
RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI
RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI #globaltv #raissamiasuluhuhassan #selfie
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

RAIS SAMIA AKIIBONDA SELFIE NA WANA WA BOMANG'OMBE MOSHI #globaltv #raissamiasuluhuhassan #selfie

The High Court’s Dar es Salaam Sub-Registry will on Friday rule on whether opposition Chadema chairman Tundu Lissu has a case to answer in the treason trial against him, after the prosecution closed its case yesterday after calling 17 of the 30 witnesses it had listed.

MAHAKAMA Kuu jana ilimwaamuru Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kuwalinda Mashahidi (WPA) kufika kortini leo, kueleza hatua zilizochukuliwa kuwalinda mashahidi katika kesi ya kutoweka kwa wanaharakati wanne wa Mathare. Jaji Alexander Muteti alimwamuru mkurugenzi huyo kufika binafsi kortini Agosti 18, 2026, ili kutoa maelezo kuhusu ulinzi wa mashahidi wanaohusishwa na kesi hiyo. Wanaharakati hao, Abdul Aziz Zizu, MacMillan Kiarie, Michael Oloo na Evans Oloo, walitekwa nyara Juni 20 na wanaume waliokuwa wamevalia barakoa na kuficha nyuso zao. Mawakili Abner Mango, Noordeen Khagai na Pius Oyoo waliambia mahakama kuwa walifika katika afisi za WPA lakini hawakupewa taarifa kuhusu mashahidi waliowasilisha majina yao. “Tulienda kwa afisi za WPA lakini hatukupata msaada wowote. Hatukuelezwa ikiwa mashahidi hao wamehojiwa na kuwekwa mahali salama ili wasitishwe na maafisa wa usalama,” alisema Mango. Jaji Muteti aliamuru WPA kuwalinda mashahidi na kuhakikisha wanatoa ushahidi bila kuhofia usalama wao. Mahakama pia iliagiza maafisa Brenda Akoth Opondo, Waceke Macharia na Jane Nyambura Njoroge kufika kutoa ushahidi kuhusu kutoweka kwa wanaharakati hao. Afisa wa polisi Humphrey Kaimenyi aliagizwa kuwasilisha kanda za CCTV zinazoonyesha matukio yaliyopelekea kutoweka kwao. Awali, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na Mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin waliambia mahakama kuwa wanaharakati hao “hawako mikononi mwa polisi.” Jaji Muteti alisema mahakama ina jukumu la kuhakikisha ukweli unapatikana na haki inatendeka kwa mujibu wa Katiba.

DODOMA: THE Parliamentary Committee on Social Welfare and Community Development has urged the government to increase staffing at the Occupational Safety and Health Authority (OSHA) to strengthen the protection of workers’ health, safety and welfare across the country. Committee Chairperson Hawa Chakoma made the call in Dodoma over the weekend while opening a committee meeting…

ALIYEKUWA Waziri wa Utumishi wa Umma Aisha Jumwa wikendi alimjibu vikali Waziri wa Afya Aden Duale baada ya kutoa madai ya kutokuwa na uwezo wa kusoma na kuelewa stakabadhi za Baraza la Mawaziri walipokuwa serikalini. Bi Jumwa alimshutumu Bw Duale kwa unafiki na kusema matamshi yake yalilenga kumdhalilisha kisiasa. Alisisitiza kuwa alikuwa na uwezo kamili wa kuelewa shughuli za Baraza la Mawaziri. “Nilikaa nawe katika Baraza la Mawaziri na hakuna siku yoyote ulizungumza nami isipokuwa siku moja,” akasema Bi Jumwa. Alidai Bw Duale alimkasirikia baada ya kumpeleka mmoja wa magavana wa zamani kumwona Rais William Ruto. “Siku hiyo ulipozungumza nami ulikuwa na hasira kubwa, ukiniuliza kwa nini nilimpeleka gavana huyo kwa Ruto,” akasema. Bw Duale alikuwa amemshambulia Bi Jumwa Jumamosi jijini Mombasa, akidai wakati walipokuwa Barazani alikuwa akimsaidia kusoma na kuelewa baadhi ya stakabadhi za serikali. Alisema mara kadhaa Bi Jumwa alishindwa kueleza baadhi ya masuala yaliyokuwa kwenye hati hizo, hivyo akalazimika kumsaidia. Bw Duale alitoa matamshi hayo alipokuwa akikosoa uhusiano wa Jumwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua pamoja na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Hata hivyo, Bi Jumwa alimtaka Bw Duale kuacha kujaribu kuamulia Pwani upande wa kisiasa wa kuunga mkono. “Hutatuamulia Pwani mahali pa kupigia kura. Pwani ina viongozi wake na ikiwa unafikiri Pwani haina kiongozi, mimi niko hapa kwao,” alisema. Mbunge wa EALA Falhada Iman Dekow pia alilaani matamshi ya Bw Duale, akisema tofauti za kisiasa hazifai kugeuka kuwa vita vya kibinafsi dhidi ya viongozi wanawake. Alisema kila kiongozi ana haki ya kidemokrasia kuchagua upande wa kisiasa anaounga mkono.

VURUGU zilizoshuhudiwa katika mikutano ya Linda Mwananchi Homa Bay mwishoni mwa wiki zimeibua tena kumbukumbu za migogoro mikali ya kisiasa iliyotikisa Luo Nyanza baada ya kifo cha Jaramogi Oginga Odinga, mwanasiasa mashuhuri wa eneo hilo. Kwa sasa, viongozi wa Linda Mwananchi, kundi lililojitenga na ODM, wanakabiliana vikali na mrengo unaoongozwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga. Linda Mwananchi inaongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi East Babu Owino. Kiini cha mzozo huo ni msimamo kuhusu uchaguzi wa 2027. Mrengo wa Dkt Oburu unaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto, huku upande wa Bw Orengo ukitaka ODM kusimamisha mgombea wake wa urais. Bw Orengo na washirika wake pia wanamlaumu Rais Ruto kwa kuchangia migawanyiko ndani ya ODM. Kifo cha Raila Odinga kimeacha pengo kubwa la kisiasa Nyanza, huku makundi mbalimbali yakijitokeza kuwania ushawishi katika eneo hilo. Vurugu za Homa Bay zimewakumbusha wengi tukio la Aprili 24, 1999, wakati uhasama kati ya Raila na Orengo ulifikia kilele katika harambee Ugunja, wakati huo ikiwa sehemu ya eneobunge la Ugenya. Raila, aliyekuwa akiongoza NDP, na Orengo, aliyekuwa mbunge wa Ugenya, walikuwa wameingia katika mzozo mkali wa kisiasa. Raila aliwasili kwenye harambee akiwa amevalia agbada ya Nigeria na kuandamana na vijana waliokuwa wakimshangilia kwa kaulimbiu yake ya kampeni “Amollo Tinga”. Bw Orengo naye aliwasili na kundi la vijana, hali iliyosababisha makabiliano na hatimaye vurugu. Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi na mbwa wa kunusa kuwatenganisha vijana hao. Bw Orengo alilazimika kukimbilia katika shamba la miti ambako alimshambulia Raila kwa madai ya kuwaleta watu kutoka nje ya Ugenya. “Magari mengi yalikuja Ugenya, malori yaliyojaa, matatu na watu hao hawatoki Ugenya,” akasema. Raila naye alijibu kwa kuuliza ni nani aliyemwalika Bw Orengo katika hafla hiyo. “Ni nani aliyesema naye na kumwalika katika hafla hii? Aliulizwa kama jina lake lingewekwa kwenye kadi ya mwaliko lakini akasema atafikiria,” alisema Raila. Mwaka huo huo, Raila pia alikabiliwa na upinzani mkali Kisumu kutoka kwa aliyekuwa Meya Akinyi Oile, mshirika wa kisiasa wa Rais wa zamani Daniel Moi. Uhasama wa Mabw Orengo na Raila ulianza baada ya kifo cha Jaramogi mwaka 1994 wakati wa uchaguzi wa naibu mwenyekiti wa Ford Kenya. Bw Orengo alishinda kwa kura moja, hatua iliyomkasirisha Raila na kumfanya kumpinga katika kinyang’anyiro cha uongozi wa chama. Mnamo Machi 18, 1995, uchaguzi wa uongozi wa Ford Kenya katika Uwanja wa Thika uligeuka kuwa vurugu, huku jaribio la kutaka kumuua Raila likiripotiwa. Leo, historia hiyo inaonekana kujirudia, lakini mara hii bila Raila. Bw Orengo anakabiliana na Dkt Oburu katika vita vya kuwania ushawishi wa kisiasa wa jamii ya Luo. Upande wa Orengo unaungwa mkono na Babu Owino na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, huku Dkt Oburu akiungwa mkono na Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga na Mawaziri Opiyo Wandayi na John Mbadi. Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo na Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kisumu Ruth Odinga nao wana msimamo vuguvugu na hawajaonyesha upande wanaounga mkono.

MKUTANO wa kisiasa wa Linda Mwananchi uliofanyika Homa Bay Jumapili ulifichua upande wa kaunti hiyo ambao Wakenya wengi huwa hawauoni. Picha za Homa Bay zinapowekwa mtandaoni, mara nyingi huonyesha fukwe za mchanga, vilima vya kijani, Ziwa Victoria na wanyamapori katika Mbuga ya Kitaifa ya Ruma. Lakini mbali na mandhari hayo kuna Homa Bay nyingine ambayo wakazi wanaijua vyema na hii ni barabara inayounganisha Kituo cha Biashara cha Kiabuya na ufuo wa Nyandiwa. Wakenya walipokuwa wakifuatilia mkutano huo kupitia simu, hawakusikiliza hotuba pekee bali pia walitazama mandhari katika maeneo yaliyotembelewa na Gavana James Orengo, Seneta Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino. Barabara ya Nyandiwa, ambako mkutano wa kwanza ulifanyika, ilivutia zaidi kutokana na hali yake ya vumbi na uchakavu. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliifananisha kwa kejeli na Afghanistan na Gaza. Picha kutoka video za moja kwa moja zilionyesha barabara za Suba Kusini ikiwa katika hali mbaya, huku baadhi ya maeneo yakiwa bila nguzo za umeme. Vilevile, picha moja ilionyesha Ziwa Victoria kwa mbali, huku mandhari yakiwa kame na bila miti mingi. Baadhi ya watumiaji waliita eneo hilo kwa mzaha “Mwanzo wa Hormuz”. Hata hivyo, wengine walisema hali ya barabara ni ushahidi wa miaka mingi ya kutengwa kwa eneo hilo na serikali zilizopita. Mbunge wa Suba Kaskazini, Millie Odhiambo, alikiri kuwa barabara nyingi eneo la Suba Kaskazini na Suba Kusini ziko katika hali mbaya. Bi Odhiambo alisema serikali ya Rais William Ruto imeweka lami kwenye Barabara ya Mzunguko ya Rusinga na kufungua Barabara ya Mzunguko ya Mfangano, huku Sindo-Mbito ikiwa miongoni mwa barabara nyingine zilizopangiwa kufanyiwa kazi. Gavana Gladys Wanga alisema kutengwa kwa eneo hilo kwa kiasi fulani kulitokana na ODM kuwa chama cha upinzani kwa miaka mingi. “Tuache kuwapotosha watu kwa kusema hizi ni barabara za mashambani na kwamba barabara kuu zilikuwa zimezuiwa. Unachoona hapa, isipokuwa barabara ya Homa Bay hadi Mbita na Barabara ya Mzunguko ya Rusinga, ni barabara kuu. Rais Kibaki na Waziri Mkuu Raila waliweka lami barabara ya Homa Bay hadi Mbita. Rais Uhuru Kenyatta alijenga daraja la Mbita,” akaandika kwenye ukurasa wa Facebook. Aliahidi barabara hiyo ingekarabatiwa. “Sasa tuko ndani ya Serikali Jumuishi, na barabara ya Suba itakarabatiwa chini ya mradi wa Barabara ya Mzunguko ya Ziwa Victoria. Waziri Mbadi ametia saini ili kuhakikisha inaboreshwa,” akasema. Bw Sifuna alishangaa kwa nini barabara hiyo ilikuwa katika hali mbaya ilhali iko karibu na nyumbani kwa Waziri wa Fedha John Mbadi. “Juzi tuliambiwa kwamba kwa sababu mnaunga mkono Serikali Jumuishi, barabara zote zimewekewa lami. Leo tumekula vumbi. Tumekula vumbi sawasawa,” akasema. Alisema kwamba wakazi wa Homa Bay bado hawajanufaika kikamilifu na miradi ya serikali kuu. “Hakuna tofauti kati yenu na sisi Magharibi. Bado mnasafiri kwenye barabara za vumbi kama sisi,” alisema. Baadhi ya picha zilizotengenezwa kwa AI pia zilisambaa mtandaoni, lakini Taifa Leo ilithibitisha kuwa barabara iliyoonyeshwa ni njia inayotumiwa kwa kawaida na wenye magari kutoka Kiabuya hadi Nyandiwa. Katika sehemu moja, magari hulazimika kuvuka kijito, huku magari yenye injini dhaifu yakitatizika kupanda mteremko mara baada ya kuvuka.

