NCHI wanachama wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (COMESA) zimetakiwa kusanifisha sera na kanuni za mbegu ili kukabiliana na kero ya uhaba wa chakula.
Takwimu za COMESA zinaonyesha kuwa ni asilimia 20 pekee ya wakulima wa mashamba madogo – milioni 90 walioko katika ukanda huo wanaopata mbegu bora na zilizoboreshwa.
Hii imewaacha watu milioni 130 kati ya jumla ya watu milioni 610 wanaoishi nchi 21 zinazounda muungano wa COMESA wakiishi katika umaskini na kukumbwa na uhaba wa chakula.
Tatizo kuu ni soko la mbegu lililogawanyika, ambapo kila nchi inatumia sera na sheria zake. Hali hii inasababisha changamoto kwa kampuni za mbegu kupanua biashara zao katika nchi jirani.
[caption id="attachment_173815" align="aligncenter" width="300"] Mkulima wa mahindi ya rangi tofauti. Picha|Sammy Waweru[/caption]
“Kampuni za mbegu hulazimika kuingia katika kila soko la kitaifa kivyake, jambo ambalo ni ghali na linalosababisha ucheleweshaji wa usambazaji mbegu bora kwa wakulima wadogo,” anasema Dkt John Mukuka, Mkurugenzi Mkuu wa ACTESA, shirika maalum la COMESA.
Dkt Mukuka anabainisha kuwa, licha ya uwepo wa soko la mbegu lenye uwezo wa tani milioni 2, nchi za COMESA huzalisha na kupata chini ya tani 500,000 pekee—sawa na asilimia 2 ya uzalishaji wa kimataifa wa mbegu.
Akizungumza katika mkutano wa kikanda wa utekelezaji wa Mpango wa Usanifishaji wa Mbegu wa COMESA, ndio Seed Harmonisation Implementation Plan (COMSHIP) uliofanyika jijini Nairobi majuzi, Dkt Mukuka alisisitiza umuhimu wa kusanifisha sera na kanuni ili kuziba pengo lililopo.
Kupitia ACTESA, COMESA imeanzisha kanuni za pamoja za biashara ya mbegu.
[caption id="attachment_173816" align="aligncenter" width="300"] COMESA inapendekeza kusanifishwa (harmonise) kwa mbegu za mimea inayozalisha chakula. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Mpango wa COMSHIP, Regional Enterprise Competitiveness and Access to Markets Programme (RECAMP) – unaofadhiliwa kupitia 11th European Development Fund (EDF), unatekelezwa kusaidia uharakishaji wa utekelezaji wa kanuni hizo katika ngazi ya kitaifa na kikanda.
Lengo kuu la COMSHIP ni kuongeza uzalishaji wa mbegu, kuhakikisha ubora, na kuimarisha biashara ya mbegu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Pia, shabaha yake ni kuongeza ushindani katika sekta ya mbegu Afrika Mashariki na Kusini. Wakati wa mkutano huo, wadau walikubaliana kuanza kutumia lebo ya mbegu ya COMESA kwa ajili ya utambuzi wa kitaifa na kikanda.
Dkt Mukuka alitaja mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na usajili wa aina 119 za mbegu kutoka kampuni 20 na taasisi za utafiti kama vile CGIAR.
[caption id="attachment_173817" align="aligncenter" width="300"] Mboga, ni mojawapo ya mbegu ambazo COMESA inataka matozo yake ya ada mipakani kusanifishwa. Picha|Sammy Waweru[/caption]
CGIAR ni muungano unaoleta pamoja mashirika ya kimataifa yanayohusika kwenye ajenda ya kuangazia usalama wa chakula duniani.
Kufikia sasa, nchi 11 zimechapisha rasmi kanuni za usanifishaji wa mbegu za COMESA kwenye magazeti yake rasmi ya serikali, zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Ethiopia, Rwanda, Malawi, Burundi, Zimbabwe, Tunisia, Misri, na Eswatini.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inatarajiwa kujiunga mnamo Mei mwaka huu, 2025.
Viwango vya Utekelezaji (SOPs) chini ya COMSHIP, vimeandaliwa kwa mazao 13 yakiwemo mahindi, maharagwe, ngano, mtama, muhogo, viazi, njugu karanga, alizeti, pamba, soya, mchele na wimbi.
Nchini Kenya, taasisi ya Mbegu na Ustawishaji wa Mimea Nchini (Kephis) inaongoza katika usimamizi wa usajili wa mbegu na utekelezaji wa viwango vya afya ya mimea.
[caption id="attachment_173818" align="aligncenter" width="300"] Mbegu za mboga asilia aina ya 'kahurura', ambazo hutumika kuandaa mukimo. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Hata hivyo, usambazaji wa mbegu feki ungali kero hasa maeneo yanayokuzwa nafaka.
“Miaka michache iliyopita tulianzisha mfumo wa ufuatiliaji wa mbegu kwa kutumia stika maalum zenye alama za kukwaruza ili kuthibitisha uhalisia wa mbegu,” akasema Joyce Karanja, Afisa Mkuu Mtendaji wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Mbegu Nchini (STAK).
STAK, ni muungano ulioleta pamoja kampuni na mashirika yanayounda na kuuza mbegu kutoka kwa sekta ya umma na kibinafsi, shabaha yake ikiwa ni kuhamasisha sera bora.
Sanifisha sera za mbegu kukabili njaa
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]