kwa huduma hizo. Uzinduzi huo ni sehemu ya maboresho yanayoendelea katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, yakiwemo upanuzi wa huduma za wagonjwa mahututi, kumbi za kisasa za upasuaji, idara ya dharura iliyoboreshwa na uwezo ulioimarishwa wa uchunguzi wa magonjwa. Maboresho hayo yanadhihirisha dhamira ya Serikali ya Kaunti ya Nairobi ya kuimarisha miundombinu ya huduma za afya ya umma. Gavana Sakaja pia aliwahimiza wakazi wanaohitaji huduma za matibabu ya figo kutembelea Kitengo kipya cha Figo katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, iliyoko Kangundo Road, Umoja II. Alisema huduma hizo zinapatikana chini ya mpango wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), hatua itakayorahisisha upatikanaji wa huduma nafuu na bora za dialysis pamoja na matibabu maalumu ya magonjwa ya figo kwa wakazi wa Nairobi.

SERIKALI inaendelea kusukuma mpango wake wa kupanda miti bilioni 15 ifikapo 2032 kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kurejesha mazingira yaliyoharibiwa. Hata hivyo, wanaharakati wa mazingira wanaonya kuwa mafanikio ya mpango huo yanaweza kutatizwa na ongezeko la miradi ya maendeleo inayopendekezwa ndani ya misitu asili. Kwa mujibu wa wanamazingira, hali ya sasa inaibua kinaya. Wanasema huku serikali ikihamasisha wananchi kupanda mabilioni ya miche ya miti, sehemu nyingine za misitu inaendelea kukatwa ili kupisha ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege, nyumba za serikali na miradi mingine ya miundombinu. Rais William Ruto, ambaye kabla ya kuingia katika siasa alisomea Botania, Zoolojia na Ikolojia ya Mimea katika Chuo Kikuu cha Nairobi, amefanya uhifadhi wa mazingira kuwa mojawapo ya nguzo kuu za utawala wake. Serikali yake imeweka lengo la kupanda miti bilioni 15 ndani ya miaka kumi ili kuongeza kiwango cha misitu nchini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, tangu alipoingia madarakani mwaka 2022, serikali imelaumiwa kwa kuruhusu miradi mbalimbali inayopangwa ndani ya misitu. Hali hiyo imezua maswali kuhusu iwapo juhudi za kurejesha mazingira zinaenda sambamba na kulinda misitu ya asili ambayo imekuwepo kwa miongo mingi. Takwimu za ripoti ya hali ya uchumi zinaonyesha kuwa eneo la mashamba ya miti ya serikali liliongezeka kutoka hekari 143,900 mwaka 2021 hadi hekari 148,600 mwaka 2025. Pia kasi ya upanzi wa miti iliongezeka baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa kitaifa, huku maelfu ya hekari zikipandwa miche mipya kila mwaka. Lakini wakati huo huo, ukataji wa miti katika mashamba ya serikali ulirejelewa baada ya kuondolewa kwa marufuku ya miaka sita, ingawa baadaye mahakama ilisimamisha uamuzi huo. Kwa wanaharakati wa mazingira, changamoto kubwa si uvunaji wa miti pekee bali kutumiwa kwa misitu asili kwa miradi ya maendeleo. Wanasema kila barabara, njia ya umeme au jengo linalojengwa ndani ya msitu hupunguza uwezo wa mfumo wa ikolojia kuendelea kufanya kazi ipasavyo. Wasiwasi huo uliongezeka baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Marekebisho ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu ya mwaka 2025, ambayo inaruhusu Huduma ya Misitu Kenya (KFS) kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara, njia za umeme na miundombinu mingine ndani ya misitu ya umma. Mojawapo ya miradi iliyozua mjadala mkubwa ni barabara ya Ihithe-Ndunyu Njeru inayopangwa kupita ndani ya Msitu wa Aberdare. Ripoti za tathmini ya mazingira zinaonyesha kuwa ujenzi huo utahitaji kukatwa kwa sehemu ya msitu wa mianzi, msitu wa milimani na maeneo ya