Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.
Baada ya kuwa na kambi ya takribani siku tisa Zanzibar, Yanga inaona ni wakati sasa wa kuvuna matatu ya kambi hiyo kwenye NBC Premier League na mashindano mengine.
Arsenal manager Mikel Arteta has revealed how he deliberately creates unexpected disruptions during pre-season to prepare his players for the chaos that can occur on matchdays.
GEITA Gold inaendelea na maandalizi ikiwasubiri Yanga kumaliza ratiba ya mechi za kimataifa. Sasa kocha wa kikosi hicho, Zuberi Katwila amefunguka hesabu zake kuelekea mchezo huo dhidi ya mabingwa hao.
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Jumamosi kwa mechi mbili kuchezwa ambapo Polisi Tanzania itaikaribisha Mbeya City, huku Coastal Union ikiwa mwenyeji wa JKT Tanzania. Pale Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Polisi Tanzania itakuwa na dakika 90 zingine za kubadilisha matokeo baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo zilizopita.
Real Madrid manager Jose Mourinho has defended Kylian Mbappe and Vinicius Junior after the two forwards were booed by the club’s supporters, comparing the stars to fruit trees that attract criticism because of their success.
Arsenal boss Mikel Arteta said he was "very surprised" by Gabriel Jesus's claim that he was forced to train alone and was given no information prior to joining Barcelona.
The Nigeria Immigration Service has extended its Special Passport Intervention Exercise in the United Kingdom to October 3, 2026, following a high turnout of applicants in London and Manchester.
UTANGULIZI “Niliwaona na niliona kila kitu kilichotokea. Wakati huo mimi nilikuwa hapa hapa kwenye kioski change.” “Mbona kuna watu wanasema sijui eti mmoja wa hao watu shingo yake ilikuwa imechinjwa?” “Sasa pale ndio sikuelewa wale watu walikuja na miujiza gani. Kweli shingo ya mmojawao ilikuwa imechinjwa na huyo jamaa ndiye aliyetoa panga na kumchinja Yule mhasibu wa kiwanda cha maji safi.” SASA ENDELEA... “Halafu inesemekana baada ya kumchinja walipora mkoba wake wa pesa na kukimbia?” “Ndiyo, walimpora mkoba wa pesa. Inadaiwa jamaa alikuwa anatoka benki. Wakachukua pesa zote.” “Walikimbilia wapi?” “Kwa kweli hakuna aliyewaona. Hawa majambazi siku hizi wanatumia haya mambo ya nguvu za giza. Hata yale mavazi waliyokuwa wamevaa yalikuwa hayaeleweki. Yaani baada ya kupora ule mkoba walitoweka pale pale.” “Unadhani kwamba kuna nguvu za kiza zilizotumika?” “Lazima. Wale si majambazi wa kawaida. Lakini kitu kilichoshangaza watu ni kwamba kabla ya kumchinja, yule jamaa aliyevaa nguo nyeusi alimwambia yule jamaa. “Baba yako amekuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana.” Amour akagutuka. “Alimwambia baba yake alimuweka dhamna wapi?” “Hakumwambia alimuweka dhamana wapi ila alimwambia umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana. Ndio akamchinja.” “Sasa huyo marehemu alipoambiwa hivyo hakuuliza ni dhamana gani?” “Nilimsikia akimuuliza. Yule jambazi akamjibu muda wako umekwisha.” “Ulitwa polisi kutoa maelezo?” “Baada ya lile tukio nilifunga kioski changu. Polisi waliita watu wengine.” “Wewe ungeweza kuwa shahidi mzuri kwa sababu ulisikia walichokuwa wanazungumza.” Kijana huyo akang’aka. “Hata kama nilisikia, siwezi kuwa shahidi. Ushahidi mara nyingi unaponza halafu unajikuta unapoteza muda mwingi wa kazi ukiwa polisi kama vile wewe ndiye uliyeshitakiwa.” “Hizo si fikira nzuri. Polisi hawawezi kufanya kitu peke yao bila ushiriikiano na wananchi na