
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


WHO imesema Ebola bado ni changamoto na inahitaji rasilimali nyingi. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus,alisema Jumatano kwamba hadi kila maambukizi yatakapobainika na kukatizwa, ugonjwa huo utaendelea kuwa hatari DRC, nchi jirani na eneo lote. Idadi ya waliofariki kutokana na mkurupuko huo imevuka 3,000, kwa mujibu wa takwimu za serikali, huku ugonjwa huo ukiendelea kuenea kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Mkurupuko huo, unaosababishwa na aina ya kirusi cha Ebola cha bundibugyo, sasa ndio mkubwa na wenye vifo vingi zaidi katika historia ya DRC na imezidi mkurupuko uliotokea mnamo na 2018–2020. Tedros alisema vifo vingi vimetokea miongoni mwa watu ambao hawakuwa kwenye orodha ya waliokuwa wamewasiliana na wagonjwa, hali inayoashiria kuwepo kwa maambukizi mengi ambayo hayajulikani. Alisema mazishi yasiyofanywa kwa njia salama pia yanaendelea kuchangia kuenea kwa virusi hivyo. WHO imeomba kuongezwa kwa fedha za mpango wa kukabiliana na Ebola unaoongozwa na serikali ya Congo, unaohitaji dola bilioni 1.3 (Sh168 bilioni). WHO imetuma tani 320 za vifaa na kuongeza uwezo wa vipimo hadi 3,000 kwa siku, lakini inahitaji fedha zaidi kuongeza vitanda katika vituo vya matibabu.

DODOMA; Serikali imewasilisha bungeni maelezo kuhusu Azimio la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani (GGGI). Akiwasilisha bungeni maelezo ya kuhusu Azimio hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Yussuf Masauni, ameeleza faida mbalimbali endapo Tanzania Mkataba huo hilo. “Chimbuko la Azimio la…

DAR ES SALAAM; Mradi wa kwanza wa kisasa na usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake, huku ukitajwa kunufaisha kaya takribani 11,000 Wilaya ya Kinondoni. Mradi huo uliopo eneo la Mbezi Beach unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na utagharimu kiasi…

DAR ES SALAAM: THE government’s decision to require all upcountry buses to begin their journeys at Magufuli Bus Terminal in Mbezi is reshaping Dar es Salaam’s transport system. While the move has raised concerns among passengers, the government has a strong case for centralising intercity bus operations. The real question is whether the policy can…
MOTO umeteketeza Msitu wa Aberdare siku nne mfululizo huku hifadhi wanyamapori, miti na maeneo muhimu ya vyanzo vya maji yakiteketea. Moto huo unateketeza Msitu wa Ndaragwa, eneo la Shamata, sehemu muhimu ya vyanzo vya maji ya Ziwa Olbolosat, Ol Kalou na maeneo mengine ya Ndaragwa. Maafisa wanashuku kuwa moto huo ulianzishwa kwa bahati mbaya na waliokuwa waliokuwa wakirina asali msituni. Hata hivyo, baadhi ya wakazi wanasema kuna imani ya zamani kwamba kuchoma msitu wakati wa ukame husaidia kuvuta mvua. Wanaamini moshi mweusi unaotokana na moto huunda mawingu ambayo baadaye huleta mvua. Serikali ya Kaunti ya Nyandarua na Huduma ya Misitu Kenya (KFS), ambazo zinaongoza juhudi za kuzima moto huo, zimesema zimelemewa na zinahitaji msaada wa dharura kutoka kwa mashirika mengine ya kuhifadhi mazingira na serikali ya kitaifa. Afisa Mkuu wa uhifadhi wa misitu wa Nyandarua Daniel Mkung alisema moto huo unateketeza eneo la nyanda za juu lenye mimea mikavu, hali inayofanya iwe vigumu kuuzima. “Moto uko katika eneo la nyanda za juu ambako kuna mimea mingi mikavu. Hali hii inafanya iwe vigumu zaidi kuudhibiti. Tunahitaji msaada wote tunaoweza kupata na tunapanga jinsi ya kuwasafirisha wazima moto zaidi hadi msituni,” alisema. Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wachunaji wa asali huenda ndio walianzisha moto huo. Hata hivyo, imani kuhusu moshi kuvuta mvua imeibua mjadala mwingine kuhusu sababu ya moto za mara kwa mara msituni wakati wa ukame. Jackson Kieru, mwenye umri wa miaka 86, alisema baadhi ya watu bado wanaamini moshi wa moto huvuta mvua. “Baadhi ya watu wanaamini moshi mweusi unaotokana na kuchoma msitu huvutia mvua. Wanaamini mawingu ya moshi hubadilika kuwa mawingu yanayoleta mvua siku chache baadaye. Ni desturi ya zamani ambayo bado inaaminiwa,” alisema. Millicent Wangui, 79, alisema amesikia imani hiyo tangu akiwa mdogo. “Miaka mingi iliyopita, vijana walikuwa wakichoma moto mashambani wakiamini utaleta mvua. Huenda hiyo ndiyo sababu baadhi yao wameanza kuchoma misitu,” alisema. Lakini Bw Mkung alikataa imani hiyo akisema ni hatari. “Hizo ni imani potofu. Kwa kweli zinaweza kuchelewesha mvua kutokana na gesi zinazotokana na moshi. Miti inajulikana kusaidia kuvuta mvua na hatuwezi kupata mvua zaidi kwa kuharibu misitu,” alisema. Alisema wazima moto wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na mimea mikavu na upepo mkali unaosambaza moto kwa kasi. Kamanda wa KWS katika Kaunti ya Nyandarua Paul Wambugu alisema wazima moto kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Aberdare wametumwa kusaidia kuzima moto huo. Afisa Mkuu wa Maji na Tabianchi wa Nyandarua Wachira Mugo alisema hali inazidi kuwa mbaya huku timu za kaunti zikishindwa kufikia baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa kutokana na eneo kuwa na miinuko mikali. “Serikali ya kaunti haina uwezo wa kutosha kudhibiti moto huu. Vifaa vyetu vya kuzima moto haviwezi kufika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa kutokana na hali ngumu ya ardhi. Wafanyakazi wetu wamelemewa,” alisema. Alisema moto huo ulikuwa ukielekea katika maeneo muhimu ya vyanzo vya maji. Aliomba msaada wa KFS, KWS na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF). Moto huo umechochewa na ukame wa muda mrefu ambao umefanya mimea kuwa mikavu sana pamoja na upepo mkali unaovuma upande wa magharibi wa msitu. Gavana wa Nyandarua Kiarie Badilisha ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuzuia moto huo usiharibu maeneo muhimu ya vyanzo vya maji.

ZANZIBAR: FORMER Zanzibar First VicePresident Othman Masoud Othman has urged Muslim parents to redouble efforts in raising their children on strong moral foundations, warning that rapid technological advancements pose growing challenges to family structures and social cohesion. Mr Othman made the remarks in Nungwi, North Unguja, where he joined Muslims in commemorating the annual Maulid…

SIASA za ugavana katika Kaunti ya Kwale zimechukua mkondo mpya baada ya mvutano kuibuka kuhusu mpango wa kumtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ubaharia cha Bandari, Bw Lung’anzi Mangale, awe mgombea mwenza wa ugavana wa aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Kilimo, Prof Hamadi Boga, katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Hatua ya kuwaunganisha wanasiasa hao wawili ambao wote waliwania ugavana 2022, inalenga kutoa ushindani mkali dhidi ya Gavana Fatuma Achani, ambaye anatarajiwa kutetea kiti hicho kupitia tikiti ya Chama cha UDA. Wazee wa jamii ya Wadigo, wakiongozwa na msemaji wao Bw Chirau Makwere, ambaye pia aliwania ugavana 2022, walisema waliamua kuunga mkono Prof Boga kuwania ugavana na Bw Mangale kuwa mgombea mwenza. Wazee hao sasa wamempa aliyekuwa Prof Boga makataa ya wiki mbili kutangaza wazi mgombea mwenza wake ili kuzima sintofahamu zilizoibuka hivi majuzi baada ya kubainika kuwa, huenda Bw Mangale akaamua kuwania ugavana. “Tumeamua kwamba Prof Boga atuambie naibu wake ni nani ndani ya wiki mbili zijazo. Pia tunataka Bw Lung’azi atangaze kwa kauli yake kwamba atakuwa naibu wa Prof Boga. Hatuna msimamo mwingine isipokuwa Prof Boga kuwa mgombea wa ugavana na Bw Lungazi kuwa naibu wake,” alisema Bw Makwere. Akiongea kwenye mahojiano ya redio, Bw Makwere alisema iwapo Bw Mangale hatakuwa tayari kuwa mgombea mwenza wa Prof Boga, watamruhusu apendekeze majina ya watu watatu ambao jamii itachagua mmoja wao. “Tumekuwa tukisikia sauti kutoka sehemu mbalimbali kwamba Bw Lungazi anataka kutangaza azma ya kuwa gavana. Sisi tumekataa. Tunataka awe naibu gavana. Na tutamimina kura mpaka waone,” alisema Bw Makwere. Kwenye mahojiano tofauti, Bw Mangale alisema yuko kwenye kinyang’anyiro cha ugavana wa Kwale wala si kama mgombea mwenza. Alieleza kuwa, yuko kwenye chama cha ODM ingawa aliwania wadhifa huo kupitia Chama cha Pamoja African Alliance (PAA) katika uchaguzi uliopita. Haya yanajiri wiki kadhaa baada ya Prof Boga na Bw Mangale kutangaza kuwa wameamua kuweka tofauti zao kando na kuungana katika harakati za kuwania kiti hicho kwa lengo la kumbandua Gavana Achani katika uchaguzi mkuu ujao. Bi Achani amepata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya viongozi wa ODM, lakini baadhi ya wanachama wamesisitiza chama hicho kina mgombea wake wa ugavana, ambaye ni Prof Boga. Katika mikutano yake ya hadhara, Bi Achani hupuuza wapinzani wake akidai wanaendeleza siasa za ukabila, na badala yake kutaka ushindani wa kisiasa uwe kwa misingi ya uwezo wa viongozi kuleta mandeleo kwa manufaa ya wananchi. “Ukabila huleta mgawanyiko katika jamii, kutokuaminiana, na hudunisha umoja wa kitaifa na kuathiri maendeleo. Kama Wakenya, tunafaa kukataa siasa za ukabila na badala yake tukumbatie umoja, uwiano na uongozi unaolenga masuala muhimu kwa manufaa ya kila mmoja,” alisema hivi majuzi. Prof Boga na Bw Lungazi waliwania ugavana wa Kwale katika uchaguzi mkuu wa 2022, ambapo waliibuka wa pili na wa tatu mtawalia.

