
HABARI ZA SAA, SAA SABA NA DAKIKA 55 - NOVEMBA 20, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania

DODOMA; Serikali imesema katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, ilitoa kiasi cha Sh bilioni 69 kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa vifaa vya mifumo ya Uhamiaji Mtandao. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo bungeni leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni, Imamu Mtumwa Vuai aliyetaka kujua serikali imejipangaje…

DODOMA; Serikali imesema imeandaa Mkakati wa Kudumu Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi. Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Agosti 26, 2026 na Naibu EWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Baraka aliyehoji lini serikali itaunda tume itakayotatua migogoro ya ardhi nchi nzima. “Mkakati huu…

DODOMA; Serikali ya Tanzania imesema tayari imeshatoa mchango wake wa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (AEC) kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ngwaru Maghembe, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Ussi Yahya. Mbunge huyo…

GEITA: SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa ufadhili wa jumla ya Sh milioni 40 kwa wazalishaji wa mkaa mbadala mkoani Geita ambao ni Taasisi ya Wanawake na Samia ili kuongeza matumizi ya nishati safi nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Samia mkoani Geita, Adelina Kabakama ametoa taarifa hiyo mbele ya viongozi wa mbio…

ZANZIBAR: ACT Wazalendo National Chairman, Mr Othman Masoud Othman, has said the party’s participation in the ongoing reconciliation process with CCM is driven by the broader interests of Zanzibar rather than personal or political gain. Mr Othman made the remarks at the party’s offices in Shangani, North Unguja, where he met party leaders from various…

WAKENYA wasio na digrii ya chuo kikuu wataweza kuwania urais, ugavana na ubunge katika uchaguzi mkuu ujao baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuthibitisha kuwa hitaji la kuwa na shahada halitumiki kwa sasa kufuatia maamuzi ya mahakama yaliyolitangaza kuwa kinyume cha Katiba. Kamishna wa IEBC Ann Nderitu alisema Jumatatu kuwa tume hiyo haiwezi kutekeleza sharti la wawaniaji kuwa na digrii kwa sababu mahakama tayari ililitupilia mbali. “Tunapoanza maandalizi sasa, hakuna sharti la digrii kwa mtu yeyote. Hiyo ndiyo hali ilivyo kwa sasa,” Nderitu alisema katika mahojiano na Citizen TV. Ufafanuzi huo unamaliza miaka ya sintofahamu iliyoshuhudia baadhi ya wagombea maarufu wakikabiliwa na maswali kuhusu vyeti vyao vya masomo. Mojawapo ya kesi zilizovutia hisia za wengi ni ile ya Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja mnamo 2022. Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE) ilieleza kuwa, digrii yake kutoka Team University ya Uganda haikuwa imethibitishwa, na kesi tatu zikawasilishwa kupinga ugombeaji wake. Hata hivyo, IEBC ilimuidhinisha kwa hoja kwamba jukumu lake ni kupokea stakabadhi, si kuzithibitisha. Mahakama Kuu iliunga mkono uamuzi huo na Sakaja akashinda uchaguzi. Kaunti ya Turkana nayo ilishuhudia mkanganyiko kama huo wakati Gavana Jeremiah Lomorukai aliidhinishwa na IEBC licha ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kudai digrii na diploma yake zilikuwa ghushi na kutaka akamatwe siku nne kabla ya uchaguzi. Mahakama ilimruhusu kuendelea kugombea na hatimaye akashinda. Kesi hizo zilifuatia maamuzi mawili muhimu ya Jaji Anthony Mrima mnamo 2021 na 2022 yaliyobatilisha Kifungu cha 22 cha Sheria ya Uchaguzi. Kwanza, jaji huyo alifuta kifungu kilichowataka wagombeaji ubunge kuwa na digrii, akisema hakikupitishwa kupitia ushirikishaji wa umma wa kutosha.

IKUNGI: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Vice-Chairman for Mainland Tanzania, Mr Stephen Wasira, has said the ruling party remains strong and united, urging opposition parties to offer constructive ideas instead of opposing government initiatives. Mr Wasira made the remarks recently during the first day of his three-day working tour aimed at holding internal meetings with CCM…

RAIS William Ruto amefichua kuwa ndovu wamekuwa wakivamia shamba lake lililoko Taita-Taveta na kuharibu mimea licha ya juhudi za kuwazuia, huku mizozo kati ya binadamu na wanyamapori ikizidi kutishia jamii katika eneo la Pwani. Rais alisema ndovu waliingia katika shamba lake na kuharibu mimea yake ya mahindi pamoja na kuangusha ua wa umeme aliokuwa ameweka kulinda mimea yake dhidi ya uvamizi huo. Alisema kuwa anafahamu changamoto zinazowakabili wakulima wanaoishi karibu na mbuga za wanyamapori. “Mimi pia ninakabiliwa na uvamizi wa ndovu katika shamba langu. Wamekula na kuharibu mimea yangu ya mahindi; pia nimepata hasara. Nilijaribu kuweka ua wa umeme lakini waliuvunja na kuendelea kula na kuharibu mimea yangu,” alisema Rais Jumapili wakati wa ibada kanisani katika kaunti hiyo. Hata hivyo, Dkt Ruto, ambaye anafuga ng'ombe wa nyama na maziwa katika shamba hilo pamoja na kuendesha kilimo cha mboga, alisema amewasiliana na Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini (KWS) kutafuta suluhu ya kudumu. “Lazima tupate suluhu ya kudumu kupitia mitaro na uzio ili kuwazuia wasiingie katika mashamba yetu,” alisema. Mbunge Mwakilishi wa Kike Taita-Taveta, Bi Lydia Haika, alisema uvamizi wa ndovu ni tatizo kubwa katika kaunti hiyo na kumtaka Rais kutafuta suluhisho ya kudumu. Haya yanajiri huku maelfu ya wakulima katika jamii zinazoishi karibu na hifadhi za kitaifa za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi, wakiendelea kulalamika kuhusu uvamizi wa wanyamapori katika mashamba na makazi wakitafuta chakula na maji. Katika kaunti za Kilifi, Kwale, Taita-Taveta, Lamu na Tana River, wakazi wameripoti uharibifu wa mimea, mali na vitisho kwa usalama wao kutokana na wanyamapori. Hivi majuzi mwanafunzi wa Gredi ya Saba alishambuliwa na kuuawa na simba Machi 29 alipokuwa akirejea nyumbani kutoka shuleni katika Kaunti ya Kilifi. Tukio hilo liliwalazimu maafisa wa KWS kuwasindikiza wanafunzi kwenda na kutoka shuleni katika baadhi ya vijiji vilivyoathirika. Hali imekuwa mbaya zaidi eneo la Ganze, ambako wakazi wanasema ndovu wamekuwa wakiingia mara kwa mara katika mashamba na makazi. Miezi minne iliyopita, zaidi ya ndovu 300 waliripotiwa kutoka katika Hifadhi ya Kitaifa ya Tsavo na kuvamia vijiji vya Kilifi, wakiharibu mimea, vyanzo vya maji na mashamba, ikiwemo mali ya Katibu Mkuu wa Idara ya Masuala ya Vijana, Bw Fikirini Jacobs. Uvamizi huo ulizua hasira na huku wakazi wakitoa wito kwa serikali kujenga uwa wa umeme kuzunguka hifadhi ya kitaifa ya Tsavo ili kuwazuia wanyamapori kuingia katika maeneo ya makazi. Katika kaunti jirani ya Kwale, Mbunge wa Kinango, Bw Gonzi Rai, alimuomba Rais Ruto kuingilia kati akisema ndovu wamekuwa wakiharibu mimea na kuzidisha ukosefu wa chakula. “Tafadhali tusaidie kutatua tatizo hili. Ndovu wanaharibu mimea yetu na ndiyo maana wakazi wanategemea misaada ya chakula kila mara. Hatutaki kutegemea misaada kwa sababu sisi ni wakulima. Changamoto pekee tunayokabili ni uvamizi wa ndovu ambao wanaendelea kuharibu mashamba yetu,” alisema Bw Rai. Hivi majuzi, Naibu Kamishna wa Magarini, kaunti ya Kilifi, Bw Michael Ololtuaa pia alilitaka Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini (KWS) kujitahidi na kuhakikisha kila mwaathiriwa wa migogoro ya binadamu na wanyamapori anafidiwa kikamilifu. Katika mahojiano na Taifa Leo Jumapili, Bw Ololtuaa alisisitiza kuwa si jambo jema kuona mwaathiriwa wa wanyamapori akikosa kufidiwa kutokana na kufeli kwake kusajili matukio kwa KWS. Kumekuwa na visa vya wanyamapori, hasa simba kuvamia, kuwaua na kuwala wanafunzi eneo hilo la Magarini. Kisa cha hivi punde zaidi ni cha juma lililopita ambapo simba-jike alimvamia,kumuua na kumla mwanafunzi wa Gredi 4 katika kijiji cha Chanjalo, Magarini, kaunti ya Kilifi. Mwanafunzi huyo kwa jina Kelvin Amani alikuwa njiani kurudi nyumbani jioni baada ya kucheza mpira wakati alipovamiwa na simba huyo. Machi, 2026, mwanafunzi mwingine wa Gredi 7 kwa jina Simon Nzaro Chai, kutoka kijiji cha Watala, eneobunge la Magarini, pia alivamiwa na kuliwa na simba wakati akitoka shule. Katika ziara yake ya awali huko Kilifi, Rais Ruto alitangaza kuwa serikali ilikuwa imetenga Sh315 milioni kujenga uzio wa umeme wenye urefu wa kilomita 140 kuzunguka hifadhi hiyo. “Nimesikia changamoto mnazokabiliana nazo kuhusu mzozo kati ya binadamu na wanyamapori. Hili lilizungumzwa pia na Gavana Gideon Mung’aro, Mbunge wa Ganze Kenneth Tungule na viongozi wengine. Nilikuwa nimeahidi kutafuta fedha na sasa nimepata Sh315 milioni za kujenga uzio wa umeme wa kilomita 140 kuzunguka hifadhi ya kitaifa,” alisema wakati wa hafla ya shukrani ya Bw Jacobs. Rais alisema uwa huo unalenga kuzuia ndovu na wanyamapori wengine kutoka katika hifadhi na kuingia kwenye mashamba na vijiji. “Tunajua kila mnapopanda mimea, wanyama wa porini huja na kuiharibu. Lakini tatizo hili litakwisha mwaka huu na hali ya kawaida itarejea. Hili ndilo ninawaahidi,” alisema. Rais Ruto pia alisema Mkurugenzi Mkuu wa KWS Prof Erustus Kanga, alikuwa akikamilisha mchakato wa zabuni na kwamba wakandarasi walitarajiwa kuanza kazi kufikia Julai.

KULIKUWA na kizaazaa katika Mahakama ya Milimani baada ya Rose Mbithe Mulwa na mwanawe Chris Mulwa kudai wanasingiziwa kuhusika katika mauaji ya Dkt Victoria Mutiso ili mali ya familia ya thamani ya Sh1.5 bilioni itwaliwe. Rose alidai hawezi kufikia akaunti zake za benki ili kupata pesa za matibabu na mahitaji ya kila siku. Alitoa madai mazito dhidi ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), akisema kesi dhidi yake imebuniwa. [caption id="attachment_191518" align="alignnone" width="1245"] Rose Mbithe Mulwa, anayeshukiwa kwa mauaji ya Dkt Victoria Mutiso. Picha|Richard Munguti[/caption] “Hawajawahi kuniona nikimuua Dkt Victoria Nthunya Mutiso,” Rose alidai. Alisema alimsomesha aliyekuwa mumewe, Profesa David Ndetei, hadi kiwango cha uzamifu (PhD), na kwamba sasa ana matatizo makubwa ya kiafya. Chris naye alidai maafisa wa DCI walimtisha ili aandike taarifa dhidi yake, la sivyo wangeomba mahakama iamuru azuiliwe kwa siku 60. “Mimi ni wakili wa mahakama hii na nina haki ya kujieleza,” Chris alisema.

