
SIMBA YAKATA RUFAA TFF KUPINGA UCHAGUZI/MANGUNGU KUCHUKUA FOMU/YANGA LEO KAZI IPO
🔴#LIVE:SIMBA YAKATA RUFAA TFF KUPINGA UCHAGUZI/MANGUNGU KUCHUKUA FOMU/YANGA LEO KAZI IPO ⚫️ OUR PLAYLISTS:
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.

🔴#LIVE:SIMBA YAKATA RUFAA TFF KUPINGA UCHAGUZI/MANGUNGU KUCHUKUA FOMU/YANGA LEO KAZI IPO ⚫️ OUR PLAYLISTS:

UTANGULIZI “Sasa wewe nenda, siku yoyote ukiona una mpango wa kupata mtu nipigie simu” “Sawa. Sasa utakapoifanya hiyo kazi utahitaji kiasi gani?” “Hii kazi ni kubwa na kima changu ni shilingi milioni mojananusu” “Mbona ni kiasi kikubwa sana?” “Ndiyo kima changu na ni kwa sababu nina uhakika kwamba utapata utajiri kwani wengi wamefanikiwa” SASA ENDELEA “Naona una uhakika na kazi yako. Nitakutafutia hiyo pesa kisha nitakupigia simu kukujulisha kama nimepata mtu.” “Sawa.” Amon akarudi Marerani na kuwaeleza wenzake mpango huo wa kutoa mtu kafara ambao wenzake walikubaliana nao. Baada ya siku tatu, mdogo wake Amon, aliyetoka Mwanza na kwenda Dar kumtafuta kaka yake na kumkosa, aliwasili jijini Arusha baada ya kuambiwa kuwa Amon alihamia Arusha. Ili twende pamoja vizuri, hebu tujikumbushe Frenk alivyofika Dar na kisha kwenda Arusha baada ya kuambiwa kaka yake Amon yuko Arusha. …..Daladala ilipomshusha Kariakoo, aliamua kwenda Ilala kwa miguu. Aliutafuta mtaa aliotajiwa. Alipoupata, aliitafuta nyumba ya Amon ambayo namba yake alikuwa ameikariri. Akaipata. Alipoiona nyumba aliyokuwa akiitafuta, alipata furaha iliyochanganyika na mshituko. Alipata furaha kwa sababu aliiona nyumba aliyokuwa akiitafuta, lakini alipata mshituko kuona nyumba yenyewe ilikuwa ya kawaida na si ya kifahari kama alivyoambiwa na baadhi ya watu huko Mwanza. Alibisha kwenye mlango. Mlango ukafunguliwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akitoka na hamsini zake. Frenk akamsalimia. Baada ya salamu, akamuuliza. “Sijui nimemkuta Amon?” “Amon nani?” kijana akamuuliza. “Amon Marwa.” “Oh! Amon aliondoka kwenda Arusha.” “Alienda lini?” “Mh! Muda kidogo, inafika miezi sita.” “Mke wake yupo?” “Alipoondoka, alimuacha mke wake, lakini alishindwa kulipa pango ikabidi aende kwao.” “Kwani Amon alikwenda kufanya nini huko Arusha?” “Siwezi kujua, lakini kuna watu walisema walikuwa wanamkuta kwenye gesti moja jirani na stendi ya mabasi pale Arusha.” Ndoto ya kumpata kaka yake ikayeyuka kichwani mwake kama bonge la barafu lililotiwa kwenye ndoo ya maji. “Kwani hapa Dar alikuwa akifanya shughuli gani?” akamuuliza yule kijana kwa sauti ya kukata tamaa. “Alikuwa akifanya biashara ya duka, lakini alifilisika. Nafikiri labda aliamua akatafute maisha huko Arusha.” Yule kijana akaondoka na kumuacha Frenk akiwa ameduwaa kando ya mlango. Jirani na hapo palikuwa na gesti. Frenk akajikuta akitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika gesti hiyo, ambapo alipanga kuchukua chumba cha kulala baada ya kumkosa kaka yake. Asubuhi kulipokucha, Frenk akapata uamuzi wa kwenda Arusha kuendelea kumtafuta Amon. Alikuwa na imani kuwa huenda alikuwa amefanikiwa huko Arusha na mahali pa kwanza