
SAMIA: WEKA MAZINGIRA SAFI KWA AJILI YA AFCON
SAMIA: WEKA MAZINGIRA SAFI KWA AJILI YA AFCON🔥 #globaltv #breaking #samiabraham
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.

SAMIA: WEKA MAZINGIRA SAFI KWA AJILI YA AFCON🔥 #globaltv #breaking #samiabraham

TRA United imeingia mapumziko ya Ligi Kuu Bara ikiwa na sura mpya baada ya kumpa mikoba Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’, ambaye sasa anasema kikosi chake kipo tayari kurejea kwenye mashindano na kupigania malengo yake, akiamini mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu unaweza kuipa timu hiyo nguvu ya kufanya vizuri.

MBIO za kuwania tuzo ya Kipa Bora msimu wa 2026-2027 zipo kwenye hatua ya kuvutia zaidi baada ya matokeo kuweka safu ya makipa hao katika ushindani wa karibu.

KIUNGO mshambuliaji wa Chipukizi, Daddy Francis amesema sababu kubwa inayofanya timu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri ni mfumo ambao unacheza timu hiyo.

ZIMAMOTO na Polisi, zimeonekana kuwa na makali zaidi katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuwa timu pekee hadi sasa ambazo hazijapoteza mechi.

KOCHA Bora Martin Stephan Chirwa wa mashindano ya Dar Youth League U-15 yaliyomalizika jana katika viwanja vya Gymkhana kwa Simba Youth U-15 kuchukua ubingwa mbele ya Bulls Football Academy amesema yamekuwa na ushindani mkubwa kuwapa makocha na wachezaji nafasi ya kujifunza, kuonyesha uwezo na kupima maendeleo.

The agreement is expected to provide a clearer framework for mobilisation and deployment of standby forces for peace and security operations in Africa.

The NFF’s complaint questioned the clearance of several foreign-born players, including Mpasi, and alleged that the Congolese federation had misled FIFA in securing their eligibility.

