Wabunifu wa mitindo ya mavazi wahudhuria hafla ya Siku ya Shampeni
WAUNDAJI na Wabunifu wa mitindo ya mavazi mbalimbali nchini wamehudhuria na kushehekea hafla ya Siku ya Shampeni iliyoandaliwa na kuadhimishwa na Moët & Chandon na kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency. Shabaha kuu ya hafla hiyo ililenga kusherehekea “Ubunifu usio na mwisho katika ufundi” ambao uliweza kuwaleta pamoja wabunifu, waundaji na watengenezaji wa mitindo ya […]
The post Wabunifu wa mitindo ya mavazi wahudhuria hafla ya Siku ya Shampeni first appeared on Millard Ayo.
WAUNDAJI na Wabunifu wa mitindo ya mavazi mbalimbali nchini wamehudhuria na kushehekea hafla ya Siku ya Shampeni iliyoandaliwa na kuadhimishwa na Moët & Chandon na kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency.
Shabaha kuu ya hafla hiyo ililenga kusherehekea “Ubunifu usio na mwisho katika ufundi” ambao uliweza kuwaleta pamoja wabunifu, waundaji na watengenezaji wa mitindo ya mavazi.
Miongoni mwa wabunifu na waundaji wa mitindo ya mavazi waliohudhuria ni Juma Jux, Ommy Dimpoz, Mtani Bespoke, Kiki Fashion, Branoh Bahati, Victoria Martin, George Williams, Seko Shamte, Grace(Nyumba ya kifahari ya mtindo. ),Howard,Bianca Mengsen,Pedaah John, Arjun, Mgece na Rio Paul.
Mwakilishi wa Chapa ya Möet na Hennesy, Janet Mwalilino alifungua jioni hiyo kwa maneno yaliyojaa bashasha kwa kaulimbiu ya usiku huo ‘Ubunifu Usio na Mwisho katika Ufundi,’ na kusisitiza kuwa kauli mbiu hiyo inaonyesha ari yetu ya kuinua nyakati za maisha kwa shampeni na kutumia usanii wetu wa kipekee tulionao.
Na kuongeza kuwa urithi wa Moët & Chandon umejengwa katika kuchanganya mila na uvumbuzi, na tunafurahi kushiriki hili na jumuiya yetu ya Kitanzania.
Katika hafla hiyo mbunifu na fundi cherehani mashuhuri, Mtani Bespoke alipata fursa ya kuelezea safari yake ya Épernay, Ufaransa ambaoo alipata fursa ya kubadilishana uzoefu na wabunifu wengine kutoka katika nchi za Afrika walioshiriki hafla hiyo nchini Ufaransa.
Alielezea safari hiyo kwa wasilisho maalum la video iliyonasa matukio muhimu aliyoyafanya yeye na mafundi wengine wa Kiafrika waliokutana kujifunza na kufahamu ubora wa Moët & Chandon kuanzia kutengenezwa kwake hadi kuingia sokoni.
Katika kutulia mkazo kuelezea mafanikio ya safari hiyo Bespoke alizindua suti maalumu iliyoitengenezwa kwa na kunakshiwa kwa ustadi na urithi wa Tanzania na Moët & Chandon, huku ikijumuisha mashamba ya zabibu mfano wa yale yanayotengeneza shampeni hiyo na utamaduni wa Kitanzania kwa mavazi ya jamii ya Kimasai.
“Kupitia kipande hiki, nilitaka kuheshimu makuzi yangu na msukumo niliopata nilipofika Épernay. Ni muunganiko wa walimwengu wawili ambao, kwa pamoja, wanasherehekea ufundi wa kweli,” Mtani alisema.
“Inatia moyo kuona utamaduni wetu wa Kitanzania ukiheshimiwa kupitia ushirikiano na kinywaji hichi maarufu. Usiku wa leo, tunasherehekea talanta na hadithi za kipekee za watu wote tuliopohapa, “alisema mshereheshaji Rio Paul.
Tukio hili la kukumbukwa lilisisitiza dhamira ya Moët & Chandon katika sanaa, ubunifu kwa kushirikiana na watu wa nchini Tanzania, kuunganisha ushawishi wa Kiafrika na Ufaransa.
The post Wabunifu wa mitindo ya mavazi wahudhuria hafla ya Siku ya Shampeni first appeared on Millard Ayo.