Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
RAIS SAMIA: "2025 TULIPATA MSUKOSUKO" -AFICHUA SIRI YA KUFANYA MARIDHIANO - MPANGO WA KATIBA WATAJWA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumzia hatua mpya…
… Only 6% of pregnant women complete iron supplementationBy Chioma Obinna Vice President Kashim Shettima on Tuesday in Lagos raised the alarm over Nigeria’s nutrition crisis, saying it poses a serious threat to the country’s human capital, as latest data show that 41.1 per cent of children under five are stunted, with the figure rising […]
By Chidinma Chukwu, ABUJA A new report by ThinkBusiness Africa has warned that the proposed increase in Nigeria’s excise duty on sugar-sweetened beverages (SSBs) could significantly raise prices of soft drinks, while its impact on obesity, diabetes and hypertension remains uncertain. The report examined the proposed amendment to the Customs, Excise Tariff, Etc. (Consolidation) Act […]
KILICHOANZA kama mazungumzo yasiyo rasmi kati ya viongozi wa wakulima waliokuwa wamechoshwa na kero za mabroka na mawakala kwenye uuzaji wa avokado Murang’a, sasa kimegeuka kuwa jukwaa linalowapa wakulima haswa wa mashamba madogo afueni kimapato. Wakulima wa matunda hayo ambayo pia yanajulikana kama maparachichi, wanaweza kuwahi soko la nje lenye faida bora. Hii ndiyo hadithi ya Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited, ambayo kulingana na Meneja wake wa Miradi na Uhamasishaji wa Raslimali, John Ruoho Wangechi, chama hicho cha ushirika kilianzishwa kutokana na changamoto zilizokuwa zikikabili wakulima. Kwa miaka mingi, wakulima walipunjwa na madalali, udanganyifu wa mazao shambani na masoko yasiyotabirika. “Mabroka wakija shambani, kando na kupunja mkulima kipesa na kisoko, walikuwa wakipakia avokado kupita kiasi au kiwango wanachokubaliana,” anaelezea. Ruoho anasema wakati wazo la kuunda chama hicho lilipoibuka, maparachichi yakuwa yakiuzwa kwa bei ya Sh2 hadi Sh10 kwa kila tunda, bila kujali ukubwa au ubora. Mfumo huo uliwaacha wakulima bila kujitetea kupata malipo bora. Hata hivyo, kuanzishwa kwa Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited kumeleta mabadiliko makubwa, hasa baada ya kuhamia mfumo wa malipo kwa njia ya kilo badala ya kuhesabu matunda. “Sasa tunatumia mfumo wa kilo. Shamba likisimamiwa vizuri na kutoa mazao bora, mkulima hulipwa vyema na zaidi,” anasema. [caption id="attachment_192191" align="aligncenter" width="300"] Avokado za Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) uliofanyika Nairobi, Juni 8, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Chama hicho cha ushirika na kilichosajiliwa rasmi Januari 2020, kilianza na vyama vidogo vinane lakini sasa vimefika 22, huku vikihudumia takriban wakulima 8,700 wanaoleta mazao bila kukosa. Kina zaidi ya wanachama 15,000 waliosajiliwa na zaidi ya wakulima 50,000 wa avokado, kulingana na rejista. Hutoa huduma za kitaalamu, ikiwemo mafunzo ya usimamizi wa mashamba, kilimo bora na matumizi ya miche iliyoidhinishwa. “Mazao hukusanywa kwa pamoja na kuuzwa kupitia wauzaji na waagizaji wa nje wanaokidhi viwango vya kimataifa kama vile GlobalGAP,” Ruoho akaambia ‘Akilimali’ kwenye mahojiano ya kipekee. Ulaya na Nchi za Milki ya Kiarabu haswa Mashariki ya Kati ndizo masoko makuu ya maparachichi ya Kenya, huku China ikiwa soko lenye uwezo mkubwa lakini lenye masharti makali ya udhibiti. Msimu uliopita, chama kilikusanya karibu kilo 574,000 za avokado. Hata hivyo, kiasi hicho kilikuwa chini ya matarajio kwa sababu ya kuchelewa kwa vibali vya udhibiti na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha matunda kukomaa mapema. Ruoho anasema wakulima kwa sasa hupata kati ya Sh80 na Sh90 kwa kilo katika soko la ndani kwa ndani, huku bei ikibadilika kulingana na mahitaji na ubora. Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited ilikuwa kati ya washirika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) wa mwaka huu, 2026, uliofanyika Nairobi kati ya Juni 8 na 11, ambapo cham hicho cha ushirika kilionyesha bidhaa zake, avokado. Kongamano hillo lilihudhuriwa na viongozi na wadauhusika wa kilimo nchini na pia kutoka sehemu mbalimbali duniani. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mutahi Kagwe alisisitiza umuhimu wa wakulima kujipanga kwenye mashirika ili kubadilisha sekta ya kilimo. “Wakulima wa mashamba madogo ndio uti wa mgongo kuboresha mifumo yetu ya chakula. Wapojipanga, hupata sauti ya majadiliano, kuimarisha sera na kupata heshima katika uzalishaji, kilele chake kikiwa kupata soko bora,” Waziri Kagwe alisema. [caption id="attachment_192192" align="aligncenter" width="300"] John Ruoho Wangechi, Meneja wa Miradi na Uhamasishaji wa Raslimali Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited, aaelezea kuhusu juhudi za chama hicho cha ushirika kusaidia wakulima kupata masoko ya nje ya nchi ya parachichi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) uliofanyika Nairobi, Juni 8, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kaulimbiu ya kongamano hilo lililoandaliwa na Shirikisho la Kitaifa la Wakulima wa Kenya (KENAFF) kwa ushirikiano na Shirika la Wakulima Duniani (WFO), ilikuwa “Future Fields: Investing in Farmers’ Organisations and Empowering Communities for Sustainable Agriculture.” Kilimo cha maparachichi kimekuwa chanzo cha utajiri maeneo ya mashambani, kikisaidia familia kugharamia elimu, kuboresha maisha na uchumi. Hata hivyo, sekta hii inakabiliwa na changamoto za hasara hasa baada ya mavuno, zinazokadiriwa kufikia asilimia 60–65, pamoja na ushindani kutoka kwa wachakataji wa mafuta ya maparachichi. Wasindikaji wa mafuta hulipa wakulima kati ya Sh18–20 kwa kilo, ikilinganishwa na zaidi ya Sh80 kwa kilo katika soko la nje. Ruoho anasema tofauti hiyo ya bei inawashawishi baadhi ya wakulima kuvuna mapema na kuelekeza mazao yao kwenye viwanda vya mafuta, jambo linalopunguza uuzaji wa avokado kwenye masoko ya nje. Kwa upande mwingine, teknolojia imekuwa nguzo muhimu katika shughuli za Murang’a Avocado Farmers’ Co-operative Union Limited, huku malipo yakifanywa kwa njia ya simu, utunzaji wa kumbukumbu kidijitali na majukwaa ya mitandao ya kijamii yakisaidia kuboresha mawasiliano na masoko. Chama hicho cha ushirika kimekuwa kikipigwa jeki na shirika la We Effect, hasa katika uimarishaji wa masuala ya uongozi, uwekezaji wa fedha, kuhamasisha usawa wa kijinsia na matumizi ya teknolojia.
The Nigerian Guild of Editors, NGE, has raised concerns over the increasing harassment, intimidation and prosecution of journalists by security agencies, warning that such actions could undermine press freedom and legitimate journalistic practice. The Guild also called on the Federal Government and the Independent National Electoral Commission, INEC, to ensure a level playing field for […]
Tanesco Director-General Lazaro Twange said construction of the Imalilo substation was 80 percent complete, while the Ibadakuli-Bariadi transmission line was 60 percent complete.
