
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


Ukandu said that the training was crucial to preparing young commanders for the increasingly complex security challenges confronting the country.

By Ochuko Akuopha ASABA — The Ndoshimili Development Union (NDU), the apex socio-cultural body of Ndokwa East Local Government Area of Delta State, has raised the alarm over aggressive shoreline erosion threatening communities in the area. The union warned that Abala-Oshimili and Onyah, which it identified as the worst-hit communities, could be wiped out within […]

KADRI uchaguzi mkuu unavyojongea ndivyo tabia ya kufadhaisha isiyoruhusu mtazamo na msimamo tofauti inavyozidi kujitokeza. Katika taifa linalojivunia demokrasia na utawala wa kikatiba, ungetarajia sote tunafahamu kila mwananchi, awe raia wa kawaida au kiongozi, amehakikishiwa kufurahia haki na uhuru kikatiba mradi hatoingilia uhuru na haki za mwananchi mwenzake. Ni kinaya kuwaona watu mashuhuri walio mstari wa mbele ‘kutetea haki’ wakijihusisha na vitendo vya kusakama na kuwakandamiza raia wenzao. Kuwaona wanasiasa wanaosimulia mara kwa mara masaibu waliyopitia watangulizi wao, wengine hata ikiwagharimu uhai wao, wakipigania demokrasia na mfumo wa vyama vingi, hii leo wakijaribu kuwanyamazisha wenzao kutoka kambi tofauti za kisiasa na wenye misimamo kinzani. Tafran zilizozuka Homa Bay wikendi ambapo polisi na raia waliripotiwa kuuawa na kujeruhiwa ni mfano hai kuhusu tabia hii ya kijadi. Kundi la viongozi lilipania kutoruhusu upinzani almaarufu Linda Mwananchi kufika eneo hilo wakisahau japo Homa Bay inachukuliwa kuwa ngome ya serikali pana, kuna Wakenya wanaounga mkono upinzani katika eneo lilo hilo sawia na ngome ‘za upinzani’ zinazosheheni wafuasi sugu wa serikali. Isitoshe, demokrasia kikatiba inamhakikishia kila mwanasiasa na vyama vyote vya kisiasa haki ya kuendesha kampeni kwa njia ya amani na kuuza sera zao kwa raia kote nchini mradi tu uhuru huo unazingatia kanuni za sheria kuhusu kampeni. Hali kwamba zaidi ya miaka 60 tangu Kenya ilipoanza kujitawala kidemokrasia bado kuna watu walioshikilia mawazo ya kijadi hususan kutumia vyombo vya dola kuzima maoni kinzani inashangaza mno. Karamu ya kufana kuhusu harusi ya kitamaduni ya bintiye rais ni mfano mwingine. Mkenya ambaye ni mwanahabari mashuhuri wa kimataifa alijipata mashakani vilevile, kosa lake pekee likiwa kuitikia mwaliko wa karamu ya kumwoza bintiye rais, huku watu wanaojitaja kuwa watetezi sugu wa haki za kibinadamu wakimkashifu vikali na kuwashawishi wafuasi wake mitandaoni kumtema. Tukio hilo lililovutia hisia mseto pia lilifichua uhalisia wa kuhofisha kuhusu Wakenya wasiofanya maamuzi kibinafsi na badala yake wanafuata upepo wakipinga vikali au kuunga mkono upande au mwanasiasa fulani bila sababu thabiti. Uhalisia ni kuwa, katiba ileile inayokupa uhuru wa kufahamishwa na kujieleza ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii, ndiyo ileile inayomhakikishia mwingine kutangamana na kujihusisha na kiongozi au kambi yeyote kisiasa. Wangari ni mwanahabari wa ‘Taifa Leo’

…faults KAGOTE allegations, explains leadership changes By Daniel Abia, P/Harcourt The Movement for the Survival of the Ogoni People (MOSOP) has assured the people of Ogoni of a fair outcome from its ongoing dialogue with the Federal Government on the resumption of oil operations in the area. The assurance followed concerns raised by the leadership […]

KENYA inapanga kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi ili kuziba pengo la nafaka hiyo lililosababishwa na ukame unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini yanayotegemewa kwa uzalishaji wake. Kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo Dijitali, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, alisema uagizaji huo utafanywa na sekta binafsi. “Ni sekta binafsi itakayonunua mahindi. Pesa hizo hazitatoka katika hazina ya Serikali,” Bw Kagwe alisema kwa njia ya simu. Uamuzi huo alisema umefikiwa baada ya ukame kuathiri kaunti zinazozalisha mahindi kwa wingi, zikiwemo Uasin Gishu na Trans Nzoia, ambako wakulima wameripoti hasara kubwa baada ya mimea kukaukia shambani. Waziri Kagwe alisema Serikali ilikuwa imewataka wakulima waliokuwa na mahindi kuyapeleka katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) ili kuongeza akiba, lakini ni magunia 180,000 pekee yaliyopokelewa na kununuliwa. Alisema kiasi hicho hakikutosha kukidhi mahitaji ya nchi. “Ni kweli wakulima wanaendelea kujiwekea mahindi kwa maghala yao, ilhali nilipokuwa kwenye ziara ya kikazi Sagana, Kirinyaga niliwaomba wayaachilie kwa NCPB,” alielezea. Alifafanua kuwa Serikali haitanunua moja kwa moja magunia milioni 25, bali itafungua soko kwa wafanyabiashara binafsi kuagiza mahindi kupitia njia za kawaida za kibiashara. “Serikali haitanunui magunia milioni 25 ya mahindi kutoka nje. Tunafungua tu soko ili mahindi yaingizwe kwa njia ya kawaida na sekta binafsi,” alisema. [caption id="attachment_191384" align="aligncenter" width="300"] Mahindi kwenye shamba la mkulima Kiambu. Picha|Sammy Waweru[/caption] Hata hivyo, Waziri Kagwe alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kununua mahindi kupitia NCPB kwa ajili ya akiba ya kimkakati, huku wafanyabiashara binafsi wakishughulikia uagizaji kutoka nje na usambazaji nchini. Serikali kwa sasa inanunua mahindi ya akiba kwa karibu Sh4,000 kwa gunia la kilo 90, ambayo huhifadhiwa kwenye maghala ya NCPB. Bw Kagwe alisema Kenya ilivuna takriban magunia milioni 71 ya kilo 90 mwaka jana, akirekebisha makadirio ya awali ya magunia milioni 60. Alisema ongezeko hilo lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mpango wa Serikali wa kutoa mbolea kupitia mpango wa ruzuku, ambao ulisaidia uzalishaji kuongezeka kutoka magunia milioni 41 hadi milioni 71 ndani ya miaka miwili hadi mitatu. Hali kadhalika, ongezeko hilo la uzalishaji mahindi nchini ulitokana na mvua bora iliyoshuhudiwa mwaka uliopita, 2025. Mahitaji ya mahindi nchini ni kati ya magunia milioni 70 na 75 kwa mwaka, hivyo Kenya inaweza kukabiliwa na upungufu wa karibu magunia milioni 25 mwaka huu kutokana na kiangazi na ukame unaoshuhudiwa. Bw Kagwe kwenye mahojiano, alisema uagizaji huo haupaswi kusababisha hofu yoyote ile kwa Wakenya, akisisitiza kuwa Serikali imeweka mipango kabambe kuhakikisha nchi haikabiliwi na uhaba wa chakula. “Tutaagiza mahindi. Tayari tumefanya mipango hiyo. Tutaweza kulisimamia hili. Nchi haitakosa chakula,” alisisitiza. Awali jana, Jumatano, Agosti 19, wakati wa Mkutano wa Makala ya Tano wa Mashauriano ya pamoja na Mawaziri kutoka Kaunti (CEC) ambapo alizindua mpango wa AgriConnect Compact, Bw Kagwe alisema ukame umedhihirisha haja ya kupanua kilimo cha mfumo wa umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa mifereji (irrigation) ili kupunguza utegemeaji wa mvua. “Tunapaswa kukumbatia kilimo kinachozingatia bunifu na teknolojia za kisasa, ili mabadiliko ya tabianchi yasiathiri uzalishaji wetu wa chakula,” alisema. Aidha, Waziri Kagwe alitaja mradi wa Galana-Kulalu kama mfano wa maeneo yanayotumia teknolojia endelevu za kilimo, huku Baringo, Garissa na Tana River zikiwa na maeneo makubwa yanayoweza kuongeza uzalishaji wa chakula iwapo teknolojia hizo zitakumbatiwa. [caption id="attachment_191385" align="aligncenter" width="300"] Mahindi yanayoendelea kukua kwenye shamba la mkulima. Picha|Sammy Waweru[/caption] Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Vyama vya Ushirika katika Baraza la Magavana Nchini (CoG), alisema mipango ya kilimo ya serikali imeonyesha kuwa kaunti zinaweza kupata matokeo bora raslimali zinapofikishwa kwa wakati ufaao. Bw Lusaka alisema mipango hiyo imesaidia wakulima kupata pembejeo, teknolojia, masoko, huduma za kifedha na fursa mpya za kujipatia riziki. “Mashirika yanayoleta pamoja wakulima ni muhimu hasa Kenya inapohama kutoka kilimo cha mtu mmoja mmoja kuelekea ukusanyaji wa mazao, uuzaji wa pamoja, masoko yaliyopangwa na upatikanaji bora wa fedha,” Lusaka alisema. Pia, alisema uwekezaji katika mifumo ya kidijitali na teknolojia umekuwa muhimu katika kuunganisha wakulima na huduma zinazoongeza uzalishaji, masoko na mikopo. Upungufu wa mahindi unajiri wakati Serikali inajiandaa kwa uwezekano wa mvua ya El Niño kati ya mwezi Oktoba na Desemba mwaka huu. Bw Kagwe alisema mvua hiyo inaweza kuwa na manufaa au kusababisha madhara kutegemea kiwango na maeneo itakakonyesha. Wakulima wa mashamba makubwa eneo la North Rift tayari walikuwa wamepunguza akiba yao baada ya Serikali kutoa ilani ya siku 30 mapema mwaka huu ya kuachilia mahindi yaliyokuwa yamehifadhiwa au kuruhusu uagizaji wa mahindi bila ushuru, hatua iliyolenga kupunguza bei ya unga. Wakulima wanasema waliwauzia wafanyabiashara na wasagaji wa unga kwa Sh5,400 kwa gunia la kilo 90, ikilinganishwa na Sh4,000 iliyokuwa ikitolewa na NCPB. James Songok, mkulima kutoka Kerita, Kaunti ya Uasin Gishu, alisema alikuwa na magunia 300 lakini aliuza kwa wasagaji na wafanyabiashara waliotoa bei nzuri zaidi kutokana na kupanda kwa gharama za mbegu, mafuta, dawa, shughuli ya vibarua na usafirishaji. “Nilikuwa na magunia 300 ya mahindi lakini niliuzia wasagaji na wafanyabiashara wengine walionipa dili nzuri,” alisema. [caption id="attachment_191386" align="aligncenter" width="300"] Hindi lililokomaa tayari kuvunwa. Picha|Sammy Waweru[/caption] NCPB ilinunua magunia 200,000 katika msimu wa 2025/2026, dhidi ya lengo la magunia milioni mbili ya akiba ya kitaifa ya chakula. Serikali inalenga kuweka akiba ya magunia milioni nne ya nafaka, ikiwemo mahindi, mchele na maharagwe, au fedha sawa na thamani ya kiasi hicho. Titus Maiyo, Meneja wa Mawasiliano NCPB, alisema bodi hiyo ilinunua magunia 156,000 ya kilo 50 msimu uliopita kwa bei ya Sh2,200 kwa kila gunia. Wakati huo huo, wataalamu na wakulima wameibua wasiwasi kuhusu makadirio ya Serikali ya uzalishaji wa magunia milioni 70, wakisema uzalishaji halisi unaweza kuwa chini ya kiwango kinachosemekana kwa sababu ya mbolea isiyo bora, mbegu bandia, magonjwa na mvua nyingi wakati wa mavuno. Mtaalamu wa kilimo kutoka Eldoret, Robert Kemboi, alisema mavuno yalikuwa chini ya makadirio ya Serikali. “Kinachojitokeza ni kwamba mavuno ya mahindi yalikuwa chini ya magunia milioni 70 yanayotajwa na Serikali,” Kemboi alisema. Kulingana na Shirika la Kitaifa la Takwimu Kenya (KNBS), Kenya imekuwa ikiagiza wastani wa tani 295,092 za mahindi kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Mahindi kutoka Uganda, Zambia, Afrika Kusini na Tanzania yamekuwa yakisaidia kuziba pengo la uzalishaji wa ndani kwa ndani wakati mahitaji yanapozidi kiwanfo cha mavuno. Kenya pia huzalisha kiasi kidogo cha ngano ikilinganishwa na mahitaji yake, hivyo kulazimika kuagiza kutoka nje ili kuziba pengo. Serikali sasa inalenga kuongeza akiba ya chakula na kuimarisha mifumo ya umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa mifereji, ndiyo Irrigation systems, ili kupunguza utegemeaji wa mvua na kuhakikisha nchi haikabiliwi na uhaba wa chakula wakati wa misimu ya kiangazi na ukame.

