MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni.
Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika.
Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani.
Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation.
Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa.
Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde.
Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika.
Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo.
Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza.
Kampuni za China baadaye zilijiondoa.
Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja.
Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo.
Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji.
Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato.
Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii.
Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale.
Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
Kampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…
NewsTAHARIRI: Wakulima walipwe kama Rais alivyoahidi kwenye hotuba
TANGAZO la Rais William Ruto kuhusu malipo ya Sh15.07 bilioni kwa wakulima 680,000 wa kahawa na bonasi ya Sh1.2 bilioni kwa wakulima wa miwa ni hatua inayostahili kupongezwa. Kiongozi wa nchi jana alitangaza malipo hayo alipotoa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge ambapo pia alizungumzia mafanikio mengine ya serikali yake. Rais alisema bei ya kahawa imeongezeka kutoka Sh69 hadi Sh130 kwa kilo, huku mapato ya kitaifa kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi yakiongezeka maradufu kutoka Sh26 bilioni hadi Sh52 bilioni. Aidha, wakulima wa miwa wanatarajiwa kupokea bonasi ya Sh1.2 bilioni kuanzia wiki ijayo. Hizi ni habari njema kwa wakulima ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakikabiliwa na gharama kubwa za uzalishaji, bei duni za mazao, madeni na mifumo ya ushirika isiyowajibika. Wakulima wa kahawa, hasa, wamevumilia misimu ya mavuno duni, ucheleweshaji wa malipo na changamoto za magonjwa pamoja na hali mbaya ya hali ya hewa. Kuongezeka kwa bei ya kahawa na mapato ya mauzo ya nje kunaashiria kuwa mageuzi katika sekta hiyo yameanza kuzaa matunda. Takwimu zinaonyesha uzalishaji wa kahawa uliongezeka kutoka tani 49,500 mnamo 2024 hadi tani 51,400 mnamo 2025. Hata hivyo, ongezeko hili bado halitoshi kuifanya sekta hiyo kuwa na nguvu ikilinganishwa na uwezo wake wa kihistoria. Serikali inapaswa kuhakikisha fedha zilizotangazwa zinawafikia wakulima wanaostahili bila kucheleweshwa, mapendeleo au mianya ya ufisadi. Malipo ya moja kwa moja, mifumo ya uwazi na ukaguzi wa mara kwa mara wa vyama vya ushirika ni muhimu ili mkulima apate faida ya jasho lake. Vilevile, bonasi ya wakulima wa miwa haipaswi kuwa tukio la mara moja linalotolewa wakati wa hotuba za kisiasa. Serikali pia inapaswa kuwekeza zaidi katika utafiti wa kilimo, mbegu bora, mbolea nafuu, kilimo cha unyunyuziaji mashamba maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kuongezeka kwa uzalishaji pekee hakutasaidia ikiwa gharama za pembejeo zitameza mapato ya mkulima. Kilimo ndicho uti wa mgongo wa uchumi na chanzo kikuu cha ajira na riziki kwa mamilioni ya Wakenya. Kukiimarisha si suala la kutoa fedha pekee, bali kujenga mazingira ambayo mkulima anaweza kupanga maisha yake, kuwekeza na kupata faida bila kutegemea misaada ya mara kwa mara. Mkulima anahitaji zaidi ya bonasi, anahitaji soko la uhakika, bei inayomfaa, huduma bora na sera zinazomweka katikati ya maendeleo ya taifa.