Video
RAIS SAMIA ATANGAZA UFADHILI WATAALAM WA AFYA 60 AFRIKA
Channel: Millard Ayo Watch on YouTube
About this video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza ufadhili wa awali wa nafasi 60 za mafunzo ya kibobezi na ya juu katika taaluma mbalimbali za afya kwa nchi za Afrika, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa afya katika bara hilo. Nafasi hizo zitajumuisha mafunzo katika fani za ukunga, usingizi na ganzi, uzazi na magonjwa ya wanawake pamoja na huduma za watoto wachanga, kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi maalumu na kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto. Rais Samia amesema hayo leo Novemba 23,2026 wakati akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), jijini Addis Ababa, Ethiopia. Amesema mafunzo hayo yatawahusisha pia wataalamu wa ngazi ya kati, wauguzi na wakunga, ili kuongeza uwezo wao katika kutoa huduma salama za uzazi, huduma za dharura, matumizi ya ganzi na huduma muhimu kwa watoto wachanga. Rais Samia amebainisha kuwa upungufu wa wataalamu wa afya wenye utaalamu maalumu ni miongoni mwa changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma bora za afya barani Afrika, hivyo mpango huo unatarajiwa kuchangia kuimarisha rasilimali watu na mifumo ya afya katika nchi za Afrika
Related stories
NewsMurray-Bruce hails Tinubu’s CNG bus initiative, urges governors to act
Former Senator Ben Murray-Bruce has commended President Bola Tinubu’s initiative to introduce compressed natural gas (CNG)-powered buses and promote local vehicle assembly, urging state governors to invest in the programme and supporting infrastructure. Murray-Bruce, founder of Silverbird Group, made the call in a Facebook post on Monday, describing the initiative as a step towards transforming […]
NewsNo electricity tariff increase in 2027 - Power minister assures Nigerians
The minister said the government was also reviewing assumptions in the electricity tariff model, but ruled out an increase.
News18-year-old man detained for killing his child after wife aged 19 allegedly dumped him
An Eldoret court grants police 14 days to detain 18-year-old Obadiah Ndiwa Omuse as they investigate his daughter's death and the discovery of her body at home.
NewsRAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA AFYA YA UMMA ETHIOPIA
RAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA AFYA YA UMMA ETHIOPIA #breaking #raissamia