
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


DODOMA; Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, leo Agosti 28 , 2026 amepokea rasmi jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Jina hilo limewasilishwa kwa Spika na Katibu wa Rais Balozi Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali, Nyamburi…

KUNA uwezekano wa Ziwa Bogoria na Ziwa Baringo kuungana hivi karibuni huku umbali kati yao ukipungua hadi chini ya kilomita tatu kutoka kilomita 20. Hali hiyo imezua hofu ya janga la kimazingira kwa kuwa maziwa hayo mawili yana sifa tofauti. Ziwa Baringo lina maji yasiyo na chumvi, huku Bogoria likiwa na maji yenye chumvi. Kwa zaidi ya muongo mmoja, wakazi wa Loboi, Baringo Kusini, wamekuwa wakishuhudia Ziwa Bogoria likipanuka na kuelekea kwenye makazi, mashamba na biashara zao. Maji hayo tayari yamemeza nyumba, kituo cha afya, maeneo ya malisho na maelfu ya ekari za mashamba. Wataalamu wanaonya kuwa iwapo maziwa hayo yataungana, mfumo wa ikolojia wa Baringo unaweza kuathirika pakubwa. Samaki, viboko, mamba na jamii zinazotegemea maji ya Baringo zinaweza kuwa miongoni mwa waathiriwa. Serikali sasa inapanga kujenga bwawa na mitaro ya kuzuia maji ya Bogoria kuelekea Baringo. Mpango huo unajumuisha ujenzi wa tuta la kilomita tano huko Sandai, bwawa katika Mto Waseges na mtaro wa takriban kilomita 40. Mtaro huo utatumika kuondoa maji mengi kutoka Baringo kuelekea Chemolingot na hatimaye Bonde la Suguta. Timu ya mashirika mbalimbali, ikiwemo Idara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, imekuwa ikichunguza eneo hilo. Gavana wa Baringo, Benjamin Cheboi, alisema mafuriko hayo yamezidi uwezo wa serikali ya Kaunti. “Mafuriko haya ni makubwa sana na kama serikali ya kaunti hatuwezi kuyakabili peke yetu. Ndiyo maana tumeomba usaidizi kutoka kwa serikali ya kitaifa na washirika wengine,” alisema. Wakazi wanasema Bogoria ilianza kupanuka kwa kasi mwaka 2010, hali iliyoongezeka mwaka 2013. Bw Bismark Kibet alisema zaidi ya vijiji sita, kikiwemo Chepng’erechi na Kaprong’uno, vimeathirika huku Bw Jonathan Tireito akisema wakazi walidhani maji yangepungua baada ya muda. “Tulidhani yangepungua lakini hayajapungua. Yamefunika nyumba, maeneo ya malisho, mashamba na hata zahanati yetu,” alisema Bw Tireito. Msimamizi Mkuu wa Hifadhi ya Bogoria James Kimaru, alisema eneo la ziwa limeongezeka kutoka takriban kilomita 34 za mraba mwaka 2013 hadi karibu kilomita 45 kwa sasa. Barabara na miundombinu mingine katika hifadhi hiyo imehamishwa, huku chemchemi za maji moto na maeneo yaliyokuwa yakivutia watalii kutazama flamingo yakizama. Profesa Simon Onywere, mtaalamu wa mipango ya mazingira na jiolojia, alisema umbali kati ya maziwa hayo ulipungua kutoka zaidi ya kilomita 20 hapo awali hadi kilomita saba mwaka 2020 na sasa ni chini ya kilomita tatu. “Kuungana kwa maziwa haya kumekaribia na ni suala la muda tu,” alisema. Alisema maji mengi kutoka Mto Waseges yanaendelea kuingia Bogoria, hivyo kuongeza uwezekano wa maji yenye chumvi kuelekea Baringo. “Ikiendelea hivi, Ziwa Baringo linaweza kuwa na maji ya chumvi na kuhatarisha samaki, viboko, mamba na jamii zinazolitegemea,” alisema. Serikali pia inapanga kutumia maji hayo kwa unyunyizaji, huku mpango mpana ukilenga angalau ekari 100,000 katika Baringo na Turkana. Wakati huo huo, Ziwa Baringo lenyewe limepanuka kutoka kilomita 178 za mraba hadi zaidi ya 260. Afisa Mkuu wa Hifadhi, Bw Jackson Komen, alisema nyumba, shule, biashara na hoteli zimeathirika.

Tanzania is targeting a return to the top of Africa’s cashew producers, with the Government seeking to raise production to one million tonnes by 2030 while increasing local processing.

KIKAO cha vinara wa upinzani kilichotarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027 kilimalizika Kiambu Jumatatu bila kutatua baadhi ya masuala muhimu yanayotishia juhudi za kuunda muungano mmoja wa kisiasa. Kikao hicho kilichopangwa kufanyika kwa siku mbili, Agosti 24 na 25, kilimalizika baada ya siku moja. Muungano huo unahusishwa na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i, kiongozi wa PLP Martha Karua, kiongozi wa Democratic Party Justin Muturi, Eugene Wamalwa wa DAP-Kenya na Peter Munya wa PNU. Viongozi hao walitia saini ahadi ya umoja na kukubaliana kumuunga mkono atakayeteuliwa kuwa mgombea wao wa urais. Hata hivyo, maswali muhimu kuhusu muungano huo bado hayajajibiwa. Yanahusu nani atakayeongoza muungano, afisi ya usimamizi itaundwaje, maamuzi yatafanywa kwa njia gani na mgombea wa urais atachaguliwa vipi. Hakukuwa na mwafaka kuhusu kubadilisha jina la Azimio wala jina jipya la muungano, ingawa Komboa Kenya Coalition bado inaonekana kuwa chaguo linalopendelewa na baadhi ya viongozi wa upinzani. “Kenya kwanza. Umoja badala ya mgawanyiko. Huduma badala ya madaraka,” viongozi hao walisema katika taarifa yao. Lakini kando na picha hiyo ya umoja, tofauti za kisiasa zinaendelea kujitokeza. Bw Gachagua hakuhudhuria kikao hicho na badala yake alimtuma naibu wake Cleophas Malala kumwakilisha. Duru zilisema Bw Gachagua alikerwa na matamshi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta katika kumbukumbu za aliyekuwa Makamu wa Rais Michael Wamalwa, ambapo alimtaja Bw Musyoka, Dkt Matiang’i na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kama baadhi ya wanasiasa wanaoweza kumkabili Rais William Ruto. Bw Gachagua, kwa mujibu wa duru hizo, hakufurahishwa na kutotajwa licha ya jukumu lake kubwa katika muungano huo. Pia kulikuwa na sintofahamu kuhusu kuhudhuria kwa Bw Musyoka. Baadhi ya watu wa karibu naye walidai alifika katika kikao hicho dakika za mwisho. Muungano huo pia bado hauna afisi inayofanya kazi kikamilifu. Duru za upinzani zilisema hakuna makubaliano kuhusu namna ya kumpata mgombea wa urais kwa sababu viongozi hao bado hawajajadili ripoti ya kiufundi iliyowasilishwa mapema mwaka huu. Hilo ni suala nyeti kwa kuwa karibu viongozi wote wakuu wa muungano huo wana matamanio ya urais au wana wafuasi wanaoamini kuwa wanafaa kumkabili Rais Ruto. Bw Gachagua alisema uteuzi wa mgombeaji urais unapaswa kufanyika baadaye. “Tutazungumzia mgombeaji wetu baada ya Krismasi. Hauwezi kusukuma mgombeaji atajwe sasa ilhali hauna idadi kubwa( ya wafuasi) na haujaanza kuhamasisha watu,” alisema. Bi Karua, Bw Wamalwa na Dk Matiang’i pia wanaendelea kuwa na ushawishi katika siasa za upinzani, huku umaarufu wa Bw Sifuna ukiongeza sura mpya katika mjadala wa urithi wa kisiasa. Hata hivyo, viongozi hao wanasisitiza kuwa swali la mgombea wa urais linaweza kusubiri. “Kuchagua mgombea mmoja wa urais ndilo jambo rahisi zaidi kati ya changamoto zote tulizo nazo. Tunaweza kukutana siku moja kwa chakula cha mchana na kabla ya chakula cha jioni tukawa tayari tuna mgombeaji,” alisema Bw Gachagua. Lakini changamoto za muungano hazikomei kwa uteuzi wa mgombea. Viongozi wanapaswa kukubaliana kuhusu nani atafanya maamuzi, iwapo maamuzi yatafanywa kwa makubaliano au kura, nani atasimamia afisi ya usimamizi na namna mizozo itakavyotatuliwa. Muungano huo pia unakabiliwa na ushindani wa kisiasa katika Mlima Kenya, ambako DCP ya Bw Gachagua inajaribu kujijenga kama chombo kikuu cha kisiasa. Kuanzishwa kwa People's Party of Kenya na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro baada ya kuondoka UDA ya Rais Ruto kumeongeza ushindani kuhusu chama kitakachodhibiti kura za eneo hilo. Kwa sasa, kikao cha Windsor kimezalisha tamko la umoja, lakini bado hakijaunda mfumo wa kisiasa unaoweza kudumishwa.Jaribio kubwa litakuwa wakati viongozi hao wataanza kugawana madaraka. Nani atakuwa sura ya muungano? Nani atadhibiti shughuli zake? Ni chama kipi kitapata nafasi gani? Na nini kitatokea viongozi wakuu wakitofautiana? Muhimu zaidi, ni yupi kati ya viongozi hao atakubali kumwachia mwingine azma ya kumkabili Rais Ruto mwaka 2027?