•If you want to lead Nigeria, your past must be clear — ACF •It’s right, proper to bare your life journey — PANDEF •Contestants must present scorecards, not promises — MBF •Background checks raise moral issues, but law remains supreme — Afenifere By Dapo Akinrefon, Samuel Oyadongha, Peter Duru and Juliet Umeh LAGOS — Ahead […]

SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna na viongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi wameanza kutekeleza mkakati wa pande mbili huku wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Huku kundi hilo likiendelea na mapambano ya kisheria kulinda jina la Linda Mwananchi, pia limeanzisha juhudi za kutafuta chama mbadala cha kisiasa litakalotumia ikiwa halitafaulu mahakamani. Hatua hiyo inajiri huku muda wa kutimiza masharti ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ukiendelea kuyoyoma, jambo linaloweka presha kwa viongozi wa vuguvugu hilo kuhakikisha wana chama cha kisiasa cha kutumia kushiriki uchaguzi wa Agosti 10, 2027. Jana, Jopo la Mahakama la kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) liliwapa afueni washirika wa Bw Sifuna baada ya kumzuia Msajili wa Vyama vya Kisiasa kusajili chama kipya kinachotumia jina la Linda Mwananchi au jina lingine linalofanana nalo hadi rufaa iliyowasilishwa na viongozi wa vuguvugu hilo isikizwe na kuamuliwa. Uamuzi huo pia umeathiri mchakato unaoendelea wa kusajili chama cha Liberty National Democratic Alliance (LINDA) pamoja na jina la Mwananchi Party, huku ukiwalinda walalamishi dhidi ya uwezekano wa jina la Linda Mwananchi kutumiwa na kundi lingine. Kesi hiyo imewasilishwa na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) Faith Odhiambo na mwanamikakati wa kisiasa Pauline Njoki Njoroge. Watatu hao wanapinga jinsi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ilivyoshughulikia ombi lao la kuhifadhi jina la Linda Mwananchi Movement. Hata hivyo, huku kesi hiyo ikiendelea mahakamani, duru za karibu na vuguvugu hilo zinasema viongozi wake hawataki kutegemea matokeo ya mahakama pekee. Tayari wameanza mazungumzo na baadhi ya vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa kikamilifu kwa lengo la kuvibadilisha jina, rangi na uongozi ili viwe jukwaa lao la kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu. Miongoni mwa vyama vinavyotajwa ni United Democratic Party (UDP), chama kilichohusishwa na mwanasiasa marehemu Cyrus Jirongo. Chama hicho kwa sasa kinapitia mchakato wa kubadilishwa jina na kuwa Ukombozi People’s Party (UPP). Kulingana na notisi ya umma iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Bernard Wafukho, kuna mipango ya kubadilisha rangi za chama, kaulimbiu na nembo yake. Pia, chama cha United Patriotic Movement (UPM) kinachohusishwa na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale kimetajwa. Kulingana na rekodi za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa, UPM kilipata usajili kamili mnamo Juni mwaka huu. Awali, Dkt Khalwale alidokeza kuwa chama hicho kinaweza kuwa makazi ya baadhi ya viongozi wakuu wanaojipanga kwa uchaguzi wa 2027. Seneta huyo ni mmoja wa wanasiasa waliojitokeza hadharani kuunga mkono azma ya kisiasa ya Bw Sifuna. Mbunge wa Saboti Caleb Amisi pia amesajili chama cha People’s Renaissance Movement (PM). Hata hivyo, baadhi ya wanachama wa Linda Mwananchi wanasemekana kuwa na mashaka kuhusu kutumia chama hicho licha ya Bw Amisi kuwa sehemu ya vuguvugu hilo. Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi amethibitisha kuwa kundi hilo lina chaguo kadhaa mezani lakini akakataa kutaja majina. Alisema kufanya hivyo mapema kunaweza kuvuruga mipango yao kutokana na kile alichodai kuwa hujuma za kisiasa kutoka kwa wapinzani wao. “Linda Mwananchi ni chapa ambayo sisi tumejenga na kuvumisha. Wakenya wanaijua na wanaifahamu vizuri. Lakini hata kama tutanyimwa kuitumia, bado tuna njia nyingi za kuendelea mbele,” alisema Osotsi. Kwa mujibu wake, kinachovutia wananchi si jina la chama bali sera, viongozi na maono ya vuguvugu hilo. Alisisitiza kuwa wafuasi wao wataendelea kuwaunga mkono hata wakishiriki uchaguzi kwa jina tofauti. Mbali na changamoto za jina, kundi hilo pia linakimbizana na muda wa kutimiza masharti yaliyowekwa na IEBC. Tume hiyo imeweka Oktoba 15, 2026 kuwa tarehe ya mwisho kwa vyama vya siasa kuwasilisha majina ya maafisa wake walioidhinishwa pamoja na sahihi zao rasmi kwa maandalizi ya uchaguzi wa 2027. IEBC pia imepanga Oktoba 30 kuwa tarehe ya kuthibitisha kanuni za uteuzi wa vyama vya kisiasa, huku vyama vikitarajiwa kuwasilisha kanuni hizo ifikapo Novemba 6. Katika maelezo yaliyowasilishwa mbele ya mahakama, viongozi wa Linda Mwananchi walisema kufikia Agosti 13, 2026, jukwaa lao la kidijitali lilikuwa na wanachama zaidi ya 55,000 waliojisajili wenyewe pamoja na zaidi ya 13,000 wa kujitolea.

Security analyst and lawyer, Dr Bulama Bukarti, has said that terrorist groups operating in Nigeria are exploiting social media, international remittance services to raise and move funds into the country.

WIZARA ya Fedha ilitengea mashirika ya usalama jumla ya Sh44.6 bilioni mwezi Julai, hatua inayodhihirisha ufadhili mkubwa wa sekta hiyo katika mwaka wa mwisho wa serikali kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kati ya fedha hizo, Wizara ya Ulinzi ilipokea Sh19.4 bilioni, huku Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na Idara ya Usalama wa Ndani kila moja ikipokea Sh9.9 bilioni. Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) ilitengewa Sh5.4 bilioni. Fedha zilizotolewa mwezi Julai ziliongezeka kwa asilimia 53 ikilinganishwa na Sh29.1 bilioni zilizotolewa kwa sekta hiyo mwezi Julai mwaka jana, ongezeko kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika mwaka unaotangulia uchaguzi mkuu. Baadhi ya maafisa wa serikali wanahusisha ongezeko hilo na mipango ya kuboresha miundomsingi ya polisi, kuimarisha uwezo wa idara za usalama na kusaidia vitengo vipya vya kiutawala. Wengine wanachukulia hatua hiyo kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao. Katibu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo, alisema fedha hizo zinalenga kuendeleza mageuzi na kuboresha huduma ya polisi. “Serikali inaendelea na mpango wa kisasa wa mageuzi ya polisi unaojumuisha uwekezaji katika usafiri, vifaa, miundomsingi, teknolojia na uwezo wa kiutendaji,” alisema. Kati ya Sh44.6 bilioni zilizotolewa mwezi Julai, Sh39.7 bilioni ni za kugharamia matumizi ya kawaida kama mishahara na gharama za uendeshaji, huku Sh4.9 bilioni zikitengwa kwa miradi ya maendeleo. Kwa jumla, bajeti ya sekta ya usalama katika mwaka wa kifedha unaoishia Juni 2027 imeongezeka kwa asilimia 26 hadi kufikia Sh510.8 bilioni. Ongezeko hilo la Sh106 bilioni ni kubwa zaidi ikilinganishwa na wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa 2017 na 2022. Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Matumizi ya Bunge la Kitaifa Samuel Atandi, alisema sekta ya usalama imekuwa ikihitaji fedha zaidi kwa muda mrefu. “Hatujawahi kufadhili vya kutosha sekta ya usalama. Tunatarajia kwamba rasilimali zaidi zitakapopatikana, tutapendekeza ongezeko zaidi hasa kwa kuwa tunakaribia mwaka muhimu wa uchaguzi,” alisema.

By Dickson Omobola Nigerian Airspace Management Agency, NAMA, has distanced itself from any purported recruitment exercise, and urged members of the public to disregard such notices. The agency said it is not currently recruiting and warned that any individual or organisation claiming to recruit, facilitate employment or issue appointment letters on its behalf is acting […]

MATAMSHI ya Gavana wa Migori Ochilo Ayacko kuhusu ziara inayopangwa ya Gavana wa Siaya James Orengo na viongozi wengine wa vuguvugu la Linda Mwananchi yanatia wasiwasi na yanastahili kulaaniwa vikali. Kauli hii imetolewa wiki moja tu baada ya ghasia za kisiasa katika Kaunti ya Homa Bay kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhiwa kwa wengine kadhaa. Kenya inahitaji viongozi wa kisiasa kupunguza joto la kisiasa, kuheshimu Katiba na kulinda haki ya kila raia kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa amani. Badala yake, Bw Ayacko ametoa matamshi ambayo yanaweza kuongeza hofu na kutoa taswira kwamba ghasia dhidi ya wapinzani wa kisiasa zinafaa kuvumiliwa. Kauli yake kwamba “kuna jambo linaweza kumfanyikia Orengo” ni uchochezi. Gavana si mwanasiasa wa kawaida tu. Yeye ni afisa mkuu wa umma ambaye maneno yake yana uzito na yanaweza kuwachochea wafuasi wake na viongozi. Iwapo Bw Ayacko anaamini kweli kwamba kuna tishio la kiusalama dhidi ya Bw Orengo au kiongozi mwengine yeyote, wajibu wake uko wazi. Anapaswa kuripoti suala hilo kwa vyombo husika vya usalama na kudai ulinzi wa kutosha. Hapaswi kutoa kauli zisizoeleweka kuhusu kile kinachoweza kumtokea mwanasiasa mwenzake. Katiba ya Kenya inahakikisha uhuru wa kutembea, kujumuika, kukusanyika na kushiriki katika shughuli za kisiasa. Hakuna gavana, afisa wa chama au kiongozi wa eneo anayepaswa kujiona kuwa na mamlaka ya kuamua ni nani anayeruhusiwa kutembelea kaunti fulani, kuzungumza na wakazi au kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa. Bw Orengo hahitaji mwaliko kutoka kwa wanasiasa wa Migori ili kutembelea kaunti hiyo, mradi shughuli zake zinafanywa kwa mujibu wa sheria. Matukio ya kusikitisha ya Homa Bay yalipaswa kuwafundisha viongozi wa kisiasa kuhusu heshima. Kabla ya ghasia za Agosti 16, kulikuwa na matamshi makali ya kisiasa. Matokeo yake yalikuwa fujo, maafa, majeruhi na kuharibiwa kwa mali. Afisa mmoja wa polisi na mfanyabiashara mwanamke walifariki, huku wakazi wasio na hatia wakibaki kuhesabu hasara za mzozo wa kisiasa ambao haukupaswa kuruhusiwa kugeuka kuwa vurugu. Mashindano ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 hayaepukiki lakini vurugu zinaepukika. Viongozi wanaweza kutofautiana vikali kuhusu mustakabali wa ODM, serikali ya Rais William Ruto na mwelekeo wa kisiasa wa eneo la Nyanza bila kugeuza miji na vijiji kuwa viwanja vya machafuko.