pa kumtafuta ni hapo gesti ambapo aliambiwa alikuwa akionekana. Alipanda basi la asubuhi sana kwenda Arusha. Karibu safari nzima alikuwa akimuwazia kaka yake. Alijiambia endapo atafanikiwa kuonana naye, atakuwa ametimiza lengo lake. Alijua kuwa angeweza kumkuta akiwa na mafanikio au akisaga lapa kama yeye. Lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, alijiambia, kule kukutana kwao tu kungeweza kuwa mwanzo wa mafanikio yao. Alifika Arusha jioni. Aliposhuka kwenye basi, alikwenda kuitafuta gesti aliyoambiwa iliyokuwa jirani na stendi. Baada ya kuulizauliza wenyeji, alielekezwa gesti hiyo. Akaenda kuonana na mhusika. Alipomuuliza kaka yake, aliambiwa walikuwa hawamfahamu. “Alitoka wapi?” kijana wa gesti akamuuliza. “Alitoka Dar kama miezi sita iliyopita. Niliambiwa alikuwa akionekana katika gesti hii.” “Hapa kwetu wanafika watu wengi kutoka Dar, hatuwezi kujua ni nani mmojawapo.” “Nimesema anaitwa Amon.” “Amon wako wengi. Hatuwezi kujua ni Amon yupi unayemuuliza wewe.” “Yeye ni Amon Marwa.” “Yukoje?” “Tuliachana Mwanza tukiwa wadogo. Sijui umbo lake lilivyo kwa sasa. Wakati huo alikuwa ni mwembamba.” “Kwa kweli itakuwa ni vigumu kumtambua.” Baada ya maelezo yake kutosaidia kumtambulisha aliyekuwa anamtafuta, aliamua kukodi chumba hapo hapo. Akajiambia atamtafuta kaka yake kwa siku mbili. Endapo hatafanikiwa kumpata, atarudi Mwanza. Baada ya kupata chumba, akaoga, akabadilisha nguo alizokuwa amevaa, kisha akatoka kwenda katika mkahawa uliokuwa karibu kupata chakula. Baada ya kula, alirudi gesti kulala. Hakukumbuka ilikuwa saa ngapi alipoamshwa usingizini. Kwanza alidhani alikuwa anaota baada ya kusikia mlango wa chumba alichokuwa amelala ukibishwa. Baada ya fahamu kumrudia vizuri, aligundua kuwa hakuwa akiota, bali mlango ulikuwa unabishwa kweli. Akainuka kitandani na kwenda kuufungua. Alimkuta kijana aliyempangisha chumba hapo gesti akiwa na mtu mmoja ambaye alimwambia alikuwa akimfahamu mtu aliyekuwa akimuulizia. “Unamfahamu Amon?” Frenk akamuuliza yule mtu kwa mshituko. “Ndiyo, namfahamu. Aliwahi kukaa hapa gesti kwa muda mrefu, hivi sasa yuko wilaya ya Simanjiro anafanya biashara.” “Sasa nitampataje?” “Mimi naenda huko huko. Kama unataka twende, nitakupeleka mahali aliko.” “Kweli tutapata usafiri usiku huu?” “Nina gari yangu binafsi, tunaweza kwenda tu.” “Basi subiri nivae twende.” Frenk akarudi ndani. Alivaa nguo haraka haraka, akachukua begi lake na kutoka. Yule mtu alikuwa akimsubiri ukumbini. “Twenzetu,” akamwambia. Walitoka nje ya gesti, ambapo palikuwa na gari aina ya Noah iliyoegeshwa. Ndani ya gari hilo kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa amekaa siti ya nyuma. Frenk aliambiwa akae siti ya mbele kando ya dereva. Akafungua mlango na kujipakia. Yule mtu naye alikaa katika siti ya dereva, akaliwasha gari na kuanza safari ya kuelekea wilaya ya Simanjiro. “Mimi naitwa Rafael, je, wewe mwenzangu unaitwa nani?” mtu huyo alimuuliza Frenk baada ya kimya kifupi. “Mimi naitwa Frenk.” “Huyu Amon ni nani wako?” “Ni kaka yangu. Tuliachana zamani sana huko