
Category
Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.


MAMIA ya wananchi wameshiriki mazishi ya mwanachama na shabiki mkubwa wa Yanga SC, Haji Omari Ramadhan Mpili maarufu Mzee Mpili aliyefariki Septemba 27, 2026.

KANO — The Central Bank of Nigeria, CBN, has urged Nigerians, particularly traders, to handle the naira with care, pride and dignity to prolong the lifespan of banknotes and reduce the cost of replacing soiled and mutilated currency. The Director, Currency Operations and Branch Management, Dr Adedeji Adetona, gave the advice on Monday during a […]

Liverpool forward Cody Gakpo has withdrawn from the Netherlands squad due to injury and will return to his club for further assessment.

Real Madrid president Florentino Perez and FC Barcelona have been summoned to appear before a Madrid court on November 25 for a conciliation hearing ahead of possible criminal proceedings for defamation against Perez, sources close to the case said on Monday.

TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23, imejikuta kwenye kibarua kizito cha kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U23) mwaka 2027, baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 ugenini dhidi ya Kenya katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa leo Septemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

The Super Eagles of Nigeria will seek to make it two wins from two when they face Guinea-Bissau in their second 2027 Africa Cup of Nations, AFCON qualifying fixture at the Estádio Nacional 24 de Setembro, Bissau, on Tuesday.


KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Rais wake, Wallace Karia, imefanya mabadiliko mbalimbali ya uongozi, baada ya kumteua Evans Mgeusa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirikisho hilo kuanzia leo Septemba 28, 2026.

Roberto Mancini says questions about his contract during his time as Manchester City manager were the club's "issue, not mine", after they were reportedly found guilty of all but one of 115 Premier League charges for breaching financial regulations.

UONGOZI wa TRA United umeanza mazungumzo ya kupata huduma ya Mtaalamu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Wachezaji (Performance & Tactical Analyst) wa Yanga, Bartalomew Prosper, ikiwa ni mchakato wa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kikosini.

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo itashuka dimbani kuumana na Madagascar, katika mchezo wa Kundi L wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, utakaopigwa kwenye Uwanja wa d’Honneur, Meknes nchini Morocco.

KATIKA kuendelea kuboresha benchi la ufundi la Kagera Sugar, uongozi wa timu hiyo umefikia makubaliano ya kuwachukua viungo waliowahi kutamba Simba, Yanga, Azam na Taifa Stars, Amri Kiemba na Frank Domayo kuwa wasaidizi wa Cedric Kaze.


VISIWA vya marashi ya karafuu, Zanzibar, vitakuwa na bashasha kubwa kuelekea tamasha kubwa la ngumi la Boxing in Paradise linalotarajiwa kufanyika leo Septemba 29, 2026, kuanzia saa 12 jioni na pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki ni lile la bondia maarufu, Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ dhidi ya Michael William.

KATIKA hali isiyotarajiwa, Kocha Mkuu wa Chipukizi United, Suleiman Mohamed’ Gamera’ amezimia uwanjani ghafla baada ya mchezaji wa timu hiyo, Ali Mwadini kukosa bao la wazi.

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Yusufu Mhilu, amesema japokuwa Ligi Kuu Bara msimu huu ni ngumu na ushindani upo wa hali ya juu, lakini anatamani kumaliza akiwa kwenye tano bora ya wafungaji wa mabao mengi.

WALIOKUWA wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu 2026-2027, KMKM, hali yao ndani ya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) ni mbaya baada ya kukusanya pointi moja kwenye mechi nne ilizocheza.