nyasi. Wanaharakati wanaonya kuwa Aberdare ni mojawapo ya vyanzo muhimu vya maji nchini, ikihudumia mabwawa ya Sasumua na Ndakaini pamoja na kuchangia uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji. Kwa sababu hiyo, Mahakama ya Mazingira ilisimamisha mradi huo kwa muda huku kesi ikiendelea kusikilizwa. Katika Jiji la Nairobi, hofu kama hiyo imejitokeza kuhusu Msitu wa Ngong Road, ambapo sehemu ya ardhi imetengwa kwa miradi inayohusiana na Uwanja wa Talanta. Wanaharakati wanasema ujenzi wa barabara ya kuingia, eneo la wakandarasi na miundombinu mingine unaweza kuendelea kugawa msitu huo katika vipande vidogo. Kadhalika, katika Msitu wa Karura, ukataji wa baadhi ya miti mapema mwaka huu uliibua maswali kutoka kwa wanaharakati. Serikali ilieleza kuwa eneo hilo linatayarishwa kwa vitalu vya miche ya miti na makazi ya muda ya vijana wa Huduma ya Kitaifa kwa Vijana (NYS) wanaoshiriki katika mpango wa kupanda miti. Katibu wa Maendeleo ya Misitu, George Tarus, amesisitiza kuwa serikali haina mpango wa kuharibu misitu asili. Alisema tayari miti takriban1.9 bilioni imepandwa chini ya mpango wa kitaifa na kwamba miradi yote inayopendekezwa ndani ya misitu lazima ifanyiwe tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kuidhinishwa. Kwa mujibu wake, lengo ni kurejesha mazingira yaliyoharibiwa katika misitu, maeneo ya malisho, mashamba na sehemu za kijani mijini, huku maendeleo muhimu yakiendelea kwa kuzingatia sheria za mazingira. Hata hivyo, wanaharakati wanasisitiza kuwa mafanikio ya mpango wa kupanda miti hayatapimwa kwa idadi ya miche iliyopandwa pekee. Wanasema kipimo kikubwa kitakuwa uwezo wa Kenya kulinda misitu yake ya kale na mifumo yake ya ikolojia dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na miradi ya maendeleo, ili juhudi za kurejesha mazingira zisiwe zinafutwa na uharibifu unaoendelea katika misitu asili.

BAADHI ya manifesto ambazo aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Amolo Odinga alitumia katika kampeni zake za urais zitakuwa sehemu ya masomo katika Chuo cha Uongozi na Utawala cha Raila Amolo Odinga kinachoanzishwa chini ya Chuo cha Serikali Kenya (KSG). Chuo hicho, kilichozinduliwa Jumanne na Rais William Ruto wakati wa maadhimisho ya miaka 100 ya KSG, kinalenga kuhifadhi na kufundisha falsafa za Raila kuhusu utawala bora, demokrasia, huduma kwa umma na maendeleo ya bara Afrika. Mkurugenzi Mkuu wa KSG, Profesa Nura Mohamed, alisema kundi la kwanza la wanafunzi linatarajiwa kuanza masomo mwezi Septemba. Alisema mtaala wa chuo hicho utajengwa juu ya nguzo tano kuu zilizotawala maisha ya kisiasa ya Raila; umoja wa Afrika, uongozi ushirikishi, utawala bora, elimu na ubunifu, pamoja na amani na haki. “Alipokuwa akiwania urais alikuwa na manifesto mbalimbali, na baadhi yake zitajumuishwa katika masomo ya chuo hiki ili maono yake yaweze kutekelezwa,” alisema. Profesa Mohamed alisema walipolinganisha manifesto ya mwisho ya Raila na Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya Kenya Kwanza, waligundua kuwa zilikuwa na mambo mengi yanayofanana. Kwa mujibu wake, masomo katika chuo hicho yatakitwa kwa kuzingatia maono ambayo Raila alikuwa nayo kwa Kenya na bara la Afrika. Mbali na masomo, chuo hicho kitakuwa na maktaba itakayopewa jina la Raila Odinga pamoja na kituo cha kuhifadhi nyaraka, hotuba, maandishi na mchango wake katika uongozi na siasa. Aidha, kutakuwa na Kituo cha Ubunifu cha Chandaria kitakachofadhiliwa na mfanyabiashara Manu Chandaria, pamoja na Kituo cha Umahiri katika Huduma kwa Wateja na Uzalishaji kitakacholenga