
HABARI ZA SAA, SAA SABA NA DAKIKA 55 - NOVEMBA 20, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania

RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta na Rais William Ruto wameendeleza mvutano wao wa kisiasa huku wakitofautiana kuhusu uchaguzi wa 2027, nafasi ya upinzani na maendeleo ya serikali. Akizungumza Jumapili katika maadhimisho ya miaka 23 ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais Michael Kijana Wamalwa, Milimani, Trans Nzoia, Bw Kenyatta alisema hana nia ya kurejea mamlakani baada ya kuhudumu kama rais kwa miaka 10. Alisema Wakenya ndio wataamua atakayekuwa rais 2027 na hakuna kiongozi anayepaswa kuwalazimisha kumuunga mkono. “Wakenya wataamua wanayemtaka kuwa Rais 2027. Hakuna mtu atakayewalazimisha kumuunga mkono upande wake. Tutafute kura kwa amani na uadilifu,” akasema. Bw Kenyatta pia alitetea uhuru wa kisiasa na haki ya viongozi wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa, akilaani vurugu zilizotokea Homa Bay wakati wa mikutano ya viongozi wa Linda Mwananchi. Aliwataja Kalonzo Musyoka, Fred Matiang’i, Edwin Sifuna na Rais Ruto kama baadhi ya viongozi ambao Wakenya wanaweza kuchagua kati yao katika uchaguzi ujao. Viongozi wa upinzani waliohudhuria hafla hiyo, akiwemo Bw Musyoka, Dkt Matiang’i, Martha Karua, Charity Ngilu na Justin Muturi, walisema wako tayari kuunda muungano wenye nguvu wa kumng’oa Ruto madarakani. Bw Musyoka alisema upinzani unafanya mipango ya kuunda muungano utakaomfanya Ruto kuwa rais wa muhula mmoja. Kwa upande wake, Dkt Ruto aliwashutumu viongozi wa upinzani kwa kutumwa kupinga miradi yote ya serikali badala ya kutoa sera mbadala. Alisema wapinzani wanapiga kelele kuhusu “must go”, “one term” na “Kasongo”, lakini hawana ajenda ya maendeleo. Rais alisema serikali yake inapaswa kuhukumiwa kwa miradi na huduma inazowaletea Wakenya, badala ya misingi ya ukabila. Akiongea katika Kaunti ya Taita Taveta, Rais Ruto alisema serikali imetenga Sh10 bilioni kushughulikia changamoto za ardhi na kuwaondoa maskwota Pwani. Pia alitaja ukarabati wa reli ya Voi-Taveta yenye urefu wa kilomita 129 kama mradi unaolenga kukuza biashara, utalii na ajira. Kule Kitale, Bw Kenyatta alimsifu marehemu Bw Wamalwa kama kiongozi mzalendo aliyependa maslahi ya taifa kuliko siasa za chuki. Aliyekuwa waziri Musikari Kombo alisema Bw Wamalwa alikuwa kiongozi mwadilifu aliyekufa bila utajiri wa kutatanisha. Aliyekuwa waziri Noah Wekesa alijitolea kuongoza jopo litakalosaidia upinzani kuunda muungano wa pamoja, akisema bila mgombea mmoja itakuwa vigumu kumshinda Ruto 2027.

RAIS William Ruto ameweka wazi tofauti kati ya viongozi wa upinzani ambao yuko tayari kufanya nao kazi huku akiweza kuwa hawezi kushirikiana kisiasa tena na Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Katika mahojiano na Taifa Dijitali katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema yuko tayari kushirikiana na viongozi kutoka pande zote za kisiasa, lakini akasema hawezi kufanya kazi na kiongozi anayechochea ukabila, anayetoa matamshi ya kugawanya Wakenya au kuwatusi raia wengine. “Ninaamini katika demokrasia na hapa Kenya watu hufanya kazi na kila mtu. Hata hivyo, sitakuwa tayari kufanya kazi na kiongozi ambaye haamini katika umoja wa taifa.” akasema Rais Ruto. Alisisitiza kuwa hawezi kushirikiana na mtu anayehusika na “ubaguzi wa kikabila” au kutumia maneno yanayolenga jamii nyingine. Pia alisema hana muda na viongozi wanaowatusi wanawake kwa kutumia lugha chafu. Kauli hizo zinaonekana kueleza kwa nini uhusiano wake wa kisiasa na Bw Gachagua ulivunjika, licha ya wawili hao kuwa washirika wakuu katika ushindi wa Kenya Kwanza mnamo 2022. Rais Ruto alitofautisha uhusiano wake na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga marehemu, akimtaja kama “mtu wa kipekee”. Alisema walifanikiwa kugeuka kuwa wapinzani hadi washirika katika serikali ya mseto kwa sababu walikuwa na maono yanayofanana kuhusu mustakabali wa Kenya na walikubaliana kuzima ukabila. Kwa hivyo, ujumbe wa Rais haukuwa kwamba hataki kufanya kazi na viongozi wa upinzani, bali kwamba ushirikiano huo lazima ujengwe kwa misingi ya umoja wa kitaifa, kuheshimu jamii zote, Katiba na kuweka maslahi ya nchi mbele ya siasa za kikabila. Hapo ndipo Bw Gachagua anakuwa tofauti, kwa mtazamo wa Rais. Kiongozi wa DCP amejijenga kisiasa kupitia kujenga himaya yake Mlima Kenya na sasa ni mmoja wa viongozi wakuu wanaopinga serikali ya Rais Ruto. Bw Gachagua, pamoja na viongozi wa upinzani akiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper, Dkt Fred Matiang’i wa Jubilee, Martha Karua wa PLP, Justin Muturi wa DP na Eugene Wamalwa wa DAP-Kenya, wameunda muungano wa kisiasa kwa lengo la kumng’oa Rais Ruto madarakani. Mnamo 2022, Bw Gachagua alikuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto na alichangia pakubwa kumsaidia kupata uungwaji mkono wa Kenya Kwanza katika eneo la Mlima Kenya. Hata hivyo, uhusiano wao ulizorota baada ya kuingia serikalini, hatimaye kusababisha Bw Gachagua kuondolewa katika wadhifa wa Naibu Rais kupitia bungeni mnamo Oktoba 2024. Tangu aondoke serikalini, Bw Gachagua amejitokeza kama sauti kuu ya Mlima Kenya na mpinzani mkali wa Rais Ruto. Kauli zake zimekuwa zikilenga zaidi maslahi, malalamishi na ushawishi wa kisiasa wa eneo hilo. Rais Ruto alisema aina hiyo ya siasa ndiyo hawezi kuikubali, akiwataja viongozi wanaowagawa Wakenya kuwa wasaliti na maadui na kutumia siasa za kikabila kuwadharau wengine. Pia alitetea kuondolewa kwa Bw Gachagua kama naibu rais, akisema mchakato huo ulikuwa wa kikatiba na uliotekelezwa na wabunge. “Kutimuliwa kwake kulikuwa zoezi la kikatiba lililofanywa na wabunge,” akasema Rais. Mzozo kati ya wawili hao ulikuwa umejikita katika masuala ya uteuzi wa viongozi, ugavi wa rasilimali za serikali, nafasi ya Mlima Kenya serikalini na mwelekeo wa utawala. Bw Gachagua alikuwa akiishutumu serikali kwa kupuuza Mlima Kenya, huku washirika wa Rais wakimpinga kwa kuendesha ajenda ya kieneo badala ya kuzingatia maslahi ya kitaifa. Sasa, wawili hao wako pande tofauti kuelekea 2027. Bw Gachagua anajenga muungano imara wa upinzani huku akijaribu kuimarisha ushawishi wake Mlima Kenya. Kwa upande wake, Rais Ruto anajaribu kujisawiri kama kiongozi aliye tayari kufanya kazi na yeyote anayekubali ajenda ya kitaifa, huku akimtenga Bw Gachagua kwa kucheza siasa za kikabila. Rais pia amewataka wapinzani wake wawasilishe sera mbadala kwa Wakenya badala ya kutegemea matusi, kauli za chuki na uvamizi wa kisiasa. Kauli yake inaashiria kuwa nafasi ya maridhiano ya kisiasa bado i wazi, lakini kwa masharti ushirikiano wowote hautatumika kukuza migawanyiko ya kikabila.

By Steve Oko UMUAHIA – Amnesty International has raised the alarm over alleged widespread human rights violations, unlawful killings and enforced disappearances in the South-East, accusing security agencies of leaving families in agony by failing to account for persons allegedly taken into custody. The organisation called on security agencies to either charge persons in their […]

Anthony Joshua and Tyson Fury's highly anticipated heavyweight showdown will go ahead, according to Joshua's promoter Eddie Hearn, despite recent doubts raised by Fury.

Nigerians planning to travel, study, work or relocate to Canada have been warned to watch out for common signs of visa fraud and scams during the application process.

KARAGWE: Shule ya Ushirika wa Wakulima wa Kahawa KDCU Nyaishozi, iliyopo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, imejikita katika masomo ya sayansi na mazingira kwa lengo la kuwaandaa wanafunzi kutumia maarifa na ubunifu wao katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo. Shule hiyo, ambayo awali ilianzishwa kwa ajili ya watoto wa…

RAIS William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kutafuta hoja bora za kupinga ajenda yake ya maendeleo badala ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya ukabila. Rais alisema hayo jana alipofanya ziara katika Kaunti ya Machakos, ngome ya kisiasa ya kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka, huku akijaribu kuvutia wakazi wa Ukambani kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais pia alishutumu upinzani kwa kukosa ajenda thabiti ya kisiasa na kudai baadhi yao wanafanya kazi kwa niaba ya viongozi wengine. “Ingawa umeajiriwa na umekubali kuwa kikaragosi, usijiaibishe. Mnaenda kusema tatizo kubwa la mpango wa nyumba za bei nafuu ni kuku kushindwa kupanda ngazi. Huo ni ujinga. Tafuteni hoja bora,” alisema Rais Ruto katika mikutano mitatu aliyoandaa Machakos. Aliongeza: “Mnaendelea pia kusema mtavunja SHA. Tafuteni hoja bora ya kuwasilisha kwa Wakenya.” Rais alisema wakati umefika ambapo Wakenya wanapaswa kuwahukumu viongozi kwa rekodi zao za uongozi, mipango na maono badala ya matusi na kauli za kisiasa. “Wakenya hawana haja na wale wanaowagawanya kwa kuwaita wengine binamu, wengine wasaliti na wengine maadui. Kenya inahitaji umoja. Sisi sote ni ndugu,” alisema katika mkutano Kimutwa Township.