DAR ES SALAAM; CHAMA cha Wazee Wanaume Tanzania kinatarajia kufanya mkutano wake wa kwanza jijini Dodoma Agosti 29, mwaka huu, ukilenga kujadili changamoto zinazowakabili ikiwamo matunzo, afya na ustawi wao. Mkutano huo utakaoshirikisha wajumbe 200 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar, unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi. Akizungumza jijini Dodoma, Mwenyekiti…

WATU saba walioangamia katika ajali ya helikopta Mlima Ololokwe, Samburu walijumuisha Mkenya, Waamerika watano na raia wa Ecuador. Waliofariki wanajumuisha rubani Mkenya na mkurugenzi wa kampuni ya African Heli Adventures Josh Outram, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ujasusi cha Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe Stephany Hollihan Yeaza. [caption id="attachment_191376" align="alignnone" width="1500"] Maafisa wa usalama wakiwa eneo la mkasa wa helikopta Mlima Ololokwe, Samburu. Picha|David Muchui[/caption] Imetambuliwa pia kwamba rais na meneja wa vituo vya runinga vya Telemundo jimbo la Florida Jose Suarez alikuwa miongoni mwa wakuu wa kampuni kutoka Amerika waliopoteza maisha yao. Wengine ni Roger Duarte, Adam Hlavaty na Henry Parra. Utambulisho wa waliofariki ulithibitishwa kupitia ripoti ya polisi huku vyombo vya habari vya Amerika vikinukuu Kitengo cha Serikali kama kilivyothibitisha majina. [caption id="attachment_191378" align="alignnone" width="1500"] Maafisa wa usalama wakiondoa miili kutoka eneo la ajali ya helikopta, Mlima Ololokwe, Samburu. Picha|David Muchui[/caption] Watalii hao walikuwa wamepaa kutoka Suiyan, katika hifadhi ya Loisaba, Laikipia, mpaka Mlima Ololokwe wakati helikopta hiyo ilipoanguka katika kilima chenye mawe makubwa. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Samburu David Nkoroi alisema kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijatambuliwa. Ripoti zinasema kwamba Outram alikuwa rubani aliye na ujuzi na tajriba kubwa na ambaye amepaisha ndege katika maeneo ya vilima kwa miaka kadha kama mdau wa utalii na kusaidia kushika doria za angani katika hifadhi za wanyamapori. Katika mahojiano ya awali na Loisaba Collection, Outram alieleza jinsi alivyopenda urubani na kutalii maeneo ya kaskazini mwa Kenya. “Kaskazini mwa Kenya kuna mandhari tofauti sana katika eneo dogo. Ninachokiona kila siku ni jambo ambalo ninaamini kila anayekuja Kenya anapaswa kuliona,” alisema. Alisema helikopta huwapa watalii nafasi ya kufikia maeneo ya mbali na ambayo hayajaathiriwa na shughuli nyingi za binadamu kaskazini mwa Kenya. Wakati huo huo, kifo cha Sensi-Contugi na mkewe kilithibitishwa na serikali ya Ecuador kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya X ya Rais Daniel Noboa. “Katika wakati huu wa majonzi makubwa, Serikali ya Kitaifa inatuma rambirambi zake za dhati kwa familia zao, wapendwa wao na marafiki wa karibu,” ilisema taarifa hiyo. Vyombo vya habari vya Ecuador viliripoti kuwa Sensi-Contugi aliwahi kuwa Waziri wa Usalama wa Ndani kati ya Aprili na Agosti 2024, kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Ujasusi (CNI). Alitajwa pia kuwa mshirika wa karibu wa Rais Noboa. Nchini Amerika, NBC 6 iliripoti kuwa kifo cha Suárez, 55, kilithibitishwa kupitia taarifa ya pamoja ya viongozi wa NBCU News Group na Telemundo. “Tumepokea kwa huzuni kubwa habari kwamba José amefariki katika ajali ya helikopta nchini Kenya. José alikuwa mfanyakazi bora aliyejali sana aliofanya kazi nao, jamii walizohudumia na jukumu muhimu la vituo vyetu katika maisha ya watu,” viongozi hao walisema. Familia ya Duarte, 39, pia ilithibitisha kifo chake na cha waathiriwa wengine. “Familia za Duarte na Valls zimevunjika moyo na kuhuzunika kutokana na ajali hii mbaya ya helikopta nchini Kenya iliyowaua wapendwa wetu,” familia hiyo ilisema. Helikopta hiyo inayomilikiwa na Lady Lori, kampuni ya kukodisha ndege, ilianguka ikijaribu kutua Mlima Ololokwe, eneo maarufu kwa watalii kutokana na mandhari yake na machweo ya kuvutia.

DAR ES SALAAM: A total of 200m/- is expected to be raised during the 2026 Rotary Goat Races to support education initiatives, including scholarships for underprivileged students, improvement of learning environments and Water, Sanitation and Hygiene (WASH) facilities. President of the Rotary Club of Dar es Salaam Oyster Bay, Paul Muhato, said the event, themed…

DODOMA: NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (anayeshughulikia afya), Jafar Seif, amesema ugatuzi wa madaraka ni miongoni mwa misingi muhimu ya kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuziimarisha Serikali za Mitaa ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi. Akifungua mkutano wa mwaka wa…

MAGAVANA kadhaa wanaowania muhula wa pili wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kutafuta manaibu wapya baada ya uhusiano wao na waliowasaidia kushinda uchaguzi wa 2022 kuvurugika. Takriban magavana 10 wamejipata katika hali hii huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, na sasa wanatafuta washirika wapya watakaowasaidia kuhifadhi viti vyao. Mzozo wa hivi majuzi kati ya Gavana wa Kericho Erick Mutai na naibu wake Fred Kirui umeongeza orodha ya magavana waliokosana na manaibu wao. Wengine wanaotafuta manaibu wapya ni magavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Elgeyo Marakwet Wisley Rotich na Siaya James Orengo. Magavana wa Homa Bay Gladys Wanga, Kisii Simba Arati na Uasin Gishu Jonathan Bii pia wametofautiana na manaibu wao. Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti na Abdi Guyo wa Isiolo pia wamewahi kuwa na uhusiano baridi na manaibu wao. Kati ya magavana 29 wanaowania muhula wa pili, ni 19 ambao hawajawahi kuripotiwa kukosana na manaibu wao tangu walipochaguliwa mwaka 2022. Kaunti hizo ni Nairobi, Kakamega, Busia, Migori, Nakuru, Nyamira, Samburu, Turkana, Kiambu, Murang’a, Nyandarua, Makueni, Embu, Meru, Mandera, Taita Taveta, Kilifi, Kwale na Mombasa. Lakini uhusiano mzuri wa sasa haumaanishi kwamba magavana hao wataendelea kuwa na manaibu hao, hasa wakati wanasiasa wanapopanga upya ushirikiano kuelekea 2027. Kikatiba, kila anayewania ugavana anapaswa kumteua mtu wa kuwa mgombea mwenza ambaye huwa naibu gavana. Uhusiano kati ya magavana na manaibu wao umekuwa ukigubikwa na migogoro, maslahi ya binafsi, makubaliano yaliyovunjwa na wakati mwingine kuvumiliana. Huko Kericho, Bw Mutai alitangaza Jumanne kwamba amekata uhusiano wa kisiasa na Bw Kirui, akimlaumu kwa kuhusika katika majaribio mawili ya kumng’atua. Alisema sasa atashirikiana na waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi wa kaunti Jackson Rop, ambaye anatoka eneo la Kipkelion Magharibi sawa na Bw Kirui katika uchaguzi wa 2027. Bw Kirui alidai awali kuwa wawili hao walikubaliana kugawana nyadhifa za serikali ya kaunti kwa uwiano wa asilimia 60 kwa 40, lakini mpango huo haukutekelezwa. Bw Mutai alinusurika majaribio mawili ya kumtimua, mwaka 2024 na 2025, baada ya Seneti kuyakataa. Huko Elgeyo Marakwet, uhusiano kati ya Bw Rotich na naibu wake Grace Cheserek pia umeharibika. Mzozo wao uliibuka hadharani hivi majuzi baada ya Bi Cheserek kumkabili gavana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Biblia iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kimarakwet. Huko Trans Nzoia, Bi Philomena Kapkory amekuwa akizozana na Bw Natembeya tangu 2023, akidai kutengwa katika maamuzi na usimamizi wa serikali ya kaunti. Siaya pia imekumbwa na mzozo kama huo, huku Naibu Gavana William Oduol akidai uhusiano wake na Bw Orengo umedorora kabisa. Na katika kaunti ya Homa Bay, Bw Wanga alimtimua naibu wake Oyugi Magwanga baada ya kumuunga mkono mgombea huru katika uchaguzi mdogo wa Kasipul badala ya mgombea wa ODM. Kisii pia ilishuhudia Naibu Gavana Robert Monda akiondolewa kupitia mchakato wa kumtimua mwaka 2024 baada ya mzozo wa kisiasa na Bw Arati. Na katika kaunti ya Uasin Gishu, Naibu Gavana John Barorot alijiuzulu mwaka 2024 na nafasi hiyo ikachukuliwa na MCA Evans Kapkea. Tangu kuanzishwa kwa serikali za ugatuzi mwaka 2013, ni manaibu gavana 15 pekee ambao wamewahi kubaki na wakubwa wao katika uchaguzi uliofuata. Hii inaonyesha ugumu wa “ndoa” ya kisiasa kati ya magavana na manaibu wao, ambayo mara nyingi huvunjika kabla ya kufika mwisho wa muhula.