By Rosemary Iwunze Pension Fund Administrators, PFAs, have pushed about N17.1 trillion from Nigerian pension monies to Federal Government, FG, securities. This amount represents 58.07 per cent of the N29.5 trillion pension industry’s Net Asset Value, NAV, in the first quarter of 2026. The National Pension Commission, PenCom, has now warned that such investments may […]

SEKTA za Kilimo, Mifugo na Uvuvi zimetakiwa kuongeza uzalishaji, kuwekeza katika teknolojia za kisasa na kuboresha tija ili kuchangia Dola za Marekani bilioni 100 katika uchumi wa Tanzania kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

ALIYEKUWA Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana anataka kubadili jina la chama chake cha Muungano Party (MP) kuwa The Mwananchi Party (TMP), hatua ambayo imeibua maswali kuhusu uhusiano wake na vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Hatua hiyo pia inaweza kuwa sehemu ya mikakati ya Profesa Kibwana kujiandaa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Sifuna na washirika wake katika Linda Mwananchi wamekumbwa na pigo kubwa kisiasa katika wiki za hivi majuzi baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) kuzuia juhudi zao za kusajili rasmi jina hilo. Huku wakikumbana na vikwazo katika juhudi za kulinda jina la vuguvugu hilo, Profesa Kibwana aliwasilisha stakabadhi za kuomba kubadili jina la chama chake. Si siri kwamba Profesa Kibwana amekuwa akimuunga mkono Bw Sifuna na vuguvugu lake kupitia mitandao ya kijamii. Katika tangazo la gazeti rasmi la serikali la Agosti 24, Msajili wa Vyama vya Kisiasa John Cox Lorionokou alisema Muungano Party imewasilisha ombi la kubadili jina. “Kwa kutumia mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 20(1)(d) cha Sheria ya Vyama vya Kisiasa, Msajili wa Vyama vya Kisiasa anatoa taarifa kwamba Muungano Party (MP) inakusudia kubadili jina na kuwa The Mwananchi Party (TMP),” ilisema taarifa hiyo. Msajili aliwaalika watu walio na pingamizi kuwasilisha maoni yao kwa maandishi katika muda wa siku saba tangu kuchapishwa kwa tangazo hilo. Hata hivyo, muda huo sasa umekamilika bila pingamizi zozote. Profesa Kibwana hakujibu maswali kuhusu sababu ya kubadili jina la chama na iwapo ana mpango wa kushirikiana na wanasiasa wa Linda Mwananchi 2027. Hivi majuzi Bw Lorionokou alisema kuwa Liberty National Democratic Alliance Party, almaarufu LINDA Party, pamoja na Mwananchi Party, zilikuwa katika mchakato wa kusajiliwa. Alisema hali hiyo ndiyo iliyofanya Bw Sifuna na washirika wake kunyimwa jina la Linda Mwananchi baada ya kubainika kuwa majina hayo yalikuwa tayari yamehifadhiwa. Kwa mujibu wa ORPP, LINDA Party ilihifadhi jina lake Novemba 15, 2024. Msajili pia alisema ombi la kuhifadhi jina Mwananchi Party liliwasilishwa na Pius Onyango Julai 2026 na bado linazingatiwa. Hii inamaanisha kuwa jina hilo haliwezi kuchukuliwa na kundi jingine bila mchakato huo kukamilika.

KENYA inapoelekea uchaguzi mkuu wa 2027, tayari kuna ishara za hatari zinazoweza kuzua vurugu na kuzamisha nchi katika mzozo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Vurugu katika mikutano ya kisiasa, matamshi ya chuki, madai ya wizi wa kura, mizozo kuhusu zabuni za mabilioni ya fedha, taarifa za uongo na kupungua kwa imani kwa taasisi za uchaguzi ni baadhi ya changamoto zinazotajwa. Masuala hayo yalijadiliwa jana katika mkutano wa kitaifa wa usalama wa uchaguzi uliofanyika Nairobi. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC), Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) na Idara ya Mahakama zilitahadharisha kuhusu umuhimu wa kujifunza kutokana na machungu ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/08. Ghasia hizo zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,100, 3,500 kujeruhiwa na hadi 600,000 kuhama makazi yao. Ripoti ya Kofi Annan Foundation ya Electoral Vulnerability Index ya 2026–2027 iliyotolewa Julai ilianika uwezekano wa Kenya kukumbwa na aina fulani ya ghasia zinazohusiana na uchaguzi kuwa asilimia 81.6. Ripoti hiyo ilitaja ukosefu wa imani kwa IEBC, ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira kwa vijana, siasa za ukabila na wasiwasi kuhusu mwenendo wa polisi wakati wa maandamano. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon alisema tume hiyo imekuwa ikielekezewa na madai mazito kutoka kwa viongozi wa kisiasa kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa 2027. Alisema madai yasiyothibitishwa yanaweza kudhoofisha imani ya wananchi katika IEBC kabla kampeni hazijaanza kikamilifu. “Tunahitaji kuchunguza ukweli kuhusu baadhi ya madai haya ya ajabu ambayo yanalenga kuwafanya Wakenya waamini kwamba uchaguzi hautakuwa huru na wa haki,” alisema. Kauli yake ilijiri baada ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kudai IEBC inapanga kuiba uchaguzi wa 2027 kupitia mfumo mpya wa usimamizi wa uchaguzi. Pia kuna mzozo kuhusu zabuni ya mabilioni ya fedha ya mfumo wa teknolojia utakaotumiwa katika uchaguzi huo. Bw Ethekon alisema IEBC italinda uhuru wake na kupinga juhudi zozote za kudhoofisha uaminifu kwa tume. Alisema hata hivyo IEBC haiwezi kufanikisha uchaguzi wa kuaminika bila ushirikiano wa polisi, mahakama na taasisi nyingine. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga alionya kuwa uchunguzi dhaifu na ukosefu wa ushahidi unatatiza juhudi za kuwafungulia mashtaka wahusika wa vurugu za kisiasa na uchochezi. Aliwataka polisi na DCI kukusanya ushahidi unaohusisha washukiwa na uhalifu, wakiwemo wale wanaofadhili au kupanga makundi ya vijana wanaotumika kuvuruga mikutano. Alisema kuwakamata vijana pekee bila kuwafuatilia wanaowafadhili hakutamaliza tatizo. Mwenyekiti wa NCIC, Askofu Kepha Omae, alisema tume hiyo ina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa matamshi ya chuki na uchochezi kadiri shughuli za kisiasa zinavyozidi. Alisema NCIC itachukua hatua dhidi ya wanasiasa na Wakenya wengine wanaokiuka sheria kupitia kauli zao. Tume hiyo pia imekuwa ikifuatilia jumbe zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp na TikTok. Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja alisema Polisi wameanza kutekeleza mpango wa usalama wa uchaguzi wa 2027. Jaji Daniel Musinga, aliyekuwa mgeni rasmi, alisema vitisho vipya kama matamshi ya chuki, taarifa za kupotosha, propaganda za kisiasa na matumizi ya teknolojia kuwanyanyasa wanawake kisiasa vinahitaji taasisi mbalimbali kushirikiana.

DODOMA:Jitihada za Serikali za kuwawezesha Watanzania kushiriki katika shughuli za kiuchumi zimeendelea kuzaa matunda katika sekta ya gesi asilia, huku viwanda vya kuchakata gesi asilia vya Madimba na Songosongo vikiendeshwa na wazawa kwa asilimia 100. Akizungumza katika Kongamano la Tano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati (Local Content) Mwaka 2026 jijini…

IRINGA: KILIO cha wakulima cha kupata mbegu bora kwa bei nafuu kimeendelea kupata majibu, huku wakulima katika Wilaya ya Iringa wakisema hatua ya serikali ya kusogeza mbegu bora karibu na mashamba yao imewapa matumaini mapya ya kuongeza uzalishaji na kipato. Wakulima hao wamesema upatikanaji wa mbegu bora, ukienda sambamba na matumizi sahihi ya mbolea na…

MARA: FOUR Swiss tourists who were involved in a safari vehicle incident near the Mara River in Tanzania’s Serengeti National Park have expressed satisfaction with the overall services they received during their trip, praising the organisation, coordination of transportation and the support provided to them before and after the incident. The tourists, who were on…