The resignation of Vice President, Dr Emmanuel Nchimbi, has opened a new political chapter within President Samia Suluhu Hassan’s government, with attention now turning to a possible successor. Dr Nchimbi announced on Tuesday, August 25, 2026, that he had written to President Hassan informing her of his decision to retire from politics and public service and resign as Vice President, effective September 4, 2026. In a statement he distributed through his social media pages, Dr Nchimbi said the decision was made pursuant to Article 50(2)(c), read together with Article 149(2), of the Constitution. “I am satisfied beyond doubt that the President wants change, so I have decided to fulfil my promise,” said Dr Nchimbi in his resignation statement, referring to a promise he made to President Hassan on August 27, 2025, that he would leave office if she felt the need for another Vice President. 14 days to find a successor Article 50(4) of the Constitution establishes a specific procedure for filling the position, stating that the President must appoint a person to serve as Vice President within 14 days of the former Vice President ceasing to hold office. The President will therefore have until about September 18, 2026, to complete the process, after which the new Vice President will be sworn in and assume office following confirmation by Parliament. Parliament begins its fourth meeting on Wednesday, August 26, 2026. A political and leadership analyst and lawyer, Advocate Dr Onesmo Kyauke, said the position was not an ordinary appointment like those of Cabinet ministers because the Constitution requires parliamentary approval. “This matter is constitutional, and the person must be appointed from the party to which the resigned Vice President belonged,” said Dr Kyauke. As discussions intensify, several names circulate in the mouths of various sources as possible successors. Dr Kyauke also explained that the Vice President’s resignation does not automatically affect or trigger the dissolution of the Cabinet, saying that would be the President’s decision. This differs from the Prime Minister’s resignation, which requires the entire Cabinet to be dissolved. Since taking office on November 3, 2025, President Hassan has largely retained her government team, including Regional and District Commissioners, regional and district administrative secretaries, council directors and heads of institutions. Mentioned names Among those being mentioned in political discussions is an economist and experienced CCM politician, Prime Minister Dr Mwigulu Nchemba. Dr Nchemba served as Minister for Finance and Minister for Home Affairs and has held various government and ruling CCM. Analysts say his experience in economics, government leadership and party administration makes him a strong contender, although he currently serves as Prime Minister. Another name associated with the position is Prof Palamagamba Kabudi, a lawyer and veteran CCM politician who previously served as Minister for Constitutional and Legal Affairs and Minister for Foreign Affairs. He is currently Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Policy, Parliament, Coordination and Persons with Disabilities. Another is the CCM politician, Dr Dotto Biteko, who rose through government ranks to hold senior ministerial positions, including that of Deputy Prime Minister. Stakeholders say his experience overseeing strategic sectors and his previous positions place him among those considered in the debate. Another veteran CCM politician with experience in various ministerial positions, including the Prime Minister’s Office and the President’s Office, Mr George Simbachawene is also included in the list. He previously served as Minister of State in the President’s Office responsible for Public Service Management and Good Governance and the former Minister for Home Affairs in President Hassan’s government before the revocation of his appointment. The current Home Affairs Minister, Mr Patrobas Katambi, succeeded him. Although the list could grow, the names currently being discussed remain part of political speculation, with the final decision resting with President Hassan. Stakeholders say the appointment will test the President’s ability to identify a candidate who meets the constitutional requirements and can secure Parliament’s support. A lecturer at Tumaini University (Turdaco), Dr Lazaro Swai, said the next Vice President should have a personality that complements the President’s to foster closeness and effective leadership. “Since internal matters were not discussed, we saw clouds, we saw drizzles, and now rain has fallen; these things were expected,” he said. “In the new appointment, we expect the person appointed to be someone who aligns with the President or someone who can consult with her and reach agreement,” he added. Meanwhile, human rights advocates want the next Vice President to defend and promote human rights through both words and actions to help build a just and equal society. “Dr Nchimbi was speaking about things we want regarding human rights, but we want the next person to be an executor, instead of telling us to fight,” said the Legal and Human Rights Centre (LHRC) Executive Director, Dr Anna Henga. “They should be able to use their position to help achieve citizens’ goals since they are the country’s number two leader,” she added.

LUSAKA, Zambia: SERIKALI ya Zambia ilifunga mahakama kuu za nchi hiyo Jumatatu, ili kuwazuia watu kuingia katika majengo hayo siku ya mwisho ambayo upinzani ungeweza kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wenye utata uliofanyika mwezi huu. Barua kutoka kwa msimamizi mkuu wa idara ya mahakama, ambao Reuters iliona, ilisema kwamba, “kwa sababu za kiusalama, wafanyakazi wote wanashauriwa kutofika kazini leo.” Msemaji wa Polisi Godfrey Chilabi aliiambia Reuters kwamba tathmini za kiusalama zilikuwa zikiendelea, lakini akakataa kutoa maelezo zaidi. Msemaji wa idara ya mahakama hakupatikana kutoa maoni. Kiongozi wa upinzani Brian Mundubile alisema wiki iliyopita kwamba alikuwa akipanga kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Kikatiba kupinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 13, ambapo alishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Hakainde Hichilema. Mwisho wa kuwasilisha kesi kama hiyo ni siku saba baada ya kutangazwa kwa matokeo, muda ambao ungeisha mapema Jumanne. Katika majengo ya Mahakama ya Juu jijini Lusaka, ambako pia kuna Mahakama ya Kikatiba, milango yote ilikuwa imefungwa huku polisi wakionekana ndani ya eneo hilo. Hichilema alichaguliwa tena kwa asilimia 60 ya kura katika taifa hilo kusini mwa Afrika tajiri kwa shaba. Hata hivyo, ripoti mbili za waangalizi huru zilipata dalili kwamba idadi ya kura alizopewa Hichilema huenda ziliongezwa. Hichilema amekanusha madai yoyote ya udanganyifu ili kuwahi ushindi. Baada ya kukamatwa kwa baadhi ya washirika wake, Mundubile aliitwa na polisi wiki iliyopita kwa mahojiano kuhusiana na madai ya vitisho kwa usalama wa taifa, madai ambayo anasema yalibuniwa. Wachanganuzi na mawakili wa haki za binadamu walisema wanashuku kuwa huenda akazuiwa kuwasilisha kesi yake, ingawa chama cha Hichilema kimesema Mundubile yuko huru kutumia njia za kisheria zinazopatikana. “Tunajaribu kadri tuwezavyo kuhakikisha kesi hiyo inawasilishwa, lakini tutaona jinsi mambo yatakavyokwenda,” alisema Rais wa New Heritage Party, Chishala Kateka, ambaye chama chake ipo pia katika muungano wa upinzani unaomuunga mkono Mundubile.

DAR ES SALAAM, Tanzania: MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dkt Emmanuel John Nchimbi, Jumanne, Agosti 25, 2026 alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake na kustaafu kabisa katika utumishi wa umma na siasa kuanzia Septemba 4, 2026. Katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa na Afisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma, Dkt Nchimbi alisema tayari amemkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan barua rasmi ya kujiuzulu. Dkt Nchimbi alisema ameongozwa na masharti ya Ibara ya 50(2)(c), na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Tanzania, ili kumpa Rais Hassan fursa ya kumteua makamu wa rais mwingine. Akikumbuka kipindi chake cha uongozi, Dkt Nchimbi alisema alikuwa ametoa ahadi kwa rais mwaka mmoja uliopita kwamba angeitumikia Tanzania kwa uaminifu na kuwa tayari kuondoka iwapo kungekuwa na haja ya mabadiliko. “Mnamo Agosti 27, 2025, nilimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba ningemsaidia yeye na nchi yetu kwa uwezo wangu wote na kwa uaminifu mkubwa,” akasema Dkt Nchimbi. “Pia nilimhakikishia kwamba wakati wowote atakapoona kuna haja ya kuwa na makamu wa rais mwengine, nitaachia wadhifa huo. Nimeridhika kabisa, bila shaka yoyote, kwamba Rais anatamani mabadiliko, na kwa hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” akasema Dkt Nchimbi alimshukuru Rais Hassan na chama tawala, CCM, kwa imani waliyoonyesha katika uongozi wake. Pia aliwashukuru raia wa Tanzania kwa kumuunga mkono katika kipindi chake cha utumishi wa umma, akiahidi kuendelea kuwa raia mzalendo. Kujiuzulu kwake hata hivyo pia huenda kunatarajiwa kuzua maoni ya kisiasa hasa baada ya Tanzania kuwa na uchaguzi mkuu uliopita uliozingirwa na utata na kukosolewa na jamii ya kimataifa. Dkt Emmanuel John Nchimbi alizaliwa Desemba 24, 1971, katika Mkoa wa Mbeya na alilewa katika familia iliyojikita katika utumishi wa umma. Babake, Mzee John Nchimbi, ambaye anatoka Wilaya ya Songea, aliwahi kuhudumu kama Kamishina Msaidizi wa Polisi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara. Mbali na kazi yake katika idara ya polisi, Mzee Nchimbi pia alijihusisha na siasa, akihudumu kwa mihula miwili kama mwanachama wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM kupitia tawi la majeshi, kabla ya baadaye kuhudumu kama katibu wa chama hicho katika ngazi ya mkoa.