KENYA inaelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 huku ndimi za moto za wanasiasa zikianza kuwaka, hali inayozua hofu ya kuibuka kwa siasa za chuki, ukabila na ghasia. Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imeanza kuchunguza matamshi ya viongozi mbalimbali ambayo inasema yanaweza kuchochea migawanyiko ya kikabila, ghasia au kuvuruga amani nchini. Miongoni mwa viongozi walioangaziwa na tume hiyo ni aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambaye ameagizwa kufika mbele ya NCIC Agosti 27 kuelezea kuhusu matamshi aliyotoa katika mikutano ya kisiasa kaunti za Vihiga, Kisii na Meru. Bw Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), atahojiwa kuhusu muktadha, nia na athari zinazoweza kusababishwa na kauli hizo. NCIC imesema matamshi hayo yanaweza kuwa ya ubaguzi au ya kuchochea. Tume imeambatanisha agizo hilo na nakala za matamshi inayochunguza. Afisa Mkuu Mtendaji wa NCIC Daniel Giti ameonya kuwa iwapo Bw Gachagua hatafika mbele ya tume, huenda akakamatwa na kuwasilishwa mbele ya tume. Uchunguzi huo unafanyika huku wanasiasa wakizidisha kampeni za mapema kuelekea uchaguzi wa 2027, mikutano ya kisiasa ikigeuka kuwa majukwaa ya mashambulizi makali dhidi ya wapinzani. Katika tukio moja linalochunguzwa, Bw Gachagua anadaiwa kutoa matamshi katika mkutano Luanda, Vihiga, Juni 12 ambayo tume inasema yanaweza kuchochea mgawanyiko wa kikabila. Pia anahojiwa kuhusu kauli alizotoa katika Uwanja wa Gusii, Kisii, Februari 23, ikiwemo zilizomhusu Mbunge wa Nyaribari Chache Zaheer Jhanda. Ziara yake ya Meru mwishoni mwa Julai pia inamlikwa na NCIC baada ya tume kusema baadhi ya matamshi aliyotoa yanaweza kuchukuliwa kuwa ya kuchochea vurugu na kulenga jamii fulani. Lakini Bw Gachagua si mwanasiasa pekee anayechunguzwa. Gavana wa Busia Paul Otuoma pia ameitwa na NCIC kujibu madai ya kuchochea hisia dhidi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mengine ya nchi katika mkutano wa hadhara huko Bulanda Junction mnamo au karibu na Juni 27. Mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma anakabiliwa na uchunguzi kama huo kuhusu matamshi aliyotoa kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi uliofanyika Homa Bay Agosti 16. Bw Kaluma aliitwa kufika mbele ya tume Jumatano. Wanasiasa wengine wanaochunguzwa ni Waziri wa Afya Aden Duale, Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, Mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia, Mbunge wa Sirisia John Waluke na Naibu Gavana wa Mandera Ali Mohamud. NCIC ilitangaza Julai 28 kuwa imeanza kuchunguza matamshi yaliyohusishwa na baadhi ya viongozi hao, akiwemo Bw Duale, Bw Ruku, Bw Otuoma na Bw Waluke. Wengine ni Mbunge wa Kipipiri Wanjiku Muhia na Mbunge wa Nakuru Town East David Gikaria. Mwenyekiti wa NCIC Kepha Omae alisema mazingira ya kisiasa nchini yanaendelea kuwa makali huku matamshi ya uchochezi, vitisho na siasa za kikabila yakizidi. “Tunaona mazingira ya kisiasa yanayozidi kuwa makali ambapo matamshi ya uchochezi, kulenga jamii fulani, vitisho na kuwachochea vijana vikiwa jambo la kawaida,” alisema. Hata hivyo, alisema NCIC haiwezi kukimbilia kufikisha kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) bila kuwa na ushahidi wa kutosha. “Hauwezi kupeleka faili kwa DPP achukue hatua bila ushahidi wa kutosha. Ndio maana kesi nyingi huishia hapo,” alisema. Bw Omae alisema wachunguzi wa tume hulazimika kusafiri hadi maeneo ambako matamshi hayo yalitolewa, kubaini muktadha wake na kutafuta mashahidi walio tayari kutoa taarifa rasmi. Alisema tatizo kubwa ni kwamba Wakenya wengi huwa wepesi kuripoti matamshi yanayowaudhi lakini husita kuwa mashahidi. “Wakenya ni wazuri katika kuripoti na kulalamika lakini wanapotakiwa wawe mashahidi na hata kuweka malalamiko yao kwa maandishi hawataki kwa sababu wanafikiri wataitwa mahakamani,” alisema. NCIC imesema imefanikisha hukumu tano huku kesi nyingine tatu zikiwa mahakamani. Hata hivyo, hakuna mwanasiasa aliyepatikana na hatia katika kesi hizo. Malalamiko yaliyohusu mwanaharakati wa haki za binadamu Khelef Khalifa, Mbunge wa Tigania East Mpuru Aburi na chifu mkuu Wilson Kaloi yalikataliwa na DPP kwa sababu ya kukosa ushahidi wa kutosha. Kesi ya mbunge Peter Salasya nayo ilisitishwa baada yake kuomba msamaha. Uchunguzi wa sasa umeibua mjadala kuhusu iwapo taasisi za serikali zinachukua hatua mapema ya kutosha kuzuia matamshi hatari kabla hayajageuka kuwa vurugu. NCIC imekuwa ikichunguza pia matukio ya nyuma tangu uchaguzi wa 2022. Wakati wa uchaguzi mdogo wa Ol Kalou, Mbunge wa Kipipiri Wanjiku Muhia na Bw Gikaria walitozwa faini ya Sh1.5 milioni na Sh2.5 milioni mtawalia na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kukiuka kanuni za maadili ya uchaguzi. Huku hayo yakijiri, baadhi ya wanasiasa wamejikuta wakilazimika kuomba msamaha baada ya matamshi yao kuzua hasira. Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar alikabiliwa na wito wa kujiuzulu mwezi Mei baada ya matamshi yake kutafsiriwa na wakosoaji kuwa yalilenga jamii fulani. Baadaye aliomba msamaha. Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga pia aliomba msamaha na kujiuzulu kama naibu mwenyekiti wa Baraza la Magavana baada ya matamshi yake kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga Novemba 2025 kuzua ukosoaji. Wakati huo huo, Bw Duale anaendelea kuchunguzwa kuhusu matamshi aliyotoa katika hafla ya umma eneo la Lafey, Mandera. Waziri huyo amekana kufanya kosa akisema matamshi yake yalipotoshwa na kutolewa nje ya muktadha. Mwakilishi wa Wanawake wa Murang’a Betty Maina pia ameangaziwa na NCIC kutokana na matamshi aliyotoa dhidi ya Bw Gachagua.

…LASCOPA begins monitoring, enforcement By Olasunkanmi Akoni LAGOS — The Lagos State Government, through the Lagos State Consumer Protection Agency, LASCOPA, has raised the alarm over the alleged manipulation of production and expiry dates on expired and near-expired products being sold in markets and retail outlets across the state. The agency said devices and chemicals […]

Serikali za Afrika Mashariki zimehimizwa kuwekeza mapema katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi badala ya kusubiri mafuriko na ukame kutokea ndipo zianze kutoa fedha za dharura. Shirika la Vi Agroforestry limesema maandalizi hayo ni muhimu huku utabiri ukionyesha uwezekano wa mvua nyingi na mafuriko katika maeneo ya Afrika Mashariki kati ya Oktoba na Desemba mwaka huu. Shirika hilo limesema El Niño haifai kuonekana kama tishio la msimu mmoja pekee, bali ni ishara ya haja ya kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga ya hali ya hewa. Kwa mujibu wa shirika hilo, uharibifu wa ardhi, maeneo ya vyanzo vya maji na maisha ya wakulima umeongeza madhara yanayosababishwa na mvua kubwa, mafuriko na ukame. Utabiri wa hivi karibuni unaonyesha kuwa baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki yanaweza kupokea mvua nyingi kuliko kawaida katika msimu wa Oktoba hadi Desemba, jambo linaloweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi, uharibifu wa mazao na kuhama kwa familia. Vi Agroforestry imesema serikali zinapaswa kuelekeza fedha zaidi kwa wakulima wadogo, wanawake, vijana na wafugaji ambao wako mstari wa mbele katika kusimamia ardhi na maji. Shirika hilo limependekeza kupanuliwa kwa kilimo-misitu, ambapo miti hupandwa pamoja na mazao na mifugo, kama njia mojawapo ya kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Limesema miti na udongo wenye afya husaidia kupunguza kasi ya maji yanayotiririka, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuongeza uwezo wa ardhi kuhifadhi maji. Kwa wakulima, miti pia inaweza kuwa chanzo cha matunda, chakula cha mifugo, kuni na kipato wakati mazao yanapoharibiwa na hali mbaya ya hewa. Vi Agroforestry pia imetaka serikali kuwekeza katika uvunaji wa maji, uhifadhi wa udongo, urejeshaji wa maeneo ya mito na vyanzo vya maji, vitalu vya miti na mifumo ya kilimo inayostahimili mabadiliko ya hali ya hewa. Shirika hilo limesema mifumo ya kutoa tahadhari mapema inapaswa kuimarishwa ili wakulima wapate taarifa kwa wakati na kuchukua hatua kabla ya mvua kubwa kuanza. Aidha, limewataka wafadhili, taasisi za kifedha na kampuni binafsi kuongeza fedha kwa miradi inayoongozwa na jamii. Limesema wanawake, vijana, wakulima wadogo na wafugaji hawapaswi kuonekana kama wapokeaji wa msaada pekee, bali washirikishwe katika kupanga na kutekeleza miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Vi Agroforestry imesema ingawa maandalizi ya dharura kama kusafisha mitaro na kuimarisha huduma za uokoaji ni muhimu, hatua hizo hazitoshi bila uwekezaji wa muda mrefu. “El Niño itapita, lakini hali ya hewa isiyotabirika itaendelea,” shirika hilo limesema. Limesema hatua zinazochukuliwa sasa ndizo zitakazoamua iwapo majanga yajayo yataendelea kusababisha hasara kubwa au jamii zitakuwa na uwezo wa kukabiliana nayo.

By Victor Ahiuma-Young & Johnbosco Agbakwuru ABUJA — The Federal Government has unveiled fresh plans to unlock Nigeria’s more than 215 trillion cubic feet (tcf) of proven natural gas reserves for industrial development, as the Nigerian Upstream Petroleum Regulatory Commission (NUPRC) said the country could raise crude oil production to three million barrels per day. […]

KATIKA eneo kame la Kinna, Kaunti ya Isiolo, ambako ukame na mabadiliko ya tabianchi yamefanya kilimo na ufugaji kuwa changamoto kubwa, kundi la wakulima limegundua kuwa kilimo endelevu kinaweza kuwa njia ya kujikomboa kutoka kwa umaskini na kutegemea chakula cha msaada. Kupitia kilimo cha mvungulio (greenhouse) na mfumo wa umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa njia ya matone chini ya Nasole SACCO, manusura wa ukatili wa kijinsia kwenye ndoa sasa wanajipatia kipato, kulea familia zao na kuandika ukurasa mpya wa maisha. Miongoni mwao ni Najma Ado, ambaye alitoka kwenye ndoa kufuatia madhila na vita vya kijinsia, na mkazi wa Kinna, ambaye leo hii analima mboga na viungo kwenye greenhouse. Anasema hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angejitegemea kupitia kilimo. “Nilipitia changamoto kibao kwenye ndoa, ikiwemo kupigwa na aliyekuwa mume wangu,” anasimulia. Maisha yalibadilika baada ya kujiunga na Nasole SACCO, chama cha ushirika Isiolo, ambako alipata mkopo wa Sh40, 000 na mafunzo ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi. “Leo hii mimi ni mkulima. Mapato ninayopata yananisaidia kulisha watoto wangu, kuwalipia karo, na kusaidia kukidhi mahitaji yao na hata kusaidia wazazi wangu,” anasema. Safari yake haikuwa rahisi. Najma aliolewa akiwa na umri wa miaka 14 na akawa mama akiwa bado mchanga. Badala ya kuendelea na masomo, aliingia kwenye ndoa iliyogeuka kuwa ngome ya mateso na ukatili wa kijinsia. [caption id="attachment_191341" align="aligncenter" width="300"] Najma Ado Mohamed, mama asiye na mume na manusura wa ukatili wa kijinsia (GBV) kutoka Kinna, Kaunti ya Isiolo, akisimulia safari yake katika kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi. Picha|Sammy Waweru[/caption] “Baada ya kupata mtoto wangu wa kwanza, mume wangu alianza kunipiga. Nilivumilia kwa miaka kadhaa kabla ya kuamua kuondoka,” akaambia Akilimali wakati wa mahojiano katika Kijiji cha Kinna. Baada ya kurejea nyumbani akiwa na watoto wawili na bila chanzo cha mapato, alikabiliwa na maisha magumu katika eneo ambalo ukame wa mara kwa mara umeathiri maisha ya wakazi wengi. Kupitia Nasole SACCO, alipata fursa ya kujifunza kuhusu kilimo cha kisasa, usimamizi wa fedha na ujasiriamali. Pia, alifunzwa jinsi ya kuweka akiba ambayo imemuwezesha kupanga maisha yake ya baadaye. “Sitaki kurudi tena katika maisha ya mateso. Watoto wangu sasa wanaishi kwa amani na wanaendelea na masomo yao,” akasema. Alidokeza kwamba mafunzo kuhusu haki za wanawake yamewapa wanawake wengi ujasiri wa kupinga ukatili wa kijinsia, dhuluma na kutafuta msaada wanapodhulumiwa. Mbali na Najma, Mariam Mohamed naye amepata matumaini kupitia kilimo. Kwenye kivungulio, analima nyanya, pilipili mboga (maarufu kama hoho) na mchicha kwa kutumia mfumo wa umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa kutumia mifereji kudondoa matone. Mariam anasema wazazi wake walitalikiana alipokuwa na umri wa miaka saba. Baadaye aliolewa akiwa bado mdogo kimiaka, lakini ndoa hiyo pia ilivunjika na kumlazimu kuanza maisha upya akiwa na watoto wake. “Nilitegemea msaada kutoka kwa watu wengine ili kuishi. Maisha yalikuwa magumu sana,” anakumbuka. Alijiunga na kikundi cha wanawake mwaka 2012 na baadaye akawa mwanachama wa Nasole SACCO. “Nilianza kuweka akiba ya Sh100 kwa wiki na baada ya miezi sita niwekeza fedha hizo kwenye kilimo,” anafichua. [caption id="attachment_191342" align="aligncenter" width="300"] Mariam Mohamed akionyesha nyanya zilizovunwa kutoka kwenye kivungulio eneo la Kinna, Kaunti ya Isiolo. Yeye ni mama asiye na mume, manusura wa ukatili wa kijinsia (GBV) na mwanachama wa Nasole SACCO. Picha|Sammy Waweru[/caption] Leo hii Mariam huuza mboga na hupata wastani wa Sh500 kwa siku, fedha zinazomwezesha kulipia watoto karo, kununua chakula na kugharamia mahitaji ya familia. “Kupitia Nasole SACCO, nimeweza kusomesha watoto wangu. Zamani nilitegemea watu, lakini sasa ninaweza kuitunza familia yangu,” anasema. Anasema kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kilimo cha kisasa; kikiwemo teknolojia ya mvungulio na mfumo wa umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa kutumia mifereji kudondoa matone, kimekuwa suluhisho muhimu kwa wakazi wa Isiolo. Kulingana na Makai Mamo, Naibu Mwenyekiti wa Nasole SACCO, chama hicho cha ushirika kilichosajiliwa rasmi mwaka 2019, sasa kina wanachama wapatao 310, wakiwemo wanawake 230. Anasema pamoja na kutoa mikopo na huduma za kifedha, SACCO hiyo inalenga kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kujitegemea kimaendeleo. “Tunawaunganisha wanawake na taasisi za kifedha, mipango ya serikali inayowapiga jeki na mashirika mbalimbali ili wapate fursa za kujijenga upya kimaisha,” anasema. Kutokana na ukame wa mara kwa mara, wanachama wamekumbatia kilimo cha mvungulio, mfumo wa umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa kutumia mifereji kudondoa matone, ufugaji wa samaki na nyuki ili kuongeza uzalishaji na mapato. Kwa ushirikiano na Heifer International, World Food Programme, Catholic Relief Services na We World Kenya Foundation, wanachama hupatiwa mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha, ujasiriamali, mahusiano bora ya kifamilia na kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