UTANGULIZI Baada ya nusu saa tu, magari mawili ya polisi yakawasili nyumbani kwa Almasi. Vile polisi walivyoambiwa kwamba wauaji hao walikuwa wamefungiwa kwenye chumba, walikuja polisi tisa. Watano wakiwa na bunduki. Inspekta Amour, ambaye huvaa kiraia, alikuwa wa kumi. Almasi aliwakaribisha. “Hao watu wamo ndani?” Amour akamuuliza akiwa ameshika bastola mkononi. “Niliwafungia chumbani mwangu na sijafungua mlango hadi sasa.” SASA ENDELEA HEBU fungua tuingie ndani. Mazungumzo ni baadaye” Almasi akafungua mlango. Polisi hao wakaingia ndani pamoja na Almasi. Alifngua mlango wa ndani. Akawapeleka kwenye mlango wa chumba chake. “Mauaji yamefanyika ndani ya chumba hiki. Mke wangu yumo humu ndani na hao watu niliwafungia humu humu” “Sasa fungua huo malango” Amour akamwambia. Almasi akatoa fungua na kufungua mlango. Amour alipojaribu kuusukuma mlango, aligundua kuwa mlango huo ulifungwa kwa nadani. “Mlango umefungwa kwa ndani” akasema. “Basi bado wamo” Almasi akamwambia. Amour akaanza kugonga mlango. Aliugonga kwa sekunde kadhaa akiwataka watu waliomo ndani ya chumba hicho wafungue mlango na kujisalimisha kwa polisi. Lakini hakukuwa na jibu lolote lililotoka. “Kama hawakutii amri ya polisi, sasa nalazimikakuvunja mlango” Amour akamwambia Almasi. “Vunja” Amour alimwambia polisi mmojawapo aliyekuwa na bunduki apige risasi zile sehemu za bawaba ili kuung’oa mlango huo. Risasi tatu za SMG zikauondoa mlango huo mahali pake. Mlango ulipokuwa umevunjwa, Amour alipiga risasi mbili za bastola humo chumbani akilenga chini ya ardhi kabla ya kuruka ndani ya chumba hicho akiwa na bastola yake mkononi. Alipotua chini akiwa katikati ya chumba hicho aliishikilia bastola yake sawasawa na kuielekeza pande zote za chumba hicho kwa haraka haraka. Kitendo cha kufyatua risasi mbili na kisha kurukia ndani ya chumba hicho kilikuwa ni cha kuwafanya watu waliokuwemo ndani ya chumba hicho, kama walikuwemo kweli, wagwae na aliruka ili kuwashitukizia. Lakini alipotupa macho pande zote za chumba hicho hakuona watu wowote zaidi ya mwili wa mke wa Almasi uliokuwa umelala chini pembeni mwa kitanda. “Hebu lete tochi” alisema huku akiinama mvunguni mwa kitanda. Polisi ambao walikuwa hawajaingia, waliingia na mmojawapo alimpa tochi Amour. Amour aliipokea tochi na kumulika chini ya mvungu. “Hakuna kitu” alisema. Akainuka na kumtazama Almasi. “Mbona hatuwaoni hao watu?” “Walikuwemo humu ndani nikawafungia” Almasi alisema huku akitupa macho yake huku na huku. “Kama wametoka, wametoka kwa wapi wakati mlango uliufunga kwa nje?” Almasi alitikisa kichwa kuonesha mshangao. “Hapo ndio sielewi” “Watakuwa ni watu wa miujiza” “Tangu mwanzo wameonekana kuwa watu wa miujiza” “Hatuoni sababu ni kwanini wamekuandama wewe peke yako!” “Na mimi najiuliza swali hilo kila siku” “Ni lazima jibu lipatikane. Hatuwezi kushuhudia hali hii ikijitokeza mara kwa mara” “Nimeshajitolea sadaka. Kama kuna aliyebaki kufa ni mimi mwenyewe. Sihitaji tena kuwasumbua polisi. Nimewaita tu kwa sababu ndio utaratibu wa kisheria kuwafahamisha polisi linapotokea tukio kama hili la mauaji” “Sisi hutusumbui, tunatekeleza jukumu letu. Na vile vile hupaswi kusema kuwa umejitolea sadaka. Ni lazima polisi tutimize wajibu wetu wa kukulinda wewe” Almasi hakusema kitu tena kwa vile alishajua sababu ya kuuawa kwa wanawe na mke wake. Polisi wakaanza kushughulika. Hatimaye mwili wa mke wa Allmasi ulitolewa ukapakiwa kwennye gari na kupelekwa hospitali. Almasi alitakiwa afike kituo cha polisi kuandikisha maelezo yake. Wakati Almasi anatoka, mdogo wa mke wake pamoja na kaka zake wawili wakafika. Walikutana kwenye geti. “Shemeji unakwenda wapi?” mmoja wa kaka wa mke wake aliyeitwa Samson akamuuliza baada ya kushuka kwenye gari. “Nakwenda kituo cha polisi” “Tumepata taarifa sasa hivi kutoka kwa mdogo wetu Maria kuwa mke wako ameuawa, ni kweli?” “Ni kweli, ndio ninakwenda kituo cha polisi kuandikisha maelezo” “Mwili wake umo ndani?” “Umechukuliwa na polisi sasa hivi” “Unaweza kutueleza sababu ya kuuawa kwa dada yetu na kututajia watu waliomuua?” “Mbona mnauliza kama vile kuna ugomvi. Hili suala liko mikononi mwa polisi…” “Kuna maneno ambayo umemueleza Maria, yametupa taharuki” “Maneno gani?” “Yale ambayo ulimueleza kwenye gari na baadaye ukamfukuza kwenye gari lako na kumuacha atembee kwa miguu usiku huu” Almasi akajifanya anatikisa kichwa kusikitika. “Jamani mmekuja kwenye msiba au mmekuja kwenye kesi?” “Tumekuja kwa vyote kwa sababu si uungwana kumfukuza shemeji yako kwenye gari usiku huu baada ya kukueleza kuwa umemuua dada yake!” “Sasa ni kwanini yeye aniambie kuwa nimemuua mke wangu?” “Kutokana na maelezouliyomueleza wewe mwenyewe kwamba ulimtoa kafara yeye na watoto wako” Almasi akatikisa kichwakukataa. “Sijamwambia kuwa nimemtoa kafara mke wangu na watoto wangu. Mimi si kichaa. Inaonekana huyu mdogo wenu si muelewa” “Sasa tueleze wewe ni nani aliyemuua mke wako na kwanini alimuua?” “Mimi sijui ni kwanini aliuawa ila najua kuwa aliuawa huu usiku. Hii kesi iko mikononi mwa polisi. Labda watakapomaliza uchunguzi wao watatueleza” “Wewe si umenieleza kuwa umeambiwa na mganga kwamba uliweka masharti kwa maganga wako ambayo hukuyatimiza na hivyo kusababisha watoto wako na mke wako wauawe na wewe ulikubali?” Maria akamwambia Almasi. “Sasa mimi siwezi kushika maelezo ya mganga. Huko kwa mganga ulinipeleka wewe na wala siamiiini kile nilichoambiwa. Cha msingi hapa ni kuendelea na msiba. Baada ya kumzika marehemu tutaweka kikao tuongelee mambo mengine lakini simu muda huu. Mimi nahitajika polisi” “Kaka tumsusie huyu marehemu, azike mwenyewe. Huyu shemeji ni mshirikina sana. Huyu ndiye amemuua dada. Ameniambia yeye mwenyewe. Hivi sasa amewaona nyinyi anabadilisha maneno” “Sasa unasikia shemeji, sisi tumeamua kukuachia huyu marehemu kwa sababu hutaki kutupa maelezo ya kuridhisha ni kwanini ameuawa na nani amemuua. Tunaamini kama anavyotueleza Maria umemuua wewe!” “Sasa hiyo ni akili gani? Mnashika maneno yaMaria! Mnasusia maiti ya dada yenu kwa kushika maneno ya Maria? Nimeshawambia uchunguzi unafanywa na polisi. Kama mnataka maelzo zaidi, nendeni mkawaone polisi watawaeleza” Almasi alipowambia hivyo shemeji zake hao waliingia kwenye gari walilokwenda nalo na kuondoka bila kuaga. “Potelea mbali. Kama ni kumzika maremehu nitamzika mwenywe. Nendeni” Almasi akajisemea peke yake. Na yeye akaingia kwenye gari lake na kuondoka. Alipofika kituo cha polisi akalikuta gari la shemeji zake likiwa nje ya kituo. Alipoingia ndani ya kituo hicho akakutana na watu hao wakizungumza na Inspekta Amour. Walipomuona akiingia walikatisha mazungumzo. Amour akamwambia Almasi. “Nimepokea mashitaka yako” “Mashitaka gani?” “Kwamba watoto wako pamoja na mke wako wameuawa kwa sababu za kishirikina” “Sasa ushirikina upi nilioufanya?’ “Ni ushirikina ambao uliufanya kwenye madini miaka iliyopita. Shemeji zako wanadai kuwa hukutimiza mashrti ya waganga na hivyo kusababisha watoto wako pamoja na mke wakokuuawa na majini” Almasi akatikisa kichwa. “Si kweli. Mimi nawaomba polisi muendelee na upelelezi wenu. Habari hizi za kishirikina muachane nazo” “Ni kweli kwamba hatuchunguzi kadhia zenye mtazamo huo na wala madai hayo hayawezikutufanya tukufungulie kesi lakini mazingira ya yale mauaji yanatisha. Kwa mfano wale watu waliomuua mke wako uliwafungia ndani lakini tulipovunja mlango hawakuwemo ndani!” Maria alliposikia hivyo akachachamaa. “Sasa ulikataa nini wakati hata polisi wammeona jinsi hao watu walivyotoweka. Bado utasema si ushirikina wako uliomuuua dada yangu?’ Kaka zake nao wakaingilia. Ikawa mzozo ndani ya kituo cha polisi, ikabidi Inspekta Amour aingilie kati kuwasuluhisha nakuwaweka sawa mpaka wakakubalina kwamba washirkiane kumzika marehemu na baada ya hapo waweke kikao kuzungumzia tatizo lililotokea lakini wazingatie ripoti ya uchunguzi itakayotolewa na polisi. Baada ya muafaka huo, shemeji zake Almasi waliondoka na kumuacha Almasi akiandikisha maelezo yake. Baada ya hapo akaondoka. Aliporudi nyumbani kwake aliwapigia simu jamaa zake na rafiki zake na kuwajjulisha kuhusu msiba wa mke wake. Lengo lake lilikuwa kupata watu wa kulala naye pale nyumbani. Alikuwa ameingia uoga wa kulala pake yake. Alihisi kama vile wauaji hao watamfuata usiku na kummaliza na yeye kama alivyoambiwa na mganga kwamba ilibaki roho yake kutoka. Saa chache baadaye, jamaa na marafiki aliowapigia simu wakaanza kufika nyumbani kwake na kumfariji. Alipata watu ambao alilala nao hadi asubuhi lakini shemeji zake hawakufika.

