
VIWANJANI | Coastal Union yajipanga kuibonda Pamba Jiji, Geita Gold kurejea upya.
Azam TV
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.

Azam TV

ASSWEHLY SC imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 katika ardhi ya Zanzibar katika mchezo wa marudiano dhidi ya KVZ uliochezwa leo Septemba 13, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex kisiwani hapa. Ushindi huo umeifanya Asswehly kuiondosha KVZ kwa jumla ya mabao 4-0, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Libya wenyeji kushinda 1-0.

Sir Nature afunguka kuhusu muziki wa sasa, AI na maadili ya wasanii

Rweyemamu: Kadi nyekundu ya Libasse Gueye ilikua hivi


MTANZANIA Barka Seif Mpanda anayekipiga katika akademi ya FC Barcelona iitwayo La Masia, ameonekana kufanya vizuri kwenye mashindano ya Virgil Legacy Trophy baada ya kufunga mabao matatu na kutoa asisti moja katika michezo miwili ya mashindano hayo.

KOCHA wa Bunda Queens, Alley Ibrahim, amesema timu hiyo imejipanga kutumia wiki nane kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania kwa lengo la kurekebisha makosa ya msimu uliopita.

KIUNGO fundi wa Nigeria, Precious Christopher maarufu kama ameanza kwa kishindo maisha yake mapya kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Uturuki baada ya kuanza katika kikosi cha kwanza na kuisaidia timu yake mpya, Unyekatadin, kupata ushindi wa bao 1-0.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Kenya, Jentrix Shikangwa anayekipiga FC Masar, ameanza vizuri maisha yake mapya kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Misri baada ya kufunga mabao matano katika mchezo mmoja uliomalizika kwa ushindi wa mabao 21-0.

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, imedhamiria kufanya vizuri katika mashindano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana, AFCON U-20 Kanda ya CECAFA.

NAHODHA wa Gaborone United, Lebogang Ditsele, amesema kwa misimu miwili mfululizo, timu za Simba na Yanga zimekatisha matumaini yao ya kufika hatua za mbele zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, japo amezisifu kutokana na aina ya uwekezaji walioufanya.

KOCHA Mkuu wa Gaborone United ya Botswana, Sean Connor amesema kasi ya Yanga dakika 15 za mwanzo katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliwavurugia hesabu zao, jambo lililosababisha wachezaji kuanza kwa kusuasua.

DAR ES SALAAM: A SMALL word before we begin: Watani wa Jadi is used here in the old East African spirit of affectionate rivalry, teasing and neighbourly banter. In Tanzania, the phrase is often applied to Kenyans, not as an insult, but as a warm acknowledgement of a relationship built on history, proximity, shared culture,…

