
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


MTWARA: WAKAZI wa Kijiji cha Kilimahewa Kata ya Mnongodi Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara wameishukuru serikali kwa kuwaletea huduma ya maji kwenye kijiji hicho mradi uliyogharimu Sh milioni 91.1 Wakizungumza kwenye halmashauri hiyo katika kijiji hicho cha kilimahewa akiwemo Shani Athumani amesema kwa sasa wakazi hao hawana changamoto ya maji ikilinganishwa na hapo awali…

DAR ES SALAAM: A total of 150 needy students are expected to benefit from scholarships through the 2026 Goat Races organised by the Rotary Club of Dar es Salaam Oyster Bay, with the club targets to raise 250m/- to support the programme. The annual charity and fundraising event is scheduled to take place on September…

MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi na Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba wanatarajiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shughuli za serikali Tanzania zinaendelea bila kusita huku Rais Samia Suluhu Hassan akiomboleza kifo cha mumewe, Hafidh Ameir Hassan. Bw Ameir alifariki Jumatatu akipokea matibabu ya ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Emilio Mzena, Zanzibar. Alizikwa siku hiyo hiyo katika kijiji cha Kizimkazi, Zanzibar, kwa mujibu wa mila za Kiislamu. Makamu wa Rais Ndejembi, ambaye aliapishwa Agosti 29 baada ya Emmanuel Nchimbi kuondoka madarakani, ndiye anayeshikilia nafasi ya pili kwa mamlaka katika nchi hiyo. Wakati huu wa maombolezo, Ndejembi anatarajiwa kumsaidia Rais katika kutekeleza majukumu ya serikali, huku Waziri Mkuu Nchemba akiendelea kuratibu shughuli za kila siku za serikali. Licha ya kuomboleza kifo cha mumewe hakiondoi mamlaka yake ya kikatiba kama Rais.

WAZIRI wa Afya, Aden Duale amekuwa akichukuliwa kama kigogo wa siasa za Kaskazini Mashariki ila kwa sasa ushawishi wake unakabiliwa na visiki huku akiendelea kurindima ngoma ya kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto. Baada ya kuhudumu kama mbunge, Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa na sasa waziri, Bw Duale amekuwa akionekana kama mwanasiasa ambaye huamua mkondo wa siasa katika eneo la Kaskazini Mashariki. Wakati huu ambapo anashikilia nafasi ya uwaziri, baadhi ya wanasiasa kutoka Garissa, Wajir na Mandera, sasa wanamtaka ajiepushe kuamua viongozi wanaostahili kushikilia nyadhifa mbalimbali eneo hilo. Mnamo Agosti 9, Mwakilishi wa Wanawake wa Wajir Fatuma Abdi Jehow alimwambia hadharani Bw Duale ajiepushe na siasa za Wajir, akidai ameingilia uongozi wa eneo hilo na kujaribu kuwagawa wakazi kwa misingi ya koo. Kauli yake ilifuatia madai ya Bw Duale kuhusu matumizi ya utajiri na helikopta kushawishi siasa na kumng’oa madarakani. Bi Jehow alijibu kwa ujasiri kwamba hatima yake ya kisiasa itaamuliwa na wapigakura, wala si watu kutoka nje. “Kuna watu wanatuambia kwamba wana utajiri na helikopta na wameazimia kuhakikisha hatuchaguliwi tena. Ni Allah pekee anayeweza kutuangusha. Unatoka wapi na wewe ni nani? Shikilia eneo ulikochaguliwa. Ikiwa unataka kuwa kinara wa kisiasa, walete watu pamoja lakini usiwagawe," akasema. Wiki mbili baadaye, mvutano huo ulihamia Garissa na ukachacha zaidi. Mnamo Agosti 20, Mbunge wa Dadaab Farah Maalim alitishia kuhamasisha wakazi kushinikiza Bw Duale aondolewe serikalini, akidai ameingilia siasa za eneo hilo na kulemaza mfumo wa demokrasia ya maafikiano unaotumiwa. “Si sisi tuliokupa jina la Sultan Hasid. Halikuwa watu wa Wajir wala Mandera, bali watu walio karibu nawe. Tukianza kushawishi, haitachukua siku 14 kukuondoa katika nafasi hiyo,” akasema Bw Maalim kwa Kisomali. Alimwonya Bw Duale dhidi ya kutumia mamlaka yake kupita kiasi. “Tafadhali nenda polepole, wewe ni kijana. Tumekuwa mara nyingi tukikulinda lakini ukiendelea, hatutakulinda tena,” akasema. Jina la ‘Sultan Hasid’, linaloweza kutafsiriwa kwa urahisi kuwa ‘Sultani mwenye wivu’, sasa limegeuka kuwa kejeli ya kisiasa dhidi ya waziri huyo. Lakini nyuma ya malumbano hayo kuna vita kubwa zaidi kuhusu nani atakayeamua mustakabali wa kisiasa wa eneo hilo. Mvutano mkubwa zaidi unaonekana Garissa, ambako Seneta Abdulkadir Mohamed Haji ametangaza wazi vita dhidi ya ushawishi wa Bw Duale. Mnamo Julai 21, Seneta Haji aliapa kufuta nyayo za kisiasa za Bw Duale kutoka kaunti hiyo. Tangu wakati huo ameungwa mkono na Baraza la Wazee wa Koo Garissa kuwania ugavana, hatua inayomweka katika njia ya makabiliano na Bw Duale na washirika wake.

WASHINGTON, Amerika: RAIS Donald Trump amesema anaamini vita kati ya Amerika na Iran vitamalizika mara tu baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula utakaofanyika Novemba. Trump amesema Iran haitaweza kuendelea na vita hivyo kwa muda mrefu na kwamba Tehran inajaribu kutumia mzozo huo kuathiri matokeo ya uchaguzi wa Amerika. Akizungumza na wanahabari Jumatano, Trump alisema vita hivyo vitamalizika mara moja baada ya uchaguzi kwa sababu Iran, kwa mujibu wake, haina uwezo wa kuendelea kupambana. Trump amekuwa akiweka muda wa kumalizika kwa vita hivyo hapo awali, lakini kauli yake ya sasa inaweka mwisho wa uchaguzi wa Novemba kama muda muhimu wa kusitisha mapigano. Uchaguzi huo wa katikati ya muhula utaamua iwapo chama cha Trump cha Republican kitaendelea kudhibiti Congress, na rais huyo anadai kuwa Iran inajaribu kuingilia mchakato huo wa uchaguzi. Hata hivyo, ripoti ya Jarida la Wall Street imesema baadhi ya washauri wakuu wa Trump katika Ikulu ya White House, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, wamemwambia kwenye kikao cha faragha kwamba vita hivyo vinaweza kuendelea hadi mwisho wa muhula wake wa urais, Januari 2029. Wakati huohuo, mapigano kati ya Amerika na Iran yameendelea kusababisha bei ya mafuta duniani kupanda huku njia muhimu za usafirishaji katika Mlango wa Hormuz na Bahari ya Shamu zikiendelea kuvurugwa. Kauli ya Trump kuhusu kumalizika kwa vita baada ya uchaguzi wa Novemba kwa sasa imezua maswali kuhusu uhalisia wa vita hivyo kuisha.

MASHAMBULIZI mapya ya majangili kwenye mpaka wa Turkana-Pokot Magharibi yanatishia mipango ya kurejeshwa kwa biashara ya kuuza petroli katika kituo cha South Lokichar Basin huku viongozi wakionya kuwa operesheni za mafuta hazitaruhusiwa kuendelea pasipo usalama. Viongozi kutoka Turkana Kusini na Mashariki wameitaka serikali kurejesha usalama, mifugo walioibiwa, kutambulisha na kuwakamata waliohusika na mashambulizi hayo. Wameonya kuwa watashinikiza oparesheni za petroli kusimamishwa ikiwa hali haitadhibitiwa. Wanasema visa vya mauaji, mashambulizi na wizi wa mifugo haviwezi kupuuzwa wakirejelea uvamizi wa majuzi katika kijiji cha Lokwar, eneo la Aroo, mapema Septemba 2, 2026, ambapo watu watatu waliuawa, mmoja akajeruhiwa na mifugo kuibiwa. “Shughuli zote za Gulf Energy katika maeneo yaliyoathirika ni sharti zisimamishwe hadi hali ya kawaida irejee na usalama kuimarishwa.”

MAHAKAMA ya Rufaa imeunga mkono hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela dhidi ya Joseph Kyalo kwa kumuua jamaa yake Paul Kiio katika baa moja Machakos. Mahakama ilikataa hoja ya Kyalo kwamba Bw Kiio alifariki baada ya wao kupigana wakiwa wamelewa. Tukio hilo lilitokea Aprili 16, 2018, katika Club Digital, Soko la Kikunuani Kaunti ya Machakos. Mashahidi walisema Kyalo alimpiga Bw Kiio kwa chupa za bia kichwani baada ya kudai kuwa alikuwa na bastola iliyotumiwa kumtishia babake. Inadaiwa Kyalo na wenzake walimpiga Kiio kwa chupa na fimbo, wakamvua nguo na kumtupa nje ya klabu akiwa amejeruhiwa. Kiio alipelekwa hospitalini, ambako alifariki. Uchunguzi wa maiti ulionyesha alifariki kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kipigo kikali. Mahakama ilisema vitendo vya Kyalo vilionyesha nia ya kusababisha madhara makubwa hata kama alikuwa amelewa.

