
KOCHA AHAMAD ALLY AWAPA ONYO SIMBA KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA SIMBA - "TUMEJIPANGA TUNAWAJUA"
KOCHA AHAMAD ALLY AWAPA ONYO SIMBA KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA SIMBA - "TUMEJIPANGA TUNAWAJUA" ⚫️ JE, UNA HABARI?
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.

KOCHA AHAMAD ALLY AWAPA ONYO SIMBA KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA SIMBA - "TUMEJIPANGA TUNAWAJUA" ⚫️ JE, UNA HABARI?

KIKOSI cha vijana chipukizi cha Zanzibar Spice Boys, chenye wachezaji 18 wenye umri wa miaka 12 na 13, kinajiandaa kwenda Brazil kushiriki mashindano ya kimataifa ya soka la watoto yaliyopewa jina la PQ CUP BRASIL 2026.

Former Manchester United manager Sir Alex Ferguson has revealed that he was “terrified” before returning to Old Trafford following the brain haemorrhage that required emergency surgery in 2018.

LIGI ya Championship msimu wa 2026/27, imeendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu, huku kesho Jumapili vinara wa ligi hiyo, KMC, wakitarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, kuvaana na Bandari Tanzania.

Manchester City confirmed on Friday that it had launched a "comprehensive appeal" after an independent commission ruled the club had broken Premier League financial rules.