wananchi ndiyo nyinyi. Huwezi kusema kwamba utapoteza muda wako kama kweli wewe ni mzalendo wa nchi hii. Ni lazima tushirikiane na polisi kutokomeza ujambazi na uhalifu mwingine.” “Ni kweli mzee nimekuelewa. Watakapokuja kuniuliza nitawapa ushirikiano.” Amour alikuwa ameshamaliza kunywa soda yake, akamrudishia chupa kijana huyo na kumlipa pesa zake. “Asante kijana. Huenda nitahitaji kukuona wakati mwiingine wowote.” Amour alimwambia bila kujitambulisha alikuwa nani. Kijana naye alimkubalia bila kutambua Amour alikusudia nini na alikuwa nani. Amour alirudi kwenye gari lake akajipakia na kuonndoka. ********** Nyumbani kwa Almasi kulikuwa na kikao. Mara tu baada ya maziko. Almasi aliwaita sebuleni wanawe wanne waliobaki ili kuwapa wasia. Alikuwepo james, John, Alex na Benjamin. James alikuwa mtoto wa pili wa Almasi akifuatiwa John. Baada ya John alizaliwa Alex akamalizia Benjamin. Katika maisha yake Almasi hakubahatika kupata mtoto wa kike. “Wanangu tuko katika kipindi cha huzuni sana. Tumempoteza kaka yenu katika tukio ambalo nyote mnalijua vizuri na sijisikii kulirudia tena.” Almasi aliwambia wanawe. Vijana hao walimkubalia kwa pamoja. “Nyinyi mliobaki nawaomba muendelee kushikamana mdumishe upendo na kuheshimiana. Kila linapotokea tukio ambalo linatukusanya pamoja ni lazima niwape nasaha zangu kwa sababu mimi ni baba yenu. Tukio lililotokea ni kubwa na limetuhuzunisha sana. Nawaomba wanangu muwe na mioyo ya subira na mumuombee kaka yenu apumzike pema peponi.” “Amin.” Sauti za vijana hao zikasikika kwa pamoja. “Martin alikuwa mhasibu wa kapuni yangu. Amefanya kazi vizuri sana na kwa uaminifu. Ni wazi kwamba kifo chake kimeacha pengo si tu kwenye familia yetu bali pia katika uongozi wa kampuni. Kwa hiyo leo ninawajibika kuteua mhasibu mwingine miongoni mwenu kushika nafasi ya marehemu Martin.” Almasi aliendelea kuwambia. Kisha ghafla akamtazama James. “James ni wa pili kuzaliwa na ndiye kaka wa nyinyi nyote mlioko hapa. Yeye ndiye niliyempendekeza ashike nafasi ya Martin. Kwa vile James alisoma chuo kimoja na Martin ninaamini kuwa ataimudu vizuri kazi yake au mnasemaje?” “Ni sawa Baba.” Ilikuwa sauti ya John. “Hiyo nafasi ni lazima aishike kaka yetu ambaye ni James,” akasema Alex. “Mimi pia ninaunga mkono uteuzi huo,” akamalizia Benjamin. “Hakuna mwenye kinyongo?” Almasi akawauliza wote kwa pamoja. “Hakuna.” Wote walijibu hivyo. “Nimefurahi kusikia kuwa nyote mmependa James ashike nafasi ya marehemu kaka yenu. Sasa kuna kitu kimoja nataka kukuuliza James.” Almasi alimwambia james huku akimtazama. “Unatuhakikishia hapa mimi na ndugu zako kwamba utamudu majukumu yako na utafanya kazi kwa uaminifu kama alivyokuwa kaka yako?” “Ninawahakikishia wewe baba yangu na ndugu zangu kwamba nitamudu majukumu yangu na nitafanya kazi kwa uaminifu kama alivyokuwa kaka yetu na lengo kubwa ni kuleta tija na ufanisi kwenye kampuni yetu. Najua hivi sasa tuko katika ushindani mkubwa wa kibiashara kwani kampuni za maji safi ziko nyingi.” “Umezungumza vizuri James na umenipa moyo. Asante sana. Sasa kuna kitu kingine ambacho nataka muwe macho nacho nyinyi wote. Ujambazi umekuwa mwingi sana hasa katika jiji la Dar. Nawaomba muwe makini sana. Na kwa upande wako James badala ya kwenda benki kuchukua pesa taslimu utakuwa unatumia hundi. Mishahara ya wafanyakazi utaiingiza benki, kila mtu kwenye akaunti yake. Umenielewa?” “Nimekuelewa baba.” ****** Ilikuwa imepita miezi sita. James alikua ndiye mhasibu wa kampuni ya maji safi ya baba yake. Tangu