VIONGOZI wa Taita-Taveta wakiongozwa na Gavana Andrew Mwadime wamewaonya wakazi wa Pwani dhidi ya kuunga mkono siasa za upinzani zinazoongozwa na kinara wa chama cha DCP, Bw Rigathi Gachagua. Bw Mwadime alisema Bw Gachagua hafai kupata uungwaji mkono kutoka eneo la Pwani kwa sababu hakufanya lolote la maana kwa eneo hilo alipokuwa Naibu wa Rais baada ya uchaguzi mkuu wa 2022. Alisema Bw Gachagua amekuwa akiwaita Wapwani binamu zake lakini alipokuwa mamlakani hakuwasaidia. “Tutakuwa sawa kweli kushirikiana na mtu ambaye alipokuwa uongozini alisema hatuna hisa kwa serikali ya Kenya Kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa 2022? Tuongee na wananchi waingie kwa mkondo wa Kenya Kwanza. Tutafunga njia za upinzani, tutazunguka nyumba baada ya nyumba kuuza sera ya Rais,” alisema. Badala yake, aliwasihi wakazi kumuunga mkono Rais William Ruto na kumpigia kura kwa asilimia 100 katika uchaguzi wa 2027, akisema serikali yake imewekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo. “Lakini wataita na wataveta mko na shida gani jamani? Tuache nongo nongo nyingi, tumuunge mkono Rais Ruto kwa muhula wa pili. Tumepokea maendeleo mengi kutoka kwa Rais Ruto kwa muhula wa kwanza tu. Wengine wamekuwa marais na hakuna maendeleo waliyotuletea,” alisema Bw Mwadime akimpigia debe Rais Ruto. Senet awa Taita Taveta Bw Jonnes Mwaruma, Mbunge wa Taveta Bw John Bwire, mwakilishi wa wanawake Bi Lydia Haika, aliyekuwa gavana wa Taita Taveta Bw John Mruttu waliapa kushirikiana na chama cha ODM kumtafutia kura Rais katika kaunti hiyo. "Tujitume kumtafutia Rais Ruto kura sababu ametuletea maendeleo hasa katika sekta ya uchukuzi. Waambie wapinzani kuwa Rais ametuletea miradi ya maendeleo ya kihistoria," alisema Bw Mruttu. Bw Mwaruma alisema wapinzani wa Bw Ruto hawataki serikali ipeleke maendeleo sehemu zote nchini. "Wanataka serikali iendelee na ubaguzi wa jadi wa miradi ya maendeleo. Rais ameleta usawa, haijalishi unatoka kabila ndogo au kubwa maendeleo yanaenda sambamba. Wale waliokuwa miaka iliyopita walitunyima maendeleo na haki yetu ndio maana lazima tumuunge mkono, hakuna tena kucheza siasa za pata potea," alisema Bw Mwaruma. Alisema atatembea kila kijiji kumtafutia kura Rais. Hata hivyo walimtaka Rais Ruto kusimama imara na kupuuza wapinzani wake ambao, alisema, wamekuwa wakimkosoa na kumchafua kisiasa. “Hata mwembe wenye maembe ndio hupigwa mawe. Utaendelea kupakwa matope kwa sababu unafanya kazi. Usipopakwa matope, inaonyesha hufanyi kazi. Kwa hivyo usijali, wewe endelea kuwafanyia Wakenya kazi,” alisema Gavana huyo. Pia aliwasihi viongozi wa kaunti hiyo kushirikiana katika kumtafutia Rais Ruto kura kutoka nyumba hadi nyumba kuelekea uchaguzi wa 2027. Alitaja ujenzi wa barabara na ukarabati wa reli ya zamani ya Voi-Taveta miongoni mwa miradi ambayo amesema imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Rais Ruto katika eneo hilo.

Former Minister of Youth and Sports Development, Solomon Dalung, has raised concerns over the initial composition of the All Progressives Congress, APC, Presidential Campaign Council for the 2027 general elections, saying allegations surrounding some members could undermine public confidence in the ruling party.

MTOTO mwenye umri wa miaka minne, Precious Wambui, ameunganishwa tena na mamake Kenya baada ya kuishi Saudi Arabia kwa miaka mitatu kufuatia kufurushwa kwa mamake, Penina Wanjiru, 2025. Precious aliwasili Nairobi Jumatatu na kukutanishwa na mamake katika afisi za Idara ya Serikali ya Masuala ya Wakenya Wanaoishi Nje ya Nchi. Bi Wanjiru alisema anafurahi kurejeshewa mwanawe baada ya kipindi kigumu cha kutengana. “Nina furaha sana kupata mtoto wangu. Haikuwa rahisi na nimekuwa mgonjwa, lakini sasa nitakuwa sawa. Nashukuru idara za serikali zilizotusaidia,” alisema. [caption id="attachment_191486" align="alignnone" width="2560"] Katibu wa Idara ya Huduma za Watoto, Carren Ogeng’o, mama Precious, Penina Wanjiru, na Katibu wa Idara ya Masuala ya Diaspora, Roselyn Njogu, wakati wa makabidhiano ya Baby Precious katika ofisi ya Idara ya Masuala ya Diaspora, Agosti 24, 2026. Picha|Fridah Okachi[/caption] Katibu Mkuu wa Masuala ya Wanaoishi Nchi za Nje Roselyn Njogu alisema serikali ililazimika kuthibitisha uraia wa mtoto na uhusiano wake na mamake kabla ya kuanza mchakato wa kumrejesha Kenya. Maafisa wa ubalozi wa Kenya jijini Riyadh walishirikiana na Serikali kufanya uchunguzi wa DNA, ambao ulithibitisha kuwa Precious ni mwana wa Bi Wanjiru. Afisa wa maslahi ya watoto pia alitumwa Saudi Arabia kuchunguza hali ya mtoto huyo, aliyekuwa akiishi na malezi ya msamaria mwema. Bi Njogu alisema idara yake imewarejesha watoto wanane nchini tangu kuanzishwa kwake 2022. Serikali itaendelea kufuatilia familia hiyo kuhakikisha Precious anapata mazingira salama na huduma zinazohitajika.

By Kingsley Omonobi The 2026 Annual Nigeria Financial Intelligence Report has revealed that terrorists and extremist groups are increasingly using crowdfunding networks to raise funds for their criminal activities. The report by the Nigeria Financial Intelligence Unit (NFIU) said terrorist financiers were also opening bank accounts in women’s names and using phone numbers for mobile […]

RAIS William Ruto ameeleza jinsi alivyopokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, mauti ambayo yalizua wingu la huzuni na kutumbukiza taifa kwenye wimbi la maombolezo. Kwenye mahojiano na Taifa Leo, Rais Ruto alisema alikuwa akielekea afisini mwake mwendo wa saa 12:30 asubuhi Oktoba 15, 2025, simu yake ilipokereza. Simu hiyo ilipigwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga, kakake mkubwa wa Bw Odinga. “Kuna tatizo, ‘kiongozi wa vijana’ (Oburu) aliniambia. Nadhani nimempoteza kaka yangu,” Rais Ruto alikumbuka Dkt Oburu akisema. Dkt Oburu hujiita “kiongozi wa vijana” licha ya umri wake pevu wa miaka 83. Raila alikuwa amefariki India, ambako alikuwa ameenda kutibiwa akiwa na matumaini ya kupona na kurejea nchini. Rais Ruto, alisema alikuwa amezungumza na Raila siku chache kabla ya kifo chake na akaambiwa alikuwa ametoka hospitalini na alikuwa akienda kupumzika. Muda mfupi baadaye, dadake Raila, Ruth Odinga, pia alimpigia simu Rais Ruto simu. Familia ilimweleza kuwa Raila alikuwa ameamka asubuhi hiyo, akafanya mazoezi kabla hali yake kuzorota ghafla. “Maisha yake hayakuweza kuokolewa,” Rais Ruto akasema akikumbuka kauli ya Ruth Odinga. Rais Ruto na Raila walikuwa wamefahamiana kwa miongo kadhaa, wakati mmoja wakishirikiana kisiasa na mara nyingine wakitofautiana vikali na kila mmoja kuchukua mwelekeo wake. “Tulianza tukiwa pande tofauti tulipokuwa Kanu, wao wakiwa Ford na wengine. Tulikutana ODM, tukaijenga pamoja. Nilijitahidi kumuunga mkono na alikuwa kiongozi mzuri wa kikosi chetu, kisha tukatengana tena,” akasema Rais Ruto. Wawili hao walikabiliana katika uchaguzi wa urais wa 2022, ambapo Rais Ruto alishinda kwa kura 7,176,141 dhidi ya 6,942,930 za Raila. Hata hivyo, maandamano ya 2024 yalibadilisha mazingira ya kisiasa na hatimaye makundi yao yakashirikiana katika Serikali Jumuishi, Raila akiwa sehemu ya serikali hiyo. Rais Ruto alisema katika wiki za mwisho za maisha ya Raila, uhusiano wao ulikuwa umeimarika sana. Walipigiana simu, kukutana na hata kula chakula cha jioni nyumbani kwa Raila. Aidha Rais Ruto alisema Raila alikuwa amepiga simu akisema hakuwa akijihisi vizuri na alitaka kumwona. Raila alimtembelea Rais katika Ikulu ya Nairobi na kujadili masuala mbalimbali kuhusu mustakabali wa nchi. Baadaye, Rais Ruto alimtembelea Raila nyumbani kwake baada ya kuambiwa alikuwa amerejea Nairobi. Walikula chakula cha jioni pamoja na Raila kumweleza kuwa alitaka kupata maoni ya pili ya madaktari kwa sababu afya yake haikuwa ikiimarika. Raila baadaye alisafiri hadi India akiwa na binti yake, madaktari na wengine. Wawili hao waliendelea kuwasiliana kwa simu. Rais Ruto alisema Raila mwanzoni alikuwa na matumaini, akimweleza kuwa madaktari kadhaa walikuwa wamemchunguza na kuamini wamepata matibabu yaliyofaa. Lakini siku chache baadaye, Rais alipokea habari kwamba Raila alikuwa ametoka hospitalini na alikuwa akipanga kupumzika. Hiyo ndiyo ilikuwa taarifa ya mwisho aliyopokea Rais Ruto kabla ya simu ya Dkt Oburu kumjulisha kuhusu kifo cha Raila. Baadaye Ruto alishiriki katika mipango ya kurejesha mwili wa Raila nchini, akiwemo kuwasiliana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ambaye alisema alimfahamu Raila binafsi. Kwa Rais Ruto, sehemu ngumu zaidi ilikuwa jinsi kifo hicho kilivyotokea ghafla, kwani siku chache tu kabla walikuwa wakijadili mustakabali wa Kenya.

VYAMA vya walimu vimekasirishwa na matamshi ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula kwamba baadhi ya wabunge hupewa barua za ajira za Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) katika Ikulu. Chama cha Walimu Nchini (KNUT), Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Anuwai (KUPPET) na Muungano wa Walimu wanaofundisha maeneo kame (KETHAWA), wote wamesema kauli hiyo imeibua upya madai ya mapendeleo ya kisiasa katika kuwaajiri walimu. Bw Wetang’ula alisema mwishoni mwa wiki kwamba baadhi ya wabunge huandamana naye hadi Ikulu na kupewa hadi barua 10 za ajira za walimu, lakini baadaye huziuza kwa Sh400,000 kwa kila mzazi. “Baadhi ya wabunge ninaowapeleka kwa Rais hupewa hadi barua 10 za ajira za walimu. Lakini baadaye unasikia wamekuwa wakiziuza,” akasema Bw Wetangúla. Alisema kitendo hicho si cha kimaadili, hasa kwa wazazi maskini wanaolazimika kutafuta fedha nyingi ili watoto wao wapate ajira. Kauli hiyo imezua wasiwasi wakati TSC imechapisha nafasi 20,000 za ajira za walimu wa shule za sekondari za chini. Naibu Katibu Mkuu wa Kuppet Moses Nthurima alisema madai hayo ni ya kusikitisha na yanalemaza uhuru wa TSC, ambayo ni tume huru ya kikatiba. Alisema walimu waliohitimu miaka mingi iliyopita na kupata alama za juu katika mahojiano wanafaa kupewa kipaumbele badala ya nafasi kupewa watu wenye uhusiano na wanasiasa. “TSC ina sera ya kuajiri. Waliohitimu mapema na kupata alama za juu katika mahojiano wanapaswa kuwa na nafasi kubwa ya kuajiriwa,” akasema. Katibu wa Kitaifa wa Kethawa Ndung’u Wangenye alisema kauli ya Spika imethibitisha madai ya muda mrefu kwamba wanasiasa huingilia mchakato wa kuwaajiri walimu. Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kuppet Omboko Milemba alisema walimu lazima waajiriwe kupitia TSC pekee, kwa kuwa hiyo ndiyo taasisi iliyopewa jukumu hilo kikatiba. Naibu Katibu Mkuu wa Knut Hesbon Otieno alisema baadhi ya walimu wameomba ajira mara nyingi bila mafanikio huku wengine wakipata nafasi kupitia uhusiano wa kisiasa. Hata hivyo, TSC imepuuza madai hayo na kusisitiza kuwa mchakato wake wa kuwaajiri walimu hufanywa kwa haki na ushindani kwa mujibu wa Katiba na sheria. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TSC Evaleen Mitei alisema ajira hufanywa katika ngazi ya kaunti ndogo baada ya nafasi kutangazwa rasmi na miongozo ya uteuzi kuchapishwa. Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba alisema serikali itashirikiana na TSC kukabiliana na uuzaji wa nafasi za ajira, akisema ni uhalifu unaopaswa kukomeshwa.