UTANGULIZI Mkewe Almasi alikuwa amelala chini hatua chache mbele yake. Kichwa chake kilikuwa kimetenganishwa kabisa na kiwiliwili! “Yesu wangu!” akaguta. Kisha akajisemea: “Mke wangu naye ameshauawa!” Aliogopa kuingia ndani zaidi, akatoka nje ya chumba na kufunga mlango. “Hawa watu wamekuja kumuua mke wangu humu humu ndani!” akaendelea kujisemea huku akipiga hatua za haraka kutoka nje. SASA ENDELEA “NI kweli alivyosema yule mganga, mauaji yataendelea. Nilipuuza, sasa yameshatokea” alijiambia wakati akijipakia kwenye gari baada ya kufunga mlango wa nyumba yake. Aliliondoa gari lakini hakujua alikuwa anakwenda wapi. Akajiuliza anakwenda wapi? Hakupata jibu kichwani mwake. Akaendelea kujiuliza aende polisi au aende kwa mchngaji wake au aende kwa Maria. Kama ni kwa mchungaji asingeweza kwenda kwa sababu alikuwa amelewa. Kadhalika asingeweza kwenda polisi kwa sababu aliona kusingekuwa na msaada wowote. Polisi hao wangefika nyumbani kwake na kumhoji maswali na kisha kuondoka na mwili wa mke wake. Akaona bora aende kwa Maria. Kama ni kwenda polisi atakwenda baada ya kutoka kwa Maria. Alifika Tegeta alikokuwa akiishi Maria. Maria alishangaa alipomuona shemeji yake akiwasili nyumbani kwake usiku ule. “Karibu shemeji, mbona umekuja usiku huu?” “Dada yako ameshachinjwa sasa hivi” akamwambia. Maria alishituka sana. “Dada yangu yupi aliyechinjwa?” “Leo humjui dada yako, kwani yule uliyempeleka kwa mganga ni nani wako?” “Shemeji usiniambie, dada yangu nayeye amechinjwa!” “Amechinjwa sasa hivi…” “Hebu nieleze imekuwaje?’ Almasi akamueleza tukio zima lilivyotokea. “Sasa huoni kwamba hao si watu wa kawaida, wameingiaje humo ndani na wametokaje?” “Walivyoingia sijui lakini hawajatoka. Nimefunga milango yote. Nilisikia wakimuuliza kama yeye ni mke wa Almasi. Alipowajibu ndiyo, nikasikia wakimwambia mume wako alikuweka dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana halafu wakamchinja” “Wewe ulikataa bure kwenda kwa mganga, sasa unaona. Yule mganga alituambia mauaji yataendelea” Almasi alitikisa kichwa kusikitika. “Ni kweli nilifannya kosa. Ninahisi mimi ndiye nitakayekuwa wa mwisho kuuawa” “Yule mganga alituambia mauaji yataendelea” “Sasa nipeleke sasa hivi kabla sijauawa” “Subiri kwanza. Kwani umeshatoa ripoti polisi” “Sijatoa ripoti polisi. Nimekuja huku kwanza” “Sasa kwanini hukutoa ripoti polisi wakati mke wako ameuawa?” “Nimeona hawanisaidii. Bora nianze na mahali nitakapopata msaada wa maisha yangu” “Ukumbuke umesema kwamba hao watu umewafungia ndani” “Nikitoka hapa ndio nitakwenda polisi. Kama hao watu wamo watatolewa na polisi” “Haya subiri twende kwa huyo mganga” Dakika chache baadaye Almasi na shemeji yake wakawa njiani kuelekea kwa huyo mganga aliyekuwa akiishi mbali kidogo na mtaa aliokuwa akiishi Maria. “Lile tukio limenishitua sana. Wale ndio watu waliowaua wanangu na leo wamemuua mke wangu. Nimewasikia waziwazi. Maneno yao ni yale yale waliyokuwa wakiwaambia wanangu kabla ya kuwaua. Sasa sijui kama wale ni binaadamu au ni mashetani?” “Kwani wewe hukumbuki kama uliwahi kuweka nadhiri?” “Sijaweka nadhiri mahali popote. Halafu mimi sina tabia ya kupenda ushirikina. Nilishampokea Yesu siku nyingi” “Yule mganga alisema uliweka nadhiri” “Sasa acha nikamsikilize mwenyewe” “Kama shemeji ungekubali mapema, haya matatizo yasingetokea” Almasi akanyamaza kimya. Maneno ya Maria yalikuwa yakimchoma moyo. Kimoyomoyo alikiri kwamba alifanya kosa kutokukubali alipoambiwa aende kwa mganga. Kichwani kwake alikuwa akijiuliza kama aliwahi kwenda kwa mganga angalau mara moja na kuweka nadhiri aliyoambiwa. Akili yake ilikataa kabisa. Walipofika nyumbani kwa mganga walibisha na kuingia ndani. Aliyewakaribisha alikuwa ni mganga mwenyewe. “Karibuni” Mganga aliwambia akiwa amemkumbuka Maria. Wakiwa wameketi katika chumba cha uganga, Maria akamwambia mganga. “Nadhani unakumbuka tulivyokuja kwako na mwenzangu?” “Nawakumbuka vizuri” “Ulituambia kwamba mauaji yataendelea na kweli huu usiku dada yangu ameuawa usiku huu katika mazingira yale yale” Mganga akashituka kidogo. “Dada yako yule yule uliyekuja naye?” akauliza kwa fadhaa kisha akaongeza. “Niliwambia mje na mume wale lakini sikuwaona tena” “Mume wake ndiye huyu niliyenaye” “Kwanini bwana umechelewa