Mwanza.” “Alikuja hapa Arusha miezi sita iliyopita. Hivi sasa anaishi Simanjiro na amefanikiwa sana kimaisha.” “Nitafurahi sana kumuona kaka yangu. Uliniambia kuwa mnafahamiana?” “Tunafahamiana na tunahisi jirani. Wewe hujawahi kufika hapa Arusha?” “Sijawahi kufika.” “Na huko Simanjiro ndiyo hukujui kabisa?” “Kwa kweli huko sikujui.” “Basi leo utakujua.” “Nitafurahi.” Safari ikaendelea. Gari hilo liliwasili Simanjiro saa nane usiku. Lilisimama mbele ya nyumba moja, ambapo aliyekuwa akiendesha alishuka akaenda kubisha mlango. Baada ya muda kidogo, mlango ulifunguliwa, mtu huyo akaingia ndani. Haikupita muda mrefu, akatoka akiwa na mwenzake aliyekuwa ameshika begi. Mwenzake alijipakia katika siti ya nyuma. Akakaa na Frenk. “Vipi bwana?” akamuuliza Frenk. “Salama tu.” Gari likawashwa moto na kuendelea na safari. “Hivi sasa tunakwenda nyumbani kwa Amon,” aliyekuwa akiendesha alimwambia Frenk. “Nimbali sana kutoka hapa?” “Hapana. Ni karibu tu.” Baada ya mwendo mfupi, walivuka daraja, wakaingia katika barabara za vichochoro. Walitokea katika eneo ambalo lilikuwa na pori. Baada ya kulipita pori hilo, gari likasimama ghafla karibu na kichaka. Aliyekuwa akiendesha alisonya kisha akafungua mlango. “Hili gari limeshaanza matatizo. Limezima ghafla,” alijisemea kabla ya kushuka na kwenda mbele ya gari hilo, ambapo alifungua boneti la mbele. Wenzake waliokuwa katika siti ya nyuma nao walishuka na kumfuata. Frenk alipoona amebaki peke yake ndani ya gari, naye alishuka. Alikwenda mbele ya gari hilo kulikokuwa na wenzake waliokuwa wakilikorokocha gari hilo. “Lina tatizo gani?” Frenk akauliza. Mtu aliyekuwa karibu yake aligeuka ghafla na kumpiga kwa kitu kizito kichwani. Frenk alipiga yowe akaanguka hapo hapo akiwa amepoteza fahamu. Mtu aliyempiga aliinama, akamshika mikono na kumburuza kwenye kichaka kilichokuwa pembeni mwa njia. Alimuingiza ndani ya kichaka hicho, akamlaza chini. Wenzake walimfuata. Yule aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ameshika begi ambalo aliliweka chini. Alitoa simu kutoka mfukoni mwake akaipiga. Baada ya muda kidogo, simu yake ilipokelewa. “Tumeshampata yule mtu na tuko naye hapa njia panda ya kuja Marerani. Sasa njoo mara moja tumshughulikie,” akasema kwenye simu. “Ni kijana?” sauti ikauliza kutoka kwenye simu. “Bado ni kijana sana na ana umbile lililotakiwa.” “Mmemfunga sawasawa?” “Samueli amempiga kichwani kwa kitako cha bastola, amezirai.” “Sasa mmemfunga? Akizinduka anaweza kuleta usumbufu.” “Sawa, tutamfunga kamba mikononi na miguuni.” “Mkishamfunga, mnisubiri hapo hapo.” “Sawa.” Yule mtu aliirudisha simu yake mfukoni, akachutama na kufungua lile begi. Alitoa furushi la kamba, akawapa wenzake. “Mfungeni kamba miguuni na mikononi. Jamaa anakuja sasa hivi.” Watu hao wakachukua lile furushi la kamba na kulichakua. Zilikuwa kamba nyingi ambazo zilikuwa vipande vipande. Walichukua vipande hivyo vya kamba, wakamfunga Frenk mikononi na miguuni. “Sasa tusubiri hapa hapa,” yule aliyekuwa akiendesha gari aliwambia wenzake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

