
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


KIGOMA; MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa Chama cha ACT Wazalendo Kiza Nayeye amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa kwenye jimbo lake, ambayo anasema imeondoa changamoto kubwa zilizokuwa zikiwakabili. Mayeye amesema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ukiweka mawe ya msingi katika miradi ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Msimba Day…

MFANYABIASHARA Suleiman Shahbal ameanza kufufua mtandao wake wa kisiasa katika kaunti ya Mombasa akijitayarisha kwa kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa 2027, huku akimuonya Rais William Ruto dhidi ya kuteua mgombea mmoja wa ugavana katika eneo hilo. Bw Shahbal alisema hatua hiyo inaweza kumnyima kura katika kaunti hiyo akimsihi ajifunze kutoka kwa makosa ya marehemu Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu wa 2022. Bw Shahbal alimuonya Rais Ruto dhidi ya mipango ya kisiasa inayoweza kuwaondoa wagombea wengine katika kinyang’anyiro cha ugavana ili kumuunga mkono mgombea mmoja anayependekezwa na ikulu. Alisema kuwa kuwepo kwa wagombea wengi kutamnufaisha Rais kwa kuwa kila mmoja atakuwa akifanya kampeni na kuwahamasisha wapiga kura. “Ikiwa kuna watu wengi katika kinyang’anyiro, Rais atapata kura nyingi kwa sababu wote watafanya kampeni kwa ajili yake. Lakini ikiwa ni mtu mmoja, ambaye ni mgombea wa Rais hapa Mombasa, wanampotosha Rais,” alisema. Bw Shahbal, ambaye hivi majuzi alipuuza ushauri wa Rais Ruto wa kutogombea kiti cha ugavana wa Mombasa, alikutana na zaidi ya wanachama 300 wa kundi lake la “Shahbal Movement” katika mkutano ulioandaliwa chini ya kaulimbiu ya “Mombasa is calling” kujadili namna ya kufufua mtandao wake wa kisiasa mashinani. Alisema mkutano huo haukuwa uzinduzi rasmi wa kampeni yake, bali ulikuwa mwanzo wa maandalizi ya kuimarisha mtandao wake kabla ya kuanza kuwafikia wananchi mashinani. “Huu ni mkutano wa viongozi wetu wa ‘Shahbal Movement’. Bado sijafanya mkutano wa mashinani. Tutakapoenda kwa wananchi, mambo yatakuwa tofauti kabisa. Nimewaambia watu wangu kwamba kwa miezi mitatu ijayo tunajitayarisha. Hatuna haraka. Tsunami itaanza Januari mwakani,” alisema. Mfanyabiashara huyo aliwashutumu baadhi ya wanasiasa wanaounga mkono mfumo wa kugawana maeneo ya kisiasa, akisema wanataka kupewa njia rahisi ya ushindi badala ya kwenda mashinani kuwashawishi wapiga kura. “Upuuzi huu wa kugawana maeneo umeanzishwa na watu wanaoogopa kwenda mashinani kukutana na wananchi. Wanataka usalama; wanataka kupewa njia rahisi ya ushindi,” alisema. “Ikiwa una imani na uongozi wako, nenda kwa wananchi uwaambie ulichowafanyia nao watakuchagua. Kwa nini una hofu kubwa kiasi cha kutaka kuwazuia watu wengine kugombea?” Bw Shahbal pia aliwakosoa viongozi wa UDA wanaodai kuwa wanaweza kumhakikishia Rais idadi kubwa ya kura bila kuwepo kwa ushindani. “Nina hakika watu wa UDA wananisikiliza. Wanampotosha Rais. Hakuna yeyote kati yao anayeweza kuhakikisha kwamba wapiga kura watatoka bila ushindani,” alisema. Alitaja Nyanza kama mfano, akidai kuwa baadhi ya wagombea wanaopata tiketi ya ODM bila ushindani wa ndani hupoteza ari ya kufanya kampeni. “Hili ndilo kosa tulilofanya Nyanza. Mara tu mtu anapopewa cheti cha ODM, anapoteza hamu, anarudi nyumbani na kulala kwa sababu tayari ameshinda. Hivyo ndivyo Bw Odinga alipoteza kura Nyanza,” alisema. Bw Shahbal pia alidai kuwa tiketi ya ODM imekuwa ikitumika Mombasa kuwashinikiza wagombea kuunga mkono chama hicho au kukosa tiketi. “Safari hii wanaweza kubaki na cheti chao. Sisi tuna mipango,” alisema. Kauli zake zinajiri wakati ambapo wanasiasa kadhaa wameanza kujipanga kwa uchaguzi wa ugavana wa Mombasa wa 2027. Miongoni mwa wanaotajwa katika kinyang’anyiro hicho ni Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar, Gavana wa sasa Abdulswamad Nassir wa ODM, Mbunge wa Nyali Mohammed Ali na aliyekuwa Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo. Wiki iliyopita, Bw Omar aliunga mkono uamuzi wa Bw Shahbal kugombea, huku akipinga mikataba ya kisiasa au mfumo wa kugawana maeneo ambao unaweza kuwalazimisha baadhi ya wagombea kujiondoa.

WATU wanaoshukiwa kutumia TikTok kuwavuta vijana katika mitego ya uhalifu wamekamatwa na polisi jijini Nairobi, huku uchunguzi ukionyesha huenda kuna wahalifu wanaowalenga Wakenya mitandaoni. Washukiwa hao, Emanuel Bosire Arisa, Brian Gatheru Nderitu na mtoto mmoja, wanazuiliwa kwa siku 21 huku wapelelezi wakikusanya ushahidi dhidi yao. Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), washukiwa hao walikuwa wakiendesha ukurasa wa TikTok usiojulikana walioutumia kuwasiliana na waathiriwa kabla ya kupanga kukutana nao ana kwa ana. Mmoja wa waathiriwa ni Nzumari, jina limebadilishwa kwa sababu ni mtoto, ambaye alikutana na washukiwa hao baada ya kwanza kumsifu kupitia TikTok na baadaye kumshawishi kuhamishia mazungumzo WhatsApp. Mazungumzo hayo yaligeuka kuwa ya kimapenzi kabla ya washukiwa kumwalika Ruai, Nairobi, akiamini angeenda kujiburudisha. Hata hivyo, inadaiwa walimpeleka eneo lililotengwa ambako walimnyanyasa kingono na kumpora simu. Washukiwa hao pia walidaiwa kumlazimisha kutoa nambari yake ya siri ya M-Pesa. Baadaye walimtishia mama yake wakimtaka atume pesa zaidi na kumuonya kuwa wangemtupa Nzumari iwapo hangetii. Hatimaye walimwacha katika eneo asilolijua akiwa amesononeka. DCI ilisema washukiwa hao wametambuliwa na waathiriwa watano katika visa tofauti vilivyoripotiwa Buruburu, Embakasi na Ruai. Afisa wa DCI wa Ruai Henry Kinyua alisema polisi wamepokea visa sita vyenye mtindo unaofanana huko Ruai tangu Julai. Kisa kingine kiliripotiwa Imara Daima na viwili Buruburu. “Baada ya anayelengwa kuwaamini, mtu huyo humwaalika walale kwake au kwenda kujiburudisha. Lakini mwaathiriwa anapofika, hugeukwa kisha huibiwa na hata kudhulimiwa kimapenzi,” akasema Bw Kinyua. Polisi walipata simu sita kutoka kwa washukiwa hao pamoja na makoti mawili yenye kofia yaliyodaiwa kutumiwa kuficha utambulisho wao wakati wa uhalifu. Bw Kinyua alisema mmoja wa washukiwa alikuwa akimtumia mdogo wake kuwachukua waathiriwa, kwa kuwa umri wake uliwafanya wasiwe na mashaka. Alisema washukiwa hao pia walitumia picha na video zinazoonyesha maisha ya kifahari kwenye mitandao kuwavutia waathiriwa. “Tulipofungua kurasa hizo tuligundua kuwa kijana huyo anachapisha sana maisha ya kifahari, hali iliyowavutia watu kwa mtu huyu anayeishi maisha ya kifahari ilhali kumbe ni mhalifu,” akasema. Mwanasaikolojia wa watoto na vijana Winnie Ndung’u alisema vijana wako katika hatari ya kutumiwa na wanyanyasaji kwa sababu akili zao bado zinaendelea kukomaa. “Wanatumia ukweli kwamba akili ya mtoto bado haijakomaa kikamilifu ili kufanya maamuzi thabiti na huanza kuwavutia kwa mambo wanayopenda kabla ya kuwanyanyasa,” akasema. Ripoti ya UNICEF ilionyehsa kuwa asilimia 67.3 ya watoto walipitia unyanyasaji. Kati yao, asilimia 25.5 hawakujua mahali pa kuripoti, asilimia 22.1 waliona aibu, huku asilimia 14.6 wakiogopa kupata matatizo iwapo wangezungumza.

MAAFISA wa polisi waliojihami kwa silaha jana walizingira makazi ya Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji huko Mutunduri, siku moja baada ya vijana wenye hasira kujaribu kuvuruga mkutano wa Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki. Baadhi ya maafisa hao walikuwa wamevalia nguo za kiraia na walikuwa wamejipanga kimkakati nje ya makazi ya mbunge huyo, wakidaiwa kusubiri kumkamata kufuatia ghasia zilizozuka wakati wa mkutano wa naibu rais katika Uwanja wa Nembure Jumamosi. Maafisa hao walifika karibu saa 12 asubuhi na kuzingira makazi hayo, hali iliyozua hofu katika boma hilo. Walikaa hapo kwa saa kadhaa huku wakijaribu kubaini iwapo mbunge huyo alikuwa ndani. Kufikia adhuhuri, maafisa hao walikuwa bado hawajaondoka. Juhudi za kumpata mbunge huyo ili kutoa maoni yake hazikufaulu kwani simu yake ilikuwa imezimwa. Wakati wa ghasia za Jumamosi katika Uwanja wa Nembure, mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa na polisi huku magari sita yakichomwa. Vijana walikuwa wakali baada ya polisi kuwazuia kuingia kwa nguvu uwanjani, ambako Profesa Kindiki alikuwa akihutubia maafisa wa UDA. Kuzingirwa kwa makazi ya mbunge huyo kulitokea baada ya Profesa Kindiki kulaani vikali ghasia zilizovuruga mkutano wake. Alisema UDA ilijutia vifo na uharibifu uliosababishwa na watu waliowapanga vijana kuvuruga mkutano huo. “Ninalaani ghasia na kutaka vyombo vya usalama kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika kuchochea vurugu za kisiasa,” akasema. Alisisitiza kuwa UDA inaunga mkono siasa zinazozingatia masuala na ushindani kuhusu ni chama gani kina rekodi bora ya maendeleo na sera nzuri kwa mustakabali wa Kenya, badala ya kulazimisha watu kuunga mkono kwa kutumia uongo, ghasia na kauli mbiu zisizo na maana. “Uongozi wa chama chetu Embu umepewa jukumu la kuthibitisha hasara na uharibifu uliotokea, na kuratibu hatua za kuhakikisha tunasimama pamoja na wote walioathirika kwa njia moja au nyingine,” akasema. Gavana wa Embu Cecily Mbarire alishutumu upinzani kwa kuhisi umeshindwa kuelekea uchaguzi wa 2027. “Upinzani unajaribu kutuuzia hofu baada ya kutambua kuwa utashindwa katika uchaguzi wa 2027. Hatutanunua hofu hiyo,” Bi Mbarire alisema huku akimhusisha Bw Mukunji kupanga ghasia hizo. Hata hivyo, mbunge huyo alijitetea akisema serikali inamtumia kama kafara. “Haiwezekani kila mara wanilaumu kwa kupanga ghasia. Sijahusika kwa njia yoyote,” Bw Mukunji aliwaambia wanahabari mjini Embu Jumamosi. Kwa upande mwingine, wanahabari wa Embu walilaani ghasia hizo ambapo magari mawili yaliyokuwa yakitumiwa na wanahabari yalichomwa. Wanahabari hao, wakiongozwa na mwenyekiti wa Muungano wa Wanahabari Embu Brian Malila, walisema usalama wa wanahabari lazima ulindwe katika kila mkutano wa hadhara au wa kisiasa. “Muungano huu umeshtushwa na ghasia na uharibifu ulioshuhudiwa katika Uwanja wa Nembure wakati wa mkutano wa wajumbe wa UDA,” akasema Bw Malila.