NAIBU Rais Kithure Kindiki amesema yuko tayari kumkabili mtangulizi wake Rigathi Gachagua katika vita vinavyozidi kupamba moto vya kudhibiti siasa za Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Prof Kindiki na Bw Gachagua wanadai kuwa wana ushawishi mkubwa katika eneo hilo lenye wapigakura wengi, huku kila mmoja akijigamba kuwa ana uwezo wa kumbwaga mwenzake katika uchaguzi ujao. Bw Gachagua ameapa kumzuia Rais William Ruto kupata uungwaji mkono Mlima Kenya, huku Prof Kindiki akijenga mtandao wa kisiasa wa kuzuia upinzani kutwaa eneo hilo. Jambo moja linalowaunganisha wapinzani hao ni juhudi za kuunganisha Mlima Kenya, lakini kila mmoja akitaka umoja huo umfaidi kisiasa. Jumamosi, Prof Kindiki aliendeleza kampeni zake za kuimarisha ushawishi wake Mlima Kenya Mashariki alipokutana na zaidi ya viongozi 20,000 wa mashinani kutoka Meru, Tharaka Nithi, Embu na Isiolo katika Uwanja wa Kinoru. Mkutano huo uliwahusisha magavana, maseneta, wabunge, wazee wa vijiji, wahamasishaji wa afya ya jamii, madiwani wa sasa na wa zamani. Ulijiri siku moja baada ya Naibu Rais kukutana na maafisa 15,000 wa UDA wanaosimamia vituo vya kupigia kura, ambao aliwataka kuwa mabalozi wa chama hicho tawala. Prof Kindiki alisema atafuta ushawishi wa upinzani katika kipindi cha mwaka mmoja kuelekea uchaguzi, akidai ana uzoefu mkubwa wa kampeni kuliko Bw Gachagua. “Upinzani usithubutu kunichokoza. Gachagua amekuwa akiona mambo ni rahisi Mlima Kenya kwa sababu sisi tulikuwa tumejishughulisha na kazi huku wao wakifanya kampeni,” alisema. Alisema amewahi kuendesha kampeni za urais katika Mlima Kenya na kushinda. “Wakati kampeni zitaanza, kura zitamiminika kwenye kapu la Rais. Bila kujali yaliyotokea Ol Kalou, tutashinda upinzani 2027,” alisema. Prof Kindiki pia alimkejeli kiongozi wa DCP akimtaja kama “simba wa karatasi” na kumtaka akabiliane naye moja kwa moja. “Tuonane ana kwa ana na tushindane kama wanaume ili kutofautisha kiongozi wa kweli na bandia. Wale wanaojigamba ni simba wa karatasi,” alisema. Naibu Rais alisema mikutano yake na viongozi wa mashinani inalenga kuunda mtandao wa wafuasi ambao wataweza kueleza mafanikio ya serikali ya Rais Ruto. Alisema viongozi hao watakuwa mabalozi wa serikali katika maeneo yao na kuwafahamisha wananchi kuhusu utekelezaji wa Ajenda ya Mabadiliko kutoka Chini kwenda Juu. Prof Kindiki aliorodhesha mafanikio ambayo serikali inadai imepata katika miaka minne, yakiwemo ruzuku za kilimo, kuajiriwa kwa zaidi ya walimu 100,000 na utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya dola. Pia alitaja kupungua kwa bei ya unga na mabadiliko katika huduma za afya kupitia Mamlaka ya Afya ya Jamii. Katika michezo, alisema serikali inajenga Uwanja wa Talanta na viwanja vingine 33 katika maeneo mbalimbali nchini. Prof Kindiki pia aliwataka wakazi kuunga mkono msimamo wa mabaraza ya wazee wa Mlima Kenya Mashariki wa kutaka eneo hilo liwe na msimamo mmoja wa kisiasa kuunga serikali. “Mlima Kenya ni mmoja kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitamaduni. Ni watu wachache wanaotaka kutugawanya,” alisema. Magavana Cecily Mbarire wa Embu, Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi na Isaac Mutuma wa Meru waliahidi kushirikiana na Prof Kindiki kuunganisha eneo hilo kumuunga mkono Rais Ruto. Gavana Mbarire alisema wakati umefika kwa wakazi wa Mlima Kenya Magharibi kuonyesha ikiwa wanaweza kuthamini uhusiano uliopo kati ya maeneo hayo. Gavana Njuki alisema watasaidia kuimarisha uungwaji mkono wa Naibu Rais na Rais Ruto. “Ni msimamo wetu kwamba Kindiki abaki Naibu Rais hata baada ya 2027,” alisema.

KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua anakabiliwa na changamoto mpya katika juhudi zake za kudhibiti siasa za eneo la Mlima Kenya, mwezi mmoja tu baada ya ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Katika uchaguzi huo wa Julai 17, mgombeaji wa DCP, Kamau Ngotho alipata kura 35,440, sawa na asilimia 85 ya kura zote, dhidi ya mgombeaji wa United Democratic Alliance (UDA) aliyeungwa mkono na Rais William Ruto, Muchina Nyaga, aliyepata kura 5,450. Ushindi huo ulimpa Bw Gachagua nguvu mpya na kumfanya kujitangaza kuwa kiongozi asiye na mpinzani wa kisiasa katika Mlima Kenya, huku akitaja DCP kama chama chaguo la wakazi wa eneo hilo. Katika uchaguzi huo, Jubilee ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ilipata kura 198 huku Party of National Unity (PNU) ya aliyekuwa Gavana wa Meru Peter Munya ikipata kura 28. Lakini mwezi mmoja baadaye, Bw Gachagua anakabiliwa na upinzani mpya, huku hatua ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kujiunga na People’s Party of Kenya (PPK) na kuwa kiongozi wake ikiwa changamoto kubwa zaidi. Bw Nyoro anasema chama chake ni sehemu ya upinzani na kinalenga kushirikiana na vyama vingine kupata mgombea mmoja wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, pamoja na kuondoa serikali ya Rais Ruto madarakani. Hata hivyo, Bw Gachagua na washirika wake wamemtaja Bw Nyoro kama mpinzani anayelenga kuvuruga juhudi za kuunganisha kura za Mlima Kenya. “Mlima ni mmoja, chama ni kimoja (DCP), na kiongozi wa eneo ni mmoja (Gachagua),” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa DCP John Methu, ambaye pia ni Seneta wa Nyandarua. Bw Nyoro, hata hivyo, amesisitiza kuwa yeye ni kiongozi halisi wa upinzani anayelenga kuimarisha ajenda ya upinzani. “Nitafanya kazi na viongozi wote wa upinzani, akiwemo Bw Gachagua, na chama changu hakitakuwa mahali pa kukimbilia watu waliokataliwa na Mlima ambao wamekuwa wakitukana DCP na uongozi wake,” alisema. “Najua kuna wanaonitilia shaka. Lakini baada ya muda mtaona msimamo wangu kamili katika kupinga na kuondoa serikali hii madarakani.” Mchanganuzi wa siasa Gasper Odhiambo alisema Bw Nyoro ana haki ya kidemokrasia kuanzisha chama na kujiunga na upinzani, lakini muda na namna alivyoingia kwenye siasa za upinzani huenda zikamfanya akabiliane na upinzani mkali. “Bw Gachagua ana haki yote kumchukulia Bw Nyoro kuwa mpinzani wake. Swali ni kwa nini Bw Nyoro alisubiri hadi Bw Gachagua aondolewe kwa kura ya kutokuwa na imani, akabiliane na makundi ya wahuni na maafisa wa polisi waliopotoka, ndipo aanze kuhamasisha Mlima Kenya kuingia upinzani,” alisema. Bw Odhiambo alisema Bw Gachagua mwenyewe alipitia upinzani kama huo baada ya kuondolewa kwenye wadhifa wa Naibu Rais. Alisema wakati huo Jubilee na PNU tayari vilikuwa katika upinzani. “Bw Nyoro ameingia kushindana na Bw Gachagua na DCP. Kisichojulikana ni kama anafanya hivyo kwa niaba yake mwenyewe au kuna nguvu iliyojificha nyuma ya pazia la siasa.” Bw Odhiambo pia alikumbusha kuwa kabla ya Bw Gachagua kuondolewa madarakani Oktoba 2024, washirika wa Bw Nyoro katika Kaunti ya Murang’a, wakati huo wakiongozwa na Seneta Joe Nyutu, walikuwa wamemuonya Rais Ruto kuwa angehatarisha kiti chake ikiwa angemwacha Bw Gachagua na kumchagua Bw Nyoro. “Upinzani wa Bw Nyoro dhidi ya Bw Gachagua si jambo jipya. Umekuwepo tangu 2022,” alisema. Alisema katika shughuli zote rasmi za Bw Gachagua katika Mlima Kenya akiwa Naibu Rais, Bw Nyoro hakuhudhuria hata moja. “Wakati Bw Gachagua aliondolewa mamlakani na kujitahidi kujijenga kisiasa upya, Bw Nyoro alikuwa amekaa katikati. Sasa kwa kuwa Bw Gachagua anaonekana kurejea kwa nguvu, Bw Nyoro anaingia katika uwanja huo akiwa na chama na azma ya kushindana naye. Bw Nyoro ana mengi ya kueleza,” alisema. Katika mkutano wa kisiasa Kiharu Agosti 19, Bw Nyoro aliwaomba wakazi wamuamini na akasisitiza kuwa yeye si msaliti. “Ni kwamba mamlaka huchukuliwa, hayapeanwi. Lazima nijionyeshe kwa njia bora itakayonisaidia kutimiza malengo yangu,” alisema. Alisema atawasimamisha wagombeaji katika uchaguzi wa 2027 na pia atamenyania nafasi ya kuwa mgombea urais wa upinzani. “Nina nia njema na nawaomba sote tuvumiliane,” alisema. Kuingia kwa Bw Nyoro katika uwanja huo kunatokea wakati Naibu Rais Kithure Kindiki anaonekana kuunga mkono juhudi za kuunda mrengo tofauti wa kisiasa Mlima Kenya Mashariki. Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku ameibuka kama mmoja wa watetezi wakuu wa mpango huo. Bw Ruku anataka Meru, Tharaka Nithi na Embu kuungana chini ya Prof Kindiki na kisha kujadiliana na Rais Ruto kuhusu nafasi yao katika serikali ijayo. Ingawa Prof Kindiki amekuwa akisema hadharani kuwa Mlima Kenya unapaswa kuwa kitu kimoja, wazee kutoka Meru na Embu tayari wamemtangaza kuwa msemaji wao. Katika ishara nyingine ya mgawanyiko huo, Prof Kindiki alisema aliyekuwa Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amepewa jukumu la kushirikiana na Rais mstaafu Kenyatta kuhakikisha kuna ushirikiano unaolenga “kuwazuia wapiga kura wa Mlima Kenya kuchagua upinzani mwaka 2027”. Wakati huohuo, Mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri na mwenzake wa Ndia George Kariuki wameanzisha mikakati ya kisiasa inayolenga kupunguza ushawishi wa Bw Gachagua. Bw Kiunjuri anaripotiwa kuratibu vyama vidogo vinavyomuunga mkono Rais Ruto katika eneo la Mlima Kenya, huku Bw Kariuki akijenga mtandao wa viongozi wa mashinani wanaounga mkono msimamo wake.