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, sasa anadai ilikuwa vigumu kumfikia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akidai kwamba mara nyingi alisita kushirikiana na mawaziri na viongozi wa kisiasa kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Akizungumza Khwisero, Kaunti ya Kakamega, jana Bw Atwoli alisema Bw Kenyatta alikuwa mgumu kufikiwa ikilinganishwa na marais wengine aliowahi kufanya nao kazi. “Nimefanya kazi na marais wote na namjua Uhuru Kenyatta. Kama si juhudi za Naibu Rais wa wakati huo William Ruto, hata kuwafanya wabunge wakutane na Rais haikuwa rahisi,” akasema. Kauli hii inajiri wakati uhusiano kati ya Bw Kenyatta na Rais Ruto ukiwa na mashaka. Mnamo Disemba 9, 2024, Rais Ruto alimtembelea Bw Kenyatta nyumbani kwake Ichaweri, Gatundu, katika juhudi za kurejesha uhusiano wao baada ya miaka kadhaa ya tofauti kali za kisiasa. Katika mahojiano ya hivi majuzi na Taifa Leo, Rais Ruto alisema pia alikuwa amemtembelea Kenyatta katika afisi yake karibu na Ikulu ili kumshawishi kuunga mkono ajenda ya kitaifa. “Nilienda kumuona Ichaweri na pia katika afisi yake iliyo hapa karibu (na Ikulu) na nikajaribu kumshawishi kwamba kama kiongozi wa zamani wa nchi, na ndiye pekee aliye hai sasa, ilikuwa bora atusaidie kujenga nchi, lakini alisita. Hakuwa na uhakika kama alitaka kufanya hivyo na hayo ni maamuzi ambayo watu hufanya. Alichagua kushirikiana na upinzani, akiwafadhili,” akasema Rais. Rais Ruto alisema wazo la viongozi hao kushirikiana lilitokana na mazungumzo yake na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyefariki Oktoba 2025. “Sasa sisi ndio wazee. Sisi ndio viongozi wa taifa hili. Kwa nini tusishirikiane, tujenge taifa ambalo tunaweza kulikabidhi kwa kizazi kijacho cha viongozi?” akasema Rais Ruto. Bw Atwoli pia aliwaonya wakazi wa Magharibi dhidi ya kugawanywa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, akionekana kumlenga Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. “Jamii ya Waluhya ni rahisi kudanganywa lakini nataka muwe macho,” alisema. Alisema pia urais hauwezi kupatikana kupitia michango midogo ya wananchi. “Njia ya kuelekea urais si rahisi. Huwezi kutembea na ndoo sokoni ukikusanya Sh50 kutoka kwa mama mboga. Hizo haziwezi kukufanya uwe rais,” akaongeza. Bw Atwoli pia alimtaka Bw Kenyatta kumruhusu Rais Ruto kukamilisha muhula wake bila kuingiliwa. “Tayari alihudumu mihula yake miwili bila chochote cha maana cha kuonyesha. Kwa nini sasa asikae chini na kumruhusu Rais Ruto kuwahudumia Wakenya?” akauliza. Kiongozi huyo wa COTU pia alimkosoa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale kwa kugeuza mazishi ya mkewe marehemu, Gloria Khalwale, kuwa jukwaa la kisiasa.

GAVANA wa Migori Ochilo Ayacko amewaonya viongozi wa kundi la Linda Mwananchi dhidi ya kuzuru kaunti hiyo, akisema ziara yao iliyopangwa inaweza kuongeza joto la kisiasa na kusababisha ghasia kama zile zilizoshuhudiwa hivi karibuni katika Kaunti ya Homa Bay. Onyo hilo linatolewa wiki moja baada ya mapigano kati ya wafuasi wa ODM na kundi la Linda Mwananchi huko Homa Bay kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa. Kwa siku tatu zilizopita, Bw Ayacko amekuwa akitoa tahadhari kuhusu mpango wa Gavana wa Siaya James Orengo na viongozi wengine wa Linda Mwananchi kuzuru Migori kama sehemu ya kampeni zao katika eneo la Kusini mwa Nyanza. Akizungumza wakati wa harambee katika Chuo cha Ualimu cha Migori, Gavana Ayacko alisema viongozi wa kisiasa wanafaa kushauriana na viongozi wa maeneo wanayonuia kuzuru, hasa pale ambapo kuna mvutano wa kisiasa. Alisema ziara ya awali ya Bw Orengo mjini Homa Bay bila maelewano ya kutosha na viongozi wa eneo ilichangia mazingira yaliyozaa machafuko. “Orengo alikuwa ameapa kufika Homa Bay hata iweje. Ziara yake bila mwaliko wa viongozi wa eneo na bila uungwaji mkono mashinani ndiyo chimbuko la matatizo yaliyoshuhudiwa,” akasema Bw Ayacko. Gavana huyo aliwauliza waliohudhuria mkutano huo ikiwa wangependa Bw Orengo kuzuru Migori, huku wengi wakijibu kwa sauti kwamba hawamtaki. Bw Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ni miongoni mwa viongozi wanaohusishwa na kampeni za Linda Mwananchi. Bw Orengo ameashiria kuwa kundi hilo linapanga kuzuru maeneo mbalimbali ya Kusini mwa Nyanza, yakiwemo Migori na Homa Bay. Katika ziara yao ya mwisho Homa Bay, viongozi hao walifanikiwa kuhutubia wakazi wa Nyandiwa na Sindo katika eneo la Suba Kusini. Hata hivyo, mpango wa kufanya mkutano mjini Homa Bay ulivurugika baada ya kundi hilo kufika jioni na kukabiliwa na mapokezi baridi. Machafuko yaliyofuatia yalisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi na mfanyabiashara mwanamke, huku mali ikiharibiwa. “Jambo muhimu zaidi ni amani kudumu. Serikali yangu imejikita katika maendeleo, hasa kuboresha miundombinu ya barabara, na hatuwezi kuruhusu siasa kuvuruga amani,” akasema Bw Ayacko. Wakati huo huo, Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga amejitenga na madai yanayomhusisha na ghasia hizo na kutaka uchunguzi ufanywe dhidi ya wote watakaopatikana na hatia. Aliyekuwa Naibu Gavana wa Homa Bay Oyugi Magwang ameonya kuwa kuendelea kwa vurugu za kisiasa kunaweza kutatiza juhudi za maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Viongozi mbalimbali sasa wamewataka wanasiasa kushindana kwa sera na hoja badala ya kutumia ghasia, huku hofu ikiongezeka kuwa mivutano ya Homa Bay inaweza kusambaa hadi kaunti jirani za Nyanza.

UGOMVI kati ya vijana wawili kuhusu mwanamke katika baa moja kwenye mpaka wa Kisii na Narok umegeuka kuwa vita vya kijamii, na kusababisha watu kujeruhiwa huku usafiri na biashara zikitatizika. Wiki mbili zilizopita, vijana hao walikuwa wakiburudika jioni katika baa inayopatikana katika kituo cha kibiashara cha Nyabitunwa walipoanza kupigana kuhusu mwanamke. Jamaa zao walijiunga, na kugeuza mzozo huo kuwa makabiliano yaliyoathiri Nyabitunwa, Kiango na Enoosaen. “Lilikuwa tukio dogo kati ya wanaume wawili ambalo lingeweza kutatuliwa hapa hapa, lakini kwa bahati mbaya lilizidi kuwa kubwa,” akasema Elvis Machoka, mkazi wa Nyabitunwa. Tangu wakati huo, baadhi ya familia zimekuwa zikilala vichakani kwa hofu ya kuvamiwa usiku. “Huwezi kupita Kiango-Enoosaen bila polisi. Waendesha bodaboda wamejiondoa. Eneo hili limeachwa,” alisema Peter Maisei, mkazi wa Enoosaen. Maafisa wa usalama na wazee wa jamii walisema mapigano hayo yameingia wiki ya pili, huku watu kadhaa wakitibiwa majeraha ya mishale. Barabara ya Kiango-Enoosaen sasa inaweza kutumiwa chini ya ulinzi wa polisi pekee. Naibu Kamishina wa Kaunti Ndogo ya Kenyenya, William Bett, alisema hali ya utulivu ilikuwa imeanza kurejea Jumapili asubuhi. “Tumepeleka maafisa wa kutosha wa usalama kukomesha mvutano huo. Kufikia asubuhi hii, utulivu wa kiasi umeanza kurejea. Jumapili tulifanya mkutano wa usalama katika eneo hilo kuwataka wakazi kudumisha amani kabla ya shule kufunguliwa kesho,” akasema Bw Bett. “Tungependa kuwahakikishia wazazi na wanafunzi ambao wamekuwa likizoni kwamba usalama utakwepo. Hatutaondoka hadi hali ya kawaida irejee kikamilifu,” akaongeza. Wakati huo huo, shughuli katika Kiwanda cha Sukari cha Transmara zimeathirika. Wafanyakazi wanaoishi upande wa Kisii wanalazimika kutumia njia ya Kisii-Kilgoris chini ya ulinzi wa polisi baada ya Kiango-Enoosaen kutopitika. “Malori yanayosafirisha sukari kuelekea Kisii na maeneo mengine hayawezi kupita Enoosaen. Hata usafirishaji wa miwa umeathirika,” akasema.

TANZANIA imeitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza uwekezaji, teknolojia na rasilimali fedha kwa ajili ya kurejesha ardhi iliyoharibika na kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda maeneo ya malisho, misitu na vyanzo vya maji. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),…

MJANE wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, Ida Odinga, amemuidhinisha mwanawe Raila Junior kuwania kiti cha ubunge Kibra katika uchaguzi mkuu wa 2027. Mama Ida alitoa kauli hiyo Jumatatu alipokuwa akiadhimisha miaka 76 ya kuzaliwa katika makazi yake Karen, Nairobi, sherehe iliyohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Kibra. Kwa mara ya kwanza, Mama Ida alizungumza wazi kuhusu nia ya mwanawe kuingia katika siasa, akisema ameamua “kumwachilia” kwa wakazi wa Kibra na viongozi wa Nairobi waliowahi kufanya kazi na Raila. “Nyinyi watu wa Kibra mmeamua na sina la kufanya. Namwachilia mwanangu mikononi mwenu. Viongozi mlio hapa, mtunzeni, mumfundishe na mumwelekeze. Wengi wenu mlianza siasa na Baba. Mwonyesheni njia,” akasema Bi Ida. Alisema Raila Junior anafaa kuendesha siasa safi bila matusi na vurugu, akisisitiza kuwa Kibra, ambayo ilijulikana kama “chumba cha kulala cha Baba”, ilikuwa nguzo muhimu katika safari ya kisiasa ya Raila. Mama Ida pia aliwataka wakazi wa Kibra kudumisha amani na umoja licha ya tofauti zao za kisiasa. Alisema hataweza kufanya kampeni kwa sababu ya wadhifa wake kama Balozi wa Kenya na Mwakilishi wa Kudumu katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), lakini aliwataka wakazi kupendana na kushirikiana. Raila Junior alisema aliamua kuwania Kibra baada ya kushauriana na wakazi na kwamba anafuata nyayo za babake ambaye alikuwa akishirikiana kwa karibu na wananchi wa kawaida. Alisema siasa za babake zilijikita katika kushirikisha wananchi mashinani, kusaidia wanawake na watu wenye mahitaji. “Nilikuwa uso wa Baba Kibra na nilimsaidia kutekeleza yale aliyoanzisha,” akasema Junior. Ingawa alikiri kuwa Peter Orero ndiye mbunge wa sasa wa Kibra, Raila Junior alisema wakati umefika mahitaji ya wakazi yashughulikiwe na mtu anayefahamu eneo hilo vyema. “Siasa za Baba hazitakufa. Lazima tuwepo, na nimesema nimeanza safari,” akasema.