UTANGULIZI “Mimi sikuwaona” “Itakuwa ni miujiza kwamba watu watatu wameingia hunu na kuua mtu bila kuonekana!” “Lakini Inspekta kitu gani kinakushangaza?’ Almasi akamuuliza Amour. “Ninashangaa kuona kwamba mnaye mlinzi anayelinda kwenye geti lenu na humu ndani kuna wafanyakazi lakini watu wasiotakiwa wameweza kuingia na kufanya mauaji!” SASA ENDELEA “Kwani hii ni mara ya kwanza kwa watoto wangu kuuawa? Hii si mara ya kwanza. Huu ni mfululizo wa mauaji ya kimiujiza ya muda mrefu. Mwanangu John aliingiliwa nyumbani kwake na kulikuwa na mlinzi!” “Sikiliza mzee Almasi sisi tunatathmini kila tukio linalotokea na kujiuliza lilifanyika katika mazingira yapi. Hatupendi kulinganisha matukio. Kama tunayalinganisha ni kwa sababu za kiuchunguzi tu” “Nimekuelewa Inspekta endelea na maswali yako” Inspekta alinyamza kwanza kutuliza taharuki. Alijua kuwa Almas alikuwa hayuko sawa na hivyo hakutaka kumchukulia. Alikumbuka kwamba aliwahi kuambiwa na Almasi kwamba mwanawe Benjamin aliajiri mlinzi ambaye atakuwa yuko naye wakati wote. “Nakumbuka kwamba uliwahi kuniambia kwamba uliajiri mlinzi kwa ajili ya usalama wa mwanao?” “Ndiyo. Lakini pia hakusaidia kitu” “Wakati tukio hili linatokea alikuwa wapi?” “Labda umuulize mwenyewe, yuko hapa” “Yuko wapi?” Mlinzi huyo aliyekuwa yupo hapo karibu akajitokeza. “Ni mimi” Inspekta Amour alimntazama kijana huyo kwa makini kabla ya kumuuliza. “Wewe ndiye uliyekuwa mlinzi wa Benjamin?” “Ndiye mimi” “Ulikuwa ukifahamu majukumu yako ni nini?” “Nilikuwa nafahamu” “Niambie majukumu yako yalikuwa ni nini?” “Kumlinda Benjamin” “Ulikuwa unamlinda Benjamin?” “Ndiyo” “Ulikuwa unamlinda dhidi ya kina nani?” “Nilikuwa namlinda dhidi ya mtu yeyote ambaye atakuwa na nia ya kumdhuru Benjamin” “Ulikuwa unaifanya kazi hiyo kwa weledi?” “Ndiyo “Na marehemu alikuamini kuwa unamlinda?” “Natumaini aliniamini” “Sasa leo Benjamin ameuawa, utatueleza nini?” “Aliuawa kwa bahati mbaya” “Unataka uniambie kuna mauaji ya bahati nzuri?” “Hakuna. Lakini Benjamin aliuawa kwa bahati mbaya” “Ni kwa sababu hukutimiza jukumu lako la kumlinda” “Benjamin alipouawa sikuwa naye karibu. Aliniambia anakwenda msalani. Nikamuacha aende msalani. Waliomuua walimuua akiwa msalani kama mwili wake ulivyokutwa” “Hukuona kuwa kumuacha peke yake ulikuwa unawapa mwanya wauaji?” “Hilo sikulitegemea kwa sababu tangu nianze kazi hii sijawahi kumfuata msalani hata siku moja. Hakuna aliyetarajia kuwa wauaji wangemfuata msalani” “Na wewe wakati wote ukiwa na Benjamin hukuwahi kunusanusa na kugundua kuwa wauaji walikuwa wanamfuatilia?’ “Sikuwa na taarifa kama hizo, nisingemuacha aende msalani peke yake” “Maana ya kukuajiri wewe ni kuwa alijiona alikuwa katika hatari. Wewe kama mlinzi wake ulipaswa kuwa na mwajiri wako wakati wote na mahali popote?” “Hata msalani pia?” “Wewe si umesema kama ungejua usingemuacha aende msalani peke yake? Sasa unashangaa nini?” Kijana huyo akanyamza kimya. “Unaonaje kama tutakukamata wewe kwa kusababisha Benjamin auawe?” “Mimi sikusababisha Benjamin auawe” “Wewe ndiye uliyechukua jukumu la kumlinda na umeshindwa kutimiza jukumu lako. Ameuawa hapakazini kwenu na wewe ukiwepo?” Amour alipomuona kijana huyo amenyamaza kimya, aliwageukia polisi aliokuwa amefuatana nao na kuwambia. “Mchukueni huyu kijana na mlinzi wa geti pamoja na yule mfanyakazi aliyeshuhudia Benjamin akiuawa ili waisaidie polisi katika uchunguzi” Vijana hao walikamatwa na kuingizwa kwenye gari lapolisi. Wakati wote amour alipokuwa akimhoji mlinzi wa marehemu Benjamin hadi kuwaamuru polisi wamchukue yeye, mlinzi wa geti pamoja na mfanyakazi wao aliyeshuhudia wakati Benjaminakiuawa, Almasi alikuwa akimtazama kwa jicho la dharau. Alikuwa akijiuliza ni kwanini kachero huyo afikirie kuwachukua vijana hao badala ya kuwajibika polisi wenyewe. “Inspekta nakukumbusha kwamba matukio ya mauaji hayakuanza leo. Yalinza tangu hao vijana mliowachukua siwajui” Almasi akamwambia Amour. “Kwanini unaniambia hivyo?” Amour akamuuliza. “Nakukumbusha tu Inspekta” Amour alitulia kidogo akayatafakari yale maneno kisha akamwambia Almasi. “Sawa. Nimekuelewa. Nitakuhitaji ofisini kwangu utakapopata nafasi kuja” “Nitafika” “Sisi tunaondoka” “Sawa Inspekta” Wakati Amour akiendesha gari kuelekea kituo kikuu cha polisi, alijiuliza ni kwanini Almasi alimwambia akumbuke kuwa mauaji ya wanawe hayakuanza leo? Ana maana kwamba hatuamini? Au ana maana kwamba vijana waliowachukua walikuwa wanawaonea? Amour akatikisa kicwa peke yake kusikitika alipowaza kwamba Almasi alikuwa amekiuka mipaka ya shutuma. Lakini tutamfanya nini wakati kuna ukweli kwamba ana uchungu wa kuuliwa watoto wake kwa mfululizo? Akajiambia. Anaweza kusema lolote analojisikia kulisema aukuwaza lolote linaloingiakichwani mwake. Lakini hatowaza hata siku moja kwamba huenda matatizo haya yanatokana na yeye mwenyewe. Amour aliwaza. “Kuna umuhimu sasa wa kuanza kumchunguza huyu mzee” akajiambia. Walipofika kituo kikuu cha polisi,vijana waliokamatwa wakatakiwa watoemaelezo yao. Alianza mfanyakazi aliyeshuhudia Benjamin akiuawa. Baada ya kuandikisha maelezo yake, Amour alimwambia. “Hebu rudia yale maneno. Yule mtu aliyemchinja Benjamin alimuuliza nini?” Alimuuliza Benjamin kama ni mtoto wa Almasi?” “Benjamin akamjibu nini?” “Alimjibu ‘Ndiyo” “Halafu huyo mtu alimwambia nini tena?” “Alimwambia baba yako alikuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana yako. Benjamin akamuuliza aliniweka dhamana wapi? Yule mtu akamwambia asingeweza kumueleza kitu kwa sababu muda wa Benjamin ulikuwa umeisha” “Ndipo alipotoa sime na kumchinja?” “Ndiyo” Amour akamgeukia kachero mwenzake ambaye walikuwa wakiandikisha yale maelezo pamoja. “Unaona, chanzo kinaweza kuwa ni kwa baba mtu. Huyu mtu alimuuliza wewe ni mtoto wa Almasi. Akamwambia baba yako alikuweka dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana. Si unaona chanzo kipo kwa baba mtu?” Amour alimwambia kachero mwenzake. “Inawezekana kabisa kwamba tatizo limetokana na baba mtu” “Huyu mzee anahitaji kuhojiwa na kuchunguzwa. Hapa kuna kitu, si bure. Haiwezekani watoto wake wauawe bure kila siku” “Kule Pakistan kuna mchezo mmoja. Unaweza kumuweka mtu dhamna ukapewa kokeni ukauze lakiniukishindwa kutimiza masharti ya dhamna, mtu wako anauawa!?” “Umetoa mfano sahihi sana. Unahisi kuna kitu kama hicho?” “Kinawezekana. Kwani yule mzee utajiri wake aliupata wapi?” “Ndiyo maana nikasema ni lazima tumhoji na kumchunguza, isije kuwa yeye ndiye anayewasababishia vifo watoto wake” “Hebu tuwe wazi. Unashuku kwamba anajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya?” “Majibu tutayapata baada ya uchunguzi wetu” “Sawa. Naona hivi sasa tuingie kazini kumchunguza yeye” “Nimemwambia aje ofiisini kwangu. Nitakualikaili tumhoji maswali” “Sawa afande. Akifika utanijulisha” Kijana aliyekuwa akitoa maelezo akaambiwa na Inspekta Amour kwamba atawekwa ndani. Kijana huyo akashituka. “Niwekwe ndani kwa kosa gani?’ akauliza kwa taharuki. “Ni kwa sababu kwa taratibu zetu wewe pia ni mtuhumiwa!” “Kwanini?’ “Kwa sababu wakati Benjamin anauawa ni nyinyi wawili mliokuwa msalani. Unadhani tutamkamata nani?’ “Lakini nimeshaeleza kwamba mimi sikuhusika” “Sasa acha tuendelee na uchunguzi wetu. Tukijiridhisha kuwa hukuhusika tutakuachia” Licha ya mfanyakazi huyo kuanza kulalamika, Amour alimuamuru polisi aliyekuwepo hapo amchukue na kwenda kumuweka ndani. Mtu wa pili aliyeitwa kutoa maelezo alikuwa mlinzi wa geti la kiwanda. Baada ya kutoa maelzo yake na kukana kuwaona watu waliomuua Benjamin wakiingia katika kiwanda hicho, Amour alimwambia na yeye atawekwa ndani. “Kwanini niwekwe ndani?” Mtu huyo akang’aka. “Tutajuaje kama wewe ulikula njama na hao wauaji?” Polisi mmoja akamwambia mlinzi huyo. “Mimi nile njama na wauaji?” Mlinzi huyo akang’aka tena. “Kama wewe ulikuwa mlinzi wa Benjamin, sasa kwanini Benjamin ameuawa?” “Ameuawa katika mazingira yanayofahamika lakini si kweli kwamba mimi nilikula njama na wauaji” “Jukumu lilikuwa mikononi mwako. Itabidi utupe maelezo ya kina ni kwanini Benjamin ameuawa” “Niwape maelezo gani tena?” “Huna budi kuisaidia polisi. Utakuwa mikononi mwetu hadi uchunguzi wetu utakapokamilika” “Lakini hii si haki jamani!” “Haki ni ipi?” Inspekta Amour akaingilia kati.

