Video
CAF YAPITISHA KISWAHILI KUWA LUGHA RASMI YA SHIRIKISHO HILO
Channel: Millard Ayo Watch on YouTube
About this video
21 Novemba, 2026 | Abuja, Nigeria Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) limeidhinisha Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi za shirikisho hilo baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya CAF. Uamuzi huo umetangazwa na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, kufuatia kupigiwa kura nyingi za kishindo na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika jijini Abuja, Nigeria. Kufuatia uamuzi huo, Kiswahili kinaungana na lugha nyingine nne rasmi za CAF ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kireno, na sasa kitatumika katika shughuli mbalimbali za shirikisho hilo, ikiwemo mikutano na matukio yanayoandaliwa na CAF. Akizungumzia uamuzi huo, Rais Motsepe ameipongeza Tanzania, Kenya na Uganda kwa mchango wao katika kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya CAF, akieleza kuwa hatua hiyo ni fursa muhimu kwa Afrika.
Related stories
SportsSimba yaendelea kutembeza kipigo Ligi Kuu
SIMBA imeendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 leo Jumamosi, Novemba 21, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
SportsJKT Tanzania 1-2 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 21/11/2026
Simba SC imepindua meza na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam, ukiwa ni ushindi wake wa 11 mfululizo kwenye ligi msimu…
SportsMagoli | JKT Tanzania 1-2 Simba SC | NBC Premier League 21/11/2026
Simba SC imepindua meza na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam, ukiwa ni ushindi wake wa 11 mfululizo kwenye ligi msimu…
SportsTanzania yapewa miji mitatu kuandaa AFCON 2027
Tanzania imepata bahati ya miji mitatu kupewa fursa ya kuandaa mechi za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.