Tanzania, Urusi kushirikiana utalii

Habari Leo
Published: Oct 29, 2024 07:25:16 EAT   |  Travel

SERIKALI imesema Wizara ya Maliasili na Utalii imekubaliana kushirikiana na Urusi kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amezungumza hayo katika kikao na ujumbe kutoka Urusi ulioongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi nchini Urusi, Maxim Gennadyevich Reshetnikov, kilichofanyika Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho, Dk …

The post Tanzania, Urusi kushirikiana utalii first appeared on HabariLeo.

SERIKALI imesema Wizara ya Maliasili na Utalii imekubaliana kushirikiana na Urusi kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amezungumza hayo katika kikao na ujumbe kutoka Urusi ulioongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi nchini Urusi, Maxim Gennadyevich Reshetnikov, kilichofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Dk Chana amesema Tanzania na Urusi imekuwa na mahusiano ya muda mrefu tangu mwaka 1961 na zimekuwa zikishirikiana katika masuala mengi ikiwemo uchumi, diplomasia na mambo ya kijamii.

Kupitia kikao hicho Tanzania na Urusi zimekubaliana kuboresha ushirikiano utakaokuza utalii ikiwemo programu za elimu ya utalii (Chuo Kikuu cha Urusi na Chuo cha Taifa cha Utalii), utangazaji utalii wa pamoja katika maonyesho ya kimataifa, Bodi za Utalii na makumbusho za taifa za nchi hizo mbili kubadilishana uzoefu, pamoja na uendelezaji wa vitega uchumi.

SOMA: Tanzania ya sita Afrika kutangaza utalii

Aidha, wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya usafiri wa anga na kurahisisha  mfumo wa malipo kwa watalii wanaotembelea nchini Tanzania ili waweze kutumia kadi za Urusi.

Maxim Gennadyevich Reshetnikov amesema sababu ya kuichagua Tanzania ni kutokana na sifa yake ya kuwa na  vivutio vingi vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro huku akisisitiza kuwa Tanzania ni nchi nzuri ya kuendeleza utalii.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya ya Utalii, Dk Thereza Mugobi, Mkurugenzi wa Bodi Utalii Tanzania, Ephraim Mafuru, Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dk Noel Luoga na maofisa waandamizi kutoka serikalini.

 

The post Tanzania, Urusi kushirikiana utalii first appeared on HabariLeo.