VURUGU zilizotokea Homa Bay Jumapili wakati wa mikutano ya kundi la Linda Mwananchi huenda zilipangwa siku kadhaa kabla, huku wanasiasa wakidaiwa kuwahamasisha vijana na kuunda mtandao wa kuratibu uvamizi. Duru kutoka kwa polisi na mahojiano na baadhi ya vijana waliohusika vilifichua kuwa mkutano wa kwanza ulifanyika Agosti 2 nyumbani kwa mwanasiasa mashuhuri, muda mfupi baada ya hafla ya kumkaribisha Mbunge wa Mwakilishi wa Kike wa Homa Bay, Joyce Osogo. Vijana hao walidaiwa kuagizwa kumzuia Gavana wa Siaya James Orengo pamoja na kikosi cha Linda Mwananchi, inayojumuisha Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, kufanya mikutano katika kaunti hiyo. Inadaiwa kila kijana aliyehusika katika fujo hizo alilipwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000. Wale waliolipwa Sh4,000 walidaiwa kusafirishwa kutoka kaunti jirani ya Migori. Siku moja kabla ya mikutano hiyo, vijana walifanya mkutano mwingine katika eneo la Lo Rateng, uliokuwa umeandaliwa na Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma. Katika video iliyosambazwa mitandaoni, Bw Kaluma aliwataka wafuasi wake kuwafukuza wanachama wa kundi pinzani aliowatuhumu kuingilia shughuli za ODM. Alisema: “Tunatoa amri sasa kwamba yeyote anayesema muhula mmoja afukuzwe.” Pia aliwataka wafuasi wake kuwatafuta wanachama wa Linda Mwananchi katika hoteli na maeneo mengine ya kulala na kuwafukuza. Muda mfupi baadaye, ripoti za uvamizi zilianza kuibuka katika maeneo mbalimbali ya Homa Bay. Vijana waliokuwa kwenye pikipiki walionekana wakiwa na panga, marungu na silaha nyingine hatari. Katika Hoteli ya Homa Bay Tourist, vijana waliingia kwa nguvu, wakawafukuza wageni na kuwashambulia wafanyakazi. Walivamia vyumba 21 na kuiba magodoro na televisheni. Pia waliharibu kanda za CCTV ili kuzuia kurekodiwa kwa matukio yaliyofuata. Baada ya hapo, vijana hao waliagizwa kukutana katika kituo cha mabasi cha Homa Bay saa 10 alfajiri Jumapili na kuweka vizuizi barabarani ili kuzuia watu wanaohusishwa na Linda Mwananchi. Mawe na vitu vingine vilitumiwa kuziba barabara, hali iliyowalazimisha wakazi kubaki nyumbani huku baadhi ya wafanyabiashara wakishindwa kufika sokoni. Mmoja wa vijana waliozungumza na Taifa Leo alisema maagizo yalipitishwa kupitia simu kutoka kwa wanasiasa na wahamasishaji wa vijana. Alidai baadhi ya vijana hutumiwa kama walinzi binafsi wa wanasiasa na hupewa silaha kabla ya maandamano. Kamishina wa Kaunti ya Homa Bay Ronald Mwiwawi alisema baadhi ya vijana walikuwa wameunganisha panga mbili kwa kuzichomelea ili kutengeneza silaha ndefu zaidi. Vurugu ziliongezeka msafara wa Bw Orengo ulipokaribia Homa Bay. Msafara huo, uliokuwa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, ulizuiwa Ndhiwa na mzunguko wa Kodoyo. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wamefunga barabara. Baadhi ya vijana waliokuwa katika msafara wa Linda Mwananchi pia walihusika katika kuwatawanya wapinzani. Magari kadhaa yalipigwa mawe na mengine kugongana. Baada ya mikutano ya Nyandiwa na Sindo, msafara ulipokuwa ukirejea Homa Bay Mjini, mapigano mengine yalizuka karibu na mzunguko wa Kodoyo. Mmoja wa vijana aliyeokolewa na wanahabari wa Taifa Leo alikuwa na majeraha makubwa shingoni, mkononi na mgongoni. Alidai alikuwa ndani ya gari lililochomwa moto. Mtu mmoja anayetajwa kama Abdi alidaiwa kuwa kiungo muhimu kati ya wanasiasa na vijana. Duru zilisema Abdi, anayetajwa kuwa kiongozi wa vijana wa ODM, ana ushawishi mkubwa na hujulikana kwa jina la “Kamanda.” Duru ziliarifu kuwa Abdi hupokea simu kutoka kwa viongozi kabla ya kuwasiliana na vijana kutoka maeneo ya Shauri Yako, Sophia, Misita na Got Rabuor. Kwa vijana wengi wasio na ajira, ahadi ya pesa za haraka imekuwa kivutio kikubwa. Baadhi yao walidaiwa kulipwa Sh2,000 baada ya kushiriki vurugu. Vurugu hizo hata ziliingia katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Homa Bay, ambako vijana walijaribu kuingia baada ya kusikia kuwa baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa wakipatiwa matibabu. Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Vincent Oduor, alisema polisi waliitwa kusaidia kudhibiti hali hiyo. Wakati huo huo, ushahidi uliokusanywa ulionyesha kuwa upande wa Linda Mwananchi pia ulikuwa umejiandaa kwa uwezekano wa makabiliano. Duru kutoka kundi hilo zilisema baadhi ya wagombea waliokuwa katika msafara walikuwa na leseni za kumiliki bunduki na walikuwa wameandaa walinzi wenye silaha. Polisi walikamata watu 15 waliodaiwa kuhusishwa na Linda Mwananchi katika Kaunti ya Kisumu na kupata silaha hatari. Watu wengine wawili walikamatwa Migori na panga tano zikapatikana. Kamanda wa Polisi wa Homa Bay Lawrence Koilem alisema watu wasiopungua 22 walikamatwa kuhusiana na vurugu hizo. Polisi pia walipata bastola aina ya Ceska iliyokuwa na risasi 13. Vurugu hizo ziliacha watu wawili, akiwemo afisa wa polisi, wakiwa wamefariki, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Magari sita yalichomwa moto na biashara kadhaa kuporwa.

KINARA wa vuguvugu la kisiasa la Linda Mwananchi Edwin Sifuna amesema wanayo katika hifadhi yao chombo cha mawasiliano anachosema kilipatikana kwa mwanamume mmoja aliyenaswa na wafuasi wa vuguvugu hilo, wakimshuku kuwa miongoni mwa waliokuwa wanaendeleza uhuni dhidi yao. Katika taarifa aliyotundika katika ukurasa wake wa Facebook, Bw Sifuna, aliye pia Seneta wa Nairobi anahadithia matukio ya Jumapili, Agosti 16, 2026 ambako msafara wao katika ziara Homa Bay ulikabiliwa na ghasia na uharibifu wa kushtua. Kufikia sasa, Kamanda wa Polisi Kaunti hiyo Lawrence Koilem amethibitisha maafa ya watu wawili, akiwemo afisa wa polisi, na majeruhi zaidi ya 45 waliokimbizwa hispitali mbali mbali. Bw Sifuna anaeleza kwenye taarifa kwamba msafara wao ulipofika eneo la Nyandiwa, wafuasi wake walimkamata mwanamume huyo na pindi alipohojiwa alijitambulisha kama afisa wa polisi. “Tulitwaa simu yake na tutaendelea kuizuilia. Kinachotushangaza ni aina ya simu zinazopigwa kwa simu hiyo, baadhi ya wapigaji wakijitambulisha kama maafisa wa ngazi za juu za serikali wanaoagiza simu hiyo irejeshwe," akasema Bw Sifuna katika taarifa. “Tunashangaa iweje simu zinazopigwa kwa chombo hicho si kutoka kwa wanafamilia wanaomtafuta mpendwa wao bali maafisa katika kitengo cha polisi.”

KANISA la SDA Lake Victoria Field liligeuka kuwa eneo la vurugu Jumapili baada ya watu waliokuwa wakitoroka makabiliano ya kisiasa Homa Bay kukimbilia humo kutafuta hifadhi. Kasisi Dan Okumu alisema mlinzi wa kanisa alifungua lango kuruhusu waliokuwa wakitoroka uvamizi kuingia, lakini vijana wenye silaha waliwafuata na kuwashambulia. “Inajulikana kwamba kanisa ni mahali ambapo watu hukimbilia kupata hifadhi. Hilo ndilo tulilokuwa tunajaribu kufanya,” akasema. Bw Okumu alisema alishuhudia watu waliokuwa ndani ya gari wakikatwa kwa mapanga. Mwanamke mmoja alifanikiwa kutoroka, lakini dereva alibaki chini akishambuliwa. Gari hilo lilichomwa moto kwenye lango la kanisa kabla ya vijana kurusha mawe kwenye afisi za SDA, kuvunja madirisha na kuharibu magari. Mkuu wa SDA Lake Victoria Field, Samson Okwach, alisema baadhi ya wafanyakazi walijeruhiwa na kulaani mashambulizi hayo. Katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Homa Bay, watu 46 walitibiwa baada ya vurugu hizo. Mkurugenzi Mkuu Vincent Oduor alisema wagonjwa saba walikuwa katika hali mbaya, mmoja akahamishwa hadi hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu. Polisi mmoja alipigwa kichwani, watu wanne walikuwa na majeraha ya risasi miguuni, huku wengi wakitibiwa majeraha ya mapanga na visu. “Mwanamke mmoja alifariki baada ya kugongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi,” alisema Dkt Oduor.