A fresh battle is brewing between former Imo State Governor, Rochas Okorocha, and his successor, Governor Hope Uzodimma, over the All Progressives Congress, APC, senatorial ticket for Imo West ahead of the 2027 general elections.

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 unapokaribia, upinzani unaanza kuashiria mwelekeo wa kuungana na vuguvugu la Linda Mwananchi, huku mjadala kuhusu nani atabeba bendera ya urais ukizidi kupamba moto. Katika ishara ya mwelekeo huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ameibua uwezekano wa tiketi ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Kalonzo Musyoka, akidai kuwa muungano huo unaweza kupatia upinzani nafasi nzuri ya kumkabili Rais William Ruto. Bw Khalwale alisema Ijumaa kwamba utafiti aliouhusisha na wasomi kutoka China unatabiri kuwa Sifuna akiwa mgombea wa urais na Kalonzo mgombea mwenza, wanaweza kupata asilimia 68 ya kura dhidi ya asilimia 29 ya Rais Ruto. “Nimesoma utafiti jana usiku ambao umefanywa na Wachina. Umesema kwamba sisi tulioko mrengo wa upinzani tukikufanya wewe kuwa mgombea urais, halafu Kalonzo Musyoka awe mgombea mwenza wako, wewe na Kalonzo mtapata asilimia 68 ya kura, huku William Ruto akienda Sugoi na asilimia 29, ” alidai Khalwale. Hata hivyo, Khalwale hakutaja taasisi iliyofanya utafiti huo, ulifanywa lini, sampuli iliyotumika au mbinu iliyotumiwa. Hakuna ripoti ya utafiti huo iliyowekwa wazi ili kuthibitisha takwimu hizo. Licha ya utata huo, kauli yake inaangazia hesabu inayozidi kutawala siasa za upinzani: je, Sifuna anaweza kuwa sura ya kizazi kipya cha upinzani huku Kalonzo akitoa uzoefu na ukomavu wa kisiasa? Sifuna amekuwa akipanda katika kura za maoni na sasa anatajwa miongoni mwa viongozi wanaoweza kupewa nafasi ya kuongoza upinzani. Utafiti wa TIFA uliotolewa Julai ulimweka Rais Ruto mbele kwa asilimia 24, Sifuna akifuata kwa asilimia 15 na Kalonzo akiwa na asilimia 13. Uchaguzi wa Kenya huamuliwa pia na miungano ya kikanda, nguvu za vyama, wagombea wenza na uwezo wa kuvutia wapiga kura nje ya ngome za viongozi. Kwa Sifuna, changamoto ni kugeuza umaarufu wake unaokua kuwa mtandao wa kitaifa. Kwa Kalonzo, changamoto inaweza kuwa kuamua ikiwa yuko tayari kuachana na azma ya kuwania urais na kukubali kuwa mgombea mwenza. Mjadala huo unajiri huku viongozi wa Linda Mwananchi wakiongeza shughuli za kisiasa na baadhi ya viongozi wa upinzani wakionyesha wako tayari kufanya kazi nao. Hata hivyo, bado hakuna makubaliano rasmi kuhusu mgombea wa upinzani, chama kitakachotumika au nafasi ya Kalonzo katika mpangilio huo. Kwa hivyo, tiketi ya Sifuna na Kalonzo bado ni uvumi wa kisiasa kuliko mpango uliokamilika. Lakini mjadala wake unaonyesha mabadiliko yanayoendelea katika upinzani huku 2027 ikikaribia: kutoka mashindano ya mtu mmoja mmoja hadi kutafuta tiketi moja inayoweza kuunganisha nguvu za kisiasa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Iwapo Linda Mwananchi itaungana rasmi na makundi mengine ya upinzani, suala la nani atakuwa mgombea wa urais na nani atakuwa mgombea mwenza litakuwa mojawapo ya maamuzi magumu zaidi kuelekea uchaguzi huo. Kwa sasa, jina la Sifuna limeingia katika hesabu hiyo. Kalonzo ana uzoefu na ngome yake ya kisiasa. Swali kubwa ni ikiwa wawili hao wanaweza kugeuza nguvu zao kuwa muungano mmoja wenye mvuto wa kitaifa — na ikiwa viongozi wengine wa upinzani wako tayari kuunga mkono mpango huo.

HAKUNA siri kwamba uhusiano kati ya Rais William Ruto na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta umeharibika. Lakini kiwango cha uhasama kati ya viongozi hao wawili, ambao wakati mmoja walionekana kuwa washirika wasioweza kutenganishwa, unaonekana katika juhudi za Rais Ruto za miaka minne zilizolenga kurejesha uhusiano wao. Katika mahojiano ya kipekee na Taifa Jumapili katika Ikulu ya Nairobi Ijumaa, Agosti 21, Rais Ruto alifichua kwa mara ya kwanza kwa undani jinsi alivyoshindwa kumshawishi Bw Kenyatta kujitenga na siasa za vyama na kuchukua nafasi ya kiongozi mstaafu anayewaunganisha Wakenya. Rais alisema aliwahi kumtembelea Bw Kenyatta nyumbani kwake Ichaweri, Gatundu, Kiambu, na pia ofisini kwake karibu na Ikulu, akimshawishi kusaidia kujenga maono mapya ya taifa. “Nilienda kumuona Ichaweri na pia katika ofisi yake hapa jirani na nikamuomba kwamba, kama kiongozi wa zamani wa nchi, na wa pekee aliye hai sasa, tafadhali tusaidie kujenga maono mapya ya nchi,” alisema. Lakini kwa mujibu wa Rais, Bw Kenyatta alichagua kuendelea kushiriki siasa za upinzani. “Mtangulizi wangu alikuwa na nafasi ya kuwa kiongozi wa kitaifa, na kuwa mtu wa kuunganisha nchi yetu. Lakini alichagua kushuka na kuwa kiongozi wa upinzani,” alisema. Uhusiano wa Ruto na Kenyatta uliwahi kuwa miongoni mwa ushirikiano wenye nguvu zaidi katika siasa za Kenya. Wawili hao waligombea urais pamoja mwaka 2013 na 2017 chini ya chama cha Jubilee. Ushirikiano huo ulijengwa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/08 na mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC) yaliyowakabili viongozi kadhaa wa Kenya. Lakini mambo yalibadilika katika muhula wa pili wa Bw Kenyatta. Handisheki ya Machi 2018 kati ya Bw Kenyatta na aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga yalimuacha Dkt Ruto ametengwa kisiasa. Mvutano huo ulifikia kilele katika uchaguzi wa 2022 ambapo Bw Kenyatta alikataa kumuunga mkono aliyekuwa naibu wake na badala yake akamuunga mkono Bw Odinga. Dkt Ruto alishinda uchaguzi huo. Sasa, miaka minne baada ya kuingia Ikulu, majeraha ya zamani bado yanaonekana. Bw Kenyatta bado ni mwenyekiti wa Baraza la Azimio, chombo kikuu cha kufanya maamuzi katika muungano huo, na pia anaongoza chama cha Jubilee. Baada ya kifo cha Bw Odinga, amempa kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka jukumu la kuongoza Azimio na anaunga mkono aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i katika juhudi za kumuondoa Dkt Ruto madarakani mwaka ujao. Lakini Rais Ruto alisema alijaribu kuzuia mgawanyiko huo. Alifichua kuwa wakati mmoja alizungumza na Bw Odinga kuhusu haja ya viongozi wakuu wa kisiasa kufanya kazi pamoja kujenga maono ya muda mrefu ya Kenya. “Sasa sisi ni wazee. Sisi ni viongozi wa nchi hii. Kwa nini tusifanye kazi pamoja, tujenge maono makubwa ambayo tunaweza kuyakabidhi kwa kizazi kijacho cha viongozi?” Rais alikumbuka akimwambia Bw Odinga. Kwa mujibu wake, Bw Odinga alikubaliana naye na wakapendekeza kumtafuta Bw Kenyatta. Mnamo Desemba 9, 2024, Rais Ruto alisafiri hadi nyumbani kwa Bw Kenyatta Ichaweri kwa mkutano wa ana kwa ana uliolenga kufungua ukurasa mpya kati ya viongozi hao wawili. Miezi kadhaa baadaye, Bw Kenyatta alirejea Ikulu mnamo Agosti 2025 na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais, yakiwemo masuala ya amani nchini DRC. Lakini juhudi hizo hazikubadilisha uhusiano wao kisiasa. Dkt Ruto sasa anamlaumu mtangulizi wake kwa kuchagua kuunga upinzani badala ya kusaidia kujenga mwafaka wa kitaifa. Uhasama huo umeenea pia katika mjadala wa uchumi. Rais alidai Bw Kenyatta alitabiri kuwa serikali yake ingeanguka ndani ya miezi mitatu kutokana na hali mbaya ya uchumi aliyokuwa ameacha. “Kenya ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni, mfumuko mkubwa wa bei, mikopo ghali na hofu kuhusu uwezo wake wa kutimiza majukumu ya nje,” alisema. Kwa mujibu wa Rais, Bw Kenyatta aliwaambia washirika wake wa Azimio kuwa serikali mpya haingeweza kudumu. “Alijua kuhusu uwezekano wa kushindwa kulipa deni, alijua hali ya uchumi,” alisema. “Nina hakika ana tatizo kwamba… niliweza kuongoza nchi na hatukushindwa kulipa.” Rais pia alilinganisha deni la umma lililoachwa na tawala zilizotangulia. Alisema utawala wa Daniel arap Moi uliacha deni la takriban Sh630 bilioni mwaka 2002, Mwai Kibaki Sh1.8 trilioni, huku Bw Kenyatta akiacha deni la karibu Sh10.3 trilioni. Kwa sasa, alisema, deni linakaribia Sh13 trilioni. Hata hivyo, Rais alikiri kwamba miradi ya miundombinu ya utawala wa Bw Kenyatta haikuwa mibaya. “Utawala wa Uhuru haukuwekeza katika mambo yasiyofaa,” alisema. Tofauti, kwa mujibu wa Dkt Ruto, ni kwamba serikali yake inatafuta njia mbadala za kufadhili miradi bila kutegemea sana mikopo ya serikali.

