
"IKIFIKA 2028/29 TAYARI TUTAKUWA NA KATIBA MPYA"/ HOTUBA YA RAIS AKIONGEA NA POLISI
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania

VIONGOZI wa Wiper wamekosoa serikali kwa kile walichosema ni ugavi usio wa haki wa rasilimali, ajira na miradi ya maendeleo nchini. Kiongozi wa chama hicho, Kalonzo Musyoka, amemtaka Rais William Ruto kutoa takwimu za Wakenya walioajiriwa hivi karibuni katika jeshi na polisi, akidai ajira hizo zimegawanywa kwa misingi ya kikabila. Bw Musyoka pia alilaani kushambuliwa kwa viongozi, akimtaka Rais kuwajibika kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi na ongezeko la ghasia za kisiasa. Alitaja pia utata kuhusu zabuni ya sare mpya za polisi, madai ya “kuuzwa” kwa nafasi za walimu na mgogoro wa ardhi ya ekari 4,000 Taita Taveta. Mbunge wa Matungulu, Mutinda Mule, alitishia kuishinikiza NCIC kuchunguza madai ya ajira za walimu kutolewa kupitia barua za wanasiasa. Alimtaka Rais Ruto ndani ya siku saba kutoa idadi ya walioajiriwa kwa njia hiyo, la sivyo Wiper itaihusisha NCIC kupitia Bunge. Madai hayo yanaibuka baada ya Spika Moses Wetang’ula kusema baadhi ya wabunge walipelekwa Ikulu kuchukua barua za ajira za walimu, ambazo baadaye ziliuzwa kwa hadi Sh400,000.

DODOMA; Serikali imesema kanuni ya kikokotoo kwa wastaafu hutumika kwa wafanyakazi wote walioajiriwa sekta ya umma na binafsi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu ametoa kauli hiyo bungeni leo Agosti 31, 2026 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Said Ali Mbarouk aliyehoji serikali ina mpango…

DODOMA; Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Mikopo kwa Dhamana za Mali Zinazohamishika wa Mwaka 2026. Akiwasilisha bungeni muswada huo leo Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omatr, amesema lengo la kutunga Sheria ya Mikopo kwa Dhamana za Mali Zinazohamishika wa Mwaka 2026 ni kuweka masharti bora ya usimamizi wa mikopo inayopatikana kwa kutumia…

WAHUDUMU wa wanaopamba miili ya waliokufa wameeleza changamoto wanazopitia katika jamii kutokana na unyanyapaa. Bi Margaret Santa Thoya, 26, mkazi wa kijiji cha Muyeye kilicho Malindi, Kaunti ya Kilifi ambaye hutekeleza ulimbwende kwa waliokufa anasema kuwa urembeshaji anaoufanya husaidia kuboresha au kuipa maiti muonekano wa utulivu bila wengine kuogopa wanapoitazama. Ni kupitia ujuzi wake ambapo hujipatia kati ya Sh1,500 na Sh7000 kwa kila kandarasi moja anayopata. Malipo yake huyakadiria kulingana na hadhi au tabaka la familia husika, umri wa mwendazake na mfumo au namna ambayo familia husika itapendekeza mpendwa wao apambwe. Amedumu katika kazi hiyo ya kupamba maiti kwa zaidi ya miaka minne sasa. Alikamilisha masomo yake ya darasa la nane (KCPE) 2016 katika shule ya msingi ya Karima iliyoko viungani mwa mji wa Malindi. Hakufaulu kuendeleza masomo yake ya juu kwani mama yake aliachwa mjane. Aliwahi kufanya kazi katika saluni mjini Malindi, hivyo kupokea ujuzi wa kazi za urembo. “Kuna siku ambapo niliraiwa na familia moja kwenda mochari Malindi kuwarembeshea mpendwa wao mwanamke aliyekuwa ameaga. Nilijikaza na kuitekeleza kazi hiyo vyema, hivyo nikalipwa fedha nzuri. Tangu hapo nikaamua kujiingiza mzimamzima kwenye nyanja hii ya kurembesha maiti,” akafichua Bi Santa. Licha ya kujijengea jina kubwa katika kazi yake, kinachomsikitisha binti huyu ni jinsi baadhi ya wanajamii wanavyomtenga au kumsuta ilihali wengine wakiogopa kutangamana naye. Analalamika kuwa miaka yote amekosa mume wa kumchumbia kwani wengi wao punde wanapomuona humtoroka huku wakimbandika majina ya ‘Maggie wa Mochari.’ “Sijapata mwanamume jasiri aliyewahi kunifuata kunichumbia. Wengi hawataki. Kuna ambao hata kuzungumza nami au kunisalimia ni shida. Wakiniona kwa mbali utasikia wakinisuta eti ni yule ‘madam wa mochari.’ Wengine hutoroka au kunipisha njia kwa mbali wakihisi mimi ni nuksi maishani kwa maamuzi yangu ya kutangamana na kurembesha maiti,” akasema. Tatizo lake hata hivyo haliwakumbi wanawake pekee wanaojihusisha na taaluma kama yake. Bw Samson Karisa, mkazi wa mjini Kilifi alilazimika kuhamia mjini Malindi, karibu kilomita 61 kutoka kwao ilmuradi ajihusisha na biashara ya kurembesha maiti. Anakiri kutekeleza jukumu lake kwa usiri mwingi kwani mamake mzazi, mkewe na wanawe wawili hawafahamu ni kazi gani hasa yeye hujihusisha nayo maishani kuleta mapato nyumbani. Amekuwa akilipwa ili kurekebisha majeraha hasa endapo marehemu alipata ajali. Yeye hutumia nta spesheli kuziba na kujenga upya sehemu zilizoharibika za mwili ili kuzipa mwonekano ufaao. “Pia humvalisha nguo marehemu na kumweka katika jeneza kwenye pozi la kulala kwa amani, kuipanga mikono vizuri katika hali ya kawaida kifuani au tumboni,” akaeleza Bw Karisa. Kutokana na kazi yake, jamii ya mjini Malindi tayari imembandika jina la ‘Karisa wa Kifa,’ Kiswahili Karisa wa Kifo. Wataalamu wa saikolojia wanasema yale ambayo wawili hao wanapitia yanatokana na imani na desturi za jamii nyingi ambazo huamini chochote kinachohusiana na kifo huwa na mabaya. Hata hivyo, jamii iliombwa itambue kuwa, kuna aina nyingi za kazi ambazo zinahusu masuala ya kifo.

DODOMA; Serikali imesema gharama za upimaji ardhi kwa maeneo ambayo yameendelezwa hutozwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Urasimishaji wa mwaka 2021. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Dickson Lutevele aliyehoji lini serikali itaanzisha utaratibu wa kupima ardhi kwa bei…

Tanzania’s land is increasingly becoming an economic asset under pressure, as climate change, population growth, expanding agriculture and weak spatial planning collide to raise the cost of doing business and threaten livelihoods.

ABIRIAkatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) waliingiwa na wasiwasi na sintofahamu kuhusu safari zao baada ya wafanyakazi wa sekta ya anga kuanza tena mgomo. Hali hiyo ilisababisha safari kadhaa za ndege ndani na nje ya nchi kucheleweshwa. Wasafiri walisema hawakupewa taarifa ya kutosha kuhusu mgomo huo, huku baadhi yao wakifika uwanjani na kugundua kuwa safari zao zilikuwa zimecheleweshwa. Muungano wa Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga nchini (KAWU) ulianza tena mgomo Jumamosi usiku kutokana na malalamishi mbalimbali, yakiwemo yale yaliyosababisha kusimamishwa kwa mgomo wa awali mwezi uliopita. Mwenyekiti wa KAWU Walter Ongeri aliambia Taifa Leo kuwa wafanyakazi waliamua kurejea kwenye mgomo baada ya serikali kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa maelewano (MoU) uliotiwa saini na muungano huo. “Tulitia saini makubaliano ya kurejea kazini lakini, kwa bahati mbaya, KAA na KCAA zimeshindwa kushughulikia malalamishi yetu. Asasi hizo mbili hazijajitolea kikamilifu katika mazungumzo na zimeshindwa kushirikiana nasi katika kutafuta suluhu ya malalamishi yetu,” akasema Katibu Mkuu wa KAWU Moss Ndiema. Glen Omindu, aliyekuwa anatarajia kusafiri Dubai kwa ndege ya saa saba mchana, alisema abiria hawakuwa wameambiwa wangetoka saa ngapi. “Hakukuwa na onyo lolote na hilo ndilo tatizo. Ndege ilikuwa iondoke saa saba lakini bado hatujaambiwa tutasafiri lini. Tutalazimika kutafuta cha kufanya kwa sasa na ninatumai mambo yatakuwa sawa au niahirishe safari,” akasema Bw Omindu. Faith Mbugua, aliyefika uwanjani saa nne asubuhi kwa safari yake ya saa saba, alisema abiria walikuwa wakihangaika kupata taarifa kuhusu safari yao. “Tumechanganyikiwa sana. Tulikuwa hapa saa nne na tukaambiwa kuna mgomo. Safari yetu sasa imepangwa kuondoka saa 2:50 usiku,” akasema. Stephen Maguro, aliyekuwa akisafiri Rwanda kuhudhuria mkutano, pia alisema safari yake ilikuwa imecheleweshwa. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (KAA) ilisema viwanja vya ndege kote nchini vilikuwa vikikumbwa na abiria kucheleweshewa safari. “KAA inashirikiana kwa karibu na mashirika husika ya anga, kampuni za ndege na wadau wengine kudhibiti hali hiyo, kupunguza usumbufu na kuhakikisha shughuli za viwanja vya ndege zinaendelea kwa utaratibu,” akasema. KAA iliwashauri abiria kuwasiliana na kampuni zao za ndege kupata taarifa kuhusu safari zao. Wakati huo huo, maafisa wa KAWU, Wizara ya Uchukuzi na mashirika ya anga walikuwa katika kikao cha dharura Jumapili kutafuta suluhu kuhusu mgomo.

By Yinka Kolawole Emzor Pharmaceutical Industries has raised a $19.8 million (N26.7 billion) Series 1 Fixed Rate Bond on the FMDQ Group Exchange, in a major move to strengthen local pharmaceutical manufacturing and complete West Africa’s first full-scale anti-malarial Active Pharmaceutical Ingredient (API) manufacturing facility. The bond, issued through Emzor’s special purpose vehicle, Emzor Pharma […]

DAR ES SALAAM: MTAALAM katika Sekta ya Mafuta nchini Dk Sajad Habib Rai amempongeza Makamu wa Rais Ndejembi kwa kuapishwa kwake kushika nafasi hiyo huku alimtabiri mambo mengi katika majukumu yake ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan Akizungumza Jijini Dar es Salaam siku moja baada ya uapisho wa Makamu Rais huyo Ikulu ya Cha Chamwino,…

GAVANA wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro, amezidi kuungwa mkono na viongozi wa Kenya Kwanza kutetea kiti hicho katika Uchaguzi wa 2027. Spika wa Seneti, Bw Amason Kingi, alisema wanachama wa UDA Kilifi watamuunga mkono mgombea wa ODM. Hii ni licha ya kuwa, spika wa zamani wa Bunge la Kaunti ya Kilifi, Bw Jimmy Kahindi, alichapishwa kunuia kuwania ugavana kwa tikiti ya UDA miezi sita iliyopita. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa Kilifi, Bw Kingi aliwataka wanachama wa UDA kutohisi wametelekezwa na uamuzi wa chama hicho kutowasilisha mgombea wa ugavana. Bw Kingi pia aliwataka wanachama wa UDA kutomuunga mkono mgombea wa ugavana ambaye atakuwa mpinzani wa Bw Mung’aro, akisema hatua hiyo itakuwa kinyume na makubaliano ya kisiasa kati ya vyama hivyo. Hata hivyo, Bw Mung’aro alisema yuko tayari kukabiliana na mgombea yeyote katika uchaguzi huo, akisema pia yuko tayari kushiriki mchujo wa ODM ili kupata tiketi ya chama hicho. Msimamo wa Bw Kingi unatofautiana na ule wa Katibu Mkuu wa UDA, Bw Hassan Omar, ambaye amekuwa akipinga mpango wowote wa kugawana maeneo ya kisiasa kati ya UDA na ODM.