By Henry Umoru ABUJA — The Peter Obi Media Office has raised concerns over the reported endorsement of President Bola Ahmed Tinubu by about 600 university lecturers, alleging that the development could undermine confidence in the 2027 presidential election. In a statement signed on Tuesday by the spokesman of the Peter Obi Media Office, POMR, […]
TANGA: WANAWAKE na watoto katika Kijiji cha Msomera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wameanza kupata fursa mpya za elimu na uwezeshaji wa kijamii, hatua inayolenga kuwasaidia kujenga maisha bora katika mazingira yao mapya. Mabadiliko hayo yanaenda sambamba na jitihada za Shirika lisilo la Kiserikali la Mimute Women Organization, kwa kushirikiana na uongozi wa eneo hilo,…
MWANAMUME anayeshutumiwa kwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu Sh1,860 kutoka kwa mwanamke kwa kisingizio cha kumuuzia jiko la gesi ya LPG kutoka Sun King, alifikishwa katika Mahakama ya Nyamira Jumanne. Geoffrey Bett Kiplangat alishtakiwa kwa kosa la kutapeli lakini alikana mashtaka hayo. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, mnamo Agosti 5 katika eneo dogo la Mau Summit, Kamara Location, Kaunti Ndogo ya Kuresoi Kaskazini, Kaunti ya Nakuru, Kiplangat alijipatia kwa hila Sh1,860 kutoka kwa Hellen Nyamisa Bosire kupitia muamala wa M-Pesa. “Mshtakiwa anadaiwa kumshawishi mlalamishi kutuma pesa hizo katika akaunti mbalimbali za kibinafsi kwa kisingizio cha kununua jiko la gesi ya LPG na kulipia gharama za usafirishaji, jambo ambalo alijua kuwa si la kweli,” mwendesha mashtaka wa kituo cha polisi cha Nyamira, Stephen Masaki, aliiambia mahakama. Bw Masaki aliendelea kueleza mahakama kwamba mshtakiwa amekuwa akitumia majina ya chapa mbalimbali halali kuwalaghai wateja wasio na taarifa za kutosha katika kaunti mbalimbali. Aliiomba mahakama kumzuilia mshukiwa kwa siku saba ili kuruhusu afisa wa probeshoni kuandaa na kuwasilisha ripoti kuhusu historia yake na kufaa kwake kuachiliwa kwa dhamana. “Mheshimiwa, tunaomba mshtakiwa azuiliwe kwa siku saba kusubiri kuwasilishwa kwa ripoti ya probeshoni. Hii itasaidia mahakama kuamua masharti yanayofaa ya dhamana,” Masaki aliwasilisha ombi. Ombi hilo lilikubaliwa. Hakimu aliamuru Kiplangat azuiliwe katika Gereza la Nyamira GK hadi Septemba 23, 2026, kesi hiyo itakapotajwa kwa maelekezo zaidi na kuzingatiwa kwa masharti ya dhamana. Kesi hiyo inajiri wakati ambapo visa vya kujifanya wawakilishi wa chapa mbalimbali vimekuwa vikiongezeka, huku walaghai wakitumia majina ya kampuni zinazotegemewa za nishati ya jua na vifaa vya kielektroniki kuwalaghai wananchi. Akizungumza nje ya mahakama, Bi Lavender Atieno, mchambuzi wa masuala ya ulaghai kutoka Sun King, kampuni inayoongoza katika bidhaa za nishati ya jua ambayo chapa yake ilidaiwa kutumiwa na mshukiwa, aliwaonya wananchi kuwa waangalifu. Alisema chapa yao, pamoja na chapa nyingine nyingi, zimewahi kutumiwa vibaya na walaghai. “Tunawaonya watu wanaowalaghai wateja kwa kutumia majina ya chapa halali kwamba mkono wa sheria utawafikia. Tumeimarisha mifumo yetu ya uthibitishaji. Wateja wanapaswa kufanya malipo kupitia nambari rasmi za Paybill za Sun King pekee,” Atieno alisema. “Usitume pesa kwa nambari za kibinafsi. Ikiwa mtu anadai kuwa anatoka Sun King au kampuni nyingine halali na kukuomba utume pesa kwenye akaunti ya kibinafsi kwa ajili ya jiko la gesi au bidhaa ya nishati ya jua, huyo ni tapeli,” aliongeza. Bi Atieno alisema kampuni hiyo inashirikiana kwa karibu na Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI) pamoja na polisi wa maeneo mbalimbali kuwafuatilia na kuwafikisha mahakamani watu wote wanaojifanya kuwa wafanyakazi wao. Aliwahimiza waathiriwa wa ulaghai wa aina hiyo kuripoti mara moja katika kituo cha polisi kilicho karibu au kupitia njia rasmi za huduma kwa wateja za Sun King ili kupata msaada.
YEMEN: Takribani watu 94,000 wamekimbia makazi yao nchini Yemen tangu mapigano kati ya waasi wa Houthi na vikosi vya Serikali yalipozidi kuwa makali mwezi huu, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM). Maeneo yaliyoathirika zaidi ni majimbo ya Taiz na Lahj, ambako zaidi ya watu 48,000 wamekuwa wakikimbia makazi yao kutokana na mapigano…
KATIBU Mkuu wa Chama cha UDA, Hassan Omar, amejitetea dhidi ya madai kwamba aliwahimiza wafu kumpigia kura Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao, akisema kauli zake zilitafsiriwa vibaya na kutolewa nje ya muktadha wake kisiasa. Akizungumza kuhusu mjadala uliotokea baada ya matamshi yake ya hivi majuzi, Bw Omar alisema wanasiasa hasa wa kutoka pwani, mara nyingi hutumia methali, tamathali za semi na kejeli kuwasilisha ujumbe wao kwa wananchi, na kwamba watu wasiofahamu mtindo wa mawasiliano wa Pwani walikosea kuelewa alichomaanisha. “Tunatumia tamathali za semi, methali na kejeli katika siasa. Ninavyozungumza Nairobi si jinsi ninavyozungumza Mombasa ninakotoka. Watu wasioelewa jinsi tunavyozungumza Mombasa wanapaswa kunyamaza,” alisema. Kiongozi huyo wa UDA alisisitiza kuwa chama chake hakitegemei kura zisizo halali bali kinaamini kitapata ushindi kupitia kura za wananchi wanaojitokeza kupiga kura. “Nina uhakika zaidi ya shaka yoyote kwamba William Ruto atachaguliwa tena. Tunataka kujenga ushindi ambao hauwezi kutikiswa. Hatuhitaji kura za wafu. Tutapigiwa kura na watu walio hai,” alisema. Bw Omar alieleza kuwa matamshi yake yalilenga kuhamasisha wananchi, hasa katika Kaunti ya Mombasa, kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi. Alibainisha kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ulikuwa na idadi ndogo ya wapigakura katika eneo hilo, hali ambayo alisema inahitaji kubadilika ikiwa Rais Ruto atapata ushindi mkubwa. “Mombasa ilikuwa na asilimia 40 pekee ya wapigakura waliojitokeza mwaka 2022. Nilichomaanisha ni kwamba watu wanapaswa kuamka na kujitokeza kuhakikisha tunapatia William Ruto ushindi,” alisema. Kwa mujibu wa Bw Omar, kuunga mkono rais kwa maneno pekee hakutoshi bila wananchi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi. “Kumpenda rais ni jambo moja, lakini kujisajili na kumpigia kura ni jambo jingine. Nilinukuliwa nje ya muktadha,” aliongeza. Aidha, alilaumu baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kupotosha kauli zake kwa maslahi ya kisiasa. “Inasikitisha sana kuona yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii. Wapo waliochukua fursa ya kupotosha maneno yangu ili kutimiza malengo yao ya kisiasa,” alisema. Katibu Mkuu huyo alisema UDA haina hofu ya kushindwa katika uchaguzi ujao, bali ina wasiwasi kuwa wapinzani wanaweza kuibua madai na visingizio mbalimbali wakishindwa. “Sisi hatuogopi kushindwa uchaguzini. Tunachohofia ni kwamba tukishinda, wale watakaoshindwa wataanza kuja na kila aina ya visingizio,” alisema. Kauli za Bw Omar zinajiri wakati shughuli za kisiasa zinaanza kushika kasi kuelekea uchaguzi mkuu ujao, huku vyama vikiongeza juhudi za kuhamasisha wapigakura na kuimarisha misingi yao katika maeneo mbalimbali nchini.
DAR ES SALAAM: MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani, huku ukiitaka Serikali, taasisi za umma, vyama vya siasa, wananchi na wadau wengine wa demokrasia kuanzisha na kuendeleza mazungumzo na maridhiano kwa lengo la kupunguza migawanyiko, kujenga umoja na kurejesha imani ya wananchi…
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta ameondoa wasiwasi kuhusu mchakato wa kukabidhi uongozi wa chama cha Jubilee, akisema yuko tayari kufanya hivyo kwa uwazi, kwa mujibu wa sheria na katiba ya chama. Kauli ya Uhuru ilijiri, siku chache baada ya Mahakama Kuu kusisitiza kwamba marais wastaafu hawapaswi kushikilia nyadhifa za uongozi wa vyama vya kisiasa kwa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka mamlakani. Katika taarifa iliyotolewa Jumanne na Mkuu wa Mawasiliano wa ofisi yake Kanze Dena-Mararo, Bw Kenyatta alisema kuchelewa kwake kuachilia uenyekiti wa Jubilee kulitokana na mzozo wa ndani uliokuwa ukisubiri mwongozo wa kisheria. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sasa hakuna kikwazo kinachozuia mchakato wa kubadilisha uongozi kufuatia ufafanuzi uliotolewa na mahakama. “Rais mstaafu anathibitisha utayarifu wake kamili wa kuona mabadiliko ya uenyekiti yakikamilishwa kwa uwazi, kwa njia halali na kwa mujibu wa katiba ya chama. Anatazamia kuona taratibu za chama zikiendelea bila vikwazo,” ilisema taarifa hiyo. Matamshi hayo yanajiri wakati Mahakama Kuu imesisitiza kuwa kifungu cha sheria kinachomzuia rais mstaafu kushikilia wadhifa wa uongozi katika chama cha kisiasa kwa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka afisini kinaendelea kutumika. Jaji Lawrence Mugambi alitupilia mbali ombi lililokuwa likipinga Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Marupurupu ya Marais Wastaafu, akisema sheria hiyo haimzuii rais mstaafu kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa au kushiriki shughuli za kisiasa. Hata hivyo, mahakama ilisisitiza kuwa kinachokatazwa ni kuendelea kushikilia uongozi katika chama baada ya muda uliowekwa kisheria. “Kinachozuiwa ni kushikilia nafasi ya uongozi katika chama kwa zaidi ya miezi sita baada ya kustaafu,” alisema Jaji Mugambi. Uamuzi huo unaangazia upya mzozo wa uongozi wa Jubilee ulioanza baada ya Bw Kenyatta kuondoka mamlakani mwaka wa 2022 huku akiendelea kuwa kiongozi wa chama hicho. Mwaka wa 2023, kundi moja ndani ya Jubilee lilitangaza nafasi yake kuwa wazi na kumteua Mbunge Maalum Sabina Chege kuwa kiongozi wa muda, likitaja sheria hiyo kama msingi wa hatua yake. Hatua hiyo ilisababisha mvutano mkali kuhusu uongozi wa chama na mamlaka ya kufanya maamuzi muhimu. Baadaye, Bw Kenyatta alirejea rasmi katika uongozi wa Jubilee mnamo Juni 2025 baada ya mahakama kubatilisha mabadiliko yaliyokuwa yamemweka Bi Chege pamoja na washirika wake madarakani. Katika taarifa yake, Bw Kenyatta alisema anakaribisha sura mpya ya Jubilee na kizazi kipya cha viongozi watakaochukua usukani wa chama. “Uhuru Kenyatta anakaribisha sura mpya ya Jubilee iliyojengwa juu ya utawala wa sheria, ikiongozwa na katiba ya chama na kuendelezwa na kizazi kijacho cha viongozi,” ilisema taarifa hiyo.
