HATUA ya serikali ya kitaifa kujenga soko kwa kima cha Sh65 milioni karibu na mengine mawili ambayo yalijengwa kwa kima cha Sh35 milioni imewaghadhabisha wakazi wa mji wa Ndaragwa, Kaunti ya Nyandarua.
Mji huo mdogo huenda ukawa na masoko matatu ilhali hata lile lililoko kwa sasa halitumiki japo kwa ujumla Sh100 milioni zimetumikwa kwenye ujenzi wa masoko hayo.
Ujenzi wa masoko mengine mawili umeibua maswali iwapo kweli serikali huthamini mikutano ya ushirikishaji wa umma ambapo raia hutoa maoni yao kuhusu miradi.
Moja ya masoko haya yalijengwa wakati wa utawala wa Gavana Daniel Waithaka kwa kima cha Sh15 milioni.
Soko la pili lilijengwa na Benki ya Dunia kupitia mpango wa Hazina ya Kimataifa ya Ustawi wa Kilimo (IFAD). Serikali ya kitaifa sasa inataka kujenga soko la tatu kwa kima cha Sh65 milioni.
[caption id="attachment_173126" align="alignnone" width="1504"] Soko lililojengwa kwa kima cha Sh15 milioni Ndaragwa, ambalo halitumiki. Picha|Waikwa Maina[/caption]
“Mbona soko la tatu lijengwe kwa mji kwa mdogo ambao una masoko mawili ambayo hayatumiki. Kuna masuala mengine mazito na kwa mfano machifu na manaibu chifu wa Muthiga na Nyakinyua hawana ofisi.
“Kule Nyakichua landlodi amemtimua naibu chifu kutoka nyumba ndogo aliyokuwa amekodisha. Wakazi wamelazimika kukusanya fedha zao kumlipia naibu chifu afisi,” akasema Jackson Kahani.
Aliongeza kuwa baadhi ya madarasa kwenye Shule ya Msingi Nyakinyua yako katika hali mbaya na yapo kwenye hatari ya kuporomoka.
Mji wa Ndaragwa nao hauna barabara ya lami, miundomsingi ni mbovu na hakuna mabomba ya kupitisha majitaka.
[caption id="attachment_173128" align="alignnone" width="1504"] Naibu Rais Kithure Kindiki akikagua ujenzi wa soko la thamani ya Sh65 milioni Ndaragwa. Ujenzi wa soko hili unafanyika ilhali kuna masoko mengine mawili mapya ambayo hayatumiki, huku kukiwa na uhitaji wa muundomsingi muhimu kama barabara, madarasa na nyumba za machifu. Picha|Waikwa Maina[/caption]
“Hakuna mkutano unaoshirikisha umma ambao ulifanyika kabla ya soko hilo kuanza kujengwa. Mbona serikali haikushauriana na raia mwanzoni? Tungewaambia hatuhitaji soko jingine,” akasema Peter Maina mnamo Jumatatu.
Wiki jana, Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki akiwa ameandamana na mbunge wa Ndaragwa George Gachagua walikagua ujenzi wa soko ambalo ujenzi wake una thamani ya Sh65 milioni mjini Ndaragwa.
Serikali yakemewa kwa kujenga soko la tatu Ndaragwa ilhali mawili mapya hayatumiki
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]