
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.


Alexis Mac Allister did his case for an improved Liverpool contract no harm with the winner as Andoni Iraola got off to a winning Champions League start by beating Atletico Madrid 2-1 on Wednesday.

Raphinha continued his superb goalscoring form with a brace as Barcelona demolished Feyenoord 5-1 to begin their Champions League campaign in perfect fashion on Wednesday.

ALIPONITHIBITISHA kuwa kweli mwanawe alikuwa ameuawa akaenda pembeni na kumpigia simu mke wake.

ALIPONITHIBITISHA kuwa kweli mwanawe alikuwa ameuawa akaenda pembeni na kumpigia simu mke wake.

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Clara Luvanga amejiunga na klabu ya Washington Spirit inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Marekani akitokea Al Nassr ya Saudia.




KOCHA MKUU wa Uhamiaji, Sheha Khamis amesema timu hiyo licha ya kupata ushindi katika mechi mbili ilizocheza katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu huu, lakini itaendelea kujipanga vyema kuhakikisha inazidi kuimarika.

Pamoja na kukiri ugumu wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kiungo mshambuliaji wa Namungo, Herbert Lukindo amesema uhakika wa namba na kiwango binafsi vinampa matumaini ya kuipa matokeo mazuri timu hiyo.

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), kimetoa amri kwa timu zote mkoani humo kuhakikisha zinakuwa na makocha rasmi na itakayokiuka haitoruhusiwa kushiriki mashindano yoyote ya soka katika mkoa huo.

RAIS wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, amesema mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji ndani ya klabu hiyo umeshakamilika rasmi, na sasa wanajiandaa kuingia kwenye hatua mpya ya utekelezaji.

ALIYEKUWA Katibu katika Wizara ya Michezo, Peter Kaberia, ni miongoni mwa maafisa 10 watakaofunguliwa mashtaka kutokana na madai ya kupotea kwa Sh330 milioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) la mwaka wa 2018. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) imethibitisha kuwa uamuzi wa kuwafungulia washukiwa hao mashtaka ulifikiwa baada ya uchunguzi uliofanywa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC). Kwa mujibu wa ODPP, kuna ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashtaka watu binafsi na kampuni zinazohusishwa na ununuzi usio wa kawaida na utovu wa nidhamu wa kifedha katika maandalizi ya mashindano hayo, ambayo hatimaye Kenya ilipoteza haki ya kuwa mwenyeji. Mashindano hayo yaliandaliwa na Morocco. “Baada ya kutathmini ushahidi kwa kina, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma amebaini kuwa kuna msingi wa kutosha wa kuwafungulia washukiwa na kampuni zinazohusika mashtaka,” ODPP ilisema katika taarifa. Watakaoshtakiwa pamoja na Balozi Kaberia ni pamoja na maafisa wakuu kutoka Wizara ya Michezo na wakurugenzi wa kampuni binafsi zinazodaiwa kunufaika kutokana na fedha hizo. Maafisa hao ni Stephen Njoroge Muthuma, Afisa Mkuu wa Fedha; Harun Chebet Komen, Mkurugenzi wa Utawala; Enock Ondwari Onditi na John Kiende Ruga. Wakurugenzi wa kampuni binafsi ni Marcos Gonzalez Puente wa Auditel Kenya, Samuel Mbaa Njoroge wa Taxwise Consulting Limited, Kitheka Muema wa Restea Enterprises Limited, Anthony Mwangi Kimanthi wa Lease Pride Limited, na Ephraim Kinyua Muchangi wa Leasepath Limited. Kampuni sita zinazokabiliwa na mashtaka ni Auditel Kenya, Taxwise Consulting Limited, Restea Enterprises Limited, Lease Pride Limited, Leasepath Limited na Liroma Assurance. Wanatarajiwa kujibu mashtaka yanayojumuisha matumizi mabaya ya mamlaka, ununuzi haramu wa mali ya umma, utovu wa nidhamu wa kifedha, na kushughulikia mapato ya uhalifu. Afisi ya DPP ilisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma. “Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma inathibitisha tena dhamira yake thabiti ya kuzingatia utawala wa sheria, kulinda rasilimali za umma, kuendeleza uadilifu, na kuhakikisha uwajibikaji katika usimamizi wa masuala ya umma,” taarifa hiyo iliongeza. Wakati huo huo, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Nick Mwendwa, ambaye pia alikuwa akichunguzwa kuhusiana na fedha za CHAN, ameondolewa katika tuhuma za makosa yoyote.


MATOKEO yasiyoridhisha kwa TRA United yametajwa kuwa sababu za timu hiyo kufikia makubaliano ya pande zote na aliyekuwa Kocha Mkuu wake, Ettiene Ndayragije kuachana, huku uongozi ukihaha kusaka mbadala.

TRA United imeachana na Kocha wake Mkuu, Etienne Ndayiragije, uamuzi uliotangazwa jana, Jumatatu, Septemba 7, 2026 saa siota usiku.

DAR City imeinyamazisha Stein Warriors katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), baada ya kuifunga kwa pointi 67-54.

BINGWA mtetezi wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), DB Lioness, ametema ubingwa baada ya kushindwa kutinga hatua ya robo fainali.