kuboresha utendaji wa watumishi wa umma. Profesa Mohamed alisema chuo hicho kinatarajia kuwaalika viongozi mashuhuri duniani kutoa mihadhara ya uongozi, akiwemo Rais wa zamani wa Amerika Barack Obama na marais wa sasa na wa zamani kutoka mataifa mbalimbali. Alisema lengo ni kufanya Kenya kuwa kitovu cha mijadala kuhusu mustakabali wa utawala bora, huduma kwa umma na maendeleo ya Afrika. Kwa mujibu wa kijitabu kinachoelezea malengo ya chuo hicho, taasisi hiyo itakuwa kitovu cha utafiti, ushauri wa sera na ubunifu wa suluhu kwa changamoto kama ufisadi, ukosefu wa ajira, umaskini, maendeleo ya miundombinu na ugatuzi. Pia itaanzisha vituo vya uchambuzi wa sera kwa wizara, Bunge, serikali za kaunti na Mahakama, kuchapisha ripoti za utabiri wa sera na kuandaa taarifa za kila robo mwaka kuhusu uzalishaji katika utumishi wa umma. Profesa Mohamed alisema chuo hicho kitawahudumia mawaziri, makatibu, viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wachanga wanaojiandaa kuingia katika sekta ya umma na binafsi. Aliongeza kuwa madarasa ya viongozi wa ngazi za juu yatakuwa na washiriki kati ya 15 na 20 pekee ili kutoa nafasi ya mijadala ya kina kuhusu mikakati ya kubadilisha nchi za Afrika kupitia uongozi bora. Alisema pia chuo hicho kitatoa mpango wa malezi kwa viongozi vijana, ubunifu, afya ya akili kwa watumishi wa umma na kujenga hazina ya kidijitali ya maarifa kuhusu maisha na urithi wa Raila Odinga. “Urithi wa Raila utaendelea kuishi. Tumejizatiti kuhakikisha maono, ndoto na falsafa zake vinaendelea kuongoza juhudi za kuijenga Kenya na kuhamasisha Afrika,” alisema Profesa Mohamed.

KILICHOANZA kama uvumi wa ajabu sasa kimegeuka kuwa chanzo cha hofu, vurugu na vifo katika baadhi ya maeneo ya Pwani, huku polisi na wataalamu wa afya wakikanusha madai kwamba mwanaume anaweza kupoteza sehemu zake za siri baada ya kuguswa na mtu mwingine. Uvumi huo, ambao hauna msingi wa kisayansi wala kitabibu, umefanya watu wengi kuishi kwa wasiwasi. Katika visa kadhaa, watu wasio na hatia wamepigwa na umati wenye hasira baada ya kutuhumiwa kwa madai hayo, huku wahalifu wakidaiwa kutumia taharuki hiyo kuiba simu, pochi na mali nyingine. Kisa kilichotikisa wengi kilitokea Nyali, Mombasa, ambapo waumini wa dhehebu ya Jehovah Witness wanne walishambuliwa walipokuwa wakihubiri kutoka nyumba moja hadi nyingine. Umati uliwalaumu kwa kuhusika na “kupotea” kwa sehemu za siri za wanaume kabla ya polisi kuwaokoa. Baadaye, wakazi wawili, Al Amin Mgunya Johnson na Kennedy Mersyden Milimo, walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kuchochea vurugu. Milimo pia alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mmoja wa wahubiri hao. Wote walikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana. Mzee wa Mashahidi wa Yehova katika Jumba la Ufalme la Bamburi, Martin Henya, alisema madai hayo ni ya uongo na kusisitiza kuwa dhehebu hilo halihusiki kwa njia yoyote na uchawi au nguvu za kishirikina. Huku kesi hiyo ikiendelea mahakamani, familia moja Mombasa inaendelea kuomboleza baada ya John Kaleghe, mwenye umri wa miaka 24, kuuawa kwa kupigwa na umati katika Soko la Marikiti baada ya kutuhumiwa kwa madai hayo. Msemaji wa familia, Leah Mwandaghina, alisema Kaleghe alikuwa kitindamimba na tumaini la wazazi wake. Alisema familia ilimtafuta kwa siku kadhaa kabla ya kupata mwili wake katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Pwani. Kwa mujibu wake, majeraha aliyopata yalikuwa makubwa kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua. Familia pia inadai kuwa alikimbilia polisi kuomba msaada lakini hakufaulu kuokolewa kwa umati. Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Pwani imesema tayari imerekodi visa 19 vinavyohusiana na uvumi huo katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale. Watu wawili tayari wameuawa kwa kupigwa na umma. Mratibu wa DCI Pwani, Benson Kasyoki, alisema watu wote waliodai kupoteza sehemu zao za siri walifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kubainika hawakuwa na jeraha lolote wala mabadiliko ya viungo vyao. Alisema uchunguzi unaonyesha makundi ya wahalifu yanatumia uvumi huo kuwalenga watu, huku washirika wao wakiiba mali wakati umati unamzingira mtuhumiwa. Wakati huo huo, DCI imeanzisha uchunguzi wa video za CCTV na ujumbe unaosambazwa mitandaoni ili kubaini wanaochochea vurugu na kusambaza taarifa za uongo. Daktari wa mfumo wa mkojo, Dkt Omar Bin Salman wa Kliniki ya Mombasa Urology, alisema kisayansi haiwezekani kwa sehemu za siri za mwanaume kutoweka kwa kuguswa na mtu mwingine. Alifafanua kuwa mabadiliko ya muda yanayoweza kutokea hutokana na misuli ya mwili kujikaza, lakini haimaanishi kuwa kiungo kimepotea. Aliongeza kuwa kama sehemu hizo zingetoweka kweli, mgonjwa hangeweza kuenda haja ndogo na hiyo ingekuwa hali ya dharura inayohitaji matibabu ya haraka. Kwa sasa, maafisa wa usalama wanatoa wito kwa wananchi kupuuza uvumi huo, kutochukua sheria mikononi na kuripoti visa vyovyote kwa polisi.

KIFO cha Cecil Ouma baada ya hafla ya katibu wa vijana Jacob Fikirini kilifungua ukurasa ambao wengi wa Wakenya hawaufahamu kuhusu siasa za nchi. Kijana huyo alifariki baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari la afisa mkuu serikalini, lakini simulizi ya maisha yake imeibua mjadala kuhusu mtandao wa vijana wanaotumiwa kuhamasisha mikutano ya kisiasa, kulinda viongozi na wakati mwingine kuhusishwa na vurugu. Kwa wengi, vijana hao hujulikana kama "magenge" au "wahuni". Lakini ndani ya siasa, wao hujiita wahamasishaji – watu wanaoweza kukusanya mamia ya vijana kwa muda mfupi kwa mkutano, kampeni au shughuli nyingine za kisiasa. Hata hivyo, si wahamasishaji wote hufanya kazi kwa maslahi ya wanasiasa. Wapo pia wanaharakati wa kijamii wanaotumia mbinu hizo kuhamasisha wananchi kuhusu uwajibikaji, haki za kijamii na ushiriki katika uchaguzi. Mpiga picha Alans Ademba asema kazi yake inaongozwa na lengo, si fedha.

MIKUTANO ya siku 45 inaoendelea nyumbani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri, imeibuka kuwa jukwaa muhimu la kujadili mwelekeo wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kwa mujibu wa duru zinazoshiriki katika mashauriano hayo, mojawapo ya mapendekezo yanayojitokeza ni kwamba, Bw Gachagua awanie urais, isipokuwa mahakama iamue kuwa hastahili kushikilia wadhifa wa umma kutokana na kesi yake ya kupinga kuondolewa mamlakani. Mkutano huo ulianza Juni 16 na unatarajiwa kukamilika Julai 31. Katika kipindi hicho, Gachagua amekutana na wajumbe kutoka Mlima Kenya, Nairobi na jamii ya Wamaasai. Akizungumza Jumamosi alipokutana na viongozi wa Ol Jororok, Gachagua alisema atatayarisha ripoti ya mashauriano hayo na baadaye kukutana na Rais (mstaafu) Uhuru Kenyatta. “Baada ya mkutano huu kukamilika nitampelekea Uhuru Kenyatta ripoti ya maoni ya wananchi. Hatutaki kurudia makosa ya 2022 ambapo tuliongoza jamii yetu kwa misimamo tofauti,” alisema. Alieleza kuwa lengo la mkutano huo ni kusikiliza matarajio ya jamii na washirika wake kuhusu uongozi wanaotaka mwaka 2027 pamoja na masuala wanayotaka yawekwe mbele katika serikali ijayo.