WABUNGE wanaounga mkono serikali ambao wanaongoza kamati muhimu za Bunge wamekosolewa kwa kushindwa kuwawajibisha mawaziri kuhusu masuala yanayowahusu wananchi. Ripoti iliyowasilishwa na Naibu Kiongozi wa Wengi katika Bunge, Owen Baiya, ilifichua kuwa kamati 19 za Bunge zilikuwa zimeshindwa kutoa majibu kwa maswali yaliyoulizwa na wabunge kwa niaba ya wananchi kufikia wakati Bunge lilipoenda likizo ya mwezi mmoja Alhamisi. Kamati ya Utawala na Usalama wa Ndani iliongoza kwa kuwa na maombi 26 ambayo hayakuwa yamejibiwa. Kamati hiyo inaongozwa na Mbunge wa Narok West, Gabriel Tongoyo. Kamati ya Uchukuzi na Miundombinu, inayoongozwa na Mbunge wa Ndia George Kariuki, ilikuwa ya pili kwa kuwa na maswali 21 ambayo hayajajibiwa kuhusu kuimarishwa kwa miundombinu. Kamati ya Elimu inayoongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly ilikuwa na maswali 18 ambayo hayajajibiwa kuhusu sekta ya elimu. Bw Tongoyo, Bw Kariuki na Bw Melly walichaguliwa kwa tiketi ya UDA, chama tawala katika serikali ya Kenya Kwanza. Ripoti hiyo iliandaliwa kwa maagizo ya Spika wa Bunge Moses Wetang’ula baada ya wabunge kutaka kujua hatua zilizochukuliwa kuhusu maombi yao ya taarifa. “Wabunge wanahitaji kujua jinsi maombi yao ya taarifa yalivyoshughulikiwa na kamati mbalimbali,” alisema Bw Baiya alipowasilisha ripoti hiyo. Bw Baiya aliwataka wenyeviti wa kamati kuhakikisha majibu kutoka kwa mawaziri na mashirika ya serikali yanawasilishwa kwa wakati. “Wanafanya hivyo kwa niaba ya wapigakura wao. Hilo linatulazimu sisi kama wenyeviti wa kamati kuhakikisha yanajibiwa kwa ufupi, kwa usahihi na kwa wakati. Hii itahakikisha Bunge halifanyi kazi bure,” akasema. Kamati za Afya na Fedha na Mipango ya Kitaifa, zinazoongozwa na James Nyikal (Seme) na Kuria Kimani (Molo), kila moja ilikuwa na maombi manane ambayo hayajajibiwa. Kamati ya Ardhi, inayoongozwa na Joash Nyamoko (Mugirango Kaskazini), ilikuwa na maswali saba, huku Kamati ya Ulinzi, Ujasusi na Uhusiano wa Kimataifa ikiwa na sita. Kamati za Kilimo na Mifugo, Nishati na Leba kila moja zilikuwa na maswali matano ambayo hayajajibiwa. Kamati ya Mazingira, Misitu na Madini ilikuwa na manne, huku kamati za Utalii na Wanyamapori na Nyumba, Mipango Miji na Kazi za Umma kila moja ikiwa na matatu. Kamati nyingine zilizokuwa na maswali ambayo hayajajibiwa ni Mawasiliano, Habari na Ubunifu (mawili), Sheria na Haki (moja), Ulinzi wa Jamii (moja), Biashara, Viwanda na Vyama vya Ushirika (moja) na Bajeti na Matumizi (moja). Wabunge hupokea posho za vikao vya kamati pamoja na mshahara na marupurupu mengine. Mwenyekiti wa kamati hupokea Sh15,000 kwa kila kikao, hadi kiwango cha juu cha Sh240,000 kwa mwezi.

SIKU chache baada ya kukumbwa na ghasia zilizosababisha vifo katika Kaunti ya Homa Bay, viongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi jana walijipigia debe katika Kaunti ya Meru wakisema hakuna kiwango cha ghasia kitakachozima kiu chao cha mabadiliko. Vuguvugu hilo linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, lilifika Meru kwa mapokezi makubwa mwenyeji wao akiwa aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, ambaye pia ni kiongozi wa Umoja na Maendeleo Party (UMP). Viongozi hao walihutubia wananchi katika maeneo ya Kiirua, Githongo, Nkubu, Meru mjini na Kianjai. “Tunawashukuru watu wa Meru kwa kudumisha amani na kuonyesha jinsi demokrasia inavyopaswa kufanya kazi,” akasema Bw Sifuna. Katika mikutano hiyo, Bw Sifuna aliishambulia serikali ya Rais William Ruto, akiilaumu kwa kupuuza Katiba, sheria na ahadi ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi. Alisema lengo la Linda Mwananchi ni kurejesha utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na kuimarisha demokrasia. “Rais Ruto alikuwa ameahidi kuheshimu Katiba, siku moja tu baada ya maadhimisho ya miaka 16 ya Katiba, wafanyabiashara walitandikwa na kurushiwa vitoza machozi Nairobi walipokuwa wakipinga ushuru wa juu,” akasema Bw Sifuna. Katibu huyo wa zamani wa ODM pia alimshambulia Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, akisema ameshindwa kukabiliana na uhuni na makundi ya vijana wanaovuruga mikutano ya upinzani. Alisema iwapo Linda Mwananchi itaunda serikali ijayo, Bw Murkomen atakuwa miongoni mwa mawaziri wa kwanza kuondolewa. Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa vyama vya upinzani kuungana ili kumenyana na Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alisema upinzani unapaswa kuwasilisha mgombea mmoja wa urais ili kuongeza nafasi ya kuwahi ushindi. Vilevile, viongozi hao waliishutumu serikali kwa kushindwa kushughulikia ukosefu wa ajira na gharama ya juu ya maisha. Bw Owino aliikosoa serikali kuhusu zabuni ya Sh2.5 bilioni ya sare za polisi, akisema fedha hizo zingetumika vyema kuanzisha viwanda na kuunda nafasi za ajira kwa vijana. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya aliitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuimarisha mifumo yake na kuhakikisha uchaguzi wa 2027 utakuwa huru na wa kuaminika. “Serikali inatoa vitambulisho kwa vijana ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 katika baadhi ya sehem za nchi. IEBC inafaa kuwa chonjo na kuzima juhudi zozote za udanganyifu,” akasema Bw Natembeya. Viongozi hao pia walimtetea Bi Mwangaza, wakidai aliondolewa madarakani kwa njia isiyo ya haki na wanasiasa wanaounga mkono serikali.

ODM inakabiliwa na mtihani mgumu katika uteuzi wa 2027 huku wanachama wa familia ya Odinga wakijitokeza kuwania nyadhifa mbalimbali, hali inayotarajiwa kuzua ushindani mkali ndani ya chama. Kuingia kwa Raila Junior, mwanawe marehemu kiongozi wa ODM Raila Odinga, katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Kibra kumeibua mjadala kuhusu iwapo familia ya Odinga itaendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Kenya hata baada ya kifo cha Raila. Mbali na Junior, Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga, 82, atatetea kiti chake cha useneta wa Siaya. Katika uteuzi wa chama, atakabiliana na aliyekuwa Gavana wa Siaya Amoth Rasanga. “Hata kama wewe ni rafiki yangu, hata kama una pesa, usifikiri kwamba pesa zinaweza kununua uongozi. Tutahakikisha kunakuwa na ushindani huru na wa haki,” akasema Dkt Oginga akiwahakikishia wawaniaji wote kuwa uteuzi utakuwa huru Bw Rasanga, ambaye ni mwanachama wa ODM, ameonya kuwa atatumia njia nyingine kuwania kiti hicho iwapo uteuzi wa chama hautakuwa wa haki na utampendelea Dkt Oginga. “Mimi ni mwanachama wa ODM maisha yote. Wakipendekeza mimi, sawa. Wasipofanya hivyo, nina njia nyingine,” akasema Kibra pia inatarajiwa kuwa uwanja wa vita baada ya Junior, 46, kuanza kufanya mikutano na wazee, makundi ya kijamii, madiwani na wanasiasa wanaounga mkono azma yake. “Kibra ilikuwa ngome ya kisiasa ya babangu, na kama familia tumekuwa na safari ndefu pamoja na watu wa eneo hili. Nikichaguliwa, nitalenga zaidi elimu kwa kuhakikisha kwamba ufadhili wa masomo unapatikana ili kusiwe mtoto anayekosa elimu,” Junior aliambia Taifa Leo. Alisema pia atajitahidi kuboresha huduma za afya na maji pamoja na maisha ya wakazi wa Kibra. Mamake, Ida Odinga, alimpa Junior baraka za kuingia katika siasa, lakini akamsihi afanye siasa safi zisizo na matusi, vurugu au fujo. “Enyi watu wa Kibra mmeamua na sina chaguo jingine. Namkabidhi mwanangu mikononi mwenu. Viongozi mlio hapa, mtunze, mumfundishe na mumwongoze,” akasema Mama Ida. Junior atakabiliana na Mbunge wa sasa Peter Orero na aliyekuwa mbunge Imran Okoth. Orero amesema anaamini uteuzi utakuwa wa haki na yuko tayari kushindana na Junior. “Aje tushindane, lakini kwa hali ilivyo sasa, kazi ambayo nimefanya itafanya mambo kuwa magumu kwa wale wanaomsukuma. Hawezi kunishinda kwa sababu kazi ambayo nimefanya inaonekana,” akasema Bw Orero. Imran, kwa upande wake, ametishia kuondoka ODM na kuwania kama mgombea huru iwapo hakutakuwa na uteuzi wa haki. “Junior yuko huru kuja kushindana, lakini anapaswa pia kujua kwamba tumekuwa kwa chama na tunasisitiza kwamba kusiwe na mapendeleo,” akasema. Winnie Odinga anahusishwa na kinyang’anyiro cha useneta Nairobi, ingawa hajathibitisha rasmi azma hiyo. “Kwa sasa napanga makumbusho ya babangu. Orero ambaye alisema nalenga useneta ananitakia mema,” akaambia Taifa Leo kwenye ujumbe. Ikiwa atawania, atakabiliana na Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor, ambaye tayari ameanza kampeni. Kisumu, Ruth Odinga analenga ugavana na anakabiliwa na wapinzani wenye uzoefu, akiwemo Joshua Oron, Aduma Owuor, Naibu Gavana Mathews Owili, Seneta Tom Ojienda na Rosa Buyu. “Ninachotaka ni ushindani sawa ili aliye bora ashinde,” alisema Ruth. Jaoko Oburu, mwanawe Dkt Oburu, anaripotiwa kulenga ubunge wa Bondo, ingawa hakupatikana kuthibitisha azma hiyo. Ingawa hivyo, amekuwa akishiriki miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo na kisiasa katika eneobunge hilo. Akijitosa, atakabiliana na Mbunge Gideon Ochanda, mfanyabiashara Andiwo Mwai na mwanahabari wa Nam Lolwe FM Haron John. Uwanizi huu wa jamaa umezua kumbukumbu za jinsi Raila alivyokuwa akiingilia kati migogoro ya kisiasa ndani ya familia. Kabla ya uchaguzi wa 2013, Raila aliingilia mzozo kati ya Dkt Oburu na James Orengo kuhusu useneta wa Siaya, na Dkt Oburu akahamia katika kinyang’anyiro cha ugavana. Baada ya mzozo katika uteuzi wa ugavana na William Oduol (sasa naibu gavana wa Siaya), Cornel Rasanga alipewa tiketi ya ODM bila kushiriki mchujo, huku Dkt Oburu akipewa nafasi ya kuwania ubunge. Mnamo 2017, Dkt Oburu alishawishiwa kutowania kiti chochote na badala yake akateuliwa kuwa mbunge wa EALA. Ruth naye mnamo 2013 alilazimika kuridhika na nafasi ya naibu gavana wa Kisumu baada ya mzozo wa uteuzi wa ODM kati yake na Jack Ranguma.