UTANGULIZI Almasi mwenyewe ndiye aliyetoa jina hilo kumpa mjuu wake. Alipofahamishwa kuwa mkwe wake alikuwa amejifungua alikwenda hospitalini alikokuwa amelazwa Hilda. Pamoja na mambo mengine, alimpa pole na hongera mkwe wake. Akakishika kichanga kilichozaliwa na kukiambia. “Wewe ni Almasi” Tangu hapo mtoto huyo akaanza kuitwa Almasi wakijua kuwa babu yake alikuwa ameshampa jina hilo.. Kuzaliwa kwa Almasi kulimfurahisha Martin na kumpa hisia kwamba alikuwa ametoka katika kundi la utoto na kuingia katika kundi la utu uzima kwani si muuda mrefu atakuwa akitwa baba.. SASA ENDELEA... ALIPOINGIA katika eneo la Mikocheni kilipokuwa kiwanda cha baba yake cha kuzalisha maji safi, Martin aliona watu wa ajabu waliokuwa wamesimama katikati ya barabara mbele yake Walikuwa watu watatu waliovaa mavazi kama kanzu. Wa kwanza alivaa kanzu nyeupe, wa pili alivaa kanzu nyeusi na wa tatu alivaa kanzu nyeupe, wakiwa miguu peku peku. Yule aliyekuwa katikati ambaye alivaa kanzu nyeusi, kichwa chake kilikuwa kikining’inia kikiwa na ishara ya kuchinjwa kwenye koo huku michirizi ya damu iliyoganda ikionekana. Kwenye mkono wake wa kulia alikuwa ameshika upanga uliokuwa unang’aa. Martin alishituka na kusimamisha gari. Wakati anafungua mlango wa gari ili atoke, wale watu walishamfikia kwenye mlango. Yule mtu ambaye kichwa chake kilikuwa kikining’inia alimuuliza Martin. “Wewe ni mtoto wa Alamsi?” “Ndiyo.” Martin alijibu kwa kiwewe. “Baba yako alikuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana!” “Masharti yapi?” “Muda wako umekwisha, huwezi kupata jibu.” Hapo hapo ule upanga ukapita kwenye koo la Martin na kulichinja! Martin hakuwahi hata kupiga kelele. Ule mshituko wa kuchinjwa ulimfanya akurupuke na kutoka mbio huku shingo yake ikining’inia baada ya kuchinjwa. Ilifanana na ya yule aliyemchinja. Martin hakuweza kupiga hata hatua tano akaanguka chini akiwa amekufa. Yule mtu aliyemchinja alitia mkono kwenye gari na kuuchukua ule mkoba wa pesa akapotea na wale wenzake. ********** Ndani ya ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya jinai, Makao Makuu ya polisi jijini Dar, Inspekta Amour alikuwa amekiacha kiti na kusimama kando ya dirisha akitazama nje ya ofisi. Anapokuwa amekabiliwa na maamuzi mazito, mara nyingi alipenda kusimama kuliko kukaa. Siku ile ilikuwa ni moja ya siku ambazo aliiona kazi yake kuwa ngumu. Tangu kulipokucha alishapokea kesi nzito zaidi ya sita ambazo zilihitaji uchunguzi wake. Kulikuwa na mauaji ya watu watatu yaliyotokea Kigamboni ambayo licha ya silaha iliyotumika katika mauaji kupatikana, muuaji alifanikiwa kutoweka. Ilidaiwa kuwa yalikuwa mauaji ya kulipa kisasi lakini kilichowashitua zaidi polisi ni bunduki ya kijeshi ambayo ilikutwa katika eneo la tukio ikiwa na upungufu wa risasi tatu ambazo polisi waliamini ndizo zilizotumika katika mauaji hayo. Licha ya polisi kuumiza vichwa kwa kujiuliza muuaji huyo alikuwa nani na watampata wapi, bado walikuwa katika taharuki baada ya kukuta silaha iliyotumika katika mauaji ilikuwa ni ya kijeshi tena mali ya jeshi la polisi! Amour alifika katika eneo la tukio ambapo aliambiwa na mkuu wake amtafute muuaji hadi amtie mikononi. Wakati huo tayari Amour alikuwa na kesi kadhaa zilizohitaji upepelelezi. Kama haitoshi nusu saa tu iliyopita alikuwa ameitwa katika tukio jingine la ujambazi uliofanyika katika benki moja ya jijini. Ingawa hakukuwa na mtu yeyote aliyeuawa, fedha za benki zilizokuwa zikitoka Benki Kuu zaidi ya shilingi bilioni tatu zilikuwa zimeibiwa. Matukio hayo ambayo yangehitaji uchunguzi wake, yalikuwa yakimuumiza kichwa. Baada ya kuwasili ofisini kwake alipekuwa majalada yaliyokuwa mezani kwake kisha akainuka na kusimama kando ya dirisha. Alifahamu kuwa uzembe wa walinzi wa benki ambao alikuwa amewatia ndani, ndio uliosababisha kuporwa kwa pesa hizo. Amour alishuku kuwa ujambazi huo ulifanikiwa kutokana na njama kati ya majambazi hao na walinzi wa benki. Wakati akiwaza hayo alishitushwa na muungurumo wa simu iliyokuwa juu ya meza yake. Alirudi kwenye meza akauinua mkono wa simu huku akiketi kwenye pembe moja ya meza. Akauweka mkono wa simu sikioni kisha akasema. “Inspekta Amour hapa.” “Amour kuna kazi gani iliyoko mikononi mwako?” Sauti ya mkurugenzi wa upelelezi ikaunguruma kutoka simu ya upande wa pili. “Kazi zilizoko mikononi mwangu ni nyingi. Kuna lile tukio la mauaji lililotokea Kigamboni na kuna ule ujambazi uliofanyika benki.” “Ziache kazi hizo, nitawapa wapelelezi wengine. Kuna tukio la mauaji ya ajabu limetokea huko Mikocheni. Tafadhali fika hapa ofisini kwangu sasa hivi.” Inspekta Amour aliurudisha mkono wa simu kwenye sehemu yake kisha akauchukua ufunguo wa gari uliokuwa juu ya meza. Wakati Amour anatoka ofisini mwake alishangaa kuona alikuwa akiongezewa kazi wakati tayari akiwa na kazi zilizomlemea. Alijiuliza kama hakukuwa na makachero wengine wenye sifa ambao wangeweza kupewa kazi aliyotakiwa kupewa yeye. Alipotoka ofisini mwake aliingia kwenye lifti akapaa hadi horofa ya saba ilikokuwa ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi. Kama afisa maalum aliruhusiwa kuingia na kuonana na mkurugenzi huyo. “Kaa kitako tafadhali” Mkurugenzi huyo alimwambia Amour alipomuona akiingia ofisini kwake. Licha ya umri wake kukaribia miaka sitini, mkurugenzi huyo alionekana mkakamavu na mwenye wajihi wa kupendeza. Nywele zake zilikuwa nyeupe tupu. Alikuwa amevaa shati jeupe na suruali nyeupe na alikuwa amefunga tai. Amour alikaa kwenye kiti mbele ya meza ya mkurugenzi. Hakumsalimia kwa sababu walishakutana asubuhi. “Amour kuna mauaji yametokea Mikocheni sasa hivi” Mkurugenzi alianza kumueleza Amour. “Nimekuita wewe kwa sababu yanaonekana ni mauaji ya kutisha kidogo na si ya kawaida kutokea” “Ni watu wangapi waliouawa?” “Ni mtu mmoja. Watu wanaodaiwa kuua ni watatu lakini walioshuhudia tukio hilo wamewaeleza polisi kuwa hao watu ni wa ajabu.” Mkurugenzi wa upelelezi alimueleza Amour jinsi tukio hilo la mauaji lilivyotokea kama lilivyoelezwa na mashuhuda. Maelezo ya mkurugenzi huyo kidogo yalimshangaza Inspekta Amour. “Umeniambia kuwa huyo mchinjaji na yeye alikuwa amechinjwa?” “Ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo. Wamesema kwamba shingo ya mchinjaji ambaye alikuwa amevaa mavazi meusi, ilikuwa ikining’inia ikionesha ishara ya kuchinjwa.” “Huyo mtu aliyechinjwa atakuwa na uwezo wa kumfuata mtu na kumchinja na kisha kutoweka?” Amour aliuliza kwa mshangao. “Ndiyo maana nimekueleza kuwa mauaji yenyewe si ya kawaida. Kuna kitu kama miujiza ndani yake. Hebu nenda kafanye uchunguzi wako. Kwanza fika katika eneo la tukio, uliza tukio lilitokeaje na uanze upelelezi mara moja. Nataka uhakikishe hao wauaji wanakamatwa haraka” ************* Amour alifika katika eneo la tukio. Alikuta bado polisi walikuwa katika eneo hilo. Pia kulikuwa na watu waliokusanyika mahali hapo kuangalia kilichotokea. Amour aliliegesha gari akashuka na kujipenyeza kwenye kundi la watu ambao walimpa nafasi ya kupita hadi akalifiikia gari la Martin. Mwili wa Martin ulikuwa bado haujaondolewa. Polisi walikuwa wakiupiga picha. Polisi wengine walikuwa wameshika futi wakipima urefu wa kutoka mwili huo ulipoanguka na gari lake lilipokuwa. Kando ya mlango wa gari upande wa dereva ambapo palikuwa na michanga, alama za miguu za watu waliomuua Martin zilionekana. Alama hizo nazo zilipigwa picha Mzee Almasi, baba yake Martin alikuwa amesimama nyuma ya polisi aliyekuwa akipiga picha huku ameshika kitambaa cha kujifutia jasho mkononi. Alikurupushwa nyumbani kwa simu aliyopigiwa na rafiki yake ambaye alimuarifu kwamba mwanawe alikuwa ameuawa. “Unasemaje?” Almasi aliuliza kwa hamaki mara tu alipoarifiwa kuhusu tukio hilo. “Mwanao Martin amekutwa ameuawa hapa Mikocheni mbali kidogo na kiwanda chenu cha maji safi.” “Ameuawa na nani?” “Haijafahamika bado lakini ungefika kwanza ili ushuhudie mwenyewe.” Almasi alikumbuka kwamba Martin alikuwa amekwenda benki kuchukua pesa za mishahara ya wafanyakazi. Akahisi huenda pesa hizo zilikuwa zimeporwa. Alikata simu aliyokuwa amepigiwa akampigia Martin. Simu ya Martin iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Ilipopokelewa sauti ilikuwa ni ya mtu mwingine. “Jitambulishe wewe ni nani?” Sauti hiyo ambayo ilikuwa ya polisi ikamuuliza. “Mimi ni Almasi, ninampigia mwanangu Martin.” “Unazungumza na polisi. Kuna kijana ambaye ameuawa hapa Mikocheni. Inawezekana ndiye mwanao. Tafadhali hebu fika hapa haraka.” Hapo ndipo Almasi alipoamini kuwa kulikuwa na tukio hilo. Aliondoka nyumbani bila kumuarifu lolote mke wake. Akajipakia kwenye gari na kuondoka. Alifika Mikocheni na kushuhudia mwenyewe kilichokuwa kimetokea. Aliliona gari la mwanawe kisha akauona mwili wa Martin uliokuwa umechinjwa. Ingawa alijikaza kiume, aliona machozi yakianza kumtiririka. Alitoa kitambaa kutoka mfukoni mwake akajifuta machozi pamoja na jasho lililokuwa limetanda usoni kwake.