DAR ES SALAAM; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeteketeza tani 39 za bidhaa za chakula zisizokidhi matakwa ya viwango, zenye thamani ya takribani Sh milioni 149. Tukio hilo limefanyika leo, Agosti 17, 2026, Mbezi Gongoni, Wilaya ya Mkuranga, Pwani, baada ya bidhaa hizo kubainika kupitia ukaguzi uliofanyika katika kipindi…

Chadema national chairman Tundu Lissu has asked the High Court to find that he has no case to answer in a treason charge, urging it to acquit him and order the government to pay him compensation. Mr Lissu submitted on Monday, August 17, 2026, after the prosecution closed its case having called 17 of its 30 listed witnesses. Mr Lissu faces one count of treason under Section 39(2)(d) of the Penal Code, arising from remarks he allegedly made regarding the 2025 General Election. The prosecution alleges that on April 3, 2025, in Dar es Salaam, Mr Lissu incited the public to prevent the 2025 General Election by uttering and publishing remarks aimed at pressuring the country’s top government leader. He allegedly said: “If they say this position amounts to rebellion, it is true... because we say we will stop the election, we will mobilise rebellion, that is how to bring change... so we are going to make trouble... especially, we are really going to disrupt this election... we are going to make serious trouble...” The case is before a three-judge bench of the High Court’s Dar es Salaam Registry led by Judge Dunstan Ndunguru, alongside Judges James Karayemaha and Ferdinand Kiwonde. When the case came up on Monday, State Attorney Ajuaye Nzegeli told the court that after reviewing the evidence of the remaining witnesses, the prosecution had concluded that the presented evidence was sufficient. “We therefore wish to inform this honourable court that the prosecution is closing its case after calling 17 witnesses,” said State Attorney Nzegeli. Following the closure, the prosecution requested to make submissions on whether the evidence established a case requiring Mr Lissu to enter his defence. Mr Lissu supported the request, and the court permitted both sides to submit, with Mr Lissu presenting first before the prosecution responds. Lissu’s submissions In his submissions, Mr Lissu argued that evidence from the 17 prosecution witnesses failed to establish a prima facie case against him. He referred to decisions of the East African Court of Appeal in Grey Likungu Mataka and Others v Republic and Hatibu Gandhi and Others. Mr Lissu said the authorities established three elements for proving treason: that the accused owes allegiance to the United Republic; that the accused had treasonable intent; and that the intent was manifested through writing or an overt act. He said allegiance was undisputed as he is a Tanzanian citizen. The central issues, he argued, were whether he had treasonable intent and whether it was manifested through writing or an overt act. Referring to the Grey Likungu case, Mr Lissu said former Chief Justice Francis Nyalali emphasised that a treason conviction requires proof of an overt act, treasonable intent, and allegiance to the United Republic. Citing the Hatibu Gandhi case, Mr Lissu noted the Court of Appeal held that mere words do not constitute an overt act unless they describe an act of treason, such as directing how to overthrow the government rather than merely stating a desire to do so. He added that the court clarified that mere words spoken by a single accused person could not amount to an overt act, unlike statements involving multiple persons establishing a conspiracy. Mr Lissu argued that the section under which he was charged concerned inciting people to call upon the government, Parliament, or the judiciary to take action, which must be proved through writing or an overt act. He argued that none of the alleged statements mentioned the government, Parliament, or the courts. “Of all the 17 witnesses, everyone who spoke about those words, I asked them: Is the government mentioned there? It is not,” he said, noting the term covers the Union government, the Revolutionary Government of Zanzibar, and local authorities. He said no witness confirmed he had mentioned the President, Prime Minister, or regional commissioners. Mr Lissu further argued that elections are administered by the electoral commission, not the government, meaning the government could not be threatened by an attempt to prevent an election. He added that statements about stopping an election were not criminalised under the 2025 Presidential, Parliamentary and Councillors’ Elections Act, the Penal Code, or other laws. “Therefore, the proof of treason as established in the Grey and Gandhi cases is absent and, in fact, there is no evidence of an intention to commit any offence under the laws applicable in Tanzania,” he said. Mr Lissu stressed he was the sole accused, arguing that under the Gandhi precedent, mere words do not constitute treason for a single accused person. “So, honourable judges, if the evidence presented has failed to prove a case of committing treason, what am I supposed to defend myself against? On that ground alone, I have no case to answer,” he said. Jambo TV video evidence On allegations that his remarks were published on Jambo TV, Mr Lissu said the prosecution should have produced the video recordings and forensic examination reports. He noted that none of the 17 witnesses presented the footage in court despite prosecution promises to tender nine documents, including video clips and forensic reports. Consequently, Lissu said, witnesses only testified to seeing videos without actual footage being admitted into evidence. Mr Lissu noted that of the 17 witnesses, only the 17th was present at the meeting where he allegedly spoke, describing the other 16 as hearsay witnesses. He added that the witness testified that he and five colleagues recorded and published the video, proving Mr Lissu himself did not publish it. Regarding event organisation, Mr Lissu said the witness admitted the invitation was issued by Chadema information officer Brenda Lupia and that Mr Lissu was not seen making preparations. Mr Lissu prayed for an acquittal without being called to enter his defence. He asked the court to deliver its decision on Monday to spare him returning to prison, with the written ruling to follow later. Mr Lissu also requested compensation from the government, stating he had spent 496 days in remand over charges he termed legally baseless.

SIKU ya kufa kwa nyani miti yote huteleza. Sijui kwa nini napenda sana kuwaona nyani wakiteleza mitini na kuanguka pu! Kufa kwao sijutii, nashabikia. Wakati mwingine mimi hujiuliza: Baada ya nyani huyo kufa, mwingine atakayefuata ni nani? Hata kabla sijajijibu, wanaanguka wengi, shughuli nzima inageuka starehe ya kuketi kitako kujionea wakianguka na kufa. Katika muktadha wa siasa za Kenya, nyani tayari wameanza kuteleza, na wanaanguka. Licha ya ujanja wao wote wameshindwa kujishikilia mitini. Ajabu! Je, unakumbuka Mbunge wa Gatundu Kaskazini, Gabriel Kagombe, aliyekuwa mtetezi wa Kasongo? Inaonekana amevunjikia mguu malishoni na sasa amerejea zizini kusaidiwa. Je, unakumbuka Mbunge Mwakilishi wa Kike Lamu, Monicah Marubu Muthoni, enzi akitumia kipaza sauti kujaribu kuwanyamazisha wasiompenda Kasongo? Huyo pia amemtoroka na kuingia upinzani. Nakuhakikishia kuwa wengine wengi watahama kutoka serikalini wakitoa visingizio vya ajabu kwa nini wanaamini Kasongo na Kenya Kwanza yake hawafai kuongoza nchi. Hata kabla hujaanza kusherehekea kuhama huko, na labda kuona taswira ya nyani akianguka kutoka mtini, jiulize nyani anayeanguka ni nani hapa. Je, ni Kasongo au hao wanaomtoroka? Labda ni wote wawili, Kasongo na watoro hao? Wengi wanaojiondoa serikalini wakati huu, hasa wanaotokea mlimani au walio na asili ya huko, wanadhani hatugundui ujanja wao. Wajinga waliisha Kenya! Wamejua kwamba kwao Kasongo ni sawa na nyama ya nguruwe Saudia, hainunuliki hata ukiinadi namna gani. Ndiposa wanamtoroka ili waweze kuchaguliwa, kisha warudiane naye. Ujanja wa ndoa ya kisiasa eti. Jiulize hivi, wakimtoroka Kasongo wanamnyima kura ngapi? Kumtoroka kutasababisha ashindwe uchaguzini? Wamemtoroka ili wajinusuru kisiasa kwani kimbunga kinachofagia wafuasi wa Kasongo huko Mlimani hakimsazi yeyote. Pale Mlimani kumla nguruwe ni haramu, na kila atakayethubutu atajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe kama ilivyo kawaida ya hayawani huyo. Swali kuu linaloibuka kila tunaposikia mtu amemtoroka Kasongo ni, kwa nini wakati huu? Labda baada ya kushiba minofu ya Kenya Kwanza? Mifupa ya kwetu wataiweza? Hivi wanadhani mpigakura ana akili za ngiri, yaani za kusahau tabia na mienendo yao? Utaona maajabu kati ya sasa na uchaguzi mkuu ujao. Watu watasalitiana, kisa na maana kuchaguliwa. Kwa kuogopa kuanguka kama nyani, wengi watatoa visingizo vya kubadili misimamo ya kisiasa, hata wamtoroke Kasongo. Usidanganyike. Kumbuka tabia za kinyonga ni zile zile za kubadili rangi kutegemea mazingira aliyomo. Nyani wa kuanguka na waanguke kishenzi! Miti na iteleze kabisa! - Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika ([email protected])

ZAIDI ya nguruwe 1,000 wamefariki katika Kaunti ya Kiambu kutokana na ugonjwa wa African Swine Fever (ASF), huku Serikali ikiongeza juhudi za kudhibiti kuenea kwa homa hiyo ya nguruwe ambayo imeendelea kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji maeneo mbalimbali nchini. Kurugenzi ya Huduma za Mifugo Nchini, ndiyo Directorate of Veterinary Services (DVS) imeagiza idara za mifugo katika kaunti kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa, usalama wa mashamba, kudhibiti uhamishaji wa nguruwe na kuzindua kikosi cha kukabiliana haraka na milipuko. Milipuko mikubwa imeripotiwa katika kaunti za Tharaka-Nithi, Kiambu, Busia, Embu, Kakamega, Siaya na Migori, miongoni mwa nyingine, na kusababisha vifo vya nguruwe wengi na hasara za kiuchumi kwa wafugaji. Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo katika Idara ya Maendeleo ya Mifugo chini ya Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Dkt Allan Azegele, alisema ASF ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi na kuenea haraka miongoni mwa nguruwe, huku kiwango cha vifo kikifikia asilimia 70 kulingana na aina ya virusi, umri na uwezo wa mnyama kukabiliana na ugonjwa huo. “Nguruwe wakubwa na wadogo wanaweza kuathirika pakubwa,” alisema kwenye mahojiano na ‘Akilimali Dijitali’. Takwimu za Kenya Animal Biosurveillance System (KABS) na Laboratory Information Management System (LIMS) za Januari hadi Juni 2026 zinaonyesha kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika maeneo kadhaa. Tharaka-Nithi ilirekodi visa 108 vya maambukizi na vifo 97 kati ya Januari 5 na 11, sawa na kiwango cha vifo cha karibu asilimia 90. Embu ilirekodi visa vitatu na kifo kimoja kati ya Mei 18 na 24. [caption id="attachment_191232" align="aligncenter" width="300"] Nguruwe wakisherehekea malisho. Picha|Sammy Waweru[/caption] Hata hivyo, mlipuko mkubwa zaidi umeshuhudiwa Kiambu, ambako zaidi ya mashamba 20 eneo la Juja, Thika na Ruiru yameathirika tangu katikati mwa Mei. Karibu nguruwe 1,470 wameripotiwa kuugua au kufa, huku baadhi ya wafugaji wakipoteza hadi asilimia 100 ya nguruwe. Kwenye mahojiano Dkt Azegele alithibitisha kuwa ASF haiambukizwi kwa binadamu wala kuwa tishio kwa afya ya umma. “Nyama ya nguruwe iliyokaguliwa na kuthibitishwa na mkaguzi aliyeidhinishwa ni salama kwa matumizi,” alisema. Hata hivyo, Homa hiyo ya nguruwe inaweza kuangamiza mifugo yote na kuvuruga biashara, kuwaacha wafugaji bila mapato. Hasara za kiuchumi zinazohusishwa na ASF nchini hukadiriwa kufikia Dola 7 milioni (Sh905.1 milioni) kila mwaka. Kwa sasa hakuna tiba wala chanjo inayopatikana kibiashara dhidi ya aina za virusi vya ASF zinazosambaa nchini. Azegele alisema kukua haraka kwa virusi kunafanya iwe vigumu kutengeneza chanjo inayofaa kwa aina zote. Aidha, aliwataka wafugaji kuimarisha usalama wa mashamba kwa kudhibiti watu, wanyama, magari na vifaa vinavyoingia katika makao ya nguruwe. “Nguruwe wapya wanapaswa kununuliwa kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika, kutengwa na kufuatiliwa kabla ya kuunganishwa na wengine,” alishauri afisa huyo. Magari yanayoingia na kutoka mashambani yanapaswa kusafishwa kwa dawa, huku sehemu za kuoshea miguu zikiwekwa karibu na makazi ya nguruwe. Wafugaji, pia, wameonywa dhidi ya kuwapa nguruwe mabaki ya chakula ambayo hayajatibiwa. [caption id="attachment_191233" align="aligncenter" width="300"] Zaidi ya nguruwe 1,000 wamefariki Kaunti ya Kiambu kutokana na Homa ya nguruwe. Picha|Sammy Waweru[/caption] Dkt Azegele alisema mabaki ya chakula kutoka kwa hoteli yanapaswa kupikwa vizuri kabla ya kupewa nguruwe, huku akisema kupika mabaki hayo kwa kutumia karibu asilimia mbili ya soda ash au magadi soda kunaweza kusaidia kuangamiza virusi. Serikali pia imewataka wafugaji kuripoti mara moja dalili zisizo za kawaida au vifo vya ghafla vya nguruwe kwa maafisa wa mifugo. Katika maeneo yaliyoathirika, wakulima wanapaswa kufuata masharti ya karantini na udhibiti wa uhamishaji wa wanyama. Mizoga ya nguruwe inapaswa kutupwa kwa usalama na uangalifu chini ya mwongozo wa maafisa wa mifugo ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Homa ya nguruwe, ASF. Dkt Azegele alisema idara za mifugo katika kaunti zimeagizwa kuongeza kasi ya ukaguzi katika masoko ya mifugo, machinjioni na maeneo ya kuuza nyama za nguruwe. Hali kadhalika, zitahakikisha visa vinavyoshukiwa vinathibitishwa kwenye maabara kwa haraka, mienendo ya wanyama inafuatiliwa na wafugaji kuelimishwa kuhusu dalili za ugonjwa huo. Virusi vinavyosambaa nchini ni vya Genotype IX, aina ambayo tafiti zimeonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kusababisha maradhi mbaya na vifo vingi. [caption id="attachment_191234" align="aligncenter" width="300"] Nguruwe wakiwa kwenye zizi safi. Picha|Sammy Waweru[/caption] Wasiwasi zaidi umeibuliwa na uwepo wa nguruwe wanaobeba virusi bila kuonyesha dalili. Utafiti ulibaini virusi vya ASF katika tishu za viungo vya ndani vya asilimia 15.9 ya nguruwe walioonekana kuwa na afya katika eneo la mpaka wa Kenya na Uganda. Serikali imezindua mfumo wa kidijitali kusajili mifugo nchini unaojulikana kama Animal Identification and Traceability System (ANITRAC), utakaosaidia kutambua wanyama na wamiliki wao, pamoja na kufuatilia historia yao, magonjwa na mienendo tangu kuzaliwa hadi kuchinjwa, kusafirishwa nje au kufariki. Kwa sasa, asasi mbalimbali za mifugo zimeagizwa kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo yaliyo katika hatari kubwa, hasa Kiambu, Tharaka-Nithi na Embu, pamoja na maeneo ya mipakani. Kenya inakadiriwa kuwa na takriban nguruwe 800,000.