UTAMADUNI wa kusoma vitabu nchini umeendelea kupungua hali inayozua mjadala kuhusu umuhimu wa vitabu katika kuongeza maarifa na kujenga uwezo wa jamii kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

ABUJA, Nigeria: KAMPENI za uchaguzi wa Januari 2027 Nigeria zilianza Jumatano huku Rais Bola Tinubu akikabiliwa na swali gumu anapowania muhula wa pili hasa kuhusu utendakazi wake. Wengi wanajiuliza iwapo wananchi wa Nigeria wanaishi maisha bora baada ya zaidi ya mwongo mmoja wa utawala wa chama cha All Progressives Congress (APC). Tinubu yupo katika kinyang’anyiro dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais Atiku Abubakar na Peter Obi, ambao wamekita kampeni zao katika masuala ambayo wananchi wanalalamikia hasa ugumu wa maisha na ukosefu wa usalama. Wapinzani wanadai kuwa miaka karibu 12 ya APC madarakani imeiacha Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi Afrika, likiwa maskini zaidi, lenye madeni mengi na lisilo salama kuliko 2015. Hali ni mbaya zaidi ikilinganishwa na chama hicho kilipoingia mamlakani chini ya aliyekuwa Rais Muhammadu Buhari. Kwa Tinubu, ambaye baadhi ya wananchi humwita “T-Pain” kutokana na gharama ya juu ya maisha, uchaguzi huo utakuwa kipimo cha iwapo wapiga kura wako tayari kuvumilia maumivu ya muda mfupi kwa matumaini ya kupata nafuu ya muda mrefu. Asilimia 80 ya raia wa Nigeria wanaamini nchi yao inaongozwa vibaya, huku asilimia 45 wakitaja ugumu wa kiuchumi na ukosefu wa usalama kuwa changamoto zao kuu. Tinubu amefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi tangu aingie madarakani. Alifuta ruzuku ya mafuta iliyokuwa ikigharimu serikali fedha nyingi na kushusha thamani ya naira mara mbili. Hatua hizo zimepongezwa na wawekezaji na wakopeshaji wa kimataifa, lakini pia zimesababisha athari za kiuchumi kwa familia na kuchochea maandamano kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. Serikali ya Tinubu inasema mageuzi hayo yameimarisha mapato ya serikali na kuongeza imani ya wawekezaji. Hata hivyo, wananchi wengi hupima hali ya uchumi kwa uwezo wao wa kununua chakula na kugharamia mahitaji ya familia. Mfanyabiashara wa nyama Abdullahi Sani alisema zamani alikuwa akiuza mbuzi sita kwa siku, lakini sasa anahangaika kuuza hata wawili. Mizigo ya madeni pia imeongezeka. Usalama nao ni changamoto kubwa kwa Tinubu. Ingawa serikali inasema operesheni za kijeshi zimepunguza mashambulizi na kuwezesha wakulima kurejea mashambani, ghasia, utekaji nyara na ujambazi bado umeenea. Wapinzani sasa wanatumia hali hiyo kumshambulia Tinubu, wakisema baada ya zaidi ya miaka 10 ya APC madarakani, wananchi wanataka kuona matokeo, si ahadi. Kwa wapiga kura wengi, uchaguzi huo utahusu maisha, usalama na chakula. Hata hivyo, mgawanyiko katika upinzani unaweza kumpa Tinubu nafasi ya kubaki madarakani licha ya changamoto zinazokabili uongozi wake.

A Tanzanian lawyer has taken legal action challenging the long-standing imposition of user fees on motorists crossing the Julius Nyerere Bridge in Dar es Salaam, setting the stage for a constitutional battle over infrastructure financing and public toll collection. In Constitutional Case No. 20632 of 2026, filed at the High Court of Tanzania, Dar es Salaam Sub-Registry, Advocate Mohamed Majaliwa asks the court to declare all tolls collected at the landmark bridge null and void. He argues that the toll collection system breaches fundamental provisions of the Constitution of the United Republic of Tanzania by failing to accord citizens equal treatment under the law. The suit names five public institutions as respondents: the Board of Trustees of the National Social Security Fund (NSSF), the Tanzania National Roads Agency (Tanroads), the Tanzania Revenue Authority (TRA), the Controller and Auditor General (CAG), and the Attorney General (AG). A three-judge bench comprising Justices Amir Mruma, who is presiding, Biswalo Muganga and Suleiman Hassan is scheduled to begin hearing the petition on Wednesday, August 19, 2026. Alleged unconstitutional discrimination At the heart of Mr Majaliwa’s constitutional challenge is his assertion that residents of Kigamboni Municipality and motorists using the cable-stayed bridge face unlawful discrimination compared with road users elsewhere in the country. In his supporting affidavit, the petitioner notes that several major bridges across Tanzania have been built using public resources but remain free to users. He cites the Tanzanite Bridge, which links Aga Khan and Coco Beach along Toure Drive in Dar es Salaam, and the Magufuli Bridge (Kigongo-Busisi), which spans the Gulf of Mwanza and links Mwanza and Geita regions. Mr Majaliwa argues that charging motorists to cross the Nyerere Bridge while allowing free passage on other state-funded infrastructure amounts to geographical and economic discrimination. According to the petition, the arrangement violates constitutional guarantees of equality before the law and provisions prohibiting discriminatory laws or actions by public authorities. The petition also alleges violations of constitutional provisions relating to civic obligations and rights, taxation, public financial oversight and the duty of every citizen and institution to respect and uphold the Constitution. Questions over PPP and toll operations The Nyerere Bridge, built across Kurasini Creek, was constructed under a joint Public-Private Partnership (PPP) between NSSF and the Central Government. Mr Majaliwa alleges that the partnership was established for an indefinite period, enabling NSSF to establish toll plazas, install payment booths and continuously collect fees from motorists. He argues, however, that decisions and administrative actions by the respondents to establish the toll plazas and impose user charges were made arbitrarily, without statutory authority and in breach of the law. While bridge tolls are regulated under the Roads and Fuel Tolls Act, the petitioner argues that the specific arrangements governing the Nyerere Bridge lack adequate legal backing and administrative transparency. He further contends that the TRA Commissioner General has the sole statutory responsibility for supervising road and fuel tolls and appointing authorised collection officers. Despite this mandate, the petition alleges that TRA delegated toll collection to NSSF personnel, despite knowing, or having reason to know, that the collection centres and payment arrangements lacked valid legal authorisation. Audit oversight questioned The petition also raises concerns over financial accountability and the auditing of public revenue generated at the bridge toll plazas since the infrastructure was commissioned. Mr Majaliwa alleges that, despite collecting significant amounts of money from the public over the years, the joint PPP entity has never undergone an independent and comprehensive audit by the CAG. He argues that the alleged failure violates the Constitution, which mandates the CAG to audit public revenue and expenditure, as well as provisions of the Public Audit Act. The petition further alleges that the CAG has failed to discharge his statutory duty to audit the revenues and publish reports on the bridge’s financial operations. Reliefs sought Mr Majaliwa, who says he is a resident of Kigamboni Municipality and a daily user of the bridge, argues that he is exercising his constitutional right to challenge what he considers administrative overreach that affects both his finances and the wider public interest. Among the reliefs sought, he wants the High Court to declare all tolls, user fees imposed on motorists using the Nyerere Bridge unconstitutional, illegal, null and void. He also seeks an order directing the respondents to immediately stop collecting tolls and user fees at the bridge. The petitioner further wants a permanent injunction restraining NSSF, Tanroads, TRA and their agents from continuing to operate toll collection plazas in breach of the Constitution. He is also asking the court to compel the CAG to conduct a comprehensive financial audit of all toll revenue collected from the bridge since operations began. Mr Majaliwa further asks that each party bear its own legal costs, together with any other orders or remedies the High Court may deem fit and proper. The hearing before the three-judge bench is expected to examine wider questions surrounding PPP governance, the legal basis for state-mandated user charges and the constitutional guarantee of equal treatment under Tanzanian law.

MAHAKAMA ya Eldoret ilipigwa na butwaa siku ya Jumatatu wakati msichana mwenye umri wa miaka 16 alipoeleza jinsi baba yake mzazi alivyomdfhulumu kingono mara kwa mara kila alipokuwa akimuuliza mahitaji ya shule. Msichana huyo, aliyetambuliwa kwa jina la siri A.W., alisimulia masaibu yake kwa majonzi kwa kukariri maahila aliyopitia mikononi mwa babake mzazi A. W wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo mahakamani. Akiwasilisha ushahidi wake mbele ya hakimu mkuu mkaazi Keyne Gweno, alieleza kuwa baada ya mama yake kufariki dunia na kuwaacha mabinti wanne akiwemo yeye, waliendelea kuishi chini ya uangalizi wa baba yao. "Wakati wowote mwalimu wangu aliponiambia nilete kitabu na kalamu, kadri nilipomwomba baba yangu aninunulie vitu hivyo ndivyo alinilazimu kushiriki naye tendo la ngono kabla ya kuninunulia vitu husika," alisimulia. Mahakama ilielezwa kuwa licha ya kutishiwa maisha iwapo angefichua unyama huo, hatimaye msichana huyo aliamua kumweleza mmoja wa walimu wake kuhusu unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa. Walimu kutoka shule hiyo walichukua jukumu la kutoa ripoti kwa polisi ambapo mshukiwa alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polis cha Langas na kufikishwa katika mahakama ya Eldoret. Mwanaume huyo alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la kufanya tendo la ngono na mtu wa familia ya karibu yani kujamiana, kinyume na Kifungu cha 20 (1) cha Sheria ya Makosa ya Kijinsia Nambari 3 ya mwaka 2006. Hati ya mashtaka inaeleza kuwa katika tarehe mbalimbali kati ya Januari 16, 2026, na Februari 6, 2026, katika eneo la Lemmok katika Kaunti Ndogo ya Kapseret, Kaunti ya Uasin Gishu, alimdhulumu kimapenzi binti yake mwenye umri wa miaka 16 kwa makusudi na kinyume cha sheria. Hata hivyo mshtakiwa alikana mashtaka hayo kabala ya kuamrishwa kuwachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 au dhamana mbadala ya pesa taslimu kiasi cha Sh100,000. Tangu wakati huo, mshtakiwa amb alishindwa kupata pesa taslimu za dhamana au dhamana ambapo amezuiliwa katika rumande ya Gereza la Eldoret GK akisubiri kesi kusikilizwa kikamilifu na kuamuliwa. Ombil la kutaka kupunguziwa dhamana ya pesa taslimu kutoka Sh100,000 hadi Sh50,000 ililikataliwa mahakamani. "Sitapunguza zaidi kiasi hicho cha dhamana ya pesa taslimu cha Sh100,000 kwa sababu najua kuwa mara tu utakapopata uhuru wako, hutawahi kurejea mahakamani hapa," aliamuru Hakimu. Akitoa ushahidi kuhusu suala hilo, Dkt Irene Simiyu, daktari katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi (MTRH), alithibitisha kuwa binti huyo alikuwa amedhulumiwa kingono. Upande wa mashtaka umepanga kuwasislihsa mashahidi watano muhimu, akiwemo afisa upelelezi kutoka Kituo cha Polisi cha Langas. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 8, 2026.

KAGERA: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Bashiru Kwakurwa, amevitaka vyama vya ushirika kushirikiana na wakulima wao kutafuta taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata elimu ya mikopo ili kuendeleza sekta ya kilimo, kuongeza thamani na ubora wa mazao pamoja na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi yanayozingatia ubora. Akizungumza wakati wa kuzindua…

the Public Protector’s findings were concerning, but not entirely surprising, given the persistent governance, administrative and system challenges at National Student Financial Aid Scheme (NSFAS).