TIMU ya Hope City Deaf imefunga msimu kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Viziwi Zanzibar katika fainali iliyochezwa Oktoba 3, 2026 kwenye Uwanja wa Mao, Unguja.

MAKOSA ya kipa Ali Athumani, yameigharimu Mafunzo baada ya timu hiyo kuendelea na mfululizo wa matokeo mabaya katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

MSHAMBULIAJI wa Muembe Makumbi City, Bactash Ali Bakari, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

MSHAMBULIAJI Clara Luvanga leo ana kibarua Marekani, wakati klabu yake ya Washington Spirit ikiikabili Houston Dash katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (NWSL) itakayopigwa kwenye Uwanja wa Audi Field.

MSHAMBULIAJI Mtanzania, Waziri Junior Shentembo anayekipiga Mombasa United ya Ligi Kuu Kenya amesema ligi ya nchi hiyo haina tofauti kubwa na ya nyumbani Tanzania.

KIUNGO mshambuliaji wa Tanzania, Ben Starkie anayekipiga Truro City FC inayoshiriki Ligi Daraja la Sita England (National League South) ameanza na mguu mzuri kwenye kikosi cha timu hiyo hiyo baada ya msimu jana kukaa nje msimu mzima.

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Kahramanmaras inayoshiriki Ligi Kuu ya Walemavu Uturuki, Ramadhan Chomelo ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kuwekeza kwenye soka la walemavu ili kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi kuonyesha vipaji vyao.

DAR ES SALAAM; Tanzania imeanza kutumia maandalizi ya mashindano ya AFCON kama fursa ya kujitangaza kimataifa, ikilenga kuvutia watalii na wadau wa michezo kupitia wageni kutoka nje wanaotembelea nchini. Mkakati huo umejidhihirisha baada ya kundi la waandishi wa habari, watu mashuhuri na watengeneza maudhui kutoka mataifa mbalimbali kutembelea Tanzania kwa ajili ya kushuhudia maandalizi ya…

Timu ya FC 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo sasa itakutana na Simba.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufutwa kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Morocco.

Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar na Stand United zimeibuka na ushindi wa bao 1-0 kila moja leo Oktoba 3, 2026 unaoziweka katika nafasi nzuri kwenye ushindani wa Ligi ya Championship msimu huu.

South Korea's Asian Games football captain apologised on Sunday for boasting that his gold medal meant he did not have to do military service.

MOROGORO: MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala ametoa hamasa kwa wanawake nchini ambao ni madereva kujitokeza kwa wingi kushiriki mchezo wa mashindano ya mbio za magari kama ilivyo kwenye michezo mingine ili kuleta ushindani . Kilakala ametoa wito huo wakati akizundua mashindano ya mbio za magari ya Serengeti Rally Tanzania 2026 yaliyoanza Oktoba Mosi…

DAR ES SALAAM: SOMEWHERE in Wekundu wa Msimbazi’s extended family, elders have reportedly turned to prayer, asking that Ibrahim Doumbia start scoring. I support this initiative, provided the application specifies several goals. One would merely give football radio six hours to establish whether he intended it, slipped, or received assistance from ancestral wind. Please also…

The Economic Community of West African States (ECOWAS) says it will deploy youth observers alongside its traditional election observation missions to monitor Nigeria’s 2027 general elections. Serigne Ka, Head of the ECOWAS Electoral Assistance Division, disclosed this in Abuja at the fifth edition of the Sectoral Reflection Series on Elections and Democracy, organised by the […]

By Hassan Karofi Under the visionary leadership of Dr. Rahila Aliyu Mukhtar, Executive Secretary of the Kano State Contributory Healthcare Management Agency (KSCHMA), Kano State is setting a new benchmark for healthcare innovation and service delivery. Through the successful deployment of a digitised service utilisation portal across Primary Healthcare Centres (PHCs) and the introduction of […]

By Kingsley Omonobi The Inspector-General of Police, Olatunji Rilwan Disu, has deployed the Deputy Inspector-General of Police in charge of Operations, DIG Shehu Umar Nadada, to Imo State to coordinate the rescue of prospective National Youth Service Corps (NYSC) members and other passengers abducted along the Owerri-Onitsha Expressway on Thursday, October 1, 2026. The Force […]

By Dayo Johnson, Akure Ondo State Governor, Lucky Aiyedatiwa, has assured corps members deployed to the state of a safe, peaceful and conducive environment throughout their one-year national service. Aiyedatiwa gave the assurance during the swearing-in ceremony for the 2026 Batch ‘C’ Stream I corps members deployed to Ondo State, held at Ikare-Akoko. Represented by […]

The Inspector-General of Police (IGP), Olatunji Disu, has deployed the Deputy Inspector-General of Police in charge of Operations, DIG Shehu Nadada, to Imo State to coordinate the rescue of the prospective National Youth Service Corps (NYSC) members and other passengers abducted along the Owerri-Onitsha Expressway on Thursday, 1 October 2026.

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 (U23), Hamad Ally, ameweka wazi kuwa benchi lake la ufundi na wachezaji wamefanya tathmini ya kina ili kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu AFCON U23 dhidi ya Kenya.

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 (U23), Hamad Ally, ameweka wazi kuwa benchi lake la ufundi na wachezaji wamefanya tathmini ya kina ili kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu AFCON U23 dhidi ya Kenya.

NAHODHA msaidizi wa Singida Black Stars, Ahmed Bakari Pipino amesema kwa ushindani uliopo katika timu hiyo, umeendelea kumjenga na kupanda levo za kiuchezaji, huku akimsifu kiungo wa zamani wa Simba na Yanga Jonas Mkude.

SIMBA Queens imerejesha heshima na kutawazwa mabingwa wapya wa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa JKT Queens bao 1-0 kwenye fainali iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex jioni hii.