The Republic has questioned the asset ownership of Chadema Mainland Vice Chairman John Heche, including vehicles, sources of income, and claims that he received money from various individuals.
The Republic has cross-examined Chadema Mainland Vice Chairman John Heche over his claims concerning the abduction of former Kibondo District Council chairman Simon Kanguye in Kigoma Region.
PWANI: SERIKALI ya Wilaya ya Kibiti imeweka mikakati ya kukabiliana na mvua za El Nino, ikiwemo kuwaandalia maeneo ya muda wanafunzi wa shule 12 za msingi ambazo zimekuwa zikikumbwa na mafuriko mara kadhaa. Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, alisema hayo jana wakati akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wilayani humo kuhusu namna…
DAR ES SALAAM: SERIKALI imewataka Watanzania kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku pamoja na vifaa vinavyotumia gesi zinazoharibu Tabaka la Ozoni, ikiwemo majokofu na viyoyozi vilivyotumika, ili kulinda mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni,…
DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ayoub Mohammed Mahmoud, ameongoza kikao kazi cha baraza hilo kujadili hali ya usalama barabarani na mikakati ya kuimarisha usalama kwa watumiaji wa barabara. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam, kimejadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya…
SERBIA: BALOZI wa Tanzania, Jamhuri ya Serbia, Mbarouk Nassor Mbarouk, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Serbia, Aleksandar Vučić, katika Ikulu ya nchi hiyo iliyopo jijini Belgrade. Uwasilishaji wa hati hizo unaashiria kuanza rasmi kwa Balozi Mbarouk kutekeleza majukumu yake ya kidiplomasia nchini Serbia na kuthibitisha dhamira ya Tanzania ya kuimarisha uhusiano wa muda…
By Folarin Kehinde, Abuja ABUJA — The Federal Government has signed a ₦728.979 billion Series 2 bond under its ₦4 trillion Power Sector Debt Reduction Programme to settle verified legacy debts owed to electricity generation companies and improve liquidity in Nigeria’s power sector. The transaction comprises ₦402 billion in cash bonds raised from the domestic […]
DAR ES SALAAM: WHAT if the next chapter of Tanzania’s economic growth is already being written on the Dar es Salaam Stock Exchange? The numbers are increasingly telling that story. By the end of last week, total market capitalisation at the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) had reached 40.6tri/-, marking a historic milestone for…
WASHINGTON, Amerika: RAIS wa Amerika, Donald Trump mnamo Jumapili alipuuza ripoti kwamba Iran ilipata picha za satelaiti za kambi ya kijeshi nchini Jordan kutoka kwa mashirika ya China kabla ya shambulizi la Julai lililoua wanajeshi watatu wa Amerika. Ripoti ya jarida maarufu la Wall Street, likiwanukuu maafisa wa Amerika ambao hawakutajwa majina, ilisema picha hizo zilitolewa kwa Iran kabla ya shambulizi hilo kutekelezwa. Ripoti hiyo haikueleza mashirika ya China yaliyohusika wala kudai kuwa Beijing ilihusika moja kwa moja. Trump alipoulizwa iwapo angezungumzia suala hilo katika mkutano ujao na Rais wa China Xi Jinping, hakujibu moja kwa moja, bali alitumia ujanja kulinganisha shughuli za ujasusi za China na Amerika. “Kimsingi wao wanafanya kile tunachofanya. Wanaposema China inatupeleleza, nasema wako sahihi, na sisi pia tunawapeleleza.” Trump aliwaambia waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya Air Force One. Trump pia alisisitiza kuwa ana uhusiano mzuri na Rais Xi, licha ya mvutano wa muda mrefu kati ya Washington na Beijing ambao unaoenekana kuwa ubabe wa kijeshi na kiuchumi. “Nadhani amekuwa akifanya kila kitu kwa njia inayokubalika, nasi tunafanya kwa njia inayokubalika,” akasema Trump alipokuwa akirejea Amerika baada ya ziara Ireland. Trump na Xi wanatarajiwa kukutana Amerika mnamo Septemba 24, ingawa China bado haijathibitisha rasmi mkutano huo. China mnamo Jumatatu ilisema imekuwa ikitimiza wajibu wake wa kimataifa kikamilifu na tena kwa udhabiti ikionekana kujibu madai kuwa inasaidia Iran kwenye vita dhidi ya Amerika. Msemaji wa Wizara ya Masuala ya Nje Guo Jiakun alisema Beijing inapinga na itaendelea kupinga madai yoyote yasiyo na msingi dhidi yake. “Tunapinga vikali tuhuma na madai yasiyo na msingi yanayotolewa bila ushahidi,” Guo alisema katika mkutano na waandishi wa habari. Kauli za Trump zinaonekana kuoana na juhudi za hivi karibuni za utawala wake kupunguza mvutano kati ya Washington na Beijing. Hii ni licha ya kwamba Amerika haijaridhishwa na uhusiano wa karibu kati ya China na Iran. Zaidi ya wanajeshi 18 wa Amerika wameuawa tangu vita kati ya Amerika-Israel dhidi ya Iran vilipoanza mnamo Februari 28.
MWANZA; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeonya wananchi kuhusu matumizi ya vipodozi visivyo salama, likisema bidhaa hizo zinaweza kusababisha madhara makubwa kiafya, ikiwemo magonjwa sugu kama saratani. Onyo hilo limetolewa na Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria wa TBS, Nuru Mwasulama, ambaye amesema shirika hilo linaendelea kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa vipodozi…
By Folarin Kehinde, Abuja The Federal Government (FG) has signed the N728.979 billion Series-2 bond under its N4 trillion Power Sector Debt Reduction Programme, in a fresh move to settle verified legacy debts owed to electricity generation companies and restore liquidity to Nigeria’s power sector. The transaction comprises N402 billion in cash bonds raised from […]
VIONGOZI wa ODM ambao wamekuwa na msimamo vuguvugu katika kuunga mkono azma ya Rais William Ruto kuwania muhula wa pili wameanza kuhisi joto kutoka kwa wapigakura wa Nyanza, wanaowataka wachukue msimamo wa wazi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Mbunge wa Suba Kaskazini, Millie Odhiambo, alizomewa Jumapili jijini Kisumu, hali iliyoonyesha kutoridhika kwa baadhi ya wapigakura na viongozi wanaoonekana kuegemea upande wa upinzani na wakati huo huo kushirikiana na Serikali Jumuishi. Bi Odhiambo, ambaye anahudumu muhula wake wa nne na pia ni Kiranja wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, alikumbana na wakati mgumu alipokuwa akihutubia wakazi wa Kisumu katika mkutano wa Rais Ruto na viongozi wa Nyanza. Baadhi ya wakazi walimpigia kelele wakisema, “Ondoka, toka hapa,” huku wengine wakimwambia, “Wewe kaa tu kwenye fensi.” “Wale wanaomuunga mkono Ruto inueni mikono. Kitu kizuri kinaporudiwa huwa kizuri zaidi. Mimi Amillo gesa gesa, mnanipigia kelele. Nilizaliwa nikiwa mkaidi na ninamuunga mkono Ruto jinsi ninavyotaka. Na ninawaambia sijali,” akasema Bi Odhiambo. Baadaye mbunge huyo aliandika kwenye mitandao ya kijamii akisema alifedheheshwa na kuzomewa huko Kisumu. “Leo nilizomewa sana Kisumu. Tangu wakati huo, niko kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, nimekufa. Ninasubiri yanayofuata. Hata hivyo, nilikuwa mjanja sana. Kubali tu ulale,” akaandika. Mbali na Bi Odhiambo, viongozi wengine ambao hawajakuwa na msimamo ni Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo, Mbunge wa EALA Winnie Odinga, Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ na Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kisumu Ruth Odinga. Mabw Kajwang’ na Amollo walihudhuria mkutano huo na kuunga mkono azma ya Rais Ruto ya muhula wa pili. “Kama Mzee Oburu angekuwa hapa angesema tunataka mamlaka kwa sababu hatuwezi kuwa bila mamlaka. Rais, tunataka kukuunga mkono kwa yale ambayo umefanyia eneo letu, unayofanya na unayonuia kufanya kwa eneo letu. Tutakuunga mkono bila masharti kwa maendeleo ambayo umetuletea,” akasema Bw Kajwang’. Wiki mbili zilizopita, Bw Kajwang’ pia alimuunga mkono mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kuwania ugavana wa Nairobi. Kwa upande wake, Bw Amollo alisema anaunga mkono Rais Ruto bila masharti kutokana na heshima yake kwa marehemu Raila Odinga, miradi ya maendeleo inayoendelea na upanuzi wa reli ya kisasa ya SGR hadi Kisumu. Hapo awali, Bw Amollo alilazimika kutetea msimamo wake wa kutoonekana kuunga mkono serikali, akisema bado ni mwanachama mwaminifu wa ODM. Bi Winnie Odinga amekuwa kimya na hajaonekana katika baadhi ya mikutano muhimu ya kisiasa ya ODM. Bi Ruth Odinga hakuhudhuria mkutano wa Kisumu kwa kuwa ameandamana na Dkt Oburu Oginga nchini Uingereza kwa uchunguzi wa kawaida wa afya. Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi ni miongoni mwa viongozi wachache wa ODM wanaopinga waziwazi azma ya Rais Ruto ya kuwania muhula wa pili. Kura ya maoni ya TIFA iliyotolewa Julai 26 ilionyesha Rais Ruto akiwa mgombea maarufu zaidi Nyanza kwa asilimia 30. Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Javas Bigambo alisema viongozi wanaokwepa kuchukua msimamo wanaweza kukumbana na shinikizo kubwa kutoka kwa wapigakura. “Kilichompata Millie kinaonyesha kuwa wale wanaokaa kwenye uzio wameketi juu ya bomu linalosubiri kulipuka na wapigakura hawaridhishwi nao. Wapigakura wanataka wapiganaji na huwezi kosa kuwa upande wowote wakati wa vita,” alisema Bw Bigambo. “Hata mgombea huru anaweza kumshinda anayekaa kwenye uzio kwa sababu ana msimamo. Kwa Millie, baadhi ya kauli ambazo amekuwa akitoa zimefasiriwa kuwa zinaunga mkono kundi la Linda Mwananchi,” akaongeza.