kuja kwangu mpaka matatatizo yanazidi kutokea?” Mganga akamuuliza Almasi. “Tatizo lililonizuia ni kwamba nilikuwa najaribu kujiuliza niliweka nadhiri wapi lakini sikupata jibu” “Uliweka nadhiri. Jaribu kukumbuka sana” “Labda kama wewe unaijua nikumbushe” “Miaka kadhaa nyuma ulikuwa masikini sana, ulipata wapi mali yako na kwa njia ipi?” Almasi alipotajiwa mali, mawazo yake yakaenda mbali sana. Kumbukumbu zikaanza kumjia. Ilikuwa ni mwaka 2001 alipomuacha mke wake pamoja na watoto wake waliokuwa wamezaliwa wakati huo na kuelekea Marerani kwenda kuchimba madini. Baada ya kufika huko, Almasi ambaye jina lake halisi lilikuwa Amon Marwa kabla ya kujibatiza jina la Almasi aligundua kuwa shughuli nzima ilikuwa imetawaliwa na ushirikina mtupu. Alipata mtu aliyemshauri kwamba ili apate uhakika wa mafanikio nilazima aende kwa mganga. Akapelekwa kwa mganga mmoja aliyekuwa Korogwe. Mganga alipomsikiliza, alimwambia Amon ili apate madini ya kumpa utajiri ni lazima atoe kafara la roho. Amon akagutuka. “Kafara la roho? Kafara la roho ndio kitu gani?” “Umtoe mtu kafara” “Kivipi?” “Hujui kutoa mtu kafara, ndiyo umeanza sasa kazi ya kuchimba madini?” “Nimeanza muda kidogo lakini sijapata mafanikio. Watu wameniambia nijaribu kwenda kwa waganga” “Kuna makafara yanayotolewa na baadhi ya watu kwenye machimbo” “Nilivyosikia ni kwamba watu wanatoa makafara ya wanyama kama mbuzi” “Sasa ili wewe upate utajiri unaoutaka ni lazima utoe kafara la roho ya mtu” “Ndiyo nilikuwa nataka ufafanuzi, kafara hilo linatolewa vipi?” “Uchinje mtu kwenye chimbo lako!” “Mama yangu…!” “Kama uko tayari na una uhakika wa kupata mtu wa kumtoa kafara, sema nikupe msaidizi wangu uende naye akakufanyie kazi yako” Amon baada ya kuwaza kidogo alimuuliza mganga huyo. “Kama tutatoa kafara la mtu, ndiyo itakuwaje?” “Utapata mali itakayokupa utajiri katika masiha yako yote.Lakini ni endapo utafuata masharti yangu” “Masharti gani hayo?” “Sharti la kwanza, ukishapata mali mara moja tu usirudi tena Marerani. Sharti la pili, kila mwakalazima ukamwage baharini sarafu zenye thamani ya robo ya utajiri wako, yaani unawapa sadaka majini waliokupautajiri huo” “Kama nimekuelewa vizuri, sharti la kwanza nikishatoa mtu kafara na kufanikiwa kupata mali niondoke Marerani na nisirudi tena. Na sharti la pili, kila mwaka nitoe sarafu zenye thamani ya robo ya utajiri wangu, si ndiyo” “Ndiyo hivyo” “Sasa mimi nina maswali” “Uliza” “Kwanza nataka kujua ina maana hayo madini nitakayopata baada ya kutoa hilo kafara, ndiyo yatakayonipa utajiri maishayangu yote?” “Sawali zuri sana. Utapata utajiri ambao utauendeleza kwa biashara nyingine” “Na hizo sarafu ambazo unasema nikamwage baharini kila mwaka nitazipata wapi?” “Unatakiwa uweke kidogo kidogo kwa mwaka mzima, zikifikia robo ya utajiri ulionao, unazifunga katika vifurshi saba vya kitambaa cha rangi nyeupe kisha unakodiboti na kwenda kuzitosa baharini” “Yaani nifanye hivyo hadi kufa kwangu” “Ndiyo, usiache. Wale majini waliokupa madini nao wanataka sadaka zao” “Kama una uhakika kuwa nitapata utajiri, naweza kufanya hivyo lakini nitampata wapi huyo mtu wa kumtoakafara” “Mtu yeyote tu” “Sasa nitampataje?” “Unatuma watu wakutafutie mtu ambaye watamfunga kamba na kumpeleka kwenye lile chimbo wakati wa usiku kisha atachinjwa pale na mwili wake utakwenda kuzikwa” “Hapo panataka kazi. Kumkamata mtu na kumfunga…!” “Mbona ni jambolinalowezekana. Yule mtu anakamatwa usku vichochoroni. Kama mna gari, mnampakia na kumpeleka kunakohusika” “Wakati huo wewe utakuwa wapi?’ “Chukua namba yangu ya simu. Siku ukiona una mpango wa kupata mtu unaniagiza ninakuja siku hiyo hiyo au ninatuma mtu wangu. Hiyo kazi inafanyika usiku wa manani” “Sawa. Nipe namba yako” Mganga alimpa Amon namba yake ya simu na Amon akampa mganga huyo namba yake. “Sasa wewe nenda, siku yoyote ukiona una mpango wa kupata mtu nipigie simu” “Sawa. Sasa utakapoifanya hiyo kazi utahitaji kiasi gani?” “Hii kazi ni kubwa na kima changu ni shilingi milioni mojananusu” “Mbona ni kiasi kikubwa sana?” “Ndiyo kima changu na ni kwa sababu nina uhakika kwamba utapata utajiri kwani wengi wamefanikiwa.” “Naona una uhakika na kazi yako. Nitakutafutia hiyo pesa kisha nitakupigia simu kukujulisha kama nimepata mtu” “Sawa”