ZANZIBAR: ZANZIBAR residents have been urged to turn the expected influx of AFCON 2027 visitors into income opportunities through culture, arts and sports. The Minister for Information, Arts, Culture and Sports, Dr Riziki Pembe Juma, made the call on Saturday evening, saying the expected influx of visitors during AFCON 2027 presents an opportunity for residents…

DAR ES SALAAM: SIMBA striker Ismail Mgunda has set his sights on scoring at least 10 league goals this season, while relishing the fierce competition for places at the club. Mgunda said he is focused on making an impact in the league, with scoring goals his main personal target as he looks to establish himself…

Taifa Gas has awarded a motorcycle to a resident of Msalala District, Shinyanga Region, for promoting the use of clean cooking energy under its Energy Ambassador campaign.

The Super Eagles of Nigeria have arrived in Bissau ahead of Tuesday’s 2027 Africa Cup of Nations (AFCON) qualifier against Guinea-Bissau.

By Rosemary Iwunze The National Pension Commission, PenCom, said it is targeting a total capital commitment of N300 billion to deepen critical infrastructure investment across Nigeria, with actual asset deployments set to commence by the second quarter of 2027. Speaking to the media at the backdrop of the Pension Industry Leaders Council (PILC) meeting in […]

([email protected]; 07066451983 SMS) Nigeria has a complicated relationship with capitalism. For the most part, it is barely understood. In Nigeria, capitalism is often presented as something inherently bad. This draws from the residual legacy of Nigerian Marxism, and a religious ethos that sometimes viewspoverty as a moral trophy. The idea that “money is the root of all evil” remains one of the most popular sayings in our public culture, even […]