FAMILIA mbili katika Kaunti ya Embu zinaandaa mazishi ya wana wao wawili waliopigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya vijana na polisi katika mkutano wa kisiasa uliohudhuriwa na Naibu Rais Kithure Kindiki Jumamosi iliyopita. Mike Macharia, 23, alikuwa ameenda kucheza kandanda katika Shule ya Msingi ya Nembure, huku Moses Munene, 30, akiwa njiani kuenda kazini mjini Embu. Wote walikumbana na ghasia zilizoibuka nje ya Uwanja wa Nembure. Familia zao zinasema vijana hao hawakuwa sehemu ya makabiliano hayo na sasa zinataka maelezo kuhusu jinsi walivyopoteza maisha. Mama ya Macharia, Charity Wanja, alisema mwanawe alikuwa mtoto wake wa pekee na alikuwa amejitahidi kumlipia masomo ili apate maisha bora. Alisema Macharia alikimbia baada ya makabiliano kati ya vijana na polisi wa kutuliza ghasia kuzuka, lakini alipigwa risasi kwenye nyonga. Wasamaria wema walimkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Embu, ambako alifariki alipowasili. “Mwanangu hakuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wakipigana na polisi na alipaswa kuachwa. Maafisa waliomuua wanapaswa kufichuliwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,” akasema Bi Wanja. Alisema anatoka katika familia maskini na alifanya kazi kwa bidii kuhakikisha mwanawe anapata elimu. “Nilikuwa nikifanya kazi kwa bidii kumsomesha mwanangu ili asiteseke kama nilivyoteseka. Kwa bahati mbaya, mwanangu aliuawa kabla hajamaliza masomo yake,” akaongeza. Katika kijiji cha Gichugu, mama mwengine, Cecilia Wambeti, 58, alikuwa akiomboleza kifo cha mwanawe Munene, ambaye hufanya kazi kwenye karakana. Bi Wambeti alisema mwanawe alikuwa ameondoka nyumbani saa moja asubuhi kuelekea kazini mjini Embu akiwa kwenye pikipiki. Alikutana na vijana waliokuwa wakikimbia polisi na akaacha pikipiki yake kabla ya kuanza kukimbia. Alipigwa risasi nyuma ya kichwa na kufariki papo hapo. “Alipigwa risasi mgongoni na akapoteza maisha,” akasema. Bi Wambeti alisema alijulishwa kuhusu kifo hicho akiwa nyumbani na baadaye akafika katika Hospitali ya Rufaa ya Embu, ambako aliambiwa aende katika chumba cha kuhifadhi maiti. Familia hiyo pia haijapata pikipiki ya Munene tangu tukio hilo. “Tulienda eneo la tukio lakini hatukupata pikipiki. Polisi watuambie iko wapi,” akasema. Alimtaja mwanawe kuwa mtu mwenye bidii na mkarimu aliyekuwa akimsaidia kifedha. “Mwanangu alikuwa mchangamfu na mkarimu. Nilipohitaji pesa za chakula na mahitaji mengine, alikuwa akinisaidia. Nimepoteza mtoto mzuri,” akasema. Wambeti alishangaa kwa nini mwanawe alipigwa risasi ilhali, kwa mujibu wake, hakuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wakikabiliana na polisi. Ghasia hizo zilizuka wakati Prof Kindiki alipokuwa akihutubia maafisa wa UDA katika Uwanja wa Nembure, Manyatta. Vijana waliokuwa nje ya uwanja walipiga kelele na kurusha mawe, hali iliyosababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati. Makabiliano hayo yalidumu kwa saa kadhaa na magari sita yakachomwa moto.
MWANZA: The Chairperson of the Parliamentary Standing Committee on Energy and Minerals, Subira Mgalu, has affirmed that one of the Committee’s key priorities is to ensure the successful establishment of the Tanzania Geoscientists’ Registration Board. Ms Mgalu made these remarks on September 14, 2026, in Mwanza while opening the Tanzania Geologists’ Annual Meeting, which she…
MAHAKAMA Kuu imesisitiza kuwa sheria inayomzuia Rais mstaafu kushikilia wadhifa wa uongozi katika chama cha kisiasa kwa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka mamlakani ipo na utekelezaji wake unastahili kuzingatiwa. Uamuzi huo unaweza kuathiri nafasi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kuendelea kuwa Kiongozi wa Jubilee na muungano wa Azimio. Jaji Lawrence Mugambi alitupilia mbali ombi lililopinga Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Marupurupu ya Marais Wastaafu, akisema sheria hiyo haimzuii rais mstaafu kuwa mwanachama wa chama au kushiriki shughuli za kisiasa. Hata hivyo, inamzuia kushikilia nafasi ya uongozi wa chama kwa zaidi ya miezi sita baada ya kustaafu. “Kinachozuiwa ni kushikilia nafasi ya uongozi katika chama hicho kwa zaidi ya miezi sita baada ya kustaafu,” akasema Jaji. Uamuzi huo unaangazia upya mzozo wa uongozi wa Jubilee ambao uliibuka baada ya Bw Kenyatta kustaafu Septemba 2022. Bw Kenyatta amekuwa kiongozi wa Jubilee tangu chama hicho kilipoanzishwa mnamo 2017 na aliendelea kushikilia nafasi hiyo baada ya kuondoka ikulu. Mnamo 2023, kundi la wanachama wa Jubilee lilitangaza nafasi yake kuwa wazi na kumteua Mbunge Maalum Sabina Chege kuwa kiongozi wa muda, likitaja sheria hiyo. Hatua hiyo ilisababisha mzozo kuhusu nani alikuwa na mamlaka ya kuitisha mikutano ya chama, kuwaondoa maafisa na kuwasiliana na Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Bw Kenyatta na washirika wake walipinga mabadiliko hayo, wakisema yalikiuka katiba ya chama. Hata hivyo, Msajili alimtambua Bi Chege kama kiongozi na Mbunge wa EALA Kanini Kega kama katibu mkuu. Bw Kenyatta alirejea uongozi wa Jubilee Juni 2025 baada ya Mahakama kubatilisha uamuzi uliomweka Bi Chege na kundi lake mamlakani. Wakati huo huo, Bw Kenyatta pia ni mwenyekiti wa Baraza la Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, jambo ambalo limekuwa likizua malalamishi kutoka kwa washirika wa Rais William Ruto wanaomshutumu kwa kuendelea kujihusisha kikamilifu na siasa. Kesi iliyosababisha uamuzi wa sasa iliwasilishwa Mei 2023 na wanaharakati Peter Odhiambo Agoro, Paul Muiruri Kiguathi na Damon Onyango Osawa. Walidai sheria hiyo inawabagua marais wastaafu na kukiuka haki za usawa, uhuru wa kujumuika na kushiriki siasa. Mahakama, hata hivyo, ilisema haki hizo si kamili na zinaweza kuwekewa mipaka chini ya Katiba iwapo vizuizi hivyo ni vya busara na vinavyoweza kuhalalishwa katika jamii ya kidemokrasia. Jaji Mugambi alisema rais mstaafu ana nafasi ya kipekee kutokana na mamlaka na ushawishi aliokuwa nao alipokuwa madarakani. Mahakama pia ilisema sheria hiyo iliyopitishwa 2003 ililenga kuzuia marais wastaafu kuendelea kudhibiti siasa kupitia washirika wao baada ya kuondoka mamlakani.