RAIS William Ruto amekuwa akitoa matamshi ambayo yanaonekana kuridhisha umma kwenye mikutano kisha kauli hizo zinabadilishwa kutokana na sera kuzimwa na sera ya serikali kukinzana na matamshi hayo. Matamshi mengi ya Rais William Ruto katika mikutano ya kisiasa na kubadilishwa kwa baadhi ya sera na maagizo ya serikali kumeibua maswali kuhusu iwapo utawala wake unaendeshwa zaidi na malengo ya kisiasa kuliko utoaji wa huduma kwa wananchi. Huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia na upinzani ukizidi kumkabili, Rais amekuwa akionekana kulegeza baadhi ya misimamo yake baada ya kukumbana na upinzani kutoka kwa wananchi. Tukio la hivi punde ni kubadilishwa kwa uamuzi wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA) kuongeza kiwango cha chini cha thamani ya mizigo iliyounganishwa inayotozwa ushuru kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni. Baada ya wafanyabiashara wadogo kupinga hatua hiyo wakisema ingeongeza mzigo wao wa kodi, Rais aliagiza KRA kupunguza kiwango hicho hadi Sh2 milioni. “KRA itapunguza kiwango kinachotumika kwa mizigo yote iliyounganishwa kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh2 milioni,” ilisoma taarifa ya Wizara ya Biashara. Wafanyabiashara wadogo ni kundi muhimu la wapigakura na mabadiliko hayo yameonekana na baadhi ya wachanganuzi kama jaribio la serikali kuwapunguza hasira kabla ya uchaguzi wa 2027. Rais pia alibadili msimamo kuhusu wafanyabiashara wa kigeni wanaojihusisha na biashara ndogo nchini. Mnamo Septemba 2, alitangaza kuwa wafanyabiashara hao walipaswa kufunganya virago ifikapo Septemba 7. Baadaye, serikali iliwapa siku 90 ili wapate leseni na kuwa nchini kihalali. “Kuanzia wiki ijayo, wafanyabiashara wote (wageni) wanaofanya biashara hizo ndogo wanapaswa kufunga,” Rais alisema baada ya kukutana na wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ikulu ya Nairobi. Hatua hiyo ilikosolewa na mashirika ya kiraia yaliyomtaka Rais kuomba msamaha na kuwalipa fidia walioathirika. Waziri wa Biashara Lee Kinyanjui alijaribu kufafanua kuwa serikali inalenga kuhakikisha wageni wanatii sheria za uhamiaji na leseni na hawashindani visivyo na wafanyabiashara raia wa Kenya. Mabadiliko hayo pia yameonekana katika mzozo wa Kiwanda cha Kemikali cha Tata kinachopatikana Magadi, Kaunti ya Kajiado. Rais alikuwa ameamuru kampuni hiyo ya India kuondoka nchini, akidai haikuwa ikitoa thamani ya kutosha kwa Wakenya. “Tumechukua uamuzi wa kisera kwamba hatutaendelea kuuza malighafi nje. Tutaandaa madini yote yanayopatikana Kenya hapa nchini,” akasema Rais alipokuwa akitafuta kura za jamii ya Maa Kaunti ya Kajiado. Hata hivyo, serikali baadaye ilibadilisha msimamo na kusema itafanya mazungumzo na wawekezaji hao kwa kuzingatia sheria, hivyo kufungua mlango wa mazungumzo na uongozi wa kampuni ya kemikali ya Tata. Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Javas Bigambo anasema ukosefu wa maelezo ya kina kabla ya serikali kutoa maagizo umeifanya ionekane kama inategemea matamshi ya kisiasa. Hata hivyo, alisema baadhi ya hatua hizo zinaweza kuwa na msingi wa kisheria. “Kuhusu kampuni ya Tata, ni kutotii Sheria ya Uchimbaji Madini ya 2016. Kwa hivyo, suala linapaswa kuwa ni kampuni ngapi za uchimbaji madini zinatii sheria,” akasema. Serikali pia imebadili msimamo kuhusu ufadhili wa elimu ya juu. Hii ni baada ya mfumo mpya wa ufadhili kukosolewa, Rais akisema wanafunzi wote watakaotimiza vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu watapata ufadhili kamili wa serikali chini ya mfumo unaopendekezwa. “Mfumo ambao tuliujaribu, haukufanya kazi na karibu ulisababisha vyuo vyetu vingi kufungwa,” akasema Rais. Mabadiliko hayo yanazua kumbukumbu kuhusu hatua nyingine zilizochukuliwa tangu Rais aingie mamlakani mnamo 2022. Miongoni mwa hizo ni kuondolewa kwa ruzuku ya unga wa mahindi na mafuta, ambayo Rais alisema ilikuwa mzigo mkubwa kwa serikali. Hata hivyo, kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, serikali baadaye ilirejesha kwa muda ruzuku ya mafuta. Hivi majuzi, Waziri wa Hazina John Mbadi alisema serikali inatafuta fedha za kutoa ruzuku kwa mafuta ili kuwalinda Wakenya kutokana na kupanda kwa bei. Serikali pia ilibadili msimamo wake kuhusu ushirikiano na upinzani. Rais Ruto aliwahi kukataa vikali kurejea kwa mfumo wa “handisheki”, lakini maandamano makubwa ya vijana mnamo 2024 yalimfanya kuingia katika Serikali Jumuishi na ODM ya marehemu Waziri Mkuu Raila Odinga. Hatua hiyo ilifuatwa na kuondolewa kwa baadhi ya mapendekezo ya kodi yaliyokuwa katika Mswada wa Fedha wa 2024. Rais pia alilazimika kuvunja Baraza lake la Mawaziri na kufanya mabadiliko kadhaa baada ya maandamano hayo. Licha ya mabadiliko hayo, Rais amekuwa akitetea Serikali Jumuishi akisema imesaidia kuleta utulivu na maendeleo nchini. “Serikali Jumuishi haikuwa kosa ila niliibuni kimakusudi,” akasema kwenye mkutano mmoja wa kisiasa Kaunti ya Kisii mnamo Aprili mwaka huu. Kwa wananchi, changamoto sasa ni kujua ikiwa mabadiliko haya ni marekebisho ya sera baada ya kusikiliza maoni yao au ni mikakati ya kisiasa ya kutafuta uungwaji mkono kuelekea 2027.

ASILIMIA 76 ya Wakenya wanaamini nchi inaelekea vibaya, huku asilimia 65 wakisema hali yao ya kiuchumi imezorota tangu Rais William Ruto aingie mamlakani mnamo 2022. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa Kampuni ya Utafiti ya TIFA. Utafiti huo uliofanywa kati ya Juni 13 na 22, 2026, kwa kuwahoji watu 2,048 katika kaunti zote 47, umeonyesha kiwango cha kutoridhika kimefika juu zaidi tangu TIFA ianze kufuatilia suala hilo mnamo 2023. Ni asilimia 14 pekee walioamini Kenya inaelekea upande unaofaa, huku asilimia 12 wakisema hali yao ya kifedha imeimarika tangu uchaguzi wa 2022. Asilimia 23 walisema hali yao haijabadilika. Mlima Kenya ndio uliorekodi hisia hasi zaidi, ambapo asilimia 90 ya waliohojiwa walisema nchi inaelekea pabaya, ikifuatiwa na Nairobi kwa asilimia 89. TIFA ilisema ukosefu wa ajira na umaskini ndio matatizo makubwa zaidi nchini, yakitajwa na asilimia 44 ya waliohojiwa. Kupanda kwa bei ya bidhaa na ushuru mkubwa ulitajwa na asilimia 25 ya waliohojiwa. Utafiti pia ulionyesha imani ndogo kwa taasisi za umma. Hakuna taasisi iliyopata imani ya zaidi ya asilimia 40. Mahakama iliongoza kwa asilimia 36, ikifuatiwa na serikali za kaunti kwa asilimia 31 na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) kwa asilimia 30. Imani kwa Rais Ruto iligawanyika kisiasa. Asilimia 58 ya wanaounga mkono Serikali ya Jumuishi walisema wanamwamini, ikilinganishwa na asilimia 16 ya wanaopinga utawala huo. TIFA ilisema iwapo hali ya kiuchumi haitaimarika mwaka ujao, huenda ikawa changamoto kwa wanasiasa wanaotafuta kuchaguliwa tena, hasa wanaohusishwa na serikali ya sasa.

… Says 53 suspected cases recorded this year… Urges parents to complete children’s 3 immunization dosesBy Chioma Obinna The Lagos state Commissioner for Health, Prof Akin Abayomi on Wednesday raised its disease surveillance and preparedness against diphtheria, warning residents not to panic but to remain vigilant as the outbreak continues to spread in parts of […]

MTWARA; WATUMISHI wa serikali kwenye Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwar, wametakiwa kuwasikiliza wananchi waliopo kwenye maeneo yao, ili kuwezesha maendeleo ya wananchi. Hayo yamejiri leo Septemba 9,2026 wakati wa ziara ya kikazi iliyofanywa na Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota kwenye Kata ya Njengwa. Mbunge huyo pia alisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao…

MWANZA; Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za upimaji nchini, huku ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na mataifa mengine pamoja na kutoa fursa kwa nchi hizo kutumia miundombinu iliyopo na Tanzania kunufaika na uwekezaji huo. Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi…

MTWARA; NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Bandari ya Mtwara, itakayosaidia kuboresha huduma za usafirishaji majini, Kanda ya Kusini. “Kwa sasa serikali ipo kwenye hatua ya kumtafuta mzabuni wa mradi huo wa ujenzi wa meli, ” amesema na kuongeza kuwa mchakato wa kumtafuta…

Treason trial accused person, Chadema national chair Tundu Lissu, failed to contain his frustration over how his witness, Ms Brenda Rupia, was cross-examined regarding her profession in relation to her responsibilities within the party.