Harambee Stars ilitoka nyuma na kunyakua alama moja dhidi ya Eritrea, katika mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa jana Uwanja wa Nyayo, Nairobi, iliisha kwa sare ya 1-1. Wageni walitangulia kwa bao la dakika ya 36 kupitia kwa Girmai Netabay Kabaka, kabla ya mshambuliaji Ryan Ogam kusawazisha dakika ya 87. Stars itasafiri hadi Conakry, Guinea, kwa mechi dhidi ya wenyeji Oktoba 1 katika Uwanja wa Stade du 28 Septembre, kabla ya dirisha la kimataifa la mapumziko kufungwa. Ingawa Stars tayari imefuzu moja kwa moja kwa fainali za AFCON 2027 kama mwenyeji pamoja na Uganda na Tanzania, kocha Bennie McCarthy amesisitiza kuwa bado analenga kumaliza miongoni mwa timu mbili bora kundini. Stars, chini ya kocha McCarthy, iliingia kambini Jumanne lakini maandalizi yake yalitatizwa na mgomo wa wachezaji waliokuwa wakidai malipo ya posho. Wachezaji walifanya mazoezi yao ya kwanza Ijumaa tu Uwanja wa Nyayo, na kuingia uwandani moja kwa moja Jumamosi baada ya mgomo. Katika kipindi cha pili, wachezaji watatu wa Stars walianguka uwandani kwa wakati mmoja, ishara kuwa ukosefu wa mazoezi umeanza kuwaathiri. Kocha McCarthy alianza na Bryne Omondi langoni , akilindwa na Hannif Wesonga, nahodha Abud Omar na Frank Onyango. Kiungoni aliwaweka Duke Abuya, Timothy Ouma na Job Ochieng, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Ryan Ogam na Micah Obonyo. Kati ya wachezaji 11 walioanza, ni watatu pekee wanaocheza ligi ya Kenya ikilinganishwa na Eritrea ambao Wachezaji wake wanacheza soka ya kulipwa Ulaya. Wachezaji chipukizi Shariff Musa na Amos Wanjala walipewa nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza. Kwa upande wa Eritrea, ni mchezaji mmoja tu kati ya 11 walioanza ndiye anayecheza ligi ya nyumbani. Golini alianza kipa anayeishi Australia, Yonathan Abiel wa Green Gully SC, akilindwa na Jonas Idris Ibrahim anayecheza Norway katika klabu ya BK Fremad, Jemal Mahmoud wa Preston Lions, Australia na Victor Stefan wa Kongsvinger, Norway. Kiungoni nahodha Ablelom Teklezghi wa RSFC ya Eritrea aliongoza safu iliyojumuisha Tesfaldet Simon wa Al Masry ya Misri, Esrom Mussie wa SAIT Trojans ya Canada na Namrud Embaye wa Wurzburger Kickers ya Ujerumani. Katika safu ya ushambuliaji waliwamo Filmon Rezene wa SV Elversberg ya Ujerumani, Ali Suleiman wa Al Masry ya Misri na Esrom Mussie wa Degerfors ya Sweden. Eritrea, inayofunzwa na Mmisri Hesham Yakan na kushika nafasi ya 184 ikilinganishwa na Kenya iliyonafasi ya 104. Wanaofahamika kama Red Sea Camels wamekuwa na mechi chache za ushindani miaka ya hivi karibuni, hali inayowafanya kuwa wagumu kutathminiwa kwa kukosekana kwa video za kutosha kwa benchi la ufundi la Kenya. Mechi hii ilikuwa ya 10 kati ya mataifa hayo mawili, Kenya ikiwa na rekodi bora zaidi ya na sasa imepata ushindi Mara tano , sare mbili na kupoteza mechi tatu. Katika mechi nyingine ya Kundi D, Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana ilipata ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Guinea jana.

DODOMA: PRESIDENT Samia Suluhu Hassan has appointed Dr Juma Homera as the Minister for Energy replacing Deogratius Ndejembi who is now the Vice President. Before the today, September 27, 2026, appointment, Dr Homera previously headed the Ministry of Constitutional and Legal Affairs. President Samia also appointed the former Tanzania Railways Corporation (TRC) Director General, Masanja…

BEKI wa Harambee Starlets, Enez Mango, amejiunga na klabu ya Politehnica Timișoara Feminina ya Romania baada ya kuitumikia Farul Constanța ya Romania kwa miaka minne. Mango, ambaye ni beki wa kushoto, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Divisheni ya Pili ya Wanawake nchini Romania, ukiwa na kipengele cha kuongeza muda wake. Akizungumza kipekee na Taifa Spoti, Mango hakuficha furaha yake kujiunga na klabu hiyo, akisema atapata fursa ya kucheza tena pamoja na kiungo Laura Rus, ambaye anamtaja kuwa mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea katika soka ya Romania. “Nina furaha kubwa kwa sababu Laura Rus, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora katika historia ya soka la Romania, yupo hapo. Nilicheza naye Farul, lakini aliondoka mapema. Kucheza naye tena ni jambo la kufurahisha kwa sababu tulikuwa na maelewano mazuri sana uwanjani,” alisema Mango. Aliongeza: “Politehnica ni klabu kubwa, na pia ninapenda jiji hilo pamoja na mazingira na hali za timu.” Mango anatarajiwa kujiunga na wenzake pindi atakapopata visa ya kwenda Romania. Beki huyo mwenye uzoefu pia alikuwa akivutia vilabu vingine viwili vya Romania, Gloria na Timișoara, kabla ya kuamua kujiunga na Politehnica. Klabu hiyo yenye makao yake katika jiji la Timișoara, magharibi mwa Romania, ilianzishwa mwaka 1921 na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Timișoara. Kwa sasa inapigania kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo msimu ujao. Uhamisho huo unamfungulia Mango ukurasa mpya katika soka ya kulipwa barani Ulaya, baada ya kipindi chenye mafanikio akiwa na Farul Constanța, ambako pia ni nyumbani kwa mlinda lango wa Starlets, Lilian Awuor. Mango alijiunga na Farul mwaka 2022 akitokea Vihiga Queens, ambapo alikuwa nahodha na mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu hiyo. Akiwa Farul, alishinda mataji mawili ya ligi na kuhudumu kama nahodha. Pia alishiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa Wanawake (UEFA ), ambako alicheza pamoja na Awuor. Kabla ya kuhamia Romania, Mango alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Vihiga Queens, akiiongoza kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF-WPL). Pia aliiongoza Vihiga Queens kutwaa ubingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa ya Wanawake ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) mwaka 2021. Ushindi huo uliiwezesha timu hiyo kufuzu kwa mara ya kwanza kwa Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake. Mango, 33, amekuwa mchezaji wa Starlets tangu mwaka 2015, akishiriki katika mechi mbalimbali za kimataifa, zikiwemo kuwakilisha Kenya katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON). Alikuwa sehemu ya kikosi cha Kenya kilichoshiriki fainali za WAFCON nchini Morocco mwaka huu, ambapo Starlets ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji Morocco, Algeria na Senegal lakini Kenya ikabanduliwa mapema baada ya kupoteza mechi zote za hatua ya makundi. Uzoefu wake wa soka ya ndani na kimataifa unatarajiwa kuwa muhimu anapoanza safari mpya na Politehnica Timișoara, huku akilenga kusaidia klabu hiyo kupanda daraja na kufikia malengo yake ya kushiriki michuano ya UEFA.