MWANZA: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu amesema kuwa miongoni mwa masuala ambayo Kamati hiyo itahakikisha inatekeleza ni pamoja na kufanikisha kuanzishwa kwa Bodi ya Usajili wa Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geoscientists’ Registration Board). Mgalu ameyasema hayo Jumatatu, Septemba 14, 2026, jijini Mwanza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa…
RAIS William Ruto anakabiliwa na kitendawili cha kuvutia uungwaji wa wapigakura wa Luo Nyanza, ikisalia miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu 2027. Kilichosawiriwa kama ishara ya umoja kabla ya ziara ya siku nne ya Rais Ruto eneo la Nyanza, kiligeuka upesi pale ushindani ulipochipuka pamoja na orodha ya matakwa kutoka kwa uongozi wa ODM. Ujumbe kutoka kwa viongozi waliochaguliwa mashinani ulikuwa rahisi: wako tayari kumuunga kinara huyo wa Kenya Kwanza kuwania awamu ya pili naye awape maendeleo na nyadhifa za kisiasa. Hata hivyo, ndani ya vifijo na nderemo, uhalisia mgumu unakabili eneo hilo ambalo bado linasaka mwelekeo wake kisiasa mwaka mmoja baada ya kifo cha Raila Odinga. Matakwa ya viongozi yalijumuisha kuanzia mgao wa nusu kwa nusu (50-50) wa serikali hadi wadhifa wa naibu rais 2027, huku wengine wakisisitiza kuwa Nyanza isalie ngome ya ODM na kumwonya Ruto dhidi ya kuingilia makabiliano ya kisiasa eneo hilo. Mkutano wa viongozi wa mashinani Jumapili ulifichua jinsi Rais anavyojaribu kujitosa kwenye siasa za Nyanza baada ya Raila, huku viongozi eneo hilo wakijitahidi kubuni masharti yao binafsi kwa ushirikiano kisiasa. Ingawa kulikuwa na muafaka wa jumla kuhusu kuunga mkono Rais Ruto kuchaguliwa tena, masharti yanayohusiana na uungwaji mkono huo yalitofautiana pakubwa na kufichua mianya katika eneo ambalo mpangilio wake kisiasa umetikiswa na kifo cha Odinga. Dan Nyibule, akizungumza kwa niaba ya vijana alitumia hotuba yake kushinikiza matakwa ya kwanza kisiasa kwamba ni sharti Nyanza izingatiwe kwa wadhifa wa naibu rais katika serikali ijayo. “Eneo letu limetembea nawe katika safari hii na hivyo basi tunaamini tunastahili wadhifa wa Naibu Rais katika serikali ijayo. Ikiwa kuna mtu unafaa kuwazia kuhusu nafasi hii ni Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi,” alisema Nyibole. Mwakilishi wa wanawake aliyezungumza katika kikao na Rais alitofautiana na kauli hiyo akihoji kuwa wanawake ni wengi na kwa hivyo wanafaa kuzingatiwa kwa wadhifa wa mgombea mwenza 2027. Mdahalo huo ulitokota zaidi Waziri wa Fedha John Mbadi alipojitokeza kama mgombea wa ngazi za juu akitaja tajriba yake serikalini, bunge, upinzani na ODM. Bw Mbadi vilevile alionekana kutangaza mapema azma ya kugombea 2032.
CHAMA cha ODM na familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, wako katika mzozo mkali kuhusu mipango ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake. Taifa litaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila mnamo Oktoba 15. Raila alifariki siku hiyo baada ya kupata mshtuko wa moyo mjini Kochi, India. Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, familia hiyo ilisema kumbukumbu hiyo si ya mtu binafsi wala taasisi yoyote, siku chache tu baada ya ODM kutangaza mipango ya misururu ya mikutano kote nchini kwa ajili ya kumuenzi mwanzilishi wake. Taarifa hiyo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na binti wa Raila, Winnie Odinga, na dada yake Ruth Odinga, ambaye pia ni Mwakilishi wa Kike wa Kisumu. Lakini Raila Junior, mwanawe Raila ambaye baada ya kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Kibra amekuwa akiandamana na viongozi wa ODM katika mikutano ya kisiasa, hakusambaza taarifa hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii. Raila Junior pia ameandamana na viongozi hao katika ziara ya siku tatu ya Rais William Ruto eneo la Nyanza. Aidha, mama yake, Ida Odinga, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Kenya na Mwakilishi wa Kudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) baada ya kuteuliwa na Rais Ruto mapema mwaka huu, hakusambaza taarifa hiyo. Hata hivyo, jana jioni Winnie alikanusha kuwa kuna uhasama kati ya chama na familia kuhusu maadhimisho hayo. Aliambia Taifa Leo kuwa kumteua Prof Adams Oloo kusimamia maandalizi ya ukumbusho huo ni njia ya kuhakikisha kwamba hakuna anayefungiwa nje kushiriki maadhimisho ya Raila. “Sidhani kama kuna mzozo. Hakuwezi kuwa na mzozo kuhusu maadhimisho,” akasema. Alisema wazo la kuwa na hafla inayoshirikisha wote itawaleta wandani na waliokuwa wapinzani wa marehemu Raila pamoja. “Hatutaki iwe siku ambayo watu wanazuiwa kwa sababu watu hawakupata muda wa kumwomboleza,” akaongeza. Winnie na Ruth wamekuwa wakikosoa namna ODM inavyoendeshwa baada ya kifo cha Raila. Katika baadhi ya matukio, wawili hao wamewashutumu hadharani baadhi ya viongozi wa chama hicho wakidai wanalemaza umaarufu wake. Taifa Leo ilipowasiliana na Ruth, ambaye kwa sasa yuko London pamoja na kaka yake aliye pia kiongozi wa ODM, Oburu Oginga, ili kujua iwapo familia hiyo ina tatizo kuhusu ratiba na mpango uliotangazwa na ODM, alikataa kutoa maoni. Badala yake, alimwelekeza mwandishi kwa Winnie, ambaye hakujibu maswali yaliyotumwa kwake. Awali, Ruth aliwataja baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao hakuwataja majina, kuwa wanalenga kutumia maadhimisho hayo kujinufaisha kisiasa. “Tunaelekea Oktoba 15 na tayari watu wa vikombe na mahema ya ODM wanapanga mambo yao. Raila alikuwa mtu wa kipekee! Acheni upuuzi!” akasema Ruth. Katika taarifa yao, familia ilisema imemteua Prof Adams Oloo kuongoza kamati itakayoratibu shughuli za kumuenzi Raila mwezi ujao. “Kwa hivyo, tunataka kumbukumbu hii ya kwanza iwe wakati wa wananchi kuwa na Baba yao, kumkumbuka, kumuomboleza, kusherehekea maisha yake na kuheshimu safari waliyoshiriki pamoja naye,” ikasema taarifa ya familia. “Kamati hii kwa sasa inaandaa mpango ambao familia itautangaza kwa wakati unaofaa. Yeyote anayetaka kushiriki, kusaidia au kuandaa shughuli yoyote kama sehemu ya kumbukumbu hiyo anaombwa kufanya hivyo kupitia kamati,” ikaeleza. ODM, wiki iliyopita ilitangaza misiruru ya mikutano ya kisiasa ya kumuenzi marehemu Raila ikilenga kuitumia kuvumisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Kwa mujibu wa chama hicho, mikutano hiyo itafanyika Siaya, Kakamega, Garissa, Mombasa, Kajiado, Turkana na hatimaye Nairobi. Maeneo hayo yalikuwa ngome za kisiasa za Raila. “Kuanzia Bondo hadi Garissa, kutoka Kakamega hadi Nairobi na kila sehemu nchini Kenya, tutamheshimu mtu aliyetufundisha kwamba mamlaka ni ya wananchi,” akasema Mwenyekiti wa kitaifa wa ODM na Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga. Mnamo Oktoba 9, wafuasi wa ODM kutoka Kakamega, Vihiga, Busia, Bungoma na Trans Nzoia watakutana Kakamega mjini kwa mkutano mkubwa wa kumuenzi Bw Odinga. Hii itafuatwa na shughuli zinazoongozwa na familia katika Kang’o Ka Jaramogi, Bondo, kuanzia Oktoba 10 hadi 15. Chama hicho kitafanya mkutano mwingine wa kumbukumbu Garissa Oktoba 17, huku viongozi wa ODM, wanachama na wafuasi kutoka Garissa, Wajir, Mandera, Isiolo na Marsabit wakitarajiwa kuhudhuria.
The Federal Government has raised about N1.23 trillion through two bond issuances to tackle N4 trillion legacy debt owed to electricity Generation Companies (GenCos).