DAR ES SALAAM: NATIONAL U-23 football team face a massive test at Uhuru Stadium today as they attempt to overturn a 4-1 first-leg defeat to Kenya and keep their hopes of reaching the 2027 Africa Cup of Nations alive. The Under-23s arrive at the return leg three goals behind, but head coach Ahmad Ally insists…

Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Ahmed Arajiga, amepewa jukumu la kuongoza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Star Sport Academy ya Sierra Leone na RS Berkane ya Morocco utakaochezwa Oktoba 17.

The three countries in August signed the Mecca Joint Defence Agreement committing them to come to each other's aid in the event one were attacked.

The 25 finalists for the 2026 Golden Boy Award have been announced, with Barcelona defender Pau Cubarsi, Real Madrid’s Yan Diomande, Manchester City’s Ayyoub Bouaddi, Chelsea forward Estêvão Willian, and Bayern Munich youngster Lennart Karl among the leading names on the list.

By John Alechenu, Abuja The Labour Party, LP, has promised to build a Nigeria where teachers are respected, adequately rewarded and equipped to shape the nation’s future. The party said it will replicate the Abia State model nationwide if voted in 2027. In a World Teachers’ Day message on Monday signed by its National Publicity […]

MOROGORO: DEREVA mzoefu Karan Patel na mwongozaji wake Tauseef Khan wameweka rekodi nyingine kwa kuiwakilisha nchi yao kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya tatu wa Afrika Rally Championship katika mashindano ya mbio za magari za Serengeti Rally of Tanzania. Mahindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 yamefanyika kwa siku nne hadi 4,2026, kwenye Shamba…

“These tools can help teachers reach learners and tailor instruction, but the judgement, encouragement and human connection of a skilled teacher remain indispensable,” he said.



UONGOZI wa Yanga Princess umeanza rasmi mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Edna Lema ambaye alijiondoa kikosini hapo baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya watani zao Simba Queens kwenye mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwa wanawake.

KOCHA wa Singida Black Stars, Papy Kimoto amesema ameridhishwa na namna kikosi chake kilivyoimarika baada ya kupata muda wa kutosha kuingiza falsafa yake mpya kwa wachezaji.

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema winga wa timu hiyo, Elizabeth Wambui anaendelea kuimarika na wanatarajia atarudi uwanjani baada ya mechi za mzunguko wa pili wa Ligi ya Wanawake unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

LEO saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya U-23 itakuwa na dakika 90 ngumu dhidi ya Kenya kwenye mechi ya marudiano kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana mwakani Misri.

KOCHA wa muda wa timu ya Taifa ya Zambia, George Lwandamina,amesema awali alikuwa na wasiwasi kuhusu Albert Kangwanda alipokwenda Yanga, lakini kiwango alichoonyesha tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania kimemfanya abadili mtazamo wake.

SIMBA imerejea nchini ikitokea Afrika Kusini ilikoweka kambi yake ya siku 10 kujiandaa na mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, sasa beki na nahodha wa timu hiyo Rushine De Reuck amenyoosha maelezo juu ya mchezo huo.

By Kingsley Omonobi Troops of Sector 2, Operation Fansan Yamma, deployed in Anka Local Government Area of Zamfara State, have rescued persons abducted by armed terrorists along the Anka–Gadan Manya Road. The rescue followed a swift response by the troops to an attack on travellers along the route, according to the Nigerian Army. The Army […]

Norway manager Stale Solbakken has raised concerns over Erling Haaland’s workload, saying the Manchester City striker is among players carrying the heaviest burden in his team and has been showing signs of fatigue after a relentless run of matches for club and country.