Kigogo Mighty Wanderers atua Dar, aiwahi mapema Simba, afunguka dozi wanavyoiandaa

DAR ES SALAAM: Khalid Shemndolwa na Yvonne Ondari wameibuka mabingwa wa jumla katika mashindano ya gofu ya Vodacom Corporate Masters 2026 yaliyofanyika katika Uwanja wa TPDF Lugalo Golf Club jijini Dar es Salaam. Shemndolwa alitwaa ubingwa kwa upande wa wanaume baada ya kukusanya pointi 42 katika mashindano hayo ya siku moja, huku Ondari akifikisha idadi…

Political parties, religious leaders, diplomats, civil society representatives and other stakeholders have called for dialogue, stronger institutions and political reforms as Tanzania seeks common ground on how to strengthen democracy and prevent a repeat of the divisions and violence witnessed during and after the 2025 General Election.

A Tribunal observed that under Kenyan law, aspects of works generated by AI are not eligible for copyright protection unless an author can distinguish or demonstrate sufficient human intervention or effort giving the work an original character.

TIMU ya Chipukizi, imeanza msimu wa 2026-2027 katika Ligi Kuu Zanzibar vibaya baada ya kuambulia vipigo viwili na sare moja.

KOCHA Msaidizi wa Mlandege, Sabri China amesema udhaifu katika eneo la ushambuliaji pamoja na hofu iliyowakumba wachezaji wakati wa mchezo ni miongoni mwa sababu zilizochangia timu hiyo kupoteza dhidi ya Polisi.