By Udeme Akpan Syria’s latest fuel crisis has highlighted the vulnerability of countries that depend heavily on imported crude, refined products or foreign energy supplies, with implications for Nigeria and other developing economies.Syria raised diesel prices by 40% and gasoline prices by up to 28% following rising global procurement costs and disruptions to its domestic […]
HUKU kiangazi na ukame ukiendelea kuathiri wakulima hasa maeneo kame na nusu-kame (ASAL), teknolojia ya uongezaji malisho thamani kurefusha muda imegeuka kuwa tegemeo kwa wafugaji. Wafugaji wanaokabiliwa na uhaba wa chakula cha mifugo wakati wa kiangazi sasa wanaweza kutumia lishe yenye virutubisho anuwai ya Sh300 pekee iliyovumbuliwa na kutengenezwa na Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo (KALRO) ili kusaidia mifugo. Lishe hiyo iliyoundwa na tawi la KALRO, Muguga, Kiambu imesheheni molasi na urea. Molasi hutoa nishati, huku urea ikisambaza nitrojeni inayohitajika kwa mifugo. Eric Too, mtafiti kutoka KALRO, anasema teknolojia hiyo inalenga kusaidia wafugaji hasa wakati wa ukame na kiangazi kirefu ambapo upatikanaji wa chakula cha mifugo huwa changamoto. Too anasema chakula hicho maalum ni muhimu hasa katika maeneo yanayokabiliwa na ukame na uhaba wa malisho. [caption id="attachment_192112" align="aligncenter" width="300"] Eric Too, mtaalamu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Kilimo Kenya (KALRO), aelezea kuhusu chakula maalum cha mifugo kilichotengenezwa na shirika hilo la utafiti, wakati wa Mkutano wa Afrika wa Chakula cha Mifugo na Virutubisho vya Chakula cha Mifugo (AFEC) 2026 katika Hoteli ya Safari Park, Nairobi mnamo Julai 15, 2026. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Watengenezaji wa Chakula cha Mifugo nchini Kenya (AKEFEMA). PICHA|SAMMY WAWERU[/caption] “Tumetengeneza bidhaa hii kusaidia wafugaji, hasa wakati wa kiangazi ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa chakula cha mifugo,” anasema. Lishe hiyo yenye uzani wa kilo mbili, anahoji haina tofauti na chakula cha kawaida cha mifugo ikizingatiwa kuwa malighafi yaliyotumika ni yaleyale ya kawaida ila tu imeboreshwa. Wafugaji wanashauriwa kuendelea kuwapa ng’ombe, mbuzi na kondoo chakula bora kama vile lucerne, Boma Rhodes na super Napier kabla ya kuwapa chakula hicho. Lishe hiyo maalum ilikuwa kati ya teknolojia na chakula kilichovutia wafugaji wakati wa Maonyesho na Kongamano la Chakula cha Mifugo Afrika (AFEC) 2026 yaliyofanyika Nairobi kati Julai 15 na 16. Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Watengenezaji na Wauzaji wa Chakula cha Mifugo Kenya (AKEFEMA), na kuleta pamoja kampuni na taasisi 200 kutoka nchi 27 ulimwenguni. Too, kwenye mahojiano na ‘Akilimali’ alisema chakula hicho maalum husaidia mifugo kuboreshe mmeng’enyo. “Ni bora zaidi kupewa mifugo saa za jioni, wakati mnyama amepumzika ili kusaidia mmeng’enyo na matumizi bora ya chakula alichokula wakati wa mchana,” akashauri. Alidokeza kwamba utafiti umebaini kupungua kwa kiwango cha kinyesi baada ya mifugo kutumia lishe hiyo yenye virutubisho tele, hasa baada ya muda wa wiki moja hadi mbili. “Hali hii inaweza kuwa na manufaa kwa mazingira kwa sababu matumizi bora ya chakula yanaweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane,” Too anafafanua. [caption id="attachment_192113" align="aligncenter" width="300"] Eric Too kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Kilimo Kenya (KALRO) akipanga chakula maalum cha mifugo kilichotengenezwa na shirika hilo la utafiti, wakati wa Mkutano wa Afrika wa Chakula cha Mifugo na Virutubisho vya Chakula cha Mifugo (AFEC) 2026 ulioandaliwa na Chama cha Watengenezaji wa Chakula cha Mifugo nchini Kenya (AKEFEMA) katika Hoteli ya Safari Park, Nairobi, Julai 15, 2026. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption] Mifugo, hasa ng’ombe, wanahusishwa na uzalishaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani. KALRO inaendelea kuboresha teknolojia hiyo kama mojawapo ya njia zinazoweza kusaidia wafugaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huku wakiboresha lishe ya mifugo. Hata hivyo, Too anasema utafiti zaidi na ukusanyaji wa data unahitajika kubaini kiwango kamili cha kupungua kwa gesi ya methane, kwani athari zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya mnyama anayelishwa chakula hicho maalum. Lishe hiyo imekuwa ikitafitiwa kwa zaidi ya miaka mitano na hutengenezwa katika tawi la KALRO, Muguga. Kifungu kimoja cha chakula hicho chenye uzani wa kilo mbili kinauzwa Sh300, na kinaweza kutosha ng’ombe mmoja kwa muda wa takriban wiki mbili.
WATU wawili walifariki baada ya ukuta kuangukia nyumba katika eneo la Jomvu, Kaunti ya Mombasa, usiku wa kuamkia Jumatatu. Bi Clemence Saru, aliyepoteza mume na mtoto wake katika kisa hicho, alieleza kwamba alikuwa katika kanisa la Anointed Rock Ministry kwa maombi wakati aliposikia kishindo kikubwa. Alitoka kanisani ili kujua kilichokuwa kimetokea kisha akasikia kilio cha mumewe na watoto wao wakimwomba msaada. Dakika chache baadaye, vilio hivyo vilikoma, hali iliyothibitisha hofu yake kubwa zaidi. Ukuta wa uzio wa kampuni ya Cevas Logistics uliangukia nyumba yake katika kijiji cha Cambodia, Jomvu, na kumuua mumewe pamoja na mwanao walipokuwa wamelala majira ya saa tano na dakika 20 usiku. Mtoto wao mwingine alinusurika lakini alijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mikindani Medical na majirani. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa Stella Cherono, alithibitisha kisa hicho. Janga hilo limeibua upya wasiwasi miongoni mwa wakazi wanaoishi karibu na kituo cha kuhifadhi na kusafirisha makontena (CFS), ambao wanasema sehemu za ukuta wake wa uzio zimeanguka mara kadhaa hapo awali. Wakazi walisema mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la Pwani wiki iliyopita huenda ilidhoofisha zaidi ukuta huo. Bw Peter Ulinda, mkazi, alisema alikuwa amelala aliposikia kishindo. “Nilitoka mbio na kumwona jirani yangu akilia akiomba msaada baada ya ukuta kuangukia nyumba yake. Mama alikuwa kanisani akiomba wakati ukuta ulipoanguka juu ya nyumba yake, na kumuua mumewe pamoja na mtoto mmoja. Inasikitisha sana,” alisema Bw Ulinda. Alisema majirani walikimbilia kuwaokoa waathiriwa na kuwapeleka hospitalini, lakini wawili walikuwa tayari wamefariki. “Polisi walifika saa tatu baadaye baada ya sisi kufanya kila kitu,” alisema. Bw Ulinda alisema wakazi walikuwa wameibua wasiwasi kuhusu ukuta huo. “Hii ni mara ya nne kwa ukuta huu kuanguka na hatujawahi kufidiwa licha ya watu wetu kujeruhiwa. Tuna ushahidi. Katika tukio la mwisho, jirani yetu alijeruhiwa na hadi leo hajawahi kuwa kama alivyokuwa awali,” alisema. Bw Ulinda pia aliachwa bila makao baada ya ukuta huo kuharibu nyumba yake. Mkazi mwingine, Bi Chenda Baya, alisema mwanawe alijeruhiwa wakati ukuta huo ulipoanguka mwaka jana lakini familia hiyo haikuwahi kufidiwa. Wasiwasi wa wakazi hao umejitokeza wakati nchi ikijiandaa kukabiliana na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño, hali inayozua hofu kuhusu usalama wa majengo katika maeneo ambayo tayari yanachukuliwa kuwa hatarini kukumbwa na mafuriko na hatari nyingine zinazohusiana na hali ya hewa. Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na Bw Beuta Mogaka waliitaka Serikali ya Kaunti ya Mombasa kukagua majengo na kuta katika kaunti nzima ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya usalama. Bw Mogaka alisema mazingira yaliyopelekea ukuta huo kuanguka yanapaswa kuchunguzwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya waliohusika iwapo itabainika kuwa kulikuwa na makosa. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Bw Mathias Shipeta pia alitaka uwajibikaji, akihoji iwapo kanuni za ujenzi zilifuatwa. Mzee wa kijiji, Bi Sally Wawuda, aliwataka wakazi wanaoishi karibu na kituo hicho cha mizigo kuzingatia kuhama eneo hilo kutokana na kile alichokielezea kuwa ni hatari inayokaribia. Kanisa la Anointed Rock Ministry lililokuwa karibu, pia liliathiriwa ambapo sehemu ya ukuta wa kanisa iliharibiwa.
Chadema Mainland Vice Chairman John Heche has recalled in court the alleged abduction of former Tanzanian Ambassador to Malawi and later Cuba, Mr Humphrey Polepole.