DAR ES SALAAM. TANZANIA imepata kibali FIFA kuendelea kutumia mfumo wa msaada wa video kwa waamuzi (Football Video Support (FVS), huku Ligi Kuu ikitajwa kuwa ya kwanza duniani kutumia mfumo huo kwa utaratibu uliokubaliwa na Shirikisho hilo la Kimataifa la Soka (FIFA). Akizungumza Dar es Salaam leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania,…

UTANGULIZI Miaka kadhaa ikapita. Mwisho akasahau kabisa kama kuna masharti alipewa na ameacha kuyatekeleza. Ndipo siku moja mtoto wake wa kwanza aliyemuita Martin alipovamiwa na watu watatu wa ajabu, akachinjwa na kunyang’anywa mkoba wa pesa…. Sasa Almasi akiwa kwa mganga waliyemwendea yeye na Maria alitingisha kichwa chake taratibu baada ya kuwaza. “Nimekumbuka kitu…” akamwambia mganga kwa sauti iliyonywea. SASA ENDELEA “Enhe… nieleze umekumbuka kitu gani?” mganga akamuuliza. Almasi akamtazama Maria na kumuomba atoke nje ya kile chumba. Maria akatoka. Almasi akamwambia mganga. “Mimi nilikuwa mchimbaji wa madini. Nikashauriwa na wenzangu kwamba ili nipate madini ya kutosha niende kwa mganga. Nikaenda kwa mganga mmoja wa Korogwe ambaye alinifanyia uganga wake, lakini ulikuwa na masharti…” Almasi aliendelea kumweleza mganga huyo jinsi alivyotakiwa na mganga huyo kumtoa mtu kafara ili apate utajiri wa madini, na yeye akafanya hivyo. “Ni masharti gani ambayo alikupa?” “Aliniambia kila mwaka nitoe robo ya mapato yangu, niyamwage baharini.” “Ulifanya hivyo?” “Nilifanya mara moja, halafu sikufanya tena.” “Ni miaka mingapi sasa tangu uache kutimiza hilo sharti?” “Ni miaka mingi.” Mganga alichungulia kwenye mdomo wa tunguri aliyokuwa ameiweka mbele yake, kisha akamwambia Almasi. “Unajua maana ya mganga kukwambia uwaweke watoto wako na mke wako kama dhamana?” Almasi akatikisa kichwa. “Sijui.” “Maana yake ni kwamba kama hutatimiza masharti uliyopewa, watawajibishwa wao. Ndiyo maana wale waliokuwa wanakuja kuwaua walikuwa wanawaambia, ‘Baba yenu aliwaweka kama dhamana na mmeshindwa kutimiza masharti ya dhamana.’” Almasi akatikisa kichwa kwa kusikitika kabla ya kuuliza. “Wale watu ni kina nani kwani?” “Wale wawili wanaovaa mavazi meupe ni majini waliotakiwa kupewa hiyo robo ya mapato yako kila mwaka, na yule aliyevaa nguo nyeusi ni mdogo wako ambaye ulimchinja. Na ndiyo maana unaambiwa kuwa shingo yake imechinjwa na kichwa chake kinaning’inia.” Almasi akashituka. “Niliyemchinja alikuwa mdogo wangu?” akauliza. “Ndiyo, alikuwa mdogo wako. Alikwenda Arusha kukutafuta wewe.” “Anaitwa nani?” “Mimi siwezi kukutajia jina lake, lakini kumbuka ni ndugu yako gani ambaye umepoteana naye kwa miaka mingi.” “Sisi tulizaliwa wawili tu, mimi na mdogo wangu anayeitwa Frenk.” “Huyo Frenk yuko wapi?” “Sijui yuko wapi.” “Mdogo wako humjui yuko wapi?” “Tulipoteana miaka mingi.” “Hamjakutana kwa miaka mingapi sasa?” “Miaka mingi.” “Sasa nakwambia ndiye huyo ambaye amechinjwa.” “Mama yangu, sikujua kama yule alikuwa mdogo wangu. Wenzangu ndiyo waliomkamata na kumchinja. Kumbe alikuwa Frenk!” “Sasa dhambi yake umeiona. Na wewe watoto wako wote wamekwisha.” Almasi aliendelea kutikisa kichwa. “Sikujua… sikujua… sasa nifanye nini jamani?” “Umechelewa. Hivi sasa huna la kufanya.” Almasi akamtumbulia macho mganga huyo. “Unasemaje?” “Nimekwambia kwamba umechelewa.” “Nimechelewa nini?” “Kuchukua uamuzi.” “Uamuzi gani sasa?” “Uamuzi wa kunusuru.” “Nitakwenda kutupa baharini zile pesa.” Mganga akatikisa kichwa. “Umechelewa. Hao majini wana hasira na huwezi kuwatuliza tena. Wanachotaka ni roho tu.” “Roho ya nani sasa?” “Roho yako wewe!” Almasi aliposikia maneno hayo kwamba hao majini waliompatia huo utajiri wana hasira na wanachotaka sasa ni roho yake tu, alimtolea macho mganga huyo. Akamtazama kwa sekunde kadhaa akiwa ametaharuki, kisha ghafla aliinuka na kutoka mle chumbani bila kuaga. Alimwambia shemeji yake, mdogo wa marehemu mke wake. “Twende zetu.” Walitoka na kujipakia kwenye gari. Aliliwasha gari hilo huku akijisemea. “Mganga amenitisha sana.” “Amekwambiaje?” “Ameniambia wanachotaka hao majini ni roho yangu tu!” “Majini gani hao?” Almasi aliliondoa gari kwa kasi. “Kumbe wewe hukuwepo wakati tunazungumza.” “Si uliniambia nitoke ili