RAIS William Ruto jana alionekana kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya ODM na UDA, akisema vyama hivyo ni washirika katika Serikali Jumuishi akiahidi kulinda urithi wa kisiasa wa marehemu Raila Odinga. Akizungumza jijini Kisumu, Rais Ruto alisema atashirikiana na ODM kuhakikisha maono na ndoto ya marehemu Raila kuhusu Kenya yanatimia. “Nataka kuwahakikishia kama kiongozi wa taifa na kama mwanafunzi wa marehemu Raila Odinga kwamba tutatembea pamoja. ODM na UDA si washindani bali ni washirika katika Serikali Jumuishi,” akasema Dkt Ruto. Alisema atahakikisha mchango wa Bw Odinga kwa Kenya unaendelea kukumbukwa, akimtaja aliyekuwa Waziri Mkuu kama mzalendo ambaye maono yake ya kisiasa yalikuwa si Nyanza pekee bali taifa zima. “Kwa heshima ya ndugu yangu Raila Odinga, nitafanya kuwa jukumu langu kuhakikisha urithi wake, chama chake na yale aliyoyaamini yanaendelea tunaposhirikiana kujenga taifa,” akasema. Dkt Ruto alikuwa akizungumza katika Kanisa la Voice of Salvation and Healing jijini Kisumu, mwanzoni mwa ziara yake ya Nyanza. Alikuwa ameandamana na Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o, Gladys Wanga (Homa Bay) , Ochilo Ayacko (Migori) na viongozi wengine wanaounga mkono serikali. Kiongozi wa ODM Oburu Oginga hakuhudhuria, kwa sababu yuko Uingereza anakoendelea kupokea matibabu. Rais alieleza uhusiano wake na Bw Odinga kuwa ulijengwa juu ya maono ya pamoja ya maendeleo, akitaja reli ya kisasa ya SGR, nyumba za gharama nafuu na ajira kama baadhi ya miradi waliyoibuni walipokuwa pamoja katika ODM. “Nasimama hapa Kisumu, jiji la ndugu yangu marehemu Raila Amolo Odinga, ambaye najua angependa kuwa hapa Kisumu leo, mtu ambaye nilishirikiana naye kutekeleza maono makubwa ya Kenya,” akasema. Dkt Ruto alisema SGR ni miongoni mwa miradi ambayo Bw Odinga angejivunia kuona ikiendelea. Alisema upanuzi wa reli kutoka Narok hadi Kisumu hatimaye utatimiza mojawapo ya malengo muhimu ya maendeleo ya Bw Odinga. Gavana Wanga alisema Nyanza inashuhudia maendeleo makubwa chini ya serikali hiyo. “Leo tunashuhudia maendeleo katika eneo hili kwa kiwango ambacho hatujawahi kuona,” akasema. Alikosoa kundi la Linda Mwananchi, akisema ODM imechagua kushirikiana na serikali ya Ruto ili kupata maendeleo kwa wakazi wa Nyanza. “Wapo watu ambao kazi yao pekee ni kutoka hoteli moja hadi nyingine ilhali hawana mgombea wala sera. Sisi katika serikali ya muungano mpana tuna mgombea,” alisema.

SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna na viongozi wa Linda Mwananchi jana walitikisa Jiji Kuu la Nairobi kupitia misururu ya mikutano mikubwa iliyovumisha ujumbe wa kumbandua Rais William Ruto madarakani mnamo 2027. Ziara hiyo ilitumiwa kama ratili ya kuonyesha ushawishi wa kisiasa wa Bw Sifuna jijini, huku idadi kubwa ya waliojitokeza ikiashiria kuunga mkono vuguvugu hilo. Tofauti na mikutano ya awali ya kundi hilo Homa Bay na Kisumu, ambako kulishuhudiwa vurugu, mkutano wa Nairobi ulikuwa wa amani polisi wakitoa usalama. Bw Sifuna aliandamana na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Gavana wa Siaya James Orengo, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya miongoni mwa viongozi wengine. Viongozi hao walianza ziara yao kwa kuhudhuria ibada katika Kanisa la All Saints Cathedral kabla ya kupitia masoko ya Marikiti na Gikomba hadi Uwanja wa Jacaranda. Wakiwa Gikomba, waliwataka wapiga kura kumng’oa Rais Ruto madarakani katika uchaguzi wa 2027, wakishutumu serikali yake kwa udikteta na kutowajali wananchi wa kawaida. Bw Sifuna alisema mapokezi waliyopata Nairobi ni ishara kwamba Wakenya wamekerwa na uongozi wa Kenya Kwanza. “Ruto hajafahamu ujumbe wetu. Mitaa ya mabanda Nairobi si tatizo la nyumba bali ni tatizo la mapato. SHA haifanyi kazi na ndiyo maana hata Rais bado anatoa pesa katika michango ya harambee, jambo ambalo aliahidi wakati wa kampeni kulikomesha,” akasema Bw Sifuna. Seneta huyo alisema anahitaji uungwaji mkono wa wakazi wa Nairobi katika azma yake ya kuwania urais, lakini akasisitiza kuwa kumng’oa Dkt Ruto kutahitaji nguvu za pamoja za viongozi wa upinzani. Alitaja kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front na naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i miongoni mwa viongozi ambao wanapaswa kuungana. “Watu katika maeneo mengine ya nchi wanataka kunipeleka kwenye kazi fulani. Je, nyinyi pia mnataka niende kwenye kazi hiyo? Haitakuwa rahisi. Lazima tutembee pamoja na Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua na viongozi wengine wote wa upinzani,” akasema Nairobi ina maeneobunge 17, wadi 85 na zaidi ya wapiga kura milioni 2.7 waliosajiliwa. Idadi hiyo inatarajiwa kufikia milioni 3.1 katika uchaguzi wa 2027, hivyo kuifanya Nairobi kuwa muhimu kwa yeyote anayelenga kuingia Ikulu. Bw Sifuna pia alieleza sababu ya kutofautiana kwake na Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga, akisema hawezi kukubali kumuunga mkono Dkt Ruto kutokana na kile alichodai kuwa ni kuongezeka kwa gharama ya maisha. Linda Mwananchi inalenga kurithi maeneo ya uungwaji mkono ya marehemu Raila Odinga, ikidai kundi la Dkt Oginga limeharibu falsafa ya uongozi wa mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani. Kwa miongo kadhaa, Bw Odinga alikuwa na ushawishi mkubwa Nairobi, jiji ambalo lilikuwa nguzo muhimu ya miungano yake ya kitaifa. Katika mkutano wa jana, viongozi wa Linda Mwananchi pia walionya kuwa hawatasita kupinga matokeo ya uchaguzi katika Mahakama ya Juu iwapo yatachakachuliwa. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya alidai Mahakama ya Juu iliwahi kutumiwa kumnyima Bw Odinga ushindi wa urais. Bw Odinga alipinga matokeo ya uchaguzi wa 2013, 2017 na 2022. Mnamo 2017, Mahakama ya Juu chini ya aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ilibatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta na kuamuru uchaguzi mpya. Katika Uwanja wa Jacaranda, viongozi hao pia walimpigia debe Bw Babu Owino kuwania ugavana wa Nairobi. Walimshtumu Gavana Johnson Sakaja kwa kushindwa kutatua matatizo ya wakazi wa Nairobi licha ya kaunti hiyo kupokea mgao mkubwa zaidi wa fedha kutoka kwa serikali kuu. Bw Owino alisema Bw Sakaja amelemewa na majukumu na akadai kuwa makubaliano ya Sh80 bilioni kati ya kaunti na serikali kuu yalilenga kuficha uzembe wa utawala wake. “Wakazi wa Nairobi huamka kila siku na kukabili jiji chafu kwa sababu Sakaja hawezi kulisafisha jiji. Hilo litakuwa jambo la zamani chini ya uongozi wangu,” akasema Bw Owino. Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Seneta Crystal Asige, aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, aliyekuwa Rais wa LSK Faith Odhiambo na Wakili Laureen Mogotsi ambaye analenga kiti cha Ubunge Ikolomani Kaunti ya Kakamega.

The September 8, 2026 blockade of Peter Obi’s convoy in Benue State, as he travelled to Yelwata to commiserate with families devastated by the June 2025 massacre, is a disturbing development that must not be dismissed as a mere quarrel between politicians. It raises a fundamental question about the health of Nigeria’s democracy, where an […]

The surge in international crude oil prices above $100 per barrel is pushing up petrol prices across Nigeria, with major marketers raising pump prices and creating fresh pressure on transporters, commuters, households and businesses.

By Chris Agbedo I have read Valentine Obienyem’s “Fr. Alia and the Seduction of Power” with a mixture of concern and sadness. Concern, because the conduct attributed to Rev. Fr. Hyacinth Alia, Governor of Benue State, raises questions that deserve serious scrutiny. Sadness, because the article, in its passionate condemnation of the priest-governor, seems to […]

By Juliet Umeh The Nigerian Communications Commission, NCC, has raised the alarm over the resurgence of call masking in the country’s telecommunications industry, warning that the practice threatens industry revenues, national security and the integrity of Nigeria’s telecommunications ecosystem. The telecom regulator described call masking as an act of economic sabotage capable of adversely affecting […]

…MRS raises pump price to N1,400/litre…NNPC stations move to N1,375/litre…Independent marketers raise prices to N1,400/litre By Udeme Akpan & Marian Eko LAGOS — The surge in international crude oil prices above $100 per barrel is pushing up petrol prices across Nigeria, with major marketers raising pump prices and creating fresh pressure on transporters, commuters, households […]

DAR ES SALAAM; Mradi wa uondoshaji majitaka eneo la Buguruni, Wilaya ya Ilala unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) umefikia asilimia 40, huku wakazi takribani 181,440 wakitarajiwa kunufaika na huduma hiyo pindi utakapokamilika. Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Khalid Upunda, amesema ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kusafirisha…

By Dickson Omobola Airline Operators of Nigeria, AON, has raised the alarm over the increasing number of Air Operator Certificates, AOCs, being issued to new airlines, saying existing aviation infrastructure may not be sufficient to accommodate the expected growth in aircraft. Spokesperson for the AON, Professor Obiora Okonkwo, who welcomed increased competition in the industry, […]

The tour forms part of the Jamii Salama project, executed by JMKF alongside the Prime Minister’s Office–Regional Administration and Local Government (PMO-RALG), the Ministry of Health and Tabora regional authorities.