GHASIA ambazo zilishuhudiwa katika mkutano wa Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki katika Kaunti ya Embu zinaonyesha kuwa kiongozi yeyote awe serikalini au upinzani anaweza kuathiriwa na tabia hii mbovu ambapo mara nyingi vijana hutumiwa. Kuna huu mtindo ambao umekuwa ukishuhudiwa ambapo baadhi ya wafuasi wa mirengo mbalimbali hufurahishwa uhuni unapokabili upande wasiounga kisiasa. Wakati ambapo viongozi wa Linda Mwananchi walivamiwa Homa Bay mwezi uliopita, baadhi ya wafuasi wa Serikali Jumuishi walisherehekea na hata kuwarejelea baadhi ya viongozi ambao walitajwa kuhusika. Kiongozi mmoja hata alirejelewa kama Ayatollah, jina la kiongozi wa kiimani wa Iran, linalotumiwa kuashiria utawala wa kiimla. Hii ni kutokana na upangaji wa ghasia zilizozuka Homa Bay ambazo kiongozi huyo anahusishwa nazo. Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen naye alizua kejeli kwa kushangaa kwa nini viongozi wa Linda Mwananchi walikuwa wakienda mahali ambapo walikuwa tayari wameambiwa kuna wahuni au megenge ya kisiasa. Yaliyomkumba Prof Kindiki katika Kaunti ya Embu yanastahili kukemewa kwa kinywa kipana na walioratibu au kuwatumia vijana wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Inasikitisha kuwa mtu mmoja aliaga dunia, wengine kujeruhiwa na hata magari kuteketezwa yakiwemo magari mawili ya wanahabari. Kama mkutano wa mtu wa hadhi ya naibu rais unaweza kutibuliwa, sasa itakuwaje kwa mwaniaji wa kawaida ama kiongozi wa ngazi ya chini? Hili jinamizi la uhuni halina mipaka na linaweza kuathiri kiongozi yeyote wala halifai kushabikiwa na upande mmoja linapokabili upande mwingine. Jinsi viongozi wa Linda Mwananchi walivyohisi uchungu Homa Bay huku majeruhi na kifo kikiripotiwa ndivyo pia upande wa Prof Kindiki ulihisi uchungu na kuumia baada ya mkutano wao kuingiliwa. Ingawa hivyo, tatizo katika suala hili lote ni wanasiasa na vijana na iwapo watajirekebisha na kuthamini demokrasia basi hivi visa vya ghasia havingekuwa vikiripotiwa. Kupiga kura ni haki ya kila Mkenya na ni Mkenya huyo atakayeamua jinsi atakavyotekeleza wajibu huo iwe kiongozi ameandaa mkutano eneo lake au la. Iwapo unahisi kwamba unaona humhitaji kiongozi, basi hakuna haja ya kuenda kwa mkutano wa mwanasiasa huyo na kuuvuruga. Kufanya hivyo ndiko huzua makabiliano na maafisa wa usalama ambao vifo huishia kuripotiwa pamoja na majeraha. Ndiyo, jinsi hali ilivyo vijana wengi hawana ajira ila kuhatarisha maisha kwa sababu ya mwanasiasa kisha ujeruhiwe au kuuawa si suluhu kwa tatizo hili ambalo limekuwepo miaka nenda miaka rudi. Kinachoudhi ni kwamba viongozi huwapa vijana kati ya Sh500 na Sh2,000 ili kuenda kuzua ghasia kwenye mkutano wa kiongozi pinzani ilhali fedha hizo ni ndogo na hata haziwezi kuyabadilisha maisha yao. Nguvu na haki ya kuwachagua viongozi iko katika kupiga kura wala si vurugu za kuzuia upande mmoja kuandaa mkutano wa kisiasa. Mikutano ya Linda Mwananchi Nairobi na Rais William Ruto iliyofanyika jijini Kisumu kwa amani inastahili kutumiwa kama mfano kwa wanasiasa. Viongozi wa Linda Mwananchi walihutubia mikutano mingi jijini na wakaenda zao naye Rais Ruto bado anaendelea na ziara yake Nyanza. Ushindani wa kisiasa si uadui na kila mwanasiasa anastahili kuruhusiwa auze sera yake kisha wananchi waachwe waamue.
By Johnbosco Agbakwuru ABUJA — THE Nigeria Union of Pensioners, (NUP) has praised President Bola Tinubu for initiating the payment of N18 billion in outstanding severance benefits to 2,700 former employees of the defunct Nigeria Airways. The union described the intervention as a long-awaited relief for the beneficiaries, who had waited for more than two […]
ZANZIBAR: President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr Hussein Mwinyi, has urged the joint committee of CCM and ACT Wazalendo to prioritise citizens’ expectations for constructive and unifying politics that seek solutions rather than deepen conflicts. Speaking today, September 14, 2026, during the launch of the committee, Dr Mwinyi said citizens expect…
ARUSHA: A two-day International Diplomatic Charitable Golf Tour held over the weekend at Kili Golf Course in Usa River, Arumeru District, Arusha Region, has raised funds to support children living in difficult circumstances. The 8th Diplomatic Golf Charity Tournament, organised by the Songea Mississippi Foundation (SOMI) in partnership with Kili Golf, has so far benefited…
ZANZIBAR: PRESIDENT of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr Hussein Ali Mwinyi, has said the formation of a Joint Dialogue Committee comprising members from CCM and ACT Wazalendo is an important step towards advancing the reconciliation process and strengthening peace, unity and political stability in Zanzibar. President Mwinyi made the remarks today, September…
MBUNGE wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, ametetea tabia yake ya kutoa fedha kwa wakazi wanaohudhuria mikutano yake ya kisiasa, akisema kuwa fedha hizo ni za kuwasaidia wananchi wanaosafiri umbali mrefu kufika kwenye shughuli zake za kisiasa. Akizungumza katika mahojiano ya televisheni Alhamisi, Jhanda alisema kuwa ana uwezo wa kutoa msaada huo kutokana na mshahara wake wa ubunge pamoja na mapato anayopata kupitia biashara zake. Kulingana naye, wananchi wengi wanahitaji maendeleo lakini pia wanahitaji fedha za kujikimu katika maisha yao ya kila siku. Mbunge huyo alieleza kuwa si haki kwa wakazi kutoka maeneo mbalimbali kusafiri kwa gharama zao wenyewe, kuhudhuria mkutano na kisha kurejea nyumbani bila msaada wowote wa kifedha. Alisema fedha hizo zinakusudiwa kufidia gharama za usafiri na changamoto nyingine wanazokumbana nazo wananchi wanaposhiriki mikutano hiyo. Jhanda alihoji jinsi wazee, vijana na watu wengine kutoka sehemu za mbali wanavyoweza kuhudhuria mikutano na kurejea nyumbani bila msaada wa kifedha. Kwa mtazamo wake, hali hiyo ni kutowatendea haki wananchi wanaojitolea kushiriki shughuli za viongozi wao. Kauli zake zimeibua mjadala mpya kuhusu desturi ya wanasiasa kutoa fedha, chakula au bidhaa mbalimbali kwa wananchi wanaohudhuria mikutano na mikusanyiko ya kisiasa. Wanasiasa wengi wamekuwa wakitaja misaada hiyo kama njia ya kuwawezesha wananchi au kuwashukuru kwa ushiriki wao. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya utawala bora na uchumi wamekosoa utamaduni huo wakisema vita dhidi ya umaskini haviwezi kushindwa kwa kugawa fedha au vifaa kwa lengo lakupata sifa za kisiasa. Huku maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 yakianza kushika kasi, mjadala kuhusu nafasi ya fedha katika uhamasishaji wa kisiasa unaendelea kugawa maoni kati ya wanaounga mkono na wanaopinga mtindo huo.
In today’s Nigerian newspapers review programme, Today in the News, Vanguard leads with the surge in international crude oil prices above $100 per barrel which is pushing up petrol prices across Nigeria, with major marketers raising pump prices and creating fresh pressure on transporters, commuters, households and businesses.