WAANDISHI wawili wa habari walijeruhiwa na biashara kusitishwa katika Mji wa Homa Bay Jumapili huku mvutano ukizuka kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi. Waandishi wa AFP Fred Ooko na Brian Ongoro walishambuliwa karibu saa tatu asubuhi walipokuwa wakiripoti matukio katika mji huo. Wawili hao walisema walivamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha za kienyeji. Vitambulisho vyao vya kazi, leseni za udereva, kamera na mali nyingine zilichukuliwa. Bw Ooko alisema alibururwa barabarani na kupigwa kwa marungu kabla ya mhudumu wa bodaboda aliyemfahamu kuingilia kati na kumsaidia kutoroka hadi Olare. “Mwenzangu Brian Ongoro pia alipigwa. Alipoteza simu na kamera. Leseni yangu, kitambulisho cha kazi na vitu vingine vilichukuliwa,” akasema. [caption id="attachment_191227" align="alignnone" width="1600"] Vioo vya magari vilivyovunjwa vyatapakaa katika barabara za Homa Bay wakati wahuni walipokabili msafara wa Linda Mwananchi. Picha|George Odiwuor[/caption] Mji wa Homa Bay ulikuwa kama eneo lisiloweza kufikika baada ya vijana kufunga barabara kadhaa kwa mawe na magogo, huku wengine wakiwasha moto. Biashara zilisitishwa huku maduka na baadhi ya maeneo ya ibada yakifungwa. Msafara wa Linda Mwananchi uliokuwa ukielekea Homa Bay ulilazimika kubadili njia baada ya baadhi ya barabara kuzuiwa. Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji na kufungua barabara. Hapo awali, polisi walikamata washukiwa 15 wa genge la uhalifu katika Kaunti ya Kisumu na kuwapokonya mapanga, visu, kamba, marungu na silaha nyingine. Polisi walisema washukiwa hao walikuwa wakielekea Homa Bay kwa magari matatu. Mmoja wao, Oliver Jaoko almaarufu Oliveti, anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lakini alitoroka wakati wa operesheni. Washukiwa hao 15 wamewekwa chini ya ulinzi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

ZANZIBAR: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) and Namibia’s ruling party, SWAPO are seeking to deepen their longstanding ties through expanded leadership training for youth and women, as well as stronger cooperation between the two political parties. The commitment was made during talks between CCM Secretary General, Ambassador Dr Asha-Rose Migiro, and her SWAPO counterpart, Ms Sophia…

MBEYA; Serikali imewekeza takribani Sh bilioni 11 katika ujenzi wa Kituo cha Saratani cha Ocean Road (ORCI) Mbeya, kinacholenga kusogeza huduma za uchunguzi na matibabu ya saratani karibu na wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk Diwani Msemo, amesema kukamilika kwa kituo hicho kutapunguza mzigo kwa wagonjwa wanaolazimika kusafiri…

The prosecution has closed its case in the treason trial facing Chadema national chairman Tundu Lissu after calling 17 of the 30 witnesses it had listed.

MBUNGE wa Wundanyi, Danson Mwashako, amefichua kwa mara ya kwanza sababu iliyomfanya kujiuzulu kutoka kwenye vuguvugu la wabunge wa Pwani (CPG), akisema alishinikizwa kukihama chama cha Wiper kinachoongozwa na Bw Kalonzo Musyoka na upinzani na kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza. Bw Mwashako, anayelenga kuwania kiti cha ugavana wa Taita Taveta katika uchaguzi mkuu wa 2027 kupitia chama cha Wiper, alisema alipewa sharti la kujiunga na serikali au kujiondoa kwenye uwenyekiti wa CPG. Hata hivyo, Mbunge huyo ambaye anahudumu kwa muhula wa pili alisema aliamua kubaki katika upinzani akisema uaminifu wake kwa Wiper na msimamo wa kisiasa wa wafuasi wake ulikuwa muhimu kuliko nafasi ya uongozi katika kundi la wabunge wa Pwani. “Nilichaguliwa kupitia tiketi ya Wiper mwaka wa 2017 na 2022, nikiwa kwenye chama hiki nahisi niko nyumbani kwangu. Hivi majuzi wamekuwa wakinishawishi kila siku nijiunge na serikali, lakini nimekataa. Hata wamenitishia, lakini nilisimama imara,” alifichua kwenye mkutano wa kisiasa huko Kakuyuni. Bw Mwashako alisema shinikizo liliongezeka baada ya baadhi ya viongozi wa Pwani kuanza kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza, huku wengine wakimuuliza kwa nini hakutaka kujiunga nao. Alisema hata aliahidiwa msaada wa kifedha wa kugharamia kampeni zake za ugavana iwapo angehama Wiper na kujiunga na Kenya Kwanza. “Nililikataa hata hizo pesa zao. Nilikuwa mwenyekiti wa CPG kwa miaka mitatu, lakini Januari mwaka huu nikaamua kujiuzulu kwa sababu ya shinikizo. Niliambiwa ili niendelee kuwa mwenyekiti nilazima kuhama Wiper. Nikaamua kujiuzulu,” alisema. Nafasi yake ilichukuliwa na mwakilishi wa wanawake wa Kilifi, Getrude Mbeyu. CPG ilianzishwa zaidi ya miongo miwili iliyopita kama jukwaa la viongozi waliochaguliwa kutoka Pwani kushirikiana kutetea maslahi ya eneo hilo, yakiwemo maendeleo na mgao wa rasilimali za kitaifa. Bw Mwashako alisema uamuzi wake wa kubaki upinzani ni kidemokrasia akiongeza kuwa wanasiasa wana haki ya kuwa na misimamo tofauti. “Kenya ni nchi ya kidemokrasia. Hakuna mtu anayepaswa kulazimishwa kujiunga na serikali,” alisema. Alitoa mfano namna alitumwa na chama chake kwenda kumshawishi aliyekuwa Waziri wa Jinsia, Bi Aisha Jumwa, kujiunga na Wiper baada ya kuhama kwenye chama tawala cha UDA. “Bi Jumwa alipoondoka UDA, walinituma nimshawishi kwa maneno matamu,” alisema. Kauli yake inajiri wakati viongozi wanaomuunga mkono Rais William Ruto wakiongeza juhudi za kuimarisha ushawishi wao Pwani kuelekea uchaguzi wa 2027. Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro hivi majuzi alimtaja Bw Mwashako kama mmoja wa viongozi wachache wa Pwani ambao bado wako katika upinzani. “Juzi tulikutana kama wabunge na magavana wote wa Pwani huko Mombasa na tukakubaliana kushirikiana na Rais Ruto. Imebakia mbunge mmoja tu, Bw Mwashako, ambaye bado yuko upande wa upinzani,” alisema. Bw Mwashako amekuwa akijiunga na kampeni za kisiasa za Linda Mwananchi inayohusishwa na viongozi wa upinzani Rigathi Gachagua na Bw Musyoka. Msimamo wa Bw Mwashako umeifanya kaunti ya Taita Taveta kuwa baadhi ya maeneo muhimu ya ushindani kati ya serikali na upinzani. Alisema anataka kuwa gavana ili kushughulikia changamoto zinazowakabili wakazi, zikiwemo uhaba wa maji, huduma za afya, elimu, kilimo na mzozo wa muda mrefu kuhusu mgao wa mapato yanayotokana na Hifadhi za kitaifa ya Wanyamapori zaTsavo. Bw Mwashako pia ameikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa kutotimiza baadhi ya ahadi ilizowapa wakazi wa Pwani, akisema kujiunga na serikali kungeathiri uwezo wake wa kuiwajibisha.

TABORA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) has expressed satisfaction with the implementation of 13 development projects worth 4.5bn/- in Tabora Region, citing quality work and value for money. Presenting a report by the Political Committee on the implementation of the CCM Election Manifesto (2025– 2030), Tabora Regional CCM Secretary Wilson Khambaku said the committee had inspected…

MBUNGE wa Aldai, Marianne Kitany amewataka viongozi wa UDA Bonde la Ufa kukosa kulumbana huku akisisitiza yupo tayari kumenyana na mgombeaji yeyote anayesaka ubunge. Bi Keitany amesema kuwa rekodi yake ya maendeleo iko wazi na kwamba yupo tayari kumenyana na kiongozi yeyote lakini akasisitiza ubabe unaoendelea bondeni utatatiza kuchaguliwa kwa Rais William Ruto. “Siasa haihusu tena kulumbana na kutusiana, inahusu kazi ambayo umefanya. Mimi naamini kwamba nitachaguliwa tena Aldai kwa sababu ya kazi ambayo nimefanya na inaonekana,” akasema Bi Kitany. Mbunge huyo alisema yupo tayari kuwania mchujo wa UDA na mgombeaji yeyote ambaye anamezea mate kiti chake kupitia chama hicho. “Saa hii wapinzani wangu wametoroka wote. Gavana wa sasa na mbunge wa zamani walikuwa wamesema watanipinga lakini sasa wamehepa hawana nia ya kuwania kiti hiki tena,” akasema Bi Kitany. “Mimi niko UDA na siendi mahali popote na iwapo wanata kurudi kuwania basi niko tayari kupambana nao. Nikishindwa kwenye mchujo, sitaenda mahali popote, nitasalia tu UDA,” akaongeza. Bi Keitany aliorodheshwa na TIFA kama mbunge ambaye ana utendakazi bora zaidi kati ya wabunge wanawake baada ya Naisula Lesuda wa Samburu Magharibi. Bw Sang’ wiki jana alitangaza kuwa amejiondoa katika kiny’anganyiro cha ubunge baada ya kushauriana na Rais William Ruto na akimaliza muhula wake wa pili kama gavana, atakwea ngazi na kushiriki siasa za kitaifa. Mbunge huyo anayehudumu muhula wa kwanza alimkashifu Bw Sang’ akisema utendakazi wake ni duni na hata iwapo angewania kiti hicho, hangeenda mahala popote. “Hospitali kadhaa hazifanyi kazi, hatuna mochari ya umma inayofanya kazi. Gavana mwenyewe ana shule za chekechea ambazo bado zimejengwa kwa udongo na hata bado tunayachota maji mtoni,” akasema. “Mengi ambayo yametimizwa yanatokana na miradi ambayo imeanzishwa na serikali kuu. Hata sasa tunakuza miwa na kuwasilisha kiwanda cha Kibos,” akasema. Gavana Sang’ alisema kuwa hana nia ya kuwania kiti hicho cha ubunge na atamakinikia siasa za kitaifa. “Nina hiari kuwania cheo cha kisiasa na nilikuwa niwanie useneta au niwanie ubunge Aldai. Hiari hizi ni muhimu lakini baada ya kushauriana na Rais aliniambia nimakinikie kuchaguliwa kwake 2027. Kwa hivyo, nitakuwa nashiriki siasa za kitaifa wala sitagombea cheo chochote cha kisiasa,” akasema Bw Sang’. Mwaka jana, Bw Sang alitangaza kuwa ifikiapo 2027 atakuwa na umri wa miaka 42 ambayo ni ya chini zaidi kwa mwanasiasa kustaafu. Hii ndiyo maana sasa alikuwa akilenga kiti cha ubunge wa Aldai. Bi Kitany alitaja kuwekwa lami kwa baadhi ya barabara, kuimarisha taasisi za elimu na kujengwa kwa masoko ya kisasa ambayo yamesaidia kuimarisha biashara katika eneobunge hilo.