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) has urged political parties to avoid turning the October 29 events into a political campaign tool, calling for patience as a commission appointed by President Samia Suluhu Hassan investigates what happened. CCM Secretary for Ideology, Propaganda and Training, Kenani Kihongosi, said the commission has been tasked with establishing…

SERIKALI imetetea mageuzi yake katika sekta ya afya, ikisema imetekeleza ahadi nyingi ilizotoa wakati wa kampeni licha ya changamoto mbalimbali. Rais William Ruto alisema maendeleo katika sekta ya afya hayapaswi kupimwa kwa idadi ya sheria zilizopitishwa au watu waliosajiliwa pekee, bali kwa uzoefu wa mgonjwa anayepata huduma. “Kipimo halisi cha mafanikio ni ikiwa mgonjwa anapata huduma za afya zinazotegemewa, nafuu na zenye kuheshimu utu wake,” alisema Rais. Alizungumza wakati wa Kongamano la kwanza la Kitaifa la Afya nchini Kenya lililoandaliwa na Wizara ya Afya chini ya kaulimbiu “Mageuzi yamewasilishwa, Afya ni Haki”, ambalo linalenga kujadili changamoto na mafanikio ya sekta hiyo. Rais alisema alipoingia mamlakani, mojawapo ya vipaumbele vyake vilikuwa kufufua mpango wa Huduma ya Afya kwa Wote (UHC), ambao alihisi ulikuwa umedorora. Hivyo, UHC ikawa moja ya nguzo tano za Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Chini kwenda Juu. Kwa mujibu wake, maradhi yanaweza kufilisi familia na kuwafanya wananchi kuingia katika umaskini, jambo lililomsukuma kutunga sheria nne mpya za afya mwaka 2023 zilizozaa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Kati ya Wakenya milioni 32.3 waliosajiliwa chini ya SHA, zaidi ya milioni nane wamepokea huduma za matibabu. Idadi hiyo inajumuisha akina mama milioni 1.2 waliosaidika kujifungua salama na zaidi ya 500, 000 kwa upasuaji tangu mpango huo uanzishwe. Rais alipuuziliaa mbali madai kwamba ameacha ajenda ya “hasla”, akisema ana ushahidi kuwa wananchi wa kipato cha chini ndio wanufaika wakubwa wa SHA. “Haya si mageuzi ya siku moja. Ni safari endelevu ya kupunguza pengo kati ya ahadi tulizotoa na huduma anayopokea kila Mkenya,” alisema. Hata hivyo, wadau wa afya walihoji kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika sera, changamoto kubwa bado ipo katika utekelezaji. Mkurugenzi Mkuu wa Reproductive Health Network Kenya, Bi Nelly Munyasia, alisema Kenya imepiga hatua katika sera za afya ya uzazi, lakini huduma hizo hazijafikishwa kikamilifu kwa wananchi. “Baadhi ya sera bora zaidi zinasalia kwenye makaratasi kwa sababu rasilimali hazijaelekezwa ipasavyo ili kuzitekeleza,” alisema. Alisisitiza umuhimu wa ufadhili endelevu, miundombinu ya kutosha, wafanyakazi wenye ujuzi na mifumo bora ya rufaa za wagonjwa. Kwa upande wake, Patrick Oyaro wa mradi wa Liverpool VCT and Research Kenya (LVCT), alisema huduma za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi zinapaswa kujumuishwa kikamilifu chini ya SHA. “Kwa muda mrefu huduma za Ukimwi zimefadhiliwa na wafadhili. Tunahitaji kubadili hali hiyo na kuhakikisha zinaingizwa kwenye SHA,” alisema. Kongamano hilo linafanyika wakati ambapo nchi inashuhudia mgomo wa wahudumu wa afya wa UHC na wauguzi. Mwenyekiti wa Muungano wa Maafisa wa Utabibu Kenya, Peterson Wachira, alisema Kenya bado iko mbali na malengo ya Ruwaza ya 2030 ya kuwa kitovu cha utalii wa matibabu barani Afrika. Aliongeza kuwa nchi pia haijafikia Azimio la Abuja linalotaka asilimia 15 ya bajeti ya taifa kutengewa sekta ya afya. “Mfumo wa usimamizi wa wahudumu katika afya umegawanyika mno. Upendeleo na ufisadi zimekithiri na wafanyakazi wengi wa afya wanateseka kutokana na uchovu na msongo wa mawazo,” alisema. Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), Dkt Dennis Miskella, alisema changamoto kubwa inayopuuzwa ni masuala ya wafanyakazi wa afya. “Kaunti zaidi ya 40 bado hazijalipa mishahara ya madaktari. Tunahitaji mjadala wa kina kuhusu uongozi na usimamizi wa sekta hii,” alisema. Alipendekeza kuwa magavana washughulikie huduma za msingi za afya huku serikali kuu ikisimamia huduma za matibabu ya kiwango cha juu ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

DAR ES SALAAM: THE ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), has dismissed reports that Vice-President Emmanuel Nchimbi has been summoned before the party’s Ethics Committee, saying it has no official communication confirming the claim. CCM Secretary for Ideology, Propaganda and Training, Kenani Laban Kihongosi, rejected the reports on Wednesday during an interview with Clouds FM’s Power…

The tragedy has raised serious questions about overcrowding, maritime safety and government oversight, particularly after earlier reports indicated that passengers had raised concerns about the dangerous conditions on the lake.

Two new collective investment schemes launched by Zan Securities are seeking to raise a combined Sh10 billion, offering investors different options ranging from regular income to long-term capital growth.

HUZUNI na mshtuko zimetanda katika kijiji cha Chabuene, Kaunti ya Meru, kufuatia mauaji ya kikatili ya Evelyne Mukiri Mbaabu, mwanamke anayekumbukwa kwa ukarimu wake na juhudi zake za kuhifadhi mazingira. Mkasa huo ulitokea mnamo Agosti 7 majira ya saa moja usiku, baada ya mwanaume asiyejulikana kuingia nyumbani kwake akiomba maji ya kunywa. Kwa mujibu wa familia, Bi Mukiri, mwenye umri wa miaka 65, alimkaribisha mgeni huyo na hata kumualika kwa kula chakula cha jioni. Kisha akamtuma mjukuu wake kwenda kuchota maji kutoka nyumba kuu huku akiendelea kuandaa chakula katika jiko lililojengwa nje ya nyumba. Hata hivyo, muda mfupi baadaye ukarimu wake uligeuka kuwa mkasa. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mjukuu huyo alipokuwa akichukua maji alisikia mayowe ya nyanya yake. “Aliporudi mbio jikoni, alimkuta mwathiriwa akiwa amelala katika dimbwi la damu amejeruhiwa,” ilisema ripoti ya polisi.

MZOZO wa kisheria kuhusu iwapo viongozi waliotimuliwa afisini kupitia bunge wanaweza kugombea nyadhifa za kisiasa kabla ya kesi zao kukamilika bado utaendelea kushuhudiwa nchini. Hii ni baada ya Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor, kukosa kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu utata huo. Suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, ambao wote waliondolewa mamlakani na Bunge na wanapinga kutimuliwa kwao kortini. Bi Oduor ameishauri Mahakama ya Juu kutosikiza ombi la kutoa ushauri wa kikatiba kuhusu iwapo viongozi walioondolewa mamlakani kupitia bunge wanaweza kugombea nyadhifa za kisiasa kesi zao zikiendelea mahakamani. Mawakili wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Meru, Ayub Bundi, hata hivyo, wamesema Mwanasheria Mkuu hakujibu maswali manane ambayo Mahakama ya Juu ilimtaka kuyashughulikia. Mawakili wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Meru, Ayub Bundi, hata hivyo, walisema Mwanasheria Mkuu hakujibu maswali manane ambayo Mahakama ya Juu ilimtaka kuyajibu. Mojawapo ya maswali hayo ni iwapo rufaa au kesi ya kupinga kuondolewa mamlakani inaweza kusimamisha amri ya kikatiba ya uamuzi huo na kumruhusu kiongozi huyo kugombea uchaguzi. “Baada ya kupitia ushauri huo, ni wazi kwamba haujajibu wala kushughulikia masuala hayo,” wakasema mawakili hao. Walimtaka Mwanasheria Mkuu kufuata maagizo ya Mahakama ya Juu kwa kutoa ushauri wa kisheria unaojibu kila swali lililowasilishwa. Bw Gachagua aliondolewa mamlakani Oktoba 2024. Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi yake Juni 2026, lakini amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa. Kiongozi huyo wa DCP ametangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi wa 2027. Bi Mwangaza naye aliondolewa kama Gavana wa Meru Agosti 2024 baada ya Bunge la Kaunti kupitisha hoja ya kumtimua na Seneti kuithibitisha. Mahakama Kuu ilikataa kesi yake Machi 2025, lakini amekata rufaa kupinga uamuzi huo. Anaongoza chama cha Umoja na Maendeleo (UMP) na analenga kuwania kiti cha ugavana tena. Bw Bundi aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Juu Aprili 2026, akitaka ufafanuzi kuhusu masharti ya Katiba yanayohusu masharti ya kugombea nyadhifa za kisiasa. Mahakama ilimwagiza kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu ndani ya siku 21. Bi Oduor alisema kesi hiyo haifai kuendelea kwa sababu inahusu maswali yenye msingi na huenda ikaathiri kesi za baadaye. “Afisi hii inaona kwamba kesi hii haikidhi masharti ya Katiba ya Mahakama ya Juu kutoa ushauri wa aina hii,” akasema. Hata hivyo, mawakili wa Bw Bundi wanasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu hakutimiza maagizo ya mahakama kwa sababu hakujibu maswali muhimu. Kwa sasa, Mahakama ya Juu bado haijatoa uamuzi kuhusu suala hilo. Hii inaacha swali la iwapo Gachagua na Mwangaza wanaweza kugombea uchaguzi wa 2027 likiwa halijajibiwa.

VUGUVUGU la Linda Mwananchi limetangaza mkakati wa kukabiliana na kile inachodai ni ongezeko la ghasia za kisiasa nchini. Mkakati huo unahusisha hatua kali za kisheria mahakamani, kushinikiza idara za usalama, uasi wa kiraia na kuhamasisha zaidi mashirika ya kiraia pamoja na vyombo vya habari. Kundi hilo limesema hatua hizo zitachukuliwa kufuatia vurugu zilizovuruga ziara yake katika Kaunti ya Homa Bay Jumapili iliyopita, ambapo watu walifariki dunia, makumi kujeruhiwa na mali kuharibiwa. Badala ya kujiondoa kwenye shughuli za kisiasa, viongozi wa Linda Mwananchi wanasema tukio la Homa Bay limeimarisha azma yao ya kupinga kile wanachokiita ghasia na vitisho vinavyofadhiliwa na serikali. Kundi hilo linasema kwa sasa litafuata njia za kisheria, lakini limeonya kuwa huenda likalazimika kutumia hatua za kiraia ikiwa serikali haitawawajibisha waliohusika na vurugu hizo. Gavana wa Siaya, James Orengo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa vuguvugu hilo, alisema Jumanne kuwa yuko tayari kukabiliana na kile alichokiita “ugaidi wa serikali” na akashutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kupanga mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa. “Tuko tayari. Niko tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayotokana na ghasia za serikali. Huu ni ugaidi wa serikali unaoendelezwa na Rais William Ruto na lazima awajibike,” alisema Bw Orengo nje ya makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika Barabara ya Kiambu, Nairobi. Alikuwa amemsindikiza Bw Oliver Jaoko, maarufu kama Olivetti, ambaye polisi wanamtafuta kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa katika mkutano wa Linda Mwananchi mjini Homa Bay. Bw Orengo pia alishutumu serikali kwa kuandaa mazingira ya kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, ingawaje hakutoa ushahidi wowote kuhusiana na madai hayo. “Rais Ruto anajaribu kutuandaa kuahirisha uchaguzi. Hilo halitawezekana,” alisema. Kundi hilo limetaja maeneo manne ya mkakati wake: mahakama, maandamano na uasi wa kiraia, kushinikiza polisi na vyombo vingine vya usalama, na kuhamasisha mashirika ya kiraia na wanahabari kufuatilia shughuli zake moja kwa moja. Njia ya kwanza ni kupitia mahakama. Katika taarifa yake ya Jumatatu, Linda Mwananchi lilisema litashinikiza uwajibikaji kupitia Katiba, mahakama na taasisi nyingine za kisheria. “Kila mhuni na afisa ambaye sura yake ilinaswa kwenye kamera akihusika katika vurugu hizi, alionekana na anatambulika,” kundi hilo lilisema. “Tutatumia Katiba, mahakama na taasisi zote za kisheria kuhakikisha kuna uwajibikaji.” Pia limetaka Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) zifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa maafisa wao wakati wa vurugu za Homa Bay. Linda Mwananchi linadai maafisa wa usalama walitazama tu huku wafuasi wake wakishambuliwa au walisaidia kuvuruga shughuli zake za kisiasa. Madai hayo hayajathibitishwa kwa njia huru na vyombo vya usalama bado havijayakubali hadharani. Kundi hilo linadai msafara wake ulikumbana na vizuizi vya barabarani tangu mpaka wa Kisumu na Homa Bay, na kuendelea kukabiliwa na vizuizi ndani ya kaunti hiyo. Linaongeza kuwa watu wenye silaha waliokuwa wamejipanga kando ya barabara walifyatulia risasi msafara huo. Moja ya madai makubwa zaidi yanahusu mtu aliyekamatwa na wafuasi wake Nyandiwa ambaye alidaiwa kujitambulisha kama afisa wa NIS. Kundi hilo linasema simu yake ilichukuliwa na baadaye watu waliojieleza kuwa maafisa wakuu wa polisi waliwasiliana wakitaka irejeshwe. Nguzo ya pili ya mkakati huo ni shinikizo la kisiasa kupitia maandamano na uwezekano wa uasi wa kiraia. Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi, alisema kundi hilo linaweza kuchukua hatua za kiraia iwapo Rais Ruto ataendelea kudumisha serikalini maafisa wanaotuhumiwa kupanga ghasia za kisiasa. “Tutarejea kwenye hatua za kiraia ikiwa Ruto ataendelea kuwaweka watu hawa serikalini,” alisema Seneta Osotsi. Nguzo ya tatu ni kishinikiza polisi moja kwa moja. Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, walimsindikiza Jaoko kwenda kujisalimisha kufuatia maslahi ya polisi katika uchunguzi wa vurugu hizo. Bw Owino alishutumu polisi kwa kushindwa kuchukua hatua wakati timu ya Linda Mwananchi ilishambuliwa Homa Bay, akisema walipaswa kurejesha utulivu na kulinda wananchi.