TIMU ya taifa ya soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, Emerging Stars, leo itaanza kampeni yake ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana (U23 AFCON) 2027 itakapokutana na Tanzania leo, katika mechi ya raundi ya kwanza katika uwanja wa Kitaifa wa Nyayo jijini Nairobi kuanzia saa tisa mchana. Tiketi za mechi zilikuwa zikiuzwa kwa Sh 200 kwa watu kawaida na Sh 500 kwa watu mashuhuri. Kocha wa Kenya Antony Kimani, Jumapili alitangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 27 kwa ajili ya mechi hiyo, huku timu hiyo ikilenga kuanza kampeni kwa matokeo mazuri dhidi ya watani wake wa Afrika Mashariki. Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kenya na Tanzania kukutana katika kiwango hiki, huku timu hizo zikitafuta tiketi ya kushiriki fainali za U23 AFCON zitakazofanyika Misri mwakani. Kenya bado haijawahi kufuzu kwa fainali za mashindano hayo, huku Tanzania pia ikiwa haijawahi kufikia hatua hiyo. Kenya iliingia uwanjani mara ya mwisho mwaka 2021 wakati wa michuano ya CECAFA, ambapo ilipoteza 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mechi ya mchujo. Tangu ianze kushiriki katika kiwango cha U23 mwaka huo, Kenya imecheza mechi saba katika mashindano mbalimbali, ikishinda mbili, kutoka sare mbili na kupoteza tatu. Tanzania, kwa upande wake, mara ya mwisho ilishiriki mechi za kufuzu U23 AFCON mwaka 2022, ilipoondolewa na Nigeria 3-1 kwa jumla ya mabao. Kwa jumla, Tanzania imecheza mechi nane tangu ilipoanza kushiriki katika kiwango hiki mwaka 2021, ikishinda tatu, kutoka sare nne na kupoteza moja. Kabla ya mechi hiyo, Kenya imekumbwa na pigo baada ya mshambuliaji Humphrey Aroko kuachwa nje ya kikosi kutokana na jeraha alilopata akiwa katika majukumu ya klabu yake, Rosengård ya Uswidi. Kiungo Aldrine Kibet anayeipigia RC Celta ya Uhispania naye hakusafiri kwa ajili ya mechi hiyo kutokana na suala la kibali chake cha kazi, ambacho muda wake wa matumizi unakaribia kumalizika na kwa sasa anashughulikia. Mshindi wa jumla kati ya Kenya na Tanzania atakutana na Ivory Coast katika raundi ya pili ya mchujo. Raundi ya kwanza inashirikisha timu 28 katika mikondo 14 ya mechi mbili, huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 20 na marudiano Oktoba 6, 2026. Mechi za raundi ya pili zimepangwa kuchezwa Novemba 9 na 17, kabla ya raundi ya tatu na ya mwisho kufanyika Machi 2027. Mshindi wa jumla katika kila mchujo saba ya raundi ya tatu atafuzu kwa fainali za U23 AFCON nchini Misri pamoja na wenyeji ambao wamepata tiketi moja kwa moja. Mashindano hayo yana umuhimu wa ziada kwa sababu yatatumika kama njia ya Afrika kupata wawakilishi katika Mashindano ya Soka ya Olimpiki ya Los Angeles 2028. Timu za Afrika zina historia nzuri katika soka ya wanaume la Olimpiki. Nigeria ilitwaa dhahabu Atlanta mwaka 1996 na kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda medali hiyo, kabla ya Cameroon kutwaa dhahabu Sydney mwaka 2000. Nigeria pia ilishinda fedha Beijing 2008 na shaba Rio 2016, na kuwa taifa la Afrika lililopata mafanikio mengi zaidi katika mashindano hayo. Ghana iliweka historia Barcelona mwaka 1992 kwa kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda medali katika soka la wanaume la Olimpiki baada ya kutwaa shaba. Kikosi cha Mwisho Walinda lango Caleb Kramer (Ado Den Haag, Uholanzi) Mateo Ochieng (Providence College, Uingereza) Collins Omondi (Kariobangi Sharks) Mabeki Ian Onyango (Mathare United) Collins Ochieng (Tusker FC) Francis Okoth (Kenya Police) Baron Ochieng (Unattached) Wycliffe Omondi (Tusker FC) Joseph Bate (Nairobi United) Price Omenda (Murang'a Seal) Viungo wa Kati Omar Ateek (Mathare United) Kevin Wangaya (Nairobi United) Kelly Madada (Afc Leopards) Oliver Machaka (Kenya Police) Andreas Odhiambo (Enkopings SK, Uswidi) Jack Onganya (Cadiz, Uhispania) Irad Mshindi (Leipja, Latvia) Washambuliaji Dancan Oluoch (Nairobi United) Lawrence Okoth (Bandari FC) Syphas Owuor (Nairobi United) Collins Okello Jeremy Bisau (Sd Huesca, Uhispania) Telena Ochieng (Tusker FC) Brooklyn Kazungu (MK Dons, Uingereza) Paul Osama (Enkopings SK, Uswidi) Henry Omollo (Mufurila Wanderers, Zambia) Hassan Beja (Red Castleue SC, UAE)