The CRDB Bank International Marathon has evolved from a sporting event into a major social impact initiative, raising more than Sh5 billion since its launch in 2020 to support healthcare, youth empowerment and community development across Tanzania.

SERIKALI inapanga mikakati ya kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za ukame huku kipindi kirefu cha kukosekana kwa mvua kikitishia uzalishaji wa mahindi katika baadhi ya maeneo nchini. Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe alisema serikali itawasaidia wakulima walioathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuweka mikakati ya kuhakikisha usalama wa chakula nchini. Bw Kagwe alisema hayo baada ya kutembelea na kutathmini hali ya kilimo katika kaunti za Eldoret, Nandi na Trans Nzoia, ambako alitambua athari za ukame kwa uzalishaji wa mahindi. Aliwahakikishia Wakenya kuwa nchi haitakabiliwa na uhaba wa chakula licha ya changamoto zinazowakumba wakulima. “Hatutaruhusu Wakenya kuteseka na kulemewa na njaa kutokana na hali ya hewa iliyopo sasa,” akasema. Waziri huyo pia alionya dhidi ya biashara ya mbegu bandia akisema inazorotesha uzalishaji wa kilimo na kusababisha wakulima kupata hasara. Alisema baadhi ya wakulima hugundua kuwa walinunua mbegu bandia miezi mitano hadi sita baada ya kupanda, wakati mimea yao inaposhindwa kustawi. Aliagiza vyombo vya usalama kuongeza juhudi za kukabiliana na wafanyabiashara wa mbegu hizo na akawataka wabunge kuunga mkono sheria itakayofanya uuzaji wa mbegu bandia kuwa uhalifu wa kiuchumi. Wakulima walishauriwa kununua mbegu zilizoidhinishwa kutoka taasisi zinazotambulika kama Kampuni ya Mbegu (KSC) na Kampuni inayohusika na Utafiti kuhusu Mbegu za Kisasa (KALRO). Mkurugenzi Mkuu wa KSC Sammy Chepsiror alisema kuna akiba ya kutosha ya mbegu nchini. Alisema mavuno ya mahindi mwaka jana yalifikia karibu magunia milioni 70 ya kilo 90.

WAZIRI wa Madini, Hassan Ali Joho amepata afueni baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali ombi la kutaka atangazwe kuwa hafai kushikilia wadhifa wa umma kutokana na madai ya kutotii amri ya mahakama alipokuwa Gavana wa Mombasa. Kesi hiyo iliwasilishwa na wafanyabiashara Ashok Labshanker Doshi na Pratibha Ashok Doshi baada ya Bw Joho kupatikana na hatia ya kudharau amri ya mahakama na kuhukumiwa mwaka 2021. Doshi walitaka mahakama itamke kuwa Bw Joho alikiuka masharti ya Katiba kuhusu uongozi na uadilifu na kumzuia kabisa kushikilia wadhifa wowote wa umma au Serikali. Mzozo huo ulitokana na kesi ya ardhi kuhusu kipande cha ardhi cha ekari mbili huko Changamwe. Mnamo Mei 2019, maafisa wa Kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Bw Joho walibomoa ukuta wa uzio uliokuwa kwenye ardhi hiyo iliyokuwa na mgogoro. Serikali ya Kaunti ilidai kuwa ardhi hiyo ilikuwa mali ya shule ya eneo hilo, huku akina Doshi wakisisitiza kuwa ilikuwa mali yao binafsi na ilikuwa imelindwa na amri ya mahakama. Ubomoaji huo ulizua mzozo , ambapo Mahakama ya Mazingira na Ardhi mnamo Februari 12, 2020, ilimpata Bw Joho na hatia ya kutotii amri ya mahakama.

KIONGOZI wa Wiper, Kalonzo Musyoka amemtaka Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo kujiuzulu, akishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti uhuni wa kisiasa. Bw Musyoka pia alidai kuwa ukosefu wa usalama unaoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ni sehemu ya mpango wa kuunda mazingira yatakayotumiwa kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao. “Wahuni wanaeneza hofu na hatuwezi kufuata mkondo huo. Katibu Omollo lazima ajiuzulu kwa sababu mkuu wake amekataa kumtimua ilhali kuna visa vya ukosefu wa usalama kila mahali,” akasema Bw Musyoka alipokuwa akizungumza katika Kanisa la Reedemed Gospel Kithimani, Kaunti ya Machakos. Alishangaa kwa nini vitendo vya kihuni vinaendelea licha ya Rais William Ruto kutoa hakikisho hapo awali kwamba serikali ilikuwa imemaliza tatizo hilo. Bw Musyoka alitaja ghasia zilizoshuhudiwa Homa Bay Jumapili, ambapo waandishi wawili wa habari walijeruhiwa na biashara kufungwa kuelekea mkutano wa Linda Mwananchi. Pia alirejelea vurugu zilizotokea katika eneobunge la Rongai Kaunti ya Nakuru Jumamosi, ambapo msafara wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ulipigwa mawe na mikutano ya kisiasa kuvurugwa. Bw Musyoka pia alielekeza lawama zake kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), akisema Wakenya wanafuatilia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. “IEBC inapaswa kuwaruhusu Wakenya kuwachagua viongozi ambao hawajatwaliwa na serikali. Tulisema hatuwezi kuelekea katika uchaguzi ujao tukiwa na Smartmatic kama kampuni inayotoa programu ya uchaguzi, na tunajua michezo hii na lazima ikome,” alisema. Bw Musyoka aliandamana na Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti, Mwenyekiti wa Wiper na aliyekuwa Mbunge wa Kigumo Jamleck Kamau, Seneta wa Machakos Agnes Kavindu na Naibu Gavana Francis Mwangangi. Bw Kamau alimuunga mkono Bw Musyoka katika azma yake ya kuwania urais 2027, akisema ana ushawishi wa kitaifa nje ya Ukambani. “Kalonzo si mwanasiasa wa Wakamba pekee, yeye ndiye rais wa sita wa Kenya. Kuanzia wikendi ijayo tutaanza ziara zetu za kisiasa na haki itakuwa msingi katika chama hiki,” alisema Bw Kamau. “Kalonzo ni mtu wa amani na 2007, kama hangeungana na Mwai Kibaki, nchi isingekuwa na amani. Amejitolea kwa dhati kwa Raila na sasa ni zamu yake. Hana doa. Ikiwa tunataka kiongozi mwenye amani, basi huyo ni Kalonzo Musyoka,” akaongeza Bw Kamau. Bw Musyoka pia alizungumzia utata wa bajeti katika Bunge la Kaunti ya Machakos, akiwataka MCA kuidhinisha bajeti hiyo ili serikali ya kaunti iweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi. “Bajeti si pesa za kibinafsi za gavana, kwa hivyo tushirikiane na tusonge mbele,” akasema kiongozi huyo wa Wiper. Gavana Ndeti alimtaka Rais Ruto na vyombo vya usalama kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vitendo vya kihuni na kurejesha usalama nchini. Pia alimuunga mkono Bw Musyoka kuwania urais 2027, huku akiwakosoa madiwani kwa kuidhinisha nusu tu ya bajeti ya kaunti, ambayo alisema inaweza kugharamia mishahara pekee. “Bila bajeti hatuwezi kutoa huduma ambazo wananchi wetu wanahitaji. Nimewaita madiwani ili tukae pamoja kwa sababu ni sisi tutakaoipeleka kaunti hii mbele,” alisema Bi Ndeti.

MAKABILIANO makali ya kisiasa yaliyoshuhudiwa Jumapili katika Kaunti ya Homa Bay yamefichua vita vinavyozidi kushika kasi vya kutaka kudhibiti ngome ya kisiasa ya marehemu Raila Odinga, huku makundi hasimu yakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027. Linda Mwananchi, inayoongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ilikaidi vizuizi vya barabarani, uvamizi na na hatimaye kuandaa mikutano Nyandiwa, Sindo na Homa Bay mjini. Kuingia kwao katika eneo hilo kulionyesha wazi mtihani mkubwa kwa juhudi za Rais William Ruto na washirika wake kuendeleza ushawishi katika eneo la Luo Nyanza. Eneo hilo lilimkataa katika uchaguzi wa 2022 na kumpigia kura mwanao marehemu Raila. Kwa sasa eneo hilo linangáng’aniwa na makundi mbalimbali ya kisiasa. Upande mmoja ni kundi la ODM linalopinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto na sasa linaendesha shughuli zake chini ya vuguvugu la Linda Mwananchi. Mrengo mwingine ni kambi inayounga mkono serikali, ambayo imekuwa ikitumia miradi ya maendeleo na teuzi serikalini kujipigia debe. Homa Bay kwa miaka mingi imekuwa ngome kuu ya kisiasa ya Bw Odinga lakini sasa ni kitovu kinachongángániwa na mirengo hii miwili Kufuatia kifo cha Bw Odinga mwaka jana, kilichoacha pengo kubwa la kisiasa, Homa Bay imekuwa eneo muhimu la kupimia ni nani atakayerithi ushawishi wake kisiasa. Gavana Gladys Wanga, ambaye ametajwa kama mmoja wa viongozi wanaoweza kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto mnamo 2027, anakabiliwa na changamoto ya kulinda ngome ya jadi ya ODM. Ana kibarua kuonyesha kuwa ushirikiano wa chama hicho na serikali ya Kenya Kwanza umeleta manufaa kwa eneo hilo. Tangu aingie mamlakani, Rais Ruto ameongeza ushawishi wake wa kisiasa na miradi ya maendeleo katika Nyanza ya Waluo. Serikali imetaja miradi kama kukamilishwa kwa Uwanja wa Raila Odinga, Gati ya Homa Bay, Soko la Samaki la Koginga, Ikulu ndogo , nyumba za gharama nafuu, Barabara ya Mzunguko ya Mfangano-Rusinga, ukarabati wa Chuo Kikuu cha Tom Mboya pamoja na ujenzi na uwekaji wa lami katika barabara mbalimbali. Hata hivyo, Linda Mwananchi inatoa hoja tofauti ikisema barabara, viwanja na miradi mingine ya maendeleo haiwezi kuchukua nafasi ya uwajibikaji, haki za kidemokrasia na kuheshimu utawala wa sheria. Bw Sifuna aliwaambia wakazi kuwa maendeleo hayafai kutumiwa kuwanyima haki za kikatiba na uongozi wenye uwajibikaji. “Baba alituambia tuweke demokrasia, uhuru na kuheshimu utawala wa sheria mbele ya kila kitu, lakini baadhi ya watu wanataka kuwahadaa kwamba maendeleo yanatosha hata kama maana yake ni kumuua Albert Ojwang,” akasema, akirejelea mauaji ya mwalimu na mwanaharakati huyo kutoka Homa Bay. Alisema serikali inayoheshimu utawala wa sheria haipaswi kuwa na tatizo la kuleta maendeleo. “Kama Sifuna, kujenga barabara na viwanja si jambo gumu kwangu, lakini ninachowaahidi ni kwamba nitaheshimu utawala wa sheria, nitalinda haki zenu na sitawahi kuwaua watoto wenu,” akaongeza. Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi pia alipinga hoja ya maendeleo, akisema eneo hilo halijastawi sana chini ya utawala wa sasa. Bw Omondi alidai serikali imewekeza Sh50 bilioni katika eneo hilo, kiasi ambacho alisema ni sawa na gharama ya mradi mmoja mkubwa katika Bonde la Ufa. Mbunge huyo pia aliishutumu serikali kwa kuchukua udhibiti wa kampuni za sukari katika eneo hilo, akitaja Miwani na Chemelil. Gavana Orengo naye aligeuza mkutano huo kuwa jukwaa la kueleza ni nani anayepaswa kubeba urithi wa kisiasa wa Bw Odinga. Alimshutumu Rais Ruto kwa kushindwa kushughulikia malalamishi ya muda mrefu ya Nyanza, yakiwemo mzozo wa Migingo, na kukosoa namna serikali ilivyoshughulikia maandamano na madai ya mauaji yaliyotekelezwa na polisi. Kauli iliyovutia zaidi ilitolewa alipokuwa akijitaja kama mrithi wa kisiasa wa Bw Odinga. “Hapa ndipo roho ya Raila ilipo, haikufa pamoja naye. Uongozi unachukuliwa, haupeanwi, na ndiyo maana mimi ndiye Raila aliyesalia,” akasema Bw Orengo. Alitangaza kuwa Linda Mwananchi itaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Bw Odinga Oktoba 15, ambapo itaitaka serikali kutoa majibu kuhusu kifo chake. Mkutano wa Homa Bay pia ulihudhuriwa na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. Bw Owino alimtaja Bw Orengo kama kiongozi anayeweza kuwa daraja kati ya viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakishindwa kuungana. “Huyu ndiye mtu atakayewaleta viongozi hawa wote pamoja mezani na kuamua kuhusu kiongozi mmoja,” akasema. Bw Natembeya na Bw Osotsi pia waliwahakikishia wafuasi kwamba miungano mipya ya upinzani haitavuruga uhusiano wa kihistoria kati ya jamii za Luo na Luhya. Bw Natembeya alisema upinzani unahitaji kuunganisha zaidi uungwaji mkono wake Magharibi na Nyanza kuelekea uchaguzi wa 2027. RIPOTI ZA GEORGE ODIWUOR, DOMNIC OMBOK na RUSHDIE OUDIA