MASHIRIKA ya habari nchini yameitaka Serikali kufanya uchunguzi huru na wa haraka kuhusu madai ya kutekwa kwa Mhariri Mwandamizi wa Standard Group, Alex Kiprotich. Wameonya kuwa mashambulizi dhidi ya wanahabari yanazua hofu nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Kiprotich alitekwa na wanaume waliokuwa na silaha katika barabara ya Gilgil-Nakuru Jumanne usiku, muda mfupi kabla ya saa tatu na dakika 20 usiku. Video ya tukio hilo inaonyesha gari aina ya Subaru lenye nambari ya usajili KDC 125E likimpita kisha kumzuia. Wanaume waliokuwa na silaha walimwamuru atoke kwenye gari lake kabla ya kumwingiza kwa lazima katika gari lao. Alipatikana ametupwa karibu na Bwawa la Masinga, Machakos Jumatano asubuhi, zaidi ya saa tisa baada ya kutekwa; umbali wa zaidi ya kilomita 200 kutoka eneo la tukio. Bw Kiprotich alipewa hifadhi na familia moja ya eneo hilo kabla ya kikosi cha Standard Group kilichoongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo, Chaacha Mwita, kumchukua karibu saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Alikuwa salama kimwili lakini alishtuka sana kiasi cha kutoweza kuzungumza na wanahabari. Tukio hilo limeibua hasira miongoni mwa mashirika ya habari na ya kutetea haki za binadamu, huku yakitaka waliohusika kutambuliwa na kufikishwa mahakamani. Chama cha Wahariri Kenya, Chama cha Wanahabari Kenya (KUJ) na Chama cha Wanawake katika Habari Kenya (AMWIK), chini ya Kenya Media Sector Working Group, vilisema tukio hilo ni sehemu ya mfululizo wa vitisho dhidi ya wanahabari. Katibu Mkuu wa KUJ, Eric Oduor, alisema shambulio dhidi ya mwanahabari yeyote ni shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari. Alisema uchunguzi wa awali umebaini baadhi ya watu waliohusika na tukio hilo na kwamba mashirika hayo yatawasilisha malalamishi kwa Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi (IPOA) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP). “Tutaandikia ODPP ichukue hatua na iwapo haitafanya hivyo, tutawafungulia mashtaka maafisa waliohusika,” alisema Bw Oduor. Hofu zaidi imezuka kutokana na madai kwamba mwezi Juni 27 pia kulikuwa na jaribio jingine la kumteka Bw Kiprotich. Uchunguzi wa ndani wa Standard Group kuhusu tukio hilo umedaiwa kubaini gari lililotumiwa na watekaji ni la kitengo cha Crime Research and Intelligence Bureau (CRIB) cha Polisi, lakini hakuna afisa aliyewajibishwa. Rais wa Chama cha Wahariri Kenya, Zubeida Kananu, alisema kushindwa kuwachukulia hatua wahusika wa mashambulizi ya awali kumewapa ujasiri wanaowalenga wanahabari. Viongozi hao pia walielezea wasiwasi kuhusu kushuka kwa Kenya katika orodha ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ya Reporters Without Borders (RSF). Kenya imeshuka kutoka nafasi ya 69 mwaka 2022 hadi ya 106 kati ya nchi 180. Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOA) pia kimetaka kufanywe uchunguzi huru, wa haraka na wa wazi. Mwenyekiti wake Agnes Kalekye alisema chama hicho kimehuzunishwa na tukio hilo lakini kimefarijika kwamba Bw Kiprotich alipatikana akiwa hai. Alisisitiza kuwa wanahabari wanapaswa kuruhusiwa kutekeleza majukumu yao bila vitisho au kuingiliwa. Rebecca Mutiso, meneja wa Uhuru wa Vyombo vya Habari na Utetezi katika Baraza la Vyombo vya Habari Kenya, aliwataka watu walio na malalamishi kutumia njia halali za kuyatatua badala ya kuwalenga wanahabari. “Leo unataka kumnyamazisha mwanahabari, lakini itakuwaje haki zako zitakapokiukwa na uhitaji mwanahabari huyo huyo kuripoti kisa chako?” akauliza. Amnesty International Kenya pia imetaka uchunguzi huru na wa uwazi, ikisema tukio hilo ni tishio kubwa kwa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imewafutia makosa baadhi ya wasanii na watengeneza maudhui mtandaoni waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa taratibu na maadili.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka nchi wanachama wa Harakati za Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) kuunganisha sauti na misimamo ili kuongeza ushawishi katika maamuzi ya kimataifa na kutetea maslahi ya nchi zinazoendelea.

MMOJA wa wanasiasa ambaye anategemewa kwa mustakabali wa umoja wa upinzani ni Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi. Zipo sababu kadhaa zinazomkweza Caroli katika siasa Kenya inapojiandaa katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 10, 2027. Kwanza, yeye ndiye msemaji wa kundi la Linda Mwananchi linaloongozwa na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na washirika wake. Pili ni katibu mkuu wa muungano wa Azimio, vyama ambavyo viliunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2022. Moja ya sifa kubwa ya Caroli ni kuwa msemaji bora wa lugha zote mbili ila Kingereza chake kinashuka taratibu na kwa ufundi mkubwa. Inawezekana Linda Mwananchi ilimteua bila kufahamu usuli wake vizuri. Caroli ana tajiriba kubwa ya upatanishi na alikuwa kiungo muhimu kwa upande wa aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila wakati wa mazungumzo baada ya ghasia za uchaguzi za 2007/2008. Katika mahojiano yangu awali kidogo, aliniambia zile wanazoita mitaani “za ndani” yaani habari ambazo ni siri. Ila sasa Caroli ana jukumu kubwa mno kupita Edwin Sifuna, Babu Owino, James Orengo na kundi lile jingine la Kalonzo Musyoka. Anatakiwa kuhakikisha makundi haya yanapatana na mgombea mmoja kukabiliana na Rais William Ruto ambaye anataka ridhaa nyingine ya Wakenya. Awali nyufa zimeanza kujitokeza katika kundi la Linda Mwananchi kuhusu anayestahili kuwa kiongozi wa chama na hata mgombea Urais. Pili, Kalonzo, Gachagua na washirika kila mtu anapaza sauti kuwa anatosha kuongoza Kenya. Tatu anatoka eneo la Nyanza ambalo linadai kuwa Raila Odinga aliwaacha kwa serikali jumuishi. Caroli alionyesha makali yake kwa kufanikisha ziara ya Linda Mwananchi katika kaunti ya Homa Bay. Pamoja na kuwa kulikuwa na vurugu kubwa na kusababisha maafa, kikosi cha Caroli kilifanikiwa kuuza sera kwa wakazi wa Homa Bay licha ya kuwepo kwa vitisho kutoka kwa wafuasi wa Gavana Gladys Wanga ambaye ndiye mwenyekiti wa chama cha ODM. Moja ya dhima muhimu inayomsubiri ni kufifisha nguvu za ODM ambazo wahafidhina kutoka eneo lake hawadhanii kuwa ni jambo linalowezekana kwa wepesi. Ruto alipo anajua uwezo wa ungaunga za Caroli. Upinzani nao una mtihani mkubwa kumpa dhamana ya kusimamia mchakato wa kuupatanisha na kusalia kama gundi endapo watataka kuwa wenyeji wa ikulu. Wafuasi wa Sifuna wanamtaka debeni, Matiang’i anasema ataikomboa nchi, Kalonzo ana huu wakati pekee huku Gachagua akijigamba kuwa nyota yake inaangaza. Kazi kwa Caroli. Je, ataonyesha njia ya upinzani ya 2002? Paul Nabiswa ni mhariri, NTV

LUSAKA, Zambia: RAIS wa Zambia Hakainde Hichilema Jumanne aliapishwa rasmi kwa muhula wake wa pili huku mpinzani wake mkuu akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini. Kuapishwa kwake kumekamilisha mchakato wa uchaguzi wa Agosti 13 ambao waangalizi walisema ulikumbwa na dosari kubwa na ukiukaji wa haki. Hichilema aliingia madarakani mnamo 2021 akiahidi kurejesha demokrasia baada ya kuishutumu serikali iliyotangulia kwa kuiba uchaguzi na kuwafunga wapinzani. Hata hivyo, waangalizi wa uchaguzi wa ndani na kimataifa wameripoti dosari kadhaa katika uchaguzi huo, zikiwemo madai ya udanganyifu katika hesabu za kura, kukamatwa kwa wabunge wa upinzani, wanajeshi kuwekwa katika vituo vya kupigia kura na kufungwa kwa mahakama. Mpinzani wake Brian Mundubile na mgombea mwenza wake Makebi Zulu pia walishtakiwa kwa uhaini mwishoni mwa wiki. Zambia, inazalisha shaba kwa wingi, imekuwa kitovu cha ushindani kati ya China na Amerika kutokana na utajiri wake wa madini. Nchi hizo mbili zilimpongeza Hichilema kwa ushindi wake na kutuma wawakilishi kwenye hafla ya kuapishwa kwake. Zambia imekuwa ikifanya uchaguzi tangu miaka ya 1990 ilipokumbatia mfumo wa vyama vingi, ingawa baadhi yake imekuwa na dosari. Wachanganuzi wanaonya kuwa uchaguzi huu unaweza kuweka mfano utakaowawezesha viongozi wa baadaye kujilazimisha madarakani badala ya kuimarisha demokrasia. “Hadhi ya Zambia ya kidemokrasia iko hatarini. Hatujawahi kushuhudia mkanganyiko wa aina hii,” akasema mwanahistoria Euston Chiputa. Alikuwa akirejelea kusimamishwa kwa kuhesabiwa kura, kuwekwa kwa wanajeshi katika vituo vya kuhesabia kura na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani. Waangalizi wa uchaguzi walisema kulikuwa na dalili za kuongezwa kwa kura katika hesabu ya Hichilema, ingawa walikubaliana kuwa angeshinda hata bila kura hizo zinazodaiwa kuongezwa. Tume ya Uchaguzi ya Zambia ilisema madai yoyote ya udanganyifu yanapaswa kuwasilishwa mahakamani. Kinaya ni kwamba mahakama ilifungwa siku ya mwisho ya kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo. Baadaye zilisema hakuna malalamishi yaliyowasilishwa. Serikali pia haijatoa maelezo ya kutosha kuhusu mashtaka dhidi ya Mundubile na viongozi wengine 12 wa upinzani waliotiwa gerezani. Licha ya machafuko ya kisiasa, wawekezaji bado wanaendelea kuonyesha imani kwa uchumi wa Zambia. Hichilema aliongoza mchakato wa kupunguza deni na kuimarisha uchumi katika muhula wake wa kwanza, hatua iliyomfanya kuwa chaguo linalopendelewa na wawekezaji wanaotaka mwendelezo wa sera. Hata hivyo, mtafiti wa Chatham House Christopher Vandome alisema mafanikio ya kiuchumi ya muda mfupi hayawezi kuficha madhara ya muda mrefu ya kuangamiza taasisi za kidemokrasia.