nisisikie mnachozungumza?” “Nilikwambia vile kwa sababu. Lakini hayo tuyaache. Zamani nilikuwa ninachimba madini. Na unajua wanaofanya kazi ile mara nyingi hupendelea kwenda kwa waganga, na mimi nilikwenda. Nikafanyiwa kafara na kuambiwa kwamba nitakapopata mali, kila mwaka nikatose baharini robo ya pesa za mapato yangu. Nilifanya hivyo kwa mwaka mmoja tu, nikaacha. Sasa huyu mganga ameniambia hao majini walionipa huu utajiri wamekasirika na ndiyo wanaoua.” “Lakini umeamini maneno yake?” “Naona yana ukweli. Alivyonieleza ndivyo vilivyokuwa. Hao majini wamemaliza watoto wangu pamoja na mke wangu, sasa wanataka roho yangu.” “Kumbe shemeji, huu utajiri wako ni wa majini?” “Zamani ndiyo, niliwahi kwenda kwa mganga wakati nashughulika kuchimba madini.” “Kwa hiyo chanzo cha pesa zako ni majini?” “Sasa hivi si unaona nafanya biashara. Nilikwenda siku moja tu kwa mganga.” “Si unajua pesa za namna hii zinasababisha umwagaji wa damu!” Almasi akanyamaza kimya. Mwanamke huyo akaendelea. “Ndiyo sababu watoto wamekuwa wanauawa ovyo na watu wasioeleweka na mwisho dada yangu naye ameuawa.” “Tatizo ni kwamba natakiwa nikamwage zile pesa baharini. Na kesho tu nitafanya hivyo.” “Lakini itasaidia nini, shemeji, wakati watoto wako pamoja na dada yangu wameshauawa?” “Kwa hiyo unataka niache na mimi niuawe?” “Si uliyataka mwenyewe, shemeji?” “Usiseme hivyo. Nani ambaye hajafaidika na utajiri wangu?” “Utajiri wa kutoa watu kafara una maana gani, shemeji? Kumbe wewe ndiyo umemuua dada yangu!” Almasi akazidi kutaharuki. “Dada yako nimemuua mimi?” “Kumbe si umesema uliliacha hilo sharti ndipo wanao pamoja na mke wako walipoanza kuuawa na watu wasiojulikana?” Almasi akiwa ametaharuki, alilisimamisha gari barabarani. “Sasa nakuuliza, ndiyo nimemuua mimi dada yako?” akamuuliza shemeji yake kwa ukali. “Ni wewe! Utasema ni nani? Dada yangu pamoja na wanao wameuawa kutokana na ushirikina wako. Tena afadhali usingeniambia. Kumbe baba wewe ni mshirikina sana!” “Shuka kwenye gari langu. Huna adabu!” Almasi akafoka. “Nitashuka, lakini tutakususia mke wako, utamzika mwenyewe. Na nitawambia ndugu wote kwamba wewe ndiyo mhusika wa haya mauaji!” Mwanamke huyo alifungua mlango wa gari, akashuka na kutembea kwa miguu. Almasi alimtazama kwenye kioo kabla ya kuliondoa gari hilo kwa hasira. Alifikiria aende kituo cha polisi kutoa ripoti ya kuuawa kwa mkewe, lakini akaona arudi nyumbani kwake. Alipofika, hakuingia ndani, alitoa simu yake na kumpigia Inspekta Amour. Amour alipokea simu, alimwambia. “Mke wangu naye ameuawa sasa hivi.” “Ameuawa na nani?” “Na wale watu walioua watoto wangu. Leo ndiyo nimewashuhudia kwa macho yangu.” “Uliwaona?” “Ndiyo, niliwaona.” “Walimuua wapi mke wako?” “Walimuulia hapa nyumbani. Waliingia chumbani mwetu, wakamuua.” “Umeshapiga ripoti kituo cha polisi?” “Wewe ndiye mtu wa kwanza kukuarifu.” “Sasa uko wapi?” “Niko nyumbani kwangu. Hawa watu nimewafungia mlango, kama bado wapo mtakuja kuwaona.” “Yaani hao wauaji umewafungia mlango humo chumbani?” “Ndiyo.” “Sawa. Tunakuja sasa hivi nyumbani kwako.” Almasi alikata simu na kuirudisha mfukoni. Alikuwa ametoka ndani ya gari lake na kujiegemeza kwenye boneti la mbele la gari hilo. Hasira ya kuambiwa kuwa amemuua mke wake ilikuwa bado ikimkereketa moyoni. Alijuta kwa nini alimweleza shemeji yake maelezo aliyoambiwa na mganga wakati akijua baadhi ya wanawake hawafikiri mbali. “Mimi nimuue mke wangu, kwani sina akili?” akajiambia peke yake. “Kweli yule msichana ni mjinga. Anaweza kuniponza,” akaendelea kujiambia. Kwanza alimuona alikuwa hodari na mwenye hekima kumwelekeza kwenda kwa mganga ambako tatizo lake lilikwenda kugundulika. Lakini alipofikia hatua ya kumwambia amemuua mke wake, alimuona mpumbavu. Baada ya nusu saa tu, magari mawili ya polisi yakawasili nyumbani kwa Almasi. Vile polisi walivyoambiwa kwamba wauaji hao walikuwa wamefungiwa kwenye chumba, walikuja polisi tisa. Watano wakiwa na bunduki. Inspekta Amour, ambaye huvaa kiraia, alikuwa wa kumi. Almasi aliwakaribisha. “Hao watu wamo ndani?” Amour akamuuliza akiwa ameshika bastola mkononi. “Niliwafungia chumbani mwangu na sijafungua mlango hadi sasa.”