GHASIA za kisiasa zilitia doa ziara ya Rais William Ruto katika Kaunti ya Narok Jumatano, baada ya watu wasiopungua sita kujeruhiwa kwa mishale huku wengine kadhaa wakipata majeraha katika mapigano kati ya wafuasi wa Mbunge wa Emurua Dikirr, David Keter na mpinzani wake wa kisiasa Bernard Ng’eno. Fujo hizo zilitokea katika kituo cha biashara cha Mamboleo kabla ya hafla ya rais kuanza, hali iliyomlazimu Dkt Ruto kuwakemea viongozi hao hadharani na kuwataka kumaliza tofauti zao za kisiasa mara moja. Wafuasi wa pande hizo mbili walikabiliana kwa kutumia silaha kali ikiwemo mishale. Afisa mmoja wa polisi kutoka Narok, aliyeomba kutotajwa jina alithibitisha tukio hilo na kusema vurugu vilisababishwa mapigano kati ya vikundi vya wafuasi wa viongozi hao wawili kabla ya Rais kuwasili. Kwa mujibu wa afisa huyo, waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya St Clare’s Kaplong katika Kaunti jirani ya Bomet, huku mmoja akihamishiwa Hospitali ya South Rift mjini Kericho kwa matibabu maalumu. Mmoja alikuwa na mshale uliopenya karibu na taya na alitarajiwa kufanyiwa upasuaji. Wengine walijeruhiwa miguuni, mkononi, begani na mmoja alinusurika kupoteza jicho baada ya mshale kupenya karibu na paji la uso. Vurugu hizo zilimfanya Rais Ruto kutoa onyo kali dhidi ya siasa za uhasama. Katika mikutano yake mbalimbali, aliwataka viongozi kuacha tofauti zao na kuzingatia maendeleo ya wananchi. “Aina ya tofauti za kisiasa zinazochochea vurugu, majeraha na umwagaji damu hazipaswi kuruhusiwa. Ghasia hizi lazima zikome mara moja,” alisema Rais. Aliwataka viongozi kutambua kuwa uchaguzi unapokwisha, wajibu wao ni kuwaunganisha wananchi badala ya kuwagawanya. Rais pia alimhimiza Mbunge Keter kuchukua jukumu la kuwaleta pamoja wakazi wa Emurua Dikirr na kuzima migawanyiko iliyojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa Mei mwaka huu. Wafuasi wa Ng’eno walionekana wakipeperusha vitambaa vya rangi ya samawati wakati wa mikutano ya rais huku wale wa Keter wakionyesha rangi za chama cha UDA, jambo lililoonyesha wazi mgawanyiko uliopo katika eneo hilo. Dkt Ruto pia alimpongeza Ng’eno kwa kubaki ndani ya chama cha UDA licha ya kushindwa katika kura za mchujo na kumhimiza kuendelea kushirikiana na viongozi wengine kwa manufaa ya wananchi. Katika kura za mchujo za UDA zilizofanyika Machi 27, Keter alipata kura 13,749 dhidi ya kura 13,394 za Ng’eno. Baadaye katika uchaguzi mdogo wa Mei 14, Keter alishinda kiti hicho kwa kura 18, 266. Tukio hilo limeibua upya wasiwasi kuhusu ongezeko la makundi ya wahuni wa kisiasa huku taifa likielekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

MSAJILI wa Vyama vya Kisiasa, John Cox Lorionokou, amefichua kuwa vyama viwili vinavyobeba maneno muhimu yanayotumiwa na vuguvugu la Linda Mwananchi Movement tayari vimo katika mchakato wa usajili wa vyama vya kisiasa. Ufichuzi huo unaweza kutatiza juhudi za Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na washirika wake za kubadilisha vuguvugu hilo kuwa chama cha kisiasa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Moja ya vyama hivyo ni Liberty National Democratic Alliance Party, kinachojulikana kwa kifupi kama LINDA Party. Chama kingine ni Mwananchi Party. Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP), LINDA Party iliwasilisha jina hilo mnamo Novemba 15, 2024. Majina mengine yaliyowasilishwa pamoja na ombi hilo ni Liberty National Democratic Party (LNDP) na Liberty Democratic Alliance (LDA). Tangu wakati huo, chama hicho kimeendelea kupitia mchakato wa usajili. Viongozi wake ni Phenasio Thuku ambaye ni kiongozi wa chama, Karen Majanga anayehudumu kama Katibu Mkuu na Purity Ndanu ambaye ni Mweka Hazina wa Kitaifa. Msajili huyo pia alithibitisha kuwa ombi la kuhifadhi jina la Mwananchi Party liliwasilishwa na Pius Onyango mwezi Julai 2026 na bado linaendelea kufanyiwa tathmini. Bw Lorionokou alisisitiza kuwa chama ambacho jina lake limehifadhiwa hakiwezi kuchukuliwa au kubadilishwa na mtu mwingine bila kufuata taratibu za kisheria. Katika mahojiano maalumu, Bw Lorionokou alisema wazi kuwa Linda Mwananchi Movement si chama cha kisiasa kilichosajiliwa. “Linda Mwananchi Movement haijasajiliwa kama chama cha kisiasa. Ukweli ni kwamba si chama cha kisiasa kwa sasa,” alisema. Kuhusu amri ya hivi majuzi ya Jopo la Mahakama la kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa (PPDT), msajili huyo alisema kuwa haijazuia michakato ya usajili ambayo tayari ilikuwa imeanza. Alifafanua kuwa mahakama ilizuia tu ofisi yake kushughulikia maombi mapya yanayohusiana na jina la Linda Mwananchi kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa. “Hukumu hiyo ilizuia msajili kuhusu maombi mapya yanayohusiana na Linda au Mwananchi Movement. Maombi yaliyokuwa tayari katika mfumo yataendelea kushughulikiwa kama kawaida,” alisema. Matamshi hayo yanamaanisha kuwa mchakato wa usajili wa LINDA Party na ombi la Mwananchi Party bado unaendelea. Akizungumzia Pius Onyango, aliyewasilisha ombi la Mwananchi Party, Bw Lorionokou alisema ofisi yake haiwezi kuhusisha mtu huyo na mrengo wa kisiasa wa Seneta Sifuna au mwanasiasa mwingine yeyote bila ushahidi rasmi. “Hatuwezi kuhusisha mwombaji na kundi lolote la kisiasa isipokuwa taarifa hizo ziwe sehemu ya maombi yaliyowasilishwa,” alisema. Aidha, alikumbusha kuwa vyama vyote vinavyotaka kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 vinapaswa kuwa vimekamilisha usajili wao kufikia Oktoba 15, 2026. Alisema usajili wa chama cha kisiasa si jambo rahisi kama wengi wanavyodhani. Mbali na kuhifadhi jina, waombaji wanapaswa kuwasilisha katiba ya chama, itikadi zake, kuwa na makao makuu na ofisi katika kaunti 24, pamoja na kusajili angalau wanachama 1,000 katika kila mojawapo ya kaunti hizo. Hata hivyo, hakufunga kabisa mlango kwa Linda Mwananchi Movement kufanikisha mchakato huo kabla ya muda uliowekwa, akisema kila kitu kitategemea jinsi watakavyotimiza masharti ya kisheria. Msajili huyo pia alipuuza madai kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani kwamba ofisi yake inatatiza usajili wa vyama vinavyoonekana kuunga mkono upinzani. Alisema tangu aingie afisini Oktoba 13, 2025, idadi ya vyama vilivyosajiliwa imeongezeka kutoka 91 hadi 99, jambo ambalo linaonyesha kuwa sheria zinatumika kwa usawa kwa wote.