alipokabidhiwa wadhifa huo alikuwa amefanya kazi vizuri sana na kuiletea mafanikio makubwa kapuni hiyo. Alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa baba yake na kwa ndugu zake na pia kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo jambo ambalo lilimuongezea moyo wa kuipenda kazi yake. Utaratibu ulikuwa ni kama ule waliopanga na baba yake pamoja na ndugu zake. Ule mtindo wa awali wa kuchukua pesa nyingi kutoka benki kwa ajili ya kugawa mishahara ya wafanyakazi uliachhwa. Wafanyakazi walikuwa wakiwekewa mishahara kwenye akaunti zao. Kadhalika matumizi mengi ya pesa yalikuwa yakifanywa kwa hundi badala ya pesa taslimu. Miezi mitatu tu baada ya James kuwa katika kiwanda hicho akajikuta ameingia katika penzi na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo aliyeitwa Grace. Penzi hilo lilianza kuchanua moyoni mwa kila mmoja na kuwa siri yake lakini taratibu likaanza kujitokeza kwa kila mmoja. James ndiye aliyeanza kumuonesha Grace kuwa alikuwa akimpenda. Siku moja James alichukua namba ya simu ya Grace. Jioni alipokuwa nyumbani kwake akampigia simu Grace na kumuomba akutane naye katika hoteli moja iliyopo Sinza ambako James alikuwa anaishi. Grace akaukubali mualiko huo bila kupingwa. Wakakutana saa mbili usiku katika moja ya kumbi za hoteli hiyo. Walikula chakula cha usiku huku wakizungumza hili na lile lakini baada ya chakula hicho, James alibadili mazungumzo na kumueleza Grace lililokuwa moyoni mwake. Grace naye bila kuonesha hiyana alimueleza wazi James kuwa hata naye alikuwa akiumia. Hapo ndipo penzi lilipoanza rasmi kati ya James na Grace. Grace alikuwa msichana wa Kihaya aliyekuwa akiishi Mwenge. Licha ya kuwa na umbo jamali na sura jamili alikuwa mrembo aliyevuta macho ya kila mwanaume. Penzi la James na Grace lilianza kama ua lililochukua muda kuchanua. Lilianza kama siri yao wawili. Hawakutaka wafahamike kuwa walikuwa wapenzi. Lakini taratibu penzi hilo likaanza kuchanua na kudhihirika. Likawa bayana kwa kila mfanyakazi wa kampuni hiyo. Kila mfanyakazi alifahamu kuwa Grace alikuwa mwandani wa bosi wao. Kufuatia kufahamika kwa penzi lao, Grace akawa bosi kivuli wa kampuni kwani alijitwalia mamlaka ya kuamrisha wafanyakazi wengine vile anavyotaka yeye na pia kuwashitakia kwa James wale ambao hawakutaka kumtii. Grace akaanza kuogopewa. Grace alikwenda kazini siku aliyotaka yeye na aliondoka kazini muda aliotaka yeye. Hakukuwa na wa kumuuliza. Habari zikamfikia mzee Almasi. Kwa kujua kuwa angeitwa na baba yake wakati wowote na kuulizwa kuhusu madai ya kuwa katika penzi na mfanyakazi wake, James alitinga nyumbani kwao akiwa amefuatana na Grace ambapo alimtambulisha Grace kama mchumba wake. Mzee Almasi na mke wake walishangaa. “Huyu si Grace?” Almasi akamuuliza. Alikuwa akimfahamu. “Ndiye yeye.” James alimjibu akitabasamu. “Uchumba wenu ulianza lini?” “Hauna muda mrefu.” “Kwa hiyo mmepanga kuoana?” “Ndiyo baba.” “Ni vizuri lakini nataka kujua bado ni mfanyakazi wetu au umeshamuachisha?” “Bado ni mfanyakazi wetu.” “Ninakushauri wakati mnaendelea na mipango yenu, umuachishe kazi.” “Sawa.” “Mnatarajia ni lini mtavalishana pete ya uchumba?” “Siku mbili hizi hizi tutafanya hivyo.” “Umeshajitokeza kwa wazazi wake?” Mama Almasi akauliza. “Nimeanza kumleta huku kwetu kwanza atambulike kisha atanifikisha kwao.” “Basi ufanye hivyo haraka ili tuweze kuendelea na taratibu nyingine.” “Umenipa maelezo ya busara mama yangu. Kitu cha msingi ninachokitaka kwenu mnieleze je mmemkubali mchumba wangu?”