RUANGWA: THE Deputy Minister for Natural Resources and Tourism Hamad Hassan Chande has directed the Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA) to deploy a team of wildlife rangers to Mandawa Ward in Ruangwa District, Lindi Region, to establish a camp and strengthen patrols against dangerous and destructive wildlife, particularly elephants straying from protected areas. Speaking to…

“So far, 125 passengers have been rescued, while more than nine others remain missing as rescue operations continue at the scene," he said.

He also urged his supporters to mobilise voters and ensure that polling agents are deployed throughout the country, saying "Our country needs unity."

Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga, ameanza kuandika historia katika soka la wanawake Marekani baada ya kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Wanawake Marekani na kuisaidia Washington Spirit kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Houston Dash.


TANZANIA stands among Africa’s most resource-rich nations, endowed with vast mineral deposits, natural gas reserves, wildlife, forests, fertile land, water resources and an extensive coastline. From gold buried beneath the ground in Geita, Shinyanga, Mwanza and Mara to strategic minerals scattered across the country; from the wildlife of the Serengeti to the beaches and islands…

Tony Elumelu, Chairman of Heirs Holdings, has acquired an additional six million shares in Seplat Energy Plc for £53.2 million. According to a notification filed with the Nigerian Exchange Limited (NGX) on Wednesday, the shares were bought by Heirs Energies Limited, a company controlled by Elumelu. The notice said the billionaire purchased shares at £8.87 […]

By Elizabeth Adegbesan Consumers’ sentiment plunged sharply in September 2026 as households grappled with intensifying price pressures. The Central Bank of Nigeria, CBN, in its latest Household Expectation Survey Report said that the overall Consumer Sentiments Index, CSI, dropped steeply to -18.7 points, down from -9.9 points in August. The decline reflects a cautious public, […]

By Shina Abubakar, Osogbo Following recent cult-related killings in Osogbo, Osun State capital, the Commissioner of Police, Ibrahim Zungura, has deployed the command’s tactical teams to the metropolis to restore normalcy. The deployment followed a series of shootings allegedly linked to rival cult groups in different parts of the city. The Police Public Relations Officer, […]





KOCHA Mkuu wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema kambi ya zaidi ya wiki moja iliyoweka kikosi hicho visiwani, Zanzibar imekuwa na matokeo chanya, kwa sababu imejenga utulivu wa wachezaji kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

KIKOSI cha Singida Black Stars kimeendelea na maandalizi yake jijini, Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mechi kali na ya kuvutia dhidi ya Dodoma Jiji ‘Walima Zabibu’, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini, Dodoma, Oktoba 9, 2026.

MABOSI wa KenGold FC wamefikia makubaliano ya kumuajiri aliyekuwa Kocha Mkuu wa Stand United ‘Chama la Wana’, Hussein Rupia, baada ya Jumanne Challe aliyeifundisha msimu wa 2025-2026, kujiunga na Polisi Tanzania akimsaidia Mbwana Makata.

BEKI wa kati wa IAA SC ya jijini, Arusha, Faisal Richard Mganga amesema ameamua kutafuta changamoto mpya katika maisha yake mapya na kikosi hicho, baada tu ya mkataba wake na KenGold FC ya Mbeya kufikia ukomo msimu uliopita wa 2025-2026.

UONGOZI wa maafande wa Transit Camp, umemrejesha tena kocha mkuu wa timu hiyo, Said Lyakuka kwa ajili ya kukifundisha kikosi hicho kwa msimu huu wa 2026-2027, wa Ligi ya Championship, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Vicent Barnabas.

MSHAMBULIAJI wa Kigamboni United zamani B19 FC, Abdulkarim Segeja amesema licha ya kusaini mkataba wa miezi sita na kikosi hicho, ila atahakikisha anapigania malengo ya timu hiyo kwa msimu wa 2026-2027, ili kuongeza ushindani zaidi.

MSHAMBULIAJI nyota wa KMC FC, Adam Uledi amesema licha ya ushindani mkali uliopo msimu huu wa 2026-2027, katika Ligi ya Championship, ila mojawapo ya malengo yake binafsi ni kukirejesha kikosi hicho Ligi Kuu Bara na kuvunja rekodi ya mabao.

DAR ES SALAAM: THE Minister of State in the Vice-President’s Office (Union and Environment), Hamad Yussuf Masauni, has urged residents living in high-risk areas along the Msimbazi River to relocate to safer places, warning that their lives and property are at risk. Emphasizing on the matter, the minister Mr asked residents to seek alternative accommodation,…