MUUNGANO wa Kitaifa wa Wauguzi na Wakunga Kenya (KNUNM) jana ulisitisha mgomo wake wa kitaifa uliodumu kwa siku 41 baada ya kufikiana na Baraza la Magavana Nchini (CoG). Uamuzi huo ulitangazwa baada ya mkutano wa siku nzima wa faragha kati ya viongozi wa KNUNM na CoG. Katibu Mkuu wa KNUNM Seth Panyako alisema mgomo huo ulioanza Julai 29, 2026, umesitishwa mara moja. “Kwa mamlaka niliyopewa na Katiba ya Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi Kenya na Katiba ya Kenya, natangaza kwamba mgomo ulioanza tarehe 29 Julai 2026 umesitishwa,” akasema Bw Panyako. Aliwataka wauguzi kurejea kazini mara moja au ndani ya saa 24 ili kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kutolewa katika hospitali. “Ninawasihi wanachama kurejea kazini mara moja na kwa vyovyote vile si zaidi ya saa 24 kuanzia sasa,” akaongeza. Kusitishwa kwa mgomo huo kumaliza kusambaratika kwa huduma za afya katika hospitali za umma kote nchini kwa karibu wiki sita. Wauguzi walikuwa wakishinikiza kuboreshwa kwa malipo na marupurupu, hali iliyosababisha baadhi ya wagonjwa kukosa huduma muhimu. Mapema wiki hii, wauguzi walikuwa wameandamana hadi katika afisi za CoG na kuahidi kuendelea kuwa hapo kila siku hadi malalamishi yao yasikilizwe. Jumanne, CoG ilionyesha dalili za kusuluhisha mzozo huo baada ya kufichua kuwa ilikuwa imewasilisha ofa kwa wauguzi. Mwenyekiti wa CoG Ahmed Abdullahi alisema wauguzi wangepata nyongeza ya Sh8,000 katika marupurupu ya mazingira hatari ya kufanya kazi na Sh5,000 ya marupurupu ya sare, jumla ya Sh13,000. “Kupitia juhudi za kamati yetu ya afya, ninaweza kuripoti kwamba hatimaye tumefikia makubaliano ikiwa hawatabadilisha msimamo wao hadi wakati mkataba utakapotiwa saini. Tumewapa nyongeza ya marupurupu ya mazingira hatari ya kazi hadi Sh8,000 na pia tumewapa nyongeza ya Sh5,000 ya marupurupu ya sare,” akasema Bw Abdullahi katika mkutano uliofanyika Ikulu. Suluhu hiyo pia imezuia mgomo ambao ulikuwa unatishia kuanzishwa na madaktari. Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno Kenya (KMPDU) ulikuwa umetoa ilani ya siku saba ukitaka mzozo wa wauguzi usuluhishwe, na kuonya kuwa madaktari wangeingia mgomoni iwapo suala hilo halingetatuliwa. KMPDU ilikuwa imesema kuvurugika kwa huduma katika hospitali za umma kwa muda mrefu kulikuwa kumeongeza mzigo wa kazi kwa madaktari na wahudumu wengine wa afya. Kusitishwa kwa mgomo huo sasa kunatarajiwa kurejesha huduma za afya kama kawaida, huku utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa ukitarajiwa kuwa hatua muhimu ya kuzuia migogoro mingine kati ya wauguzi na serikali.

As stakeholders are fighting for a new Constitution to address complained-about challenges, the Alliance for Democratic Change (ADC) party chairman, Mr Shaban Itutu, has raised a new point regarding the need to campaign for the establishment of a Constitutional Court. Mr Itutu clarified this while contributing to the debate at a national stakeholders' meeting aimed at reflecting on the country's political situation, the 2025 General Election, and the nation's future, organised by the Tanzania Centre for Democracy (TCD). Mr Itutu said the establishment of that court will help lay a solid foundation to supervise and guarantee the execution of matters specified in the Constitution. He says the major challenge he sees is not merely the existence of a Constitution, but how it is supervised and executed, stating that even the current Constitution faces this challenge. He says the existing Constitution has minor shortcomings and that even the new Constitution proposed by stakeholders will be meaningless if there is a vacuum in its supervision and execution. "The current Constitution does not have major shortcomings. Even this new Constitution which we are proposing and which is the outcry of stakeholders, if obtained but accompanied by a supervision vacuum like the current one, it will seem like nothing," said Mr Itutu. The politician says that, along with the debate on the new Constitution, it is important to also look at the system of ensuring that constitutional provisions are respected and executed properly to bring equality of rights without one group appearing to be pointed at. History of constitutional amendments In that debate, retired Prime Minister Joseph Warioba said the debate on the new Constitution has taken a long time because the current Constitution does not differ significantly from the one left by colonialists, except that it has undergone amendments and been translated from English to Swahili. He says some of the changes made include introducing presidential term limits, recognising human rights, and establishing the position of Prime Minister. "For 25 years, major changes were made, but after restoring the multi-party system, the debate to change the Constitution began, especially after the Justice Nyalali Commission offered advice," he said. Justice Warioba says that the debate continued until the time of retired President Jakaya Kikwete's government, which established a Commission to gather citizens' opinions from various areas across the country, while he (Justice Warioba) was assigned the duty to lead it. "The process continued until we obtained the Proposed Constitution. Although I regret to say many things expressed by citizens were removed, especially the issue of leaders' ethics. That is why currently the issue of ethics for public leaders is a problem and needs improvement," he said. He said a new Constitution is needed, first, to restore power to citizens in deciding the leader they want, saying that the right does not fully exist. "Even election supervisors lack ethics. That is a problem and has contributed to bringing us to the situation we are in today. Even the procedure used to disqualify candidates is unfair and has contributed to bringing us problems," he said. Justice Warioba said for Tanzania to return to its foundations, citizens must be restored the power to elect leaders they want, saying corruption is widespread and citizens are unsatisfied with this state of affairs. He said another area needing improvement is the separation of powers, emphasising that all branches of government should execute their duties independently without interference. "The area of powers, especially within all three branches, means each branch should work independently without interference. Parliament currently lacks significant powers because the government is inside Parliament," he said. The current one should be amended The Tanzania Labour Party (TLP) chairman, Mr Richard Lyimo, said there is no need for Tanzania to obtain a new Constitution, but what is needed is to make amendments to the current Constitution to include necessary matters. He said having a good Constitution alone is not enough if there are no good supervisors to execute it. "We can have a good Constitution, but lack good supervisors. We must ask ourselves what the problem is. We see our neighbours, despite having a new Constitution, continuing to falter," he said. Mr Lyimo builds this argument by referencing the speech of the meeting’s chief guest, Justice Warioba, who said the current Constitution has been amended whenever a major event occurred in the country. "I have understood, and I say no major event has occurred. I see it as ordinary as such. I see we should make amendments to the existing Constitution by putting the things we want. Let us respect history," he said. Reconciliation before Constitution Chaumma’s director of communications, Mr John Mrema, advised that before entering the process of obtaining a new Constitution, it is important first to talk and remove the existing misunderstanding. "We cannot enter the process of getting a new Constitution as we are, fractured into pieces. We need to reconcile first by speaking the truth and agreeing," he said. The Tanzania Episcopal Conference (TEC) deputy decretary-general, Father Faustine Furaha, offered three recommendations that will help Tanzania return to the foundations of peace, including leaders speaking the truth and executing what they say. Another matter is restoring competitive elections, alongside building a discipline of respecting other people's ideas, saying that holding press conferences in every corner to respond to others' arguments does not build a peaceful nation. Father Furaha said when a leader says something, it is important they mean it and ensure it comes from the heart, as that helps build trust among citizens. "So that we can build foundations of mutual trust from the first day to the last, there are things that happened in between that caused problems and brought about many things happening in the country," he said. He said the second matter is restoring competitive elections, explaining that young people like competing, and if given that opportunity, they will be happy, while continuing with the current system risks increasing challenges. "I have read the Constitution of Tanzania. Article 18 says everyone is free to express opinions. As days go by, I see that situation disappearing. When you give ideas, you are attacked; people emerge here and there holding press conferences to respond, while the country has elders and adults. Without removing that situation, we cannot move forward," he said. He said the current situation in the country is that a person can offer ideas, and the next day you see people from various places using platforms to oppose those ideas. "We must accept there are adults who will offer advice; let us listen. If you have your opinion or want to raise an argument, do not attack the person; raise the argument," he said. Women and politics The Women Politicians Association (Ulingo) national coordinator, Dr Ave-Maria Semakafu, said the ongoing uncertainty in the country affects women's participation in politics and decision-making systems. She said that the situation has been making it difficult for women to participate in politics, while emphasising the importance of amending systems to provide more opportunities for women. "The ongoing situation affects and creates difficulty for women to participate in politics. We said we would like systems amended to provide opportunities for women. Even in the discussion of what occurred on October 29, 2025, some people have taken authority upon themselves to speak about what happened," she said. She said that even on the issue of reconciliation being spoken about by the President, there are still people emerging to clarify what the President has said. Dr Semakafu said women's participation at decision-making levels remains a challenge, noting that even the criteria for securing special seat positions through political parties are not openly known. "Without having money, you cannot be a leader at a democratic level. That challenge becomes more than twice as hard. We need to change systems and remove the notion that to be a leader you must have money," she said. Use of state organs ACT-Wazalendo Mainland vice chairman, Mr Isihaka Mchinjita, said the problem present in the country is failure to follow the Constitution and existing laws, while alleging that state organs have been used in political matters. "At polling stations, ballot papers for electing leaders are stolen. We must stop high-handedness and observe the Constitution and existing laws," he said. Regarding the constitutional debate, Mr Mchinjita said he does not support getting a patched-up Constitution, saying the current Constitution has had many problems, including failing to prevent challenges involving civilian killings. "It is important we obtain an implementation calendar for a new Constitution. Let us submit a Constitutional Law Amendment Bill so that we obtain a Constitution capable of solving challenges troubling citizens," he said. Former NCCR-Mageuzi chairman, Mr James Mbatia, said since the conduct of last year's general election, anger has been high among citizens, saying that situation is a man-made disaster and has birthed various perspectives. "Since we will seek consensus and the truth has become known, people died last year, although we differ regarding numbers. But let us know prevention is better than cure. Let us strive to use our tongues well because they can be a source of disaster," he said. Mr Mbatia said what is needed is building tolerance and mutual trust, emphasising the importance of treating peers in the manner they deserve, considering the broader future of building the nation.