…579 cases, 304 deaths recorded in one week as outbreak spreads to six provincesBy Chioma Obinna The deadly Bundibugyo virus disease (BVD) outbreak in the Democratic Republic of the Congo (DRC) has escalated sharply, with 4,665 confirmed cases and 2,184 deaths recorded as of August 12, 2026, raising fresh concerns over the risk of international […]

— Calls for stronger security, action against vote buying By Shina Abubakar, Osogbo Election observation organisation, Yiaga Africa, has commended voters in Osun State for their resilience during the governorship election held on Saturday. The organisation also praised residents who not only participated in the election but remained at polling units to protect their votes […]

DAR ES SALAAM: THE CRDB Bank Foundation pledged to serve to promote healthcare services, sports, youth participation and community development banking on funds it raises through various sporting events. Chairman of the CRDB Bank Foundation Board of Directors, Oswald Urassa, said the Board will continue overseeing policies and guidelines aimed at strengthening the Foundation’s capacity…

WANANCHI wa Kata ya Msangamkuu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea Kituo cha Afya cha Msangamkuu, kilichogharimu zaidi ya Sh milioni 25, wakisema kimewaondolea changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya. Wakizungumza wakati Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, alipotembelea kituo hicho, wananchi wamesema awali walilazimika kwenda…

DAR ES SALAAM: OVER 5bn/- raised through the CRDB Marathon has been collected and directed towards the healthcare sector, enabling more than 400 children with heart conditions to undergo surgery and providing 240 women with high-risk pregnancies with medical treatment and safe delivery services. CRDB Bank Chief Executive Officer, Abdulmajid Nsekela, made the statement today,…

Peterside raised the concerns in a post on X on Sunday, a day after INEC declared Governor Ademola Adeleke of the Accord Party winner of the election.

AJALI za barabarani zimeendelea kuwa tishio kubwa Kenya, huku zaidi ya watu 40,000 wakifariki katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kulingana na takwimu za serikali. Jana, huzuni ilitanda eneo la Nthongoni, Kaunti ya Makueni, baada ya ajali mbaya ya barabarani kusababisha vifo vya watu saba na kujeruhi zaidi ya 60. Abiria walikuwa wakielekea sherehe ya kulipa mahari katika kijiji cha Inyoni, safari iliyotarajiwa kuwa ya furaha ikageuka kuwa ya majonzi. Kiongozi wa jamii Joseph Kyonda alieleza kuwa alipoteza majirani sita na kuomba msaada wa kifedha kwa mazishi yenye heshima. Basi dogo lenye viti 46 lilikuwa limebeba watu 71 wakati ajali ilitokea. Afisa Mkuu wa Afya wa Kaunti, Harvey Mulei, alisema Hospitali ya Matiliku ilipokea majeruhi 28 na Hospitali ya Rufaa ya Makueni ikapokea 36. Manusura walieleza kuwa taa za gari zilikatika kabla ya kuacha barabara na kutumbukia shimoni. Haya yanajiri huku takwimu zikionyesha kuwa miundombinu duni ya barabara, ukosefu wa madaraja ya watembeao kwa miguu na alama za trafiki na uzembe wa madereva na watembea kwa miguu ni sababu nyingi zinazochangia ongezeko la vifo na majeraha barabarani. Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonya kuwa idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko inavyoonyeshwa na takwimu rasmi. WHO inaeleza kwamba, Kenya huhesabu tu vifo vinavyotokea mara moja baada ya ajali, huku wengi wanaofariki hospitalini siku au miezi kadhaa baadaye wakiachwa nje ya rekodi hizo. Kwa mujibu wa Shirika la Kitaifa kuhusu Takwimu Kenya (KNBS), watu 114,466 walihusika katika ajali za barabarani kati ya 2021 na 2025. Katika kipindi hicho, watu 22,894 walifariki huku zaidi ya 90,000 wakijeruhiwa. Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) inasema ongezeko la idadi ya watu, magari na msongamano wa trafiki limefanya hali kuwa mbaya zaidi.

RAIS William Ruto alipozindua mjadala wa kitaifa kuhusu mustakabali wa Kenya baada ya Ruwaza ya 2030 wiki hii, aliutaja kama juhudi mpya za kuwapa mwongozo wa muda mrefu utakaonufaisha vizazi vya sasa na vijavyo. Hata hivyo, nyuma ya kauli za kuunda mwongozo mpya wa maendeleo, unafanana pakubwa na pendekezo la aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuhusu Kongamano la Kitaifa la Vizazi ambalo lilizinduliwa miezi michache kabla ya kifo chake. Mipango yote miwili inaweka wananchi katikati ya maamuzi kuhusu mustakabali wa taifa. Pia inakusudia kuwahusisha vijana, wataalamu, viongozi wa kaunti, wanavyuo, sekta ya biashara, mashirika ya kiraia na viongozi wa kidini katika kujadili mwelekeo wa Kenya. Pendekezo la Raila lilijikita zaidi katika kutafuta suluhu kwa changamoto za kisiasa, kiuchumi na kiutawala zinazokabili taifa. Kwa upande mwingine, mjadala wa Ruto unalenga kufafanua Kenya itakuwa taifa la aina gani baada ya kufikia mwisho wa mpango wa Ruwaza ya 2030. Licha ya tofauti hizo, misingi ya miradi hiyo inaonekana kufanana kwa kiasi kikubwa. Yote inatokana na imani kuwa mustakabali wa Kenya haupaswi kuamuliwa na wanasiasa wachache katika mikutano ya Nairobi pekee. Ruto amependekeza mchakato wa kitaifa utakaowahusisha wadau kutoka sekta mbalimbali ili kuamua dira mpya ya taifa. Kwa mujibu wa vyanzo vya Ikulu, Gavana wa Kisumu Profesa Anyang’ Nyong’o amepewa jukumu la kuongoza timu itakayobuni mfumo wa majadiliano hayo. Timu hiyo itapendekeza namna mashauriano yatafanyika kutoka mashinani hadi kiwango cha kitaifa. Muundo huo unafanana pakubwa na mpango ambao Raila alikuwa amependekeza mwaka 2025. Akizungumza katika mahojiano akiwa nyumbani kwake Karen Julai 19, 2025, Raila alisema kongamano hilo lingeanzia katika vituo vya kupigia kura kabla ya kuendelea hadi ngazi za wadi, maeneo bunge na kaunti. Hatimaye, wawakilishi wangekutana katika kongamano kubwa la kitaifa la takribani wajumbe 3,000 kutoka sehemu mbalimbali za nchi. “Hilo lingekuwa baraza halisi la wananchi,” alisema Raila wakati huo. Alisisitiza kuwa wananchi wa kawaida walipaswa kupewa nafasi ya kueleza changamoto zao na kuamua vipaumbele vya taifa kabla ya wanasiasa kuingilia mchakato huo. Kwa upande wake, Ruto alipokuwa akizindua mjadala huo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), alisisitiza mara kadhaa kwamba si mradi wa serikali bali wa wananchi. “Huu si mradi wa serikali. Huu ni mradi wa wananchi,” alisema Rais. Aliongeza kuwa serikali itatoa jukwaa na rasilimali lakini haitawalazimisha wananchi maamuzi ya kufanya. Kauli hiyo inaendana kwa kiwango kikubwa na mawazo ambayo Raila alikuwa ametetea kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia mamlaka yao ya kikatiba kuamua hatima ya taifa. Raila alipendekeza kwamba nusu ya wajumbe katika mikutano ya mashinani wawe vijana hasa wa kizazi cha Gen Z. Naye Ruto amesema mjadala wa baada ya Ruwaza ya 2030 lazima uzingatie maslahi ya vijana ambao watarithi Kenya ya baadaye. Hata hivyo, kuna tofauti muhimu. Kongamano la Raila lilizaliwa wakati taifa lilikuwa linakabiliwa na malalamishi kuhusu utawala, ukosefu wa ajira, ufisadi na madai ya ukatili wa polisi. Hivyo lilikuwa na mwelekeo wa kisiasa na kikatiba zaidi. Kwa upande mwingine, mjadala wa Ruto umejikita katika maendeleo ya muda mrefu na namna ya kuhakikisha Kenya inabaki na mwongozo mmoja hata baada ya mabadiliko ya serikali. Naibu Rais Kithure Kindiki na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah wamependekeza kwamba mwongozo huo mpya upewe msingi wa kisheria ili serikali zijazo zisibadilishe mwelekeo wa taifa kila baada ya uchaguzi. Hata hivyo, changamoto kubwa kwa utawala wa Ruto itakuwa kuwashawishi wakosoaji kwamba mchakato huo ni wa kweli na haujalenga kuendeleza ajenda za kisiasa za serikali iliyopo madarakani. Baadhi ya viongozi wa upinzani tayari wanataka ukaguzi wa kina wa utekelezaji wa Ruwaza ya 2030 kabla ya kuanzishwa kwa mpango mwingine mpya. Kifo cha Raila Odinga Oktoba 2025 kilikatiza ndoto ya kongamano lake la kitaifa kabla ya kutekelezwa. Sasa mjadala wa Ruto kuhusu Kenya baada ya Ruwaza ya 2030 unaonekana kufufua kwa namna fulani baadhi ya mawazo hayo, lakini kwa sura mpya ya maendeleo na mipango ya muda mrefu ya taifa.

