ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua amesema hatafika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) Agosti 27 kama alivyoamrishwa.
NCIC ilimtaka kiongozi huyo wa DCP kufika saa nane alasiri kujibu madai ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea chuki za kikabila katika maeneo ya Vihiga, Kisii na Meru.
Tume ilionya kuwa kutofika kunaweza kusababisha hati ya kukamatwa kutolewa.
Hata hivyo, mawakili wa Gachagua wameiambia NCIC kuwa mteja wao atakuwa nje ya nchi kati ya Agosti 26 na Oktoba 20 kwa safari iliyopangwa kabla ya kuitwa.
Mawakili hao pia wamelalamikia kutowasilishwa kwa ushahidi kamili, wakitaka rekodi halisi za video na sauti pamoja na tafsiri rasmi za baadhi ya matamshi yaliyotolewa kwa Sheng na Gikuyu.
Wanadai matamshi hayo yamechukuliwa nje ya muktadha na hayakuwa na nia ya kuchochea chuki za kikabila.
NCIC bado haijajibu barua hiyo.
Wafuasi wa Bw Gachagua wamekosoa wito huo wakisema tume inatumiwa kisiasa dhidi ya upinzani.
Gachagua asema hatafika mbele ya Tume ya NCIC kama alivyoamrishwa
Taifa Leo 1 min read

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsMAGAZETI NOV 21, 2026: SAMIA KATIBA MPYA ITAPATIKANA 2028/29
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
ITV Tanzania Video
NewsTinubu’s re-election campaign backed by visible evidence, not just promises — Oshiomhole
"The real campaign is not about promising what we will do. It is about showing what President Tinubu is already doing"
Vanguard News 1 min read
NewsTAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI: NOV 21, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
ITV Tanzania Video
News