DODOMA; Serikali imetaja hatua mbalimbali inazochukua kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhamasisha michezo kwa watu wenye ulemavu. Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Septemba 2, 2026 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Nyamizi Mhoja, aliyehoji serikali ina mkakati gani wa kuendeleza michezo…

DODOMA; Serikali imesema itaendelea kufanya maboresho ya sheria, ili kuhakikisha kuwa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 iliyopitishwa na Bunge inatekekelezwa ipasavyo. Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Septemba 2, 2026 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, alipokuwa akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2026. “kwa mara nyingine naomba, kwa…

DODOMA; Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283, ili kuweka masharti kuhusu uhifadhi, usimamizi, ulinzi na matumizi endelevu ya wanyamapori. Sheria hiyo ni miongoni mwa sheria saba zilizopo kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2026 uliowasilishwa leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,…

Events from the 2025 General Election emerged in the treason trial of Chadema national chairman Tundu Lissu, as state prosecutors questioned a defence witness over the poll and post-election violence.

Dr Emmanuel Nchimbi is undeniably not the first political heavyweight within the ruling CCM to suffer the ultimate sanction of expulsion.

GEITA: CHATO District Commissioner, Mr Louis Bura, has called on the Occupational Safety and Health Authority (OSHA) to scale up inspection and advisory services to match rising demand driven by rapid economic growth in the district. He made the call during the opening of an occupational safety and health training for welders and carpenters at…

MZOZO wa bajeti kati ya Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti na baadhi ya madiwani wa Bunge la Kaunti umechacha baada ya gavana huyo kukataa marekebisho yaliyofanywa kwenye bajeti ya Sh17.8 bilioni ya mwaka wa kifedha wa 2026/2027. Hatua hiyo imeibua makabiliano mapya katika Bunge la Kaunti, huku madiwani wakiwa na chini ya wiki mbili za kutathmini upya uamuzi wa kupunguza Sh853 milioni kutoka kwa bajeti hiyo. Bi Ndeti aliwasilisha barua ya kupinga marekebisho hayo alipofika katika Bunge la Kaunti Jumatatu akiwa ameandamana na Katibu wa Kaunti Muya Ndambuki, Waziri wa Fedha Catherine Mutanu na maafisa wengine wakuu. Alimkabili Karani wa Bunge la Kaunti Peter Mbatha, akimshtumu kwa kushirikiana na Spika Anne Kiusya kumzuia kuwasilisha mapendekezo yake. “Kwa nini usipokee tu barua hiyo kama sheria inavyohitaji na uniachie nikabiliane na madiwani?” akamuuliza Bw Mbatha. Baada ya barua hizo kupokewa, Bi Ndeti alisema hawezi kuidhinisha bajeti iliyorekebishwa kwa sababu inatishia huduma muhimu kwa wakazi. “Siwezi kutia saini bajeti inayokiuka wazi mipaka iliyowekwa kisheria, kubomoa huduma muhimu za umma na kuhatarisha moja kwa moja maisha ya watu wetu,” akasema. Marekebisho hayo yameathiri zaidi fedha za miradi ya barabara na baadhi ya mipango muhimu ya gavana, ikiwemo Huduma ya Vijana ya Machakos, mpango wa maziwa kwa watoto wa shule za chekechea na mpango wa mikopo nafuu uliotengewa Sh100 milioni. Bi Ndeti anasema kupunguzwa kwa fedha kutalemaza utoaji wa huduma, huku madiwani wanaomuunga mkono wakisisitiza kuwa walifanya marekebisho hayo baada ya kuchunguza matumizi yenye utata. “Gavana anaita mabadiliko haya kupunguzwa kwa bajeti. Sisi tunaita uchunguzi wa bajeti, kuweka kipaumbele upya na kugawa fedha upya. Tunapinga ubadhirifu na kurudiwa kwa miradi. Tunataka thamani ya fedha,” akasema Diwani wa Kalama, Bw Boniface Maeke. Mzozo huo unaendeleza mvutano wa kisiasa kati ya Bi Ndeti na baadhi ya madiwani. Waziri wa Fedha, Bi Mutanu amekuwa katikati ya mzozo huo baada ya kufutwa kazi na gavana Julai, siku ambayo Bi Ndeti alikabiliwa na hoja ya kumtimua. Bi Mutanu alirejeshwa kazini wiki moja baadaye baada ya Mahakama Kuu kuingilia kati. Mzozo wa sasa ulianza baada ya Bunge la Kaunti kuruhusu gavana kutumia asilimia 50 ya bajeti ya 2026/2027 kusubiri kupitishwa kwa Mswada wa Matumizi.

WAUGUZI wanaoendelea na mgomo katika Kaunti ya Kisii, jana walishambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wahuni walipokuwa wakijiandaa kushiriki mgomo wa amani na kuwasilisha malalamishi yao kwa serikali ya kaunti hiyo. Walishambuliwa katika uwanja wa Hospitali ya Rufaa ya Kisii, tukio ambalo viongozi wa muungano wao walilikemea na kulitaja kuwa la kuhofisha mno. Wauguzi ambao hawakutaka kutajwa, walisema wanaume wapatao 40 waliojihami kwa mipini ya majembe walivamia walipokuwa wakijiandaa kuandamana. Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi (KNUN), Seth Panyako, alitaja shambulizi hilo kuwa la kipuzi, akilalamika kuwa polisi waliofahamishwa awali kuhusu mipango ya maandamano hayo walifeli kuwalinda wauguzi. “Polisi Kisii wameingiliwa. Tulitoa notisi bayana kwa polisi kuwa tutafanya maandamano ya amani. Maafisa wa polisi walikuja lakini badala ya kutoa ulinzi, waliagiza wauguzi kuondoka, wakisema ikiwa watakaidi, wahuni hao wa kulipwa wataachiliwa kwao,” akasema Bw Panyako akihutubia vyombo vya habari. “Tunalaani vikali tukio hili. Tunauliza polisi mjini Kisii kwa nini waliruhusu wahuni kushambulia wauguzi wasio na fujo, kana kwamba hawaugui. Hatutakuwa na huruma kwa wasio na huruma nasi. Sisi ni wauguzi; wanaweza kuwa na bunduki na silaha, lakini tunaweza pia kuwa hatari.” Homabay, wauguzi wameapa kukaidi wito wa Baraza la Magavana (CoG) kurejea kazini huku majadiliano yakiendelea. Mwenyekiti wa Baraza, Bw Ahmed Abdullahi, aliwahimiza wauguzi nchini kote kurejelea majukumu yao huku magavana wakishughulikia malalamishi yao. Gavana huyo wa Wajir, alisema baraza limejadili Mkataba wa Makubaliano kuhusu Malipo (CBA) lakini baadhi ya kaunti zimeshindwa kuutekeleza, huku wauguzi wakisema hawatasikiza ombi hilo. Mkurugenzi wa Muungano Kitaifa wa Wauguzi na Wakunga (KNUNM) tawi la Homa Bay, Emmadick Okeyo, alisema kususia kazi ndiyo hatua yao. “Hatutarejea kazini hadi malalamishi yetu yatakaposhughulikiwa,” akasema Bw Okeyo. Mwenyekiti wa tawi hilo, Bw Enock Ocharo aliitaka CoG kukoma kuwatishia wauguzi. “CoG ijishughulishe na kuangazia malalamishi yetu. Vitisho wanavyotoa havina athari yoyote,” akasema Bw Ocharo. Kisumu, baadhi ya wagonjwa wanageukia maduka ya kuuza dawa huku mgomo unaoendelea wa wauguzi ukitatiza huduma katika hospitali ya rufaa Kisumu. Wauguzi wanataka mkataba wao wa CBA utiwe saini ili uthibitishwe kisheria. Mkataba huo unatoa mwongozo kuhusu maendeleo kitaaluma, marupurupu na malipo mengineyo. Aidha, wanataka wenzao walioajiriwa chini ya mpango wa Afya kwa Wote (UHC) wakati wa hatamu ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuajiriwa kwa kandarasi za kudumu. Wauguzi wa UHC kwa sasa wameajiriwa kwa kandarasi za muda. Wanaitisha vilevile utekelezaji kamili wa Muafaka wa Kurejea Kazini 2017 uliotiwa saini kati ya muungano wao na CoG.

WANASIASA wanaounga mkono serikali kutoka Nyanza na Magharibi wametangaza mipango ya kuendesha kampeni za pamoja kwa lengo la kumwezesha Rais William Ruto kupata kura milioni 7 maeneo hayo 2027. Mpango huo unalenga kuvutia kura katika ngome za kisiasa za marehemu Waziri Mkuu Raila Odinga chini ya Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi. Sehemu ya mikakati hiyo pia ni kushinikiza watengewe nafasi ya Naibu Rais. ODM imependekeza Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya kama mmoja wa wanaoweza kuchukua nafasi ya Profesa Kithure Kindiki. Luo Nyanza, inayojumuisha kaunti za Kisumu, Migori, Siaya na Homa Bay, ina wapiga kura milioni 2.41 kwa mujibu wa sajili ya sasa ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC). IEBC inakadiria idadi hiyo kufikia milioni 2.78 katika uchaguzi wa Agosti 10, 2027. Magharibi nayo ina kaunti za Kakamega, Busia, Bungoma, Vihiga na Trans Nzoia zina wapiga kura milioni 2.9 kwa sasa, huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia milioni 3.4 ifikapo uchaguzi ujao. Hata hivyo, mpango huo unakabiliwa na upinzani kutoka kwa vuguvugu la Linda Mwananchi, ambalo limekuwa likipata umaarufu katika maeneo hayo. Baadhi ya viongozi wa Magharibi, akiwemo Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Seneta wa Kakamega Boni Khakwale, wamejipanga kumuunga mkono Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kwa urais. Nyanza pia inapitia mabadiliko makubwa ya kisiasa tangu kifo cha Bw Odinga. Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi wameungana na Bw Sifuna kupinga ushawishi wa uongozi wa sasa wa ODM. Hata hivyo, washirika wa Rais Ruto wanasema wataunganisha jamii za Luo na Luhya ili kumuunga mkono katika uchaguzi wa 2027. Jamii hizo kwa kiasi kikubwa zilimuunga mkono Bw Odinga katika uchaguzi wa 2022.