UTANGULIZI Mtu aliyekuwa karibu yake aligeuka ghafla na kumpiga kwa kitu kizito kichwani. Frenk alipiga yowe akaanguka hapo hapo akiwa amepotewa na fahamu. Mtu aliyempiga aliinama akamshika mikono na kumburuza kwenye kichaka kilichokuwa pembeni mwa njia. Alimuingiza ndani ya kichaka hicho akamlaza chini. Wenzake walimfuata. Yule aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ameshika begi ambalo aliliweka chini. Alitoa simu kutoka mfukoni mwake akaipiga. Baada ya muda kidogo simu yake ilipokelewa.. SASA ENDELEA... ““TUMESHAMPATA yule mtu na tuko naye hapa njia panda ya kuja Marerani. Sasa njoo mara moja tumshughulikie,” akasema kwenye simu. “Ni kijana?” Sauti ikauliza kutoka kwenye simu. “Bado ni kijana sana na ana umbile lililotakiwa.” “Mmemfunga sawasawa?” “Samueli amempiga kichwani kwa kitako cha bastola, amezirai.” “Sasa mmemfunga? Akizinduka anaweza kuleta usumbufu.” “Sawa, tutamfunga kamba mikononi na miguuni.” “Mkishamfunga mnisubiri hapo hapo.” “Sawa.” Yule mtu aliirudisha simu yake mfukoni akachutama na kufungua lile begi. Alitoa furushi la kamba akawapa wenzake. “Mfungeni kamba miguuni na mikononi. Jamaa anakuja sasa hivi.” Watu hao walilifungua lile furushi la kamba na kulichakua. Zilikuwa kamba nyingi ambazo zilikuwa vipande vipande. Walichukua vipande hivyo vya kamba wakamfunga Frenk mikononi na miguuni. “Sasa tusubiri hapa hapa.” Yule aliyekuwa akiendesha gari aliwambia wenzake. Alitazama saa yake kisha akatoa sigara na kujiwashia. Baada ya kupita kama nusu saa hivi, simu yake ikaita. Aliitoa mfukoni na kuipokea. “Sasa mpakieni kwenye gari, muje naye chimboni. Mganga amesema kafara lake ni lazima lifanyike kwenye chimbo na huu ndio muda muafaka.” Sauti ikasikika kwenye simu.. “Sawa.” Mtu huyo aliirudisha simu mfukoni akawambia wenzake wambebe yule kijana na kumpakia kwenye gari. “Kwanini?” Mmoja akamuuliza. “Amesema kafara lake linatakiwa lifanyike chimboni.” “Yaani tutakwenda naye huko huko?” “Hakuna tatizo. Hivi sasa ni saa nane usiku, kila mtu amelala. Nani atatuona?” Walimbeba Frenk wakampakia katika siti ya nyuma ya gari hilo. Mtu mmoja alikaa naye kwenye siti. Mwingine alikaa siti ya mbele pamoja na aliyekuwa akiendesha gari hilo. Gari likawashwa moto na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari hilo likaingia katika viunga vya eneo la Marerani. Lilisimama karibu na chimbo moja lililokuwa karibu na kibanda kimoja kilichojengwa kwa miti. Aliyekuwa akiendesha alishuka na kwenda kwenye kile kibanda ambako kulikuwa na watu wawili waliokuwa wamekaa. “Tumekuja naye.” Mtu huyo aliwambia watu hao. “Amezinduka?” Mmoja kati ya wale watu wawili waliokuwa wamekaa, akauliza. “Hajazinduka na tumemfunga kamba.” “Sasa mtoeni kwenye gari. Mumburuze hadi pale kwenye chimbo. Fanyeni haraka. Hivi sasa watu wengi wamelala.” Mtu huyo alirudi tena kwenye gari akawambia wenzake wamtoe Frenk na kumburuza kwenye chimbo. Wakati watu hao wakifanya hivyo, mtu aliyetoa agizo hilo alimuacha mwenzake amekaa, akaenda kwenye chimbo akiwa ameshika mfuko. Alipofika kwenye chimbo hilo aliuweka chini ule mfuko akatoa pembe mbili zilizofungwa kwa vitambaa vyeusi na vyekundu. Pia alitoa tunguri mbili alizoziweka karibu na mlango wa chimbo hilo. Frenk aliletwa mahali hapo kwa kuburuzwa chini ambapo isingekuwa rahisi kwa mtu aliyekuwa mbali kumuona usiku huo kutokana na kutokuwepo kwa mwanga wa taa. Frenk alilazwa kichalichali karibu na mlango wa chimbo. Yule mtu aliyetoa pembe na tunguri alichukua pembe moja na kumzunguka Frenk huku akimmwagia mavumba. Alimzunguka mara saba. Alipomaliza aliziweka zile pembe akachukua tunguri na kuzunguka nazo mara saba huku akitabana maneno ya kichawi. Alipomaliza alivua nguo zake zote akafanya mauzauza kabla ya kuwambia wale watu kwamba wamchinje kijana huyo. Mtu mmoja akamshika Frenk ili asifurukute na mwingine alitoa kisu na kukishika kichwa cha Frenk. Hapo hapo Frenk akazinduka. “Kitu gani?” Akauliza kwa mshangao. Hakukuwa na aliyemjibu. “Niko wapi hapa na kwanini nimeshikwa hivi na kufungwa?” Akaendelea kuuliza. Aliyekuwa amemshika alimshika vizuri. Yule aliyeshika kisu akaanza kumchinja harakaraka huku yule aliyevua nguo akisaidia kumshikilia asifurukute. Kisu kilipoanza kukata koo, Frenk alianza kukoroma. Alijaribu kufurukuta lakini waliomshika walikuwa wamemdhibiti sawasawa. Damu ikaanza kumwagika. Dakika tatu tu baadaye kichwa kilikuwa