ALIYEKUWA Jaji Mkuu David Maraga amempa Rais William Ruto muda wa siku saba kuchapisha ripoti ya jopo la marekebisho ya polisi iliyowasilishwa kwake mnamo 2023, akionya kwamba asipofanya hivyo ataichapisha mwenyewe. Maraga, ambaye alikuwa mwenyekiti wa jopo hilo, alisema mojawapo ya mapendekezo makuu katika ripoti hiyo ilikuwa kurejesha uhuru wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) ili kuzuia kile alichokitaja kama kutekwa, kutumiwa vibaya na kuingiliwa kwa taasisi hiyo. “Kwa kuwa ripoti hii iliandaliwa kwa gharama ya umma na kwa mujibu wa Kifungu cha 35 cha Katiba, ninakutaka uichapishe mara moja na bila kuhaririwa ndani ya siku saba. Usipofanya hivyo, nitaitoa mimi mwenyewe,” alisema Maraga. Alisisitiza kuwa NPS ni huduma huru ya usalama wa taifa ambayo haipaswi kupewa maagizo na mtu yeyote, ikiwemo Rais, katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Hata hivyo, Maraga alisema hivi majuzi nchi imeshuhudia kile alichokiita “ghasia za kisiasa zilizopangwa, matumizi ya magenge ya wahuni na upendeleo wa polisi” katika maeneo ya Homa Bay, Keumbu na Ol Kalou, pamoja na matukio ya vurugu katika makanisa ya Kisumu, Nairobi na Witima. Homa Bay ilikumbwa na vurugu Jumapili wakati mkutano wa kisiasa wa Linda Mwananchi ulipovurugwa, ambapo watu wawili, akiwemo afisa wa polisi, waliuawa huku wengine 46 wakijeruhiwa. Kulingana na Maraga, matukio hayo yaliyotokea chini ya utawala wa Rais Ruto yanaashiria kurejea kwa siasa za ghasia na matumizi ya idara za usalama kuzima sauti za wanaopinga serikali. “Hii ni njia ambayo nchi iliwahi kupitia hapo awali kwa gharama kubwa. Haipaswi kuirudia tena,” alisema mgombea huyo wa urais wa chama cha United Green Movement (UGM), akihusisha hali hiyo na kile alichokiita “kutekwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi.”

FAMILIA ya marehemu Sharon Otieno imesema iko tayari kupatanishwa na familia ya aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado, licha ya maumivu makali waliyopitia tangu marehemu alipotekwa nyara, kubakwa na kuuawa mnamo Septemba 2018. Obado, aliyekuwa msaidizi wake wa kibinafsi Michael Oyamo na Caspal Obiero, walipatikana na hatia ya mauaji ya Sharon mnamo Julai 23, 2026. Katika taarifa ya athari kwa waathiriwa iliyowasilishwa mahakamani, wazazi wa Sharon walisema hawana chuki dhidi ya familia ya Obado na wanatumaini juhudi za maridhiano zitaendelea. Familia hiyo ilieleza kuwa mkutano wa maridhiano ulifanyika Agosti ukiongozwa na kaka yake Obado, Dominic Peter Akugo, pamoja na Daudi Okoth na Lenah Awino. Wazazi wa Sharon, Douglas Zacharia Otieno na Melinda Auma, walihudhuria pamoja na jamaa wengine wa familia. Familia ya Sharon pia ina matumaini kuwa Obado atatimiza ahadi aliyompa Sharon kabla ya kifo chake ya kumnunulia ardhi na kumjengea nyumba. Ripoti hiyo ilisema wawakilishi wa Obado walikubali kuwa ahadi hizo zilikuwepo na walijitolea kuhakikisha zitatimizwa kwa manufaa ya watoto watatu wa Sharon, ambao sasa wanalelewa na wazazi wake. Watoto hao wana umri wa miaka 12, 10 na minane. Familia ilisema kifo cha Sharon kilivunja matumaini yao kwani alikuwa nguzo ya mustakabali bora wa familia. Pia walieleza kuwa bado ni vigumu kuwaeleza watoto kilichompata mama yao. Sharon alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo akisomea stashahada ya rekodi za matibabu. Alikuwa na umri wa miaka 26 na alikuwa mjamzito wa wiki 28 alipopoteza maisha. Mahakama ilielezwa kuwa Sharon alikuwa amepokea vitisho vya kuuawa kabla ya kifo chake, hali iliyomlazimu hata kutorokea Tanzania kwa muda kabla ya kurejea nchini. Jaji Cecilia Githua aliamua kuwa upande wa mashtaka ulithibitisha kuwepo kwa njama iliyohusisha Obado, Oyamo na Obiero. Mahakama ilikubaliana kuwa ujauzito wa Sharon na uhusiano wake na Obado vilitishia hadhi ya kisiasa ya gavana huyo wa zamani. Hata hivyo, wazazi wa Sharon wanasema maridhiano hayawezi kufuta maumivu waliyonayo. Wanaendelea kuhitaji usaidizi wa kisaikolojia na kifedha huku wakiwalea watoto aliowaacha Sharon. Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 16 wakati Obado na washtakiwa wenzake watahukumiwa.

MAJAMBAZI wanaoshukiwa kuwa wanachama wa genge la watu sita walivamia nyumba ya aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Kukabiliana na Fujo (GSU), Ranson Lolmodooni, katika eneo la Kitengela Police Sacco Estate, Kaunti ya Kajiado, na kuiba kiasi kisichojulikana cha fedha taslimu. Kulingana na taarifa za polisi na mashahidi, washukiwa hao walijifanya waumini waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa maombi na kufanikiwa kuingia katika mtaa huo wa makazi ya kifahari mnamo Jumapili, Agosti 16. Mtaa huo unaoishi maafisa wa polisi wanaohudumu na waliostaafu, yanachukuliwa kuwa miongoni mwa maeneo yenye ulinzi mkali zaidi mjini Kitengela. Ripoti ya polisi inaonyesha kuwa wahalifu hao walitumia mashine za kukata, kuvunja na kuingia ndani ya nyumba ya Bw Lolmodooni, ambaye alistaafu wadhifa wa Kamanda wa GSU mnamo Juni mwaka huu baada ya kuhudumu kwa miaka miwili. Inadaiwa kuwa waliondoka na masanduku yaliyokuwa yamejaa fedha taslimu. Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo zilipatikana barabarani baada ya kuanguka walipokuwa wakiondoka. Majirani waliambia Taifa Leo kuwa noti za Sh1,000 zilionekana zimetapakaa kwenye Barabara ya 5 ndani ya mtaa huo. Pia walidai kuwa wahalifu waliwatupia walinzi na watu waliokuwa karibu noti za fedha walipokuwa wakitoroka. Katika ujumbe uliosambazwa kwenye kundi la WhatsApp la usalama katika mtaa huo, ilielezwa kuwa wanaume wanne wenye silaha na wanawake wawili waliingia kwa hila kabla ya kuvamia nyumba hiyo na kuiba fedha. Wahalifu hao walipokuwa wakijaribu kutoroka, mmoja wa walinzi alijaribu kuzuia gari lao katika lango kuu. Kamera za CCTV zilinasa wawili wa washukiwa wakimshambulia kwa ngumi, mateke na fimbo hadi wakamshinda na kufanikiwa kutoroka kuelekea Isinya. Baadaye, moja ya magari yaliyotumiwa na washukiwa lilipatikana mjini Isinya, kilomita 21 kutoka eneo la tukio. Polisi walipata nambari kadhaa za usajili wa magari, bastola inayodaiwa kumilikiwa na afisa huyo wa zamani wa polisi pamoja na fedha zaidi. Hata hivyo, Bw Lolmodooni alikanusha madai kuwa fedha ziliibwa nyumbani kwake. “Kwangu kulikuwa jaribio la wizi. Majirani waligundua kilichokuwa kinaendelea na kupiga kamsa. Hakuna fedha zilizoibwa. Sisi hatuweki fedha nyumbani. Huo ni uvumi tu,” alisema. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kajiado Alex Shikondi, alithibitisha kuwa uchunguzi unaendelea na hakuna mshukiwa aliyekuwa amekamatwa. Tukio hilo linajiri wakati Kitengela inakumbwa na ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama. Katika muda wa wiki mbili zilizopita, wanaume watatu wameuawa katika matukio tofauti huku wakazi wengi wakijeruhiwa na magenge ya wahalifu wanaoshambulia usiku.

RAIS William Ruto aliwahi kumtaja Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, kama mwanasiasa chipukizi ambaye angepewa malezi kuwania uongozi wa kitaifa. Katika mahojiano ya pamoja na wanahabari yaliyofanyika Sagana State Lodge mnamo Machi 31, 2025, Rais Ruto alimtaja Nyoro kama “kiongozi mzuri sana” na kufichua kuwa alikuwa akimlea kisiasa. “Ni kijana ninayemlea kisiasa. Kuna mambo siwezi kuyasema hapa. Ndindi Nyoro ni kiongozi na ni mmoja wa vijana ninaowakweza kisiasa,” alisema Rais Ruto wakati huo. Hata hivyo, chini ya miezi 18 baadaye, uhusiano huo wa kisiasa unaonekana kufikia kikomo baada ya Nyoro kujitenga rasmi na chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) na kutangaza kujiunga na upinzani. Mnamo Jumatatu usiku, mbunge huyo wa Kiharu alizindua rasmi chama kipya kiitwacho Peoples’ Party of Kenya (PPK) katika Hoteli ya Safari Park, Nairobi, na kutangaza kwamba, sasa atashirikiana na viongozi wa upinzani kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa na kiuchumi kwa Kenya. Tangazo hilo lilimaliza miezi ya uvumi kuhusu hatima yake kisiasa, lakini pia likaibua maswali makubwa kuhusu nia yake halisi ya kisiasa. Je, Nyoro anajenga vuguvugu huru la kisiasa lenye mtazamo wa kitaifa? Je, anajiandaa kuwania urais mwaka 2027? Au chama chake kipya ni sehemu ya mkakati wa kupunguza nguvu za upinzani na kugawanya kura za eneo la Mlima Kenya? Maswali hayo yamezua mijadala mikali miongoni mwa wachambuzi wa siasa. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Multimedia nchini Kenya, Profesa Gitile Naituli, anaamini hatua hiyo inaweza kumfaidi Rais Ruto kisiasa, hasa katika eneo la Mlima Kenya ambalo limezidi kuonyesha kutoridhishwa na serikali ya Kenya Kwanza. “Huu ni mpango wa Ruto,” alisema Profesa Naituli. Kwa mujibu wake, Mlima Kenya ni eneo muhimu kutokana na idadi kubwa ya wapigakura, na njia moja ya kudhoofisha upinzani dhidi ya Rais ni kugawanya viongozi wa kisiasa wa eneo hilo. “Lengo la Ruto ni Mlima Kenya, ambao una idadi kubwa zaidi ya wapigakura. Njia pekee ya kushinda bila uungwaji mkono wa eneo hilo ni kuligawanya kisiasa,” alisema. Hata hivyo, wafuasi wa Nyoro pamoja na baadhi ya wachambuzi wamekataa mtazamo huo wakisema viongozi wengi kutoka Mlima Kenya tayari wameonyesha nia ya kuwania urais bila kusawiriwa kuwa wanatekeleza ajenda ya Rais. Kwa sasa eneo hilo lina wanasiasa kadhaa wenye matarajio ya urais wakiwemo kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, Martha Karua wa PLP, Jimmy Wanjigi wa Safina, Justin Muturi wa Democratic Party na Peter Munya wa PNU. Mchambuzi mwingine wa kisiasa, Dismas Mokua, anasema si sahihi kukichukulia chama cha Nyoro kama mradi wa Ikulu. “Kenya ni nchi ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuanzisha chama, kuwania katika uchaguzi na kufuatilia ndoto zake za kisiasa,” alisema Mokua. Aliongeza kuwa hata kama Nyoro angekuwa anatekeleza ajenda ya mtu mwingine, Katiba bado inamruhusu kuongoza chama cha kisiasa na kuwania nafasi yoyote ya uongozi. Mokua alisema kuwabeza viongozi wanaoanzisha vyama vipya bila ushahidi ni aina ya siasa za upotoshaji. Aidha, alionya kuwa Wakenya hawapaswi kushangaa iwapo Rais Ruto atatumia mbinu mbalimbali za kisiasa kujinufaisha kabla ya uchaguzi wa 2027. “Hakuna viwango vya ubora katika siasa. Wagombeaji wa urais hutumia mbinu zote zinazoweza kuwasaidia kushinda uchaguzi,” alisema. Lakini Profesa Naituli anahisi Nyoro yuko katika hatari ya kuonekana kama sehemu ya mfumo wa utawala badala ya mwanasiasa huru. “Alikuwa kiongozi mchanga aliyekuwa akiibuka, lakini sasa ameanza kuvunja matumaini ya watu,” alisema. Kwa upande wake, Nyoro amesisitiza kuwa uamuzi wake hauna uhusiano na makubaliano yoyote ya siri na Ikulu bali umetokana na maslahi ya taifa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa PPK, alisema amekuwa akifanya mashauriano kwa miezi mingi na viongozi wa vyama mbalimbali kabla ya kuondoka UDA. “Moyo wangu umelemewa kwa miezi mingi. Nimekuwa nikiomba kwamba uamuzi wowote wa kisiasa nitakaochukua uwe na maslahi ya Wakenya mbele,” alisema. Alisisitiza kuwa alijitenga na serikali na chama tawala muda mrefu uliopita. “Ni wazi tuliondoka serikalini zamani. Kwa kumbukumbu sahihi, tulijitenga na UDA na serikali ya wilibaro kitambo sana. Kuanzia leo, Peoples’ Party of Kenya iko rasmi katika upinzani,” alisema. Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa kwa mwanasiasa ambaye hapo awali alikuwa miongoni mwa vijana waliotambulika zaidi ndani ya serikali ya Kenya Kwanza. Umaarufu wake uliongezeka kwa kasi kiasi cha kuwafanya wengi kumchukulia kama mmoja wa viongozi ambao wangemrithi Rais Ruto siku zijazo. Ingawa hakutangaza waziwazi kwamba atawania urais mwaka 2027, kauli zake zilionyesha kuwa anajitayarisha kwa wadhifa mkubwa zaidi nchini. Alifichua kuwa amefanya mashauriano ya kina na viongozi wa upinzani wakiwemo Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Peter Munya, James Orengo na Dkt Fred Matiang’i. Changamoto kubwa sasa kwa Nyoro, kwa mujibu wa wachambuzi, ni kuwashawishi Wakenya kuwa kuvunja kwake uhusiano na UDA ni jambo la kweli na si mbinu nyingine ya kisiasa.