ARUSHA: NAIBU Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, Dk Steven Kiruswa, amesema mwakani mashindano ya Kiruswa Jimbo Cup yatakuja kwa sura mpya kwa kuongeza michezo mingine, ikiwemo mpira wa pete, mpira wa wavu na mpira wa kikapu, kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana. Kiruswa alisema hayo baada ya kuzindua…

MZOZO wa miezi kadhaa kati ya ODM na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna umefikia kikomo baada ya Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) kutupilia mbali ombi lake la kutaka kubatilisha kuondolewa kwake kama Katibu Mkuu wa chama hicho. Uamuzi huo wa Alhamisi wiki hii unafunga ukurasa muhimu katika safari ya kisiasa ya Bw Sifuna ndani ya ODM, chama ambacho alihudumu kama Katibu Mkuu kwa miaka minane tangu 2018. Lakini zaidi ya nafasi ya Bw Sifuna, mzozo huo umeonyesha mpasuko mkubwa kuhusu mwelekeo wa ODM, nidhamu ya chama na nafasi ya viongozi wanaotofautiana na msimamo rasmi wa chama. PPDT ilisema Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) ya ODM ilikuwa na mamlaka ya kuunda jopo maalum la kusikiliza tuhuma dhidi ya Bw Sifuna. Jopo hilo pia lilibaini kuwa mwanasiasa huyo alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya NEC kumwondoa katika wadhifa huo Juni 22, 2026. Hii ilikuwa hatua ya pili katika mzozo huo. Mnamo Juni 18, PPDT iliamua kuwa ODM ilikiuka haki ya Bw Sifuna ya kusikilizwa kwa haki ilipomwondoa kwa mara ya kwanza Februari 11, 2026. Hata hivyo, chama kiliruhusiwa kuanza tena mchakato wa kinidhamu kwa kufuata katiba yake na sheria za vyama vya kisiasa. ODM ilitumia nafasi hiyo kuendesha mchakato mwingine ambao sasa umeidhinishwa na PPDT. Chanzo kikuu cha mzozo kilikuwa madai ya utovu wa nidhamu. Chama kilimtuhumu Bw Sifuna kwa kutoa matamshi yaliyopingana na misimamo rasmi ya ODM, kutohudhuria baadhi ya mikutano muhimu na kushiriki shughuli za kisiasa ambazo hazikuwa zimeidhinishwa na chama. Miongoni mwa shughuli hizo ni mikutano ya Linda Mwananchi, vuguvugu ambalo limekuwa likimjenga katika siasa za upinzani. Mvutano ulianza kuchukua sura mpya Julai 2025 baada ya Bw Sifuna kuonekana katika kipindi cha televisheni na kusema Makubaliano ya Ushirikiano kati ya ODM na UDA yalikuwa “yamekufa”. Kauli hiyo haikupokelewa vyema na uongozi wa chama. Aliyekuwa kiongozi wa ODM, Raila Odinga, wakati huo alisisitiza umuhimu wa Katibu Mkuu kufuata na kutetea misimamo rasmi ya chama anapozungumza hadharani. Baada Raila kufariki, Sifuna aliendelea kushikilia msimamo wake na ODM ikamtumia notisi ya kujitetea. Seneta huyo alipinga notisi hiyo akisema haikuwa imeeleza kwa kina malalamishi dhidi yake. Chama kilitoa maelezo zaidi na kuongeza muda wa mchakato wa kusikilizwa. Wakili wa Bw Sifuna alifika mbele ya jopo la chama lakini akaibua pingamizi kuhusu uhalali na muundo wake kabla ya kujiondoa bila kujibu tuhuma zilizowasilishwa. Jopo lilitupilia mbali pingamizi hizo na kupendekeza Bw Sifuna aondolewe. NEC baadaye ilikubali pendekezo hilo. Katika kesi yake mpya, Bw Sifuna alisisitiza kuwa jopo hilo halikutambuliwa katika katiba ya ODM na hivyo halikuwa na mamlaka ya kushughulikia suala lake. PPDT, hata hivyo, ilikubaliana na chama kwamba NEC inaweza kuunda kamati au majopo ya muda kushughulikia majukumu maalum kwa niaba yake. Uamuzi huo sasa unaweka wazi kuwa kuondolewa kwa Bw Sifuna kama Katibu Mkuu wa ODM kumesalia. Kwa ODM, huu ni ushindi kwa wale ambao hawakumtaka Sifuna kwa sababu ya kuwakosoa. Kwa Bw Sifuna, hata hivyo, uamuzi huo unafungua swali la hatua yake inayofuata kisiasa. Seneta huyo amekuwa mmoja wa wanasiasa wanaohusishwa na Linda Mwananchi, pamoja na Gavana wa Siaya James Orengo, Mbunge wa Embakasi East Babu Owino na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. Kwa hivyo, kuondoka kwake katika uongozi wa ODM kunatazamwa kama baraka kwa kuwa ushawishi wake umeongezeka kwa kasi. Kwa upande mwingine, ODM sasa inakabiliwa na jukumu la kujenga upya uongozi wake na kueleza nafasi yake katika siasa za upinzani baada ya mzozo huo. Kwa sasa, uamuzi wa PPDT umefunga mzozo wa Sifuna na ODM lakini haujazima nyota yake inayozidi kung’aa.

SONGWE: THE Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) and China-based TBEA Company have signed a 198.67bn/- contract for construction of a 220kV electricity transmission line from Iganjo in Mbeya Region to Saza in Songwe Region, alongside construction of a substation at Saza. The 18-month project is expected to improve electricity supply in Songwe and Chunya District…

KINARA wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, amesema upinzani umeamua kuchelewesha kuunda afisi ya pamoja kwa sababu ya hofu ya kuingiliwa na serikali, huku akisisitiza kuwa lengo lao kuu ni kumng’oa Rais William Ruto mamlakani katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Akizungumza Ijumaa jioni mbele ya wafuasi wake mjini Portland, Oregon, Amerika anakozuru, Bw Gachagua alidai Rais William Ruto atashindwa kwa tofauti ya kura zaidi ya milioni saba. Alisema anatarajia kupokea simu kutoka kwa Rais Ruto usiku wa manane wa Agosti 10, 2027, akikubali kushindwa na kuomba kulindwa baada ya kuondoka madarakani. Gachagua pia alidai Rais amepenyeza watu wake ndani ya baadhi ya makundi ya upinzani ili kupata taarifa za siri kuhusu mikakati yao. “Majuzi tulikuwa katika kikao cha mkakati katika hoteli moja Nairobi. Kulikuwa na mmoja wa viongozi wa upinzani aliyekuwa amejiunga na muungano wetu akiwa na wanawake wawili. Hatukuwa hata tumemaliza kikao nilipoona taarifa ya kile tulichokuwa tunajadili ikiibuka kwenye simu yangu,” alisema. Hata hivyo, alionya kuwa serikali ya upinzani haitawalinda wale watakaopatikana na makosa ya ufisadi, mauaji au utekaji nyara wa vijana waliokuwa wakishiriki maandamano. “Nataka iwe wazi kuwa serikali ya upinzani haitawalinda wezi wa rasilimali za umma, wauaji au waliotekeleza utekaji nyara. Wote watawajibishwa kwa mujibu wa sheria,” alisema. Gachagua pia alikanusha madai kwamba anapanga kukutana na Rais Ruto wakati wa ziara zao nchini Amerika. “Puuzeni propaganda zinazoenezwa kwamba nina nia ya kukutana na Rais Ruto hapa Amerika. Hilo halipo kabisa katika mipango yangu,” alisema. Alieleza sababu ya kucheleweshwa kwa sekretarieti ya pamoja ya upinzani, Gachagua akisema ni rahisi kuvurugwa na serikali.

POLISI wa kutuliza ghasia Jumamosi walizuia jaribio la kundi la vijana kuvuruga mkutano wa kisiasa wa Naibu Rais Kithure Kindiki katika Uwanja wa Nembure, Kaunti ya Embu. Maafisa hao walirusha gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya vijana hao waliokuwa wakipiga kelele na kurusha mawe. Vurugu hizo zilianza wakati Profesa Kindiki alipokuwa akihutubia maafisa wa chama cha UDA kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura katika kaunti hiyo. Alipokuwa akizungumza, vijana waliokuwa nje ya uwanja huo walianza kupaza sauti na kurusha mawe kwa lengo la kuvuruga mkutano huo. Wakati mmoja walijaribu kuvamia uwanja huo lakini walizuiwa na maafisa wa usalama. Hatimaye polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi, hatua iliyozua mapambano ya kukimbizana kati yao na vijana hao yaliyodumu kwa saa kadhaa nje ya uwanja huku Kindiki akiendelea na hotuba yake bila kusitisha mkutano. Baadaye, vijana hao walitawanyika lakini walikusanyika tena baada ya mkutano kumalizika na kuzua vurugu katika eneo hilo. Walivamia barabara iliyo karibu, kuwashambulia madereva na wakazi huku wakichoma magari kadhaa, jambo lililozua hofu. Miongoni mwa magari yaliyochomwa moto ni la mwanahabari wa eneo hilo. Mfuasi mmoja wa UDA pia alijeruhiwa usoni baada ya kupigwa na jiwe na kupatiwa huduma ya kwanza.