By Bunmi Sofola RECENTLY, Frieda, the head of a leading private school, lamented that modern parents are praising their children to the hilt and bringing up their daughters as if they can do no wrong. She argued that being showered with too much praise and too many presents is not a good thing for a child […]

UTETE: PRESIDENT Samia Suluhu Hassan has directed the Ministry of Energy and the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) to fast-track completion of power transmission and distribution infrastructure to ensure Tanzanians and key economic sectors fully benefit from electricity generated by the Julius Nyerere Hydropower Project. The Head of State issued the directives earlier on Saturday…

UTETE: THE Tanzanian government said it bets on the Julius Nyerere Hydropower Project to transform its electricity generation capacity and strengthen the country’s position as a major business and investment hub in East Africa. This was revealed by the Managing Director of the Tanzania Electricity Supply Company Limited (TANESCO), Lazaro Twange during the launching ceremony…

The DR Congo government recently requested the release of Ervebo vaccines from the global Ebola virus disease vaccine stockpile, managed by the International Coordinating Group on Vaccine Provision (ICG).

The Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) has become a pillar of Tanzania’s national electricity grid, contributing nearly half of all power fed into the grid this year, according to the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco).

Passengers using Magufuli Bus Terminal in Dar es Salaam have raised concerns over inadequate seating and waiting areas, with some forced to stand for long periods or sit on their luggage while waiting for buses.

KIOMBOI: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Vice-Chairperson (Mainland), Stephen Wasira, has warned that the party will no longer tolerate illegal use of money in political related matters especially during its internal elections, saying future candidates must be chosen on merit, integrity and competence. Mr Wasira made the remarks in Kiomboi, Iramba District, on Thursday during an…

MKE wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, Winnie Byanyima, amelaani kuendelea kwa kesi ya mumewe huku mwanasiasa huyo akiwa amelazwa kutokana na hali yake mbaya ya afya. Besigye, 70, anakabiliwa na mashtaka ya uhaini yanayohusiana na madai ya kupanga njama ya kumpindua Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986. Byanyima, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, amesema si haki kesi hiyo kuendelea wakati mumewe hawezi kufika mahakamani kwa sababu ya ugonjwa. Amesema Besigye hawezi hata kuzungumza kutokana na hali yake. Awali, mwanasiasa huyo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuanguka akiwa mahakamani, lakini alirejeshwa gerezani mapema mwezi huu licha ya madaktari kuonya kuhusu hali yake. Besigye alikamatwa nchini Kenya mwaka 2024 na kupelekwa Uganda, ambako awali alifikishwa katika mahakama ya kijeshi kabla kesi yake kuhamishiwa mahakama ya kiraia. Byanyima ameitaka serikali kumwachilia kwa dhamana ili apate matibabu yanayohitajika.

DAR ES SALAAM: THE High Court’s SubRegistry in Dar es Salaam has ruled that Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Chairman Tundu Lissu has a case to answer in the treason case facing him, paving the way for the opposition leader to begin presenting his defence. A three-judge panel, headed by Justice Dunstan Ndunguru, delivered…

COAST REGION: ALL eyes will be on Rufiji District in Coast Region today as President Samia Suluhu Hassan officially commissions the 2,115-megawatt Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP), a landmark investment expected to transform Tanzania’s energy sector and provide fresh impetus to industrialisation. The 7.45tri/- project, financed entirely by the government, raises the country’s installed electricity…
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewapa wanasiasa na wanaowania nyadhifa mbalimbali waliochapisha mabango ya kampeni yenye nembo ya tume hiyo siku tano kuyaondoa mara moja, ikiongeza juhudi za kukabiliana na kampeni za mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Katika taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, IEBC ilisema matumizi ya nembo yake […]

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema eneo la Kurasi Logistics Park linatarajiwa kuanza kutumika kama sehemu ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (Port Extension) kuanzia Novemba mwaka huu, hatua inayolenga kupunguza msongamano bandarini na kuongeza ufanisi wa huduma za mizigo. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya eneo…

TANGAZO la Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar kuwania ugavana Mombasa mwaka 2027 limezua mgawanyiko katika ushirikiano unaoibuka kati ya UDA na ODM, huku juhudi za kugawana maeneo ya kisiasa Pwani zikikabiliwa na changamoto. Bw Omar ametangaza kuwa ataendelea na azma yake ya kuwania kiti hicho, hatua inayotishia mpango wa vyama hivyo kuepuka kushindana moja kwa moja katika baadhi ya kaunti. Kwa zaidi ya mwezi mmoja, viongozi wa UDA na ODM wamekuwa wakijadili uwezekano wa kugawana maeneo, ambapo kila chama kingepewa nafasi ya kuongoza katika kaunti fulani huku kingine kikimuunga mkono mgombea wake. Hata hivyo, Bw Omar amekataa mpango huo akisema wapiga kura wanapaswa kuwa huru kuchagua viongozi wanaowataka. “Tuungane na tuchague viongozi wetu kwa uhuru. Kwale tumeona ODM haitaki ugawaji wa maeneo, nasi UDA hatutaki. Hatuwezi kuamriwa na mtu, tutafanya maamuzi yetu,” alisema Bw Omar. Kauli hiyo imeweka mashakani juhudi za kubadilisha ushirikiano wa kitaifa kati ya UDA na ODM kuwa muungano wa kisiasa wa kuelekea uchaguzi wa 2027. Mombasa ni ngome ya muda mrefu ya ODM, huku UDA ikijaribu kupanua ushawishi wake katika eneo hilo. Kuingia kwa Bw Omar katika kinyang’anyiro hicho kunaweza kuwa mtihani wa uwezo wa UDA kuvunja ngome hiyo na pia wa ODM kuhifadhi umaarufu wake baada ya kuingia katika serikali ya muungano mpana. Changamoto hiyo pia imejitokeza Kwale, ambako baadhi ya wanachama wa ODM wanataka chama hicho kutoa mgombea wake wa ugavana badala ya kumuunga mkono Gavana Fatuma Achani anayehusishwa na UDA. Wiki iliyopita, Waziri wa Madini, Hassan Ali Joho alikumbana na upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama wa ODM katika mkutano Vingujini, Kwale. Mkazi Donate Mwavale alimtaka Bw Joho kuwasikiliza wananchi, hasa wanawake, kabla ya viongozi kufanya maamuzi kuhusu ushirikiano wa kisiasa. “Huo uongozi wako tutauvua usipotusikiza,” aliambia Bw Joho. Mivutano hiyo inaonyesha ugumu wa kutekeleza makubaliano ya kisiasa yanayofanywa na viongozi wa kitaifa bila kuzingatia matarajio ya wanasiasa na wapiga kura wa mashinani. Kwa mujibu wa vyanzo vya kisiasa, Mombasa, Kilifi na Tana River zimekuwa zikitajwa kuwa maeneo ambayo ODM inaweza kupewa nafasi zaidi, huku UDA ikitarajiwa kuzingatia Kwale, Taita-Taveta na Lamu. Hata hivyo, azma ya Bw Omar inaweza kuvuruga mpango huo na kuongeza ushindani kati ya vyama hivyo. Kwa UDA, kushinda Mombasa kungeipa nafasi ya kupanua mizizi yake Pwani na kubadilisha ramani ya kisiasa ya eneo hilo. Kwa ODM, kupoteza kaunti hiyo kungekuwa pigo kubwa kwa chama kinachojaribu kujenga upya nguvu zake baada ya kifo cha kiongozi wake wa muda mrefu Raila Odinga. Huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, Mombasa na Kwale huenda zikawa maeneo muhimu ya kupima iwapo UDA na ODM zinaweza kuwa washirika wa uchaguzi au zitaendelea kuwa washirika wa serikali pekee.
ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua ametaka maafisa kutoka Scotland Yard ya Uingereza na Shirika la Upelelezi la Amerika (FBI) waalikwe nchini kuchunguza ajali ya helikopta iliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno na watu wengine watano. Bw Gachagua alisema Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA) haziwezi […]

WATU watatu walijeruhiwa baada ya walinzi wanaodaiwa kuwa wa Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir kufyatua risasi katika hafla ya umma katika Uwanja wa Bomu, Changamwe, Mombasa, Ijumaa alasiri. Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano wa kuhamasisha wananchi kuhusu mpango wa Biashara Mtaani, unaoendeshwa kupitia Hazina ya Mzunguko ya Kaunti ya Mombasa kwa wakazi wa Changamwe na Jomvu. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa, Stella Cherono alisema uchunguzi umeanzishwa na akawataka wote wenye taarifa kutoa kwa polisi. “Tunachunguza tukio ambapo watu watatu walipigwa risasi na kujeruhiwa katika Uwanja wa Bomu. Tunawaomba wahusika wote kutoa taarifa uchunguzi ukiendelea,” alisema Bi Cherono. Alisema vijana hao watatu walijeruhiwa kwa risasi na kukimbizwa katika kituo cha afya kilicho karibu, huku baadhi wakihamishiwa katika Hospitali ya Coast General kwa matibabu zaidi. Walioshuhudia walisema kundi la vijana lilimsogelea gavana likiimba “Wantam”, na walinzi wake wakaingilia kati na kufyatua risasi kadhaa. Afisa mmoja aliyekuwa kwenye hafla hiyo alisema polisi waliokota maganda kadhaa ya risasi eneo la tukio. Mwanaharakati wa haki za binadamu, Francis Ouma alilaani tukio hilo na kutaka uchunguzi kufanywa kuhusu matumizi ya bunduki dhidi ya raia. Alitaka IPOA kuchunguza na kubaini waliowafyatulia risasi vijana hao.