UTANGULIZI Aliendelea kujiambia kuwa atawaeleza polisi kuwa baada ya kuznguka nyumba na kutowaona watu hao alikuja kumkuta bosi wake ameshachinjwa na pia aliwaona watu watatu waliokuwa wameshika masanduku wakimalizia kutoka kwenye geti. Mlinzi huyo alijiambia kama polisi hao watamuuliza iwapo aliwafuatilia majambazi hao, atawambia kuwa aliwafuatilia lakini hakuwaona. SASA ENDELEA... Aliporidhika na maelezo aliyoyapanga ndipo alipotoa simu yake na kuwapigia polisi. Nusu saa tu baadaye gari la polisi likasimama nje ya nyumba ya James. Polisi sita waliokuwa na bunduki walishuka kwenye gari ambapo mlinzi huyo aliyekuwa akiwasubiri aliwakaribisha ndani. “Wewe ndiye mlinzi uliyetupigia simu?” Polisi mmoja aliyeonekana kuwa na cheo cha usajenti alimuuliza mlinzi huyo. “Ndiye mimi.” Mlinzi huyo akamjibu. “Hii ndiyo nyumba iliyoingiliwa na majambazi?” “Ndiyo hii.” “Wewe ulikuwa wapi wakati majambazi hao wanaingia?” Mlinzi huyo akaeleza kama alivyokuwa amepanga. “Hebu tuoneshe huo mwili wa marehemu aliyechinjwa.” Mlinzi huyo akawapeleka polisi hao mahali ulipokuwa mwili wa James. “Wamemchinja namna hii!” Polisi mmoja akamaka. “Wameiba nini na nini?” Polisi mwingine akauliza. “Waliiba masanduku.” “Masanduku ya nini?” “Sijajua ni masanduku ya nini lakini yalikuwa humu ndani” “Hebu twende ukatuoneshe humo ndani.” Mlinzi huyo akawaingiza polisi hao ndani ya nyumba hiyo. Waliingia hadi chumbani mwa James. “Huyu mtu hana mke?” Mmoja wa polisi hao akamuuliza mlinzi. “Hana mke.” “Humu ndani wanaishi watu wangapi?” “Alikuwa akiishi pake yake.” “Alikuwa akiishi peke yake jumba lote hili?” “Ndiyo, alikuwa akiishi peke yake.” “Hebu tutoke huku nje.” Wakatoka tena nje ya ile nyumba. “Umesema bosi wako aliamka na kukwambia uzunguke nyuma ya nyumba baada ya kusikia sauti za watu, ni upande upi? Hebu tuoneshe.” “Ni huku.” Mlinzi huyo aliwapeleka polisi hao upande wa nyuma wa ile nyumba. “Sasa wakati narudi tena ndio nikakuta wameshamchinja.” Mlinzi aliwambia. “Unajua maelezo yako hayaeleweki lakini utakwenda kutueleza vizuri kituo cha polisi. Ngoja kwanza tushughulikie huu mwili wa marehemu.” Polisi hao walipiga simu ambapo gari la hospitali lilifika na kuuchukua mwili wa James ambao ulipelekwa moja kwa moja hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi. Nyumba ya James ikafungwa na polisi ambapo mlinzi huyo alichukuliwa kituo cha polisi. “Sasa hebu tueleze vizuri nini kilitokea?” Mmoja wa polisi wa kituo hicho aliyekuwa na kalamu na karatasi alimuuliza mlinzi huyo aliyekuwa amekaribiswa kwenye kiti. Mlinzi alieleza kama alivyokuwa amepanga. “Hao walinzi hawakuvunja geti?” “Hawakuvunja.” “Waliingiaje mle ndani?” “Nafikiri waliruka ukuta.” “Wewe uliwasikia?” “Kusema kweli mimi sikuwasikia lakini marehemu aliwasikia, akatoka na kuniambia amesikia sauti za watu nyuma ya nyumba.” “Wewe ukafanya nini?” “Nikazunguka nyuma ya nyumba.” “Ukaona nini?” “Sikuona kitu.” “Sasa hawa majambazi walitokea wapi na walimchinja vipi bosi wako?’ “Sijui. Wakati mimi natokeza upande wapili wa nyumba nikamuona bosi wangu amelala chini akiwa tayari ameshachinjwa. Niliwaona pia watu watatu waliokuwa wamebeba masanduku wakitoka kwenye geti.” “Hao watu uliwafuatilia?” “Niliwafuatilia lakini nilipotoka kwenye geti sikuwaona.” “Hebu tueleze wakoje hao watu?” “Wawili walikuwa wamevaa mavazi meupe, mmoja mavazi meusi.” Mlinzi huyo akawaelezea watu hao kwa jinsi alivyowaona. Polisi huyo alipotajiwa yale mavazi waliyokuwa wameyavaa na kusikia maelezo kwamba shingo ya aliyekuwa amevaa mavazi meusi ilikuwa kama imechinjwa na kwamba kichwa cha mtu huyo kilikuwa kinaningi’inia, polisi huyo alishituka. Kumbukumbu za mauaji ya Martin zikaanza kumjia. Japokuwa mauaji ya Martin yalishughulikiwa katika kituo kingine cha polisi, taarifa zake zilisambaa katika vituo vyote vya polisi jijini Dar. “Mbona watu hao ni kama wale waliodaiwa kumuua Martin?” polisi huyo akajiuliza moyoni mwake kisha akamwambia yule mlinzi. “Kulikuwa na mauaji yaliyotokea huko Mikocheni hivi karibuni. Watu wanaodaiwa kufanya mauaji hayo ni kama hao uliowaona!” “Unazungumzia mauaji ya Martin” “Ndiyo Martin” “Huyu jamaa aliyeuawa leo ni mdogo wake baba mmoja, mama mmoja!” Yule polisi alishituka akawatazama polisi wenzake waliokuwa wamesimama kwa pembeni. “Si mnamkumbuka yule jamaa aliyeuawa Mikocheni juzi juzi tu?” Akawauliza. “Si yule jamaa aliyechinjwa na majambazi waliopora mkoba wake uliokuwa na pesa!” Polisi mmoja akamwambia. “Ndiye huyo huyo. Sasa huyu mlinzi anasema yule jamaa na huyu aliyeuwa leo ni ndugu. Na wauaji wanaonekana kama ni wale wale!” Suala hilo likazua taharuki zaidi. “Inabidi tuwafahamishe wakubwa wetu usiku huu.” Yule aliyekuwa akiandikisha maelezo ya mlinzi akawambia wenzake. Mkuu wa kituo alikuwa hayuko, akaitwa kwa radio coll. Alipofika kituoni hapo alielezwa kuhusu tukio hilo. Mkuu huyo wa kituo akaanza kumhoji yule mlinzi. Alipothibitisha kuwa wauaji wa James walikuwa ni wale wale waliomuu Martin na kwamba Martin na James walikuwa ndugu, akapiga simu makao makuu ya polisi. Katika muda wa saa moja, makachero watatu akiwemo Inspekta Amour walikuwa wameshaamshwa usingizini. Walifika makao ya polisi na kuchukua gari iliyowapeleka katika kituo hicho. Baada ya kupata maelezo kuhusu tukio lililotokea, Inspekta Amour alimhoji mlinzi huyo. “Kama wewe ndiye mlinzi wa nyumba ya marehemu, hao watu waliingia vipi na kuweza kumchinja marehemu na kuiba na kisha wakaweza kuondoka wakati wewe ukiwepo?” “Naona ilikuwa kama miujiza hivi….” Ilikuwa ndiyo sentensi aliyoanzia mlinzi huyo kabla ya kutoa maelezo ambayo alishayatoa kwa polisi alipohojiwa kwa mara ya kwanza. Inspekta Amour alikuwa amemkazia macho mlinzi huyo wakati