By Obas Esiedesa, Abuja ABUJA — Consumers have expressed concern over the continued volatility in petrol prices across the country, calling on the Federal Government to intervene and ensure stability in the downstream petroleum sector. Checks by Vanguard on Sunday showed that retail outlets in the Federal Capital Territory, FCT, had again increased their pump […]

RAIS William Ruto ametetea vikali rekodi ya serikali yake kuhusu deni la taifa, akisema Kenya imefanikiwa kupunguza kasi ya kukopa ikilinganishwa na tawala mbili zilizotangulia. Kwa mujibu wa Rais, kipimo muhimu si iwapo nchi imeacha kukopa kabisa, bali ni kiwango ambacho deni la umma limekuwa likiongezeka. Alisema deni la taifa lilikuwa takriban Sh10.3 trilioni alipoingia madarakani mnamo 2022 na linatarajiwa kufikia karibu Sh13 trilioni kufikia mwisho wa mwaka huu, ongezeko analodai ni la asilimia 27 pekee katika kipindi cha miaka mitano. “Moi alipoondoka madarakani, deni la taifa lilikuwa Sh630 bilioni. Kibaki alilirithi na kuliongeza hadi Sh1.8 trilioni ndani ya miaka 10. Hilo ni ongezeko la karibu mara tatu,” alisema Rais Ruto. Aliongeza kuwa Rais Uhuru Kenyatta alipomaliza muhula wake 2022 aliacha deni la Sh10.3 trilioni, kiwango ambacho kilikuwa kimeongezeka mara tano kutoka alichokuta Kibaki. “Katika miaka yangu mitano, deni limeongezeka kutoka Sh10.3 trilioni hadi Sh13 trilioni. Hilo si ongezeko la mara kadhaa bali ni asilimia 27 pekee,” alisema. Kauli hiyo ndiyo msingi wa hoja yake kwamba, alitimiza moja ya ahadi zake kuu za kampeni za mwaka 2022 za kudhibiti tabia ya kukopa kupita kiasi. “Nilisema ukiwa ndani ya shimo, jambo la kwanza ni kuacha kuchimba. Hivyo ndivyo tulivyokuta nchi ikiwa,” alisema. Rais alisema alinuia kupunguza kutegemea mikopo, ushuru na madeni kwa kubadilisha jinsi miradi ya maendeleo inavyofadhiliwa. Anasema serikali yake imeendelea kuwekeza katika miundombinu na miradi ya kijamii bila kuongeza deni la kawaida la serikali kwa kasi iliyoshuhudiwa miaka ya nyuma. Miongoni mwa miradi mikubwa aliyotaja ni barabara ya Rironi-Nakuru-Mau Summit, Mradi wa Northern Kenya Gateway, upanuzi wa reli ya kisasa (SGR) kuelekea Kisumu na Malaba, pamoja na miradi ya maji na nishati. Pia alitaja Mpango wa Nyumba Nafuu, ambao una zaidi ya nyumba 300,000 katika hatua tofauti za ujenzi, mabweni ya wanafunzi na masoko ya kisasa. Kwa mujibu wa Rais, uwekezaji katika nyumba, masoko na mabweni pekee umefikia takriban Sh1.2 trilioni. Hata hivyo, wakosoaji wake wanaonya kuwa kuangalia tu kiwango rasmi cha deni hakutoshi. Wanasema kuna majukumu mengine ya kifedha yanayoibuliwa kupitia mbinu mbadala za ufadhili ambayo huenda hayajaonekana moja kwa moja katika deni rasmi la taifa. Mojawapo ya hoja hizo ni kutumia mapato ya baadaye ya ushuru wa matengenezo ya barabara kama dhamana ya kufadhili miradi au kulipa wakandarasi. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pia limekuwa likihimiza kutambuliwa kwa aina mbalimbali za madeni na wajibu wa kifedha yanayotokana na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Rais Ruto anasema suluhisho lake ni kuanzisha Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu, inayolenga kuvutia uwekezaji kutoka kwa sekta binafsi, hazina ya pensheni na taasisi za maendeleo badala ya kutegemea mikopo ya serikali pekee. Lakini mafanikio ya mpango huo yatategemea uwazi, usimamizi na uwezo wa miradi hiyo kuzalisha mapato bila kuwaachia walipakodi mzigo wa siri wa kifedha.
TAHARUKI ilitanda kwa muda mfupi eneo la Makutano, Meru wakati mwanamume anayeaminika kuwa afisa wa polisi aliporusha gesi ya kutoa machozi kwa mkutano wa Linda Mwananchi. Hata hivyo umati ulizima mkebe wenye gesi hiyo na mkutano ukaendelea.

KAMATI ya wataalamu walioteuliwa kuandaa mwongozo wa kisiasa na manifesto ya pamoja ya vyama vya UDA na ODM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 imeanza kazi rasmi huku ikipanga kufanya mashauriano kitaifa yatakayohusisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini. Mkurugenzi Mkuu wa UDA, Nicodemus Bore, ambaye ni mwanachama wa kamati hiyo alisema wataalamu hao tayari wamefanya mkutano wao wa kwanza na sasa wanajipanga katika makundi ya kiufundi ili kuanza kazi ya kuandaa msingi wa ushirikiano wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Oginga. “Tayari tumekutana na kufanya kikao chetu cha kwanza. Sasa tunaandaa mikutano mingine na kupanga jinsi ya kufanya kazi kupitia makundi ya kiufundi. Kazi imeanza rasmi,” alisema Bore. Alisema wananchi wanapaswa kutarajia mashauriano makubwa kote nchini ili kuhakikisha maoni ya makundi mbalimbali yanazingatiwa kabla ya mapendekezo ya mwisho kuandaliwa. Kwa mujibu wa Bore, hatua ya kwanza itakuwa kupitia upya manifesto za UDA na ODM za 2022, kutathmini utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na kubaini maeneo yaliyofanikiwa na yale yanayohitaji kuboreshwa. “Tunataka kuhakikisha ahadi tulizotoa 2022 zinatimizwa kikamilifu,” alisema. Kamati hiyo ina wanachama 12, ambapo kila chama kimetoa wataalamu watano huku Bore na Mkurugenzi Mkuu wa ODM Oduor Ong’wen wakihudumu kama wanachama wa moja kwa moja. Kwa upande wa ODM, wanachama ni Isaac Wanuge, Maryam Abdullahi Mbaruk, Profesa Leonida Kerubo Omosa, Carey Orege na Profesa Bernard Muok. UDA imewakilishwa na Dkt Emmanuel Nzai, Dkt Daniel Mwai, Bramwel Simiyu, Mohammed Hassan na Dkt Cecilia Ng’etich. Orege, ambaye ni mwenyekiti wa muda wa kamati hiyo, alisema wamemaliza mkutano wa utangulizi na sasa wanasubiri mwongozo rasmi wa majukumu yao kabla ya kuandaa ratiba kamili ya kazi. Muundo wa kamati hiyo unaonyesha kuwa UDA na ODM zimeweka mkazo katika badala ya umaarufu wa kisiasa. Wanachama wake wanatoka katika sekta za uchumi, afya, miundombinu, elimu, sayansi, maendeleo, utawala wa umma na uongozi wa vyama vya siasa. Changamoto kubwa inayowakabili wataalamu hao ni kuoanisha sera za vyama viwili ambavyo vilikuwa katika pande tofauti za kisiasa katika uchaguzi uliopita na kuandaa ajenda moja itakayowavutia wapigakura. Bore alisema kamati hiyo itachunguza mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizobaki na maeneo ambayo serikali ingeweza kufanya vizuri zaidi. “Hatutaki kuonekana tunaishi katika ulimwengu wa njozi. Tunataka matarajio ya wananchi kutoka maeneo yote ya nchi yawe sehemu ya manifesto,” alisema. Rais Ruto alitangaza kuundwa kwa kamati hiyo baada ya mkutano wa viongozi wa UDA na ODM, akisema kazi yao haitakuwa tu kuandika manifesto ya kampeni bali pia kuweka msingi wa maono ya maendeleo ya taifa.

ALIYEKUWA Waziri Moses Kuria ameibua mjadala kuhusu uchaguzi wa urais wa 2027 baada ya kutoa kauli tata kuhusu atakayeapishwa kuwa rais baada ya uchaguzi huo. Kuria, ambaye ni kiongozi wa Chama Cha Kazi (CCK), aliandika kwenye mitandao ya kijamii Jumatano usiku, Agosti 26, 2026, akionekana kudokeza kuwa tayari anajua kitakachotokea katika uchaguzi huo. “2027: Sijui nani atashinda. Lakini najua nani ataapishwa,” Kuria aliandika. Katika kauli hiyo fupi hakutaja jina la mtu anayetarajia ataapishwa kuwa rais, hali iliyowaacha wafuasi wake wakikisia maana aliyokusudia. Kuria ameendelea kumuunga mkono Rais William Ruto hata baada ya kuondoka serikalini. Tangu ajiuzulu kama mshauri wa Rais Ruto, Kuria amerejea kikamilifu katika siasa akitoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa. Alitoa kauli hiyo siku ambayo aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua alitoa madai kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa 2027. Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha upinzani cha DCP, alishutumu utawala wa Rais Ruto na IEBC kwa kuweka mazingira ya kuvuruga uchaguzi wa 2027. Gachagua alielekeza wasiwasi wake hasa kwenye ununuzi wa teknolojia ya uchaguzi, akidai mchakato huo unaweza kutumiwa kuathiri matokeo ya uchaguzi. Pia alimuonya Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon kusimama na Wakenya, akisema jaribio lolote la kuvuruga uchaguzi litakuwa na madhara makubwa. Aidha, alidai kushindwa kwa Ruto 2027 kutakuwa kwa kishindo kiasi kwamba hakutaweza kufichwa kupitia kuvuruga mchakato wa uchaguzi. Hata hivyo, madai hayo yamepuuzwa na maafisa wakuu wa serikali. Katika hali hiyo, kauli tata ya Kuria imeongeza mwelekeo mpya katika mjadala wa kisiasa unaozidi kushika kasi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

KAGERA: Serikali imezitaka shule nchini kuweka kipaumbele kwenye mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wanafunzi wao ili kwenda sanjari na dunia ya sasa ya utandawazi na teknolojia inayokua kwa kasi. Serikali imeeleza kwa dunia ya sasa teknolojia inakwenda kwa kasi kubwa hivyo shule zinapaswa kuwa na miundombinu bora ya wanafunzi wake kujifunza…

By Godwin Oritse APM Terminals Apapa, Nigeria’s largest container terminal, recorded a 6 per cent increase in export volumes in the first half of 2026, re-enforcing its continued efforts to boost the country’s non-oil exports and enhance Nigerian businesses’ access to international markets. Terminal Managing Director of APM Terminals Apapa, Kamal Alhraishat, attributed the growth […]

