HUDUMA katika kaunti zote 47 huenda zikavurugika baada ya chama cha wafanyakazi wa serikali za kaunti (COGWU) kutishia kuchukua hatua kupinga mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) ya kudhibiti nyongeza za mishahara.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Roba Duba, alisema mapendekezo ya tume inayoongozwa na Mary Chebukati yatawaathiri wafanyakazi kwa kusababisha kupunguzwa kwa mishahara, kusimamishwa kwa ajira mpya na kuongezeka kwa changamoto kazini.
Pendekezo hilo limezua mvutano wakati serikali za kaunti zinakabiliwa na shinikizo la kulipa mishahara na kugharamia huduma muhimu kwa wananchi.
“Pendekezo la kuwafuta wafanyakazi, kusimamisha ajira na kuweka masharti makali ya kifedha kwa kisingizio cha kudhibiti matumizi ya mishahara ni uchokozi wa moja kwa moja na tangazo lisilo la kikatiba la vita dhidi ya msingi wa ugatuzi,” alisema Duba katika taarifa.
Chama hicho kilionya kuwa hakitakubali hatua zozote zitakazohatarisha ajira na maisha ya wafanyakazi wa kaunti, kikisema maamuzi yanayowahusu lazima yazingatie sheria.
“Ugatuzi hauwezi kujengwa kwa kuharibu maisha ya wafanyakazi,” kilisema chama hicho.
Mvutano huo umeibuka wiki moja baada ya CRA kukutana na Baraza la Magavana (COG), ambapo magavana walikataa pendekezo la Sh440.8 bilioni kama mgao wa mapato kwa kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2027/28.
Magavana walitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao huo kwa Sh100 bilioni, wakisema fedha zaidi zinahitajika ili kaunti ziweze kutekeleza majukumu yake.
Katika mkutano huo, CRA iliwataka magavana kuzingatia kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kudhibiti matumizi ya mishahara yanayozidi uwezo wa baadhi ya kaunti. Baadhi ya serikali za kaunti zimekuwa zikikopa fedha za muda mfupi ili kulipa mishahara ya kila mwezi.
Hata hivyo, COGWU ilisema CRA haina mamlaka ya kikatiba kusimamia wafanyakazi wa kaunti, kuamua masharti ya ajira au kuelekeza kufutwa kwa wafanyakazi.
Duba alitaja Kifungu cha 216 cha Katiba ya Kenya, akisema jukumu la CRA ni kutoa mapendekezo kuhusu ugavi wa mapato kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti, pamoja na mgao kati ya kaunti zenyewe.
Alisema mamlaka ya kuajiri, kuadhibu na kusimamia wafanyakazi yako chini ya Bodi za Utumishi wa Umma za Kaunti (CPSBs).
“CRA haina mamlaka ya kisheria ya kupuuza bodi hizi au kuingilia majukumu yake ya kusimamia ajira,” alisema.
Chama hicho pia kilitaja Kifungu cha 6(2) cha Katiba, kinachotambua serikali za kitaifa na za kaunti kuwa tofauti lakini zinazotegemeana.
Duba alionya kuwa chama kitapinga hatua yoyote itakayotekelezwa na CRA au serikali za kaunti ikiwa itahatarisha ajira za wanachama wake.
Aliitaka tume hiyo kuondoa mapendekezo hayo na badala yake kutafuta njia za kuhakikisha kaunti zinapata fedha za kutosha kutekeleza huduma na kuwalipa wafanyakazi mishahara inayostahili.
“Wanachama wetu wawe tayari kutetea ajira zao, familia zao na haki zao za kikatiba,” alisema.
Kwa sasa, tishio la chama hicho linaongeza presha kwa serikali za kaunti, ambazo zinapaswa kusawazisha matumizi ya mishahara na mahitaji ya wananchi ya huduma bora za afya, barabara na huduma nyingine za umma.