DAR ES SALAAM: TANZANIA is set to mark a major milestone in its energy sector next Saturday when President Samia Suluhu Hassan commissions the 2,115-megawatt Julius Nyerere Hydropower Plant (JNHPP), raising the country’s installed electricity generation capacity to 4,646MW. The commissioning will mark the completion of the country’s largest electricity generation project undertaken using domestic…

MVUTANO wa kisiasa, tamaa ya uongozi na mapambano ya kumrithi Rais William Ruto 2032 yanaanza kutishia kampeni yake ya kutafuta muhula wa pili 2027 katika Bonde la Ufa, eneo ambalo ni ngome yake kuu ya kisiasa. Makundi mawili yanaonekana kumakinikia siasa za urithi wa uongozi wa eneo huku baadhi ya viongozi wakituhumiwa kuelekeza nguvu zao kwenye uchaguzi wa 2032 badala kuhakikisha Rais Ruto anashinda uchaguzi wa 2027. Kiini cha mzozo huo ni ushindani wa kisiasa kati ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot. Baadhi ya wabunge na viongozi wengine wameanza kujiunga na pande zinazowapigia debe wanasiasa hao wawili. Juhudi za kuwatafuta Mabw Murkomen na Cheruiyot kuhusu suala la kuanzisha kampeni za mapema za 2032 hazikufua dafu kwa kuwa hawakujibu simu au jumbe walizotumiwa Mbunge wa Belgut, Nelson Koech, amekiri kuwa mjadala kuhusu nani atamrithi Rais Ruto 2032 umeanza kutawala siasa za Bonde la Ufa, hali ambayo anasema inaweza kuvuruga kampeni za 2027. Bw Koech alikanusha kuwa anaegemea mrengo wa Seneta Cheruiyot, lakini akasema ushindani huo umeanza kusababisha migawanyiko unaotatiza kampeni za Rais Ruto. “Watu wamesahau kwamba kwanza tunapaswa kushughulikia 2027 kabla hata ya kufikiria 2032. Wanaojihusisha na siasa za urithi wanamdharau Rais kwa sababu huwezi kurithi kile ambacho baba yako bado anamiliki,” akasema Bw Koech kwenye mahojiano na Taifa Leo. Mbunge huyo, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Kitaifa, alionya kuwa viongozi wanaoanza kampeni za kumrithi kiongozi aliye madarakani kabla ya muda wake kuisha mara nyingi huishia kupoteza ushawishi na kuzama kisiasa. Alisema baadhi ya viongozi wenye nyadhifa za juu serikalini wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kumsaidia Rais Ruto kupata muhula wa pili badala ya kufuatilia maslahi yao ya kibinafsi. Kwa mujibu wa takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kaunti zinazokaliwa na jamii ya Kalenjin—Nandi, Uasin Gishu, Bomet, Kericho, Elgeyo-Marakwet, West Pokot na Baringo—zinatarajiwa kuwa na zaidi ya wapigakura milioni 3.2 waliojiandikisha kufikia uchaguzi wa 2027. Idadi hiyo inaweza kuwa juu zaidi kutokana na uwepo wa Wakalenjin pia kwenye sehemu kubwa ya Kaunti ya Nakuru na pia Narok. Bw Koech alisema changamoto ya usajili wa wapigakura inapaswa kuwa kipaumbele badala ya viongozi kujihusisha na siasa za 2032. Alisema Wakalenjin milioni 1.2 bado hawajajisajili kupiga kura, hali ambayo inaweza kuathiri pakubwa juhudi za Rais Ruto kutafuta muhula wa pili. “Tunapaswa kutafuta mikakati ya kutatua tofauti zetu ili kwanza tushughulikie 2027. Kwa sasa kura kutoka Murang’a na Kiambu karibu zinaweza kufuta kura zote za Wakalenjin,” akasema. Seneta wa Nandi Samson Cherargei naye amemvamia Bw Murkomen, akidai hamakinikii kampeni za Rais Ruto huku akimakinikia kuwasambaratisha viongozi wasiokuwa kambi yake . Bw Cherargei alisema hatakubali kulazimishwa kumuunga mkono Bw Murkomen na akapinga madai kwamba yuko katika kambi ya Bw Cheruiyot. “Sitamwaabudu. Hata akidhamini mgombea dhidi yangu, hatafanikiwa. Kwa nini anaendesha kampeni za 2032 na kuzua mvutano miongoni mwa viongozi badala ya kumsaidia Rais?” akauliza. Mnamo Agosti 5, Mbunge wa Keiyo South Gideon Kimaiyo pia alimkosoa Bw Murkomen hadharani, akidai anaingilia siasa za eneobunge lake. Bw Kimaiyo alisema viongozi wanapaswa kuacha za urithi na kuelekeza nguvu zao katika kuhakikisha Rais Ruto anamaliza muhula wake wa kwanza akiwa na rekodi nzuri ya maendeleo. Mbunge wa Aldai, Marriane Kitany, naye amewataka viongozi wa Bonde la Ufa kuwa na umoja, akisema ushindi wa 2027 haupaswi kuchukuliwa kuwa ushatimia. “Tusidhani kwamba tuna urais na kwamba Rais ashachaguliwa. Ukweli ni kwamba kura zetu zinahitajika ili Ruto achaguliwe tena na ashinde kwa idadi kubwa,” akasema Bi Kitany pia alitetea rekodi ya maendeleo ya Rais Ruto katika eneo hilo, akitaja miradi mbalimbali ya miundombinu, viwanja vya michezo, nyumba za gharama nafuu na usambazaji wa umeme. Alisema viongozi wanapaswa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ili iweze kuwa msingi wa kampeni za 2027. Mzozo huo unatokea wakati Rais Ruto mwenyewe amekuwa akionyesha wasiwasi kuhusu kiwango cha usajili wa wapigakura Bondeni. Akizungumza katika mazishi Bomet mnamo Mei 1, Rais alisema Wakalenjin milioni 1.8 wenye vitambulisho hawajajisajili kupiga kura, huku wengine 500,000 waliofikisha umri wa miaka 18 pia wakiwa hawajajisajili. Alisema hali hiyo inamlazimisha kutafuta uungwaji mkono katika maeneo mengine ilhali ngome yake ina idadi kubwa ya wapigakura ambao bado hawajajiandikisha.

Olajengbesi also praised Tinubu for, according to him, keeping his promise to allow the election to be conducted freely.

SENETA wa Nyandarua John Methu amesema pesa nyingi hazitahakikishia Rais William Ruto ushindi katika uchaguzi mkuu wa 2027. Methu alisema matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ol Kalou yalidhihirisha kuwa wapigakura wanaweza kukataa ushawishi wa pesa na kuchagua viongozi wanaowataka. “Kutoka Ol Kalou, imethibitishwa kuwa pesa ni kipengele kidogo cha uchaguzi mkuu ujao,” Methu alisema katika mahojiano ya runinga Jumatano usiku. Seneta huyo, ambaye aliongoza kampeni za upinzani Ol Kalou, alisema alitumia takriban siku 60 katika eneo hilo na kwamba uchaguzi huo ulikuwa somo muhimu kwa upinzani kuhusu namna ya kumkabili Rais Ruto mwaka 2027. Methu alidai kuwa Rais Ruto anaamini wapinzani wake hawana uwezo wa kifedha wa kushindana naye. “Kitu kimoja anachoamini William Ruto ni kwamba hatuna pesa, na ako nazo. Ni kweli ana pesa.

CHAMA cha Wiper Patriotic Front (WPF) kimeunda kikosi cha viongozi watatu kuongoza kampeni zake eneo la Pwani huku kinyang’anyiro cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 kikishika kasi. Kikosi hicho kinajumuisha Mbunge wa Nyali Mohammed Ali, Mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako na aliyekuwa Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa. Viongozi hao wanawakilisha maeneo yenye ushawishi mkubwa kisiasa ya Mombasa, Taita Taveta na Kilifi. Hii ni katika hatua ambayo kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema inalenga kuimarisha upinzani na kuteka Pwani kama ngome yake. Hatua hiyo imeongeza ushindani Pwani ambako washirika wa Rais William Ruto wanajaribu kuunganisha magavana, wabunge na viongozi wengine chini ya mwavuli wa Kenya Kwanza ili kudhibiti kura za eneo hilo. Kwa upande wa upinzani, viongozi hao watatu wanatarajiwa kusuka mtandao wa kisiasa utakaosaidia kukabili ushawishi unaoongezeka wa muungano tawala Kenya Kwanza, na kuzuia Pwani kuwa eneo linaloegemea upande mmoja wa kisiasa. Akizungumza akiwa Kakuyuni, Kaunti ya Kilifi, wakati wa kumpokea rasmi Jumwa katika chama cha Wiper Patriotic Front (WPF), kinara Musyoka alipendekeza achaguliwe kuwa naibu kiongozi wa chama hicho. Alisema tajriba ya Jumwa katika siasa, pamoja na ushawishi wa Mohammed Ali na Mwashako, zitaipa Wiper nguvu mpya Pwani na kusaidia upinzani kujenga kampeni imara. “Jumwa amepanda ngazi za uongozi kutoka Mwakilishi wa Wanawake, Mbunge hadi Waziri. Sasa nawaomba mnipe Jumwa ili twende pamoja kukomboa nchi hii. Nitampa tiketi ya chama kugombea ugavana na pia nataka awe katika siasa za kitaifa. Kama kiongozi wa WPF, napendekeza awe naibu kiongozi wa chama,” alisema Kalonzo. Aidha, alidai kwamba mazingira ya kisiasa Pwani yanabadilika na kwamba Wiper inaelekea kuchukua nafasi iliyoshikiliwa na ODM kama chama kikuu cha upinzani katika eneo hilo. “Ninatangaza kuwa ngome iliyokuwa ya ODM sasa ni ya Wiper,” akasema. Kalonzo alikumbusha wakazi wa Pwani kuhusu ushirikiano wake wa muda mrefu na kinara wa zamani wa ODM Raila Odinga katika harakati za kukuza demokrasia na haki za kijamii. Kwa upande wake, Ali alisema viongozi hao watatu wataanzisha kampeni kubwa ya hamasisho kuanzia Lamu hadi Taita Taveta na Lunga Lunga ili kuwashawishi wananchi kuunga mkono Kalonzo na upinzani. “Bi Jumwa na mimi ni kama Ronaldo na Messi. Kuanzia Lamu hadi Taita-Taveta na Lunga Lunga, tutaondoa serikali hii mamlakani,” alisema. Alishutumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kuwasahau baadhi ya viongozi walioisaidia kupata ushawishi katika Pwani. Kulingana naye, hatua ya Jumwa kuondoka UDA ni ishara ya kutoridhika miongoni mwa baadhi ya washirika wa zamani wa serikali. Naye Mwashako, ambaye anatazamiwa kuwania ugavana Taita-Taveta mwaka 2027, alisema amesalia Wiper licha ya kushinikizwa kujiunga na serikali. Alifichua kuwa amekuwa akishawishiwa mara kwa mara kujiunga na serikali jumuishi, ikiwemo kuahidiwa msaada wa kifedha kwa azma yake ya kugombea ugavana. “Nilichaguliwa kupitia Wiper mwaka 2017 na chama hiki ni nyumbani kwangu. Wamekuwa wakinishawishi mchana na usiku nijiunge na serikali lakini nimekataa. Hata walinitishia lakini sikuyumba,” alisema. Mwashako pia alifichua kuwa alijiuzulu kama mwenyekiti wa Kikundi cha Wabunge wa Pwani mwezi Januari baada ya kudaiwa kuambiwa kwamba angeendelea kushikilia nafasi hiyo tu ikiwa angeondoka Wiper. “Hata pesa zao nilikataa. Nilikuwa mwenyekiti wa kikundi hicho kwa miaka mitatu lakini nikajiuzulu kwa sababu ya shinikizo. Niliambiwa lazima nitoke Wiper ili nibaki katika nafasi hiyo,” alisema. Kauli yake imeonyesha ushindani mkubwa unaoendelea nyuma ya pazia huku kila upande ukijaribu kuvutia viongozi wenye ushawishi eneo la Pwani kabla ya uchaguzi wa 2027. Mwashako alisema upinzani hautaruhusu viongozi wake kuvutwa kwa ahadi za nyadhifa serikalini au fedha. “Kenya ni nchi ya kidemokrasia na hakuna mtu anayepaswa kulazimishwa kujiunga na serikali,” alisema. Mbunge huyo wa Wundanyi alisema hatua ya Jumwa kujiunga na Wiper imepatia upinzani nguvu mpya Pwani na kwamba sasa viongozi hao watatu watashirikiana kuhamasisha wapigakura katika kaunti zote sita za eneo hilo. “Kwa sasa tuko watatu; mimi, Jumwa na ndugu yangu Mohammed Ali. Kazi yetu ni kuwashawishi wananchi wasivutiwe na pesa ili kuunga mkono serikali,” alisema. Kuundwa kwa timu hiyo kunajiri huku viongozi wa Kenya Kwanza nao wakiongeza juhudi za kuimarisha ushawishi wao katika eneo la Pwani. Mohammed Ali tayari ametajwa na viongozi wa upinzani kama mmoja wa wanaoweza kuwania ugavana wa Mombasa mwaka 2027, hatua inayomfanya kuwa miongoni mwa nyuso kuu za upinzani katika eneo hilo. Mwashako alisema ana imani viongozi wengine watajiunga na kundi hilo kadri kampeni zinavyoendelea. “Kwa sasa tuko watatu lakini nina uhakika wengine watajiunga nasi. Tuna Mohammed Ali, Shakila Abdalla kule Lamu, mimi Taita-Taveta na wengine Tana River na Kwale. Lakini lengo kuu ni kuhakikisha Kalonzo Musyoka anashinda urais mwaka 2027,” alisema. Bi Jumwa aliwasihi wakazi wa Pwani kujifunza kutoka kwa wapigakura wa Ol-Kalou ambao, kwa mujibu wake, walipokea miradi na fedha za serikali lakini bado wakachagua mgombea wa upinzani. Aliwaonya kwamba serikali itatumia rasilimali nyingi kabla ya uchaguzi wa 2027 lakini akawasihi wapigakura kutoruhusu ahadi na zawadi za kampeni kuathiri maamuzi yao. Alisema wananchi wanaweza kupokea maendeleo na manufaa yanayoletwa kwao, lakini watumie haki yao ya kidemokrasia kwa uhuru wakati wa kupiga kura.