By Godwin Oritse APM Terminals Apapa, Nigeria’s largest container terminal, recorded a six per cent increase in export volumes in the first half of 2026, reinforcing its efforts to support the country’s non-oil exports and improve Nigerian businesses’ access to international markets. The Terminal Managing Director, Kamal Alhraishat, attributed the growth to the resilience of […]

JUHUDI za kuwaokoa waathiriwa wa mafuriko makubwa katika mpaka wa Nepal na Tibet nchini China zilirejelewa jana, baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na hofu ya kutokea kwa mafuriko tena kutokana na kuyeyuka kwa barafu mlimani. Idadi ya waliofariki katika mkasa huo imefikia 633, huku karibu watu 3,000 wakiripotiwa kutoweka. Polisi nchini Nepal ilisema jana kuwa watu 626 wamefariki kutokana na mafuriko hayo, huku Mamlaka ya Kudhibiti Majanga ikiripoti kuwa watu 2,426 bado hawajulikani waliko. Kati ya waliotoweka nchini Nepal, 517 ni raia wa kigeni, ambao huenda ni watalii au wafanyakazi kutoka mataifa mengine. Nchini China, mamlaka ilisema watu wasiopungua saba wamefariki katika eneo la Tibet, huku wengine 554 wakiripotiwa kutoweka. Kutokana na ukubwa wa janga hilo, serikali ya Nepal iliomba msaada maalumu kutoka India na China ili kuongeza uwezo wa operesheni za uokoaji. Timu kutoka mataifa hayo, zikiwemo wataalamu wa uokoaji zilitarajiwa kuwasili jana. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Nepal, Lok Bahadur Poudel Chhetri, alisema uamuzi huo ulifanywa kwa dharura kutokana na maisha ya watu kuwa hatarini. “Maisha yako hatarini na hali ni ya dharura sana. Hapo awali Nepal haikutaka msaada kwa sababu haikutaka mkanganyiko unaoweza kutokea wakati timu kubwa zinaelekezwa katika maeneo tofauti,” alisema Chhetri. Awali, Nepal ilikataa msaada wa kimataifa kwa hofu kuwa kuwasili kwa vikosi vingi vya uokoaji kungeleta mkanganyiko katika operesheni hizo. Mkasa huo ulianza Jumatano asubuhi baada ya sehemu ya barafu katika milima ya Himalaya kuyeyuka kutoka urefu wa takriban mita 5,200. Barafu hiyo ilishuka kwa kasi kwa zaidi ya mita 1,200, ikikusanya mawe na vifusi kabla ya kutumbukia katika Mto Lende. Mafuriko yaliyofuata ulisomba maeneo ya Rasuwa, Nuwakot na Dhading nchini Nepal, na kusababisha kina cha Mto Trishuli kupanda kwa mita tisa ndani ya dakika 30. Mto Trishuli uliongezeka kina kwa takriban mita tisa ndani ya dakika 30, na kusababisha uharibifu mkubwa katika maeneo yaliyo karibu. Uchunguzi wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Amerika, USGS, ulidai kuwa tetemeko la ardhi ndilo lililosababisha mkasa huo. Hata hivyo, uchunguzi wa baadaye ulionyesha kuwa mawimbi ya mtikisiko yaliyorekodiwa yalitokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na kuyeyuka kwa barafu. Waokoaji jana waliendelea na shughuli za kuwatafuta manusura na waliotoweka, huku matumaini yakipungua kutokana na muda uliopita tangu mkasa huo utokee. Wakazi katika maeneo yaliyo hatarini wameonywa kuwa tayari kwa uokoaji. Nepal hupokea mvua nyingi wakati wa msimu wa monsoon, lakini wataalamu wameonya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza hatari ya kuyeyuka kwa barafu na kutokea kwa mafuriko makubwa.

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 unatarajiwa kuwa ghali zaidi katika historia ya Kenya, huku makadirio yakionyesha kuwa serikali, vyama vya kisiasa na wagombea watatumia zaidi ya Sh272 bilioni katika mchakato mzima wa uchaguzi. Kiasi hicho kinajumuisha bajeti ya Sh74.8 bilioni ambayo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekadiria kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo pamoja na takriban Sh197.35 bilioni ambazo wagombea wanaweza kutumia katika kampeni zao iwapo watazingatia viwango vya matumizi vilivyowekwa na tume hiyo. Kwa miaka mingi, uchaguzi nchini Kenya umejulikana kwa nyimbo, kauli mbiu na kampeni za kuvutia. Hata hivyo, matumizi makubwa ya fedha yameibua maswali kuhusu vipaumbele vya taifa wakati sekta muhimu kama afya, elimu na kilimo zinaendelea kukabiliwa na changamoto za ufadhili. Kiasi cha Sh272 bilioni ni zaidi ya nusu ya fedha zilizotumiwa kuendesha kaunti zote 47 nchini katika mwaka wa kifedha uliomalizika Juni 2025, ambazo zilikuwa Sh470.7 bilioni. Pia fedha hizo zinaweza kulipa kikamilifu madeni ambayo serikali za kaunti zinadaiwa ya zaidi ya Sh156 bilioni. Kwa mtazamo mwingine, kiasi hicho ni kikubwa kuliko bajeti za baadhi ya sekta muhimu katika uchumi. Kwa mfano, sekta ya afya ilitengewa Sh177.2 bilioni, elimu ya juu Sh163.9 bilioni na elimu ya msingi Sh136.6 bilioni katika bajeti ya hivi karibuni ya serikali. IEBC inasema gharama kubwa ya uchaguzi inatokana na teknolojia ya uchaguzi, vifaa vya kutambua wapigakura, mifumo ya kutuma matokeo, karatasi za kura zenye vipengele vya usalama pamoja na ongezeko la idadi ya wapigakura. Tume hiyo inalenga kusajili wapigakura milioni 28.5 kufikia mwaka 2027, ikilinganishwa na milioni 22.1 waliopiga kura mwaka 2022. Ongezeko hilo litahitaji vituo vya kupigia kura 55,393 kutoka vituo 46,229 vilivyotumika mwaka 2022. Kwa upande wa wagombeaji, viwango vipya vya matumizi ya kampeni vinaonyesha kuwa kinyang’anyiro cha kisiasa kitahitaji fedha nyingi zaidi. Mgombea urais ataruhusiwa kutumia hadi Sh6.1 bilioni, kutoka Sh4.7 bilioni mwaka 2022. Wagombeaji wa ugavana, useneta, ubunge na uwakilishi wa wanawake pia watatumia mabilioni ya fedha katika kampeni zao. Mbunge wa Likuyani, Innocent Mugabe, anasema kiwango cha matumizi kilichowekwa na IEBC ni cha chini ikilinganisha na hali halisi ya kampeni. “Nilitumia takriban Sh50 milioni mwaka 2022. Ukiwa na nia ya kushinda, lazima utumie fedha zaidi,” alisema. Kwa mujibu wa IEBC, mipaka ya matumizi ya kampeni inalenga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki, uwazi na uwajibikaji, na kwamba matokeo ya uchaguzi yanaamuliwa na wapigakura badala ya nguvu ya fedha. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wamehoji jinsi sheria hizo zitakavyotekelezwa, wakisema bado Kenya ina mfumo mkubwa wa matumizi ya fedha taslimu ambao ni vigumu kufuatilia. Iwapo makadirio ya sasa yatatimia, uchaguzi wa 2027 utaweka rekodi mpya kama uchaguzi wa gharama kubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Kenya.

…as new spending commitments hit N30.6trn …Raises fresh concerns over $5bn Abu Dhabi facility ….Says Nigeria remains heavily dependent on borrowing despite subsidy removal ‘How Naira lost 29% of value in four years’ By Nnamdi Ojiego The Federal Government’s economic reform figures have raised a fresh fiscal question, with former President of the Nigerian Association […]

KUJITOSA kwa Raila Junior katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Kibra, Nairobi, kumeanza kuzua pingamizi miongoni mwa baadhi ya wawaniaji wa ODM, huku mwana huyo wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga akisaka kiti hicho 2027. Kibra kwa miongo imekuwa ngome ya kisiasa ya familia ya Odinga. Marehemu Raila aliwakilisha eneo hilo bungeni kuanzia 1992 hadi 2013, wakati Kibra ilikuwa sehemu ya Lang’ata. Kila mara nchi ilipokabiliwa na maamuzi magumu ya kisiasa, Raila alirejea Kibra kutoa mwelekeo ambao baadaye ulikumbatiwa na maeneo mengine nchini. Mnamo Novemba 30, 2009 wakati wa mvutano kuhusu uamuzi wa kufurusha watu kutoka msitu wa Mau, Raila alitangaza hadharani kwamba alikuwa tayari kurejea Kibra akapike mandazi iwapo suala hilo lingemgharimu kisiasa. Kuingia kwa Raila Junior katika kivumbi hicho kumezua ushindani mkali wa kisiasa kati yake, mbunge wa sasa wa Kibra Peter Orero na aliyekuwa mbunge wa hapo Imran Okoth. Junior amekuwa akishiriki miradi ya kijamii na kukutana na makundi mbalimbali huku akiweka misingi ya kampeni zake kuelekea 2027. “Kibra ilikuwa ngome ya kisiasa ya babangu, na kama familia tumekuwa na safari ndefu pamoja na watu wa eneo hili. Nikichaguliwa nitamakinikia sana elimu kwa kuhakikisha basari zinapatikana ili pasiwe na mtoto anayekosa fursa ya kupata elimu,” mwana huyo mdogo wa Raila alisema katika mahojiano na Jamvi. “Najua baadhi ya sekta kama afya na maji zimekabidhiwa serikali za kaunti, lakini nitafanya kila niwezalo kuhakikisha huduma hizo zinafikia watu wa Kibra. Tutazingatia sana kuboresha maisha ya wakazi kwa kila njia iwezekanavyo,” akaongeza. Junior pia alifichua kuwa kwa miaka mingi alikuwa miongoni mwa wandani waliompangia babake mikakati ya kisiasa huko Kibra. Wiki hii mama yake, Ida Odinga, alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, alitangaza kwamba amempa Raila Junior baraka za kutimiza ndoto zake za kisiasa, ikiwemo azma yake ya kuwania ubunge wa Kibra. “Nyinyi watu wa Kibra mmeamua na sina chaguo jingine. Namkabidhi mwanangu mikononi mwenu. Viongozi mlio hapa mtunze, mfundishe na mpe mwongozo. Wengi wenu mlianza siasa pamoja na Baba. Mwonyesheni njia,” akasema Mama Ida. Alisisitiza kuwa siasa za Junior zinapaswa kuwa safi na zisizo na matusi wala vurugu, akisema Kibra ilikuwa msingi wa safari ya kisiasa ya familia ya Odinga. “Washawishi watu kwa maneno yako na uwaambie kile unachoweza kuwafanyia,” akasema. Hata hivyo, mbunge wa sasa Orero anadai Junior anasukumwa na baadhi ya wawakilishi wadi (MCAs) maalum ambao hawana ushawishi wa kisiasa Kibra. Alisisitiza yuko tayari kukutana na Junior kwenye debe. “Baadhi ya wawakilishi wadi maalum wanaomsukuma wamepoteza uchaguzi mara nne, na wanalenga maslahi yao binafsi. Hata hivyo, kazi yangu Kibra iko wazi kwa kila mtu kuona. Sina mpinzani. Aje tushindane, nami nitamshinda,” akahoji Orero. Alishangaa kwa nini Junior amejitosa kwenye kinyang’anyiro hicho ilhali dada yake, Winnie Odinga, aliwahi kukinyemelea kabla kujiondoa na kuelekeza nguvu zake katika kivumbi cha useneta Nairobi. Orero alisema licha ya kuwa karibu na familia ya Odinga hajazungumza na Mama Ida kuhusu azma ya Junior. “Kuna nini cha kuzungumza? Junior ana haki yake ya kidemokrasia na sitaki kuwadharau au kuonekana niko kwenye vita nao. Waache watu waamue,” akasema mbunge huyo. Kwa upande wake aliyekuwa mbunge Imran Okoth ametishia kuondoka ODM na kuwania kiti hicho kama mgombea huru iwapo chama hakitaendesha uteuzi wa haki na huru. “Junior yuko huru kuja kuwania lakini ajue sisi ni wanachama wa ODM na tunasisitiza kusiwe na mapendeleo yoyote. Orero, Junior na mimi tushindane kwa haki, na atakayeshinda apewe tiketi ya ODM,” akahoji.