akieleza. Hata baada ya kutoa maelezo yake ambayo yalizua maswali mengi, Amour aliendelea kumtazama lakini bila kumuuliza chochote. Yale macho ya Amour yalimfanya yule mlinzi aanze kujishuku mengi. Baada ya kimya cha sekunde kadha ndipo Amour alipomuuliza tena. “Hao watu watatu waliomchinja marehemu uliwaona vizuri?” “Niliwaona wakimalizia kutoka?” “Swali langu nimekuuliza uliwaona vizuri?” “Sikuwaona vizuri kwa sababu niliwaona wakimalizia kutoka kwenye geti.” “Walivaa mavazi gani?” “Wawili walivaa mavazi meupe, mmoja alivaa mavazi meusi?” “Umesema huyo aliyevaa mavazi meusi alikuwaje?” “Kichwa chake kilikuwa kinaning’inia na shingo yake ilikuwa imechinjwa.” Amour akanyamaza tena kwa muda kabla ya kumuuliza. “Walipotoka kwenye geti wewe ulifanya nini?” “Niliwafuta lakini nilipotoka tu nje ya geti sikuwaona tena.” “Umesema waliiba nini?” “Niliona wakitoka na masanduku.” “Masanduku mangapi?” “Masanduku matatu.” “Waliyachukua wapi?” “Nafikiri chumbani kwa marehemu.” “Hivi wakati wote huo, watu hao wakimchinja bosi wako wakaingia ndani na kuiba, wewe ulikuwa unazunguka nyumba tu?” “Ndiyo. Nilikuwa nyuma ya nyumba baada ya marehemu kuniambia nizunguke nyumba kwa kuwa alisikia sauti za watu.” “Kuizunguka nyumba ungeweza kutumia dakika tatu au nne, si nyumba ya kawaida tu au ina ukubwa gani?” “Ni nyumba ya kawaida tu.” “Sasa hizo dakika tatu au nne za kuizunguka nyumba ndizo zilizowawezesha watu hao kumchinja marehemu, kuingia ndani na kuiba…?” “Ndiyo maana nikasema lile tukio lilitokea kimiujiza ujiza tu. Hata sijui lilitokeaje?” “Hebu twende hapo nyumbani tukapaone.” “Sawa.” Dakika chache baadaye gari moja la makachero likiwa na makachero watatu kutoka makao ya polisi na gari jingine la polisi wa kituo hicho likiwa na polisi watatu akiwemo mkuu wa kituo hicho pamoja na mlinzi wa nyumbani kwa marehemu James, yalielekea katika eneo la tukio. Walipofika nyumbani kwa marehemu, mlinzi huyo aliwaonesha mahali alipochinjwa james. Pia aliwaingiza ndani na kuwaonesha chumba cha James. “Huyu kijana hakuwa na mke?” Amour akamuuliza mlinzi. “Hakuwa na mke lakini alikuwa na mchumba wake ambaye alikuwa akifika naye hapa nyumbani.” “Hakuna watu wengine wanaoishi humu ndani?” “Alikuwa anaishi peke yake.” Walipotoka mle chumbani, Amour alimwambia mlinzi awaoneshe alivyoizunguka nyumba hiyo wakati James alipomwambia alisikia sauti za watu. Mlinzi alionesha jinsi alivyoizunguka nyumba huku Inspekta Amour na wenzake wakimfuata kwa nyuma. Walipotokeza upande wa pili, Amour alimwambia mlinzi. “Hatukutumia hata dakika tatu wakati tumetembea kwa taratibu.” Mlinzi akanyamza kimya. “Sasa hebu tuambie kwa kadiri ulivyofikiria hao watu walijificha kwa wapi wakati marehemu akiwasikia wakiwa nyuma ya nyumba?” “Kwa kweli sijagundua hadi sasa.” “Unadhani nani atatueleza wakati wewe ndiye uliyekuwa pamoja na marehemu?”