IRINGA: WAKULIMA mkoani Iringa wamehimizwa kutumia mbegu bora na zilizoidhinishwa ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao, huku Serikali ikiimarisha mikakati ya kudhibiti mbegu bandia na kuwawezesha wakulima kupata pembejeo zenye ubora kwa wakati. Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za kuongeza uzalishaji wa kilimo mkoani humo, hasa wakati wakulima wakijiandaa kwa msimu mwingine…

The huge disparity had raised questions of whether some farmers or their cooperatives submitted fake claims.

The proposal requiring ISPs to submit subscriber-level internet usage data to the Communications Authority of Kenya has raised privacy concerns.

SERIKALI imepunguza zaidi bei ya mbolea na mbegu za mahindi katika juhudi za kuwasaidia wakulima wa Bonde la Ufa waliopata hasara kutokana na ukame. Bei ya mfuko wa kilo 50 wa mbolea umepunguzwa kutoka Sh2,500 hadi Sh2,000, huku bei ya kilo moja ya mbegu bora za mahindi ikishushwa kwa nusu kutoka Sh300 hadi Sh150. Hii inamaanisha pakiti ya kilo mbili itauzwa kwa Sh300 badala ya Sh600, huku mfuko wa kilo 10 ukigharimu Sh1,500 kutoka Sh3,000. Mfuko wa kilo 25 utauzwa Sh3,750 badala ya Sh7,500. Serikali italipa tofauti hiyo kupitia mpango mpya wa ruzuku. Rais William Ruto alitangaza hatua hizo wakati wa ziara yake Pwani, akisema serikali yake inalenga kupunguza mzigo kwa wakulima waliopata hasara kutokana na ukame. “Serikali yangu ilihama kutoka kutoa ruzuku kwa matumizi hadi kutoa ruzuku kwa uzalishaji kwa kupunguza gharama ya pembejeo. Hii itawawezesha wakulima kuzalisha zaidi katika hatua itakayoimarisha usalama wa chakula nchini,” akasema Rais Ruto. Kiongozi wa nchi alisema bei hizo mpya zitaanza kutumika Septemba katika vituo vilivyoteuliwa, kikiwemo Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB). Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe alisema mpango wa ruzuku ya mbegu unalenga kilo milioni 40 na utagharimu serikali Sh6 bilioni.

MUSOMA: SERIKALI imefikia asilimia 70 ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Musoma mkoani Mara, unaogharimu Sh bilioni 36.3, huku ikielezwa kuwa ujenzi huo upo katika hatua za mwisho za kuukamilisha. Ufafanuzi huo umetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ambapo amesema serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa…

CHAMA cha ODM kinataka baadhi ya sera zake muhimu zijumuishwe katika manifesto ya uchaguzi ya Rais William Ruto ya 2027 kama sehemu ya makubaliano ya kabla ya kuunda muungano kati ya chama hicho na UDA. Chini ya uongozi wa Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga, ODM pia inataka kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha kiufundi kati yake na UDA ili kubaini maeneo ambapo vyama hivyo vinaweza kukubaliana kusimamisha wagombea wa pamoja au kutopambana. Kutengwa huko kwa maeneo kumekuwa suala lenye utata, huku UDA ikipinga lakini ODM ikisema ni miongoni mwa masharti yake muhimu ili kumuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi wa 2027. Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga alisema chama hicho kinashinikiza sera zinazohusisha ushirikishaji katika masuala ya umma, kuimarishwa kwa ugatuzi, kugawanywa kwa haki kwa rasilimali ya taifa na kuimarishwa kwa vita dhidi ya ufisadi. Masuala mengine ni elimu bora na huduma za afya nafuu. ODM pia inaunga mkono mpango wa Nyumba za Gharama Nafuu, lakini inataka ugawaji wake uwe wa haki na uwazi. Rais Ruto na Dkt Oburu tayari wameunda kikosi cha kiufundi cha watu 10 kuandaa manifesto ya pamoja, huku kikosi kingine kikitarajiwa kushughulikia mazungumzo ya muungano.

President Samia Suluhu Hassan and African Diaspora Development Institute (ADDI) president Arikana Chihombori-Quao have discussed ways of strengthening cooperation between Tanzania, the institute and the African diaspora to support development across the continent. Their talks on Monday, August 24, 2026, at State House in Dar es Salaam focused on equipping young Africans with knowledge of the continent’s history, their role in development and the political and economic changes shaping the world, according to a statement from the Directorate of Presidential Communications. The discussions come at a time when African countries seek to strengthen the participation of young people and the diaspora in shaping the continent’s development and responding to global economic and political changes. According to the statement, President Hassan said young people needed knowledge that would help them understand the changing global environment and participate more effectively in shaping the future of their countries and Africa. She also stressed the importance of teaching young people patriotism and civic responsibility, including leadership, responsible use of information and participation in community and development activities. The talks also covered the role of women in raising children, building communities, leadership, preserving African culture and promoting indigenous knowledge. Ms Chihombori-Quao, who leads the ADDI, commended President Hassan for her leadership and Tanzania’s ongoing development initiatives. She said cooperation between Africa and the institute could help promote investment, connect knowledge and build a more positive narrative about the continent. The discussions also highlighted the role of Africans in the diaspora in contributing to the continent’s development through investment, knowledge and stronger links with their countries of origin. President Hassan commended Ms Chihombori-Quao for her longstanding efforts to advance Africa’s interests and strengthen relations between the continent and people of African descent living abroad.

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Dk Bashiru Ally, amefungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (4tFAR4ViBE), huku akisisitiza matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika kuendeleza sekta hizo kwa manufaa ya Taifa. Kongamano hilo la siku tatu limeanza leo, Agosti 24, 2026, katika Kituo cha Mikutano cha…

Foreign judges appointed to Tanzania’s Commission of Inquiry into violence and alleged breaches of the law during and after the October 2025 General Election have pledged to use their judicial and regional experience to help establish what happened and ensure the investigation is conducted independently. Namibia’s Deputy Chief Justice Petrus Tileinge Damaseb and Uganda’s Court of Appeal Judge Barishaki Bonny Cheborion are among the six commissioners appointed to investigate those who planned, financed, coordinated or participated in the violence, as well as allegations of excessive use of force, deaths, injuries and disappearances. Speaking in Dar es Salaam on Monday, August 24, 2026, Justice Damaseb said his appointment reflected the seriousness of Tanzania’s efforts to establish the facts surrounding the violence. He said he hoped his experience, particularly in judicial independence, would contribute to the commission’s work. “I hope that the small contribution that I will make in service of this commission strengthens that, most importantly, independence,” he said. Justice Damaseb said his appointment followed a request to Namibia’s Chief Justice and consideration of the experience required for the assignment. Justice Cheborion also pledged to use his abilities to help the commission complete its work. “We are here to ensure that we use our abilities to the best of our capacity, as God blesses us, so that we can conclude this matter safely and in the spirit of good neighbourliness,” he said. He cited the historical ties between Tanzania and Uganda, recalling Tanzania’s support to Uganda during the rule of former President Idi Amin. “Tanzania helped us during the time of Idi Amin Dada, and we have maintained good cooperation up to now. It is now time for us to contribute as well,” he said. Justice Cheborion, who also serves as an appellate judge at the East African Court of Justice, brings regional judicial experience to the inquiry. Their appointment has, however, attracted criticism in Namibia, where opposition parties Affirmative Repositioning (AR) and Independent Patriots for Change (IPC) have questioned Justice Damaseb’s participation. AR has urged him to reject the appointment, arguing that the involvement of a serving senior judge in a foreign inquiry could raise questions about Namibia’s judicial independence. The party has also asked Namibia’s Judicial Service Commission to explain the legal and ethical basis for his participation. President Samia Suluhu Hassan has defended the decision to include foreign judges, saying their involvement was intended to bring a broader perspective to the inquiry. “We decided to involve our colleagues from Namibia and Uganda to get a broader perspective,” President Samia said when launching the commission at State House in Dar es Salaam on August 7. The six-member commission is chaired by retired Court of Appeal Judge Shaban Ally Lila and has 150 days to complete its work. It was established following recommendations by a previous commission led by retired Chief Justice Mohamed Chande Othman, which investigated violence surrounding the 2025 election. That commission reported that 518 people died and thousands were injured in the violence.

Head of the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT), Dr Alex Malasusa, has urged believers to use their tongues wisely, saying the small organ can bring gain or loss, promote or destroy peace, and earn a person honour or contempt. Dr Malasusa said that, when used well, the tongue could be a great blessing, noting that some people are respected because of how they use it. He was speaking on Sunday, August 23, 2026, at the 17th General Assembly of Meru Diocese in Arumeru District, Arusha Region. He said that although the tongue is a small organ, its improper use could cause loss and disrupt peace. He likened it to a ship's rudder, explaining how a small object can determine the direction of something much larger. “The tongue is a very small organ and sometimes doesn't hurt, perhaps if someone gets an accident, but not something you can swallow a painkiller (pain medicine) for because it hurts,” he said. “The tongue is a small organ but one bringing gain; we can preach, and that is why we are here, but also at the same time it can bring loss and breach of peace; there are many people honoured in this world for no other reason than because they use their tongue well,” added Dr Malasusa. He reminded believers to use their mouths and tongues well, including strengthening unity within Meru Diocese. “This Sunday, we are reminded to use our mouths and tongues well. I am not sure whether I would say more if this were another diocese, but here I know that you have used your tongues well, even in coming to this assembly. There were no harsh words concerning the agendas we know about. You used them well, and where you may have erred, we thank Jesus because he gives us time to repent,” he explained. “Your tongue, my tongue is small, but it can rock a large ship or a marriage; it doesn't matter how many years it has, but if the tongue moves a bit it can rock it,” he added. “It can rock the good unity present within Meru Diocese; it is just a tongue, but it can heal, and the tongue has good work for one using it well to heal, and it can honour you or cause you to be despised,” he insisted. Head of ELCT Northern Diocese, Dr Fredrick Shoo, said the history of Meru Diocese showed how God's hand had guided the church and urged believers to remain hopeful as they prepare to elect a new bishop. “Looking back, we see how God's hand has been with you people of Meru Diocese, and we are filled with hope that this hand of the Lord will continue to be with you even this period when the Bishop's election will be held,” he said. “The word I would like to tell you and emphasise to you, as this matter has been spoken, let us leave it to God,” added Dr Shoo. Outgoing Meru Diocese Bishop, Dr Elias Nasari, thanked believers for praying for, supporting and encouraging him during his 10 years in office. “Thank you for supporting me, embracing me, and even where I failed the church and where I saw it was over, God told me the journey continues. I thank you very much for that period, and I cannot believe 10 years have passed since you elected me. Today is a very important day for the Diocese,” he said. “That is where we are going to humble ourselves under God's hand so that he can raise another leader who will carry this Diocese cooperating with him for another period that God will appoint,” added the Bishop.