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Kitengo cha Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Felix Chakila, amesema Kongamano la Tano la Kimataifa la Uchumi wa Buluu limekuwa fursa muhimu kwa Tanzania kupata mawazo na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuhusu namna bora ya kuimarisha…

KAGERA: Maelfu ya wafugaji katika mikoa ya Kagera wanatarajiwa kunufaika na programu ya iMbeju Kilimo Kopa Ng’ombe, Lipa Maziwa, inayolenga kuongeza uzalishaji wa maziwa, kipato na kuwawezesha wafugaji wadogo kujenga biashara endelevu ya mifugo. Programu hiyo imezinduliwa na CRDB Foundation kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ikiwa na lengo la kuwawezesha…

TAKRIBAN wanawake 22 walifariki dunia kutokana na matatizo yanayohusiana na uzazi katika kipindi cha wiki moja huku mgomo wa wauguzi ukiendelea nchini. Aidha, vifo vya watoto wachanga 44 na vifo 130 vya watoto kabla au wakati wa kuzaliwa pia vimeripotiwa, hali inayofichua ukubwa wa janga la afya linalokumba taifa. Takwimu hizo zimetolewa wakati ambao wauguzi wamesusia kazi kwa zaidi ya mwezi mmoja, jambo ambalo limevuruga huduma katika hospitali nyingi za umma kote nchini. Wataalamu wa afya wanaonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo madaktari nao watatekeleza tishio lao la kugoma katika siku chache zijazo. Mgomo wa wauguzi ulianza Julai 29, 2026, kufuatia mzozo kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Pamoja wa Kazi wa mwaka 2017, marupurupu mbalimbali na kuajiriwa kwa wahudumu wa mpango wa Afya kwa Wote (UHC) kwa masharti ya kudumu. Kaunti za Nakuru, Kisumu, Kakamega na Kajiado zimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mgomo huo. Hospitali ambazo awali zilikuwa zikihudumia mamia ya wagonjwa kila siku sasa zimebaki na shughuli chache huku wagonjwa wakikosa huduma muhimu. Katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Nakuru ambazo kwa kawaida huwa zimejaa wagonjwa na wahudumu wa afya zimekuwa tulivu isivyo kawaida. Huduma chache zinazotolewa sasa zinategemea maafisa wa utabibu na wanafunzi wa udaktari, huku wagonjwa wakisema kiwango cha huduma si sawa na kile walichokuwa wakipata kabla ya mgomo. Pwani nayo imeathirika vibaya. Katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Coast General mjini Mombasa, huduma za uzazi, meno, masikio, pua na koo pamoja na vitengo vingine muhimu zimekwama. Baadhi ya familia zimehamisha wagonjwa wao hadi hospitali za kibinafsi kwa hofu ya kupoteza maisha. “Tumeamua kumtoa mgonjwa wetu hospitalini kwa sababu hajapata matibabu ya maana kwa wiki tatu. Tunampeleka hospitali ya kibinafsi kwa matumaini ya kupata huduma bora,” alisema mmoja wa jamaa za mgonjwa. Katika Kaunti za Meru, Laikipia, Narok, Bomet na Uasin Gishu, hali si tofauti. Wagonjwa wanaohitaji huduma za kulazwa hospitalini wamekuwa wakielekezwa katika hospitali za kibinafsi na za makanisa, jambo ambalo limeongeza mzigo wa gharama kwa familia nyingi. Wajawazito ni miongoni mwa walioathirika zaidi. Milka Kimani kutoka Mpeketoni, Lamu, alisema amelazimika kutafuta huduma katika kliniki za kibinafsi baada ya kukosa kuhudumiwa katika hospitali ya serikali. “Unafika hospitalini kwa kliniki lakini hakuna anayekuhudumia. Nililazimika kutafuta huduma mahali pengine ingawa gharama ni kubwa,” alisema. Katika baadhi ya maeneo, wanaougua magonjwa sugu kama pumu, kisukari na shinikizo la damu pia wamekosa huduma za kawaida. Wengine wanalazimika kununua dawa katika maduka ya kibinafsi kwa gharama kubwa huku baadhi ya hospitali za serikali zikiripotiwa kukosa dawa. Huku mazungumzo kati ya viongozi wa Chama cha Wauguzi na Baraza la Magavana yakikosa kuzaa matunda, wananchi wanaendelea kulipa gharama kubwa zaidi. Wengi wanasema serikali za kaunti na serikali kuu zimekuwa zikilaumiana huku maisha ya wagonjwa yakiendelea kuwa hatarini. Sasa hofu kubwa ni kwamba iwapo mgomo utaendelea kwa muda mrefu zaidi, vifo vitaongezeka na hospitali za umma, ambazo ndizo tegemeo la mamilioni ya Wakenya maskini, zitaendelea kuwa maeneo ya mateso badala ya vituo vya kuokoa maisha.

MIPANGO ya Wizara ya Fedha katika mwaka wa kifedha uliomalizika Juni 2026 ilikumbwa na kizingiti kikubwa, baada ya Mdhibiti wa Bajeti, Margaret Nyakang’o, kuzuia matumizi ya Sh72 bilioni. Hiki ndicho kiasi kikubwa zaidi ambacho ofisi yake imewahi kuzuia katika miaka ya hivi punde. Dkt Nyakang’o, ambaye Katiba imempa jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za umma, alikataa maombi ya kutolewa kwa fedha hizo. Hatua hiyo ilimzuia Waziri wa Fedha, John Mbadi kutoa idhini ya matumizi ya fedha kwa baadhi ya taasisi za serikali ambazo hutumia mabilioni kuendesha shughuli zao. Fedha hizo ziliombwa chini ya Kifungu cha 223 cha Katiba, kinachoruhusu serikali kutumia fedha bila idhini ya kawaida ya Bunge katika hali maalumu. Utaratibu huo hutumika pale ambapo fedha zilizotengewa shughuli fulani hazitoshi au wakati wa dharura kama majanga. Hata hivyo, matumizi hayo lazima yaripotiwe Bungeni ndani ya miezi miwili. Tangu Julai 2022, Wizara ya Fedha imeidhinisha taasisi za serikali kutumia Sh523 bilioni chini ya Kifungu cha 223. Kati ya kiasi hicho, Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti imekataa matumizi ya Sh158.6 bilioni. Ofisi hiyo sasa inapendekeza sheria zinazodhibiti matumizi ya kifungu hicho zipitiwe upya ili kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na kulinda uaminifu wa bajeti. Dkt Nyakang’o amekuwa akionya dhidi ya matumizi mabaya ya kifungu hicho kukwepa idhini ya Bunge. Miongoni mwa taasisi zilizozimiwa matumizi ya mabilioni ni Ofisi ya Rais, inayojumuisha Ikulu pamoja na ofisi za Rais, Naibu Rais na Mkuu wa Mawaziri. Dkt Nyakang’o alikataa maombi ya kutolewa kwa Sh7.8 bilioni ambazo wizara ya fedha ilikuwa tayari imeidhinisha. Katika mwaka wa kifedha wa 2025/26, wizara hiyo iliidhinisha ofisi hizo kutumia Sh12.9 bilioni chini ya Kifungu cha 223. Hata hivyo, Mdhibiti wa Bajeti aliidhinisha Sh5.1 bilioni pekee, sawa na asilimia 39 ya fedha zilizoombwa. Ripoti hiyo inasema baadhi ya maombi yalihusu shughuli za kawaida za kila siku ambazo zingetarajiwa wakati wa kuandaa bajeti. “Matumizi chini ya Kifungu cha 223 yanapaswa kufanywa kwa kuzingatia masharti yake,” Dkt Nyakang’o alisema. Kwa mwaka uliomalizika Juni 2026, wizara ya fedha iliidhinisha Sh281.5 bilioni kutolewa chini ya kifungu hicho kwa taasisi mbalimbali za serikali. Lakini Mdhibiti wa Bajeti aliidhinisha Sh209.4 bilioni pekee. Hii ina maana kuwa maombi ya kutumia Sh72 bilioni yalikataliwa. Ikulu ilizimiwa Sh7.3 bilioni. Kati ya Agosti 9, 2025 na Aprili 6, 2026, Waziri Mbadi alitoa idhini sita za Ikulu kutumia Sh11.8 bilioni kwa kile kilichoelezwa kuwa “gharama nyingine za uendeshaji”. Hata hivyo, Mdhibiti wa Bajeti aliidhinisha Sh4.45 bilioni pekee na kukataa maombi manne yenye thamani ya Sh7.3 bilioni. Miongoni mwa maombi yaliyokataliwa ni Sh5 bilioni yaliyoidhinishwa Desemba 12, 2025, Sh1 bilioni ya Aprili 6, 2026 na maombi mawili ya Sh800 milioni kila moja. Ofisi ya Naibu Rais Kithure Kindiki pia ilizuiwa kutumia Sh418.7 milioni, ambazo kwa kiasi kikubwa zilikusudiwa kugharamia ukarimu na ukodishaji wa magari. Wizara ya Fedha iliidhinisha ofisi hiyo kutumia Sh1.05 bilioni chini ya Kifungu cha 223. Lakini Mdhibiti wa Bajeti aliidhinisha Sh245.5 milioni pekee kutoka kwa moja ya maombi hayo. Ofisi ya Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi pia ilizuiwa kutumia Sh80 milioni ambazo wizara ya fedha ilikuwa imeidhinisha. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ofisi zilizo chini ya urais zilitumia jumla ya Sh33 bilioni katika mwaka huo. Fedha nyingi zilitumika katika shughuli za kawaida kama mishahara, kuandaa hafla na safari za maafisa wakuu wa serikali.