VIONGOZI wa upinzani Jumamosi walivamia Taveta, eneo linalotajwa kuwa ngome ya kisiasa ya Rais William Ruto, wakitumia mzozo wa ardhi na madai ya kufurushwa kwa wakazi kuishambulia serikali. Msafara huo uliongozwa na kiongozi wa Wiper Patriotic Front, Kalonzo Musyoka, Ulifika Mkocheni, karibu na shamba la Rais Ruto la Eldoro, ambako familia kadhaa zilizofurushwa takriban mwaka mmoja uliopita bado zinaishi katika kambi. Viongozi hao walishutumu serikali kwa madai ya kutumia maafisa wakuu kuwaondoa wananchi kwenye ardhi na kuwaacha bila makao. Katika msafara huo walikuwa kiongozi wa Democratic Party, Justin Muturi, kiongozi wa DAP-Kenya, Eugene Wamalwa, aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma, Aisha Jumwa, Mbunge wa Wundanyi ,Danson Mwashako na zaidi ya wabunge 20. Bw Musyoka aligeuza mzozo huo kuwa shambulizi kali dhidi ya Rais Ruto, akidai Rais alinunua takriban ekari 2,000 kutoka kwa mfanyabiashara Basil Criticos lakini baadaye akaongeza eneo hilo, hatua aliyosema imewaacha wenyeji bila makao. “Rais aliuziwa ekari 2,000 pekee na Basil Criticos lakini ameongeza, na kuwaacha wenyeji bila makao,” alisema Bw Musyoka. Pia alikosoa matumizi ya fedha za umma kujenga barabara zinazoelekea katika shamba la Rais, akisema rasilimali za serikali zinafaa kuwanufaisha wananchi. “Leo tumeshangaa kuona Ikulu nyingine ikijengwa Taveta kwa gharama ya watu wa Taveta,” alisema. Bw Muturi naye alitoa madai mazito akisema alipokuwa Mwanasheria Mkuu aliidhinisha stakabadhi za kuharakisha ujenzi wa barabara Taveta bila kujua kuwa zingemfaidi Rais moja kwa moja. “Ningejua stakabadhi nilizokuwa nikitia saini zingemfaidi Rais moja kwa moja, ningechukua hatua tofauti,” alisema. Wakati huo huo, wakazi wa Jipe wamekuwa wakitaka ua unaozunguka ardhi yenye mzozo kuondolewa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi uliowaunga mkono. Wakazi hao wanadai ekari 3,000 zilitolewa kwa mpango wa Jipe-Taveta Settlement kuwawezesha maskwota kupata ardhi. Sasa wanataka serikali kutekeleza uamuzi wa mahakama, kuwarejesha waliofurushwa na kuwapa hatimiliki ili kumaliza mzozo huo wa miaka mingi. Kalonzo alimlaumu rais kwa kushindwa kukabili gharama ya maisha na kuongezeka kwa umaskini nchini. Bw Musyoka alisema serikali ya Kenya Kwanza imekuwa ikitumia vitisho, pesa na ahadi za kisiasa kuwavutia viongozi wa upinzani kwa lengo la kuimarisha nafasi ya Rais Ruto kuelekea uchaguzi ujao. Aliwashutumu viongozi wa serikali kwa kujaribu kudhoofisha upinzani kwa kuwashawishi wabunge, maseneta na magavana kujiunga na Kenya Kwanza. Bw Musyoka alimlenga Mbunge wa Taveta John Bwire, ambaye alisema alimsaidia kushinda uchaguzi wa 2022 lakini sasa anafanya kazi kwa karibu na chama tawala cha UDA. “Ninawashukuru viongozi wangu wa Wiper walioamua kutojiunga na Kenya Kwanza. Chama tawala kijue kuwa Wiper bado ni chama imara. Inasikitisha kumuona mbunge wangu wa Taveta John Bwire, ambaye nilimpigia kampeni, sasa akiwa msemaji wa UDA hapa,” alisema.

MZOZO kuhusu kifo cha Rosemary Chemutai Koech, meneja mkuu wa Benki ya KCB, na ‘umiliki’ wa mwili wake umechukua mkondo mpya baada ya familia yake kumzika usiku wa kuamkia Jumamosi licha ya amri ya mahakama iliyositisha mazishi hayo kwa muda. Rosemary, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa data KCB, alifariki Agosti 21 akiwa na umri wa miaka 40 katika nyumba yake ya Ngong, Kaunti ya Kajiado. Kifo chake kilitokea alipokuwa amejitenga na mumewe, Kevin Migwe Kimwatu, kufuatia matatizo ya ndoa. Mapema Ijumaa, Mahakama ya Milimani jijini Nairobi iliamuru kwa muda mazishi yake kufanyika na ikazuia Lee Funeral Home kutoa mwili huo hadi kesi iliyowasilishwa na mumewe isikizwe na kuamuliwa. Hakimu Mkuu Mwandamizi Agnes Mwangi alitoa amri ya kuzuia wanafamilia, Lee Funeral Home na KCB kuhamisha mwili wa marehemu. Pia alisema mazishi yasifanyike bila idhini ya mume wa marehemu. Hata hivyo, mazishi yalifanyika saa saba na nusu usiku katika kijiji cha Chepseon, eneo la Kipkelion Mashariki, Kaunti ya Kericho. Akizungumza na waombolezaji Jumamosi, mwenyekiti wa ukoo Samwel Keter alisema familia iliamua kufanya hivyo kwa kuzingatia mila za Kalenjin. “Yanayosambazwa mitandaoni si ya kweli. Binti yetu alifariki na kwa mujibu wa utamaduni wetu, mtu wa aina hiyo hapaswi kukaa bila kuzikwa kwa zaidi ya siku tatu au nne. Pia, baada ya uchunguzi wa maiti kufanyika, mazishi yanapaswa kufanyika ndani ya siku mbili. Tulifanya tulichofanya kwa kuzingatia mila zetu ili tukio kama hilo lisijirudie,” alisema Keter. Mwanachama wa Shirika la Koo za Jamii ya Kipsigis, Joseph Towett Kalyasoi, alisema si jambo la ajabu kwa jamii hiyo kufanya mazishi baada ya jua kutua. “Zamani, miili ilikuwa ikizikwa usiku miongoni mwa jamii ya Kipsigis, ndiyo maana hadi leo baadhi ya shughuli za mwisho za mazishi hufanyika jioni sana. Hii ni mila ya muda mrefu,” alisema. Towett aliongeza kuwa wazazi wa mwanamke aliyeolewa wakiamua kumzika kutokana na tofauti kati yake na mumewe, basi wanapaswa kurejesha mahari iliyolipwa wakati wa ndoa. Wakati huo huo, imebainika kuwa mwili wa Rosemary ulihamishwa kutoka Nairobi kwenda Kericho siku tatu kabla ya mazishi huku mvutano ukiendelea kati ya wazazi wake na mumewe. Chanzo cha familia kilichozungumza kwa siri kilisema hata baadhi ya wanachama wa kamati ya mazishi hawakujua mahali mwili ulikokuwa hadi ulipoondolewa mochari. Ulinzi mkali wa polisi katika makazi ya familia ulivutia hisia za majirani huku ndugu wa karibu wakisimamia taratibu za mazishi. Kwa upande wake, Kimwatu alikuwa ameenda mahakamani kuomba wazazi wa marehemu, Paul Kipkorir Koech na Beatrice Koech, pamoja na dadake Judy Koech-Oyamo na KCB, wazuiwe kuendelea na mipango ya mazishi. Alidai kuwa alikuwa ametengwa katika maandalizi ya mazishi licha ya kuwa mume halali wa Rosemary. Stakabadhi za mahakama zinaonyesha kuwa wawili hao walifunga ndoa katika Kanisa Katoliki la St Austin mjini Nairobi mnamo Agosti 24, 2013 na walibarikiwa kupata watoto wanne. Kimwatu alikiri kuwa ndoa yao ilikuwa na changamoto lakini akasema walikuwa katika juhudi za kumaliza tofauti zao na waliendelea kuwasiliana mara kwa mara hadi siku ya kifo chake. “Ndoa yetu kwa ujumla ilikuwa ya upendo, furaha na ushirikiano. Kama ndoa nyingine zote, ilikuwa na changamoto zake, lakini hazikuwahi kufikia kiwango cha kuondoa upendo na furaha iliyokuwepo kati yetu,” alisema katika stakabadhi za mahakama. Aliongeza kuwa walikuwa wameachana kwa muda wa miezi minne pekee na kwamba kabla ya kifo chake, Rosemary alikuwa amekubali kurejea nyumbani kwa familia yao. Kimwatu alisema kuwa kama mume wa kisheria alikuwa na haki ya kupanga mazishi ya mkewe na alikusudia kumzika katika makazi ya familia yao huko Matasia, Ngong, Kaunti ya Kajiado. Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani Agosti 31 huku maswali yakisalia kuhusu utekelezaji wa amri ya mahakama na uhalali wa mazishi yaliyofanyika Kericho.

“Let justice be done, though the heavens fall” – Lord Mansfield, 1705-1793 “Once to every man and nation comes the moment to decide; in the strife of truth with falsehood, for the good or evil side” – James Russell Lowell, 1819-1891 Until now, there was no reason to raise the question about substantial justice untainted with […]