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Uvuvi Tanzania (TAFICO), limesaini mkataba wa ujenzi wa meli mbili za uvuvi wa bahari kuu na Kampuni ya Rongcheng Xinyang Ship Industry Limited ya China, ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kuongeza tija katika sekta ya uvuvi nchini. Mkataba huo umesainiwa leo, Agosti 24, 2026,Jijini Dar es Salaam kupitia Programu…

BURUDI Nabwera alikuwa miongoni mwa wanasiasa wasomi zaidi waliohitimu kutoka taasisi mashuhuri za Uingereza wakati wa ukoloni. Elimu hiyo ilimwezesha kuelewa mifumo ya ubepari wa Magharibi na ujamaa wa Mashariki, maarifa yaliyomsaidia katika siasa na diplomasia baada ya Kenya kupata uhuru. Baada ya uhuru, Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, alimteua kuwa balozi nchini Amerika. Chini ya Rais Daniel arap Moi, Nabwera alipanda kutoka kuwa Katibu Mkuu wa KANU hadi kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, moja ya nyadhifa zenye ushawishi mkubwa serikalini. Alizaliwa mwaka 1924 na kusomea Maseno School, Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na London School of Economics. Akiwa Maseno, alikutana na Jaramogi Oginga Odinga, ambaye baadaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Kenya. Wengine waliosoma hapo ni Masinde Muliro na Wycliffe Wasia Awori, ambao baadaye walikuwa miongoni mwa wabunge wa kwanza wa Kenya katika Baraza la Kutunga Sheria (Legco). Akiwa Makerere, Nabwera alikutana na wasomi kama Bethwel Ogot, Thomas Odhiambo, Josephat Karanja, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais chini ya Moi, pamoja na mshairi wa Uganda Henry Muwanga Barlow, mwandishi wa shairi maarufu Building the Nation. Katika kitabu chake How it Happened, Nabwera alisema watu hao walimhimiza na kumsaidia kujenga taaluma yake ya baadaye. Katika uchaguzi wa kwanza wa kitaifa baada ya enzi ya Kenyatta mwaka 1979, Nabwera alishindwa na Joshua Angatia katika kiti cha ubunge cha Lurambi North. Wakati wa utawala wa Kenyatta, alikuwa mwanasiasa mwenye ushawishi na Waziri Msaidizi wa Mashauri ya Kigeni. Moi alitaka kuwatumia wanasiasa wakongwe pamoja na rafiki yake Moses Mudavadi kukabiliana na siasa kali za Martin Shikuku, Lawrence Sifuna na Waziri Elijah Mwangale, ambaye rais hakumwamini. Baada ya Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo kuporomoka kisiasa kufuatia uchunguzi kuhusu madai ya “uhaini”, Moi alianza kupanga upya KANU. Alimteua David Okiki Amayo kuwa mwenyekiti na Nabwera kuwa Katibu Mkuu wa tatu wa chama hicho. Katika kipindi hicho, Nabwera alijenga sifa ya kuwa mwanasiasa mkali, akitangaza sera za chama na kutishia wanachama waliokiuka maagizo kwa hatua za kinidhamu au kutimuliwa. Alipata umaarufu mkubwa mwaka 1986 baada ya kuonekana kwenye runinga ya taifa, Voice of Kenya (VoK), na kutangaza kwamba KANU ilikuwa tayari kuwasamehe wanasiasa waliofahamika kama “watu wa Njonjo”. Kauli hiyo ilizua hasira ndani ya KANU kwa sababu wakati huo ilikuwa mwiko kufikiria kuwasamehe wanasiasa waliokuwa wamehusishwa na Njonjo. Moi alikuwa amemshutumu Njonjo kwa kupanga njama na nchi ya kigeni kuangusha serikali. Rais alianzisha tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Jaji Cecil Miller, ambayo hatimaye ilimsafisha Njonjo. Hata hivyo, wanasiasa kadhaa waliodaiwa kuwa washirika wake walikuwa tayari wameanguka kisiasa. Kauli ya Nabwera ilipewa uzito mkubwa na vyombo vya habari, lakini ndani ya Ikulu na miongoni mwa viongozi wakuu wa KANU haikupokelewa vyema. Baadhi yao walimshutumu kwa kuwa mfuasi wa Njonjo. Muda mfupi baadaye, aliondolewa kama Katibu Mkuu na nafasi hiyo ikachukuliwa na Mudavadi. Akiwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Nabwera alikuwa na ushawishi mkubwa kuliko hata Katibu Mkuu wa KANU. Ofisi yake katika Harambee House ilitembelewa na wafanyabiashara, watu waliokuwa wakitafuta ajira na mabroka wa kisiasa waliotaka apelekee ujumbe wao kwa Rais Moi. Hata hivyo, kosa lake kubwa lilikuwa kushindwa kutofautisha masuala ya serikali na chama. Ushindi wake wa moja kwa moja katika eneo bunge la Lugari katika uchaguzi wa 1988 wa mlolongo, ulimfanya aamini zaidi nguvu za KANU. Katika uchaguzi wa 1992, alishindwa na Apili Wawire wa FORD-Asili. Kabla ya kuondoka Bungeni, Nabwera alihamishiwa Wizara ya Habari ambako aliendelea kutetea KANU. Alifanya mabadiliko katika taasisi za habari akilenga kuhakikisha zinaunga mkono chama hicho kabla ya uchaguzi wa vyama vingi wa 1992. Aliondoa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC), zamani VoK, James Kangwana, pamoja na bodi yake kupitia ilani ya serikali na kuwaweka watu alioamini walikuwa waaminifu kwa KANU. Nabwera pia alikosoa Benki ya Dunia kwa masharti yake makali ya misaada kwa Kenya, akipinga hasa pendekezo la kupunguza idadi ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vikuu.

SERIKALI imekataa wito wa upinzani na mashirika ya kiraia kwa Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC) kuchunguza kuongezeka kwa ghasia za kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Serikali imesisitiza kuwa idara za usalama na taasisi za sheria nchini zina uwezo wa kukabiliana na vitisho hivyo. Msimamo huo unajiri Amerika ikiongeza kampeni yake dhidi ya ICC, huku Muungano wa Ulaya na washirika wengine wa kimataifa wakitetea mahakama hiyo kama chombo huru cha haki duniani. Mjadala huo umeibua kumbukumbu za ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007, ambapo ICC ilianzisha uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata. Mkuu wa Mawaziri na Waziri wa Masuala ya Nje na Wakenya wanaoishi ng’ambo, Musalia Mudavadi, alisema Kenya imejitolea kuzingatia utawala wa sheria na haina haja ya kupeleka uchunguzi wa uhalifu wa ndani kwa taasisi za kimataifa. “Tuna wajibu wa kuimarisha na kulinda taasisi kama ICC,” alisema Bw Mudavadi katika mahojiano. Alisema Kenya haijawahi kukataa kuheshimu utawala wa sheria, iwe katika uwanja wa kimataifa au ndani ya nchi. “Serikali hii imefikishwa katika mahakama za humu nchini mara nyingi. Hatujawahi kukaidi maamuzi ya mahakama; daima tumeyaheshimu,” alisema. Bw Mudavadi alikataa wito wa taasisi za kimataifa kuingilia kati, akisema mahakama za Kenya na idara za usalama zina uwezo wa kukabiliana na ghasia na uvunjaji wa sheria kuelekea uchaguzi wa 2027. Alikumbusha Rais William Ruto alivyowahi kufikishwa ICC kuhusu tuhuma za ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007. “Rais wetu wa sasa, Ruto, alikuwa na ujasiri wa kukabiliana na ICC. Hii inaonyesha kwamba, mwishowe, anaheshimu utawala wa sheria,” alisema. Kesi dhidi ya Rais Ruto iliondolewa baadaye kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha. Kwa jumla, Wakenya sita waliwahi kushtakiwa katika ICC, akiwemo Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Kesi zote zilitibuka. Msimamo wa serikali unatofautiana na ule wa viongozi wa upinzani na mashirika ya kiraia yanayotaka uchunguzi wa kimataifa kuhusu kile wanachosema ni dalili za kuandaliwa kwa ghasia za kisiasa. Mnamo Jumatano, Muungano wa Upinzani, muungano usio rasmi wa wakosoaji wa Rais Ruto, uliitaka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ICC kuanza kuchunguza matukio ya hivi majuzi ya ghasia za kisiasa nchini. Kiongozi wa People’s Liberation Party Martha Karua, aliyesoma taarifa hiyo kwa niaba ya muungano huo, alitaja mashambulizi yaliyolenga aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua Rongai, Nakuru; tukio lililomlenga aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i Mulot, Bomet; ghasia zilizokumba mkutano wa Linda Mwananchi Homa Bay; na makabiliano ya awali Keumbu, Kisii. “Huu ni wito wa kuchukua hatua kuhusu ghasia za uchaguzi nchini Kenya,” alisema Bi Karua. “Matukio ya ghasia za kisiasa yanayoongezeka katika maeneo mbalimbali ya Kenya hayawezi tena kupuuzwa kama makabiliano ya kawaida kati ya wafuasi wa kisiasa wanaopingana.”

Chadema Chairman Tundu Lissu on Monday, August 24, 2026, named regional, international and national organisations that he said had opposed his prosecution on treason charges, describing the case as politically motivated. Mr Lissu, who is defending himself before the High Court’s Dar es Salaam Sub-Registry, gave the names as he continued presenting his defence in the case, which is being heard by a three-judge panel led by Justice Dunstan Ndunguru, assisted by Justices James Karayemaha and Ferdinand Kiwonde. The Chadema leader, who is also a lawyer, faces a treason charge under Section 39(2)(d) of the Penal Code, Revised Edition 2023. The prosecution alleges that on April 3, 2025, a Tanzanian citizen, Mr Lissu, with intent to incite, encouraged the public to prevent the holding of the 2025 General Election through statements and written messages aimed at pressuring Tanzania’s top government leader. Among the statements cited by the prosecution, Mr Lissu allegedly said: “If they say this position amounts to rebellion, it is true, because we are saying we will prevent the election, we will encourage rebellion... this election we will disrupt it completely.” Mr Lissu began his defence on Friday, August 21, 2026, after the court ruled that he had a case to answer. He first outlined his professional and political background, including his work as a lawyer and his political responsibilities. He also referred to honorary awards he has received from international organisations in recognition of his contribution to democracy and good governance, as well as statements by various regional and international organisations opposing his prosecution. Mr Lissu said the recognition and support demonstrated that he was a person of integrity and standing, rather than someone lacking credibility. Organisations cited Continuing his defence on Monday, August 24, 2026, Mr Lissu maintained that the case was political despite its treason prosecution. He told the three judges that several legal and political organisations in Tanzania, Africa and beyond had challenged his prosecution, arguing that the case was politically motivated. He cited the East Africa Law Society, the Southern African Development Community (SADC) Lawyers Association, the Pan African Lawyers Union, the Law Association of Zambia, the Law Society of Kenya and the Tanganyika Law Society. Other organisations he named included the International Commission of Jurists (ICJ), Amnesty International’s Regional Office for Eastern and Southern Africa and the Uganda Law Society. Mr Lissu also mentioned the Democrats Union of Africa (DUA), which brings together African political parties with political orientations similar to Chadema, and the Platform of Democratic Parties, a forum bringing together democratic political parties from 17 African countries. African commission resolution Mr Lissu also referred to the African Commission on Human and Peoples’ Rights, saying it had discussed his case during an emergency session on July 30, 2025. “Your Lordships, specifically on July 30, 2025, the African Commission on Human and Peoples’ Rights, whose headquarters are in Arusha, Tanzania, held an emergency session to discuss these charges,” Mr Lissu told the court. He said the commission subsequently adopted a resolution titled Resolution on the Human Rights Situation in the United Republic of Tanzania, which expressed concern over his arrest and prosecution. According to Mr Lissu, the commission also stated that the Tanzanian government had an obligation to comply with the African Charter on Human and Peoples’ Rights. Mr Lissu’s defence is continuing before the High Court as the court considers his evidence and legal arguments surrounding the treason charge.