WABUNGE kutoka eneo la Magharibi wamempa Rais William Ruto orodha ya matakwa wanayotaka yashughulikiwe kabla ya eneo hilo kumuunga mkono katika uchaguzi wa 2027. Miongoni mwa matakwa makuu ni wadhifa wa Naibu Rais ambao wanataka utengewe mwanasiasa kutoka Magharibi katika muhula wa pili wa Rais Ruto. Pia wanataka eneo hilo kuhifadhi nafasi yake katika Tume ya Huduma za Bunge na miradi ya Serikali iliyokwama ikamilishwe. Wabunge hao pia wanataka Serikali kuingilia kati matatizo yanayokumba sekta ya sukari, kushughulikia mzozo wa ufadhili wa elimu na kuweka umeme katika maeneo ambayo bado hayajaunganishwa. Matakwa hayo yaliafikiwa Jumatatu wakati wa mkutano wa wabunge wa Magharibi uliofanyika Kisumu ulioandaliwa na Waziri wa Vyama vya Ushirika, Bw Wycliffe Oparanya. Kuhusu wadhifa wa Naibu Rais, wabunge hao walisema: “Kama jamii ya Magharibi, tunataka wadhifa wa Naibu Rais ili kumsaidia Rais William Samoei Ruto katika uchaguzi mkuu ujao.” Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa ukanda wa Magharibi, Bw John Waluke, alisema wanataka wadhifa huo kwa niaba ya eneo hilo bila kumuunga mkono mwanasiasa yeyote kwa sasa. Msimamo huo ni tofauti na ule wa Mei ambapo wabunge hao walimuunga mkono Bw Oparanya kwa kiti hicho. Wabunge hao pia walitaka nafasi inayoshikiliwa na Bi Rachael Ameso katika Tume ya Huduma za Bunge ibaki mikononi mwa mwakilishi kutoka Magharibi. Walitaka pia miradi ya Serikali iliyokwama ikamilishwe katika eneo hilo na Serikali itafute suluhu ya changamoto zinazowakabili wakulima na viwanda vya sukari. Hata hivyo, walipinga vikali Mswada wa Marekebisho ya Mazao. “Serikali inapaswa kushughulikia masuala yanayoathiri sekta ya sukari. Hata hivyo, tunasisitiza kuwa tunapinga kabisa Mswada wa Marekebisho ya Mazao,” walisema. Wabunge hao pia walitaka Serikali ishughulikie tatizo la ufadhili wa elimu, wakisema wanafunzi kutoka familia maskini ndio wanaoathirika zaidi. Walipendekeza usajili wa wapigakura uendelezwe kwa pamoja na kampeni za kuwahamasisha wananchi ziongozwe na wabunge. Aidha, walitaka Wizara ya Kawi kuunganisha umeme katika maeneo ambayo bado hayana huduma hiyo na kutatua hitilafu za mara kwa mara. Bw Oparanya alisema viongozi hao wataendelea kufanya mikutano ili kuimarisha uungwaji mkono wa Rais Ruto. “Tutakuwa na mikutano ya mara kwa mara kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu ujao. Viongozi wote mnaowaona hapa wanampigia debe Rais Ruto kwa muhula wa pili,” alisema. Wabunge 22 walihudhuria mkutano huo, huku watano wakisema hawangefika kwa kuwa walikuwa nje ya nchi. Mbunge wa Budalang’i, Bw Raphael Wanjala, alisema Magharibi ina haki ya kudai kiti cha Naibu Rais kwa kuwa liliunga ODM na marehemu Raila Odinga kwa muda mrefu. Alisema viongozi wa eneo hilo wamekubaliana kudai kiti hicho katika muungano wowote utakaohusisha ODM.

Tanzania’s Union will need honest dialogue, constitutional clarity, and a willingness to protect its benefits if it is to remain strong for the next generation, speakers said on Tuesday, September 8, 2026, during a national meeting to discuss the country’s political situation following the 2025 General Election and the nation’s future. Speaking at the event, the ruling CCM Vice Chairman for Tanzania Mainland, Mr Stephen Wasira, argued that the Union itself has delivered important benefits and that its stability cannot be separated from peace in either part of the country. He said the movement of people between Zanzibar and the Mainland was among the practical benefits of the Union, while stressing that instability on one side would inevitably affect the other. “The peace and stability of Zanzibar and the stability of the United Republic depend on each other,” he said. Mr Wasira also questioned ACT-Wazalendo’s call for a ‘Zanzibar with full authority’, saying the phrase needed to be understood within the existing Union framework. “Zanzibar has its own Revolutionary Government which deals with almost all matters concerning Zanzibar, except for a few matters that fall under the Union. So, when we talk about Zanzibar having full authority, we have to ask: does it remain part of the Union, or does it become sovereign? There is one sovereignty of the United Republic of Tanzania, while responsibilities are divided between the Union and Zanzibar,” he said. “Any challenges should be addressed in a way that does not undermine the future of our Union,” added Mr Wasira. For former Zanzibar First Vice President and ACT-Wazalendo National Chairman Othman Masoud Othman, the central issue is how the constitutional framework is interpreted and implemented. He warned that if the current Constitution were followed strictly in some areas, it could create serious disputes over matters such as revenue, ports, immigration, oil, and gas, potentially placing the Union itself under severe pressure. “If there is a major threat to the Union, it is the Constitution itself as it stands now and the way we have implemented it. We really need to sit down and resolve these issues to protect the Union,” he said. Mr Othman said the answer was not simply to debate whether Zanzibar should have more or less authority, but to revisit the constitutional fundamentals and agree clearly on what belongs to the Union and what falls under each side’s exclusive authority. For the next generation, Mr Othman said, the task was to use the peace and benefits already secured rather than take them for granted. “We have benefited from this country. I strongly ask Tanzanians not to lose that benefit,” he said. For his part, veteran Zanzibar politician, Mr Ali Mzee Ali said the Union should be understood through the country’s history, particularly Zanzibar’s experience of political conflict and reconciliation. Recalling efforts that brought political rivals together, he said Zanzibar had shown that differences could be overcome when national interests were placed above political divisions. He reminded the younger generation that political parties were not the foundation of their identity: “Political parties are things that came later. All of us here today are Tanzanians.” Mr Ali acknowledged that the Union was not perfect, arguing that its human origins meant it would inevitably have shortcomings. “This Union is not from God; it is a Union made by human beings, and therefore it has some weaknesses, but we need it more than anything in our country,” he said. For him, strengthening the Union requires compromise, patriotism, and learning from the experiences of previous generations.

The Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) in Shinyanga Region has conducted a special operation at the Mwime Mine in Zongomela Ward, Kahama Municipality, uncovering several small-scale miners illegally diverting electricity and connecting unauthorised users.

Tanzania’s gaming industry is targeting more than Sh300 billion in government revenue this financial year, as regulators step up efforts to curb illegal gaming and promote responsible betting.

MTWARA: MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara Abdallah Chikota amesema uwepo wa ujenzi wa kongani ya viwanda ya korosho iliyopo kijiji cha Maranje Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara ni faida kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo hasa suala la ajira kwa vijana. Hayo yamejiri leo Septemba 7,2026 wakati mbunge wa jimbo hilo alipotembelea…

The High Court’s Dar es Salaam Sub-Registry has extended by 14 days the hearing of treason charges facing Chadema chairman Tundu Lissu, directing both sides to cooperate to ensure the case is concluded within the additional period. The hearing, which began on August 10, 2026, was scheduled to end on September 7 before the case was adjourned to another date. However, proceedings continued after the scheduled period ended, with the fourth defence witness yet to complete her evidence-in-chief. Justice Dunstan Ndunguru, who is leading the three-judge panel alongside Justices James Karayemaha and Ferdinand Kiwonde, announced the extension on behalf of the panel. “You will recall that, according to the cause list, today was the final day scheduled for hearing this matter,” said Justice Ndunguru. “However, the matter has been extended for 14 days from today, with the aim of ensuring that it is concluded within this period," he added. Justice Ndunguru urged both sides to avoid unnecessary questions and issues that had no bearing on the case or would not be used in determining the matter, saying such interventions only wasted the court’s time. Lissu speaks on remaining witnesses Following the judge’s directive, Mr Lissu said that once the witness who began testifying on Monday completed her evidence, he would have only one more witness remaining before the court ruled on objections raised against some of his proposed witnesses. “That is fine, My Lord. Apart from this witness who is giving evidence today, Brenda, I have only one witness remaining to conclude the witnesses I have listed. I will then await your decision regarding the other witnesses,” said Mr Lissu. Among the witnesses Mr Lissu has listed but whose testimony has been challenged are President Samia Suluhu Hassan, former Vice-President Philip Mpango, former Prime Minister Kassim Majaliwa and senior officials of the security and defence organs. Mr Lissu, who is also a lawyer, is facing a treason charge under Section 39(2)(d) of the Penal Code, Revised Edition 2023. The prosecution alleges that on April 3, 2025, while a Tanzanian citizen, Mr Lissu intentionally incited the public to prevent the 2025 General Election from taking place by making and publishing statements online intended to pressure the Head of State. Among the statements attributed to him are: “This position signals rebellion ... because we are saying we will stop the election, we will encourage rebellion ... that is how we will bring change ... so we are going to stir things up ... especially this election, we are going to disrupt it completely ... we are going to stir things up very badly.” Defence witness denies Lissu organised media event The fourth defence witness, Chadema Director of Communications and Dissemination Brenda Rupia, 34, began giving evidence on Monday. Among other things, Ms Rupia told the court that Mr Lissu was not involved in organising a meeting of aspiring candidates at which he is alleged to have made statements threatening the government, nor was he responsible for inviting journalists to the event. Led in her evidence-in-chief by Mr Lissu, Ms Rupia said the meeting, held on April 3, 2025, at Chadema headquarters in Mikocheni, was organised by the party secretariat under Secretary-General John Mnyika. She said she was responsible for inviting journalists to cover the meeting. According to Ms Rupia, the meeting was organised for aspiring candidates seeking various positions in the 2025 General Election to discuss the party’s “No Reforms, No Election” campaign. She told the court that on March 27, 2025, she issued a media statement announcing the meeting and inviting journalists. The statement was subsequently posted on the party’s social media platforms. Ms Rupia therefore maintained that Mr Lissu neither invited the media nor organised the meeting, adding that the invitation sent to journalists contained no instructions on what they should bring or how they should carry out their work. She said the meeting was attended by aspiring candidates, members of the party secretariat and senior Chadema leaders, including chairman Mr Lissu, Zanzibar deputy chairman Said Mzee, Mainland deputy chairman John Heche and Secretary-General Mr Mnyika, as well as deputy secretaries-general from both Mainland Tanzania and Zanzibar. The media organisations present included Mwanzo TV, Chanzo TV, Jambo TV, ITV, Mwananchi and other online outlets. Ms Rupia told the court that Mr Lissu was the main speaker at the meeting and had no other role in organising the event. “The chairman did not stream the broadcast because he is not an employee of Jambo TV, nor was he aware that Jambo TV was present,” she said. “I do not know whether the chairman was aware that journalists had been invited because that is not part of his responsibilities.” She further explained that the owner of a media organisation owns the content it records, meaning that content produced by Jambo TV during the meeting belonged to the broadcaster. The case was adjourned until Tuesday, September 8, 2026, when Ms Rupia is expected to continue with her evidence-in-chief before being cross-examined by the prosecution.