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Libasse Gueye, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Agosti 2026 katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026-2027, huku Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi, akibeba tuzo ya kocha bora wa mwezi huo.
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Libasse Gueye, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Agosti 2026 katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026-2027, huku Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi, akibeba tuzo ya kocha bora wa mwezi huo.
DAR ES SALAAM: MENEJA wa timu ya wavu ya Korosho Queens ya Mtwara, Hussein Kibombwe amesema timu hiyo imejipanga vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo baada ya kuanza kwa ushindi katika michezo yake mitatu, huku wakilenga kufika hatua ya fainali. Akizungumza na DailyNews Digital, Kibombwe amesema tofauti na mzunguko wa kwanza ambao walikabiliwa…
DAR ES SALAAM; Kiungo mshambuliaji wa Simba ya Dar es Salaam, Libasse Gueye, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2026/27, huku Manqoba Mngqithi wa Yanga, akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo. Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi…
DAR ES SALAAM: KOCHA wa Gaborone United ya Botswana, Sean Connor, amesema presha kubwa ipo kwa Yanga kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, akisema wenyeji watakuwa na mzigo wa kucheza mbele ya mashabiki wao. Yanga itakuwa mwenyeji wa Gaborone United kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, katika mchezo ambao una umuhimu…
Enzo Maresca faces his first major test since stepping into Pep Guardiola's shoes as City visit United in the Manchester derby on Sunday, while Arsenal aim to extend their flawless start at Sunderland.
KIUNGO wa Azam FC, Himid Mao amewapongeza wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake U-20, Tanzanite Queens, kwa kuifikisha Tanzania kwenye hatua ya Kombe la Dunia la vijana, Poland.
MWENYEKITI wa Taasisi ya Rise and Restore Foundation ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kijini, Badria Natai amezindua rasmi maandalizi ya tamasha la michezo na kijamii lijulikanalo kama Kijini Shangwe Bonanza 2026.
SHINYANGA: THE Tanzania Communications Regulatory Authority Consumer Consultative Council (TCRACCC) this week formed the Shinyanga Regional Communications Services Consumers Committee to strengthen the protection of consumers’ rights and safety. The move aims to ensure challenges facing users are brought to the attention of relevant authorities for appropriate action. The five-member committee represents youth, women, entrepreneurs,…
DAR ES SALAAM: AS the country prepares for what meteorologists warn could become one of the strongest El Niño events on record, Tanzania’s history tells a bigger story. The country has suffered devastating floods for decades. Some came during El Niño years. Others did not. From Dar es Salaam’s overflowing Msimbazi River to the Lake…
KWA miongo mingi, ndoa na mahusiano ya kimapenzi yamekuwa yakitazamwa kama msingi wa furaha na utulivu wa kihisia. Hata hivyo, utafiti mpya umeonyesha kuwa maisha ya useja yanaweza kuleta manufaa makubwa kwa maendeleo binafsi, ustawi wa kisaikolojia na kuridhika na maisha kwa ujumla. Utafiti huo, uliochapishwa hivi majuzi kupitia mfululizo wa tafiti tatu zilizojumuisha majaribio na uchambuzi wa kumbukumbu za washiriki, uligundua kuwa watu wasio katika mahusiano ya kimapenzi hupata nafasi kubwa ya kujitambua, kujikuza na kushiriki katika uzoefu mpya unaoongeza ubora wa maisha yao. Kwa mujibu wa watafiti, watu wanaochukulia useja kama fursa ya ukuaji binafsi huwa na kiwango kikubwa cha kuridhika na maisha yao. Aidha, wanaripoti kutosheka kwa mahitaji yao ya kisaikolojia, furaha zaidi na hofu ndogo ya kubaki bila uwepo wa mpenzi. Utafiti huo, uliopewa jina la Riding Solo: The Associations Between Singlehood Self-Expansion Potential, Self-Expansion Experiences, and Singlehood Outcomes, unaeleza kuwa zaidi ya asilimia 40 ya watu wazima hupitia kipindi cha maisha ya useja katika hatua mbalimbali za maisha yao. Hii inajumuisha wale ambao hawajawahi kuingia