LEO, Jumamosi katika Uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni kuna mechi ya kukata na shoka, fainali ya Ngao ya Jamii inayowakutanisha mabingwa watetezi kwenye soka la wanawake, JKT Queens mabingwa watetezi wa kombe hili na Simba Queens ambao ni mabingwa wa ligi.

HATIMAYE mabaharia wa KMKM wamepata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuteseka kwa muda mrefu kwenye ligi hiyo.

KATIKA kujiweka sawa na mbio za ubingwa Ligi Kuu Zanzibar, JKU imekatishwa spidi njiani kwa kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KMKM huku lawama zote ikipewa safu ya ulinzi.

KOCHA Msaidizi wa Mlandege, Sabri China amesema makosa yaliyofanya na wachezaji wa timu hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kupoteza mechi yao ya Ligi Kuu Zanzibar kwa mabao 2-0 dhidi ya KVZ.

VITA ya ufungaji bora katika Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) imeshika kasi huku wanne kati yao wakiwemo watatu washambuliaji na mmoja kiungo wakionesha kiu kubwa ya kuzifumania nyavu kila wanaposhuka dimbani.

The English Football Association said on Friday that an independent commission's findings that Manchester City had broken financial rules had "implications for the integrity of the game".

ARUSHA: Ujenzi wa barabara zinazounganisha maeneo mbalimbali na Uwanja wa AFCON jijini Arusha umefikia zaidi ya asilimia 60, hatua inayolenga kuboresha usafiri na kuimarisha shughuli za kiuchumi katika maeneo yanayozunguka uwanja huo. Mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unahusisha ujenzi na uboreshaji wa jumla ya kilomita 21.4 za barabara…

ARUSHA: FOOTBALL fans heading to Arusha for the 2027 Africa Cup of Nations (AFCON) finals will have more than matches to look forward to, with a new cultural festival planned to give visitors a taste of Tanzanian traditions. The inaugural Arusha International Cultural Festival (AIC Festival) is expected to run during the continental tournament, which…

By Cynthia Alo & Kafayat Kokumo Stakeholders in the agriculture sector have called for a change in the way agriculture is described, saying a shift in language could help attract more young people and investors into the sector. Lagos State Commissioner for Agriculture and Food Systems, Ms Abisola Olusanya, specifically proposed replacing the term ‘agricultural […]

UK Prime Minister Andy Burnham has clarified his position on Manchester City’s financial rule case after facing backlash over his comments that he would be “really concerned” if the club’s owners decided to sell.

UEFA is continuing its review of the Negreira case involving Barcelona after Real Madrid submitted a substantial amount of new documents to European football’s governing body.

Manchester City are expected to argue that key sponsorship deals were funded by the Abu Dhabi government rather than the club's owners as part of their appeal against the independent commission's findings in the Premier League's 115-charge case.

By Peter Egwuatu Heirs Holdings, has acquired an additional six million shares in Seplat Energy Plc valued at £53.2 million.According to a statement filed with the Nigerian Exchange Limited (NGX) the shares were bought by Heirs Energies Limited, a company controlled by Tony Elumelu.The statement signed by Edith Onwuchekwa, Director, Legal/Company Secretary, of Seplat stated:” […]

By Adesina Wahab LAGOS — The Federal Government has announced plans to subsidise the conversion of vehicles owned by university lecturers and other workers to Compressed Natural Gas, CNG, as part of efforts to reduce transportation costs on university campuses. The government also said it would deploy CNG-powered buses to selected universities, with fares capped […]


— Pledge 10m votes for president By Johnbosco Agbakwuru ABUJA — Heads of federal parastatals have launched a coalition to support President Bola Tinubu’s re-election bid in 2027, pledging to deploy messaging, mobilisation and technical support alongside the All Progressives Congress, APC, Presidential Campaign Council, PCC. The group, operating as the Forum of Chief Executives […]


NUSU fainali ya timu za vijana wenye umri chini ya miaka 15 katika mashindano ya Dar Youth League (Dar Youth League U15) itafanyika Oktoba 3 na 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Gymkhana.

KIUNGO mshambuliaji wa JKT Tanzania, Fredrick Magata, amesema ushindani wa nafasi katika kikosi hicho cha maafande ni tofauti na msimu uliopita wa 2025-2026, kutokana na aina ya wachezaji wengi na wazuri aliokutana nao kwenye timu hiyo.