GAVANA wa Siaya James Orengo amemtaka Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na wagombeaji wengine ndani ya Linda Mwananchi kukubali uteuzi wa wazi wanaposaka mwaniaji wao wa urais kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Katika mahojiano na Taifa Leo Jumanne, Bw Orengo alisema hana tatizo kushindana na Bw Sifuna au mgombea mwingine yeyote wa upinzani. Alisisitiza jambo muhimu ni kuhakikisha vuguvugu hilo linapata mgombea mmoja wa kukabiliana na Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027. “Hakuna ubaya kwa wagombea mbalimbali kuwa na azma ya urais ndani ya Linda Mwananchi au upinzani. Muhimu ni kuwapa wote fursa ya kupitia mchakato wa uteuzi wa wazi na wa kuaminika, ili hatimaye tupate mgombea mmoja wa kukabiliana na Ruto. Huo ndio msingi wa umoja wa upinzani,” akasema Bw Orengo. Gavana huyo mkongwe alisisitiza kuwa uteuzi haupaswi kuamuliwa katika vikao vya siri, akitaja uchaguzi wa urais wa ODM wa 2007 ambapo Raila Odinga, William Ruto, Musalia Mudavadi, Najib Balala na Joe Nyaga walishindana kabla ya chama kumpata mgombea wake. Alitaja pia uchaguzi wa 2002, ambapo vyama vya upinzani vilifanya mashauriano kabla ya Bw Odinga, aliyekuwa akiongoza LDP, kumuunga mkono Mwai Kibaki kupitia kauli ya “Kibaki Tosha”. Bw Orengo alisema mifano hiyo inaonyesha kuwa umoja wa upinzani hauhitaji kuondoa mapema azma za wagombea mbalimbali wenye nia ya kusaka urais. Ingawa hivyo, msimamo wake umemweka pabaya na washirika wa Bw Sifuna, ambao wamekuwa wakisema wafuasi wa Linda Mwananchi tayari wameamua kumuunga mkono seneta huyo wa Nairobi. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ni miongoni mwa viongozi wa Magharibi waliomuunga mkono Bw Sifuna na kusema wananchi wamekuwa wakisema “Sisi Ndio Sifuna” katika mikutano ya vuguvugu hilo. Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga alisema hakuna haja ya kuchanganya wafuasi kwa kujitokeza kwa wagombea wengine. “Hatupaswi kuchanganyikiwa. Wakenya wamejitokeza katika kila mkutano wa Linda Mwananchi na kusema wanamtaka Edwin Sifuna kuwa mgombea wa urais,” akasema Bw Kalasinga. Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, hata hivyo, alisema vuguvugu hilo linamheshimu Bw Orengo kutokana na uzoefu wake wa kisiasa na mchango wake katika masuala ya mageuzi. “Vuguvugu linamheshimu sana Gavana Orengo kutokana na hadhi na uzoefu wake mkubwa katika masuala ya mageuzi,” akasema Bw Osotsi, akiongeza kuwa kutakuwa na utaratibu wa kutatua suala hilo wakati ufaao. Mwanasiasa wa Jubilee Pauline Njoroge pia akiongea katika Kaunti ya Meru wakati wa mkutano wao wa kisiasa alisema suala la mgombeaji wao wa urais lishaamuliwa. “Wafuasi wetu wameweka wazi kuwa wanayemtaka ni Sifuna. Hilo limethibitishwa kupitia mikutano yetu maeneo mbalimbali nchini,” akasema Bi Njoroge. Bw Orengo pia alisema jamii mbalimbali zina haki ya kufanya mashauriano kuhusu maslahi yao ya kisiasa, akitaja mijadala inayoendelea Mlima Kenya na Ukambani. Kando na kambi ya Bw Sifuna, azma ya Bw Orengo pia imewachemsha viongozi kutoka Nyanza wanaounga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto. Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amemshutumu Bw Orengo kwa kutumiwa kugawanya kura za Waluo, akilinganisha hali hiyo na uchaguzi wa 2002. “Jinsi alivyotumiwa na Daniel arap Moi kugawanya kura zetu 2002, sasa anatumika tena na Uhuru kugawanya kura zetu, lakini hilo halitatokea,” akasema Bw Wandayi. Waziri huyo pia alisema viongozi wa Siaya wamekubaliana kumuunga mkono Rais Ruto na sasa wanamakinikia usajili wa wapiga kura. Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga, pia amepuuzilia mbali uwezekano wa Bw Orengo kushinda urais, akisema hana umaarufu wowote wa maana nchini. Huku mjadala ukiendelea, Linda Mwananchi pia inajaribu kujigeuza kutoka jukwaa la kisiasa hadi chama kitakachoshiriki uchaguzi wa 2027. Hata hivyo, ombi lake la kuhifadhi jina Linda Mwananchi Party lilikataliwa na Afisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, hatua ambayo imeongeza changamoto kwa vuguvugu hilo. Bw Orengo pia alitetea uamuzi wake wa kukosa mkutano wa Linda Mwananchi Meru mnamo Jumapili akisema haikuhusiana na ubabe kati yake na Bw Sifuna. “Nilikuwa na shughuli nyingine nzito na Babu aliwasilisha salamu na udhuru wangu. Bado namakinikia wazo la kuwa na mgombeaji mmoja wa upinzani,” akasema. Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Chris Omore naye anasema ukosefu wa chama thabiti huenda ukalemeza azma ya Mabw Orengo na Sifuna kumpa Rais Ruto upinzani mkali 2027.

TANGAZO la Gavana wa Siaya, James Orengo, kwamba analenga kuwania urais wa Kenya mwaka 2027 kupitia vuguvugu la Linda Mwananchi linatibua donda jipya katika siasa za upinzani nchini. Hatua hiyo inazua maswali mazito kuhusu mustakabali wa upinzani, urithi wa kisiasa wa Raila Odinga na hatima ya siasa za Nyanza baada ya kuondoka kwa mwanasiasa huyo aliyekuwa mhimili wa eneo hilo kwa miongo kadhaa. Si mara ya kwanza Orengo anaonekana kuwa na msimamo tofauti na wanasiasa wengine katika chama. Historia yake na Raila ni ya ushirikiano uliochanganyika na ushindani wa kisiasa na tofauti za kimtazamo. Orengo si mgeni katika siasa za urais; aliwahi kuwania kiti hicho mwaka 2002, wakati Raila naye alikuwa akijenga ushawishi wake katika siasa za kitaifa kisha kushirikiana naye tena katika serikali pana. Kwa mtazamo wa kisiasa, ushirikiano huo haupaswi kutafsiriwa kama kutoweka kwa tofauti zao za kimkakati. Orengo alilazimika kufanya kazi ndani ya mfumo ambao tayari ulikuwa na kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kisiasa kumzidi baada ya kivuli cha Raila kumfunika na kumzidi uwezo. Orengo huenda aliona kuwa ushindani wa moja kwa moja dhidi ya Raila ungeweza kupunguza nafasi yake ya kisiasa. Pengo la kuondoka kwake Raila limempa ujasiri wa kuibuka na sasa anaonekana kutaka kuwa mmoja wa wahusika wakuu katika mapambano hayo. Kujikita kwake katika Nyanza kupitia Linda Mwananchi kunaweza kutafsiriwa kama mkakati wa kujenga kituo kipya cha mamlaka ambacho kinaweza kushindana moja kwa moja na ODM na uongozi wake wa sasa. Katika hatua za awali za Linda Mwananchi, Orengo alionekana kumuunga mkono Edwin Sifuna katika matarajio yake ya kuwania urais. Sifuna amekuwa akijijenga kama sura mpya ya kisiasa yenye uwezo wa kuvuka mipaka ya ODM na kuunganisha kizazi kipya cha wapiga kura. Sasa Orengo anabadili rangi na kuvalia ngozi ya mgombea wa urais chini ya mwavuli huo huo. Je, Orengo amebadilisha wazo lake, au ameingia katika mradi wa Sifuna akiwa na njama tofauti ya baadaye? Kwa wafuasi wa Sifuna, hii inaweza kuonekana kama usaliti wa kisiasa. Kwa upande wa Orengo, inaweza kutetewa kama haki yake ya kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa nchi. Changamoto kubwa sasa ni iwapo Linda Mwananchi inaweza kubeba matarajio mawili ya urais bila kugawanyika. Ikiwa Orengo na Sifuna watashindwa kufikia makubaliano kuhusu uongozi, vuguvugu hilo linaweza kugeuka kutoka chombo cha kuunganisha upinzani na kuwa uwanja wa mapambano ya madaraka. Kwa Orengo tajriba yake ya kisiasa na ujasiri wa kupambana dhidi ya mababe wa kisiasa sharti itazamwe kwa jicho la pili. Hii ni fursa yake kujijenga kama mrithi wa nafasi ya kisiasa iliyoachwa wazi na Raila. Lakini pia ni kamari kubwa. Hesabu zake Orengo kogombea kiti cha urais zinaweza kutia pilipili katika macho ya Sifuna na viongozi wenza katika ndoto ya kuwania urais. Pambano kuelekea 2027 halitakuwa tu upinzani dhidi ya rais Ruto. Itakuwa pia vita vya ni nani atadhibiti urithi wa Raila, ni nani atamiliki Nyanza kisiasa, na nani atakuwa uso mpya wa upinzani nchini Kenya.

