ESTHER Ngina ni mwasisi wa Taste Kenya Exporters, kampuni inayouza mimea asilia ng’ambo ambaye hadithi yake inatia motisha – hakuna lisilowezekana kupitia bidii.
Aliingilia biashara ya uuzaji wa mimea ya kiasili, ndiyo herbs kwa Kiingereza, baada ya kuhudumu katika sekta ya maua.
Licha ya kuwa na Stashahada ya Usimamizi wa Masoko, safari ya Esther haikuanza kwa urahisi.
Wakati mmoja – akiwa katika shule ya upili, anafichua kwamba alifanya kazi kama yaya ili kugharamia karo yake.
Hata baada ya kuandika Mtihani wa Kitaifa Kidato cha Nne (KCSE), aliendelea na kazi hiyo hadi akafanikiwa kukusanya hela kuondoa malimbikizo ya karo ili aweze kujiunga na taasisi ya juu ya masomo.
[caption id="attachment_173828" align="aligncenter" width="300"] Esther Ngina akiwa shambani mwake Kajiado, ambako hupanda mseto wa mimea asilia (herbs). Picha|Sammy Waweru[/caption]
“Mwajiri wangu, alijitolea kunisomesha nikapata Stashahada,” anasema.
Baada ya kuhitimu, Esther anadokeza kwamba alipata nafasi ya kazi katika kampuni ya kuuza maua nje ya nchi. Mwanya huo, ulimfumbua macho.
Alikuwa akisafiri na bosi wake nchi mbalimbali, na anasema safari ya kufikia alipo sasa ilishawishiwa na wateja aliokutana nao.
“Kampuni niliyofanyia kazi ilijishirikisha na uuzaji wa maua, na wateja wengi walikuwa wakiulizia mimea asilia kama vile mint na rosemary,” Esther anaelezea.
Swali hilo lilimpa wazo la uwekezaji.
Mwaka 2012, licha ya changamoto za kifamilia ikiwemo kupoteza mama yake, Esther alikata kauli ya kuacha kazi na kufukuzana na wazo jipya alililopata.
Anadokeza kuwa maamuzi hayo aliyafanya akiwa na miaka 30, umri ambao kwa wengi ni muhimu sana kujituma kusaka mianya tele ya ufanisi kupitia ajira.
[caption id="attachment_173829" align="aligncenter" width="300"] Esther Ngina wakati mmoja aliwahi kuhudumu kama yaya. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Hata hivyo, kwake hilo halikuwa hoja. Aliamua – na liwe liwalo, ataingilia biashara angaa naye pia awe mwajiri.
Mtaji, haukuwa kikwazo vile kwani alikuwa amejiunga na chama cha ushirika kuweka akiba.
“Nilichukua mkopo wa Sh1.2 milioni,” Esther anasema.
“Nilianza kwa kushirikiana na marafiki wachache kusafirisha bidhaa kama vile French beans na snow peas ng’ambo,” anaongeza.
Baadaye, walijumuisha mimea ya kiasili kama coriander, thyme, na dill.
Changamoto hazikukosekana. Kukosa mtaji wa kutosha kupanua biashara na ujuzi wa usimamizi kulimlazimu kuuza asilimia 25 ya hisa za biashara yake ili kujisimamia.
Akiendelea tu kuboresha biashara, Esther anafichua kwamba aliwahi pia kupoteza shamba la ekari 10 – la kukodi lililokuwa na vivungulio 31, eneo maalum la kupakia mazao na ofisi, kutokana na mmiliki aliyetamatisha makubaliano ya kandarasi kabla muda kukamilika. Hakukata tamaa.
[caption id="attachment_173830" align="aligncenter" width="300"] Mkulima Esther Ngina akielezea kuhusu kilimo cha rosemary. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Alianzisha kampuni tanzu kama Herbspice Market Link Ltd, inayoshughulika na wakulima wa mashamba madogo wanaomsambazia mazao kusafirisha ng’ambo, na Makena Paradise Herbs Ltd inayolenga kuongeza bidhaa thamani, iliyopewa jina la binti yake.
Mengine yamekuwa historia, Taste Kenya Exporters sasa ikiwa kati ya kampuni zinazoletea Kenya mapato kupitia uuzaji wa bidhaa za shambani ughaibuni.
Katika shamba lake la robo ekari lililoko Enkasiti, Kajiado, ana kivungulio cha kuoteshea miche ya mimea asilia kama rosemary na oregano.
Akiwa na leseni kutoka kwa taasisi ya Mbegu na Ustawishaji wa Mimea Nchini (Kephis) mjasiriamali mali huyu huagiza mbegu kutoka Uhispania, Italia, na Uingereza.
“Huotesha miche mara mbili kwa mwezi, na ninakadiria kuzalisha zaidi ya miche 200,000 ninayouza kati ya Sh2 hadi Sh8 kila mche,” akaambia Akilimali wakati wa mahojiano.
[caption id="attachment_173831" align="aligncenter" width="300"] Esther Ngina amekumbatia mfumo wa mifereji kunyunyizia mimea maji shambani ili kuhakikisha ana mazao mfululizo. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Ni hatua anayosifia kuokoa wakuzaji wa mimea asilia, ikizingangatiwa kuwa mbegu zake ni bei ghali.
Aidha, Esther anashirikiana na wakulima wapatao 400 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kama vile Nairobi, Machakos, Laikipia na Kajiado.
Huwasambazia miche na pia kuwasaidia kuuza mazao masoko ya ng’ambo.
Taste Kenya Exporters inalenga masoko ya Ulaya – nchi kama Uholanzi na Ujerumani, pamoja na mataifa ya Milki za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia.
“Kwa wasio na kampuni, huwauzia moja kwa moja kupitia kampuni yangu ambayo ina kibali na wenye kampuni ila hawaelewi taratibu huwasaidia kimikakati,” anasema.
Kwa sasa, mama huyu wa watoto wawili ameajiri wafanyakazi 20, akiwemo mtaalamu wa masuala ya kilimo, na anaendelea kupanua uwekezaji wake, akihimiza vijana kuwekeza muda na maarifa yao katika ujasiriamali.
[caption id="attachment_173832" align="aligncenter" width="300"] Kando na kuzalisha mimea asilia, Esther Ngina pia huiongeza thamani ili kuwahi soko bora. Picha|Sammy Waweru[/caption]
‘Yaya’ anayemiliki kiwanda cha kuuza mimea asili ng’ambo
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]