Video
Simba SC yaweka wazi dhamira ya kuendeleza Unbeaten.
Channel: Azam TV Watch on YouTube
About this video
JKT TANZANIA vs SIMBA SC: “Ili kuendeleza rekodi ya kutofungwa, lazima uwe na mtazamo wa ushindi...” Kocha wa Simba SC, Steve Barker amesema ana imani na kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho Novemba 21, 2026 dhidi ya JKT Tanzania, kutokana na maandalizi waliyoyafanya wakati wa mapumziko ya ligi. Barker amesema mapumziko hayo yamekuwa muhimu kwa kikosi chake kupata nafasi ya kujipanga upya na kurekebisha maeneo yenye mapungufu hasa baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo miwili iliyopita ya ligi. Kwa upande wa mchezaji wa Simba SC, Charles Semfuko amesema mchezo huo ni kama fainali kwao kutokana na umuhimu wa alama tatu wanazozihitaji, hivyo wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanapata ushindi. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #JKTTanzania #SimbaSC #JKTTanzaniaSimbaSC
Related stories
SportsBalozi Qatar awanunulia tiketi mashabiki kuisapoti Serengeti Boys Kombe la Dunia U17
KUTOKA QATAR: “…tutawapiga Coasta Rica 3-0, hatutakuwa na huruma” Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed, amenunua tiketi 100 pamoja na jezi kwa ajili ya watanzania wanaoishi nchini…
SportsHATA MASIKINI WANAWEZA KUONGOZA TIMU YA SIMBA
SportsMagoli | Polisi Tanzania 0-2 Yanga SC | NBC Premier League 20/11/2026
Cheikh Ibrahim Toure na Peter Shalulile wametikisa nyavu za Polisi Tanzania wakiipa Yanga ushindi wa 2-0 kwenye Dimba la Ushirika, Moshi. Hii ni Ligi Kuu ya NBC.
SportsMziki wa Fadlu wavunja mwiko Ushirika, Moshi
“MMEUONA mziki wa Fadlu!” Hiyo ndiyo kauli iliyotawala kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, leo, wakati Yanga ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo mkali wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na matukio mengi ya kusisimua.