katika ndoa au mahusiano ya kudumu pamoja na wale waliorejea kwenye useja baada ya talaka au kuvunjika kwa mahusiano. Watafiti walibaini kuwa watu wanaochagua kwa hiari kubaki bila wachumba huwekeza muda mwingi katika taaluma zao, masomo, biashara, usafiri, michezo, burudani na mahusiano ya kifamilia. Wengi wao huchukulia shughuli hizi kama njia ya kujenga maisha yenye maana na mafanikio. Miongoni mwa shughuli zilizotajwa kuwa chanzo kikuu cha ukuaji binafsi ni mazoezi ya mwili, sherehe za kijamii, kujumuika na marafiki, kula nje, mafanikio ya kitaaluma, matamanio mbalimbali na safari za mapumziko. Kinyume na dhana kwamba watu wasio na wachumba huishi maisha ya upweke, utafiti ulionyesha kuwa asilimia 83 ya washiriki walifanya shughuli zao za maendeleo binafsi wakiwa pamoja na watu wengine. Marafiki walikuwa kundi kubwa zaidi la waliowasaidia, wakifuatiwa na wanafamilia, huku asilimia 18 pekee wakifanya shughuli hizo wakiwa peke yao. Wanasaikolojia wanaeleza hali huu ni mchakato wa mtu kupanua maarifa, uzoefu na mtazamo wake wa maisha kupitia shughuli na mahusiano mbalimbali. Ingawa tafiti nyingi zimehusisha mchakato huo na mahusiano ya kimapenzi, utafiti huu unaonyesha kuwa ukuaji huo unaweza pia kupatikana nje ya mapenzi. Hata hivyo, watafiti waligundua kuwa watu wanaotamani kuingia katika mahusiano ya kudumu au wanaoamini kuwa furaha inapatikana tu kupitia mapenzi walikuwa na uwezekano mdogo wa kuona useja kama fursa ya maendeleo. Kwa upande mwingine, watu wenye kiwango kikubwa cha kujiamini walionekana kufurahia zaidi maisha ya useja na kuona fursa nyingi za kujikuza. Watafiti waliongeza kuwa matokeo hayo yalitokana na washiriki walio katika umri wa miaka ya 30 na 40, hivyo huenda yasiwakilishe kikamilifu uzoefu wa makundi yote ya watu wasio katika mahusiano. Hata hivyo, utafiti huo unaibua mtazamo mpya kwamba maisha ya useja yanaweza kuwa kipindi muhimu cha ukuaji, mafanikio na kujitosheleza binafsi.
Yesufu said Obi’s supporters would deploy representatives to polling units and monitor the movement of election materials and results from polling units through the various collation centres to Abuja.
Before the advent of religion, before the coming of missionaries with their books and bells, our forefathers had a way of naming men who walked among them with the grace of the divine. Such men were set apart. They did not eat like ordinary men, they did not think like ordinary men, and they did […]
Manchester United celebrated their return to the Champions League with a 4-0 thrashing of Sabah on Thursday, as Cesc Fabregas's Como impressed on their debut in Europe's premier club competition.
ABUJA: The Chairman of the Independent National Electoral Commission, INEC, Prof. Joash Ojo Amupitan, SAN, has said the successful deployment of Artificial Intelligence, AI, in electoral administration will depend more on strong institutions, governance structures and safeguards than on the sophistication of the technology. Amupitan stated this on Thursday, September 10, 2026, in Ottawa, Canada, […]
Rashford scored 14 goals in all competitions as Barcelona won La Liga and the Copa del Rey, but Deco said Gordon's style was considered a better fit for Hansi Flick's team.
Arsenal are close to finalising a new long-term contract for manager Mikel Arteta, with talks between the club and the Spaniard progressing positively.
—Stations to offer self-service fuel, EV charging, LPG, CNG By Obas Esiedesa, Abuja ABUJA — The Nigerian National Petroleum Company Limited, NNPC Ltd., has announced plans to deploy between 50 and 70 smart, self-service energy stations across the country within the next six months. The company said the initiative was part of its strategy to […]
KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amesema amejipanga kisaikolojia kwa lolote litakalotokea kwenye kibarua chake, ikiwamo kuondolewa kutokana na matokeo yasiyoridhisha, akisema mwenendo wa ligi umeanza kushuhudia baadhi ya makocha wakiondoka kwenye timu zao.
HESABU za kupanda Ligi Kuu Bara au kubaki Ligi ya Championship na presha ya kushuka daraja kwenda First League, zinatarajia kuanza leo Ijumaa Septemba 12, 2026 kwa timu nne kushuka uwanjani.
