Video
WATU WAWILI WAFARIKI AJALI YA LORI TABORA
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
#HABARI: Watu wawili wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.127 AUP/T.708 AFL mali ya kampuni ya Nyanza Bottles, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mayombo wilayani Uyui mkoani Tabora. Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba na dakika 28 usiku wa kuamkia leo wakati lori hilo likisafirisha vinywaji baridi kutoka Mwanza kwenda Tabora. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mayombo, Dina Masalu, ajali hiyo ilisababisha taharuki kwa wakazi wa eneo hilo ambapo dereva wa lori hilo, Donald Mashauri (25), alifariki dunia papo hapo. Msaidizi wa dereva huyo alifariki dunia baadaye wakati wa juhudi za uokoaji zilizokuwa zikitekelezwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. RADIO ZETU KWENYE VING’AMUZI: Radio One: Azam 061, Digitek 110, Capital Radio: Azam 383, Digitek 112, Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Mix by Yas, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania @itv2tanzania
Related stories
NewsMoses Wetang’ula to release CCTV footage capturing MP pocketing colleague's phone
Wetang'ula will submit CCTV footage of a male MP taking colleague's phone to the Powers and Privileges Committee, then recuse himself from its review.
NewsRAIS SAMIA AWAAPISHA MABALOZI IKULU - ATOA MAAGIZO MAKALI KUZINGATIA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI...
RAIS SAMIA AWAAPISHA MABALOZI IKULU - ATOA MAAGIZO MAKALI KUZINGATIA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI... Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha mabalozi na wakuu…
News2027: Tinubu has fulfilled promise made to Igbo after civil war – Kalu
Deputy Speaker of the House of Representatives, Hon. Benjamin Kalu, has said that President Bola Tinubu has fulfilled the promise made to the Igbo after the civil war in 1970.
NewsMiddle Belt Forum condemns renewed killings, abductions
…Urges governments to rescue abductees, protect communities and prosecute perpetrators By Henry Umoru ABUJA — The Middle Belt Forum (MBF) has condemned renewed attacks, killings, abductions and destruction of property in parts of Plateau, Niger, Benue, Kaduna and Borno states, calling on the Federal Government and security agencies to intensify efforts to protect vulnerable communities. […]