MSHAMBULIAJI wa Pamba Jiji, Deogratius Mafie amesema kipindi hiki cha kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kimekuwa kizuri kwao kwa ajili ya kujadili mipango mbalimbali, hasa baada ya kuanza vibaya msimu wa 2026-2027.

MSHAMBULIAJI mpya wa Kagera Sugar, Ally Salum ameanza rasmi mazoezi na timu hiyo, baada ya kushindwa kuitumikia tangu alipojiunga na kikosi hicho, Agosti 3, 2026, akitokea Kariobangi Sharks inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Bernard Kamungo, tayari ametatua changamoto aliyokumbana nayo na tayari ameondoka kambini na kurejea Marekani kujiunga na FC Dallas, huku akitarajiwa kuungana tena kwenye majukumu ya kitaifa hadi Novemba 2026.

BAADA ya Yanga Princess kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026, inaelezwa kocha mkuu wa timu hiyo, Edna Lema, amejiuzulu nafasi yake, huku mwenyewe akifafanua ishu hiyo.

MSHAMBULIAJI wa JKT Queens aliyesajiliwa kutoka Tanzanite Queens, Fatma Muhibu ameanza kuonyesha thamani yake kwenye kikosi hicho kipya, baada ya kufunga bao la dakika ya 48 dhidi ya Mashujaa Queens lililoipa tiketi ya fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026.

KAMISHNA wa Jeshi la Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan, amelishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kusimamia klabu na waamuzi kudumisha nidhamu ili kuifanya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) yenye mvuto na hamasa.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amewapongeza wazazi wa wachezaji chipukizi wa timu ya Zanzibar Spice Boys kwa kuwaunga mkono kushiriki fursa ya mashindano ya PQ Cup Brazil 2026.

BODI ya Ligi Zanzibar (ZLB) imewaonya mashabiki wanaohudhuria viwanjani kushuhudia michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Zanzibar kuacha vitendo vya utovu wa nidhamu, ikiwemo matusi, vurugu na kuingia katika maeneo yasiyoruhusiwa uwanjani.

KOCHA wa JKT Queens, Kessy Abdallah, amesema kikosi chake kimeanza kujiandaa kwa ajili ya kutetea ubingwa wa Ngao ya Jamii Wanawake baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Queens.

KOCHA Mkuu wa Mashujaa Queens, Rajab Ally, amesema bao walilofungwa na JKT Queens limewapa funzo na kubaini maeneo wanayopaswa kuyafanyia kazi, hasa namna ya kudhibiti mabadiliko ya mchezo wakati wa kushambulia.