UTANGULIZI Yule mtu aliirudisha simu yake mfukoni akachutama na kufungua lile begi. Alitoa furushi la kamba akawapa wenzake. “Mfungeni kamba miguuni na mikononi. Jamaa anakuja sasa hivi” Watu hao wakachukua lile furushi la kamba na kulichakua. Zilikuwa kamba nyingi ambazo zilikuwa vipande vipande. Walichukua vipande hivyo vya kamba wakamfunga Frenk mikononi na miguuni. “Sasa tusubiri hapa hapa” Yule aliyekuwa akiendesha gari aliwambia wenzake. SASA ENDELEA Alitazama saa yake kisha akatoa sigara na kujiwashia. Baada ya kupita kama nusu saa hivi simu yake ikaita. Aliitoa mfukoni na kuipokea. “Sasa mpakieni kwenye gari, muje naye chimboni. Mganga amesema kafara lake ni lazima lifanyike kwenye chimbo na huu ndio muda muafaka” Sauti ikasikika kwenye simu. “Sawa” Mtu huyo aliirudisha simu mfukoni akawambia wenzake wambebe yule kijana na kumpakia kwenye gari. “Kwanini?” mmoja akamuuliza. “Amesema kafara lake linatakiwa lifanyike chimboni” “Yaani tutakwenda naye huko huko?” “Hakuna tatizo. Hivi sasa ni saa nane usiku, kila mtu amelala. Nani atatuona?” Walimbeba Frenk wakampakia katika siti ya nyuma ya gari hilo. Mtu mmoja alikaa naye kwenye siti. Mwingine alikaa siti ya mbele pamoja na aliyekuwa akiendesha gari hilo. Gari likawashwa moto na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari hilo likaingia katika viunga vya eneo la Marerani. Lilisimama karibu na chimbo moja lililokuwa karibu na kibanda kimoja kilichojengwa kwa miti. Aliyekuwa akiendesha alishuka na kwenda kwenye kile kibanda ambako kulikuwa na watu wawili waliokuwa wamekaa. “Tumekuja naye” Mtu huyo aliwambia watu hao. “Amezinduka?” Mmoja kati ya wale watu wawili waliokuwa wamekaa, akauliza. “Hajazinduka na tumemfunga kamba” “Sasa mtoeni kwenye gari. Mumburuze hadi pale kwenye chimbo. Fanyeni haraka. Hivi sasa watu wengi wamelala” Mtu huyo alirudi tena kwenye gari akawambia wenzake wamtoe Frenk na kumburuza kwenye chimbo. Wakati watu hao wakifanya hivyo, mtu aliyetoa agizo hilo alimuacha mwenzake amekaa, akaenda kwenye chimbo akiwa ameshika mfuko. Alipofika kwenye chimbo hilo aliuweka chini ule mfuko akatoa pembe mbili zilizofungwa kwa vitambaa vyeusi na vyekundu. Pia alitoa tunnguri mbili alizoziweka karibu na mlango wa chimbo hilo. Frenk aliletwa mahali hapo kwa kuburuzwa chini ambapo isingekuwa rahisi kwa mtu aliyekuwa mbali kumuona usiku huo kutokana na kutokuwepo kwa mwanga wa taa. Frenk alilazwa kichali chali karibu na mlango wa chimbo. Yule mtu aliyetoa pembe na tunguri alichukua pembe moja na kumzunguka Frenk huku akimmwagia mavumba. Alimzunguka mara saba. Alipomaliza aliziweka zile pembe akachukua tunguri na kuzunguka nazo mara saba huku akitabana maneno ya kichawi. Alipomaliza alivua nguo zake zote akafanya mauzauza kabla ya kuwambia wale watu kwamba wamchinje yule kijana. Mtu mmoja akamshika Frenk ili asifurukute na mwingine alitoa kisu na kukishika kichwa cha Frenk. Hapo hapo Frenk akazinduka. “Kitu gani?” akauliza kwa mshangao. Hakukuwa na aliyemjibu. “Niko wapi hapa na kwanini nimeshikwa hivi na kufungwa?” akaendelea kuuliza. Aliyekuwa amemshika alimshika vizuri. Yule aliyeshika kisu akaanza kumchinja harakaraka huku yule aliyevua nguo akisaidia kumshikilia asifurukute. Kisu kilipoanza kukata koo, Frenk alianza kukoroma. Alijaribu kufurukuta lakini waliomshika walikuwa wamemdhibiti sawasawa. Damu ikaanza kumwagika. Dakika tatu tu baadaye kichwa kilikuwa kimetenganishwa na kiwiliwili. Ile damu iliunda mchirizi na kuchirizikia kwenye Mlango wa chimbo. Mwili wa Frenk uliendelea kushikiliwa mpaka ulipotulia kabisa. Ndipo yule mtu aliyekuwa amekaa kwenye kile kibanda alipoinuka na kwenda mahali hapo. “Tayari?” akauliza. “Tayari” Mtu mmoja akamjibu. “Sasa mrudisheni kwenye gari mwende mkamzike” Yule mtu aliyevua nguo alisema huku akivaa suruaIi yake. Watu hao walishika miguu ya Frenk wakamburuza hadi kwenye gari. Wakafungua boneti la nyuma na kuutia mwili huo. Mmoja alirudi kufuatia kichwa cha frenk ambacho pia alikitia ndani ya boneti. Aliyekuwa akiendesha gari hilo alikuwa amesimama akizungumza na yule mtu waliyemkuta hapo pamoja na yule mganga. “Mtamzika mahali mbali na hapa. Mtakwenda kuchimba shimo refu ili mwilli wake usifukuliwe na fisi. Si mmesema hafahamiki?” Mtu huyo alimuuliza yule aliyekuwa akiendesha gari. “Hafahamiki.Tumeambiwa kwamba alifika leo pale gesti, anamtafuta ndugu yake” “Alitokea wapi?” “Alitokea Dar es Salaam.” “Atakuwa ni