UTANGULIZI “Umeshajitokeza kwa wazazi wake?” Mama Almasi akauliza. “Nimeanza kumleta huku kwetu kwanza atambulike kisha atanifikisha kwao.” “Basi ufanye hivyo haraka ili tuweze kuendelea na taratibu nyingine.” “Umenipa maelezo ya busara mama yangu. Kitu cha msinngi ninachokitaka kwenu mnieleze je mmemkubali mchumba wangu?” SASA ENDELEA... “Sijui baba yako lakini mimi nimemkubali.” “Baba unasemaje?” “Sipendi kusengenya katika hilo, umeniuliza mbele yake na nitakujibu mbele yake. Jibu langu ni kuwa kama nyinyi wenyewe mmekubaliana kuwa mke na mume, mimi siingilii hapo. Mimi ninachosema ni kuwa ninawaombea Mungu.” Nyuso za james na Grace zikachanua tabasamu wakati Almasi na mke wake waliangua kicheko cha furaha. Siku ya pili yake, James akafikishwa kwa wazazi wa Grace. Huko nako walipata baraka kutoka kwa wazazi wa Grace. Siku chache baadaye James akamvisha Grace pete ya uchumba. Taratibu zikaendelea kufanyika hadi ikafikia hatua ya ndoa. Zilikuwa zimebaki siku saba tu James akamilishe mpango wake wakuoana na Grace. Kulikuwa na kitu kingine kilitokea. Siku hiyo James alikuwa na Grace hadi saa tatu usiku alipomrudisha nyumbani kwao Oysterbay. Grace aliyekuwa amekaa katika siti ya mbele kando ya James alifungua mlango wa gari kisha akamtazama James. “Baby ninashuka.” “Shuka kwa amani baby wangu.” Grace alishuka kwenye gari kisha akazunguka upande wa dereva akaupleka uso wake kwenye uso wa Jamea kisha akambusu. “Mmwaaa…!” James naye akambusu. “Mmwaaa…!” “Bye bye…” “Bye…” Grace akageuka na kuelekea kwenye geti la nyumbani kwao. Akabisha kwenye geti huku akiita. “Eliza! Eliza….njoo unifungulie.” Sekunde chache baadaye geti lilifunguliwa. Grace akageuza uso na kumtazama James aliyekuwa akisubiri Grace afunguliwe geti. James akaliondoa gari. Aliendesha kwa taratibu huku akijisifu kimoyomoyo kumchagua Grace kuwa mwenza wake wa maisha. Alijiambia hakika hakufanya kosa kumchagua msichana huyo mrembo ambaye tangu alipoanza kusuhubiana naye alimgundua alikuwa msichana mwenye sifa zote ambazo mwanaume anazihitaji kwa mke wake. Si tu alikuwa na ushauri wa busara, alikuwa na hekima, mjanja na mwenye upeo wa kutosha wa kuyaelewa maisha. Aliiwazia harusi yake ambayo ingefanyika baada ya wiki moja. Akajiambia kutokana na maandalizi yake itakuwa harusi itakayofana sana. Walikuwa wametenga kiasi cha shilingi milioni tisini kwa ajili ya harusi hiyo ya kitajiri japokuwa mke wake alitoka katika familia ya kawaida. James alipofika nyumbani kwake aliliingiza gari kwenye geti akaliegesha kwenye banda na kushuka. Dakika chache baadaye alikuwa bafuni akioga. Alipomaliza alitoka bafuni. Aliona hakuwa na jingine lolote la kufanya zaidi ya kupanda kitandani na kulala kwani alihitajika kuamka asubuhi na mapema kwenda kazini kwa ajili ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa kampuni yao. Kilikuwa ni kipindi cha mwisho wa mwezi. Alipojitupa tu kitandani, usingizi ukampitia. Wakati akiwa usingizini alisikia kama kuna sauti za watu zilizomuita jina lake na kumuamsha. Akafumbua macho na kuwasha taa. Ndani ya nyumba ile alikuwa akikaa peke yake. Zaidi yake alikuwa ni mlinzi wa nyumba yake ambaye hukaa kwenye geti. Akajiuliza ni sauti za kina nani alizozisikia zikimuita. Aliuhisi moyo wake ukianza kupata hofu. Akashuka kitandani na kwenda kufungua kabati akaingiza mkono na kutoa bastola yake ambayo wakati wote ilikuwa na risasi ndani. Akafungua mlango wa chumbani na kutoka ukumbini. Akiwa ukumbini alisikia kama hatua za watu waliokuwa wakitembea nyuma ya nyumba yake. Alikwenda sebuleni akapenua pazia na kumchungulia mlinzi wake, akamuona amekaa barazani macho yake yakitazama kwenye geti. James akafungua mlango na kutoka uani. “Vipi umelala?” Akamuuliza mlinzi huyo aliyeshituka kumuona Jemes amefungua mlango. “Niko macho. Kuna shida gani?” “Nimesikia kama hatua za watu nyuma ya nyumba, hebu zunguka uangalie.” Mlinzi akainuka haraka. Aliishika sime yake vizuri kisha akapiga hatua kuelekea kwenye kona moja ya jumba hilo la kifahari. Wakati mlinzi anapotea katika kona hiyo ya nyumba, watu watatu wa ajabu wakatokea katika kona nyingine. Jinsi James alivyoshituka kuwaona watu hao, ile bastola aliyokuwa ameshika ilimponyoka ikaanguka chini. Mara moja aliwaona watu hao watatu wameshamfikia mahali alipokuwa amesimama. Miongoni mwa watu hao watatu, aliyekuwa amesimama katikati ya wenzake alikuwa amevaa mavazi meusi. Wenzake walivaa mavazi meupe. Yule wa katikati shingo yake ilikuwa imechinjwa. Na kichwa chake kilikuwa