VideoUpcoming
TAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI: NOV 29, 2026
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : bit.ly/itvtanzania Facebook : bit.ly/2KeQNl3 Twitter : bit.ly/2XG7aii Instagram : bit.ly/34KItmg
Related stories
NewsGachagua sasa amfunika Uhuru Mlimani wimbi la DCP likizoa wengi
CHAMA cha Jubilee kilichomuingiza madarakani Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kilichowahi kutawala siasa za Mlima Kenya, sasa kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Democracy for Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Mei 2025, DCP imevutia viongozi waliokuwa wanachama wa Jubilee, na hivyo kuzidisha vita vya kisiasa kuhusu nani atatawala eneo hilo kuelekea uchaguzi wa 2027. Baada ya Gachagua kung’olewa mamlakani Oktoba 2024, Jubilee ilianza juhudi za kurejesha ushawishi wake. Uhuru alitangaza kuwa chama hicho kingerejea chini ya uongozi wa Dkt Fred Matiang’i, aliyekuwa akitajwa kuwa mgombeaji wake wa urais. Lakini Gachagua alipozindua DCP, ushindani wa kisiasa ulizidi. Alisema chama chake ndicho kingekuwa chombo pekee cha kisiasa cha Mlima Kenya, huku vingine vikijivuta. Miongoni mwa viongozi waliohama kutoka UDA na kujiunga na DCP ni magavana Irungu Kang’ata wa Murang’a na Kiarie Badilisha wa Nyandarua, pamoja na wabunge Wachira Karani, Muchangi Karemba, Rahab Mukami na Martha Wangari. Aliyekuwa Mbunge wa EALA Kanini Kega, ambaye alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa Uhuru, pia alihamia DCP mwaka 2025. Alisema Jubilee ilikosa uongozi na kwamba wanachama walikuwa wakiondoka kwa wingi. Huko Nairobi, wabunge wote watatu waliochaguliwa kwa tiketi ya Jubilee—Yusuf Hassan wa Kamukunji, Mark Mwenje wa Embakasi Central na Amos Mwago wa Starehe—wametangaza kuwa watatetea viti vyao kupitia DCP. Chama hicho pia kimepokea madiwani wa Jubilee jijini Nairobi. Pigo jingine lilitokea katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou, ambapo DCP ilipata asilimia 86 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 13 za UDA. Jubilee ilipata kura 128 pekee. Mnamo Septemba 22, Uhuru alimkabidhi Matiang’i uongozi wa Jubilee. Hata hivyo, viongozi wa DCP walianza kueneza ujumbe kuwa chama hicho kilikuwa kimeelekezwa zaidi eneo la Gusii, huku DCP ikijikita Mlima Kenya. Baadaye, Uhuru alipohudhuria mazishi ya babake Martha Karu
News2027: Don’t gag opposition in Ogun, ADC guber candidate warns
The governorship candidate of the African Democratic Congress (ADC) in Ogun State for the 2027 general election, Dr. Biodun Collins Ogundipe, has warned against attempts to suppress opposition voices and undermine a credible electoral contest in the state, insisting that the next governor must emerge through a transparent democratic process.
NewsRuto Urges ODM and UDA to Stay United as 2027 Coalition Talks Hit Turbulence
Ruto urges unity in the broad-based government as ODM demands the deputy presidency and 50-50 power share, while UDA backs Kithure Kindiki for 2027 polls.
NewsEdwin Sifuna Declares Ruto Most Beatable President in Africa
Edwin Sifuna says William Ruto is beatable, but warns unseating the Kenyan president will demand hard work as he predicts support for his 2027 bid on US tour.