kimetenganishwa na kiwiliwili! Ile damu iliunda mchirizi na kuchirizikia kwenye mlango wa chimbo. Mwili wa Frenk uliendelea kushikiliwa mpaka ulipotulia kabisa. Ndipo yule mtu aliyekuwa amekaa kwenye kile kibanda alipoinuka na kwenda mahali hapo. “Tayari?” Akauliza. “Tayari.” Mtu mmoja akamjibu. “Sasa mrudisheni kwenye gari mwende mkamzike.” Yule mtu aliyevua nguo alisema huku akivaa suruaIi yake. Watu hao walishika miguu ya Frenk wakamburuza hadi kwenye gari. Wakafungua boneti la nyuma na kuutia mwili huo. Mmoja alirudi kufuatia kichwa cha frenk ambacho pia alikitia ndani ya boneti. Aliyekuwa akiendesha gari hilo alikuwa amesimama akizungumza na yule mtu waliyemkuta hapo pamoja na yule mganga. “Mtamzika mahali mbali na hapa. Mtakwenda kuchimba shimo refu ili mwilli wake usifukuliwe na fisi. Si mmesema hafahamiki?” Mtu huyo alimuuliza yule aliyekuwa akiendesha gari. “Hafahamiki.Tumeambiwa kwamba alifika leo pale gesti, anamtafuta ndugu yake.” “Alitokea wapi?” “Alitokea Dar es Salaam.” “Atakuwa ni mgeni. Hakuna anayemfahamu. Sasa nendeni mkachimbe kaburi mumzike. Tukutane asubuhi.” “Sawa,” aliyekuwa akiendesha gari alisema kisha akaondoka kuelekea lilikokuwa gari hilo. Alifungua mlango akajipakia na kuliondoa gari. Mganga alikuwa akiitia michanga ile damu ya Frenk ili isionekane. Alipomaliza alimsogelea yule mtu aliyekuwa naye ambaye alikuwa amesimama kando yake. “Naona kazi imekwisha. Sasa zingatia vile nilivyokueleza. Asiingie mtu kwenye chimbo hili mpaka baada ya siku tatu. Wataingia watu watatu tu wakiwa uchi. Umenielewa?” “Nimekuelewa vizuri.” “Hawatafukua umbali mrefu watakuta mwamba ambao watautoboa. Huo mwamba una mali za majini ambazo huwezi kuzipata mpaka ufanye kafara la roho kama tulilolifanya hapa. Wakishapata hizo mali watatoka wakiwa uchi. Watavaa nguo watakapotoka. Sijui kama unanielewa vizuri?” “Nakuelewa vizuri.” “Mali watakayopata itatosha kukupa utajiri katika maisha yako yote na hutakiwi kurudia mara ya pili. Ukishapata hiyo mali nenda katafute biashara nyingine ufanye, ukirudia mara ya pili utakufa.” “Sawa mzee.” “Kingine ninachotaka kukukumbusha ni kuwa katika utajiri wako kila mwaka ukazamishe baharini fedha za mapato yako ambazo ni sawa na theluthi moja ya mapato yako. Hiyo ni zaka ya majini waliokupa mali.” “Kama kweli nitafanikiwa nitafanya hivyo. Lakini ningependa kujua hizo fedha niziweke kwenye nini kabla ya kuzizamisha baharini?” “Swali zuri sana. Hizo pesa utazitia kwenye mfuko mweupe. Utashona mfuko mweupe. Utaweka na jiwe ili ziweze kuzama chini. Unaweza kukodisha boti ikupeleke mbali kidogo.” “Sawa. Nimekuelewa.” ************ Miaka kumi na mitano baada ya kuuawa Frenk. Martin Almasi aliuondoa mkoba wake wa kiofisa kutoka katika kaunta ya benki baada ya kuzipanga noti alizozitoa hapo benki. Akiwa ameushika mkoba huo kimadhubuti aligeuka na kuelekea katika mlango wa kutokea benki. Aliusukuma mlango wa benki akatoka nje na kulifuata gari lake alilokuwa ameliegesha katika eneo la maegesho. Kila mwezi alikuwa akienda mwenyewe benki kutoa pesa za mishahara ya wafanyakazi wao. Siku ile alikuwa amekwenda kuchukua pesa za mishahara. Alipofika kunako gari lake la kifahari, Martin alijipakia na kuliwasha gari hilo, akatia gea na kuliondoa. Huku akiendesha kwa mwendo wa kasi kidogo, Martin alijiona alikuwa mmoja wa vijana waliofanikiwa katika jjiji la Dar. Alikuwa ameshaoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja aliyekuwa akimpenda sana. Alimuoa mwanachuo mwenzake wa chuo cha uhasibu ambaye alipendana naye tangu wakiwa wanasoma. Baada ya kuanza kazi kwa baba yake ndipo alipofunga uchumba na Hilda ambaye kwa wakati huo alikuwa ameajiriwa serikalini. Miezi michache baadaye Hilda alipata ujauzito ambapo alikuja kujifungua mtoto wa kiume waliyempa jina la Almasi ambalo ni jina la babu yake. Almasi mwenyewe ndiye aliyetoa jina hilo kumpa mjuu wake. Alipofahamishwa kuwa mkwe wake alikuwa amejifungua alikwenda hospitalini alikokuwa amelazwa Hilda. Pamoja na mambo mengine, alimpa pole na hongera mkwe wake. Akakishika kichanga kilichozaliwa na kukiambia. “Wewe ni Almasi” Tangu hapo mtoto huyo akaanza kuitwa Almasi wakijua kuwa babu yake alikuwa ameshampa jina hilo.. Kuzaliwa kwa Almasi kulimfurahisha Martin na kumpa hisia kwamba alikuwa ametoka katika kundi la utoto na kuingia katika kundi la utu uzima kwani si muuda mrefu atakuwa akitwa baba.