Katika wakati ambapo migogoro kati ya binadamu na wanyamapori inaongezeka, Kenya imeandaa mkutano mkubwa wa kubadilishana uzoefu wa uhifadhi wa bioanuwai kati ya China na Afrika, ukiwa na lengo la kuimarisha juhudi za kulinda wanyamapori, mazingira na jamii zinazotegemea maliasili. Mkutano huo wa China-Africa Biodiversity Conservation Exchange and Training, uliofanyika Nairobi sambamba na maonyesho ya kimataifa ya “Eagle City”, uliwaleta pamoja wataalamu wa uhifadhi, maafisa wa serikali, watafiti na mashirika ya kijamii kutoka China, Kenya na Tanzania. Kenya na Tanzania zinashirikiana katika maeneo kadhaa ya uhifadhi wa bioanuwai, jambo linaloruhusu wanyamapori kuhama kwa uhuru kupitia njia zao za asili katika kaunti za Kajiado na Narok. Washiriki wa mkutano huo walijadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka dhidi ya bioanuwai. Miongoni mwa masuala yaliyopewa kipaumbele ni uhifadhi unaoshirikisha jamii, matumizi ya teknolojia kulinda wanyamapori na elimu ya mazingira kwa vijana. Mwenyekiti wa Adept Conservation Network, Eston Murithim, alisema jamii za wenyeji zina mchango mkubwa katika kulinda misitu, mito na maeneo tengefu. Alisema shirika hilo hushirikiana na jamii kupitia mafunzo ya ujuzi, doria za mazingira, uzalishaji wa miche ya miti na programu za uhamasishaji wa mazingira. “Mbinu hii inasaidia kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori huku ikikuza kuishi kwa amani kati ya jamii na wanyama hao,” alisema Murithim. Mwanzilishi wa Joy and Hope for Rural Community Foundation nchini Tanzania, Zakayo Lairumbe Kipuyo, alieleza kuwa taasisi yake imekuwa ikihusika katika urejeshaji wa misitu, ulinzi wa njia za kupita wanyamapori na vyanzo vya maji katika eneo la Arusha. Alisema jamii pia zinasaidiwa kupata njia mbadala za kujipatia riziki zisizoathiri mazingira. Kwa upande wake, mtafiti mwandamizi wa Huduma ya Wanyamapori Kenya (KWS), Dkt Duncan Aminga, aliwasilisha mfumo wa uhifadhi wa simba unaotumika Maasai Mara ambapo simba huvalishwa vifaa vya GPS kufuatilia mienendo yao. Teknolojia hiyo husaidia kutoa tahadhari mapema kwa jamii wanapokaribia makazi ya watu, hivyo kupunguza mashambulizi dhidi ya mifugo na mauaji ya kulipiza kisasi dhidi ya simba. Mtaalamu wa faru na duma katika Hifadhi ya Taifa ya Mara, Stephen Kenta, alisema vifaa vya kisasa kama kamera za miale ya joto, vitambulisho vya kielektroniki na kituo cha kisasa cha usimamizi vinatumika kulinda faru. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mazingira ya Chongqing nchini China, Liu Ming, alisema China imepiga hatua kubwa katika uhifadhi wa bioanuwai kupitia ufuatiliaji wa viumbe, urejeshaji wa makazi yao na ushiriki wa umma. Alitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya China na Afrika kupitia kubadilishana utaalamu, teknolojia na mafunzo ya wataalamu wa uhifadhi. Katika mkutano huo, vifaa vya kisasa vya kufuatilia wanyamapori, vikiwemo kamera za infrared na vifaa vya kutambua sauti za ndege, vilitolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara na Adept Conservation Network. Mkutano huo umefanyika wakati mamlaka nchini Kenya zikichunguza vifo vya tembo 18 katika mfumo ikolojia wa Amboseli kati ya Juni na Julai mwaka huu. Wakulima wanne wamekamatwa kuhusiana na madai ya kuhusika katika sumu iliyosababisha vifo hivyo.

Miaka 16 baada ya Kenya kupitisha Katiba ya 2010, mizozo kati ya magavana na Seneti imeibua maswali kuhusu mipaka ya ugatuzi. Swali kuu ni moja: Serikali za kaunti zinawezaje kuwa huru huku zikimulikwa kuhusu matumizi ya pesa za umma? Mzozo mkuu ulizuka Februari 2026 baada ya baadhi ya magavana kususia wito wa Seneti. Magavana walidai baadhi ya maseneta walikuwa wakiwaitisha mamilioni ya pesa ili kuwapendelea katika masuala ya ukaguzi wa hesabu. Maseneta walipinga madai hayo. Mzozo huo ulitatuliwa baadaye, lakini uliweka wazi mvutano kati ya uhuru wa kaunti na mamlaka ya Seneti ya kusimamia matumizi ya fedha za umma. Magavana zaidi ya 30 walikutana Kilifi baada ya magavana saba kukosa kufika mbele ya kamati mbili za Seneti Februari 9. Magavana wa Nandi Stephen Sang na Siaya James Orengo walikuwa wameitwa mbele ya Kamati ya Seneti ya Hesabu za Kaunti. Magavana wa Laikipia Joshua Irungu, Muthomi Njuki wa Tharaka-Nithi, Irungu Kang’ata wa Murang’a, Issa Timamy wa Lamu na Cecily Mbarire wa Embu walitarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Uwekezaji wa Kaunti na Fedha Maalum. Kamati hizo zilikuwa zikichunguza ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Nancy Gathungu, za mwaka wa fedha 2024/25. Magavana walidai baadhi ya maseneta walikuwa wakiwaitisha kati ya Sh9 milioni na Sh12 milioni ili wapate msaada katika masuala ya ukaguzi. Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ahmed Abdullahi alisema magavana hawapingi uwajibikaji. Alisema walikuwa wakipinga matumizi mabaya ya mamlaka ya Seneti. “Imetosha. Ikiwa tutalazimika kurudi kortini kutafuta tafsiri ya maana ya usimamizi huu na magavana kufika mbele ya kamati, tutafanya hivyo,” alisema. Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang alipinga madai hayo. Aliwataka magavana kuwasilisha ushahidi katika taasisi husika. Alisema Katiba imepatia Seneti mamlaka ya kuchunguza ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kumwita mtu yeyote kutoa ushahidi. “Uwajibikaji si hisani kwa Seneti; ni wajibu kwa umma,” alisema. Kifungu cha 96 cha Katiba kinapatia Seneti jukumu la kumulika kaunti na kulinda ugatuzi. Seneti pia hushiriki katika kutunga sheria zinazohusu kaunti na kusimamia matumizi ya fedha zinazotumwa kwa serikali za kaunti. Lakini ugatuzi hauzuii uwajibikaji. Kifungu cha 174 kinataja matumizi ya mamlaka kwa uwajibikaji, ushiriki wa wananchi na kujitawala kuwa miongoni mwa malengo ya ugatuzi. Seneti pia ina mamlaka ya kumwita mtu kutoa taarifa au ushahidi chini ya Kifungu cha 125. Hata hivyo, Kifungu cha 189 kinataka Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti kushirikiana na kuheshimu mamlaka ya kila upande. Hivyo, kaunti haziwezi kutumia uhuru wao kukwepa uchunguzi halali. Vilevile, Seneti haiwezi kutumia usimamizi kuingilia majukumu yaliyopewa kaunti. Mvutano kama huo ulijitokeza pia wakati Seneti ilipochunguza mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali ya Kitaifa na Kaunti ya Nairobi. Mkataba huo ulitiwa saini Februari 2026. Kamati ya Seneti ilipendekeza usitishwe kwa muda, ikisema baadhi ya vipengele vilionekana kuhamisha majukumu ya kaunti badala ya kuwa ushirikiano. Gavana Johnson Sakaja alitetea mkataba huo. Alisema Nairobi ina majukumu ya kitaifa na kimataifa ambayo yanahitaji usaidizi mkubwa kutoka Serikali ya Kitaifa. Mizozo hii inaonyesha changamoto inayoendelea katika mfumo wa ugatuzi. Magavana wanataka uhuru wa kaunti uheshimiwe. Seneti inataka kuhakikisha pesa za umma zinatumika ipasavyo.

SARE mpya ya polisi imezinduliwa huku kukiwa na maswali kuhusu zabuni inayokadiriwa kugharimu hadi Sh3 bilioni. Rais William Ruto alizindua sare hiyo jana katika hafla ya kuhitimu kwa maafisa wapya katika Chuo cha Kitaifa cha Polisi Kiganjo, Nyeri. Sare hiyo mpya ina shati au blauzi ya samawati hafifu na suruali ya samawati iliyokolea. Takriban maafisa 60,000 wa zamu ya kawaida wanatarajiwa kuvaa sare hiyo. Kulingana na taarifa zilizomo katika Idara ya Polisi, seti moja ya sare inakadiriwa kugharimu Sh25,000. Seti hiyo inajumuisha shati au blauzi, suruali, koti, fulana, kofia, sweta, soksi, mkanda na koti la mvua. Sare ya sherehe inakadiriwa kugharimu Sh30,000, bila kujumuisha viatu vinavyogharimu kati ya Sh3,000 na Sh5,000 kwa jozi. Hata hivyo, Idara ya Polisi imekuwa kimya kuhusu kampuni zilizoshinda zabuni na gharama kamili ya mkataba. Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja hakujibu maswali kuhusu mshindi wa zabuni hiyo. Vyanzo vimedai kuwa zabuni hiyo iligawanywa katika sehemu kadhaa na kila sehemu kupewa kampuni tofauti. Miongoni mwa kampuni zilizotajwa ni Nalitex Ltd ya Nairobi, ambayo rekodi za Huduma ya Usajili wa Biashara zinaonyesha inamilikiwa na Selpha Chesimi Temoi. Kamati ya Bunge kuhusu Utawala na Usalama wa Ndani pia haikushirikishwa katika mchakato huo. Wabunge wa kamati hiyo walisema walifahamu kuhusu sare hizo walipotembelea Kiganjo Agosti 21. Mmoja wao alisema kamati inapanga kumwita IG Kanja na maafisa wake kueleza kuhusu zabuni hiyo. Sare mpya inalenga pia kuongeza uwajibikaji. Majina ya maafisa na nambari zao za utumishi zimeshonwa moja kwa moja kwenye sare na haziwezi kuondolewa. Sare ya samawati iliyotumika tangu 2018 ilikosolewa kwa rangi yake, ubora wa kitambaa na kutoshirikisha maafisa wa ngazi za chini katika mchakato wa kuichagua. Sare mpya ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwaka 2023 na aliyekuwa Inspekta Jenerali Japhet Koome. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amekosoa mabadiliko hayo, akisema serikali inapaswa kuangazia mageuzi ya polisi badala ya mabadiliko ya sare. “Tusidanganywe na vitu vinavyong’aa. Tunataka mageuzi ya polisi, si sare,” alisema Sifuna.

DODOMA: MEMBERS of Parliament yesterday unanimously endorsed Deogratius Ndejembi’s nomination as VicePresident, praising the former Energy Minister for his integrity, humility, discipline and leadership experience. Mr Ndejembi secured all 324 votes cast in the National Assembly in Dodoma, becoming the youngest person to hold the country’s secondhighest office. Contributing to the motion to approve his…