MOROGORO; Watanzania wameombwa kujenga utamaduni wa watu majirani kutambuana na inapotokea jirani yako humuelewi vizuri toa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali ya mtaa au polisi. Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 27, 2026 na Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania, Alex Mkama alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua Banda la Polisi Jamii katika Tamasha…

A Nigerian woman has raised the alarm after returning from Dubai to discover that her savings of about ₦3 million had allegedly disappeared from her bank account.

ABUJA — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has described the reported mass abduction of residents in Borgu Local Government Area of Niger State as “one case too many”, calling on the Federal Government to urgently rescue those still in captivity. Obi raised the alarm in a statement posted on his […]

RAIS William Ruto ameibua mjadala kuhusu nafasi ya Serikali iliyochaguliwa kutekeleza manifesto yake bila kuingiliwa na mahakama. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya 16 ya Katiba ya 2010 jijini Nairobi, Rais Ruto aliuliza ni kiasi gani cha nafasi Katiba inapaswa kupatia serikali iliyochaguliwa kutekeleza mpango ambao uliifanya ishinde uchaguzi. “Serikali iliyochaguliwa inapaswa kuwa na nafasi ya kikatiba kiasi gani kutekeleza mpango ambao ilichaguliwa kuutekeleza?” Rais aliuliza. Alisema changamoto hujitokeza wakati mipango ya Serikali inapopingwa mahakamani, akitaka kuwe na tofauti kati ya mahakama kuchunguza uhalali wa hatua za Serikali na kufanya maamuzi ya sera ambayo ni jukumu la taasisi zilizochaguliwa. Hata hivyo, Rais alisema uhuru wa Mahakama haupaswi kuhojiwa. “Mahakama lazima ibaki huru kutafsiri Katiba, kulinda haki na kubatilisha hatua zisizo halali,” alisema. Aliongeza kuwa Serikali inapokiuka sheria, inapaswa kuheshimu maagizo ya mahakama na kurekebisha mwenendo wake. Lakini alisema sera halali zinazotekelezwa ndani ya mamlaka ya taasisi zilizochaguliwa zinapaswa kuheshimiwa. “Kura hutoa mwelekeo. Katiba huweka mipaka. Taasisi za umma huhakikisha mambo hayo mawili yanaheshimiwa,” alisema. Kauli hiyo inajiri huku baadhi ya miradi mikuu ya Kenya Kwanza ikikumbwa na changamoto za kisheria, hasa kuhusu haki za wananchi, matumizi ya fedha za umma na mipaka ya mamlaka ya Serikali. Rais alitaja huduma ya afya kwa wote, nyumba za bei nafuu, utoshelevu wa chakula, elimu na ulinzi wa kijamii kuwa nguzo za ajenda yake ya mabadiliko ya kiuchumi. Aliuliza iwapo uchunguzi wa mahakama unaweza wakati mwingine kusababisha utekelezaji wa sera halali za Serikali kucheleweshwa. “Tunawezaje kulinda uchunguzi wa mahakama bila kuzorotesha utekelezaji halali wa Serikali? Tunawezaje kuhakikisha mfumo wa kuangalia na kusawazisha mamlaka unabaki kuwa chombo cha uwajibikaji badala ya kusababisha taasisi kukwama?” aliuliza. Rais pia alizungumzia maandamano ya Gen Z ya 2024, akisema vijana walikuwa wakitumia haki zao za kikatiba na walitaka kusikilizwa. Alisema vijana walitumia haki za kuzungumza, kukusanyika, kuandamana na kuwasilisha malalamiko kwa serikali. “Ujumbe wao ulikuwa wazi: walitaka kusikilizwa. Walitaka uwajibikaji zaidi, serikali bora na nafasi ya maana katika kuamua mustakabali wa taifa lao,” alisema. Kauli hiyo ni tofauti na ile aliyotoa Juni 25, 2024, alipotaja maandamano hayo kuwa “uhaini”. Rais pia alikiri madai ya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano hayo, yakiwemo kukamatwa kiholela, watu kutoweka na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Alisema kila madai ya ukiukaji wa haki yanayoweza kuthibitishwa yanapaswa kuchunguzwa kwa kina na kwa uwazi, na waliohusika wawajibishwe. Hata hivyo, alisisitiza kuwa haki ya kuandamana haijumuishi vurugu, uporaji au uharibifu wa mali. Naibu Rais Kithure Kindiki alisema maadhimisho hayo yalikuwa fursa ya kutafakari hatua ambazo Kenya imepiga katika kudumisha umoja na kuvumiliana. Kwa upande wake, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alisema kutoheshimiwa kwa maagizo ya mahakama ni tishio kwa utawala wa sheria. Alisema pia ukiukaji wa haki za waandamanaji na kutotekelezwa kwa Sura ya Sita kuhusu uongozi na uadilifu kunaweza kudhoofisha Katiba. Alionya kuwa uchaguzi ukisimamiwa vibaya au matokeo yake kuibwa, suala hilo linaweza kubadilika kutoka tatizo la kisheria na kuwa la kiusalama na kibinadamu. “Hatupaswi kurudi huko tena,” alisema.

The group raised its loan-loss provision by 30 percent to Sh273.9 million from Sh210.6 million, signalling continued caution over potential credit losses.

TotalEnergies stations also raised their price from N1,250 to N1,275 per litre, while Bovas stations adjusted theirs from N1,253 to N1,275 per litre.

DAR ES SALAAM: Tanzania inalenga kuvutia mitaji mikubwa zaidi kutoka Ulaya kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa sekta binafsi, hatua inayotarajiwa kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi. Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ameeleza hayo leo Agosti 27, Dar es Salaam, katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na wawakilishi wa wafanyabiashara…

KAGERA: Mkoa wa Kagera, kupitia Tume ya Umwagiliaji umepokea vifaa vya umwagiliaji kutoka Wizara ya Kilimo, vyenye thamani ya Sh bilioni 1.2 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kuendelea na uzalishaji wa mazao bila kutegemea mvua. Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uzalishaji wa kilimo kwa kuwawezesha wakulima kutumia teknolojia ya umwagiliaji…

DODOMA: Minister for Agriculture Daniel Chongolo has commended the Chief Parliamentary Draftsman and his team at the Office of the Chief Parliamentary Draftsman (OCPD) for their role in successfully drafting the Agricultural Laws (Amendments) Bill, 2026, which was unanimously passed by lawmakers in Dodoma on Thursday afternoon. Presenting the Bill in the National Assembly on…

By Chinedu Adonu ENUGU — Motorists plying the Enugu-Onitsha Expressway have raised the alarm over an abandoned heavy-duty truck obstructing the highway at 9th Mile Corner, describing the situation as a death trap for road users. The truck, which reportedly broke down about five days ago, has allegedly remained on the expressway, causing traffic congestion […]

Lawyers are divided over when Emmanuel Nchimbi ceased to be Tanzania’s Vice President after the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) expelled him from the party, two days after President Hassan accepted his resignation.

