MAHAKAMA kuu imeratibisha kuwa dharura kesi ya kuzima tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) kuipa kampuni ya Amerika –Smartmatics International Holdings B.V zabuni ya Sh17.6 bilioni kutengeneza vifaa vya kieletroniki vya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Kesi hii imewasilishwa kortini siku moja baada ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kudai kandarasi ya ununuzi wa vifaa hivi vya kura almaarufu KIEMS kati ya IEBC na kampuni ya Amerika inatamatika Novemba 24, 2026 (Jumanne).

Jaji David Mburu alisema kesi hiyo iliyowasilishwa na Mabw Koome Kevin na Zedekiah Samson imezua masuala mazito ya kisheria na kwamba inapasa kuamuliwa pasi na kusita.

Jaji Mburu alimwagiza wakili Elly Okoth aliyewasilisha kesi chini ya sheria za dharura aikabidhi IEBC nakala za kesi hiyo mnamo Novemba 24, 2026 na kuiamuru tume iwasilishe ushahidi kujibu madai kwamba imeshikana na kampuni inayokabiliwa na madai ya ufisadi wa kimataifa.

Jaji huyo aliamuru kesi hiyo itajwe Novemba 30, 2026 kwa maagizo zaidi.

Akiwasilisha ushahidi, Bw Okoth alimweleza jaji huyo kwamba kampuni ya Smartmatics inakumbwa na kashfa za ufisadi hata imeshtakiwa katika nchi ya Ufilipino kwa ufisadi wa USD ($)1 milioni.

Inadaiwa kampuni hiyo ya Smartmatics ilimlisha mlungula aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Ufilipino kwa kuipa kandarasi ya vifaa vya kieletroniki vya kupiga kura.

Mbali ya kesi hiyo ya Ufilipino, Jaji Mburu alifahamishwa bado Smartmatics pamoja na wakuu fulani walishtakiwa katika mahakama ya Southern Florida kufuatia uchunguzi na makachero wa FBI.

Kesi hiyo pia inahusu uuzwaji wa vifaa vya kieletroniki kwa nchini ya Ufilipino.

Mabw Kevin na Samson wamelalamikia mahakama kwamba wakuu wa IEBC waliipa zabuni kampuni hii inayokabiliwa na ufisadi wa kimataifa.

“IEBC imekaidi Sheria za ununuzi wa bidhaa za umma (PPRA) na kifungu na 227 kuhusu usimamizi wa pesa za umma,” Bw Okoth alieleza mahakama kuu.

Mahakama ilielezwa pia IEBC haikuzingatia sheria za uangavu na uwajibikaji ilipoipa Smartmatics kandarasi ya kuinunulia KIEMS.

Bw Okoth alisema kampuni hii ya Smartmatics ilipewa kandarasi hii ya Sh17.6bilioni ilihali kuna kampuni nyingine ambayo ilikuwa imewasilisha ombi kwa IEBC na kufichua ingeipa vifaa hivi vya kutumika wakati wa uchaguzi mkuu kwa bei ya Sh14.3bilioni.

Wakili aliambia korti kwamba ununuzi wa vifaa hivi vya kutumika wakati wa uchaguzi vimeongezwa bei kwa zaidi ya Sh3.3bilioni.

Jaji Mburu alielrzwa IEBC inatumia vibaya pesa za umma kwamba lazimima izimwe na mahakama.

Jaji Mburu alielezwa kampuni hii ya Smartmatics iko na madoa doa ya kushtakiwa kwa ufisadi na kamwe maafisa wa IEBC hawakasi kuipa kazi hii ya kuiwasilishia vifaa vya KIEMS ilhali sheria za nchi hii haziipi fursa ya kutoa hudumu kama hii ikiwa inakabiliwa na madai ya ufisadi.

Jaji Mburu alifahamishwa kampuni hii imeshtakiwa kwa kutoa mlungula wa USD ($)1,000,000 kwa aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Ufilipino.

Jaji Mburu aliagiza kesi hii isikizwe Novemba 30,2026.