ZIARA ya siku tano ya Rais William Ruto katika eneo la Nyanza kuanzia Jumapili, Septemba 13, imeibua mjadala mpana wa kisiasa huku wachambuzi wakisema ni zaidi ya ziara ya kawaida ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Ziara hiyo inafanyika katika kipindi nyeti kisiasa baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, jambo lililoacha pengo kubwa la uongozi katika eneo ambalo kwa miongo kadhaa lilikuwa ngome yake ya kisiasa. Rais Ruto anatarajiwa kuzuru kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay akizindua na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo barabara, maji na usafi wa mazingira, masoko, hospitali, nyumba za gharama nafuu, viwanja vya michezo pamoja na miundombinu mingine ya umma. Mbali na kuhudhuria ibada ya kanisa Kisumu, Rais pia anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali na hata kuendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika Ikulu Ndogo ya Kisumu. Kwa serikali ambayo imekuwa ikitumia maendeleo kama silaha yake kuu ya kisiasa, ziara hiyo ni nafasi muhimu ya kuwashawishi wakazi wa eneo ambalo kwa muda mrefu lilimuunga mkono Raila Odinga na chama cha ODM. Hata hivyo, umuhimu wa kisiasa wa ziara hiyo unazidi miradi inayozinduliwa. Kifo cha Raila Odinga mnamo Oktoba 15, 2025, kiliondoa mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa zaidi Nyanza na kuacha swali kubwa kuhusu ni nani atakayerithi mtandao wake wa kisiasa na kura zake. Katika mahojiano maalum yaliyopita, Rais Ruto alikiri kuwa uwepo wa Raila ungeathiri kwa kiasi kikubwa mazingira ya kisiasa ya sasa. Alimtaja Raila kama mwanasiasa wa kipekee aliyekuwa na ujasiri, maono na uelewa wa masuala ya taifa. Vilevile alisema yeye na Raila walikuwa na sera walizokubaliana, ikiwemo mpango wa nyumba za gharama nafuu na huduma ya afya kwa wote. Ruto sasa anaonekana kutaka kuwashawishi wakazi wa Nyanza kuwa ushirikiano kati ya serikali yake na viongozi waliokuwa karibu na Raila unaweza kuendelea kunufaisha eneo hilo. Tayari baadhi ya viongozi wa zamani wa ODM wanahudumu katika serikali yake, wakiwemo Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi, Waziri wa Fedha John Mbadi, Waziri wa Madini Hassan Joho na Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya. Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa, Rais atajaribu kuunganisha ujumbe wa maendeleo na ujumuishaji wa kisiasa kwa kuonyesha kuwa Nyanza haifai kuwa upande wa upinzani ili kupata rasilimali za kitaifa na uwakilishi serikalini. Lakini upinzani pia unajipanga. Makundi mbalimbali yanayowania urithi wa kisiasa wa Raila tayari yameanza kufanya ziara katika eneo hilo. Miongoni mwao ni vuguvugu la Linda Mwananchi ambalo limekuwa likisisitiza kuwa maendeleo peke yake hayawezi kuchukua nafasi ya uwajibikaji, utawala bora na kuheshimiwa kwa Katiba. Hali hiyo inakita ujumbe wa serikali wa maendeleo dhidi ya ujumbe wa upinzani unaojikita katika masuala ya utawala. Katika kaunti ya Kisumu, Rais anatarajiwa kuzindua mnara wa kudhibiti safari za ndege katika uwanja wa ndege, kukagua makao ya polisi na kuzuru barabara ya Mamboleo-Miwani-Chemelil-Muhoroni pamoja na miradi ya maji. Atazuru pia sekta ya Jua Kali. Katika Siaya, atakagua Daraja la Dhogoye, hospitali ya Siaya, miradi ya makazi, viwanja vya michezo na mtandao wa barabara katika maeneo ya Bondo, Ugenya, Alego Usonga na Rarieda. Mbunge wa Bondo Gideon Ochanda amesema Daraja la Dhogoye yatakuwa hatua kubwa kwa wakazi kutokana na umuhimu wake katika kurahisisha mawasiliano, usafiri na biashara. Migori nayo iko katika ratiba ya Rais ambapo atakagua barabara katika maeneo ya Uriri, Awendo na Suna Mashariki pamoja na kituo cha umeme cha Masaba katika Kuria Magharibi. Katika Homa Bay, Rais anatarajiwa kuzindua masoko, barabara za mji na miradi ya taasisi ya mafunzo ya matibabu ya KMTC ya Sindo. Wakati huo huo, viongozi wa eneo hilo wanataka miradi mikubwa kama Bwawa la Koru-Soin, Uwanja wa Moi Stadium na barabara ya Mamboleo-Miwani-Chemelil kukamilishwa haraka. Hatua za usalama pia zimeimarishwa kufuatia tukio la hivi majuzi Siaya ambapo vijana walidaiwa kujaribu kuzuia msafara wa viongozi waliohudhuria hafla ya kuwawezesha wanawake kiuchumi iliyoongozwa na Mama wa Taifa Rachel Ruto. Kamishna wa eneo la Nyanza, Onesmus Kyatha, amesema ziara hiyo inalenga maendeleo na kwamba maandalizi yote ya usalama yamekamilika ili kuhakikisha shughuli zinaendeshwa kwa utulivu.

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 umeingia katika mdahalo mpya baada ya Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar, kudai kwamba hata wapiga kura waliokufa wanaweza kutumiwa katika juhudi za kumhakikishia Rais William Ruto ushindi. Kauli hiyo aliyotoa Mombasa Ijumaa imezua mjadala mkali kuhusu uaminifu wa uchaguzi wa 2027, huku masuala ya sajili ya wapiga kura, taarifa za vitambulisho vya waliofariki na matumizi ya teknolojia ya kibayometriki yakipewa uzito mpya. Bw Omar alionekana kudokeza kuwa mianya katika mfumo wa uchaguzi inaweza kutumiwa kwa kutumia utambulisho au taarifa za kibayometriki za watu waliokufa ili kuongeza kura katika uchaguzi wa urais na nyadhifa nyingine. “Siku ya uchaguzi, hata sisi lazima tupambanie kila kura. Hata kama mtu amefariki, tuchukue kidole chake kabla hajazikwa, tukitumie katika mfumo wa BVR na tupige kura hata kama mtu huyo amefariki siku hiyo hiyo,” alisema Bw Omar. Kauli hiyo inatarajiwa kuzua mjadala mkali huku vyama vya kisiasa vikijipanga kwa uchaguzi ambao tayari umeanza kuonekana kuwa wenye ushindani mkubwa. Bw Omar aliunganisha madai hayo na azma ya kuhakikisha Rais Ruto anahifadhi kiti chake na washirika wake wanapata nafasi kubwa zaidi katika serikali ijayo. “Hata yule tunayemzika leo, hiyo kura ndiyo risasi yetu, ngao yetu. Haiwezekani kurudi tena pale tulipokuwa,” akaongeza. Alisema kuwa kuongeza idadi ya watu waliosajiliwa kuwa wapiga kura kungeipa serikali nafasi kubwa ya kudai nyadhifa zaidi, zikiwemo nafasi za uwaziri na nyadhifa nyingine za juu serikalini. Kauli hizo zimeibua maswali iwapo Bw Omar alikuwa akionya kuhusu mianya inayoweza kutumiwa katika uchaguzi au alikuwa akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila kura inahesabiwa katika kampeni za 2027. Aidha, zimeibua tena suala la usahihi wa sajili ya wapiga kura, hasa kuhusu kuondolewa kwa majina ya watu waliofariki na usalama wa taarifa zao za kibinafsi. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) huenda ikakabiliwa na shinikizo zaidi kueleza namna inavyotambua wapiga kura waliofariki na kuwaondoa kwenye sajili, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuzuia mtu mwingine kutumia utambulisho wa marehemu kupiga kura. Suala hilo ni nyeti kutokana na historia ya uchaguzi nchini ambapo madai ya wapiga kura hewa, sajili yenye dosari na udanganyifu wa kura yamekuwa yakizua mivutano mikubwa ya kisiasa. Kauli ya Bw Omar pia imepewa uzito kwa sababu yeye si mwanasiasa wa upinzani anayekosoa mfumo wa uchaguzi, bali ni Katibu Mkuu wa chama tawala cha UDA. Wakati huohuo, Bw Omar anajiandaa kuwania tena kiti cha ugavana wa Mombasa, katika kinyang’anyiro kinachotarajiwa kuwahusisha wanasiasa kadhaa wenye ushawishi. Amekataa wazo la kugawana maeneo ya kisiasa kwa vyama, akisisitiza kuwa wananchi ndio wanaopaswa kuamua viongozi wao. “Siku ile nilisema hakuna ‘zoning’, akasema atakwenda kuzungumza na boss wangu, sijui ni nani. Hawa ndio boss wangu. Kujeni zungumza na watu hapa,” alisema.

Calls for closure of illegal sand mining sites By Jeff Agbodo AWKA — The International Society for Civil Liberties and Rule of Law, Intersociety, has raised the alarm over what it described as devastating gully erosion at Ugo Community in Aguata Local Government Area of Anambra State. The group, in a petition to Governor Chukwuma […]

ZANZIBAR: CHAMA cha Mawakili Zanzibar (ZLS), kimetoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan. Salamu hizo zimewasilishwa leo, Septemba 12, 2026, katika makazi binafsi ya Rais Dk Samia yaliyopo Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Ujumbe wa…

By Udeme Akpan, Energy Editor The Dangote Petroleum Refinery has increased its Premium Motor Spirit, PMS, popularly known as petrol, gantry price by 6.7 per cent to N1,350 per litre from N1,265 per litre, effective September 12, 2026.The refinery also raised its coastal price to N1,783,530 from N1,669,543, representing an increase of N113,987, or 6.8 […]

TANGA: COASTAL Union Assistant Coach Luhaga Makunja has said the team has completed preparations for its match against JKT Tanzania, with all players in good condition and ready to fight for a positive result. The teams are expected to meet today in the mainland league and game to be played at the CCM Mkwakwani stadium…

At least 23 prisoners have died in Tunisia in recent weeks due to extreme heat, as harsh detention conditions raise concerns

ARUSHA: KAMPUNI ya kimataifa ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Barrick Gold, kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Kiseriani, Kata ya Engikaret, Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha, Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Steven Kiruswa na Serikali, imefanikisha ujenzi wa shule shikizi kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 230. Akizungumza katika uzinduzi wa…

IRINGA: Ziara ya Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bashiru Ally Kakulwa, katika eneo la Pawaga, Jimbo la Isimani, imeelezwa kuwa na tija kwa wananchi baada ya kuwezesha serikali kuona kwa pamoja changamoto za kilimo, mifugo na maji na kuanza kuweka mikakati ya kuzitatua. Mbunge wa Isimani, Emanuela Mtatifikolo Kaganda,…

MWANAWE aliyekuwa Waziri mwenye nguvu Simeon Nyachae amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuiba Sh1.2 milioni kutoka kwa kampuni ya familia. Michael Moragia Nyachae, ambaye pia ni mwenyekiti wa Development Bank of Kenya, amekana shtaka moja la kuiba fedha hizo kutoka kwa kampuni ya familia ya Sansora Group Limited. Kwa mujibu wa mashtaka, Moragia alidaiwa kuiba fedha hizo tarehe tofauti kati ya Machi 28, 2019 na Septemba 28, 2021, katika Kaunti ya Kisii kinyume na Kifungu cha 268(1), kikisomwa pamoja na Kifungu cha 275 cha Sheria ya Adhabu. Kupitia mawakili wake, Moragia aliomba mahakama imwachilie kwa dhamana. “Tunaomba mahakama kutumia busara yake. Bila shaka, mtu aliye mbele yenu anatoka katika familia inayoheshimika,” wakili wake alisema. Upande wa mashtaka haukupinga ombi hilo. Mahakama ilisema masharti ya dhamana yanalenga kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani anapohitajika. “Kwa kuwa hakuna hofu kwamba mshtakiwa anaweza kutoroka, mahakama itatumia busara yake na kumpa dhamana kwa masharti yafuatayo,” mahakama ilisema. Moragia aliamriwa kuweka dhamana ya Sh50,000 taslimu au mdhamini wa kiasi sawa na Sh200,000 ili kuachiliwa. Kesi hiyo itatajwa Septemba 29 kwa maelekezo ya kabla ya kusikilizwa. Simeon Nyachae alifariki Februari 1, 2021, na watoto wake wamekuwa katika mzozo wa urithi kuhusu usimamizi wa mali yake. Katika wosia wake wa mwisho wa Septemba 9, 2015, Bw Nyachae aliwateua watu watatu wa familia kuwa wasimamizi wa urithi wake na kutaja wanafamilia waliosalia, akiwemo wajane wake watatu. Januari mwaka huu, Mahakama Kuu ilikataa ombi la Margaret Kerubo Chweya na watoto wake wawili kutambuliwa kama wanufaika wa urithi huo.