ABUNGE watakaochaguliwa kwa tiketi huru katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 huenda wakapata kiongozi wao rasmi katika Bunge la Taifa pamoja na ofisi inayofadhiliwa na walipakodi, iwapo mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge yatapitishwa. Katika barua iliyoelekezwa kwa Spika wa Bunge la Taifa, Moses Wetang’ula, wabunge hao huru wanataka kiongozi wao awe na ofisi, sawa na ilivyo kwa viongozi wa walio wengi na walio wachache bungeni. “Spika anaweza, kufuatia ombi la maandishi kutoka kwa angalau wabunge huru 10, kutambua rasmi kundi la wabunge huru kwa madhumuni ya kuwawezesha kutekeleza wajibu wao katika Bunge la Taifa,” inasema sehemu ya barua hiyo. Barua hiyo, iliyotiwa saini na Mbunge wa Kisumu Mashariki Shakeel Shabbir, ambaye ni mwenyekiti wa kundi la wabunge huru, pia inapendekeza marekebisho ya Kanuni ya Kudumu nambari 259(1) ili kujumuisha kiti maalum kilichotengwa kwa kiongozi wa wabunge huru. “Kutakuwa na viti maalum ndani ya ukumbi wa Bunge kwa matumizi ya kipekee ya Naibu Spika, Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi, Kiongozi wa Chama cha Walio Wachache, wabunge wenye ulemavu na wabunge huru,” inasema barua hiyo. Wabunge hao wanaeleza kuwa kutengwa kwa viti maalum kutamsaidia Spika kuwatambua kwa urahisi wanapokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge. Aidha, wanataka uwakilishi maalum katika Kamati ya Uteuzi, ambayo husimamia kuweka wabunge katika kamati mbalimbali za Bunge, ili kulinda maslahi yao. “Hili litahakikisha kundi la wabunge huru linatambuliwa rasmi badala ya kujumuishwa kwa jumla kama ilivyo sasa,” inasema barua hiyo. Kwa mujibu wao, kwa sasa wanategemea hisani ya viongozi wa walio wengi na walio wachache katika ugavi wa nafasi za kamati. “Tunapoenda kwa viongozi wa walio wengi na walio wachache, tunaambiwa hawawajibikii wabunge huru ambao hawajaegemea upande wowote. Matokeo yake ni kwamba wabunge huru huachwa nje ya kamati; kwa kweli wanabaguliwa na kupuuzwa kabisa,” inasema barua hiyo. Wabunge hao pia wanataka sauti kubwa zaidi katika uundaji wa Kamati ya Hesabu za Umma (PAC), wakitaka kiti maalum kitengwe kwa mwakilishi wao. Kwa sasa, Kanuni ya Kudumu 205(4) inaeleza kwamba katika uanachama wa PAC, vyama visivyo sehemu ya serikali ya kitaifa vinapaswa kuwa na wingi wa mwanachama mmoja. Barua hiyo imeungwa mkono na wabunge wote 12 huru walio katika Bunge la Taifa. Hao ni Shakeel Shabbir, Caroline Ng’elechei (Elgeyo Marakwet), Monicah Marubu (Lamu), Joshua Mbithi (Masinga), Benard Muriuki (Mbeere Kusini), Elijah Njoroge (Gatundu Kaskazini), Ronald Karauri (Kasarani), Timothy Toroitich (Marakwet Magharibi), Fatuma Mohammed (Migori), Geoffrey Mulanya (Nambale), Kitilai Ole Ntutu (Narok Kusini) na Rahim Dawood (North Imenti). Mbunge huru ni yule anayechaguliwa bila ufadhili wa chama chochote cha kisiasa. Kisheria, mtu anayepania kugombea kama mgombea huru lazima awe amejiuzulu kutoka chama chochote cha kisiasa angalau miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Hata hivyo, ingawa kisheria hawapaswi kuhusishwa na vyama vya kisiasa, wengi wa wabunge huru wanaochaguliwa hujiunga au kushirikiana na vyama au miungano ya kisiasa. Mara nyingi hufanya hivyo ili kupata nafasi katika kamati muhimu za Bunge na pia kusaidia serikali kupata idadi inayohitajika ya kura wakati wa maamuzi muhimu. Katika siku za hivi majuzi pia kumekuwa na wito wa kuwafadhili wagombea huru kupitia Hazina ya Vyama vya Kisiasa, sawa na vyama vya kisiasa. Mwaka jana, wakati wa mjadala kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa wa 2024, baadhi ya wabunge walipendekeza sheria ibadilishwe ili wagombea huru wanufaike na hazina hiyo. Mbunge wa Suba Kusini, Caroli Omondi, alipendekeza wagombea huru wanaopata angalau asilimia tano ya kura zote zilizopigwa wanufaike na fedha hizo. Alisema Katiba inaruhusu mtu kuingia katika uongozi wa kisiasa kupitia chama cha kisiasa au kama mgombea huru, na kwamba hakuna njia iliyo bora kuliko nyingine.

Former Minister for Energy Deogratius Ndejembi has been sworn in as Tanzania’s new Vice President, succeeding Dr Emmanuel Nchimbi, who announced to resign from the position last week. Mr Ndejembi took the oath of office at State House in Dodoma on Saturday, August 29, 2026, a day after the Parliament unanimously approved his nomination by the ruling party Chama cha Mapinduzi (CCM). Speaking after the swearing-in ceremony, President Samia Suluhu Hassan congratulated Mr Ndejembi on his new role and urged him to use the opportunity to develop wisdom and sound judgement as he takes on the responsibilities of the country’s second-highest office. President Hassan also acknowledged the significant responsibility placed on Mr Ndejembi at a relatively young age, saying it could give him the energy and determination needed to execute his duties. “By consensus, we decided that the position of Vice President should be returned to the youth so that we can continue nurturing them. It has moved from a young person and we have returned it to a young person,” President Hassan said. She urged the new Vice President to focus on growing in wisdom rather than simply advancing in age. “I ask you to grow, not in age but in wisdom. Do not be like a fish, whose intelligence deteriorates as it grows. Go and grow; I have given you a great responsibility and I believe you can do it,” she said. Mr Ndejembi’s appointment was approved by Parliament on Friday, August 28, with all 324 MPs who voted supporting his nomination. There were no votes against the appointment. He replaces Dr Nchimbi, whose resignation from the Vice President’s position was accepted by President Hassan last week. CCM expelled Dr Nchimbi from the party after his resignation announcement, citing disciplinary issues.

By Dickson Omobola Following the runway excursion involving Enugu Air at Benin Airport, aviation experts have raised the alarm that random location of structures at airports is putting aviation safety at risk. They particularly identified the presence of buildings and uncompleted buildings in and around airports, saying poorly sited infrastructure could interfere with the safe […]

Kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi na hatimaye kufukuzwa katika chama tawala cha CCM kumefufua mjadala mkubwa kuhusu kiti cha wagombea wenza na wasaidizi wakuu wa nchi katika Afrika Mashariki. Ingawa mazingira ya kuondoka kwake yanaonekana tofauti na yale yaliyomkumba aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, tukio hilo limeibua swali moja muhimu: Je, kiti cha makamu wa rais au naibu rais kimegeuka kuwa kiti cha mikosi na laana katika siasa za Afrika Mashariki? Dkt Nchimbi alitangaza kuwa ataondoka rasmi madarakani Septemba 4, 2026, chini ya mwaka mmoja tangu aapishwe kushika nafasi hiyo. Katika barua yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan, alieleza kuwa uamuzi wake unatokana na ahadi aliyompa rais kwamba angeendelea kuhudumu kwa uaminifu na angeondoka pale ambapo rais angeona kuna haja ya kufanya mabadiliko. Kauli hiyo haikueleza wazi kama kulikuwa na mgogoro kati yake na Rais Samia hadi siku moja baadaye alipotimuliwa chama tawala kwa kile kilichotajwa kama kukosa nidhamu. Hata hivyo, kujiuzulu kwake kumekuja baada ya miezi ya tetesi za kisiasa kuhusu nafasi yake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo ambalo limeongeza uzito wa kisiasa wa tukio hilo. Kwa Kenya, kuondoka kwa Nchimbi kunakumbusha mzozo mkubwa uliotikisa utawala wa Rais William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Tofauti kubwa ni kwamba Gachagua hakujiondoa mwenyewe bali aliondolewa madarakani kupitia mchakato wa bunge na Seneti. Kisa cha Kenya kilionyesha jinsi tofauti za kisiasa kati ya rais na msaidizi wake zinaweza kubadilika kutoka migogoro ya ndani hadi kuwa mgogoro wa kikatiba unaogusa utulivu wa taifa. Kwa Tanzania pia, iliibuka kuwa kuondoka kwa Nchimbi kulisababishwa na mzozo wa aina hiyo. Kuna tetesi kwamba alilazimika kujiuzulu alipobaini kuwa chama kilinuia kumtimua kwa kile kinachotajwa kama kukaidi mwelekeo wa utawala. Kwa miaka mingi, siasa za Sudan Kusini zimezunguka mikataba ya kugawana madaraka, miungano ya kisiasa na migogoro ya mamlaka kati ya viongozi wakuu wa serikali. Tajiriba ya Sudan Kusini inaonyesha kuwa nafasi za wasaidizi wa rais si suala la watu binafsi pekee, bali ni sehemu muhimu ya uthabiti wa kisiasa wa nchi. Mahusiano yanapobadilika ndani ya uongozi wa juu, athari zake huweza kugusa usalama wa taifa na mustakabali wa serikali. Matukio ya Tanzania, Kenya na Sudan Kusini yanaweza kuwa tofauti kwa sura, lakini yanaonyesha changamoto moja ya msingi. Mara nyingi manaibu rais huingia madarakani wakiwa washirika wakuu wa rais, lakini baada ya muda, tofauti za kisiasa, matarajio ya urithi wa madaraka au ushindani wa ushawishi ndani ya vyama tawala huibuka. Matokeo yake yanaweza kuwa kujiuzulu, kuondolewa madarakani au kukaziwa ushawishi wao katika serikali. Hali hii imefanya kiti cha makamu wa rais au naibu rais kuonekana kama mojawapo ya nyadhifa hatari zaidi kwa maisha ya kisiasa. Mjadala huu unajiri huku Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiendelea kusukuma mbele mpango wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki kupitia hatua ya Shirikisho la Muungano.Iwapo ni laana au la, ni wazi kuwa kiti cha makamu wa rais na naibu rais kimekuwa na changamoto nyingi kisiasa.

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Bandari nchini (KPA) wameingiwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa ajira zao huku serikali ikijiandaa kuwapa wawekezaji binafsi nafasi ya kuendesha baadhi ya shughuli katika bandari za Mombasa na Lamu. Wasiwasi huo umeibuka baada ya Kamati ya Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) kuidhinisha tafiti za uwezekano wa kuhusisha sekta binafsi katika vituo muhimu vya bandari. Mkurugenzi Mkuu wa tume ya mipango ya uwekezaji kati ya umma na kampuni za kibinafi (PPP) Kefa Seda alisema Alhamisi kuwa uamuzi huo umefungua njia ya kuanza mchakato wa zabuni mwezi Septemba. Mali zitakazohusika katika awamu ya kwanza ni Gati 11 hadi 14 za Bandari ya Mombasa, Mombasa Container Terminal 1, Lamu Container Terminal na Eneo Maalum la Kiuchumi la Lamu (SEZ). “Uidhinishaji huu unahamisha mali hizi muhimu za bandari kutoka hatua ya utafiti hadi hatua ya ununuzi chini ya mfumo wa PPP,” Bw Seda alisema. Mpango huo ni sehemu ya mabadiliko ya bandari za Mombasa na Lamu kuwa mfumo wa 'landlord port', ambapo serikali itaendelea kumiliki mali hizo huku sekta binafsi ikisimamia shughuli za kila siku. Hata hivyo, wafanyakazi wana hofu kuwa mpango huo unaweza kusababisha kupunguzwa kwa nafasi za ajira au kubadilishwa kwa mikataba yao. Wasiwasi huo umeongezwa na zabuni ya KPA ya kukodisha vifaa na huduma za uendeshaji, inayotaja kuajiri takriban wafanyakazi 4,700 wenye ujuzi maalum. “Kufikia sasa hatujui hatima yetu baada ya zabuni hii kuchapishwa. Wasiwasi wetu mkubwa ni aina ya wafanyakazi wanaohitajika bandarini,” alisema mfanyakazi mmoja wa KPA. Nyaraka za mpango huo zinawapa wafanyakazi chaguo la kubaki KPA, kuhamishiwa taasisi nyingine za serikali au kutumwa kwa kampuni binafsi kwa hiari. Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Kapteni William Ruto, amekanusha madai kwamba bandari inauzwa, akisema serikali itaendelea kuwa mmiliki wa miundombinu. Alisema sekta binafsi italeta mtaji na utaalamu ili kuboresha ufanisi wa bandari. Bandari ya Mombasa ilihudumia tani milioni 45.45 za mizigo mwaka jana, kutoka tani milioni 40.99 mwaka 2024, huku trafiki ya makontena ikizidi TEU milioni 2.11. Kwa sasa, wafanyakazi wanataka serikali iwape hakikisho kuhusu ajira zao kabla ya mchakato wa zabuni kuanza mwezi ujao.