ALIANZA kama kijana wa miaka 18 aliyekuwa na kazi katika shirika la posta na mawasiliano. Hakujua kwamba hatua yake ya kwanza ya kuwakilisha wafanyakazi wenzake ingebadilisha maisha yake na kumweka katika uongozi kwa zaidi ya nusu karne. Leo, jina la Francis Atwoli ni kubwa katika ulimwengu wa wafanyakazi Kenya. Kwa miaka 25 amekuwa akiongoza Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (Cotu-K), akihudumu katika awamu za kisiasa za marais tofauti na misukosuko ya kiuchumi iliyobadilisha maisha ya mamilioni ya Wakenya. Na Machi mwaka huu, wafanyakazi walimwambia bado hawataki aondoke. Atwoli alichaguliwa bila mpinzani kwa muhula wa sita wa miaka mitano katika mkutano wa wajumbe wa Cotu uliofanyika Tom Mboya Labour College, Kisumu. Muhula huo utaendelea hadi 2031. Kwa mwanamume ambaye amekuwa katika uongozi wa shirika hilo tangu 2001, uchaguzi huo ulikuwa zaidi ya ushindi mwingine. Ulikuwa thibitisho la uimara wa uongozi wake ndani ya shughuli za wafanyakazi. Lakini nyuma ya jina la Atwoli kuna safari ndefu. Safari yake katika vyama vya wafanyakazi ilianza baada ya kumaliza shule ya sekondari. Aliajiriwa na East African Posts and Telecommunication Administration akiwa na umri wa miaka 18. Ndani ya miezi miwili tu, alichaguliwa bila mpinzani kuwa mwakilishi wa wafanyakazi katika tawi la Nairobi la Union of Posts and Telecommunication Employees. Akiwa na miaka 21, alichaguliwa kuwa katibu wa tawi la Nairobi. Hapo ndipo safari yake ya muda mrefu katika harakati za wafanyakazi ilipoanza kwa nguvu. Mwaka 1967, alijiunga rasmi na harakati za wafanyakazi, safari ambayo Cotu baadaye iliitaja alipoadhimisha miaka 50 katika harakati hizo mwaka 2017. Kwa Atwoli, uongozi haukuwa suala la cheo pekee.Ulikuwa kuhusu uwezo wa wafanyakazi kujitetea. Alitumwa Italia kusomea masuala ya ajira katika Turin College of Labour Studies, ambako alipata nafasi ya kupanua uelewa wake kuhusu harakati za wafanyakazi duniani. Aliporudi Kenya, aliendelea na shughuli za chama.Mwishowe, msimamo wake ulimgharimu kazi. Kwa mujibu wa wasifu wa Cotu, alistaafishwa mwaka 1986 kwa kile kilichoelezwa kuwa kushiriki katika shughuli za chama cha wafanyakazi. Lakini kuondoka kazini hakukumaliza safari yake.Kulikuwa mwanzo wa hatua nyingine. Atwoli baadaye akawa Katibu Mkuu wa Kenya Plantation and Agricultural Workers Union (KPAWU). Alijenga jina katika sekta ya kilimo, hasa katika masuala yaliyohusu wafanyakazi wa mashambani. Kufikia 2001, alikuwa tayari amejijengea ushawishi mkubwa katika harakati za wafanyakazi. Mwaka huo, mpenzi huyo wa rhumba alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Cotu baada ya kuungwa mkono na vyama 26 kati ya 29 vilivyokuwa wanachama wa shirika hilo. Huo ulikuwa mwanzo wa enzi yake. Na miaka 25 baadaye, bado yuko katika kiti hicho. Ingawa Cotu ni shirika la wafanyakazi, Atwoli hakuwahi kujitenga kabisa na siasa za Kenya. Shirikisho hilo lilifanya kazi pamoja na upinzani wa National Rainbow Coalition (Narc) mwaka wa 2002, uliokuwa ukimuunga mkono Mwai Kibaki katika uchaguzi wa urais. Kibaki alishinda uchaguzi huo na kumaliza utawala wa Kanu uliokuwa umechukua miaka 40. Tangu wakati huo, Atwoli amekuwa mtu ambaye kauli zake kuhusu siasa za Kenya zimekuwa zikifuatiliwa kwa karibu. Huwa anaunga mkono au kukosoa serikali kulingana na masuala yaliyo mbele yake huku akisisitiza lazima Cotu ifanye kazi na serikali iliyo mamlakani kwa maslahi ya wafanyakazi. Lakini pia amesisitiza kwamba Cotu ni shirika la wafanyakazi na si chama cha kisiasa. Kwa mujibu wa msimamo rasmi wa Cotu, wanachama wake wana uhuru wa kuunga mkono vyama tofauti, huku shirika likishirikiana na serikali iliyoko madarakani kwa masuala yanayohusu wafanyakazi. Hapo ndipo moja ya mambo yanayomfanya Atwoli kuwa mtu wa kipekee yanapoonekana. Anaweza kuwa mkosoaji wa serikali katika suala moja na kuiunga katika suala jingine mradi tu linahusu maslahi ya wafanyakazi. Kwa miaka yake yote Cotu, suala la mishahara limekuwa mojawapo ya ajenda zake kuu. Atwoli amekuwa akisisitiza umuhimu wa mshahara wa chini unaomwezesha mfanyakazi kuishi kwa heshima.
VIONGOZI wa upinzani wakiongozwa na vinara wa Wiper Patriotic Front, Bw Kalonzo Musyoka, Democratic Party Bw Justin Muturi na mwenzao wa DAP-Kenya Bw Eugene Wamalwa, wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama nchini, wakionya kuwa ghasia za kisiasa zinaweza kuhatarisha uchaguzi mkuu wa 2027. Viongozi hao walinukuu tukio la hivi majuzi kaunti ya Embu ambapo Naibu Rais Kithure Kindiki alilazimika kukimbilia usalama wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kuzuka kwa ghasia. Walisema tukio hilo limeibua maswali kuhusu usalama wa viongozi na Wakenya wa kawaida. Bw Musyoka aliwataka Wakenya kuombeana amani, huku akiikosoa idara ya usalama kwa kile alichokitaja kuwa ni kumdhulumu Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji kufuatia tukio hilo. “Kama viongozi, tunalaani tukio hilo. Kuuzingira nyumba ya mbunge ni jambo la kusikitisha… kwa sababu tumeambiwa kwamba wakazi walisikia kuwa kulikuwa na pesa zikigawiwa, hivyo wakakimbilia kwenye mkutano kupata sehemu yao. Hilo ndilo lililosababisha vurugu, lakini kwa nini kumlaumu mbunge?” aliuliza. Bw Musyoka alisema aliwahi kumtetea Bw Mukunji kama wakili wakati mbunge huyo alishtakiwa kwa kujihusisha na ugaidi. “Alifikishwa mahakamani na kushtakiwa chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi,” alisema, akiongeza kuwa Bw Mukunji hapaswi kudhulumiwa. Alisema Bw Muturi atamtetea mbunge huyo. Bw Musyoka alihoji hali ya usalama nchini, akisema tukio lililomhusisha Naibu Rais linaonyesha kuwa hata maafisa waandamizi wa serikali wako katika mazingira hatarishi. “Tuombeane. Kwa kweli, kwa wakati kama huu, nchi yetu iko katika hali mbaya. Unapomwona Naibu Rais wa Jamhuri akikimbilia msituni kwa usalama, lazima ujiulize, usalama uko wapi? Ikiwa Naibu Rais anakimbilia msituni kwa usalama, raia wa kawaida ataenda wapi?” aliuliza Bw Musyoka. Pia alirejelea tukio la hivi majuzi ambapo msafara wa viongozi wa upinzani ulipigwa mawe walipoingia Garissa. “Tulikuwa na tukio Garissa, lakini tulikaribishwa vizuri sana Kaskazini Mashariki. Sasa tuko katika eneo la Pwani kuzungumza na Wakenya kuhusu changamoto zinazoikabili nchi hii,” alisema. Bw Wamalwa alisema viongozi wa upinzani wameazimia kuendelea kutembelea maeneo mbalimbali nchini licha ya uhasama waliokumbana nao katika baadhi ya maeneo. Alifananisha kuingia kwao Garissa na kuingia kwa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Kismayu, Somalia, akisema walikumbana na upinzani kutoka kwa makundi aliyodai yalikuwa yamehamasishwa dhidi yao. “Tulihangaika kuingia katika eneo hilo, kwa sababu hii ni timu ya Serikali Mbadala ya Umoja, upinzani wa kwanza kuingia Kaskazini Mashariki. Hata hivyo, serikali haikutaka tuende kueneza ujumbe wetu Kaskazini Mashariki,” alisema. Bw Wamalwa alidai kuwa makundi yaliyowakabili yalikuwa yamehamasishwa na Serikali, madai ambayo hayakuweza kuthibitishwa kwa njia huru. Alisema makabiliano kati ya upinzani na tukio la Embu yanapaswa kuwa onyo dhidi ya matumizi ya ghasia katika siasa. “Hakuna mtu anayeweza kudhibiti uhuni,” alisema Bw Wamalwa, akitaja Haiti ambako alisema wanasiasa waliwahi kutegemea magenge kabla ya kuyapoteza kabisa mamlaka ya kuyadhibiti. “Hatutaki kwenda katika njia hiyo; tunataka nchi yenye amani na uchaguzi wa amani. Wale walio serikalini, wale wanaotaka kupanda chui wa ghasia, mwishowe mtaliwa na huyo chui kwa sababu hamtakuwa na uwezo wa kudhibiti uhuni au ghasia,” alisema. Bw Wamalwa aliwataka Wakenya kudumisha amani huku nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu wa 2027. “Ni lazima tuombee nchi hii, tuwe vyombo vya amani. Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu, zikiwa zimesalia miezi 10 pekee kabla ya uchaguzi. Wakenya wote waruhusiwe kuwachagua kidemokrasia viongozi wanaowataka madarakani,” alisema. Aliwataka viongozi kuruhusu wanasiasa kufanya kampeni kwa uhuru katika maeneo yote ya nchi bila kujali misimamo yao ya kisiasa. “Iwe uko muhula wa pili au wa kwanza, ni lazima tuwe mabalozi wa amani na tuchague yeyote tunayemtaka kidemokrasia. Hiyo ni haki yenu. Viongozi pia wanapaswa kuwa huru kutembelea sehemu yoyote ya nchi kutafuta kura,” alisema. Bw Muturi alisema mazingira ya kisiasa nchini yamezidi kuwa yenye vikwazo, akidai kuwa maafisa wa usalama walizunguka kanisa ambako viongozi wa upinzani walikuwa wameenda kuomba. “Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, kanisa linazingirwa na maafisa wa usalama wenye silaha kwa sababu viongozi wa upinzani wameenda kuomba,” alisema. “Hata wakati wa siku za giza za mfumo wa chama kimoja, haikuwahi kuwa hivi. Wakenya, tuombe kwa Mungu. Wakenya lazima wawe na uhuru wa kuwa na misimamo yao, kuieleza na kushirikiana na yeyote wanayemtaka. Hiyo ndiyo demokrasia,” alisema Bw Muturi. Alimtetea Bw Mukunji, akisema mbunge huyo hapaswi kulaumiwa kwa vurugu zilizotokea Embu. Bw Muturi alidai kuwa zaidi ya watu 20,000 walikusanyika baada ya kusikia kuwa pesa zilikuwa zikigawiwa katika mkutano huo. Aliitaka serikali kuhakikisha usalama wa kutosha kwa wakenya wote na viongozi wa kisiasa huku nchi ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2027.