IKIWA kuna jambo ambalo wachambuzi wa siasa wanakubaliana nalo, ni kwamba uchaguzi mkuu wa 2027 unatarajiwa kuwa wa gharama kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini. Kuanzia matumizi ya helikopta za kukodi, wataalamu wa kampeni, mikakati ya kidijitali hadi kampuni za tafiti za maoni, siasa zimegeuka kuwa biashara inayohitaji mabilioni ya fedha. Hali hii imezua hofu kwamba demokrasia inageuka kuwa uwanja wa matajiri na wafadhili wao pekee. Kutokana na hali hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imependekeza kanuni mpya za kudhibiti matumizi ya fedha za kampeni ili kuongeza uwajibikaji na uwazi. Chini ya mapendekezo hayo yaliyochapishwa Julai 6, 2026, mgombea urais ataruhusiwa kutumia hadi Sh4.44 bilioni katika kampeni, huku vyama vya kisiasa vinavyowasilisha wagombea kuanzia udiwani hadi urais vikipewa matumizi ya juu ya Sh17.7 bilioni. Wagombeaji wa ugavana, useneta na uwakilishi wa wanawake watatumia kati ya Sh12.3 milioni na Sh123 milioni kulingana na ukubwa wa eneo lao, huku wagombeaji wa ubunge wakiruhusiwa kutumia kati ya Sh17.5 milioni na Sh123 milioni. Wagombea udiwani watatakiwa kutumia kiwango cha juu cha kati ya Sh2.5 milioni na Sh20 milioni. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon alisema kanuni hizo zinalenga kuhakikisha fedha za kampeni zinatumika kwa uwazi na uwajibikaji. Hata hivyo, kabla ya kanuni hizo kuanza kutekelezwa, mjadala kuhusu matumizi ya fedha umechacha, hasa kufuatia kampeni za uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Rigathi Gachagua wameshutumu serikali kwa kutumia fedha nyingi na rasilimali za umma kushawishi wapigakura. “Maafisa wa serikali Ol Kalou ni wengi kuliko wapigakura. Helikopta zimejaa angani kiasi cha karibu kugongana,” alisema Bw Gachagua. Katika taarifa ya pamoja, David Maraga, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Fred Matiang’i na Edwin Sifuna walidai vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Makosa ya Uchaguzi, ikiwemo kutoa hongo kwa wapigakura na matumizi ya rasilimali za umma kisiasa. Lakini msemaji wa serikali Isaac Mwaura alitaja madai hayo kuwa ya kupotosha, huku Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah akidai ni ya uongo na propaganda. Mbali na kampeni zinazoonekana hadharani, kuna mtandao mkubwa wa wafadhili ambao hufadhili wagombeaji kwa siri licha ya sheria kuwataka kujitokeza wazi. Katika uchaguzi wa 2022, aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta aliwashawishi wafanyabiashara wa eneo la Mlima Kenya chini ya Mt Kenya Foundation kumuunga mkono Raila Odinga kupitia michango ya mabilioni ya fedha. Kwa upande mwingine, viongozi wa muungano wa upinzani wanakiri kuwa kukabiliana na nguvu za kifedha za serikali iliyoko madarakani ni changamoto kubwa. Profesa Karuti Kanyinga wa Chuo Kikuu cha Nairobi amewahi kukadiria kuwa kampeni za urais nchini hugharimu takriban Sh14 bilioni. Hata hivyo, Martha Karua anasema uchaguzi haupaswi kuamuliwa na fedha bali uadilifu na uwezo wa mgombeaji. Si mashindano ya fedha. Wakenya wanapaswa kuwachagua viongozi kwa tabia, rekodi na uwezo wao wa kuhudumia wananchi,” alisema. Aliongeza kuwa chama chake hakitakopa wala kutumia rasilimali za umma kufadhili kampeni. Nao Dkt Fred Matiang’i, Seneta Okong’o Omogeni na aliyekuwa Waziri