By John Alechenu ABUJA — The Council for the Regulation of Engineering in Nigeria, COREN, has approved tougher compliance and enforcement measures aimed at curbing engineering failures, raising professional standards and protecting public safety. Registrar and Chief Executive Officer of COREN, Prof. O.A.U. Uche, disclosed this in a statement on Thursday. He said the decisions […]

GEITA: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’oda, ameagiza viongozi wa serikali kushiriki, kufuatilia na kusimamia kikamirifu miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR). Mwang’oda ametoa maagizo hayo alipoongoza msafara wa mbio za mwenge kutembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha kata…

MJADALA kuhusu amani na uwajibikaji wa viongozi unapaswa kupewa uzito unaostahili uchaguzi mkuu wa 2027 unapokaribia. Hivyo basi, Uzinduzi wa Mwongozo kuhusu Uchaguzi Usio na Vurugu wa 2027 uliotayarishwa na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utengamano (NCIC) umejiri kwa wakati muafaka, ambapo dalili za kutovumiliana kisiasa, matamshi ya chuki na taarifa za kupotosha zinaanza kujitokeza. Historia ya Kenya imeonyesha kwamba uchaguzi ni nguzo muhimu ya demokrasia, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha migawanyiko iwapo hautasimamiwa kwa busara na uwajibikaji. Kwa sababu hiyo, wito wa NCIC kwamba ushindani wa kisiasa usije ukawa kwa gharama ya maisha ya wananchi, umoja wa taifa au utulivu wa nchi unapaswa kuungwa mkono na kila Mkenya. Ni jambo la kutia moyo kwamba, mwongozo huu haijawekwa kama jukumu la taasisi moja pekee. Badala yake, unahimiza ushirikiano kati ya serikali za kitaifa na kaunti, idara za usalama, vyama vya siasa, mashirika ya kiraia, viongozi wa dini, vyombo vya habari, vijana na wadau wa maendeleo. Mtazamo huu wa pamoja unatambua ukweli kwamba, amani na mshikamano haviwezi kujengwa na kundi moja peke yake. Msingi wa uchaguzi wa amani hujengwa kabla ya siku ya kupiga kura. Hujengwa kupitia lugha ya heshima, kuimarishwa kwa taasisi za umma, kushughulikiwa kwa malalamiko ya raia na kukuza mahusiano mazuri kati ya jamii mbalimbali. Kauli za viongozi zina nguvu kubwa katika kuunganisha au kugawanya wananchi. Ndio maana viongozi wa kisiasa, wanaowania nyadhifa na watu wote wenye ushawishi wanapaswa kujizuia, kuonyesha uzalendo na uwajibikaji katika matamshi yao. Vilevile, suala la vijana linastahili kuangaliwa kwa jicho pevu. NCIC imeeleza wazi kwamba vijana hawapaswi kuonekana kama nyenzo za kutekeleza vurugu za kisiasa, bali washirika wa kujenga amani. Huu ni ujumbe muhimu kwa jamii na kwa viongozi wa kisiasa ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia nguvu na hamasa ya vijana kwa malengo yanayohatarisha utulivu wa nchi. Mapambano dhidi ya matamshi ya chuki, ukabila na kupotosha pia yanahitaji kupewa kipaumbele. Katika enzi ya mitandao ya kijamii, ujumbe unaochochea uhasama unaweza kusambaa kwa haraka na kuathiri maelfu. Ni wajibu wa kila mwananchi kupima taarifa kabla ya kuzisambaza na kukataa kushiriki katika kampeni zinazolenga kugawanya taifa. Kenya ina nafasi ya kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia na nguvu ya mshikamano wake wa kitaifa. Uchaguzi wa 2027 unapaswa kuwa mfano wa ushindani wa kisiasa unaoheshimu tofauti za maoni bila kuzigeuza kuwa sababu za uhasama. Matheka ni mhariri wa habari

DODOMA; Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kilimo wa mwaka 2026 (The Agricultural Laws (Amendments) Act, 2026), ambao unapendekeza marekebisho katika Sheria Nne. Akiwasilisha muswada huo leo Agosti 27, 2027, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo amezitaja sheria hizo kuwa ni, Sheria ya Usalama wa Chakula, Sura ya 249, Sheria ya…

DAR ES SALAAM: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa ziara maalumu ya ujumbe kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Diaspora wa Kiafrika (ADDI) katika Makumbusho ya Taifa la Tanzania, jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyofanyika Agosti 26, 2026, imelenga kuwapa wageni fursa ya kujifunza historia, utamaduni na urithi wa Tanzania,…

TANGA: MBUNGE wa Jimbo la Mkinga, Twaha Mwakioja, ametekeleza ahadi yake baada ya kukabidhi pampu ya maji kwa ajili ya Shule ya Sekondari Lanzoni, pamoja na kutoa fedha taslimu na vifaa mbalimbali vya maendeleo na michezo katika wilaya hiyo. Katika ziara yake iliyofanyika katika Kata ya Mhinduro, Mbunge Mwakioja alikabidhi pampu hiyo inayolenga kupunguza kero…

MAHAKAMA Kuu jana ilizima kesi ya mauaji dhidi ya maafisa 15 wa usalama waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kuwateka na kuwaua raia wawili wa India na dereva wa teksi Mkenya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022. Jaji Francis Olel alikubali ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga la kusitisha kesi hiyo hatua iliyohitimisha mashtaka yaliyokuwa yamesubiriwa kwa zaidi ya miaka miwili. Jaji Olel alisema DPP alitumia mamlaka aliyopewa na Katiba kwa njia halali. “Nimebaini kuwa kuwasilishwa kwa ombi hili kulifanywa kwa mujibu wa sheria, kwa nia njema na kwa kuzingatia maslahi ya umma,” jaji alisema. Hata hivyo, mahakama ilifafanua kuwa kuachiliwa kwa washukiwa hao hakumaanishi hawana hatia, wala hakuzuii kushtakiwa tena iwapo ushahidi mpya utapatikana. Maafisa hao walitoka katika Kikosi Maalumu SSU kilichovunjwa, Idara ya Ujasusi wa Kitaifa (NIS) na shirika la KWS.

KAGERA: Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 unatarajiwa kuzindua, kufungua, kutembelea kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 54 ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 23.7 mkoani Kagera. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Kido, amesema mwenge huo utapokelewa wilayani Muleba katika Kijiji cha Nyakabango ukitokea…

ULAANBAATAR: Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi endelevu wa maeneo ya malisho na rasilimali za udongo, huku ikieleza kuwa ukame, malisho kupita kiasi na mabadiliko ya tabianchi vinaendelea kuongeza tishio kwa maisha ya wananchi na usalama wa chakula. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alitoa kauli…