UTANGULIZI Kazi ya kuchimba madini imegeuzwa ya kishirikina. Mauaji na makafara ni vitu vya kawaida. Almasi aliimaliza familia yake yote. Na mwisho aliimaliza familia yake yote pamoja na yeye mwenyewe. SASA ENDELEA... Aliwasili jijini Dar dakika chache kabla ya saa nne usiku. Safari ya mchana kutwa kutoka Mwanza ambako aliondoka asubuhi ilimfanya ajisikie kuchoka. Mara tu aliposhuka kwenye basi, Frenk alitoka katika stendi ya Mbezi akapanda daladala iliyokuwa inakwenda Kariakoo. Ilikuwa mara yake ya pili kuwasili katika jiji hilo. Mara ya kwanza ilikuwa miaka mitano iliyopita. Alikuja kumtafuta kaka yake Amon Marwa aliyekuwa amehamia Dar miaka mingi iliyopita. Kwa vile hakuwa na anuani ya mahali alipokuwa anaishi, Frenk alijikuta akichanganywa na jiji hilo. Aligundua jiji la Dar halikuwa kama lilivyo jiji la Mwanza ambalo alikuwa amelizoea. Aligundua kuwa Dar es Salaam lilikuwa jiji kubwa na kwa mgeni kama yeye lilikuwa linatatiza. Aligundua haikuwa rahisi kumpata mtu anayemtafuta bila kuwa na anuani yake sahihi ya mahali anapoishi, mtaa na namba ya nyumba. Yeye hakuwa navyo. Frenk baada ya kuhangaika kwa siku tatu bila mafanikio ya kumpata kaka yake, akaamua kurudi Mwanza. Miaka mitatu baadaye akapata anuani ya kaka yake. Kuna mtu ambaye alimwambia kwamba alikutana na Amon na alimkaribisha nyumbani kwake Ilala jijini Dar. Alimwambia kwamba Amon alikuwa ameoa mwanamke wa Kirufiji na alikuwa amezaa naye watoto watatu. Kwa vile alitajiwa mtaa na namba ya nyumba aliyokuwa anaishi Amon, Frenk alitafuta nauli, alipofanikiwa kuipata akaamua kurudi tena Dar kumfuata kaka yake. Walikuwa wamepoteana kwa miaka mingi iliyopita tangu wakiwa watoto. Mara tu wazazi wao ambao walikuwa wakulima walipofariki dunia, Amon akafanikiwa kwenda Dar akamuacha mdogo wake akilelewa na shangazi yake. Baada ya kuja Dar, Amon hakurudi tana Mwanza. Shangazi yao alipofariki, maisha yalizidi kuwa magumu kwa Frenk. Hivyo aliamua kwenda kumtafuta kaka yake ili kama amefanikiwa kimaisha amsaidie kupata kazi. Kulikuwa na watu waliokuwa wakimpa matumaini waliomwambia kwamba kaka yake alikuwa tajiri mkubwa jijini Dar, akifika Dar na kumuulizia tu atapelekwa hadi kwenye geti la nyumba yake. Daladala ilipomshusha Kariakoo, aliamua kwenda Ilala kwa miguu. Aliutafuta mtaa aliotajiwa. Alipoupata aliitafuta nyumba ya Amon ambayo namba yake alikuwa ameikariri. Akaipata. Alipoiona nyumba aliyokuwa anaitaka alipata furaha iliyochanganyika na mshituko. Alipata furaha kwa sababu aliiona nyumba aliyokuwa anaitafuta lakini alipata mshituko kuona nyumba yenyewe ilikuwa ni ya kawaida na si ya kifahari kama alivyoambiwa na baadhi ya watu huko Mwanza. Alibisha kwenye mlango. Mlango ukafunguliwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akitoka na hamsini zake. Frenkk alimsalimia. Baada ya salamu akamuuliza. “Sijui nimemkuta Amon?” “Amon nani?” Kijana akamuuliza. “Amon Marwa.” “Oh! Amon aliondoka kwenda Arusha.” “Alienda lini?” “Mh!Muda kidogo, inafika miezi sita sasa.” “Mke wake yupo?” “Alipoondoka alimuacha mke wake lakini alishindwa kulipa pango ikabidi aende kwao.” “Kwani Amon alikwenda kufanya nini huko Arusha?” “Siwezi kujua lakini kuna watu walisema walikuwa wanamkuta kwenye gesti moja jirani na stendi ya mabasi pale Arusha.” Ndoto ya kumpata kaka yake ikayayuka kichwani mwake kama bonge la barafu lililotiwa kwenye ndoo ya maji. “Kwani hapa Dar alikuwa akifanya shughuli gani?” Akamuuliza yule kijana kwa sauti ya kukata tamaa. “Alikuwa akifanya biashara ya duka lakini alifilisika. Nafikiri labda aliamua akatafute maisha huko Arusha.” Yule kijana akaondoka na kumuacha Frenk akiwa ameduwaa kando ya mlango. Jirani na hapo palikuwa na gesti. Frenk akajikuta akitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika gesti hiyo ambapo aliamua kupangisha chumba cha kulala baada ya kumkosa kaka yake. Asubuhi kulipokucha Frenk akapata uamuzi wa kwenda Arusha kuendelea kumtafuta Amon. Alikuwa na imani kuwa huenda alikuwa amefanikiwa huko Arusha na mahali pa kwanza pa kumtafuta ni hapo gesti ambapo aliambiwa alikuwa akionekana. Alipanda basi la asubuhi sana kwenda Arusha. Karibu safari nzima alikuwa akimuwazia kaka yake. Alijiambia endapo atafanikiwa kuonana naye atakuwa ametimiza lengo lake. Alijua kuwa angeweza kumkuta akiwa na mafanikio au akisaga lapa kama yeye. Lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, alijiambia, kule kukutana kwao tu kungeweza kuwa mwanzo wa mafanikio yao. Alifika Arusha jioni. Aliposhuka kwenye basi alikwenda kuitafuta gesti aliyoambiwa ilikuwa jirani na stendi. Baada ya kuulizauliza