Mithika Linturi wameeleza wasiwasi kuhusu matumizi makubwa ya fedha na helikopta katika chaguzi ndogo za hivi majuzi. Mashirika ya kutetea demokrasia yameonya kuwa sheria za kufadhili kampeni tayari zipo lakini hazitekelezwi ipasavyo. Mkurugenzi wa Centre for Multiparty Democracy (CMD), Frankline Mukwanja, amesema IEBC inapaswa kusimamia kikamilifu utoaji wa taarifa za michango na matumizi ya kampeni kwa wakati halisi pamoja na kuwaadhibu wanaokiuka sheria. Kwa upande wake, mratibu wa Elections Observation Group (ELOG), Mulle Musau, alisema Sheria ya Ufadhili wa Kampeni ya mwaka 2013 tayari inaeleza vyanzo vinavyoruhusiwa vya fedha na inawataka wagombeaji kufichua wafadhili wao. Mchambuzi wa siasa Mark Bichachi anaamini upinzani utahitaji kutumia teknolojia zaidi kuliko fedha ili kushindana na serikali, huku Profesa Gitile Naituli akisisitiza kuwa ingawa fedha ni muhimu, hazitoshi kushinda uchaguzi. Bila utekelezaji madhubuti wa sheria na uwazi kuhusu fedha za kampeni, wadau wanaonya kuwa uchaguzi wa 2027 unaweza kutawaliwa na nguvu ya fedha badala ya sera, uongozi na maslahi ya wananchi.

Chadema’s Central Zone, which covers Morogoro, Dodoma and Singida regions, announced the suspension of Mr Okola as Morogoro Regional Secretary over allegations that he breached party ethics by publicly accusing Mr Heche.

Tanzania, which provide for freedom of expression, association and citizens’ duty to uphold the Constitution.

DAR ES SALAAM: KATIKA jitihada za kuzuia uharibifu wa barabara na kuhakikisha zinapitika wakati wote, hususan kipindi cha mvua, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanzisha mpango wa Vikundi vya Jamii (Community Based Routine Maintenance) unaolenga kutunza na kuboresha zaidi ya kilomita 15,000 za barabara kupitia vikundi hivyo. Akizungumza na Daily News Digital,…

LICHA ya serikali kuanzisha vitengo vipya vya utawala nchini tangu mwaka 2023 kwa lengo la kupeleka huduma karibu na wananchi, kuimarisha usalama na kuboresha uratibu wa shughuli za serikali, uchunguzi umebaini baadhi ya vitengo hivyo bado havijaanza kufanya kazi kikamilifu. Sababu kuu zinazochelewesha utekelezaji ni ukosefu wa fedha, kuchelewa kuajiri machifu na manaibu wao, pamoja na ukosefu wa ofisi na miundombinu muhimu. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaskazini Mashariki na Bonde la Ufa, ambako vitengo vingi vilianzishwa ili kukabiliana na changamoto za usalama. Katika eneo la Kaskazini Mashariki pekee, angalau tarafa saba, kata 26 na kata ndogo 38 bado havijaanza kutoa huduma. Kaunti ya Wajir inaongoza kwa kuwa na vitengo 40 visivyofanya kazi, ikifuatiwa na Garissa ikiwa na 19 na Mandera 12. Wakazi wanasema changamoto za usalama, migawanyiko ya koo na uhaba wa watumishi zimekwamisha utekelezaji. Garissa kwa mfano, baadhi ya wakazi bado husafiri zaidi ya kilomita 150 kupata huduma muhimu kama vitambulisho vya kitaifa na vyeti vya kuzaliwa. Kamishna wa Kanda ya Kaskazini Mashariki, Bw John Otieno, hata hivyo alisema mchakato unaendelea, akibainisha kuwa machifu na manaibu wao wanaendelea kuajiriwa huku manaibu wa makamishna wa kaunti tayari wakipelekwa katika maeneo mengi mapya. Kaunti ya Turkana imeonyesha mafanikio na changamoto kwa pamoja. Vitengo vipya kama Lokichogio, Aroo, Lokiriama na Suguta vimechangia