WAPELELEZI mjini Mombasa wanachunguza kisa cha picha ya Mbunge wa Mvita, Mohamed Machele, kubadilishwa na kuonyesha kana kwamba alikuwa mhudumu katika harusi ambako alikuwa mgeni mkuu, katika kile kinachodaiwa kuwa njama ya kumwaibisha. Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imewasilisha ombi mahakamani ikitaka kupewa ruhusa ya kuchunguza simu ya mkononi inayohusishwa na aliyekuwa mshirika wa karibu wa mbunge huyo, Bw Haani Omar Swaleh, huku uchunguzi wa madai ya unyanyasaji wa mtandaoni ukiendelea. Bw Machele alihudhuria harusi ya mwana wa Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Pwani, Ali Nuno, mnamo Juni 20 katika eneo la Nyali, Mombasa, ambako alipigwa picha kadhaa akiwa pamoja na wageni wengine. Kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama, mbunge huyo alishtuka baadaye alipojulishwa kuwa picha yake ilikuwa ikisambaa kwa wingi mitandaoni. Picha hiyo ilikuwa imehaririwa na kuonyesha kana kwamba alikuwa amevalia mavazi ya mhudumu katika harusi hiyo na kuchapishwa kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp ya Bw Swaleh. “Baada ya kuhudhuria hafla hiyo, aliarifiwa kwamba alikuwa akivuma mtandaoni. Picha yake akiwa amevalishwa mavazi yaliyomwonyesha kama mhudumu katika harusi hiyo ilikuwa imechapishwa kwenye akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp ya mshukiwa,” stakabadhi hizo zilisema. Akiwa amekerwa na picha hiyo, Bw Machele aliripoti tukio hilo katika Kituo Kikuu cha Polisi Mombasa, chini ya nambari ya OB 49/23/7/ 2026. Inspekta Joseph Ngatia, mpelelezi wa DCI, alisema mbunge huyo aliripoti tukio hilo miongoni mwa sababu nyingine kwa kuwa yeye ni mtu mashuhuri na mbunge anayehudumu. Jumanne, DCI iliwasilisha ombi mahakamani ikimtaja Bw Swaleh kama mshukiwa anayechunguzwa kuhusu picha hiyo iliyohaririwa. Wapelelezi wanasema Bw Swaleh alikamatwa Agosti 20 na simu aina ya iPhone 11 ikachukuliwa kutoka kwake. Simu hiyo ina nambari mbili za IMEI na, kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama, inaaminika kuwa ndiyo iliyotumika kubadilisha picha hiyo. Orodha ya vitu vilivyopatikana iliandaliwa baada ya simu hiyo kuchukuliwa. DCI inataka idara ya Uchunguzi wa Kisayansi cha Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) kipewe ruhusa ya kuishikilia simu hiyo, kuifikia na kuifanyia uchunguzi pamoja na kutoa taarifa kutoka kwa akaunti za WhatsApp, Facebook na TikTok kwa kipindi cha Juni 20 hadi Julai 20, 2026. Inspekta Ngatia alisema uchunguzi huo wa kisayansi utawasaidia wapelelezi kubaini mazingira ya picha hiyo na kupata ushahidi utakaotumika mahakamani. Wapelelezi pia wanataka mahakama iagize kitengo hicho cha ATPU kuandaa ripoti kuhusu taarifa zilizotolewa kwenye simu hiyo na kutoa cheti cha ushahidi wa kielektroniki kwa mujibu wa Kifungu cha 106B (4) cha Sheria ya Ushahidi. Inspekta Ngatia alisema taarifa wanazotaka kupata ni za kibinafsi na zinaweza kufikiwa tu kwa idhini ya mahakama. “Ni kupitia amri hii pekee ambapo ATPU inaweza kufikia, kuchunguza kwa njia ya kisayansi na kutoa taarifa hizo za kibinafsi zilizohifadhiwa kwenye simu ya mshukiwa,” alisema. Aliongeza kuwa taarifa zitakazopatikana zitawasaidia wapelelezi kukusanya na kuthibitisha ushahidi unaohusiana na malalamishi hayo. Uchunguzi huo unahusu madai ya unyanyasaji wa mtandaoni unaotokana na kuundwa, kuhaririwa na kusambazwa kwa picha ya mbunge huyo kwenye mitandao ya kijamii. Kosa hilo linachunguzwa chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandaoni ya mwaka 2018. Wapelelezi wanataka kubaini jinsi picha hiyo ilivyohaririwa, aliyehusika katika kuisambaza na iwapo vitendo hivyo vinaweza kuainishwa kama kosa chini ya sheria hiyo.

KAMPALA, Uganda: MKUU wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa Rais Yoweri Museveni, ametangaza kuwa atawania urais katika uchaguzi wa mwaka 2031. Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 52, kwa muda mrefu ametajwa kuwa mrithi anayetarajiwa wa baba yake mwenye umri wa miaka 81, ambaye ametawala Uganda kwa miongo minne. Mkuu huyo wa jeshi pia anafahamika kwa jumbe zake zenye utata kwenye mtandao wa kijamii wa X, zikiwemo tishio la kumkata kichwa kiongozi mkuu wa upinzani, Bobi Wine. Katika ujumbe mmoja kati ya mfululizo wa machapisho aliyoweka X Jumanne usiku, Kainerugaba alisema alikuwa tayari kuwania wadhifa wa juu zaidi nchini humo. "Nitawania wadhifa wa juu zaidi nchini mnamo 2031. Na tutashinda kwa neema ya Mwenyezi Mungu," akasema Kainerugaba. Aliongeza kuwa kwa kuungwa mkono na baba yake, ambaye huwa anamrejelea kwa heshima kama “Mzee”, ana uhakika wa kupata asilimia 90 ya kura katika uchaguzi huo. Kainerugaba, ambaye anaongoza kundi la wazalendo wa Uganda (PLU), hapo awali alikuwa ametangaza kuwa angewania urais katika uchaguzi uliofanyika Januari mwaka huu, lakini baadaye akajiondoa na kumuunga mkono baba yake. Alikuwa na nafasi muhimu katika kampeni za kuhakikisha Museveni anachaguliwa tena Januari, huku akiamuru hatua kali dhidi ya wapinzani na kuzimwa kwa intaneti, kulingana na ripoti zilizozingira uchaguzi huo tata. Museveni, ambaye anaongoza chama tawala cha National Resistance Movement (NRM), amekuwa madarakani tangu 1986. Wakosoaji wamekuwa wakiilaumu serikali yake kwa ukiukaji wa haki za binadamu, yakiwemo mateso, utekaji nyara na kuwazuilia watu kiholela, madai ambayo serikali imekanusha. Bobi Wine alikimbilia Amerika mapema mwaka huu, akisema alihofia maisha yake baada ya kupinga ushindi wa Museveni akidai kulikuwa na visa vya udanganyifu. Mwanasiasa mwingine mkongwe wa upinzani, Kizza Besigye, amekuwa gerezani tangu 2024 na anakabiliwa na kesi ya uhaini. Licha ya afya ya Besigye kuendelea kudorora, utawala wa Museveni hauonekani kumakinikia kumwaachilia huru. Haijulikani iwapo Museveni mwenyewe atawania tena urais 2031 baada ya tangazo lake, huku serikali ikisema uamuzi huo utafanywa na rais pamoja na chama chake kwa wakati mwafaka. Mnamo 2031, Museveni atakuwa na umri wa miaka 86 na akiwania, atakuwa kati ya viongozi wakongwe zaidi ambao wamewahi kuwania wadhifa wa urais ulimwenguni.

Recurring incidents of violence at football grounds in Zanzibar, including pitch invasions, attacks on referees, fights between players and abandoned matches, are raising concerns about safety in the sport.

CHAMA cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kinazidi kujitokeza kama tishio kubwa kwa Jubilee, chama cha aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, huku kikivamia ngome zake za kisiasa za Mlima Kenya na Nairobi. Huku Uchaguzi Mkuu wa 2027 ukikaribia, Jubilee imepata pigo jingine, viongozi wake kadhaa waliochaguliwa wakitangaza kuhamia DCP. Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan ndiye wa hivi punde kuondoka Jubilee, hatua inayoonyesha kuwa ushindani kati ya vyama hivyo haupo katika eneo la Mlima Kenya pekee. Nairobi, wabunge wote watatu waliochaguliwa kwa tiketi ya Jubilee wametangaza kuwa watatetea viti vyao kwa tiketi ya DCP. Hao ni Bw Hassan, Mark Mwenje wa Embakasi Magharibi na Amos Mwago wa Starehe. Mlima Kenya, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Kega, aliyedhaminiwa na Jubilee, pia amehamia DCP. Viongozi wengine wa Jubilee, wakiwemo wabunge walioteuliwa Sabina Chege, Aden Keynan (Eldas), Samuel Arama (Nakuru Mjini Magharibi), John Waluke (Sirisia) na Racheal Nyamai (Kitui Kusini), wameegemea Serikali Jumuishi. Kuhama huku kunaweza kudhoofisha uwezo wa Bw Kenyatta kujadiliana kisiasa kuelekea 2027 na kumfanya Bw Gachagua kuwa mhusika mkubwa katika siasa za upinzani. Akizungumzia hatima ya Jubilee, Bw Kega alisema wazi kuwa chama hicho kimekufa kisiasa Mlima Kenya na Nairobi. “Hakuna Jubilee Mlima Kenya na Nairobi. Tatizo linaloikabili Jubilee ni ukosefu wa uongozi. Tulipojaribu kufanya mabadiliko, yalipingwa, na sasa mnaona kinachotokea. Kila mtu anaondoka,” akasema Bw Kega. Hata hivyo, Naibu Kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alipuuza kuhama kwa viongozi hao, akisema wengi wao hawakuwa waaminifu kwa chama hicho na walikitumia tu kupata nyadhifa serikalini. “Si hasara mpya kwetu kwa sababu hawajawahi kujitambulisha na Jubilee. Kwa kweli, ni fursa kwetu kutafuta vijana ambao wamejitolea kuwa nguzo wa chama,” akasema Bw Kioni. Alidai kuwa DCP inaonekana kujishughulisha zaidi na kupambana na Jubilee kuliko UDA. Bw Gachagua, hata hivyo, alitangaza Jumanne kuwa DCP imechukua usukani wa siasa za Nairobi baada ya Bw Hassan kujiunga na chama hicho. “Ninataka kutangaza leo kwamba DCP imechukua Nairobi,” akasema kiongozi huyo wa DCP. Naibu kiongozi wa DCP Cleophas Malala alisema kuhama kwa Bw Hassan ni ushahidi kuwa chama hicho kinageuka kuwa na sura ya kitaifa, huku Katibu Mkuu John Methu akiahidi uteuzi wa haki kwa wagombeaji. “Nimejiunga na DCP kwa sababu ni chama kinachotaka mabadiliko halisi,” akasema Bw Hassan. Kwa kuhama huku, vita vya kisiasa kati ya DCP na Jubilee vinaonekana kuingia katika hatua mpya, huku Nairobi na Mlima Kenya zikitarajiwa kuwa maeneo muhimu ya mapambano kuelekea 2027.