UTANGULIZI “Unajua kuna kuua kwa mdomo. Unaweza kumwambia mtu nitakuua na kesho akakutwa ameuawa kweli, basi muuaji utakuwa wewe” “Mimi nilikuwa sijui. Nilisema kwa mzaha tu” “Elias kamuweke ndani mpaka pale atakapokuwa tayari kutueleza anachokijua” “Yesu wangu! Mnataka kuniweka ndani, kwani Almasi ameuawa?” “Watoto wake wameuawa na umesema na yeye atauawa” SASA ENDELEA “Sasa ndiyo niwekwe ndani?” “Ndiyo. Umesema Almasi atauawa. Tukikuachia halafu akaja kuuawa kweli, tutamlaumu nani?” Mosha akatikisa kichwa kusikitika. Elias alimchukua Mosha na kwenda kumweka ndani. Baada ya mazishi ya Benjamin, mke wa Almasi alianza kuwa katika hali kama ya kuchanganyikiwa. Mdogo wake wa kike aliyeitwa Maria, ambaye alikuwa akiishi Tegeta, alikwenda kumchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akiishi huko huko Tegeta. “Mna tatizo gani?” mganga aliwauliza. “Tuna shida kubwa. Dada yangu amekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa tangu mtoto wake alipouawa. Walianza kuuawa kaka zake mmoja baada ya mwingine…” “Hao watoto wameuawa na nani?” Mganga akauliza. “Kusema kweli ni matukio ya ajabu…” Maria alimueleza mganga huyo mkasa mzima wa kuuawa kwa watoto wa dada yake, tangu alipouawa mtoto wa kwanza hadi wa mwisho, na kusababisha mama yao aanze kuchanganyikiwa. Mganga, baada ya kumsikiliza kwa makini, alimwambia: “Hebu subiri nimuite jini wangu.” Wote walidhani kuwa mganga huyo angepandisha mashetani kama ilivyo kwa waganga wengine, lakini walimuona akisema peke yake kwa sauti ya chini. Alikuwa akiuliza maswali kisha akiitikia yeye mwenyewe, kama aliyekuwa akipewa majibu. “Sasa subiri niwaeleze,” mganga akasema baada ya kusema peke yake kwa sekunde kadhaa. Akamtazama Maria pamoja na mke wa Almasi. “Mliwahi kuweka nadhiri hapo zamani?” akawauliza. Maria akamtazama dada yake. “Sisi hatujawahi kuweka nadhiri,” mke wa Almasi akajibu. Mganga akaendelea kusema peke yake, kisha akamuuliza mke wa Almasi: “Mume wako hakuwahi kuweka nadhiri?” “Hakuwahi.” “Hapa kuna nadhiri inamhusu mume wako. Huenda wewe hujui, lakini mume wako anajua. Aje yeye nizungumze naye.” “Sijui kama atakubali kuja huku.” “Hili tatizo bado lipo, halijakwisha.” “Una maana gani?” “Mauaji yataendelea.” “Yataendelea kwa nani wakati watoto wote wamekwisha?” Maria akauliza. “Yataendelea katika hii familia ya Almasi.” Maria akatazamana na mke wa Almasi kwa taharuki. “Sasa ngoja mke wake akajaribu kumshawishi ili aje akusikilize. Kwa maana hili tatizo limetutisha,” Maria akamwambia mganga. “Sawa. Nendeni mkamueleze, kama atakubali kuja itakuwa vizuri,” mganga aliwaambia. Maria na mke wa Almasi wakatoka. Gari likawarudisha nyumbani kwa Almasi. Walimkuta Almasi amekaa sebuleni akipekua kurasa za Biblia, mguu mmoja akiwa ameuweka juu ya mwingine. Wakamsalimia. Almasi aliwaitikia kisha akaiweka Biblia juu ya stuli iliyokuwa kando yake. “Habari za huko?” akawauliza. “Nzuri. Tulienda kwa mganga mmoja, naye ametupa maelezo ya kutisha,” mke wake akamwambia. “Amewapa maelezo gani?” Almasi akamuuliza. Mke wake akamueleza walivyoambiwa na mganga. Almasi, baada ya kumsikiliza, alitikisa kichwa. Alichukua ile Biblia akamuonyesha mke wake huyo. “Mimi naamini hiki kitabu. Waganga ni waongo sana. Mara nyingi wanakuwa na maono ya kishetani. Wao na mashetani wanakaa nyumba moja. Ndiyo maana unaona kila mganga lazima awe na shetani. Mimi sijaweka nadhiri mahali popote. Huyo mganga ni mnafiki mkubwa. Alikuwa anataka kuwala pesa zenu tu.” “Ni kweli, lakini ungekwenda kumsikiliza tu, shemeji. Kama utaona ni muongo, utaachana naye,” Maria akamwambia. “Sitathubutu kuinua mguu wangu kwenda huko. Kama ni watoto wangu wameshakufa wote, sasa nani tena atauawa na kwa kosa lipi?” “Hata hali ya dada si unaiona si nzuri?” “Dada yako amechanganyikiwa kutokana na haya matukio. Ninaamini baadaye atakaa sawa tu. Kila Jumapili anafanyiwa maombi. Msiwe na wasiwasi.” Juhudi za Maria na mke wa Almasi kumshawishi Almasi aende kwa mganga zikakomea hapo hapo. Almasi aliendelea kusoma Biblia yake kwa utulivu. Baada ya nusu saa hivi, alimuaga mke wake akamwambia kwamba anakwenda kumuona mchungaji. Akatoka na gari lake na kuelekea katika ofisi ya mchungaji huyo iliyokuwa ndani ya kanisa lao. Aliliegesha gari katika