Kigoma Urban Member of Parliament (CCM) Clayton Chipando, popularly known as Baba Levo, will be forced to return to court following the High Court’s decision to set aside a Sh100 million award he won in a defamation suit against Webiro Wasira.

Police in Arusha Region have confirmed that they detained activist and Gifted Heart Foundation (GH Foundation) executive director, Mr Godlisten Malisa, over criminal allegations under investigation, after a lawyer and the opposition political party Chadema Western Zone chairman Dickson Matata raised concerns about his whereabouts. Arusha Regional Police Commander Justine Masejo said Mr Malisa was arrested on Monday night, August 31, 2026, alongside another person and was later released on bail after questioning. “Arusha Regional Police Command arrested Godlisten Malisa and another person on the night of August 31, 2026, over criminal allegations that were under investigation against him,” said a statement released on Tuesday, September 1, 2026, signed by Commander Masejo. “After questioning, they were released on bail pending completion of other legal procedures,” added the regional police chief. The police confirmation followed reports on social media that Mr Malisa had been detained after returning to Tanzania from the United States through Kenya. Mr Malisa, a human rights advocate, had spent more than nine months in the United States, where he attended leadership training after being selected by the US Department of State. According to Mr Matata, Mr Malisa arrived in Nairobi on Monday morning but was unable to continue his journey to Tanzania by air because of an ongoing workers' strike at Jomo Kenyatta International Airport. He said Mr Malisa subsequently travelled by road to Namanga, on the Tanzania-Kenya border, to enter the country before continuing to Arusha. Mr Matata said Mr Malisa arrived at Namanga at about 3 pm and proceeded to the immigration offices to have his passport stamped as required before entering Tanzania. “After reaching the immigration officers, they took his passport and told him it could not be read by the system, so they could not do anything until their officer in charge arrived to check the system,” he said. Mr Matata said Mr Malisa remained at the immigration offices waiting for the officer in charge to resolve the problem with the passport. However, he alleged that at about 7 pm, his client was taken away in a white double-cab vehicle that did not belong to the law enforcement organ, but was driven to Longido Police Station. “However, the vehicle did not stay there for long before leaving towards Arusha,” alleged Mr Matata. The lawyer said the circumstances surrounding Mr Malisa’s movement from the immigration offices raised concerns about his safety and whereabouts, prompting him to call on the police and immigration authorities to provide an explanation. Mr Matata also called on the authorities to clarify why Mr Malisa had been taken into custody and whether there was a legal basis for his detention. Human rights defenders also raised similar concerns, demanding an official explanation from the authorities. Following Mr Matata’s statement, the Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) said on Monday that it was closely following reports of his detention and his transfer to Longido Police Station after spending several hours at the immigration offices in Namanga. The organisation said it had contacted Mr Matata, who told it that he was in Arusha following up on the matter. “THRDC calls on the police and immigration authorities to immediately provide official information on where Malisa is being held, the reasons for his detention and the legal basis for the action,” said the THRDC national coordinator, Mr Onesmo Olengurumwa. The coalition also urged the authorities to ensure Mr Malisa’s safety and respect his rights while in custody. It called for him to be allowed to communicate with his family and have access to his lawyers without restriction. The concerns emerged against the backdrop of Mr Malisa’s return to Tanzania after spending more than nine months in the US, where he had been undertaking leadership training following his selection by the US Department of State. His return journey took him through Kenya, with the disruption at Jomo Kenyatta International Airport forcing him to travel by road towards the Tanzania-Kenya border, according to Mr Matata.

DODOMA; Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026). Muswada huo uliwasliishwa bungeni leo Septemba 1, 2026 asubuhi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, aliyesema mapendekezo ya marekebisho ya sheria 21 ni miongoni mwa hatua muhimu za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa…

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho. Akiwasilisha muswada huo leo Septemba Mosi, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ametaja miongoni mwa sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura…

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho. Akiwasilisha muswada huo leo Septemba Mosi, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ametaja miongoni mwa sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za…

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho. Akiwasilisha muswada huo bungeni leo Septemba 1, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, amesema marekebisho ya sheria ni miongoni mwa hatua muhimu za Serikali katika kuweka mazingira…

MOROGORO: MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timotheo Mnzava, ameitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza nguvu katika kuboresha na kupanua Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) ili kiweze kuongeza uwezo wa kuzalisha wataalamu wengi katika sekta ya ardhi. Aidha, ameitaka Wizara hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka…

DODOMA; Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi amehoji bungeni mkakati wa serikali kuhakikisha taaluma na kazi ya udereva inakuwa na staha, hadhi na heshima sawa na kada nyingine. Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi yya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray amesema serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha taaluma na kazi ya…

JAMII ya Waluo inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa uongozi, wazee wakigawanyika katika makundi mawili yanayodai kumtambua kiongozi halali wa Baraza la Wazee wa Waluo. Upande mmoja unaongozwa na Nyandiko Ongadi huku mwingine ukiongozwa na Odungi Randa. Wote wanajitambua kuwa Ker halali na walezi wa utamaduni wa jamii hiyo. Mzozo huo umedumu kwa zaidi ya miaka 10 na sasa umeenea hadi mashinani, ambako baadhi ya wazee wamejiunga na Bw Ongadi huku wengine wakimuunga mkono Bw Randa. Mgawanyiko huo umeibua wasiwasi kwamba baraza hilo limepoteza ushawishi wake katika masuala ya jamii, hasa siasa na uongozi. Kiongozi wa Bunge la Wananchi Homa Bay Walter Opiyo, alisema baraza hilo haliwezi tena kutoa mwelekeo wa kisiasa kama ilivyokuwa awali. Alisema ushawishi wa baraza hilo uliimarishwa zaidi na aliyekuwa kiongozi wa ODM, marehemu Raila Odinga. “Raila alikuwa mwanasiasa pekee aliyejulikana kwa kuendeleza utamaduni. Kifo chake kilifuta yote hayo na sasa baraza limeachwa bila ushawishi wa kisiasa,” akasema Bw Opiyo. Mkazi wa Kakuajuok, Zedekiah Ouma, alikosoa baadhi ya wazee kwa kuruhusu wanasiasa kuwashawishi kwa fedha. “Tofauti na wazee wa jamii nyingine kama Wamaasai, wazee wa Luo wamepoteza mwelekeo,” akasema. Hata hivyo, mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma alitetea baraza hilo, akisema si taasisi ya kisiasa. “Baraza halijihusishi na siasa na nadhani katiba yao haiwaruhusu kushiriki siasa. Wale unaowaona pamoja na wanasiasa ni baadhi ya wazee wa ukoo ambao wamealikwa na uwepo wao hauwakilishi baraza,” akasema Bw Kaluma. Mzozo huo ulizuka baada ya kifo cha Ker Riaga Ogalo mnamo Agosti 2015. Bw Ongadi, aliyekuwa naibu wake, aliteuliwa katika hafla iliyofanyika Ofafa Memorial Hall. Hata hivyo, Bw Randa alichaguliwa kuwa Ker wakati wa Tamasha la Piny Luo Homa Bay mnamo Julai 2023, na kutawazwa rasmi Disemba 22, 2023. Uteuzi huo ulipingwa vikali na kundi la Bw Ongadi. Bw Ongadi, ambaye anatoka Kendu Bay, Karachuonyo, anasisitiza kuwa yeye ndiye Ker halali kwa sababu anamiliki cheti cha usajili wa baraza pamoja na hati za wadhamini. Bw Ongadi pia amesema anapanga kuwaongoza wazee hadi Got Ramogi kwa ajili ya maombi ya kuunganisha jamii. Hata hivyo, Bw Randa amesema anaunga mkono mazungumzo ya kuleta amani lakini akasisitiza kuwa yeye ndiye Ker halali. Alimshutumu Bw Ongadi kwa kushikilia stakabadhi za baraza na kusema hakuwepo wakati yeye alipochaguliwa 2023.