… Restrict access to dangerous drugs, Abayomi tells Lagos pharmacistsBy Chioma Obinna The Pharmaceutical Society of Nigeria, PSN, Lagos State branch, has raised the alarm over a weakening drug regulatory system in the state, warning that shortage of pharmacists in key regulatory positions and the prolonged absence of a fully inaugurated Governing Council of the […]

… 2,300 dead as epidemic spreads across 55 health zones in DRC … Says outbreak moving at “unprecedented speed” .. Two new vaccines enter human trials as response races against time By Chioma Obinna The World Health Organisation (WHO) yesterday warned that the deadly Bundibugyo virus disease epidemic in the Democratic Republic of the Congo […]

By Steve Oko UMUAHIA — The family of detained leader of the Indigenous People of Biafra, IPOB, Mazi Nnamdi Kanu, has raised concerns over what it described as undue delay in the hearing of his pending cases, urging the Chief Justice of Nigeria, CJN, and the President of the Court of Appeal to urgently list […]

KIWANGO cha njaa duniani kimepungua kwa mwaka wa tatu mfululizo, lakini dunia bado i mbali kuwahi lengo la kutokomeza njaa ifikapo 2030, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa (UN) imefichua. Makala ya 2026 ya ripoti ya Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani, kwa Kiingereza ‘the State of Food Security and Nutrition in the World (SOFI)’ inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ilipungua kutoka asilimia 8.6 mwaka 2022 hadi asilimia 7.8 mwaka jana, 2025, punguo hilo likiwa sawa na karibu watu milioni 645 duniani. Hata hivyo, mafanikio hayo bado yako hatarini kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa bei ya chakula, migogoro katika nchi zinazounda malighafi ya mbolea na ukosefu wa usawa kiuchumi. Akizindua ripoti hiyo mwezi uliopita, Julai, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Dkt Qu Dongyu, alionya kuwa athari za tabianchi zinaweza kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana na kusababisha mamilioni ya watu kukabiliwa na ukosefu wa chakula. “Athari za mabadiliko ya tabianchi zisipodhibitiwa, zaidi ya watu milioni 500 duniani wanaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na njaa,” alisema Dkt Qu. Aidha, alizitaka nchi kuongeza uwekezaji katika mifumo ya chakula inayostahimili tabianchi, kuimarisha uzalishaji, kuboresha mitandao ya usambazaji na kufanya chakula kupatikana kwa bei nafuu. Ripoti hiyo ilitolewa kwa pamoja na FAO na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo IFAD, WFP, WHO na UNICEF. [caption id="attachment_191310" align="aligncenter" width="300"] Ukame unaendelea kushuhudiwa katika baadhi ya kaunti nchini. Picha|Sammy Waweru[/caption] Dkt Qu alisema ingawa kiwango cha njaa duniani kimepungua, Afrika bado inakabiliwa na baa la njaa. Ripoti inaonyesha kuwa watu milioni 309 barani Afrika wanakabiliwa na njaa, sawa na mtu mmoja kati ya kila Waafrika watano. Aidha, asilimia 66.6 ya Waafrika hawawezi kumudu lishe bora. Huku dunia ikiandikisha kupungua kwa njaa, Kenya inakabiliwa na tishio la uhaba wa chakula kutokana na taarifa za kukauka kwa mazao katika maeneo muhimu ya uzalishaji, hasa Bonde la Ufa. Wakulima wameelezea wasiwasi kuhusu mahindi kukaukia mashambani kutokana na kuchelewa kwa mvua na vipindi virefu vya ukame. Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kufuatia El Niño inayopaniwa kushuhudiwa Oktoba 2026, wakulima wakihofia mimea na mazao kidogo yaliyosalia shambani kusombwa na mafuriko. Athari za mabadiliko ya tabianchi haswa kiangazi na ukame zinatishia mavuno, usalama wa chakula na mapato ya wakulima wadogo wanaotegemea kilimo cha kutegemea mvua. Data kutoka AGRA pia inaonyesha kuwa shinikizo la tabianchi ni tishio kubwa kwa uzalishaji wa chakula barani Afrika. Mvua ya El Niño inayotarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa 2026 na mwanzoni mwa 2027, kilele chake wataalamu wa hali ya hewa wanaonya kitakuwa joto kali na ukame Afrika Mashariki na Kusini. FAO imezitaka nchi kuharakisha ukumbatiaji wa matumizi ya teknolojia zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi, kuboresha mifumo ya upatikanaji wa fedha, mbegu bora na mifumo ya umwagiliaji mimea na mashamba maji kwa kutumia mifereji (irrigation). “Ni muhimu serikali za nchi za Afrika zijiandae vilivyo ili kukabiliana na tabianchi,” akahimiza Dkt Qu. [caption id="attachment_191311" align="aligncenter" width="300"] Wataalamu wanahimiza wakulima kukumbatia teknolojia za kisasa kuzalisha chakula. Pichani, kabichi zilizokuzwa Isiolo ambayo ni kaunti kame. Picha|Sammy Waweru[/caption] Ripoti ya UN pia inaonyesha kuwa watu bilioni 2.7 hawakuweza kumudu lishe bora mwaka 2025, ingawa idadi hiyo ilipungua kutoka bilioni 3 mwaka 2021. Gharama ya lishe bora duniani imefikia dola za PPP 4.28 kwa mtu kwa siku, huku Afrika ikiwa dola 4.33. Bei ya juu ya matunda, mboga na vyakula vingine vyenye virutubisho inaendelea kuzuia familia nyingi kumudu mlo bora na kamilifu. Abdurakhmonov Ibrokhim Yulchievich, Waziri wa Kilimo wa Uzbekistan, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo alisema mageuzi katika kilimo yanahitaji matumizi ya teknolojia za kisasa na mifumo mipya ya ufadhili. “Teknolojia za akili bandia, ndiyo Artificial Intelligence (AI) zinaweza kusaidia kuunda hifadhi ya data za wakulima, kurahisisha upatikanaji wa mikopo na kupunguza hatari kwa taasisi za kifedha,” akasema Waziri Ibrokhim. FAO imesisitiza kuwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unahitajika, huku uwekezaji zaidi ukipaswa kuelekezwa katika teknolojia zinazolinda uzalishaji wa chakula na kusaidia wakulima kustahimili athari za tabianchi.

DODOMA; Serikali imewapa siku saba wamiliki wa viwanda vya kuzalisha saruji nchini kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto ya bei ya saruji inayotajwa kuwa juu katika soko pamoja na upatikanaji wake. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, kukutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa viwanda…

MWAKA mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027, Gavana wa Kericho Erick Mutai, ametangaza wazi mwisho wa ushirikiano wake wa kisiasa na Naibu Gavana Fred Kirui, akihitimisha uhusiano ambao umekuwa na misukosuko ya kisiasa na kiutawala kwa miaka minne iliyopita. Akizungumza katika wadi ya Chilchila, eneo bunge la Kipkelion West, Dkt Mutai alisema hadharani kuwa amempa Bw Kirui uhuru wa kutafuta mshirika mwingine wa kisiasa kuelekea uchaguzi ujao, iwe kama mgombea wa ugavana au mgombea mwenza. Gavana huyo alidai kuwa Naibu wake alihusika na majaribio yaliyotibuka ya kumng’atua madarakani. Alisema sasa ataungana kisiasa na aliyekuwa Mbunge wa Kipkelion, Bw Jackson Rop, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kaunti anayesimamia Fedha na Mipango ya Kiuchumi. “Uhusiano wetu wa kisiasa umefikia mwisho. Kuanzia sasa nitafanya kazi na Jackson Rop na nitatafuta muhula wa pili nikiwa na mgombea mwenza mpya,” alisema Dkt Mutai. Kwa upande wake, Mhandisi Kirui alimshutumu gavana kwa kumdhalilisha na kutomheshimu tangu walipochaguliwa mwaka 2022. Alisema hali hiyo imefanya ushirikiano wao usiwezekane. “Wananchi wa Kipkelion West wataamua mwelekeo wao wa kisiasa mwaka 2027 kutokana na namna ulivyonitendea licha ya kutupatia kura kwa wingi,” alisema Kirui. Mzozo kati ya viongozi hao unadaiwa kuchochewa na makubaliano ya kugawana madaraka kwa uwiano wa asilimia 60 kwa gavana na asilimia 40 kwa naibu wake, madai ambayo Dkt Mutai amekuwa akikanusha. Tofauti zilianza mara tu baada ya kuapishwa kwao wakati wa uteuzi wa Mawaziri wa Kaunti na maafisa wakuu, ambapo Kirui alidai hakushirikishwa. Huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, kinyang’anyiro cha ugavana Kericho kinaonekana kuwa na ushindani mkali, huku Charles Keter, Florence Bore na Spika wa Bunge la Kaunti Dkt Patrick Mutai wakitajwa miongoni mwa wanaotaka kuwania.

The Assembly also disclosed that no fewer than 38 houses were burnt during the attacks, while several hectares of farmlands, barns containing stored grains and other valuables were destroyed.