MAPANGA yanabadilishwa kutoka zana ya kawaida ya shambani kuwa silaha ya kutisha na kuwashambulia watu, huku ripoti ya kijasusi ikifichua kuwa angalau mapanga 500 yalisambazwa kwa vijana waliozua vurugu wakati wa ziara ya Linda Mwananchi, Homa Bay. Huku joto la kisiasa likipanda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, vijana wanaobeba mapanga katika mikutano ya hadhara na makabiliano ya kisiasa wamekuwa chanzo cha wasiwasi. Zana iliyokuwa ikitumika hasa mashambani sasa inatumika kama silaha ya vitisho na vurugu. Baadhi ya vijana hata wameunda utamaduni wa mapanga, wakitumia nyimbo na densi kama mapangale, inayoiga kitendo cha kutumia panga kukata au kucharaza. Hali hii inazua swali: Ni rahisi kiasi gani kununua mapanga kwa wingi, na je, Kenya ina sheria za kutosha kudhibiti uuzaji wake? Kwa sasa hakuna mfumo maalum wa leseni unaohitaji kibali ili mtu anunue au kumiliki panga kwa kuwa inatambuliwa kama kifaa cha kilimo na matumizi ya nyumbani. Hata hivyo, inaweza kugeuka haraka kuwa silaha hatari ikitumiwa na mtu mwenye nia mbaya. Mara kadhaa, maafisa wa usalama wamewakamata watu wakisafirisha idadi kubwa ya mapanga yanayoshukiwa kunuiwa kutumiwa katika makabiliano. Jumapili iliyopita, wapelelezi waliwakamata watu wawili waliokuwa na mapanga matano mapya kando ya Barabara ya Ndhiwa, Yamase, Kaunti ya Migori, katika njia iliyotumiwa na msafara wa Linda Mwananchi. Mapanga pia yamehusishwa na makabiliano ya kisiasa Kisumu na Nairobi. Video inayosambazwa mtandaoni inaonyesha watu wakikabidhiwa panga na Sh1,000 kwa kazi ambayo haijaelezwa. Matukio hayo yanaibua maswali kuhusu idadi ya mapanga ambayo mtu anaweza kununua kwa wakati mmoja, iwapo maduka yanapaswa kurekodi ununuzi wa mapanga mengi na hatua zinazochukuliwa kuzuia zana hizo kuingia mikononi mwa wahalifu. Pengo hilo limewaacha baadhi ya wafanyabiashara wakitumia uamuzi wao wenyewe. Fred Ogolla, mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi Kondele, Kisumu, huruhusu mteja kununua mapanga mawili pekee kwa wakati mmoja na hayabandiki hadharani katika duka lake. “Mtu akija kwangu kununua mapanga zaidi ya mawili, simruhusu,” alisema Bw Ogolla.Alisema uamuzi huo unatokana na dhamiri yake. “Kama Mkristo, nahisi nitakuwa mshirika wa uhalifu. Ikiwa panga itatumiwa kufanya uhalifu au kusababisha kifo, sitaweza kuishi na jambo hilo,” alisema. Audi Ogada, mwenyekiti wa Kisumu Residents Voice Association na mwanachama wa zamani wa genge, alisema ujasiri wa vijana kubeba na kutumia mapanga kuwashambulia watu ni jambo la kutia wasiwasi. Alisema ingawa kuna sheria zinazodhibiti kubeba silaha hadharani, hakuna udhibiti wa kutosha kuhusu ununuzi wa mapanga kwa wingi. Hata hivyo, maafisa wa usalama wanasema tayari wanachukua hatua kukabiliana na tatizo hilo. Kamishna wa Kaunti ya Kisumu Mohamed Mwabudzo alisema maafisa huwa macho zaidi kabla ya mikutano ya kisiasa na wakati wa kampeni za uchaguzi. “Tunategemea mitandao yetu ya kijasusi. Tunaposhuku kuwa kuna shughuli haramu au ununuzi unaofanywa, tunatoa tahadhari na kuchukua hatua kabla ya jambo kutokea,” alisema. Alisema maafisa wa usalama wanaweza pia kushirikiana na maduka ya vifaa vya ujenzi ili yaripoti ununuzi unaotia shaka. Bw Mwabudzo pia aliwataka wananchi kuripoti wanapoona ununuzi wa mapanga kwa wingi. Alisema mtu anayebeba au kutumia panga hadharani anaweza kukamatwa iwapo polisi wataamua kuwa linatumika kama silaha hatari.

Chadema chairman Tundu Lissu has told the High Court in Dar es Salaam that the treason case against him stems from his long-running campaign for a new Constitution, the rule of law and electoral reforms.

DODOMA: Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) Executive Director Dr Adam Mrisho said the Commission had continued to implement deliberate strategies to ensure HIV/AIDS interventions were effectively implemented and reached all groups, particularly young people. Dr Mrisho made the remarks in Dodoma recently while responding to concerns raised by the Parliamentary Standing Committee on Health and…

*As OADC, Analytics Intelligence deal, media’s Big Tech battle fuel push for homegrown AI By Prince Osuagwu Nigeria’s dream of achieving artificial intelligence AI sovereignty may have received an unexpected boost from Anambra State, where the state’s ICT Agency has begun deploying a locally trained AI system to automate government operations and explore new ways […]

SONGWE: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Mkoa wa Songwe unapaswa kutazamwa kipekee utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa kujenga uchumi unaozalisha fursa, ajira. Akizungumza katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Dira 2050 mkoani Songwe, Prof Mkumbo amesema lengo ni kuubadilisha mkoa kutoka kuwa wa kiutawala…

The prosecution has objected to Chadema chairman Tundu Lissu’s request to call President Samia Suluhu Hassan and other senior government officials as defence witnesses in his treason trial.

…Appeal to Ondo, Delta govts over land dispute By Dayo Johnson, Akure Leaders and residents of 19 coastal and oil-rich communities in Ilaje Local Government Area of Ondo State have raised the alarm over an alleged invasion of their ancestral land by armed persons from neighbouring communities in Delta State. The communities, all located in […]

DAR ES SALAAM: WITH the 2026 Basketball Dar es Salaam League (BDL) regular season nearing its decisive stage, Tausi Royals and Reel Dream have emerged as two of the women’s competition’s biggest threats, challenging the established order. The two relatively new sides have made a strong impression through a series of impressive results, raising the…