wenyeji alielekezwa gesti hiyo. Akaenda kuonana na mhusika. Alipomuuliza kaka yake, aliambiwa walikuwa hawamfahamu. “Alitoka wapi??” Kijana wa gesti akamuuliza. “Alitoka Dar kama miezi sita iliyopita. Niliambiwa alikuwa akionekana katika gesti hii.” “Hapa kwetu wanafika watu wengi kutoka Dar, hatuwezi kujua ni nani mmojawapo.” “Nimesema anaitwa Amon.” “Amon wako wengi. Hatuwezi kujua ni Amon yupi unayemuuliza wewe.” “Yeye ni Amon Marwa.” “Yukoje?” “Tuliachana Mwanza tukiwa wadogo. Sijui umbo lake lilivyo kwa sasa. Wakati huo alikuwa ni mwembamba.” “Kwa kweli itakuwa ni vigumu kumtambua.” Baada ya maelezo yake kutosaidia kumtambulisha aliyekuwa anamtafuta, aliamua kukodi chumba hapo hapo. Akajiambia atamtafuta kaka yake kwa siku mbili. Endapo hatafanikiwa kumpata atarudi Mwanza. Baada ya kupata chumba alioga akabadili nguo alizokuwa maevaa kisha alitoka kwenda katika mkahawa uliokuwa karibu kupata chakula. Baada ya kula alirudi gesti kulala. Hakukumbuka ilikuwa saa ngapi alipoamshwa usingizini. Kwanza alidhani alikuwa anaota baada ya kusikia mlango wa chumba alichokuwa amelala ukibishwa. Baada ya fahamu kumrudia vizuri aligundua kuwa hakuwa akiota bali mlango ulikuwa unabishwa kweli. Akainuka kitandani na kwenda kuufungua. Alimkuta kijana aliyempangisha chumba hapo gesti akiwa na mtu mmoja ambaye alimwambia alikuwa akimfahamu mtu aliyekuwa akimuulizia. “Unamfahamu Amon?” Frenk akamuuliza yule mtu kwa mshituko. “Ndiyo namfahamu. Aliwahi kukaa hapa gesti kwa muda mrefu, hivi sasa yuko wilaya ya Simanjiro anafanya biashara.” “Sasa nitampataje?” “Mimi naenda huko huko. Kama unataka twende nitakupeleka mahali aliko.” “Kweli tutapata usafiri usiku huu?” “Nina gari yangu binafsi, tunaweza kwenda tu.” “Basi subiri nivae twende.” Frenk akarudi ndani. Alivaa nguo haraka haraka akachukua begi lake na kutoka. Yule mtu alikuwa akimsubiri ukumbini. “Twenzetu,” akamwambia. Walitoka nje ya gesti ambapo palikuwa na gari aina ya Noah iliyoegeshwa. Ndani ya gari hilo kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa amekaa siti ya nyuma. Frenk aliambiwa akae siti ya mbele kando ya dereva. Akafungua mlango na kujipakia. Yule mtu naye alikaa katika siti ya dereva akaliwasha gari na kuanza safari ya kuelekea wilaya ya Simanjiro. “Mimi naitwa Rafael, je wewe mwenzngu unaitwa nani?” Mtu huyo alimuuliza Frenk baada ya kimya kifupi. “Mimi naitwa Frenk.” “Huyo Amon ni nani wako?” “Ni kaka yangu. Tuliachana zamani sana huko Mwanza.” “Alikuja hapa Arusha miezi sita iliyopita. Hivi sasa anaishi Simanjiro na amefanikiwa sana kimaisha.” “Nitafurahi sana kumuona kaka yangu. Uliniambia kuwa mnafahamiana?” “Tunafahamiana na tunaihsi jirani. Wewe hujawahi kufika hapa Arusha?” “Sijawahi kufika.” “Na huko Simanjiro ndiyo hukujui kabisa?” “Kwa kweli huko sikujui.” “Basi leo utakujua.” “Nitafurahi.” Safari ikaendelea. Gari hilo liliwasili Simanjiro saa nane usiku. Lilisimama mbele ya nyumba moja ambapo aliyekuwa akiendesha alishuka akaenda kubisha mlango. Baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa, mtu huyo akaingia ndani. Haikupita muda mrefu akatoka akiwa na mwenzake aliyekuwa ameshika begi. Mwenzake alijipakia katika siti ya nyuma. Akakaa na Frenk. “Vipi bwana?” Akamuuliza frenk. “Salama tu.” Gari likawashwa moto na kuendelea na safari. “Hivi sasa tunakwenda nyumbani kwa Amon,” aliyekuwa akiendesha alimwambia Frenk. “Ni mbali sana kutoka hapa?” “Hapana. Ni karibu tu.” Baada ya mwendo mfupi walivuka daraja, wakaingia katika barabara za vichochoro. Walitokea katika eneo ambalo lilikuwa na pori. Baada ya kulipita pori hilo, gari likasimama ghafla karibu na kichaka. Aliyekuwa akiendesha alisonya kisha akafungua mlango. “ Hili gari limeshaanza matatizo. Limezima ghafla,” alijisemea kabla ya kushuka na kwenda mbele ya gari hilo ambapo alifungua boneti la mbele. Wenzake waliokuwa katika siti ya nyuma nao walishuka na kumfuata. Frenki alipoona amebaki peke yake ndani ya gari naye alishuka. Alikwenda mbele ya gari hilo kulikokuwa na wenzake waliokuwa wakilikorokocha gari hilo. “Lina tatizo gani?” Frenk akauliza. Mtu aliyekuwa karibu yake aligeuka ghafla na kumpiga kwa kitu kizito kichwani. Frenk alipiga yowe akaanguka hapo hapo akiwa amepotewa na fahamu. Mtu aliyempiga aliinama akamshika mikono na kumburuza kwenye kichaka kilichokuwa pembeni mwa njia. Alimuingiza ndani ya kichaka hicho akamlaza chini. Wenzake walimfuata. Yule aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ameshika begi ambalo aliliweka chini. Alitoa simu kutoka mfukoni mwake akaipiga. Baada ya muda kidogo simu yake ilipokelewa.