Wafanyakazi wa kaunti zote 47 watishia kugoma
HUDUMA katika kaunti zote 47 huenda zikavurugika baada ya chama cha wafanyakazi wa serikali za kaunti (COGWU) kutishia kuchukua hatua kupinga mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) ya kudhibiti nyongeza za mishahara. Katibu Mkuu wa chama hicho, Roba Duba, alisema mapendekezo ya tume inayoongozwa na Mary Chebukati yatawaathiri wafanyakazi kwa kusababisha kupunguzwa kwa mishahara, kusimamishwa kwa ajira mpya na kuongezeka kwa changamoto kazini. Pendekezo hilo limezua mvutano wakati serikali za kaunti zinakabiliwa na shinikizo la kulipa mishahara na kugharamia huduma muhimu kwa wananchi. “Pendekezo la kuwafuta wafanyakazi, kusimamisha ajira na kuweka masharti makali ya kifedha kwa kisingizio cha kudhibiti matumizi ya mishahara ni uchokozi wa moja kwa moja na tangazo lisilo la kikatiba la vita dhidi ya msingi wa ugatuzi,” alisema Duba katika taarifa. Chama hicho kilionya kuwa hakitakubali hatua zozote zitakazohatarisha ajira na maisha ya wafanyakazi wa kaunti, kikisema maamuzi yanayowahusu lazima yazingatie sheria. “Ugatuzi hauwezi kujengwa kwa kuharibu maisha ya wafanyakazi,” kilisema chama hicho. Mvutano huo umeibuka wiki moja baada ya CRA kukutana na Baraza la Magavana (COG), ambapo magavana walikataa pendekezo la Sh440.8 bilioni kama mgao wa mapato kwa kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2027/28. Magavana walitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao huo kwa Sh100 bilioni, wakisema fedha zaidi zinahitajika ili kaunti ziweze kutekeleza majukumu yake. Katika mkutano huo, CRA iliwataka magavana kuzingatia kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kudhibiti matumizi ya mishahara yanayozidi uwezo wa baadhi ya kaunti. Baadhi ya serikali za kaunti zimekuwa zikikopa fedha za muda mfupi ili kulipa mishahara ya kila mwezi. Hata hivyo, COGWU ilisema CRA haina mamlaka ya kikatiba kusimamia wafanyakazi wa kaunti, kuamua masharti ya ajira au kuelekeza kufutwa kwa wafanyakazi. Duba alitaja Kifungu cha 216 cha Katiba ya Kenya, akisema jukumu la CRA ni kutoa mapendekezo kuhusu ugavi wa mapato kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti, pamoja na mgao kati ya kaunti zenyewe. Alisema mamlaka ya kuajiri, kuadhibu na kusimamia wafanyakazi yako chini ya Bodi za Utumishi wa Umma za Kaunti (CPSBs). “CRA haina mamlaka ya kisheria ya kupuuza bodi hizi au kuingilia majukumu yake ya kusimamia ajira,” alisema. Chama hicho pia kilitaja Kifungu cha 6(2) cha Katiba, kinachotambua serikali za kitaifa na za kaunti kuwa tofauti lakini zinazotegemeana. Duba alionya kuwa chama kitapinga hatua yoyote itakayotekelezwa na CRA au serikali za kaunti ikiwa itahatarisha ajira za wanachama wake. Aliitaka tume hiyo kuondoa mapendekezo hayo na badala yake kutafuta njia za kuhakikisha kaunti zinapata fedha za kutosha kutekeleza huduma na kuwalipa wafanyakazi mishahara inayostahili. “Wanachama wetu wawe tayari kutetea ajira zao, familia zao na haki zao za kikatiba,” alisema. Kwa sasa, tishio la chama hicho linaongeza presha kwa serikali za kaunti, ambazo zinapaswa kusawazisha matumizi ya mishahara na mahitaji ya wananchi ya huduma bora za afya, barabara na huduma nyingine za umma.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…