KWA Atieno, kumbukumbu ya siku aliyomkaribisha kifungua mimba wake duniani haikujumuisha tu furaha ya kumwona mwanawe, bali pia hofu aliyokuwa nayo kabla ya kujifungua kwa upasuaji (Caesarean Section). Alipofahamishwa kuwa angelazimika kujifungua kwa upasuaji, jambo lililomtisha zaidi halikuwa upasuaji wenyewe bali sindano ya kufisha ganzi inayodungwa kwenye uti wa mgongo. Alikuwa amesikia kutoka kwa marafiki kwamba dawa hiyo inaweza kusababisha maumivu ya kudumu ya mgongo, kupooza au hata matatizo ya kumbukumbu baadaye. “Nilikuwa na hofu sana. Nilijiuliza kama baada ya kujifungua ningebaki na matatizo ya mgongo au kama dawa hiyo ingeathiri afya yangu miaka ya baadaye,” anasema. Utaratibu wa kufisha ganzi Hata hivyo, baada ya kuelekezwa na wataalamu wa afya kuhusu jinsi utaratibu wa kufisha ganzi unavyofanya kazi na kwa nini ilikuwa inafaa katika hali yake, hofu yake ilianza kupungua. Kulingana na Shirika la Kitaifa la Takwimu Nchini (KNBS), uzazi kwa njia ya upasuaji nchini umefikia asilimia 20.1 ya jumla ya uzazi unaofanyika katika vituo vya afya, hatua inayomaanisha kuwa zaidi ya mmoja kati ya kila watoto watano huzaliwa kwa upasuaji. Idadi hiyo imevuka kiwango cha juu cha asilimia 15 kinachopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Kisa kama cha Atieno kinaweza kuwa cha kawaida kwa wanawake wengi wanaofaa kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo, huku baadhi yao wakiamini kwamba dawa za kufisha ganzi uti wa mgongo au nusukaputi zinazotumiwa wakati wa upasuaji zinaweza kubaki mwilini na kusababisha matatizo ya kudumu. Lakini wataalamu wanasema kuna tofauti kubwa kati ya hofu kuhusu ganzi na kile ambacho sayansi ya tiba inaonyesha. Kulingana na Dkt Ong’ech Odero John, daktari wa akina mama katika hospitali ya Nairobi Reproductive Health Services ambaye amekuwa katika taaluma hiyo kwa zaidi ya miaka 23, aina ya ganzi inayotumiwa wakati wa upasuaji huo huamuliwa kulingana na hali ya mama, mtoto na mazingira ya upasuaji. “Kwa upasuaji mwingi uliopangwa na hata dharura, kufisha ganzi uti wa mgongo au nusukaputi ndiyo hupendelewa iwapo hakuna sababu ya kimatibabu inayozuia matumizi yake,” anasema. Kwa wale wanaodungwa aina hiyo ya dawa kwenye uti wa mgongo, (spinal anaesthesia), kiasi kidogo cha dawa ya kuondoa maumivu hudungwa kwenye majimaji yanayozunguka neva katika sehemu ya chini ya mgongo. Sehemu ya chini ya mwili huwa ‘imekufa’ kwa muda na mama kwa kawaida hubaki macho wakati wa upasuaji. Hii humwezesha mama kuwa macho wakati mtoto anazaliwa, huku maumivu ya upasuaji yakizuiwa. Utaratibu wa nusukaputi Kwa baadhi ya wanawake, uwezo wa kuwa macho na kumsikia mtoto akilia kwa mara ya kwanza pindi tu anapozaliwa ni mojawapo ya faida kubwa za aina hii ya dawa. Pia, kwa kawaida haihitaji kuwekwa mrija wa kupitisha hewa kwenye koo, jambo ambalo ni tofauti na utaratibu wa nusukaputi (general anaesthesia). “Faida nyingine ni kwamba kiwango cha dawa kinachomfikia mtoto huwa kidogo sana, na kwa kutumia dawa inayofaa ya kupunguza maumivu, uti wa mgongo unaweza pia kusaidia kutoa unafuu wa maumivu baada ya upasuaji,” anasema Dkt Ong’ech. Hata hivyo, kufisha ganzi uti wa mgongo kuna madhara yake. “Shinikizo la damu la mwathiriwa linawezakushuka, mama anaweza kusikia kichefuchefu, kutetemeka au kuwashwa mwilini,” anaeleza Dkt Ong’ech. Shinikizo la damu, Dkt Ong’ech anasema, hufuatiliwa kwa karibu wakati wote wa upasuaji na linaweza kutibiwa kwa haraka kwa kutumia maji ya mishipa au dawa. Pia kuna madhara ambayo hayatokei mara nyingi, kama vile maumivu makali ya kichwa, sehemu za mwili kutofanya kazi ipasavyo na hivyo kuhitaji dawa zaidi au kubadilishwa kuwa nusukaputi. Katika hali nadra zaidi, kunaweza kutokea maambukizi, kutokwa damu karibu na neva za uti wa mgongo, kuumia kwa neva au mzio mkali wa dawa. Kwa upande mwingine, nusukaputi humfanya mgonjwa kupoteza fahamu wakati wa upasuaji. Dawa hutolewa ili kumfanya mama alale, na kwa kawaida mrija huwekwa kwenye njia ya hewa huku mashine ikimsaidia kupumua wakati wa upasuaji. Baada ya dawa kuanza kuisha nguvu, mama huanza kuamka. Dkt Ong’ech anasema nusukaputi ni muhimu sana katika hali fulani na si sahihi kwa mwanamke kuamini kwamba aina hii ya ganzi ni hatari kila wakati. “Inaweza kutumika wakati upasuaji ni wa dharura kiasi kwamba hakuna muda wa kutosha kufisha ganzi uti wa mgongo au wakati kufisha ganzi uti wa mgongo hakuwezi kutumiwa,” anaeleza daktari huyo. Pia utaratibu huo unaweza kuhitajika mama akiwa anatokwa na damu nyingi, ana matatizo makubwa ya moyo na mishipa, ana tatizo la kuganda kwa damu au anatumia dawa za kupunguza kuganda kwa damu. “Nusukaputi pia ni mbinu salama na muhimu inapohitajika. Hasa katika hali za dharura, inaweza kuokoa maisha,” anasema. Je, dawa hubaki mwilini? Mojawapo ya hofu zinazowasumbua baadhi ya wanawake ni kwamba dawa inaweza kubaki mwilini kwa miaka mingi na kusababisha matatizo ya kumbukumbu, akili au afya ya uzazi. Dkt Ong’ech anasema ni muhimu wanawake kupata maelezo kutoka kwa wataalamu badala ya kutegemea simulizi za watu. Anasema aina ya dawa huzingatia hali ya kila mgonjwa na aina ya upasuaji unaofanywa. Kwa hivyo, mwanamke aliyekufishwa ganzi uti wa mgongo hapaswi kudhani kwamba kwa sababu alipokea aina hiyo ya upasuaji, dawa hiyo itaendelea kuwa mwilini na kumletea matatizo miaka ijayo. Vipi kuhusu uti wa mgongo? Hofu nyingine maarufu ni kwamba sindano ya kufisha ganzi hasa inayodungwa kwenye uti wa mgongo inaweza kusababisha maumivu ya mgongo ya kudumu au hata kupooza. Ingawa matatizo ya neva ni miongoni mwa madhara yanayoweza kutokea, Dkt Ong’ech anasema matatizo makubwa ni nadra. Kabla ya kudungwa dawa, daktari huangalia historia ya afya ya mama mjamzito, dawa anazotumia na hali nyingine zinazoweza kuongeza hatari. “Hii ndiyo sababu wanawake wanashauriwa kumweleza daktari husika kuhusu dawa zote wanazotumia, hasa dawa za kupunguza kuganda kwa damu,” anasisitiza daktari huyo. Pia anasema waathiriwa wanapaswa kumweleza daktari iwapo wana matatizo ya kuganda kwa damu, idadi ndogo ya chembechembe za damu, matatizo ya mgongo, wamewahi kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo au wana ugonjwa wa neva. Kwa mama mjamzito, usalama wa mtoto ni sehemu muhimu ya uamuzi kuhusu aina ya upasuaji. Kwa kufisha ganzi uti wa mgongo, mama huwa macho na kiwango cha dawa kinachomfikia mtoto kwa kawaida huwa kidogo. Kwa nusukaputi, dawa hupitia kwenye kondo la nyuma na zinaweza kumfikia mtoto. Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba aina hiyo ya upasuaji ni hatari kwa kila mtoto. Aina hiyo inaweza kuwa muhimu katika hali ambapo kuchelewesha upasuaji ili kutumia njia mbadala kunaweza kuhatarisha maisha ya mama au mtoto. “Kwa hivyo, uamuzi haupaswi kufanywa kwa kuogopa jina la dawa bali kwa kuzingatia hali halisi ya mama na mtoto wakati huo.” Kwa mujibu wa Dkt Ong’ech, mojawapo ya mambo muhimu zaidi ambayo mama anaweza kufanya ili kupunguza hatari ni kumpa daktari taarifa kamili kuhusu afya yake. “Hii inahusisha dawa zote anazotumia, tatizo alilowahi kuwa nalo, matatizo aliyowahi kupata kutokana na ganzi, matatizo ya kuganda kwa damu, magonjwa ya moyo au mapafu na muda aliokula au kunywa mara ya mwisho. Pia mama anapaswa kueleza hofu na mapendeleo yake. “Usiogope kuuliza kuhusu aina ya dawa, kwa nini imechaguliwa na madhara yanayoweza kutokea,” anashauri.

The High Court has ruled that Chadema chairman Tundu Lissu has a case to answer in his treason trial, requiring him to present his defence.

KWA zaidi ya miongo mitatu, wakazi wa Lorogon, mpakani mwa Turkana na West Pokot, wameishi kwa hofu ya majangili wenye silaha. Lakini sasa bunduki zimetulia kwa kiasi kikubwa kufuatia operesheni ya serikali ya kuwapokonya silaha wahalifu hao, na wakazi wanataka amani hiyo iwaletee ajira, maji, umeme na maisha bora. Lorogon iko kati ya Mto Turkwel na vilima vyenye mabonde magumu kufikika, ambayo kwa miaka mingi yamekuwa maficho ya majangili. Hapo, maisha yalitawaliwa na milio ya risasi huku watoto, wanawake na wazee wakiathirika. Baadhi ya familia zimebaki na makaburi ya wapendwa wao waliouawa katika ghasia hizo. Ukosefu wa usalama pia uliathiri uchumi. Wakulima walishindwa kufikia mashamba yao, huku mifugo, ambayo ndiyo tegemeo la familia nyingi, ikiibwa mara kwa mara. Hata safari ya kutafuta maji iligeuka kuwa hatari. Bi Leah Natuk alisema wakazi walikuwa katika hatari ya kushambuliwa wakati wowote makundi hasimu yalipofanya mashambulizi ya kulipiza kisasi. Alikumbuka tukio la mwaka 2013 ambapo majangili walizingira kijiji hicho kwa siku tano baada ya kuziba barabara kutoka Kainuk kupitia Sarmach na Turkwel. Walikata miti mikubwa, kuchimba mashimo na kuweka mawe barabarani kuzuia magari kuingia au kutoka. “Majangili walitaka kutulazimisha kuondoka katika kijiji cha mababu zetu kwa sababu tulisisitiza kuwa kiutawala na kisiasa tunahusishwa na Kaunti ya Turkana,” alisema. Sasa usalama unaporejea, wakazi wameanza kuangalia zaidi ya kuishi kwa hofu. Katika mkutano wa wadau uliofanyika Shule ya Msingi ya Lorogon, walishukuru serikali kwa kurejesha usalama na kusema wanaweza kusafiri hadi Kainuk bila kusindikizwa na polisi. Naye Bi Esther Piarai, alitaka idadi ya Polisi wa Akiba iongezwe, akisema kijiji hicho kina askari watatu pekee. Pia alitaka wenyeji wapewe ajira katika ujenzi wa bomba la maji linalotarajiwa kujengwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya. “Tunaomba tupewe nafasi ya haki katika ajira zitakazopatikana wakati wa ujenzi wa bomba la maji,” alisema. Wakazi pia wanataka mfumo wa zamani wa maji urejeshwe na kijiji kiunganishwe na umeme. Mkazi Peter Lochuge alisema hali hiyo ni ya kushangaza kwa kuwa Lorogon iko takriban kilomita mbili kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Turkwel chenye uwezo wa kutoa megawati 106. “Tuko kilomita mbili tu kutoka kituo hicho lakini tumekosa umeme kwa zaidi ya miaka 30,” alisema. Wakazi pia wanatarajia kunufaika na mradi wa unyunyuzaji wa Lower Turkwel wa thamani ya Sh1.8 bilioni. Mradi huo utahusisha ekari 1,000 na kutumia maji kutoka Bwawa la Turkwel Gorge. Waziri wa EAC ASAL na Maendeleo ya Kikanda Beatrice Askul alisema mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuunda ajira na kuimarisha amani. Gavana wa Turkana Jeremiah Lomorukai alisema ushirikiano wa jamii ni muhimu ili mradi huo ufanikiwe. Alitaka serikali kuharakisha kupokonya wakazi silaha haramu, akisema ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo na utulivu wa eneo hilo.

For some patients, treating Helicobacter pylori (H. pylori) is no longer a straightforward process, with doctors reporting cases in which commonly used medicines fail to clear the infection.