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Ndumumwe raia wa Burundi ambaye kwa sasa anaichezea MC Algiers ya Algeria aliyojiunga nayo Agosti 7, 2026, amesema kwa muda aliyocheza Ligi Kuu Bara, kaviona vipaji vikubwa vya wazawa ambao wakiamua kutoka nje, watafanya makubwa.


The Premier League released a statement on Tuesday saying Manchester City committed serious breaches during a nine-season period between 2009/10 and 2017/18.



Mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere, amewabariki waendesha baiskeli wanaoshiriki Nyerere Cycling Tour, safari inayolenga kuunganisha mchezo huo na shughuli za kijamii.

KIPA Molly Nabitaka ameibuka shujaa wa Yanga Princess baada ya kuokoa penalti moja na kuifanya timu hiyo kutwaa mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii kwa Wanawake kwa kuifunga Mashujaa Queens kwa mikwaju 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo.

MAMBO yameharibika! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema, kubwaga manyanga ghafla na kuacha benchi la ufundi la timu hiyo katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii unaoendelea leo hii Uwanja wa KMC Complex.

By Joseph Erunke, Abuja The Federal Government has introduced a digital system for selecting recipients of the 2026 President’s Teachers’ and Schools’ Excellence Awards, replacing the manual process used in previous years. The new system, according to the government, is aimed at improving transparency, accountability and documentation in the identification and recognition of outstanding teachers […]

MWANAMKE pekee Afrika anayeshiriki mashindano ya African Rally Championship 2026, Susan Muwonge, amesema amejiandaa kikamilifu kuingia kwenye ushindani na madereva wa kiume na kuhakikisha anapata ushindi.

Former Nigeria international and one time assistant coach of the Super Eagles, Sylvanus Okpala said the Super Eagles display against Guinea-Bissau was the worst he had witnessed in a long while.

By Sola Ogundipe For men undergoing surgery for prostate cancer, removing the tumour may solve the immediate threat, but it can leave behind another deeply personal problem: erectile dysfunction. Researchers are exploring an unusual way to help sexual function return. The approach, according to a publication in New Scientist, involves placing thin sheets of dehydrated […]

DAR ES SALAAM: Tanzania imeendelea kutumia fursa ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kujitangaza kimataifa kupitia kampeni ya Destination Tanzania, kwa kuwaalika wanahabari na watengeneza maudhui kutoka mataifa mbalimbali kutembelea na kujionea vivutio vya utalii, utamaduni pamoja na maandalizi ya nchi kuelekea michuano hiyo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,…

DAR ES SALAAM: TANZANIA is continuing to use the Africa Cup of Nations (AFCON) as an opportunity to promote the country internationally through the Destination Tanzania campaign, under which it has invited journalists and content creators from various countries to experience first-hand the country’s tourism attractions, culture and preparations for the tournament. Permanent Secretary in…

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka wazi kwamba sio wachezaji wa Yanga pekee waliopo kwenye kikosi Cha Taifa Stars walioruhusiwa kuondoka kwenye kambi hiyo nchini Morocco.

Computer hacker Rui Pinto, the man behind the Football Leaks website which helped trigger the Premier League probe into Manchester City's finances, faces "dire consequences" after having his protected witness status removed, his lawyers said on Friday.

Thomas Tuchel said that Manchester City were the talk of the England camp after the club were found guilty of multiple breaches of Premier League financial rules, but insisted that the case would not affect his selection for Saturday's match in Croatia.

FAINALI ya Ligi ya Viziwi Zanzibar kati ya Hope Deaf City na Wakombozi, itachezwa kesho Jumamosi jioni, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein.

ARUSHA: THE construction and upgrading of roads linking various areas to the AFCON stadium in Arusha has reached more than 60 percent, in a move aimed at improving transport and boosting economic activities in areas surrounding the stadium. The project, being implemented by the Tanzania Rural and Urban Roads Agency (TARURA), involves the construction and…



KIUNGO Pacome Zouzoua, amepiga hatua ya pili ya uponaji wake wa jeraha la kifundo cha mguu ambapo sasa ameacha kutembea kwa msaada wa magongo.

WAKATI Dabi ya Kariakoo ikizidi kusogea, Yanga imeanza kusuka mipango ya kuongeza makali ambapo leo Jumamosi itakabiliana na wanajeshi wa JKT Tanzania.

KIKOSI cha vijana chipukizi cha Zanzibar Spice Boys, chenye wachezaji 18 wenye umri wa miaka 12 na 13, kinajiandaa kwenda Brazil kushiriki mashindano ya kimataifa ya soka la watoto yaliyopewa jina la PQ CUP BRASIL 2026.