kuimarisha usalama katika baadhi ya maeneo ya mpakani, ingawa wizi wa mifugo, ukosefu wa magari ya doria na barabara mbovu bado vikitatiza utoaji wa huduma. Katika mpaka wa Kenya na Sudan Kusini, wakazi wanasema hali ya amani imeimarika tangu kuanzishwa kwa vitengo hivyo mwaka 2024, huku kamati za amani na usimamizi wa rasilimali zikisaidia kuzuia migogoro. Katika Kaunti ya Kilifi, Tarafa ya Chasimba ndiyo pekee inayokaribia kuanza kufanya kazi kikamilifu, huku maeneo mengine kama Kitsoeni na Mwakambi yakiwa bado hayana machifu wala ofisi. Hali kama hiyo inashuhudiwa Taita Taveta ambako baadhi ya maeneo yanasubiri maafisa kupelekwa licha ya mahojiano kukamilika. Kaunti za Homa Bay na Kisumu pia zina vitengo vipya ambavyo bado haviwezi kutoa huduma zote za serikali kutokana na ukosefu wa watumishi na miundombinu. Wakazi wengi bado hulazimika kusafiri hadi makao makuu ya kaunti ndogo kupata huduma za usajili wa vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na huduma za polisi. Hata hivyo, Busia, baadhi ya wakazi wanasema vitengo vipya vimepunguza gharama na muda wa kupata huduma za serikali. Lakini katika maeneo jirani ya Mumias West, vituo vipya vya polisi bado havijaanza kufanya kazi licha ya fedha kutumika kujenga miundombinu hiyo. Huko Samburu, zaidi ya miezi sita baada ya kutangazwa kwa kaunti ndogo mpya, utekelezaji bado umekwama kutokana na ukosefu wa fedha.

IRINGA: Mabadiliko ya maisha ya wanawake, wasichana na watoto mkoani Iringa yameendelea kushika kasi kupitia programu za uwezeshaji zinazolenga kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii, huku Serikali ikieleza kuwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ni msingi muhimu wa kufikia jamii yenye uwezo wa kujitegemea. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake…

RAIS William Ruto Ijumaa alizindua rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuwawezesha wafanyabiashara vijana (NYOTA), katika maeneo mbalimbali nchini kupitia mawaziri na maafisa wengine wakuu. Hatua hiyo ilionyesha mkakati mpya wa serikali wa kutumia mawaziri kufikisha sera na mipango yake moja kwa moja kwa wananchi huku ikipanua utekelezaji wa mpango huo wa kuwawezesha vijana. Rais Ruto aliongoza uzinduzi katika Uwanja wa Michezo wa Ulinzi jijini Nairobi, huku Naibu Rais Kithure Kindiki akiongoza shughuli za kaunti za Nakuru, Baringo na Nyandarua mjini Nakuru. Mkuu wa Mawaziri Waziri, Musalia Mudavadi aliongoza uzinduzi eneo la Magharibi uliohusisha Kakamega, Vihiga, Busia na Bungoma katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro. Naye Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, aliongoza uzinduzi Meru, Embu na Tharaka Nithi mjini Chuka, huku Waziri wa Ardhi, Alice Wahome, akiongoza shughuli za kaunti za Nyeri, Kirinyaga na Murang'a. Waziri wa Kazi, Alfred Mutua alisimamia uzinduzi Machakos, Makueni na Kitui mjini Kitui. Shughuli kama hizo zilifanyika pia Nanyuki, Kapenguria, Eldoret, Bomet, Malindi, Mombasa, Kisumu, Kisii pamoja na Mandera, Wajir, Garissa na Marsabit. Ingawa alikuwa Nairobi, Rais Ruto alihutubia taifa kupitia matangazo ya moja kwa moja yaliyotangazwa katika vituo vyote vya uzinduzi, jambo lililoruhusu mawaziri na viongozi wengine kuwasilisha ujumbe mmoja wa kitaifa kwa wakati mmoja. Mpango huo unaolenga