KATIBU Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), Hassan Omar, ameungana na mfanyabiashara Suleiman Shahbal kupinga juhudi zozote za kisiasa zinazolenga kuwazuia wagombeaji wengine kuwania ugavana kaunti ya Mombasa na kumpa Gavana Abdulswamad Nassir njia rahisi ya kutetea kiti chake mwaka wa 2027.
Omar alisema uamuzi wa nani anapaswa kuongoza Mombasa unapaswa kuachwa mikononi mwa wapigakura na si kufanywa kupitia makubaliano ya viongozi wa kisiasa.
Alisisitiza kuwa kila mwanasiasa anapaswa kurejea kwa wananchi na kujieleza kuhusu rekodi yake ya uongozi badala ya kutegemea mipango ya kutangaza wagombeaji.
“Kusiwe na makubaliano ya kisiasa wala mtu kulazimishwa kujiondoa. Wananchi ndio waamue wanayetaka kuwa kiongozi wao,” alisema Omar.
Kiongozi huyo wa UDA, ambaye pia anawania ugavana Mombasa, alikosoa vikali utawala wa sasa wa kaunti hiyo akidai kuwa umeshindwa kutimiza matarajio ya wakazi.
Alisema wakazi wa Mombasa wana haki ya kuchagua kiongozi mpya na kwamba kiti cha ugavana hakipaswi kuamuliwa kwenye meza za mazungumzo.
Kauli za Omar zinaoana na msimamo wa Shahbal ambaye amekuwa akipinga kile anachodai ni njama ya kisiasa ya kumzuia kuwania ugavana.
Shahbal amesisitiza kuwa atawania kiti hicho licha ya Rais William Ruto kumshauri aendelee kuwekeza katika sekta ya biashara badala ya kuingia tena katika siasa za uchaguzi.
Akizungumza katika hafla ya uwekezaji Ikulu Nairobi hivi majuzi, Rais Ruto alisema mchango mkubwa wa Shahbal kwa taifa ni kupitia uwekezaji unaozalisha ajira na kukuza uchumi.
Hata hivyo, Shahbal alikataa ushauri huo na kutangaza kuwa jina lake litakuwa kwenye kura mwaka wa 2027.
Mfanyabiashara huyo pia alidai kuwa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanatumia miundo ya vyama na hoja ya kutengewa maeneo ya kisiasa ili kuamua nani anapaswa kugombea viti mbalimbali vya uongozi.
Wakati huo huo, baadhi ya madiwani kaunti ya Mombasa wamemtetea Gavana Nassir na kumtaka Shahbal kutii ushauri wa Rais.
Wamesisitiza kuwa gavana huyo ana rekodi nzuri katika sekta za afya, elimu na maendeleo mengine ya kijamii.
Mvutano huo umeweka Omar na Shahbal katika muungano usio wa kawaida.
Ingawa wote wawili wanapania kugombea ugavana wa Mombasa na huenda wakawa wapinzani wakubwa baadaye, kwa sasa wanashirikiana kupinga juhudi zozote za kumhakikishia Nassir muhula wa pili kupitia makubaliano ya kisiasa.
Huku Shahbal akisisitiza kuwa hatajiondoa kwenye kinyang’anyiro, Omar akiendelea kufanya kampeni zake na Nassir akitetea utawala wake, ushindani wa ugavana Mombasa unaonekana kuwa miongoni mwa vita vya kisiasa vitakavyovutia macho ya wengi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Omar aunga Shahbal kupinga mpango wa kukinga gavana Nassir

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]