VITA vya kisiasa vya kusaka kura za jamii ya Maa vinazidi kupamba moto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, huku Rais William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua wakiongeza juhudi za kutafuta uungwaji mkono katika jamii ya wafugaji. Maa ina ushawishi mkubwa katika kaunti za Kajiado, Narok na Samburu, na pia ina idadi kubwa ya wakazi katika baadhi ya maeneo ya Laikipia. Takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) zinaonyesha kuwa kaunti hizo tatu zinaweza kuwa na zaidi ya wapigakura milioni 1.4 waliosajiliwa kufikia uchaguzi wa 2027. Kwa miaka mingi, siasa za Maa zilidhibitiwa pakubwa na mwanasiasa mkongwe William Ole Ntimama, aliyefariki Septemba 1, 2016. Baada ya kifo chake, eneo hilo lilibaki likimuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, ambaye alifariki Oktoba mwaka jana na kuacha pengo la kisiasa ambalo viongozi mbalimbali sasa wanajaribu kujaza. Hakuna mwanasiasa kutoka jamii hiyo ambaye ameweza kujaza nafasi iliyowahi kushikiliwa na Bw Odinga na Bw Ntimama. Juhudi za Seneta wa Narok Ledama Ole Kina kujijenga kama kinara wa Maa pia zinaonekana kudidimia, huku ushawishi wa familia ya Ntutu, inayojumuisha Gavana wa Narok Patrick Ole Ntutu na Mbunge wa Narok Kusini Kitilai Ole Ntutu, ukiendelea kupungua. Rais Ruto alitembelea Narok Jumanne na kuwataka wakazi kumpima kwa rekodi yake ya maendeleo. “Wakenya wanataka maendeleo wala si maneno matupu. Narok ni kaunti yenye utajiri wa kilimo na hakuna sababu kwa nini msipate barabara nzuri,” akasema Rais. Alizindua ujenzi wa barabara ya Enengetia-Olkurto-Olposimoru yenye urefu wa kilomita 59 na kutaja miradi mingine ya barabara inayoendelea katika kaunti hiyo. Pia alisema Sh2.8 bilioni zitatumika kuunganisha nyumba 15,000 zaidi na umeme. Alisema nyumba 14,000 zimeunganishwa na umeme katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kwa upande wake, Bw Gachagua ameendelea kuvutia jamii ya Maa kwa usaidizi wa Seneta wa Kajiado Seki Lenku na Mbunge wa Kajiado Kusini Samuel Parashina. Alitembelea Narok Agosti 21, ambako alizuru Emurua Dikirr na kaburi la aliyekuwa mbunge Johana Ng’eno. Mbunge wa Kajiado ya Kati Memusi Kanchory alisema viongozi wanaounga mkono Serikali Jumuishi wanaunga mkono azma ya Rais Ruto ya kuchaguliwa tena 2027. “Hapa tuko kwa mihula miwili na tunafanya kazi katika Serikali Jumuishi, lakini kuna viongozi ambao wameazimia kutugawanya kwa sababu hawafurahishwi na ushirikiano wetu,” akasema Bw Kanchory. Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku, hata hivyo, amekosana na ODM na ametishia kutafuta chama kingine atakachotumia kuwania useneta wa Kajiado. “Tulipata ODM ikiwa dhaifu na kwa sababu tulimheshimu aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga, tuliimarisha chama hicho Kajiado. Kama vile madiwani wa UDA walivyojiunga na DCP, sisi pia tutaondoka na kujiunga na Linda Mwananchi,” akasema Bw Lenku.“ODM itafunga shughuli zake katika Kaunti ya Kajiado. Sisi ndio tulileta ODM hapa na kuifanya iheshimike,” akaongeza. Kwa upande wake, Bw Gachagua amejitaja kama mtetezi wa maslahi ya Maa, hasa kuhusu suala la ardhi. “Raila Odinga amekuwa akiwatetea tangu zamani. Mungu amemchukua. Nataka mnifanye kuwa mtetezi wenu. Nitatetea na kusimamia maslahi yenu bila woga, hasa kuhusu suala la ardhi,” akasema wakati wa ziara yake Kajiado Februari mwaka huu. Katika uchaguzi wa 2022, Raila alishinda Ruto katika kaunti zote tatu. Kajiado alipata kura 158,526 dhidi ya 148,439 za Ruto, Narok alipata 102,279 dhidi ya 92,894, huku Samburu akipata 41,737 dhidi ya 28,319.

The decision marks a major turn in Dr Nchimbi’s political career. He previously served as CCM Secretary-General before becoming President Samia’s running mate in the October 2025 General Election.