kikining’inia kama vile kilitaka kuanguka. Mtu huyo ndiye aliyemsemesha James. “Wewe ni mtoto wa Almasi?” “Ndiye mimi” James alimjibu huku akitetemeka. “Baba yako alikuweka kama dhamana lakini umeshindwa kutiimiza masharti ya dhamana yako!” “Dhamana gani, sijawekwa kama dhamana mahali popote!” “Una hakika?” “Kwani nyinyi ni akina nani?” “Muda umekwenda sana, huwezi kupata jibu kwa sasa.” Mtu huyo akatoa panga na kulishika vyema. James akakurupuka. Alikumbuka hata kaka yake aliyefariki dunia aliulizwa hivyo hivyo na watu waliomuua. Licha ya kukurupuka alijikuta akiishia mikononi mwa wale watu wawili waliovaa mavazi meupe. Yule mtu aliyetoa upanga akamchinja James kama kuku. James alikoroma kama mbuzi aliyekuwa anachinjwa. Sekunde chache tu baadaye mwili wake ulianguka chini. Mlinzi aliyekuwa akiizunguka ile nyumba alishazisikia zile sauti, akawa anarudi mbio ili kujua walikuwa ni kina nani waliokuwa wakizungumza na bosi wake. Alipofika aliwakuta watu hao wakimalizikia kutoka kwenye geti wakiwa wameshika masanduku huku mwili wa James uliochinjwa ukiwa chini. Mlinzi huyo alishituka hasa alipouona mwili wa bosi wake umelala chini ukiwa umechinjwa. Alichokiwaza ni kuwa watu aliowaona wakimalizia kutoka walikuwa majambazi ambao waliingia humo ndani wakamchinja bosi wake aliyekuwa ametoka hapo nje kisha wakaingia chumbani mwake na kuiba masanduku alioyaona wakitoka nayo. Lakini yale mavazi ya watu hao yalimsababishia mshangao mwingine. Hakuwahi kuona majambazi waliokuwa wamevaa mavazi ya aina ile. Kwa vile kwenye geti hilo taa ilikuwa inawaka alikiona kichwa cha mmojawao aliyekuwa amevaa mavazi meusi kikining’inia kutokana na kuchinjwa kwenye koo. Akiwa katika mastaajabu, mlinzi huyo alikwenda kuitazama maiti ya bosi wake ambayo ilikuwa bado ikivuja damu kisha akakimbilia kwenye geti ambalo sasa lilikuwa wazi baada ya watu hao kutoka. Alichungulia nje lakini hakuona mtu yeyote. Akajiuliza watu hao walitoweka vipi kwani tangu walipotoka katika geti hilo hazikupita hata sekunde kumi na tano. Kwa sekunde hizo alipaswa awaone watu hao wakiendelea kutokomea. Kama wangekuwa na gari, mlinzi alijiambia, angeusikia muungurumo wa gari hilo wakati linaondoka lakini hakusikia muungurumo wowote. Mlinzi huyo alisali kimoyo moyo akajifanyia ishara ya msalaba kwenye uso na mabega yake kabla ya kurudi tena mahali ulipolala mwili wa James. Alichutama na kuutazama kwa makini mwili huo. Kutokana na uchunguzi wa macho yake, mlinzi huyo aligundua kuwa James alikuwa amechinjwa. Akiwa bado amechutama mahali hapo mlinzi huyo alijiuliza, watu hao waliingia kwa wapi kwani wakati bosi wake anatoka na kumtaka aizunguke nyumba, geti lilikuwa limefungwa kwa ndani. Alipokuwa nyuma ya nyumba ndipo aliposikia sauti za watu, akarudi mbio na kuwakuta watu hao wakimalizia kutoka wakiwa wamebeba masanduku. Watu hao waliingiaje humo nadani? Akajiuliza. Akaendelea kujiuliza, wakati bosi wake anatoka na kumwambia amesikia sauti za watu, watu hao walikuwa wapi? Baada ya kukosa majibu,aliinuka akaingia ndani ya ile nyumba kufanya uchunguzi. Mlango wa chumba cha James ulikuwa umeachwa wazi. Mlinzi huyo alichungulia ndani ya chumba hicho kisha akatoa kichwa chake na kurudi ulipokuwa umelala mwili wa James. Sijui wameiba nini na nini? Akajisemea peke yake. Sasa nifanye nini? Akajiuliza. Akajiambia ni lazima apige simu polisi. Alikuwa ameshatia mkono mfukoni kuitoa simu yake, aliposita. Alijiuliza polisi hao watakapofika atawaeleza nini? Alijiambia ni muhimu apange maelezo yake kwa usahihi vinginevyo ni yeye atakayewekwa ndani kutokana na tukio hilo lililohusisha mauaji. Akaanza kupanga maelezo ya kuwambia poolisi. Alijiambia awambie polisi kuwa majambazi hao waliruka ukuta upande wa nyuma wa nyumba hiyo ambapo bosi wake aliwasikia. Baada ya bosi wake kuwasikia alitoka na kumuarifu kuwa alisikia sauti za watu nyuma ya nyumba. Mlinzi huyo aliendelea kupanga maelezo yake kwamba alizunguka nyuma ya nyumba lakini tayari majambazi hao walikuwa wameshajificha sehemu ambapo baada ya yeye kuzunguka nyumba, majambazi hao walijitokeza na kumchinja bosi wake kisha waliingia ndani na kuiba masanduku. Aliendelea kujiambia kuwa atawaeleza polisi kuwa baada ya kuznguka nyumba na kutowaona watu hao alikuja kumkuta bosi wake ameshachinjwa na pia aliwaona watu watatu waliokuwa wameshika masanduku wakimalizia kutoka kwenye geti. Mlinzi huyo alijiambia kama polisi hao watamuuliza iwapo aliwafuatilia majambazi hao, atawambia kuwa aliwafuatilia lakini hakuwaona.

