GAVANA wa Kirinyaga, Anne Waiguru, Alhamisi alitangaza kwamba hatastaafu siasa hata baada ya kukamilisha mihula yake miwili ya uongozi.
Waiguru kwa sasa anahudumu katika muhula wake wa pili na wa mwisho kama gavana.
“Siendi popote, bado nitakuwa kwenye siasa,” alisema.
Bi Waiguru alidokeza kuwa analenga wadhifa wa juu zaidi baada ya kumaliza muda wake kama Gavana.
Wakati huo huo, Gavana alithibitisha kujitolea kwake katika kutengeneza sera faafu kwa biashara ili kuvutia uwekezaji zaidi wa viwanda katika kaunti hiyo.
Alisema kuwa Kaunti hiyo imepiga hatua kubwa kuelekea mageuzi ya kiuchumi huku viwanda vya kuongeza thamani ya mazao vikifunguliwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kiwanda cha kusaga unga cha Nice Extra Premium Flour Milling cha thamani ya mamilioni ya pesa huko Ngurubani, Waiguru alisema serikali yake imeunda mazingira bora kwa biashara kustawi.
“Kirinyaga ni eneo mpya la uwekezaji kutokana na mazingira tuliyoyaweka. Huna haja ya kumjua mtu yeyote ili uweze kuanzisha biashara Kirinyaga,” alisema Waiguru.
Aliongeza kuwa mbali na kuwekeza katika miundombinu bora, kisasa na sera bora kwa biashara, upatikanaji wa malighafi kwa uzalishaji unawavutia wawekezaji kuja Kirinyaga.
Waiguru: Sitastaafu hata muhula wangu ukiisha
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]