LUSAKA, Zambia: RAIS wa Zambia Hakainde Hichilema alishinda uchaguzi wa urais na kuwahi muhula wa pili wa miaka mitano, kulingana na matokeo ya Tume ya Uchaguzi ya Zambia. Uchaguzi huo uligubikwa na madai ya wizi wa kura na visa vya udanganyifu. Matokeo yaliyotangazwa mapema Jumanne yalionyesha Hichilema alipata asilimia 61.4 ya kura, dhidi ya asilimia 38 za mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile. “Kwa hivyo ninamtangaza Hichilema Hakainde kuwa Rais mteule wa Jamhuri ya Zambia leo Agosti 18, 2026,” akasema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mwangala Zaloumis. Uchaguzi huo ulikuwa wa saba kwa Hichilema kuwania urais, huku ukiwa wa kwanza kwa Mundubile. Baada ya ushindi wake kutangazwa, mamia ya wafuasi wake walijumuika Lusaka wakiwa wamevalia rangi nyekundu za chama chake cha United Party for National Development (UPND), wakishangilia, kuimba, kucheza na kulipua fataki. Hichilema, 64, alisema alikuwa nimeguswa sana na imani raia walimwekea ili aendelee kuongoza. Pia aliwatumia ujumbe waliomuunga mkono wapinzani wake akisema, “Tumewasikia, na tutaendelea kuwafanyia kazi.” Mundubile, kiongozi wa upinzani, hakutoa taarifa mara moja kuhusu matokeo hayo. Mvutano ulikuwa umeongezeka Zambia kuelekea uchaguzi huo wa Agosti 13, licha ya kampeni kuwa tulivu. Usiku wa uchaguzi, polisi waliwakamata watu 11, akiwemo viongozi wa upinzani, katika oparesheni iliyohusisha ufyatulianaji wa risasi. Mundubile alikuwa katika eneo hilo. Serikali ilisema operesheni hiyo ililenga “shughuli za wanamgambo”, huku waliokamatwa wakidaiwa kupatikana na silaha hatariChama cha Mundubile, National Reconciliation Party for Unity and Prosperity (NRPUP), kilipinga madai hayo, kikisema uvamizi huo ulifanyika nyumbani kwa kiongozi wao na kumuacha mbunge mmoja akiwa amejeruhiwa kwa risasi. Siku iliyofuata, Tume ya Uchaguzi ilisimamisha kwa saa kadhaa zoezi la kuhesabu kura kutokana na ripoti za vurugu dhidi ya maafisa wa uchaguzi na wizi wa karatasi za kura. Mundubile alisema alipokea taarifa kuhusu uwezekano wa kubadilishwa kwa fomu za matokeo kutoka vituoni na kutaka uchunguzi huru tena haraka. Kambi ya Hichilema ilikanusha madai hayo. Waangalizi wa kimataifa, akiwemo Umoja wa Ulaya, walisema uchaguzi ulikuwa wa amani kwa kiasi kikubwa, lakini wakaonya kuwa ulifanyika katika mazingira yaliyozima uhuru wa kimsingi. Kura milioni tano zilipigwa katika uchaguzi huo. Zambia, yenye wakazi milioni 22 na ikiwa mzalishaji wa pili kwa ukubwa wa shaba Afrika, ina historia ya mabadiliko ya uongozi kwa amani kupitia uchaguzi. Tangu mfumo wa vyama vingi kurejeshwa 1991, mabadiliko katika uchaguzi wa wanaoshikilia afisi za rais yamefanyika kupitia uchaguzi.

KILIMANJARO; Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhan Mahanyu, amewataka viongozi wa chama na serikali kuendelea kushirikiana na kujenga umoja badala ya kuweka mbele tofauti zao, akisema mshikamano wa viongozi ni muhimu katika kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi. Mahanyu amesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha…

ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua jana aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliothibitisha kuondolewa kwake mamlakani na Seneti mnamo 2024. Rufaa hiyo, yenye kurasa 121, inapinga uamuzi wa Juni 8, 2026 uliotolewa na Majaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Frida Mugambi. Miongoni mwa hoja kuu ni madai kwamba Mahakama Kuu “ilibadilisha uamuzi wa mwisho wa maandishi na kuufanya kutofautiana na uamuzi uliotolewa hadharani mahakamani.” Bw Gachagua anadai vifungu vinne vilivyosomwa baada ya aya za 484, 488, 503 na 508 viliondolewa katika uamuzi wa maandishi licha ya kusomwa hadharani na kupeperushwa moja kwa moja kwenye runinga. “Kwa kubadilisha uamuzi isivyofaa, mahakama imemnyima hoja nzito za mahakama zilizotolewa katika vifungu vilivyosomwa baada ya aya za 484, 488, 503 na 508,” akasema. Pia anapinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuunga mkono kuondolewa kwake licha ya majaji kubaini kuwa Seneti ilikiuka haki zake za kikatiba wakati wa mchakato huo. Majaji walibaini kuwa haki yake ya kusikilizwa na kuchukuliwa hatua za kiutawala ilikiukwa baada ya Seneti kukataa kuahirisha kikao alipougua na kushindwa kukamilisha utetezi wake. Bw Gachagua anasema ukiukaji huo ulipaswa kufanya uamuzi wa Seneti kuwa usiofaa. “Mahakama Kuu ilikosea kimsingi kisheria kwa kushindwa kubaini kwamba uamuzi wa Seneti wa kumuondoa mamlakani ulikuwa batili na usio na nguvu za kisheria,” akasema. Anapinga pia msimamo kwamba uamuzi wa Seneti kuhusu kutimuliwa kwake hauwezi kuchunguzwa na mahakama, akisema mahakama zinaweza kuingilia mchakato huo iwapo Katiba imekiukwa. Pia anasema mahakama ilikosea kuzingatia hoja ya uwezekano wa kuwepo kwa Naibu Rais wawili iwapo angewarejeshwa mamlakani, kwani alikuwa amebadilisha ombi lake na hakutaka kurudi ofisini bali alitaka kutimuliwa kwake kubatilishwe na apewe fidia. Pia anapinga mchakato wa Seneti, akisema uchunguzi ulikuwa wa lazima na kamati maalum ilipaswa kuundwa. Ushirikishaji wa umma ni hoja nyingine. Bw Gachagua anasema Seneti haikuwashirikisha wananchi baada ya kupokea ripoti ya Bunge la Kitaifa. Pia anapinga mchakato wa uteuzi na kuidhinishwa kwa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais. Zaidi ya hayo, anasema mahakama ilishindwa kuamua kuhusu haki yake ya kulipwa hela za kustaafu. Anapinga fidia ya Sh50 milioni, akisema haikutosha. Bw Gachagua anaiomba Mahakama ya Rufaa itangaze uamuzi wa Seneti wa Oktoba 17, 2024 kuwa kinyume cha Katiba, batili na usiokuwa na nguvu za kisheria.

KANUNI za kuimarisha nidhamu miongoni mwa walimu ni hatua inayofaa, hasa katika enzi hii ambapo mitandao ya kijamii imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Mwalimu si mfanyakazi wa kawaida. Yeye ni mlezi, mshauri na kioo cha jamii. Kwa hivyo, mwenendo wake shuleni na nje ya shule unaweza kuwa na athari kubwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Mitandao ya kijamii imeleta fursa kubwa za mawasiliano, kujifunza na kubadilishana mawazo. Lakini pia inaweza kuwa chanzo cha mienendo inayodhalilisha hadhi ya mwalimu. Lugha chafu, matusi, picha zisizofaa, ulevi wa kujionyesha hadharani na matusi dhidi ya watu wengine vinaweza kumfanya mwalimu apoteze heshima anayopaswa kuwa nayo mbele ya wanafunzi na wazazi. Mwalimu anayewafundisha wanafunzi kuhusu heshima, nidhamu na uwajibikaji hawezi kuhubiri maadili hayo darasani halafu akafanya kinyume chake kwenye mitandao. Hata hivyo, kanuni hizo hazipaswi kutumiwa kuwanyamazisha walimu au kuwanyima haki yao ya kutoa maoni. Mwalimu ni raia mwenye haki ya kujieleza. Kinachohitajika ni mipaka ya wazi kati ya uhuru wa kujieleza na tabia inayokiuka maadili ya taaluma. Walimu pia wanapaswa kuelewa kwamba kile wanachoweka mtandaoni kinaweza kubaki huko kwa muda mrefu. Chapisho moja la hasira au picha isiyofaa linaweza kusambaa kwa maelfu ya watu ndani ya dakika chache na hatimaye kuathiri heshima ya mwalimu, shule na hata taaluma nzima. Kwa upande mwingine, mamlaka zinazowasimamia walimu zinapaswa kuhakikisha kanuni hizo zinatumika kwa haki. Nidhamu haimaanishi adhabu kali pekee. Walimu wanahitaji pia kuelimishwa kuhusu matumizi salama na yenye uwajibikaji ya mitandao ya kijamii. Ni muhimu kuwe na mafunzo ya mara kwa mara kuhusu maadili ya taaluma katika mazingira ya kidijitali. Walimu wafundishwe namna ya kulinda faragha yao, wanafunzi na taasisi wanazofanyia kazi. Hatua hiyo ni muhimu kwa sababu jamii inawatazama walimu kama vielelezo. Watoto hujifunza si kutokana na vitabu na masomo pekee, bali pia kutokana na tabia za watu wanaowaongoza. Mwalimu ni kioo cha jamii. Kioo hicho kinapaswa kuonyesha maadili tunayotarajia watoto wetu kuiga.

IRINGA: Mikopo inayotolewa na Serikali kwa watu wenye ulemavu imeanza kubadili maisha ya baadhi ya wanufaika mkoani Iringa, huku baadhi yao wakifanikiwa kuanzisha biashara, kuongeza kipato na kutoa ajira kwa wengine. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, alipofanya ziara mkoani Iringa kwa ajili ya…

DAR ES SALAAM; KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Tausi Kida amewataka wavumbuzi, watafiti, wajasiriamali na wadau wa maendeleo kuchunguza namna mawazo mapya, teknolojia, utafiti, ujasiriamali, fedha na ushirikiano wa kimkakati vinavyoweza kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili kuharakisha maendeleo jumuishi…

MTWARA: Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba nchini (TANCCOOPS) umeipongeza Kamati ya Pamoja ya Vyama Vikuu vya Ushirika vya Korosho nchini (KCJE) kwa faida mbalimbali zinazopatikana kwa wakulima wa zao la korosho kupitia mradi huo, ikiwemo upatikanaji wa pembejeo kwa wakati. Hayo yamejiri leo, Agosti 18, 2026, wakati wanachama wa TANCCOOPS…

DAR ES SALAAM: Wanawake vijana 50 wanatarajia kujengewa uwezo na kukuzwa kiuchumi kupitia sekta ya urembo inayokua kwa kasi nchini Tanzania. Hatua hiyo iMetangazwa leo na Shirika la Her Initiative kupitia mpango wao wa Panda Academy 2026. Kupitia programu hiyo, wahitimu wamepata mafunzo ya vitendo pamoja na ujuzi wa ujasiriamali na uongozi unaohitajika kuanzisha na…

WAFANYAKAZI saba raia wa Amerika kutoka Shirika la misaada la Samaritan’s Purse wameachiliwa kutoka kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola cha Laikipia Air Base baada ya kukamilisha siku 21 za karantini. Walikuwa chini ya uangalizi kama tahadhari walipokuwa wakisaidia shughuli za kukabili visa vya dharura katika eneo hilo. Mkurugenzi wa Samaritan’s Purse Kenya, Alex Kuria, alisema wote hawakuonyesha dalili zozote za Ebola na sasa wamerejea nyumbani. “Watu hao wameondoka na kurejea nyumbani. Wamekuwa nyumbani kwa wiki mbili sasa wala hawakuonyesha dalili zozote. Walikuwa salama na hakuna wengine wapya waliofika,” akasema. Wafanyakazi hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Amerika cha kukabiliana na majanga na waliishi katika mahema maalumu ya kijeshi kwenye kituo hicho. Kuachiliwa kwao kunafanyika wakati Kenya ikiimarisha maandalizi kukabili mkurupuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na maeneo ya jirani. Kenya bado haijathibitisha kisa chochote cha Ebola. Hadi sasa, wasafiri 413,017 wamepimwa katika vituo vya kuingia nchini, huku sampuli zote 196 zilizochunguzwa zikiwa hazina virusi. Wizara ya Afya imezindua maabara tano za Ebola, zikiwemo mbili katika vituo vya mpakani vya Busia na Lwakhakha. Pia kuna sehemu za kuwatenga wagonjwa ambazo zimeandaliwa katika hospitali kadhaa, zikiwemo Hospitali ya Kenyatta, Hospitali ya Police, ile ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi na Port Reitz. Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt Patrick Amoth, amesema Ebola bado ni tishio kwa Kenya kutokana na nafasi yake kama kitovu cha usafiri kwenye ukanda huu. “Ebola bado ni tatizo la afya ya umma. Hali nchini Congo bado ni mbaya japo Uganda imefanikiwa kudhibiti mkurupuko, lakini kwa sababu sisi ni kitovu cha usafiri kati yetu, DRC na eneo hili, tumeweka mifumo ya kukabiliana na mkurupuko iwapo utafika nchini,” akasema. Alisema Kenya imechunguza zaidi ya watu 183 na wote walipatikana bila virusi. Dkt Amoth alisema kiwango cha maandalizi ya Kenya kimeongezeka kutoka asilimia 66 hadi 88 kulingana na tathmini ya Shirika la Afya Duniani (WHO). “Tunataka kuwahakikishia Wakenya kwamba tumeweka mifumo inayohitajika kuzuia, kugundua na kukabiliana ipasavyo na ugonjwa huu,” akasema. Hata hivyo, ripoti ilionyesha kuwa vituo 23 vya afya katika kaunti zilizo hatarini vinahitaji kuboreshwa ili kufikia viwango vya WHO. Kufikia Agosti 12, jumla ya visa 4,665 vya Ebola vilikuwa vimethibitishwa DRC, Uganda na Ufaransa, huku watu 2,184 wakifariki, kulingana na Kituo cha Kudhibiti magonjwa ya Kuambukizana (CDC) Amerika.