NAIBU Rais Kithure Kindiki anaendelea kutumia wazee kuunganisha eneo la Mlima Kenya ili kuwa na umoja wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Wiki jana, alikutana na wazee wa jamii ya Ameru Njuri Ncheke waliompa baraka zao. Jana, Profesa Kindiki alikutana na maelfu ya wazee kutoka Mlima Kenya Mashariki na kuwaomba wazungumze na wenzao wa Mlima Kenya Magharibi kuhusu jinsi eneo hilo lenye wapigakura wengi linavyoweza kuwa na msimamo mmoja. Akizungumza katika Uwanja wa Nembure, Embu, Profesa Kindiki alisema maeneo hayo mawili yanapaswa kubaki pamoja kwa ajili ya maendeleo. Hata hivyo, alimshmbulia vikali na mtangulizi wake, Rigathi Gachagua, akimtuhumu kumdhalilisha na kumshambulia kisiasa. “Nilijaribu kumwambia Gachagua awe na tabia nzuri na apunguze kasi ili Mlima Kenya Mashariki na Magharibi ziishi kwa amani, lakini alikataa. Badala yake aliendelea kunidharau. Hana heshima. Akiendelea kuchafua jina langu, nitamuanika na kushughulika naye,” Kindiki alisema. Profesa Kindiki pia alimkejeli Gachagua akisema hana hadhi ya kumfundisha siasa. Profesa Kindiki alisema umoja wa Mlima Kenya Mashariki na Magharibi ni muhimu ikiwa eneo hilo litaendelea kuwa na nafasi katika uongozi wa kitaifa na kunufaika kimaendeleo. Aliahidi kuhakikisha maeneo hayo yanaungana na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu siasa na maendeleo. Pia alisema maeneo hayo yanapaswa kushirikiana kuhakikisha Rais William Ruto anachaguliwa tena mwaka ujao. Alimtuhumu Gachagua kwa kugawanya Mlima Kenya kwa maslahi yake ya kisiasa. “Gachagua anataka Mlima Kenya ugawanyike ili usinufaike na rasilimali za kitaifa. Gachagua ni mtu mbaya na wananchi hawapaswi kumsikiliza,” alisema. Mkutano huo uliwakutanisha viongozi na wanachama wa mabaraza ya wazee ya Njuri Ncheke kutoka Meru, Nyaangi Ndiriri kutoka Mbeere, Kiama Kia Muembu kutoka Embu na Mwea Council of Elders. Wazee hao, zaidi ya 30,000 walitaka Profesa Kindiki aheshimiwe kama Naibu Rais na kiongozi wa juu kutoka Mlima Kenya Mashariki. Walisema wakati umefika kwa Mlima Kenya Magharibi kulipa fadhila kwa kuunga mkono Kindiki bila masharti katika wadhifa wake wa Naibu Rais na katika matarajio yake ya baadaye ya kuwa rais wa kwanza wa Kenya kutoka Mlima Kenya Mashariki. Wazee hao pia walitangaza Kindiki kuwa msemaji wa kisiasa wa Mlima Kenya, wakisema yeyote anayetaka kuzungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusu siasa anapaswa kufanya hivyo kupitia Naibu Rais. Walitaja miaka ambayo Mlima Kenya Mashariki uliunga mkono viongozi kutoka Magharibi, akiwemo Jomo Kenyatta, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta, pamoja na manaibu wa rais Joseph Karanja na George Saitoti. Profesa Kindiki alisema watu wa Mlima Kenya Mashariki wamekuwa wakiunga mkono viongozi kutoka Magharibi bila malalamiko. Alisema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya viongozi wakimlipa kwa matusi na kumshambulia kwa maneno, licha ya kuwa yeye ndiye mtu wa kwanza kutoka Mlima Kenya Mashariki kushikilia wadhifa wa pili kwa ukubwa nchini. Alisema alimpa heshima Gachagua alipokuwa Naibu Rais na hakuwahi kumtukana alipokuwa Waziri wa Usalama wa Ndani. Kindiki pia aliunga mkono ombi la wazee la mazungumzo rasmi na wenzao kutoka Mlima Kenya Magharibi ili kuunda msimamo mmoja kuhusu mustakabali wa kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kimaendeleo wa eneo hilo. “Tunaunga mkono ombi la wazee wa Mlima Kenya Mashariki kuzungumza na wazee wa Mlima Kenya Magharibi kuhusu jinsi ya kuunganisha jamii zetu. Tutaheshimu watakachokubaliana,” alisema. Wazee pia waliomba miradi ya maendeleo ikamilishwe haraka, ikiwemo ujenzi wa barabara ya njia mbili kutoka Makutano kupitia Embu, Chuka, Meru hadi Maua na Daraja la Nithi.

The Imole Campaign Council, ICC, has alleged there is a plot by lNEC to declare the Osun governorship election inconclusive.

The governor called on Tinubu to direct the heads of the security agencies to ensure the protection of voters and the integrity of the electoral process.

By Henry Umoru ABUJA — National Leader of the Nigeria Democratic Congress, NDC, Senator Seriake Dickson, has raised the alarm over what he described as the decline of Nigeria’s political culture, calling for a return to the ideals, values and sacrifices that shaped the country’s early democratic politics. Dickson, a former governor of Bayelsa State, […]

The national disaster management agency (BNPB) raised the death toll from 40 late Saturday, and rescue official Fathur Rahman said 50 people were injured in the 7.7-magnitude quake.

Galatasaray striker Victor Osimhen has called on his teammates to raise their level and give their all on the pitch following their 2-2 draw against Çorum in the opening week of the Turkish Super Lig.

MABADILIKO ya tabianchi, ukame wa muda mrefu na mvua zisizotabirika vinaendelea kuathiri uzalishaji wa mazao nchini Kenya, hali inayowasukuma watengenezaji wa chakula cha mifugo kuhimiza kilimo cha mahindi ya manjano ili kupunguza utegemezi wa malighafi kutoka nje na gharama za uzalishaji. Chama cha Watengenezaji wa Chakula cha Mifugo Kenya (AKEFEMA) kinaitaka serikali, watafiti na wakulima kuhamasisha uzalishaji wa mahindi ya manjano kwa ajili ya chakula cha mifugo, huku mahindi meupe yakitengwa zaidi kwa matumizi ya binadamu. “Malighafi huchangia kati ya asilimia 70 na 80 ya gharama ya kutengeneza chakula cha mifugo. Kenya bado inaagiza malighafi nyingi kutoka nje, licha ya kuwa na uwezo wa kuzalisha sehemu kubwa humu nchini,” alisema Mwenyekiti wa AKEFEMA Joseph Karuri. [caption id="attachment_191153" align="aligncenter" width="300"] Mahindi shambani yakiendelea kukua. Picha|Sammy Waweru[/caption] Karuri alisema mahindi ndiyo chanzo kikuu cha virutubisho vya wanga (carbohydrates) katika chakula cha mifugo, lakini uhaba wa mahindi kwa matumizi ya binadamu unalazimisha wafugaji kushindana na watu kwa nafaka hiyo. Chama hicho pia kinataka kuongezwa kwa uzalishaji wa alizeti, soya, pamba na canola, ambazo mabaki yake baada ya kukamua mafuta hutumika kama chanzo muhimu cha protini katika chakula cha mifugo. Karibu asilimia 80 ya malighafi hizo za protini huagizwa kutoka Tanzania, Uganda, Malawi na Zambia. Kenya hutumia takriban magunia milioni saba ya mahindi ya kilo 90 kila mwaka kutengeneza chakula cha mifugo, sawa na tani 630,000. Ingawa uwezo wa viwanda vya kutengeneza chakula cha mifugo ni karibu tani milioni nne kwa mwaka, uzalishaji halisi ni tani milioni 2.5 pekee kutokana na uhaba wa malighafi. [caption id="attachment_191155" align="aligncenter" width="300"] Mkulima akikagua shamba lake la mahindi katika kaunti ya Kiambu. Picha|Sammy Waweru[/caption] Karuri alisema kuboresha lishe ya mifugo ni muhimu kuongeza uzalishaji wa maziwa, nyama na mayai. Kenya huzalisha karibu lita bilioni tano za maziwa kwa mwaka, lakini ng’ombe mmoja hutoa wastani wa lita saba hadi nane kwa siku. Aidha, AKEFEMA pia inahimiza matumizi ya teknolojia ya Near Infrared (NIR), inayowezesha kuchanganua ubora wa malighafi ndani ya dakika tano hadi 10 na kusaidia wataalamu kutengeneza mchanganyiko sahihi wa chakula. Makamu Mwenyekiti wa AKEFEMA, Dkt David Murumba, alisema teknolojia hiyo inaweza kupunguza upotevu wa malighafi wakati wa uundaji wa malisho, kuongeza ufanisi na kuboresha afya ya mifugo. [caption id="attachment_191156" align="aligncenter" width="300"] Chama cha Watengenezaji wa Chakula cha Mifugo Kenya (AKEFEMA) kinaitaka serikali, watafiti na wakulima kuhamasisha uzalishaji wa mahindi ya manjano kwa ajili ya chakula cha mifugo. Picha|Sammy Waweru[/caption] Katibu Mkuu wa AKEFEMA, Dkt Wilfred Kamau, alisema uwekezaji katika mashine za kisasa, wataalamu na mikopo nafuu ni muhimu kupunguza gharama za uzalishaji na hatimaye bei ya maziwa, mayai na nyama ya nguruwe kwa walaji pia itashuka.

He said the alleged non-recognition of party agents occurred in 10 local government areas, prompting him to report the matter to relevant authorities, who, he said, were looking into it.

By Chioma Obinna The Human Rights Writers Association of Nigeria (HURIWA) has called for the investigation and prosecution of alleged financiers and organisers of vote-buying in the Osun State governorship election. The rights group raised concerns over alleged widespread vote-buying during the election, warning that the practice could undermine the integrity of the electoral process […]

MWANZA: THE Mwanza-based Premier League side,Pamba Jiji FC, have extended a one-year sponsorship contract with Jambo Company, with the club stating that it will continue to strengthen the partnership with the aim of promoting competitiveness and team development. Speaking today at CCM Kirumba stadium, Pamba Jiji’s Information Officer, Moses William, said the club will continue…

ARUSHA: Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) imefanya maboresho ya kimkakati katika mifumo yake ya mafunzo kwa kuingiza rasmi masuala na moduli za Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika mitaala ya programu zake za kitaaluma. Hatua hiyo inalenga kujenga jeshi la wataalamu wenye ujuzi wa kusimamia miradi ya kimkakati…