Manchester United captain Bruno Fernandes has been ruled out of Portugal’s Nations League clash against Norway on Sunday after suffering a fitness issue in the team’s 1-0 win over Wales.

…As experts lament cultural, religious barriers By Jeff Agbodo, Abakaliki Residents of Ebonyi State have been urged to take advantage of free family planning services to reduce maternal mortality, unintended pregnancies and unsafe abortions in the state. The call was made as the state joined the rest of the world to commemorate the 2026 World […]

By Ibrahim Hassan-Wuyo Chairman of the Northern Christian Association, NCA, Rev. Joseph John Hayab, has urged Christians across the country to participate in the ongoing Initial Public Offering, IPO, of Dangote Petroleum Refinery, saying religious considerations should not influence investment decisions. Hayab made the call on Saturday at a media parley in Kaduna, where he […]

Liverpool forward Alexander Isak has suffered another injury setback after withdrawing from Sweden's squad due to a minor thigh problem.




UTANGULIZI “Akamfanya nini mwanangu?” “Sisi tulimkuta tayari ni marehemu…” “Una mmaana hao watu wamemuua?” “Nasikitika kukueleza kwamba ndiyo hivyo” “Wewe ulikuwa wapi?” “Yeye Ben aliniambia kuwa anakwenda msalani. Hao watu aliwakuta huko huko. Mimi sikuwaona” Mke wa Almasi akaanza kupiga kelele kwenye simu hali iliyomfanya mlinzi huyo kukata mawasilino. SASA ENDELEA Akarudi chooni na kumkuta Almasi anapiga simu polisi. Alipiga moja kwa moja kwa Inspekata Amour. “Amour sasa hutakuwa tena na kazi ya kuwatafuta wale wauaji” akamwambia. “Kwanini unasema hivyo. Sisi tutaendelea kuwatafuta usiku na mchana. Hatutawaachia” Amour akamjibu kwenye simu bila kumuelewa. “Kwanini mpaka hivi leo hamjawakamata?’ “Hao watu ni wauaji wazoevu. Lakini serikali ina mkono mrefu. Pengine tumechelewa tu kuwakamata lakini ni lazima tutawakamata watake wasitake” “Kazi imekwisha. Mwanangu Benjamn niliyekuwa nikimpigania asiuawe, ameshauawa sasa hivi” “Unasemaje?” “Nakwambia kwamba mwanangu Benjamin naye ameshachinjwa sasa hivi. Hivi sasa sina mtoto tena. Huhitajiki tena kuwatafuta hao watu” “Unasema kweli mzee?” “Sasa mimi na wewe tunataniana? Ninakwambia ukweli mwanangu amelala hapa mbele yangu. Tena amechinjwa chooni kama kuku masikini!” “Ilikuwaje?” “Mimi siwezi kukueleza ilivyokuwa, ngoja nimpe simu aliyekuwa mlinzi wake akueleze…” Almasi akampa simu mlinzi huyo. “Hebu mueleze Inspekta kilichotokea” Almasi akamwambia mlinzi huyo ambaye alipokea simu. “Ndiyo Inspeta. Hapa unaongea na aliyekuwa mlinzi wa Benjamin. Huyu mtu ameuawa sasa hivi kwa kuchinjwa” “Nataka unieleze ilikuwaje?’ Mlinzi huyo akamueleza mwanzo mpaka mwisho. Inspekata Amour aliguna. “Mmepiga simu katika kituo chochote cha polisi?” “Ngoja nimpe mzee akujibu” Almasi akarudishiwa simu. “Unasemaje?’ Almasi akamuuliza Inspekta huyo kwa sauti ambayo haikuwa tulivu. “Umewaarifu polisi wa kituo chochote au bado” Amour akamuuliza. “Kwani nikikupigia wewe si ndio nimewaarifu polisi?” “Kabla hujanipigia mimi, hujapiga simu kwenye kituo chochote?’ “Bado sijapiga. Hata ningepiga wangefanya nini wakati mtoto ameshauawa. Nimekupigia wewe ili kukuarifu tu…” Amour aligundua kuwa Almasi alikuwa amechanganyikiwa kutokana na hamaki ya mauaji ya mwanawe. Akamwambia. “Tunakuja sasa hivi” Almasi akakata simu. Alipokata simu ikaingia simu iliyotoka kwa mke wake. Akaipokea. “Sasa mume wangu kama Benjamin ameuawa, hali hii unaitafsiri vipi?” Sauti ya mke wake ikauliza. “Mimi sina tafsiri labda polisi wakija watatupa tafsiri” “Kwani polisi hawajafika bado?” “Ndiyo nimewaarifu sasa hivi, wameniambia wanakuja” “Na mimi ninakuja huko huko” “Hapana, wewe usije. Hutaweza kumtazama mtoto wako. Tafadhali usije” “Nisije kwanini mume wangu wakati mtoto wangu ameuawa?’ Mke wake akaanza tena kulia. Almasi akakata simu. Wafanyakazi walikuwa wamerudi tena chooni baada ya kutofanikiwa kuwaona watu watatu waliokuwa wakiwatafuta. “Polisi wanakuja. Yule kijana aliyewaona wale watu atahitajikakutoa maelezo” Almasi akawambia wafanyakazi hao. “Mimi nipo hapa” Sauti ya mfanyakazi huyo ikasikika kutoka katika kundi la wafanyakazi. Baada ya muda wa saa moja hivi Inspekta Amour akiwa na kundi la makachero aliwasili kiwandani hapo kwa kutumia magari mawili. Waliingizwa katika eneo alilouawa Benjamin na kuushuhudia mwili wake uliolala ukiwa macho wazi. Amour baada ya kuutazama mwili huo alitikisa kichwa kusikitika. Kilichomsikitisha ni kuona watu wa familia ya Alamsi walikuwa wakiendelea kuuawa licha ya kuwepo na juhudi za kuzuia mauaji hayo. Alikereka kuona kikundi cha watu wasiofahamika walikuwa wanataka kuizidi serikali. Wakati