MAAFISA wa polisi nchini wataanza kuvalia sare mpya kuanzia Ijumaa na kutelekeza ile ya rangi ya samawati iliyozinduliwa wakati wa utawala wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Sare hizo mpya zitachukua nafasi ya sare za sasa zinazovaliwa na maafisa wa polisi wa kawaida, huku Polisi wa Utawala (APS) na Kitengo cha Kupambana na Ghasia (GSU) wakitarajiwa kuendelea kutumia sare zao za sasa. Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja alisema mabadiliko hayo yamekumbatiwa baada ya malalamishi ya polisi kuhusu mavazi ya sasa. “Tumeitumia sare ya rangi ya samawati iliyokolea, kwa hivyo sasa tumerudi kwenye ile tuliyokubaliana. Ninataka pia kubainisha kuwa Jumatatu nami nitakuwa nimeivaa hiyo sare mpya,” akasema Bw Kanja. Inspekta Jenerali huyo alizungumza Jumanne baada ya kuhudhuria gwaride la mazoezi la polisi wa cheo cha konstebo waliokuwa wakipata mafunzo katika Chuo cha Polisi cha Kiganjo, Kaunti ya Nyeri. Alisema polisi wanaotarajiwa kuhitimu Ijumaa watakuwa wa kwanza kuvalia sare hizo mpya. [caption id="attachment_191564" align="alignnone" width="2560"] Maafisa wa polisi wakiwa wamevalia sare mpya katika Kenya School of Government (KSG) Alhamisi, Septemba 13, 2018. PICHA | MAKTABA[/caption] Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua rasmi sare hizo katika Chuo cha Polisi cha Kenya wakati wa hafla ya kuhitimu kwa polisi 10,000 wa cheo cha konstebo, ambao baadaye watajiunga na idara ya polisi. Bw Kanja alisema hatua ya kubadilisha sare inalenga kuinua ari ya maafisa na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Mabadiliko hayo yanajiri kufuatia zoezi la ushirikishaji wa umma lililofanyika 2023, ambapo maafisa wengi wa polisi walikataa sare za sasa za samawati iliyokolea na kutaka zibadilishwe ili ziwe za starehe zaidi na zinazostahili mahitaji ya kazi yao. Mnamo 2018, Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) ilianzisha sare za sasa za rangi ya samawati kama sehemu ya ajenda ya mageuzi katika idara ya polisi. Hata hivyo, muundo huo wa rangi, haukupokelewa vyema na baadhi ya maafisa. Wengine walidai kuwa sare hizo hazikuwa za starehe wala za kuvutia. Baadhi yao hata walizilinganisha na mavazi yanayovaliwa na wanakwaya makanisani. Lakini hatua ya serikali ya Rais Ruto kuanzisha sare mpya inaibua maswali kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na Jopo la Kuangazia Mageuzi ya Polisi aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga. Jopo hilo lilipendekeza polisi wavae sare zao za zamani kwa muda wa miaka mitatu huku mchakato wa kubuni sare mpya ukianzishwa kwa kufuata mapendekezo yaliyomo katika ripoti yake. “Kuhusu sare za NPS, kwa kuzingatia maoni mengi ya wananchi, maafisa wa polisi wenyewe na uongozi wa NPS, jopo linapendekeza NPS irejee kwa sare zake za zamani kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya mchakato wa kubuni sare mpya utaanzishwa kwa mujibu wa mapendekezo katika ripoti hii,” ikasema ripoti hiyo. Ripoti hiyo pia ilipendekeza kuanzishwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Sare, ambayo ingejumuisha wawakilishi kutoka huduma mbalimbali za usalama na taasisi za maafisa wanaovaa sare. Kulingana na mapendekezo hayo, Waziri wa Ulinzi, kwa kushauriana na Waziri wa Usalama wa Ndani, angeandaa sheria ya kuanzisha kamati hiyo yenye jukumu la kuidhinisha viwango, rangi na ubora wa sare zinazotumiwa na kila huduma. “Kamati hiyo inapaswa pia kushughulikia matumizi mabaya ya sare na wananchi,” ripoti hiyo ilisema. Mbali na sare, ripoti ya jopo hilo ilibaini mapungufu katika usimamizi wa rasilimali za polisi. Ilibaini kuwa huduma hizo hazikuwa zimeweka kikamilifu mifumo yao ya rasilimali watu katika mfumo wa kidijitali, hali ambayo imekuwa ikizua mianya ya udanganyifu, ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka. Pia, baadhi ya kazi za rasilimali watu zinafanywa na maafisa wenye sare ambao hawana mafunzo ya kitaalamu katika usimamizi wa wafanyakazi, jambo ambalo limechangia makosa katika masuala ya kiutawala. Jopo hilo lilipendekeza kuwa, isipokuwa masuala ya kiutendaji yanayohusu kupelekwa kwa maafisa katika maeneo mbalimbali, kazi nyingine zote za rasilimali watu zisimamiwe na wataalamu wenye mafunzo, tajriba na uwezo unaohitajika. “Uwekaji kamili wa huduma zote za rasilimali watu katika mfumo wa kidijitali, ikiwa ni pamoja na malipo ya marupurupu, utahakikisha mahitaji ya maafisa wote wa NPS yanashughulikiwa kwa haraka,” ripoti hiyo ilisema.

DAR ES SALAAM: THE ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) has expelled former Vice President of the United Republic of Tanzania, Dr Emmanuel Nchimbi, from the party. CCM Secretary-General Dr Asha-Rose Migiro said the decision was reached by the party’s organs, including the Central Committee, as part of disciplinary and ethical measures taken against some party…

A local Kiswahili weekly tabloid “Mwana Halisi” was recently banned by the Tanzanian government after it published a lead story claiming that the Vice President was being forced to resign but refused to bow to the pressure.

DAR ES SALAAM – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempendekeza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kujiuzulu kwa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi. Pendekezo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za CCM, Lumumba, Dar…

DAR ES SALAAM: THE ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) has appointed the Energy Minister, Deogratius Ndejembi, to serve as the Vice President of the United Republic of Tanzania. The decision follows the resignation of the former Vice President, Dr Emmanuel Nchimbi. CCM Secretary-General Dr Asha Migiro announced the decision today, August 26, 2026, while addressing…

DAR ES SALAAM – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemfuta uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, kwa tuhuma za utovu wa nidhamu. Uamuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi ndogo za CCM,…

DAR ES SALAAM; Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 26, 2026.

ARUSHA: TIMU ya TRA United imezindua Wiki ya Shamra Shamra yenye matukio mbalimbali ya kijamii na uhamasishaji kuelekea mechi yake ya kwanza ya nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji itakayochezwa Jumamosi, Agosti 29, 2026. Mchezo huo pia utatumika kutambulisha wachezaji wao wa msimu huu wa 2026/2027. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Meneja wa Mamlaka…

A public policy and good governance think tank, Neo Africana Centre (NAC), has called on President Bola Tinubu to withdraw the Chairman of the Nigeria Revenue Service (NRS), Zack Adedeji, from the All Progressives Congress (APC) Presidential Campaign Council. The group said Adedeji’s reported appointment as Deputy Director of Fundraising for the President’s campaign could […]

PWANI; Polisi mkoani Pwani inamshikilia dereva Josia Arute (34) mkazi wa Mlandizi, Kibaha kwa tuhuma za kugonga na kusababisha vifo vya askari wawili wa jeshi hilo. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Salim Morcase imeeleza kuwa askari hao walifariki dunia baada ya kugongwa na gari kwenye kivuko cha waenda…

WAZIRI wa Madini na Uchumi wa Baharini, Hassan Joho, amemshambulia aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kuhusu madai ya njama ya kutumia teknolojia kuiba uchaguzi wa 2027. Bw Joho amemtaka Bw Gachagua kuacha kumhusisha na madai yasiyothibitishwa, akisema hatatishwa na mwanasiasa huyo. “Jana aliyekuwa naibu rais Gachagua alitaja jina langu. Namwomba aache kunitaja katika kashfa zozote,” alisema Bw Joho. Akizungumza eneo la Ganze Kaunti ya Kilifi, Jumanne, Waziri huyo alisema yuko tayari kupambana na Bw Gachagua iwapo ataendelea kumhusisha na tuhuma mbalimbali. “Mimi si mwoga na usinijaribu. Nikifungua mdomo wangu hamtaamini,” alisema. Bw Joho pia alimtaka Bw Gachagua kwanza ajibu madai yanayomhusu ya kunyanyasa familia ya ndugu yake marehemu kabla ya kuanza kuwashtaki viongozi wengine. Kauli hizo zilijiri siku moja baada ya Bw Gachagua kudai kuwa baadhi ya maafisa wakuu serikalini na katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wanahusika katika njama ya kuingilia uchaguzi mkuu wa 2027. Akizungumza katika makazi yake ya Wamunyoro Jumatatu, Bw Gachagua alidai kuwa kuna mpango wa kuleta mfumo mpya wa kusimamia uchaguzi ambao unaweza kutumiwa kuiba kura. Alimtaja Rais William Ruto, Bw Joho na naibu mwenyekiti wa IEBC kama baadhi ya watu anaodai wanahusishwa na mpango huo. “Kuna kitu kingine wanataka kufanya hapo kwa IEBC wakiwa na Joho, na Naibu Mwenyekiti wa IEBC. Kuna mfumo wanataka kuleta ya kuiba kura,” alisema. Kiongozi huyo wa DCP alidai kuwa IEBC ilikuwa ikiandaa zabuni maalum ya Integrated Election Management System (IEMS), ambayo alidai ingeipendelea kampuni ya Korea Kusini, Miru Systems Company Ltd. Hata hivyo, hakutoa ushahidi wa madai hayo na alisema bado alikuwa akithibitisha taarifa kabla ya kutoa maelezo kamili kwa Wakenya. Bw Gachagua pia alidai kuwa baadhi ya wanasiasa hutumia taarifa nyeti kufanya mazungumzo ya kisiasa na serikali, akisema yeye hangefanya hivyo bali angewafahamisha Wakenya. Madai hayo yameibua mjadala mpya kuhusu uhuru wa IEBC na uwazi katika maandalizi ya uchaguzi wa 2027. Hadi Jumanne, serikali na IEBC hazikuwa zimethibitisha madai maalum kuhusu mpango huo wa ununuzi wa mfumo wa uchaguzi. IEBC imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kutoka kwa vyama vya kisiasa na washikadau kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi yanafanywa kwa uwazi na bila kuingiliwa kisiasa. Mzozo huo unatarajiwa kuongeza wasiwasi kuhusu teknolojia itakayotumika katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2027.

