WATAALAM wa afya wameitaka Wizara ya Afya kuharakisha msako wa watu 15 ambao hawajapatikana, licha ya kuwa miongoni mwa watu 128 waliotangamana na mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Kenya.
Wizara ilisema kufikia Oktoba 13, watu 113 walikuwa wamepatikana, wakiwemo 108 waliowekwa karantini nchini Kenya na wengine watano walio nje ya nchi. Haijafichua waliko watu 15 ambao hawajapatikana.
Wasiwasi huo umeongezeka baada ya Kenya kuthibitisha kisa cha pili cha Ebola Oktoba 14. Mgonjwa huyo, mwanamume wa miaka 39 na jamaa wa karibu wa mgonjwa wa kwanza aliyefariki, alianza kuonyesha dalili akiwa karantini.
Mtaalamu wa magonjwa na mtafiti wa afya ya umma Dkt Ahmed Kalebi alisema kuwapata watu hao ni kipaumbele cha dharura ili kuzuia maambukizi zaidi.
Alionya kuwa ikiwa bado wako miongoni mwa wananchi, wanaweza kuwaweka wengine hatarini. Alisema kila mtu aliyekutana na wagonjwa hao anapaswa kufuatiliwa kwa siku 21.
Profesa Shem Otoi, mtaalamu wa hali ya kuenea kwa magonjwa katika Chuo Kikuu cha Daystar, alisema kisa cha pili kinaonyesha kuwa huenda maambukizi yamevuka kutoka kwa mgonjwa wa kwanza hadi kwa mtu mwingine.
Alitaka watu hao 15 wapatiwe tathmini ya hatari na kuwekwa karantini inapohitajika.
Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt Patrick Amoth alisema timu za afya zinawachunguza watu walioweza kukutana na mgonjwa wa pili, wakiwemo wahudumu wa afya na wafanyakazi wa karantini.
Wataalamu pia wametaka wizara itoe taarifa kila siku kuhusu watu walio karantini, waliopimwa, waliopata dalili na waliomaliza ufuatiliaji.
Dkt Kalebi alisema kimya cha serikali kinaweza kuchochea uvumi na kupunguza imani ya wananchi.
Profesa Omu Anzala, mtaalamu wa virusi na mwanachama wa jopokazi ya kitaifa kuhusu Ebola, alisema wananchi wanahitaji kuhakikishiwa kila siku ili wasiwe na hofu.
Wataalamu hao pia walisisitiza kufuatwa kikamilifu kwa taratibu za mazishi ya wanaofariki kutokana na Ebola, wakionya kuwa mazishi yanaweza kusababisha maambukizi mengi ikiwa tahadhari hazitazingatiwa.
Wizara imesema kwa sasa hakuna ushahidi wa maambukizi yaliyoenea katika jamii na Kenya inaendelea kuruhusu safari, biashara na mikusanyiko ya umma.
Watu 15 wanaohusishwa na Ebola hawajapatikana, wataalam wataka watafutwe upesi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…