SERIKALI ya Rais William Ruto imeanza kuimarisha kampeni ya mawasiliano kwa umma kuhusu sera, miradi na mafanikio yake huku uchaguzi mkuu wa 2027 ukikaribia. Hatua hiyo inafuatia barua ya Mkuu wa Utumishi wa Umma na Wafanyakazi wa Ikulu, Felix Koskei, kwa mawaziri, makatibu, msemaji wa serikali na wakuu wa mashirika ya serikali. Katika barua iliyoandikwa Agosti 17, 2026, Bw Koskei aliwaagiza maafisa hao kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na kuelezea juhudi za serikali, sera zake na miradi inayotekelezwa. “Kuna haja ya dharura ya kuwasiliana kikamilifu na wananchi kwa wakati kuhusu sera, mipango na shughuli muhimu za serikali,” alisema katika barua hiyo. Hatua hiyo inajiri mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2027, huku serikali na upinzani tayari zikianza kujipanga kisiasa. Ingawa barua hiyo haitaji uchaguzi au kampeni, muda wake umeibua maswali kuhusu nafasi ya mawasiliano ya serikali katika uchaguzi ujao. Kwa miaka minne iliyopita, serikali imekuwa ikikosolewa kuhusu gharama ya maisha, ushuru, deni la taifa, mageuzi katika afya, makazi, elimu na ukosefu wa ajira. Upinzani nao umefanya rekodi ya serikali katika uchumi kuwa hoja kuu katika juhudi za kumng’oa Rais Ruto madarakani. Bw Koskei alisema serikali imekuwa ikijibu masuala yanapozuka badala ya kutoa taarifa kwa wananchi mapema. Wakati mwingine, alisema, maafisa wa serikali wamekuwa wakitoa taarifa zinazokinzana. Hali hiyo, kulingana na barua hiyo, imechangia kupungua kwa imani ya wananchi kwa serikali. Sasa kila wizara, idara na shirika la serikali litaandaa mkakati wa mawasiliano unaoendana na Sera ya Kitaifa ya Mawasiliano iliyoidhinishwa na Baraza la Mawaziri. Mikakati hiyo itahusisha kueleza sera na miradi, namna ya kushughulikia majanga na dharura, kushirikisha wananchi, kutenga fedha za mawasiliano na kuwasiliana mara kwa mara na vyombo vya habari. Mawaziri, makatibu na wakuu wa mashirika pia wameagizwa kuchukua “jukumu kamili” la kutoa taarifa kwa wakati na kwa njia iliyoratibiwa. Aidha, wameagizwa kukabiliana na taarifa potovu na kuzuia watu wengine kutawala mjadala wa kitaifa. Katika enzi ya mitandao ya kijamii, serikali inaonekana kuongeza nguvu katika simulizi kuhusu utendaji wake. Kituo cha Kitaifa cha Mawasiliano pia kitaanza kutekeleza majukumu yake mara moja. Kituo hicho, kilichoanzishwa kupitia Amri ya Rais nambari moja ya mwaka 2025, kitatumika kama hifadhi kuu ya taarifa za serikali. Kituo hicho kitakusanya, kuchambua, kuthibitisha na kuandaa taarifa kabla ya kusambazwa kwa wananchi. Msemaji wa Serikali Charles Owino atakuwa na jukumu la kusambaza taarifa hizo kupitia majukwaa mbalimbali. Serikali inataka mawasiliano yake yawe na “uwiano, uthabiti na ufanisi” ili kuzuia taasisi zake kutoa ujumbe unaokinzana. Miradi mikubwa ya serikali pia italazimika kuwa na mpango wa mawasiliano tangu hatua ya kuandaliwa kwake. Hii ina maana kuwa miradi kama barabara, hospitali, nyumba za bei nafuu, maji na mipango ya elimu itapaswa kuelekezwa kwa wananchi kuhusu maendeleo yake na manufaa yanayotarajiwa. Mawasiliano hayo pia yataingizwa katika mikataba ya utendakazi ya maafisa wakuu, hivyo kuwafanya kuwajibika moja kwa moja kwa taarifa wanazotoa kuhusu kazi za serikali. Majukwaa yatakayotumika ni pamoja na Kenya Broadcasting Corporation, Kenya News Agency, Kenya Yearbook Editorial Board, Government Advertising Agency, tovuti za serikali na mitandao rasmi ya kijamii. Serikali pia imeagiza matumizi zaidi ya simu za mkononi na majukwaa kama X, Facebook, TikTok, YouTube na WhatsApp. Hata hivyo, wakosoaji wanaweza kuhoji iwapo hatua hiyo itatumika kutoa taarifa kwa umma au kubadilika na kuwa kampeni inayolipiwa na walipa kodi. Wakili Chris Omore alisema sheria za uchaguzi na mfumo wa matumizi ya fedha za umma zinaweka mipaka kuhusu matumizi ya rasilimali za serikali kwa shughuli za kisiasa. “Mawasiliano ya serikali lazima yabaki kutoa taarifa halali kwa umma na yasivuke mpaka na kuwa kampeni ya moja kwa moja ya kisiasa,” alisema.

MAHAKAMA ya Makadara imefunga faili ya uchunguzi dhidi ya mlinzi wa Katibu wa Masuala ya Vijana, Fikirini Jacobs kuhusu kupigwa risasi na kuuawa kwa kiongozi wa vijana mtaani Kariokor, Cecil Ouma, huku ikisubiri uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP). Mahakama ilisema faili hilo haiwezi kuendelea kuwa wazi kusubiri wachunguzi kukamilisha mchakato wa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa kisayansi kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma. Afisa wa polisi, Rashid Charo alikamatwa kufuatia kifo cha Bw Ouma aliyepigwa risasi Juni 30 katika eneo la Kariokor, Nairobi, wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Bw Fikirini Jacobs. Baadaye aliachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000 huku uchunguzi ukiendelea. Katika kikao cha mahakama kilichoendeshwa kwa njia ya mtandao Jumatano, Hakimu James Juma Maiya alimkosoa afisa wa uchunguzi kwa kupotosha mahakama kuhusu hali ya kesi hiyo. Katika kikao kilichotangulia siku 10 zilizopita, afisa huyo alikuwa ameambia mahakama kuwa faili ya uchunguzi tayari ilikuwa imewasilishwa kwa DPP na polisi walikuwa wakisubiri uamuzi wake. Hata hivyo, ilibainika kuwa faili iliwasilishwa kwa DPP Agosti 18, siku moja tu kabla ya kikao cha Jumatano. “Faili hii imefungwa. Afisa wa uchunguzi atasubiri maelekezo ya ODPP. Kwa sasa, faili imefungwa,” hakimu aliamuru. Kufungwa kwa faili hakumaanishi kuwa suala hilo limefikia kikomo. Sasa macho yote yako kwa DPP, ambaye atapitia matokeo ya uchunguzi wa kisayansi pamoja na faili ya uchunguzi kabla ya kuamua iwapo Bw Charo au mtu mwingine yeyote atafunguliwa mashtaka kutokana na kifo hicho. Wakili wa Bw Charo, Cliff Ombeta, aliomba mahakama kumruhusu mteja wake kurejea kazini, akisema amezingatia masharti yote ya mahakama na amekuwa akihudhuria vikao kila alipohitajika. “Hadi sasa, hajakuwa akienda kazini kwa sababu lazima aendelee kufuatilia hali hii,” alisema Bw Ombeta. Wachunguzi wamekuwa wakitegemea kwa kiasi kikubwa ushahidi wa kisayansi kubaini aliyefyatua risasi iliyomuua Bw Ouma. Polisi walipata bunduki mbili kutoka kwa walinzi wa Katibu huyo na kuziwasilisha kwa uchunguzi wa kitaalamu wa silaha. Katika kikao kilichotangulia, wachunguzi waliambia mahakama kuwa matokeo ya uchunguzi huo yalikuwa tayari na faili ingewasilishwa kwa ODPP aipitie kabla ya hatua zaidi. Bw Charo alikuwa miongoni mwa watu walioitwa kutoa taarifa kwa wachunguzi baada ya kubainika kuwa alikuwa ndani ya gari ambalo inadaiwa risasi ilifyatuliwa. Uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na madaktari waliowakilisha serikali na familia ya Bw Ouma ulionyesha kuwa alifariki kutokana na jeraha moja la risasi kifuani. Madaktari walibaini kuwa risasi hiyo ilisababisha majeraha makubwa ndani ya mwili na akavuja damu kwa wingi ndani ya kifua, hali iliyosababisha kifo chake. Uamuzi wa ofisi ya DPP utaamua iwapo uchunguzi huo utaishia kwa afisa huyo au mtu mwingine yeyote kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa kuhusika na kifo cha Bw Ouma.

KONSTABO Jim Richardson Onkundi, aliyefariki baada ya kupigwa na jiwe wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi Homa Bay, alikuwa akisubiri kupandishwa cheo kuwa koplo. Onkundi, 36, alikuwa akiendesha gari la polisi lililokuwa limewabeba maafisa watano kutoka Kituo cha Polisi cha Chemelil, Muhoroni, Kaunti ya Kisumu. Alikuwa amemaliza mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo cha Polisi Kiganjo na alikuwa akisubiri kuthibitishwa rasmi kabla ya kupewa cheo kipya. Hata hivyo, ndoto yake ilikatizwa Jumapili baada ya jiwe kurushwa kwenye gari lao katika kituo cha kibiashara cha Olare walipokuwa wakirejea kutoka Homa Bay. Jiwe hilo lilivunja kioo cha mbele na kumpiga Onkundi usoni na kichwani karibu na sikio la kulia. “Aliyerusha jiwe alilenga gari letu moja kwa moja na kwa bahati mbaya jiwe lilimpata dereva. Alipoteza fahamu akiwa anaendesha,” alisema Kamanda wa Polisi wa Muhoroni Fredrick Ombaka. Gari hilo aina ya Isuzu D-Max lilitoka barabarani na kugonga jengo baada ya Onkundi kupoteza fahamu. Maafisa wengine waliokuwa ndani ya gari hilo pia walijeruhiwa. Onkundi alipelekwa Jeneiro Hospital, Nyangeswo, kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga, Kisumu, ambako alitangazwa kufariki. Afisa huyo alijiunga na polisi mwaka 2015 na alikuwa tegemeo la familia yake. Ndugu yake Peter Onkundi alisema alizungumza na marehemu Jumapili asubuhi. “Aliniambia alikuwa kazini Homa Bay na angenipigia simu baada ya kumaliza kazi. Hakupiga simu hiyo. Siku iliyofuata, mwenzake ndiye aliyenipigia na kunijulisha kuwa amefariki,” alisema. Onkundi ameacha mjane na mtoto mmoja. Mwili wake ulihamishiwa mochari ya St Joseph’s Ombo Mission Hospital, Migori, huku mipango ya mazishi ikiendelea. Afisa mmoja wa polisi alisema kifo cha Onkundi kinaonyesha hatari ambazo maafisa hukabili wanapotekeleza majukumu yao. “Kila mtu ana haki ya kuishi, bila kujali taaluma yake au anatoka wapi,” alisema. Alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na polisi na kuepuka vurugu wakati wa mikutano ya kisiasa.