WAKATI mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) ukikamilika Septemba 4, 2026, huku mzunguko wa tatu ukianza jana Jumapili, timu tatu zimeonekana kuanza kinyonge baada ya kushindwa kupata pointi.
Okonkwo insisted that Nigerians had a legitimate right to scrutinise the educational background and eligibility of presidential candidates ahead of the 2027 election.
Gabriel Martinelli has completed his move from Arsenal to Saudi Pro League club Al Hilal in a £60 million deal, bringing an end to his seven-year spell with the Gunners.
Real Madrid defender Raul Asencio has been acquitted in a case involving the sharing of a sexually explicit video without the victims’ consent, after the women involved told a court in Gran Canaria that they had forgiven him.
The qualification race for the 2027 Africa Cup of Nations (AFCON) is officially underway, with 21 spots remaining to complete the final 24-nation lineup.
Real Madrid manager Jose Mourinho has paid tribute to Lionel Messi following the Argentina captain’s retirement from international football, describing the eight-time Ballon d’Or winner as a player the football world will miss.
“There used to be games that we used to have; as a laugh, we used to say, ‘Right, we’ll kick off now, right? See how long we can go without blowing a whistle’,” Dean said.

LIGI Kuu Bara msimu wa 2026/27 inaendelea kwa kasi na wiki hii timu nyingi zitakuwa zinacheza mechi zake za sita huku ushindani ukiendelea kuwa mkubwa kuanzia timu, wachezaji na hata makocha wakionyeshana ubabe wa mbinu uwanjani.

Soma zaidi hapa

Soma zaidi hapa

BAADA ya Simba kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kiungo raia wa Senegal, Alassane Maodo Kante, kwa sasa nyota huyo amejiunga na Klabu ya JS El Biar iliyopanda daraja msimu huu kushiriki Ligi Kuu ya Algeria.

KATI ya timu ambazo zinaumiza kichwa kuweka vizuri mikakati yao katika Ligi Kuu Bara ili kupata ushindi wa kwanza, TRA United inayofundishwa na Etienne Ndayiragije ni mojawapo na leo Ijumaa, ina kibarua nyumbani dhidi ya Mbeya City.

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), limefungua rasmi mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Tanzania Woodball Association (TWBA), huku wanachama wenye sifa wakipewa nafasi ya kuanza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema kikosi chake hakijaingia Ligi Kuu Bara msimu huu kwa ajili ya kushiriki tu, bali kina mpango wa kuendelea kusalia kwenye nafasi za juu na kuvuruga hesabu za vigogo Simba, Yanga na Azam katika mbio za ubingwa.
“But I'm happy now. I have a lot of quality in the team. Now it is the moment for me and the players to develop what we have."
The Blues have contacted former Liverpool midfielder Georginio Wijnaldum as they urgently assess options to strengthen Xabi Alonso’s midfield, according to French outlet Foot Mercato.

ARUSHA: MBEYA City’s Head Coach, Salumu Mayanga, says his side has improved technically and tactically after collecting nine points from their opening four matches of the Tanzania Mainland Premier League. Mbeya City have won three matches and lost one, collecting nine points to sit fifth in the NBC Premier League standings. Speaking during the team’s…

Mshambuliaji wa Yanga, Peter Shalulile, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Namibia, Brave Warriors, kitakachoshiriki mechi za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2027.

WAKATI Ligi ya Championship ikitarajia kuanza Septemba 11, 2026, Tanzania Prisons imesema ipo tayari kuianza upya safari ya matumaini ya kuisaka tena Ligi Kuu, huku ikichekelea ratiba ya kuanzia mechi mbili ugenini.

KIKOSI cha wachezaji 20 cha KVZ kimebeba matumaini ya Zanzibar katika kuanza vizuri safari ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kinapojiandaa kuikabili Al Swehly SC ya Libya katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali.

POLISI Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu, imetaja siri ya ushindi wao dhidi ya KVZ ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo.

MSHAMBULIAJI raia wa Kenya, Diana Cherono ameondoka Ceasiaa Queens ya Tanzania na kutua Kibera Soccer Women FC ya Kenya, huku suala la fedha likitajwa miongoni mwa sababu zilizochangia kutoendelea kusalia kikosini humo.