NAIBU Rais, Profesa Kithure Kindiki Ijumaa aliambia chama cha Orange Democratic Movement (ODM), kinachoongozwa na Seneta wa Siaya Oburu Oginga, kwamba hawezi kuondolewa kirahisi, na kwamba atapambana ili kuhifadhi wadhifa wake. Kauli hiyo ilitolewa huku akimshambulia pia kiongozi wa Wiper Democratic Movement, Kalonzo Musyoka, akimtaka asahau ndoto ya urais. “Wadhifa wa Naibu Rais hauko wazi, na ODM inapaswa kuusahau,” alisema Profesa Kindiki. Alizungumza katika Uwanja wa Nembure, Kaunti ya Embu, alipokutana na viongozi 20,000 wa mashinani kutoka eneo hilo. Aliambia ODM kwamba hata mwaka 2027 atakuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto, ambaye anatarajiwa kutetea muhula wake wa pili. “Mimi ni mtu mgumu sana na hawawezi kuniondoa katika kiti changu,” alisema akiwarejelea viongozi wa ODM. Katika miezi ya hivi majuzi, mjadala kuhusu wadhifa wa Naibu Rais umeongezeka huku viongozi kadhaa ndani ya serikali jumuishi wakionyesha nia ya kuumezea mate. Miongoni mwa waliotajwa kutamani wadhifa huo ni Oburu Oginga, Mawaziri Wycliffe Oparanya na Hassan Joho, pamoja na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula. Akiwa Embu, Prof Kindiki alieleza imani yake kuwa Rais Ruto atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 na kuwaonya viongozi wa upinzani kujiandaa kwa mapambano makali ya kisiasa. “Siwezi kuruhusu watu wetu watoke serikalini na kuingia upinzani. Baadhi ya wanaosema tutahudumu muhula mmoja hata hawatakuwa kwenye kura. Wanataka kutuletea watu ambao hawana rekodi yoyote ya maendeleo, hawajabadilisha maeneo yao wala kujulikana kwa maendeleo. Hatutaki kubahatisha. Tunajua tunakopeleka taifa hili,” alisema. Prof Kindiki aliwataka viongozi wa upinzani kueleza rekodi zao za maendeleo. Aliwahimiza wakazi wa Embu kutovutwa na misemo ya kisiasa bali wawapime viongozi kwa misingi ya yale waliyofanya walipokuwa madarakani. Alisema serikali ya Kenya Kwanza imepiga hatua kubwa katika kaunti zote 47 tangu ilipoingia madarakani mwaka 2022 na iko tayari kutetea rekodi yake mbele ya wananchi. “Kiwango cha maendeleo tulichofikia si kile tulichokuta mwaka 2022 tulipoingia madarakani. Kazi imefanyika na wananchi wanaweza kuiona,” alisema. Naibu Rais alisema yuko tayari kukutana na wananchi wa Embu na Wakenya wote kueleza mafanikio ya serikali katika sekta za kilimo, elimu, afya, miundombinu na nyanja nyingine muhimu. “Niko tayari kueleza kwa wananchi kile ambacho serikali imefanya kubadilisha nchi hii na kuwawezesha wananchi kiuchumi,” alisema. Aliwataka wakosoaji wa serikali pia waeleze walichofanikisha walipokuwa katika nyadhifa za umma. “Waambie wananchi walifanya nini walipokuwa na mamlaka makubwa zamani. Ukweli ni kwamba hawana chochote cha kuonyesha,” alisema. Kuhusu kilimo, Kindiki alisema serikali imeboresha bei za kahawa na maziwa. Alisema wakulima wa kahawa sasa wanapata kati ya Sh120 na Sh150 kwa kilo, huku bei ya lita moja ya maziwa ikiongezeka kutoka Sh33 hadi Sh50. Aliongeza kuwa bei ya mbolea ilishuka kutoka Sh7,000 mwaka 2022 hadi Sh3,500, baadaye Sh2,500 na sasa Sh2,000 baada ya punguzo zaidi la Sh500.

Public spat between President Kiir and his vice Rebecca Nyandeng raises fresh questions regarding cohesion.

MBEYA; Kaimu Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya Wizara ya Afya, DK Winfrida Kidima,amesema jamii bado ina uelewa tofauti kuhusu tiba asili, hivyo Wizara ya Afya inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa huduma hizo, hasa katika kuboresha afya ya wananchi. Dk Kidima amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari…

Chadema secretary-general John Mnyika has taken responsibility for organising a meeting that the prosecution alleges was used by the party’s chairman, Tundu Lissu, to make statements amounting to treason.

DODOMA: CHAMA Cha Mapinduzi’s (CCM) Women’s Wing (UWT) has congratulated Deogratius John Ndejembi on his appointment and subsequent confirmation as Vice-President of Tanzania, describing the decision as a reflection of the confidence the ruling party has placed in him. UWT Chairperson Mary Chatanda said on Friday that the appointment demonstrated Mr Ndejembi’s integrity, hard work…

By Golok Nanmwa, Jos JOS — A middle-aged man was rescued on Friday after reportedly jumping into the water from the British American Bridge in Jos North Local Government Area of Plateau State. The incident attracted the attention of passers-by, who raised the alarm and mobilised to rescue the man from the water. An eyewitness, […]

LUBUMBASHI: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), zimeazimia kuanza mchakato wa kuwarejesha wakimbizi wa DRC wanaohifadhiwa nchini Tanzania ambao wako tayari kwa hiari yao kurejea nchini kwao. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo…

Attorney General Hamza Johari has said Dr Emmanuel Nchimbi ceased to be Vice President after losing his membership of Chama Cha Mapinduzi (CCM), despite his resignation having been set to take effect on September 4, 2026.

DODOMA; Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo leo Agosti 28, 2026 amewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto wa Mwaka 2026. “Lengo la kufutwa kwa Sheria hii ni kuendeleza juhudi za Serikali za kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuunganisha taasisi mbalimbali zinazotekeleza majukumu yanayofanana kwa lengo la kupunguza wingi wa taasisi…

DODOMA: THE National Assembly has unanimously endorsed the nomination of Chama cha Mapinduzi (CCM) Stewarts and Energy Minister Deogratius Ndejembi to be the next Tanzania’s Vice Preisent with all 324 lawmakers who voted backing his appointment, representing 100 percent support. Ndejembi was confirmed today, August 28, 2026, during the Fourth Meeting, Third Session of the…

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imefichua mtandao mpana wa ufisadi katika serikali za kaunti ambapo maafisa wa umma wanadaiwa kutumia watoto, wake na jamaa zao wa karibu kupata zabuni za serikali. Kesi nyingi zilizochunguzwa na tume hiyo zinaonyesha kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakikwepa sheria zinazowazuia kufaidika na zabuni za taasisi wanazofanyia kazi kwa kusajili kampuni kwa majina ya ndugu zao. Katika Kaunti ya Kitui, EACC ilibaini kuwa kati ya mwaka 2018 na 2025, kampuni za Shanel Construction Company Ltd, ECO Stone Company Ltd, AZ Links Company Ltd, DTK Construction Company Ltd na 4 Walls Company Ltd zililipwa jumla ya Sh14.1 milioni na serikali ya kaunti. Kwa mujibu wa rekodi, kampuni hizo zinamilikiwa na Josephine Mwikalu Wambua, Makoma Wambua na Emmanuel Wambua. Hata hivyo, uchunguzi wa EACC ulibaini kuwa watu hao ni jamaa wa karibu wa Gladys Mami Kivoto, Afisa Mkuu katika Idara ya Kilimo, Uvuvi na Unyunyuzaji ya Kaunti ya Kitui. Wakati zabuni hizo zilipokuwa zikitolewa na malipo kufanywa, Bi Kivoto alikuwa ndiye afisa mwenye mamlaka ya kuidhinisha matumizi katika idara hiyo. Tume hiyo inadai kuwa alitumia nafasi yake kuhakikisha jamaa zake wanapewa zabuni na kulipwa. Uchunguzi pia ulifuatilia mzunguko wa fedha kati ya kampuni hizo, wamiliki wake na Bi Kivoto. Watu hao wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ulaghai katika shughuli za ununuzi wa umma. Katika Kaunti ya Turkana, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma imeanza mashtaka dhidi ya Peter Long’ole Apua, afisa mkuu wa fedha wa kaunti hiyo na mkurugenzi wa Apuco Holdings Group. Jamaa zake Christopher Imuron Apua na Moses Along’ole Apua pia ni wakurugenzi wa kampuni hiyo iliyolipwa Sh62 milioni na serikali ya kaunti. Kaunti hiyo pia inahusishwa na kesi ya Lilian Akiru Louruka, mwalimu wa chekechea, ambaye kampuni yake ya Natiltila Company Ltd ilipewa zabuni tano zenye thamani ya Sh30 milioni. EACC inadai kuwa yeye na mume wake ndio wakurugenzi wa kampuni hiyo. Katika Kaunti ya Nakuru, kampuni tatu za Denken Building and Construction Limited, Murinchamba Investments Limited na Windcom Solutions Limited zilipokea zaidi ya Sh120.6 milioni kutoka kwa serikali ya kaunti kati ya mwaka wa fedha wa 2020/21 na 2024/25. Uchunguzi ulionyesha kuwa kampuni hizo zinamilikiwa na mchumba wa mfanyakazi wa kaunti anayehudumu kama mwanauchumi. EACC ilibaini kuwa baadhi ya fedha zilitumwa kwa maafisa waliokuwa wakihusika katika mchakato wa zabuni, ukaguzi wa kazi na uthibitishaji wa malipo. Mojawapo ya kampuni hizo pia ilidaiwa kuwasilisha stakabadhi za kughushi wakati wa zabuni. Katika uchunguzi mwingine wa Nakuru, kampuni za Tirzah Logistics, Purim Logistics na Nemoca Enterprises zilipokea Sh45.64 milioni kutoka kwa serikali ya kaunti. Wakurugenzi wa kampuni hizo walibainika kuwa watoto wa afisa mkuu mmoja. Kaunti ya Migori pia imekumbwa na tuhuma sawa. EACC ilichunguza kampuni za Enigma Solutions na Enigma Solutions Limited na kubaini kuwa zilihusishwa na afisa mkuu wa afya ya umma, huku mume wake akiwa mkurugenzi pekee na mtia saini wa akaunti za benki za kampuni hizo. Kampuni hizo zilipata mikataba 19 ya thamani ya Sh27.2 milioni kati ya mwaka 2023 na 2024 kwa usambazaji wa chakula, vifaa vya ofisi, utengenezaji wa magari na huduma nyingine. Katika Wajir, maafisa wawili wa kaunti walidaiwa kuhamisha hisa za kampuni yao kwa mtu mwingine lakini wakaendelea kuwa watiao saini wa akaunti zake za benki. Kampuni hiyo ililipwa Sh3.99 milioni bila kufuata taratibu za ununuzi. Kaunti ya Marsabit nayo ilitajwa baada ya afisa wa afya kudaiwa kuwa mkurugenzi wa kampuni iliyolipwa Sh45.6 milioni kwa bidhaa na huduma ambazo baadhi yake hazikuwasilishwa. Uchunguzi wa EACC unaonyesha kuwa mtindo wa kutumia wanafamilia kupata zabuni umeenea hata nje ya serikali za kaunti. Katika Taasisi ya Rift Valley Institute of Science and Technology (RVIST), kampuni ya Afripath Care Kenya Limited ilipewa zabuni ya Sh57 milioni. Tume ilibaini kuwa mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo ni shemeji wa Mbunge wa Kitutu Chache North. Baada ya malipo kufanywa, karibu Sh40 milioni zilihamishwa kutoka kwa akaunti ya kampuni hiyo kwenda kwa mbunge huyo. EACC ilisema mbunge huyo alitumia Sh10 milioni kununua ardhi.

DODOMA; Picha za matukio mbalimbali, wakati Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, akipokea rasmi leo Agosti 28, 2026 jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Jina hilo limewasilishwa kwa Spika na Katibu wa Rais, Balozi Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais…