The Cape of Good Hope SPCA will monitor the relocated Simon's Town baboons at Kogelfontein but warns it will legally challenge any future moves to permanently confine healthy troops.
Read the full article
The Cape of Good Hope SPCA will monitor the relocated Simon's Town baboons at Kogelfontein but warns it will legally challenge any future moves to permanently confine healthy troops.
Read the full article
This story was originally published by Sowetan Live.
Read the full story at Sowetan Live
News…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…
NewsTANGAZO la Rais William Ruto kuhusu malipo ya Sh15.07 bilioni kwa wakulima 680,000 wa kahawa na bonasi ya Sh1.2 bilioni kwa wakulima wa miwa ni hatua inayostahili kupongezwa. Kiongozi wa nchi jana alitangaza malipo hayo alipotoa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge ambapo pia alizungumzia mafanikio mengine ya serikali yake. Rais alisema bei ya kahawa imeongezeka kutoka Sh69 hadi Sh130 kwa kilo, huku mapato ya kitaifa kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi yakiongezeka maradufu kutoka Sh26 bilioni hadi Sh52 bilioni. Aidha, wakulima wa miwa wanatarajiwa kupokea bonasi ya Sh1.2 bilioni kuanzia wiki ijayo. Hizi ni habari njema kwa wakulima ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakikabiliwa na gharama kubwa za uzalishaji, bei duni za mazao, madeni na mifumo ya ushirika isiyowajibika. Wakulima wa kahawa, hasa, wamevumilia misimu ya mavuno duni, ucheleweshaji wa malipo na changamoto za magonjwa pamoja na hali mbaya ya hali ya hewa. Kuongezeka kwa bei ya kahawa na mapato ya mauzo ya nje kunaashiria kuwa mageuzi katika sekta hiyo yameanza kuzaa matunda. Takwimu zinaonyesha uzalishaji wa kahawa uliongezeka kutoka tani 49,500 mnamo 2024 hadi tani 51,400 mnamo 2025. Hata hivyo, ongezeko hili bado halitoshi kuifanya sekta hiyo kuwa na nguvu ikilinganishwa na uwezo wake wa kihistoria. Serikali inapaswa kuhakikisha fedha zilizotangazwa zinawafikia wakulima wanaostahili bila kucheleweshwa, mapendeleo au mianya ya ufisadi. Malipo ya moja kwa moja, mifumo ya uwazi na ukaguzi wa mara kwa mara wa vyama vya ushirika ni muhimu ili mkulima apate faida ya jasho lake. Vilevile, bonasi ya wakulima wa miwa haipaswi kuwa tukio la mara moja linalotolewa wakati wa hotuba za kisiasa. Serikali pia inapaswa kuwekeza zaidi katika utafiti wa kilimo, mbegu bora, mbolea nafuu, kilimo cha unyunyuziaji mashamba maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kuongezeka kwa uzalishaji pekee hakutasaidia ikiwa gharama za pembejeo zitameza mapato ya mkulima. Kilimo ndicho uti wa mgongo wa uchumi na chanzo kikuu cha ajira na riziki kwa mamilioni ya Wakenya. Kukiimarisha si suala la kutoa fedha pekee, bali kujenga mazingira ambayo mkulima anaweza kupanga maisha yake, kuwekeza na kupata faida bila kutegemea misaada ya mara kwa mara. Mkulima anahitaji zaidi ya bonasi, anahitaji soko la uhakika, bei inayomfaa, huduma bora na sera zinazomweka katikati ya maendeleo ya taifa.
NewsMDHIBITI wa Bajeti (CoB) Margaret Nyakang’o, amezua wasiwasi kuhusu hatua ya Kaunti ya Nairobi kukopa Sh1.5 bilioni kila mwezi kutoka Sidian Bank kulipa mishahara, licha ya serikali kuu kutoa mgao wa fedha kwa wakati. Ripoti iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inaonyesha kuwa kaunti hiyo ilikopa Sh1.56 bilioni Septemba na Sh1.49 bilioni Oktoba. Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara. Hata hivyo, baadhi ya makato ya wafanyakazi yaliyopaswa kupelekwa kwa vyama vya akiba na mikopo (SACCO), hazina za pensheni na taasisi nyingine hayakulipwa kikamilifu. Benki hiyo ilionyesha kuwa Sh249.3 milioni za makato hayo Agosti bado hazijalipwa Septemba sawa na Sh254.5 milioni za Septemba zilizopaswa kulipwa Oktoba. Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara. Alisema mpango huo ulilenga kushughulikia changamoto za haraka za kulipa wafanyakazi huku kaunti ikiimarisha mapato na usimamizi wa fedha. Hata hivyo, Nyakang’o alihoji sababu ya kaunti kukopa ilhali mgao wa fedha kutoka Serikali ya Kitaifa haukuwa umechelewa. “Hadi Oktoba, kaunti zilikuwa zimepokea mgao wao. Nairobi hata imepokea fedha za Novemba, lakini bado inakopa kutoka Sidian Bank,” alisema. Alisema ofisi yake iliitaka serikali ya Gavana Johnson Sakaja kueleza gharama ya riba inayolipwa kwa mkopo huo. Wasiwasi mwingine ni matumizi ya mfumo wa malipo ya mishahara nje ya Mfumo wa Taarifa za Rasilimali Watu (HRIS), ambao unaunganisha malipo ya mishahara na makato ya kisheria. Nyakang’o alisema utaratibu huo unaweza kusababisha wafanyakazi kulipwa mishahara huku michango ya pensheni, makato ya SACCO na marejesho ya mikopo yakikosa kuwasilishwa. “Hatari yake ni kuwa makato ya kisheria hayalipwi. Hili ni janga linalosubiri kutokea,” alisema. Aliongeza kuwa baadhi ya michango ya pensheni na malipo ya mikopo ya wafanyakazi hayakuwa yamewasilishwa kwa taasisi husika.