KAMPUNI ya teknolojia kutoka Amerika imefichua operesheni ya kisiasa Kenya iliyotumia Akili Unde (AI) kueneza ujumbe wa kisiasa kwa njia iliyolenga kuonekana kana kwamba unatoka kwa wananchi wa kawaida. Kampuni ya Anthropic, inayomiliki mfumo wa AI wa Claude, ilisema iligundua akaunti iliyokuwa ikitumiwa na mtu mmoja kuzalisha kwa wingi maudhui ya kisiasa. Ujumbe huo uliundwa ili kuonekana kama maoni ya kawaida ya wananchi huku ukimsifu Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi na wakati huo huo kueneza madai kwamba, upinzani ulikuwa ukisambaratika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, sehemu kubwa ya maudhui hayo ilimsifu Wandayi kwa madai ya kusaidia kusitisha ongezeko la ushuru wa umeme wa Kenya Power. Ujumbe huo ulitumia lebo za mitandaoni kama #PowerReliefKE na #PoweringTheNewKenya ili kuongeza usambazaji wake na kuonekana kama unaungwa mkono na wananchi wengi. Anthropic ilisema operesheni hiyo ilikuwa imepangwa kwa ustadi mkubwa, huku AI ikitumika kuzalisha makundi ya ujumbe 50 kwa wakati mmoja uliokuwa tayari kuchapishwa kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii. Mbali na kumsifu Wandayi, mtandao huo pia ulisambaza madai kuwa muungano wa upinzani ulikuwa ukikumbwa na migawanyiko. Ripoti hiyo ililenga moja kwa moja aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na Rais (mstaafu) Uhuru Kenyatta kwa kuendeleza simulizi za migawanyiko ndani ya upinzani. Hata hivyo, Anthropic ilisema kampeni hiyo haikufanikiwa kuwashawishi wananchi halisi. Kampuni hiyo iliorodhesha operesheni hiyo katika kiwango cha chini kabisa cha ushawishi, ikisema shughuli zake zilibaki miongoni mwa akaunti bandia na kushawishi wachache mtandaoni. Ripoti hiyo imeibua hofu kuhusu matumizi ya AI katika siasa za Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027. Wataalamu wanaonya teknolojia hiyo inaweza kutumiwa kutengeneza hisia za umma zisizo za kweli kwa kuzalisha maelfu ya jumbe zinazoonekana kutoka kwa raia wa kawaida.

KIGOMA: Halmashauri za Mkoa wa Kigoma zimetakiwa kuipa kipaumbele miradi ya sekta ya afya ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kwa gharama nafuu. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, Wazo Mwang’onda, alisema hayo katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu wakati mwenge wa uhuru ukiweka Jiwe la Msingi la ujenzi…

MTWARA: SERIKALI imekabidhi gari kwenye Kituo cha Afya Kiromba kilichopo Kata ya Kiromba Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara litakayotumika kubeba wagonjwa kwenye maeneo hayo. Zoezi la kukabidhi gari hilo limefanyika leo Septemba 11,2026 katika kijiji na kata ya kiromba wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika kwenye kijiji hicho. Mkutano huo umefanywa na Mbunge wa…

KATIBU Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), Hassan Omar, ameungana na mfanyabiashara Suleiman Shahbal kupinga juhudi zozote za kisiasa zinazolenga kuwazuia wagombeaji wengine kuwania ugavana kaunti ya Mombasa na kumpa Gavana Abdulswamad Nassir njia rahisi ya kutetea kiti chake mwaka wa 2027. Omar alisema uamuzi wa nani anapaswa kuongoza Mombasa unapaswa kuachwa mikononi mwa wapigakura na si kufanywa kupitia makubaliano ya viongozi wa kisiasa. Alisisitiza kuwa kila mwanasiasa anapaswa kurejea kwa wananchi na kujieleza kuhusu rekodi yake ya uongozi badala ya kutegemea mipango ya kutangaza wagombeaji. “Kusiwe na makubaliano ya kisiasa wala mtu kulazimishwa kujiondoa. Wananchi ndio waamue wanayetaka kuwa kiongozi wao,” alisema Omar. Kiongozi huyo wa UDA, ambaye pia anawania ugavana Mombasa, alikosoa vikali utawala wa sasa wa kaunti hiyo akidai kuwa umeshindwa kutimiza matarajio ya wakazi. Alisema wakazi wa Mombasa wana haki ya kuchagua kiongozi mpya na kwamba kiti cha ugavana hakipaswi kuamuliwa kwenye meza za mazungumzo. Kauli za Omar zinaoana na msimamo wa Shahbal ambaye amekuwa akipinga kile anachodai ni njama ya kisiasa ya kumzuia kuwania ugavana. Shahbal amesisitiza kuwa atawania kiti hicho licha ya Rais William Ruto kumshauri aendelee kuwekeza katika sekta ya biashara badala ya kuingia tena katika siasa za uchaguzi. Akizungumza katika hafla ya uwekezaji Ikulu Nairobi hivi majuzi, Rais Ruto alisema mchango mkubwa wa Shahbal kwa taifa ni kupitia uwekezaji unaozalisha ajira na kukuza uchumi. Hata hivyo, Shahbal alikataa ushauri huo na kutangaza kuwa jina lake litakuwa kwenye kura mwaka wa 2027. Mfanyabiashara huyo pia alidai kuwa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanatumia miundo ya vyama na hoja ya kutengewa maeneo ya kisiasa ili kuamua nani anapaswa kugombea viti mbalimbali vya uongozi. Wakati huo huo, baadhi ya madiwani kaunti ya Mombasa wamemtetea Gavana Nassir na kumtaka Shahbal kutii ushauri wa Rais. Wamesisitiza kuwa gavana huyo ana rekodi nzuri katika sekta za afya, elimu na maendeleo mengine ya kijamii. Mvutano huo umeweka Omar na Shahbal katika muungano usio wa kawaida. Ingawa wote wawili wanapania kugombea ugavana wa Mombasa na huenda wakawa wapinzani wakubwa baadaye, kwa sasa wanashirikiana kupinga juhudi zozote za kumhakikishia Nassir muhula wa pili kupitia makubaliano ya kisiasa. Huku Shahbal akisisitiza kuwa hatajiondoa kwenye kinyang’anyiro, Omar akiendelea kufanya kampeni zake na Nassir akitetea utawala wake, ushindani wa ugavana Mombasa unaonekana kuwa miongoni mwa vita vya kisiasa vitakavyovutia macho ya wengi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

By Valentine Obienyem Seneca was a notable philosopher who lived under Emperor Nero. He preached ascetic virtues but was accused of accumulating enormous wealth. Being a man of letters capable of defending himself, Seneca wrote: “I persist in praising not the life that I lead, but that which I ought to lead. I follow it […]

KENYA inakabiliwa na hatari aina tatu za mafuriko wakati wa msimu wa mvua miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba, huku hali ya El Niño ikiimarika na baadhi ya maeneo tayari yakianza kupokea mvua kubwa. Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema kuna uwezekano wa karibu asilimia 100 kwamba, hali hiyo itaendelea hadi Februari 2027. Nchini Kenya, El Niño inahusishwa na mvua nyingi kuliko kawaida katika maeneo mengi. Takriban watu milioni 1.5 katika kaunti zote 47 wanaweza kuathirika, kwa mujibu wa tathmini ya awali ya serikali. Hata hivyo, ripoti kamili kuhusu maandalizi ya nchi bado haijakamilika. Mamlaka ya Hali ya Hewa Kenya (KMSA) imetambua hatari ya mafuriko mijini, mafuriko ya mito na mafuriko ya ghafla. Hatari hizi zinatofautiana kulingana na aina ya ardhi, mifumo ya mitaro na ukaribu wa mito na maziwa. Zacharia Mwai, mkurugenzi msaidizi wa Huduma za Hali ya Hewa na Maji katika KMSA, alisema Nairobi ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya mafuriko mijini. Mito ya Nairobi, Mathare na Mbagathi ni miongoni mwa maeneo yanayofuatiliwa. Ramani iliyofanywa na Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Maafa, Shirika la Msalaba Mwekundu na Idara ya Usimamizi wa Maafa ya Kaunti ya Nairobi imetambua maeneo 246 yanayoweza kuwa hatarini. Katika maeneo ya mijini, majengo na barabara nyingi zenye lami huzuia maji kupenya ardhini. Hivyo, mvua kubwa huongeza kiwango cha maji yanayotiririka na kuzidisha shinikizo kwenye mabomba. Eneo la Nyali, Mombasa, ambalo limekuwa likikumbwa na mafuriko mara kwa mara, pia limetajwa kuwa eneo hatari. Kisumu ni miongoni mwa miji inayofuatiliwa kutokana na uwezekano wa mafuriko. Lakini hatari hiyo haiko mijini pekee. Bonde la Tana ni miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kuathirika zaidi. Eneo la chini la Tana linaanzia karibu na Garissa na kuendelea hadi Madogo, Bura, Hola na delta ya Tana. Delta ya Tana ni eneo hatari kwa sababu ardhi yake ni tambarare. Wakati wa mvua za El Niño za 2023/2024, baadhi ya maeneo yalikatizwa na mafuriko. Katika Magharibi mwa Kenya, Bonde la Mto Nzoia, hasa maeneo ya Budalangi na Bunyala, pia liko hatarini. Maji kutoka Ziwa Victoria yanaweza kurudi kwenye mto na kuongeza hatari kwa wakazi wanaoishi karibu na mto. Mito ya Nyando na Yala pia imetajwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko. Katika Bonde la Ufa, Narok ni miongoni mwa maeneo yaliyotajwa kuwa hatarini. Mito mingine kama Ewaso Ng’iro inaweza pia kusababisha mafuriko ya ghafla, hasa karibu na Isiolo, ambapo maji yanaelekea Lorian Swamp. Kaskazini mwa Kenya, Turkana, Wajir, Mandera, Marsabit na Garissa zinakabiliwa na hatari ya mafuriko ya ghafla kutokana na kuwepo kwa mito ya msimu. Maeneo haya yanaweza kupokea mvua nyingi baada ya kipindi kirefu cha ukavu. Maji yanaweza kutiririka kwa kasi kabla hayajapenya ardhini, na kusababisha mafuriko ya ghafla. Kitui na maeneo mengine ya mashariki mwa Kenya pia yana mito mikubwa ambayo huwa mikavu kwa muda mrefu lakini hujaa maji kwa kasi mvua inaponyesha. Serikali imeanza maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hiyo. Lengo ni kuepuka madhara yaliyotokea wakati wa mvua ya 2023/2024 ambayo ilisababisha hasara kubwa.

By Polycarp Ifeanyi History was made in Onitsha, the commercial hub of Anambra State, as thousands of people from across the state and neighboring states converged on the city to participate in Ave Maria Praise 2026. The event, themed “Fill the Jars, Make Room for Fresh Wine”John 2:1-11, was organized by Faithspiration Initiative, led by […]

KIGOMA: MKOA wa Kigoma umefanikiwa kusajili makundi maalumu 1,359 katika Mfumo wa Manunuzi ya Umma (NeST), hatua inayoyawezesha makundi hayo kushiriki katika utekelezaji wa mpango wa manunuzi ya umma katika taasisi za Serikali. Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kati na Magharibi, Mhandisi Suma Atupele, ametoa taarifa hiyo kwa…