UFICHUZI wa aliyekuwa Waziri wa Leba, Bw Kazungu Kambi, kwamba anapanga kuzindua chama kipya cha kisiasa, umeibua mwelekeo mpya wa kisiasa katika eneo la Pwani kuelekea kwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Kulingana na Bw Kambi, Rais William Ruto alipokutana naye katika Ikulu ya Nairobi mnamo Julai alimuuliza iwapo alikuwa na chama, akamwambia kuna vyama vitatu ambavyo angechagua kimoja kwa ajili ya mpango wake wa kuwania ugavana Kilifi. Picha za mkutano huo zilisababisha mdahalo mkali ziliposambazwa mitandaoni, hasa ikizingatiwa kuwa mbunge huyo wa zamani wa Kaloleni wiki chache awali alikuwa mmoja wa wajumbe wa Mijikenda waliokutana na kinara wa Chama cha Democray for the Citizens Party (DCP), Bw Rigathi Gachagua, katika Kaunti ya Kwale. “Nilipoitwa na Rais Ruto hivi majuzi, tuliongea kuhusu siasa. Aliniuliza kama nina chama. Nilimwambia kuna vyama vitatu na nitachagua kimoja ambacho tutakizindua rasmi hivi karibuni. Ni chama cha wakenya, si cha Wamijikenda pekee,” alisema, kwenye mahojiano ya redio. Bw Kambi alisema chama hicho kinalenga kuwaleta pamoja watu wote wanaoishi Pwani, na viongozi watakuwa kutoka jamii zote nchini. “Mimi nataka umoja wa Pwani kwa sababu kwa sasa hatuna umoja. Tuna utajiri, lakini tatizo la umaskini Pwani si watu wa nje. Tatizo ni sisi wenyewe, Wapwani. Kitu cha kwanza, hatupendani; pili, tuna fitina,” alisema. Hatua hiyo imetokea wakati ambapo vyama vingi vya kisiasa vilivyoanzishwa Pwani vimekosa nguvu. Chama cha Pamoja African Alliance (PAA) ambacho kiliundwa kabla uchaguzi uliopita, kiliamua hakitasimamisha wagombeaji katika uchaguzi ujao na badala yake kitaunga mkono wagombeaji wa UDA. Hatua hiyo imewaacha wanasiasa waliokitumia kuwania viti 2022 na waliotarajia kukitumia mwaka ujao katika njiapanda, huku wengine wakilazimika kutafuta vyama vipya. Bw Kambi alisema aliporejea katika siasa alijaribu kufufua vyama vya Kadu-Asili na Shirikisho kwa kushirikiana na wamiliki wa awali, lakini juhudi hizo hazikufanikiwa, hali iliyowalazimu kuanzisha chama kipya. Aliongeza kuwa, hatua ya PAA imeathiri mipango mingi ya siasa za Pwani. “Sitaki kudandia chama cha mtu, nataka tuwe na chama chetu. Tulikuwa na Shirikisho ambacho kilianzishwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Bw Chirau Makwere lakini kilinunuliwa,” alisema. Alisema dhamira yake ni kusaidia wakazi wa Kilifi na kuimarisha umoja wa Pwani. Bw Kambi pia alionya dhidi ya siasa za ukabila na ubaguzi, akisema jamii zote zinazoishi Pwani zinapaswa kuchukuliwa kuwa wenyeji. Alimpongeza Bw Gachagua kwa kuanzisha chama chake na kutetea maslahi ya watu wa Mlima Kenya, akisema kila jamii ina haki ya kuwa na jukwaa la kisiasa la kuwasilisha maslahi yake. “Ni Wapwani peke yao ambao wamekuwa na vyama lakini hawako pamoja,” alisema.

CHAMA cha ODM kinakabiliwa na kibarua kigumu katika kuamua mgombea wake wa ugavana Nairobi baada ya baadhi ya wabunge kujitokeza hadharani kumuunga mkono Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, anayehusishwa na mrengo wa Linda Mwananchi. Hii ni licha ya mbunge wa Makadara George Aladwa, ambaye ni mwenyekiti wa ODM katika Kaunti ya Nairobi, kutangaza azma yake ya kuwania kiti hicho. Gavana Johnson Sakaja naye anadaiwa anatathmini iwapo atawania ugavana kupitia ODM. UDA na ODM zinapanga kushirikiana kisiasa, kugawana nafasi na kuimarisha ushawishi wao katika jiji kuu kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Mwishoni mwa wiki, Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ alitangaza hadharani kumuunga mkono Bw Owino, ambaye ametofautiana na uongozi wa ODM na anahusishwa na mrengo wa Linda Mwananchi unaoongozwa na Edwin Sifuna na James Orengo. “Babu usifanye mzaha na Nairobi, ichukue Nairobi,” akasema Bw Kajwang’ akiwa Oyugis huku umati ukishangilia. Seneta huyo alikuwa akizungumza wakati wa mazishi ya mwanawe mwanasiasa wa Kasipul, Newton Ogada. Bw Owino na Gavana Orengo pia walihudhuria. Mbunge wa Awendo Walter Owino pia amemuunga mkono Bw Owino, akisema ndiye mtu anayefaa zaidi kuongoza jiji. “Babu anataka kuwa gavana wa Nairobi na Waluo wote wa Nairobi wanapaswa kumuunga mkono. Baada ya kutathmini jinsi atakavyotekeleza majukumu hayo ndipo tunaweza kufikiria na kumpa nafasi yenye mamlaka zaidi,” akasema Bw Walter Owino katika mahojiano na kituo kimoja cha eneo hilo. Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwour, almaarufu Jalang’o, pia amewahi kumuunga mkono Bw Owino, ambaye yuko katika muhula wake wa pili kama Mbunge wa Embakasi Mashariki. “Ninajiandaa kwa uongozi wa Babu Owino kama gavana wa Nairobi. Najua anakuja kuhudumu kwa muhula mmoja, na baada ya hapo, atanipisha mimi huku yeye akipanda hadi nafasi ya juu zaidi,” akasema Bw Odiwuor. “Ikiwa Babu Owino atapewa tiketi ya ODM, atakuwa gavana wa Nairobi. Asipopewa, atasababisha tabu kwa wagombea wengine,” akaongeza. Huko Homa Bay, Bw Owino alishangaa kwa nini ODM inataka kumpa Bw Sakaja tiketi ya ugavana, ilhali hakuwahi kumuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa ODM, marehemu Raila Odinga. “Mimi ndiye gavana ajaye wa Kaunti ya Nairobi. ODM inataka kumpa Sakaja tiketi ilhali 2007 alimuunga mkono Kibaki, kisha 2013 na 2017 akamuunga mkono Uhuru kabla ya kumuunga mkono Ruto 2022. Hakumtaka Raila, lakini sasa anapendekezwa kuwania ugavana,” akasema Bw Owino. Matarajio ya Bw Sakaja kujiunga na ODM pia yamezua wasiwasi kwa Bw Aladwa, ambaye amesisitiza kuwa uteuzi wa chama hicho unapaswa kuwa huru na wa haki. "Nimeunga mkono na kukiimarisha chama hiki cha ODM kwa miaka mingi na kila mtu anajua kwamba tulifanya kazi kwa karibu na kiongozi wetu wa chama aliyefariki, Raila Odinga. Wale wanaopanga kujiunga na ODM wawe tayari kwa mchujo. Madiwani wote na wajumbe wako nyuma yangu," alisema Bw Aladwa. Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga aliwahi kusema chama hicho kinaweza kumuunga mkono Bw Owino iwapo watakuwa katika kambi moja ya kisiasa. "Babu aliniambia kwamba analenga kura za Mlima Kenya na Wakamba, na kubaki ODM kutahatarisha nafasi zake. Hata hivyo, ninamhofia kwa sababu anaweza kupoteza kura zetu iwapo hatashirikiana nasi," alisema Dkt Oginga mwezi Machi baada ya kukutana na Bw Owino.

ABIRIA waliokuwa wakisafiri kuelekea Nairobi na Entebbe kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kisumu jana walikwama kwa muda mrefu huku shughuli uchukuzi angani zikitatizwa. Mgomo wa Muungano wa Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege (KAWU) ambao unaingia siku yake ya tatu leo ndio ulisababishia abiria kadhia hiyo ya safari. Miongoni mwa waliokwama ni Kaimu Katibu wa Kaunti ya Siaya, Elizabeth Adongo, ambaye safari yake ya Safarilink kuelekea Nairobi ilisukumwa mbele baada ya kukaa uwanjani kwa saa kadhaa. Bi Adongo alisema alifika Uwanja wa Ndege wa Kisumu saa moja asubuhi ili asafiri hadi Nairobi, ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano muhimu wa kaunti saa nne asubuhi. Hata hivyo, alisema alikaa uwanjani kwa saa kadhaa bila kupewa taarifa kuhusu hatima ya safari yake. Bi Adongo alisema baadaye alipokea ujumbe kutoka kwa shirika hilo ukimfahamisha kuwa safari ilikuwa imeahirishwa. “Ujumbe kutoka Safarilink ulifika karibu saa saba mchana ukisema safari ilikuwa imeahirishwa,” alisema. Abiria mwingine, Lennox Omondi, mfanyakazi wa Serikali ya Kaunti ya Siaya, pia aliathiriwa na mgomo huo. Baada ya kupokea ujumbe wa kuahirishwa kwa safari yake saa saba mchana, Bw Omondi alielekea kituo cha mabasi na akaamua kusafiri kupitia barabara. Usumbufu huo uliwaacha abiria wengi uwanjani, huku baadhi wakitafuta njia mbadala za kufika walikokuwa wakielekea. Kufikia Jumatatu alasiri, uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kisumu ulikuwa katika kikao cha dharura kutathmini hali na kupanga hatua za kuchukua. Baadhi walibaki uwanjani wakisubiri taarifa kutoka kwa mashirika ya ndege na mamlaka ya nyuga za ndege, huku wengine wakiachana na mipango ya kusafiri kwa ndege na kutumia mabasi.