TAKRIBAN vijana 500 walilipwa kuziba barabara kuwazuia wafuasi wa Linda Mwananchi kuingia Homa Bay wakati wa mkutano wao Jumapili iliyopita, huku polisi wakifichua kuwa mapanga 500 na silaha nyingine zilisambazwa kabla ya ghasia hizo. Ripoti ya kijasusi iliyotayarishwa baada ya polisi kunasa silaha hizo imeibua wasiwasi kuhusu kiwango cha maandalizi yaliyofanyika kabla ya mkutano wa Agosti 16. Kamanda wa Upelelezi wa Jinai (DCI) wa Kaunti ya Homa Bay Jimmy Kisobo alisema polisi wanaendelea kuchunguza matukio yote yaliyotokea kabla, wakati na baada ya mkutano huo. Alisema baadhi ya silaha zilisambazwa angalau siku moja kabla ya mkutano huo. “Baadhi ya vijana si waaminifu kwa waliowafadhili kuzua vurugu. Wengine walioshiriki mapigano walishirikiana na maafisa na kutueleza idadi ya silaha zilizotolewa,” alisema Bw Kisobo. Kulingana na polisi, uchunguzi umebaini kuwa hadi vijana 500 walihusika katika vurugu zilizotokea katika maeneo mbalimbali wafuasi wa Linda Mwananchi walipokuwa wakielekea Homa Bay. Polisi pia wanachunguza matamshi ya baadhi ya viongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) waliokuwa wameapa kumzuia Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuingia Homa Bay. Wakati huo huo, polisi walisema wafuasi wa Linda Mwananchi walikuwa wamechochea vijana kukabiliana na upinzani wowote ambao wangekutana nao njiani. Maafisa wa usalama waliweka vizuizi kadhaa barabarani na kukagua magari yaliyokuwa yakielekea Homa Bay kabla ya mkutano huo. Operesheni hiyo ilisababisha polisi kunasa silaha na kuwakamata baadhi ya washukiwa. Wakati wa mkutano huo, vijana wenye silaha kutoka pande mbili walikabiliana huku wanasiasa wakielekea katika maeneo mbalimbali ya mikutano. Polisi walisema matukio kadhaa ya uhalifu yaliripotiwa kabla ya mkutano huo na baada ya wafuasi wa Linda Mwananchi kuondoka Homa Bay. Maafisa katika eneo hilo walisema baadhi ya vijana wameanza kujitambulisha na wanasiasa fulani na mara nyingi hutoa ulinzi kwa viongozi wanaowaunga mkono wakati wa mikutano ya kisiasa. Polisi walionya kuwa makundi kama hayo yanaweza kuhusika katika vurugu joto la kisiasa linapopanda. Bw Kisobo pia alisema polisi wanamtafuta Khassim Abdi, ambaye amehusishwa na ghasia hizo na ambaye hakutii agizo la kujisalimisha. Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi Muchiri Nyaga alisema Abdi aliamriwa kuripoti katika makao makuu ya DCI katika kaunti baada ya vurugu hizo. Hata hivyo, kufikia Alhamisi hakuwa ametii wito huo, hali iliyosababisha mahakama kutoa kibali cha kukamatwa kwake. Polisi pia wanachunguza uvamizi katika biashara mjini Homa Bay kabla ya mikutano hiyo. Miongoni mwa zilizolengwa ni Homa Bay Tourist Hotel, ambako mali ya thamani ya zaidi ya Sh300 milioni iliharibiwa. Washambuliaji waliingia hotelini wateja wakila na kuwalaumu kwa kutounga mkono serikali ya sasa. Bw Kisobo alisema mtu aliyelengwa katika tukio hilo ni mwanasiasa anayewania kiti cha ubunge. “Mwanasiasa huyo alijaribu kueleza kuwa anaunga mkono serikali na alikuwa ameonyesha nia ya kuwania kwa tiketi ya UDA. Lakini Abdi, ambaye pia anadai kuunga mkono tutam, hakutaka kusikia maelezo hayo,” alisema. Mwanasiasa huyo, ambaye ana leseni ya kumiliki bunduki, alidaiwa kutoa bastola yake na kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya vijana hao na kuzuia uharibifu zaidi. Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga, hata hivyo, alikanusha kuhusishwa na ghasia hizo. “Hakuna tukio hata moja ambapo nimehusishwa na vurugu au ghasia katika kampeni zangu. Hatujawahi kufanya hivyo na hatuwezi kuanza sasa,” alisema. Alisema hayo akitoa pole kwa familia ya Noreen Nalangwa, raia wa Uganda aliyefariki Jumapili baada ya kugongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi wakati wa vurugu zilizohusishwa na mkutano wa Linda Mwananchi. Gavana huyo aliwataka vijana na wanasiasa waliotembelea eneo hilo kujizuia na kuepuka uchochezi. Ghasia hizo zilisababisha vifo vya watu wawili na uharibifu wa mali, ikiwemo hoteli ya Homa Bay Tourist na ofisi za kanisa la Seventh Day Adventist (SDA). Raia, polisi na wanahabari kadhaa walijeruhiwa, huku biashara katika baadhi ya maeneo ya Homa Bay Town zikifungwa kutokana na ghasia.

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameapa kutembelea Emurua Dikirr, Narok, leo Ijumaa licha ya vitisho kutoka kwa viongozi wa eneo hilo. Chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP) kimesema Bw Gachagua atatumia ziara hiyo kuwashukuru wakazi waliounga mkono chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika hivi majuzi. Pia, anatarajiwa kuzungumzia masuala ya ardhi na kile anachodai ni kushindwa kwa serikali kulinda haki za wakazi kuhusu ardhi. Mvutano kuhusu ziara hiyo umeongezeka huku viongozi wanaounga mkono serikali na wale wa upinzani wakibadilishana kauli kali. Katika uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr, mgombea wa DCP Vincent Rotich alipata kura 10,760, huku mgombea wa UDA David Keter akishinda kwa kura 18,266. Bw Gachagua amesema kura hizo ni ishara kwamba chama chake kinaanza kupata uungwaji mkono katika eneo linalochukuliwa kuwa ngome ya Rais William Ruto. Nitakuwa Emurua Dikirr Agosti 21 kuzungumza na watu walioniamini na kuunga mkono chama cha DCP licha ya changamoto zote,” alisema. Bw Gachagua pia atatembelea familia ya aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno katika kijiji cha Mogindo kutoa rambirambi, miezi mitano baada ya kiongozi huyo kufariki katika ajali ya helikopta. Jumatano, Bw Gachagua alizungumza kwa simu na mama wa marehemu, Mama Mary Temas, na kumthibitishia kwamba angemtembelea leo. Pia amesema atatumia ziara hiyo kuzungumzia kifo cha Bw Ng’eno na kucheleweshwa kwa ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo. Ajali hiyo ilitokea Februari 28, 2026 katika kijiji cha Chepkiep, kaunti ya Nandi. Watu sita walifariki. Waliofariki ni Bw Ng’eno, rubani George Were, mpiga picha Nick Kosgei, afisa wa Huduma ya Misitu Kenya Amos Kipngetich Rotich, mwalimu Carlos Robert Kibet Keter na afisa wa itifaki wa Serikali ya Kaunti ya Narok Wycliff Kiprotich Rono. Serikali iliahidi kutoa matokeo ya uchunguzi, lakini ripoti hiyo bado haijatolewa hadharani na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA). Bw Gachagua na marehemu Ng’eno walikuwa washirika wa karibu kisiasa kabla ya mchakato wa kumuondoa Bw Gachagua kama Naibu Rais kuanza. Wakati huo, Bw Ng’eno alikuwa miongoni mwa wabunge waliosemekana kuwa hawakuunga mkono kwa dhati juhudi za kumtimua Bw Gachagua. Mbunge Keter amemuonya Bw Gachagua kutotembelea Emurua Dikirr, akisema ziara yake inaweza kuvuruga amani. “Nataka kumuonya Bw Gachagua asikanyage Emurua Dikirr kwa sababu hajaribishwi hapa. Aelekeze nguvu zake kwingine kwa kuwa hapa ni eneo la UDA,” alisema. Mbunge huyo pia alimlaumu Bw Gachagua kwa kuwakosoa mara kwa mara wanachama wa jamii ya Kalenjin katika mikutano ya kisiasa huku akitafuta uungwaji mkono wao kuelekea uchaguzi wa 2027. Naibu Gavana Koech pia alisema ziara hiyo haitakuwa rahisi. “Imekuwa wazi kwamba Bw Gachagua amejaribu uvumilivu wetu. Hatuwezi tena kukaa kimya. Hawezi kututukana halafu aje katika eneo letu kutafuta uungwaji mkono,” alisema. Lakini Bw Gachagua amepuuzilia mbali vitisho hivyo. Amesema amekuwa mwathiriwa wa mashambulizi zaidi ya 25 ambayo amedai yalifanywa na makundi yanayoungwa mkono na serikali pamoja na maafisa wa polisi. “Mpaka sasa nimeshambuliwa zaidi ya mara 25. Hii haijapunguza kasi yangu. Niko tayari kukabiliana na mengi zaidi,” alisema akiwa Murang’a. Amesema hakuna vitisho vitakavyomzuia kutembelea Emurua Dikirr. “Wacha watuletee vurugu. Nimepata taarifa kwamba wanapanga kufanya hivyo, lakini hilo halitatuzuia. Tutaendelea na ziara yetu bila woga,” alisema. Kiongozi wa Wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot na Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago wamesema Bw Gachagua ana haki ya kutembelea Rift Valley. Bw Cheruiyot alisema jamii ya Kipsigis haiwafukuzi wageni na kwamba Bw Gachagua atakaribishwa kama mwanasiasa mwingine. “Katika utamaduni wetu kama jamii ya Kipsigis, hatuwafukuzi wageni. Tunawakaribisha wafanye shughuli zao na waondoke kwa amani. Tutajitokeza kukusalimia, lakini usifikirie kwamba hiyo itakuletea kura mwaka ujao,” alisema. Bw Mandago alisema jamii ya Rift Valley haitakubali kuchochewa kufanya vurugu kwa misingi ya siasa.

DODOMA; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Mwenyekiti wak, Deodatus Mwanyika, imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake ya udhibiti ubora kwa ufanisi. Mwanyika amesema kuwa juhudi zinazofanywa na TBS kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa zinazotumiwa na Watanzania…

DODOMA; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo imeipongeza TBS kwa kutekeleza majukumu yake ya udhibiti ubora kwa ufanisi. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deogratias Mwanyika wakati wa kikao cha Kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu,katika, ofisi za Bunge jijini Dodoma mapema leo. Mwanyika amesema juhudi zinazofanywa na…

The party said the report raised fresh questions about how much was actually saved, how much was shared among the three tiers of government, and what the funds were used for.

DODOMA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Jijini Dodoma leo. Ayoub amesema wizara inaendelea kuimarisha amani na usalama wa raia pamoja na mali zao. Amebainisha…

— Says lives of Christians, Muslims, traditional worshippers matter By Chimaibi Nwaiwu NNEWI — The Christian Elders and Professionals Consultative Council of Nigeria (CEPCCN) has expressed support for concerns raised by the United States over the safety of Christian communities and the worsening security situation in Nigeria. The group, however, stressed that all Nigerian lives […]