MBUNGE wa Makadara George Aladwa Ijumaa alisema ODM haina nia ya kuvuruga wala kuingilia mkutano wa Linda Mwananchi ambao utafanyika mnamo Jumapili katika uwanja wa Jacaranda, Nairobi. Bw Aladwa alisema Linda Mwananchi ina haki ya kufanya shughuli zake za kisiasa na kuwafikishia wakazi wa Nairobi ujumbe wake. Alisisitiza kuwa ushindani wa kisiasa unafaa kujikita katika sera na mawazo badala ya makabiliano kati ya wafuasi wa vyama. “Linda Mwananchi iko huru kufanya mkutano wake na shughuli zake za kisiasa Nairobi. Kenya ni nchi ya kidemokrasia inayohakikisha kila kundi au mrengo wa kisiasa una haki ya kukusanyika, kuhamasisha wafuasi na kuwasilisha ajenda kwa wananchi,” akasema Bw Aladwa. Aliongeza kuwa ODM Nairobi haina sababu ya kuingilia mkutano huo na haitafanya hivyo. Vinara wa Linda Mwananchi Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wanatarajiwa kuongoza mkutano huo wa Jacaranda. “Waache wafanye mkutano wao na waambie wakazi wa Nairobi wanachosimamia na kile wanachonuia kuwapa Wakenya. Wananchi wana akili ya kusikiliza jumbe mbalimbali za kisiasa na kufanya maamuzi yao,” akasema Bw Aladwa. Pia mbunge huyo alimpongeza Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kwa kujitolea kuhakikisha usalama unadumishwa wakati wa mkutano huo. Alisema ODM Nairobi kwa sasa imejikita katika kuimarisha chama hicho jijini kupitia mikutano mbalimbali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. “Lengo letu kama ODM Nairobi liko kwingine. Kwa sasa tunaendesha mpango wa kuimarisha chama katika maeneo yote ya Nairobi,” akasema mwenyekiti huyo wa ODM Nairobi. Bw Aladwa alisema chama hicho pia kinajiandaa kwa sherehe za kuadhimisha mwaka moja baada ya kifo cha marehemu aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Akizungumza kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa 2027, Bw Aladwa aliwataka wafuasi wa ODM kuwa watulivu na kuepuka kuchokozwa na kuingia katika makabiliano yasiyo ya lazima. “Hatuna chochote cha kuthibitisha kupitia vurugu au kuvuruga shughuli za wengine,” akasema. Bw Aladwa pia alitoa wito kwa wafuasi wa Linda Mwananchi kuheshimu shughuli za ODM kama ambavyo chama chake kitaheshimu shughuli zao. Alisema ODM itaendelea kuwafikia wananchi katika maeneobunge na wadi zote za Nairobi ili kueleza ajenda yake na kuimarisha chama kabla ya uchaguzi wa 2027. “Nairobi ni yetu sote ni jiji kuu ambalo sauti na makundi mbalimbali ya kisiasa yanapaswa kuruhusiwa kufanya shughuli zao kwa uhuru na amani,” akasema.

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kutumia teknolojia za kisasa katika kufuatilia mtiririko wa maji ili kupunguza upotevu wa maji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa mamlaka hiyo kupunguza utegemezi wa taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu changamoto za…

KWA muda wa miezi kadhaa, wataalamu wa hali ya anga wamekuwa wakiutahadharisha ulimwengu kuhusu ujio wa mvua ya El Nino. Kulingana na ripoti za kitaalamu, kipindi cha kuanza kwa mvua hiyo inayotarajiwa kuzua madhara tele kimewadia. Huku mvua hiyo kubwa ikitarajiwa kunyesha katika maeneo mengi ya Kenya kuanzia Oktoba, Serikali imewaonya wananchi wanaoishi kando ya mito, katika maeneo ya mabonde na maeneo mengine yenye hatari kuhama mapema na kutafuta makao salama. Ushauri huu haupaswi kupuuzwa. Ni wito wa kuokoa maisha. Historia ya Kenya imejaa mifano ya madhara yanayosababishwa na mvua kubwa. Mafuriko huvamia makazi, mito huvunja kingo, hubomoa madaraja na kuvuruga barabara. Katika maeneo yenye miinamo, udongo uliolowa maji unaweza kusababisha maporomoko ya ardhi, huku nyumba zisizo imara zikiwa katika hatari ya kuporomoka. Wakazi wanaoishi kando ya mito na katika maeneo yaliyotambuliwa kuwa hatari wanapaswa kuzingatia maagizo ya kuhama. Familia katika maeneo kama vile Budalang’i na Nyando zinapaswa pia kuwa na mpango wa dharura unaoeleza mahali pa kwenda, njia salama za kufika huko na namna ya kuwasiliana iwapo wanafamilia watatenganishwa na mafuriko. Aidha, wananchi wanapaswa kusaidia mamlaka kusafisha mifereji na njia za kupitisha maji. Mifereji iliyozibwa na taka huzidisha mafuriko, hasa mijini. Serikali za kaunti nazo zinapaswa kuhakikisha mifereji inasafishwa, madaraja na barabara zinazohitaji matengenezo zinashughulikiwa na vituo vya kuhifadhi waathiriwa vinaandaliwa mapema. Madereva nao hawapaswi kujaribu kuvuka maji yanayotiririka kwa kasi. Maji yanayosonga yana nguvu kubwa na yanaweza kulisomba gari pamoja na abiria wake. Wazazi wanapaswa kuwaonya watoto dhidi ya kucheza au kuvuka mito na mifereji iliyojaa maji. Muhimu zaidi, wananchi wanapaswa kufuatilia taarifa za hali ya hewa na maonyo kutoka kwa mamlaka badala ya kutegemea uvumi mitandaoni. Serikali imesema imeanza kutumia viongozi wa mashinani, wakiwemo machifu na viongozi wa Nyumba Kumi, kufikisha tahadhari kwa wananchi. Madhara ya El Nino yanaweza kupunguzwa ikiwa tahadhari zitachukuliwa mapema. Serikali na wananchi wana jukumu la kuhakikisha kuwa tahadhari hizi kuhusu mvua hiyo zinazingatiwa kwa dhati. Wakati wa kuhama ni kabla ya mafuriko, nao wakati wa kujiandaa ni sasa. Tusisubiri maafa yatufundishe thamani ya tahadhari na maisha yetu.

UAMUZI wa mfanyabiashara na mwanasiasa Suleiman Shahbal kukataa jaribio la Rais William Ruto kumshawishi asigombee ugavana wa Mombasa, na kutangaza kujiondoa katika Chama cha ODM, kumesababisha mwelekeo mpya wa kisiasa katika ushindani wa ugavana wa kaunti hiyo. Awali, Bw Shahbal alitarajiwa kushindania tikiti ya ODM dhidi ya Gavana Abdulswamad Nassir kuwania ugavana 2027, kabla Dkt Ruto kujaribu kumshawishi ajiondoe kwenye kinyang’anyiro Jumanne. Katika mahojiano na wanahabari wa Mombasa Jumatano usiku, mwanasiasa huyo alisisitiza atakuwa debeni hata kama ODM haitampa tikiti. Alidai kuwa, Rais Ruto alishawishiwa na watu wanaotaka kumtoa kwenye kinyang'anyiro hicho. “Ninaamini Rais alichochewa kutamka maneno hayo, kwamba mimi ni mfanyabiashara na ninapaswa kuwaachia wanasiasa siasa. Ndiyo maana wanasukuma suala la kugawana maeneo. Kwa nini hamwaachi wananchi waamue?” Bw Shahbal alisema. Huku akitangaza kujiondoa kutoka ODM, alisema anaamini chama hicho hakitamteua. “Tuko katika ‘talaka ya kirafiki’ na ODM. Chama hakitaniteua na ninajiandaa na jukwaa jipya la kisiasa. Tuna chama chetu cha kisiasa ambacho tutakitangaza hivi karibuni,” Mjumbe huyo wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) alisema. Katika uchaguzi wa mwaka wa 2022, Bw Shahbal alijiondoa katika kinyang'anyiro cha ugavana na kumuunga mkono Bw Nassir. Jumanne, Rais Ruto alimshauri kutorejea katika kinyang'anyiro hicho, akisema Kenya ingenufaika zaidi kutokana na ujuzi wake wa biashara, uwekezaji na uundaji wa nafasi za ajira kuliko kuingia katika siasa. Rais alikuwa akizungumza wakati wa kutiwa sahihi kwa makubaliano ya Sh12 bilioni kati ya GulfCap Group ya Bw Shahbal na kampuni ya kimataifa ya shughuli za bandarini ya DP World, kwa ajili ya kuanzisha eneo maalumu la kiuchumi lenye ukubwa wa ekari 535 Jomvu. Bw Shahbal alikiri kuwa ana urafiki na Dkt Ruto na akamsifu Rais kwa kutambua mafanikio yake katika biashara. Hata hivyo, alisema hakubaliani na ushauri wa kuachana na siasa. Alihoji kwa nini Rais, ambaye pia ni mfanyabiashara, angemwomba achague kati ya biashara na uongozi wa kisiasa. Kulingana naye, wanasiasa wengi wa Kenya wamewekeza katika biashara, akisema biashara na siasa zina malengo tofauti. “Unajua biashara ni jambo la kibinafsi; unapata hasara na faida ambazo hunufaisha familia yako na wafanyakazi wako. Lakini katika siasa, unapogombea uongozi, ni tendo la kujitolea kuwahudumia wananchi,” alisema. Alikosoa ODM kwa kutumia vibaya uteuzi wa wagombea kwa manufaa ya watu wachache, akidai kwamba baadhi ya madiwani waliotaka kumuunga mkono mwaka wa 2022 walitishiwa kunyimwa tiketi za chama. “Enzi ya kuamua wanasiasa wanaopaswa kugombea na wale wanaopaswa kujiondoa imepitwa na wakati,” alisema. Uamuzi wake wa kuondoka katika chama hicho unaweza kujaribu uwezo wake wa kujenga nguvu za kisiasa nje ya chama ambacho kimekuwa nguvu kubwa katika siasa za Mombasa kwa zaidi ya muongo mmoja. Hata hivyo, Bw Shahbal amekuwa akitumia vyama tofauti katika azma zake za uongozi, vikiwemo Wiper na Jubilee, tangu mwaka 2013. Alikanusha pia uwezekano wa kukubali nafasi ya uwaziri iwapo atapewa. Bw Shahbal anasema hagombei wadhifa huo kwa ajili ya kujipatia fedha, bali anataka kuwatumikia wananchi. Amependekeza kutengwa kwa Sh50 milioni kila mwaka kwa kila wadi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta za afya, vijana, wanawake na usalama, akisema rasilimali zinapaswa kugawanywa moja kwa moja zaidi hadi ngazi ya mashinani.

MZOZO wa kisheria umeibuka kuhusu kampuni zinazostahili kuchapisha karatasi za kura za uchaguzi wa 2027, huku Mahakama ikichunguza masharti ya zabuni ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Kampuni ya humu nchini, Oilmax Ventures Ltd, imewasilisha mzozo huo Mahakama Kuu baada ya Bodi ya Mapitio ya Ununuzi wa Umma (PPARB) kukataa malalamiko yake kuhusu masharti ya uzoefu na uwezo wa kifedha. Mahakama imesimamisha mchakato wa zabuni hadi kesi hiyo itakapoamuliwa. Mzozo huo unahusu zabuni iliyotangazwa na IEBC Agosti 11, 2026 ya kusambaza karatasi za kura, vifaa maalumu kwa wapigakura wenye ulemavu wa kuona, Sajili ya Wapigakura na fomu za kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Zabuni hiyo ilihitaji kampuni zinazowania kuwa zimekamilisha angalau mikataba miwili ya awali ya uchapishaji wa stakabadhi za uchaguzi zenye alama za usalama, mmoja ukiwa wa angalau karatasi za kura milioni 150 ndani ya miaka mitano iliyopita. Pia, zilitakiwa kuwa na wastani wa mapato ya Sh6 bilioni kwa mwaka 2023, 2024 na 2025, pamoja na uwezo wa kupata Sh10 bilioni kwa mtiririko wa kifedha wa kugharamia usambazaji. Oilmax ilipinga masharti hayo ikisema ni ya kibaguzi, yenye kuondoa ushindani na yasiyolingana na zabuni hiyo. PPARB ilikataa malalamiko hayo Septemba 3, ikisema Oilmax haikuthibitisha kuwa masharti hayo yalikuwa kinyume cha sheria. Bodi hiyo ilikubali maelezo ya IEBC kwamba uchaguzi wa 2027 utahitaji takriban karatasi za kura milioni 168. Ilibaini kuwa hitaji la karatasi milioni 150 lilikuwa sawa na asilimia 89.3 ya mahitaji hayo na lilihusiana na ukubwa wa zabuni. Hata hivyo, Oilmax sasa imeibua suala jingine kuhusu sharti la asilimia 40 ya maudhui ya ndani katika zabuni hiyo. Kampuni hiyo inasema kampuni za kimataifa zenye uwezo wa kuchapisha karatasi milioni 150 huenda zisitimize sharti la asilimia 40 ya ushiriki wa kampuni za Kenya. Mkurugenzi wa Oilmax Mohammed Ali alisema angalau asilimia 40 ya mkataba ilipaswa kutekelezwa na watengenezaji wa Kenya au wakandarasi raia wa Kenya. Kesi hiyo itatajwa Oktoba 7.