DAR ES SALAAM;Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar Es Salaam leo Agosti 26, 2026.
OPERESHENI kali ya siku tatu iliyohusisha taasisi mbalimbali katika hifadhi ya wanyamapori ya Amboseli imewawezesha maafisa kuwakamata wakulima wanne. Wakulima hao wanaojumuisha wanaume watatu na mwanamke mmoja wanashukiwa kuhusika na vifo vya ndovu vilivyosababishwa na sumu katika Kaunti ya Kajiado. Kukamatwa kwao kunajiri huku idadi ya ndovu waliofariki ikiongezeka kati ya mwezi Juni 24 na Julai 26 ikifikia idadi ya tembo 18. Maafisa wa huduma ya wanyamapori nchini KWS, pia wamekamata aina mbalimbali za kemikali hatari zinazokisiwa kuwa za sumu, zinazoshukiwa kuingizwa nchini kwa njia ya magendo kutoka nchi jirani. Hatua hiyo imeongeza kasi ya uchunguzi wa chanzo cha vifo hivyo vya kutatanisha. Operesheni hiyo iliyokamilika Ijumaa ilitekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja na walinzi wa (KWS), maafisa wa idara ya upepelezi wa jina (DCI) na maafisa wa huduma ya kitaifa ya ujasusi. Aidha Uchunguzi huo umejumuisha shughuli za utafiti wa maeneo, uchanganuzi wa kina wa maabara pamoja na uchukuaji wa sampuli za mazingira, kwa lengo la kubaini chanzo cha vifo hivyo na kuwafichua waliohusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa takwimu za KWS, Kati ya tembo 16, 10 kati yao walionyesha dalili zinazowiana, zikiwemo kupooza kwa sehemu ya mwili kulikopelekea tembo hao kushindwa kusimama kabla ya kufariki ndani ya siku moja hadi mbili. Kulingana na ripoti ya awali ya KWS, mizoga mingine ilikuwa imeoza sana au kuliwa na wanyama wengine, hivyo kufanya iwe vigumu kubaini chanzo cha vifo. Vifo hivyo viliathiri zaidi tembo majike waliokomaa pamoja na ndama wao, huku dume mmoja pekee akiwa miongoni mwa waliofariki. Pembe za tembo hao ziliripotiwa kuwa salama wakati wa vifo vyao na baadaye kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba maalum mbugani humo. Tembo wengine wawili waliokuwa wakipokea matibabu walifariki wiki iliyopita, huku tembo mwingine akiwa katika hali mbaya na akiendelea kutibiwa na madaktari maalum waliobobea kwa masuala ya wanyamapori. Alipothibitisha tukio hilo waziri wa utalii na wanyamapori Rebecca Miano, alitoa taarifa rasmi kwa umma siku ya jumamosi, ambapo alisema matokeo ya awali ya maabara yanaashiria uwezekano wa kuwepo kwa sumu. Dalili za awali zinaonyesha huenda tembo hao walikufa kutokana na sumu aina ya cyanide, baada ya kula nyanya zilizokuwa zimenyunyiziwa dawa za kuulia wadudu kutoka katika mashamba yaliyopakana na mbuga ya wanyamapori.

ADDIS ABABA: THE Deputy Minister for Health, Dr Florence Samizi, has praised Dr Senait Fisseha for her significant contribution to strengthening women’s health, reproductive health and health systems across Africa, alongside other stakeholders in the health sector. Dr Samizi made the remarks on Wednesday, August 26, 2026, during an event held in honour of Dr…

NAFASI ya Mwakilishi wa Wanawake katika Bunge la Kitaifa iliundwa kuongeza sauti za wanawake katika chombo cha kutunga sheria. Lakini nafasi hii inapokuwa kiti cha kudumu cha mwanasiasa mmoja, tunapaswa kujiuliza ikiwa bado inatimiza dhima yake pana. Mwanamke anapopewa nafasi ya kuingia Bungeni kupitia kaunti, anapata uzoefu, mwonekano na mtaji wa kisiasa. Kwa nini asitumie jukwaa hilo kuwavisha wengine viatu na kuingia katika ushindani wa kawaida wa ubunge? Hapa ndipo uamuzi wa Esther Muthoni Passaris wa kutetea tena kiti cha Nairobi unapozua mjadala. Passaris alikuwa amedokeza nia ya kuwania ubunge wa Makadara. Lakini sasa anaonekana kurudi kwenye kiti anachokalia. Hakuna kosa la kisheria kwa yeye kufanya hivyo. Lakini kisiasa, jambo hili linahitaji kutafakariwa. Millie Odhiambo, Martha Wangari na Beatrice Elachi kwa mfano walitumia nafasi za uwakilishi wa wanawake kama jukwaa la kujijenga, kabla ya kuhamia katika maeneo bunge ya kawaida. Walipoondoka, nafasi hiyo iliweza kumpa mwanamke mwingine fursa ya kuingia Bungeni. Tatizo si Passaris pekee. Tatizo ni mfumo wa fikra. Ikiwa kila Mbunge wa Kike wa Kaunti ataona nafasi hiyo kama kiti cha kutetea milele, nafasi hiyo itageuka kuwa mwisho wa safari badala ya kuwa daraja. Usawa wa kijinsia hautafikiwa kwa kuhesabu wanawake wale wale kila baada ya uchaguzi. Utahitaji wanawake wapya kuingia, kukua kisiasa na kuchukua nafasi katika maeneo bunge ya kawaida. Mwandishi ni msomi na mtafiti wa taaluma za Kiswahili

BENKI ya KCB imepiga ripoti kwa DCI ikitaka ichunguze kampuni ya Foxcapital inayodai ilituma Sh146 bilioni kwenye akaunti yake kutoka ng’ambo kuhusiana na uwekezaji wa dhamana za serikali. Benki hiyo inadai kwamba stakabadhi zilizowasilishwa na kampuni hiyo kortini kudai fedha hizo ni ghushi na inataka DCI kubaini ni nani aliziandaa, kusambaza na kuziwasilisha kortini. Mzozo unahusisha €978,675,835 (Sh146.3 billion), ambazo Foxcapital inasema ilituma kwa akaunti yao ya KCB Oktoba mwaka jana kama malipo kwa kampuni ya Uingereza, Bay Bionics Ltd, iliyotambuliwa zamani kama BB Biotech AG Limited. Foxcapital iliwasilisha kesi mapema mwezi huu ikidai kwamba KCB ilipokea fedha hizo za kigeni lakini ikakosa kuziweka kwenye akaunti yake, na kufanya Mahakama Kuu kubana hela hizo ikisubiri iamuliwe iwapo benki hiyo kweli ilipokea pesa hizo na kukataa kuzipeana kwa kampuni husika. Katika kilio chake kwa DCI kitengo cha Ulaghai wa Benki, KCB Group, kupitia Afisa Mkuu Mtendaji Paul Russo anatilia shaka stakabadhi zilizotumiwa na Foxcapital kudai pesa hizo. Stakabadhi zinajumuisha arafa za SWIFT, ripoti ya tukio ya Aprili 17, barua ya Mei 18 ya kuangazia kosa la kiuchumi na utathmini wa kiufundi wa Julai 1. KCB inasema stakabadhi zinazodaiwa kutoka UBS Switzerland AG na maafisa wa KCB sio halisi.

Millers say they have not received the required C60 import permits, raising concerns that prolonged bottlenecks could tighten wheat stocks.