wote tangu makachero hao walipoingia katika eneno hilo, Almasi alikuwa akimtazama Amour kwa jicho la lawama kama vile yeye ndiye aliyetaka mauaji hayo yatokee. Baada ya kuukagua mwili wa Benjamin Amour aliinuka nakumshika bega Almasi. “Kuwa mvumilivu mzee wangu, usifadhaike” alimwambia kisha akawaagiza wale makachero wengine waubebe mwili wa Benjamin na kuupakia kwenye gari. Wakati mwili huo unapelekwa kwenye gari, Amour alimwambia Almasi kwamba wangetaka kupata maelezo jinsi Benjamin alivyouawa. “Kuna kijana ambaye aliona kila kitu” Almasi akamwambia na kulitupia macho lile kundi la wafanyakazi waliokuwa wamesongana mahali hapo kuona kilichokuwa kinaendelea. Yule kijana ajitokeze hapa” akawambia. Mfanyakazi aliyewaona watu waliomuua Benjamin akajitokeza mbele. Almasi akwambia Amour. “Huyo kijana aliona kila kitu” “Hebu tueleze nini kilitokea?” Amour akamuuliza. Mfanyakazi huyo akaeleza alichokiona alipoingia msalani kabla ya Benjamin kuuawa. Alieleza kuwa aliwaona watu watatu, wawili walivaa mavazi meupe na mmoja alivaa mavazi meusi. “Yule aliyevaa mavazi meusi alimuuliza Benjamin…” :Kwanza kabla ya kuendelea nataka unieleze hao watu watatu walitokea wapi?” “Niliwakuta humu humu chooni, sikuweza kujua waliingiaje” “Kuna uwezekano wa watu kuingia katika eneo lenu bila kuonekana?” “Kusema kweli haiwezekani. Pale kwenye geti la kuingilia kuna mlinzi, naye anasema hakuwaona. Na huwezi kufika katika eneo hili la choo bila kuonekana na wafanyakazi wa humu ndani” “Sasa mnadhani hao watu waliingia kwa wapi?” “Haijafahammika hadi sasa” “Enhe…hebu endelea kueleza” “Yule aliyekuwa amevaa mavazi meusi alimuuliza marehemu ‘Wewe ni mtoto wa Almasi?’ Benjamin akamjibu ‘Ndiyo’ Akamwambia baba yako alikuweka dhamana lakini umeshindwakutimiza masharti ya dhamana yako” “Alimwambia alimuweka dhamana mahali gani?” Amour akamuuliza. “Benjamin aliuliza hilo swali akajibiwa na yule mtu kwamba muda wake wa kuishi ulikuwa umekwisha ndipo alipotoa panga na kumkata shingo” “Muda wote huo wewe ulikuwa wapi?” “Nilikuwa nimesimama kando ya mlango” “Hao watu watatu hawakukuona?” “Walikuwa wameshughulika na marehemu” “Mpaka hapo wanamkata panga ulikuwa umesimama unawaona?” “Ndiyo” “Kwanini hukupiga kelele kuita wafanyakazi wenzako ili wawakamate wale watu?’ “Kusema kweli kwanza sikujua kama wangemkata panga. Nilipoona lile panga linatolewa ndipo nilipozinduka na kupiga kelele” “Baada ya kupiga kelele nini kilitokea?” “Yaani wakati napiga kelele ndio nilitoka mbio kwenda kuita watu” “Lakini wakati huo walikuwa wameshamkata?” Mfanyakazi huyo akanyamza kimya kwa kuona huenda alikuwa amefanya kosa kusubiri hadi Benjamin alipouawa. Amour alipoona mfanyakazi hiyo amenyamaza alimuuliza. “Unashindwa kujibu kwa sababu umegundua kosa lako, si ndiyo?” “Muda ule nilipigwa na butwaa kwa sababu hata yule mtu aliyetoa panga hakuwa wa kawaida” “Alikuwaje?” “Kichwa chake kilikuwa kinaning’inia kama vile shingo yake ilikuwa imechinjwa” “Hivyo ndivyo alivyokuwa?’ “Ndiyo” “Na wale watu wengine walikuwaje?” “Wale wengine walikuwa watu wa kawaida tu isipokuwa walikuwa weupe sana” “Kwa hiyo baada ya wewe kutoka, kupiga kelele na kuita watu, nini kilitokea?” “Tulikuja humu chooni tukakuta Benjamin ameshachinjwa” “Na wale watu waliishia wapi?” “Hatukuwaona. Tuliwatafuta kila mahali. Wafanyakazi walikuwa na hasira walitaka kuwapiga lakini hatukuwaona tena” “Walitoka kwa wapi?” “Haijulikani” Amour akamtazama Almasi. “Mzee umesikia huyu mfanyakazi wako anaeleza kuwa huyo mtu aliyekuwa amevaa mavazi meusi alimsikia akimwambia marehemu kwamba wewe ulimuweka dhamana. Je ulimuweka dhamna wapi?” Almasi alibetua mabega yake “Ni maneno ya kiwendawazimu! Nimemuweka dhamana wapi! Mimi sijui!” “Nafikiri kuna kitu amekusudia. Sidhani kama alimwambia hivyo bure tu” “Kama kitu gani Inspekta?” “Mimi siwezi kujua ndio sababu ninahoji” “Mimi pia siwezi kujua” “Lakini ni kitu cha ajabu sana kwamba wauaji wameingia katika eneno lenu bila kuonekana. Ninataka kumuona mlinzi anayekaa kwenye geti” Mlinzi aliitwa. Akaja mbele ya inspekta Amour. “Wewe ndio unalinda geti?” “Ndio” “Kuna watu wasiotakiwa wameingia humu na kuua mtu na wewe ndiye mlinzi, utatueleza nini?” “Mimi sikuwaona hao watu” “Kuna mlango mwingine wa kuingilia?” “Mlango ni huu mmoja” “Sasa hao watu waliingilia kwa wapi kama si kwenye mlango huo?” “Mimi sikuwaona” “Itakuwa ni miujiza kwamba watu watatu wameingia hunu na kuua mtu bila kuonekana!” “Lakini Inspekta kitu gani kinakushangaza?’ Almasi akamuuliza Amour. “Ninashangaa kuona kwamba mnaye mlinzi anayelinda kwenye geti lenu na humu ndani kuna wafanyakazi lakini watu wasiotakiwa wameweza kuingia na kufanya mauaji!”