kuwawezesha vijana unatoa mtaji wa kuanzisha biashara, mafunzo ya ujasiriamali pamoja na ushauri wa kitaalamu ili kuwasaidia vijana kuanzisha na kukuza biashara zinazoweza kuzalisha ajira. Zaidi ya vijana 14,000 kutoka Nairobi, Kiambu na Kajiado walihudhuria uzinduzi huo jijini Nairobi, huku uzinduzi wa wakati mmoja ukiwawezesha vijana kutoka kaunti zote 47 kushiriki bila kulazimika kusafiri umbali mrefu. Serikali ilitenga Sh5.5 bilioni kufadhili vijana 110,000 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 29 katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Kwa jumla, NYOTA inatarajiwa kuwafikia takriban vijana 820,000 kupitia ufadhili wa biashara, ukuzaji wa ujuzi na fursa za ajira. “Tunataka kuhakikisha hakuna Mkenya anayeachwa nyuma. Zamani baadhi ya maeneo na wananchi walibaki nyuma, lakini sasa tumedhamiria kila Mkenya ajivunie nchi yake. Ndiyo maana mpango huu unatekelezwa katika wadi zote 1,450 nchini,” alisema Rais Ruto. Alisema mpango huo umeundwa ili kuwapa vijana nafasi ya kushiriki katika ukuaji wa uchumi bila kujali kiwango cha elimu, hali ya kijamii au mwelekeo wao wa kisiasa. “Nataka kuwaambia vijana kuwa huu ni mpango wa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 29. Umeundwa kwa ajili ya vijana wa Kenya,” alisema. Rais alisema walengwa wakuu ni vijana ambao kwa muda mrefu wamekosa mikopo kutoka taasisi za kifedha kutokana na ukosefu wa dhamana, mtaji au mitandao ya kibiashara. Alisisitiza kuwa uteuzi wa wanufaika utaongozwa na uwazi na uwajibikaji, wala si upendeleo wa kisiasa. "Hauhitaji kuwa gavana, chifu au mtu maarufu ili kufaidika. Mpango huu ni wa uwazi na uwajibikaji, na hautaendeshwa kwa misingi ya upendeleo," alisema. Aliwataka wanufaika kuripoti mtu yeyote atakayewaitisha fedha au kuwaelekeza kuunga mkono chama fulani cha kisiasa ili wapate nafasi katika mpango huo. "Huu si mpango wa kisiasa. Ni mpango wa biashara unaolenga kuwawezesha vijana," alisisitiza. Rais pia alisema hata vijana ambao hawakumaliza masomo ya sekondari au waliosoma hadi darasa la nane watapewa nafasi sawa. "Vijana wote ni Wakenya na serikali yetu ina wajibu wa kuwajali," alisema. Mbali na mtaji, wanufaika watapatiwa mafunzo ya biashara, ushauri na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha biashara zao zinakuwa endelevu. Hatutawapa fedha pekee. Tutawafunza, tutawashauri na tutatembea nanyi hadi mfanikiwe," alisema Rais. Kwa baadhi ya wanufaika, mpango huo tayari umeanza kubadili maisha yao. Kaunti ya Bungoma, Musembe alitumia fedha hizo kufungua duka la vifaa vya kielektroniki baada ya miaka mingi ya kukosa mtaji wa kununua bidhaa. Katika Kakamega, Sonya Wembo aliwekeza fedha hizo katika ufugaji wa kuku, akisema sasa ana nafasi ya kujenga biashara itakayomwezesha kujitegemea. Huko Kitui, Masoso Kituti alifungua bucha na anasema mtaji huo umempa fursa ya kujenga chanzo cha kudumu cha mapato. Garissa, Najma alipanua biashara yake kwa kuongeza bidhaa dukani, huku Kiprono wa Eldoret akiwekeza katika kilimo cha parachichi akisema ni uwekezaji wa muda mrefu utakaomletea kipato cha baadaye. Mbali na uzinduzi wa NYOTA, shughuli za Ijumaa zilionyesha jinsi serikali ya Kenya Kwanza inavyozidi kutumia mawaziri kueneza sera zake kote nchini kwa wakati mmoja badala ya kutegemea ziara za Rais pekee.