NAHODHA msaidizi wa KMKM, Martin Charles, amesema licha ya mshambuliaji wa Al Ahli Tripoli, Fiston Mayele kutupia bao kwenye mechi yao ya kwanza, lakini haikuwa kazi ngumu kumdhibiti.
VITA ya pointi tatu na heshima inatarajiwa kurindima usiku wa leo Ijumaa, Septemba 11, 2026, wakati Dodoma Jiji FC itakapoikaribisha Namungo FC kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuanzia saa 1:00 usiku ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Bara.
MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Maabad Maulid Maabad, amechekelea kuanza kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu, huku akibainisha kwamba anataka kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita.
…Spend hours in gridlock as LASTMA, TRACE deploy more personnel By Olasunkanmi Akoni LAGOS — Motorists and commuters plying the Lagos-Ibadan Expressway have continued to groan over severe traffic congestion following the commencement of repair works on the Kara Bridge. The two-week rehabilitation project, directed by the Minister of Works, Senator David Umahi, involves the […]
ZANZIBAR: President Samia Suluhu Hassan has expressed gratitude to Tanzanians, government leaders, diplomats, religious leaders and the international community for messages of condolence, prayers and support following the death of her husband, Hafidh Ameir Hassan. In a message issued from Zanzibar, President Samia thanked those who had extended messages of peace, comfort and prayers to…
Citizens of two African countries can travel to Canada without applying for a traditional visitor visa if they meet certain eligibility conditions and travel by air.
UTANGULIZI Ofisi ya polisi ni ya polisi tu. Unapoingia hata kama huna kosa ni lazima unywee. “Jina lako tafadhali.” Amour alimuulliza akiwa ameshika kalamu. “Naitwa Shefa Ibrahim.” Amour aliandika jina lake kabla ya kumuuliza. “Una umri gani?” “Mwezi ujao nitatimiza miaka ishirini na tisa.” SASA ENDELEA... “Unaishi wapi?” “Sinza.” “Unafanya kazi gani?” “Kazi?” “Ndiyo.” “Ndiyo niko kwenye mipango ya kazi.” “Tuache huko, tuje katika hili tukio lililotokea kule Mikocheni, ulilishuhudia?” “Ndiyo, nililishuhudia.” “Uliniambia unaishi Sinza, ulifuata nini Mikocheni?” “Huwa naenda kwa washikaji zangu kupiga stori.” “Wakati hilo tukio linatokea, ulikuwa wapi?” “Tulikuwa tumekaa masikani na washikaji wenzangu.” “Masikani yenu ilipo na mahali lilipotokea tukio hilo kuna umbali gani?” “Si mbali sana.” “Ni kama hatua ngapi?” “Kama hatua hamsini hivi.” “Sasa hebu eleza ulichoona.” “Kusema kweli lile gari la yule jamaa huwa tunaliona mara kwa mara likipita. Yule mshikaji ana kiwanda fulani cha maji, kipo pale pale Mikocheni…” “Ndiyo.” “Sasa lile gari lilikuwa linaelekea kwenye kile kiwanda cha maji safi. Ghafla wakatokea watu watatu mbele ya gari hilo.” “Hao watu walitokea wapi?” “Hatukuona walikotokea. Tuliwashitukia wakiwa wamesimama mbele ya gari hilo.” “Hilo gari lilikuwa linakwenda kwa mwendo gani?” “Lilikuwa linakwenda taratibu.” “Baada ya hao watu kuonekana hapo mbele ya gari nini kilitokea?” Inspekta Amour akauliza. “Lile gari lilisimama halafu yule jamaa aliyekuwa kwenye gari alifungua mlango. Wale watu watatu wakamvamia pale pale kwenye mlango. Tuliona wakisemeshana kisha yule mtu aliyevaa mavazi meusi alitoa kitu kama panga akamchinja yule jamaa.” “Hebu subiri. Huyo aliyevaa mavazi meusi ndiye yule ambaye inadaiwa shingo yake ilikuwa