POLISI wa kutuliza ghasia Jumamosi walizuia jaribio la kundi la vijana kuvuruga mkutano wa kisiasa wa Naibu Rais Kithure Kindiki katika Uwanja wa Nembure, Kaunti ya Embu.
Maafisa hao walirusha gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya vijana hao waliokuwa wakipiga kelele na kurusha mawe.
Vurugu hizo zilianza wakati Profesa Kindiki alipokuwa akihutubia maafisa wa chama cha UDA kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura katika kaunti hiyo.
Alipokuwa akizungumza, vijana waliokuwa nje ya uwanja huo walianza kupaza sauti na kurusha mawe kwa lengo la kuvuruga mkutano huo. Wakati mmoja walijaribu kuvamia uwanja huo lakini walizuiwa na maafisa wa usalama.
Hatimaye polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi, hatua iliyozua mapambano ya kukimbizana kati yao na vijana hao yaliyodumu kwa saa kadhaa nje ya uwanja huku Kindiki akiendelea na hotuba yake bila kusitisha mkutano.
Baadaye, vijana hao walitawanyika lakini walikusanyika tena baada ya mkutano kumalizika na kuzua vurugu katika eneo hilo.
Walivamia barabara iliyo karibu, kuwashambulia madereva na wakazi huku wakichoma magari kadhaa, jambo lililozua hofu.
Miongoni mwa magari yaliyochomwa moto ni la mwanahabari wa eneo hilo. Mfuasi mmoja wa UDA pia alijeruhiwa usoni baada ya kupigwa na jiwe na kupatiwa huduma ya kwanza.
Polisi wazima jaribio la kutibua mkutano wa Profesa Kindiki

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]