mgeni. Hakuna anayemfahamu. Sasa nendeni mkachimbe kaburi mumzike. Tukutane asubuhi” “Sawa” aliyekuwa akiendesha gari alisema kisha akaondoka kuelekea lilikokuwa gari hilo. Alifungua mlango akajipakia na kuliondoa gari. Mganga alikuwa akiitia michanga ile damu ya Frenk ili isionekane. Alipomaliza alimsogelea yule mtu aliyekuwa naye ambaye alikuwa amesimama kando yake. “Naona kazi imekwisha. Sasa zingatia vile nilivyokueleza. Asiingie mtu kwenye chimbo hili mpaka baada ya siku tatu. Wataingia watu watatu tu wakiwa uchi. Umenielewa?” “Nimekuelewa vizuri” “Hawatafukua umbali mrefu watakuta mwamba ambao watautoboa. Huo mwamba una mali za majini ambazo huwezi kuzipata mpaka ufanye kafara la roho kama tulilolifanya hapa” Mganga huyo aliendelea kumwambia Amon. “Wakishapata hizo mali watatoka wakiwa uchi. Watavaa nguo watakapotoka. Sijui kama unanielewa vizuri?” “Nakuelewa vizuri” “Mali watakayopata itatosha kukupa utajiri katika maisha yako yote na hutakiwi kurudia mara ya pili. Ukishapata hiyo mali nenda katafute biashara nyingine ufanye, ukirudia mara ya pili utakufa” “Sawa mzee” “Kingine ninachotaka kukukumbusha ni kuwa katika utajiri wako kila mwaka ukazamishe baharini fedha za mapato yako ambazo ni sawa na theluthi moja ya mapato yako. Hiyo ni zaka ya majini waliokupa mali” “Kama kweli nitafanikiwa nitafanya hivyo. Lakini ningependa kujua hizo fedha niziweke kwenye nini kabla ya kuzizamisha baharini” “Swali zuri sana. Hizo pesa utazitia kwenye mfuko mweupe. Utashona mfuko mweupe. Utaweka na jiwe ili ziweze kuzama chini. Unaweza kukodisha boti ikupeleke mbali kidogo” “Sawa. Nimekuelewa” ************ Kilichotokea ambacho Amon hakukijua ni kuwa wale watu aliokuwa akishirikiana nao waliyempelekea kijana ambaye alikuwa ni ndugu yake aliyekwenda Arusha kumtafuta yeye. Mhudumu wa pale gesti alipofikia alishaambiwa akipata mtu ambaye ataweza kutolewa kafara kwenye machimbo atapewa shilingi milioni mbili. Alipomuona Frenki alikuwa mgeni na alikuwa akimtafuta mwenyeji wake ambaye hakuwa akifahammika ndipo alipowapigia simu kina Amon na kuwambia waje usiku kumchukua Frenk. Jamaa hao wakafika usiku na kumwambia Frenk kuwa wanamfahamu kaka yake aliyekuwa anamtafuta na kwamba wanaweza kumpeleka aliko. Wakaenda kumchinja bila Amon kujua kuwa aliyechinjwa alikuwa ni ndugu yake aliyekwendaArusha kumtafuta. Kama walivyoambiwa na mganga baada ya kafara hilo walilofanya, Amon alipata madini yaliyompatia fedha nyingi. Akafuata masharti ya mganga kwamba asiendelee tena kuchimba. Akaondoka Marerani na kurudi Dar. Alirudi Dar akiwa na ugomvi na wenzake waliokuwa wakidai aliwapunja pesa, mmojawapo akiwa Mosha aliyewahi kukamatwa na polisi wilayani Kibaha kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watoto wa Almasi kutokana na uhasama waliokuwa nao. Kutokana na fedha alizopata, Amon aliweza kujenga nyumba ya kifahari pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya biashara. Baadaye akanunua kiwanda cha maji safi kutoka kwa mfanyabishara mmoja mwenye asili ya kiasia. Kiburi cha pesa kikamfanya Amon alibadili jina lake na kujiita Almasi. Baada ya kupata utajiri Amon sasa akiwa na jina la Almasi akawa mcha Mungu akitubu makosa yake lakini siku moja moja akinywa pombe. Katika mwaka wake wa kwanza wa utajiri, Almasi alitimiza lile sharti aliloambiwa la kumwaga robo ya mapato yake baharini. Ilimpa usumbufu mkubwa kufanya mahesabu ili kupata robo ya pesa alizokuwa nazo. Pia alipata usumbufu kupata sarafu za mamilioni ya shilingi ambazo alitakiwa akizimwage baharini. Alipofanya hivyo mara ya kwanza akaona ulikuwa upuuzi kuendelea na zoezi hilo. Mbali ya usumbufu alioupata kubadili pesa zake katika sarafu, pia aliona alikuwa akipoteza pesa zake bure kuzimwaga baharini. Hakutaka kuamini kuwa kulikuwa namajini chini ya bahari waliokuwa wakihitaji pesa hizo. Alichotaka kukiamni ni kuwa masharti mengine ya waganga si lazima yafuatwe, mradi ameshapata utajiri hakukuwa na haja tena ya kuendelea kutekeleza masharti ambayo yalikuwa yanamtia hasara. Akaacha. Miaka kadhaa ikapita. Mwisho akasahau kabisa kama kuna masharti alipewa na ameacha kuyatekeleza. Ndipo siku moja mtoto wake wa kwanza aliyemuita Martin alipovamiwa na watu watatu wa ajabu, akachinjwa na kunyang’anywa mkoba wa pesa…. Sasa Almasi akiwa kwa mganga waliyemwendea yeye na Maria alitingisha kichwa chake taratibu baada ya kuwaza. “Nimekumbuka kitu…” akamwambia mganga kwa sauti iliyonywea.