imechinjwa?” “Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, karibu robo tatu ta shingo ya yule mtu ilikuwa imechinjwa, yaani pale kwenye koo palikuwa pamekatwa kabisa.” “Sasa kama alikuwa amechinjwa kama unavyosema, kichwa chake kilikuwaje?” “Kilikuwa kinaning’inia kama vile kinataka kuanguka.” “Ndiyo unasema mtu huyo ndiye aliyetoa panga na kumchinja marehemu?” “Ndiye huyo huyo, yaani tulishangaa sana.” “Sasa wakati anamchinja, wale watu wengine walikuwa wanafanya nini?” “Walikuwa wakisaidia kumshika yule jamaa ili achinjwe.” “Baada ya kumchinja ilikuwaje?” “Yule mchinjaji akatia mkono kwenye gari na kutoa mkoba fulani akaufungua na kuutazama ndani. Nafikiri ule mkoba ulikuwa una pesa. Baada ya hapo wakatoweka na ule mkoba.” “Walitoweka vipi?” “Tuliona hawapo tena mahali pale. Hatukuweza kuona waliondoka vipi. Ilikuwa kama miujiza.” Inspekta Amour baada ya kuyasikiliza maelezo hayo alinyamaza kimya akafikiri kisha akamuuliza kijana huyo. “Una hakika kwamba maelezo yako ni sahihi?” “Nina hakika.” Kwa vile Amour alikuwa akiyaandika maelezo hayo alimwambia kijana huyo aweke sahihi yake. Baada ya kijana huyo kuweka sahihi Amour alimwambia. “Nipatie namba yako ya simu.” Shefa alimpa namba yake ambayo Amour aliiandika. “Unaweza kwenda. Mwambie mwenzako mmoja aingie.” Shefa akainuka na kutoka. Punde tu akaingia kijana mwingine. “Kaa kwenye kiti.” Amour alimwambia. Kijana huyo hakupishana sana kiumri na yule aliyetoka. “Jina lako nani?” “Naitwa Rich.” “Rich nani” “Temba” “Wewe ni mchaga.” “Ndiyo.” Amour alimsalimia kwa kutumia lugha ya kichaga na Rich akamjibu. Wakacheka. “Wewe pia ni mchaga?” “Hapana. Niliishi kule kwa miaka mingi.” Amour alipachika karatasi mpya kwenye jalada, akaandika jina la Rich. “Una umri gani?” “Miaka ishirini na tisa.” “Unaishi wapi?” “Mikocheni.” “Unafanya kazi gani?” “Mimi nasoma chuo cha utumiishi.” “Enhe hebu na wewe tueleze nini kilitokea hapo Mikocheni.” Rich alitoa maelezo ambayo hayakutofautiana na maelezo aliyotoa kijana aliyetoka. “Unadhani wale watu walikuwa kina nani?” Inspekta Amour alkamuuliza. “Wale walikuwa majambazi.” “Unazungumzia nini kuhusu yule mtu mnayesema kuwa shingo yake ilikuwa imechinjwa?” “Sijui yule alikuwa mtu wa aina gani lakini ni kweli shingo yake ilikuwa imechinjwa.” “Na ndiye unayesema kuwa amemchinja marehemu?” “Ndiye huyo huyo.” “Na baada ya kuchukua mkoba uliokuwa ndani ya gari waliondoka ghafla?” “Ndiyo waliondoka ghafla.” “Waliondokaje ghafla, hebu nieleze?” “Yaani wale watu baada ya kufanya kile kitendo walitupotea tu. Sijui ilikuwaje.” “Unaamini kwamba walikuwa na miujiza?” “Yaani ni kama walikuwa na miujiza Fulani.” “Sawa. Sasa nipatie namba ya simu yako. Ninaweza kukuhitaji tena.” Richa alitoa namba yake ya simu akampa Inspekta Amour. “Sawa. Unaweza kwenda. Huyo mwenzako aliyebaki mlilishuhudia pamoja hili tukio?” “Ndiyo, tulilishihudia pamoja.” “Nadhani maelezo yake yatakuwa haya haya. Kwa hiyo ukitoka mnaweza kwenda, nisipoteze muda wake bure.” ************ Nyumbani kwa Almasi tayari kulikuwa kumeshajaa watu. Yeye na mwanawe Martin walikuwa wakikaa Masaki lakini katika mitaa tofauti. Baada ya tukio la kuuawa Martin, Almasi aliuhamisha msiba nyumbani kwake. Ndugu, jamaa, marafiki na majirani walikuwa wamekaa vikundi vikundi nje ya nyumba ya Almasi ambako kuliwekwa viti pamoja maturubai ya kukinga jua. Hata hivyo watu wengi walikuwa wamesimama wakionekana kupatwa na sintofahamu kutokana na tukio