The husband of President Samia Suluhu Hassan, Mr Hafidh Ameir Hassan has been buried in Kizimkazi, South Unguja Region, leaving behind two widows, four children and 15 grandchildren. The funeral prayer held on Monday, September 7, 2026, was led by Zanzibar Grand Mufti Sheikh Saleh Omar Kaabi. Government, religious and political leaders attended the funeral, led by Vice President Deogratius Ndejembi, Zanzibar President Dr Hussein Ali Mwinyi and Prime Minister Mwigulu Nchemba. Who was Hafidh Ameir? Reading the deceased's biography, Deputy Director of State House Communications, Mr Shabaan Kisu, said the deceased was born on January 1, 1946, in Kisakasaka village, West B District, Urban West Region, Unguja. He said the deceased began his education at Kombeni Shakani School in West B District, completing primary education in 1960 before proceeding to secondary education at Tumekuja Secondary School in Mkunazini, where he graduated in 1965. “Throughout his life, the deceased continued to take advantage of various educational and training opportunities to advance his professional knowledge, particularly in teaching and agriculture,” he said. According to Mr Kisu, in 1970 Hafidh joined the Zanzibar Teachers’ College and graduated in 1973. He was subsequently employed as a teacher and taught at various schools in Tanzania. He said in 1980 Hafidh was selected to study agriculture at Uyole Agricultural College in Mbeya, enabling him to expand his knowledge and skills in agriculture, which became an important part of his professional life. In 1982, he was employed as an agriculture instructor at Fidel Castro School in Pemba. In 1986, he secured an opportunity to further his studies in agriculture in Sri Lanka, where he pursued a diploma and graduated in 1988, specialising in coconut farming. After returning to Zanzibar in 1988 following his studies in Sri Lanka, the deceased continued working at the Ministry of Agriculture. Mr Kisu said that, determined to further his academic qualifications, the deceased pursued a master’s degree in agricultural machinery engineering in Britain in 1990. After completing his studies in Britain, he returned to Zanzibar and continued working at the Ministry of Agriculture until his retirement in 2005. After retirement, the deceased continued teaching at Kizimbani Agricultural College in Unguja. Before his death on September 7, 2026, he had been suffering from heart disease and had received treatment at various hospitals. Others who attended the funeral included Zanzibar Second Vice President Hemed Suleiman Abdullah, retired fourth-phase President Jakaya Kikwete, former Zanzibar President Amani Abeid Karume, former Zanzibar President, Dr Ali Mohammed Shein, and former First Vice President of Zanzibar Othman Masoud Othman. Others were CCM Mainland Vice Chairman Stephen Wasira, CCM Zanzibar Deputy Secretary General Abdi Mahmoud Abdi, as well as ministers and deputy ministers from the Union Government and Zanzibar Revolutionary Government.

DAR ES SALAAM: SERIKALI imeendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali, mifumo ya kisasa ya usimamizi wa bandari na biashara, pamoja na matumizi ya taarifa za kisayansi katika kufanya maamuzi kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya uchumi wa buluu nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamadi Masauni, amesema hayo…

DAR ES SALAAM: WIZARA ya Katiba na Sheria imeanza kupitia sheria mbalimbali za kisekta nchini ili kuhakikisha zinaendana na mahitaji ya sasa pamoja na malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ili kuweka mfumo imara wa kisheria utakaowezesha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi, ikiwemo uwekezaji katika sekta ya Uchumi wa Buluu, huku ukilinda…

KATIKA mikutano ya kisiasa, ni kawaida kwa baadhi ya viongozi wa United Democratic Alliance (UDA) kumpigia debe Rais William Ruto ili achaguliwe tena mnamo Agosti 10, 2027. Kisheria, viongozi hao bado ni wanachama wa vyama vilivyowapitisha katika uchaguzi wa 2022. Lakini hadharani, wamehamia vyama vingine na sasa wanatafuta kuchaguliwa kupitia vyama hivyo. Baadhi yao wamepewa […]

DODOMA: SPEAKER of the National Assembly, Mr Mussa Zungu, has urged officials under the Prime Minister’s Office— Regional Administration and Local Government (PMORALG) to change their mindset and stop frustrating Public-Private Partnership (PPP) initiatives aimed at improving waste management in Dar es Salaam and other cities. Mr Zungu issued the call in Dodoma yesterday, a…

MWANAUME mmoja Mkenya anataka matatizo kama vile ukosefu wa nguvu za kiume yatambuliwe kisheria kama ulemavu. Katika ombi alilowasilisha Bungeni, Dkt Benson Kibore amesema tatizo la nguvu za kiume na ukosefu wa hamu ya kushiriki mapenzi, hali inayojulikana kama HSDD, linahitaji kushughulikiwa kupitia sheria na sera za afya. Anasema matatizo haya, ambayo hapo awali yalihusishwa zaidi na wazee, sasa yanaonekana pia miongoni mwa vijana. Dkt Kibore anarejelea utafiti wa 2026 uliofanywa Nairobi na kuchapishwa kwenye medRxiv, ambao ulionyesha kuwa asilimia 10.4 ya vijana waliofanyiwa utafiti walikuwa na tatizo la nguvu za kiume. Wastani wa umri wao ulikuwa miaka 27. “Kwa hivyo, ukosefu wa hamu ya ngono unaohusishwa na tatizo la nguvu za kiume si tatizo la wazee pekee bali ni hali inayowakumba vijana pia,” alisema katika ombi lake kwa Bunge la Kitaifa na Seneti. Dkt Kibore pia anataka HSDD itambuliwe kama suala la afya ya umma ili wanaohitaji matibabu waweze kupata huduma hiyo. Anasema matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume yanaweza kuathiri afya ya akili, ndoa, mahusiano na afya ya uzazi. Katika ombi hilo la Julai, anataja kutoridhika katika ndoa, kutengana kihisia, msongo wa mawazo, kuvunjika kwa mahusiano na ukosefu wa uaminifu katika ndoa kama baadhi ya madhara yanayoweza kuwapata waathiriwa. Iwapo Bunge litaidhinisha pendekezo hilo, sheria kadhaa zitalazimika kufanyiwa marekebisho, zikiwemo Sheria ya Watu Wenye Ulemavu na Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii (SHA). Mabadiliko hayo yanaweza kuwezesha watu wenye matatizo sugu ya kingono yaliyothibitishwa kutambuliwa chini ya vigezo vya ulemavu. Pia, huduma kama uchunguzi, ushauri nasaha na matibabu zinaweza kugharamiwa kupitia Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Dkt Kibore anasema gharama ya matibabu imekuwa kikwazo kwa Wakenya wengi. Wagonjwa wengi hulipia huduma kutoka mifukoni mwao, huku ada za mashauriano katika hospitali za kibinafsi zikianzia takriban Sh5,000 na gharama ya matibabu kufikia mamia ya maelfu ya shilingi. Upasuaji wa uume, unapohitajika, unaweza kugharimu zaidi ya Sh1 milioni. Dkt Kibore pia anasema tatizo hilo linaweza kusababisha mtu kukosa kujiamini na kuathiri afya ya akili. Anarejelea pia utafiti mwingine unaoonyesha uhusiano kati ya hamu ya kushiriki ngono na afya ya moyo. Anasema kuwa kudumisha hamu nzuri ya ngono kunaweza kuwa na manufaa kwa afya ya moyo na mwili kwa ujumla. Dkt Kibore anasema unyanyapaa unaohusishwa na matatizo ya kingono huwazuia wanaume na wanawake wengi kutafuta matibabu. “Unyanyapaa unaozunguka matatizo ya kingono kwa wanaume na wanawake mara nyingi huwazuia kutafuta msaada, hivyo kuongeza muda wa mateso ndani ya familia,” alisema.