eneo la kuegeshea, akaingia ndani ya kanisa hilo. Punde tu alitokea kwenye mlango wa ofisi ya mchungaji. Alibisha mlango, alipojibiwa aliufungua na kuingia. “Oh, Bwana Almasi, karibu sana,” mchungaji aliyekuwa amevaa suti nyeupe alimkaribisha. “Asante. Bwana na asifiwe.” “Ameen. Karibu kiti.” Almasi akakaa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza ya mchungaji. “Kuna tatizo lolote au umenitembelea tu?” “Matatizo yangu ni yale yale. Kuna jambo limetokea leo.” “Jambo gani?” “Mke wangu amepelekwa kwa mganga na mdogo wake hata bila ruhusa yangu.” Mchungaji akatikisa kichwa kusikitika. “Kwanini? Alifuata nini kwa mganga? Na ameambiwa nini huko?” “Ameambiwa eti kuna nadhiri iliyokuwa inawaua watoto wangu.” “Nadhiri gani?” Almasi akabetua mabega yake. “Siijui. Tena mganga amekwenda mbali zaidi. Amemwambia kuwa mauaji yataendelea iwapo mimi sitakwenda kwake.” “Mara nyingi katika kutubu makosa ni lazima uungame makosa yako. Almasi, hebu niambie uliwahi kufanya kosa gani huko nyuma?” “Sikuwahi kufanya kosa lolote.” “Hukuwahi kuwa mshirikina?” “Sikuwahi hata siku moja.” “Kwanini mganga alikwambia uliwahi kuweka nadhiri?” “Ni muongo.” “Umesema kweli. Kazi za uganga zimetawaliwa na uongo na maono ya kishetani. Usiende huko na umkataze mke wako aache kwenda kwa waganga. Yesu ndiyo jibu la kila kitu. Umenielewa?” “Nitamkataza mke wangu na mimi sitathubutu kuingia katika majaribu mengine.” Wakati Almasi anarudi nyumbani, aliyatafakari maneno ya mchungaji wake na kuona yalikuwa sahihi. Tangu mtoto wake wa mwisho alipouawa, alikuwa amemrudia Mungu wake na kuwa muumini mzuri wa kanisa. Lakini bado mambo yalikuwa yakimchanganya kichwani mwake kiasi kwamba aliona akili yake ilikuwa haifanyi kazi kabisa. Akaona si vibaya aende akapate angalau bia moja kuchangamsha akili. Akasimamisha gari mbele ya hoteli moja na kuingia hotelini humo. Aliagiza chupa moja ya bia. Baada ya kunywa bia moja, aliona aongeze ya pili. Akili yake ilipoanza kuchangamka, akaongeza bia ya tatu. “Baada ya hii siongezi tena,” akajisemea moyoni. Lakini baada ya kunywa bia ile, alijikuta akiongeza bia ya nne. “Ewe shetani niachie, hii iwe bia ya mwisho,” akajiambia. Alipomaliza tu kupiga funda la mwisho la bia, akainuka haraka kwenye kiti. Kwa vile alikuwa ameshalipia bia hizo, aliondoka haraka. Alitoka nje ya hoteli, akajipakia kwenye gari lake na kurudi nyumbani. Alipofika nyumbani kwake, alimuita mke wake na kumfokea kutokana na kitendo chake cha kwenda kwa mganga. Maria alikuwa ameshaondoka. Alimwambia alikuwa amekwenda kumshitakia kwa mchungaji wao na akampa ujumbe uliotoka kwa mchungaji huyo kwamba aache kabisa kwenda kwa waganga. Baada ya mke wake kumuomba msamaha, Almasi alikwenda kuketi kwenye kochi. Usingizi ukampitia hapo hapo, akalala fofofo. Ilikuwa kama saa nne usiku alipozinduka. Aliona taa za nyumba nzima zilikuwa zimezimwa. Akatazama saa yake na kuona ilikuwa saa nne usiku. Akajiuliza ni nani aliyekuwa amezima taa. Kabla ya kupata jibu, akasikia sauti ya mwanaume ikiuliza kutoka chumbani mwake. “Wewe ni mke wa Almasi?” Akatega masikio yake kusikiliza. “Ndiyo, mimi ni mke wa Almasi,” sauti ya mke wake ikajibu. “Mume wako alikuweka kama dhamana, lakini umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana,” sauti hiyo ya kiume iliendelea kumwambia. Maneno hayo yakamshitua Almasi. Kutokana na ule ulevi, akataka ainuke ili akimbie, lakini lile giza likamzuia. “Aliniweka dhamana wapi?” akaisikia sauti ya mke wake ikiuliza kutoka chumbani. “Muda wako ndio umeishia hapa. Huwezi kupata jibu.” Hapo hapo akasikia sauti ya mtu anayekoroma. Ghafla akaona taa zinawaka. Ni nani aliyeziwasha? Akainuka kwenye kochi na kupiga hatua za haraka kuelekea chumbani kwake. Aliusukuma mlango akapiga hatua kuingia ndani. Kama angepiga hatua ya pili, angeukanyaga mchirizi wa damu ulioelekea kwenye mlango. Mke wake alikuwa amelala chini hatua chache mbele yake. Kichwa chake kilikuwa kimetenganishwa kabisa na kiwiliwili! “Yesu wangu!” akaguta. Kisha akajisemea: “Mke wangu naye ameshauawa!” Aliogopa kuingia ndani zaidi, akatoka nje ya chumba na kufunga mlango. “Hawa watu wamekuja kumuua mke wangu humu humu ndani!” akaendelea kujisemea huku akipiga hatua za haraka kutoka nje.

