BENKI ya KCB imepiga ripoti kwa DCI ikitaka ichunguze kampuni ya Foxcapital inayodai ilituma Sh146 bilioni kwenye akaunti yake kutoka ng’ambo kuhusiana na uwekezaji wa dhamana za serikali.
Benki hiyo inadai kwamba stakabadhi zilizowasilishwa na kampuni hiyo kortini kudai fedha hizo ni ghushi na inataka DCI kubaini ni nani aliziandaa, kusambaza na kuziwasilisha kortini.
Mzozo unahusisha €978,675,835 (Sh146.3 billion), ambazo Foxcapital inasema ilituma kwa akaunti yao ya KCB Oktoba mwaka jana kama malipo kwa kampuni ya Uingereza, Bay Bionics Ltd, iliyotambuliwa zamani kama BB Biotech AG Limited.
Foxcapital iliwasilisha kesi mapema mwezi huu ikidai kwamba KCB ilipokea fedha hizo za kigeni lakini ikakosa kuziweka kwenye akaunti yake, na kufanya Mahakama Kuu kubana hela hizo ikisubiri iamuliwe iwapo benki hiyo kweli ilipokea pesa hizo na kukataa kuzipeana kwa kampuni husika.
Katika kilio chake kwa DCI kitengo cha Ulaghai wa Benki, KCB Group, kupitia Afisa Mkuu Mtendaji Paul Russo anatilia shaka stakabadhi zilizotumiwa na Foxcapital kudai pesa hizo.
Stakabadhi zinajumuisha arafa za SWIFT, ripoti ya tukio ya Aprili 17, barua ya Mei 18 ya kuangazia kosa la kiuchumi na utathmini wa kiufundi wa Julai 1.
KCB inasema stakabadhi zinazodaiwa kutoka UBS Switzerland AG na maafisa wa KCB sio halisi.
Benki ya KCB yadai kuna njama ya kuilaghai Sh146 bilioni

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]