RAIS William Ruto ameanza ziara ya siku tatu katika Kaunti ya Kajiado, hatua inayotafsiriwa na wachambuzi kama juhudi za kuimarisha maendeleo na wakati huo huo kujiweka katika nafasi nzuri kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Rais anatarajiwa kuzuru maeneo mbalimbali ya Kajiado kati ya jana Septemba 3 na Septemba 7 kukagua na kuzindua miradi ya umeme, barabara, unyunyuzaji, masoko ya kisasa, nyumba za gharama nafuu na mabweni ya wanafunzi. Ingawa ziara hiyo imewasilishwa kama ya maendeleo, wengi wanasema ina uzito wa kisiasa kutokana na umuhimu wa kura za jamii ya Maa inayopatikana hasa katika kaunti za Kajiado, Narok na Samburu. Kaunti hizo tatu zina zaidi ya wapigakura milioni 1.09 waliosajiliwa. Ziara hiyo imejiri wiki chache baada ya Rais Ruto kufanya ziara ya siku mbili Narok, ambapo alizindua miradi kadhaa ya maendeleo na kusisitiza ushirikiano kati ya UDA na ODM. Akiwa Narok, Rais alisema kuwa hapo awali kura za eneo hilo zilikuwa zikigawanywa kati yake na aliyekuwa kiongozi wa ODM, Raila Odinga, lakini sasa ana matumaini ya kupata uungwaji mkono mkubwa kutokana na ushirikiano wa vyama hivyo viwili. Akiwa Kajiado, Rais atakagua miradi mbalimbali ikiwemo soko la kisasa la Kimana, mpango wa nyumba za bei nafuu Oloitoktok, mradi wa umeme wa Sultan Hamud-Loitoktok, masoko Namanga na Kajiado Town pamoja na miradi ya maji na barabara. Hata hivyo, Rais anakabiliwa na ushindani kutoka kwa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP) kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Bw Gachagua amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara katika maeneo ya Maa akijaribu kuvutia viongozi na wapigakura wa eneo hilo. Kwa zaidi ya wapigakura nusu milioni Kajiado pekee, eneo hilo linaonekana kuwa uwanja muhimu wa mapambano ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027. Wachambuzi wanasema ziara ya Rais ni uwekezaji wa mapema wa kisiasa pamoja na juhudi za kuonyesha rekodi ya maendeleo ya serikali yake.

SERIKALI imelaumiwa kwa kupuuza sekta ya afya ya umma iliyoathiriwa na mgomo wa wauguzi huku ikishughulikia sekta nyingine na kuacha wagonjwa kuteseka. Wakati wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga walipogoma Agosti 30 na kutatiza shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) pamoja na viwanja vya ndege vya Moi, Eldoret na Kisumu, serikali ilichukua siku mbili pekee kufanya mazungumzo na kutia saini makubaliano ya kurejea kazini. Kufikia Septemba 1, mgomo ulikuwa umemalizika na safari za ndege kurejea kawaida. Lakini kwa upande mwingine, wauguzi wamekuwa mgomoni kwa siku 39 huku maafisa wa maabara, afya ya umma, lishe, wafamasia, maafisa wa utabibu na wahudumu wa Mpango wa Afya kwa Wote (UHC) wakiendelea kugoma kwa karibu siku 50. Katika kipindi hicho, akina mama wamekuwa wakifariki wakiwa wodini wakijifungua, watoto wachanga wakipoteza maisha kabla hata ya kupumua kwa mara ya kwanza, huku serikali ikikosa kufikia makubaliano yoyote na wahudumu wa afya. Rais wa Chama cha Kitaifa cha Wauguzi nchini (NNAK), Collins Ajwang alisema, hatua ya haraka iliyochukuliwa na serikali kumaliza mgomo wa wafanyakazi wa anga inaonyesha tofauti ya namna sekta ya afya inavyoshughulikiwa. “Tulianza kushinikiza utekelezaji wa Mkataba wa Pamoja wa Mishahara (CBA) pamoja na madaktari na maafisa wa utabibu. Wao walipata mikataba yao na hata wakalipwa. Serikali inasema wauguzi ni wengi hivyo haina bajeti ya kutulipa. Hiyo haina mantiki kwa sababu idadi yetu kubwa ndiyo imewezesha hospitali kufanya kazi ipasavyo,” alisema Ajwang. Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi Kenya (KNUN), Seth Panyako, alisema suala hilo linahusu maslahi na vipaumbele vya serikali. “Walio madarakani wanaweza kwenda hospitali za kibinafsi. Lakini mwananchi wa kawaida hutegemea hospitali za umma. Hali hii inaonyesha wazi kuwa hawajali afya ya wananchi wa kawaida,” alisema. Takwimu kutoka mfumo wa Every Woman, Every Newborn, Everywhere (EWENE) zinaonyesha hali ya janga hilo. Kati ya Jumatatu na Alhamisi wiki hii pekee, wanawake wanane walifariki kutokana na matatizo ya uzazi, watoto wachanga 16 walio na chini ya mwezi mmoja walikufa na vifo 55 vya watoto wa kipindi cha kujifungua vilirekodiwa. Mwezi uliopita pekee, wanawake 75 walifariki kutokana na matatizo ya uzazi huku watoto 458 wakifariki kabla au mara tu baada ya kuzaliwa. Ajwang alisema kaunti za Kisumu, Nakuru, Kakamega na Kajiado zimeathirika zaidi. “Hakuna dalili kuwa hali inaimarika. Wanawake wengi sasa hawafiki hospitalini. Wanaojifungulia nyumbani au maeneo yasiyo rasmi hawahesabiwi katika takwimu hizi,” aliongeza. Kwa mujibu wa vyama vya wahudumu wa afya, mgomo huo umeathiri pia mafunzo ya wanafunzi wa uuguzi, udaktari na maafisa wa utabibu ambao hutegemea hospitali za umma kupata ujuzi. “Wauguzi ni karibu asilimia 70 ya wafanyakazi wote wa afya nchini. Kutokuwepo kwao hospitalini si suala la mzozo wa wafanyakazi pekee tena. Sasa ni suala la usalama wa wagonjwa na afya ya umma,” alisema Ajwang. Chanzo kikuu cha mgogoro huo ni utekelezaji wa CBA ambayo wauguzi wamekuwa wakidai tangu 2017. Ingawa mgomo wa miezi sita mwaka huo ulisitishwa baada ya makubaliano ya kurejea kazini, viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanasema hadi leo CBA hiyo haijatekelezwa kikamilifu. Wauguzi wanashutumu Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC), Wizara ya Afya na Baraza la Magavana kwa kuchelewesha hatua zinazohitajika ili mkataba huo usajiliwe na kutekelezwa. Akizungumza wakati wa maandamano katika ofisi za SRC, Panyako alisema maafisa wa tume hiyo walifunga ofisi zao na kuondoka kabla ya kukutana na wauguzi. “Tumekuwa wavumilivu kwa zaidi ya miaka tisa. Serikali haiwezi kuendelea kutupa ahadi halafu ishindwe kuzitimiza ilhali wauguzi ndio wanaobeba mzigo mkubwa katika hospitali nyingi za umma,” alisema. Hata hivyo, alisema kuna maendeleo katika mazungumzo kuhusu mwongozo wa maendeleo ya taaluma na ajira za kudumu kwa wafanyakazi wa UHC. Kwa sasa, suala kubwa lililosalia ni kutiwa saini kwa CBA. Panyako pia alitaka mfumo wa usimamizi wa wafanyakazi wa afya uwe wa kitaifa badala ya kuachwa mikononi mwa kaunti pekee. “Hauwezi kufanikisha Afya kwa Wote bila kuwa na mfumo wa pamoja wa kusimamia wahudumu katika sekta ya afya,” alisema. Ajwang alitoa wito kwa serikali ya kitaifa, serikali za kaunti, vyama vya wafanyakazi na wadau wengine kuketi pamoja na kutatua mgogoro huo haraka. “Kila siku ya kuchelewa inamaanisha maisha zaidi yanapotea. Wauguzi wanataka kurejea hospitalini ili Wakenya wapate huduma wanazohitaji,” alisema.

The National Drug Law Enforcement Agency (NDLEA) has raised the alarm over attempts by international drug cartels to establish production bases in Nigeria, disclosing that Mexican-linked criminal networks are behind efforts to set up industrial-scale methamphetamine laboratories in forests across Ogun and Oyo states.

The legal suits come with a contingent liability of Ugandan shillings 777 billion equivalent to US$ 206 million, raising concern among Members of Parliament over the potential impact on public finances and electricity service delivery.

..2026 spending rises to N1.102trn By Adeola Badru IBADAN — The Oyo State House of Assembly has approved a N210 billion supplementary appropriation for the 2026 fiscal year, raising the state’s total approved budgetary provision to N1.102 trillion. The approval was given during plenary on Thursday following consideration and adoption of the report of the […]

…Governor signs Supplementary Appropriation, two other laws By Emma Una CALABAR — Cross River State Governor, Senator Bassey Otu, on Wednesday signed the state’s 2026 Supplementary Appropriation Law, increasing the 2026 budget from N961,624,047,275.08 to N963,074,438,018.60. Otu also signed the Cross River State Social Investment and Protection Law and the Health Quackery (Prohibition) Law. The […]

WATUMIAJI wa maziwa jijini Nairobi na miji mingine huenda wakakumbwa na uhaba mkubwa zaidi wa bidhaa hiyo iwapo ukame unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini utaendelea, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe ameonya. Onyo hilo linajiri wakati ambapo watu wengi wanalalamikia kupungua kwa maziwa katika maduka makubwa na maduka ya rejareja, huku picha za rafu zisizo na bidhaa hiyo zikisambaa mitandaoni na kuzua wasiwasi miongoni mwa watumiaji. Hata hivyo, Bodi ya Maziwa Kenya (KDB), imesema hali inayoshuhudiwa kwa sasa si upungufu mkubwa wa maziwa bali ni changamoto ya muda katika usambazaji. Kulingana na bodi hiyo, hali hiyo imesababishwa na msimu wa ukame na baridi kali katika maeneo muhimu ya uzalishaji wa maziwa, jambo ambalo limepunguza malisho na chakula cha mifugo. Takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha maziwa yanayowasilishwa kwa viwanda vya usindikaji kilishuka kwa asilimia 3.7 kutoka lita milioni 84.4 mwezi Juni hadi lita milioni 81.3 mwezi Julai mwaka huu. Aidha, taarifa za awali zinaonyesha kiwango hicho kiliendelea kupungua mwezi Agosti kutokana na hali ya ukame. Maziwa yasiyoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu yaliyosindikwa yameathirika zaidi ikilinganishwa na maziwa yanayodumu kwa muda mrefu wa matumizi, hali iliyosababisha baadhi ya maduka kuweka kiwango maalum cha ununuzi kwa kila mteja. Akizungumza na vyombo vya habari, Bw Kagwe alisema kuwa licha ya Kenya kuongoza kwa uzalishaji wa maziwa yaliyosindikwa barani Afrika, nchi haiwezi kujinasua dhidi ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa. “Ni kweli uzalishaji wa maziwa umeathiriwa na ukame wa hivi majuzi. Iwapo hali itaendelea, huenda tukalazimika kuagiza maziwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Tanzania,” alisema. Kenya huzalisha takriban lita 5.5 bilioni za maziwa kila mwaka, lakini sekta hiyo bado inategemea kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa malisho na maji ya kutosha. Katibu wa Idara ya Mifugo, Jonathan Mueke, alisema serikali imeanza kutekeleza mikakati ya muda mfupi na mrefu ili kupunguza athari za uhaba huo. Hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha wafugaji wanapata chakula cha mifugo kwa bei nafuu. “Tunakusudia kushirikiana na watengenezaji wa chakula cha mifugo ili kuwasaidia wafugaji kupata lishe ya mifugo katika maeneo yote ya nchi,” alisema. Katika Bonde la Ufa Kaskazini, hali ni mbaya zaidi huku baadhi ya vituo vya kukusanya maziwa vikishuhudia kiwango cha maziwa kikishuka kwa karibu nusu. Mwenyekiti wa Kenya Dairy Farmer Federation Stanley Ngombe, alisema kituo chake hupokea chini ya lita 2,000 kwa siku kutoka zaidi ya lita 10,000 hapo awali. Uhaba huo pia umeongeza bei ya maziwa. Katika baadhi ya maeneo, pakiti ya mililita 500 iliyouzwa kati ya Sh50 na Sh52 sasa inauzwa hadi Sh60, huku baadhi ya maduka yakiruhusu mteja kununua pakiti mbili pekee. Wakati huo huo, KDB imewaonya wananchi dhidi ya kununua maziwa yasiyoidhinishwa, ikisema maafisa wake wameagizwa kuwasaka wanaouza bidhaa zisizokidhi viwango vya usalama. Wataalamu wana matumaini kuwa mvua za Oktoba na Novemba zitasaidia kuboresha malisho na kurejesha uzalishaji wa maziwa, ingawa serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu.

KUNA ukatili wa aina yake katika kumwambia kijana aliyefaulu mtihani, akapata nafasi ya chuo kikuu na kuanza safari ya kubadili maisha yake kwamba sasa anapaswa kusubiri ili ajue kama Serikali itamfadhili. Hii si hadithi ya kuchelewa kwa karatasi ofisini. Ni hadithi ya taifa linalochezea mustakabali wa kizazi chake. Katibu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Beatrice Inyangala amesema wanafunzi wa vyuo vikuu huenda wakalazimika kusubiri kwa muda zaidi kabla ya kupata uamuzi kuhusu ufadhili wao, huku Serikali ikiendelea kufanyia marekebisho mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu. Lakini swali ni: Mwanafunzi afanye nini wakati Serikali bado “inafanya marekebisho”? Aende darasani bila kujua nani atalipa karo? Aanze muhula bila kujua kama ataweza kulipia nyumba na chakula? Mzazi au mlezi aanze kukopa bila kujua kama msaada wa Serikali utawahi? Haya si maswali ya kinadharia. Ni maisha halisi. Kenya imekuwa ikizungumza kwa miaka mingi kuhusu elimu kama ngazi ya kutoka katika umaskini. Lakini ni vigumu kueleza mantiki ya taifa linalomwambia kijana elimu ndiyo ufunguo wa maisha bora, halafu linamfikisha mlangoni mwa chuo na kumwambia: subiri kwanza, hatujui tutakusaidiaje. Hapo ndipo sera nzuri inapogeuka kuwa mzigo kwa maskini. Familia tajiri inaweza kusubiri. Mwanafunzi mwenye wazazi wenye uwezo anaweza kulipa karo huku Serikali ikijadiliana. Lakini mwanafunzi wa familia inayohangaika kulipa kodi ya nyumba, chakula na usafiri hana anasa hiyo. Kwake, kuchelewa kwa ufadhili kunaweza kumaanisha kukosa masomo. Na kukosa masomo kunaweza kumaanisha kupoteza muhula. Kupoteza muhula kunaweza kumaanisha kuacha chuo kabisa. Hivyo basi, “subiri” si neno dogo. Kwa baadhi ya wanafunzi, ni hukumu.

DAR ES SALAAM: TANZANIA has conveyed condolences to the government and people of Norway following the death of King Harald V, with the government praising the late monarch for his leadership and contribution to national unity. Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Dr Ngwaru Maghembe, signed the condolence book at the Norwegian…

By Dapo Akinrefon LAGOS — Governor Babajide Sanwo-Olu of Lagos State has praised President Bola Tinubu’s commitment to democratic principles, saying the outcome of the recent Osun governorship election demonstrated that Nigeria’s ruling party could lose an election without undermining the democratic process. Sanwo-Olu spoke on Thursday at the seventh annual lecture of Freedom Online, […]

DAR ES SALAAM: SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India imeanza kuchukua hatua mahsusi za kuendeleza sekta ya kilimo, ikiwemo kuandaa majukwaa yatakayounganisha wadau wa sekta hiyo na kuwawezesha kujifunza, kujenga mitandao ya mahusiano pamoja na kuingia katika ubia wa kibiashara. Hayo yamesemwa leo, Septemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi…

DAR ES SALAAM: SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India imeanza kuchukua hatua mahsusi za kuendeleza sekta ya kilimo, ikiwemo kuandaa majukwaa yatakayounganisha wadau wa sekta hiyo na kuwawezesha kujifunza, kujenga mitandao ya mahusiano pamoja na kuingia katika ubia wa kibiashara. Hayo yamesemwa leo, Septemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi…

Sokoto State Police Command has on Thursday raised its security alert level in Kebbe Local Government Area following intelligence reports of a planned attack by bandits who have imposed a ₦40 million compulsory levy on residents of Kebbe town and neighbouring communities.

RAIS William Ruto amemshambulia vikali mwekezaji wa kimataifa, Tata Chemicals, eneo la Magadi, Kajiado, akisema kampuni hiyo imeshindwa kuwanufaisha Wakenya licha ya kufanya biashara nchini kwa zaidi ya miaka 100. Rais alisema kampuni hiyo imekuwa ikisafirisha malighafi ya Kenya nje ya nchi badala ya kujenga viwanda vya kutengeneza vioo na kemikali nchini. “Nimewaambia waondoke. Wameshindwa kujenga kiwanda cha vioo nchini. Wanasafirisha tu rasilimali zetu hadi nchi yao. Serikali italeta mwekezaji mpya kwa masharti mapya,” alisema. Alisema serikali pia itafadhili usambazaji wa maji kwa wakazi wa Magadi, akisema maji ni miongoni mwa huduma ambazo Tata Chemicals imekuwa ikitoa kwa jamii. Rais alimuomba Gavana wa Kajiado Joseph Lenku kumuunga mkono katika kuhakikisha kampuni hiyo inaondoka katika kaunti hiyo. Kauli hiyo inajiri mwezi mmoja baada ya Wizara ya Madini na Uchumi wa Baharini kuamuru kampuni hiyo kusitisha shughuli za uchimbaji kutokana na madai ya kutofuata masharti ya kisheria. Kesi kuhusu suala hilo bado iko katika Mahakama Kuu na itasikilizwa Oktoba 6, 2026. Rais Ruto alikuwa Kajiado kuanza ziara ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo bunge matano. Ziara hiyo pia imeonekana kama juhudi za kuimarisha uungwaji mkono wa chama cha UDA kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais aliahidi kukamilisha kiwanda cha kusindika nyanya cha Rombo chenye thamani ya Sh1.2 bilioni, ambacho kimekamilika kwa asilimia 70. Alisema kiwanda hicho kitawasaidia wakulima wa nyanya kupata soko bora na kuongeza mapato yao. Eneo la Rombo huzalisha takriban tani 70,000 za nyanya kwa mwaka. Rais pia alitetea Hazina ya Michezo, Sanaa na Maendeleo ya Jamii (SASDF), akisema imewezesha ujenzi wa viwanja 32 nchini. Aidha, aliwataka viongozi wa upinzani kukutana naye kwenye uchaguzi wa 2027 badala ya kutumia kauli mbiu za kisiasa. “Tutakutana kwenye sanduku la kura,” alisema. Tata Chemicals, zamani ikijulikana kama Magadi Soda, ni moja ya waajiri wakubwa katika sekta ya uchimbaji madini nchini. Kampuni hiyo iko takriban kilomita 120 kusini-magharibi mwa Nairobi, karibu na Ziwa Magadi, eneo linalojulikana kwa madini ya chumvi aina ya trona. Kampuni hiyo pia ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa bidhaa nje ya Kenya, ikichangia takriban asilimia sita ya mauzo ya nchi nje. Kwa miaka mingi, Tata Chemicals imeendesha miradi ya kijamii katika afya, maji, elimu na uwezeshaji wa jamii. Hata hivyo, imekuwa ikikabiliana na mzozo wa muda mrefu na Serikali ya Kaunti ya Kajiado kuhusu ushuru wa ardhi na malipo ya mrabaha wa madini.

The third defence witness in the treason trial of Chadema Chairman Tundu Lissu detailed to the High Court’s Dar es Salaam Sub-Registry on Wednesday the origins and motives behind the party’s ‘No Reforms, No Election’ campaign.

Chadema national chairman Tundu Lissu, who is in remand facing a non-bailable treason charge, has sent a message to people spreading reports that his assistant, the party’s Vice Chairman for the Mainland, Mr John Heche, is the reason he remains in custody.

Serikali imeainisha mfululizo wa maboresho ya kisera na programu za kuwawezesha kiuchumi vijana, kwa lengo la kuwaweka katika nafasi ya msingi katika maendeleo ya taifa, huku Umoja wa Ulaya (EU) ukisisitiza upya dhamira yake ya kuunga mkono ubunifu, ujasiriamali wa vijana na upatikanaji wa masoko ya kimataifa. Akizungumza wakati wa kikao shirikishi na wawakilishi wa…