MTANZANIA Adolf Mtasingwa ameendelea kupata nafasi kwenye kikosi cha Kaizer Chiefs baada ya kucheza dakika 23 akitokea benchi katika mechi ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Polokwane City.

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Fahmar Santos amerejea rasmi uwanjani baada ya kukaa nje kwa takribani msimu mzima akiuguza jeraha la goti, huku sasa akiwa na shauku ya kuanza upya safari yake ya soka akiwa na Ciutat Meridiana FC ya Hispania inayoshiriki Ligi daraja la nne maarufu Catalunya.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na nahodha wa Twiga Stars, Opah Clement ameendelea kuandika historia katika soka la wanawake baada ya kujiunga na Al Ula SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia, akitokea SD Eibar ya Hispania.

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Miguel Gmaondi ameita kikosi cha wachezaji 41 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili za kuwania kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Guinea Ikweta na Madagascar na ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Ghana, mwezi huu.

KOCHA wa Wembe, Said Mbarouk amesema pointi nne walizovuna katika mechi nne za Ligi Kuu ya Zanzibar walizocheza Unguja si matokeo mabaya, akisisitiza ni ishara ya mwanzo ya mkakati wao wa kushindana ugenini kuanza kuzaa matunda.

KOCHA MKUU wa JKU, AbdulSaleh Mohammed amesema timu hiyo imeanza kuwa bora baada ya kuifunga Wembe mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja na amefurahi kuvuna pointi tatu za mchezo huo.

Raskazone imesema licha ya ugeni wao kwenye Ligi Kuu Zanzibar, lakini bado wanaendelea kujiimarisha ili kupata matokeo mazuri dhidi ya KMKM.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema kukabidhiwa kwa Uwanja wa Malindi ni miongoni mwa juhudi za Serikali kuhakikisha vipaji vinaendelezwa.

Kylian Mbappe struck twice to help Real Madrid smash Rayo Vallecano 4-1 on Saturday to pull level with Barcelona at the top of La Liga.

Kylian Mbappe struck twice to help Real Madrid smash Rayo Vallecano 4-1 on Saturday to pull level with Barcelona at the top of La Liga.

Liverpool remain unbeaten under Andoni Iraola but there were boos at Anfield after Fulham picked up their first point under Alvaro Arbeloa.

Former Liverpool playmaker Philippe Coutinho has joined Santos, team-mate Neymar announced on Saturday, although his new club has yet to officially confirm the move.

COASTAL Union imepata ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara nyumbani msimu huu baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku mshambuliaji wake, Maabad Maulid Maabad akihusika moja kwa moja katika mabao yote mawili ya timu hiyo.

Andoni Iraola said it was obvious Liverpool suffered from fatigue in a 0-0 draw at home to Fulham on Saturday, but insisted his players have to adapt to a gruelling schedule.

Yanga imetumia vyema faida ya kucheza nyumbani, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Gaborone United ya Botswana, katika mechi ya marudiano ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika iliyochezwa leo Jumamosi, Septemba 12, 2026.

In five games against top-flight opposition since Xabi Alonso took charge, Chelsea have scored 16 times and conceded 12.

Governor Okpebhoko of Edo carried out a minor reshuffle in his cabinet as he redeployed three commissioners from their initial ministries



MSHAMBULIAJI wa Yanga, Cheikh Ibrahima Touré amesema hana presha licha ya kutofunga kwa ki-wango anachotarajia tangu alipowasili Tanzania, akisisitiza anaamini muda wake wa kufunga utafika na ataanza kuifungia timu yake mabao mengi.

KOCHA Juma Mgunda amesema kutotumia vizuri nafasi wanazotengeneza katika safu ya ushambuliaji, pamoja na kufanya makosa katika eneo la ulinzi, ni miongoni mwa sababu kubwa zinazowagharimu na kuwafanya kupoteza pointi katika mechi zao za Ligi Kuu Bara.

KOCHA wa Azam FC, Florent Ibenge ameomba timu yake icheze mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kipindi hiki cha kalenda ya FIFA, huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa kwenye mpango wa kuileta nchini Union Maniema ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

UHAMISHO wa mshambuliaji Clara Luvanga kutoka Al Nassr kwenda Washington Spirit ya Marekani umemfanya aweke rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi katika soka la wanawake duniani.

TANZANITE Queens imeondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia U-20 nchini Poland ikiwa na somo kubwa baada ya kukutana na uhalisia wa kiwango cha dunia.

KOCHA Mkuu wa KVZ, Hababuu Ali, amesema wamebadili mbinu kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asswehly ya Libya, wakitamba sasa watashambulia ili kusaka ushindi wa mabao 2-0.

Barcelona coach Hansi Flick warned his players Saturday that any drop in focus could bring them crashing back down to earth after a spectacular start to the season.

DAR ES SALAAM: YOUNG Africans will be looking to use home advantage into a decisive result when they face Botswana’s Gaborone United today at the Azam Complex in Dar es Salaam in a crucial CAF Champions League return-leg encounter. The two sides played to a 1-1 draw in the first leg in Botswana last Saturday,…

Two men involved in a violent burglary of Manchester City's Italy international goalkeeper Gianluigi Donnarumma and his pregnant girlfriend at their home in Paris were on Friday given prison sentences.

Abuja has deployed a team to Karshi and surrounding rural and urban communities to track contacts, administer preventive antibiotics

ABUJA — Former Minister of Aviation, Femi Fani-Kayode, has condemned the alleged killing of two Nigerians in South Africa, warning that continued discrimination and attacks against Nigerian nationals could have consequences. Fani-Kayode, in a post on his Facebook handle on Friday, said he was “mortified and deeply shocked” by the reported murder of Bishop Michael […]

By Vincent Ujumadu AWKA: The wife of the Anambra State Governor, Dr Nonye Soludo, has expressed deep concern over the alleged sexual abuse and exploitation of a child by her mother in Onitsha, describing the report as “deeply disturbing”. The Anambra State Police Command had on September 10, 2026, arrested 36-year-old Anulika Onyeanusia in connection […]

By Providence Ayanfeoluwa ABUJA: The National Democratic Congress, NDC, has said it is fully prepared for the 2027 general elections, dismissing reports that the opposition party lacks governorship candidates in 12 states. Senator Victor Umeh, representing Anambra Central Senatorial District, also said the party would deploy agents to every polling unit across the country to […]

President Vladimir Putin warned on Friday that any deployment of European troops to Ukraine would amount to "a war against Russia" and said Moscow did not "pose a threat".

Manchester United have banned 685 ticketing accounts and sanctioned or warned a further 464 supporters following a summer-long crackdown on ticket misuse and touting.

Real Madrid forward Kylian Mbappe has hit back at criticism of his defensive work, insisting that a goalscorer will never be a problem for his team.