ARUSHA: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Tanzania imewata wafanyabiashara kuendelea kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu kwa kuuzaa bidhaa kwa usahihi kama ilivyoelekezwa.
Meneja wa EWURA, Kanda ya Kaskazini, Lorvii Long’idu amesema hayo katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Arusha ambapo mamlaka hiyo imefika kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya taasisi hiyo inavyofanya kazi katika udhibiti wa bidhaa kama ilivyoelekeza.
Amesema EWURA ni mdhibiti wa masuala mazima ya maji, mafuta kwa ajili ya magari na kuendesha mitambo ya umeme pamoja na usafi wa Mazingira.
“Tumejikita katika maeneo mawili makubwa ambayo ni ya kiufundi, kiuchumi na kibiashara na katika masuala ya kiuchumi tunaangalia sana huduma hizi kuwa zinatakiwa kupatikana kwa usahihi na kwa gharama ambayo mwananchi anaweza akaimudu pia kuhakikisha huduma hii inakuwa endelevu,”amesema Long’idu.
Amesema wafanyabiasha wanaouza mitungi ya gesi waendelee kuzingatia sheria taratibu na kanuni ikiwemo kuuza mitungi yenye kiwango cha gesi sahihi na sio zilizochakachuliwa bali zitolewe kwa mwananchi kwa ubora ulele uke uliothibitisgwa .
Amesema EWURA inachakata bei za bidhaa zm ambazo wanazizibiti ikiwemo utoaji wa bei za mafuta mara moja kila mwezi lengo ni kuhakikisha mwananchi anapata bei sahihi lakini pia mtoa huduma anaweza kutoa bei sahihi bila kuteteleka na akahamasishwa sana katika uwekezaji .
“Huduma za mafuta zimeendelea kuimarika hapa nchini ,ujenzi wa vituo vya mafuta ambavyo viko katika viwango bora kabisa vinaendelea kuongezeka na hii maana yake sisi kama wadhibiti tumeendelea kumlinda mwekezaji pia kulinda mwananchi kuhakikisha anapata bei ambayo ni himilivu na kulipa,”ameongeza.
Amefafanua kuwa ubora wa bidhaa hizo za mafuta wanahakikisha zinauzwa kwa bei iliyowekwa na shirika lao la viwango hivyo wanatembea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vituo vya mafuta kuona ubora na uuzwaji unafanyika katika miundombinu ambayo ni salama.
“Kama EWURA tunajikita kuhakikisha hakuna majanga yoyote yanaweza kutokea na kuleta athari kwenye mazingira afya au usalama katika maeneo hayo na ndio maana tumekuwa tukikagua na tukikuta kituo hakikidhi ubora huwa tunakifunga hivyo hivyo katika masuala ya maji na usafi wa mazingira tunaendelea kuona uimarikaji na upatikanaji wa huduma na kama wadhibiti tunazisimamia kuhakikisha wanatoa huduma bei sahihi na wakati ni sawa,”ameeleza.
Amesema wananchi wanapopata changamoto katika maeneo ambayo wanayasimamia wafike katika mamlaka hiyo na yatafanyiwa kazi na haki zao zitapatikana pia amewasihi kuendelea kutumia nishati safi ya kupikia kama ilivyo mpango mkakati wa serikali ifikapo 2034 zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati salama.




