ALIYEKUWA waziri, mbunge na Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amesema upinzani na kizazi cha Gen Z vinahitaji mikakati thabiti na miundo ya kisiasa ili kuleta mabadiliko ya kudumu nchini.
Katika kitabu chake Illusions of Democracy: A Political Memoir, Kiraitu anasema ushindi wa Rais William Ruto katika uchaguzi wa Agosti 2022 ulitokana na siasa za watu wa kawaida dhidi ya tabaka la matajiri na familia za kisiasa zilizokuwa zimezoea mamlaka.
Anasema chama cha UDA kilitumia hisia na hasira za wananchi maskini, vijana wasio na ajira na wafanyabiashara wadogo, wakiwemo mama mboga na waendesha bodaboda, kuwashawishi wakipigie kura.
Hata hivyo, Kiraitu anasema ahadi za kupunguza umaskini, kutoa huduma bora za afya na elimu, kupambana na ufisadi na kuwawezesha vijana hazijatekelezwa kikamilifu, hali inayochangia kutoridhika kwa wananchi.
Anasema muungano wa upinzani unaopinga serikali ya Ruto umehamasisha wafuasi kupitia mikutano ya kisiasa, lakini bado haujaweka wazi mwelekeo mmoja wa taifa wala mpango madhubuti wa kutatua ukosefu wa ajira, ufisadi na changamoto za utawala.
Kiraitu anaonya kuwa baadhi ya viongozi wa upinzani wanaweza kuwa wanachochewa na hasira ya kupoteza nyadhifa serikalini badala ya kuwa na ajenda ya mageuzi. Pia anatilia shaka uwezo wa muungano huo kudumu na kukubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais.
Kuhusu Gen Z, Kiraitu anasema maandamano ya Juni 2024 yalionyesha nguvu za vijana katika kudai uwajibikaji, kupinga ushuru na kukemea ufisadi, utekaji nyara na mauaji yanayodaiwa kufanywa na maafisa wa serikali.
Anasema vijana hao walilazimisha serikali kubadili msimamo, Rais Ruto akaondoa Mswada wa Fedha wa 2024 na kuvunja Baraza la Mawaziri kabla ya kuingiza baadhi ya viongozi wa upinzani serikalini.
Hata hivyo, anasema juhudi hizo zilikumbwa na changamoto za ukosefu wa uongozi, migawanyiko, ufadhili na wanasiasa kuziteka kujinufaisha kisiasa.
Kiraitu pia anaonya kuwa mitandao ya kijamii inaweza kutumiwa kusambaza chuki na taarifa za kupotosha, huku vijana wakikabiliwa na hatari ya kununuliwa au kutumiwa na wanasiasa.
Anapendekeza vijana kuunganisha uhamasishaji wa mitandaoni na usajili wa wapigakura pamoja na kushiriki uchaguzi ili kuleta mabadiliko ya kidemokrasia.
Anataja kampeni ya Tuko Kadi kama juhudi zinazolenga kuwahamasisha vijana kujisajili kupiga kura na kushiriki katika siasa za mashinani.
Hata hivyo, anasema mageuzi ya kijamii hayawezi kutokea mara moja kwa kuondoka kwa kiongozi mmoja madarakani, bali yanahitaji juhudi za muda mrefu.
Kitabu hicho kilichochapishwa na Queenex Publishers kinatarajiwa kuzinduliwa Ijumaa.
Siri ya Gen Z kumkabili Ruto 2027

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…