WALIMU wamelalamika kuwa ahadi ambazo walipewa na Rais William Ruto kwenye mkutano ulioandaliwa Ikulu ya Nairobi mwaka mmoja uliopita, bado hazijatimizwa. Wakati wa mkutano huo uliowashirikisha zaidi ya walimu 10,000, uliofanyika Septemba 13, 2025, Rais alitoa ahadi kadhaa za kushughulikia changamoto zao lakini hadi sasa hakuna kilichotimizwa. Miongoni mwa ahadi kuu ilikuwa serikali kutenga asilimia 20 ya nyumba za gharama nafuu kwa walimu na kuongeza mara mbili idadi ya walimu wanaopandishwa vyeo kila mwaka hadi 50,000. Ongezeko hilo lingesaidia kukabiliana na tatizo la walimu kukwama katika daraja moja ya kazi. Hata hivyo, ahadi hiyo haijatimizwa kwa kuwa Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) imetangaza nafasi 34,000 za kuwapandisha vyeo. Hii inamaanisha asilimia 68 pekee ya ahadi hiyo imetimizwa. Katibu Mtendaji wa Chama cha Walimu Nchini (KNUT) tawi la Nairobi Mugwe Macharia, alisema nafasi zilizotangazwa na TSC ni chache kuliko zilizoahidiwa. “Hatujaona ongezeko la mara mbili la nafasi za kupandishwa vyeo kutoka 25,000 za sasa kwa sababu TSC imetangaza nafasi 30,000 pekee, na kuacha pengo la 20,000,” akasema Bw Macharia. Rais pia aliahidi kupunguza muda wa kutekelezwa kwa Mkataba wa Makubaliano (CBA) wa 2025–2029 kutoka miaka minne hadi miwili na kuwapandisha walimu wa masomo wa masomo spesheli daraja moja la kazi. Aidha, Rais aliahidi kuwapa walimu wakufunzi 20,000 ajira ya kudumu na pensheni, pamoja na kuagiza mabadiliko ya Mwongozo wa Maendeleo ya Kitaaluma (CPG) unaotumiwa na TSC katika kuwapandisha walimu vyeo. Katibu Mkuu wa Muungano wa Walimu Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET), Akello Misori, jana alisema utekelezaji wa ahadi hizo unategemea asasi husika za serikali. “Mkutano huo haukuhusu CBA, kwa hivyo hatukujadili masharti hayo na Rais. Ikiwa alitoa ahadi fulani, hizo ni ahadi za kisiasa, na tunazifuatilia kupitia taasisi husika,” akasema Bw Misori. Kuhusu ahadi kupunguza muda wa utekelezaji wa CBA kutoka miaka minne hadi miwili Bw Misori amesema utekelezaji halisi ulipaswa kujadiliwa kati ya walimu na TSC. “Jambo la muhimu sana kwa walimu ni suala linalohusiana na CBA, ambalo Rais, akiwa mshirika, alipaswa tu kulianzisha ikiwa ingewezekana. Lakini hilo lilikuwa kati yetu na TSC ili litekelezwe,” akasema. Kuhusu mabadiliko ya CPG, ambayo yamekuwa yakilaumiwa kwa kusababisha walimu kukwama katika daraja moja la kazi, TSC imependekeza CPG mpya ya 2026 itakayowaruhusu walimu kufikia daraja la juu zaidi bila kuacha kufundisha. TSC pia imependekeza njia mbili tofauti za maendeleo ya taaluma, moja kwa walimu wanaoendelea kufundisha madarasani na nyingine kwa wanaotaka kushikilia nyadhifa za uongozi na utawala. Hata hivyo, mapendekezo hayo bado hayajaanza kutekelezwa. Knut, Kuppet na Muungano wa Walimu wa Elimu Maalum (KUSNET) walitia saini makubaliano hayo na TSC Juni 18, 2026, na kuyawasilisha kwa Tume ya Kutathmini Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma (SRC) ili yapitiwe, lakini hakuna hatua zaidi iliyochukuliwa. Katika utekelezaji wa ahadi ya kuwapandisha walimu wa masomo spesheli daraja moja ambao umekwama, Katibu mkuu wa KUSNET, James Torome, alisema CPG ya 2018 ilitoa nafasi kwa walimu hao kupandishwa madaraja mawili. Hata hivyo, ahadi hiyo haikutekelezwa ndiyo maana walimwomba Rais aingilie kati. Kuhusu nyumba za gharama nafuu, Kuppet ilisema mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi walimu watakavyopata asilimia 20 ya nyumba hizo kupitia mpango wa Boma Yangu. “Tumekuwa tukishirikiana na wizara na idara inayohusika. Tumekutana na Waziri wa Nyumba na tumeunda kamati ya kiufundi kubaini jinsi walimu watakavyopata nyumba hizo,” akasema Bw Misori. Kuhusu matibabu, TSC iliwahamisha walimu kutoka mpango uliokuwa ukiendeshwa na Minet Kenya hadi Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) Disemba mwaka jana. Mpango huo unajumuisha matibabu ya kulazwa na kutolazwa, huduma za uzazi, magonjwa sugu, meno, macho, gharama za mazishi na matibabu nje ya nchi. Bw Misori alisema muungano huo unaendelea kushirikiana na SHA kuhusu masuala ya kiufundi ili kuhakikisha walimu wanaendelea kunufaika na mpango huo. “Vituo vya uzazi tayari vimetambuliwa na walimu tayari wanaenda kupata matibabu nje ya nchi,” akasema. Hata hivyo, KNUT ilisema bado kuna changamoto katika SHA, huku baadhi ya hospitali zikikataa kuwahudumia walimu chini ya mpango huo mpya.

There are moments when an institution must pause—not necessarily because it has acted unlawfully, but because a particular decision raises deeper questions about judgment, standards and institutional identity. The decision to invite Martins Vincent Otse, popularly known as VeryDarkMan, as a panellist at the Nigerian Bar Association’s Annual General Conference has generated considerable debate within […]

MBEYA; Picha za matukio mbalimbali ya waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wakisajiliwa katika Banda la Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwenye maandimisho ya Wiki ya Tiba ya Asili ya mwafrika yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya Usajili wa watoa huduma hao umeelezwa kuwa miongoni mwa hatua zinazoongeza uaminifu wa Jamii na kuimarisha utoaji…

By Gabriel Ewepu ABUJA — The Because Of Our Tomorrow, BOOT Party, has urged the Independent National Electoral Commission, INEC, to address glitches in its Candidate Nomination Portal to prevent political parties from being subjected to unnecessary agitations. The party’s call followed an alarm raised by the National Democratic Party, NDC, over alleged discrepancies in […]

KAMPALA, Uganda: MFALME Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV wa Tooro Uganda alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 34. Waziri Mkuu wa ufalme huo, Calvin Armstrong Rwomiire Akiiki, alitangaza kifo chake Alhamisi usiku. Mfalme huyo alifariki mwendo wa saa nne usiku, bila kilichosababisha mauti yake kusemwa hadharani. Oyo alitwaa ufalme 1995 akiwa na umri wa miaka mitatu, baada ya kifo cha babake, Rukirabasaija Patrick David Matthew Kaboyo Olimi III, na kuwa mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani. Uganda ni jamhuri inayoongozwa na rais aliyechaguliwa, lakini ina falme kadhaa za jadi ambazo zinaendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kitamaduni na kijamii, licha ya uwepo wa utawala wa urais. Tooro iko magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Akiiki alisema mfalme huyo hakuwa ameoa, lakini aliacha mrithi na mwendelezo wa uzazi wake ambao umehakikishwa. Kifo chake kimezua huzuni kubwa Uganda. Kiongozi wa upinzani Bobi Wine alisema: “Habari za kusikitisha sana! Roho ya Mfalme ipumzike kwa amani ya milele.”

DODOMA: THE Chairperson of CCM Women’s wing, Mary Chatanda, has described the newly sworn-in Vice-President Deogratius Ndejembi as a capable, principled and patriotic leader who can effectively support President Samia Suluhu Hassan in executing her responsibilities. Speaking in Dodoma, the UWT Chairperson stated that Ndejembi’s track record in public service demonstrated his ability to deliver…

JAJI Mkuu Mstaafu David Maraga ameonya kuwa Idara ya Polisi inayopendelea kisiasa inaweza kuingiza Kenya katika machafuko baada ya uchaguzi huku akimtaka Rais William Ruto kutekeleza kikamilifu Katiba. Bw Maraga alisema hayo Jumatatu alipoweka wazi mapendekezo ya Jopokazi kuhusu Mageuzi ya Polisi aliloongoza mnamo 2023. “Polisi wanaoegemea mrengo mmoja kisiasa ndio walikuwa kiini cha ghasia za 2007/2008. Wakenya hawapaswi kusahau kwamba vifungu vya Katiba ya 2010 kuhusu taasisi huru viliandikwa kwa damu hiyo,” akasema Bw Maraga. Wiki iliyopita, Bw Maraga alimpa Rais Ruto makataa ya siku saba kuchapisha ripoti ya jopo kuhusu mageuzi ya polisi iliyowasilishwa kwake, akisema atachapisha mwenyewe iwapo serikali haitafanya hivyo. SOMA PIA: Maraga ampa Ruto siku saba achapishe ripoti iliyopendekeza mageuzi ya polisi lau sivyo aitoe yeye Alisema jopo lilipendekeza idara huru ya polisi ili kukomesha kile alichokiita kutekwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na kutumiwa vibaya kwa idara hiyo. Hayo ni miongoni mwa mapendekezo zaidi ya 200 yaliyotolewa na kikosi hicho kulingana naye. Bw Maraga ametaka mapendekezo hayo yote kutekelezwa, yakiwemo kuhakikisha uhuru wa NPS na kubadilisha sare za polisi. Hata hivyo, alisema mabadiliko ya sare hayakuwa jambo la dharura. NPS ilizindua sare mpya wiki iliyopita. Alisema Kenya sasa inashuhudia kile alichowahi kukiita “vurugu za kisiasa zilizopangwa, magenge na polisi wenye misimamo ya kisiasa”. Alitoa mfano huo kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa Homa Bay, Keumbu na Ol Kalou, pamoja na visa vya vurugu katika makanisa ya Kisumu, Nairobi na Witima. Katika kisa cha Homa Bay, watu wawili, akiwemo polisi mmoja, waliuawa na wengine 46 kujeruhiwa katika mapigano yaliyovuruga mkutano wa Linda Mwananchi. “Jibu la tatizo hili ni kutii Katiba na Huduma ya Kitaifa ya Polisi lazima iwe huru. Ni hitaji la kuvunja mfumo wa polisi wa kikoloni na kukomesha kutekwa kwa mfumo wa usalama na serikali,” akasema Bw Maraga. Alisema ingawa Katiba iko wazi kuhusu uhuru wa polisi, Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Usalama ya 2014 iliondoa kinga hizo na kusababisha NPS itekwe. Jopo la Bw Maraga lilipendekeza kufutwa kwa marekebisho hayo ya 2014 lakini anadai mapendekezo hayo yalipuuzwa. Alisema pia sheria kuhusu umri iligeuzwa na matokeo yake yakawa kwa faida ya wazi ya kisiasa.