la kuuawa Martin. Kila mtu ambaye alielezwa jinsi mauaji hayo yalivyotokea alikuwa akishangaa. Kikubwa kilichowashangaza watu yalikuwa yale maelezo kwamba mtu aliyemchinja Martin na yeye alikuwa amechinjwa! “Mtu aliyekatwa koo angewezaje kuwa hai na kumchinja mwenzake?” Hilo ndilo swali ambalo kila mmoja alikuwa akijiuliza bila kupata jibu sahihi. Ndani ya nyumba ya Almasi kulikuwa na sauti za vilio vya waombolezaji zilizokuwa zikisikika hadi nje. Mke wa Martin na mama yake Martin ndio waliokuwa wakiongoza kwa kulia. Baadhi ya ndugu na marafiki walikuwa wakiwabembeleza na kuwataka wawe na subira. Almasi mwenyewe alikuwa amekaa katika moja ya sebule za nyumba yake huku baadhi ya wanawe wengine pamoja na marafiki wakishughulika kukaribisha wageni waliokuwa wakiwasili. Baadaye msemaji wa familia ya Almasi alitoa tangazo akaeleza kwamba maziko ya marehemu Martin yatafanyika kesho yake hapo hapo Masaki. Alieleza kwamba mwili wa marehemu utaagwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita na utazikwa saa tisa alasiri. Kama ilivyokuwa imepangwa, saa tatu asubuhi ya siku iliyofuata mwili wa Martin ulitolewa nje kwa ajili ya kuagwa. Zoezi hilo liliendelea hadi saa sita mchana. Mpaka inafika saa nane, mwili wa Martin ulikuwa umeshafikishwa makaburini kwa ajili ya kuzikwa. Kila aliyehudhuria maziko ya Martin alikiri kuwa yalikuwa maziko yaliyosikitisha watu wengi. Si tu kwa vile Martin mwenyewe alikuwa bado kijana na ndiyo kwanza alikuwa amepata mtoto wake wa kiume bali mauaji yaliyomtokea yalikuwa yakikatili sana. Inspekta Amour ambaye pia alihudhuria maziko ya Martin aliwasha gari lake na kuondoka katika eneo hilo mara tu Martin alipozikwa. Alikwenda tena Mikocheni kuangalia mandhari ya mahali alipouawa Martin. Lengo lake lilikuwa ni kutengeneza picha ya mawazo ya jinsi Martin alivyouawa. Alipofika katika eneo hilo aligundua kulikuwa na kioski cha vinywaji baridi upande wa pili wa barabara karibu kabisa na mahali ambapo tukio la mauaji hayo lilitokea. Alisimamisha gari mbele ya kioski hicho akashuka na kwenda kwenye kidirisha cha kioski hicho. Muuzaji alikuwa kijana mmoja aliyekuwa akizungumza kwenye simu lakini alipomuona Amour alikata simu na kumsikiliza. “Kijana habari ya kazi?” Amour akamuuliza. “Nzuri. Nikusaidie nini?” “Nipatie kokakola baridi” “Unataka ya kuchukua au ya kunywa hapa hapa?” “Nataka ya kunywa hapa hapa.” Kijana akamtolea Inspekta Amour soda ya kokakola kutoka kwenye friji. Baada ya kuifungua chupa alimpa Inspekta Amour. Amour aliichukua na kugugumia funda moja la kokakola baridi kisha akamtazama kijana huyo. “Juzi palitokea patashika kubwa katika eneo lako,” akamwambia. “Oh! Juzi mzee kulikuwa na hekaheka. Majambazi waliua mtu hapa!” Kijana akadakia. “Lakini walikuwa majambazi kweli au…?” “Walikuwa majambazi.” “Wewe uliwaona?” “Niliwaona na niliona kila kitu kilichotokea. Wakati huo mimi nilikuwa hapa hapa kwenye kioski change.” “Mbona kuna watu wanasema sijui eti mmoja wa hao watu shingo yake ilikuwa imechinjwa?” “Sasa pale ndio sikuelewa wale watu walikuja na miujiza gani. Kweli shingo ya mmojawao ilikuwa imechinjwa na huyo jamaa ndiye aliyetoa panga na kumchinja Yule mhasibu wa kiwanda cha maji safi.”
BAADA ya Timu ya taifa ya Tanzania kwa wasichana U-20, Tanzanite Queens kupoteza mechi mbili mfululizo za Kundi B la Kombe la Dunia kwa wanawake leo itakuwa na dakika 90 ngumu za jasho na damu kuamua hatma ya kufuzu hatua ya 16 bora.