FOR more than 150 kidney patients gathered under canopies in Enugu, and thousands of others across the country, the struggle goes beyond the pain of a failing organ. It is a daily battle to raise the money needed to stay alive. Recently, videos and pictures of some of the patients in Enugu surfaced on social media, drawing.

KIONGOZI wa ODM, Oburu Oginga, amesafiri Uingereza kwa uchunguzi wa kawaida wa afya huku akitarajiwa kushiriki shughuli za kisiasa na Wakenya wanaoishi nchini humo. Safari hiyo imejiri wakati ambapo chama cha ODM kimezindua ratiba ya shughuli za mwezi mzima za kumuenzi marehemu Raila Odinga, ambazo zitafanyika katika sehemu mbalimbali za nchi hadi mwishoni mwa Oktoba. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ODM, Philip Etale, alisema kuwa safari ya Dkt Oburu haipaswi kutafsiriwa kama jambo la dharura la kiafya kwani ni ukaguzi wa kawaida ambao kiongozi huyo hufanyiwa mara kwa mara. Alifafanua kuwa Dkt Oburu, ambaye wiki iliyopita alionekana katika hospitali moja jijini Nairobi kwa matibabu ya kawaida, ameelekea Uingereza kwa uchunguzi zaidi pamoja na majukumu ya kisiasa. “Oburu ni binadamu wa kawaida kama wengine. Ameenda kwa ukaguzi wa afya pamoja na shughuli za kisiasa,” alisema Bw Etale. Kwa mujibu wa afisa huyo wa ODM, Dkt Oburu pia anapanga kukutana na Wakenya wanaoishi jijini London ambao wamemualika kwa mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa nchini Kenya na mustakabali wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. “Watakuwa na mazungumzo kuhusu nchi yetu na masuala mbalimbali yanayohusu Kenya,” aliongeza Bw Etale. Safari hiyo imezua mjadala kutokana na historia ya changamoto za kiafya ambazo zimewahi kumkumba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 83. Hata hivyo, ODM imesema hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi kwani ratiba yake ya afya na shughuli za kisiasa zinaendelea kama kawaida. Tangazo la safari ya Dkt Oburu limejiri huku chama hicho kikitangaza mpango wa kitaifa wa kumuenzi Raila Odinga, ambaye ODM inamtaja kama mmoja wa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kupigania demokrasia na haki za kisiasa nchini. Mbunge wa Kisumu Magharibi, Bi Rosa Buyu, alisema shughuli hizo zitatoa nafasi kwa wanachama na wafuasi wa ODM kuadhimisha maisha, kazi na maadili ya Raila huku wakijitolea upya kuyasimamia. Ratiba hiyo itaanza rasmi Oktoba 12 kupitia shughuli zitakazoandaliwa na familia ya Raila kabla ya kufikia kilele katika hafla ya kumbukumbu itakayofanyika Kango Ka’Jaramogi huko Bondo. Baadaye, Oktoba 17, chama hicho kitafanya mkutano mkubwa wa kumbukumbu katika mji wa Garissa utakaowaleta pamoja wanachama na viongozi kutoka kaunti za Garissa, Wajir, Mandera na Marsabit. Vilevile, shughuli za kumbukumbu zitafanyika katika eneo la Pwani kati ya Oktoba 18 na 19 kabla ya taifa kuadhimisha Siku ya Mashujaa Oktoba 20. Baada ya hapo, shughuli hizo zitaendelea Kaunti ya Kajiado Oktoba 21 kabla ya Turkana ambako mikutano mbalimbali itafanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 25. ODM imesema lengo la ratiba hiyo ni kupeleka urithi wa Raila katika maeneo mengi ya nchi na kuwafikia wafuasi nje ya ngome za jadi za chama hicho. Hii ni pamoja na maeneo ya Kaskazini mwa Kenya, Pwani, Kajiado na Turkana. Shughuli zote zitahitimishwa Oktoba 31 jijini Nairobi katika mkutano mkubwa wa kumbukumbu ambao ODM imetaja kama kilele cha maadhimisho ya “Mwezi wa Baba”. “Mnamo Oktoba 31, 2026, ambao ni mwezi wa Baba, tutakuwa na mkutano mkubwa wa kumbukumbu Nairobi. Tunawaomba wafuasi wote kujitolea upya kwa maadili na misingi aliyotuachia Baba,” alisema Buyu.

SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna, anaendelea kuimarika kisiasa kitaifa huku akivutia viongozi wa upinzani na wanadiplomasia wa kimataifa, jambo linaloashiria kuongezeka kwa ushawishi wake katika siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Katika siku za hivi majuzi, ofisi ya Sifuna imekuwa kitovu cha mikutano muhimu ya kisiasa na kidiplomasia. Miongoni mwa waliomtembelea ni Balozi wa Ufaransa nchini Kenya, Arnaud Suquet, pamoja na Kaimu Balozi wa Australia nchini Kenya, Andrew Barnes, waliokutana naye katika nyakati tofauti. Sifuna alisema Balozi Suquet alimtembelea kumuaga kabla ya kumaliza kipindi chake cha huduma nchini Kenya. Katika ujumbe wake, Seneta huyo alimtaja mwanadiplomasia huyo kama rafiki yake. Siku moja kabla ya hapo, Sifuna alikuwa mwenyeji wa Barnes na ujumbe wake katika ofisi yake jijini Nairobi. Seneta huyo alisema walijadili masuala mbalimbali ya maslahi ya pamoja, huku ziara hiyo ikiongeza uzito wa hadhi yake inayoongezeka kimataifa. Mikutano ya kidiplomasia imekuwa sehemu muhimu ya kuongezeka kwa hadhi ya kisiasa ya Sifuna. Amewahi kukutana na Balozi wa Amerika nchini Kenya, Marc Dillard, katika Ubalozi jijini Nairobi, ambapo walijadili ushirikiano wa muda mrefu kati ya Kenya na Amerika pamoja na mikakati ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili. Katika taarifa baada ya kikao hicho, Dillard alisema walijadili namna ya kujenga uchumi imara wa ubunifu unaowanufaisha wananchi wa nchi zote mbili. Agosti 27, 2026, Sifuna alikutana na Balozi wa Uingereza nchini Kenya Matt Baugh, katika makazi ya mwanadiplomasia huyo jijini Nairobi. Mkutano huo ulifanyika wakati Seneta huyo anaendelea kuimarisha vuguvugu la Linda Mwananchi na kupanua mtandao wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Mikutano hiyo ya kidiplomasia inafanyika wakati Sifuna anapitia mabadiliko makubwa ya kisiasa. Mwanzoni mwa mwaka, alikuwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini. Hata hivyo, kuondolewa kwake katika wadhifa huo mnamo Juni kumemjenga kama kiongozi wa kitaifa anayevuka mipaka ya chama chake cha zamani. Ingawa kuondolewa kwake kulionekana kama pigo kisiasa, wachambuzi wengi wanaamini hatua hiyo imempa uhuru wa kujijenga nje ya mfumo wa chama. Badala ya kutetea maamuzi ya taasisi ya ODM, sasa ameonekana kuwa sauti ya kundi la viongozi wanaotaka upinzani uwe huru na mkali zaidi dhidi ya serikali. Katika miezi ya hivi majuzi, Sifuna amejenga vuguvugu la Linda Mwananchi, linalohimiza uwajibikaji serikalini na kulinda maslahi ya wananchi. Kupitia vuguvugu hilo, amefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo amekuwa akihutubia mikutano mikubwa ya umma na kujenga mtandao wake wa kisiasa. Umaarufu wake unaonekana kuongezeka hata miongoni mwa wafuasi wa ODM. Tafiti za maoni zimeonyesha kuwa, sehemu kubwa ya wanachama wa chama hicho wanaunga mkono msimamo wake wa kuendeleza upinzani huru badala ya kushirikiana na serikali kupitia mpango wa serikali jumuishi. Kadri umaarufu wake unavyoongezeka, ndivyo viongozi wakuu wa upinzani pia wameanza kujihusisha naye kwa karibu zaidi. Jana, Sifuna aliongoza ujumbe wa Linda Mwananchi katika mkutano na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani na mgombea urais wa Jubilee, Fred Matiang’i. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, Seneta wa Kisii Richard Onyonka na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino. Akizungumza baada ya kikao hicho, Osotsi alisema viongozi hao walijadili namna ya kuimarisha vuguvugu la “Wantam” pamoja na kueneza ushirikiano ndani ya upinzani mpana wa kitaifa. Kwa mujibu wa Osotsi, mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za kuwaleta pamoja viongozi wanaotaka mabadiliko ya kisiasa nchini. Alisisitiza kuwa mashauriano hayo yataendelea kuwahusisha viongozi wengine wa upinzani katika siku zijazo. Kabla ya kukutana na Matiang’i, Sifuna pia alikuwa amefanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, nyumbani kwake Karen. Kundi la Linda Mwananchi lilisema viongozi hao walijadili umuhimu wa kushirikiana katika kulinda demokrasia ya kikatiba na kuimarisha misingi ya taifa. Sifuna amekuwa akisisitiza haja ya viongozi wa upinzani kuungana ili kukabili serikali ya Rais Ruto. Amesema ni lazima viongozi hao washirikiane kulinda katiba na kuhakikisha sauti za wananchi hazipuuzwi. Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili kwa Sifuna na Kalonzo kukutana. Ushirikiano huo unaongeza hisia kuwa viongozi wa upinzani wanapanga mikakati ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Wachambuzi wa siasa wanaamini kuwa kinachomtofautisha Sifuna na viongozi wengine wa upinzani ni uwezo wake wa kuvutia kizazi kipya cha wapiga kura. Akiwa mmoja wa viongozi vijana zaidi katika siasa za kitaifa, amejijengea taswira ya mwanasiasa anayewakilisha mabadiliko ya kizazi ncha Gen Z na siasa mpya zinazolenga uwajibikaji. Kwa mujibu wa mchambuzi wa siasa na mwanasheria Thomas Maosa, ongezeko la mikutano kati ya Sifuna na wanadiplomasia wa mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani linaonyesha kwamba kiongozi huyo sasa anatambulika zaidi ya mipaka ya ODM na siasa za eneo la Nairobi. “Mabalozi hukutana na viongozi wengi, lakini wanapomtafuta mwanasiasa mara kwa mara, inaonyesha kuwa wameanza kumwona kama sauti muhimu katika mazungumzo ya kitaifa. Sifuna ameanza kujijenga kama sura inayoweza kuathiri mwelekeo wa siasa za upinzani na hata siasa za Kenya kwa ujumla,” alisema Maosa.