ZANZIBAR: KAMPUNI ya Vodacom imeendelea kutumia mchezo wa gofu kuunganisha viongozi wa biashara, maafisa watendaji wakuu (CEO), wanadiplomasia na wadau wa sekta mbalimbali kupitia udhamini na ushiriki wake katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026. Mashindano hayo yalifanyika Septemba 26, 2026, katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course, Zanzibar, yakishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka…

WINGA wa Yanga, Celestin Ecua amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Al-Shoulla FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Saudi Arabia, baada ya kushindwa kuwika na JS Kabylie ya Algeria aliyoitumikia kwa mkopo tangu, Januari 28, 2026.

KIUNGO wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Bashiri Kibaila amesema anajifunza vitu vingi kutoka kwa kiungo wa Simba, Clatous Chama kutokana na ubora na uzoefu alionao kwenye soka la Tanzania.

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars raia wa DR Congo, Malanga Horso Mwaku amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Homs Al-Fidaa SC ya Syria, kwa mkopo wa msimu mzima, baada ya dili lake la kujiunga na Pamba Jiji ya Mwanza kugonga mwamba.

UONGOZI wa Geita Gold umesema sababu kubwa ya kipa mpya wa timu hiyo raia wa Nigeria, Kayode Bankole Iyanu kukosekana katika mechi za Ligi Kuu Bara tangu msimu wa 2026-2027 umeanza ni kutokana na kuchelewa kibali cha kazi.

BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Ligi Kuu ya Wanawake inarejea ikianza kupigwa mechi mbili za Ngao ya jamii itakayozikutanisha timu nne zilizomaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

GIZANI! Ndivyo unavyoweza kueleza hali halisi ndani ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) baada ya klabu zinavyoshiriki ligi hiyo kufikia hatua ya kuomba kusitisha kushiriki kutokana na ukata na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kila msimu, huku vikilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukaa navyo mezani kusaka suluhu.

ALIYEWAHI kuwa Kocha Mkuu wa Ceasiaa Queens msimu uliopita, Sultan Juma amerejea rasmi ndani ya kikosi cha Alliance Girls baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wa kuifundisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake.

The opening round of the 2027 Africa Cup of Nations, AFCON qualifying campaign produced a number of standout attacking performances, with two players emerging as the early leaders in the race for the tournament's qualifying scoring charts.

The Super Eagles will face Guinea-Bissau in their second Group L fixture of the 2027 Africa Cup of Nations, AFCON qualifiers on Tuesday, with the encounter carrying significant importance for Nigeria’s hopes of reaching the tournament.

Mwanariadha nyota wa Tanzania wa Marathon, Gabriel Geay amevuna kiasi cha Sh30 milioni kwa kumaliza katika nafasinya tatu kwenye mbio za Berlin Marathon zilizofanyika leo Jumapili, Septemba 27, 2026 huko Ujerumani.

KIUNGO mshambuliaji wa Enppi SC inayoshiriki Ligi Kuu Misri, Arafat Ally amesema tofauti kubwa aliyogundua kati ya soka la Misri na Tanzania ni namna walivyowekeza na kuweka mfumo mzuri wa kuendeleza vipaji vya vijana.

BEKI wa kushoto wa timu ya vijana ya Polissya Zhytomyr U19 ya Ukraine, Ismail Ally Omar amesema kitendo cha kucheza soka la kulipwa nchini humo kimemsaidia kukua na kukomaa kiakili kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi hiyo ya Ulaya.