TANZANIA: FITCH Ratings has raised Tanzania’s credit outlook to positive from stable, citing stronger foreign-exchange reserves, contained fiscal deficits and robust economic growth that should help put government debt on a downward trajectory. The ratings agency affirmed Tanzania’s longterm foreign- and localcurrency issuer default ratings at B+, according to its latest assessment. Fitch forecasts Tanzania’s…

DAR ES SALAAM; Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amewapongeza washiriki wa shindano la urembo la Miss Universe Tanzania kwa jitihada zao za kuwa mabalozi wa nishati safi ya Kupikia kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia nishati hiyo nchini. Naibu Waziri Salome amesema serikali itaendelea kushirikiana na jukwaa hilo muhimu katika kuifikisha ajenda ya…

BUNGE la Kenya linakabiliwa na kibarua kigumu cha kupitisha kwa haraka sheria muhimu za uchaguzi, huku mapendekezo kadhaa yakikwama kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang'ula alikuwa ameahidi kuharakisha miswada hiyo, lakini mwaka mmoja baadaye hatua kidogo ndiyo imepigwa hali inayozua wasiwasi kuhusu maandalizi ya nchi kufanya uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeonya kuwa kutungwa au kubadilishwa kwa sheria za uchaguzi karibu sana na siku ya uchaguzi kunaweza kutatiza pakubwa mipango yake ya utekelezaji na ununuzi wa vifaa na huduma. Mageuzi mengi yanayohitajika yalitokana na mapendekezo ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) na yanahusu marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi, Sheria ya Makosa ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Kisiasa. Pia kuna Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ufadhili wa Kampeni za Uchaguzi na kanuni zake, zinazolenga kuhakikisha wagombeaji na vyama vya kisiasa wanapata nafasi sawa katika mashindano. Miswada hiyo ilichapishwa mnamo 2024, ikapitishwa na Seneti na kuwasilishwa kwa Bunge la Kitaifa. Hata hivyo, marekebisho ya Sheria ya IEBC kuhusu kuundwa kwa jopo la kuchagua makamishina panapotokea nafasi wazi ndiyo mafanikio makubwa pekee yaliyopatikana hadi sasa. IEBC inasema hali hiyo inakiuka mapendekezo ya Tume Huru ya Uchunguzi wa Uchaguzi (IREC), iliyoongozwa na Jaji mstaafu wa Afrika Kusini Johann Kriegler, kwamba mageuzi ya sheria za uchaguzi yafanywe angalau miaka miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu. “Tabia hii inakinzana na mapendekezo ya Tume ya Kriegler kwamba mageuzi ya kisheria yafanywe angalau miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu,” IEBC iliambia bunge. Bw Wetang'ula hakujibu maswali kuhusu hatua iliyopigwa katika kuharakisha miswada hiyo. Hata hivyo, Oktoba 2025 alisema Bunge lilikusudia kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi miwili au mitatu. Miongoni mwa miswada inayosubiri ni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa 2024, ambao unapendekeza kampuni huru kufanya tathmini ya mchakato wa uchaguzi ndani ya mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu. Mswada mwingine unapendekeza adhabu ya faini ya hadi Sh2 milioni au kifungo cha miaka mitano kwa mtu anayefanya uchaguzi katika kituo ambacho hakijatangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali. Pia unalenga maafisa wanaochelewesha bila sababu kutangaza matokeo au kuyabadilisha kimakusudi. Wakati huohuo, Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa unapendekeza kufutwa kwa Kifungu cha 14A, hatua ambayo inaweza kurahisisha wanasiasa kuunga mkono vyama pinzani bila kupoteza moja kwa moja nyadhifa zao za uchaguzi.

WANASIASA sasa wanamtaka Gavana Abdulswamad Nassir awajibike baada ya walinzi wake kuhusishwa na ufyatuliaji wa risasi uliowajeruhi vijana watatu Changamwe. Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Mombasa, Bi Stella Cherono, vijana hao walimshambulia Gavana Nassir alipokuwa katika hafla ya kuhamasisha wakazi kuhusu mradi wa kutoa mikopo kwa makundi Changamwe. Bi Cherono alisema vijana hao walianza kuimba nyimbo za kumkejeli Gavana huyo, wakimtaja kama kiongozi wa “muhula mmoja”. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wamejitokeza kumshutumu Gavana Nassir kuhusu tukio hilo na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliohusika. Bi Cherono alisema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo umeanzishwa ili kubaini kilichotokea na waliohusika. Wanasiasa wakiongozwa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bw Hassan Omar, na Seneta mteule Bi Miraj Abdalla, walilaani tukio hilo wakisema wakazi wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu viongozi wao bila kutishiwa. “Kuna uhuru wa kuzungumza kwenye Katiba yetu. Jana nilikerwa sana. Naskia Gavana aliambiwa yeye ni wa muhula mmoja, na hiyo si siri, kila mtu anajua. Lakini akakasirika sana na ile hasira ikadhibitiwa na walinzi wake ambao walifyatua risasi na kujeruhi vijana wetu,” alisema Bw Omar. Bw Omar, ambaye anawania ugavana Mombasa, alisema wakazi wa Mombasa wana haki ya kumkosoa Gavana bila kuhofia usalama wao. “Kila mtu hapa Mombasa atasema wewe ni gavana wa muhula mmoja. Tuone kama watapigwa risasi. Haiwezekani tuogope. Haiwezekani ukatuambia sisi tumesimama pamoja, mwingine anajenga na wewe unavunja,” alisema. Walimtaka Gavana Nassir kuchukua jukumu kuhusu tukio hilo na kuhakikisha waliohusika wanawajibishwa. “Ukipiga watoto risasi unaharibia hii serikali. Na sisi wengine katika hii serikali hatuko na wewe. Usiwadhulumu wanyonge sababu ya umaskini. Serikali italinda hadhi ya maskini,” alisema Bw Omar. Tukio hilo limezua mjadala kuhusu matumizi ya nguvu na uwajibikaji wa maafisa wa usalama wanaolinda viongozi wa umma, huku polisi wakiendelea na uchunguzi. Wiki kadhaa zilizopita, mlinzi wa Mbunge wa Likoni, Bi Mishi Mboko, alinaswa kwenye kamera akifyatua risasi hewani wakati wa mkutano wa kisiasa. Watetezi wa haki za kibinadamu pia wamelaani tukio hilo na kumtaka Gavana Nassir awajibike. Haya yanajiri siku mbili baada ya tukio hilo, huku mmoja wa vijana waliojeruhiwa akinaswa kwenye kanda ya video akiwaomba wanasiasa kukoma kuingiza siasa katika kisa hicho. Kijana huyo, Sammy Owino, 24, alifichua kwamba awali alikuwa akifanya kazi katika serikali ya kaunti lakini baadaye alisimamishwa kazi. Hata hivyo, alisema alipata fursa ya kumwona Gavana Nassir na kumfuata ili kuzungumza naye, lakini vurugu zilizuka na risasi kuanza kufyatuliwa. “Mimi ndiye yule kijana nilipigwa risasi, na mahali imefikia nashukuru Mungu, hasa ndugu zangu ambao wamenishika mkono nikapata matibabu. Naomba hili swala lisiwekwe siasa kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa nafanya kazi kwa kaunti lakini kulikuwa na kutoelewana. Jana tulimfuata Gavana tukitaka kumuongelesha na alikuwa ameshatupokea, mara ghafla risasi zikaanza kupigwa. Risasi imeniingia,” alisema kijana huyo. Alisema ameona kwenye mitandao ya kijamii wanasiasa wakitumia suala hilo kama mada ya kisiasa. Kijana huyo alisema Gavana Nassir ndiye kiongozi pekee aliyemtembelea hospitalini baada ya kujeruhiwa. “Usitumie siasa kwa swala langu. Mimi si mhalifu, mimi ni mnyang’anyi? Mimi ni mmbangaizaji, hatuibi watu chochote. Mimi naangalia maisha yangu, mamangu na watoto wangu. Sitaki siasa,” alisema. Alisema anataka suala lake lichukuliwe kama tukio la kawaida la raia aliyejeruhiwa na si kama silaha ya kisiasa. Hata hivyo kiongozi wa chama cha Vibrant Democratic Party Bw Awiti Bollo aliitaka idara ya polisi kuwapokonya bunduki walinzi wa Gavana Nassir bunduki kwa kuhusika na ufyatuliaji risasi kiholela na kujeruhi vijana. "Hatutaki kuona vijana wa watu wakiumizwa sababu ya siasa na kusema Bw Nassir hatarudi mamlakani. Bw Nassir badala ya kujeruhi watoto wetu wapatie ajira wasafishe mji ambao umekuwa mchafu sana. Lakini kwenye uchaguzi mkuu wa 2027 utakiona cha mtema kuni, sababu umezoea kutetewa kinara wa ODM Bw Raila Odinga hayuko kupigia debe," alisema.

RUFIJI: TANZANIA has emerged as East Africa’s leading electricity producer, following the commissioning of the 2,115-megawatt Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP), a milestone that has more than doubled the country’s generation capacity. The project, inaugurated on Saturday by President Samia Suluhu Hassan in Rufiji, Coast Region, raises Tanzania’s total installed electricity capacity to 4,646MW against…

ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua amesema hatafika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) Agosti 27 kama alivyoamrishwa. NCIC ilimtaka kiongozi huyo wa DCP kufika saa nane alasiri kujibu madai ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea chuki za kikabila katika maeneo ya Vihiga, Kisii na Meru. Tume ilionya kuwa kutofika kunaweza kusababisha hati ya kukamatwa kutolewa. Hata hivyo, mawakili wa Gachagua wameiambia NCIC kuwa mteja wao atakuwa nje ya nchi kati ya Agosti 26 na Oktoba 20 kwa safari iliyopangwa kabla ya kuitwa. Mawakili hao pia wamelalamikia kutowasilishwa kwa ushahidi kamili, wakitaka rekodi halisi za video na sauti pamoja na tafsiri rasmi za baadhi ya matamshi yaliyotolewa kwa Sheng na Gikuyu. Wanadai matamshi hayo yamechukuliwa nje ya muktadha na hayakuwa na nia ya kuchochea chuki za kikabila. NCIC bado haijajibu barua hiyo. Wafuasi wa Bw Gachagua wamekosoa wito huo wakisema tume inatumiwa kisiasa dhidi ya upinzani.