By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — The Indigenous People of Biafra, IPOB, has raised concerns over the delay in the hearing of the appeal filed by its leader, Mazi Nnamdi Kanu, challenging his conviction by the Federal High Court. IPOB, in a statement yesterday by its Media and Publicity Secretary, Emma Powerful, said it was concerned […]

KENYA kwa mara nyingine imejipata katika hali ya kutatanisha na inayotishia hadhi na sifa yake Afrika na kwenye jukwaa la kimataifa, safari hii ikiwa ni zaidi ya siasa. Ni mdahalo tata wa kufedhehesha kidiplomasia ambao kando na kuweka wananchi na taifa kwenye njiapanda, vilevile unawahatarisha Wakenya wanaoishi, kufanya kazi, au kusomea katika mataifa jirani hususan Afrika. Kauli ya Rais Ruto kuhusu msako dhidi ya raia wa kigeni wanaoendesha biashara kwa njia haramu imesababisha visa vya kuhofisha ambapo Waafrika kutoka nchi jirani, wameshambuliwa, kujeruhiwa, biashara zao kuporwa au kuharibiwa. Ukatili huu dhidi ya raia wa kigeni waliokimbilia nchini ama kuomba hifadhi au kusaka riziki unatekelezwa na wenyeji ambao wameishi nao pamoja kwa miaka mingi wengine hata wakioana na kujaaliwa watoto pamoja. Kenya imekuwa mstari wa mbele barani na kimataifa kupigia debe umoja na udugu wa Waafrika, huku ikihimiza mataifa ya Afrika kuondoa vikwazo vya mipaka ili kuruhusu biashara na usafiri huru. Hata katika matukio yasiyotuhusu moja kwa moja, Rais amejitokeza kutoa taarifa akilaani vikali nchi zinazoripotiwa kuendesha ubaguzi kama vile Urusi-Ukraine, Israeli-Palestine, na Iran. Mwezi mmoja tu uliopita, Afrika Kusini ilikejeliwa mno na kutengwa kiasi cha Waafrika wenzao kuhiari kushangilia Canada badala ya timu yake ya kitaifa katika Kombe la Dunia 2026, baada ya kuwafurusha kikatili Waafrika. Wakenya waliokuwa mstari wa mbele kudhihaki Afrika Kusini mitandaoni, sasa hawana pa kuweka nyuso zao wakitamani ardhi ipasuke iwameze mzimamzima huku masaibu sawia yakiwakabili. Huenda amri ya rais ilidhamiriwa vyema kuhakikisha utekelezaji wa sheria zinazohusu uhamiaji, leseni na udhibiti wa biashara. Kenya kama taifa huru ina kila haki na jukumu la kuhakikisha wafanyaiashara wote wanazingatia sheria. Hata hivyo, agizo la rais, ama kwa bahati mbaya au kimaksudi, lilitafsiriwa visivyo na kuwatumbukiza Wakenya ghafla miongoni mwa mataifa yanayoendeleza ubaguzi kwa misingi ya asili. Licha ya kubuni sera kuhusu masuala ya kigeni, kauli ya Rais Ruto, kwa mara nyingine, imeiweka Kenya kwenye mtanziko kidiplomasia, na kutishia nafasi yake kama kitovu cha kiuchumi na kidiplomasia.wageni Utangamano barani utasalia ndoto iwapo mataifa wanachama wa EAC wataendelea kukosa kuaminiana. Itakuwa unafiki kwa Kenya kuitisha ulinzi kwa Wakenya wanaoishi, kufanya kazi au kusomea nchi jirani au ulaya ilhali inawadhulumu Waafrika waliomo nchini.

Kwa miaka mingi, biashara ya pombe haramu imekuwa changamoto kubwa katika Kaunti ya Nandi. Kulingana na wakazi wa eneo hilo, biashara hii imekuwa chanzo cha umaskini, kuzorota kwa afya, na mizozo ya kifamilia. Ili kukwepa misako ya polisi, watengenezaji wamekuwa wakiendesha biashara hiyo kwa siri kwa kuficha pombe katika vichaka, mapango, kando ya mito, na misituni. Hata hivyo, maafisa wa polisi wamekuwa kwenye mstari wa mbele kukabiliana nayo. Hivi karibuni, ripoti za polisi zilionyesha kuwa walifanikiwa kuharibu lita 5,000 za kangara zilizokuwa zimefichwa mapangoni, huku operesheni nyingine huko katika kata ndogo ya Kapkerer, Nandi South ikifanikisha uharibifu wa lita 3,010 za kangara na kukamatwa kwa lita 60 za chang’aa. Baadhi ya wahusika wakuu kwenye biashara hiyo wamekuwa wanawake, waliokuwa wakiitengeneza na kuiuza kama njia ya kuchuma riziki ya kukidhi mahitaji ya familia zao. Lakini kwa baadhi ya wanawake katika kaunti hiyo, simulizi imeanza kubadilika. Wameasi biashara hiyo haramu na kugeukia ukuzaji wa miche ya miti ya kiasili na matunda. Kwao, shughuli hiyo imekuwa njia ya kujichumia riziki huku wakichangia katika kurejesha misitu iliyoharibiwa. Kulingana na Hellen Meli, uamuzi wa kuanza kukuza miche uliafikiwa baada ya kuachana na shughuli ya pombe iliyokuwa imeweka maisha yao hatarini. “Tuliamua kuanza mradi huu kwa sababu tulikuwa tunatengeneza pombe aina ya chang’aa na tuliona haikuwa na manufaa kwetu. Ilikuwa inahatarisha maisha yetu kama wanawake wa Muruguiywet. Kama tungeendelea kutengeneza chang’aa na kukunywa, tungekuwa tumekufa kitambo.” Kwa Meli, uzalishaji wa miche umewaletea mabadiliko makubwa. Shughuli hiyo imewaunganisha na kuwapa njia mbadala ya riziki. Fedha wanazozipata sasa zinawasaidia kugharamia mahitaji ya familia, ikiwemo elimu ya watoto wao. “Tumependa mradi huu kwa sababu umetusaidia kwenye nyumba zetu. Watoto tumesomesha na tumenunua vitu vingi nyumbani kutokana na kazi hii.” Mabadiliko hayo pia yameanza kupunguza utegemezi wa rasilimali za misitu, na hivyo kuchangia katika uhifadhi wa mazingira. Hapo awali, baadhi ya wanawake walitegemea rasilimali za misitu kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Walikuwa wakikata miti kwa ajili ya kuni na wakati mwingine kutumia maeneo ya misitu kuchunga mifugo yao, shughuli zilizochangia uharibifu wa misitu na maeneo yenye chemchemi. Lakini kipato wanachopata kutokana na uzalishaji wa miche kimewawezesha kupata njia mbadala za nishati nyumbani. Kulingana na Lucy Jepkemboi, baadhi ya wanawake wametumia mapato hayo kununua mitungi ya gesi, hatua ambayo imepunguza utegemezi wao wa kuni. “Miche hii imetusaidia sana kwa maana kama kina mama, pesa tunazozipata tumeweza kununua mitungi ya gesi. Kwa sasa hatukati miti kutafuta kuni za kupikia, na hivyo tumeweza kuhifadhi mazingira.” Kwa viongozi wa vikundi hivi, uhamasishaji wa jamii pamoja na ushirikiano na mashirika ya uhifadhi umeifanya jamii kuhusisha uhifadhi wa mazingira na shughuli zao za kila siku. Kulingana na Jonah Lelei, Katibu wa kikundi cha SSG Muruguiywet, mradi huo ulianzishwa baada ya jamii kutambua kiwango cha uharibifu katika msitu wa Nandi North. “Tulianza mradi huu kwa sababu tuliona uharibifu uliokuwa umefanyika ndani ya msitu wa Nandi North. Hivyo tukaja na lengo moja la kuhifadhi msitu. Mradi huu umesaidia kupunguza ujangili, ukataji wa miti, na uharibifu wa maeneo yenye chemchemi.” Kwa Lelei, mradi huo haujawa tu chanzo cha kipato kwa wanawake, bali pia sehemu ya juhudi za jamii kulinda rasilimali za misitu. Wanawake wameanza kuona thamani ya kuhifadhi msitu huku wakitafuta njia endelevu za kujipatia kipato. Mtindo huu wa kukuza miche pia umezidi kuenea katika maeneo mengine ikiwemo Bonde la Ufa. Katika msitu wa Kessup, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, wanawake wamejitwika jukumu la kurejesha misitu kwa kuzalisha miche ya miti ya kiasili. Kufikia sasa, wamezalisha na kupanda takriban miche milioni moja na laki tano. Kulingana na Florence Cherop, shughuli hiyo imewasaidia kujikimu, kujitegemea, na hata kutoa ajira kwa watu wengine katika jamii. “Tunatumia rasilimali zetu kutoka nyumbani na tunawaajiri watu. Pia, miche hii imefanya tumejisajili na SHA, tunasomesha watoto wetu, na tunavaa kutokana na kazi hii.” Kwa wanawake hao, vitalu vya miche vimekuwa zaidi ya shughuli ya uhifadhi; vimegeuka kuwa chanzo cha kipato kinachowasaidia kukidhi mahitaji ya familia zao. Licha ya mafanikio hayo, wanawake hawa wanakabiliwa na changamoto zinazotishia ukuaji wa biashara zao. Mojawapo ya changamoto kubwa ni ukosefu wa soko la miche, licha ya kuwa na idadi kubwa ya miche iliyo tayari kupandwa. Kulingana na Florence, kikundi chake kimekuza miche mingi lakini kinakosa wanunuzi na rasilimali za kutosha kuendeleza shughuli hiyo. “Sasa tuko na miche zaidi ya milioni moja. Changamoto ni soko na hatuna pesa. Tunaomba mtusaidie ili watoto waende shule.” Licha ya changamoto hiyo, Florence anasema wanawake hawajakata tamaa kwani mafanikio ya mradi huu yanategemea uvumilivu na juhudi za kutafuta masoko. Mbali na ukosefu wa soko, uhaba wa maji kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni pigo jingine. Kulingana na Hellen Meli, ukame umeathiri ukuaji wa miche katika baadhi ya maeneo, huku uhaba wa mvua ukifanya iwe vigumu kupata maji ya kunyunyizia. “Maeneo mbalimbali hayapati mvua kwa sababu haijapanda miti, na hii inachangia ukame. Wakati wa ukame tunakosa maji, jambo linalosababisha miche kukauka.” Kutoka kwa kutengeneza na kuuza chang’aa hadi kuzalisha miche ya miti ya kiasili, safari ya wanawake hawa wa Nandi na Elgeyo Marakwet ni mfano wa kuigwa wa jinsi shughuli za kiuchumi zinavyoweza kuunganishwa na uhifadhi wa mazingira. Hata hivyo, ili juhudi zao zisipotee bure, kuna haja ya haraka kwa serikali za kaunti, wadau wa mazingira, na mashirika ya kibinafsi kujitokeza na kusaidia kuunda masoko ya miche hii. Kwao, kila mche unaopandwa sio tu hatua ya kurejesha msitu, bali ni fursa ya kujenga maisha bora na yenye staha kwa familia zao.

ARUSHA: TANZANIA is moving to reduce reliance on imported seeds as the government pushes for increased local production of quality and affordable seeds to transform agriculture and raise farmers’ incomes. Minister for Agriculture Daniel Chongolo said this during the inauguration of a Seed Co Tanzania plant in Arusha, noting that the investment by the company…