MANCHESTER: FORMER manager Pep Guardiola has backed Manchester City’s owners and leadership and says he will “always” be behind the club after they were found guilty of all charges related to breaches of the Premier League’s financial rules. An independent commission found that City arranged “sham contracts” with a number of commercial partners as part…

By Musa Ubandawaki, Sokoto SOKOTO — The Sultan of Sokoto and President-General of the Nigeria Supreme Council for Islamic Affairs, NSCIA, Alhaji Muhammad Sa’ad Abubakar, has called for intensified community action to protect women and children from preventable deaths. The Sultan made the call on Tuesday in Sokoto while declaring open a two-day orientation programme […]

By John Alechenu, Abuja ABUJA — The Economic and Financial Crimes Commission, EFCC, has raised concerns over the deployment of illicit funds, including proceeds from drug trafficking, cybercrime and stolen public funds, to finance elections in Nigeria. The Commission and the Independent Corrupt Practices and Other Related Offences Commission, ICPC, also pledged to intensify efforts […]

SIMBA QUEENS imefuzu kucheza fainali ya Ngao ya Jamii kwa Wanawake baada ya kuichapa Yanga Princess mabao 3-0 katika nusu fainali ya pili iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, na sasa itakutana na JKT Queens Oktoba 3, 2026 kwenye fainali.

UK Prime Minister Andy Burnham has said he would be “really concerned” if Manchester City’s owners decide to sell the club following its guilty verdict over Premier League financial rule breaches.

JKT QUEENS imefanikiwa kutinga fainali ya Ngao ya Jamii kwa wanawake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Queens katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa leo Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.



BAADA ya kukosekana kwa kipindi cha miezi sita, kiungo wa Fountain Gate, Daniel Joram ameanza mazoezi rasmi na kikosi hicho, jambo lililomuibua kocha mkuu wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’ anayefurahia kurejea tena kwa mchezaji huyo.

The Court of Arbitration for Sport (CAS) has fixed October 8, 2026, for the hearing of the dispute between Senegal and Morocco over the outcome of the 2025 Africa Cup of Nations final.

Fulham manager Álvaro Arbeloa has been charged with misconduct by the Football Association over comments he made after his side’s 1-1 draw with Manchester United.

By Davies Iheamnachor PORT HARCOURT — A Federal High Court sitting in Port Harcourt has fixed November 4, 2026, to hear a suit challenging the eligibility of Kingsley Ogundu Chinda to contest the 2027 Rivers State governorship election on the platform of the All Progressives Congress (APC). The suit, marked FHC/PH/CS/3/2026, was instituted by Samuel […]

TAIFA Stars imeingia katika kipindi cha maswali mengi kuhusu uwezo na maandalizi ya kikosi hicho kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, huku wadau wa soka wakibainisha changamoto mbalimbali zinazotakiwa kufanyiwa kazi licha ya Tanzania kufuzu moja kwa moja kwa mashindano hayo kwa kuwa mwenyeji.

MWENGE SC imejiondoa kwenye kundi la timu ambazo hazijapata ushindi katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu huu baada ya juzi kuwachapa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, KVZ bao 1-0.